Muimbaji wa nyimbo za Injili kuimba nyimbo za mapenzi?

Marvin Sapp ni muimbaji wa Injili anayependwa na kutokana na nyimbo zake zenye kumsifu Mungu album yake ya mwisho kufanya I WIN imemfanya awe na mafanikio na kuinuliwa zaidi. Lakini kwa sasa anaongea na vyombo vya habari kusema anataka kutoa nyimbo za mapenzi kuanzia.

Hivi hii imekaaje? nyimbo za mapenzi zina shida gani zikiimbwa na waimbaji wa injili? Nakumbuka muimbaji wa Injili aliwahi kuimba wimbo mzuri MAISHA YA NDOA kutoka kwenye album yake ya kwanza Jipe moyo. Sikiliza wimbo wa Flora Mbasha

Advertisements

7 thoughts on “Muimbaji wa nyimbo za Injili kuimba nyimbo za mapenzi?

 1. Nilikuwa sijaiona hii mada. Napenda mada za namna hii (controversial topics) maana huwa zinasaidia sana kujua mawazo ya wakristo juu ya mambo fulani.

  Rev. Lee Cosmas nimependa mchango wako!

  Ni kwa sababu ya mzamo hasi na ulionajisika juu ya neno “mapenzi” wakristo wanapata shida sana na neno hilo.

  Na ni kwa sababu ya mtazamo huo huo kwenye harusi za wapendwa tupiga nyimbo za utanitambuaje kama nimeokoka, nibebe, wewe ni alfa na omega nk, kwa sababu waimbaji wengi wa injili wanadhani kuimba wimbo wa mapenzi ni dhambi.

  Asili ya mapenzi ni Mungu, na ndiye aliyeweka hisia zote zilizo ndani ya mapenzi.

  Pengine niwakumbushe wanaodhani kuwa Sapp kuimba nyimbo za mapenzi ni kitu kibaya kwamba warudie tena kusoma kitabu cha wimbo ulio bora. Na wala wasijaribu kusema kuwa aliyekuwa anaimbiwa ni Mungu, bali Sulemani alikuwa anaandika hayo mashairi akijibizana na mwanamke aliyekuwa anaitwa Abishagi.

  Hata mimi siku si nyingi nitatoa album ya nyimbo za kawaida ikiwa ni pamoja na za mapenzi.
  Mimi naamini kuwa kila kitu tunachokifanya kwa nia njema kinampa Mungu utukufu “directly or indirectly” maana ndiye asili ya mema yote.

 2. KAMA KWELI HUYU MWIMBAJI NI MATATA BORA ANGEANZA NA NYIMBO ZA MAPENZI NA AKAMALIZIA NYIMBO ZA INJILI ANGEBARIKIWA SANA DA KARUKA MAJI KAKANYAGA MATOPE. AMRUDIE MUNGU MAPEMA KWA KUTUBU MANA KAMSALITI’

 3. Kweli watu wengi wanachanganya mapenzi na ngono. Mapenzi si ngono na tena ngono si mapenzi. Ni vema tunapozungumzia jambo tujue maana ya neno na asili yake. Ngono ukisoma katika Kamusi ya Kiswahili Sanifu kutoka Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili Dar-es Salaam inasemwa kwamba: ni kitendo cha mke na mme kuingiliana. Mapenzi ni hali ya kuingiwa moyoni na kuthamini mtu au kitu zaidi ya mwingine au kingine. Kumthamini mchumba, mke wangu mbele ya watu huku nikimshukuru Mungu kwa ajili yake hakumaanishi kuleta shauku ya tendo hilo kama asemavyo Dada Sayuni. Pia ni vema tujue matumizi ya maneno ya lugha yetu ili tusije tukawapotosha watu. Kitendo cha mke na mme kuingiliana si dhambi iwapo kitakuwa kwa wakati wake uliokubalika na maadili ya Mungu.
  Tusiangalie jambo hili kwa upande potofu ya kwamba mapenzi hayakubaliki kwa wana wa Mungu.

 4. nyimbo za mapenzi zinashawishi ngono hata kwa ambao hawajaingia kwenye ndoa. Kama mtu ana mashairi mengi ya mapenzi amuimbie mke/mume wake. Sio kumuimbia kila mtu, hata hivyo hazina utukufu wa Mungu. Mtu aliyeanza na gospel anaishia duniani, amekaukiwa kiroho.

 5. Muimbaji wa nyimbo za Injili kuimba nyimbo za mapenzi?

  Ninamshukuru kwanza Mungu ambaye ametukirimia karama ya mapenzi. Ninakubali kabisa mwimbaji anaweza kutunga na kuimba nyimbo za mapenzi; kuonyesha upendo na penzi kwa watu. Pia hapa ni lazima kutafakari na kujiuliza lengo la mwimbaji aimbaye wimbo au nyimbo hizo ni nini au lipi. Utukufu wa Mungu wapatikana pote pale ambapo sifa na tukuzo zamwendea YEYE. Upendo au penzi ni tunda la roho iwapo liatakuwa limetawaliwa na Roho wa Mungu.
  Katika kitabu cha Wimbo Ulio Bora wa Sulemani yapo mengi yahusuyo mtu kumwimbia ampendaye; hapa sioni katazo wakati Sulemani anatumia maneno ya kimapenzi kuhusu mpenzi wake. Nakushauri uSome Wimbo ulio Bora). Frola Mbasha kama alimwimbia mpenzi wake; kweli amefanya lililo jema.

 6. YAP! is not bad but kuacha kuimba nyimbo za kumsifu MUNGU na kuanza kuimba nyimbo za mapenz sidhani kama kitamvutia MUNGU,unajua swala la ndoa ni asili yetu hata iweje kila mtu lazima ataoa au ataolewa kama ilivyoandikwa, kwa hiyo mara nyingi kitu cha asili Si cha kukiangakia sana, hangakia sana vitu ambayo vinahitaji juhudi zako mwenyewe mapaka uvipate eg; upako, mafanikio e.t.c. kusema kweli mtu kama Daudi alieupendeza moyo wa MUNGU alikuwa mtu wa sifa na hakuwahi kuimba nyimbo za mapenz,amen

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s