KKKT-DMP KIJITONYAMA WAZINDUA JENGO LA KITEGA UCHUMI

Hilo ndilo jengo lililozinduliwa,Wanaoonekana kwenye picha ni wadau mbalimbali waliojihusisha katika kazi mbalimbali za kuhakikisha ujenzi hata uzinduzi unakwenda kama ulivyopangwa

Askofu mkuu wa kanisa la Kiinjili la kilutheri Tanzania ambaye pia ni askofu wa dayosisi ya mashariki na pwani Dkt.Alex Gehaz Malasusa, jumapili iliyopita aliwaongoza mamia ya waumini wa kanisa hilo usharika wa Kijitonyama jijini Dar es salaam katika uzinduzi rasmi wa jengo lao la kitega uchumi lijulikanalo kama Kijitonyama Lutheran Centre pamoja na kubariki nyumba iliyonunuliwa na kanisa hilo kwa shughuli za kanisa, katika ibada maalumu iliyohudhuriwa na wachungaji,watenda kazi wa kanisa hilo pamoja na wageni waalikwa akiwemo waziri mkuu mstaafu mh.Fredrick Sumaye, mama Anna Mkapa na wageni wengine.

Akizungumza wakati wa mahubiri kanisani hapo Askofu Malasusa kwanza aliwapongeza waumini wa usharika wa Kijitonyama kwa kazi nzuri ya ujenzi wa kitega uchumi hicho kilichogharimu kiasi cha shilingi bilioni 3.5 za kitanzania,kazi ambayo wameifanya ndani ya kipindi kifupi na ya kupendeza ambapo akalitaka kanisa kutumia vitega uchumi kama hicho cha Kijitonyama kulea yatima na wajane zaidi akaliambia kanisa kuwajali watu wa aina zote kwakupewa kipaumbele isiwe kwa wenye uwezo mkubwa wa pesa bali kipaumbele kiwe kwa wote katika matumizi ya jengo hilo. 

Aidha amewataka wakristo kuacha kuwa watumwa wa dhambi,kwani Yesu kristo ametoa msamaha wa dhambi lakini watu bado wanang’ang’ania dhambini hali ambayo ni hatari,kisha akatoa mfano wa mtu aliyekutana naye kwa jina la Anyosisye ambaye alihukumiwa kifungo gerezani baada ya muda akapata cheo cha kuwa nyapara,mara ukatoka msamaha wa rais kwa wafungwa akiwemo Anyosisye ambaye aliposikia yupo huru akataka wampe muda kidogo akae gerezani kwani ndio kwanza kapewa cheo cha unyapara anataka kukitumia kidogo.Akasema watu wanatakiwa kuachana na dhambi kwani hivyo vyeo na mambo mengine yavutiayo ni ya muda dawa ni kuokoka kumfuata Kristo.

KUHUSIANA NA KATIBA.

Akizungumzia suala la katiba askofu Malasusa amewataka wakristo kujitokeza kwa wingi katika mchakato wa uchangiaji upatikanaji wa katiba mpya ya nchi kwakuwa si ya chama,kikundi wala taasisi ni mali ya watanzania wote hivyo kuwataka kutumia haki yao katika upatikanaji wa katiba kwani endapo hawatasimama imara watashangaa kukuta mambo mengine ambayo yapo kinyume na maadili yao yanaingizwa na kuharibu sura ya taifa na kuweka wazi jinsi anavyochukizwa kuona baadhi ya makundi kutaka mambo ya ovyo kama ushoga kuingizwa kwenye katiba jambo ambalo amesema ni hatari na kuacha mara moja kujadiliwa ili kuingizwa kwenye katiba kwani ni kinyume na Mungu na kutaka hayo mambo kuwaachia wenye tamaduni zao.

Uzinduzi huo ulipambwa kwa vikundi vya sifa kama kwaya alikwa ya Winners kutoka Ubungo KKKT,kwaya wenyeji kama Uinjilisti Kijito,kwaya ya vijana, kwaya ya Uamsho,Shule ya jumapili,Kwaya kuu,Matarumbeta pamoja na kwaya ya waumini kwa maana kwa kuimba nyimbo za vitabuni.

 Upande wa nyuma linaonekana hivi

 Maandamano yalioongozwa na kundi la wapiga tarumbeta, kuelekea kwenye jengo hilo kwa shughuli ya uzinduzi

 Watoto wa sunday school wa kanisa hilo nao wakiwa kwenye maandamano

 Wazee wa kanisa wakiwa na nyuso za furaha na wakiwa katika hali ya utanashati na kupendeza nao walihusika katika maandamano hayo.

 Parish wokers na watumishi wengine wa kanisa nao hawakuwa nyuma katika maandamano

 Wachungaji wa sharika mbalimbali nao wakiwa kwenye maandamano

 Na mwisho wa maandamano walikaa wakuu wa jimbo makatibu wa kuu pamoja na Askofu A.G. Malasusa

 Viongozi,waumini na vikundi vya kwaya wakiwa tayari wakisubiri uzinduzi wa jengo hilo

 Askofu Alex G. Malasusa akianza ibada ya uzinduzi wa jengo hilo

 Jopo la watumishi wa Mungu wakisikiliza kwa makini

 Kwa mbali ni kwaya aalikwa ya Winner toka Ubungo 

 Wazee wa kanisa nao wakiwa makini

 Parish wokers nao pia wakiwa katika hali ya uchaji

 Katibu wa baraza la wazee wa kanisa la Kijitonyama akisoma taarifa ya ujenzi wa jengo hilo

 Eng. Sanyiel Kishimbo aliyekuwa msimamizi wa ujenzi huo nae akitoa taarifa kabla ya kulikabidhi kwa katibu wa dayosisi

 Wakati ukafika na utepe ukakatwa tayari jengo likazinduliwa kelele za shangwe na vigelegele vikasikika

 Askofu akiwa amegusa lango kuu la jengo hilo huku akibariki kila aingiaye na kutoka katika mjengo huo

 Hii ni sehemu ya basement iliyomo ndani ya jengo hilo itakayotumika maalum kufundishia darasa la Sunday school kwa watoto wa kanisa hilo la Kijitonyama

 Watoto wakaonyesha furaha yao kwa kuimba wimbo wakifurahia sehemu ya ukumbi huo itakayotumika kama darasa kwao

 Hatua iliyofata ni ile ya kufungua sehemu ya jiwe la uzinduzi

 Askofu Malasusa akifungua sehemu ya jiwe la ufunguzi

 Jiwe la uzinduzi linaonekana hivi

 Hii ndiyo Kijitonyama Lutheran Centre Annex kabla ya kuzinduliwa

 Askofu Malasusa akizindua nyumba hiyo ya ghorofa moja kwa kukata utepe

 Watumishi mbalimbali ikiwa ni pamoja na wazee wa kanisa wakipozi katika picha ya pamoja

 Wachungaji wote waliokuwepo nao wakapozi katika picha ya pamoja

 Kwaya ya Winners toka Ubungo wakihudumu katika ibada

 Kwaya ya Umoja ya usharikani hapo wakihudumu katika ibada

 Askofu Malasusa akihubiri

 Hii ni kwaya ya uamsho, wakimwimbia Mungu wakati wa ibada

—Habari na Picha kutoka kwa Gospel Kitaa na K-Junior blog


Advertisements

11 thoughts on “KKKT-DMP KIJITONYAMA WAZINDUA JENGO LA KITEGA UCHUMI

 1. ;KIJITONYAMA MMEONYESHA NJIA SHARIKA ZOTE TUIGE MFANO HUU MZURI,KWA MUNGU YOTE YANAWEZEKANA. MATUNDA YA KITEGA UCHUMI HIKI YAWASAIDIE WASIOJIWEZE BILA UBAGUZI WA AINA YOYOTE ILE. BIG UP KIJITONYAMA KKKT.CANGAMOTO PIA KWA DAYOSISI IWE NA UWANJA TUJENGE KITEGA UCHUMI CHA DAYOSISI SI CHINI YA GHOROFA 16[Mchumi wa Dayosisi kazi kwako]

 2. BIG UP KIJITONYAMA.Kumbe hata sisi tunaweza bila kutegemea wale wanotulazimisha kuingia kwenye ufreemasonry na ushoga.

 3. Usharika wa KIJITONYAMA mmeonyesha mfano BORA mbele ya MUNGU na wanadamu.MUNGU awaongoze muwe na maono ya mbali zaidi katika kumhudumia mwanadamu KIROHO na KIMWILI

 4. Hongereni KKT mmeonyesha mfano kuwa kwa nia moja mambo makuu yanawezekana.

  Albert (Johannesburg)

 5. Ndugu Mwangomo N,
  Je unaweza kufafanua zaidi swali lako ili wapendwa waweze kujua nini hasa unahitaji kukijua juu ya maono ya kanisa na mtu mmoja mmoja!
  Sijui labda wenzangu wamekuelewa, lakini kimsingi mimi sijakuelewa kabisa, una maana hawa ndugu wa Kijitonyama wamejenga mnara wao wa Babeli?

 6. Ahsante Yesu kwa kuwa kkkt sasa inaweza kufanya mambo makubwa ya maendeleo bila kutegemea msaada, hii ni changamoto na sharika nyingine ziige mfano huu ili tujikwamue na umaskini kwa kupitia kanisa, Mwenyezi Mungu na abariki kazi za mikono yetu. Amen.

 7. Je haya ndiyo maono ya kanisa(kanisa na mtu mmoja mmoja) ili limiliki uchumi kabla ya kuja kwake YESU Kristo mara ya pili. Kamaa Mnara wa Babeli yaani penye kunia na kuzamilia mamoja mengi yanafanikiwa

 8. Hongereni sana waumini na wadau wote wa Usharika wa Kijitonyama, kazi hiyo sio bure Mungu atawalipa kwa wakati wake kama mtalitumia jengo hilo kwa utukufu wake.

  Hii iwe changamoto kwa Sharika za Dayosisi zingine kuiga mfano huu na hii imeonyesha wazi kwamba watu wakimtanguliza Mungu na kuwa wazi (hasa kwenye mapato na matumizi ya makusanyiko yao) kwa kila mipango wanayoipanga, atawawezesha kutimiza ndoto (vision) zao.

  Nasema tena hongereni kwa kitega uchumi hicho na kila revenue itakayopatikana kutokana na hilo itumike kwa ajili ya Ufalme wa Mungu na kamwe isitumike kwa ajili ya wajanja wachache.

 9. Wamejaribu, wameshirikiana wakaweza. Madhehebu mengine pesa inachangwa haionekani, lawama na kanisa halikui. BIG UP KKKT

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s