Nani ni mume wangu?

Naomba maombi kwa ajili ya ufunuo juu ya nani ni Mume wangu, niliolewa na kijana mmoja wakati huo mimi nilikua nimezaa na mtu mwingine miaka ya nyuma. Nimeishi na huyu kijana sasa ni mwaka wa 8 sijabahatika kupata mtoto naye, akaamua kuzaa na mtu mwingine ila bado anaishi na mimi, sasa tatizo linakuja kuwa mimi nikaanza uhusiano na kijana mwingine na anataka anioe ila huyu mwingine ninayeishi naye hatuongei wala nini, ni mwezi sasa umepita.

Naomba maombezi yenu nipate mtoto na nitambue mume wangu ni yupi, niombeeni kwa jina la Yesu nipate mapacha hata watatu ili huyu baba asininyanyase. Asanteni

Teckla

Advertisements

15 thoughts on “Nani ni mume wangu?

 1. HUYU DADA NI MTU ALIYEPOTEZA KABISA MWELEKEO WA MAISHA. NI VIGUMU KUMSHAURI MTU WA JINSI HII PASIPO KUMSAIDIA KUWA NA MWELEKEO MAALUM WA MAISHA, MANAKE NAONA ANAISHI TU MRADI YUPO, KAZAA NA HUYU, KAOLEW NA MWINGINE , ANA MAHUSIANO YA KIMAPENZI NA MWINGINE TENA. DUH? HUO MOYO SIDHANI KAMA UNA NAFASI YA YESU HUMO NDANI, NA NADHANI PIA ANA TATIZO LA KUTAMBUA SELF WORTH AND VALUE OF HER BODY, KAMA MWILI AMBAO MUNGU ALIUUMBA KWA MIKONO YAKE MWENYEWE, TENA AMEUITA KIUNGO CHA KRISTO. PASIPO KUMSAIDIA KUTAMBUA THAMANI YA MWILI ALIOPEWA NA MUNGU, SURA NA MFANO WA MUNGU ULIO NDANI YAKE, HAIWEZEKANI KUMSAIDIA. IT NEEDS A CHANGE FROM INSIDE OUT. hizo ishu za watoto na mume ni vitu vidogo sana, anahitaji foundation itakayo sustain mume, watoto na mambo mengine, na hiyo ni kujitambua kwanza, THAMANI YA MWILI WAKE, SURA NA MFANO WA MUNGU NDANI YAKE, YEYE KAMA KIUNGO CHA KRISTO…
  KWELI DUNIA INA WAHARIBU WATU

 2. Pole, mie naona uombewe hiyo roho ya uzinzi ikutoke, lakini kwanza umpokee Yesu hutahangaika na hayo unayokutana nayo kwani Kristo ni tumaini letu.
  Unapaswa kuachana na uzinzi, ukipungukiwa hiki tu, ukinuniwa tu….tayari umehamia kwa mwanaume mwingine na uko tayari kumvulia nguo! Samahani kwa lugha kali ila naomba jichunguze hii hali utaenda nayo vipi, utalala na wangapi maana si kila mtu ni mkamilifu, si kila ndoa ni paradiso lakini tukiwa ndani ya Kristo tunayaweza yote kwa Yeye atutiaye nguvu. Hivyo ndugu yangu kwanza mpokee Yesu na tubu makosa yako haya, kila kitu kitaenda sawa. Ubarikiwe

 3. NAOMBA KUULIZA SWALI HIVI UKIOA AU KUOLEWA HALAFU UKAACHIKA JE UNAWEZA KUOA AU KUOLEWA TENA?

 4. Wapendwa Mbarikiwe sana?

  Kama nilivyoahidi awali naomba nirudi kwenye kona hii ya ushauri kwa Dada Tekla ambaye hakutaja yuko nchi gani na mkoa gani?
  Bila shaka anaendelea kufuatilia wadau wa mada hii wanatoa ushauri gani kwake.

  SOMO KWAKO: KWA NINI WAKRISTO TUNAZAA WATOTO?

  Swali hili ukimuuliza Mkristo atakujibu kwa urahisi kuwa tunazaa ili kuijaza dunia kama Mungu alivyoagiza. Hata da Tekla ukimuuliza anataka watoto wa nini lazima atakwambia hivyo. Pia ukisoma maelezo yake utaona kwamba anataka watoto kwa ajili ya kuwafanya wawe kama hirizi yake ya kumkinga dhidi ya manyanyaso ayapatayo toka kwa “mume” wake?

  Ukifanya utafiti utagundua kuwa wapendwa wengi hazaa watoto bila wao wenyewe na dhamiri zao kupenda. Utagundua kwamba wengi hujikuta wamenasa mimba ambayo hawakuikusudia. Lakini ukiwahoji watakwambia huyo ni Mungu amependa na watakwambia wanatimiza agizo la Mungu la “ZAENI MUONGEZEKE MKAIJAZE NCHI”

  Wengine wanapoolewa hufanya tendo la ndoa kwa ajili ya kujifurahisha tu. Tendo la ndoa ni sehemu ya starehe ya mke na mume katika ndoa. Wanandoa wengi hufanya tendo la ndoa ili kujiliwaza baada ya kazi nyingi za mchana, au kama wajibu wa ndoa. Na hapo hujikuta wanapata mimba na hatimaye mtoto.

  Wajibu wa kufanya mimba itunge tumboni huwa siyo la wanandoa. Wanandoa wana wajibu wa kufanya tendo la ndoa. Kama wewe Tekla umetimiza wajibu huo na hujapata mtoto, hilo siyo jukumu lako. Wewe umefanya jukumu lako, mtoto kuumbika tumboni mwako, hiyo ni kazi ya Mungu wala siyo yako.

  Dada Tekla Kumbuka Mara nyingi wanawake wa Afrika hulazimishwa na waume zao kufanya tendo la ndoa hata kama wao hawataki kwa ajili ya kutaka kupata muda wa kutosha kulea watoto ambao bado ni wadogo.

  Ndoa nyingi zina migogoro (Ikiwa ni pamoja na za wakristo tena walokole wakati mwingine) inayotokana na kutoelewana katika TENDO LA NDOA. Ukiona mume na mke hawaelewani ujue chanzo kikuu ni tendo la ndoa halijafanyika kama mume atakavyo au mke apendavyo.

  Ukitaka kusuluhisha migogoro ya ndoa za wapendwa walio wengi hasa wakristo peleleza tendo la ndoa linavyofanywa na wanandoa hao kabla ya kuingilia kutoa ushauri. Dada Tekla ni mfano wa kuigwa hapa.

  Kutokana na migogoro hiyo ya ndoa inayotokana na ukosefu wa mpangilio wa kufanya tendo la ndoa, Wanawake wengi (wasiotaka ugomvi na waume zao) huamua kukubali kufanya tendo la ndoa hata kama mtoto waliyenaye bado ni mchanga ili ugomvi uishe. Matokeo yake ndiyo kubeba mimba nyingine ambayo hakuwa ameitaka hata kidogo.

  Kutokana na sababu kama hizo watoto wengi huitwa majina kama , sikujuwa(waswahili), Tinkamanyire (wahaya/wanyambo) Sindamenya (waha), Ya mungu, Bikorimana , nk.

  Ukweli ni kwamba Wakristo wengi kama ilivyo kwa watu wengine (wasio wakristo) huzaa watoto bila kukusudia au tuseme hubeba mimba ambazo hawataki. Wengi waonapo mimba imetungwa hubaki na majuto rohoni na kutamani waende kwa madktari kuomba mimba hizo zitolewe matumboni mwao. Lakini baadaye huamua kukubali kwa shingo upande hadi wanapojifungua.

  WAPO WAJASIRI walioamua kuzitoa mimba bila kujali dhamiri itokanayo na IMANI YA DINI ZAO.

  Dada Tekla elewa kwamba Wapendwa wengi huzaa watoto wengi kuliko uwezo wa kiafya, kiuchumi na kifedha kutokana na sababu zifuatazo:

  1. Kutaka pesa zitokanazo na mahari ya kuoza wato wa kike.
  2. Kupata nguvu kazi ya kutosha shughuli za kilimo na ufugaji.
  3. Kuzaa watoto watakaokusaidia enzi za ukubwani au uzeeni.
  4. Hitaji la kuheshimika katika jami. Kwamba wingi wa watoto ulionao unakufanya upewe heshima na jamii. Eti kama huna watoto hupati heshima.
  5. Hitaji la mtoto wa jinsi ya kike au kiume (Hunting a babygir/babyboyl). Wazazi wanaozaa watoto wa jinsi ya kike tu hundelea kutamani kuzaa hadi pale watakapopata mtoto wa kiume na wale wanaozaa wa kiume tu huendelea kutamani kuzaa hadi watakapopata mtoto wa kike. Hii husababisha wazazi kujikuta wamezaa watoto wengi kuliko uwezo wao kiuchumi.
  6. Wengine huzaa watoto ili kutafuta Mrithi wa mali za wazazi.
  7. Wengine huendelea kuzaa ili wapate watoto watakaosababisha ukoo wao uwe mkubwa
  8. Hamu ya kutaka kunyonyesha huwafanya wanawake watamani kupata mtoto hata kama wana umri mkubwa na wameshazaa watoto wa wengi. Hii hutokana na kuona wivu pale wanapoona wenzao wakinyonyesha watoto.

  9. Wengine huzaa watoto ili wawe ngao ya ndoa yao isisambaratike. Eti kama hujazaa naye atakuacha na wakati wewe hupendi mwachane. Hili tunaliona kwako Da Tekla.

  Baada ya kuelewa sababu hizo, utagundua kwamba hakuna sababu hata moja ya Mungu wala ya kimaandiko bali ni MITIZAMO TU ya mapokeo na tamaduni.
  (Soma zaidi: Taz. Zab. 127:3-5; 128:3-6, Mwa 33:5 na Mambo -Walawi 16:7-9.)
  Nakazia tena kwa kusema: SABABU HIZO ZOTE SIYO ZA KIMUNGU. NI ZA KIMILA AU KIBINADAMU TU.

  SWALI KUU: JE, USIPOZAA WATOTO NI DHAMBI KWA MUNGU?

  Je, kutozaa kabisa mtoto ni dhambi itakayomwangamiza mtu? Kama jibu lako ni ndiyo, je akina Paulo wa Biblia ambao hawakuzaa watoto kimwili wataangamia? Je, watakatifu waliondoka duniani bila kuzaa watoto hawataurithi ufalme wa Mungu. Mpendwa, Majibu unayo wewe mwenyewe.

  Mtume Paulo hakuoa wala hakuzaa watoto. Hakuna mahali Biblia imesema aliacha watoto na mke akaenda kumtumikia Kristo. (Soma nyaraka zake zote hutaona jambo hilo)

  Sasa kama kuna watakatifu ambao walienda mbinguni bila kuacha watoto duniani, wewe ni nani unayemlazimisha Mungu kwamba upate watoto kwa mbinde zote?

  Kwa nini ifike mahala uanze kutangatanga kwa wanaume wengine kutafuta mtoto kwao kisa huyo uliye naye hajakutungisha mimba? Hapa inaonekana kwamba kila mmoja anampima mwenzie. Kwa nini mnapimana uwezo wa kuzaa kwa njia ya kutenda dhambi ya Uzinzi? Dada Tekla hebu waza tena. Hivi ukiwa umelala na huyo bwana asiyekuwa mumeo unajisikiaje? Hata dhamira haikuhukumu? Roho wa Mungu unamweka wapi unapofanya ngono au zinaa na mwanamume asiyekuwa wako?

  Unataka watoto (ampacha watatu) ili baadaye ndoa yako iwe na amani, lakini je, umejipanga vizuri kuhusu hatima ya watoto hao, kielimu, kiafya na kiuchumi?

  Unataka watoto 3 mkupuo ili wawe mkogo kwa mumeo na asikuache au unataka watoto ili uwe mtumishi wao na hatimaye wawe watumishi bora wa Taifa na Mungu wao?

  Natamani tungeonana uso kwa uso ili nikueleze mengi zaidi. Naomba leo niishie hapa.

 5. Kabla sijaanza kukushauri, kubali kuachana na huyo anayetaka kukuoa mke wa mtu.
  Baada ya hapo kumbuka moja ya Vitu ulivyokosa ni upendo wa kweli kwa mume wako na pengine ni namna mlivyoweka msingi wa ndoa yenu ….nitaendelea…

 6. nimepata wazo km upo ktk jiji la dsm jaribu kuwacliana na m2mishi wa mungu mama tedy kwilasa nina imani atakusaidia. cz kabla ya yote unahitaji uijue kweli na kweli ikuweke huru

 7. binafc nashindwa kukushauri, cz ww ni mke wa m2 yalikupataje ya kuanzisha mahucano na mwanaume mwingine. ngoja kwanza nikafikirie nitarudi baadaye.

 8. Da Tekla, nina uhakika haujamjua Kristo. Naomba kwanza chukua hatua ya kuokoka na upate mafundisho juu ya Imani hii kwa njia ya Yesu Kristo. Kuhusu ni yupi mume wako? Huyo unayeishi naye ndiye mumeo. Suala la kutopata mtoto hilo ni jaribu lenu na mlipaswa (wote) kulishinda. Lkn mpaka sasa mume ameshindwa na wewe unafuata nyao hizohizo kwa kutoka nje ya ndoa yako. Kaa chini tafakari upya, achana kabisa na mahusiano hayo mapya uliyaanzisha nje ya ndoa yako. Ukimtegemea Mungu kamwe hautashindwa, hata kama mkikosa mtoto bado mngeza kuishi kwa amani. Watoto ni baraka toka kwa Mungu hatuna uwezo wa sisi kuumba bali Mungu hutupa kwa jinsi apendavyo na kwa wakati aupendao. Na Mungu wetu hajawahi kushindwa. Umeomba maombezi, sawa lkn unapaswa kuishi kwa kufuata misingi hii ya Imani na unapoombewa kumbuka imani yako ndiyo itakayokuwezesha kupokea.
  Barikiwa!

 9. Muombe Mungu mana mke au mme anatoka kwa Bwana, itulize akiLi yako pia zidisha maombi maana hayo ni majaribu, kama Mungu hajakujalia mtoto kwa huyo mme usilazimishe, kuolewa ni sheria kuzaa ni majaliwa.

 10. Dada yangu, hebu Mkiri huyu Yesu kuwa Bwana na mwokozi wako, ndiye atakaye kuokoa wewe na mumeo,
  wewe ndio mjenzi wa nyumba yako (mwanamke mwenye hekima hujenga nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe, bali……………….

  ukisha mpokea naye atakupa msaidizi naye ni ROHO MTAKATIFU, ukimpata huyo umepata msingi imara wa ndoa yako. kama umeolewa jua wazi ndoa ni watu wa wili tu, kumbuka unapotoka nje ya ndoa yako wewe ni mzinzi, kwani unaenenda kwa matendo ya mwili na c ya Roho.

  Hivyo dada mumeo sahihi ni huyo aliye kuoa na c mwingine, Mkumbuke mama yetu Sarah, Elizabeth utaona walipomtegemea MUNGU walipata nini kama sio watoto.
  Mwite YESU dada yangu.

 11. Ushauri. biblia inasema mkumbuke mume wa ujana wako inamaana wewe unapaswa kukaa magotini mwa MUNGU Yesu ndiye anayetoa watoto, usiangalie mambo ya nje weka maagano na Mungu, hata kama ulikosea MUNGU ni mwenye rehema atakukumbuka,OMBA REHEMA.

 12. Kusema ukweli bado watu wengi wanafungwa na tamaduni zilizopitwa na wakati. Hivi kupata mtoto au kutopata mtoto ndiyo nini? Kwa nini mtu anapokosa mtoto kutoka kiunoni mwake anakuwa na majonzi na simanzi hadi ndoa inasambaratika?

  Ni nani aliyeturoga kiasi kwamba mtu anaingia kwenye ndoa kwa lengo moja tu la kupata mtoto. Nani aliyekwambia kwamba kupata mtoto ni LAZIMA unapoolewa au kuoa. Hivi nani aliyekwambia kwamba mtoto ndiyo ngao ya kukulinda usinyanyaswe na mwenzi wako wa ndoa? UTAMADUNI HUU UNATOKA WAPI?

  Hivi ukiwa kwenye ndoa ukawa huna watoto wa kuzaa na huyo uliye naye ndiyo kusema kwamba DUNIA IMEKWISHA?

  Hebu washiriki wa Blog Hii niambieni, nani aliyeturithisha ujinga huu wa kuamini kwamba usipozaa mtoto na mke au mume wako SASA NDIYO MWISHO WA MAISHA YA NDOA? Huu upuuzi unahubiriwa na nani katika makanisa yetu au sera za maendeleo ya nchi zetu?

  Dada Tekla anaomba maombezi eti apate muujuza wa mapacha hata watu kwa mkupuo ili amukoge mume asimtese tena wala kumnyanyasa. Huu ni mtazamo HASI tena wenye ubinafsi. Kama kuna wanawake au wanaume wanaowaacha wenza wao kwa sababu tu hawajapata kuzaa watoto, napenda kuwakaripia kwamba watafakari upya mtazamoo huo HASI.

  Mimi nawahimiza watu wasiomwombee dada Tekla ajifunze kwanza Neno la Mungu alielewe, amjue Mungu wa kweli na aelewe Ndoa ni nini kwani inaonekana kwamba hajui maana ya Ndoa, hajui Mungu anataka nini katika ndoa, Hajui ni kitu gani anataka katika Maisha ya Ndoa. Hebu Dada Tekla kaa kanisani ujifunze zaidi kwa undani. Kaa na watumishi wa Mungu wenye uelewa mpana wa Neno la Mungu. Kaa mahali Mungu akufundishe kwanza kwa unyenyekevu zaidi maswala ya Ndoa ya Kikristo na miiko ya ndoa ya Kikristo. Ukijifunza juu ya ndoa ya Kikristo (Siyo ya kiislam au kipagani kwani najaribu kukuona kama mtu usiye kuwa na Imani thabiti ya Kristo kutokana na maelezo yako) ndipo utaelewa mume wako ni yupi kati ya hao unaowataka.

  Nitarudi tena baadaye kuchangia mjadala huu. Ni ajabu sana. Nimeshangaa sana kwa maneno ya Tekla. Ajabu sana.

 13. Hapa kazi ipo. Nitarudi wakati mwingine! labda nikuulize swali ndugu yangu. Je umempokea Bwana Yesu Tayari?

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s