Tumuombe Mungu atupe Raisi anayetufaa watanzania!

Kusema ukweli kuhusu uraisi wa 2015 ni kigugumizi ambacho hata mimi kimenichanganya akili nashindwa kuwaelewa watanzania! Wengine wanasema Mcha Mungu ndiye atakuwa raisi wa nchi ya Tz mwaka 2015 na tunaona Lowasa saizi kampokea Mungu kuwa ndiye mkombozi wa maisha yake na kutoa misaada kanisani, Vipi kuhusu tuhuma za ufisadi wake na wengine wanaotajwa?

Fedha ambazo zilitakiwa kwa ajili ya umeme wa Tz, mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu, mafao ya wafanyakazi, kurekebishia miundo mbinu ya Tanzania n.k , fedha zote hizo kachukua mtu 1 na wenzie wachache alafu anaenda kucheza harambee makanisani anaambiwa amebarikiwa!

Mi ninachoamini ni kwamba swala la uongozi hasa uraisi anayepanga ni Mungu, ijapokuwa tutafurahi sana endapo atakaye kuwa raisi wa 2015 ni Mcha Mungu kwa sababu atajitahidi kuirekebisha nchi kimwili na kiroho.

Alex E. Mwaibambe


Advertisements

7 thoughts on “Tumuombe Mungu atupe Raisi anayetufaa watanzania!

 1. HAKUNA JIPYA!!
  I think the important thing here is to remove the whole ruling system.That is the only SOLUTION and nothing else.Huku ni kubadilisha bucha tu lakini nyama ni ile ile.The problem was not those Ministers but the one who appointed them,LIKE FATHER LIKE SON.

  There are many issues ambazo zilikuwa sirious zaidi ya hizi which till now we do not know zimeishia wapi,where are those people in EPA issue,RICHMOND,IPTL,DOWANS,B.O.T TWINS TOWERS,doubtful mines contracts and many more!!.Hiki to me ni KIINI MACHO TU! I do not expect anything new.

  There is a problem of Leadership in this country especially in the presidential position.

  We need to be serious in 2015.

 2. BARAZA LA MAWAZIRI LIMETAJWA

  OFISI YA RAISI

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu)
  Ndugu Stephen M. Wasira, Mb.,

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, (Utawala Bora)
  Ndugu George Mkuchika, Mb.,

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (UTUMISHI)
  Ndugu Celina Kombani, Mb.,

  2. OFISI YA MAKAMU WA RAIS

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (MUUNGANO)
  Ndugu Samia H. Suluhu, Mb.,

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (MAZINGIRA)
  Dr. Terezya P.L. Huvisa, Mb.,

  3. OFISI YA WAZIRI MKUU

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji)
  Ndugu Mary M. Nagu, Mb.,

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI)
  Ndugu Hawa Ghasia, Mb.,

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge)
  Ndugu William V. Lukuvi, Mb.,

  4. WIZARA

  Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki
  Ndugu Samuel J. Sitta, Mb.,

  Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
  Ndugu Shamsi Vuai Nahodha, Mb.,

  Waziri wa Ujenzi
  Dr. John P. Magufuli, Mb.,

  Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii
  Dr. Hussein A.H. Mwinyi, Mb.,

  Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
  Dr. Shukuru J. Kawambwa, Mb.,

  Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
  Ndugu Sophia M. Simba, Mb.,

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
  Ndugu Bernard K. Membe, Mb.,

  Waziri wa Katiba na Sheria
  Ndugu Mathias M. Chikawe, Mb.,

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
  Ndugu Emmanuel Nchimbi, Mb.,

  Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
  Dr. David M. David, Mb.,

  Waziri wa Kazi na Ajira
  Ndugu Gaudentia M. Kabaka, Mb.,

  Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia
  Prof. Makame M. Mbarawa, Mb.,

  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
  Prof. Anna K. Tibaijuka, Mb.,

  Waziri wa Maji
  Prof. Jumanne Maghembe, Mb.,

  Waziri asiyekuwa na Wizara Maalum
  Prof. Mark Mwandosya, Mb.,

  Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika
  Eng. Christopher Chiza, Mb.,

  Waziri wa Uchukuzi
  Dr. Harrison Mwakyembe, Mb.,

  Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
  Dr. Fenella E. Mukangara, Mb.,

  Waziri wa Maliasili na Utalii
  Ndugu Khamis Kagasheki, Mb.,

  Waziri wa Viwanda na Biashara
  Dr. Abdallah O. Kigoda, Mb.,

  Waziri wa Fedha
  Dr. William Mgimwa, Mb.,

  Waziri wa Nishati na Madini
  Prof. Sospeter Muhongo, Mb.,

  5. NAIBU MAWAZIRI

  OFISI YA RAIS

  HAKUNA NAIBU WAZIRI

  6. OFISI YA MAKAMU WA RAIS

  Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais
  Ndugu Charles Kitwanga, Mb.,

  7. OFISI YA WAZIRI MKUU

  Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI)
  Ndugu Majaliwa K. Majaliwa, Mb.,

  Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI)
  Ndugu Aggrey Mwanry, Mb.,

  8. WIZARA MBALIMBALI

  Naibu Waziri wa Kazi na Ajira
  Dr. Makongoro M. Mahanga, Mb.,

  Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika
  Ndugu Adam Malima, Mb.,

  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
  Ndugu Pereira A. Silima, Mb.,

  Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara
  Ndugu Gregory G. Teu, Mb.,

  Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
  Ndugu Benedict N. Ole-Nangoro, Mb.,

  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
  Ndugu Mahadhi J. Maalim, Mb.,

  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,
  Ndugu Goodluck J. Ole-Medeye, Mb.,

  Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
  Ndugu Ummy A. Mwalimu, Mb.,

  Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
  Ndugu Philipo A. Mulugo, Mb.,

  Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki
  Dr. Abdulla Juma Abdulla, Mb.,

  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii
  Ndugu Lazaro Nyalandu, Mb.,

  Naibu Waziri wa Ujenzi
  Ndugu Gerson Lwenge, Mb.,

  Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,
  Dr. Seif Suleiman Rashid, Mb.,

  Naibu Waziri wa Nishati na Madini
  Ndugu George Simbachawene, Mb.,

  Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia
  Ndugu January Makamba, Mb.,

  Naibu Waziri wa Uchukuzi
  Dr. Charles J. Tizeba, Mb.,

  Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
  Ndugu Amos Makala, Mb.,

  Naibu Waziri wa Maji
  Eng. Dr. Binilith Mahenge, Mb.,

  Naibu Waziri Nishati na Madini
  Ndugu Stephen Maselle, Mb.,

  Naibu Waziri wa Katiba na Sheria
  Ndugu Angela Jasmine Kairuki, M

 3. MWACHENI MTU AMPOKEE YESU MANA YEYE NDIYO ANAJIJUA VIZURI KTK NAFSI YAKO SIYO KOSA KUMURUDIA MUNGU, ILA UCHAGUZI NDO TUOMBE KWELIKWELI MANA 2015 SIYO MBALI DA MUNGU ATUSAIDIE

 4. Nakubali kuwa wakati wa Agano la Kale na hata sasa Mungu anaweka viongozi siyo kwa mambo ya wanadamu lakini kwa kazi zake. Nakubali pia tunapaswa kuomba tupate hekima ya kuchagua kiongozi ama Rais anayefaa tena atakayetimiza kusudio la Mungu kwa nchi.

  Tuna wajibu wa kusikiliza sera za vyama,kupima nani atatufaa, na kuamua kupiga kura.Hili Mungu HATATUFANYIA.
  Tena Askofu wangu akisema FULANI ni chaguo la MUNGU mimi nimwulize ROHO MTAKATIFU IWAPO NI UFUNUO WAKE AU NI MAMBO YA KAMPENI NA KURA ZA PESA CHAFU!

 5. Kama suala ni kumwomba Mungu hatuna haja kabisa ya kumpangia Mungu mtu awaye yote ambaye kwa akili zetu twadhani ndiye atakayetufaa! Mungu ana watu wengi sana katika nchi ya Tanzania wanaoweza kukaa katika kiti cha urais na kuiongoza nchi katika kweli na haki! Kumbuka nabii Samweli alipokwenda kwa nyumba ya Yese kwa ajili ya kumpaka mafuta mfalme aliyechaguliwa na Mungu.Kila aliyemwona kati ya watoto wa Yese alidhani ndiye aliyechaguliwa! Na Mungu alimwambia maneno haya “Usimtazame uso wake,wala urefu wa kimo chake;kwa maana Mimi nimemkataa.BWANA haangalii kama binadamu aangaliavyo;maana wanadamu hutazama sura ya nje,bali BWANA huutazama moyo….. YESE akawapitisha wanawe saba mbele ya Samweli.Samweli akamwambia Yese,BWANA hakuwachagua hawa! (1 Samweli 16:7,10)
  Pamoja na kampeni zote za mzee Yese kwa wanawe wakubwa,kura ilikuja kumwangukia mdogo wao ambaye hata katika mahesabu ya kifamilia hakuwepo kwani yeye alikuwa busy na kuchunga kondoo. Mimi nadhani,Mungu haitaji kampeni zetu za kisiasa, cha muhimu ni maombi tu kwani YEYE anaweza yote!

 6. Kampokeaje huyo YESU??, mimi naona WATU WANAMPOKERESHA Yesu ili waendelee kupate michango yake. Zambia ilikuwaje enzi zile za ——–???. YESU ANAZO FEDHA NYINGI KULIKO ZA HUYO FISADI, NA KAMA ANATAKA ASAMEHEWE ARUDISHE PESA ZOTE NA KUKIRI KWAMBA ALIIBA. MAANA YESU AKIINGIA NDANI MWAKO KAMA ULIJENGA NYUMBA KWA DHURUMA HUTATAMANI KUISHI HUMO. NINAO MIFANO YA WATU WALIOBADILIKA KWELI KWELI SI KWA AJILI YA URAIS 2015 Paulo Mtume ni mmojawapo.

  Wakristo pamoja na wachungaji tusifilisike kifedha na hata Kiroho kwa kiasi hicho.
  MUNGU ISAIDIE TANZANIA NA WATU WAKE.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s