Fahamu maswali muislamu anayoweza kukuuliza

Una ujasiri wa kuongea na muislamu? usiogope uwe msomaji wa Neno la Mungu. Wiki iliyopita nilikuwa Mombasa ambapo nilipata nafasi ya kufanya mjadala na Imam. Nimeona ni vyema niwashirikishe maswali ambayo wanatumia kama silaha kwa mkristo asiyekuwa na majibu.

1. Kwa mujibu wa mafundisho ya uislamu ni wazi kwamba watapata wake 72 wakienda peponi, alipokuwa akielezea Imam huyo, akasema kwa wakristo ni tofauti kwani tutapata wake 100 mbinguni. Kwa mujibu wa mafundisho ya Kikristo. Unaweza kuona maneno haya ameyatoa wapi, ni katika Mathayo 19:29 “Na kila mtu aliyeacha nyumba, au ndugu wa kiume au wa kike, au baba, au mama, au watoto, au mashamba, kwa ajili ya jina langu, atapokea mara mia, na kuurithi uzima wa milele”

Hivyo wakristo watapewa wake 100 mbinguni????

Swali la pili, kama Yesu ni Mwana wa Mungu, hiyo ni wazi kwamba Mungu ana mtoto, Mungu alikuwa na mke? Na kama kuna familia hiyo, inawezekana pia hata Yesu alioa???

Swali la tatu. Wakristo wanasema Yesu ni Mungu kamili, na tena wanasema Yesu alikufa na akafufuka siku ya tatu. Hii inamfanya Mungu afe kwa siku tatu??? Inakuwaje Mungu afe???

Ebu jiangalie ni kwa jinsi gani utajibu hayo maswali yao “magumu”

–Aaron

Advertisements

9 thoughts on “Fahamu maswali muislamu anayoweza kukuuliza

 1. BWANA YESU ASIFIWE MTUMISHI MM NILIPENDA KUONGEZA KWAKUSEMA TEAU NDIYE MUNGU KWA KUTHIBITISHA HILO SOMA 1YOHANA 5:10 NA UREJEE KATIKA YOHANA 1:1 KISHA MALIZA NA 1YOHANA 5:9, UKIPITIA HIYO MISTARI UTAONA KUWA SISI TU NDANI YA YESU KWA MAANA YESU NI NENO NA NENO HUKAA NDANI YETU NA VILE VILE MBINGUNI KUNA WASHUHUDIAO YANI BABA ROHO NA NENO ,NA KUMBUKA HILI NENO NI YESU NA UKIRUDI YOHANA 1:1 UTAONA NENO HILO AMBAYE NI YESU NDIYE MUNGU , KIFUPI MUNGU YUPO KWA UTATU (BABA ,MWANA NA ROHO) KWA UTATU HUU NDIO MUNGU KAMILI

 2. kila NENO LA MUNGU LAFAA KWA MAFUNDISHO. NI LAZIMA KILA MTU AJUE KUWA HAKUNA DINI DUNIANI KOTE YENYE UWEZO WA KUMPELEKA MTU MBINGUNI ILA NI KWA KUMKIRI YESU PEKE YAKE YOHANA 14:6

 3. BWANA YESU APEWE SIFA….kazi unayofanya ni nzuri lazima tutafute kilichopotea.Wakristo wengi hawaijui biblia vizuri ndiyo maana hawajiamini.lazima tumtafute na kumshinda ibilisi aliyewashikilia ndugu zetu waislamu na wapagani kwa kuwa ndiyo tuliyoagizwa kwamba TUJIBU HOJA NA KUIHUBIRI INJILI IPASAVYO…WASIJE WAKASINGIZIA KUWA HATUJA WAJIBU HOJA ZAO NA KUWAHUBIRIA INJILI.,…kimsingi maswali yao ni marahisi sana sana nakwenda kujibu kama ifuatavyo:Nataka nikufundishe jinsi biblia inaposema kitu fulani inamaanisha nini.Swali lake la kwanza” ETI TUTAPEWA MABIBI MIA KWENYE(Mathayo 19:29)…Hivi aliyemwambia biblia inaakili kama za quruani ni nani?..jibu:(waebrania waebrania 10:34-36)..inajibu hivi:”MAANA MLIWAONEA HURUMA WALE WALIOKUWA KATIKA VIFUNGO TENA MKAKUBALI KWA FURAHA KUNYANG’ANYWA MALI ZENU MKIJUA KWAMBA NAFSINI MWENU MNA MALI ILIYONJEMA ZAIDI IDUMUYO.Biblia imejibu kuwa tukiachana na vitu vya dunia hii basi tutapokea thawabu kutoka kwa mungu mara dufu ya mambo ya hapa duniani yanayoharibika…..swali la pili “ETI YESU NI MWANA WA MUNGU JE ALIOA AU MUNGU ANA MTOTO?…Jibu:hivi wanamjua mungu hawa au wanamfananisha na mwanaadamu tu?…kawajibu kuwa”MUNGU NI ROHO KWA HIYO TUNAPOONGELEA MAMBO YA MUNGU TUNAONGELEA MAMBO YA ROHO NA WALA SIO KAMA WAO WANAVYOFIKIRI…Biblia inatuambia waziwazi kwamba:”KIVULI CHA MUNGU KILIMFUNIKA BIKIRA…NAYE BIKIRA AKAZAA MTAKATIFU”MWANA WA MUNGU ALIE HAI”Soma(luka 1:34-35)…Tena cha ajabu hata kuruani yao inalitambua hili!!…kiufupi ni kwamba:mungu ni roho mwenye uwezo na nguvu zote,yeye hana mwili wa kibinaadamu kama sisi kwa hiyo anafanya mambo yake kwa mamlaka na uwezo wake…hata sisi wanadamu tunasema tumezaa lakini kiroho ni kwa uwezo wa mungu,mungu ndiye anayetuwezesha yote…yeye ndiye anayetuzaa si kwa njia yetu ya kibinadamu bali kwa uwezo wake wa kutuwezesha kiroho.SISI NI MACHIPUKIZI YA MUNGU AU MAZALIWA LAKINI UWEZO NA MAMLAKA YOTE YA UZAZI TUNAMRUDISHIA YEYE….swali la tatu”ETI YESU KAMA NI MUNGU ALIPOKUFA KWANI MUNGU HUFA?….Hili peke yake ndiyo naliona kuwa ni swali la msingi hata wakristo wa sikuhizi wanaohubiri injili zao za pesa..huwa wanababaika sana kujibu.Biblia iwazi inapotuambia”UZIMA WA MILELE NDIYO HUU WAKUJUE MUNGU WA PEKEE NA WA KWELI NA YESU KRISTO ULIYE MTUMA.Soma(yohana 17:3)….pia lile tangazo la malaika alietuletea habari ya mwana wa mungu alituambia hivi:”NAWE MTOTO UTAITWA NABII WAKE ALIE JUU.Soma(luka1:76)…sasa iweje wahubiri wa leo wanafundisha “YESU NI MUNGU WAKO SIJUI WATATU…Acheni injili zenye mafumbo magumu yasioweza kuteguka kirahisi wakristo wenzangu..mnachelewesha wokovu wa watu wengi kwa sababu ya mambo ya siri ya mungu.Mungu mwenyewe alituonya hivi:MAMBO YA SIRI NI YA BWANA MUNGU WENU.(Kumbuk 29:29).Tusijifanye twajua siri zote za mungu tujibu kulingana na biblia inavyotaka.Kiufupi uungu wote wa yesu kristo ni wa kiroho katika kuwezeshwa afanye mapenzi ya mungu na wala yesu kristo sio YEHOVA MUNGU MWENYEWE..Mwenyewe pia maranyingi anakiri hivi:NAFANYA MAPENZI YA BABA ALIYENITUMA KWA KUWA BABA NI MKUU KULIKO MIMI….yesu kristo alishuka kutoka mbinguni ili ajekuwa NENO LA HAKI LA MUNGU .Soma(kumbuk18:18-19)(yohana 1:14)(ufunuo19:13).Yesu kristo ni MWANA WA MUNGU/NABII WA MUNGU KUTOKA MBINGUNI/MTUMISHI WA MUNGU ALIYEKUJA KUFANYIKA HAKI YETU KWA NJIA YA KUMWAGA DAMU YAKE MSALABANI ILI AIBATILISHE ILE YA NDAMA NA KONDOO NA KUWA MJUMBE WA AGANO JIPYA…BIblia inatuambia wazi kuwa hata yesu mwenyewe mwisho wa yote atajitiisha kwa mungu ili mungu awe wa wote katika yote.( 1wakorintho 15:27-28).Kwa hiyo namalizia kujibu swali la tatu hivi:ALIYEKUFA MSALABANI SIYE MUNGU MWENYEZI “YEHOVA”BALI ALIKUWA NI YESU KRISTO MWENYEWE AMBAYE ALIKUWA NI NENO LETU LA HAKI AU KAFARA YA MUNGU KWA AJILI YETU WOTE.SOMA(ISAYA 53:4,5,10)….naitwa mhina rudi tena mombasa ukalete maswali mengine yanayokupa tabu.MBARIKIWE.

 4. Rafiki hongera kwa kazi nzuri ya Bwana uliyofanya huko Mombasa. Nafikiri umetufungua macho na sisi wengine.Kusoma Neno ni muhimu lakini zaidi sana wakristo tumuhitaji Roho Mtakatifu kwani huyo ndiye anayeweza kujibu zaidi kuliko vile tunaweza sisi.

 5. Imeandikwa andiko uua bali Neno uuhisha,Pia YESU anasema kondoo wake anawajua na wanaisikia sauti yake pia anasema anao kondoo wengi walioko zizini humu na wale walioko nje anajua njinsi ya kuwakusanya na kuwafanya kuwa na mchungaji mmoja ambaye ndiye YESU

  Kwahiyo wewe mkristo endelea kuwa kielelezo kwao ili wazidi kumjua YESU huyu wanayesema wanamwamini ila hawaamini kama YESU alikufa na kufufuka,Mpaka leo hii imeenea hila hii ya shetani pale mafarisayo walipodai yesu hajafufuka bali wanafunzi wake walimwiba

  Kila siku waislamu wanaokoka kwa jina la YESU Kristo,Mabishano ya dini hayana tija kwa sisi Tuliopewa dhamana ya Kuokoa nafsi za watu walioonewa na Shetani kwa MAANA WAKIIFAHAMU KWELI,HIYO KWELI ITAWAWEKA HURU.
  AMEN

 6. Kweli hawa ndugu wamekariri maswali na wanajitahidi kutumia nguvu zote kufanya mihadhara nakadhalika. Ila Yesu wetu sisi anatupigania hakuna haja ya kubishana nao.

 7. sielewi kwanini wakristo wapoteze muda wao kubishana na waislam badala ya kutumia muda wao kujifunza Neno la Munngu wao wana imani yao nasisi tuna imani yetu.

 8. Kuhusu mahojiano na ndugu zetu waislamu,sidhani kama ni njia ya kusaidia. Kitakachosaidia kwetu Wakristo si kukaa kwenye mahojiano ambayo mengi yao si ya kusaidia bali kukuza migongano. Tunalopashwa kufanya ni kuonyesha upendo kwa ndugu zetu. Rum.12:9-18.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s