Mungu ni mwenye Rehema

Mch Piason Ndala wa Huduma ya Maombezi ya Matatizo Sugu na Ushauri wa Kibiblia (BCIC), Tawi la Temeke lililopo Mbagala Maji Meupe amewaambia waumini wa Huduma hiyo kuwa, “unaweza kuwa na sura nzuri kama malaika, kama huna rehema na kweli mbele za Mungu na wanadamu, wewe ni sawa na sifuri”

Mchungaji huyo ameyasema hayo jana wakati wa Ibada ya kumshukuru Mungu kwa matendo yake makuu aliyoyafanya katika Kitongoji cha Igonambogo, Kijijini Mayaha Kata ya Minyughe Tarafa ya Ihanja Singida Vijijini iliyohitimishwa na Mch Kiongozi, Mch Michael Peter Imani kwa waumini hao kumshukuru Mungu kwa maombi na kumtolea sadaka ya shukurani.

Mch Ndala akijikita katika somo lake, amewahubiri waumini hao na kuwaambia na hapa ninanukuu, “Unaweza kuwa na sauti nzuri kama chiriku, kama huna Rehema na Kweli, wewe ni sawa na sifuri”. Mwisho wa kunukuu. Akifundisha somo la Roho Mtakatifu, aliloliita, Rehema na Kweli, alisema, kweli Mungu ni wa Rehema. Kwa vile Mungu huwasamehe watu wenye makosa au waliotenda dhambi wakitubu na kuziacha, lakini kama ukitubu na kurudia tena dhambi, utaona Mungu alivyo mwenye hasira nyingi!

Huku akithibitisha mahubiri yake kutoka katika Biblia, alisoma kitabu cha kutoka 34:6-7 na kufafanua kuwa Mungu aliwatokea wana wa Israel katika Mlima Sinai, katikati yao katika wingu zito, akisema kwa mithili ya mchungaji anayemwongoza mwenye dhambi kutubu, Musa akafuatisha na kutangaza, Mungu ni mwingi wa huruma, mwenye fadhili, si mwepesi wa hasira, Akaendelea kusoma, mwingi wa rehema na kweli, mwenye kuwaonea huruma watu elfu elfu, mwenye kusamehe uovu na makosa na dhambi; wala si mwenye kumhesabia mtu mwovu kuwa na hatia kamwe, mwenye kuwapatiliza watoto uovu wa baba zao na wana wa wana wao pia, hata kizazi cha tatu na cha nne.

Mchungaji huyo alihitimisha somo lake kwa kuwauliza wasikilizaji wake kama je, wanajua ni kwa nini shetani alikosa kibali kwa Mungu? Akajibu na kusema, shetani alikuwa ni muuaji tangu mwanzo, wala hakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake, asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe. Kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa huo (Yohana 8:44)

Advertisements

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s