Wachungaji na Mitindo ya Mavazi

Tulishawahi kujadili hapa https://strictlygospel.wordpress.com/2009/12/04/mchungaji-wa-kanisa-na-miradi/ kuhusu wachungaji wanaojihusisha na biashara tofauti na kazi waliyoitiwa. Hivi karibuni Mchungaji maarufu Ed Young amefungua label yake ya kuonesha ubunifu wa mavazi yake, kuhusu uchaguzi wa mashati ya kuvaa na jinsi ya kutengeneza kola. Pastor amepania kuona watu wanakuwa smart.

Mchungaji huyo amesema alipokuwa akizindua mtandao wake wa PastorFashion.com kwamba ni mahali wachungaji wanaweza kupata uzoefu wa jinsi ya kujiweka sawasawa. Alisema alipokuwa akizindua mtandao wake huo.

Kwa wanaojulikana kwa aina ya uvaaji wao ni pamoja na pastor Jamal Brynt kwa muonekano wake nadhifu akiwa anafundisha madhabahuni, kwetu Afrika Mashariki naamini wachungaji wapo siyo wa-congo peke yao wanaojua kupangilia mavazi.

Ni pamoja na Mwalimu Christopher Mwakasege.

Advertisements

6 thoughts on “Wachungaji na Mitindo ya Mavazi

 1. Hahahaaa, Uweza Elisha!

  Niliposoma tu ule mstari wako wa mwisho kabisa, ndipo nilipogundua unatoka katika kundi la watu ambao wanamezeshwa maarifa yasiyo sahihi sana kama bezaleli.

  Hebu nipe tofauti ya kufanya kazi ya Mungu na kufanya kazi na Mungu tafadhali.

  Nani aliwahi kumuuliza Mungu jinsi ya kuvaa mpaka tuifanye hiyo kuwa fundisho?

  Ni hayo tu!

 2. UNAJUA MUDA MWINGINE MUNGU TU ATUSAMEHE KWA SISI TULIOKUSUDIWA NA MUNGU KUURITH UFALME WAKE ILA BADO NAELEWA SANA(SIELEW) KUWA WACHUNGAJI WALIOTUMWA KUFANYA KAZI YA MUNGU NI WANAMNA GANI ;JAMAN TAMBUENI KUWA HATA HARUN ALIJENGA MADHABAHU YAKE WAKAISUJUDU LAKN HAIKUTOA MAJIBU KUMBE ALIJITUMA MWENYEWE SASA KUNA KUFANYA KAZ NA MUNGU NA KUFANYA KAZ YA MUNGU KWA KUWA WANAFANYA KAZ YA MUNGU BASI WAENDELEE KUJITUMA TU NA KUDISIGN MAVAZ YAO WENYEWE ILA KAMA WANGEKUWA WAMETUMWA NA WANA AGIZO LA MUNGU NINGEWASHAURI KUWA WAMULZE MUNGU NI KWA JINSI GANI WAVAE NA SI VINGINEVYO. SHIKA NENO ULIYOPEWA NEEMA KUBWA NA BWANA:

 3. suala la PASTOR kufanya kazi mi naona sio tatizo kwani ni njia mojawapo ya kupata mahitaji yake binafsi

 4. kuhusu mavazi kama ni katika utumishi, lipo vazi moja tu kizazi hiki cha nne, nalo ni vazi Jeupe. kanisa sasa lipo katika agano la Vazi JEUPE.

  KUHUSU MTUMISHI KUFANYA KAZI, wapo wanaosimama madhabahuni full time, wao kazi yao ni kuwalisha kondoo, wengine wanasimamisha mikono yao yote na kuitegemeza (yaani kuangalia mahitaji yao, na wajibu wa wafuasi kutoa sadaka ya nabii), wengine wanahitajika kufanya kazi za mawe ya thamani na kaziza dhahabu ili utajiri wote uingie kanisani,na hapatakuwa hatamtu mmoja aingiaye nyumbani mwa bwana mikono mitupu.

  SHIKA NENO ULIYEPEWA NEEMA KUBWA SANA, TENDA NENO ULIYEBARIKIWA NA BWANA.

 5. Bwana Yesu Asfiwe, naomba kuuliza hv mchungaji anaruhusiwa kufanya kazi? km kuajiriwa kwenye kampuni nk.

 6. Shalom wapendwa
  mimi sioni kama mtumishi wa Mungu kufanya kazi za mikono ili asiwaelemee waumini ni tatizo. Na kama ni biashara siku hizi ni matangazo pia hivyo sishangai akiitangaza biashara yake kwa kuanzia na wachungaji wenzie ila natuamaini kama ni nguo za heshima hata wengine watanunua na kukuza biashara yake. Mtume Paulo alikuwa fundi mshonaji sikumbuki ni kitu gani na pia tunamuona Dorcas ktk matendo akiwahudumia watumishi kwa ushonaji. Mtumishi wa Mungu anapaswa kutumia kipaji chake ili kujikimu na kuinua kazi ya Mungu na si kuwaelemea tu waumini hata kwa mahitaji madogo madogo.
  Angalizo ni ukwasi ktk mavazi na maadili kama yanakuwa si ya kumsitiri vema mtu, pili biashara iswe juu ya wito wako hapo tena ndio inabidi kuchagua mojawapo, vinginevyo sioni tatizo wala tofauti na anayekwenda shambani kulima apate chakula. Mbarikiwe

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s