Askofu aandika kitabu, Mungu siyo Mkristo!

Askofu maarufu wa kanisa la kipentekoste Carlton Pearson alitoa kitabu chenye kichwa cha habari. GOD IS NOT A CHRISTIAN, NOR A JEW, MUSLIM, HINDU….God Dwells with Us, in Us, Around Us, as Us

Kwa maelezo yake ndani ya kitabu kwamba Yesu alisema, Mimi ndimi njiana kwelina uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwanjia ya mimi.Yohana 14:6 Kwa kauli hiyo inaonesha Mungu siyo mfuasi wa Bwana Yesu hivyo siyo Mkristo, ila wanadamu wanaweza kuwa wa-kristo!

Hivi vitabu vingine, kazi ipo kutafuta, kujua na kuelewa Neno la Mungu.

Advertisements

5 thoughts on “Askofu aandika kitabu, Mungu siyo Mkristo!

  1. Ni kweli kabisa Mungu si Mkristo wala si mwenye dini yeyote. Kimsingi hata mitume hawakuwa Wakristo (kwa maana ya dini ya Kikristo), maana maandiko yanasema: kuwa hata mitume waliitwa wakristo kwa mara ya kwanza kule Antiokia. sasa je, kabla ya hapo walikuwa ni watu gani? Maana kwenye masinagogi ya kiyahudi walikuwa wanapingwa na hata kuuawa! Ukweli ni kwamba, Yesu au Mungu hana haja na dini, Ujumbe wake mkuu ulikuwa ni: Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima …

  2. mimi namuunga mkono kabisa kwamba Mungu siyo Mkristo wala muislam wala muhindu au budha. Mungu ni wa watu wote. Kusema kwamba Yesu ndiye njia, kweli na uzima hakumaanishi kwamba Yesu alikuja kuanzisha dini ya kikristo, bali yeye ni mwokozi wa watu wote. jmambo lamsingi la kuzingatia ni kwamba, wote wanaomwamini hawafanyiki kuwa wakristo, bali wanakuwa wa Kristo (of the Christ). Yaani hawawi na dini ya kikristo, bali wanakuwa mali ya Kristo. Na sisi kuwa mali ya Kristo, hakumfanyi Mungu kuwa mkristo.

  3. Sijakisoma kitabu, lakini nadhani maana yake ni kuwa Mungu hana dini..hata japo sisi Wakristo (wafuasi wa Yesu Kristo) tunaamini kuwa njia pekee ya kwenda kwa Baba Mungu ni Yesu Kristo…haimaanishi Mungu ni “mkristo”…ila kama anakwenda kinyume na mafundisho ya Bibli, basi huyo na mwingine awaye yeyote ni tatizo

  4. Ni vema kuyaangalia maandiko, Sijapata kuiona sehemu yoyote katika Biblia, inayosema kwamba Mungu kama Mungu ni MKRISTO, ila Biblia inasema Yesu ni KRISTO, na kama Yesu ndiye Mungu, basi Mungu ni KRISTO! Na kama yupo Mtu anamcha Mungu huyu ambaye ndiye Kristo, Mcha Mungu huyo, ndiye MKRISTO! Hivyo naweza kusema Mungu si mfuasi wa Kristo, ila Yeye ndiye KRISTO! Na Kristo anao wafuasi, Naam ndiyo Wakristo wa kweli! Tusaidiane katika hili tafadhali.

  5. Ni maoni yake, kimsingi tunaposema Mungu ni mkristo ni kutokana na tunaamini kuwa Yesu ni Mungu na hivyo Mungu ni kristo. Nyakati hizi wataibuka watu na vitu vipya vya kila namna, watu watadai wamefunuliwa lkn ukweli hakuna ufunuo zaidi ya biblia, na kama mtu akidai amefunuliwa na kupingana na Biblia huyo ni pepo tu.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s