Manny Pacquiao atumia Biblia kumkemea Obama

Baada ya Obama kuunga mkono ndoa ya jinsia moja mapema wiki hii, Pacquiao ameelezea kwamba Raisi amekosea. Aliyasema hayo kwenye moja ya mahojiano yake akielezea Jamii inahitaji kumweka Mungu wa kwanza.

Manny Pacquiao aliyeacha kucheza ndondi, alinukuu kitabu cha Mambo ya Walawi 20:13 “Tena mtu mume akilala pamoja na mtu mume, kama alalavyo na mtu mke, wote wawili wamefanya machukizo; hakika watauwa; damu yao itakuwa juu yao

Hata hivyo, Obama ameelezea uamuzi wake wa kuunga mkono ndoa ya jinsia moja kwa kutumia amri kuu ya kumpenda jirani yako kama kisingizio cha kutokujali mistari ya biblia inayopinga vitendo vya jinsi moja.

“Fanya kwa wengine yale ambayo ungependa wakufanyie wewe” Raisi alisema kwenye habari ABC “Binafsi nimeamua kwamba watu wa jinsia moja waruhusiwe kuoana” kauli iliyoleta mjadala.

“Pacquiao” kama jina lake la utani,  amesema anamheshimu Obama, na kutoa ushauri Raisi angesoma Biblia kama mwongozo wa maisha mazuri kwa jamii.

Advertisements

8 thoughts on “Manny Pacquiao atumia Biblia kumkemea Obama

  1. Kuna haja na umuhimu mkubwa wa kumwomba Mungu atusaidie kutuongoza kuwachagua viongozi watakao simamia makusudi ya Mungu na wala si ya wanadamu pindi wakipewa nafasi za kuongoza nchi,kanisa na hata jamii. Uchaguzi uko mbele yetu je! Unakumbuka kuiombea nchi yako? hatukujua kama Obama atapitisha kama hayo. kadhalika tuwakamate viongozi katika maombi

  2. Kwani ni nani aliwaambia/ wadanganya kuwa huyo kiongozi ana hofu ya Mungu?
    Alifanya usanii wa kutafuta kura makanisani na wengi wakapotoshwa…

  3. Obama amelewa madaraka na anatafuta kura ambazo zitaua kabisa kibali chake na endapo akishinda utawala wake hautaduma na atayumba mno mpaka atakapotubu, Mungu wa mbinguni amsaidie ili ajigundue maana anaelekea kubaya.

  4. Thanx pacquiao, msimlaumu sana obama sabab hana hofu ya MUNGU, SULEIMAN katika mhubiri amesema tazama binadamu ameumbwa mnyoofu lkn amevumbua mapumbavu yao, nailaani hii kauli ya obama kwa jina lenye uweza la YESU KRISTO.

  5. MCMLAUMU SN HUENDA HANA DINI. MANAKE ANGEKW NA DINI ACNGESEMA HY. KWA7BU HAKUNA DINI INAYORUHUSU HYO MAMBO. 2MUOMBEE WAPENDWA

  6. Kwa kweli Rais Obama Ingekuwa vema kama angebadilisha uamuzi wake na kubadilisha kauli yake ambayo inakwenda kinyume na biblia takatifu.
    Rose K.K.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s