Matangazo ya kualika watu kanisani!

Kumekuwa na matangazo mengi ya kukaribishana kanisani, vipeperushi, kwenye radio, TV na mabango ya barabarani! Kwamba njoo kanisa fulani yupo Mungu, Njoo sehemu fulani kuna muujiza wako nk nk. Je makanisa yanahitaji kujitangaza hivi?

Advertisements

12 thoughts on “Matangazo ya kualika watu kanisani!

 1. “Chema chajiuza, kibaya chajitangaza” wahenga walisemaga hivyo be. Yesu mwenyewe alipowatendea watu miujiza aliwakataza wasiwaambie watu. Ingawa mtu alikuwa mkoma, kipofu au kiwete miaka nenda rudi na watu wameishi nae watakapoona hana ule udhaifu tena ni lazima watauliza imekuwaje? Hivyo jibu litapatikana tu. Tatizo kama wengi walivyochangia watumishi wengi wamekuwa kibiashara zaidi, wanafanya huduma maeneo yale ambayo watu wana kipato kizuri tu, hawataki kwenda sehemu ambazo badala ya kulipwa wewe ndo unatakiwa utoe fedha zako mfukoni uwasaidie watu waliookoka kutoka na hali duni ya kiuchumi.

 2. Ivi hapa Yesu alikuwa anajitangaza eh! Tafakari!

  Mathew 11:28-30:28. Come unto me, all ye that labour and are heavy laden, and I will give you rest.
  29. Take my yoke upon you, and learn of me; for I am meek and lowly in heart: and ye shall find rest unto your souls.
  30.For my yoke is easy, and my burden is light.

  Tubarikiwe

 3. Wapendwa, matangazo siyo mabaya kama matangazo haya yanalenga kuwaleta watu kwa Yesu ili wahubiriwe injili yake watu wapate kuokolewa.Isipokuwa mimi sikubaliani tu na yale matangazo ambayo yako kibiashara zaidi.Kumbuka siku hizi kuna makanisa yanayohubiri injili ya Yesu na mengine yako kibiashara tu na kuongeza idadi ya waenda kuzimu maana watu hawapati mabadiliko rohoni na mwilini.
  Rafiki yangu mmoja aliwahi kusema eti hayaelewi makanisa ya wokovu kwa nini yanakuwa mengi mtaa mmoja unaweza kuwa na makanisa zaidi ya mawili.
  Kwani shida iko wapi kama injili ya kweli inahubiriwa?Mbona baa,kumbi za starehe zinaongezeka lakini hakuna anaelalamika?mabango ya waganga wa kienyeji yamejaa kila kona hayupo wa kulisemea hili?
  Mchangiaji mmoja hapo juu amesema eti makanisa ya ukweli (ambayo ameyataja kama mfano)yenyewe hayajitangazi. Sielewi, sijui amejihakikishiaje hadi kufikia kusema hayo ndiyo ya ukweli na mengine labda siyo ya ukweli.
  Watu wanataka wasikie matangazo ya kidunia tu?ya kuhusu injili ya Yesu yasiwepo?Watu watajuaje Yesu anaokoa?kuna watu wengi wamefungwa na roho ya udini watu hawa wanahitaji kusikia habari njema ya Yesu kuwa ndiye mwokozi pekee na hakuna mwingine.
  Mwisho mimi naamini matangazo si mabaya bali yasilembwe sana na kuwekewa vionjo visivyo na umuhimu wowote.Yesu kwanza

 4. Lwembe umeeleza vizuri, lakini Lazarus inawezekana hajatuelewa katika maelezo yetu hapo juu, na wala asifikiri sisi ni wapinzani wa wokovu bali nimemwamini Kristo kama Bwana na mwokozi wa maisha yangu. Cha muhimu tuangalie hayo matangazo wanaalika waliokwisha kuokolewa au wanapaswa kuwafuata watu wasiomjua Yesu kuwashuhudia na kuwahubiria neno na kumpokea Yesu. Leo hii watumishi wanataka watu wahamie kwao yaani sawa na mvuvi kuvua kwenye tenga la mtu badala ya kuingia baharini. Hatuwezi kuiga waganga wa kienyeji mbinu yao, tufanye lile agizo la kuwaendea watu, tusidhani kuwa tunaweza kumpigania Mungu kama wafanyavyo watu wa imani nyingine, Mungu wetu anajitosheleza na hahitaji kupiganiwa. Kimsingi matangazo sio mabaya ila jinsi yalivyokaa ndio kero.

 5. Lazarus,
  Kristo aliagiza hivi: “Enendeni ulimwenguni kote mkaihubiri injili… Na ishara hizi zitafuatana na waaminio…”

  Na sio “Enendeni mkawaponye watu na kuwatajirisha kwa injili. Yaani Kristo hakuagiza tukazihubiri ishara wala kuzitangaza. Kwanza ulimwengu unaopelekewa habari ya Wokovu ni wa wapagani wasio na ahadi, kwa hiyo unapochukua mbinu za ulimwengu ili kuwavuta watu, kanuni ya imani hutumika nayo hukulazimisha kukihubiri hicho ulicho waahidi ambacho ni ishara zilizo ndani ya”Jina la Yesu”, kabla ya Injili, nayo nguvu iliyomo ndani ya Jina hilo, huwatimizia haja zao, mhubiri na mhubiriwa na kuwapumbaza wote hata wasiwe na haja tena ya ile INJILI IOKOAYO, hii inayotutaka tujinyenyekeze kwa Bwana au Neno lake! Kristo anasema mtu haji kwake asipovutwa na Babaye na si kwa matangazo yetu yenye maudhui ya kilimwengu, yakiwafuatisha mithili ya waaguzi na wasoma nyota!

  Basi, matangazo na mahubiri yetu, vyote vimelenga mambo hayo ya mwilini, nayo Injili ya kweli iokoayo haipo, na ni  adimu. Kwanza, Injili huikimbiza dhambi kwa kukuhukumu. Nasi wengi wetu hatupendi kuhukumiwa, kwa kuogopa kukimbiwa na watu, hawaihubiri kabisa! Kila mmoja anajitahidi kumshinda mwingine; njoo katika nyumba ya Mungu; njoo kwa Bwana wa mafanikio, leo Bwana kaniambia atashusha Moto, ibada ya leo itakuondoa katika ufukara… nk! 

  Basi matangazo yenye kuzitukuza huduma au makanisa, yakitoa ahadi ya Uwepo Mkuu wa Bwana, hayo ndiyo tunayoyaangalia na madhara yake kwa hao wanaovutwa na mambo hayo. Hao, wengi wao hufanikiwa katika hayo wanayoyaendea, na jambo hilo ndilo linalowaaminisha watu katika njia hiyo ambayo sijui itaishia wapi. Kwani wengi wa waliowaendea hao wamewatii katika walichoambiwa na kufanikiwa kama vile watu tunavyowatii waganga wa kienyeji na kufanikiwa, kimwili lakini si kiroho! Kwa sababu mafanikio ya kiroho huambatana na Injili na si vipawa. Angalau basi wakiisha kuwavuta hao watu wawahubiri Injili ili wawe Huru, hakuna, badala yake ni mahubiri yanayowafungia ndani ya zizi wasijevutwa na mwingine!

  Bali matangazo yenye kumtukuza Mungu na si mtumishi, yapo na yanaeleweka kama yanavyoeleweka hayo mengine kwa wote wanaovutwa nayo!!

 6. Matangazo ktk makanisa ya kukaribisha watu sioni km ni shida kwani ktk nyakati tulizonazo shetani amejalibu kutumia kila mbinu kuwavuta watu mfano ukitembea mjini utakutana na matangazo yenye wanawake waliouchi wakicheza na kuonesha maungo yao pia miziki ya kidunia inayowaalika watu kwenda kwenye kumbi za starehe na kama shetani anaenda na sayansi na teknorojia ili kuwavuta watu pia sioni shida kama watu wa makanisa wakitangaza ibada zao na kuwaeleza watu matendo makuu ya Mungu kwani neno la Mungu linasema yatangazeni matendo makuu ya Mungu! ninachofahamu ni hiki kwamba shetani hapendi kusikia ibada zozote zenye lengo la kuponya watu na kuwasaidia anataka aone kuna ukimya kabisa unaohusiana na mambo km hayo ya maombezi kwani kazi zake zinaharibika…so yeyote mwenya mapepo au anayetumia nguvu za giza japo anawezakuwa anaenda kanisani mtu kama huyu lazima atachukizwa na matangazo km hayo..kinachonishangaza ni hiki mkiona watu wanatembea uchi wamevaa lakini mbaka chupi zao zinaonekana hamsemi kitu pia watu wakitangaza pombe hamnavitanao matangazo ya sigara hamna vita nayo matangazo ya uganga na ushirikina hamna shidanayo matangazo ya kuongeza makalio ya wanawake na nyeti za wanaume hamna vita nayo mkiona vipepelushi vya watu wanafanya ngono hamna vita nayo lakini mnakelwa na matangazo yanayo mtangaza kristo na matendo yake makuu hapo lazima kuna maroho wachafu wanawasukuma kusema hayo bila kujijuwa…lakini pamoja na hayo yote mseme msiseme bado kristo atatangazwa tena kwa nguvu sana.na maombi yangu ni haya makanisa yaendelee kuongezeka mabaa ya pombe yafe madanguro ya umalaya yafe…na makelele ya kumtangaza Mungu yaendelee usiku na mchana….

 7. Ukiambiwa Kristo yuko jangwani, au yuko Kimara au yuko Mlandizi; usiende…!
  Wengi wetu hukaa katika matarajio ya matukio fulani, lakini mambo hayo hututimilia machoni petu, hata sisi wenyewe kuhusika katika kutimia huko pasi sisi wenyewe kujua! Miito yote mnayoisikia katika matangazo hayo ndio hizo sauti zinazotuitia twende huko ambako Kristo yupo huko!!! Nayo makundi yetu huitikia miito hiyo na kuishia kuzunguka kama pia!!!

  Tuutafuteni Ufalme wa Mungu kwanza!

 8. Bwana alituamuru akisema “Basi enendeni ulimwenguni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi” Siku hizi ni wangapi wanaenda kutafuta roho na kuziokoa? Wote wamebaki makanisani mwao na kuweka matangazo barabarani ya kuita wagonjwa na wenye laana. Kusema kweli hawana tofauti na matangazo ya waganga wa kienyeji kwa sababu magonjwa yale yale wanoyatangaza waganga wa kienyeji ndiyo hayo hayo makanisa yanayoyatangaza. Wanaohitaji wokvu ni nani atawaleta kwa Yesu?

 9. Mimi sioni kama ni vibaya sana ila kitu cha msingi ni je unawaalika ili iweje. Nia ya ndani ya mtu ndio hasa ya kuangalia. Je unawaalika ili waje upate sadaka nyingi au ufundishe neno la kweli la Mungu ili kuwasaidia kuwatoa dhambini na kumjua Mungu wa kweli. Na pia sii vyema kuvua samaki katika tenga la mvuvi ila ni vyema ikiwa wewe ni mvuvi uingie baharini na kwenda kuvua. Shamba la Bwana lina mavuno mengi sana hivyo watendakazi wanahitajika ili kuingia shambani kuvuna na sio kuchukua mavuno yaliyopo kwenye gunia au kihenge. Matangazo sio mabaya kwani hata yule mwanamke msamaria aliyekutwa na Yesu kisimani akaambiwa mambo yake alienda kutangaza na watu wengi wakaja kwa Yesu kwani ilikuwa ni habari njema Yoh-4:1-30. soma zaidi mstari wa 27 hadi 30. Mimi nachukia zaidi haya matangazo yanayofanana kama ya waganga wa kienyeji yanayotolewa na makanisa kama lete wenye kansa, kisukari, ukimwi na mengineyo lakini husikii wakisema njoo utafundishwa neno la kweli. Wamebaki ku-advertise kuhusu kuponya tu bila neno, Mungu atusaidie. Barikiwa

 10. Bwana Yesu asifiwe!!
  Binafsi nawaunga mkono wachangiaji mada waliopita. Kuna msemo usemao “kizuri chajiuza kibaya kujitembeza/chajitangaza. Wapendwa 2kumbuke kwamba hizi nyakati za kuibuka manabii wa uongo tena wamevaa mavazi ya kondoo.Hawa ni mbwa mwitu wakali na ndio hao wanaotumia makanisa kibiashara. Jamani nashauri 2waepuke sana kwa kujitenga nao. Ndugu shika sana ulichonacho(IMANI) ndio silaha pekee dhidi yao.
  Mbarikiwe!!

 11. NDIYO MAANA WA2 WANASEMA KANISA LIMEKUWA NI BIASHARA. C WANASEMA BIASHARA MATANGAZO. KINACHONISHANGAZA HUWEZI KUSIKIA KANISA LA ROMAN AU RUTHELAN WANAWAALIKA WA2 IBADANI. MUNGU A2SAIDIE JAMANI.

 12. Mimi kwa mtazamo wangu sioni kama kanisa linahitaji kufanya matangazo kwa ajili ya kuita watu kwenye ibada, ndo maana watu wanasema makanisa mengi especially haya yanayoota kama uyoga yapo kibiashara zaidi, MUNGU hatakiwe kufanyiwa advertisement bana. ”Biashara matangazo” so kwa kufanya matangazo ya kuita watu ibadani na kujiproud kwamba ndo mahali salama, cjui yesu yupo, cjui kuna miujiza nk hiyo ni biashara live. Mbona makanisa ya ukweli yaani lutheran, catholic, sabato, anglican na mengine kama hayo hayafanyi matangazo na watu wanajihimu on time wanawahi ibadani? Mimi nafikiri watu wanatakiwa kufunguka jamani yaliyoandikwa yametimia. Wewe can u imagine mchungaji anatangaza wenye sadaka ya 10,000.00 & 5,000.00 wasimame wafanyiwe maombi wewe unaionaje hii? wakati nijuavyo maandiko yamesema sadaka ni siri hata mkono wa kushoto usjue mkono wa kuume una nini.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s