Nassari Atoa Shukrani Kanisani

Mbunge Joshua Nasari na Kangi Lugora wakitoa shukurani zake kanisani.
 

Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki Bw Joshua Nassari  jana tarehe 20 May 2012, alitoa sadaka ya shukrani katika kanisa la FPCT Kilinga Wilayani Meru mara baada ya kuchaguliwa kama Mbunge wa jimbo hilo.  

Akiongea na Mamia ya wananchi wa jimbo hilo katika kanisa hilo Bw Nassari alisema kuwa ameamua kutoa sadaka maalum ya kushukuru Mungu mara baada ya kumaliza vema uchaguzi huku wapiga kura wake wote wakiwa salama tofauti na wengi walivyodhania.

Hata hivyo aliwataka viongozi wa vyama vingine kuhakikisha kuwa wanakuwa mstari wa mbele kutetea maslahi ya wananchi na kuachana na tofauti za kivyama ambazo kama zitaendelezwa basi zitachangia kwa kiwango kikubwa sana umaskini wa Meru.

Akiongea katika kanisa hilo kwenye ibada hiyo mchungaji Langaeli  Kahaya  naye alisema kuwa wananchi wanapaswa kuhakikisha kuwa kamwe hawamchagui kiongozi yoyote kwa ajili ya maslahi ya Rushwa kwa kuwa wote wanaotoa rushwa  ndio wanaosababisha hata umaskini na umwagaji damu ndani ya  nchi.

Kutokana na hali hiyo alisema kuwa ni mwiko kwa wananchi wa Jimbo la Arumeru Mashariki kujihusisha na Rushwa kwa vipindi vyote vya uchaguzi kwa kuwa mpaka sasa Rushwa imeshaacha madhara makubwa sana ndani ya jimbo hilo na pia Rushwa ni dhambi kubwa sana.

Gladness Mushi wa Full shwangwe -Arusha

6 thoughts on “Nassari Atoa Shukrani Kanisani

  1. God bless u mheshimiwa ,usimpoteze yesu hata kwa sekunde maana ubunge utapita lakini yesu hatapita kamwe,tunatamani viongozi wetu wote watambue umuhimu wa kumcha mungu tu,si kitu kingine.

  2. Uwepo Bungeni ukawe Balozi Mzuri wa YESU. Kataa dhambi ya aina yoyote ile. Epuka collective responsibilty ya kudanganya wanannchi. Usikubali kabisa kuruhusu ufisadi, udanganyifu wowote. Kubali kupoteza ubunge kuliko kumsaliti YESU.Bunge hili lina wachungaji wengi lakini hatuoni impact badala yake tunaona watu wa kawaida tu Wanasimama kidete kutetea haki,

  3. Hongera sana Mh.Nassari. Sisi 2nakuombea ili Mungu akuzidishie nguvu zaidi ktk utendaji wako.Epuka sana rushwa na usaliti timiza ahadi zako kwa wananchi.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s