Tukiwa Kwenye Giza Nene, Kuna Mwanga Utatokea!

Kuna ushuhuda wa mama mmoja ambaye alikuwa na maumivu mengi moyoni mwake.

Ni mjane aliyelea watoto wake saba, ilikuwa ni family kubwa yenye furaha na kila sikukuu ya Krismas walikutana na kufurahia pamoja.

Lakini furaha yake ikaanza kutoweka baada ya mtoto wake wa mwisho kufariki ghafla. Alikuwa ni kijana mwenye miaka 27 pekee, huyu mama alilia sana alitamani angekufa pia, alijitesa kwa kulaumu kwanini imetokea kwa kijana wake.

Alimuomba Mungu ampe nguvu na baada ya muda mrefu kupita akakubaliana na hali kwamba kijana wake hayupo tena.

Baada ya miaka miwili kupita, kijana wake mkubwa na mkewe, wakauawa na majambazi. Imani ya mama huyu iliyumba zaidi, alimuuliza Mungu, mbona mimi? Mbona familia yangu unaiacha ipoteze sana?mchana alijiweka busy ili asahau ikifika usiku amejaa uchungu na majonzi, alianza kudhoofika mwili na kutaka kujimaliza.

Alikuwa ni mama aliyelea watoto kwa taabu, akapoteza watoto wake wawili na mkwe wake. Hivyo akajua hakuna kitakachoweza kumpa furaha tena!

Kazi yake hakuifurahia tena, marafiki zake na hata watoto wake waliobaki. Uchungu ulimuathiri kimwili na kiroho pia. Akipata nafasi ya kualikwa na marafiki zake, atatafuta sababu ya kutojumuika pamoja nao. Alijiona mpweke hana matumaini.

Alijiuliza kama atasherehekea sikukuu ya Krismas tena. Siku moja alikuwa chumbani kwake akilia “Mungu wangu Mungu wangu, Mbona umeniacha? Alijifunika uso wake kwa mikono yake, akijijibu mwenyewe “haya maswali Yesu alimuuliza Mungu alipokuwa ameteswa, amekataliwa na yuko peke yake anakufa msalabani”

Ghafla akasikia moyoni aende kanisani, ilipita miaka mingi hajaenda, (alizira) kwenda huko. Alipofika kanisani akapiga magoti na kuomba  Mungu ampe amani, ampe Neema yake aweze kuangalia vile alivyonavyo badala ya kuangalia alivyopoteza. Akashukuru kwa unyonge na kusema “Nashukuru kwa kunipa zawadi ya watoto, hata kama ilikuwa niwe nao kwa muda mfupi”

Alipokuwa akisema hivyo, ghafla akasikia sauti moyoni mwake “Siyo kwa muda mfupi vijana wako ni zawadi yangu ya milele, kwako”

Ghafla akapata jibu, kwamba maisha tunayoishi ni zawadi kutoka kwa Mungu, pia hata kama tutakufa, tutaishi milele. Akapata amani, uchungu wake ukaondoka, akafurahia kazi yake na marafiki zake. Aliweza kusherehekea sikukuu za Krismas zilizobakia na kuelezea Upendo wa Mungu kwetu, haulinganishwi na upendo wa familia zetu tulizo nazo, haulinganishwi na kitu chochote. Upendo unatoka kwa Mungu, hata tukiwa kwenye giza nene, Kuna Mwanga utatokea.

Yawezekana ndugu nawe uko na jambo linasumbua moyo wako, umepoteza sana, kazi, ndoa, watoto, nyumba nk nk. Hakuna anayeweza kuondoa uchungu wako isipokuwa Bwana Yesu Pekee, Hakuna pengine utakapopata amani, isipokuwa kwa Yesu pekee ambaye ndiye mfalme wa Amani, Upendo wa vitu vyote unapita, lakini Upendo wa Mungu, Unadumu Milele!

—twitter @MARYDAMIA

Advertisements

6 thoughts on “Tukiwa Kwenye Giza Nene, Kuna Mwanga Utatokea!

  1. Bwana Yesu apewe sifa,kwani watu wengi wamekuwa wakiabudu dini za kishetani(illuminate /freemasonry)kulikoni?

  2. Dada Mary, Mungu akubariki kwa mafundisho yako. Nafarijika nikisoma jumbe hizi, moyo wangu unainuka tena, Bwana Yesu ninaomba uniondolee uchungu moyoni mwangu.

  3. Ndiyo, ni kweli,
    Katika hili Giza Nene tulimo, yuko Mtu anayeweza kuiwasha Taa; Bwana Yesu Kristo! Yeye ni Nuru yetu, nalo giza haliwezi kustahimili Nuru!!
    Bwana na azidi kutuangazia!!!

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s