Catholics do not worship statues—Lwanga OH! Really

Lwanga said Catholics use holy images to recall important people or situations. PHOTO by Juliet Lukwago

Thou shalt not make unto thee any graven image, or any likeness of any thing that is in heaven above, or that is in the earth beneath, or that is in the water under the earth” (Exodus 20:4)

http://www.newvision.co.ug/news/630374-catholics-do-not-worship-statues-lwanga.html

Publish Date: Apr 16, 2012

By Juliet Lukwago

The Archbishop of Kampala Dr. Cyprian Kizito Lwanga has clarified that Catholics do not worship statues, but instead use them to reflect on their saintly life and behaviour.

He said Catholics use the holy images, paintings and other artistic devices to recall persons or things depicted.

“Just as it helps one to remember one’s mother or father by looking at her or his photograph; images also help Christians to recall saints by looking at their pictures or statues,” Lwanga said on Sunday.

The church leader was showing hundreds of followers parts of the remains of Sr. Faustina Krakow of Poland, the witness of the Devine Mercy which were brought from Poland by Rev Fr. Achiles Mayanja.

Fr. Mayanja, the administrator of Lubaga Cathedral, had just returned from a pilgrimage in Poland, the the home country of the late Sr. Faustina.

Lwanga declared Rubaga Cathedral Parish the home of the Divine Mercy in Kampala Archdiocese and urged believers to make an effort there and reflect on and venerate Jesus Christ.

The prelate was at Lubaga Cathedral during a holy mass to celebrate the day of Divine Mercy (Jesus Christ) on which he conveyed God’s great message through Sr. Faustina Kraków of Poland to the world.

The message was a revelation of the pattern of Christian perfection based on trust in God.

Faustina, who is now a saint, was born on August 25, 1905 in Gogowiec in Poland in a religious peasants’ poor family and she died at a tender age on December 5, 1938. She was the third of ten children.

Throughout her life, she reported a number of visions of Jesus Christ and conversations with Him, which she wrote about in her diary and was later published as a book diary titled Divine Mercy in My Soul.

Lwanga said the use of images of Christ and the saints in the Catholic faith is misunderstood by many. “It does not only show their lack of knowledge about the use of these items, but also ignorance of what the Bible says.”

“The people who accuse Catholics of adoring images should consult those who are knowledgeable in their respective religions before making such criticisms and other comments about the Catholic Church and other peoples’ religions,” he said.

He gave an example of a Ugandan woman singer who sarcastically sang a song titled Nsonyiwa Father , which according to Lwanga, belittles and despises the Catholic religion as far as the Sacrament of Penance, is concerned.

“Why do some people find pleasure and pride in despising other peoples’ religions?” Lwanga sounded firm.

The prelate stressed that images and pictures help Catholics to reflect on Jesus Christ Himself and his saints just as one would look at a picture of his or her beloved one or parent and vividly remember as if that person was still living

His justification was clear: “God has never banned the religious use of statues.”

The function was attended by hundreds of Christians from 54 parishes that form the Kampala Archdiocese.

Kizito Michal George Library, April 16 2012

Advertisements

25 thoughts on “Catholics do not worship statues—Lwanga OH! Really

 1. wapendwa katika bwana,tumsifu yesu kris2.mimi ni mkatoriki halisi mwenye kumwabudu Mungu katika roho na kweli.sanamu kama alivyotolea ufumbuzi kiongozi wa kanisa ha2ziabudu.kutoka 20:4 inakataza kabisa kujifanyia sanamu,kumb5:8,kutoka 34:17 zote hizi znazungumzia juu ya kutoabudu sanamu.swali ni je wakatoriki tunaabudu sanamu?la hasha sanamu zile zpo kwa ukumbusho na kulifanya hekalu la Mungu kupendeza kama alivyomwamuru Solomoni na mafundi stadi wakati wa kulitengeneza sanduku la agano.kutoka 25:16-22,kutoka 26:1-31,kutoka 37:7-9,1falme 6:23-35 angalia pia yn 3:14-15 katika agano jipya.kutoka 35:30-35 hapa bazaleli anateuliwa na Mungu anajazwa roho na akili ya kuchonga sanamu kwa ajili ya hekalu,kutoka 36:35,kutoka 38:23,hesab21:6-9,waamuzi17:1-13.ndugu zangu,huwezi kusema mtu fulani ni mwabudu sanamu bila kujiuliza kwanza maswali haya.sanamu ni nini?na nani mwabudu sanamu? waefeso5:5,wakolosai 3:5 je mimi na wewe ni waabudu sanamu?hili ni swali la muhimu sana kujiuliza km MKRISTU.ni mara ngapi tunawashu2mu wa2 na kuwahukumu kuwa ni waabudu sanamu huku kujihesabia haki pasipokujua 2natenda yaliyosemwa katika wakolosai 3:5?.hata ela tunazozitumia jamani zina picha za waasisi wa taifa letu mfano noti ya elfu moja ina kichwa cha nyerere ni kwa ajili ya kumbukumbu ya mwasisi huyu na kutambua mchango wake kwa taifa hili.je tunaweza kusema ati tukiitumia tunamwabudu Baba wa taifa?au kwani ule mkanda wa yesu unaouangalia na pengine kusikitika zaidi na kutoa machozi kwani yule ni yesu kweli?ama na we unaabudu sanamu sema tofauti yako na sisi ni kwamba sanamu yako iko mfumo wa soft copy sisi ni hard copy?la hasha wapendwa,nadhani sasa tumeijua kweli na kweli itatuweka huru.Mkatoriki shika sana ulichonacho. ufunuo 3:11.kanisa katoriki haliwezi hata siku moja kuteteleka kwa maana Yesu mwenyewe ndiye mlinzi na msimamizi wake (lipo juu ya mwamba) Mathayo 16:18 na ndiyo maana YESU mwenyewe anatusisitiza kwanba mk 10:19,rumi 13:8-10. ahsanteni sana na tumsifu YESU kristu

 2. Lenda,
  Unajua, Mungu ameyaficha sana mambo yake, haswa hayo yanayohusu wokovu. Hebu jaribu kuliwazia jambo hili, kwamba juu ya taratibu nzuri na za kuheshimika zihusuzo ibada, na sadaka zote, huko Agano la Kale, bado wahusika kumbe wasingeweza kumuona Mungu, kwamba HAWAKUSTAHILI!

  Kumbe mambo yote hayo na Sheria zake, na Amri zake zote, kazi yake ilikuwa ni kuwaongoza, yakiwaleta kwa Kristo, hapa ndipo ulipo ukomo wa shughuli hiyo pamoja na mambo yake yote, yaani unalitua zigo na kutulia mikononi mwa Kristo!

  Katoliki hawawezi kuyaelewa ya Wokovu kwa sababu hawakulipokea Neno la kuhesabiwa Haki kwa Imani, ndio maana unawaona wanahangaika na Sheria au zile Amri Kumi ambazo ni sehemu ya hiyo Torati, kama ambavyo nanyi mnahangaika nazo, zikiwafungia nje ya Wokovu ambao hupatikana kwa Neema isiyohusisha matendo, yawe ya kuitii Sheria au chochote kile!

  Basi ukimuona mtu anazunguka na hilo zigo la Sheria na Amri zake, jua kwamba hajamfikia Kristo, ule wokovu, bado hajavuka Yordani kuingia katika Nchi ya Ahadi, angali jangwani akihangaika na mizunguko isiyokwisha! Ndio maana nilikuambia Katoliki wameiba furushi la Sheria lililopitwa na wakati, tulipovuka Yordani tuliliacha furushi hilo hapo kando ya mto, huku tumepewa Amri Mpya:
  “” Na hii ndiyo amri yake, kwamba tuliamini jina la Mwana wake Yesu Kristo, na kupendana sisi kwa sisi, kama alivyotupa amri.”” (1 YOH. 3:23 SUV)

  Hebu rudi katika Agano Jipya ujifunze vizuri ili upewe RM ambaye atakuongoza huko AK upate kuujua na uhusiano wake na AJ, badala ya jinsi hii unayohangaika na Maandiko bila Maarifa, maana Maarifa yanapatikana ktk Wokovu tu!!!!

  Gbu, my brother!

 3. !!!!!!!!!!ALERT!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! DANGER!!!!! A WOLF BETWEEN THE SHEEPS!!!!

  SOMA HAPA CHINI : HATARI KATI YETU

  NILIPOSEMA KUNA WATU WANATAKA KUPOTEZA WATU TAZAMENI MANENO HAYA ALIYOSEMA MNENAJI ALIYEPITA.

  LWEMBE ANASEMA: “Hata hizo Amri Kumi walizozibadili, kwa kweli hazina kazi yo yote ile kwa mkristo, Katoliki kuzichezea kwao ni sawa na mwizi anaye libeba furushi la nguo ulilolitoa nje kwa ajili ya kukusanywa na wazoa taka!

  BIBLIA INASEMA: BASI TORATI NI TAKATIFU, NA ILE AMRI NI TAKATIFU, NA YA HAKI, NA NJEMA” WARUMI 7:12

  BIBLIA INASEMA: BADO MITUME WANASEMA: “ENYI WATOTO, WATIINI WAZAZI WENU KATIKA BWANA, MAANA HII NDIYO AMRI YA KWANZA YENYE AHADI . UPATE HERI UKAE SIKU NYINGI KATIKA DUNIA.” WAEFESO 6:1-3

  HALAFU KASEMA HIVI HAPA CHINI KUONYESHA ANAKUBALI AMRI

  “Neno la Mungu ndilo linalokataza masanamu, kwa ujeuri Katoliki wameyajaza kwenye nyumba zao za “ibada”,

  SIMAMENI KATIKA MWAMBA MSIKUBALI AIBU KAMA HIZI, MSIJE KUJIKWAA KWENYE MWAMBA UKWAZAO /NENO WANAOUPINGA (ANTI-GOSPEL)
  TUNUNUE VAZI LA HAKI (NENO) KUFICHA UCHI/AIBU HIZO

  TUISIKILIZENI BIBLIA SIO MASIMULIZI (STRICTLY GOSPEL HAWAKUKOSEA KUITA HIVYO WEBSITE)

  NIMEMKUMBUKA MNYAMA WA UFUNUO 13:11

 4. !!!!!!!!!!ALERT!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! DANGER!!!!! A WOLF BETWEEN THE SHEEPS!!!!

  SOMA HAPA CHINI : HATARI KATI YETU

  NILIPOSEMA KUNA WATU WANATAKA KUPOTEZA WATU TAZAMENI MANENO HAYA ALIYOSEMA MNENAJI ALIYEPITA.

  LWEMBE ANASEMA: “Hata hizo Amri Kumi walizozibadili, kwa kweli hazina kazi yo yote ile kwa mkristo, Katoliki kuzichezea kwao ni sawa na mwizi anaye libeba furushi la nguo ulilolitoa nje kwa ajili ya kukusanywa na wazoa taka!

  BIBLIA INASEMA: BASI TORATI NI TAKATIFU, NA ILE AMRI NI TAKATIFU, NA YA HAKI, NA NJEMA” WARUMI 7:12

  BIBLIA INASEMA: BADO MITUME WANASEMA: “ENYI WATOTO, WATIINI WAZAZI WENU KATIKA BWANA, MAANA HII NDIYO AMRI YA KWANZA YENYE AHADI . UPATE HERI UKAE SIKU NYINGI KATIKA DUNIA.” WAEFESO 6:1-3

  HALAFU KASEMA HIVI HAPA CHINI KUONYESHA ANAKUBALI AMRI

  “Neno la Mungu ndilo linalokataza masanamu, kwa ujeuri Katoliki wameyajaza kwenye nyumba zao za “ibada”,

  SIMAMENI KATIKA MWAMBA MSIKUBALI AIBU KAMA HIZI, MSIJE KUJIKWAA KWENYE MWAMBA UKWAZAO /NENO WANAOUPINGA (ANTI-GOSPEL)
  TUNUNUE VAZI LA HAKI (NENO) KUFICHA UCHI/AIBU HIZO

  TUISIKILIZENI BIBLIA SIO MASIMULIZI (STRICTLY GOSPEL HAWAKUKOSEA KUITA HIVYO WEBSITE)

  NIMEMKUMBUKA MNYAMA WA UFUNUO 13:11

 5. Dada Bupe,

  “Ukatoliki au Ulokole” ni kweli haviwezi kutupeleka mbinguni; lakini VINAWEZA kutupeleka Jehanamu!!!

  Kwa taarifa yako, Mapepo ya dini ni majeuri kupindukia, Mungu mwenyewe hayamuogopi, sembuse wewe! Tena huduma yake kubwa ni kukubadilisha mpaka nawe uzoelee kulikanyaga Neno zuri la Mungu kama nguruwe!

  Neno la Mungu ndilo linalokataza masanamu, kwa ujeuri Katoliki wameyajaza kwenye nyumba zao za “ibada”, halafu wanakudanganya mchana kweupe kuwa eti hawaziabudu, ilhali unawaona makasisi wakizipigia magoti kila wanapoendesha ibada, lakini unajionea sawa tu; Uongo wa dini umeyapofua macho yako ya kiroho, nakukuacha kuwa msukule wa dini!!!

  Biblia inafundisha wazi wazi kwamba Kanisa hilo lina mafundisho ya mashetani, 1Tim 4:1-5 “Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani; kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe; wakiwazuia watu wasioe, na kuwaamuru wajiepushe na vyakula, ambavyo Mungu aliviumba vipokewe kwa shukrani na walio na imani wenye kuijua hiyo kweli…”

  Sasa Bupe dada yangu, ni nani anayehukumu hapa, ni sisi tunaokutahadharisha uukimbie huo uharibifu au Neno lenyewe ndilo linalokuhukumu?

  Wewe mwenyewe una jua wazi kabisa kwamba Kanisa Katoliki linawazuia makasisi wake wasioe, sasa usichokielewa hapa ni nini kama si ujeuri ulioambukizwa?

  Haya, wengine hao hapo Wasabato, wao wanawaamuru wafuasi wao wajiepushe na vyakula, sasa unataka uambiwe nini ndio uelewe?

  Unapokidhi viwango vya Neno, ndipo unapokuwa hilo Neno, tayari kwa aidha Mbingu au Jehanumu!!!

  Hao dada yangu hawana Safari yoyote ile wanayoitegemea kama wanavyokudanganya kuhusu habari za “mbinguni”; hivyo ni vituo vya Yatima wa Kiroho tu!

  Hata hizo Amri Kumi walizozibadili, kwa kweli hazina kazi yo yote ile kwa mkristo, Katoliki kuzichezea kwao ni sawa na mwizi anaye libeba furushi la nguo ulilolitoa nje kwa ajili ya kukusanywa na wazoa taka!

  Bupe, wokovu haupatikani kwa Katekesimu bali kwa Neno la Mungu, hilo ambalo umeambiwa USIONGEZE wala USIPUNGUZE, basi jiulize unapolipunguza au kuliongeza ni mbingu gani utakayokwenda, maana Mbingu ni hilo Neno Kamili la Mungu, ndiyo Mbingu yenyewe!!!

  Mungu na akufungue macho yako!

 6. TUJITAHIDI KUTOMLINGANISHA MUNGU NA KITU TUPATE KUPONA

  ISAYA 40:18-19

  “BASI, MTAMLINGANISHA MUNGU NA NANI? AU MTAMFANANISHA NA MFANO WA NAMNA GANI?. SANAMU FUNDI MMOJA HUIYEYUSHA, NA MFUA DHAHABU HUIFUNIKA DHAHABU, HUIFULIA MIKUFU FEDHA.”

  INAENDELEA..

  ISAYA 40: 20-22
  “YEYE ALIYE MASKINI SANA HATA HAWEZI KUTOA SADAKA YA NAMNA HII, HUCHAGUA MTI USIOOZA, HUJITAFUATIA FUNDI MSTADI WA KUSIMAMISHA SANAMU YA KUCHONGA ISIYOWEZA KUTIKISIKA. JE! HAMKUMJUA? HAMKUMSIKIA HAMKUAMBIA TOKEA MWANZO? HAMKUFAHAMU TANGU KUWEKWA MISINGI YA DUNIA? YEYE NDIYE ANAYEKETI JUU YA DUARA YA DUNIA NA HAO WANAOKAA NDANI YAKE HUWA KAMA PANZI; YEYE NDIYE AZITANDAYE MBINGU KAMA PAZIA NA KUZIKUNJUA KAMA HEMA YA KUKALIWA”

 7. Best fuatilia kauli fulani za Yesu kwenye biblia zilivyokuwa kali halafu uone kama zilikuwa zinawavuta watu kwake. Kwa mfano: siwezi kuwapa mbwa chakula cha watoto, kamwambieni huyo mbweha, ninyi ni wa baba yenu ibilisi, n.k.

  Naona kama unachanganya kati ya kuhukumu na kuambia mtu ukweli.
  Tunaokwambia haya hata sisi tumezaliwa kwenye ukatoliki na tukafanya mafundisho ya katoliki, baadae kwa neema ya Mungu tukakutana na Yesu.
  Maisha yetu hayakubaki yalivyokuwa.

  Jaribu kuokoka halafu utaona tofauti. Tena ukiweza uokoke halafu ubaki hukohuko katoliki.

  Halafu anachosema Bupe kwamba unaweza ukafanya kosa bila kujua ni kwa sababu hajui kazi ya Roho mtakatifu ndani ya mkristo.

  Ubarikiwe rafiki.

 8. Sikuona kilichonivutia kwenu mnaojiita walokole,mmekalia hukumu japo si kazi yunu. someni comments za Bupe ktk mada hii,pamoja na za Wangali ktk mada ya inayohusu KILEO. Hamuwezi kuwavuta watu waje kwa Yesu kwa style hiyo hata siku moja! MLOKOLE = WEMA,UPOLE,UNYENYEKEVU,HURUMA,UPENDO,SHAURI,UAMINIFU NA MAMBO KAMA HAYO.

 9. Marekebisho ya Nukuu hapo juu kwa lenda fungu la mwisho kutajwa ni la

  2 wakorintho 6:16

  lakini pia la

  waefeso 5:5 huongelea juu ya sanamu

 10. ukatoliki au upentekoste hauwezi kukupeleka mbinguni, watu badala ya kuihubiri injili mnakaa kuangalia wengine wanafanya nini? angalia moyo wako kwanza kabla ya kuanza kuhukumu wengine, na wewe ni nani mpaka uhukumu wengine, walokole wengi tunadhani tu kwa kuokoka basi tumekamilika kuna makosa tunafanya bila kujua ni makosa, daima naomba rehema ya mungu ili aniongoze katika njia impasayo.TUTASHANGAA SIKU IKIFIKA WALE TULIOONA WAMEPOTEA WAKINYAKULIWA NA SIYE KUACHWA.

 11. Hivi ndivyo walivyofanya wakatoliki kwenye Amri kumi. Baada ya kuona watu wansema sana juu ya sanamu na Jumapili wakatengeneza katekisimu ili watoto wanapoata mafundisho waigundue tofauti ya amri hizo na ya pili ya sanamu wakaitoa na ya nne ambazo walikiuka walipogundua kuwa wamekosea wakajiita hawawezi kukosea kuficha aibu hivyo. Kuzuia waumini wasisome Biblia na kutowasisitiza wasome wasione ukweli.
  Fananisha A MRI HIZI ZA MUNGU ZA KATEKISIMU YA PERAMIHO TOLEO LA 2002

  AMRI ZA MUNGU KUTOKA 20:1-17 Amri katoliki katekisimu 2002

  1.Usiwe na Miungu wengine ila mimi 1. usiabudu miungu mingine

  2.Usijifaanyie sanamu ya kuchonga, 2.Usilitaje bure jina la Mungu wako
  wala mfano wa kitu chochote kilicho juu mbinguni
  wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini
  ya dunia,usivisujudie,wala kuvitumikia; kwa kuwa
  mimi Bwana Mungu wako ni Mungu mwenye wivu;
  nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi
  cha tatu na cha nne cha wanichukiao,namia
  nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika
  amri zangu.

  3.Usilitaje bure jina la Bwana, Mungu wako, maana 3.Shika kitakatifu siku ya mungu wako;
  bwana hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajae
  jina lake bure.

  4.Ikumbuke siku ya Sabato uitakase siku sita 4.waheshimu baba yako na mama yako
  fanya kazi, utende,mambo yako yote; lakini siku ya upate miaka mingi na heri duniani.
  saba ni Sabato ya Bwana, Mungu wako, siku hiyo
  usifanye kazi yoyote, wewe,wala mwana wako,
  wala binti yako,wala mtumwa wako, wala mjakazi
  wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni
  aliye ndani ya malango yako.Maana, siku sita Bwana
  alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyo
  mo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo Bwana akai
  bariki siku ya sabato akaitakasa.

  5.waheshimu baba yako na mama yako;siku zako 5. Usiue
  zipate kuwa nyingi katika nchi apewayo na Bwana,
  Mungu.

  6.Usiue 6.Usizini

  7.Usizini 7.Usiibe

  8.Usiibe 8.Usiseme uongo wala usitoe ushahidi
  wa uongo;
  9.Usimshuhudie jirani yako uongo 9.usitamani mwanamke asiye mke wako

  10. Usitamani nyumba ya jirani yako, usimtamani 10.Usitamani mali ya mtu mwingine.
  mke wa jirani yako; wala mtumwa wake,wala
  mjakazi wake, wala ng’ombe wake, wala punda
  wake, wala chochote alicho nacho jirani yako.

  Amri katoliki wameigawa mara mbili amri ya kumi ya Mungu ili kuwa hadaa wasomaji kuonesha amri ziko kumi huku wakitoa ya tatu na nne.

  wakatoliki hutumia vigezo vifuatavyo kuwa wamepewa mamlaka ya kufanya lolote duniani
  kwa ukuu wa Petro.

  wakipotosha maana halisi ya Petro -petra=small rock= kwa kigiriki Peter ni kamwamba kamwamba Yesu alikuwa anajitaja yeye ndio Mwamba kanisa limenzishwa juu yake.

  hutumia hii kuhalalisha ibada zao zaasili na waumini wake huibusu miguu ya sanamu ya Peter/Jupiter Yule mungu wa warumi. sananu hiyo inasadikia kuhamishiwa kutoka katika mahekalu ya kirumi ya
  mungu Jupiter ambayo huvishwa duara kichwani na vidole viwili vikionyesha juu.(wao huita baraka !!!!!)

  lakini pia Dini yao ya asili ya mithraism ambayo mithra aliyezaliwa kama mwamba wa jiwe kutoka chini ya ardhi huabudiwa.

  tembelea vaticann utazame sanamu Jupiter ambayo huvishwa nguo kama papa na kuabudiwa
  ndani ya kanisa la Vatican.

  “TENA KUNA MAPATANO GANI KATI YA HEKALU NA SANAMU” WAEFESO 5:5

 12. Hakuna UFUFUO katika Ukatoliki! Ukatoliki ni kaburi, na iwapo kuna nafasi kwa Mkatoliki yeyote yule kufufuliwa, basi nafasi hiyo ni wakati huu, mnapoitwa mtoke katika kaburi hilo, kama alivyoitwa Lazaro, mumpokee Bwana Yesu Kristo, yeye pekee, kuwa Bwana na Mwokozi na Muombezi katika maisha yako yote. Tubia masanamu uliyoyachanganya katika ibada kinyume na maagizo ya Mungu, na sala zote ulizozifanya kupitia Maria; Nenda UKABATIZWE katika maji mengi, kwa Jina la Bwana Yesu Kristo upate Ondoleo la Dhambi zako nawe uwe kiumbe Kipya katika Kristo Bwana uliyejazwa furaha ya kweli ya kiungu!!!!

 13. There is absolutely no RESURRECTION in Catholicism! It’s a tomb, and if there’s going to be a resurrection for any Catholic, then its now as you are being called out of that tomb, to receive The Lord Jesus Christ, and Him only, as your Savior and the Intercessor for your sins! Repent and be baptized in the Name of The Lord Jesus Christ for the remission of your sins!!!

 14. Ndugu zangu wakatoliki,sio kwamba tunawachukia au
  kuchukia ukatoliki hapana.Mungu mwenyewe aliyeumba
  mbingu na nchi na vitu vyote vinavyoonekana na
  visivyoonekana hapendi sanamu. Kutoka (20:4-5)
  kwake vitu hivi ni chukizo.Watu wanaoabudu sanamu anawaita
  makahaba au wazinzi(Hosea 4:12-14;17-18)
  Siku moja nikiwa kidato cha 5 miaka mingi tu
  imepita,wakati tukiwa kwenye kipindi cha dini
  na mwalimu alikuwa padri wa kizungu ndipo alipoulizwa
  swali na mwanafunzi mwenzetu kwamba kwa nini sisi
  wakatoliki tunaabudu sanamu?yule mwanafunzi alikuwa
  amesoma neno hilo hapo juu ambapo tumekatazwa
  kujifanyia sanamu.Majibu ya yule padri hayatofautiani
  na majibu aliyoyatoa huyu askofu!Wakati nikiwa mkatoliki
  nakumbuka nilikuwa nakerwa sana na jambo hili pale
  nilipokuwa naambiwa na walokole au madhehebu mengine
  ambao hawatumii sanamu katika ibada zao kwamba sisi
  wakoliki tunaabudu sanamu.Nilikuwa nikichukia sana kiasi
  cha kusema kuwa hawa hawautakii mema ukatoliki kwamba
  wanauchukia ukatoliki tu hawana jipya.
  Ndugu zangu ebu nawaomba mkaviangalie vile vitabu
  mnavyotumia kama hii amri ipo au imenyofolewa?
  Wakati wa jumuiya kila tulipokutana kwa ajili ya
  ibada,kisanamu ama cha Yesu au Maria lazima
  kiwepo tena cha kushangaza kinawekwa mbele ili
  wote mkitazame.Swali:je bila hivi visanamu au vinyago
  ibada haiendi au itakuwa batili?
  Siwashangai wale wachangiaji wanaotetea jambo
  hili na kukasirika wanapoambiwa kuwa si vyema na
  ni kuabudu sanamu.Vile vijumba vilivyojengwa pale
  kanisani ambamo ndani yake kuna aidha sanamu
  ya Yesu au Maria ukiingia ndani lazima uiname au
  kupiga magoti mbele yake.Na hata ukipita mbele
  yake kwa nje ukihisi uko mkabala na kijumba hicho
  ambamo ndani yake kuna hizo sanamu au vinyago
  lazima uiname na kutoa heshima.Kitu kingine ile
  sanamu ya Yesu au ya Maria unaweza ukaenda
  pale ukapiga magoti au kuinama mbele yake,kusali
  na kutoa shida zako kwa mategemeo ya kujibiwa
  maombi yako.Hii siyo kabisa! hakuna kifungu chochote
  kwenye biblia kinachoruhusu jambo hili.Wapendwa
  wenzangu hawa ndugu zetu tuwaombee hilo ndilo
  la msingi zaidi maana macho wanayo lakini hawaoni,
  masikio wanayo lakini hawasikii.Usitegemee kiongozi
  atoe majibu yaliyo kinyume na hayo ya askofu ,never!
  Na akitoa majibu kinyume na hayo ataitwa kwa papa
  mara moja maana atakuwa ameenda kinyume na
  msingi wa ukatoliki kwa sababu umejengwa kwenye
  traditions za kirumi za kuabudu kimungu kike.Chanzo
  cha mambo hayo yote ni mfalme Costantino historia
  iko wazi kabisa.
  Ndugu zangu siku zimeisha tuache kukumbatia udini
  badala yake tuliangalie neno la Mungu linasemaje.

 15. Napenda kumjibu huyu Kazana,Ndiyo tunamwabudu Mungu ktk Roho,mwanzo tulikuwa huko upande wako lakini Roho Mtakatifu mwaminifu akikukamata na kushuka ndani mwako lazima utaamini kweli huyu ni Mungu mbona mwanzo sikuwa hivi?Na ninakwambia Yesu anarudi sijui wengi atawakutaje ,wanamtazamia kwa macho haya ya nyama,Hapana ni macho ya rohoni,na macho ya rohoni lazima ule gombo kweli na kujazwa nguvu za Roho Mtaktifu,tukiangalia zekaria 13:8 mafungu mawili yatakatiliwa mbali bali fungu la tatu litasafishwa km dhahabu isafishwavyo nao wataita nitasema mimi ndiye Mungu wao nao watakuwa watu wangu,ngoja nikufafanulie huyu huyu ni Roho anansaidia si kwa fahamu zangu,mafungu mawili ni zile dini,watu tumekazana dini yangu au dhehebu langu lakini hauendi sawawa na neno la Mungu that means utakatifu,maana ktk mji ule kinyonge hakitaingia yaani ndani mwako moyoni mwako dhambi haitakiwi,mawazo mazuri ndio Yesu anataka akikuangalia anakuta upendo,furaha,amani,uvumilivu,n.k,sasa basi ili ufikie hatua ya kuitwa fungu la tatu lazima ujaze moyo wako mafungu sita ambayo ni( tunda la roho Ebrania 16;22,Roho saba Isaya 11:2huduma 5 efeso8;12,Karama tisa, mitume kumi na wawili na maneno saba yenye nguvu msalabani,ukiviwek

 16. Huyu Askofu ni lazima aseme hivyo kwa sababu toka utoto wake amekuwa akilishwa hizo dogma za kikatoliki. Kwa vyovyote vile ni lazima atetee hizo dogma na statues zake. Swali la msingi la kumuuliza huyu Askofu ni hili kwamba kipi kinacho-reflect zaidi maisha na kazi za Yesu alizizofanya hapa duniani katika mwili huu wa nyama- ni hizo statues au maandiko ndani ya biblia? Na je kama kweli hawaabudu hizo sanamu (statues), ni kwa nini wanapiga magoti kwenye statue ya bikira Maria?

 17. nawahurumia huruma sana nyie wachangiaji. nyie wenyewe mnaabudu katika roho na kweli au ni mafarisayo mamboleo? take care

 18. Tatizo ni kuwa unahamishia imani yako yote kwenye hivyo visanamu. Mungu tunaona toka mwanzo alikataa kabisa hili. Mifano ni wana wa Israel walipotoka Misri, Musa alikuwa akiongea na Mungu na kuwajulisha na kuwaongoza, lakini alipoitwa mlimani siku 40 tayari wakabadili ibada kutoka kumuabudu Mungu wa kweli na kusema kile kinyago cha mbuzi ya dhahabu ndio Mungu wao. Mahali kwingi tuanaona ktk Biblia jinsi walivyoasi kwa kuweka masanamu ya baali na miungu wengineo kisha kuwafukizia uvumba na kuwasujudia. Huu uasi mara nyingi unatokea iwapo wanajiona uwepo wa Mungu haupo ndani yao hivyo kutafuta Mungu anayeonekana kwa macho ya mwili na kumwabudu. Kama unamwamini Mungu na anaonekana ktk maisha yako wewe mwenyewe unatembea naye daima, unaongea naye, ukimuinua anakuinua, ukimpenda anakuonyesha upendo wake zaidi, ukianguka anakuonya huna haja ya kubeba kinyago au kusimama mbele ya sanamu usikiwe kwani hazioni wala kusikia. Jamani hebu mjikague ndani hasa ya mioyo yenu mnamkosea Mungu na wakati ni huu anasema nanyi acheni hizo ibada zinamchukiza.

 19. Jamani ni kweli kabisa,badala ya kumwabudu Mungu ktk roho wamekazana kuiangalia statue ya Yesu! kuomba mpaka wapange vistatue vyao ndio maombi yanaanza,utakuta mtu haombi hata siku moja lakini shingoni ana rozari, Yesu alisema waniabuduo halisi wataniabudu ktk Roho na kweli.

 20. Kweli kekundu. Wakristo hasa wakatoriki mwayasomaje maandiko? Mwandishi wa makala kanukuu vizuri kutoka 20:4. Ukilielewa andiko hili litakuweka Huru. Lwanga Kekundu…

 21. Nafurahi askfu kutoa ufafanuzi wengi wanahukumu wakati siyo wakatoliki. Ujumbe umewafikia.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s