Mchungaji atamka dawa ya mashoga na wasagaji ni kuuawa!!

Mchungaji Charles L. Worley wa Providence Road Baptist Church, North Carolina, amezua gumzo baada ya video yake kusambaa mtandaoni akielezea jinsi ya kufanya kutatua tatizo la mashoga kwenye jamii…wawekwe kwenye uzio wa umeme waachwe mpaka kufa”

“Build a great, big, large fence — 150 or 100 mile long — put all the lesbians in there,” do the same thing for the queers and the homosexuals and have that fence electrified so they can’t get out…and you know what, in a few years, they’ll die out…do you know why? They can’t reproduce!”

Kweli hata kama hatupendi kuona mashoga na wasagaji wakiendelea na vitendo hivyo, Hii kauli ya mchungaji si sahihi kutumika. Dawa pekee ya kuuwa dhambi ni kumpokea Bwana Yesu Kristo. Article Here!

Advertisements

25 thoughts on “Mchungaji atamka dawa ya mashoga na wasagaji ni kuuawa!!

 1. Mpendwa Haule,
  Nimefurahi kukusikia, ninaamini mkono wa Bwana ungali unakushikilia katika upendo wake!
  Bwana azidi kukutia nguvu!!

 2. Kwa kwel itumekula na kunywa , nimebarikiwa nanyi nyote niseme Bwana amejisazia vyombo vya kutosha(,watumishi wake) pamoja na changamoto na yale yote yalyojilii .Asante watumishi Millinga,Haggai,Lwembe na wote waliochangia Mpendwa Lwembe wivu wa Bwana unakutafuna…, ndio… endelea kukamatia hapo hapo, ,Millinga Bwana akubariki/kukutunza,kazi zenu si bure ni faida tupu.

  Ndugu zangu Mpendwao na Bwana wetu Yesu Kristo, nyakati hizi za mwisho ni za hatari(2Timotheo3) tusienende ktk utauwa ili hali tikizikana nguvu zake. tuenende kwa hekima na maarifa ili ,Maandiko yasije yakatimia kwangu/kwenu Tuwe hodari ktk Bwana na uweza na nguvu zake….. , tusimame imara siku ile ya uovu tukiwa tumevaa silaha zake Bwana…. kweli,haki,utayari,imani,wokovu na neno la Mungu ili kuzipinga ila zake mtawala wa ufalme wa anga,tamaa za mwili na mawazo yake,tusiwe wana wa ghadhabu….,tukemee injili ya ushoga kwa nguvu zote

  Na Mungu wa amani Atatutakasa kabisa roho/nafsi/mwili ili tusiwe na lawama siku ile ajapo Bwana ili tuingie mji ule wa Mbinguni kwa kupitia malango yake na tukiuendea ule mti wa uzima tukiwa tumeoshwa mavazi yetu kwa damu ya mwana kondoo.

  Bwana awatunze watumishi.

  Amen

 3. Kumbukeni kilichoisababisha sodoma na Gomora ichomwe iliki ni pamoja na huu uovu wa wasenge mashoga na wafirwaji na wafiraji pamoja na wasagaji au wanawake wanaojichezea kutimiza haja zao. Huyu pastor anaongea kama angekuwa na uwezo angeomba sheria ipitishe wawatenga watu wa aina hii ili waone kama watazaana na jibu lake ni kwamba watakufa wala hawataongezeka maana hawana uwezo wa kuzaana watu wa jinsia moja yupo sahihi sana tuache kuleta huruma za kibinadamu ziletazo mauti.

 4. Ndugu Hagai
  Kwanza nikushukuru kwa mchango wako na maswali yake. Pili napenda niseme kuwa majibu nitakayoyatoa nimeyaegemeza katika Biblia, kama tulivyoletewa na kama Kristo alivyoithibitisha kuwa hakuna kilichopitwa na wakati, isipokuwa Neema yake ndiyo inayotupitisha juu ya Sheria, si kwa kuzivunja bali kwa kuzitimiza!

  Katika kuyajibu maswali yako, kwanza ni vizuri tukaelewa kuwa Wokovu si mpango wetu, bali ni wa Mungu, naye ndiye Muasisi wa Wokovu. Hakuna mtu aliyejipangia jinsi ya kuokoka. Kwa hiyo Wokovu ni kwa nani, hilo liko mikononi mwa Mungu mwenyewe na si wanadamu. Ndio maana Kristo anasema mtu haji kwangu asipovutwa na Baba.

  Katika kukujibu swali lako la kwanza, umeandika hivi: “Injili ni Habari Njema ya Wokovu kwa watu wote, je Habari hii njema inamlenga nani-mwenye dhambi au asiye na dhambi?” Jibu ni kwamba Injili ni habari njema kwa wote, pamoja na Kaini, lakini wokovu ni kwa ukoo wa Seth! Yachunguze Maandiko ukifika katika kuelewa “PREDESTINATION” basi usemi nilioutumia hapo utauelewa vizuri zaidi. Ndio maana kuna wanaopofushwa wasione, wengine wanatiwa uziwi wasisikie, wakisikia wasielewe nk. yote ni katika kuulinda ule Mti wa Uzima!

  Swali 2. Kama inamlenga mwenye dhambi apate kuokolewa, je inaokoa baadhi ya dhambi tu na zingine kama za mashoga si ruhusa kuokolewa na Injili hii?
  Jibu: Mashoga, mimi na wewe si rahisi kuwajua kwa kutumia akili zetu, tunapaswa kufuata kile anachotuongoza yeye mwenye kuwajua. Tukianza kufuata maoni ya ulimwengu na huruma zao, nadhani tutakuwa tunamkosea Mungu. Licha ya kwamba Mungu ni mwenye Huruma lakini ni mwenye ghadhabu pia. Yuda 4 inazungumzia watu walioandikiwa TOKA ZAMANI hukumu. Sasa huwezi kuwa mtu wa zamani halafu ukawepo leo! Basi hayo wapaswa kuyachukua kiroho ndipo waweza kuyaelewa na yakakusaidia katika mwendo wako wa wokovu ili usije ukamhuzunisha Roho Mt kwa kujiunga na hao walioandikiwa Hukumu toka zamani! Kwa hiyo jifunze kumtazama Mungu katika anachosema na ubakie hapo hata ikibidi upingane na dunia nzima, au maisha yako yawe hatarini, na iwe hivyo!

  Swali 3. Mmoja wenu amesema kwamba sasa kanisa linaruka na bawa moja tu la Agano Jipya na kulisahau bawa lingine la Agano la Kale, Je kwa nini kipindi hiki kanisa halitoi sadaka za kutekeza kama wanyama n.k kama ilivyokuwa hapa kwenye Agano la Kale?
  Jibu: Sikusema kanisa limesahau bawa la Agano la Kale, la, nimesema limevunjwa! Kwa hiyo kanisa litafia hapa chini na mashoga wake linaochukuliana nao!! Sadaka iliyotolewa katika Agano jipya ilikuwa ikizikamilisha sadaka zote zilizotolewa kama dhabihu za dhambi ambazo zilizifunika tu dhambi. Ndio maana watakatifu wa Agano la Kale, hakuna aliyeingia Mbinguni mpaka ilipotolewa hiyo yenye kuwaondolea dhambi. Kazi ya Roho Mtakatifu ni kukuleta katika ufahamu kamili wa nini kilichofanyika na kiliwakilisha nini, na sasa uko wapi. Ndio maana Maandiko yanatuambia kuwa ijapo ya KAMILI ile ya SEHEMU huachia, ila mpaka uyajue hayo, vinginevyo hayatakusaidia. Agano Jipya limejengwa juu ya Msingi wa Torati!

  Kwa swali la nne na la tano, nitaomba nikujibu kwa pamoja. Kwanza mimi si kigezo cha jinsi ya kuokoka, wala mtu yeyote yule. Kigezo cha Wokovu ni Neno la Mungu, Je, unalipenda kwa moyo wako wote na nguvu zako zote? Basi kwa uchache waweza kuupima wokovu wako katika jinsi hiyo. Ndipo hebu tuyatazame sote Maandiko haya ili tujionee wenyewe katika nafsi zetu iwapo huo wokovu tunaosema tunawapelekea mashoga au yeyote aliyelaaniwa, inaendana na Biblia au ni akili zetu tu katika kuyaona mapungufu ya Mungu!?
  1. Kum 23: 17 “ Pasiwe na kahaba katika binti za Israeli wala pasiwe na hanithi (sodomite) katika wana wa Israeli wanaume”
  2. Law 18 : 22 “Usilale na mwanamume mfano wa kulala na mwanamke; ni machukizo”
  3. 2Fal 23 : 7 “ Akaziangusha nyumba za mahanithi, waliokuwamo nyumbani mwa Bwana, …”

  Swali ambalo nigependa niwaulize ndugu zangu Milinga na Hagai : Je, mnafahamu kwamba Israeli ni mfano wa Kanisa? Kama hamfahamu basi sina la zaidi. Lakini kama mnafahamu hivyo, Maandiko yanaposema pasiwe na shoga kati yenu, nanyi mkiwa ndilo Kanisa mnaelewaje jambo hilo?? Au ndio mambo hayo ni ya Agano la Kale, na sasa kwenu ninyi ni Ruksa?? Kwani hao walioziangusha nyumba za mashoga na kuwafukuzilia mbali, wasingeweza kuwakanya au kuwatolea sadaka hekaluni, wakasamehewa? Wao walijua kuwa Mungu akiisha kukulaani ndio basi tena, hakuna Injili ya wokovu itakayokusaidia, kwa hiyo walijua nini cha kufanya kama Mungu mwenyewe alivyowaamuru, hawakuhangaika kuwaokokoa watu wasioweza kuokolewa! Kwani Kristo aliposhuka kuzimu akawahubiri Injili, kuna aliye Okoka??

  Ndio maana Maandiko yanasema wazi kuwa ukitembea kimwili hutayajua ya rohoni! Labda niwaulize kwa mara ya pili; Hivi mtume Paulo alipowabandikia bango mashoga kuwa hawataurithi Ufalme wa Mungu alikuwa hajui kuhubiri wokovu kama mnavyojua ninyi leo hii? Mungu ndiye anayejua wa kuokoka na wa kupotea. Msipende kujituma kazi kwa hisia, mnaweza kujikuta mmeungana na mashoga na mwishowe kuwakaribisha kundini kama walivyofanya wenzenu Walutheri na Waanglikana na madhehebu mengineyo, hiyo ndiyo nguvu ya Masonic Gospel, inatumia sana akili badala Ufunuo wa Neno!

  Hebu someni kitabu cha Waamuzi 19 : 22 na kuendelea mjionee wenyewe mabaradhuli walivyouletea balaa ukoo wa Benjamini, kama ambavyo wanao ushabikia ushoga kwa kumfanya Mungu mkatili wanavyojipalilia mabalaa!

  Neno linasema wafukuzeni, asiwepo shoga kati yenu. Tena linawaambia ninyi mnaojidanganya kuwa eti mtawahubiria mashoga waokoke kuwa hao mnaohangaika nao, “HAWATA URITHI UFALME WA MUNGU” nanyi mnavyojaribu kung’ang’aniza kuwaokoa, angalieni msije mkajumuishwa nao kwa kupewa roho za kuamini uongo mlioufuata badala ya Neno la Mungu alilowawekeeni WAZI, yakawapata ya Waanglikani na wengineo waliojiingiza upotevuni kwa akili zao!

  Wokovu ni kutenganishwa na ulimwengu, yaani Mapokeo. Kwa kujichanganya na Mapokeo, kanisa limebaki katika kundi la Lutu kwa kuikataa Injili yote. Hata mambo haya ya kuwafukuza mashoga yamekuwa mageni kwao; kwanini? Wameukataa Ubatizo wa Ondoleo la Dhambi (Mdo 2:38, ubatizo wa maji mengi, kwa Jina la Bwana Yesu Kristo), wamejiridhisha na ‘wokovu wa Lutu’!

  Ndugu zangu, kazi ya kuokoa roho ni ya Mungu naye ndiye pekee anayezijua roho alizozifuata ili aziokoe. Kwa hiyo si vyema kulazimisha mambo, mafungu ya watu yako matatu tu. Ni vizuri kuyajua hayo ili usijisumbue nafsi yako katika jambo lisilo na tija. Yaangalie haya makundi yanavyojieleza wazi wazi: Kundi la kwanza ni la ABRAHAMU. Hili ndilo kundi lenye Ahadi ya Wokovu. Hawa huuifurahia Injili! Kundi la pili ni la LUTU. Hawa ni lukewarm, si baridi, si moto. Hawa licha ya kwamba wanajua ushoga ni dhambi na hawapendezwi nao, lakini huchukuliana nao. Mambo yaliyomfika Lutu sote twayajua! Kundi la tatu ni WANASODOMA, ambao ndio dunia yote. Hao ndio wanaokwenda kuijaza dunia na ndio wenye kuzishikilia nyenzo zote kiutawala katika maana ya kiuchumi. Basi kama mnavyoliona wimbi la kuhalalisha ushoga linavyofanikiwa kwa msaada wa akina LUTU, pale wanapochukuliana nao, mapishi ndiyo yanakolea, si muda mrefu GHADHABU YA MUNGU ITAPAKULIWA!!

  Bwana aliponye bawa mlilovunjwa!

 5. Wapendwa watazamaji na wasomaji wa SG, nadhani tumeongea sana peke yetu mimi na Lwembe kuhusu mada hii, naomba tujipe break kidogo ili tuwape nafasi wengine waongee. Hii meza ya duara naona mimi na Lwembe tumeongea sana. Kama nikuelewa maandiko tumeelewa au siyo? Lwembe ametoa maandiko mengi kuhus mada hii, nami pia nimeeleza ninavyoelewa na wengine pia wamechangia.

  Naomba nirudishe usukani kwa wasimamizi wa kipindi hiki hasa Mhariri wa SG aendelee.

  Nawatakia usiku mwema nakuwataka wote tunaochukia ushoga tusilegeze kamba. Ni matumaini yangu kwamba watanzania wote watapingana na roho ya ushoga hadi kieleweke. Tukutane tena katika mada NYINGINE zinazoenelea au unasemaje mtumishi wa Bwana?

 6. Mpendwa Milinga,
  Kwanza, angalau kwa kauli yako ndugu Milinga, umenithibitishia kile nilichokua nakitilia shaka; kuwa huwajui mashoga, si kwa mitaani tu, bali hata katika Maandiko! Pia, kwa taarifa yako, Hukumu inaendelea hata sasa hivi, labda Adhabu ndiyo inayosubiri huko kiyama. Mungu hata uhukumu ulimwengu kwa mawazo yetu au mafundisho yetu, bali kwa Neno lake. Kwa hiyo unapokutana na Neno lake, usipolitii unakuwa tayari umehukumiwa. Kama unavyolikiri Neno lake na kupata wokovu, ndivyo unapolikataa unavyo hukumiwa. Kwa hiyo suala la hukumu si la kesho, bali ni la leo leo!

  Unasema kuwa, “Huwezi kuwatenganisha hapa duniani? HAIWEZEKANI HADI SIKU YA KIYAMA.” Hili ni wazo finyu linalojaribu kuichukua ile kauli ya “kuviacha vikue pamoja” na kuyajumuisha mambo yote yanayohusiana na uchafu na kuyalazimisha yakubalike katika jamii kinyume na Maandiko. Yawezekana ni katika uchanga, unayachanganya hivyo, au katika hila, ambavyo ni mbaya zaidi, lakini ukweli ni kwamba Mungu amekuwa akitenganisha tangu kule Mwanzo! Yeye daima ametenganisha Nuru na Giza, na hajawahi kuvichanganya! Hata hivyo vilivyoachwa vikue pamoja, ni katika kuvileta katika ukomavu tu, lakini katika kuvitenganisha yeye alikwisha vitenga pale alipoviona! Kwa hiyo Neno linaendelea kutenganisha hata leo hii, ambayo ndiyo Hukumu yenyewe, nalo Neno likiwa ndani ya muaminio huifanya hiyo Hukumu! Kama mchungaji alivyoyatikisa manyigu kwa Hukumu!

  Hata Kanisa, ni watu walioitwa watoke katika jamii isiyomcha Mungu, kama hao mashoga, ambao Mungu anawaacha waangamie, hao walioandikiwa tangu zamani Hukumu, kwani ni watu wasioweza kuokolewa! Nilijaribu kukupa maelezo ambayo yangekuonesha ushoga ni kitu gani, lakini kwa bahati mbaya hujaweza kufika katika uelewa huo. Pia nilijaribu kukuonesha jinsi serikali nyingi duniani zisivyoukubali ushoga na hutoa adhabu kali kwa watu wa jinsi hiyo, pamoja na serikali yetu, ndio maana ilimfunga jela yule kasisi wa Kikatoliki aliyekamatwa na JAMII pale Chuo Kikuu Dsm akiwa katika ufuska huo! Kama watu wa mwilini wanawaona hao ni chukizo, halafu wewe na Biblia yako mkononi, unasimama bila ya aibu na kuzilaani serikali zinazowafunga, sijui Mungu unamuonaje!

  Je, haujasoma hapo mnapoambiwa TOKENI KATIKATI YAO? Unajua Maandiko yako kiroho zaidi kuliko kimwili, basi jibidiishe kwa utulivu! Usiwe na one track of mind, nadhani hii ndiyo inayokusumbua, unashindwa kupata spiritual context ya Maandiko, na kubakia na ile ya kimwili ambayo sio extensive.

  Mungu ndiye anayelitenga Kanisa lake. Mwangalie Ibrahim aliye mfano wa kanisa kwa kuitwa kwake atoke kati ya nduguze. Alipoambiwa atoke yeye alimchukua na Lutu akaambatana naye wakati Mungu hakumuagiza hivyo. Na kwa kujiambatanisha na Lutu, kama ambavyo kanisa linavyojiambatanisha na mashoga, baraka hazikumjia mpaka alipotenganishwa naye, licha ya kwamba alikuwa na ahadi. Pia jiulize, kwanini Lutu hakuenda kwa mjomba wake Ibrahim alipotolewa Sodoma siku ulipochomwa moto? Tunawaona watu wa mabondeni wakihifadhiwa na ndugu zao katika nyakati za shida za mafuriko, hata tumemuona Ibrahim akiondoka na nyumba yake kwenda kupigana ili kumkomboa Lutu baada ya Sodoma kutekwa. Kulikoni Lutu akiwa yeye na bintize tu, katika hali ile ya kupoteza vyote, hakwenda kwa mjomba wake na badala yake kaenda kujibanza maporini? Mungu AKITENGANISHA, hakuna akili, wala hekima, wala hila, wala maarifa yanayoweza kuunganisha tena!!

  Unasema, “Halafu jambo lingine linalonishangaza, ni kwa jinsi gani watu wameshupalia swala la mashoga kana kwamba ni umati wa watu wanaotishia uhai wa dunia.” Ni kweli yaonekana hivyo unapoyatazama mambo hayo katika hilo jicho la mwilini. Lakini hakuna anayeshupalia jambo hilo la mashoga bali mashoga wenyewe na washirika wao wanaohubiri “Injili ya Upendo kwa Mashoga” ile ya New World Order ambayo in principle ni Masonic, inayopingana na Injili ya Kristo! Hawa wahubiri wa Injili hizi mbili, ndio “wanaoachwa wakue pamoja”, yaani leo, wote wawili wapo uwanjani!

  Kuhusu mashoga hapa Tanzania, officially, tutakapokubaliana na hiyo injili ya masonic ya upendo, utawaona watakavyojimwaga barabarani wakisherehekea “Ushindi”. Lakini ukitaka kuwaona kwa siku hizi, wametapakaa katika manightclub yote. Zamani, mashoga waswahili ungewakuta kwa wingi pale Safari Bar Kariakoo, tena ukiingia tu wanakugombea bila aibu kuliko hata ma barmaids, ukienda chooni wanakufuata wawili watatu, kama ni mgeni unaweza kupiga kelele ukadhania wezi, kitakacho kushangaza ni kule kujinyorombosha kwao! Mashoga wa kihindi ungewakuta Zanzibar Hotel mtaa wa Zanaki, Georges Grill na Mawenzi Hotel. Wazungu Motel Agip na Oysterbay Hotel. Hao ni wale mashoga wa biashara kama makahaba wa kike unaowakuta Skyway, Maggot na sehemu nyinginezo. Kwa siku hizi magomeni kwa Macheni utawakuta sampuli zote mbili!!! Amerika (USA) takwimu za mwaka 1959 zilionesha ongezeko la 20%, kwa leo ongezeko hilo unaweza kuliona jinsi yake katika hako kasehemu kadogo ka nchi hapo walipoandamana, yaani hao ni ka tip ka iceberg la mashoga katika jamii hiyo!

  Pia nimeona unazungumzia kuwapo kwa makundi mawili kanisani ambayo unasema hayatenganishwi. Jambo hilo ni kweli kwa kadiri unavyolielewa kimwili, lakini kiroho Mungu amewatenganisha tayari, ila hili kundi la mwilini ni kipofu lisiloweza kujua mambo ya Rohoni, maana wao huzungumzia dini katika maana ya Kanisa! Nayo maana ya Kanisa ni walioitwa watoke. Basi kama wapo waliojiingiza kwa siri, hao walioandikiwa tangu zamani Hukumu, kwa Neno hao hujulikana licha ya kujificha!

  Maswali yako mengine Milinga, nadhani nilikwisha kukujibu. Hayo ya ujenzi wa fence na mambo yake, nilikuambia mambo ya Mungu kwa leo ni ya kiroho na si kimwili. Miili yetu inatiishwa kulingana na kile kilicho ndani yetu kiroho. Kwa hiyo unapozungumzia ujenzi, physical, wa hiyo fence, uelewa wako unakuwa uko chini kuliko hao mashoga walioielewa hiyo kauli kiroho! Wao ni wa kiroho kuliko unavyodhania, wanajua mchungaji kasema nini, nao katika umoja wao wamejua cha kumjibu, kiroho! Hii si vita ya mwilini!!! Ndio maana nikasema mbona mnakuwa kama watoto wachanga, juu ya wokovu mnaoukiri, kweli hamjui ni nini kinachoendelea?!

  Mimi nawashangaa sana, hivi katika mkasa kama huu, unaweza kweli ukaanza kuishughulisha akili yako ukiiwazia hiyo fence itakavyokuwa, sijui itajengwa kwa kokoto za Msolwa au ubuyu wa Kigamboni au nguzo zitakuwaje, sijui itagharimu shilingi ngapi, na mambo ya mwilini ya jinsi hiyo! Hivi, hata ukiweka huo umeme, kwani hawawezi kuchimba chini na kutokea upande wa pili nje ya fence??? Kwani kuzimu wamefungiwa na nini? NENO!!!! Na kuzimu iliyopo hapa juu ya nchi nayo imefungiwa kwa Neno licha ya kuwaona wanavyozurura, nayo kauli aliyoitoa mchungaji inaendana na ukweli huo, akiwafukuzia mbali kutoka kusanyiko lake. Wewe kama umewaona wazinzi kwa macho yako ya mwilini na hawajatimuliwa humo kusanyikoni mwenu, hicho ni kigezo tosha kukuonesha kuwa kusanyiko hilo haliko chini ya uongozi wa Roho Mt., maana yeye hulisafisha kusanyiko kwa kuwafukuza wote watendao maovu, akiwatenganisha!

  Changamka ndugu yangu Milinga, acha kulala, Mbinguni hakuna kitanda!!

 7. Mpendwa Kinyau Haggai,

  Asante kwa kuungana nasi katika mjadala huu ambao wengi wametuachia sisi wawili tuundeleze. Nashukuru kwamba umetongezea nguvu ya majadiliano kwenye meza hii ya SG.

  Mimi hadi kesho nitakachopinga ni hoja hii ya kujenga fence yenye ukubwa wa kilomita za mraba au mduara zipatazo 241.4016 au sawa na Maili 150 kisha kuwakamata waitwao mashoga na kwapakia ndani ya magari na kuwapeleka kwenye uwanja huo na kuanza kuwalisha kwa kutumia ndege angani.

  Unajua mahubiri kama haya naona kama ni yale ya kutafutia ujiko au umaarufu. Mhubiri anayedandia hoja za wanasiasa na kuanza kuzihubiri baada ya wanasiasa kutoa tamko fulani mimi humhesabu kama aliyeishiwa cha kuhubiri.

  Hivi kujenga uwanja wenye urefu wa Kilomita za mraba 241.4016 unajua ni eneo kubwa eti. Ni zaidi ya mkoa wote wa Dar es salaam na Pwani.

  Halafu zoezi la kuwakama hao mashoga litaendeshwa na nani? Askari wa UN au AU au jeshi la nchi gani. Halafu utawakamata kwa kutumia sheria gani ya bunge? Utatumia Biblia au Qorani? Utatumia kigezo gani kuthibitishia umma kwamba hao unaowakamata na kuwapakiza ndani ya karandinga ni mashoga? (What criteria will be used to capture them?)

  Ili mahubiri hayo yatekelezeke, Utalazimika kupeleka mswada wa sheria bungeni sijui bunge la Congress au House of the Commons au Dodoma sijui ili mswada huo wa kuwaswaga mashoga kama ngombe waondoke ndani ya jamii upitishwe na bunge. Sheria hiyo itaanzisha Mamlaka kama ilivyo TRA, SUMATRA au EWURA ili mamlaka hiyo ndiyo ifanye kazi ya kuwakamata nyumba hadi nyumba na mtaa kwa mtaa na mkoa kwa mkoa. Kisha wote wapakizwe ndani ya karandinga kama lile la Polisi wa magereza wote ndani kuelekea uwanja wa upweke yaani “MASHOGA STADIUM” kule ndani ya poli la wapi sijui.

  Naomba niseme kwamba haya mafundisho hayatekelezeki. Wanaoyaunga mkono kama Mpendwa CK Lwembe nawahurumia kwamba wanaunga mkono “Non-implementable doctrines”. Mafundisho yasiyoweza kutekelezeka hata kidogo hadi watakaposhuka Malaika wa Vita toka Mbinguni wakiruhusiwa na Mungu.

  Nategemea Lwembe atajibu badhi ya hoja za Kinyau na za kwangu ili meza hii ya majadiliano ifike mwisho wa kipindi.

 8. Wapendwa CK Lwembe na Millinga,

  Nimefuatilia kwa shauku kubwa sana mjadala huu. Labda kwa faida yangu na watu wengine, naomba kujibiwa kwa kifupi tu maswali yafuatayo ili kuweza kuupanua mjadala huu;

  1. Injili ni Habari Njema ya Wokovu kwa watu wote, je Habari hii njema inamlenga nani-mwenye dhambi au asiye na dhambi?

  2. Kama inamlenga mwenye dhambi apate kuokolewa, je inaokoa baadhi ya dhambi tu na zingine kama za mashoga si ruhusa kuokolewa na Injili hii?

  3. Mmoja wenu amesema kwamba sasa kanisa linaruka na bawa moja tu la Agano Jipya na kulisahau bawa lingine la Agano la Kale, Je kwa nini kipindi hiki kanisa halitoi sadaka za kutekeza kama wanyama n.k kama ilivyokuwa hapa kwenye Agano la Kale?

  4. Je Yesu Kristo alipokufa pale msalabani, alikufa kwa ajili ya baadhi ya dhambi na hakufa pia kwa ajili ya kusamehewa kwa dhambi ya ushoga?

  5. Je hivi leo shoga akiamua kwa dhati kumpokea Yesu kama Bwana na Mwokozi wake, kama ambavyo wewe CK Lwembe na Millinga mliamua, Je Mungu hatamsamehe mtu huyo na kumfanya aishi maisha matakatifu? Je Mungu amekuwa mmbaguzi kiasi hicho?

  Ushoga ni mbaya sana katika jamii lakini ni dhambi kama ilivyo dhambi zingine na kwa Mungu hukumu yake ni moja tu, asiyeacha matendo hayo mpaka kufa kwake, sehemu yake ni kwenye lile ziwa liwakalo moto sawa sawa na yule mwizi aliyeiba kuku au aliyeiba mabilioni ya hela ya serikali au kahaba au mtenda dhambi yoyote. Dawa ya dhambi yoyote ni moja tu yaani TOBA. Sijaona mahali popote kwenye biblia palipoandikwa dhambi fulani na fulani hazisameheki isipokuwa ile tu ya kumkufuru Roho Mtakatifu. Sasa sielewi labda ushoga ni dhambi ya kumkufuru Roho wa Mungu hivyo haiwezi kusameheka mbele za Mungu, naomba Lwembe atufafanulie hilo.

 9. Mpendwa Lwembe,

  Hauko mbali na kile ninachoamini na kueleza hapa. Nimesema awali kwamba hatuwezi kuwacharaza bakora watu waitwao mashoga katika jamii hii ya sasa. Nikasema tena kwamba hukumu itafanywa na Mungu mwenyewe kama ulivyonukuu maandiko ya Ezekieli Nabii. Maandiko yanaposema hukumu itaanzia katika nyumba ya Mungu, ina maana kwamba hadi siku ya kiyama, kanisani watakuwemo watu wa aina mbili: 1. watakatifu, 2. Waovu. Huwezi kuwatenganisha hapa duniani? HAIWEZEKANI HADI SIKU YA KIYAMA. Waovu ikiwa ni pamoja na Mashoga wataendelea kuhukumiwa dhamiri zao kwa mahubiri yenye uvuvio wa Roho Mtakatifu, ili uovu ujitenge na utakatifu, lakini haitakuwa Kibiblia kuwatenga kimwili na jamii pana ukasema eti umeagizwa na Mungu uisafishe jamii kwa njia hiyo. Maandiko yanasema, “Watakatifu walioko duniani ndio walio bora, ndio Mungu anaopendezwa nao”. Ili watakatifu wawepo lazima waovu wawepo. Utawatenganisha kwa matunda yao tu. Au maandiko haya umeyasahau. Watakatifu watajulikana kwa Matendo yao mema na uadilifu wawapo katika jamii mbovu na ovu. Waasi na waovu nao pia utawatambua kwa matendo yao wawapo katika jamii siyo kwa kuwatenga pekee yao. Utenganishwaji utafanywa siku ya hukumu ya mwisho na wala siyo sasa. Mungu hajatutuma kwenda kufanya kazi ya kutenganisha waovu miongoni mwa watakatifu. Acha vyote vikue pamoja.

  Haya makundi mawili hapa duniani , there is no way you can seperate them until the end of the world order. Wewe unajichanganya sometimes. Upande mmoja unasema waovu (mashoga) watengwe au tuseme wapigwe bakora watoke katika jamii wasituharibie kizazi chetu na watoto wetu mara unatoa maandiko yanayoonesha kwamba hukumu itaanzia nyumbani mwa Mungu. Sasa hukumu itaanzia nyumbani mwa Mungu kwa sababu gani?

  Hivi Yesu aliposema acheni ngano na magugu vikue pamoja alimaanisha nini tunapojadiliana mada kama hii? Anaposema atabagua kondoo na mbuzi wewe unaelewaje mpendwa? Unataka kazi hii ianze sasa hivi au tusubiri siku ya hukumu ijayo ya Mungu mwenyewe?

  Halafu jambo lingine linalonishangaza, ni kwa jinsi gani watu wameshupalia swala la mashoga kana kwamba ni umati wa watu wanaotishia uhai wa dunia. Sehemu fulani Lwembe umesema kwamba hawa jamaa ni kundi linalokua kama nimekunukuu sawasawa umesema hivi, “……. Ushoga unatengeneza kajamii ka watu wa jinsi hiyo ndani ya jamii, nako kajamii hako hukua kwa kuwaingiza wafuasi wapya na kuwanyemelea watoto wadogo kama unavyowaona makasisi wa Kikatoliki wanavyoshutumiwa na mapesa wanayoyalipa kama fidia kwa mambo hayo, na mwishowe huwa mtandao mkubwa unaozimeza jamii ongofu kama ilivyokuwa huko Sodoma na Gomora!……”

  Mimi napenda nikuulize ukiwa unatembea mitaani kwako hapo unapoishi unaweza kukutana na mashoga wangapi kwa siku moja. Au hapo ulipo kwa sasa unawajua mashoga wangapi waliopo? Mimi kwa sasa niko mkoani Kigoma Tanzania, nina miaka 2 hapa mjini. Nimetembea wilaya zote za Mkoa huu. Kabla sijaja mkoa huu wa Kigoma nilikuwa naishi Mwanza. Nimetembea mikoa yote ya kanda ya ziwa na Wilaya zake zote hadi vitongoji vyake. Mkoani Dodoma nimeishi kwa muda wa miaka 2. Dar es salaam nimeishi tangu 1999 hadi 2006. Nimeishi Magomeni Mapipa na Kigamboni. Katika mikoa ya Tanzania bara nadhani nimebakiza mikoa 3 tu ndiyo sijawahi kutembelea. KATIKA MAENEO YOTE HAYO SIJAWAHI KUMWONA SHOGA. Kwanza siwaelewi mashoga wakoje na wana alama gani? Kwanza wanaishi wapi sijui. Hapa Tanzania mashoga nasikia wapo, lakini naapa kwa Mungu mimi sijawahi kuwaona. Lakini kusema ukweli katika maeneo hayo yote niliyowahi kuishi au kutembelea MAKAHABA NA MAJAMBAZI NA WEZI NIMEWAHI KUWAONA, LAKINI SIYO MASHOGA.

  Unaposema kwamba ni kundi kubwa wewe takwimu unazipata wapi? Nani aliyefanya sensa ya kuhesabu mashoga Tanzania au dunia nzima na ikaonekana ni kundi kubwa hata kuliko Makahaba na Wazinzi ambao wao hujaona kama ni sawa na wao watengwe na jamii?

  Hebu tazama ajabu nyingine, hapa Tanzania peke yake wagonjwa wanaoishi kwa kumeza dawa za ARVs ni zaidi ya Milioni 2. Kwa kuwa HIV inasambaa zaidi kwa ukahaba, je utanikubalia kwamba Tanzania kuna makahaba zaidi ya 2,000,000? Kwa kuwa HIV imesomba watu wengi kuelekea kaburini, kwa nini sasa mahubiri yetu hayajawahi kutoa pendekezo la kuwachoma moto au basi kuwatenga na jamii makahaba? Mbona mwazungumzia kundi moja tu katika makundi mengi ya watendao maovu? Huoni kwamba Injili hiyo imepinda au inabagua(bias)?.

  Hivi kundi la mashoga lina watu wangapi hadi liwe tishio kwa dunia au Tanzania? Halafu huo mradi wa kujenga fence kubwa namna hiyo nani ataugharimia? Ni serikali ya Marekani au Tanzania au UN, au NATO ? Hiyo gharama ya kuwalisha kwa kutumia ndege ya kudondosha vyakula nani ataibeba? Ardhi ya kujenga hiyo fence kubwa nani ataitoa? Au tutaenda mbuga za wanyama tuwaondoe wanyama wote kule Serengeti ili mashoga (kama wapo sijui) wote wakamwagwe kule? Mradi huo wa kuwatupa mbali mashoga wote utasimimamiwa na nani? Nchi gani? Rais gani? NGOs zipi? Kanisa lipi?

  Mpendwa Lwembe, maswali kama haya ndiyo yanayonifanya nisiikubali Injili yako na ya huyo pastor wako. Halafu, siyo kila Mchungaji anayesimama mimbarani anamwakilisha Mungu eti!!! Hata kama anao watu wanaomuunga mkono sana kwa mahaubiri yake. Siyo wote wanaohubiri Injili wanaihubiri kwa Roho na Kweli. Kila mtu anaweza kuhubiri Biblia lakini si kila mtu anaweza kuhubiri katika Roho na kweli.

  Ubarikiwe kwa kuelewa Injili ya kweli.

 10. Ndugu yangu,
   Unaniona nimetoka nje ya mada kwa mtazamo wako na wengi wamuonao mchungaji huyo amechemsha, ingawa sivyo. Msimamo wako ulio uandika kwa herufi kubwa unasema mengi kuliko uliyoyaandika! 

  Katika hiyo nukuu ya mchungaji,  ukimsikiliza katika ile clip, anasema hivi, yaani baada ya kuwafungia humo ndani ya fence, “Fly over and drop some food…” yaani hataki ushirika nao! Anataka wadondoshewe chakula kutoka kwenye ndege!!

  Nikirudi katika maelezo yako kwamba nimetoka nje ya mada, mimi naona wewe ndiye hujatambua kinachojadiliwa. Unanitaka nijadili kauli ya mchungaji, katika context ipi?kama context ya mashoga hutaki, je tuzungumzie fence? Yaani iwe ya makuti, au iweje? Au tumzungumzie mchungaji, katika lipi? Maana kauli aliyoitoa iliwahusu mashoga. Na fracas yote iliyofuatia pamoja na maandamano ya mashoga kumlaani mchungaji huyo na haya majadiliano tuliyonayo hapa katika blogu yanatuunganisha na makundi hayo; aidha kundi la mchungaji huyo ama la hao waandamanaji!! Sioni jinsi nyingine unayoweza kujiwakilisha katika suala hili.  Ni vizuri ukajua kwa uhakika kuwa: “there is NO drunk, sober man!”

  Pia ndugu yangu Milinga, nakuona una tatizo la kuchanganya mambo. Napenda kukuelewesha kuwa mchungaji anaposimama mimbarani, humuwakilisha Mungu. Kwa hiyo kauli anazozitoa hapo huzitoa katika kuwakilisha wazo la Mungu, nyumba ya Bwana ni sehemu ya masahihisho au Hukumu, na si mambo ya siasa. Kwa hiyo, sijui nani atajenga fence, au kuwakamata, hayo ni irrelevant! Halafu unaniambia nisiongelee mashoga au ushoga bali niongelee kauli ya mchungaji kama ina mashiko ya Kiroho! Yaani unategemea nifungue Marko 17:22 “Na mtawachukua mashoga na wasagaji muwatie katika fence ya umeme …” hapo ndipo utaona ni ya kiroho! Huyo mchungaji alikuwa kanisani waliko watu wa kiroho na waliomuelewa sitegemei atakuwepo wa “kuwapenda mashoga” katika namna ya jirani yako kiasi kwamba kwa upendo wako kwake, aanze kuandamana na watoto wako! Hakuna mwenye akili timamu anayeweza kuchukuliana na hao. Ukiona wanasiasa wanaanza kuyatambua makundi hayo yaliyolaaniwa, jua kuwa wameongezeka sana na sasa wanaweza kutumiwa katika kura! 

  Kwa hiyo, wakristo wanaoshabikia mashoga ni bora waende kwa huyu mchungaji akawahubiri Injili halisi iwaponye na ghadhabu ya Mungu inayosubiri kikombe kifurike, nadhani ni huku Afrika kwetu, hizi nchi za kishamba ndizo zinazochelewesha kikombe kujaa. Lakini kwa jinsi ninavyouona mjadala huu, nadhani tumesogea, hatuko mbali sana!!

  Hebu Milinga yaangalie haya Maandiko halafu itafute nafasi yako itakuwaje. Ezk 9:4 “Bwana akamwambia, pita kati ya mji, kati ya Yerusalem, ukatie alama katika vipaji vya nyuso vya watu wanaougua na kulia kwa sababu ya machukizo yote yanayofanyika kati yake.” Sasa ukiwa ni mwenye kuwahurumia mashoga katika jinsi ya kuwapa uhuru wa kuendeleza ufuska wao na kuiharibu jamii, nawe ukiwa ni mhubiri na kiongozi wa familia yako, bila shaka kundi lako lote litakuwa katika ushawishi wako na hivyo HALITA TIWA ALAMA! Basi endelea katika kifungu cha 5-6 “Na hao wengine aliwaambia, … mkapige; jicho lenu lisiachilie, wala msione huruma; waueni kabisa, mzee, na kijana, na msichana, na watoto wachanga, na wanawake; lakini msimkaribie mtu yeyote mwenye hiyo alama; tena anzeni katika patakatifu pangu. Basi, wakaanza kwa wazee waliokuwa mbele ya nyumba.” Basi ndugu yangu Milinga hivyo ndivyo hali itakavyokuwa, Hukumu inaanzia kanisani, nasi katika Strictly Gospel tukiwa ni kanisa nawe ukiwa ni ‘mzee’ katika huduma tuyategemee hayo!

  “Yesu Kristo ni yeye yule, jana, leo na hata milele”

  Mbarikiwe!

 11. Mtumishi,

  Mimi naona wewe unachotetea kiko nje ya mada. Mchungaji alichoeleza wewe sicho unachojadili. Hoja ya huyu mchungaji umeiacha na unajadili swala lingine. You are arguing out of topic context.

  Umejitahidi sana kujadili kwa kina na mifano na maandiko lakini unazidi kwenda nje ya mada hii. Hebu soma tena alichosema huyu mchungaji unayemuunga mkono matamushi yake,

  “Build a great, big, large fence — 150 or 100 mile long — put all the lesbians in there,” do the same thing for the queers and the homosexuals and have that fence electrified so they can’t get out…and you know what, in a few years, they’ll die out…do you know why? They can’t reproduce!”

  Malezo hayo wewe unayaelewaje? Hebu jadili hoja hii bila kwenda mbali sana. Hii hoja unaiona ina mashiko gani kiroho. Nani unamwambia ajenge hiyo “fence”? Ni serikali, kanisa, au mahakama? Ukishajenga hiyo fence, nani atafanya kazi ya kuwakata hao mashoga? Kwanza unaanzia wapi? Unatumia ushahidi gani ili kuwakamata au hadi wajitangaze?

  Hebu tujadili hoja hii na wala tusiwajadili mashoga na ushoga wao.

 12. Strictly Gospel,
  Shalom!
  Ninawashukuru kwa yote, pamoja na kujitoa kwenu katika kumtumikia Mungu katika njia hii mliyomo ambayo kwayo tumekuwa kusanyiko kubwa la kiroho! Bwana awazidishie Hekima yake!

  Baada ya hayo, napenda kuleta ombi, kwamba mtuwekee clip ya yale maandamano ya mashoga kuipinga kauli ya mchungaji, ili itusaidie kupata taswira nzima ya jambo hilo nao wachangiaji wapate mwanga zaidi!

  Nawashukuru kwa hilo na Bwana awabariki katika yote myafanyayo yenye kumtukuza yeye!

 13. Ndugu yangu Millinga,
  Ni kweli nilikuwa sijakuelewa, wakati wote nilidhani umevaa Macho ya Mungu ndiyo unayoyatazamia suala hili la Ushoga, ndio maana umeona naishangaa hiyo injili. Lakini sasa nimekupata sawa sawa, kumbe unahubiri “wokovu” katika version ya New World Order, ambayo inamuona Mungu ni katili sana kwa ushahidi wa Agano la Kale, lakini amejirudi katika Agano Jipya na sasa anawapenda wooote!

  Hii ni Injili nzuri inayowaleta watu pamoja na matokeo ya Injili hiyo ndio hao maaskofu mashoga na waumini mashoga, wote wakiwa officially accepted ndani ya kanisa, Injili mpya ya Upendo! No wonder mchangiaji mmoja kwa uchungu wa kubaguliwa mashoga, akimlaani mchungaji akasema huenda na mtoto wa mchungaji huyo aweza kuwamo kwenye ushoga. Asilolijua ni kwamba kwa kuutetea ushoga Mungu alisema anavipatiliza vizazi vya hao, hadi cha nne, nadhani hajayaelewa Maandiko vizuri kuwa anaweza kuwa amejiletea balaa juu yake na kizazi chake kwa kumtania Mungu!!!

  Ukristo, ni kama hua au tai, huruka juu ya mambo haya ya mwilini na kuyaendea yaliyo juu mbinguni katika ulimwengu wa Roho. Huko ndiko unayakuta mambo ya Mungu, Rehema yake na Laana alizozitoa! Mbona mnakuwa kama watoto wachanga? Ni Maandiko gani yanayoonesha kuwa mwenye laana ana dhambi? Shetani ana dhambi?? Mnalibeza Agano la Kale ili mjihesabie haki kwa hiyo “injili ya upendo” iliyoingizwa na Freemasons, nanyi mmetekwa na hamjui. Mtarukaje huko juuu katika anga za kiungu kwa ubawa mmoja wa Agano Jipya? Sijawahi kumuona ndege yoyote yule akiruka kwa bawa moja, akivunjwa bawa moja yeye hubakia hapa chini na kufia hapo! Kanisa nalo limevunjwa bawa moja, hilo hapo chini linachakura majalalani na kuokoteza Mungu alivyovitupa huko na kuurudisha ndani uchafu likiinajisi nyumba ya Bwana, nalo HALIJUI!!!

  Ndugu yangu Millinga, nimekuomba Maandiko yanayoonesha Mungu alipochukuliana na Ushoga, hujanionesha, badala yake unaniletea mambo ya wazinzi na walevi, mafisadi, nk. Hebu waangalieni wacha Mungu jinsi walivyoongozwa kuishughulikia JAMII YA MASHOGA:
  1Fal 14:24 ” Na mahanithi walikuwako katika nchi, wakafanya sawasawa na machukizo yote ya mataifa BWANA aliwafukuza mbele ya wana wa Israeli”
  1Fal 15:12 “akawafukuza mahanithi katika nchi, akaziondoa sanamu zote walizofanya baba zake” (Kumbe wanaowakubali mashoga huanza na kuabudu sanamu!) Hayo yalifanyika katika ufalme wa kimwili huko katika Agano la Kale na hao wacha Mungu waliwafukuza katika nchi, mngekuwepo huko nadhani mngeanzisha zogo kuuubwa kama la leo! Kama nilivyokuonesha kuwa watoto wa Mungu huruka kwa mbawa mbili, hilo ni bawa moja, Agano la Kale; bawala pili ni Agano jipya, angalia Mt Paulo anavyopiga bawa hilo katika 1Kor 6:9 “Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi Ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, …” hapo yale ya mwilini yametafsiriwa katika roho, maana sasa ni mambo ya rohoni, ndio maana nikakuambia kanisa linahangaika na wafu, maana wamekwisha hukumiwa kifo!

  Basi hukumu nimekuonesha kuwa imekwisha pita, hata hao wazinzi ambao ni mmoja mmoja na si jamii kama mashoga, wote wamekwisha kuhukumiwa, hata yule mwanamke aliyeletwa kwa Kristo alikwisha kuhukumiwa na Torati, ilibakia utekelezaji wa Hukumu tu, ambao kwa vigezo vya Torati hakuwepo mtekelezaji, maana mwenye Torati yake alikuwepo, wakakimbia! Lakini kwa leo ni kiroho na mtekelezaji ni Mungu mwenyewe. Basi mnapojihusisha na mambo hayo mkitegemea kufanya maombi, mnajidanganya! Mambo hayo yamekwisha vuka viwango vya mwili na sasa yako rohoni ambako ni vigumu kueleweka kwa watu wa mwilini na wanaodhani wako rohoni! Ndio maana yule mchungaji alipotoa tamko lake la kuwatenga, maana hajui atawafukuzia wapi, hao waliochini ya Laana, akiwatazama kwa Macho ya Mungu na kuwajua kile walicho, watu wa mwilini si rahisi kuyajua hayo, maana injili waliyonayo ni hiyo iliyokuwa peverted kama hao mashoga wenyewe, hiyo ndio “Injili ya Upendo” usio na mipaka!

  Wakoma walitengwa, mashoga WALIFUKUZWA! Pia tunawaona wakoma wakitakaswa, ila mashoga hatuwaoni popote pale wakitakaswa, wala wakishughulikiwa katika namna ya kuokolewa kama mnavyojidangaya ninyi!

  Katika kukujibu hoja zako nne ulizoniletea, labda nikuoneshe kwanza tabia za kishoga huenda ikakusaidia kujua ni kwa nini Mungu aliwafukuza kati ya wanaye!
  Ushoga ni perversion, yaani mwanamume aliye yakana maumbile yake ya asili, kwa hiyo huyo hawezi kuwa na uzao, yaani ni kizazi kilichojikatilia mbali chenyewe, ndio maana ni chukizo. Ushoga unatengeneza kajamii ka watu wa jinsi hiyo ndani ya jamii, nako kajamii hako hukua kwa kuwaingiza wafuasi wapya na kuwanyemelea watoto wadogo kama unavyowaona makasisi wa Kikatoliki wanavyoshutumiwa na mapesa wanayoyalipa kama fidia kwa mambo hayo, na mwishowe huwa mtandao mkubwa unaozimeza jamii ongofu kama ilivyokuwa huko Sodoma na Gomora! Kwa hiyo jamii ikisimamiwa na wahubiri kama ninyi mnaochukuliana na mambo hayo, mkiyafananisha na wazinzi ambao katika jamii huwa ni mmoja mmoja tu, matokeo yake hayawezi kuwa tofauti na Sodoma, ndio maana tunajaribu kuzipambanua roho hizo zenye kucompromise Neno la Mungu!

  Kwa hiyo unaponiuliza kuwa kuwatenga au kuwafunga mashoga ndipo ondoleo la dhambi litapatikana? Inanishangaza sana kuwa hujui Ondoleo la dhambi linapatikanaje! Jaribu kusoma Kitabu cha Matendo ya Mitume (2:38), kitakupa mwongozo na sifa za kanisa lililojazwa Roho Mtakatifu wa kweli, ili ufumbuliwe macho yako ya kiroho umjue hata Musa alikuwa ni nani, halafu ujilinganishe na wewe uliyeipokea hiyo injili ya Kristo inayowahurumia mashoga (sijui kutoka wapi?), ukiona uko juu yake Musa, hilo ni jema pia!!! Ila Mungu alimpiga ukoma Miriam kwa jambo kama hilo!

  Kuhusu Yesu na yule mwanamke, yeye alichofanya ni kuwaruhusu waitekeleze adhabu hiyo kulingana na vigezo vya Torati ambavyo viliwashinda, kwani wao pia walipaswa wapigwe mawe, kwa hiyo wakajiondoa! Hilo ndilo lililotokea, sio Yesu alimaanisha nini, Yeye ndiye Torati, ndiye Musa, ndiye manabii wote, yeye huzisoma siri za mioyo yetu, huwezi kumdanganya!

  Pia nikukumbushe kidogo, nakuona ulivyokata tamaa na ‘injili yako mpya ya upendo’, Unasema, “katika enzi hizi za Agano Jipya huwezi ukawa na askari kanisani wanaofanya kazi ya kuwafumua watenda dhambi … waumini wanafiki, waongo, wasiokuwa waaminifu, wachoyo, wakaidi, wenye kiburi, nk.” Halafu unamalizia kwa “HUWEZI” nyingine; “ kama huwezi kuwachuja wote watendao dhambi zote, kwa nini ufanye hivyo kwa mashoga pekeeee?” Tatizo lako ndugu yangu, ni kutumia saana akili mahali isipohitajika. Mambo ya Mungu hayahitaji akili zetu, bali yanahitaji utii tu. Ungekuwa mtiifu kwa neno la Mungu, usingetoka nje kiasi ulichotoka hata bila ya uoga, eti unauliza Injili ya kuwafukuza mashoga katika jamii, “Injili hiyo imetoka wapi? Labda TORATI ya Musa na wala siyo INJILI ya Kristo!!” Hivi, kwako wewe, Musa ni nani, na Kristo ni nani???

  Punguza kidogo hizo akili, na hizo “HUWEZI” zako Mungu atakuondolea. Hizo ulizoziorodhesha kama dhambi, kwa taarifa yako si dhambi bali ni matunda ya dhambi. Dhambi ni kutokuamini, kama hizo “HUWEZI” zako, ndiyo dhambi! Basi tunakuambia Mungu alikwisha kuwaweka hao askari unaosema “HUWEZI” kuwaweka. Roho Mtakatifu ndani ya kusanyiko, hulisafisha kanisa hata shoga yoyote yule asipate fursa ya kuingia humo, maana hamkaliki, si kwa mashoga wala wazinzi wala mafisadi na uchafu mwingineo! Hivi, kama hata hujui kuwa Roho Mtakatifu ndiye askari alilindae kanisa, kweli wewe kwa akili zako unaweza kutatua “matatizo ya kiroho” waliyonayo mashoga kuliko Mungu aliyewafukuzia nje ya Ufalme wake?? Hiyo ndiyo version mpya ya “injili yenu ya upendo”, injili ya Neema? Hiyo inayo yaToratisha mafundisho ya msingi ya ukristo na kuyafanya LAANA! Yaani Mt Paulo anapowahakikishia mashoga kufukuzwa kwao katika Ufalme wa Mungu, alikuwa akitafuta kuhesabiwa haki kwa matendo ya sheria na hivyo amelaaniwa! Milinga usitafute umaarufu kwa kasi hiyo, mawazo yetu yote yatakuwa wazi “Katika siku ile Mungu atakapozihukumu siri za wanadamu sawa sawa na Injili yangu, kwa Kristo Yesu” Rum 2:16. Basi, jaribu kukagua hiyo Injili yako ya kuwaingiza mashoga kanisani mkawaombee waokoke, iwapo mt. Paulo aliihubiri, kama hakuihubiri, basi jua kwa uhakika kuwa ile laana aliyoiweka katika Gal 1:8 kulingana na alivyoyaona mafundisho hayo yakiingia kanisani, hautaikimbia!

  Mungu anataka watu wenye msimamo thabiti, hata kama ni wa kupotea, sio ukigeugeu; hatua mbili, ooh mashoga watupwe na wenye dhambi wengine Jehanum, mbele kidogo, ooh tusiwatenge mashoga!!! Chagua MOTO, au BARIDI sio vuguvugu!!!

 14. Mtumishi wa Bwana,

  Kusema ukweli sijaelewa msimamo wako. Sijaelewa kama unatetea wenye dhambi wafe yaani wauawe wakiwa dhambini au unatetea watu wote waokolewe toka dhambini bila kujali dhambi yao? Unatetea kipi?

  Hivi Mungu anafurahia kifo cha mwenye dhambi? Imeandikwa wapi kwamba Mungua anafurahia kufa kwa mtu mwenye dhambi?

  Hivi mzinzi na shoga nani mtenda dhambi mkubwa mbele za Mungu? Mimi naelewa kwamba maandiko yanasema Mungu hapendi mwenye dhambi hata mmoja afe akiwa dhambini. Au wewe maandiko hayo unayasahau? Mbona husemi watenda dhambi wengineo nao watengwe mbali na wanadamu wengine?

  Mimi siyo kwamba nawatetea mashoga kwamba wanayoyafanya ni haki. Mimi nashangaa watu wanaopiga panda mbele za watu kuhusu mashoga peke yao kana kwamba ushoga umekuwa ndiyo dhambi kabambe dunian ambayo inapaswa kuchukiwa sana kuliko dhambi nyinginei!!!!!!

  Mimi naomba ujibu hoja hizi chache:

  1. Mashoga wakifungwa kama ulivyotoa mifano ya Uganda na Malawi ndipo ondoleo la dhambi yao ya ushoga litapatikana? Hivi siku hizi za Agano Jipya waweza kuwafanya watu waache uovu kwa kuwafunga gerezani? Injili hiyo imetoka wapi? Labda TORATI ya Musa na wala siyo INJILI ya Kristo!!

  2. Ushoga na dhambi nyingine, je, vyote ni sawa? Kama zote ni dhambi, ni mtenda dhambi yupi anayepaswa kutengwa na wanadamu wenzake? Mbona watu hawapigi panda kwamba walevi wa gongo, bia, sigara, nk watengwe kana kwamba ndipo wokovu wao utawaijia?

  3. Ukiacha enzi za Musa, niambie ni wapi katika Kanisa la kwanza watu wowote watendao dhambi ilipendekezwa watengwe au wafungwe jela au kwenye uzio wa umeme kama suluhisho la uovu huo?

  4. Yesu alipowaambia waliomtega kuhusu mwanamke aliyefumaniwa akizini akawaambia kuwa asiyekuwa na dhambi awe wa kwanza kurusha jiwe kumuua yule mzinzi, Yesu alimaanisha nini? Mbona Yesu hakuwaruhusu walalamikaji kumuua yule mwanamke kama ilivyosema torati?

  Injili ya kweli ambayo naona wengi hapa wanaikwepa ni ile kwamba Ushoga ni tatizo la kiroho wala siyo la mwilini. Hivyo nadhani ni vyema Injili ikabakia kwamba mtu mwenye tatizo la kiroho (ushoga) tatizo lake litatuliwe kiroho zaidi na wala siyo kwa kumweka kwenye kifungo cha mwili huu unaoharibika. Ushoga ni roho ya uasi kama ilivyo kwa dhambi yoyote ile unayoielewa.

  Mwisho, nadhani mawazo yangu uliyasoma haraka haraka bila kutafakari. Mimi sijatetea ushoga hata siku moja na wala sitakuja nifanye hivyo. Yawezekana hoja zangu hukuzielewa. Maelezo yako haya hapa ndiyo yaliyotaka kunionesha kwamba umeelewa mawazo yangu lakini mwishoni unarudi kwenye mtazamo tofauti. Hebu tazama umesemaje “, ….. Wengi wetu Maandiko yanaposema katika siku za kufunuliwa kwake Mwana wa Adam, hali ya dunia itakuwa kama ya Sodoma, huyaangalia mambo hayo huko nje, lakini hayo yatakuwa kati ya hao wanaokiri wokovu…….” Haya uliyaeleza ndio msingi wa maoni yangu kwamba huwezi katika enzi hii ya Agano Jipya ukawa na askari kanisani wanaofanya kazi ya kuwafumua watenda dhambi ili wakatengwe katika viwanja vilivyofungwa mageti na senyenge zenye moto wa umeme (electrical fences) utakuwa unajidanganya kabisa.

  Utawatenga mashoga ili wakafie mbali, lakini hutaweza kuwatenga waumini wanafiki, waongo, wasiokuwa waaminifu, wachoyo, wakaidi, wenye kiburi, nk. Kama huwezi kuwachuja wote watendao dhambi zote kwa nini ufanye hivyo kwa mashoga pekeeee? Huoni kwamba utakuwa umeondoka katika Injili ya Neema na umeenda kuhubiri TORATI? Wamelaaniwa wote watakao kuhesabiwa haki kwa matendo ya sheria.

  MSIMAMO WANGU NI HUU:

  DHAMBI ZOTE NI MBAYA NA MACHUKIZO KWA MUNGU. HUKUMU YAKE NA GHADHABU YA MUNGU KWA DHAMBI ZOTE PAMOJA NA USHOGA NI HUKUMU YA MILELE JEHANAM YA MOTO NA SIYO KWENYE FENCE ZA UMEME WALA KUWAPIGA MAWE, WALA KUWAFUNGA JELA DUNIANI.

 15. Ndugu yangu Milinga,
  Unapozungumzia hukumu, Mungu atakapo watenganisha kondoo na mbuzi; pia unapaswa ufike mpaka pale Injili inapotuasa tusipelekane mahakamani, “Je, hamjui kuwa mtauhukumu ulimwengu?” ukiyaelewa hayo, itakuwa rahisi kuyajua majukimu yaliyopewa kanisa liyatekeleze na kujitambua nini ulicho au unawakilisha nini! Hukumu hainaga mapatano; ikifika wakati wake Hutolewa hata kama ‘in absentia’, kwa hiyo kulalamika mashoga wasitengwe haisaidii kitu, maana huyo mtoa hukumu alikwisha itoa Hukumu ya mashoga, wengine kabla hata hawajazaliwa au hawajauanza ushoga. Amesema hao hawataurithi Ufalme, sasa sijui ninyi akina Milinga mtawapeleka katika ufalme gani, ufalme wa kanisa? Labda huo, maana tumewaona maaskofu mashoga na waumini mashoga na ndoa zikifungishwa kati yao makanisani, kwenye hayo madanguro yanayo pose kama kanisa! 

  Sijawahi kusikia sehemu yoyote ile duniani ambako “Ustawi wa Jamii” waliwatenga mashoga ili wafe, ila naliona Neno la Mungu likiwatoa ndani ya miji na kuwatenga na wakati mwingine kuwaua! Na wala sijawahi kusoma popote pale mashoga wakihudumu katika makusanyiko ya Bwana wala kuchanganyika na waumini wengine. Na wala sijawahi kusoma popote pale kuwa mashoga ni maadui zetu, ninavyo fahamu mimi hao ni machukizo. “Abomination”. Kwa hiyo kuwatengeneza mashoga kwa hila kuwa ni maadui ili utumie Injili kuwaleta makanisani ni michezo ya hatari ambayo gharama yake sijui kama kweli mmejitayarisha kuilipa. Acheni kuzitegemea akili zenu ; Neno la Mungu sio ” ustawi wa jamii” kama unavyotaka kutuaminisha, Mungu ni zaidi ya vyote unavyoweza kuviwaza! Sodoma walitoka watu wanne tu, na kwa Nuhu watu nane tu, wengine wote waliangamia, kati ya milioni mbili waliotoka Misri, ni wawili tu walioingia Kaanan! Usijidanganye kuwa Mungu ana huruma isiyo na mipaka, kama amewakataa mashoga, yeye anajua kwa nini, wewe au mimi siyo kazi yetu kuwaonea huruma, labda tuwe tumeichoka huruma ya Mungu ndipo tutaweza kujihusisha na Injili kwa mashoga kama wengi waliojidanganya kuwa Mungu ana mapenzi sana hawezi kutuua wote! Aliwaua mpaka watoto wachanga wasio jua dhambi ni nini kwa akili yetu finyu ya kibinadamu, sembuse hawa mashoga na washirika wao!!

  Wengi wetu Maandiko yanaposema katika siku za kufunuliwa kwake Mwana wa Adam, hali ya dunia itakuwa kama ya Sodoma, huyaangalia mambo hayo huko nje, lakini  hayo yatakuwa kati ya hao wanaokiri wokovu, kanisa, hilo ndilo linaloingia katika dimbwi la ushoga na usagaji kama linavyojitumbukiza sasa hivi!! Nimewahi kusoma ushuhuda wa wainjilisti waliojipachika jukumu la kuwahubiri mashoga waokoke kwa nia njema kabisa, wakiamini kuwa Roho Mt kawatuma, mashoga wale wakawavuta mpaka wakalala nao, walipoulizwa imekuwaje tena ninyi kutembea na mashoga? Jibu lao lilikuwa rahisi kabisa: we were trying to win them to Christ!!! 

  Kwa hiyo ndugu yangu Milinga, ingawa wengi mnaliona Agano la Kale kuwa limepitwa na wakati, yaani ni kitabu cha historia, mawazo hayo hayawezi kulibadili Wazo la Mungu, Yeye hajawahi kuchukuliana na mashoga kama ambavyo ninyi mnajaribu kumfanya kwa kuihusisha Injili ya thamani aliyowaletea ambamo ndani yake amewaonya kuhusu mambo hayo ya ushoga, yaani mkiitukanisha Injili, au kama ule mfano wa kuwapa nguruwe lulu! Yaonekana ninyi mnawajua mashoga kuliko Mungu. Kwamba ninyi mnayo Injili inayoweza kuwaokoa mashoga ni kichekesho! 
  Unaweza kudhani kuwa nayakuza mambo, lakini hebu kichunguze hiki ulichoandika :
  “Hapa tunapaswa kujadili hoja aliyoitoa huyu Mchungaji kama iko valid au ni invalid and out of biblical context. Hebu tujiulize kuwatenga hao mashoga na kuwaweka peke yao ili watoweke, duniani “die-out” ndiyo Injili tuliyotumwa kuhubiri ulimwengu huu.”
  Hiyo Biblical context unayoitaka ni ipi? Maana sijaona mahali mashoga wanakubaliwa na Mungu naona wanapigwa mawe na kutengwa, labda wewe ndio ungetuletea hapa ushahidi wa kimaandiko wa hayo ya ushoga na usagaji unayoyatetea, utupe Nuru iliyokuangazia mambo hayo. Tuna hamu ya kuijua source ya injili yako hiyo!!! Hata dunia inakusuta! Dunia, chini ya uvuvio wa Injili, serikali zilitunga sheria za kuwafunga mashoga, yaani kuwatenga na jamii, nimekupa mfano wamashoga wa Malawi waliofungwa miaka 14, Uganda wanataka wahukumiwe kifo, sehemu nyingi tu duniani wako watu wenye hofu ya Mungu inayowaongoza kuitamka hukumu ya Mungu bila hofu ya kinafiki, ingawa mwishoni machukizo yatashinda, lakini twafahamu ni kule “kukijaza kikombe cha ghadhabu ya Mungu” ndio maana unaziona kejeli za kuwaokoa mashoga zikiyateka makanisa!

  Mungu alikwisha kuwalaani mashoga, basi ninyi kama mnayo injili ya kuwafufua hao, na jinsi mnavyokazania, sina shaka Ibilisi kaikusanya kuzimu yote wanawaangalia akina Millinga na wenzako kwenye projector kubwa mnavyohangaika na mapepo ya ushoga yaliyojichukulia miili mkiigiza kuokoana, yaani comedy!

  Ulizungumzia, nikiandaa mkutano mkuuuubwa wa Injili halafu mashoga wakajikusanya hapo. Nikiwa ni yule mwenye kutumia akili, nitawabembeleza waache tabia zao hizo wampokee Kristo awe Bwana na Mwokozi wao! Jambo ambalo watalifurahia, nawe Milinga ukiwa Shemasi wangu utawaongoza “Sala ya Toba” nao watakuwa wanajumuia wenzetu! Lakini nikiwa chini ya uongozi wa Roho Mt, yeye anazijua roho zilizo juu ya hao mashoga, “Enyi Uzao wa Nyoka” ; “Enyi majoka” … Hawatakaa, Yuda mwenyewe na ungangari wake aliukimbia Ubatizo wa Roho Mt sembuse hivyo vipepo vya ushoga!!!

  Acha wafu wawazike wafu wenzao!!

 16. Ndugu Millinga,

  Awali ya yote nichukue nafasi hii kukupongeza kwa mawazo yako mazuri sana uliyoandika hapo juu, kuhusu mada hii hasa kujibu kile alichokisema ndugu yetu CK Lwembe. Sifa na utukufu ni kwa Bwana wetu Yesu Kristo.

  Siku zote huwa inanishangaza sana pale mtenda dhambi anapotengwa ama kanisani kwake au kwenye makusanyiko yetu.

  Tunaposoma biblia kwa ujumla wake toka baada ya lile anguko la mwanadamu kwenye bustani ya Edeni, tunaona Mungu akihangaika na mwanadamu aliye mdhambi ili kumuokoa toka dhambini na kumrudishia tena ile heshima aliyoumbwa nayo.

  Yesu mwenyewe aliaacha enzi na utukufu wake huko mbinguni ili azaliwe na mwanamke katika mwili huu wa nyama ili atuokoe wenye dhambi na kuna sehemu nyingi sana alizoeleza bayana kwamba amekuja kwa ajili ya wenye dhambi. Sasa sisi ni nani hasa hata tufikie kuwatenga wenye dhambi na kuwaacha wajifie taratibu na hatimaye watoweke hapa duniani?

  Ufunuo 5:9-10 inasema kila aliyenunuliwa kwa damu ya Yesu amekuwa kuhani na mfalme, mbona sasa tunasahau kuwa wajibu mkubwa wa kuhani ni kupambana na dhambi ili wenye dhambi wapate kuokolewa. Kwa maana hiyo kila aliyeokoka anatakiwa pia kuwapenda na kuwaleta wote wenye dhambi kwa Yesu ili nao waweze kuona wema wa Bwana, mashoga wakiwa mojawao.

  Dhambi ni mbaya kwa kuwa isipotubiwa inampoteza mwanadamu milele, lakini sisi tulio okoka tusipofanya kazi ya kuwavuta wenye dhambi kwa Yesu tutatoa hesabu gani kwa Bwana wetu?

  Naweza kusema bila woga wowote kwamba ofisi ya kuhani yeyote yule ni dhambi. Yesu hajatuita kukanyaga red carpets ili kuifanya kazi yake, bali ametuita ili kukanyaga ng’e na nyoka (dhambi) ili watu wa Mungu wapate kuokolewa. Mhubiri yeyote anayedhani kuwa anatakiwa kuwahubiri wale walio okoka tu, huyo hajaitwa na Bwana, amejiita yeye ndio sababu anawatenga wenye dhambi. Yesu alikula na wenye dhambi, sembuse mchungaji huyu anapata wapi hili la kuwatenga na kuwafungia mashoga sehemu moja ili wafe a natural death?

  Mchungaji yeyote anayemtenga muumini wake mwenye dhambi au aliyekengeuka kutoka kwenye kundi lake, huyo sio mchungaji. Mchungaji wa kweli huwatafuta kondoo wake na kuwarudisha zizini. Mchungaji wa kweli anawaacha kondoo wengine wote walioko zizini na kwenda kumtafuta yule mmoja aliyepotea.
  Mungu aturehemu!!

 17. Mtumishi CK Lwembe,

  Ubarikiwe sana. Nadhani kuna jambo watu wengi wamesahau. Watu wanasahau kwamba Yesu aliwapenda wenye dhambi. Kuwapenda wenye dhambi isichanganywe na kuipenda dhambi. Yesu aliwapenda wenye dhambi lakini hakuipenda dhambi kamwe.

  Nadhani tunapaswa kuichukia dhambi sana. Tena kila siku. Lakini hatupaswi kuwachukia wenye dhambi. Mungu anawapa mvua wenye haki na waovu. Mungu anawapa Jua wenye haki na wasio na haki. Mimi nadhani hii ndiyo Injili ya Ufalme.

  Biblia inasema yaacheni magugu na ngano yakue pamoja. Aidha, maandiko yanaeleza kwamba siku ya hukumu Mungu atawabagua mbuzi na kondoo, wenye haki na waovu. Yote haya yatafanyika siku ya hukumu na kiama ya wafu na wala siyo kwa sasa.

  Hapa tunapaswa kujadili hoja aliyoitoa huyu Mchungaji kama iko valid au ni invalid and out of biblical context.

  Hebu tujiulize kuwatenga hao mashoga na kuwaweka peke yao ili watoweke, duniani “die-out” ndiyo Injili tuliyotumwa kuhubiri ulimwengu huu.

  Tunapaswa kuelewa kuwa utendaji wa Mungu katika Agano la Kale ni tofauti katika Agano Jipya. Enzi za Musa wachawi, wakoma, mashoga, wazinzi, wezi, nk. walitengwa na jamii au waliuawa kwa mawe hadi kufa. Wakati ule wa Musa ilikuwa ni sahihi. Lakini je, Kristo ametuagiza kufanya hivyo.

  Yesu ametuagiza kwenda ulimwenguni mwote kuhubiri Injili kwa kila kiumbe (wakiwemo mashoga) kila aaminiye na kubatizwa ataokoka asiyeamini atahukumiwa (Math. 28:16-20, Mrk 16:15-18) Hili ndilo Agizo Kuu la Kristo. Tuihubiri Injili kwa kila kiumbe. Yesu hajaagiza wanafunzi wake waende ulimwenguni kote kuwakamata mashoga au watenda dhambi wowote na kuwatenga mahali pa peke yao ili watoweke duniani.

  Mimi siyakubali mahubiri kama haya kwa sababu siyo ya kweli. Kama mpendwa Lwembe unayaunga mkono mimi siyakubali kabisaaaaa.

  Siamini kwamba kuna siku dunia itakuwa haina watenda dhambi. Naamini kwamba mashoga ni watenda dhambi kama watenda dhambi wengine tu. Dhambi ya ushoga siyo tofauti na Uzinzi, ulevi, wizi, uongo, nk. Ushoga ni dhambi ifanywayo na watu wa jinsi ya aina moja wakati uzinzi ni dhambi ifanywayo na jinsi mbili tofauti lakini zote ni dhambi.

  Ukisema mashoga waondolewe katika jamii na watengwe eneo la pamoja ili hatimaye watoweke duniani (die-out) huku ukiwaacha wazinzi na mafisadi wakiendelea kuwepo duniani mimi nakuona kama umeacha kufanya kazi ya Injili na umegeuka kuwa “Afisa Maendeleo ya Jamii” yaani Community Development Officer. Huna tofauti na Afisa Ustawi wa Jamii. Mhubiri wa namna hiii kama ameacha kazi ya Injili na kuamua kuwa Afisa Ustawi wa jamii nitamwelewa kwa uashihi lakini siyo muhubiri wa Injili.

  Tukumbuke kwamba Ushoga ulikuwepo tangu enzi za Yesu, tangu enzi za Musa tena hata kabla ya Musa wakati wa Ibrahim na Luthu, ushoga ulikuwepo kama ilivyokuwa kwa dhambi zote. HAKUNA JIPYA CHINI YA JUA, YOTE YALIKUWEPO.

  Huwezi kuokoa watu kwa nguvu. Huwezzi kuokoa watu toka dhambini kwa kuwatenga peke yao ili baadaye watoweke duniani. Yesu angeweza kufanya hivyo na angeweza kumtowesha Ibilisi kabisa na kmuftilia mbali, lakini Mungu hatumii mabavu kuwaokoa watu bali hiari ya moyo bada ya kushukiwa na Neema ya wokovu. Hakuna ajaye kwa Yesu asipovutwa na Baba wa Mbinguni.

  Hebu ndgu CK Lwembe, niambie siku ukiandaa mkutano wa Injili pale Furahisha Mwanza au pale Ungalimited Arusha, au Biafra na Jangwani Dar es salaam, ukawaona waitwao mashoga wanakuja kwenye mkutano huo ili wasikilize Neno la wokovu, utawatimua? Kama hutawatimua kwenye mkutano wa Injili je ukiwaona wamekuja kanisani kwako utawatimua waondoke? Kama jibu lako ni NDIYO, sasa wewe mikutano yote ya Injili unayoiandaa, unamwandalia nani aje kwenye mkutano? Unataka watakatifu ndiyo waje peke yao?

  Kama unaandaa mkutano ili wenye dhaambi waokoke, je ukiona changudoa au kahaba mkutanoni naye utamfukuza asiwepo kanisani au mkutanoni? Sasa ukiwaangamiza mashoga ni lini utawahubiri Neno la WOKOVU?

  Hebu tafakari tena hoja hizo hapo juu kisha urekebishe mtazamo wako.

  Karibuni kwa mjadala.

 18. Kweli inashangaza sana kuona kanisa lilivyokosa mwelekeo! Hiyo Injili ya kuwaokoa mashoga mnaipata katika Biblia ipi? Biblia niliyonayo mimi, humo naona wafalme wote waliomcha Mungu wakiwaondoa mashoga katika miji waliyoitawala na naona Mungu akiiangamiza miji ya mashoga kwa moto! Hakuna mahali Biblia inatuonesha Mungu akichukuliana na ushoga. Sasa ninyi leo hii mnawakaribisha makanisani mwenu eti, “Kama humpendi shoga unayemwona utasemaje kwamba unampenda Mungu usiyemwona?” ama kweli sikio la “kufa”! Hiyo ndio Injili mpya mnayoihubiri! Mlipo ukiri wokovu mapepo ya dini yaliwakimbia, mlipo ukataa ubatizo wa Ondoleo la Dhambi kama ulivyo katika kitabu cha Matendo (2:38 nk), ili ile dhabihu ya dhambi iliyotolewa pale Kalvari iwasafishe, na Roho Mt aje akae ndani yenu; basi kama Maandiko yanavyo onya, maadamu nyumba imesafishwa na imebaki tupu, yule pepo wa dini akirejea humo huwachukua na wenzake saba!! Angalia ushoga unavyotetewa na “wacha Mungu” hata Mungu mwenyewe anaona aibu kwa ukatili wake! Kanisa lake linawapenda na kuwahurumia majirani zao mashoga!!! Mnamchezea Mungu eenh?

  Ama kweli tumefika; Mchafu na azidi kuwa mchafu … Na mtakatifu na azidi kutakaswa! 
  “Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo”

  Acheni ushabiki, mtakuja ulipia huo ushabiki kwa nafsi zenu kutumbukizwa pamoja na hao mashoga wenu ambao wala hamuwajui kwenye ziwa la moto buree! Mnamshambulia yule mchungaji bila hata kujua alichokisema ni nini. Oh huyu mchungaji muuaji, ni wapi aliposema mashoga wauawe? Yeye kwa jinsi ya mwenendo wao, ameshauri watengwe katika eneo litakalo zungushiwa umeme ili wasitoroke halafu wawekwe humo ndani. Kwa tabia yao hawataweza kujizaa humo maana nyendo zao ni kinyume na maumbile kwa hiyo hawatajizaa na mwishowe kizazi chao kitamalizika- “die out” kabla hujamsikiliza mtu vizuri unamkurupukia na shutuma na ushabiki mwingi eti, “Nawaomba tusisahau kwamba kuua ni dhambi mbaya” kama Mungu aliamuru watu wa jinsi hiyo wauawe, wewe unayemuona Mungu ana dhambi ya kuua umetokea wapi? Ukristo umewashinda mmeamua kuungana na Umoja wa Mataifa kutetea haki za mashoga! Tumemuona Katibu Mkuu wa UN akiacha ofisi na shughuli nyingine zenye tija akasafiri hadi Malawi kwenda kuishinikiza serikali kuwaachia huru mashoga wawili iliyowafunga miaka 14, na sasa roho ya kuwapenda mashoga ndio hii imetufikia,

  Nawatakia mafanikio!

 19. Wapendwa,

  Nawaomba tusisahau kwamba kuua ni dhambi mbaya. Nawaomba wachungaji wasitake kukalia kiti cha Mungu na kutaka kuanza kutoa hukumu ambayo ni Mungu pekee angeweza kuitoa.

  Kutaka mashoga wauawe kwa moto wa umeme haina tofauti kabisa na kuua kwa kutumia rungu, au upanga. Yesu alisema tuwapende maadui zetu na majirani zetu. Hivi jirani yako pale mtaani akiwa ni shoga utampenda? Kama humpendi shoga unayemwona utasemaje kwamba unampenda Mungu usiyemwona. Wewe ni Mwongo tu.

  Wachungaji wenye mawazo kama huyu pastor, ni wauaji kabisa. Hawana tofauti na wauaji au majambazi wa kawaida. Utasemaje kwamba wale wote ambao ni mashoga wachomwe moto? Hivi kama kila mtu anayemkosea Mungu angetiwa moto wa umeme au wa kiberiti, nani hapa duniani angepona?

  Upendo wa Agape utuongoze ili kuweza kuuleta ulimwengu kwa Kristo aliyejitoa kwa ulimwengu wote bila kujali maovu tuliyokuwa nayo ili tuokolewe. Mashoga nao wanahitaji wokovu siyo Kifo.

  Wewe ni nani hata uwahukumu wanadamu wenzako kifo? Mungu pekee ndiye atawahukumu. Acheni ngano na magugu vikue kwa pamoja. Huwezi ukaisafisha dunia yote ikawa yenye watu walio walokole watupu au watakatifu. Wewe fanya wajibu wako wa kuhubiri Neno la kweli atakayeokolewa aokolewe asiyeokolewa siyo juu yako kumhukumu.

  Kwa kweli mahubiri ya namna hiyo yamenisikitisha sana.

 20. Labda tukumbushane mambo ya msingi ili kadiri tunavyosonga mbele safarini yasije yakatutoka mioyoni mwetu na tukaanza kuhubiri Injili mpya ya upendo usio na mwelekeo!

  Ndugu zangu, Torati haijawahi “kupitwa na wakati”. Adhabu zote na Hukumu zake hazijawahi kuondolewa bali makosa yaliyokuwa yakipelekea adhabu hizo, wigo wake umepanuliwa katika ujio wa Kristo kama tunavyoona wigo wa uzinzi sasa si lazima muwe mmelitenda kosa hilo kimwili tu, bali sasa hivi hata kumtamani tu mwanamke, hilo linakuingiza katika uzinzi ambao adhabu yake ni kupigwa mawe mpaka ufe; ila kwa vile hakuna mwenye mikono safi, na pia sasa hivi mambo ni ya rohoni ambavyo Mungu hutuchunguza mioyo yetu, basi kama zilivyo Hukumu, za kiroho, na adhabu zake pia ni za kiroho katika maana ya kifo cha kiroho badala ya cha kimwili ambavyo madhara ni yale yale. Hakuna anayefufuliwa ili ahubiriwe Injili kwa ajili ya kuokolewa! Vivyo mfu wa kiroho, hana nafasi tena ya kuokolewa, mnaweza kuwa mnahangaika na wafu!!!

  Mnavyo hangaika nao mnaishia kuwaingaza katika makusanyiko yenu na mwishowe ushoga unaingia makanisani mwetu kwa vile tu tumetumia akili zetu kuwahubiri watu, badala ya ROHO MTAKATIFU ambaye angeuondoa uchafu uliojipenyeza na kuingia katika makusanyiko yetu. Lakini sisi tunawaalika mashoga kanisani tukijiaminisha kuwa wataokoka; nao mashoga hutuona kama limbukeni wa Injili, ndipo huigiza kuokoka na mwishowe kudai haki ya kutambuliwa! Na kwa vile makanisa hayaongozwi tena na Roho Mt, kura hupigwa, na kwa MSHANGAO wa wengi, MASHOGA WAMESHINDA, sasa ni ruksa wote ni watoto wa Mungu!!!!

  Kanisa msilale usingizi mchana, fanyeni kazi ya Mungu. Alichokilaani Mungu msijaribu kukibariki, mtazivaa shida zake! Ni sawa na kwenda kuununua ule mti alioulaani Kristo ukiwa umeyasikia aliyouambia ule mti, ukajidanganya kuwa hajaulaani, mbona ni mti mzuri tu, nikiuwekea mbolea kidogo utazaa sana. Nawe ukatoa akiba yako yooote, ukaununua, pole sana UMENUNUA KESI!!!!

 21. OH! MY GOD! ni aina gani ya injili inaletwa tena Hapa duniani,Yesu alisema nilikuja kwa ajili ya wagonjwa ndio wanahitaji tabibu,bali mzima tabibu wa nini?so mashoga na wasagaji huo ni ugonjwa wao wanamhitaji Yesu kama tabibu wao,ni kuwapa neno tu mpaka Bwana Yesu aguse mioyo yao si kuwahukumu kwa maana sisi sote tutakaa mbele za Mungu kusubiri hukumu,AMIINA!!!!!!!!!!!!!!

 22. Hawa watu wanamhitaji YESU. Ni vizuri wakahubiriwa wakamjua mwokozi wa ulimwengu. Duniani dhambi siyo hiyo mbona dhambi ziki nyingi tu tena za kutisha. Hakuna jipya linalotokea duniani ambalo halikusemwa ndani ya Biblia. Tulio wanafunzi wa YESU tunatakiwa tuzidi kuomba zaidi na zaidii.

 23. huyu mchungaji bado anahubiri torati, na kusahau kuwa kuna agano jipya na injili ya Yesu Christ. mbona tutakuwa na mishikaki mingi ya nyama za watu? maana ni wengi, si ajabu hata na watoto wake wapo kwenye idadi hii pasipokujua.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s