Kanisa, Gari la Askofu Vyachomwa moto, Uamsho wakana kuhusika

Katibu wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) Sheikh Abdallah Said Ali ambaye ni miongoni mwa wanaotafutwa na jeshi la polisi akizungumza na Radio DW asubuhi mapema kabla ya taarifa ya kutafutwa kwao kutolewa kwa vyombo vya habari

Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) liliopo mtaa wa Kariakoo mjini Unguja limechomwa moto jana usiku wa kuamkia leo na watu wasiojulikana

Gari la Kiongozi wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Bishop Dickson Maganga lililochomwa moto na watu wasiojulikana usiku wa jana katika eneo la Kariakoo nje ya kanisa hilo ambapo uharibifu wote unaelezwa kuwa umegharimu shilingi millioni 120

Kiongozi wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Bishop Dickson Maganga akiongea na waandishi wa habari

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Kila sifa njema anastahiki ALLAH (S.W) na Rehma na Amani zimuendee Mtume Muhammad (S.A.W), ahli zake, Maswahaba zake na walio wema katika Uislamu.

Jumuia ya UAMSHO inatoa taarifa rasmi kwa umma wa Wazanzibari na Watanzania wote kwa ujumla kwamba haihusiki na vitendo vyote vya uvunjaji wa amani vilivyotokea usiku wa tarehe 26 Mei 2012. Kama alivyosema Mtume (S.A.W) katika Hijatul Wadaa, kwamba ni haramu kumwaga damu zenu, kuharibiana mali zenu, kuvunjiana heshma zenu ila kwa haki ya Uislamu (maana yake pale mtu anapofanya kosa na likathibitika atahukumiwa kwa hukmu ya Kiislamu). Vile vile Uislamu unaheshimu nyumba za ibada (Makanisa, Mahekalu na n.k) zisivunjwe wala zisiharibiwe.

Jumuia inatoa wito kwa Waislamu na Wazanzibari wote kuendelea kudumisha amani na utulivu wa nchi na kutoharibu mali za serikali, mali za wananchi, mali za taasisi za dini zenye imani tofauti, kwani kufanya hivyo ni kwenda kinyume na mafundisho ya dini ya Kiislamu. Jumuiya inayachukulia matukio yaliyotokea usiku wa jana, na yanayoendelea tangu alfajiri leo, kama ni njama za makusudi za wale wasioipendelea amani nchi hii, pamoja na kutaka kuipaka matope jumuiya na kutaka kuzuia lengo la Wazanzibari kudai nchi yao.

Tunatoa wito kwa Jeshi la Polisi na Vyombo vyote vya Dola wafanye kazi zao kama wanavyotakiwa kwa mujibu wa muongozo wa haki za binadamu kwa Polisi na vikosi vingine unaosema kwamba polisi na vyombo vingine vya dola wana jukumu la kutunza amani na utulivu na jukumu la kutoingilia haki za watu. Kila mtu anayo haki ya kuwekewa mazingira muafaka ya kitaifa na kimataifa yatakayomuwezesha kupata haki zake za binadamu.

Polisi na vyombo vingine vya dola wana jukumu la kutunza amani na utulivu na jukumu la kutoingilia haki za watu isipokuwa tu kwa minajil ya kulinda haki za wengine.

Polisi na vyombo vingine vya dola wana jukumu la kuheshimu, kulinda na kutetea haki za binadamu kwa watu wote.

WABILLLAH TAWFIQ

—————————————————-

WAFANYA MAANDAMANO YA AMANI

Maelfu wa wazanzibari wakiongozwa na Taasisi za Kiislamu na Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) wakifanya matembezi ya amani katika barabara za Zanzibar na kupeleka ujumbe wao kwa viongozi wa serikali za Zanzibar na ile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Umoja wa Mataifa wakitaka Zanzibar huru

Akizungumza na maelfu ya wazanzibari kabla ya kuanza maandamano hayo yaliitwa ni matembezi ya amani, Sheikh Farid alisema wazanzibari wana haki kama walivyokuwa na haki wananchi wengine ulimwenguni kote kudai haki yao ndani ya nchi yao 

Source: Zanzibar Yetu, Swahili Vila bblogs
Advertisements

8 thoughts on “Kanisa, Gari la Askofu Vyachomwa moto, Uamsho wakana kuhusika

 1. THe Sovereign Lord is watching and He will not keep silent!
  I call upon all those who know Jesus to stand firm and be strong the battle must be won at present time! God bless you.

 2. Ama kweli Wazanzibari Mna Mambo.Muungano na Ukristo wapi na wapi.Mna uhuru wa kufuatilia madai yenu,lakini fuateni utaratibu mzuri.Tofautisheni dini na siasa wapendwa.MUNGU IBARIKI TANZANIA:UDUMU MUUNGANO WETU:AMINA

 3. Shalooom wapendwa!nilikua zanzibar wiki mbili zilizopita kwa kwel hali ni mbaya sana kule,ni kweli kabisa jamaa zetu hawtaki ukristo,hawataki muungano na pia kuna ushawishi mkubwa sana wanaoupata kutoka nchi fulan tulan hiv za kiarabu,sijui tutafika wapi kama tukisema na ss wa tanganyika tuanze kuchinja na kuchoma mali za wazanzibar wanaoishi dar,au juvunja na kuharibu mali za waislamu>Inaniuma sana but all in all tumuachie mungu yy aliyesema tusiende tena kwea sheria ya JINO KWA JINO.tuzidi kuomba kwa ajili ya nchi yetu,kuna mfumuko utalipuka kuliko hata huo uliotokea jaman,kule watu wamepandikizwa chuki sana kuhusu bara na ukristo

 4. Shalom kutakuwa na maombi maalumu kwa ajili ya hili, yoyote atakayependa kushiriki kwa hali na mali kutetea haki za wa Kristo Zanzibar nitaweka maelezo hapa kwenye blog jinsi ya kuwafikia. Jinsi gani kujipanga na kuomba kwa ajili hili. Vita ni vya Bwana na pia vita vyetu sisi si juu ya damu na nyama bali juu ya roho lakini vina uwezo wa kuangusha NGOME HATA IWE KUBWA KIASI GANI. MUNGU ANAENDA KUTENDA MUUJIZA KUPITIA HILI TUKIO, IT’S A BREAKTHROUGH NOW…
  Mbarikiwe

 5. Wapendwa katika Bwana!Nawasalimu kwa jina lililo kuu kupita yote la Yesu Kristo mwana wa Mungu aliye hai.
  Kwa kweli hali inasikitisha sana kwa mambo yanayoendelea huku visiwani Zanzibar!kwani sasaiv suala la katiba limekuwa la kidini jumla!Jana Jumapili Mchungaji wetu wa T.A.G -Pemba nae katumiwa sms mpaka kashindwa kuonekana kanisani.
  Hatuna budi kuingia ktk maombi zaidi ndugu zangu kwn vita hii si ya kimwili bali ya kiroho zaidi.Shetani yupo kazini akilitafuta kanisa nasi hatuna budi kuzidisha maombi kwa Mungu wetu nasi hakika tutashinda.

 6. Tanzanian we have live peacefully since independence without anybody care your tribe religion or color of your skin we take pride of brotherly love (sisi sote ni ndugu) for those of us who are overseas when we meet and find out you come from Tanzania we don’t care what part of country you come from this as to stop now those who did this need to be brought to the fullest extent of the law. May God be with all of us who love peace.

 7. Wapendwa waislam, Takbiir?

  Kama hali hii inaanza kuwa hivyo, na mnataka nchi huru ya jamhuri ya Zanzibar, ni hali ya hatari sana. Utabiri alioutoa Mwalimu Nyerere kwamba mkijitenga toka Tanganyika dhambi hiyo itawagharimu sana na hamtaishia hapo tu, mtaendelea kugawanyika mpaka siku ya kiama.

  Ukweli ninaouona mimi siyo kwamba mnapinga muungano bali mwapinga Ukristo. Mwatamani hivyo visiwa vyote viwe jamhuri ya kiislam. Mwataka shariah ndiyo itawale badala ya katiba ili Zanziba iwe dola ya kiislam. Hao wote wanaolalamika wakitaka kujitenga toka kwenye muungano ajenda yao siyo ya kisiasa bali ya kidini. Wengi wao ni walafi wa mali za kutoka mataifa ya kiarabu na kiislam. Wanajua kwamba siku Zanzibar ikiwa na serikali yake watapata misaada toka uarabuni kwa wingi na hivyo wanadhani ndiyo neema itakuwa imeshukia.

  Tukio la kuchoma makanisa halijaanza jana. Lina siku nyingi sana. Zanziba limeanza zamani na limekuwa likisambaa kwa kasi hata upande wa bara.

  Sisi wachambuzi wa mambo tunaomba amani itawale. Lakini inashangaza sana kama serikali zote 2 za Muungano na Zanzibar hazitalaani matukio haya.

  Tunaiomba Serikali ya Muungano itamke wazi kwamba inalaani matukio yale ya kuchoma makanisa na kama wakristo nao watalipiza kisasi nao pia wakemewe na kulaaniwa kwa vitendo hivyo.

  Kama serikali ya umoja wa kitaifa (SUK) na serikali ya mapinduzi ya Zanziba (SMZ) hawatalaani vitendo dunia yote itawaelewa kwamba munaunga mkono vitendo hivyo vya kijinga.

  Rais wa nchi Mh. J. M. Kikwete naye anatakiwa atoe tamko la kulaani matukio hayo. Atoe yeye mwenyewe wala asimtume waziri au msemaji wa Ikulu. Atamke yeye mwenyewe kuvilaani vitendo hivyo. Kutofanya hivyo kutazidi kuchochea ghadhabu kwa makundi yote.

 8. Mpaka sasa hali siyo nzuri Zanzibar, zaidi ya makanisa matatu yamechomwa moto. Kwanini ndugu zetu wakristo wanaishi kwa shida huko Zanzibar wakati sisi tuko nao huku bara wanaishi bila shida? huu ni uonevu

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s