Mungu anatukuzwa kwa wanaobadili miili yao?

Bwana Yesu asifiwe, kumekuwa na tatizo la watumishi wa Mungu hasa wanawake kuongeza vitu kadhaa kwenye maumbile yao, mfano kujichubua, kuongeza makalio, kupachika nyusi, wanaopunguza mwili, nk nk

Hivi kweli kama kuna mtumishi wa namna hii, anapoimba au kuhubiri kwa watu, Mungu anajitwalia Utukufu? na siku hizi kuna hata wanaume wanajichubua! wako makanisani.

Unatafsiri gani kuhusu uzuri au urembo?

Advertisements

9 thoughts on “Mungu anatukuzwa kwa wanaobadili miili yao?

 1. Kimuingiacho mtu sio najisi (yaani tunavyoviona na kuvisikia au kuvila endapo hatuna njia ya kuvikwepa) lakini vile vinavyotoka ndani yetu ndio vinatutia najisi.
  Kama ndani ya moyo wako umejaa utauwa una hofu ya Mungu na unamwabudu Mungu ktk roho na kweli utajidhihirisha ktk mavazi yako pia. Mimi binafsi mtu hata aniimbie au anihubirie Biblia nzima lakini mwonekano wake uko vingine kwakweli nitakuwa na mashaka na wokovu wake hata na huduma yake pia.
  Ukiwa na Yesu ndani yako amani yake itatawala ndani yako, hutahangaika saaana kutaqfuta jinsi uvae ili uwe tofauti ili uonekane maana Roho aliye ndani yako atakufundisha yote.
  Binafsi ninaelewa muda na wakati tuliomo na ninatambua hata ktk Biblia wanawake walikuwa wakijipamba na kuvalishwa vito hata vya thamani kubwa mfano mtum ishi wa Ibrahim alipotumwa kumposea mke Isaka alimvisha vikuku vya dhahabu shingoni na mikononi, kama unaona ndani ya moyo wako unazo hela za kutosha kumtolea Mungu na kuvaa vito au mapambo mengineyo sio tatizo maana Mungu alisema nchi na yote yaliyomo ni yake sio ajabu watu kumiliki hivyo. Nywele za bandia, kusuka, vilemba nk vyote ni vitu vya nyongeza ambavyo mtu wa Mungu unapaswa kuvivaa kwa kiasi na kuendana na muda na wakati. Kuna wanaopinga sana mawigi lakini wanawake zao wanapiga lemba kuuubwa mno kichwani hata kusababisha kila jicho kutupwa kwako. Kama ni mtumishi watu watakazia macho hiyo kilemba kama ilivyokuwa kwa Musa na waisraeli ule uso wake uliong’ara na amri za Mungu.
  Nadhani mtumishi yoyote wa Mungu anapaswa kujua kupitia Roho mt namna gani avae, ajipambe ili kutowakwaza wengine ktk Kristo.
  Kuwa na kiasi pia ni muhimu wapendwa wengi wanajali mno mwonekano wa nje kuliko hata wanvyomiliki hii ndio kukosa utashi kabisa, utamkuta mtu kavaa nguo za bei mbaya sana, nywele na mapambo mengine ya gharama kisha anaomba watu nauli baada ya ibada mtu wa namna hii kweli ana roho ya namna gani ndani yeke? Kujipamba kwetu kuwa kwa staha na kiasi, sio kujiharibia afya yako, bajeti yako, mwonekano wako na pia kuwakwaza wengine. Ni mtazamo wangu.

 2. kwanza tujue nini maana ya kuongeza kitu,katika kitu unakuwa unamaanisha kukosoa kwamba yule aliye fanya cha mwanzo amekosea alitakiwa kufanya huvi.na tujue kuwa kitu bandia sio halisi japo kuna halisi yake,unaposema kuwa kujikwatua,kuvaa nywele za bandia ukavaa,ukaongeza makalio ya bandia nk.vyote hivi wewe mkristo uliyeokolewa na Yesu na ukamjua kuwa ni Bwana wa yote.unapofanya hivyo unakuwa unamkosoa Mungu aliye kuumba ukimaanisha kuwa Mungu alikosea kuniumba hivi alitakiwa aniumbe nikiwa hivi.biblia inasema yeye ni Mungu awezaye kufanya chochote kile na hakuna awezaye kumkosoa je! wewe ni nani ukamkosoa muumba aliyezifanya mbingu na nchi.

  Ukweli ni kwamba dunia imeingia kanisani na walokole wamekubaliana nayo dunia.biblia inasema kuipenda sana dunia kumpenda Mungu hakumo,jamani haya mambo yote unayo oona kuvaa mawigi,kuweka kucha za bandia,kuvaa nguo za kubana,kujikwatua na mengine yote ni shetani kabisa ndani mwa mtu.muda wa kujipamba na kujikwatua mpaka kuwaza kuongeza makalio, mwanaume kujikwatua,wakati dunia inakwenda mwisho Yesu karibu kuja unaupata wapi?.ebu tuone sifa za mtu kahaba unazipata kwa habari ya jezeberi mama wa makahaba,kabla ya kwenda kumjaribu nabii wa bwana alifanya nini soma.alijipambaa ili amnase nabii wa bwana.sasa wewe mtu wa Mungu unataka kumjaribu nani? kama upo kanisani na unafanya hayo moja kwa moja jehanam kama hautabadilika….

 3. MUNGU HAANGALII HAYO BALI KAMA MIILI YETU NI HEKALU LA ROHO MTAKATIFU SIO HALI KUFANYA HIVO WALA MUNGU HAPENDI

 4. Our appearance is very important as it can also preach before,it is not true that a woman reading a praise with skintight can make people concentrate rather they will be bored and concentrate looking to her.Let us be care that the world can not devour the church because many thing of this world have yet came into the church and no body bother of it.

 5. wote wanaotetea kujichubua co dhambi wanatabia hiyo, MUNGU alikuumba kwa ajili ya utukufu wake, MUNGU aliweka rangi, kabila, na mataifa mbalimbali kwa makusudi yake, sasa wewe unaejichubua na kuwa mweupe ni sawa na chungu kinachomkosoa mfinyanz wake, hata kuweka kope BANDIA c vizuri, MUNGU yupo dunian wakati wote akiangalia kazi za mikono yake vyovyote ulivyo kwa MUNGU utukufu, sisemi msijirembe wala kujipodoa hiyo ni asili ya mwanamke, mm naongelea wanaobadilisha rangi zao na maumbile yao NI DHAMBI KUBWA KWA MUNGU NA PIA HAULEWEKI KWA MUNGU( Tazama nimemfanya binadamu mnyoofu lkn wamevumbua mavumbuzi yao, soma mhubiri 7;29)

 6. Bwana YESU asifiwe,

  Tunachotakiwa ni KIASI katika mambo.
  ukishindwa kulifanya hilo lazima tu utapingana na kweli ukiamini kuwa uko sahihi

  Tusome neno na kulitafakari

 7. My Conclusion:

  Here’s the point, folks: The New Testament repeatedly makes it clear that God wants inner purity and holiness. On at least one occasion (1 Tim. 2:9-10) Paul instructs women to be more concerned with that than with outward beauty. However, the New Testament never dictates any rules of apparel–whether it be clothing, jewelry, or make-up. For that matter, the OLD TESTAMENT never taught against make-up either. It’s just not there.
  Folks, holiness is necessary, but it works from the inside out. The Bible never gave any church the right to dictate standards of dress (such as no make-up). The Bible is the rule of authority, not us. If a woman has a problem with vanity and she feels that she needs to give up wearing make-up, then that’s between her and God. We have no right to create a universal rule that says make-up is inherently sinful, and women should not wear it. When we do that we are trying to force holiness into a person from the outside, and that just doesn’t work.

 8. Bwana asifiwe ndugu juu ya swali yako juu ya UREMBO pande yote mbili. Kama vile wababa na wamama.Kweli UREMBO sio zambi lakini matunda yake kama imekomala inazala zambi. kwa nini? ujuwe UREMBO ikipita sana inazala maringo na ndani ya maringo inakuwa kiburi na ndani ya kiburi na ndani yake pia kujisifu na ndani ya yote Tamaa ndio shina ya yote.na tujuwe kama watu wote hawawezi kuwa hali moja ama tabia moja na ndio kupotea njia kubwa.Fanya UREMBO na kumueshimu Mungu mafalio,kutembea, na kusema. Ndio enye inabeba IMANI yetu…………………………………….NA MIMI NAULIZA KUVAA DHAHABU IKO MACHUKIZO MBELE YA MUNGU ?

  MUBARIKIWE

  MONGA

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s