Je kila anayejiua anaenda Jehanamu?

Hapa karibuni nimekutana na maswali mengi sana. Nilikuwa na rafiki yangu wa karibu sana (msabato) ambaye alipata shida kidogo lakini kwa kuwa niligundua ni ya kiroho, nikaanza kumshirikisha neno na zaidi nikampeleka kanisani aonane na mchungaji. Alipowasili kanisani ghafla alikataa kuombewa na kumpokea Yesu, akisema kuwa anaamini Mungu ni mmoja. Hatukuweza kumlazimisha, baada ya miezi mitatu tukamkuta amejiua chumbani kwake kwa msaada wa Polisi. Katika ujumbe wake ambao aliniachia mimi ili nimfikishie kwa mchumba na familia yake, miongoni mwa aliyoandika ni haya ‘Nimejitahidi sana kuvumilia lakini nimeshindwa, nimeamua kutangulia mbele ya haki’

Ni katika jambo lililoniumiza sana katika maisha kuona nampoteza rafiki yangu kwa anakata tamaa ya maisha mpaka kujiua. Siwezi kumlaumu kwa kuwa ni siri nzito aliyoondoka nayo ila nilisikitika sana.. 

Sasa juzi nilikuwa nasoma makala iliyoandokwa na mchungaji mmoja (jina nalihifadhi) akisema kuwa si kila mtu anayejiua anaenda jehanamu sababu kinachompeleka mtu jehanamu ni ‘kutompokea Yesu’. Pia akasema inawezekana mtu akatubu kabla ya kujiua.

Akatolea mfano Samsoni katika Biblia (Waamuzi 16) ni miongoni mwa mfano wa mtu aliyejiua yeye mwenyewe na kusanyiko lote (the Philistines) baada ya kutubu na jambo lile limekuwa likionyesha ushindi mkubwa sana Mungu alioufanya kupitia Samsoni.


Mbarikiwe

Dada Imani

11 thoughts on “Je kila anayejiua anaenda Jehanamu?

 1. Jamani hili swali tusidhani kuwa ni jepesi, ni suala la kitheolojia zaidi. Kwa hiyo kuliendea kwa haraka kuna kukosea kwa urahisi sana. Lazima kwanza tukubaliane kujiua nini na jehanamu ni nini.
  Biblia hakuna mahali imesema moja kwa moja kuwa kujiua ni dhambi. Ila Biblia imesema usiue. Na ijulikane kuwa neno KUJIUA ni tofauti kabisa na neno KUUA.
  Nilikuwa sijawahi kufikiri kuwa Samson alijiua, lakini sasa nimegundua kuwa si yeye peke yake, kumbe ni pamoja na Yuda of course,pia Sauli ukisoma vizuri utagundua alijiua pia.
  Hebu kwanza tuangalie matukio ya watu hao halaf tujiridhishe kama ilikuwa ni sahihi au makosa mbele za Mungu kisha tuendelee.

 2. Bwana asifiwe.

  Nafikiri Samson si mfano mzuri wa kupendekeza katika mada hii. Ijulikane ya kuwa katika agano la kale wana wa Israeli waliishi wakipigana na Mungu akawasaidia kwa vita. Na Samson ni katika murorongo ule tu. Alikuwa vitani pamoja na kupoteza macho yake. Kila step ina fundisho kwa mukristo:
  -Samson alokuwa mnaziri wa Mungu: ilibidi afanye mambo Mungu alimtuma pamoja na kuhakikisha iko katika njia safi.
  -Samson alioa mwanamke mufistini umbalimbali na ukubaliano na wazazi wake. Hii ikasabisha macho yake yaondolewe..”Mithali 30:17 Jicho la mtu amdhihakiye babaye, Na kudharau kumtii mamaye; Kunguru wa bondeni wataling’oa, Na vifaranga vya tai watalila..”
  Zingatia hii inahusu nafsi tu na wala si roho. Mategemeo ya nafsi yake kufanikiwa duniani yalikuwa yamekwisha kabisa. Lakini bado yeye kuamua kujiua, sivyo angeliifanya kabla karamu ile ya kumtesa iwe. Hapa kitu alichokifanya kwa moyo wake mwenyewe ni kuzarau wazazi, naye amepata tayari malipo. Kuna hata watumishi wengi wanoazarau wazazi kwani labda wao si walokole…. Hange na nafsi jamani….
  -Samson, kwa kuangusha hiyo gorofa, ilikuwa mbinu tu za kuteketeza wafilistini wala si kwa kupenda kujiua. Mungu alijua kama kazi aliompa imefika mwisho, na kwamba inambaki tu afe, akampa tena nguvu ili afike mwisho ya kazi ingawaje nafsi yake ilikuwa imekwaa. Kujiua kwa Samson si tofauti na Daudi kuuwa Goliata, hio si zambi.
  Nafikiri kwamba Samson hakufanya kosa ya mauti ya roho. Alifanya kosa iliyompeleka kwenye mauti ya nafsi pamoja na kuondolewa macho.
  -Yuda, kwa kukamata hatuwa yeye mwenyewe kusaliti Yesu alianguka ndani ya zambi ipasayo mauti ya roho. Ndio maana akakuwa tayari amelaaniwa. Kujuta yake yaikuondoa laana. Ina maana hakutubu kweli kwani laana ilikuwa juu yake. Lliofwata ni kwamba hakutoa tunda ipasayo toba; akaamua yeye mwenyewe kujiua bila fununu hata moja ya kutimiza kazi ya Mungu. Huyu jamaa wakati alipotoa Yesu alitimiza maandiko, lakini alipojiua mwenyewe akasibitisha laana juu yake mwenyewe.

  Mada hata hivi inatosha jasho…. Tuendelee

  Mungu awabariki.

 3. Samson alijiua na kujiua ni kosa hivyo sisi hatuna namna tunavyoweza kusema Samson hana kosa ila Mungu mwenyewe ndiye anajua kama yupo Jehanam au Mbinguni. Yuda nae ana hatia ya kujiua na anastahili hukumu. ikumbukwe Yuda baada ya kumsaliti Yesu alitubu kwa kusema anajuta kwa kuisaliti damu isiyo na hatia na kurudisha vile vipande vya fedha, Math-27:3-5, pale alikuwa salama na ameshasamehewa lakini kosa lake baada ya hapo alienda kujiua. Kwahiyo kimsingi tunasema yupo Jehanam. kumbuka maelezo ya Bwana Yesu aliyosema ole wake yeye amsalitie mwana wa Adamu, ingekuwa heri kwake mtu yale kama asingalizaliwa Marko-14:21.

 4. Ninavyofahamu mimi ni kuwa hakuna mtu anayeweza kujiua kutokana na sababu NZURI. Yaani kwa kuwa mtu amekutana na hali fulani nzuri, au kafurahishwa sana na jambo fulani ndipo anaamua kujiua! Bali mtu hufikia uamuzi wa kuamua kujiua kwa sababu kuna jambo fulani LIMEHARIBIKA!…….

  Kwa kuwa kuna kitu fulani kilichokuwa kimekusudiwa kufanyika kimefanyika vinginevyo, au kwa kuwa amechoshwa na kuteseka na ugonjwa au maradhi fulani, au mwingine kwa kushindwa kuvumilia kuhusu jambo fulani (kama huyo aliyetajwa mwenye mada), ndipo mtu HUAMUA kujiua! Kwa maneno mengine mtu anayefikia uamuzi wa kujiua MOYO WAKE HUWA TAYARI UMESHAHARIBIKA!

  Kukata tamaa ni silaha anayotumia shetani kutujaribu watu. Kushindwa kuvumilia, kuchoka, kukosa matumaini, yote ni mambo ambayo shetani huyatumia ili kunasa mtu. Ayubu wakati anajaribiwa, mke wake alimshauri AMKUFURU MUNGU AFE, YAISHE. Hilo lilikuwa ni jaribu la kumkatisha Tamaa Ayubu ili aondoe tumaini lake kwa Mungu. Kumkufuru Mungu ilikuwa sawa na kujiua, kwa Ayubu!

  Sasa kama mtu anayefikia uamuzi wa kujiua huwa moyo wake umeshaharibika, ameshakata tamaa, imani kwa Mungu imekwisha, amepoteza tumaini kabisa nk, kwa hali ya namna hii SIAMINI kama mtu wa namna hiyo anaweza kuwa bado ana usafi wa Moyo wa kuweza kuingia mbinguni. Hakuna mtu anayemwamini Mungu anayeweza KUJIUA.

  Mtu huwezi fukuzwa kazi halafu ukaamua kujiua ikiwa bado unamtumaini Mungu. Sawa, kazi imekwisha lakini Mungu yuko wapi? Mungu yuko juu ya vitu vyote. Unakuta mtu anajiua halafu anaacha ujumbe eti kwa sababu “mpenzi wake alikuwa amemtosa”. Ukisikia hivyo ujue hizo ni anga za shetani kabisa. Eti mtu kapata hasara kubwa katika biashara hadi anaamua kujiua. Hapo kuna tumaini la Mungu kweli?

  Hata kama mambo yataharibika vipi, yuko Mungu, ambaye ndiye anatakiwa kuwa tumaini la pekee! Mungu yu juu ya vitu vyote. Kama ni kujiua Ayubu ndiye angejiua, kwa kuwa kila kitu kilikwenda vibaya. Mambo yake yote yaliharibika. Mali iliharibika. Familia iliharibika. Mwili wake ukaharibika. Roho tu ndiyo haikuguswa!

  Kwa hiyo mtu anayejiua huwa ameshakuwa mbali na Mungu tayari hata kabla hajakata roho! Na katika hali ya namna hii ni vigumu sana kuingia mbinguni!

  Tukisema mtu anaweza kutubu kabla hajajiua sidhani kama tutakuwa sahihi. Labda tuseme mtu anaweza kutubu kabla hajakata roho. Mfano mtu alikunywa vidonge kisha wakati anahangaika ndipo akatubu. Lakini ya nini yote hiyo? Kwa nini mtu ukose tumaini hadi uamua kujiua? Lakini hata kama itatokea hivyo hiyo inaweza kuwa neema tu kwa wachache mno, kwa kuwa mtu anapofikia kujiua moyo wake huwa umeshapagawa na roho mbaya, mi naamini hivyo. Kwa hiyo kunaweza kuwa na nafasi ndogo sana ya kurudi katika hali ya kawaida ili mtu atubu.

  Suala la Samson, mimi siami kama alifanya vile kwa kuwa ALIKUWA ANAJIUA. Samson HAKUJIUA. Alikuwa anawaua Wafilisti. Lakini kwa kuwa naye alikuwa ndani ya jengo lile ndiyo maana naye akafa.

  Waamuzi 16:30 “Samsoni akasema: Na nife pamoja na hawa Wafilisti. Akainama kwa nguvu zake zote, ile nyumba ikawaangukia hao wakuu, na wati wote waliokuwa ndani yake. Basi wale watu aliowauwa wakati wa kufa kwake walikuwa wengi kuliko aliowaua wakati wa uhai wake”

  Maandiko hayo yanaonyesha jinsi ambavyo lengo la Samsoni lililvyokuwa, yaani KUWAUA Wafilisti. Na kwa kuwa naye alikuwa ndani ya jengo lile ndiyo maana akasema tu “Na nife pamoja……”.

  Kwa hiyo sioni kama ni sahihi kabisa kusema Samson aliamua kujiua. Na sidhani kama kuna andiko lolote linalotoa matumaini kwa mtu anayejiua!

  Tuendelee kujifunza.

 5. Dada Imani, Bwana Yesu apewe sifa?

  Nadhani kuna watu wengi wapo hapa duniani bila kuelewa kwa nini wako hapa duniani?

  Ukijua kwa nini upo duniani wala huwezi kujiua. Wote wanaojiua au kuua wenzao wana akili finyu na bongo zao na roho zao zina ugonjwa wa kupungukiwa uwezo wa kufikiri kwa kina na kupata majibu ya “KWA NINI TUPO DUNIANI?”

  Naomba nikusaidie majibu ya jumla ya kwa nini tupo duniani?

  1. Tupo duniani ili kuifanya dunia hii iwe mahali pa kupendeza viumbe wote kuishi. Kwa kuboresha makazi yetu, kwa kupanda miti na majani, kwa kupanda bustani nzuri za matunda na miti ya dawa, kwa kuilima ardhi hii na kuitunza.

  2. Tupo duniani ili kuwatumikia watu wengine. Mtu asiyewatumikia wanadamu wenzake huyo haelewi sababu ya kuishi duniani. Unapoamua kujiua unakuwa umeingia na pepo linalokuonesha kwamba, dunia nzima wewe ni mbaya na hakuna awezaye kukuona na kukusaidia mateso uliyonayo.

  3. Tupo duniani kutimiza lengo la Mungu la kuhakikisha dunia inakaliwa na watu. Isiwe ukiwa.

  4. Tupo duniani ili kuendeleza kizazi cha wanadamu duniani kisitokomee kabisa. Ukiamua kujiua unakuwa umetuma ujumbe kwa Mungu kwamba hutaki duniani iwe na watu, bali iwe na ukiwa bila ya watu.

  6. Tupo duniani ili kushawishi viumbe wote wamwabudu Mungu muumba wa vyote. Unaweza kufanya hivyo kwa kufanya ibada za kumwelekea Mungu muumba wa mbingu na nchi na kuwafundisha wanadamu wenzako kumwelekea Mungu wako Mkuu na kuachana na miungu wengine.

  7. Tupo duniani ili kula mema ya nchi yaliyoumbwa na MUNGU ambayo twayakuta tunapozaliwa, tunapowaheshimu wazazi wetu na kumtii Mungu. Ukiona mtu anajiua ujue hakuwa anawaheshimu baba na mama yake. Maana imeandikwa, waheshimu wazazi wako upate heri na kuishi miaka mingi duniani. Kama unajiua utapataje heri na kusihi miaka mingi?

  8. Tupo duniani ili kutawala viumbe wote. Mwanadam ni mtawala wa wanyama, samaki, kuku, mbwa, kware, nguruwe, paka, panya, sisimizi, nk. Hebu anza kutafuta kuku au mbuzi au ngombe uwatawale hapo ulipo na utapata raha nafsini mwako kwa kutawala viumbe hao. Mtu asiyejifunza kutawala viumbe wengine ataishia kuishi maisha ya kukata tamaa na kuamua kujiondoa duniani.

  Ukishaelewa hayo ya kwa nini upo duniani natumaini hautajiondoa. Utajiondoaje duniani wakati hata hujatimiza miaka 70 au 80 anayoitaka Mungu kila mtu aifikie?

  Kama unakufa au kujiua kabla ya miaka 70 au 80 umefanya dhambi kubwa ingawa sina maana kwamba ukitimiza umri huo wa miaka 70 au 80 ujiue au wakuue. Uhai wa mtu wapaswa kulindwa kwa gharama yoyote.

  Karibuni kwa mjadala zaidi. Barikiwa zaidi.

 6. Bwana Yesu asifiwe ,Napenda kuchangia swali la dada Imani,Nikinukiszia na Jehanam wanakwenda watu gani?Ni wale waliokiuka au wasiofata maandiko au neno la mungu,sasa basi Tukiangalia amri za mungu alizompa Musa katika kitabu cha kutoka ile ya pili inasema usiue,mtu anayejiua that means amekiuka amri ya mungu,ameutoa uhai wake kwa matakwa yake mwenyewe huyo moja kwa moja ni jehanamu,hata kama ukatubu halafu ukachukua uamuzi wa kujiua bado uko tofauti,ni sawa sawa umeruka majivu ukakanyaga moto,kujiua ni roho ya mauti inamwingia mtu anaona bora akatishe uhai wake ndipo atapata solution ya tatizo lake,kumbe anakwenda kukumbana na hukumu iliyo kuu zaidi ya hiyo,maana roho zote zitakazokwenda jehanamu zitajitambua si kwamba mateso ndio yamekwisha alivyochukua uamuzi wa kujiua,so many people wanaamini kuwa bora afe aondokane na mateso ya dunia hii,hawajui kuna maisha mengine ya milele unakwenda kuyaanza kama ni jehanamu au ya uzima wa milele kulinganana matendo yako yalivyokuwa hapa duniani,ukisoma ufunuo 21:8 inasema bali waoga ,wasiamini,wauaji,wazinzi na waabuduo sanamu sehemu yao ni ziwa liwakalo kiberiti ambayo ndio Jehanamu.Barikiwa woote,AMEEN!

 7. Kitendo 7cha kujiua ni dhambi kwasababu unakuwa umeweka matumaini kwako si kwa Mungu.soma flp 4:6-7,mt 11:28 YESU anasema tumpelekee aja zetu so rafiki yako alijitumainia yeye ndiyo maana akajiua ukisoma 2the 7:10 “Maana huzuni iliyo kwa jinsi ya Mungu hufanya toba liletalo wokovu lisilo na majuto; bali huzuni ya dunia ya dunia hufanya mauti” MAUTI amemaanisha kifo . rum 6:23 kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya MUNGU ni uzima wa milele katika kristo YESU BWANA wetu.ufu 2:8 Bali waoga , na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu na waongo wote,sehemu yao ni ktk lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. hii ndiyo mauti ya pili .
  mwisho kutokuamini kama rafiki yako alivyo shindwa kuamini kwamba YESU atampumzisha na mizigo yake na yeye kujitumainia mwenyewe nakuamua kujiua kutokana na maandiko ATAKUWA JEHANAMU kujiua kwa namna yoyote utajikuta upo jehanamu atakama umeokoka miaka 100 KUJIUA NI KUTOKUWA na imani NA YESU ambaye amesema NJOONI YETU MSUMBULIKIWAO NA MIZUNGO NAMI NITAWAPUNZISHA’ mwisho soma walaka wa paulo kipindi walipokuwa safarini kwenda asia walipopatwa na maswaibu paulo alijitumainia nafsi yake lakini alimwomba MUNGU amsamee kwani uai wake ulikuwa si mkononi mwake bali ni kwa BWANA hivyo basi mkristo kwa namna yoyote ile usijitumainie kwa jambololote bali kwa kuomba na kusali.kuhusu samson ni kitu kingine yeye alitoa uai kwa ajiri ya watu wake lakini sisi NI YESU tu aliyeutoa uai wake kwa ajiri yetu SOTE kwaiyo akuna sababu ya MWANADAMU kujitoa uai wake kwaajiri ya watu wake HISIPOKUWA KWA YESU PEKEE.AMEN

 8. Shalom, nafikiri title haijakaa vizuri, nilikuwa nataka ieleweke kama ‘Je kila anayejiua anaenda Jehanamu’? Ntamuomba dada Maria kama ataweza kuchange.

 9. Sijakupata au kwa kifupi kama article yako hujamalizia vile……. hitimisho ni Je kujiua siyo dhambi? Au inakuwa dhambi ukijiua kabla hujampokea Kristo? Na ile amri inatuambia “usiue” je?

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s