TAMKO LA ASKOFU MKUU WA TAG, KUHUSU MATUKIO YANAYOASHIRIA UVUNJIFU WA AMANI NCHINI

 

Kwa kipindi kirefu sasa kumekuwa na mfululizo wa matukio yanayoashiria uvunjifu wa amani, umoja na utengamano wa taifa letu la Tanzania, haya ndiyo yanayonisukuma kutoa tamko hili leo ili kuonya na kushauri.

Katika siku za karibu kiumeibuka makundi mbalimbali ya kidini ambayo yalianza kutoa matamko yenye kuchochea ghasia za kidini Tanzania, na pengine kauli hizo ndizo zinazotimizwa kwa vitendo hivi sasa.

Miongoni mwa matukio hayo ni:

Januari sita mwaka huu, kikundi kimoja kinachoitwa JUAKATA, kiliitisha kongamano la kujadili katiba mpya Tanzania, kwa upande wa Waislam. Katika  kongamano hilo lililofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam kauli zifuatazo:

1.     Lazima Rais ajaye atoke Zanzibar

2.     Kukabiliana na ukuaji wa kasi wa dini ya Kikristo

3.     Kupinga Muungano ili kuupa nguvu Uislamu

4.     Kupigana kufa na kupona kutetea maslahi yao wakati huu wa kuandaa katiba mpya.

Kauli hizo zilitolewa na Sheikh Nasor Mohameed, kutoka Zanzibar, ambaye alikuwa mgeni rasmi. Baadaye zikaandaliwa kanda za CD zilizosambaza ujumbe huo.

Uchunguzi  unaonesha kuwa miongoni mwa makanisa yaliyochomwa hivi karibuni huko Zanzibar ni ya EAGT, Elimu Pentecost  na TAG, Anglikana, Katoliki na FPCT, hivyo kujenga taswira ya ubaguzi wa kidini ambao kama hautapatiwa dawa unaweza kuligawa taifa la Tanzania kama ilivyotokea Nigeria na kwingineko barani Afrika.

Hofu yangu ni kuwa, roho hii ya ubaguzi wa kidini ambayo Baba wa Taifa hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere aliifananisha na dhambi ya kula nyama ya mtu, imekuwa ikiyatafuna mataifa ya Afrika kama ifuatavyo:

1.      Mwaka  2000, vuguvugu la kuanzishwa kwa utawala wa Kiislamu (Sharia), lilianza kwenye majimbo ya Kaskazini mwa Nigeria, miaka michache baadaye majimbo kadhaa yakajitangazia sheria hizo na tangu wakati huo kumekuwa na mapambano yasiyoisha. Takwimu zinaonesha kuwa katika miaka ya karibuni zaidi ya Wakristo 500 wameuawa kikatili na makanisa kuchomwa moto.

2.     Roho hii imekuwa ikienea kwa kasi katika maeneo mbali mbali ya Afrika ambapo imelikumba taifa la Mali, majimbo ya kaskazini tayari yametangaza  kujitenga na kuna vuguvugu lenye kuhusisha mapigano ya silaha.

3.     Itakumbukwa kuwa wiki chache tu zilizopita vuguvugu hili la kudai utawala wa kidini liliibuka nchini Kenya ambapo watu wanaojiita wanaharakati walianzisha madai ya kutaka eneo la Pwani kujitenga na Jamhuri ya Kenya na kujitangazia taifa la Kiislamu.

4.     Ni wakati huu ambao kundi la Uamsho linalopinga kuandikwa kwa katiba mpya kabla ya kuitishwa kwa kura ya maoni  ili wanzazibar waamue kuhusu Muungano liliibuka na kuanzisha ghasia Zanzibar ambazo zimepelekea makanisa kadhaa kuchomwa moto na mali kuharibiwa, huku watu wa bara wakitishiwa maisha.

      USHAURI WANGU KWA SERIKALI NA VIONGOZI WA DINI

Ni wajibu wa kila Mtanzania kutii sheria  na mamlaka kwa kuwa zimewekwa/kuruhusiwa na Mungu, hivyo kuziasi ni Kumuasi Mungu, yaani ni dhambi. Hivyo kila Mtanzania anastahili kukumbuka wajibu wake wa kutii mamlaka.

Viongozi wenzangu wa dini wakumbuke kuwa wana wajibu mkubwa katika jamii, na jamii inawasikiliza hivyo ni vyema wakawa makini katika matamshi na maelekezo yao  ili wasiwe chanzo cha kuchochea vurugu za kidini na uvunjaji wa amani.

Ni vyema wakati huu wa kuandikwa kwa katiba mpya, kila kikundi kikafuata utaratibu uliowekwa badala ya kuchochea ghasia ambazo madhara yake yatawakumba watanzania wote ikiwa ni pamoja na wao wenyewe watoto na wajukuu zao.

Pia ningependa kuwashauri viongozi wa serikali kusimama imara katika kusimamia sheria na haki, na kuepuka kauli au vitendo vitakavyofanya baadhi ya watanzania kudhani kuwa hawatendewi haki.

Ni vema ieleweke kuwa matukio kama haya ya uvunjaji wa amani yasipodhibitiwa na kukomeshwa haraka yanaweza kuumba chuki ambayo inaweza kuibua mlipuko mkubwa na machungu kwa wananchi na matokeo yake yakawa mabaya kwa Taifa zima. Hekima na busara inatufundisha kuwa tusipoziba ufa tutajenga ukuta.

Ni vyema wenye dhamana ya kuongoza wakakumbuka kuwa wanawajibu mbele ya Mungu aliyewaweka au kuwaruhusu kuingia madarakani na siku moja watatoa hesabu mbele zake.

Mwisho, natoa wito kwa watanzania wenzangu tuulinde umoja, amani na utengamano wa taifa letu, tuikimbie  dhambi ya ubaguzi kwa kuwa tukiiruhusu itatuangamiza sote. Tuliombee taifa letu  na kukiwa na mbegu ya chuki tuimalize kwa njia ya majadiliano na vikao vya pamoja vinavyohusisha viongozi wa dini zote na serikali pia.

Imetolewa leo 28/05/2012
Na Dk. Barnabas Mtokambali
Askofu Mkuu wa TAG
Advertisements

9 thoughts on “TAMKO LA ASKOFU MKUU WA TAG, KUHUSU MATUKIO YANAYOASHIRIA UVUNJIFU WA AMANI NCHINI

 1. Wapendwa Waislam, Asalaamalyekuum?

  Napenda kuwakumbusha waislam wote nchini Tanzania kurejea kwenye maandiko matukufu ya Munyazi Mungu Subhaaanah Wataala. Waislam wote hata na wale wasiokuwa waislam wanaoamini kwamba .. hakika Qur’an ni kitabu cha MWENYEZI MUNGU, Mola Muumbaji hawawezi kutenda kinyume na Maandiko Matuku ya waislam.

  KUHUSU KASHFA ZA KUELEKEZWA DINI NYINGINE. Mwenyezi Mungu amewakataza waja wake kwamba wasitukane dini au imani za watu wengine. Au wewe mwislam rafiki yangu huwa husomi aya hizi? Au ukizisoma unazitolea ufafanuzi wa vipi? Hebu soma aya hizi uone mwenyezi Mungu anavyowakataza waislama kutukana dini ya wengine……

  SURATUN AN NAHL 16: 125

  Nanukuu, “….Waite (waite watu) katika njia ya Mola wako kwa hikima na mauidha mema, na ujadiliane nao kwa namna iliyo bora (siyo kwa kuwatukana wao au kutukana dini yao. Kwa njia hii huwezi kumvuta mtu) Hakika Mola wako ndiye anayemjua aliyepotea katika njia yake, naye ndiye anayewajua walioongoka.

  Hata kama unaona kama vile Wakrsito wanaabudu kinyume na Imani yako, Bado Qur’an tukufu haijakuruhusu kuwabeza wala kuwakejeli. Kufanya hivyo ni kujiletea hukumu kwako na utaenda finale Jihanam kwani Mwenyezi Mungu amekukataza kuwatukana na kuwachomea au kuwaharibia mali zao. Hebu sasa soma aya hii:

  QUR’AN SURAT AL AN-AM 6: 108

  Naomba ninukuu kwa Kiswahili kama ilivyoandikwa, “…….Wala msiwatukane wale ambao wanaabudu, kinyume cha mwenyezi Mungu, wasije wakamtukana Mwenyezi Mungu kwa jeuri zao bila kujua. Namna hivyo tumewapambia kila watu vitendo vyao. Kisha marejeo yatakuwa kwa Mola wao. Naye atawaambia (yote) waliyokuwa wakiyatenda”. Mwisho wa kunukuu.

  Wewe mwislam hizi aya huwa unaziacha wapi pale unapopandwa na jaziba za Ibilisi hadi kuwatukana au kuwachomea Biblia Wakristo? Huoni kwamba unajigeuza kuwa Mshamba na mpumbavu anyeenda kinyume na Qur’an tukufu?

  KUHUSU HOJA YA KULAZIMISHA WATU KUINGIA KATIKA UISLAM

  Mwenyezi Mungu amewakataza waislam wote duniani kutojaribu kuwalazimisha watu wote waingine katika dini ya Kiislam. Sisi tunashangaa kuona waislamu wanataka Zanzibar yote na Tanzania Bara iwe nchi ya kiislam wakati ni kinyume na maagizo ya Mwenyezi Mungu. Hebu soma aya hii ujionee……

  QUR’AN SURAT AL BAQARAH 2: 256

  Aya hii imewakataza waislam wote duniani kote kujaribu kuwalazimisha watu waingine katika Uislam, naomba ninukuu kwa kiswahili tena hapa…..

  “Hakuna kulazimishwa (mtu kuingia) katika dini. Uongofu umekwisha kupambanuka na upotofu. Basi anayemkataa shetani na akamwamini mwenyezi Mungu bila shaka yeye ameshika kishiko chenye nguvu kisichokuwa na kuvunjika. Na mwenyezi Mungu ni mwenye kusikia mwenye kujua”. Mwisho wa kunukuu.

  Pia naomba uongezee kusoma QUR’AN SURAT YUNUS 10: 99-100

  Inasema hivi, “Na kama angalitaka Mola wako (kuwalazimisha kwa nguvu kuamini) bila shaka wangaliamini wote waliomo katika ardhi (asibaki hata mmoja) (Lakini Mwenyezi Mungu hataki kuwalazimisha watu kwa nguvu) Basi je, wewe utawashurutisha (utawashurutiza) watu kwa nguvu hata wawe Waislamu?

  Na hakuna mtu anayeweza kuamini isipokuwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Naye hujaalia uchafu uwafike wale ambao hawatumii akili zao”

  Mwislam safi ni yule mnyenyekevu ambaye hayuko tayari kulipiza kisasi. Nashangaa waislam wenye roho za kisasi. Hivi wanatokea wapi? Wanasoma Qur’an ipi. Hivi kuna Qur’an ngapi duniani? Kuna dini ngapi za Kiislam? Waislam naomba mnipe majibu. Mbona aya za Munyazi Mungu zinapinga vitendo vya kuchoma makanisa, kulipiza kisasi na kupora mali za wengine?

  Hebu soma aya hii nayo uone inavyowaelekeza waislam kuishi kwa upole na upendo.

  QUR’AN SURAT AL FURQAN 25:63

  Naomba ninukuu kwa Kiswahili, “….Na waja wa Mwenyezi (anaowapenda ni wenye sifa hizi): Ni wale wanaokwenda (na kurejea kwa unyenyekevu; na wajinga wakisema nao (maneno mabaya) huwajibu (maneno ya) salama”.

  Wapendwa Waislam, naomba kama kuna ajenda ya kisiasa isichanganywe na dini hii tukufu ya Munyazi Mungu. Ombeni usajili wa chama cha siasa ili ijulikane kwamba ni siasa mnazozitaka badala ya kutumia mwamvuli wa kikundi cha dini kufanya siasa za kijinga za kuchoma Biblia au makanisa.

  Mshukuruni Mungu kwamba viongozi wa Kikristo wengi wao wanaelewa Maandiko yote ya Biblia na Qur’an vinginevyo nao wangelipiza kisasi na nchi nzima ingelipuka kwa vita vya kidini.

  Hivi wewe unapochoma Biblia moja unadhani umwekomoa wakristo au umejikomoa wewe mwenyewe? Mbona pale Mwanza ilisikika kuwa kuna mganga wa jadi alieamua kujiunga na Ukristo na akakubali yeye mwenyewe manyangala yake ya uchawi yachomwe moto. Waislam bila kufanya utafiti wa kina wakaambizana eti Qur’an imechomwa mkaanza kuandamana kila kona za jiji la Mwanza na kutaka Jiji zima likose amani na baadaye ikaonekana kwamba hakuna Quran iliyochomwa.

  Mbona wakrsito wao wanapochomewa Biblia hawaingiwi na mashetani ya kuchoma misikiti yenu? Kwani wao haiwaumizi roho zao? Wakristo nadhani wanayo busara nyingi na wanaelewa zaidi yenu.

  Someni QUR’AN VIZURI NA WALA MSIWE NA TAFSIRI POTOFU.

 2. Askofu kanena na kuonyesha data ukumbini Diamon. Serikali iwe sikivu kushughulikia matamko kama hayo. Sisi nasi tutatii alichosema Askofu Dr. Barnabas Mtokambal “tuikimbie dhambi ya ubaguzi kwa kuwa tukiiruhusu itatuangamiza sote”. Tuliombee taifa letu. HAYA NI MANENO YA HEKIMA Watanzania tujitoe kuitakia nchi etu amani na kuilinda amani kama mboni ya jicho.

 3. Askofu Mungu akubariki sana kwa tamko hil.
  Tulitegemea Rais shein naye angetoaa tamko.
  Hicho kikundi kilichokaa Diamond Jubilee ni cha ajabu kweli. Wao wanataka Rais ajae atoke Zanzibar
  upande mwingine hawataki muungano,
  Sasa kama hawataki muungano kwa nini Rais ajaye atoke Zanziba tena? Mimi nadhani nikikundi hicho kifuatiliwe na kihojiwe.

 4. Mungu akubariki mtumwa wa Bwana kwa kuujua wajibu wako mtumishi.Mungu wetu hapendi manung`uniko ila anataka tulie aba kwa ajili ya taifa letu.Hakutakuwa na maana kabisa kama hakuna upendo kati ya watu wa nchi moja.Hivyo umefanya la maana sana Mtumishi kutoa tamko ili Mungu atakapoamua kuingilia kati wasije wakajitetea.Mwenye kuua naaue sana,mwenye kudhulumu naazidi sana,mwenye kudharau naadhidi sana kwakuwa siku inakuja na kilamtu atatoa jawabu la mambo aliyoyatenda.Bwana Mungu naye atahukumu kwa haki.Pole sana Mtumishi kwa kazi ya Bwana.Wala usinyamaze.Watanzania na tumwombe Mungu kwakuwa anaweza kufuta kila roho za mpinga Kristo.Na ninakemea kila roho za yezebel zinazolifuatilia kanisa KWA DAMU YA YESU.Roho Mtakatifu uchunguze nchi hii na Kusudi la Bwana lisimame mahali pake.Amen

 5. Shalom ni kweli tunapaswa kuingia ktk maombi hasa kwa ajili ya kanisa, Tukitaja Tanzania ni pamoja na Zanzibar, iwapo nyumba ya Mungu inanajisiwa na watu wanashindwa kumwabudu kwa hofu ni kitu kibaya cha kumchukiza Mungu. Sisi ni kama tunakaa ndani ya sodoma na Gomora kipindi cha Lutu tumewaacha hawa watu wanaoitwa watanzania wakipotea hadi wanaleta chukizo mbele za Mungu kama hivi.

 6. Mungu akubariki sana Askofu Mkuu wa TAG kwa kwa Tamko hili muhimu wakati huu kwa Taifa letu Linalowalenga viongozi wa Dini na Serikali. Asante kwa maneno mazito na ya hekima ndani yake ambayo viongozi wenzako kama watayasoma na kutafakari vizuri naamini hatua muhimu za pamoja zitapaswa kuchukuliwa ili kunusuru hali ya usalama wa Taifa letu Zuri la Tanzania. Naomba viongozi wote wa Dini Tanzania ikiwa ni pamoja na wa Serikali yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania waungane pamoja kulaani na kukemea vitendo vinavyoashiria uvunjiivu wa amani katika Taifa tulip. Naomba Mungu awoongeze na kuwapa hekima kubwa katika kulitengeneza jumbo hili muhimu. Baba Askofu Dr. Barnabas Mtokambali hakuishia hapo, bali ameomba watumishi wote waungane kuliombea Taifa liepukane na majanga ya uvunjiivu wa amani. Naomba viongozi wa dini zote shime tuungane pamoja katika kuliombea Taifa letu. Amen!

 7. Amina mtumishi,
  tunashukuru kwa tamko hili maana naona viongozi wengine hawasemi chochote kweli tunawajibika kwa jamii nzima ya Tanzania. Hizi ni roho za watanzania zinazopotea ktk chuki, kwanini tumeamua kujirundika miji kama Dar Arusha Mwanza nk lakini hakuna huduma za kutosha visiwani, na wala hakuna kujitoa kwa hao waliopeleka huduma huko wakipatwa na matatizo kama hivi. Tutatoa hesabu yetu siku y mwisho jinsi tunavyoacha vibanzi hivi machoni mwetu. shime tuamke watanzania hawa wanatuhitaji, kwa upendo tukihubiri injili hii wataokoka la tutavuna chuki waliyonayo na wanayohubiriwa na wengine. Mbarikiwe

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s