Maombi kwa ajili ya kanisa la Tanzania 1 June, 2012

Kuanzia tarehe 1 June 2012 tunaanza maombi maalumu kwa ajili ya toba, amani, upendo na ustawi na kukua kwa kanisa Tanzania. Tunamkaribisha yeyote atakayeweza kushiriki nasi popote pale ulipo, atakayeweza kufunga atafunga, ni maombi ya mwezi mzima!

Mistari ya kusimamia
2 Wafalme 5: 16-17
2 Nyakati 7: 14-18
Nehemia 1: 4-6
Nehemia 2: 4 na Nehemia 2: 7-8
Nehemia 4: 7-8 na 1Timotheo 2: 1-6

Mjipe moyo ndugu zetu wa Zanzibar, aliye ndani yetu ni mkuu kuliko wote!

Mungu Ibariki na kuilinda Tanzania!

–Rose Lusinde

Advertisements

13 thoughts on “Maombi kwa ajili ya kanisa la Tanzania 1 June, 2012

 1. Bwana Yesu asifiwe wapendwa!
  Haleluyah haleluyah!
  Napenda kumshukuru Mungu kwa kuwa nasi kipindi chote hiki cha maombi, napenda kumshukuru kila mmoja wwenu aliyesimama zamuni kuitikia wito huu kuombea kanisa, kuombea Taifa Tanzania. Maungu wetu mwema na azidi kuwabariki na akutane na haja za mioyo yenu, Yeye anasema atauwazia mema tu siku zote na pia tukimwita atatuitikia na ututonyesha makubwa na magumu tusiyoyawazia.
  Naomba tu kuwashirikisha maono yangu kuhusu haya maombi, wiki mbili kabla ya makanisa kuchomwa moto Zanzibar nilishiriki ibada ktk kanisa mojawapo, ktk ya ibada nilionyeshwa mchoro kama nyumba ya buibui au network habu tuseme kama kitovu cha kitu na kikisambaa pande zote, kisha sauti “Hili ni lango” kwa kweli nilishtuka nikawaza lango la kwenda wapi? lakini nilipotoka hapo na kurudi huku nikasahau, ajabu jumapili iliyofuata kanisani kwetu waliimba tenzi liko lango la mbinguni nsiye Yesu…ghfal nikakumbuka yale maono nikajiuliza kwanini mimi mbona siko huko tena…usiku nilipoamka kuomba kama kawaida nikafungua mtandao wa Habari leo juu kabisa ilikuw apicha ya kanisa limechomwa moto, niliogopa nililia na kumuuliza Mungu ni kwanini mbona ndio lango…..baada ya hapo niligundua kule kuchomwa moto kutaleta namna fulani ya upenyo kwa kanisa (lango) na sasa mimi ni ninahusikaje ilibidi nimuulize Mch husika akajibu ni kweli mara nyingi wamewatesa, wamebomoa, na si hapo tu kwingine kwingi ila na wao wanahisi Mungu anakwenda kutenda jambo sasa….
  Maombi haya niliwashirikisha wote ninawafahamu, ahdi askosfu wangu achingaji wote ninawajua bara na visiwani, wana SG nadani na nje na timu ya maombi, namshukuru Mungu nilipata support bila hata kueleza nini kimenisukuma….
  Wiki ya kwanza ya maombi ndio nilipomsikia Raisi Shein akisema “Ukristo ulianzia Zanzibar baada ya kukomeshwa biashara ya watumwa…” na hapo Kkoo ndipo watumwa waliuzwa ina maana na kukomeshwa ilikuwa hapo zanzibar pia
  Wiki 2 zilizofuata sikuona chochcote cha kukututia moyo….
  wiki ya tatu watu hata ndani ya chama tawala wakaanza kujidhihirisha wazi msimamo wao, na hata kudai waachiwe nchi nilijiuliza mengi nini mwisho wake
  wiki ya mwisho iliyopita ndipo mengi yamedhihirika, wakati nikiwa nimekata tamaa na nini kinaendelea na kuomba tuingie vitani na Mungu atuinulie wakuu nilikuwa na maana serikali lakini Mungu ameona zaidi ya sisi Yeye anajibu hata tusiyoyawazia. Kama mmefatilia Tanzania tumepewa onyo kufanya biashara na Iran, zaidi kutumia bendera zetu kuuza mafuta yao…..Mungu wetu Yeye anatuwazia mema hiki ndio kilichokuwa chanzo, basi tusichoke kuliombea taifa letu, tusichoke kuliombea kanisa, tuzidi sana kumhubiri Kristo ili watu wasidanganywe kwa Imani potofu zenye kujenga chuki na uuaji. Tuangalia Kenya ilipo tuendelee kusimama ktk zamu zetu. Mungu azidi kuwabariki nyote.

 2. Shalom shalom wapendwa!
  Ni wiki nyingine tena hii, ni wiki ya mwisho ya maombi yetu haya, bahati ni mwezi ambao wenye mamlaka pia wanakutana na kufanya maamuzi ya mwaka mzima.
  Bado hali ya kanisa sio imara na hali ya amani sio nzuri, hali ya uchumi ya walio wengi inakatisha tamaa, rushwa imejaa, haki hakuna isipokuwa kwa wenye pesa, kibaya zaidi walio na mamlaka ni kama wamepigwa na upofu: wanakimbizana na posho, vimada, itikadi, ujimbo nk hakuna aonaye hata mmoja……

  1. Tunapaswa kuwaamsha, tunapaswa kusimama ktk nafasi zetu kama ilivyokuwa kwa Mordekai kumwamsha malkia Esta asimame kwa ajili ya taifa lake:
  Esta 4: 13 – 14 Naye Mordekai akawaagiza wampelekee Esta jibu la kusema, Wewe usijidhanie kuwa wewe utaokoka nyumbani mwa mfalme, zaidi ya Wayahudi wote. Kwa maana wewe ukinyamaza kabisa wakati huu, ndipo kutakapowatokea Wayahudi msaada na wokovu kwa njia nyingine; ila wewe utaangamia pamoja na mlango wote wa baba yako; walakini ni nani ajuaye kama wewe hukuujia ufalme kwa ajili ya wakati kama huo?
  Hivyo nawasihi wapendwa tutumie nafasi zetu tulizomo kuombea kanisa Tanzania, kuombea roho zinazopotea gizani, kuombea wenye mamlaka wafunguke macho, kuombea haki na ustawi kuomba Mungu alegeze roho ngumu walizonazo hata hawasikii kilio cha wanyonge wanapoonewa.
  Nehemia 2: 17 Kisha nikawaambia, Mnaona hali hii dhaifu tuliyo nayo, jinsi Yerusalemu ulivyo hali ya ukiwa, na malango yake yalivyoteketezwa kwa moto; haya! Na tuujenge tena ukuta wa Yerusalemu, ili tusiwe shutumu tena

  2. Ni wiki ya vita pia juu ya wenye mamlaka ya giza, juu ya ngome za yule mwovu, juu ya mpinga Kristo. Tuvunje roho zote za kunyanyaswa, kunyimwa uhuru wa kuabudu, kufungwa kwa sababu ya Ukristo, umaskini, kutoamini, ujinga na roho za kushindwa; udini, ufisadi, ukabila nk
  Efeso 6; 13 – 20 Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.
  …………kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote; pia na kwa ajili yangu mimi, nipewe usemi kwa kufumbua kinywa changu, ili niihubiri kwa ujasiri ile siri ya Injili;

  3. Tumwombe Mungu afungue njia kwa kukua kwa Kanisa, kumiliki na kutawala. Tuwaombee watumishi wa Mungu ambao wengi wao hali zao ni duni wanashindwa hata kumtumikia Mungu kwa ukamilifu na amani. Tuombee kanisa liwezeshwe ili kuweza kupeleka injili sehemu zisizofikiwa bado, tuombe Roho mt aongoze na si kimwili, uwepo wa Mungu uwe dhahiri ndani ya kanisa Tanzania, Mungu akalipe macho na masikio ya kiroho kuweza kutambua na kusimama ktk kusudi lake.Tuombe Mungu akaliponye na kuliinua kanisa na taifa letu.
  2 Timotheo 2: 1 – 4 Basi, kabla ya mambo yote, nataka dua, na sala, na maombezi, na shukrani, zifanyike kwa ajili ya watu wote; kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, tuishi maisha ya utulivu na amani, katika utauwa wote na ustahivu. Hili ni zuri, nalo lakubalika mbele za Mungu Mwokozi wetu; ambaye hutaka watu wote waokolewe, na kupata kujua yaliyo kweli.

  2 Nyakati 7: 14 – 16 ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao. Sasa macho yangu yatafumbuka, na masikio yangu yatasikiliza maombi ya watu waombao mahali hapa. Maana sasa nimeichagua nyumba hii na kuitakasa, ili kwamba jina langu lipate kuwako huko milele; yatakuwako na macho yangu, na moyo wangu daima.
  Yeremia 29: 12 – 13 Nanyi mtaniita, mtakwenda na kuniomba, nami nitawasikiliza. Nanyi mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote……

  Tuombee taifa letu, tuombee kanisa, tuwaombee watumishi wa Mungu.

  Mbarikiwe nyote.

 3. Shalom wapendwa
  ni wiki ya pili sasa tuendelee kuiombea Tanzania,
  Mungu azidi kuonekana kiuchumi, kiroho ktk kanisa lake.
  Mavuno ni mengi sana sehemu nyingi bado hawajafikiwa na injili, hata kuliko na makanisa unakuta hamna watendaji siku za wiki au usiku ikitokea tatizo hivyo watu kugeukia nguvu za giza.
  Tumwombe Bwana wa majeshi alete watenda kazi shambani mwake, akatuinulie watumishi wa Mungu wenye kiu ya kuokoa watu na si wa mshahara.
  Tumwombe Mungu afungue milango ktk watu wake na kanisa lake ili kuwezesha kupeleka injili…..watahubirije wasipopelekwa?
  Tumwombe Mungu atupe kibali kanisa lake kwa wenye mamlaka ktk kumiliki, ktk fursa mbalimbali za kiroho na kimwili ili kuliwezesha kanisa kukua na kusonga mbele.
  Tuvunje roho zozote zinazokwamisha ukuaji wa kanisa Tanzania ushirikina, chuki, udini, matengano, umaskini na roho za visasi. Mungu akubariki kw akushiriki kuiombea nchi yetu.
  Mungu Ibariki Tanzania

 4. Amina Kevin tunashukuru tuendelee kuomba kanisa Tanzania likavuke vikwazo vyote vinavyozuia kukua roho za udini, udhehebu, mafarakano, uzinzi, ubinafsi, ukwasi, kushindwa, umasikini, roho za wivu na masengenyo nk
  Tumwombe Mungu atujalia roho ya ushindi, upendo, umoja, amani, utajiri, kuwezeshwa, kumiliki na kutawala. Tuombe kanisa liongozwe na Roho Mtakatifu na si kimwili, nguvu na uwepo wa Mungu uwe dhahiri.
  Katika Isaya 45: 1-5 Bwana Mungu anasema atatushika kwa mkono wake. atakwenda mbele yetu na kuangusha ngome. malango na milango ya shaba. Atasawazisha mabonde na milima.
  Joshua 1: Mungu anamwambia Joshua akisimama ktk njia yake hapatakuwa na mtu wa kusimama mbele yake au mkumzuia, anasema atakuwa pamoja naye siku zote za maisha yake. Tumwombe Mungu aonekane hasa ktk kanisa letu, ktk watumishi, familia, watoto wetu ambao ni taifa la kesho. Mungu akatangulie kila tufanyacho. Mungu akatubariki na kuturidhisha milki zake kama ilivyokuwa ahadi yake. Mungu akatupe hekina na nguvu ya kusonga mbele ktk kazi ya kueneza injili ktk Jina Yesu.
  Mungu awabariki nyote kwa kujitoa kuombea hili.

 5. Its true that we all decided to do this commitly but let every one of us note this
  .No one weak can go in war
  .No one forced to fight for himself/herself if he/she can’t fight.
  Mungu atutie nguvu maana ni Yeye pekee atushindiaye

 6. We keep on praying brethren. Remember “PRAY WITHOUT CEASING”.
  I think most of you heard and saw what they said “WE WILL FIGHT UNTIL IT IS UNDERSTOOD” -One of them.
  They mean they are doing what they do with all they can until they see their desire fulfilled. They have confidence in what they do and they are confident that “they are protected”, that’s why they can speak such words through media.

  SO WE SHOULD PRAY UNTIL WE SEE “RESTORATION” IN THE LAND. Darkness will never prevail against LIGHT OF GOD THE CREATOR.

  MAY GOD STAND FOR HIS PEOPLE IN JESUS NAME.

 7. Amen tukianza na toba Nehemia 1: 4-7
  kwani haya yanayofanyika ktk nchi yetu ni unajisi kwa kanisa la Mungu,
  tutubu kwamba hatukusimama ktk zamu zetu kuomba, kuhubiri, kujitoa kwa kanisa hadi sehemu ya nchi imekuwa hivi. Tumwombe Mungu atujalie uvumilivu na roho ya kusamehe na kuwaombea wote wanaolikosea kanisa la Mungu.
  Mungu wetu ni mwenye rehema anasema atasikia na kuturudisha tena nyumbani mwake, tuombe kwa ajili ya waliorudi nyuma, ambao hawamjui Mungu kabisa tuombe toba kwa ajili ya familia zetu wenza na watoto wetu. Toba kwa ajili ya kazi zetu, biashara na miliki zetu, Toba kwa ajili ya nchi, viongozi na wenye mamlaka, watumishi wa Mungu. Toba kwa ajili yetu tunapoenda kusimama mbele za Mungu kama kuhani aweze kutusikia. Mbarikiwe

 8. Amina, huu ni mpango mzuri sana. Ninawasihi tuunganishe nguvu zetu katika hili nae Bwana atajibu kwa “kuiponya nchi hii”. Wote walio ndani na nje ya Tanzania tuwe pamoja kama Jeshi linavyotakiwa. Mungu awatie nguvu wote watakaojitoa kumsikizisha Bwana.

 9. amen asante natumaini kila mmoja atasimama kwa zamu yake ikiwa ni pamoja na kuwaamsha wenzetu wote tuma ujumbe huu kwa wote unaoona wataguswa kuomba. Mbarikiwe

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s