Kusifu na Kuabudu Kwa Kiingereza

Vikundi vingi vya Kusifu na Kuabudu au Waongoza Vipindi vya Kusifu na Kuabudu, nchini Tanzania, hupendelea sana kuimbisha nyimbo za Kiingereza. Na hata wengine husema kuwa hupenda kuimbisha Nyimbo za Kiingereza kwa kuwa zina Nguvu za Mungu kuliko nyimbo za Kiswahili!

Je, Ni kweli kuwa Nyimbo za Kiingereza Zina nguvu za Mungu zaidi ya Nyimbo za Kiswahili?

Advertisements

29 thoughts on “Kusifu na Kuabudu Kwa Kiingereza

 1. Wapendwa
  msingi sio ni.lugha gani unaitumia ktk kusifu.
  Kwani wanaonena kwa lugha siwananena katika roho?
  nao pia wanaosifu.WASIFU KTK ROHO NA KWELI:YOH:4:24
  Je wewe unaabudu mungu ktk nini?
  je kuchunguza watu wanao mtumikia mungu kwa maono kadri mungu anavyowaongoza kumtumikia.

 2. SI KWELI KWAMBA NYIMBO ZA KIINGEREZA ZINA UPAKO WA KUTOSHA KULIKO ZA KISWAHILI
  LUGHA YA MTU NDIO ITAKAYOTAFUTA UKARIBU WAKE NA MUNGU..KAMA MTU ANAONA KUWA KIINGEREZA NDIO MUHIMU ZAIDI KUTUMIKA ,HAYO NI MAWAZO YAKE KWA KADRI YEYE ALIVYOONA KUWA INA UKARIBU NA UHUSIANO MKUBWA NA MUNGU
  NA NDIO MAANA HATA KUOMBA NI LAZIMA UOMBE KWA LUGHA UNAYOIELEWA NA SIO ILE USIYOIJUA.
  LUGHA INAMPA MTU UJASIRI WA KUAMINI KILE ANACHOKIOMBA KULIKO AKIOMBA KWA LUGHA ASIYOIJUA
  KADHALIKA NA KUABUDU AMA KUSIFU UPAKO HUSHUKA TU KWA KADRI YA IMANI YAKE INAYOAMBATANA NA LUGHA YAKE ANAYOIELEWA ZAIDI.

 3. Bwana Lwembe nimesikitika sana uliponiona kuwa nimepumbazika, yaani kwamba mimi ni mpumbavu. Nisema tu kwamba mimi si mpumbavu kama ulivyojaribu kusema, namjifunza Mungu vizuri na kwa umakini na niko so logical. Labda tu ni kwa vile hunijui na mimi sikujui ndio maana unawaza hivyo. Mimi huangalia mambo nje kabisa ya mapokeo na huwa sifuati mkumbo.

  Kwanza hakuna sehemu Biblia inasema kuwa ibilisi ndiye mkuu wa dunia hii. Ila kuna sehemu Yesu kamwita mkuu wa ulimwengu huu.(Yoh 14:30). Dunia na ulimwengu ni vitu viwili tofauti. Dunia ni sehemu na ulimwengu si sehemu ila ni mfumo. Kwa hiyo Yesu alimaanisha kuwa shetani ni mkuu wa mfumo wa uovu unaoendelea hapa duniani. Mkuu wa dunia ni Mungu.

  Umesema kuwa nisikurupuke na single ili kuwa super star. Lwembe nimekuwa worship leader kwa zaidi ya miaka 15, kwa hiyo unaponiambia nisikurupuke ni kwa vile tu hunifahamu nafananaje. Subiri utaniona na utaelewa kama nimekurupuka au niko under divine mission. Maana kama ingekuwa kukurupuka ungeshaniona.

  Hakuna mahali biblia imesema kanisa la kwanza au hata wayahudi wallimba nyimbo zao kwa style gani. Najua akina Petro na akina Paul waliimba ila sijui ni style gani.

  Ukristo sio utamaduni Lwembe, ila ni ile hali ya kuwa mfuasi wa kristo. Ambapo kila mfuasi hubaki na utamaduni wake. Yaani wewe ukiwa mkristo unaendelea kuongea lugha yako, unaendelea kula aina yako ya chakula, unaendelea kuvaa aina ya mavazi ya jamii yako, unaendelea kuimba nyimbo za style ya jamii yako.Na huo ndio utamaduni. Huwezi mhindi akaokoka ukamlazimisha aimbe kwa style ya kiyahudi. Ila kuna namna ya ufanano wa mambo fulani kwa wakristo wote. Soma kitabu kinaitwa “Music Through The eyes of Faith” utagundua mambo mengi sana.

  Halaf hakuna mlevi ambaye ni mtakatifu, mlevi ni mlevi na mtakatifu ni mtakatifu. Wimbo hubeba nguvu ya yule anayeuimba wala si tu yule aliyeutunga.

  Kama kanisa linaloiangazia dunia haliwezi kuimba chakacha wewe kanisani kwenu mnaimba nyimbo zipi, na je unajua style ya hizo nyimbo?
  Sijui ninaongea na mtu mwenye ufaham gani wa muziki na ni kwa kiasi gani unafuatilia haya mambo au kusoma vitabu, maana sijaona logic katika argument zako.

  Umejaribu kusema nni katika paragrafu yako ya mwisho Lwembe? Maana kama shetani alikuwa na zile funguo, ina maana Yesu alivunja mlango akaenda kuzichukua, wala hakuchonga funguo mpya. Shetani hana chake vyote ameiba. Hizo rege,chakacha, hip hop, nk zote kaiba. Mimi simwachii abaki nazo

  Nina mengi,lakini acha nikomee hapa.
  Ubarikiwe.

 4. Mpendwa Sungura,
  Kwanza nikukubalie kuwa ni kweli, “… bado tuna safari ndefu katika kuelewa jinsi Mungu anavyofanya kazi”, kama unavyosema.

  Kuhusu muziki, au asili, ni vizuri ukafahamu kwamba asili ya chochote kile huhifadhika katika kitu hicho. Kwa hiyo asili ya mkristo pia huhifadhika katika Kristo pale anapofanywa kuwa kiumbe kipya tu, na si vinginevyo! Basi mkristo hupewa asili hiyo mpya ANAPOZALIWA MARA YA PILI.

  Pia unapaswa kuyaamini Maandiko yanapokuambia kuwa Mtawala wa Dunia hii ni Ibilisi kwanza ndipo ujue wokovu wako ni nini na ndipo utaijua GHARAMA iliyolipwa kwa ajili hiyo ya kupewa au kurejeshewa asili tuliyoondolewa pale Dunia yote na vyote vilivyomo vilipopoteza Asili ya kwanza na kuingia katika ASILI mpya tuliyomo ambayo ni PERVERTED, pamoja na Rege, Hip hop, Mchiriku, Chakacha, ndombolo nk! Nafahamu inakuwia vigumu kuyaelewa mambo haya, labda ni kutokana msukumo mkubwa uliopo leo hii wa “Utumishi” katika kuihubiri Injili ili watu waokoke. Hilo ni jema lakini ‘Vigezo na Masharti” ni lazima kuzingatiwa!

  Ibilisi sio “Cha Matusi” kama wengi wetu tunavyopenda kumtambulisha. Ibilisi ni wa kidini kuliko unavyoweza kuwaza! Alikuwa kiongozi wa “Sifa” kabla ya kuasi, hebu niambie akitaka kukupindisha katika kuimba kwako, unadhani unaweza kumshtukia, na kundi la kukushabikia akiwa tayari amekutayarishia?!

  Mimi nimekuambia hivi; jaribu kumuona Kristo akiimba hizo reggae zako au mchiriku au hip hop zako, ukimuona anaimba hizo, au mtume Paulo au Petro, ukijiridhisha hivyo endelea maana umepewa ‘Maono” hayo, ni nani wa kukubishia? Ila tunakuonesha tu kuwa Dunia imo Kanisani; kimuziki, kimitindo, kiunafiki nk kwa hiyo muombe Mungu akuvuvie katika tungo zako, usikurupuke tu na nia ya kutoa Single au Album upate u super star. Hakuna kitu kama hicho kwa Mungu, ni uongo wa Ibilisi anao usambaza makanisani mpaka waimbaji karibu wote wameuza haki yao ya “KUSIFU” kwa ujira mdogo sana katika kipimo cha UZIMA!

  Unapozungumzia Utamaduni, sijui unazungumza katika kigezo gani. Mimi ninavyofahamu ni kwamba Ukristo ndio utamaduni mpya anaopewa yeyote yule Aliyezaliwa Mara ya Pili, na ya kale yote hupita!! Kwa hiyo kabila ya mtu haina maana yoyote pale mtu huyo anapompokea Kristo, yeye hutengwa kwa Neno na Michiriku, hip hop, reggae, rastafari, ndombolo na mambo yote yaliyo na uvuvio wa kuzimu katika mifumo ya Ibada na utamaduni naye huongozwa katika njia mpya yenye kumpendeza Mungu na si makundi ya wanadamu usiowajua hata wanakotokea!

  Unajua wako walevi ambao ni watakatifu kwa asili, Neema ya Mungu huwashikilia hata kuwatoa katika ulevi katika wakati wao. Basi hao wanapokuwa katika hali fulani hupata uvuvio, nao huyatimiza hayo hata leo hii nyimbo walizozitunga kwa uvuvio wa Roho Mtakatifu, zimebaki kama ukumbusho wa Neema ya Mungu kwa mlevi kama huyo tofauti na hip hop zako ambazo hazikatizi hata miezi sita, ila ndani ya miezi hiyo zitakulipa vizuri ujira wa utunzi wako kulingana na aliye kuvuvia!!

  Pia jua kwamba WOKOVU kwanza kwa MYAHUDI halafu ndio wewe na mimi tuliokuwa ndani ya furushi liendalo kuzimu! Basi katika Neema tuliyokirimiwa, tusijidai sana hata kuwaona Wayahudi si kitu, kwa ajili ya tusifa twa kuimba huto tunyimbo twa hip hop tukijiliwaza eti ndio utamaduni wetu, hivi wewe Sungura ni kabila gani huko mnakoimba Hip hop?!!! Usijipumbaze na vitu visivyo na thamani katika Ufalme wa Mungu!

  Kanisa linaloiangazia dunia halichezi Chakacha kanisani!!

  Mwisho, nikuulize hivi; utaingiaje ndani ya nyumba alimojifungia mtu kwa ndani bila ya kuchonga ufunguo? Maandiko hayasemi Kristo alivunja mlango, ndio maana alimnyanga’anya funguo!
  Changamsha akili Sungura!

  Ubarikiwe

 5. Bwana Ck Lwembe, mchango wako umenionesha jinsi gani bado tuna safari ndefu katika kuelewa jinsi Mungu anavyofanya kazi.
  Muziki asili yake siyo kuzimu, maana muziki umekuwepo kabla ya kuzimu. Na muziki kwa asili ni kitu chema ila watumiaji/wapigaji/waimbaji ndio wanaoufanya uwe msafi au najisi.
  Na mfano wako sijaukubali maana kanisa halituangazii sisi maana sisi ndio kanisa,ispokuwa lenyewe ndo linaangazia dunia-sisi ni nuru ya ulimwengu.

  Kama kwa kusema kwako muziki wa dunia umeingia kanisani unamaanisha mitindo ya miziki mf. Rege,hip hop, mchiriku,taarabu n.k umepotoka vibaya sana. Maana aina za muziki ni kutegemeana na tamaduni za watu. Siku utakapowasikia waarabu waliookoka wanaimba mbele za Mungu hautakaa hata dakika moja maana ni kama vile unavyowasikia waislam wanaimba wakati wanapunga pepo.

  Kwa damu yake Yesu kamnunulia Mungu watu wa kila kabila na lugha, hivyo watu hao humsifu Mungu kwa tamaduni za makabila yao na lugha zao, hapo nakwambia ni zaidi ya tenzi za rohoni.

  Tutokeni ndani ya boksi wapendwa tumwelewe huyu Mungu maana leo hii haitwi Mungu wa Israel peke yake bali ni Mungu wa mataifa. Wakristo wengi wanadhani Mungu ni myahudi au utamaduni wake ni wa kiyahudi. Kwa taarifa yako mpendwa hata kanisa halipaswi kuishi kwa utamaduni wa kiyahudi kwa sababu sio wote walio wa kanisa ni wayahudi; kuna wanyakyusa, wahaya, wasukuma, wamasai,wachina, wahindi,wazulu,waarabu, wayahudi n.k ndani ya kanisa. Na mitindo ya nyimbo kama hip hop, mchiriku,sebene,taarabu n.k ni utamaduni wa watu hao, ni lazima wamsifu kwa huo utamaduni- maana vyote kaviumba kwa ajili wake.
  Tenzi za rohoni tunazozipenda wengi wetu hata sio utamaduni wetu ni mazoea tu a.k.a dini.
  Gitaa analopiga mtu wa dunia ndio lielile analopiga mtu wa kanisani, lakini tofauti ni nia.Mziki ni muziki tofauti inakuja kwenye nia. Utajisiliaje ukiambiwa leo kuwa wimbo wa “Bwana Mungu nashangaa” ulitungwa na mlevi?

  “”Karibu na mimi naanza kurekodi album yangu na nitafanya kama Mungu alivyonipa kufanya-matokeo yake yatakuwa ndio nia yangu ya kuirekodi. Wadini hawataipenda lakini matunda yake watayakubali bila kujali ni hip hop,mchiriku,jazz, R&b,chakacha n.k””.

  Ndugu zangu namaliza hivi; Kwa nini Yesu alimnyang’anya shetani funguo badala tu ya kuchonga funguo mpya?

 6. Ndugu Milinga,

  Licha ya kukuunga mkono kwa sehemu kubwa mawazo yako, lakini napenda kuuliza WINGI WA WATU NA UPAKO vina uhusiano? Watu kujazana kwa wingi kumsikiliza Rose Muhando kuna maana kuna UPAKO? Au Ukienda mikoa ya Kilimanjaro nyimbo za Dini ziwe za Rose Muhando zinapigwa kwenye mabaa na sehemu za Starehe……Je ni mvuto wa UPAKO katika uimbaji au aina ya uimbaji (style) ya Rose Muhando inayowavutia…..Hivyo naomba tusichangaye WINGI NA MVUTO WA WATU Tukahusisha na “UPAKO” labda neno “Upako” litahitaji ufafanuzi……

 7. Mpendwa Pelesi,

  Nashukuru kwa pongezi zako. Ila naomba kukuambia kwamba sijaongea kwa ukali bali mieoongea kwa hoja kali. Hoja kali ni hii, HAKUNA LUGHA YENYE UPAKO DUNIANI BALI WATUMISHI WA MUNGU NDIO WENYE UPAKO.

  Kama kuna watu wanadhani nyimbo za kimombo zina upako wamepotea mtaa wa Kongo Kariakoo Dar. Nawaomba watafunte njia warudi kwenye barabara kuu ili waendelee na safari. Hakuna cha kusema kimombo kina wazungumzaji wengi, sijui nyimbo za kimombo zimeimbwa na watungaji wenye ujuzi wa mziki na ghani za kitalaam, nk yote haya hayana mashiko. Siyo hoja kali. Hivyo wenye mtazamo huo hawana hoja zenye kuweza kushikilia maji yasimwagike.

  Tatizo lingine ni kwamba wabongo wengi wakiwemo “waitwao wapendwa” wana tabia ya “kunakili na kutumia nakala yaani “copy and paste” nyimbo za waimbaji wenye upako nakudhania kwamba nao wakiziimba zinawapa upako. Huu ni uongo wa shetani na mawazo potofu ya watu wasiojua utendaji kazi wa Mungu.

  Narudia kusema kwamba, “NYIMBO ZA KIMOMBO HAZINA UPAKO KABISA KAMA ILIVYO KWA NYIMBO ZA KIBONGO NA LUGHA YOYOTE”.

  Kwa mfano Jana Jumapili (10/06/2012) hapa mjini Kigoma tulikuwa na mkutano mkubwa wa Injili ambapo mwimbaji wa nyimbo za INJILI Dada Rose Mhando na Team yake walikuwepo. Kudhilisha kwamba Rose Mhando ana upako wa kuimba umati mkubwa ambao sijawahi kuuona mjini Kigoma ulikusanyika kupata huduma ya nyimbo zake pale Viwanja vya Mwanga Centre Kigoma. Watu walibarikiwa sana kwa nyimbo zake ingawa anaimba zilezile za siku nyingi. Mimi pia nilikuwepo kwenye mkutano, nilibarikiwa kwa nyimbo zake. Sasa watu wasioelewa siri ya mwimbaji huyo wanaweza kudhania kwamba nyimbo za Rose Mhando zina upako kumbe chenye upako siyo nyimbo ni mwimbaji mwenyewe.

  NAMALIZIA KWA KUSEMA KWAMBA, “SIYO YATAMKWAYO AU KUIMBWA NDIYO YENYE UPAKO BALI MWIMBAJI AU MHUBIRI NDIYE MWENYE KUWA NA UPAKO”

  Kama kuna wenye Ubishi sasa basi watulie na waimbe wimbo wa lugha yoyote wakiwa na upako nao wataona mapepo yanavyotimua makanisani kama yapo(Maana naona makanisa mengi siku hizi hayana waumini wenye pepo).

 8. Mh! Kaka Millinga umezungumza kwa ukali! Ni kweli matumizi ya kiingereza sehemu kubwa ni kasumba ya ukoloni, mbaya zaidi bado tunatawaliwa hadi kiakili. Tunaamini kwenye kiingereza kuna upako zaidi, hili naliona ni tatizo la kiakili/kisaikolojia zaidi. Ubarikiwe!

 9. Mpendwa Edwin Seleli,

  Nimebarikiwa sana na jinsi unavyofafanua. Maelezo yako katika mada hii nimeyasoma neno kwa neno yaani between lines. Nimebarikiwa sana. Kumbe tangu tulivyokuwa pamoja pale Milambo Secondary School Tabora miaka ileee ya 90 ndivyo unavyoendelea kuchapa kazi ya Bwana?

  Nadhani mada hii umeifafanua vyema. May the Almighty God bless you and your off-springs? Nadhani ufafanuzi wako umewatoa wengi kasumba waliyonayo kudhani eti nyimbo za kimombo zina upako ikilinganishwa na kibongo.

  Hebu wapendwa tubadilike, tuache mbwembwe tuwapo mbele ya umma wa Mwenyezi Mungu yaani wapendwa. Mambo ya kuanza kudhani ukiongea kimombo ndo umebarikiwa ni kasumba ya roho ya kikoloni.

  Naomba kusema kwamba kinachokuwa na Upako siyo Lugha bali mtu mwenyewe. Kwa nukta hiyo lugha ya kimombo haina upako hata kidogo hali kadhalika kibongo nacho hakina upako. Upako ni mafuta apakwayo mtumishi wa Bwana. Kama wewe huna upako wa Bwana hata ungeimba kwa lugha gani wala hutamwona Bwana akishuka. Hata ungeimba kichina ….nhuu ngwaaa, nchi…. au kimombo, Yes Lord… My God my God, Praiiiiiiiiise Loooooooooord? Kama huna upako wewe mwenyewe unachofanya unaigiza wengine tu uliowaona wakifanya hivyo wakiwa katika upako. Nakumbuka kuna wahubiri wa EAGT walikuwa wakimwiga Moses Kulola kwa kusema , Iyoooooooo, unapenda nisemee? wakidhani eti nao watayafanya mapepo yatimuke kama Moses Kulola afanyavyo…. kumbe sifuri. Mungu hatoi upako kwenye Lugha bali huwapaka watu wake watumishi.

  Kama wewe huna upako usiwaige wenye upako kwa kuigiza hadi lugha zao. Wimbo hata kama utaimbwa kwa kufuata vina na mizani ya mashairi ya Shake Spear, au kwa kufuata waimbaji maarufu wa kimarekani au UK, nk.; bado kama waimbaji wenyewe hawajapakwa mafuta yaani hawana upako, nyimbo zao ni kama madebe matupu yavumayo na upatu uliao tu. Yaani hakuna Mungu humo kwenye nyimbo zao iwe kizungu, kichina, kiswahili, kimakonde, kichaga, kiha, kirusi, nk.

  Naomba waimbaji wote na sisi ambao siyo waimbaji au waimbishaji wote tutafute kuwa na UPAKO siyo kutafuta kiitwacho , “NYIMBO ZENYE UPAKO” au kiitwacho, LUGHA YENYE UPAKO”. Kamwe hutakuja kupata nyimbo hizo kutoka lugha yoyote duniani.

  TAFUTENI KWA BIDII KUWA NA UPAKO AMBAO BILA HUO HAKUNA MTU ATAKEYEWEZA KUWAVUTA WATU KWA KRISTO ASIPOKUWA NAO HATA KAMA ANAWEZA KUIMBA NYIMBO ZOTE DUNIANI KWA LUGHA ZOTE.

  Mpendwa Edwini Selelii, nakusalimu sana. Natamani kukuona hapo ulipo. Chapa kazi ya Bwana Mpendwa.

 10. Ktk kuabudu na kusifu kinachomatter ni
  Unamsifu na kumwabudu nani?-focus
  Ili iweje?-motives behind
  Hali na mahusiano yako na huyo umsifuye au kumwabudu?-relationship/fellowship
  Ufahamu kumuhusu anaeabudiwa-well versed in his word
  Sasa mambo hayo juu nayacombine hivi…. Unamsifu na kumwabudu nani-Kama unayemuabudu ni Mungu aliye hai,Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo ambaye Biblia inasema hukaa ktk sifa ( yaani haumwabudu mtu, nafsi yako,mambo yako, miungu, sanamu)….Ili iweje-ili kumuinua yeye, kumstailisha yeye, kumwambia aliyo mzuri, mwema, anavyostaili(yaani si kujionesha,kurembesha sauti watu wakufagilie,kutwanga drums ili watu wakuadimaye,kuweka madoido ktk keyboard ili watu wasema waaawo jamaa mkali)…. Hali yako kiroho ktk mahusiano yako na huyo umsifuye au kumwabudu-kwamba kuna floo, mahausiano mazuri na umuabudiye na kufahamiana via his neno na Roho wake na kua hakuna vizingiti moyoni na ktk nafsi eg dhambi isiyotubiwa na kuachwa, vinyongo, kutosamehe, majaribu mpaka unamchukia au kuzira mambo ya Mungu moyoni tho kwa nje waweza sema amen na kuimba mapambio na kwamba …….Ufahamu kumuhusu anaeabudiwa-kupitia neno lake au ufahamu anaojaliwa mtu kua nao kumuhusu Yeye eg. siku za agano la kale kabla ya written neno-logos kuwepo kama siku za leo tunapoweza kusoma na kujua tumnamuabuduje Mungu, therefore hayo yote yakiwapo KWANZA…….Napenda kurudia…. hayo yakiwepo KWANZA……then kiingereza, kichina, kichaga, Kiswahili, kindengeleko kije sasa kikichanganywa na vyombo vya muziki wenye adabu na nidhamu tena unaopigwa kwa kicho na utiisho wa Kimungu kwakua Mungu wetu ni Mungu wa utaratibu na nidhamu kubwa, uwepo wa Mungu utashuka tu.
  Icho watu wanachosema kua kuabudu kwa kiingereza ndio kuzama rahisi, Mungu kushuka faster na kunena kwa ndimi ize ni mentality set up/mind set up..a colonial effects kuadimaya ya wazugu hata kama tunayo yetu very powewerfull. Sincerely, mi napenda sana kiingereza na kuzama hasa na kupenya faster but equally napenda sana Kiswahili na kuzama faster na kunena ize tu. Nimeshakutana na wapendwa yaani wala kiingereza hawajui na hata Kiswahili hawana mpago ….wao wanatumia lugha ya mama tena na vifaaa vya kienyeji kama ngoma…tututu..tutut tutut ututut ututut……misumari kwa chupa ya fanta….kweche….kweche…, vimawe vya mtoni tudogodogo au vimbegu vya matumnda vinakaushwa na kuwekwa ktk cherezo ya majani matende…chwakachwaka….chwaka…..filimbi…..pipi…pipi pipi..pipippiiiiiiii……zomari…tatalalatata….tatalalatatata nk… full kinyemwezi na Mungu anashuka na wapendwa wanazamu hujawahi kuona…ooh my God, Jesus Christ tembea uone…. Nikajikuta mimi na kiingereza changu plus kiswahili cha Dar, nazubaaga tu manake ingawa mi myamwezi but sikijui saaana, so my fellow wanyamwezi wapendwa, yaaani wanakua mbingu ya saba huko kwa Baba ktk kuabudu kwao ‘’kienyeji’’(kama kweli ni kienyeji na si matatizo yetu sisi wa bongo na wazungu wazungu people), wao wako wameshapenya mimi ndo kwanza nipo ‘’mbingu’’ ya manasi na matikitiki pale chalinze!
  So kinachomatter ni yale ya juu then yaje ya nje ya lugha na vyomba vyetu hivi vya dot com
  On the other hand, ni ukweli usiopingika kua muziki kwa lugha yoyoye usaidia watu kua ktk mood njema ya kuabudu eg. mfalme aliitisha mpiga kinanda ktk agano la kale na baada ya kupigwa roho ya kutabiri ikamjia but note sio kuabudisha watu…..kufikiri kua kwa kutumia kiingereza au music wa kiyueusi yuesi vile na mabluuzi na maslow ndio unabudisha na kumleta Mungu, ni totally wrong kimaandiko, kimantiki ktk mahausiano na Mungu wetu na ki maturity ktk kumjua na kutembea na Mungu kama mtu wa rohoni….sauti, muziki, lugha hutusaidi kua ktk atmosphere ya ready kuabudu but ibada halisi, kusifu na kuabudu kwenyewe kunakua tayari ndani yetu then kunamiminikia nje kwa kusaidiwa na hali ya hew hiyo(sauti/lugha/music/instruments)
  Nilisema vyombo siyo lazima ila tukiwa navyo jina la Bwana libarikiwe…otherwise unaweza jifungia kwako bila vyombo ukanyanyua mikono na kwa kinyamwezi ukamsifu na kumwabudu,,tosha kabisaaa, pia ukitembea ktk huduma utakutana na makanisa ya wilayani na tarafani huko, ni pambio na makofi na mbingu inaternka nzima nzima na vipendwa huko unakuta vinanguvu za rohoni…we acha kabisa usipime…full upako..kutimua pepo ni faster tu…siyo kama siye, after getting chips na mayai ya Dar then unameet pepo ngangari unakemea tokaa….tttttkkkkkaaaa…aa wapi…ngoma kavu, halitoki ndio kwanza linadansi…. mpaka tmr ukajikoki vizuri unakuja litimua.
  Pia sauti au lugha siyo ishu sana kwa wengine ila kama tunazo na tumejaliwa kutoa sauti na tunaweza kuzungumza lugha libarikiwe Jina la Bwana, otherwise namfahamu Bubu mmoja mpendwa pentecost church of God at ushirombo Bukombe, Mkoa mpya wa Geita..wala hajui makiingereza yenu,Kiswahili wala kinyamwezi chetu but hutaamini anavyoabudu na kudance mpaka anzama sana tu….machozi ya furaha na uwepo wa Roho mt ndani yake mpaka niliachaga kuimba na kufumba macho, namshangaa Mungu na mambo yake jamani
  Besides, yapo makanisa na huduma hutumia kiingereza, kifaransa na kireno kwa sababu nzuri tu mfano washirika wao wengi wamekwenda shule na wanapata wageni wengi wasiojua Kiswahili au kanaisa lina watu eg wakimbizi wanajua kifaransa na ndio washirika wako na kiswahikli hawajui eg labda wanatoka Rwanda, Burundi au makanisa yanaanzishwa na watumishi toka brazili eg miaka michache dar wameingia then automatically watatumia kipotogiizi kama wengi wao kama sio wote wanajua hicho
  Otherwise, kama washirika wako ni nusu kwa nusu au robo kwa nusu au ulingano wowote, ni vema kua na ibada mbili ili kila mtu na amwabudu Mungu wa lugha na hali ya hewa inayombaliki au tumieni lugha mbili kuwepo na kutafsiri nahata nyimbo mnachanganya kwa wote wote-kiswah na kiingereza, sio kukosa hekima na kuuzi uzi watu hapa kwa kushow-show off na kiingereza kila wakati na kila mara…yes Lord….oooo yessshii…..Jesus…toch….golori golori to God, sawa, unaweza sema ivyo then changanya pia ….ndio …ooooo ndio Yesu….gusa…utukufu…utukufu kwa Mungu

 11. Sungura, maelezo uliyoyatoa ni mazuri sana, lakini yanahitaji umakini kidogo katika kuyaendea. Kimsingi muziki wowote ule husisimua roho. Ni katika uelewa huo ndipo utunzi wetu wapaswa kupangwa. 

  Twafahamu kuwa Kristo ndiye Nuru yetu, labda tuseme ndiye JUA letu. Nalo kanisa pale JUA lilipoondoka, kanisa katika nafasi ya MWEZI, ndilo linalotuangazia likiipokea Nuru kutoka kwa Kristo yaani JUA. Sasa dunia inapojipachika kati ya Jua na Mwezi huizuia Nuru isiufikie Mwezi yaani kanisa, nacho kivuli cha dunia huutia giza mwezi! Kwa hiyo muziki wa dunia umeingia kanisani na kukubalika kwa visingizio vingi kutokana ile Nuru kuzuiwa kulifikia kanisa. Ndio maana kwa siku ya leo ni vizuri kujikagua ili kujua roho iliyo nyuma ya aina ya uimbaji wetu maana miziki ya dunia ina asili ya kuzimu kwa hiyo nazo roho hizo zimejiingiza makanisani polepole kutokana na muziki wa Injili kugeuka biashara kubwa sana, hivyo kuleta ushindani badala ya sifa kama ilivyokuwa huko nyuma.

  Kwa hiyo ninawashauri watunzi na wote, hebu tujaribu kujiuliza, tunapomuimbia Bwana hizi nyimbo za kufoka foka, au mchiriku au chakacha; je, twaweza kumuona Kristo katika mic akifoka foka au akiimba mchiriku au chakacha kama tunavyojaribu kuziingiza makanisani mwetu?? Mimi nina uhakika kuwa Kristo akitukuta tunaimba Tenzi za Rohoni, atajumuika nasi mwanzo mwisho!!!

 12. Nguvu ya kusifu/kuabudu haipo kwenye lugha, kinachofanya lugha iwe kigezo ni hali binafsi ya mwenye kusifu/kuabudu, kwa mfano kama wewe ni mpenzi wa kuzungumza kiingereza automatically utaona kuabudu kwa kiingereza kuna upako zaidi, vivyo hivyo kwa anaependa kiswahili au lugha nyingineyo. Kuna kitu kinaitwa “mother tongue” kwa tafsiri ya haraka tuseme lugha ya kuzaliwa nayo au lugha uliyoizoea au kuipenda zaidi, au tuseme hali ya lugha husika kukukaa sana kiasi kwamba huwezi kusema chochote bila kutumia hiyo lugha, ndiposa mmoja anahisi lugha fulani ina upako zaidi. Kuna wengine wanaposifu lazima watanena kwa lugha yaani bila kushandaraizi wanaona hawajasifu/hawajaabudu. Labda tutoe tahadhari kwa wanaoongoza sifa/kuabudu kuwa makini na matumizi ya lugha maana yeye upako wake unaweza kuwa katika lugha ya kiingereza lakini anaowaogoza hata hicho kiingereza hawakijui, kumbuka lengo au jukumu kuu la muongoza sifa ni kuliongoza kundi kutoka pale walipo hadi kwenye uabudu halisi katika roho na kweli, waongozaji waache ubinafsi wa kuridhika na upako wanaoupata ndani yao WAFIKIRIE ZAIDI KUNDI LILILO MBELE YAO/WANAOWAONGOZA.
  Mr. Pelesi.

 13. Mchango kupitia jicho la mwimbaji na mwandishi wa nyimbo: Hakuna wimbo wenye nguvu ya Mungu kwa asili, nguvu na uwepo wa Mungu husababishwa na mwenye kuimba huo wimbo, nae ikitegemea na jinsi anavyomfahamu Mungu. Kuna nyimbo za kiingereza na Kiswahili zenye theolojia isiyo sahihi lakini kuna watu huziimba na kujawa na uwepo wa Mungu kulingana na ufahamu wao.

  Pamoja na kasumba ya kuthamini sana vya watu wa magharibi,nyimbo za kiingereza hupendwa kwa sababu zimezingatia zaidi kanuni ya mziki hasa katika mpangilio wa mziki (Music arrangement) na hivyo huwarahisishia waimbaji na wapigaji kuziiga.Pia nyingi zimezingatia kanuni za ushairi katika kuandikwa.
  Hebu fikiria “Above all powers”

  Kitu kingine kinachopungua katika nyimbo nyingi za kiswahili na ambacho ni kigumu kwa sisi watunzi wa nyimbo ni uchaguzi wa maneno. Na hii husababishwa na umasikini wa msamiati wa ushairi wa kiswahili tulionao watunzi wengi wa nyimbo za kiswahili za injili,Matokeo ya Uhaba wa msamiti ni nyimbo nyigi kurudia maneno yaleyale.Mfano; maneno Nakupenenda, nakwabudu, uinuliwe, unastahili,unaweza, nakushukuru,nakusifu n.k. yameimbwa sana

  Lakini pia kuna suala la nyimbo nyingi za kiswahili kuwa na theolojia mbovu, hata kama mtu amenakiri mistari ya biblia inategemea sana anautumiaje. Mfano mtu anapoimba maneno kama “karibu Yesu moyoni mwangu”, hata kama melodi ni nzuri hiyo theoloji siyo sahihi maana tayari Yesu yuko ndani yetu baada ya kuwa tumeokoka.

  Jambo jingine ni watunzi wa nyimbo za kiswahili kushindwa kujua namna nyingi za kumwimba Mungu. Mfano; kuna kumwambia Mungu moja kwa moja jinsi alivyo,kuna kuwaeleza wengine jinsi alivyo,kuna kujiambia mwenyewe jinsi alivyo, kuna kuimba tu maandiko kama yalivyo,pia kuna kujiweka katika nafasi ya Mungu na kuwaambia watu jinsi ulivyo( yaani wewe Mungu) mfano wimbo wa Cece Winans wa “It wasn’t easy” ameimba kana kwamba yeye ndiye Yesu aliyesikia maumivu ya msalaba.
  Kumbuka kila wimbo ni wimbo uwe wa vita,shukurani,mavuno,sifa,maombolezo,ushindi n.k kama utaimbwa mahali pake na kwa ustadi kama biblia inavyosema, unaweza kuwa sababu ya uwepo na nguvu za Mungu kudhihirika bila kujali umeimbwa kwa mtindo gani(haraka,polepole,kimoyomoyo) hata kama ni mchiriku.

  Hebu kwa mnaofahamu nyimbo hizi zifikirini utofauti wake:
  1.You are the Alpha and Omega – Wewe ni Alfa na Omega
  Fikiria huu wimbo unavyoimbwa ktk kiswahili na waimbaji wengi katika makanisa yetu ulinganishe na ulivyoimbwa na waimbaji kama Israel Houton – hapa angalia mpangilio wa sauti na muziki utaona tofauti
  2. Niguse tena lile toleo letu la zamani na lile toleo la Kristaal (hawa ni wakongo walioishi Tanzania baadae wakahamia Canada)- hapa angalia mpangilio wa wimbo na muziki kati ya hayo matoleo.

  Kwa kifupi waswahili(waafrika) huwa hatuzingatii taaluma (profession) iliyo katika fani husika tofauti na watu wa magharibi. Lakini hata nyimbo za kiingereza zenye theolojia mbovu zipo, japo zina ushairi mzuri na mpagilio mzuri wa vyombo.

  …….Jamani kiingereza ni lugha ya kimataifa kuliko lugha zingine zote leo, kwa hiyo kukijua kuna faida yake pia. Liko pia tatizo kubwa kwa watanzania “wengi ni wavivu wa kusikia. Wakisikia wimbo wa kufoka wanasema hawauelewi na ni wa kihuni kumbe tu ni wavivu wa kusikiliza. Kwa maana kama huna bidii ya kusikiliza hip hop huwezi kueielewa wala kuipenda. Lakini wenye bidii wimbo wa kufoka unaweza kuwafanya waogelee katika uwepo wa Mungu.

  Nimeongoza sifa na kuabudu kwa miaka mingi, nimeona utukufu wa Mungu ukifunika watu kwa namna ya ajabu kwa nyimbo zote za kiswahili na kiingereza na hata nyimbo za lugha isiyojulikana.

  Wanaigeria hawana matamshi mzuri ya kiingereza lakini nakwambia huimba nyimbo za kiingereza na nguvu ya Mungu huwafunika.
  Kumbuka kuna kumwimbia Mungu kwa akili na kwa roho. Matokeo ya hizi namna mbili yanatofautiana japo kote ni kumwimbia Mungu ambako biblia imesema tunaweza kuimba au kuomba.

  Mara nyingi makanisa yenye ibada za kiingereza huwa ni kwa ajili ya wanaojua kiingereza na huwa kuna ibada za kiswahili pia.

 14. shaloom waoooh! ninajisikia sana furaha na kiu nina sikia kuabudu na kusifu kwani huwa na barikiwa sana ninapoabudu, na ninapenda sana sana sanaaaaaa kuabudu, KUMBUKA MUNGU AWAPENDA WAMUABUDUO KATIKA ROHO NA KWELI, NA HIYO NDIO IBADA MUNGU ANAYOTAKA, BARIKIWA

 15. Suala la lugha katika ibada lapaswa kutazamwa katika mapana yake. Lugha ni utamaduni na ni uhuru wa mawasiliano, hata yakiwa na Mungu. Wakati mwingine Mungu anapotaka kuwasiliana na wewe, huamua kukunenesha kwa lugha ili akufikishe katika kiwango cha uelewa kulingana na anachokuzungumzisha. Basi yeye hufanya hivyo kutokana na upungufu wa maneno yanayoweza kuelezea hali katika lugha zetu. Ndio maana mt. Paulo anasema amekosa maneno yanayoweza kuuelezea uzuri aliouona katika ile Mbingu ya tatu! 

  Basi lugha ya English ikiwa na maneno zaidi ya elfu saba, ina nafasi kubwa ya kujieleza kuliko kiswahili chenye maneno chini ya elfu tano na zaidi ya robo ya maneno hayo yakiwa ni mapya kama anayoyatumia ndugu Milinga, “kimofolojia na kisemantikia” ambayo sidhani kama watu wa kawaida watayaelewa hayo iwapo utayatumia katika tungo zako  za nyimbo za kuabudu!

  Jambo la kwanza katika lugha, ili uwe ‘fluent’, ni kuwa na uwezo wa kufikiri katika lugha hiyo. Ni katika kiwango hicho ndipo unaweza kuitumia lugha hiyo katika ibada. Lakini ikikubidi uwaze kwa kiswahili halafu ndipo utafsiri mawazo yako katika english au lugha yoyote ile, hayo ni “mateso laini” yanaowapata waigizaji wote, hata wakiwa ibadani na katika hali hiyo huwezi kuyaona hayo “mafuriko”  maana wote mishipa ya kichwa imewatoka wanapojitahidi kwenda sawa na jambo walilolianzisha, kiongozi kwa mfuasi! Tofauti na hali hiyo ni pale unapowakuta wale walio fluent, hao hujiachilia kikamilifu, na ukubwa wa lugha huwafaidia pia waliobado mwilini na kuwasogeza zaidi uweponi wakiingizwa katika “mafuriko” kama ambavyo Roho angewafanyia kusanyiko la kiswahili na kuliingiza katika “mafuriko” akijihusisha nao katika ibada hiyo na kuyafunika kabisa mapungufu ya lugha!

  Kwa hiyo mimi nadhani suala la lugha ipi inayompendeza Mungu zaidi, au yenye nguvu za Mungu zaidi, ni mtazamo unaotokana na hali tunayokuwa katika ile initial stage, au tunapopasha moto misuli, basi kingereza kwa wingi wa maneno yake hujiwakilisha kivyepesi zaidi kuliko kiswahili kwa mwenye kuijua lugha hiyo, lakini kwa aliyejikita katika kiswahili au lugha yoyote ili, pia huenda sambamba katika kina kama hicho; HUO NDIO MUUJIZA WA IBADA KATIKA ROHO!!!

 16. Ndg Milinga,

  Nashukuru sana kwa kupingana nami mia kwa mia. Nimefurahi sana kwa hilo. Hayo uliyoyaandika kwa kweli nakubaliana nawe moja kwa moja. Ila nilichoelezea mimi nilisema ni wale waimbishaji, mara nyingi ndio wanaopenda kuwaburuza wale wanaowaongoza kwenye ibada! Hata sasa , kwa makanisa ninayoyafahamu kuwa yanaendesha ibada za kimombo, nyingi zinakwenda kwa ugumu. Ni za watu wachache na wengine wanakuwa kenge katika msafara wa mamba! Hilo ni tatizo!. Asante sana.

 17. watu wengi wanaopenda nyimbo za kizungu wanajua kizungu na hawataka kutafuta nyimbo za kiswahili.nyimbo km nyimbo inaweza kuleta uwepo wa Mungu km maneno yakipewa nafasi kwa mwimbaji au msikilizaji.nyimbo yoyote yenye Neno la Mungu ikiimbwa na mwimbaji kutoka rohoni inauwepo wa Mungu ukiipa nafasi ktk moyo wako sio kichwa chako bila kujali lugha ya aina yoyote. tulipo pata neema ya kujua kizungu tusikose kuupa wimbo wa kiswahili nafsi. Fanya utafiti kwanini wanaoimba kwa kizungu bongo uwepo wa Roho Mtakatifu ni mdogo kuliko wanaosifu kwa kiswahili?

 18. Mpendwa John Paul,

  Nimefurahishwa na uchambuzi wako kuhusu mada hii. Umejitahidi kutoa hoja zenye kutazama upande huo wa kizungu au kimombo na kueleza kwa nini watu wampendao Mungu Baba hupenda kimombo pia.

  Mimi nilikuwa mshirika wa kanisa la KLPT Mtaa wa Lindi jijini Dar tangu mwaka 1999 hadi 2003. Nilikuwa nikuhudhulia ibada ya kwanza ya Kingereza. Ibada ya sifa pale ilikuwa inaendeshwa kwa kimombo. Kwa uzoefu nilioupata pale napenda nitofautiane na wewe kabisa mia kwa mia.

  Nikiwa pale KLPT Lindi Street Dar, nilikuwa naona jinsi watu walivyokuwa wanamung’unya maneno, waimbishaji wanazijua nyimbo lakini washiriki hawazifahamu nyimbo hizo za kimarekani au kimombo. Walichokuwa wanafanya ni kutumia Projector mbele ya kanisa na kuanza kuimba nyimbo kwa kutazama mbele kwenye ubao huo wa kitambaa mbele ya kanisa. Mimi sikuona kama ibada zile zilikuwa na upako kuzidi zile ibada za kiswahili zilizokuwa zinafuatia mara baada ya Ibada ya kimombo iliyokuwa inaanza saa 2.00 hadi saa 5.00 asubuhi. Baada ya Ibada ya kimombo mimi nilikuwa napenda kuhudhulia na ile ya kiswahili, nilikuwa naona jinsi watu wanavyofurika na kujaa nguvu za Mungu sana na Roho Mtakatifu kumiminika baada ya nyimbo za Sifa kuliko kwenye ibada ya kimombo.

  Hebu fuatilia makanisa ya bongo yote yanayoendesha Ibada za Kimombo, fanya utafiti kwa kutembelea hata makanisa 2 tu usali ibada ya kimombo na ya kiswahili kisha urudi uniambie ni ibada gani uliona watu wanapata mafuriko ya Roho Mtakatifu, je ni ya kimombo wanakoimba nyimbo zenye vigezo ulivyotaja?

  Niliwahi kuhudhuria ibada moja katika kanisa la Mzee Zakaria Kakobe “Full Gospel Bible Fellowship” miaka ya 1995. Walipoanza kuimba tu, mapepo machafu yalilipuka kila kona yalikokuwa yamejificha ndani ya watu. Hapo Muhubiri hajaanza hata kunena.

  Miaka ya 1990 pale Tabora mjini niliwahi kuhudhuria mikutano ya Injili ya Mzee Moses Kulola. Kuna kwaya moja toka Ulyankulu Barabara ya 13 ilisimama kuimba jukwaani, wakati inaendelea kuimba tu watu wenye mapepo walianza kupata uponyaji. Nikiwa Jijini Mwanza mwaka 2006 hadi 2009 tulianzisha ibada ya kimombo kanisani pale EAGT- Mabatini. Ibada ile kwa kweli waliokuwa wanaipenda ni vijana wa kisasa wanaotamani kujua kimombo. Tulilazimika kuweka mkarimani ili kuwasaidia hata wale wanaopenda ibada hiyo lakini kimombo hawakielewi. Wengine wanahudhulia tu ili kujifunza misamiati ya kimombo na wala siyo kuabudu katika Roho na Kweli.

  Kwa hiyo naomba nimalize nikiamini kwamba umejifunza kutokana na hizo shuhuda zangu za kiutafiti. Utaona kwamba swala hapa siyo mpangilio wa nyimbo za kimombo na utungaji wake au ghani zao wanazotumia. Bali mimi naona ni swala la waimbaji na waimbishaji wenyewe wanavyoimudu Lugha husika na walivyokaa kiroho na kanisa lilivyotulia katika utakatifu.

  Tuachane na ukoloni wa kudhania kwamba wazungu ndio wanaojua kutunga na kupangilia nyimbo. Huu ni ukoloni mamboroho.

 19. Bwana Yesu atusaidie, Kwa upande wangu naona kuwa si kweli tukiamini kuwa nyimbo kiingereza ndio zenye nguvu ya Mungu, ila upako unategemea na mtu Mwenyewe alivyojiweka kukutana na Mungu wake.

 20. Wapendwa,

  Mtazamo wangu binafsi ni kwamba nimekuwa natatizika na wimbo /Nyimbo zipi ni za ni kusifu na kuabudu…Je ni wimbo unaoimbwa taratibu….na Polepole…..? Na zipi sio…. Kwangu mimi naona wimbo wowote ule ni wa kumsifu au Kumwabudu Mungu licha ya style yake ya uimbaji…..yaani iwe ya haraka haraka au ya taratibu…….!Na kuhusu “kuuvuta” uwepo wa Mungu…..hilo nalo natatizika nalo….Je ni wapi katika Maandiko tunasimamia hilo…?Biblia inasema wawili watatu wanapokusanyika kwa Jina langu….Mungu yuko nasi…..licha ya kuimba au la…! Sisi ni Hekalu la Mungu……Hivyo Uwepo wa Mungu u nasi siku zote….Hauvutwi na kushuka kwa style ya Uimbaji tu..Biblia imeonyesha hivyo, Uwepo wa Mungu na Nguvu zake ulijihidhirisha kwa njia ya Pekee Petro alipokuwa amelala usingizi gerezani kifungoni usiku wakati kanisa likiwa linaomba mbali na hapo gerezani akiwa katika vifungo vya minyororo…..(Matendo 12:5-9) Lakini kwa Paulo yeye alikuwa AKIOMBA NA KUMSIFU MUNGU….! “Kumwimbia nyimbo za kumsifu” Matendo 16:25.

  Kwangu mimi kusifu na kumwabudu Mungu kunaanzia ndani ya moyo wa Muumini mwenyewe licha ya aina ya Muziki…..! Uwepo wa Mungu sio kama switch ya umeme ukutani ambayo unasema haya sasa njoo tuaanze kuimba aina fulani ya Muziki “Kuuita uwepo wa Mungu”

  Na hata hii aina ya Miziki ya kusifu na kuabudu ambayo katika majukwaa ya muziki inaitwa “Contemporary” Music….ina historia yake……katika ulingo wa Imani inajulikana ilianza lini…Ukipenda kusoma aina hii ya uimbaji imeanza lini na wapi Marekani unaweza kabisa kupata….

  Na sasa swala la kutumia lugha ya Kiingereza, hapo unaweza kuzungumza mengi….inawezekana maneno ya kingereza yana mvuto na yanaweza kubeba maana nzito…..kama alivyosema Ndugu John Paul…..lakini vile vile labda ni kuathiriwa toka kwenye CD’s Tv tunazoziona zikitokea nje leo ambazo zinapatikana kwa wingi leo Kama alivyosema Ndugu Milinga…..ambayo naona ametumia lugha kali kidogo….

  Kwa kifupi Lugha yoyote ile chini ya jua inaweza kabisa kuwasiliana na Muumba…..kumsifu na kumwabudu……Hebu angalia Biblia…..”Baada ya hayo nikaona na tazama mkutano mkubwa sana ambao hapana awezaye kuuhesabu WATU WA KILA TAIFA…NA KABILA NA JAMAA NA LUGHA WAMESIMAMA MBELE YA KITI CHA ENZI CHA MUNGU……WAKILIA KWA SAUTI KUU WAKISEMA WOKOVU UNA MUNGU WETU AKETIYE AKETIYE KITI CHA JUU……

  Lakini vile vile tukubali ukweli huu kuwa hali ya Tanzania inabadilika haraka sana, hali ya sasa (trend) ya vijana wa leo ni kuzungumza Kiingereza, vijana waliotoka shuleni na ambayo ni wengi (kwa mtazamo wangu) ndio waanaandaa makongomano ya Kusifu na Kuabudu……..na ndio hao hao wanaguswa na uimbaji toka nje….hivyo tegemea sana kukuta utumiaji wa Lugha ya Kiingereza….

 21. Wapendwa, mi nafikiri kuwa kuna sababu kadhaa zinazochangia waimbishaji wanaofahamu nyimbo za Kizungu [siyo tu za kiingereza kwa lugha bali na utunzi wake ni wa kizungu, pamoja na kimarekani maana nao wanatumia kizungu] zionekane kama zina uhai zaidi wa kiroho, au zina mguso zaidi wa Mungu, au zinampeleka mtu kwa haraka zaidi mbele za Mungu kuliko nyimbo za Kiswahili!

  Baadhi ya sababu hizi, ambazo hata hivyo mtu anaweza kuzikosoa na wala nisikwazike kabisa, ni hizi:

  1. Wazungu wanapotunga nyimbo huchukua muda kuandika na kuhariri maneno ili yaendane kweli na kusudi la wimbo. Nyimbo nyingi za kitanzania ni za taratibu tu lakini maneno yake yanakuwa siyo yakuabudu. Utakuta ni ya maombi, kuonya, kujipa moyo nk.

  2. Wazungu wanapotunga wimbo wa kuabudu huhakikisha kweli ni wa kumuabudu Mungu. Na hulinda ujumbe uwe ule ule hadi mwisho. Nyimbo nyingi (siyo zote) za kiswahili zinatungwa zikiwa na jumbe zaidi ya mmoja. Utakuta wimbo unaanza ukiwa wa kuabudu halafu mwishoni unaishia wa mahubiri.

  3. Labda kwa sababu ya UJUZI na VIPAJI vya uimbaji wao, Nyimbo zao nyingi utakuta ghani (melody) zake zimeendana kabisa na maneno ya wimbo husika na kukubaliana huko kwa maneno na wimbo huleta nguvu fulani ya kimuziki kwa muimbaji au msikilizaji. [Tuna nyimbo nyingi za kishwahili ambazo kama zingepatiwa nafasi, maneno yake yakapewa sauti nyingine, zingekuwa ni nzuri sana. Ghani ya wimbo ni muhimu sana katika kubeba aina ya ujumbe unaokusudiwa].

  4. Upangiliaji wao wa muziki kwenye nyimbo za kuabudu huwa nao upo katika hali ya kuabudu. Ala za muziki nazo “huzungumza”. Hawapigi muziki kwa “kujionyesha”. Kwetu unaweza ukakuta mtu katunga wimbo wake mzuri tu wa kuabudu lakini upigaji wake wa muziki unakuwa ni wa “fujo” na kuufanya wimbo usiweze kuwapeleka watu mbele za Mungu kwa urahisi.

  Hizo ndiyo sababu chache ambazo mimi binafsi nimefikiri huwafanya waimbaji wa Sifa na Kuabudu wanaofahamu nyimbo za Kizungu wavutiwe nazo. Sasa ukichunguza sababu hizo utaona kuwa suala SIYO LUGHA bali ni KANUNI au sifa zinazopatikana katika nyimbo za Kizungu.

  Kwa maana hiyo ni kuwa na NYIMBO ZA KISWAHILI ZENYE SIFA HIZO au zilizofuata kanuni hizo Nazo utakuta ni nzuri sana tu na zinakuwa na nguvu au msukumo wa kumfanya mtu aingie kwa haraka katika Wingu la kuabudu.

  Changamoto inabakia kwa waimbaji na watunzi wa nyimbo pamoja na wapangiliaji wa muziki kwenye nyimbo za kuabudu. Maombi, Umakini pamoja na unyenyekevu vinatakiwa ili nyimbo za kiswahili nazo ziwe zimejitosheleza.

  Tuendelee kujifunza!

 22. Sijaona kama kuna uhusiano wa Ibada,Uwepo wa Mungu na Lugha ya kiingereza au kiswahili au Lugha yoyote inayotumika,ila ninachofahamu Ibada au sifa ya kweli inaanzia moyoni.
  Biblia imetupa msingi ulio wazi kabisa..
  “Kusifu kunawapasa wanyofu wa moyo”, pamoja “Mwabuduni BWANA kwa uzuri wa utakatifu”,
  hivyo hatuwezi kutenganisha kiwango cha maisha ya Ibada ya mtu aliye-compose, anayeongoza huo wimbo,na impact ya huduma yake kwenye maisha ya watu,
  kuongoza sifa na Ibada kama ni kwa kumtumikia Mungu then hatuwezi kuvuka mpaka wa maisha yetu binafsi kuwa ya Ibada na utakatifu kwa Mungu..
  Kinachowafanya watu waone nyimbo za kiingereza ziko vizuri zaidi kwenye uwepo wa Mungu tofauti na za kiswahili naweza kusema ni mazingira na “exposure”,
  sababu hujawa exposed kwenye nyimbo za kiswahili zilizo vizuri hazina maana kwamba hazipo au kwamba hazigusi moyo wa Mungu kama vile Mungu anabagua lugha,kama alitununua watu wa kila taifa,kila kabila,kila lugha ninao uhakika ankubali na lugha zetu pia..
  baseline ya yote najua ni kwamba “Mungu anaangalia Moyo”

  Nawasilisha..

 23. Mimi naona sio kweli Mungu wetu anasikia kila lugha hata ukisififu kwa kimatumbi Mungu anaskia. Hii nikasumba tu ambayo hata viongozi wetu bungeni ili aweke msisitizo basi lazima achanganye kiingereza.

  Nyimbo za kiingereza kwanza hazina mvuto maana hata huyo anayeimba hawezi kukitamka vizuri na yule anayesikiliza hawezi kuelewe.

 24. minaona english and kiswahili vyote vina leta maana sawa katika kuabudu isipokuwa anayeabudu anatumia lugha ipi anayoielewa zaidi kati ya english na kiswahili.

 25. Kwa kweli sina hakika na Nguvu za Mungu kwenye Kiingereza zaidi tu ya mtazamo, nyimbo za Kiswahili tena zile za zamani zina upako zaidi aisee,

 26. Bwana Yesu akubariki?

  Roho chafu ya ukoloni bado inazitesa nchi zote za Afrika. Wenzetu wa nchi za bara la Asia angalau roho hii chafu ni kama imewatoka. Afrika sijui kwa nini hatuponi kasumba hii mbaya. Nchi za Asia zimepiga hatua kiuchumi na kiroho kuliko Afrika kwa sabu wamekemea pepo hili la kikoloni na limewatoka kabisa kwa aslimia zaidi ya 80 wakati hapa kwetu pepo hili bado linatamba kwa zaidi ya asilimia 80.

  Ni nani aliyekwambia kwamba Mungu anaongea kizungu zaidi kuliko lugha zingine. Ni kama waislam wanavyotukuza kiarabu eti ndicho kina upako wa Allah wao na usipotumia kiarabu wewe siyo mwislam aliyebobea.

  Wakrsito nao wanadhani eti usipotumia kizungu cha hao wamisionari walioeneza ukristo kwetu wanaona kama upako unakauka. UJINGA. UJINGA, UJINGA MTUPU.

  Hata kama ungeimba kwa lugha za malaika kama huna Upendo yote ni bure. Au niseme kwamba hata ungeimba kwa lugha zote za duniani kama hauko rohoni, yaani kama wewe una mikwaruzo ya kiroho uimbaji wako ni sifuri.

  Mbona watu wanakuwa na ujinga wa kikoloni? Hivi watu wa Burundi, Rwanda, DRC, Ivorycoast, Ufaransa, Ujerumani, Uswis, Korea, China, India, nk wanatumia kizungu ambacho kinawazuzua ninyi wapendwa?

  Unamkuta mtu amekazana kuimba kwa kizungu. Unamkuta mhubiri fulani amekazana kukemea maapepo kwa kizungu, UJINGA MTUPU. UKOLONI MTUPU UMEWAJAA WATU. Unamkuta mtumishi anakazana kuongea kiingereza mbele ya watu ambao 90% hawajui hata kuomba maji ya kunywa kwa kizungu. Ajabu sana. Hii ni kizunguzungu kabisaa na wala siyo kizungu. Kizungu chenyewe wanachoongea ni cha kibantu mtupu, kimejaa lafudhi ya kisukuma, kichaga, kiha, kimanyema, kizaramo, kiswahili badala kusema “utakwenda na maji” anasema , “you will go with water” eti na yeye aonekane anajua kizungu kwa hiyo anao upako.

  Nilisikiliza Mtumishi mmoja akiwa anahubiri Mkutano wa Injili pale Tabora mjini, katika kuwahamasisha watu wamwendee Mungu mwenye kila kitu asiyefiliska wala asiyekuwa na mipaka katika utendaji wake akasema, “….. Mungu wetu ana kila kitu yaani yeye ni LIMITED……” Eti Mungu ni “LIMITED” nikasema huyu naye analingia kizungu ambacho hata hakijui. Unasemaje Mungu ni LIMITED? Hivi unaelewa unachoongea au unapakua na kushusha (Copy and Paste)?

  Waimbaji na wahubiri hebu acheni ujinga wa kikoloni. Okokeni kweli kweli. Huwezi ukasema UMEOKOKA kama bado una kasumba ya Kizungu na Kikoloni.

  Kama siyo ibada yenye wageni ambao ni zaidi ya 50% ya waliohudhulia ibada ya nini kuimba nyimbo za kizungu. HUU NI UJINGA NA UKOLONI MTUPU!!!!!!!!

  Kama ibada ni ya kizungu kitupu kama makanisa mengine yafanyavyo siku hizi hapo hakuna shaka. Lakini na zenyewe huwa hazina mantiki yoyote. Waumini wote ni wazaramo watupu, wasukuma watupu, wanyakyusa, nk unaanzisha Ibada ya Kizungu ili iweje? Hivi hapa Tanzania watu wanaojua kuongea na kusikiliza kizungu ni wangapi? Mimi nadhani hawazidi hata milioni 2 kwa nchi nzima. Hapo kanisani kwako ukiangalia waumini walisoma sana hadi chuo Kikuu au Form 6 wamo wangapi? Fanya sensa kwanza kabla ya kuanzisha Ibada ya kizungu. Kama utakuta wengi yaani 50% na kuendelea ni wasomi wa zaidi ya FOMU 4 basi waweza kuanza ibada za kizungu na kuimba nyimbo hizo za kizungu.

  NAWAOMBEA WAAFRIKA WAOKOKE KATIKA KONGWA LA UKOLONI.

 27. Shalom
  hii inategemea na mtunzi na waimbaji pia
  mfano nyimbo zilizokusanywa na kutengeneza tenzi nyingi zilikuwa za Kiingereza ila nyingine ni za Kiuganda nyimbo hizi zina uwepo wa Mungu kwani mtunzi anakuwa alitunga akimaanisha anachosema na hivyo zimevuviwa na Roho Mtakatifu unakuta mara nyingi zikiimbwa na watu wa Mungu uwepo wa Mungu unashuka sana mfano pia nyimbo za Abiud Misholi, Kilahiro, marehemu Sedekia, Reuben Kigame siko biased bali hizi ndio nimekutana nazo binafsi na ni za kiswahili kuna kwaya pia za kanisa nyingi tu ambazo nyimbo nzuri za kuabudu wanazo.
  Hata uimbe kifaransa kama hakuna uwepo wa Mungu kwako na ktk nyimbo na maneno yenyewe basi ni kujilisha upepo.
  Kumbuka waabuduo halisi watamwabudu Mungu ktk Roho na kweli, ibada itoke ndani ya moyo wako na sio nje. Barikiwa

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s