Tanzania yapata mwakilishi tuzo za Africa Gospel Music Awards

Christina Shusho

Mwimbaji wa muziki wa gospel nchini Christina Shusho ameingia kwenye kinyang’anyiro cha kuwania tuzo za Africa gospel music awards zinazotarajiwa kutolewa tarehe 7 mwezi July mwaka huu huko jijini London nchini Uingereza.

Mwimbaji huyo amepata nafasi hiyo baada ya kupigiwa kura za kupendekezwa na watu mbalimbali hapa nchini na nje ya nchi kutokana na huduma yake njema katika tasnia ya muziki wa injili kwa ujumla. Ambapo mwimbaji huyo amependekezwa kuwania kwenye vipengele viwili ambavyo ni mwimbaji bora wa kike wa mwaka tuzo ambayo anawania pamoja na

1.Emmy Kosgei-Kenya
2.Dena Mwana – Congo
3.Ntokozo Mbambo- South Africa
4.Rebecca- UK
5.Gifty Osei- Ghana
6.Kefee -Nigeria
7.Onos Ariyo- Nigeria
8.Diana Hamilton-UK
9.Christina Shusho -Tanzania
10.Lara George- Nigeria

Katika kipengele cha pili anachowania tuzo mwimbaji huyo ni mwimbaji wa mwaka anayowania pamoja na waimbaji wengine 9 ambao ni

1.Eko Dydda- Kenya
2.Emmy Kosgei – Kenya
3.Exodus- Uganda
4.Christina Shusho- Tanzania
5.Lam Lungwar- South Sudan
6. Sarah K- Kenya
7.Dawit Getachew-Ethiopia
8.Kambua-Kenya
9.Willie Paul- Kenya
10.Ann Marie Mutesi – Burundi


Christina Shusho akiwa kwenye huduma na muimbaji wa Kenya Geraldine Hephzibah Oduor

Katika waimbaji wanaowania tuzo hizo nchi ya Kenya inaongoza kwa kutoa waimbaji watano katika nchi za Afrika mashariki, huku Tanzania tukitoka kimasomaso na mwimbaji mmoja ambaye tukijipanga vyema kwakumpigia kura nyingi ataibuka na tuzo zote mbili kwakuwa waimbaji wengine mfano kama kutoka Kenya kwakuwa wanawakilishwa na waimbaji wengi watakuwa wakigawana kura jambo ambalo litakuwa faida kwa watanzania kwa pamoja kumwezesha Shusho kuibuka na tuzo mwaka huu baada ya kukosa mwaka jana.

Lakini pia katika tuzo hizo mwaka huu kutakuwa na mchuano mkali kwa waimbaji wa nchi nyingine kama Afrika ya kusini ambako waimbaji nyota kama Ntokozo Mbambo, Solly Mahlangu, Keke, Uche,S’fiso,Hlengiwe na wengineo wanaowania tuzo mbali mbali huku kundi la Joyous Celebration likiingizwa kwenye kipengele cha tukio kubwa la mwaka kupitia recording yao ya 16.

Kumekucha sasa Mtanzania tuna mwimbaji mmoja tu ni wakati wa kuunganisha nguvu kwa pamoja ili tuzo hizo zije nchini kwa utukufu wa Mungu, na kupanua muziki wa injili wa Tanzania katika nchi nyingi zaidi.Utaratibu unafanywa kuhakikisha kura ambazo zimeanza kupigwa hii leo mpaka tarehe 29 mwezi huu.
Ili kupiga kura yako fuata maelekezo yafuatayo baada ya kuingia kwenye tovuti hiihttp://www.africagospelawards.com/nominate.html

VOTE NOW
AGMA 2012 VOTING GUIDELINES
1. Click on the ‘VOTE NOW’ button.
2. Register your email address, confirm and submit.
3. Check your email (inbox) and you will find the link to vote.
4. If you do not find the link in your email inbox, please check your junk mail folder.
5. Once you have connected to the voting page please make your selections and submit (you can only vote for one nominee from each category).
6. You do not have to vote in every category.

5 thoughts on “Tanzania yapata mwakilishi tuzo za Africa Gospel Music Awards

  1. Cong’s Christina.i admire you! Yesu wa nazareth na akupe ushindi milele na milele,Amen!!!

  2. sioni km kuna ubaya wwt christina amewabariki watu na nyimbo zake wameamua kumtunuku. kila la kheri dada Mungu akubariki sana, unachonifurahisha dada yngu Utukufu wa Mungu huguc bali unamridishia. naamini dada Christina unaongozwa na Roho Mtakatifu. manake ukickiliza thamani ya wokovu wangu, nipe macho nione, nataka ushirika na roho, nk. jamani mie hata sisemi bali sifa na Utukufu vimrudie Bwana milele.

  3. Poleni na tena aksati kweli iyi mutiani ni safi .lakini tuombe Mungu sana juu ya waimbanji wetu ya injili kugombaniya mamulaka ya Dunia iyi.Afazali tugombaniye kwa IMANI zetu kama majina yetu imeandika kwenye kitabu cha UZIMA.pande yangu mimi sio ukumu ila tu ,Tulize Roho Mutakatifu atuakikishiye kama ni safi mwimbanji ao muinjiliste ya NENO la MUNGU anaweza kufanya mashidano kama iyi. Atuko washabiki ya Mtu ila tuko Bibi arusi wa YESU
    NB …wandugu tuombe Mungu sana juu ya safari yetu ya kwenda mbinguni. Tujuwe adui wetu anazunguhuka akitafuta mutu amumeze Kweli kama nimeandika vibaya munihurumiye

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s