UPONYAJI WA NDOA

—Sharti wanawake wasimame kwenye nafasi zao ndipo wataona uponyaji kwenye ndoa zao. 

Hili lilikuwa jambo la kwanza Bwana kunijulisha, ili niwakumbushe tena akina mama. Nimeshaandika kuhusu nafasi za Mwanamke huko nyuma, Kwa kifupi niseme uponyaji wa wa ndoa yako upo kwa wewe kuwa kwenye nafasi yako. Mungu hana namna ya kukusaidia kama hauko kwenye nafasi yako.

Ni lazima uzijue nafasi ambazo Mungu amekupa na kisha kusimama vema ukiwajibika kwenye hizo nafasi. Kinamama wengi leo wanalia sana Mungu aponye ndoa zao na matokeo yake yanakuwa tofauti na matarajio yao. Endapo kama na ndoa yako ipo kwenye eneo kama hili, angalia kama umekaa vizuri kwenye nafsi ambazo Mungu amkupa katika ulimwengu wa roho. Nina uhakika unaweza ukawa kuna maeneo ulijisahau hivyo tengeneza, maana uponyaji na uharibifu wa ndoa yako kimaandiko upo katika uwezo wako mama.

Ni maombi yangu kwamba Roho Mtakatifu akujulishe jambo hili, uponyaji wa ndoa yako haupo kwa Mungu, bali Mungu ameweka uwezo huo ndani yako. Ili uwezo huo uweze kufanya kazi sawasawa ni jukumu lako kuwa kwenye nafasi zako.

Unahitaji hekima ya Mungu ili kujenga ndoa yako 

Ukisoma kitabu cha Mithali 14:1 Biblia inasema “Kila mwanamke aliye na hekima huijenga nyumba yake; Bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe”. Biblia imeshaweka wazi kwamba wewe unaweza kuijenga au kuibomoa nyumba yako. Uwezo wa kufanya jambo hili unategemea kiwango cha hekima ya Mungu ambayo ipo ndani yako na juu yako pia. Hekima ya kuponya ndoa yako ambayo sasa unajua iko mashakani, ipo kwenye neno la Mungu na si kwa waganga wa kienyeji.

Unaipataje hekima ya Mungu?

Katika Mithali 8:1 Biblia inasema ‘Je! Hekima halii? Ufahamu hatoi sauti yake?’ mstari wa 10 unasema ‘Pokea mafundisho yangu, wala si fedha, Na maarifa kuliko dhahabu safi’. Ule mstari wa 14 unasema ‘Shauri ni langu, na maarifa yaliyo sahihi; Mimi ni ufahamu, mimi ni nguvu’. Na ule wa 16 unasema ‘Kwa msaada wangu wakuu hutawala, Na waungwana, naam, waamuzi wote wa dunia’.

Siku zote kama unataka hekima ya Mungu ya kukusaidia kwenye eneo lolote la maisha yako utaipata kwenye neno la Mungu au kwa Mungu. Imeandikwa katika Mithali 12:1a “Kila apendaye mafundisho hupenda maarifa’. Hekima ya Mungu kwa mtu ni matokeo ya kiwango cha neno la Mungu ambalo mtu ameliweka na kulitafakari kwa wingi moyoni mwake. Kwa hiyo kwa Watawala, hekima ya Mungu kwa Mtawala inategemea kiwango cha neno la Mungu kuhusu utawala ambalo Mtawala amekiweka ndani yake. Naam hekima ya Mungu kwa Mwanamke itategema kiwango cha neno la Mungu kuhusu nafasi zako ambacho umekiweka ndani yao nk.

Sharti neno la Mungu kuhusu nafasi zako, wajibu wako nk liwe kwa wingi ndani yako ndipo hekima ya Mungu ya kujenga nyumba/ndoa/familia yako itakapokaa ndani yako na juu yako. Na kwa kuwa hekima ni ufahamu, maarifa, shauri na nguvu, itakusaidia katika kuijenga ndoa yako, kama inavyowasaidia watawala, waung’wana na waamuzi katika majukumu yao (Mithali 8:16). Naam hekima hiyo itaongoza kinywa chako kuleta uponyaji wa ndoa na nyumba yako, kama Biblia inavyosema katika Mithali 31:26 “Hufumbua kinywa chake kwa hekima, Na sheria ya wema i katika ulimi wake”.

Mithali 8:17 inasema ‘nawapenda wale wanipendao, na wale wanitafutao kwa bidii wataniona’. Naam siku zote, hekima inawasiaidia wale wanaoitafuta na wakaipata’. Na njia kubwa ya kupata hekima hiyo ni kwa njia ya kusoma na kuatafakari neno la Mungu kila siku na kuomba kama nilivyokufundisha hapo juu.

Uwe makini kufuatilia maisha ya mume wako/watu wa nyumbani mwako 

Mithali 31: 27 “Huangalaia sana njia za watu wa nyumbani mwake; wala hali chakula cha uvivu”. Tafsiri ya kiingereza ya BBE inasema “She gives attention to the ways of her family; she does not take her food without working for it”. Moja ya nafasi za mwanamke ambayo nilishaandika huko nyuma ni kuwa mlinzi wa mwanaume, hii ikiwa ni pamoja na mume wake.

Naam jukumu la ulinzi ni kubwa sana ambalo Mwanamke umepewa, siku zote mlinzi ana wajibu wa kufuatilia kwa karibu sana maisha/nyendo za yule anayemlinda. Kwa dhana ya ndoa yako, ni jukumu lako kama mlinzi kufuatilia maisha ya mume wako na kujua kama anaishi katika mapenzi ya Mungu. Naam ukijua anaishi nje ya mapenzi ya  Mungu unanafasi kubwa kumsaidia kwa kusuguwa goti lako kwa maombi.

Patrick Sanga

6 thoughts on “UPONYAJI WA NDOA

  1. kokusima ni maandiko kubali nafasi yako na usimame hapo Mungu amesema ujenge nyumba yako, ulinde mume wako, usiulize kwanini mimi tu nimlinde na nijenge nyumba yangu? ukikosea Mungu atakuuliza umefanya nini?, kama alivyoulizwa eva mke wa adam

  2. Kokusima, ni kweli hata maisha tuliyolelewa tangu utotoni mabinti ndio wanaonekana kupewa mafunzo na maonyo kuliko wanaume, na hata ukubwani wanaolaumiwa ni wanawake, kila kitu wanawake. Hivi ni kweli ndio wanaolewa matatizo ya ndoa?

  3. Asante kwa ujumbe mzuri wa ndoa, ila huwa napata shida sana, hivi ndoa inapokuwa na matatizo kwanini wanaume nao hawaambiwi wasimame katika nafasi zao? siongei hili kwa kuwa labda ni mfuasi wa masuala ya kijinsia ila natamani kweli kama wanaume nao wangekuwa wanapewa somo kwasababu kwa kiasi kikubwa wanachangia sana katika matatizo ya ndoa na si tu kwamba ndoa ikuyumba basi mwanamke hajasimama katika nafasi yake na hivyo Mungu hawezi kumsaidia. Ningeomba pia wanaume wakumbushwe kusimama katika nafasi zao kwani wao ndio hasa kichwa cha familia.

  4. Ubarikiwe mtumishi kwa ujumbe mzuri ambao umekuja kwa wakati muafaka.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s