Mstari Unaoniliza Kuliko Yote Katika Biblia – XIX

Ndugu zangu, leo tunaendelea na MISINGI ya Mkristo katika sehemu hii ya Kumi na Tisa na ambayo ndiyo ya mwisho katika Somo hili la Mstari unaoniliza Kuliko Yote Katika Biblia.  Katika sehemu iliyopita, ya Kumi na Nane, tuliishia msingi wa Tatu ambao ni Mafundisho ya Mabatizo. Sasa tuendelee…

4.Kufufuliwa Kwa Wafu. Jambo tunalopaswa kuelewa hapa ni kuhusu UFUFUO WA WAFU. Tuelewe vizuri kabisa kuwa kuna maisha baada ya kufa, japo hili si tatizo kubwa kwa watu wengi maana inapotokea mtu amekufa utasikia wanasema MUNGU AMWEKE MAHALI PEMA PEPONI. Japo ni maombi lakini hayo ni maombi SIFURI. Fuatana nami vizuri ili uelewe, wengine wanapeleka sadaka kwa viongozi wa dini kila mwaka kuwaombea ndugu zao waliokwisha kufa! Ndugu yangu unapoteza hela yako bure, hakuna kitu kama hicho.

Katika Mhubiri 12:7 Biblia inasema siku  ya mtu kuondoka duniani roho humrudia aliyeiumba, na mwili unarudi mavumbini. Nadhani hilo halina tatizo wengi wetu tunajua hilo.

Kwenye Kumb 34:1-7 tunaona Musa alipokufa mambo yake yaliishia hapo katika mwili.

Tukisoma pia katika 2Falme 2:7-11 Hapo tunamwona Eliya akipaa kwenda Mbinguni, kama Biblia inavyotueleza.

Kwenye Math 17:1-5, Hapo sasa tunaona baada ya miaka mingi ilipita tangu Musa afe na Eliya apae, Yesu akaja duniani, na tunaona hapo Eliya na Musa wanamtembelea (Yesu). Unaona jambo la ajabu kidogo: Musa alikufa, Eliya alinyakuliwa, kumbe walikutana, na wote wakafunga safari kuja kumtembelea Yesu katika mlima aliogeukia Sura. Hii inatupa matumaini, kwamba, kumbe mtu akifa huwa yuko mahali!

Math 27:51-54. Hapo ni wakati Bwana wetu Yesu alipokata roho msalabani, jambo kubwa lilitokea, makaburi yalifunguka, miili ya wengi waliokuwa wamekufa kitambo ikainuka na kuwatokea wengi. Hii pia inatuonyesha, na kuthibitisha kile Bwana wetu Yesu alichosema kuwa MIMI NDIO HUO UFUFUO.

Yoh 11:38-44. Hapo utaona uthibitisho kabisa kuwa siku moja katika kuishi kwake katika mwili, mtu mmoja aliyejulikana kama Lazaro aliugua.Dada zake wakatuma mtu akamwite Yesu. Alipokwenda kumwita, Yesu hakufanya haraka kuja, mpaka zikapita siku nne, mwisho Lazaro akafa, akazikwa, na wakawa wamekaa katika matanga, mwisho Yesu alikuja, akamkuta amekuwa kaburini kwa siku nne tayari!  Maandiko yanaonyesha jinsi Yesu alikuja, akamfufua Lazaro, akaendelea kuishi tena.

Maandiko niliyoweka hapo juu yanatuhakikishia kabisa kuwa kuna maisha baada ya kufa. Na watu wengi sana kama si wote wanaamini hivyo! Ila sasa mahali panapochenga watu ni namna gani wajiandae kabla hawajafa. Hilo ndilo tatizo. Wengi, kama nilivyosema, hawajiandai kwa kuwa wanafikiri kuwa wataombewa. Sasa nakuomba ufuatane nami kwa makini nikuonyeshe kitu.

Kabla mtu hajafa anatakiwa achague. Yeye mwenyewe aamue, na hakuna njia nyingine ambayo mtu atapita ili aweze kumuona Mungu. Maandiko yanasema kuwa baada ya kufa ni HUKUMU siyo baada ya kufa ni KUOMBEWA. Ebu thibitisha hili katika Waebrania 9:27 “Kwa kuwa watu wanawekewa kufa mara moja na baada ya kufa hukumu”- Unaona mstari huo unavyosema? Wengi hawajauona, ndio maana  wanangoja kuwa baada ya kufa WATAOMBEWA.  Ndio maana wengi pia huombea wafu, wengine humwambia Mungu: “MUWEKE PEMA PEPONI”. Ndugu yangu mtu mwenyewe ndiye anachagua kwenda pema peponi au kwenda kubaya motoni. Unaamua kwa njia gani.?

Rumi 10: 9-10. “Kwa sababu ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako kuwa Mungu alimfufua katika wafu utaokoka. Kwa maana kwa kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu”  (unaona vile wokovu wako ili uwe na maana ni pale unapokiri kwa kinywa, na kupata haki ni pale utakapoamini kwa moyo wako).

Nimesema baada ya kufa huwa hakuna nafasi tena ya KUTUBU  wala KUOMBEWA. Ebu tuangalie Yesu alivyofundisha hilo katika Luka 16:19-31:

“Akasema palikuwa na mtu mmoja tajiri, aliyevaa nguo za rangi ya  zambarau, na kitani safi, na kula siku zote kwa anasa, na maskini mmoja jina lake Lazaro, huwekwa mlangoni pake, ana vidonda vingi, naye alikuwa akitamani kushibishwa kwa makombo yaliyoanguka mezani pa yule tajiri. Hata mbwa wakaja wakamramba vidonda vyake. Ikawa yule masikini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani mwa Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa, akazikwa. Basi kule kuzimu aliyainua macho yake alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahim kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake. Akalia akasema; ee baba Ibrahim nihurumie! umtume Lazaro achovywe ncha ya kidole chake majini aburudishe ulimi wangu, Kwa sababu ninateswa katika moto huu. Ibrahim akajibu  akasema kumbuka ya kwamba wewe uliyapokea mambo mema yako katika maisha yako, na Lazaro vivyo alipata mabaya, na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa, na wewe unaumizwa. Na zaidi ya hayo kati yetu sisi na ninyi kumewekwa shimo kubwa, ili wale watakao kutoka huku kwenda kwenu wasiweze, wala watu wa kwenu wasivuke kuja kwetu. Akasema ninao ndugu watano, ili awashuhudie, wasije wao pia wakafika mahali hapa pa mateso. Ibrahimu akasema wanao  Musa na Manabii wawasikilize wao. Akasema; la! baba Ibrahim, lakini kama akiwaendea mtu atokaye kwa wafu watatubu. Akamwambia, Wasipowasikiliza Musa na Manabii, hawatashawishika hata mtu akifufuka katika wafu”

Ndugu yangu, hebu tazama jinsi Bwana Yesu alivyoeleza suala hilo wazi wazi. Kama kungekuwa na kuombewa, basi huyu tajiri angeombewa, lakini hakuna, na unaona ndipo alikumbuka hata ndugu zake, akatamani awaambie wao wasije wakaenda aliko, lakini unaona hakukuwa na uwezekano wowote. Ukitaka kuwasaidia ndugu zako ni wakati wakiwa hai, baada ya kufa hakuna namna utakavyoweza kuwasaidia tena!

5. Hukumu ya Milele. Uf 20:11-15 “Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake, ambaye Nchi na Mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana, nikawaona wafu wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi, na vitabu vikafunguliwa, na kitabu kingine kikafunguliwa ambacho ni cha uzima, na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawa sawa na matendo yao. Bahari ikawatoa wafu waliokuwemo ndani yake, na mauti na kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake, wakahukumiwa kila mtu kwa kadri ya matendo yake. Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto.Hii ndiyo mauti ya pili, yaani hilo ziwa la moto. Na iwapo mtu yeyote hakuonekana ameandikwa katika cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto”.

Ndugu zangu habari ndiyo hiyo, kuwa, kuna HUKUMU ya MILELE. Ni vizuri tufahamu hivyo, maana pia kuna mafundisho yasiyo ya kweli kuwa kuna mahali ambapo watu watawekwa wateswe kidogo, kisha wapelekwe mahali pazuri baada ya hayo mateso kidogo. HAPANA! (kwa herufi kubwa). Tunafundishwa kabisa na Biblia kuwa kuna ufufuo wa watu wote, ili kila mtu apokee zawadi, au ujira wa kazi yake aliyoifanya duniani akiwa katika mwili. Biblia inaeleza wazi kabisa. Hebu tuthibitishe tena na hili katika Daniel 12:2: “Tena wengi wa hao walalao katika mavumbi ya nchi wataamka, Wengine wapate uzima wa milele, wengine aibu na kudharauliwa milele.”

Ndugu yangu, Biblia haikuficha kitu. Sisi tunapaswa kufuata kile inachosema. Tunapaswa kuiamini. Mungu aliishaweka utaratibu wake. Sisi tunatakiwa kukubali na kuufuata ndipo tutakuwa salama. Unaona hata kuingiza watu Jehanam aliweka mpangilio, sio holela, wapo watakaotangulia, na watakaomalizia, ona jinsi ilivyopangiliwa, tuendelee kujifunza kutoka kwenye Biblia kwenye Uf unuo19:20, “Yule mnyama akakamatwa, na yule Nabii wa uongo pamoja naye, yeye aliyezifanya hizo ishara mbele zake, ambazo kwa hizo aliwadanganya watu wale walioipokea ile chapa ya huyo mnyama, nao walioisujudia sanamu yake, hao wawili wakatupwa wangali hai katika lile ziwa la moto liwakalo kwa kiberiti”. Hao ndio watakaofungua Jehanam…

Ufunuo 20:10 “Na yule ibilisi mwenye kuwadanganya, akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule mnyama na nabii wa uongo, nao watateswa mchana na usiku, hata milele na milele”. Huyo ndiye atafuatia kuingia Jehanam…

Ufunuo 20:1- “Mauti na kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto,hii ndiyo mauti ya pili, yaani hilo ziwa la moto”. Hao nao watafuata kuingia Jehanam…

Ufunuo 20:15- “Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.”. Jehanam haikuumbiwa mwanadamu, Mungu alimpenda mtu mno, ndio maana unaona atamwingiza mwishoni kabisa! Atakuwa ni mwanadamu aliyeamua kumkataa Yesu, ndiye atakutana na moto huo. Anayesubiri akifa aombewe. Hebu nikushauri hivi: Amua kuchagua Yesu awe mwokozi wako kabla hujaondoka  katika mwili wako!

Ndugu yangu tumeiangalia misingi ya Mkristo tunayotakiwa kuiimarisha katika maisha yetu ya kiroho ikiwa tunataka kuyaona maisha yetu ya baadae, baada ya kutoka mwilini huu. Kwa kuwa bado ungali hai, fanya uamuzi leo. Njia pekee ni YESU. Hakuna  njia nyingine ya kufika kwa Mungu  muumba Mbingu na Nchi!

Mungu atusaidie tufanye uamuzi sahihi, tusije tukajuta mwishoni. Kumbuka ile mithali ya kiswahili inayosema- MAJUTO NI MJUKUU!

Mbarikiwe na Bwana kwa kufuatana nami kuanzia sehemu ya Kwanza ya somo hili. Na ninamuomba Mungu wa mbinguni azidi kuwajalia kuyatafakari yote tuliyopitia katika somo hili ili kila mtu aweze kuyafanyia kazi.

Ni mimi Ndugu yenu Mch. Samweli Imori.

 

Advertisements

13 thoughts on “Mstari Unaoniliza Kuliko Yote Katika Biblia – XIX

 1. Nimebarikiwa Sana Na Mafundisho Yako Mch.Mungu Akubariki Sana,japo Mimi Sijaokoka Na Wala Siudhuri Katka Ibada Ya Kanisa Lolote Lakin Napenda Kuona Neno La Mungu Linasambaa Na Kumfikia Kila Mtu,nampenda Sana Mungu Na Mungu Huyo Akutie Nguvu Katka Kazi Ya Mungu.

 2. Nimfuatilia vizuri mafundisho haya ila kuna utatanishi kidogo naupata.
  Tunaona baada ya tajiri kufa hapohapo akazikwa kaburin,na alipokua katika mateso ya moto alimuomba Ibrahim amtume lazaro achovye kidole ili auburudishe ulimi wake.
  Na hapo mwishoni umemalizia kua jehanamu haikuumbiwa mwanadamu na pia mtu ataingia hukumuni mwishoni ndio kutupwa kwenye ziwa la moto

 3. Ndugu Wapendwa,

  Tunamshukuru sana Mungu kwa SOMO hili ambalo ametuletea KUPITIA kwa Mchungaji Samuel Imori.

  Kwa ndugu Lazaro na mwingine anayeguswa moyoni mwake kwa ajili ya kufanikisha UCHAPISHWAJI wa Kitabu cha Somo hili, Mungu ambariki sana, sana!

  Namna ya KUTUMA PESA kwa mchungaji Samuel Imori ni kupitia M-PESA, kwa namba ya mchungaji, +255 765 446611. Asante kwa mchango wako.

  Tunamwamini Mungu kuwa kazi hiyo itakamilika na mchungaji Samuel Imori ataendelea kutupatia ushuhuda wa mambo yanayoendelea huko.

  …..amina!

 4. Nadhani hakuna sababu ya kila anayeona kubarikiwa na mafundisho haya kutokujitia nguvu katika kuhusika kwenye njia ya kufanya ukamilishaji wa kuandaa kitabu hiki unafikiwa. Nawaomba ndugu wenzangu tuliopata nafasi hii kumtaka Pastor Imori kututumia njia rahisi ya kutoa michango yeto ili lengo la Mungu lifikiwe. Kama inawezekana tungepata mchanganuo wa kufikia lengo hili la uaandaaji wa kitabu.
  Ni mimi na niko tayari kuchangia 50,000. sasa ni wapi naweza kupata njia ya kutuma?

 5. Muda wa Mungu ukifika umefika, ni Mungu anasema nanyi kuthibitisha kuwa muda wa kutoa kitabu hicho umefika, ninakiandaa, naamini muda mrefu kuanzia sasa kitakuwa kinatoka, ambacho kitabeba tangu somo la kwanza mpaka la 19. Naamini kitakuwa msaada kwa watoto wa Mungu. Ombi langu ninahitaji maombi yenu, ili aniwezeshe, kinahitaji kuhaririwa, na kuchapwa, hela pia inatakiwa. Pia nawashukuru sana wote mliofuatilia mfululizo wa masomo hayo, nawashukuru wote mliochangia mawazo ama kwa kuuliza maswali, ama kwa kutoa ushauri, au kwa kunitia moyo, Mungu awabariki wote. Amina.

 6. Bwana Yesu akubariki na kukutia nguvu mchungaji ninabarikiwa sana na mafundisho yako.Ombi langu ni kwamba kama upo uwezekano uyaweke pamoja kuanzia sehemu ya kwanza hadi ya mwisho kwenye kitabu au cd kama alivyopendekeza mpendwa Aika hapo juu. Mimi binafsi kuna sehemu nyingi zilinipita.

 7. Mungu akubariki sana mch Imori, nimekuwa mfuatiliaji mzuri wa mstari unaoniliza kuliko yote kwenye biblia, ingependeza tuone kwenye kitabu au kwenye CD, Ubarikiwe kwa kazi njema.

 8. Asante Joseph, ubarikiwe nawe pia. Shirikisha na wengine ili waweze kujifunza Neno la Mungu katika Blog hii.

 9. Asante sana mch. Imori kwa kunijuza habari njema za blog hii. Mungu akutie nguvu uzidi kutufundisha.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s