Mwimbaji wa nyimbo za Injili awa Raisi Shirikisho la Muziki Tanzania

Addo November na binti yake

Mwanamuziki Wa Injili Tanzania Addo November Mwasongwe ambaye pia ni Rais wa Shirikisho la Muziki wa Injili Tanzania ameshinda katika Uchaguzi wa Kutafuta Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania inayoundwa na (CHAMUHADA, TAFOMA, INJILI, KIZAZI KIPYA, ASILI, DISCO).

November ameteuliwa Kuwa Rais Wa Mashirikisho hayo Tanzania. Uchaguzi huo Uliofanyika BASATA mchana huu umempa Ushindi wa Kishindo Muimbaji huyo wa Injili.

Addo November Amewashinda Washiriki wengine wa Kinyang’anyiro hicho wanne Abdul Elsavador, Mkoloni (Tanga Kunani) na Samuel Semkuruto ambapo Addo alipata Kura 8 Mkoloni Semkuruto Kura 4 na Elsavador Kura 4. Uchaguzi huo Uliomalizika Mchana huu saa 7:40 Unamfanya Addo November kuwa Rais Wa mashirikisho hayo kwa Muda wa Miaka 3 Mfululizo.

Addo November ni Mwanamuziki wa Injili anayetamba na Albam yake ya “Utabaki Kuwa Mungu”, Ni Baba wa Watoto Wawili na Mke Mmoja, Ni Mwanasheria (Advocate) na Sasa ni Mwajiriwa pia Wa Taasisi Moja Nyeti Ya Serikali Kama Mwanasheria wa Taasisi hiyo ya Fedha hapa Tanzania.

Addo alipochukua fomu za kugombea kiti cha ubunge jimbo la Iringa mjini kwa tiketi ya CCM, 2010

Sam Sasali Blog

Advertisements

5 thoughts on “Mwimbaji wa nyimbo za Injili awa Raisi Shirikisho la Muziki Tanzania

  1. Mpendwa,

    Kazi unayo. Tunaomba waimbaji wote wanaoimba wakiwa wamevaa nguo fupi au zisizokuwa na viwango vya maadili ya maandiko ya Biblia uwaweke kwenye ajenda kuu ya kufanyia kazi.

    Aidha, Rose Mhando na Band yake naomba siku moja umwitishe ukae naye umuulize ni kwa nini mara nyingi huvalia nguo ambazo hazina viwango vya maandiko? Siyo Rose Mhando pekee yake na wengine pia.

    Mungu akupe roho ya Ujasiri na Ushujaa.

  2. Miziki isiyokuwa na maadili katika jamii naamini utaliona hilo mtumishi wa Mungu.

  3. safi sana Ado kwa kushinda ,kitu kimoja tu ni kwamba shikilia imani yako ,na uchuchumalie yaliyo juu mbinguni si ya duniani,kuna kusudi Mungu kukupa hiyo chance,Aonekane Yesu ktk utendaji wako kila siku.

  4. Hongera Addo November, Mungu amekuweka kwa makusudi hapo fanya kazi kama Roho atakavyokuongoza.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s