Waimbaji ”KWETU PAZURI” Wawasili Dar Leo

Sarah Uwera mmoja wa waimbaji wa kundi hilo, walipotembelea nchini mwaka jana

Kwaya ya Ambassadors of Christ kutoka jijini Kigali nchini Rwanda imewasili leo Jijini Dar es salaam wakitokea nchini kwao Rwanda, tayari kwa ajili ya kutoa huduma ya uimbaji katika mkutano mkubwa wa kimataifa unaofanyika katika viwanja vya Biafra Kinondoni jijini Dar es salaam.

Kundi la kwanza la kwaya hiyo liliondoka jana kwa njia ya basi kuja jijini, huku kundi la pili ndio limewasili leo mchana.

Hii itakuwa mara ya nne kwa waimbaji hao kufika nchini ambako wamekuwa na mashabiki lukuki, kutokana na uimbaji wao, ambapo safari hii wanatarajia kuwepo kwa wiki nzima jijini Dar es salaam ikiwa maalumu kwa mkutano huo,Pia wanatarajia kuwasili na toleo lao jipya la kanda ambalo baadhi ya nyimbo zimeanza kusikika katika vituo vya radio za injili jijini Dar es salaam.

Kanda mpya ya Ambassadors of Christ Rwanda.

—GospelKitaa blog

8 thoughts on “Waimbaji ”KWETU PAZURI” Wawasili Dar Leo

  1. Hongereni sana na barikiwa na nyimbo zenu na mavazi yenu kwa ujumla nimeyapenda hii itawabadilisha hata watanzania amboa hawatumii mavazi ya heshima katika kutangaza injili wabadilike kimavazi Mungu azidi kuwatia nguvu zaidi katika kumtumikia. amen

  2. hongereni jamani kwa kumwimbia Bwana, nyimbo zenu zinanibariki sana Mungu awabariki sana wapendwa katika Bwana.

  3. Mungu awabariki sn. mbali ya kutubariki na nyimbo zenu waimbaji wetu wa Tanzania nao hujifunza kitu kutoka kwenu.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s