Nukuu ya TB Joshua kuhusu ajali ya Kenya

Jumatatu ya tarehe 4, June 2012, Nabii T.B Joshua alitabiri kuhusu kiongozi wa nchi. Aliona ajali na kusema kwenye ibada hiyo kama ifuatavyo:

Ninety percent of what we’re doing here is all about other nations all over the world. Like today, around 3am and what happened. I saw the leader of a country. Whether he is the Vice President of a country or the present— I saw all of them having an accident. Is it on the air or on the ground? Sometimes, when I want to know what is happening, how does it happen, what is this, I keep asking.

Baada ya siku sita, Jumapili ya tarehe 10. Helicopter ya Kenya ikapata ajali na kuua waziri George Saitoti na wote waliokuwa ndani ya ndege hiyo.

Advertisements

100 thoughts on “Nukuu ya TB Joshua kuhusu ajali ya Kenya

 1. Nawauliza ni wapi mnapata ujasiri wa kum-disqualify TB Joshua.

  For me I believe 100% that P/TB Joshua is a man of God. I will always pray for you TB Joshua, and please pray for me, I now see light starting on my life, thank you man of God.

 2. Milinga, ndugu yangu mbona unakuwa kama pendlum! Yaani unabakiza jino moja tu uwe umemaliza mzunguko uingie katika umilele, lakini unarudishwa tena chini kama kifaranga cha kuku na kuanza kuchakura tena mavumbini! 

  Unabii kwetu sote hauko mbali kama ulivyoaminishwa na akina TB Joshua. Haujaelewa mpaka leo Maandiko yanachokufunza? Achana na utumwa wa miujiza na unabii uchwara, yatazame mambo makuu Mungu aliyokufanyia wewe usiyestahili! Fungua moyo wako huo mgumu wa jiwe usioyatazama Maandiko ktk shauku ya kumjua Mungu ni nani na uhusiano wako binafsi na yeye ni upi, badala yake wahubiri wamekugeuza chombo chao cha kueneza himaya zao ukijidhania unamtukuza Mungu, kumbe kwa jinsi ulivyolaghaiwa, Mungu mwenyewe ulimuacha siku nyingi nawe hujui!! 

  Kristo anasema hivi: akija huyo Roho  Mt atawaweka ktk kweli yote, atawakumbusheni mambo yaliyopita na kuwaonesheni ya sasa na yajayo! Umeelewa maana yake? Huo unabii unaoupapatikia uko katika kuoneshwa hayo yajayo!!! Sasa kipi ni bora, kukumbushwa yaliyopita na kuoneshwa ya sasa na yajayo au kuoneshwa yajayo tu?? Agabo alipomtolea unabii Paulo, je, mtume Paulo alishtuka?? Haujilizi kwanini alitulia na kuendelea na safari yake hukohuko kwenye hiyo shida aliyotabiriwa? Au Maandiko unayoyaona ktk Biblia, hayo yaliyotokana na mitume, hauyaoni kuwa ni prophetic, yakitanukia nyakati mpaka huu tulionao and yet kati ya hao mitume hakuna hata mmoja anayetambulika kama nabii?? 

  Wakati mwingine huwa unanishangaza sana, nashangaa unawezaje kufika katika kiwango cha kuyatafuta Maandiko kama hayo unayoniambia nisome Hes 11:23-30 na kuniwekea msisitizo kwa kifungu cha 29 halafu hata hujui kuwa hao 70 walikuwa ni kivuli tu, bali hicho kifungu cha 29 kinatimia kuanzia siku ya Pentekoste, Mungu amemwaga unabii bwerereee! Wewe ulikuwa wapi? Ulikuwa kwenye ile ibada ya miungu watatu??

  Acheni mambo ya mapokeo mfunguke macho yenu ya kiroho. Mungu mwenyewe mmemgawa sehemu tatu halafu mnategemea awafanyie nini ktk siku kama hii ya leo ambapo nyote mmpewa fursa ya kuyakagua Maandiko nanyi mmeyang’ang’ania mafundisho yenu? Haushangai kuinuka kwa ghafla kwa marundo ya manabii? Unadhani wameinuka bure au kwa njaa yao? Pole sana, mlipoikataa kweli kwamba Mungu ni mmoja mkang’ang’ania miungu watatu mliodanganywa kuwa ni mmoja licha ya kupewa fursa ya kuukimbia uongo, sasa mmeletewa a strong delusion, ndio hao manabii wenu wasio na Andiko lolote ila miujiza tu! 

  Milinga, Roho mt ndani yako ndiye Nabii, atakuonesha yote, mpaka Uongo wa TB Joshua utauona, maana Roho Mt atakukamilisha akikuweka katika kweli yote, ndipo utajua kuwa hiyo HolyGhost Fire in the name of Jesus ni enchantment tu ktk realm za spiritualism!! Kwa taarifa yako Yuda Iskariote alifanya miujiza na bado alikuwa Ibilisi, je ungekutana naye leo akakuomba umsindikize akachukue zile shs 30, si ungeongozana naye! Basi elewa Maandiko yanachokufundisha, roho iliyokuwa juu ya Yuda ilirudi kanisani kama ilivyorudi Roho ya Kristo na roho hizo mbili zinaendelea kama ilivyokuwa huko nyuma, ila roho ya Yuda inaukwepa UBATIZO WA ROHO MT kwavile inajua utamuua ! Kama alivyoukimbia Yuda asiifikie siku ya Pentekoste, nayo roho hiyo leo hii inaukimbia Ubatizo kama ulivyo ktk Mdo 2:38 ambao unaokuleta ktk UBATIZO WA ROHO MT ambao ni moto ulao!!!  Jihadharini na ushabiki wa miujiza mtapotea nayo!

  Nabii humuwakilisha Mungu, au mitume walikuwa ni timu ya mpira? Acheni kumdhalilisha Kristo! Hivi Mungu anaweza akafanya kazi yote ile ya kupigwa mijeredi, kupigiliwa misumari butu, kuchomwa mikuki na kudhihakiwa jinsi ile ili aje awatabirie mpira wa afcon? Halafu of all the people wewe Milinga ambaye najua ni smart, unasema eti it is worth it!!! Hebu fikiria ni roho ngapi ulizoziongoza kwa huyo Balaam? Huna hata andiko moja la kujitetea nalo ukiitwa Hukumuni, mimi mwenzio nakomaa, sio kibwege. Nikiitwa Hukumuni nitamwambia Mungu anioneshe mahali alipotuambia kuwa “Roho Mt alishirikiana na Baba na Mwana kuumba ulimwengu” HAKUNA!!! Wewe je???

  Bwana na akupe macho ya rohoni!

 3. Milinga na Orbi, nimependa sana na nasikia raha hapa na kubarikiwa mnavyomenyeshana katika upendo lakini but pia kwa hoja nzito tena with nukuu za maandiko, this is real what we need here . Powerful mandiko Milnga umetoa a very correct ufafanuzi na poweful again maandiko Orbi umeoa na very correct ufafanuzi, so nadhani mmetusaidia sasa tuamue na kuhitimisha kwa anayekwenda upande wa kamanda Milinga na achanje mbuga na anyebaki kwa mjeshi Orbi na atulie…..mi niko kwa Orbi ila balance yangu binafsi ni manabii wa kanisani kwangu na Tanzania wananiitosha sana kujua mambo ya Mungu kuhusu my persona life, familia, jamii yangu, Nchi, Mabara an ulimwengu

 4. Milinga,

  Nilipoiona post yako niliikimbilia nikijua umekuja na hitimisho research ambayo uliisema unaifanya kuhusu Nabii huyu, lakini naona unaturudisha kule kule tena, sijaona jipya lolote unalolizungumza.

  Kwangu mimi naona umejikita pale pale…yaani Yesu anahuburiwa….Miujiza kwa jina La Yesu inafanyika……watu “wanafunguliwa” Mahali ambapo ni kinyume kabisa na Mafundisho ya Yesu na hata Paulo mwenyewe.

  Hivyo kwa nini Yesu katika Mathayo alisema “wengi wataniambia hatukufanya unabii kwa jina lako…? Na kufanya Miujiza mingi kwa jina Lako…..? Mbona Yesu hakusema maadam wanatoa unabii kwa jina langu….au maadam wanatoa Pepo kwa jina langu…basi Wasikilizeni hao…!

  Jiulize sana kwa nini Yesu alirudia tena maneno haya katika Mathayo 24….”Na manabii wa uongo nao watatoa ishara kubwa na maajabu hata kuwapoteza yumkini hata Wateule” Kama hayakuwa na msisitizo kwa yamerudiwa na Paulo naye karudia maneno kama haya hayo?

  Paulo Mwenyewe kasema si kila INJILI ni injili ya Kristo…! Si kila Yesu anayezungumzwa ni Yesu wa Biblia..! Kwa hiyo si kila Nabii anayemzungumza Yesu ni ni Nabii aliyetumwa na Yesu….! Na si kila Muujiza haya ukifanyika kwa jina Yesu umetoka kwa Yesu aliyejidhirisha katika Maandiko…!

  Kwangu mimi huyu Nabii wa Nigeria anaangukia katika kundi hilo…! Mtihani wa awali kabisa ambao kwangu mimi unamwondoa ni wa Nabii zake…..sina haja kabisa ya kuzirudia hizo nabii hapa…..na kuanzia hapo ananipa hata mushkeli wa hiyo inili yake……!

  Hivyo ndugu yangu Milinga kama wewe umepata ufunuo kuhusu huyu Nabii kuwa ni Bwana ubarikiwe…….kwa wengine tunamashaka ni nguvu nyingine kabisa…….Kwa mtu anayeangalia kiroho hasa akiliangalia kanisa la leo na nini hasa kinatakiwa ili kuleta uamsho wa Mungu, tunamshangaa hiyo “roho” ya unabii inayokuja mara na matokeo ya mpira wa miguu……! mara na Helkopta ya mwanasiasa wa Kenya….mara kifo cha raisi wa Malawi…..! Hiyo mbingu inayoleta mafunuo haya hakika si Mbingu ile inayopokea maombi ya watakatifu wanaolia usiku na mchana juu ya hukumu itakayoupata ulimwengu…..! Mbingu inayomleta mafunuo haya ni hakika kabisa ni mbingu ya kuzimu…..!

 5. Wapendwa, CK Lwembe

  WEWE HUTAMANI WATU WOTE WANGEKUWA MANABII?

  MIMI NATAMANI WAPENDWA WOTE WANGEKUWA MANABII, KAMA MUSA ALIVYOWAHI KUTAMANI ENZI ZAKE(Soma kisa cha Musa uone hapa chini)

  Enzi za Nabii Musa kuliwahi kutokea kutoelewana kuhusu Nabii Musa. Kuna watu walianza kuwa na maswali sana kuhusu unabii na mafundisho ya Musa lakini Musa akawakemea wote na Mungu akalazimika kutwaa sehemu ya roho ya kinabii ya Musa akawamwagia wale wazee sabini aliokuwa nao.

  Hebu soma Hesabu 11: 23-30 naomba ninukuu maneno machache tu, “………..Ndipo Bwana akashuka ndani ya wingu, akanena naye, akatwaa sehemu ya roho iliyokuwa juu ya Musa akaitia juu ya wale wazee sabini, ikawa, roho hiyo ilipowashukia wakatabiri, lakini hawakufanya hivyo tena. ………. lakini watu wawili waliosalia kambini…. walikuwa hakutoka kwenda kambini; nao wakatabiri kambini. Mtu mmoja akapiga mbio kwenda kumwambia Musa, akasema Eldadi na Medadi wanatoa unabii kambini……”

  Ukisoma zaidi utaona kwamba Joshua mwana wa Nuni alipatwa na roho ya wivu moyoni mwake akaenda kumwomba Musa awakataze waachane na maswala hayo ya kutoa unabii kambini. Yoshua alijawa na ghadhabu akisema kwamba hakuna Nabii zaidi ya Musa aliyepaswa kutoa unabii pale kambini.

  Sasa tazama Musa Nabii alichomjibu Joshua mwana wa Nuni. Soma mstari wa 29. Musa alivyomjibu. Nanukuu, “Musa akamwambia (Yoshua), Je, umekuwa na wivu kwa ajili yangu, INGEKUWA HERI KAMA WATU WOTE WA BWANA WANGEKUWA MANABII……..”

  Wapendwa wote kama wangekuwa manabii wa Bwana wanaotabiri mambo yajayo na yaliyopo au yaliyopita, kwa kweli dunia ingefaa kuishi. Lakini leo hii kuwapata manabii imekuwa nadra sana katika nchi zetu na makanisa yetu. Nadhani hii inatokana na mafundisho mengi kama ya akina CK Lwembe yanayokataza ka nguvu zote watu kuwa manabii kwamba nabii ni Roho Mtakatifu tu basi. Lakini je, hiki alivhokuwa anatamani Musa enzi zile kwa leo hakiwezekani?

  Nadhani watu wanasahau kwamba maandiko yanasema kwamba siri nyingi za Kristo zimefunuliwa kwa kanisa kupitia watumishi wa Mungu Manabii na Mitume. Juzi juzi nilisikiliza mhubiri mmoja anayeitwa Mzee wa Upako au Antony Lusekelo akasema kwamba nyakati hizi hakuna mitume wala manabii. Akaongeza kwamba haya ni mafundisho potofu toka Nigeria na nchi za Afrika ya magharibi. Lakini hebu ona maandiko yasemavyo: Efeso 3: 5-6, “……Siri hii haikudhihirishwa kwa wanadamu katika vizazi vingine kama vile sasa ilivyodhihirishwa na Roho kwa mitume na manabii watakatifu wa Mungu. Siri hii ni kwamba, kwa njia ya Injili, watu Mataifa ni warithi pamoja na Israeli, viungo vya mwili mmoja na washiriki pamoja wa ahadi katika Kristo Yesu….” Kwa hiyo unaona kwamba kanisa limepewa manabii ili waweze kuleta siri zaidi za Kristo kwa kanisa na kwa dunia yote.

  HATA KAMA WATU HAWANA NIA NJEMA TUSIWAKATAE

  Wapendwa kumezuka utamaduni hapa Tanzania na kwingineko duniani wapendwa wengi kuwakataa manabii na mitume kwa hoja kwamba hawakubaliani na mafundisho yao au unabii wanaoutoa. Huku ni kwenda kinyume na Biblia.

  Wengi wanadiriki kuwakataza waumini wao, wengine huwatenga kabisa endapo watabaini kwamba waumini wao wamekuwa wakifuatilia TV, Mikutano au semina za hao waitwao manabii au mitume. Huku pia ni kuingiwa na ukengeufu. Haifai.

  Si, Mungu wala Maandiko yake wanaosema hivyo. Ni kweli maandiko yanasema kwamba zipimeni roho hizo muone kama zimetokana na Mungu, pia maandiko yanatuka tuwatambue kwa matunda yao hao waitwao manabii au mitume au wachungaji, wainjilisti tuone kama ni kondoo na wala siyo umbwamwitu.

  Pamoja na maandiko haya kusema hivyo, Mtume Paulo anatuasa akitukumbusha kwamba wengine wanahubiri Injili kwa sababu ya husuda na fitina, wengine kwa nia njema. Paulo anasema kwamba wapo wanaohubiri kwa pendo ili kuitetea Injili na wapo wanaoihubiri Injili wala si kwa moyo mweupe. Mtume Paulo anauliza, Yadhuru nini? Ikiwa ni kwa hila au ikiwa ni kwa kweli KRISTO ANAHUBIRIWA na kwa hiyo Paulo alifarahishwa na hilo tena sana (Soma Filip 1:15-18).

  Hata mimi naungana na Mtume Paulo kusema kwamba kama kuna watu wanamhubiri Kristo kkwa hila yaani wana ajenda zao za kujipatia fedha yaani wanamtumikia Mungu kwa sababu ya Matumbo yao au ni wachungaji wa mishahara, au siyo manabii wa kweli, kwa kuwa wanamtangaza YESU KRISTO MIMI NINAFURAHI SANA.

  Kama TB Joshua na wengine wanaokataliwa na wapendwa wengi ataendelea kumhubiri Kristo na akaendelea kuombea watu wamfuate Kristo na kuachana na uovu, kama ataendelea kuharibu kazi za giza na kusimamisha utawala wa Mungu, iwe ni kwa hila au kwa nia njema moyoni mwake mimi nitaendelea kufurahia.

  Naelewa kwamba unabii hautampeleka mtu mbinguni awe ametabiri sawa au isivyo sawa, mimi nafurahi kwa sababu anafanya kazi ya Injili na kama Paulo alivyosema, hata mimi nitafurahi sana.

  Lwembe unaonaje ujumbe wa leo? Karibu.

 6. Ndg Leons,
  Time has already done the Telling, kilichobakia ni masikio sikivu tu, yanayoweza kuisikia sauti ya Mungu!

  Kwamba unaendelea kumchunguza nabii wako, hilo ni jambo jema, ila nakushauri usipime kwa miujiza bali kwa Neno la Mungu. Litangulize hilo utakuwa salama.

  Kwamba sote tuko safarini, hilo ni kweli, hata mimi sijafika bado, bali safari ni tamu sana ninapowafuata mitume wakiwa ndiye Roho Mt!! Kwa hiyo si suala la kumuamini nabii fulani, la hasha, bali tunaliamini Neno la Mungu na mtumishi yeyote anayelifuata Neno hilo hata akiwa ni TB Joshua.

  Kwa hiyo ndugu yangu, hatushindani, bali tunajitahidi kutembea ktk njia ya Injili ili furaha yetu iwe kamili. Ndio maana tunakumbushana maagizo yanayotupasa kuyafuata, kama huo ubatizo wa Ondoleo la Dhambi anaotakiwa mkristo aupitie, yaani kuwa initiated, kama ulivyo kuanzia Mdo 2:38 hadi Ufunuo, ubatizo wa maji mengi kwa Jina la Bwana Yesu Kristo ili uwe salama ktk safari yako, angalau ukiwa na uhakika wa kuondolewa dhambi zako achilia mbali kujazwa Roho Mt, maana huwezi kujazwa Roho Mt kabla ya dhambi zako kuondolewa, zikitupwa huko katika kilindi cha usahaulifu!

  Bwana azidi kutuongoza ktk NJIA yake!

 7. Bwana CV Lwembe Nashukuru kwa mchango wako, Nimemchunguza na bado naendelea kumchunguja kwa uweza wa Roho Mtakatifu naamini Ataniongoza, Yesu Kristo ni yule yule jana leo na kesho na ni yeye anaejua manabii zake, only time will Tell! Ila ndugu yangu Hata wewe Mchunguze huyo unaemwamini upate uhakika maana sisi sote Hamna ambae amefika ila kama umejihakikishia basi Hongera.

 8. Beloved Donna,
  Another plane crash prophecy! Yes, this is great news, and the stir it is causing to a perishing people befits the tribulation’s cold chill he is sending forth! 

  What does it do to them? It throws them into confusion, timing them to fall into his lap, at the applauding of the such as you Donna, thereby totally sealing you all outside of the Kingdom of God! Why, simply because “the wonders” and miracles perfomed caught you napping and you got carried away mesmerised by it and now you dont even know if God exists, otherwise you would constantly, I repeat CONSTANTLY checkout with the Word to see if all runs as per IT, the WORD! 

  Now, as the church is looking to THE COMING OF THE LORD, what a great prophecy would that be! Or has God forgotten about it and He is busying Himself with plane crashes, football matches and deaths??

  Wake up Donna, signs and wonders are fine but they must be accompanied by a Divine Message pertaining to the EVENT of the TIME not some evengelical stupor that totally hangs on signs!

  May The Lord bear with our shortfalls!

 9. T.B.Joshua on sunday service 15th july,revealed that another horrible plane crash looms in Nigeria.

  He said the plane crash if not averted would involve the top politicians and bigwigs in Nigeria,that its not for poor people like us.

  He further revealed that it will happen when they will be going for a conference or meeting,that they will be around 9-12 in number,and they will all perish.

  He said that the crash will shake Nigeria if it happens.

  He further said that the devil will strike if they are together on one flight,but it could be averted if instruction is followed,(they should never board one flight).

  Read more: http://omgghana.com/tb-joshua-predicts-another-plane-crash-in-nigeria/#ixzz20wV1bwk8

 10. Mpendwa Leons
  Kwanza napenda kukuhakikishia kuwa mimi sijui Neno kuliko wote na sidhani kama kuna mtu ajuaye Neno kuliko wote, bali sote tunafahamu kwa sehemu tu ndio maana unaona kuna majadiliano ambayo hutuleta pamoja ktk kulitafakari Neno la Mungu na hivyo kujifunza zaidi ile Kweli.

  Swali unaloliuliza, kwamba Manabii wa Kweli ktk karne hii ni akina nani na kuomba utajiwe list ya angalau wachache, kwangu mimi naona unatafuta kupotezwa zaidi kuliko kuwa Huru! Kwa mfano mimi ni mfuasi wa nabii Mwingira, unanitegemea nikuoneshe nabii mwingine? 

  Kigezo cha kumpima nabii yeyote yule, ni Neno la Mungu tu. ikiwa ametoka kwa Mungu atafundisha kama walivyofundisha watangulizi wake mitume. Akifundisha chochote kinyume na mitume jua huyo ni Mt 24:24! Roho Mt ndiye Nabii wa Kweli, hakuna mtumishi anayetoa unabii apendavyo yeye bali kwa kuongozwa na Roho Mt. Na Roho Mt hawezi kufundisha jambo kinyume na Neno, ndio maana mtume Paulo anasema ktk Gal 1:8 kuwa yeyote atakayefundisha kinyume na injili waliyoifundisha wao na ALAANIWE! 

  Basi kwa vile yaonekana una bidii ya kujifunza, chunguza nabii wako anabatizaje, ukiona anabatiza sawa na Paulo, endelea naye; lakini ikiwa ni tofauti, huo ndio wakati wako wa kujipima una amini nini!!

  Kuhusu ujio wa manabii kufungwa, kwamba hakuna tena, hii ni dhana ambayo nimeisikia kwa wapendwa wengi wakiyarejea mafundisho ya makusanyiko yao, lakini hayo ni mafundisho ya uongo kama yale yanayosema mambo ya ishara na miujiza pamoja na maombezi vilikwisha na mitume!! Huo ni uongo wa kidini ambao pia kwa kadiri unavyoendekezwa utawasababishia wengi wanaourudia kuingia kwenye Laana wasiyoilalia maana Injili hiyo si ya mitume!! 

  Maandiko yako wazi, ahadi za ujio wa manabii zimo humo na hakuna wa kuzitangua, na pia makusanyiko yetu yote yanapaswa kuwa na manabii ktk zile huduma 5, kama hayana basi jua kuna tatizo!

  Ubarikiwe

 11. Bwana CK Lembwe na wengine wengi wanaojua Neno La mungu kuliko wote hapa Naombeni msaada wa kuniambia Ni kina nani ambao ni manabii wa ukweli Katika Hii karne, naomba angalau list ya watu wachache ambao ninyi mnaona ni manabii wa ukweli, maana nimejaribu kutafuta sehemu kubwa ya intaneti imejaa habari za unabii wa uongo sasa je wa ukweli ni wapi?? maana unajua sisi wengine bado tunajifunza. na je ni wapi kwenye biblia pameandikwa hapatukuwa na manabii tena baada ya kina mtume Paulo na wengi walio wa ukweli kwenye biblia? Asanteni

 12. Mpendwa John Haule,
  Kwanza nikushukuru kwa maelezo uliyoyatoa ingawa hayana mwelekeo, lakini yanatosha kuelezea upande wa pili wa shilingi! Una uchungu mwingi rohoni mwako ambao ni hatari kwa afya yako ya kiroho. Unawabambikia watu shutuma za “kejeli” zisizokuwepo, kwa vile tu mmetofautiana katika mtazamo, huo ni udhaifu!! Kumtaja kiongozi katika kutafuta confirmation ya jambo linalozungumziwa, sioni kama ni kejeli, labda uwe ni mtu wa kulalamika lalamika! Au wewe unavyomuona mchungaji mstaafu wa kanisa la KKKT wa Samunge kuwa hafai kuwa katika mlolongo wa watumishi wa kutegemewa na hivyo kumuona ni “uchafu” unafanya hivyo kwa mamlaka gani na kwa kigezo gani? Tazama ulichosema: “…ukiangalia hizo URL na Lugha za kuwashambulia watumishi wa Mungu na kuwaweka kundi moja na Mzee ambilikile wa samunge.” Kwa taarifa yako tunawathamini sana viongozi wote wa dini, tunafahamu wanamtumikia Mungu, na tunawapenda kwa hilo. Mimi napenda kujadili HUDUMA na si watu. Watu ni wazuri, na jitihada zao tunaziona!

  Pili pale iliposemwa kuwa Nabii wa Kweli ni Roho Mtakatifu pekee, unasema, “Ni kweli kabisa simkubali huyo nabii Roho mtakatifu… hakika namkataa nabii Roho mtakatifu” Kwa kadiri ya umbali uliofika unaotokana na kuongozwa kwa “uchungu”, sishangai sana unapomkataa Roho Mtakatifu kuwa ndiye Nabii wa Kweli, labda kwa vile kauli ya kumtukuza Roho Mt imetolewa na Sam au Mabinza ama Lwembe, nawe chuki ikukutawala moyoni mwako, ni lazima UMKATAE, faida au hasara yake utaipambanua mwenyewe!

  Katika mlolongo wa malalamiko yako, pia kwa makusudi unachanganya maana ya maelezo yaliyotolewa kuhusu Kunena kwa Lugha ambapo yalikusudia kuonesha tu unenaji kama ulivyotukia katika Biblia kwamba Babeli Lugha iliwatawanya kwa kuwachanganya na siku ya Pentekoste Lugha iliwakusanya wakalipokea kusudi la Mungu! Sasa kama hilo hukulielewa vizuri, ni bora kuuliza, tena na tena mpaka likae sawa na si kupotosha maana.

  Tena sehemu nyingine ya malalamiko yako unazungumzia “kiburi cha kuongeza maandiko kwenye Biblia kuwa kwenye bustani ya kulikuwa na miti 4 na siyo 2 Mw2:9” mimi nadhani wewe ndiye uliye na “KIBURI” cha kuyakataa Maandiko, swali uliloulizwa ni hili, “ Pale Mw 3:3 Maandiko yanapotuambia, ‘ … lakini matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema, Msiyale wala msiyaguse, msije mkafa’; je, Hawa ni muongo au ni Mungu akiendelea kujifunua ktk Maandiko?? Ulipaswa uje na jibu lako kwa kadiri unavyoliona wewe baada ya kuyasoma hayo na mtazamo wa mwalimu wako, au ukae kimya kama huna jibu lake!! Kama umetatizika na jambo ni vizuri kuchukua wasaa kidogo ukiliacha kando mpaka Bwana atakapopenda kukufunulia kile alichokiandika na si kukurupuka na shutma na kuyakejeli Maandiko ktk kile yanachokisema!

  Nimeyaona maelezo yako mengi uliyoyajenga ili kunipinga mimi katika hayo usiyokubaliana nayo. Jambo linalonishangaza zaidi ni pale unaponiambia, “Mpendwa Lwembe nisipopinga hii injili yenu BWANA atainua mtumishi kupinga…” Hivi mimi ndiye niliyeandika hiyo Mw 3:3? Au mimi ndiye niliyeandika Mdo 2:38? Au mimi ndiye niliyeandika Mw 1:26? Unajilazimishaje upofu kwa jambo lililowazi kiasi hicho? Kwa faida gani? Umaarufu??? Sasa sijui unampinga nani, mimi au Maandiko?? Angalia injili yako unayoifundisha: “Math 28:19“Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;” KUBATIZWA KWA JINA LAKE YESU
Tunatubu na kubatizwa kwa Jina la Yesu,ni wakati tunanapobadilisha nia zetu(mtazamo)Roho Mtakatifu anakupiga mhuri ya moto(Arabuni ya Roho) Yeye ndiye Mbatizaji,hiyo ndio alama shetani akiiona anajua wewe sio wake maana hata ukifa wakati umeshabadilisha mtazamo wako na hujabatizwa kwa maji unakwenda mbinguni,…” umeendelea kwa maelezo mengi kujenga hoja ya kuukataa ubatizo halali kwa mafunuo yasiyo na mbele wala nyuma! Kama si mafundisho ya UONGO haya ni kitu gani? Kama si kuwapoteza watu ni nini? Yeyote mwenye kuyasikiliza Maandiko kwa utulivu atagundua kuwa Roho aliyekupa mafunuo haya unayoyafundisha SI Yule Roho aliyewaongoza mitume!!!

  Mwisho unadhihirisha “KIBURI” chako hapa unapobadilika kutoka kumkataa Roho Mt. kuwa ndiye Nabii wa Kweli, na sasa unatuambia, “Roho Mtakatifu ambaye ndio Nabii aliyefunua ufunuo wa UTATU, nami ninaweka maandiko yanayosimamia huo unabii.” Ikifika kwenye suala la UTATU, Roho Mt ni nabii wa Kweli, lakini akikuambia “Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nayi mtapokea kipawa cha Roho Mt.” unaniambia eti hii ni injili yangu ambayo ni lazima uipinge!!! Nakosa hata neno la kukuambia, labda nije na ‘misale ya waumini’!

  Mwisho nikushukuru kwa kukiri kwako kuwa UTATU ni mafunuo mliyoletewa ambayo umesema ni Unabii, ambao unafanana na ile kauli ya imani ya SCOAN, basi kama nilivyokuambia kutokumuelewa vizuri kwako TB Joshua, kusikucheleweshe kushiriki ‘Ibada ya Damu ya Yesu’ ukakosa kufunikwa na “Damu yake”!

  Pia, niseme kuwa tofauti zetu zitaendelea kuwepo kulingana na jinsi tunavyolichukulia Neno la Mungu. Kwa mfano tukija katika suala la UTATU, umeniwekea vifungu vingi vinavyothibitisha Unabii huo uliotuletea unaoambatana na mafundisho yote unayotuletea; labda katika kukudhihirishia utofauti wetu nami ninakuletea vifungu vinavyo jidhihirisha kuwa Yehova wa Agano la Kale ndiye Bwana Yesu Kristo wa Agano Jipya!

  Zab 89:6-9 “ Maana ni nani ktk mbingu awezaye kulinganishwa na BWANA? Ni nani afananaye na BWANA miongoni mwa malaika? Mungu huogopwa sana barazani pa watakatifu, ni wakuhofiwa kuliko wote wanaomzunguka. BWANA, Mungu wa majeshi, Ni nani aliye hodari kama wewe, Ee YAHWEL? Na uaminifu wako unakuzunguka. Wewe ndiwe ukitawalaye kiburi cha bahari. Mawimbi yake yainukapo wayatuliza Wewe.” Huyo ni Yehova wa Agano la Kale, yule Baba.

  Sasa muangalie Yesu Kristo wa Ag/Jipya: Mt 8:23 “Akapanda chomboni, wanafunzi wake wakamfuata. Kukawa msukosuko mkuu baharini, hata chombo kikafunikizwa na mawimbi; naye alikuwa amelala usingizi. Wanafunzi wake wakamwendea, wakamwamsha, wakisema, Bwana, tuokoe, tunaangamia. Akawaambia, mbona mmekuwa waoga, enyi wa imani haba? Mara akaondoka, akazikemea pepo na bahari; kukawa shwari kuu. Wale watu wakamaka wakisema, Huyu ni mtu wa namna gani hata pepo za bahari za mtii?” hao waliomaka chomboni wanamfahamu anayeweza kutuliza bahari na mawimbi yake kama walivyofunzwa katika Zaburi, sasa yanawatimilia!

  Isaya 44:6 “ BWANA, Mfalme wa Israeli, Mkombozi wako, BWANA wa majeshi asema hivi; Mimi ni wa Kwanza, na mimi ni wa mwisho; zaidi yangu mimi hapana Mungu.”
  Ag/Jipya: Ufu 1:17 “nami nilpomwona, nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kuume juu yangu, akisema, Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho, na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti na kuzimu.

  Sasa hebu tazama UTATU, iwapo huo ni kweli, angalia Maandiko yanavyoji contradict:
  Kut 34:5-6 “ … BWANA akapita mbele yake, akatangaza, BWANA, BWANA, Mungu mwingi wa huruma…” hebu nifundishe ndg Haule, huyo BWANA aliyepita mbele yake na kutangaza “BWANA, BWANA”, ni nafsi zipi hizo, specifically, zinazoongea?
  Tena, katika Zek 3:1-2 “ Kisha akanionesha Joshua, kuhani mkuu amesimama mbele ya malaika wa BWANA, na Shetani amesimama mkono wa kuume ili kushindana naye. BWANA akamwambia Shetani, BWANA na akukemee, Ewe Shetani;…” na hizo nafsi za hapa zinajiwakilishaje, ni nafsi ipi hiyo BWANA inayosema BWANA na akukemee na huyo BWANA mwenye kukemea ni nafsi ipi? Je, anapokuambia, “Na tuumbe mtu kwa mfano wetu, …” Mungu akitupa karne nyingine si utaishia kuwa na UTANO kama si USITA, kama ambavyo unaukubali UTATU halafu unawakana Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu, hivi unaijua sawa sawa tafsiri ya UTATU, au umekutana nao barabarani tu?!

  Ila kumbuka, Roho Mtakatifu anajifunua katika Maandiko yake tu na si katika elimu zetu! Jitahidi kuyapokea Maandiko kama yalivyo utajazwa ROHO MT wa Kweli, Yule Nabii!!

  Ubarikiwe ndg yangu!

 13. Wapendwa,

  Nilisema sitachangia na nabaki katika msimamo wangu……nimepitia hoja mpya yenye nukuu hiii…

  “….inakuwaje naye anatabiri mchezo wa soka wa timu za ulaya kama Pweza? Msipende kuamini kila Roho zilitalo jina la YESU KRISTO,lazima tuzipime kwenye mizani (Biblia). …..

  Nikajiuliza kama Pweza aliweza kutabiri matokeo ya mpira yakawa Kweli…….sasa ilimhitaji tena Roho Mtakatifu…..Roho wa Mungu aliye hai….aliyemuumba Pweza ….. kutufunulia haya….?

 14. Hi! Friends in Christ
  Nimesoma karibia michango yenu yote na nimebarikiwa na mmenipa ufahamu wa mambo mengi na pai yapendeza kuona namna Bwana alivyomjaaliwa kila mmoja wetu capacities mbalimbali. Ni kweli sio rahisi sana kukubaliana kwa kila kitu lakini niwaamie kitu… ni rahisi sana kukubaliana ktk mambo ya msingi ya Ki-Mungu, Ki-kanisa na Ki-Neno la Mungu. Kwakua best friend wangu toka miaka ile ya Milambo sec. nilipookoka na akanilea mtumishi wa Mungu haswaaa Mr. Juma Obedi Milinga amesisitiza sana kuongea kwa hoja na si porojo,kitu ambacho hata mie nakiunga mkono na nakipenda, basi nitajielekeza kutirika points kwa kujikita kihoja zaidi na si maneno matupu.Narespond hoja zenu na hasa hoja za John Paul aliyenijibu pia maswali yangu moja kwa moja, yapo nitakuabaliana naye na mengine sitakuabaliana na kusisitiza nilichosema kua ni still very true Godly, Biblically and customarily kama watu wa mbinguni. Hatimaye, nitahitimisha kwa kutoa maoni ya jumla ktk mambo ya rohoni kwa sasa na kule tulikotoka. Nachukua swali langu lililopita na jibu lake then naweka na responses yangu kama ifuatavyo:
  1. Swali: “Tell me guys tofauti iyo ni ipi kwa kutumia viwango vya Ki Mungu na ki Biblia inapokuaja maswala ya utumishi na kumtumikia Mungu na Mungu anavyopima na atakavyo pima watu wake kuwalipa sawasawa na kazi zao?”

  Jibu: Kwa kuwa Mungu atalipa watu sawa sawa na kazi zao, mi naona hivi, yule afanyaye kazi kubwa atalipwa sawa sawa na ukubwa wake. Muinjilisti ambaye anahubiri kwenye mikutano ya Injili, mfano Moses Kulola, and allies, na watu wakaokoka maelefu kwa maelfu, mi naona kama watalipwa zaidi kuliko muinjilisti ambaye kwa mwaka mzima atakuwa amesababisha mtu mmoja tu kuokoka!. Kwa kuwa Mungu ni wa haki, naamini kabisa watumishi ambao walitoa maisha yao yote, wakitembea kwa miguu kwenye milima na mabonde, mito na misitu, wakipeleka Injili, hao watalipwa zaidi kutokana na tabu waliyopata.Sasa, mchungaji ambaye kanisani kwake ana washirika kumi naamini atalipwa sawa na kazi anayoifanya, na T.B Joshua naye, kwa wingi wa watu anaowahudumia, naye atalipwa sawa na kazi yake. Hii ndiyo tofauti yao. Na hii ni ikiwa tu wawili hawa wote wanamtumikia Mungu, Maana uchache wa washirika kanisani nacho SIYO KIGEZO KUWA MCHUNGAJI HUYO NDIYE WA KWELI!

  Response: Umejibu sawa kabisa kuhusu kumlipa kila mtu sawa sawa na ujira/kazi yake isipokua sentensi yako hii…kwa wingi wa watu TBJ anaowahudumia…umeshau kua wengi wa wahubiri wa leo wakubwa wakubwa ktk miji na majiji wanatumia media sana kuvua walivuliwa tayari tofauti na basic Biblical formulae—-Bwana alivyowaambia peter na wenzake …I will make thee fishers of men…(Matayo 4:19 na (Mt 28:19-20)..Basi enendeni mkawafanye watu… Kama sisi wachangiaji tu wakweli, mtakuabaliana na mimi kua gospel outreaches to win fresh souls kama agizo kuu sio major characteristic ya so called makanisa ya mitume na manabii wa leo. Hii Ki Mungu, ni very serious foul ambayo mtumishi John Paul anapomalizia majibu yake kwa maswali yangu na kusema hivi “………sababu ambazo ukizichunguza hazileti MAANA YOYOTE, Kikristo wala Kimwili”, anatia mashaka status yake ya kuona/uelewa( spiritual perception/discernment) ya mambo ya kipentecost kua tumetoka wapi na tunakwenda wapi kama watu wa Mungu na nini hasa kimetokea kizazi chetu cha leo kuhusiana na kutimiza duniani hasa kilichomfanya Yesu aache mbingu na uungu wake na kuja duniani.Umeshawahi kujiuliza kati ya wanohudhuria hapo kwa TBJ na huduma na makanisa ya ivyo,wapi ni wengi kati ya waliohamia huko wakiwa ameokoka tayari na waliookoka toka dhambini ktk ibada yake? Niambie kama Mungu analipa kwa uaminifu, TBJ analipwaje kuhusu watu wengi uliosema anawahudumia waliookoka tayari na hakuwavua yeye but ni maombi, jasho, kilio, pesa, mikakati ya watumishi wengine wasio na TV na pesa ya kuonekana na kutangazia na kuvutia watu kwao ktk media?
  Kama mtu aliyeookoka na hata baada ya uchunguzi wake anashindwa kuona hili tatizo( kuvua waliovuliwa na kum-credit kua anahudumia wengi ambao kimsingi walishahudumiwa huko walikotoka na kukimbilia kwa manabii na mitume hawa kwa sababu…(2Tim4:3-4) na kwamba hakuna regular and pure gospel campaigns kama one of the core church characteristics), kushindwa kuona hiki ni kitu kibaya, it is tatizo by itself! Kwa kushindwa kuona something is wrong somewhere kwa wakristo wa aina ya John Paul wanaojua Neno na tulikotoka wapi,Unaweza elewa kwa kiasi gani kanisa lilivyozidiwa, si ajabu sasa kua wakristo wa leo based only on miujiza, ishara na baraka-baraka badala ya wokovu na utumishi kwanza kasha hayo yaje baadae.Kama Mungu analipa kwa haki, ni vema basi kwa John Paul na wenzake kuchunguza na kujua kabla ya kumchukulia mtu kua ana huduma kubwa na anahudumia wengi na anaonekana ni nabii kweli kweli, tukajizuia kidogo kwakua ninawasiwasi kama kuna ujira mbele za MUNGU mwaminifu wa kiasi hicho tumjuavyo kwa wahubiri- wachungaji, mitume na manbii wa kileo wavuao waliovuliwa kwa mikakati ya nguvu ya pesa na media zao badala ya kicho, hofu,mzigo wa ki-Mungu na nguvu ktk Roho Mtakatifu kupata fresh souls from hell.

  2. “Swali: Hivi kutoa unabii kuhusu mtu au wtu, taifa, jamii na ulimwengu na kusafisha maliwato ya kanisani kwako, kuosha magari ya mchungaji kanisani, kumsaidia mdada mmoja gauni mbili tu yule anayekuja na nguo moja tu nusu mwezi kanisani, kumshuudia mtu mmjoa teja akaookoka, kuna tafauti mbele za Mungu? nani zaidi? nani kapiga kazi kuuuuuuubwaaaaa ya utumishi mbele za Bwana?”

  Jibu: Neno la Mungu linatuagiza kutenda mambo pasipo MASHINDANO. Yule anayefagia kanisani ASIJIDHARAU kuwa anafanya kazi ndogo wala yule Anayehubiri pale Jangwani, mbele ya watu elfu 10, naye hatakiwi KUJISIFU kwamba nafanya zaidi. Jambo la Muhimu hapa hapa ni KILA MTU AFANYE KWA UAMINIFU katika nafasi yake aliyopo na huduma anayojisikia ndani yake. Hivyo ukubwa wa Kazi kwa Mungu ni ULE UAMINIFU WAKO katika kazi unayoifanya. Gari la uwezo wa kubeba mzigo tani 5, likitumika kubeba tani 4.5 litakuwa limetumika VIZURI ZAIDI kuliko gari lenye uwezo wa kubeba tani 60 likitumika kubeba tani 20. Kwa hiyo unaweza kushangaa kuwa Mtu anayefagia kanisani, mbele za Mungu anaweza kuwa kafanya kazi kubwa zaidi kuliko anayehubiri mikutano ya injili ya watu elfu 10 kwa kuwa kilichoko ndani kilitakiwa kiwafikie watu laki 1
  Kwa hiyo yule aliye na KARAMA anatakiwa atende kwa kuliingana na kiwango cha Karama kilichowekwa ndani yake, na yule aliyeko upande wa HUDUMA ZA MASAIDIZANO naye anatakiwa afanya kwa nguvu zake na kwa uaminifu.

  Response: Kama ukweli ndio huo na umejibu vizuri sana kua what matters ni uaminifu na naongezea mambo kama bidii, ukweli, moyo, willingness kutumika nk, then why all these campaigns na kuadmire watu wa mbali wakati watu wa kwetu na kanisani kwako na kwangu na hapa hapa Tanzania tupo, wapo? Why mioyo, furaha na nguvu nyingi zenu ziwe kwa miisho ya nchi kabla ya Judea, Samari na Yesrusalaem? Hamuoni kua ni mambo tu ya kibinadamu yasiyo na tija nani madhara ya utandawazi hata ktk mambo ya rohoni kwa kua globalization negative effects haziko ktk social-economical sphere tu even spiritual too?

  3. Swali: “What real made TB Joshua TB Joshua the “true prophet of God” to you? Is it TV and other media advertisements or……what if there was not media to bring him to your room, country, who would be your prophet?”

  Jibu: Mimi nikiangalia namna wanavyohudumiwa watu, baada ya kufanyiwa maombezi, huwa inanipa kuamini kuwa pale panafanyika kazi sahihi ya Injili. Watu huwa wanashahuriwa kuwa kwa kuwa sasa ameshapokea muujiza toka kwa Mungu, kilicho cha muhimu zaidi sasa ni kUKABIDI MAISHA YAKE MIKONONI MWA MUNGU, KWA KUMFANYA YESU AWE BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YAKE. Maneno haya ni adimu kwa watumishi wetu wa hapa nyumbani, ambao habari za huduma zao huonekana kwenye TV na kusikia kwenye maredio. Sitasahau siku niliposikika mtumishi mmoja, anayefahamika sana nchini, akitangaza kwamba BAADA YA MAOMBEZI KILA MTU ARUDI TU ALIKOTOKA. HATA WA MSIKITINI ARUDI TU MSIKITINI KWA KUWA MUNGU NI WA WATU WOTE! Japo siwezi kuamua moja kwa moja kuwa yule ni Nabii wa Uongo lakini bado naendelea kuyatfakari maneno hayo kama Nayo yana lengo la KUMFANYA ANAYEYASIKIA AMGEUKIE YESU.
  Mara nyingi sana T.B Joshua amekuwa akisema kuwa SIYO LAZIMA mtu ahangaike kwenye SCOAN, Bali anaweza kutafuta MAHALI POPOTE AMBAPO NENO LA MUNGU LINAFUNDISHWA KATIKA USAHIHI. Hayo nayo ni maneno adimu nchini kwetu Tanzania!Nimekuwa Mkristo kabla ya kumfahamu T.B Joshua, na hata pasipo T.B Joshua nitaendelea kuwa Mkristo. Mwokozi ni Yesu na si T.B Joshua. Yako mengi ambayo Mungu ananitendea kwa kupitia MIMI MWENYEWE. Hivyo sitegemei NABII ye yote kuendesha maisha yangu BALI NAMTEGEMEA Yesu. N wala T.B Joshua SIYO NABII WANGU bali namuona kama Mtumishi tu wa Mungu sawa na watumishi wengine. Napenda kujifunza kwake kwa habari ya utoaji na mafundisho anayoyatoa kwa kuanzia yeye mwenye kuwa MFANO. Akifundisha watu wawe watoaji, yeye mwenyewe ANAONYESHA JINSI ANAVYOTOA. Hii ni tofauti sana na watumishi wengi, hasa wa Tz, ambao wakifundisha kutoa BASI HUWATAKA WATU WATOE WAMPE YEYE/HUDUMA YAKE!

  Response: Excellent kwa jibu hili, jinsi ulivyomreccomend mpendwa TBJ kama mtu tu na mtumishi kama wewe na mchungaji wako na si semi-God au super-human kama viashiria vya michango ya baadhi yenu vinavyoindicate hata kama hamjasema straight! This is maturity na in fact Roho Mt aliona nature ya wanadamu kuadmire wanadamu wenzao mpaka kupitiliza, akaweka balansi kiaina ktk Yak:5:17-18 …Eliya alikua mwanadamu… in the same nature with us but aliomba kwa bidii na……. kuhusu kujifunza kwake badhi ya mambo hili nalo ni jibu zuri kwakua Bwana YESU kuna wakati aliweka kabalansi kidogo akiwaambia wanafunzi wake kua wanaweza kuwasikiliza na kujifunza toka kwa mafarisayo strictly kwa kua wanaketi ktk kiti cha Musa… lakini kwa matendo yao…..wajitenge nao(Mt. 23:2-3). Angalizo ni kwamba sio wote wenye uwezo wa kutenganisha pumba kama zile za ibada ya namna ile ya Damu ya YESU, faith statement ya ukakasi kama ile, uuzwaji wa mafuta ya upako…..such a serious spiritual foul of exchanging God’s gift to material things contrary to the Biblical basics…mmepewa bure…toeni bure (Mt. 10:7-8) na karipio kali la Petro kwa mchawi mmoja aliyetaka kutrade karama ya Mungu (Mdo 8:9,18-20) kama wanovyotrade huko ktk so called makanisa ya ki-born again if not burn again ya Western African Countries e.g. TBJ, Kenya,Uganda na Tz kwa baadhi na kimya kimya ….such huge spiritual problem John Paul na Milinga sijui why hawaoni na kuisemea wazi wazi kama kuconduct mambo ya mbinguni kwa namna hii ni Kibiblia au kibinadamu au kipepo kabisa? ktk hili Milinga na John Paul plus wafuasi wenu hamjasema kabisaaa na at least siamini kama kuna mtu kati yenu anaweza sema kwa ujasiri na kwa reference ya right scriptures contextually and in a Pentecost customarily manner kua ni sahihi doing this way God’s business in the born again congregations. John Paul ni sahihi this hanky-panky spiritual gift trading?

  Kuhusu kuwahubiriwa watu na wakiookoka kuwaambia wayatafute makanisa yoyote ya kweli ya Kiroho, mimi na hata kwetu hufanya ivyo sana na hata mikutano ya big November Dar iliyovuma sana, watu walikua wakielezwa sana ila few cases za baadhi kusema watu waende kwao tu au warudi huko huko walipotoka ni peculiar na weakness ya few na sio common practice ya watumishi na makanisa mengi. However, siyo vibaya kama wazazi wazaaji, waliofunga na kuomba na kugharimia mkutano kwa pesa na mikakati mingi, kwa nguvu kabisa kuwakaribisha waliookoka kwenda ktk kanisa lao, hakuna dhambi hapo hata kidogo nani haki ya mzazi aliyeza kupenda kulea, kibiblia inakubalika kwakua kuna siku Paul kwa uchungu wa kuzaa na kulea na kuhakikisha watoto aliowazaa mwenyewe wanabaki wake na salama alisema hivi (Gal.4: 12-19) …vitoto vyangu vidogo navionea utungu….. na kuna wakati alikua very protective nakazi yake na kusema kwa ukali (1kor 4: 14-19)… kua na waalimu kumi elfu but baba ni mmoja niliyewazaa ktk Kristo…Therefore kua na hamu, ukali wa kuwatunza watoto wako na bidii ya kutaka ubaki na watoto wako uliowazaa mwenyewe ni Kiblia kabisaa, no question about that kwa anayejua Neno la Mungu na maana hasa ya uzaaji kiroho ingawa hata kimwili ni ivyo ivyo, kwa kua ni mzazi mwenye pepo I think atakayebeba mimba kisha kuzaa na kufurahia wengine( wazazi strangers) wachukue watoto wake wa thamani na kulelewa huku akijua kwa hakika kila wazazi na malezi yao kwa watoto wao hutofautiana!

  Kuhusu utoaji, ushauri wangu ni tembelea makanisa mengine ya TZ hapa hapa, utashangaa kua watumishi wanaotuhudumia wanajua nini maana ya kungoza ….kwa kuonyesha mifano. Mchungaji wangu mimi ktk michango ya kujenga kanisa, alitoa gari yake mpya aliyopewa kama muujiza ana aliyokua anahihitaji sana, aina ya Haria ya mil. 27, wengine wanatoa mpaka viwanja tena vya Dar na unaelewa nini maana ya viwanja dar sasa, wengine walitoa mishahara yao yote kabisaa, nadhani do the search Mr. Paul watoaji tupo, wapo basi tu Neno linatimia …nabii hana heshima kwao but nabii wa nje…..lo! akina Paul na Milinga haoooooo. Je hamjawahi kuuhudhuria ibada za vijijini hasa wakati wa mavuno, wapendwa wanavyompenda Mungu na waposomba magunia ya mazao, kuku, mbuzi, ng’ombe kuleta kanisani kumbaliki Mungu wao, mtumishi na mipango ya kanisa lao? Au kwakua hanjaonyeshwa kwa TV basi ndio inakua nongwa? Afterall, hata wasipoonyeshwa utoaji wao kwa Tv na kukosa sifa za akina John Paul na Milinga, so what? Inawacost nini? Wakati wanaatwa ma-credits kibao toka kwa Mungu hata wasipojulikana na kuonekana mpaka Yesu arudi, what was is the problem banaaa? Pressure na mahangaiko yenu tu wazee wa kazi.

  4. Swali. “Sasa where was Holy Spirit siku izo atofautiena na wa leo ktk mambo ya msingi?au roho mtakatifu wenu wa leo ameaamka sana na yuko makini saaaana na creative sana kuliko Roho Mt wa wazee hawa ambao wengi wetu ni matunda ya kazi yao ktk nchi hii?”

  Jibu: Mi ninachoona ni kuwa Siyo kwamba Roho mtakatifu amebadilika wala kuamka. Siku za akina mzee Haris Kapiga, Andrea Shimba, Mosea Kulola na wenzake, teknolojia haikuwepo, Hatukuwa na magazeti yenye kusambaa nchi nzima kwa wakati. Hapakuwa na redio sehemu kubwa ya nchi. Hatukuwa na TV kabisa katika Tanzania. Hali hiyo ilisabaisha wanayoyafanya yafayike kama kimya kimya. Ila naamini Kama KUNGEKUWA NA TV, na kazi ya huduma ya wazee hao ikawa inarushwa angani, naamini kabisa wazee hao wangekuwa maarufu sana sana Tanzania, Africa na hata duniani kwa ujumla.
  Mfano mmoja: Palikuwa na mkutano wa Injili pale Nzega, eneo maarufu la PARKING, miaka ya 90, ambapo waliokuwa wanahudumu hapo ni pamoja na Mzee Andrea Shimba. Wakati mkutano unaendelea, kijana mmoja akawa anazunguka na baiskeli. Hata baada ya kuonywa na watu aache yeye aliendelea. Baada ya kuona hivyo, mzee Andrea Shimba aliinuka na kusema kwa sauti: “Bwana na akukemee!” Yule kijana alianguka, akawa kama aliyezimia. Alibebwa na kupelekwa kwenye chumba cha maombezi hadi baadaye alipozinduka. Tukio hilo lingerushwa kwenye TV, nalo lingetosha kabisa kuleta mchango wa kumfanya mzee huyo kuwa “maarufu”!
  Suala la Injili kwa sasa limevamiwa. Na haihitaji hadi kumuangalia T.B Joshua ndipo mtu aone kuwa hali ya Injili kwa sasa ni mbaya. Injili ya sasa ni Ya “mafanikio”. Hivyo kama ni suala la kuhoji HALI YA ROHO MTAKATIFU wa sasa na Wa zamani, Maswli yako mengi sana, hapa hapa nchini Tanzania. Siyo T.B Joshua TU ndiye anayetofautiana na akina Moses Kulola, [Japo ninahitaji kufahamu MAMBO YAMSINGI AMBAYO T.B Joshua anatofautiana na wazee uliowataja], ila ni wengi sana, wanaohubiri Injili ya Mafanikio, ambao ni naamini hao NDIO wanatofautiana na akina Kulola kwa mambo mengi ya msiingi, maana hata hawataki tena kuwaambia watu waache dhambi!

  Response: Tena umejibu vema kuhusu impact ya media kua kama zingekuwepo, wazee hao pia wangefahamika au kua maarufu lakini hasa hilo ndio tatizo langu na baadhi yenu, why umarufu ktk au via media uwe kigezo cha kudhani fulani na mambo yake yatetemekewe na kuchukuliwa kwa uzito wakati hata bila media, tulionao wanatutosha na yanayotendeka yanatutosha kumtukuza Mungu na kusikia toka kwa Mungu? Kwanini basi natusiyache basi yaletwayo na media kama kwetu yapo pia, unless kwenu akina Jonh Paul hayatendeki, hayasiskiki na Bwana asemagi kupitia manabii mambo ya kikanisa, kitaifa na kimabara na kimaisha binafsi ya kiroho hapo kweli papatikieni ya hao waletwao na media. Kama nyumbani kwako Bwana kajaa tele kuna haja gani na chakula cha jirani? Kujifunza SOME issues kwa jirani fine but moyo, hamu, jitihada,ushabiki, admiration kuhamia fully kwa jirani ni kasoro ya mleaji aliyemlea mtoto huyo au ni stubbornness and cronicness ya mtoto mwenyewe japokua atakua amelelewa vema kutunza maadili mojawapo ikiwa ni kupenda na kuthamini vya nyumbani kwanza.

  5. Swali: “From Biblical point of view, all prophesies given in the Bible were at the end of the day aimed to restore back people to God (in the old testament) or bring people to Jesus (in the new testament) or rarely prepared the saints of the prosecution coming for the sake of the work of God (Paul, Peter), nothing more, nothing less, therefore….
  • Can sb tell me what has been the purposes of TB prophesies in reference to the above Biblical context?
  • Will you also categorically establish the differences btn prophesy given out of holy motives vs. human proudness, famousness, uniqueness building, human creativity (crowd pulling), satani/darkness powers etc?
  • Has there been any advantage of his prophesies to the church, children of God, and unsaved?”

  Jibu: From Biblical point of view, ziko Nabii za Hukumu/Adhabu. Wako watu waliotabiriwa KUFA na kweli walikufa, kwa magonjwa, katika Vita na hata kuliwa na Wanyama. Ni aina ya UNABII ambalo lengo lake siyo “kurejesha” bali “kupatiliza”. Yusuph alionyeshwa habari ya NJAA na ile njaa ikaja kweli. Kuna vita vilitabiriwa na kweli vikatokea. Hata Bwana Yesu naye alitabiri habari ya Mti, na mti ule ukanyauka. [Siami kama kunyauka kwa mti ule kulikuwa na lengo la kuwaelekeza watu katika Ufalme wa Mungu]

  Response: nirudie tena kusisitiza kua kila unabii uliotokea lengo ni restorations, salvation and preparation. Kupatiliza simply refers to kuadhibu na kutransfer adhabu from the present generation to the next ….why this, the aim was the same….restoration! wakati watu walivyoambiwa Mungu ni mkali, mwenye ghadhabu na anaweza adhibu mpaka kizazi kijacho…that fear ya kutandikwa na Mungu na mpaka kizazi kifutacho kukumbwa na consequences…made people respect God, come back to him, keep his commandments na ndio kurejeshwa uko. Utabiri wa mnyama kutokea na kuangamiza watoto wale, bado ni restoration ile ile kwa kua hofu iliingia na kuadibisha watu kutotania watumishi na mambo ya Mungu… (1Tim: 1:20). Nachosema Mr. John, umetofautisha wrongly, all unabii aimed ONLY at restoration, salvation and preparation…nothing more nothing less! As a matter of fact, even the other two elements, salvation and preparation can also be summarized in only one major aspect of any unabii wa Mungu and that is Restoration. Nabii zote aidha zilitoka kuonya, kurekebisha, kuleta utiisho, kuua, kuhuisha, kuadhibu, kutoa mwelekeo ujao, kuonyesha yaliyofichika, kuumba imani zaidi kwa Mungu, kutia moyo nk, at the end of day…nikurejesha wanadamu kwa Mungu, basi, hamna kingine.
  Kwa hiyo pamoja na sababu za unabii ulizozitaja, lakini kuna Nabii ambazo lengo lake ni KUJENGA IMANI mioyoni mwa watu, kama ule mti ulionyauka. Kuna mambo yakitabiriwa, kisha yakatokea, huwafanya watu Waamini kuwa kumbe kweli Mungu yupo. [Japo Yesu alisema Heri aaminiye pasipo kuona].

  Response Kujenga imani na kuwafanya au waamini kujua Mungu yupo, wamjue sana na kwa karibu Mungu….bado ni restoration ile ile, hamna jipya hapo mtakatifu John!
  i). Kwa upande wa Nabii za T.B Joshua, Ziko ambazo amekuwa akitoa kuhusu hali iliyoko mbele ya mtu fulani na kumwambia kuwa ushindi wa mtu huyo ni katika Kukaa na Mungu. Wengi huwa anawaonywa juu ya mambo mabaya yaliyoko mbele kama mtu huyo hatabadilika. Ziko nabii amekuwa akizitoa kwa mambo mabaya yajayo na kuwaomba watu wawe katika maombi ili Mungu aepushe jambao hilo {Ndg Milinga alitoa mifano}, na ziko ambazo zimekua ni kuwafanya watu wajenge imani ndani yao, na kubadili mwelekeo walio nao juu ya Mungu.
  Ukitazana Emmanuel TV unaweza kuona Waislam wakishuhudia na Kukiri kuwa Hakika T.B Joshua anatumiwa na Mungu na kumuomba andelee hivyo na pia awaombee na wao hili waweze kumfahamu Mungu huyo anayemtumia.

  Response:Ni jambo jema kwa wiislamu kukiri na kusema hivyo but umeshindwa kuona kwa mapana kua kwa mtu ambae ni empty….hana Mungu wa kweli, doctrine, hana uzoefu na kutembea na Mungu, hawezi kua na reference yeyote aonapo mambo kama hayo ya TBJ! Mtu kama mimi, wewe na wengine ambao tayari tunahazina ya kumjua Mungu wa kweli, hayo kwangu na kwako ni normal and minor issues, na ndio maana wakristo wengi waliookoka kizazi hiki cha media influence, kwakua hawajui tumetoka wapi na kwakua hawakuwahi kumjua Mungu kabla ya vurugu hizi za leo, ni rahisi kwenda na kila kiibukacho na hawawezi kujua nini maana ya imani potofu, watumishi matapeli wa hapa Dar, Tz na nje. Hawawezi kujua ivi hasa mtumishi wa kweli ni yupi na wa kufanya wanadamu kama family na personal project ni yupi? Ni kazi kweli kumng’oa aliookoka wa kileo ktk imani za misukule, kuoga maji kama damu ya Yesu, kutumia socks, vitambaa, miwani, tai, mashuka, chupi zilizoombewa na kuzitumia kila leo kama hirizi, kuvunja laana, kutapishwa mikosi, kuuziwa mafuta ya mti wa mizeituni toka bustani ya gestemane, maji ya Jordan, chumvi ya galilaya, na mbwembwe nyingi, usiniambie mtumishi Paul na ufahamu wa Mungu wote niliouona kwako, umo na wewe ktk utoto kama si uhuni na utapeli huu wa mitume na manabii wa leo hawa?Tena wanokaa town, cities kwa wingi but village, kata na tarafani..weee…thubutu..kwani wao wajinga, they know where misimbazi are easily flowing! siyo kwetu uko ushirombo au mpanda wilayani nilipofanyga kazi ambapo sadaka nilikuta katikati ya wiki alfu 5, jumapili labda alfu kumi na x.mass at least alfu 20 na hapo mchungaji anena kwa ndimi na machozi akimshukuru Mungu kwa kua amemuona! kwa misimbazi 2 tena end of the year..x-mass! TB J anaweza kukomaa na kazi ya Bwana huko mpanda na watoa sadaka dizaini hiyo ambao wanatoa sana vitu kuliko pesa live na bado akaendelea kutoa unabii wa vifo vya Bingu wa Mutharika, Saitoti, plane crush Nigeria na may be Bill Clinton, Bush, Barak Obama? manake kuwatabiria kudead wazungu wakubwa hao hafanyagi but yeye anawadedisha wabongo wenzetu tu, da! Milinga unabii huu mkali eeee, kuwalenga wabongo tu but Putin wa Urusi, Sakozy wa Ufaransa wapete kama kawa? mbona Bwana Yesu anawatoto dizaini za ajabu jamani? La!

  ii). Namna ya kutofautisha “btn prophesy given out of holy motives vs. human proudness, famousness, uniqueness building, human creativity (crowd pulling), satani/darkness powers etc?” ni kuwa hizi za PILI huwa hazina jambo lolote la Kufanya mtu amrudishie Mungu utukufu. Baada ya unabii wa namna hiyo watu hubaki wanasifia tu mtu yule na wala hakuna mwongozo wowote kuwataka watu WATOE MAISHA YAO KWA YESU! Lakini kwa SCOAN watu huelekezwa kuwa njia salama ya kulinda miujiza na unabii wanaoupokea ni KUKAA NDANI YA YESU!

  Response: Kusema ni jambo moja na kufanya kwa dhati ni jambo jingine, japo huelekezwa, but the practice on the ground ni tofauti kabisa, embu angalia ktk mitandao waumini wake wa Dar na TZ mnavyo comment na kumrank! Kwahiyo general practice haiendani na specific practice…iyo ya kuwaelekeza tu! Hii inanikumbusha hapa TZ na hasa Dar mtumishi mmoja alipoaanzisha kazi, waumini wake waliiigiliza mpaka sauti achilia mbali kumtukuza na kumuinua hata kama kanisani kwakwe ali…so called waeelekeza watu….geresha tu…kwa kua kama mchungaji wa kweli na uko makini na kundi lako na unajua tabia ya jumla ya kundi lako ni kukuinua na kukupambapamba, na almost kukutukuza na kusifanyike serious jitahada za makusudi na endelevu za kuwatrain watu to never glorify human, nani hata amini kwamba kuna namna mchungaji, mtume au nabii huyo anaenjoy hiyo unGodly crediting attitude?

  iii) Kutokana na sababu nilizoeleza, ni dhahiri kuwa unabii wake umekuwa na faida kwa kanisa, watoto wa Mungu na hata kwa wasioamini pia!

  Response: Kama unabii wake unatija… je kutabiri ushindi na ushindwa wa timu ktk mpira una aim nini au tija gani ktk mambo ya mbinguni na ya kikanisa na ya kuwin souls to heaven? Jibuni tafadhari Paul au Milinga na wengine humu wa pande hiyo and why he always goes for the huge things (national team), people (presidents) and never see kiroho small things-(viteam vya ligi za nchini kwake), small people (me and u)? Tena plz niwaombeni kitu rafiki zangu, mwambieni anitabirie jamani faster ili BoT iwe yangu au niwe TZ next president, nitawakumbuka tu, nitamteua Milinga awe mshauri wangu wa ndani kuhusu religious organizations and faith and Paul atakua international relation religious organizations envoy to Nigeria ili afanye correspondences tumlete TB Bongo..tehe

  6. Swali: “Kwani what happened huko nyuma kabla ya kumfahamu TB Joshua na nabii zake? Tulipata hasara gani kwa kutofuatilia nabii izi au tumeshaadhirika na nini kama kanisa, mtu mmoja mmoja na Africa kwa kutotekeleza nabii izi? mbona ilikua peace tu siku zote za nyuma until recently after tv na settelite technology kuja third world ,yaani tena waaalaa kulikua hatuna mapressure mnayotupa sasa kwa kutuambia anayotabiri kila mara! Na kama ilikua lazima tupate nabii hizi, why Mungu akusababishaga kwa njia yeyote tuzipate? Au kwa wapendwa waliopovijini sasa hivi wasiofuatilia mambo haya wanampenda Yesu na hawana hata tv au ving’amuzi kunasa wahubiri wa nje, wanakosa nini mnafikiri? Watapata hasara gani ambazo nyie wa town/cities hamtatazipata? Hamuoni ni matatizo yetu tu aliyosema Mfalme Suleimani…aongezaye maarifa houngeza masikitiko…au in my own way…the more much know/informed you are…..the more majaribu, mapito an confusion you will have?”

  Jibu: Swali hili ni refu na lina mambo mengi lakini nitajitahidi kujibu kwadri nitakavyoweza:
  Dunia ni kubwa na ina mambo mengi. Kila mtu alipo kuna mambo ambayo huyasikia na mengine ambayo hayasikii. Wahubiri ni wengi na watumishi wa Mungu ni wengi. Ukikaa kwenye TV ukatafuta chaneli zinazorusha habari za Neno la Mungu unaweza kushangaa kuona mambo mengine ambayo yanashangaza zaidi kuliko yanayoonekana kwa T.B Joshua na hata mafundisho yako mengine zaidi ya yale ambayo hufundisha yeye. Jambo ambalo naona limezidi watumishi wengi, T.B Joshua ni MTOAJI. Sijawahi kuona kiwango hicho cha utoaji wa watumishi.Kwa hiyo ukisema tulikuwa tunakosa nini kwa kutokumfahamu T. B Joshua ni vigumu hasa hadi pale Mtu ATAKAPOJUA AMEPATA NINI KWA KUMFAHAMU T.B JOSHUA. Kama kuna mtu hapati chochote toka kwa T.B Joshua basi huyo yeye HAKUWA ANAKOSA CHOCHOTE kwa kutokumfahamu

  Response: Kuhusu utoaji, ni bahati mbaya kua haujakutana na watoaji katika nchi hii na nimekupa mfano wa kanisani kwetu mchungaji alichokifanya ktk utoaji, lakini muda hautoshi kukuorodheshea wapendwa wa kawaida waliotoa mpaka viwanja tena vya Dar kwa kumpenda Mungu wao, unaishi wapi kama hujawaona watu wa Mugu nchi hii walio watoaji mpaka kushangaa utoaji wa mbaaaaali? Hata ivyo sikutegemea kama ungetoa mfano huu na kuufanya kua big issue kwakua, kwa watu makini na wanojua utoaji ktk Biblia na wanaojua namna Mungu ashangazavyo wanadamu kwa njia zake zilivyojuu kuliko zetu ktk kujaji mambo na kuamua, angesita kusema TBJ anatoa .Unamkumbuka yule mwanamke aliyetoa senti but akina TBJ wa wakati ule wakamwaga mapesa na comments za YESU zilivyokua kwa who actually gave much?..Mark 12:41-44. Huo utoaji hautoao kaka TBJ, a u sure kweli umekidhi viwango vya Mungu au viwango vya John Paul na wengine humu? Unajua kiasi akipatacho? Je Alisha wahi kutoa financial statement yeyote ya mapato yote? Ana wakaguzi? Unajua kiasi anachobaki nacho akisha toa hicho kinachowavutia wengi kusema jamaa mtoaji? Mtu makini hawezi toa jibu hili bali atasema……no comment but kwa bw. John labda unajibu muzee…karibu ukizingatia mark 12:41-44
  Jambo jingine ninalofahamu ni kuwa T.B Joshua SIYO MUNGU. Siyo muumbaji wa hayo anayoyatabiri. Ni mambo ambao HATA KAMA ASINGETABIRI, yangetokea tu! Kwa hiyo kutabiri au kutokutabiri HAKUONDOI UWEZEKANO WA MAMBO HAYO KUTOKEA. Kwa hiyo hofu inayopatikana kwa sababu ya kujua kuwa kuna jambo fulani linakwenda kutokea, wale wenye mtazamo CHANYA WANAIBADILISHA HOFU HIYO NA KUWA KATIKA HALI YA MAOMBI ili ikiwezekana Mungu aondoshe hayo mabaya ambayo yameonekana kuwa yanakwenda kutokea. Ndugu Milinga ametoa mfano ambapo T.B Joshua alionyeshwa kuhusu ajali ya Ndege kisha akawasihi watu wawe katika maombi makubwa, na hata alichukua hatua ya kushauri mamlaka husika waangalie namna ya kuepuka tatizo hili. Lakini badala yake watu walidharau, wakafikiri anashida na pesa. Dharau dharau ikaleta madhara.

  Response: Ingawa nakubaliana na Milinga na kwakua nasoma Neno kua moja wapo ya njia sahihi za kibiblia kupima unabii kujua kua umetoka kwa Bwana ni kungojea kuona alivyosema yatokee exactly, lakini utakubaliana nami kua kwa machanganyiko na utapeli wa kizazi cha leo cha mitume na manabii wa ujanja ujanja, pesa-pesa and umaarufu looking, kamwe na haiwezekani kwa mkristo mwenye kujitunza kulainika tu haraka jambo likitokea kama lilivyotabiriwa hasa siku za leo, ni vema kwenda mile nyingine tena, to be patient, why pressure? Je huwajui au hamjawahi kukutana na hata kuwasikia watumishi nje na ndani ya Bongo na Tz, wamtumikiao Mungu na wameookoka na kila kitu kama wapetekoste haswa na wanatabiri exactly na yanatokea perfectly yet ni matapeli, wazinzi, wauza unga, viungo vya albino, watumiaji ndumba, anasa people, wenye kununua ndege, magari ya fahari, maviwanja na kufungua benki account nje ya nchi, kua na miradi mikubwa wakati ndani ya kanisa au huduma hiyo anayoongoza kuna maskini wakutupwa na watu wenye huitaji maalumu kama wajane, yatima, walemavu? Ivi mtumishi wa ivi atakua na mvuto na mamlaka gani kwa mtu mweye Mungu mzima kama mimi na wewe kumsikliza na hata kutii mambo yake?mhuni na dhulumati wa aina izi? To hell with them, wanaudhi sana na nasika hasira kabisa, watu hawa wameharibi picha yetu mbele ya mataifa, ndio maana tuonaonekana waliokoka wote ni matapeli na watafutaji ulaji na life kwa kutumia huduma na makanisa..am serious nasika hasira na nimekwaza siku nyingi na apendwa na watumishi wa aina hii, wanatuvua nguao mbele ya jamii, hatuaminiki na inakua kazi siku izi kushuudia manake ukikukutana na watu wanaojua issues, wanakuachallenge kwa kukutajia watumishi na makanisa na hudama kibao za hawa mitume na manabii wapumbavu kabisa hawa….Ndiyo maana Yesu alikua sometime anakerwa kwelikweli na kuwarurua watu hekaluni,binua mameza yao,chapa bakora na wengine kuwachana live kwa kuwaambia uso kwa uso … wana wa ibilisi, kizazi cha nyoka, kizazi kiovu cha uzinzi na maneno mengine makali kuzidi ya kwangu. Kuliko kuwaamini faster hawa manabii na mitume wa kileo, I can buy my time hata miaka kumi na tano, kwani kuna uharaka gani? Hata ivyo wananiongezea au kunipunguzia nini anyway ktk maisha yangu ya kwenda mbinguni? Will they stop me or in anyway contribute for me to enter mbinguni hata nisiposikia chochote na kufanya chochote chao? Are my pastors whom at least and reeasonably I know closer and for years not enough? Nonsense! Nauliza na kujibu hivi kwa usahihi kabisa kwakua nimeshakutana na wanaotoa utabiri, mitume na manabii wa dot com ya leo na kweli yanatokea exactly but nyuma ya pazia wanavyoishi na walivaa nguvu gani walipokua wanatabiri, utakua na taadhari zaidi yangu mara mia tano! wanadamu hawa ni wanadamu tu, siku zote kuwepo na tahadhari, mwanadamu anaweza akawa chochote wakati wowote.

  Ninanukuu; “Na kama ilikua lazima tupate nabii hizi, why Mungu akusababishaga kwa njia yeyote tuzipate?” Mwsho wa kunukuu.Maneno haya nimeyafananisha na yale ambayo watu husema: “Kwa nini Mungu hakutafuta njia mbadala ya kuleta wokovu badala ya hiyo ya kufa msalabani”Lakini, Hivi ndg Seleli unafikiri wale ambao INJILI HAIJAWAFIKIA ni kwamba MUNGU HATAKI IWAFIKIE? Maana tunaweza kusema “kama anahitaji injili iwafikie, kwa nini hatafuti njia mbadala ya kuwafikishia Injili kuliko kusubiri hadi wahubiri wafike huko? Kwamba kwa nini Mungu hakusababisha njia yoyote, hadi asubiri TV na Satellite ndiyo tupate habari za Unabii wa T.B Joshua? Hapana. Nadhani kuna haja ya kupanua ufahamu na kuangalia kwa upana zababu tunazotoa kama mapingamizi kwa huduma hii ya T.B Joshua.

  Response: Picha iliyojengwa nanyi ni kama vile kuna something special to hear and do what this man of God or god is saying or prophesying while the reality is, hayo hayasemayo(kama yanatokana na devo, yeye au Mungu) si mageni na atakayoyasema(kama yatatokana na devo, yeye au Mungu), si mageni kwakua Roho Mt huwatumiaga watu wa kawaida kanisani kwangu hapa Dar na hata huko nilipokuwepo mkoani, kuona mambo mazito na kuyatabiri ya kikanisa la mahali pamoja, Tanzania, Africa na Ulimwengu, si issue kwangu, sijui why mnaona ya TB ni very special sana? Sisi wenzenu tumeona na nanajua Bwana anawatumia wengi hapa hapa TZ from village to cities ambao huonaga mambo mazito na kuyasema yakatokea exactly na hata baada ya kuyapima na kubuy time na pia kwakua at least tunayajua maisha yao maiaka na miaka, tunadhibitisha ni kweli. Ninamfahamu dada mmoja, akiwa shambani mwake Igunga darasa la 7 failure, very interior uko village, hana hili na lile, Bwana akamtokea na kumwambia kuhusu Rais wa Nchi hii ajaye baada ya Mkapa, Mungu akafanya mazingira mpaka wakakutana na JK, huyu dada alitembea na team ya JK muda wote wa kampeni 2005 akiwa anaomba na kufunga for JK victory na protection ya nguvu za Mungu dhidi ya uchawi, mizimwi, majini na matambiko yaliyokua yanamtandika JK alipokua anakwenda kinyume kwa kutaka kumpata Mungu wa kweli wa dada huyo, mtakumbuka alivyobilingita jukwaani Jangwani siku ya ufunguzi wa kampeni na watanzania mkapigwa fix eti alikua kachoka wakati ktk ulimwengu wa roho, sisi wengine we knew nini haswa kilichotokea. Hatimaye dada huyo from village alikuja kuishi Dar, ikatokea kufahamiana nae kwakua alihitaji nimfundishe English course, ndipo tukafahamiana kwa kirefu na kuniamini kunipa shuhuda hiyo, Tunaweza kaa ivi, ghafla simu za from big house there zinaita, inatumwa benzi jeusi kumchua kanisa or home kwake to ikulu, JK anakua amemuita kwa ajili ya kufanyiwa maombi au yeye mwenyewe akionyeshwa jambo na Mungu kuhusu maisha ya JK au jambo ktk nchi, anapiga na kufuatwa. Kwa ushuuda au taarifa yenu tu, manake kuliwahi kua na debate huko nyuma ktkt ya wapendwa kama JK alikua kweli changuo la Mungu kwa kipindi kile cha kwanza kama watumishi waliosemaga ivyo walikosea ua vipi, kupitia dada huyu ambaye tuliendelea kuishi nae kanisani kwa miaka kadhaa, ni kweli MUNGU alimchagua JK but kama mwandamu, hua wanaachiwa na Mungu kutumia will yao kumfuata Mungu kabisa au kutomfuata, Mungu halazimishi mtu, siku zilivyoendelea kama mtu wa kawaida tu hasiye na Mungu au hasiyemshika Mungu halisi kwa moyo wake wote ili Mungu aliyemuita atende aliyokusudia kwake na kwa Taifa lake, alijichanganya mwenyewe, mara mungu bagamoyo mara Mungu mbinguni, mnajua nasema nini hapa, na hakuna rais aliyewahi kuombewa from day one mpaka anaingia ikilu kama JK. Todate hofu ya Mungu anayo kidogo kama Sauli mteule wa Bwana alayeanza vema na Mungu , madaraka yakamlewesha na kujitenga na Mungu polepole na kutotenda haki…imagine from interior God uses such very local mpendwa…so why mnatetemeka saaaana about TBJ tena from Nigeria! Hahahaha! cheers

  Mfano mwingine ni wa askofu mstafu Emmanuel Lazaro, mnaofuatilia issue za kipentecost nchini mnamjua this one of the long time Tz man of God ambaye 1989 akiwa anaomba chumbani kwakwe, KIUMBE cha mwadamu(siyo picha ukutanai…ni kiumbe skeleton ya mtu kilimtokea na kikawa kinatembea chumbani kwakwe, akaona ni kitu kibaya na akakikema..wala hakikumtii..Mwishowe akakaa aone mwisho wa maono yale ni nini….kisha sauti ikasikika…. KAMA TANZANIA HAITAACHA MAOVU YAKE HAKIKA HAITAPONA. KILE ULICHOKIONA KTK CHUMBA CHAKO CHAKUOMBEA NI MAUTI YATANZANIA. TANZANIA HAITAPONA WALA BURUNDI na RWANDA NAYO. Ilipofika 1992, manajua yalitokea Burundi na Rwanda, sisi tupo ktk grace period sijui…in case tukiacha, tutapona.Therefore, we have very powerful manabii from village to town/cities, from normal wapendwa to leaders, so why do I need to concentrate to TBJ? Ningeweza toa shuuda hata mia za wapendwa kanisani kwangu na nje ya kanisa kwangu, manabii wa kweli walio ktk basics za kipentekoste na kibiblia ktk kuishi na kufanya huduma zao na sisi mambo ya allah kama faith statement na damu ya YESU kuoga na kuuza mafuta ya ‘upako’, nonsense kabisa! Unashangaeje mimi kusita kwa habari ya huduma hii ya TBJ Mr. John na my mate milambo sec school best yangu Milinga? Sababu zipi za kikristo za kumkataa zaidi ya hizo?

  Kipengere kingine ni hili kuwa Yule ambaye hasikii wala kuona habari za T.B Joshua atakosa kile ambacho Wanaoona WANAKIPATA. Lakini pia naomba nikuulize ndugu Seleli Hivi Watu ambao SIYO WASHIRIKA WA KANISANI HAPO ULIPO, WANAKOSA NINI KWA KUTOKUPATA MAHUBIRI YA MCHUNGAJI WAKO? Ukiweza kujibu swali hili, BASI hilo ndilo jibu pia kwa wale ambao wanakosa kuzipata habari za T.B Joshua.

  Response: Kwa msingi wa hoja nilizozieleza juu hapo, hukuna cha msingi anachokosa kwa hasiyeona, kufuatilia, kushabikia na kua mfuasi wa TBJ ikiwa kanisani kwakwe, huduma yake, mchungaji, mtume na nabii wake atakua na haya yafuatayo ambayo yako kanisani kwangu na kwa wachungaji wangu na makanisa na huduma nyigine ninazozifahamu kwa hakika na kwa miaka na udhibitisho mwingi na wa muda mrefu kwa maisha.Baadhi tu ya mambo hayo yaliyoyomo kanisani kwangu na kwa wachungaji wangu ambayo John umeniuliza na ambayo hata niisipofuatilia TBJ sina nalopoteza ni haya:
  • Kanisa linaendeshwa kama taasisi na si mali ya mtu au familia ivyo vipo vyomba vya kuadibisha na kuelekeza toka ngazi ya chini mpaka juu
  • Wako wakaguzi na wasimamizi wa mapato na matumizi ya kanisani wa ndani kanisa la mahali pamoja na kanisa kitaifa ivyo nidhamu ya mali na maamuzi ya kutumia kipatikanacho hayaachwi yote kwa mtu mmoja anayeweza kua mwehu anytime au mwizi au mtu wa tabia ya mwilini na kufuja mali na mapato ya kanisa ndio maana makanisa ya aina yetu, huwezi kuta eti mchungaji na mkewe, mtume na mkwe au nabii na mkwe wananua ndege au hammer ya mil 600 wakati vipao mbele viko vingi. Tukinunua Jet au meli au gari hammer kwa mtumishi ni sawa but after serious vipao mbele kiMungu na kikanisa vimefanyika kwanza. Hata ivyo wachungaji wangu walivyoiva ki Mungu, wasivyo selfish, hawawezi kukubali kununuliwa such deadly expensive material things, never! huu ubitozi na unyonyaji wa kuswaga sadaka za watu kwa Mungu wao kwa ajili ya mambo ya Mungu ya msingi badala yake kuzitumia kihuni kununua mandege, magari ya kutisha, ufyatu huu huukuti kwetu labda kwa private project run churches/ministries kama za manabii wenu!
  • Kanisa lina faith statements, all summarized in one phrase -UTAKATIFU NA UMISHENI, hii haina ukakasi kwakua inaendendana na kusudi la sisi kuokoka na kuendelea kuishi hapa duniani
  • Vikao huutishwa kwa muda ukiopangwa na mara kwa ghafla ikitokea huitaji kama vile kuna mtumishi aliyetamka au kwenda kinyume na Neno na pia desturi sahihi za makanisa na imani ya kipentekoste kama mambo ya kihuni kama kuuza mafuta ya upako ua kutoa toa unabii kama vile kunywa chai, kupitia vikao ivyo vinadhibitiwa kwa utaratibu wa maongozi ya Kibiblia, kihekima ya kitumishi kupitia uongozi uliopo madarakani au wazee wa imani waliotangulia ktk imani na utumishi nchini na kimataifa.
  • Kuna nafasi kubwa ya watumishi wengine wa nje ya kanisa na ndani ya kanisa kuhudumu madhabahuni ili kufaidia karama na vipawa tofauti tofati Mungu alivyoweka ndani ya Watu wake kwa kua kamwe hakuna mwenye vyote na kwaahiyo swala la mtu mmoja tu from jan-dec kua kila kitu ktk yote madhabahuni hakitokei kwakua tunatambua Mungu hutumia watu wote na si lazima mtu mmoja tu
  • Maendeleo ya maisha haya ya watu wenye mahitaji maalumu kanisani kama yatima, walemavu, wajane nk yanatiliwa maanani na yanatatuliwa kwanza ndani kabla ya kukusanya ela zao tuu( sadaka) na kusaidia nje, kutaka sifa na umaarufu wakati ndani mwako watu wanashida kali na frustration nzito na kujuta kwanini walikuja dunuani…mfano siku ya kuwatia moyo wachungaji kanisani kwetu ambapo washirika huja na chochote iwe pesa na vitu na kuviweka madhabahuni ili kuwaambia watumishi kwa matendo kua tunawapenda na kuthamini huduma yao kwetu, mchungaji wetu ameamua vyote vinavyopatikanaga siku iyo ingawa ni haki yake kimadhabahu na kibiblia hasa kwa mtumishi wa kweli wa Mungu kama kuhani wa watu mahali pamoja, hugawanywa kwa wajane wote wa kanisa na hata siku kuu za x-mass, wajane wote hupewa zawadi na kanisa, yatima husomeshwa na walemavu hupewa misaada ya kiutu…..Na mengine mengi, muda haotoshi

  “aongezaye maarifa huongeza masikitiko…au in my own way…the more much know/informed you are…..the more majaribu, mapito an confusion you will have?”
  Sasa ndg Seleli, hivi unamaanisha kuwa SASA TUSITAFUTE TENA KUJIFUNZA HABARI ZA MUNGU? Hatuna haja tena ya kuendelea kuhudhuria semina kwa kuwa the more we know/we are informed the mora majaribu, mapito and confusion we will have? Mi naona kama ni hivyo basim tuache hata kwenda kanisani. Maadam mtu ameshaokoka, hana haja tena ya KUENDELEA KUJIFUNZA maana akishajua ZAIDI atakuwa anakaribisha ajaribu zaidi? Kama ni hivyo Basi wale watu wa Beroya, kwa KUYACHUNGUZA MAANDIKO walikuwa wanajitafutia MATATIZO. Tutawezaje kuzijaribu kila roho kama hatuwezi kujifunza zaidi habari ya Neno la Mungu? Tutajuaje roho zidanganyazo kama hatuna MAFUNDISHO ndani ya mioyo yetu? Ndugu Seleli, unataka kusema WANAFUNZI WA DARASA LA KWANZA WASIENDELEE KUJIFUNZA MAANA WAKIJUA ZAIDI WATALETEWA MASWALI/MITIHANI MIGUMU ZAIDI? Kwa hiyo unawashauri waendelee kubakia katika Darasa LA KWANZA maana hapo ndipo kuna mitihani RAHISI?

  Namalizia kwa kusema hivi, KUJIFUNZA ni jambo jema. Ni vizuri tukaendelea kujifunza. Ni vizuri tukaendelea kujifunza habari za watumishi wa Mungu wanavyofanya kazi ya Mungu. Ni vizuri tukaendelea kujifunza Neno la Mungu. Biblia inasema kuwa KIILA JARIBU HULINGANA NA IMANIYA MTU lakini pia HERI ASTAHIMILIYE MAJARIBU…..! Majaribu ni kama mitihani. Majaribu ndiyo yanafanya mtu amfahamu Mungu zaidi na zaidi. Huu Ukristo wa BILA MAJARIBU au Ukristo wa KUTAKA MAJARIBU MALAINI MALAINI au MAJARIBU MACHACHE nao ni Ukristo Mpya! Ukristo DUMAVU.Mtu huwezikutokoa UTUKUFU HADI UTUKUTU au NGUVU HADI NGUVU ikiwa huongezi lolote katika maarifa ya Mungu au hupitishwi kwenye MOTO WA MAJARIBU. Ayubu alipata MAJARIBU MAKUBWA kwa kuwa ALIKUWA MCHA MUNGU MZURI. Lakini alipopita alitoka kama DHAHABU. Majaribu Makubwa Yanaleta THAWABU KUBWA!

  Response: Ufafanuzi: niliposema…much know ur…the majaribu come, I meant not majaribu uliyosema ambayo ofcoz kwa mtu anayejua Neno hawezi kujenga hoja ya kuishi kwa kukwepa majaribu yatokayo kwa Mungu(tests and trials) kwa kua hii ni portion ya wateule. However, Biblia inatuhimiza kujiepusha na mambo yatutiayo unajisi kwa haraka, au dhambi zituzingazo kwa upesi au majaribu yatokayo na yenye nia ya kumfaidisha devo( tempatations), Ni kweli kjifunza na kutafuta maarifa na elimu ni jambo jema sana, imeandikwa Mshike/kupata sana Elimu- maarifa, ufahamu, kujifunza, ujuzi, kupata habari nk- (Mit 4:13)…… nevertheless, Mungu siku zote huweka self control meachnism au kabalansi katika mambo yahusuyo yale yale aliyoagiza ndio maana ktk (2Tim 4:3-4)…amesema tujiepushe na kujitafutia waalimu wengi, masikia ya utafiti, watu wanaopelekwa huku na kule kwa kila upepo uvumao. Mwamini akijikuta ktk hali hii ndio nimeeita confusion au majaribu kwa maana ya yatokanayo na u-much know na kusaka kila elimu na kujifunza kwa yeyeto na mambo yeyote kwa kisingizio cha kupata maarifa. Mambo yote natuyatende kwa hekima na kuangalia kama yanaleta tija ktk maish yetu ya kiroho. Ni sawa na wapendwa waliookoka miaka ya juzi juzi kidogo waliibuka wengi wenye shuhuda za walipokua kuzimu na shetani na wengine wakajitoa ktk kusaka elimu kwa kusoma aina za majini na kazi zake zote na uchawi na aina ya uchawi… huu ni wehu pia upotofu wa vipao mbele tunavyopaswa kukazania kuvitenda kama wana wa Mungu wenye muda mchache duniani hapa, tuzitende kazi zake, tukiokoa muda kuliko kupoteza kwa kusoma na kusaka elimu juu ya majini, nguvu za giza, manabii mbalimbali duniani na kazi au huduma zao

  Lakini la msingi hapa ni kuwa KAMA TUNAMKATAA T.B JOSHUA tumkatae kwa Sababu za Kikristo na kwa wakati Huo huo TUNAPOKUBALI WENGINE nao tuwakubali kwa Sababu za Kikristo pia na wala SI sababu ambazo ukizichunguza hazileti MAANA YOYOTE, Kikristo wala Kimwili.

  Response: Sababu nilizozitaja hapo juu na Neno la Mungu linalothibitisha Mungu nae anasemaje mbali na ufahamu wangu tu, zinatosha kuonyesha sababu za Kikristo za kusita kukubali huduma hii yenye ukakasi mwingi kwa watu wenye uzoefu na ufahamu wa jinsi imani ya kipentekoste ktk Tanzania, Afrika na ulimwengu kwa ujumla zilivyokumbwa na kuvamiwa na mambo mengi yasiyo na tija na yanayotoa picha ngumu sana kwa wanadamu huko nje wenye uwezo wa kungalia mambo na kuchambua nidhamu zetu kama watu wa Mungu wanaotegemewa kua ni wanamna fulani but ukweli tunakua tofauti na kukatisha tamaa. Kama mtu mwenye Roho wa Mungu kama John Paul alivyoshindwa kuona ukweli na akasema akijibu maswali yangu kwa mara ya kwanza kua ukichungaza sana mambo niliyosema yaliyopita kua HAYANA MAANA YOTOTE kikristo na kimwili ni wazi unaweza kuona mtu alieyeookoka na kuanza na misingi mizuri ya huko nyuma lakini akaishia kukamatwa na wimbi la aina ya upentekoste wa kileo wenye porojo za kibinadamu kibao, A man made Christianity vs. Biblical made christianity

  Dawa ya kusaidia aina ya hawa wapendwa walikua ktk basics vizuri sana but wakatekwa na move ya negative side ya power of globalization and televised Pentecost World, ni Mungu mwenyewe maana aina hii ya wapendwa pia ni wagumu kushaurika. Sishangai kwakua kama wakristo wenye basics za kipentecoste kama Milinga na John Paul wanaweza kuwa twisted na moves za kileo, vipi kwa wanaookoka leo na wasio na references za original Pentecost faith way of life tulioshi na kujua vitu halisi na mbembwe ni zipi? Kwaiyo ktk mjadala huu kwa wale waliookoka wakati wa move hizi za watumishi wa kileo, kweli siwashangai kwakua lazima mtajenga hoja as per todays’ all knowledge u have…..the todays dot com petecost faith but kwa wakongwe kama Milinga na I think John Paul nao wakibehave hivi badala ya kuplay role ya kutoa guidance ya kiutu uzima kiroho na KiMungu, then we are finished! Ops! Sorry, I mean..You are finished…you guys not me!

  Conclusion: Dondoo zifuatazo zinaweza kumsaidi mtu yeyote humu atayetaka kusaidiwa kujilinda na kupambanua mambo kabla ya kuachilia moyo, nafsi, roho, akili na mwili wako ktk imani za kileo za kipentecost na aina ya watumishi tulionao: Watumishi wa kileo
  • Wengine hua kweli wameitwa na Mungu original na wanahuduma ya Mungu kweli na wakaanza vema kweli but utoto,ujana, uanadamu, nguvu ya mapato, umaarufu ukatawala sana huduma zao na wakajikuta kwa kujua au kutojua wamesererekea mbali ingawa watabaki kama vile wana basics za kipentecost. Na kusererekea huku pia huchangiwa na kiburi na mafanikio wayapatayo haraka ivyo kutoonyeka na mtu yeyote hata kaka, dada na baba zao waliowatungaulia kiimani na kiihuduma, ningeweza kutaja majina ya watumishi hapa Tanzania kwa majina ambao I KNOW KWA HAKIKA WALIITWA NA WALIOKOKAGA( lakini nachelea haitakua hekima njema sana hasa kwa points hizi za conclusion nazomalizia) but ujana, utoto-utoto wa kihuduma,ulevi na kiburi cha uzima, pesa, mafanikio yamewatwist na they are no longer watu wale nilio/tulio wajua kwa hakika ktk huduma tulizowahi fanya kwa muda. Habari njema ni kua, wa kundi hili hubaki na wokovu na Mungu wa kweli but si ktk conduct ya kipentekoste inayokubalika

  • Wengine ni kama hao wa group ya kwanza but huenda mbali zaidi wakaacha imani safi na kutumia nguvu ya pepo, uchawi na giza, Hapa pia ningeweza taja mtumishi mmoja ambaye anavuma sana Dar but alikutana na mtu mmoja kwa gwiji mmoja wa uganga wa kuvuta watu na nguvu za kuponesha magojwa kwa njia ya majini,huyo mtu aliyekutana na mtumishi huyo, ni rafiki wa mchungaji wetu msaidizi aliyetushuudia hicho kituko pia yuko rafiki yangu anayemjua mganga mwingine ambaye mpendwa huyu huendaga…namuongelea moja ya watumishi vijana Dar wanaovuma sana…..but tafadhari sijataja jina jamani but ni kijana au kijana mtu mzima kidogo…..btn 35-44 years I think.

  • Wengine ni kama wa group ya kwanza…..huanza na maduduuuu, ukakasiiiiii na mbwembweee but kwa neema ya Mungu na kwakubali kukemewa na kukosolewa, hujirudi, ua-djust mambo mengi na kukua ktk huduma na hatimaye kua watu wa uhakika wenye kuishi na kuendesha huduma zao ktk basics za kipentekoste….hapa nataja kwa mfano bila jina la mtumishi mmoja maeneo ya Dar wilaya ya Kinondoni ambaye toka anaanza huduma yake miaka ya tisini na kitu….. alikua na vituko na madudu mengi but siku izi ni mtu mzima sana ktk hudma na amekuja na kukaa ktk level

  USHAURI KWA WANA TBJ: Give it time, may be TBJ ni pure na atajirekebishika later au ni bomu kabisa, wakati mnaendelea kubuy time, concentrate na makanisa yenu na mchungaji wenu, chapeni kazi ya injili hapo kwenu na Bwana atawabariki, leave TBJ alone! Afterall, hawaitaji kiviiiiiile, ni mahangaiko na pressure zenu tu na sijui kua anajua mnaexist this part of the World! Hahahah, mnakazi watumishi nyie, kaaaaazi kwelikweli.

  TUFANYEJE? Very simple! Vitu viwili kwa hakika vinasaidia na kamwe ni ngumu kutekwa
  • Matayo7:15-16: Kuwatambua kwa matunda yao! Angalia neno Matunda- linawakilisha hints zifuatazo:
  i. Muda umepita mpaka tunda litokee maana tunda haliwezi kutokea kwa muda mfupi, therefore msiwapapatikie, ngojeni, buy time, acheni tu, endeleeni kanisani kwenu kwa uaminifu, yawengine yapeni muda au achana nayo kabisa
  ii. Tunda ni kitu dhahiri shahiri- litaonekana tu, hamna ufunuo hapo
  iii. Tunda ni kitu cha kuliwa na wanadamu, au ndege, mengine huliwa na wanyama, wadudu na kwakua kuonja ni moja ya vitambuzi, kama tunda lina ukakasi au bichi au ni tunda jipya au pori hujaelezwa taarifa zake na kujua au kudhibitisha kwa hakika, kwanini kulila? Why don’t u consume matunda kibao kanisani kwako unayoyajua kwa hakika na ni matamu, unless kama hayapo, go and look for them outside though be carefull when looking for matunda outside, utaconsume poisonous fruits au ni yale no poison but ni yale matunda yakiingia kwa stomach, hayawi-digested na inabidi kumtapisha mtu kitu amabacho ni shughuli nyingine!

  • Yohana 10:1-5: Kondoo wake huisikia sauti yake…wanaijua sauti yake…..hawatamfuata mgeni, watamkimbia kwa kua hawazijui sauti za wageni, angalia neno “kusikia sauti”… kondoo wako so smart mpaka wanajua sauti haswa ya mchungaji wao! Wow! this is so sweet, isn’t it?….hint hapa ni kua jamani Mungu wetu kupitia YESU na Roho Mt huongeaga, huzungumza nasi, husemaga, hutunong’oneza, hutuambiaga, therefore, kama moyoni mwako humeshambiwa kua TB Joshua ni ktk group gani mfano kwa yale niliyoeleza fine, but with me, am sorry, network zote ndani zimezima, zimegoma na kwakua Bwana husemaga nami kwa mambo mengi na kwa namna nyingi, I will wait. However, ni sahihi vilevile kusita kumkubali mtu na huduma yake hata kama anafufua wafu na kutabiri mpaka kujua ya miaka mia ijayo ikiwa hata kwa vigezo vingine vya kawaida tu mbali na kutumia hivi viwili deep, unaona ukakasi zaidi than utamu kuhusu BAADHI ya mambo(siyo yote ofcoz) ayafanyayo kaka huyu TBJ na wengine wa dizaini hii West Africa, Tz, Kenya, Uganda,Congo na USA.

  Amani ya Mungu wetu iwe nanyi wote

 15. Hi! Friends in Christ
  Nimesoma karibia michango yenu yote na nimebarikiwa na mmenipa ufahamu wa mambo mengi na pai yapendeza kuona namna Bwana alivyomjaaliwa kila mmoja wetu capacities mbalimbali. Ni kweli sio rahisi sana kukubaliana kwa kila kitu lakini niwaamie kitu… ni rahisi sana kukubaliana ktk mambo ya msingi ya Ki-Mungu, Ki-kanisa na Ki-Neno la Mungu. Kwakua best friend wangu toka miaka ile ya Milambo sec. nilipookoka na akanilea mtumishi wa Mungu haswaaa Mr. Juma Obedi Milinga amesisitiza sana kuongea kwa hoja na si porojo,kitu ambacho hata mie nakiunga mkono na nakipenda, basi nitajielekeza kutirika points kwa kujikita kihoja zaidi na si maneno matupu.Narespond hoja zenu na hasa hoja za John Paul aliyenijibu pia maswali yangu moja kwa moja, yapo nitakuabaliana naye na mengine sitakuabaliana na kusisitiza nilichosema kua ni still very true Godly, Biblically and customarily kama watu wa mbinguni. Hatimaye, nitahitimisha kwa kutoa maoni ya jumla ktk mambo ya rohoni kwa sasa na kule tulikotoka. Nachukua swali langu lililopita na jibu lake then naweka na responses yangu kama ifuatavyo:
  1. Swali: “Tell me guys tofauti iyo ni ipi kwa kutumia viwango vya Ki Mungu na ki Biblia inapokuaja maswala ya utumishi na kumtumikia Mungu na Mungu anavyopima na atakavyo pima watu wake kuwalipa sawasawa na kazi zao?”
  Jibu: Kwa kuwa Mungu atalipa watu sawa sawa na kazi zao, mi naona hivi, yule afanyaye kazi kubwa atalipwa sawa sawa na ukubwa wake. Muinjilisti ambaye anahubiri kwenye mikutano ya Injili, mfano Moses Kulola, and allies, na watu wakaokoka maelefu kwa maelfu, mi naona kama watalipwa zaidi kuliko muinjilisti ambaye kwa mwaka mzima atakuwa amesababisha mtu mmoja tu kuokoka!. Kwa kuwa Mungu ni wa haki, naamini kabisa watumishi ambao walitoa maisha yao yote, wakitembea kwa miguu kwenye milima na mabonde, mito na misitu, wakipeleka Injili, hao watalipwa zaidi kutokana na tabu waliyopata.Sasa, mchungaji ambaye kanisani kwake ana washirika kumi naamini atalipwa sawa na kazi anayoifanya, na T.B Joshua naye, kwa wingi wa watu anaowahudumia, naye atalipwa sawa na kazi yake. Hii ndiyo tofauti yao. Na hii ni ikiwa tu wawili hawa wote wanamtumikia Mungu, Maana uchache wa washirika kanisani nacho SIYO KIGEZO KUWA MCHUNGAJI HUYO NDIYE WA KWELI!
  Response: Umejibu sawa kabisa kuhusu kumlipa kila mtu sawa sawa na ujira/kazi yake isipokua sentensi yako hii…kwa wingi wa watu TBJ anaowahudumia…umeshau kua wengi wa wahubiri wa leo wakubwa wakubwa ktk miji na majiji wanatumia media sana kuvua walivuliwa tayari tofauti na basic Biblical formulae—-Bwana alivyowaambia peter na wenzake …I will make thee fishers of men…(Matayo 4:19 na (Mt 28:19-20)..Basi enendeni mkawafanye watu… Kama sisi wachangiaji tu wakweli, mtakuabaliana na mimi kua gospel outreaches to win fresh souls kama agizo kuu sio major characteristic ya so called makanisa ya mitume na manabii wa leo. Hii Ki Mungu, ni very serious foul ambayo mtumishi John Paul anapomalizia majibu yake kwa maswali yangu na kusema hivi “………sababu ambazo ukizichunguza hazileti MAANA YOYOTE, Kikristo wala Kimwili”, anatia mashaka status yake ya kuona/uelewa( spiritual perception/discernment) ya mambo ya kipentecost kua tumetoka wapi na tunakwenda wapi kama watu wa Mungu na nini hasa kimetokea kizazi chetu cha leo kuhusiana na kutimiza duniani hasa kilichomfanya Yesu aache mbingu na uungu wake na kuja duniani.Umeshawahi kujiuliza kati ya wanohudhuria hapo kwa TBJ na huduma na makanisa ya ivyo,wapi ni wengi kati ya waliohamia huko wakiwa ameokoka tayari na waliookoka toka dhambini ktk ibada yake? Niambie kama Mungu analipa kwa uaminifu, TBJ analipwaje kuhusu watu wengi uliosema anawahudumia waliookoka tayari na hakuwavua yeye but ni maombi, jasho, kilio, pesa, mikakati ya watumishi wengine wasio na TV na pesa ya kuonekana na kutangazia na kuvutia watu kwao ktk media?
  Kama mtu aliyeookoka na hata baada ya uchunguzi wake anashindwa kuona hili tatizo( kuvua waliovuliwa na kum-credit kua anahudumia wengi ambao kimsingi walishahudumiwa huko walikotoka na kukimbilia kwa manabii na mitume hawa kwa sababu…(2Tim4:3-4) na kwamba hakuna regular and pure gospel campaigns kama one of the core church characteristics), kushindwa kuona hiki ni kitu kibaya, it is tatizo by itself! Kwa kushindwa kuona something is wrong somewhere kwa wakristo wa aina ya John Paul wanaojua Neno na tulikotoka wapi,Unaweza elewa kwa kiasi gani kanisa lilivyozidiwa, si ajabu sasa kua wakristo wa leo based only on miujiza, ishara na baraka-baraka badala ya wokovu na utumishi kwanza kasha hayo yaje baadae.Kama Mungu analipa kwa haki, ni vema basi kwa John Paul na wenzake kuchunguza na kujua kabla ya kumchukulia mtu kua ana huduma kubwa na anahudumia wengi na anaonekana ni nabii kweli kweli, tukajizuia kidogo kwakua ninawasiwasi kama kuna ujira mbele za MUNGU mwaminifu wa kiasi hicho tumjuavyo kwa wahubiri- wachungaji, mitume na manbii wa kileo wavuao waliovuliwa kwa mikakati ya nguvu ya pesa na media zao badala ya kicho, hofu,mzigo wa ki-Mungu na nguvu ktk Roho Mtakatifu kupata fresh souls from hell.
  2. “Swali: Hivi kutoa unabii kuhusu mtu au wtu, taifa, jamii na ulimwengu na kusafisha maliwato ya kanisani kwako, kuosha magari ya mchungaji kanisani, kumsaidia mdada mmoja gauni mbili tu yule anayekuja na nguo moja tu nusu mwezi kanisani, kumshuudia mtu mmjoa teja akaookoka, kuna tafauti mbele za Mungu? nani zaidi? nani kapiga kazi kuuuuuuubwaaaaa ya utumishi mbele za Bwana?”
  Jibu: Neno la Mungu linatuagiza kutenda mambo pasipo MASHINDANO. Yule anayefagia kanisani ASIJIDHARAU kuwa anafanya kazi ndogo wala yule Anayehubiri pale Jangwani, mbele ya watu elfu 10, naye hatakiwi KUJISIFU kwamba nafanya zaidi. Jambo la Muhimu hapa hapa ni KILA MTU AFANYE KWA UAMINIFU katika nafasi yake aliyopo na huduma anayojisikia ndani yake. Hivyo ukubwa wa Kazi kwa Mungu ni ULE UAMINIFU WAKO katika kazi unayoifanya. Gari la uwezo wa kubeba mzigo tani 5, likitumika kubeba tani 4.5 litakuwa limetumika VIZURI ZAIDI kuliko gari lenye uwezo wa kubeba tani 60 likitumika kubeba tani 20. Kwa hiyo unaweza kushangaa kuwa Mtu anayefagia kanisani, mbele za Mungu anaweza kuwa kafanya kazi kubwa zaidi kuliko anayehubiri mikutano ya injili ya watu elfu 10 kwa kuwa kilichoko ndani kilitakiwa kiwafikie watu laki 1
  Kwa hiyo yule aliye na KARAMA anatakiwa atende kwa kuliingana na kiwango cha Karama kilichowekwa ndani yake, na yule aliyeko upande wa HUDUMA ZA MASAIDIZANO naye anatakiwa afanya kwa nguvu zake na kwa uaminifu.
  Response: Kama ukweli ndio huo na umejibu vizuri sana kua what matters ni uaminifu na naongezea mambo kama bidii, ukweli, moyo, willingness kutumika nk, then why all these campaigns na kuadmire watu wa mbali wakati watu wa kwetu na kanisani kwako na kwangu na hapa hapa Tanzania tupo, wapo? Why mioyo, furaha na nguvu nyingi zenu ziwe kwa miisho ya nchi kabla ya Judea, Samari na Yesrusalaem? Hamuoni kua ni mambo tu ya kibinadamu yasiyo na tija nani madhara ya utandawazi hata ktk mambo ya rohoni kwa kua globalization negative effects haziko ktk social-economical sphere tu even spiritual too?
  3. Swali: “What real made TB Joshua TB Joshua the “true prophet of God” to you? Is it TV and other media advertisements or……what if there was not media to bring him to your room, country, who would be your prophet?”
  Jibu: Mimi nikiangalia namna wanavyohudumiwa watu, baada ya kufanyiwa maombezi, huwa inanipa kuamini kuwa pale panafanyika kazi sahihi ya Injili. Watu huwa wanashahuriwa kuwa kwa kuwa sasa ameshapokea muujiza toka kwa Mungu, kilicho cha muhimu zaidi sasa ni kUKABIDI MAISHA YAKE MIKONONI MWA MUNGU, KWA KUMFANYA YESU AWE BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YAKE. Maneno haya ni adimu kwa watumishi wetu wa hapa nyumbani, ambao habari za huduma zao huonekana kwenye TV na kusikia kwenye maredio. Sitasahau siku niliposikika mtumishi mmoja, anayefahamika sana nchini, akitangaza kwamba BAADA YA MAOMBEZI KILA MTU ARUDI TU ALIKOTOKA. HATA WA MSIKITINI ARUDI TU MSIKITINI KWA KUWA MUNGU NI WA WATU WOTE! Japo siwezi kuamua moja kwa moja kuwa yule ni Nabii wa Uongo lakini bado naendelea kuyatfakari maneno hayo kama Nayo yana lengo la KUMFANYA ANAYEYASIKIA AMGEUKIE YESU.
  Mara nyingi sana T.B Joshua amekuwa akisema kuwa SIYO LAZIMA mtu ahangaike kwenye SCOAN, Bali anaweza kutafuta MAHALI POPOTE AMBAPO NENO LA MUNGU LINAFUNDISHWA KATIKA USAHIHI. Hayo nayo ni maneno adimu nchini kwetu Tanzania!Nimekuwa Mkristo kabla ya kumfahamu T.B Joshua, na hata pasipo T.B Joshua nitaendelea kuwa Mkristo. Mwokozi ni Yesu na si T.B Joshua. Yako mengi ambayo Mungu ananitendea kwa kupitia MIMI MWENYEWE. Hivyo sitegemei NABII ye yote kuendesha maisha yangu BALI NAMTEGEMEA Yesu. N wala T.B Joshua SIYO NABII WANGU bali namuona kama Mtumishi tu wa Mungu sawa na watumishi wengine. Napenda kujifunza kwake kwa habari ya utoaji na mafundisho anayoyatoa kwa kuanzia yeye mwenye kuwa MFANO. Akifundisha watu wawe watoaji, yeye mwenyewe ANAONYESHA JINSI ANAVYOTOA. Hii ni tofauti sana na watumishi wengi, hasa wa Tz, ambao wakifundisha kutoa BASI HUWATAKA WATU WATOE WAMPE YEYE/HUDUMA YAKE!
  Response: Excellent kwa jibu hili, jinsi ulivyomreccomend mpendwa TBJ kama mtu tu na mtumishi kama wewe na mchungaji wako na si semi-God au super-human kama viashiria vya michango ya baadhi yenu vinavyoindicate hata kama hamjasema straight! This is maturity na in fact Roho Mt aliona nature ya wanadamu kuadmire wanadamu wenzao mpaka kupitiliza, akaweka balansi kiaina ktk Yak:5:17-18 …Eliya alikua mwanadamu… in the same nature with us but aliomba kwa bidii na……. kuhusu kujifunza kwake badhi ya mambo hili nalo ni jibu zuri kwakua Bwana YESU kuna wakati aliweka kabalansi kidogo akiwaambia wanafunzi wake kua wanaweza kuwasikiliza na kujifunza toka kwa mafarisayo strictly kwa kua wanaketi ktk kiti cha Musa… lakini kwa matendo yao…..wajitenge nao(Mt. 23:2-3). Angalizo ni kwamba sio wote wenye uwezo wa kutenganisha pumba kama zile za ibada ya namna ile ya Damu ya YESU, faith statement ya ukakasi kama ile, uuzwaji wa mafuta ya upako…..such a serious spiritual foul of exchanging God’s gift to material things contrary to the Biblical basics…mmepewa bure…toeni bure (Mt. 10:7-8) na karipio kali la Petro kwa mchawi mmoja aliyetaka kutrade karama ya Mungu (Mdo 8:9,18-20) kama wanovyotrade huko ktk so called makanisa ya ki-born again if not burn again ya Western African Countries e.g. TBJ, Kenya,Uganda na Tz kwa baadhi na kimya kimya ….such huge spiritual problem John Paul na Milinga sijui why hawaoni na kuisemea wazi wazi kama kuconduct mambo ya mbinguni kwa namna hii ni Kibiblia au kibinadamu au kipepo kabisa? ktk hili Milinga na John Paul plus wafuasi wenu hamjasema kabisaaa na at least siamini kama kuna mtu kati yenu anaweza sema kwa ujasiri na kwa reference ya right scriptures contextually and in a Pentecost customarily manner kua ni sahihi doing this way God’s business in the born again congregations. John Paul ni sahihi this hanky-panky spiritual gift trading?
  Kuhusu kuwahubiriwa watu na wakiookoka kuwaambia wayatafute makanisa yoyote ya kweli ya Kiroho, mimi na hata kwetu hufanya ivyo sana na hata mikutano ya big November Dar iliyovuma sana, watu walikua wakielezwa sana ila few cases za baadhi kusema watu waende kwao tu au warudi huko huko walipotoka ni peculiar na weakness ya few na sio common practice ya watumishi na makanisa mengi. However, siyo vibaya kama wazazi wazaaji, waliofunga na kuomba na kugharimia mkutano kwa pesa na mikakati mingi, kwa nguvu kabisa kuwakaribisha waliookoka kwenda ktk kanisa lao, hakuna dhambi hapo hata kidogo nani haki ya mzazi aliyeza kupenda kulea, kibiblia inakubalika kwakua kuna siku Paul kwa uchungu wa kuzaa na kulea na kuhakikisha watoto aliowazaa mwenyewe wanabaki wake na salama alisema hivi (Gal.4: 12-19) …vitoto vyangu vidogo navionea utungu….. na kuna wakati alikua very protective nakazi yake na kusema kwa ukali (1kor 4: 14-19)… kua na waalimu kumi elfu but baba ni mmoja niliyewazaa ktk Kristo…Therefore kua na hamu, ukali wa kuwatunza watoto wako na bidii ya kutaka ubaki na watoto wako uliowazaa mwenyewe ni Kiblia kabisaa, no question about that kwa anayejua Neno la Mungu na maana hasa ya uzaaji kiroho ingawa hata kimwili ni ivyo ivyo, kwa kua ni mzazi mwenye pepo I think atakayebeba mimba kisha kuzaa na kufurahia wengine( wazazi strangers) wachukue watoto wake wa thamani na kulelewa huku akijua kwa hakika kila wazazi na malezi yao kwa watoto wao hutofautiana!
  Kuhusu utoaji, ushauri wangu ni tembelea makanisa mengine ya TZ hapa hapa, utashangaa kua watumishi wanaotuhudumia wanajua nini maana ya kungoza ….kwa kuonyesha mifano. Mchungaji wangu mimi ktk michango ya kujenga kanisa, alitoa gari yake mpya aliyopewa kama muujiza ana aliyokua anahihitaji sana, aina ya Haria ya mil. 27, wengine wanatoa mpaka viwanja tena vya Dar na unaelewa nini maana ya viwanja dar sasa, wengine walitoa mishahara yao yote kabisaa, nadhani do the search Mr. Paul watoaji tupo, wapo basi tu Neno linatimia …nabii hana heshima kwao but nabii wa nje…..lo! akina Paul na Milinga haoooooo. Je hamjawahi kuuhudhuria ibada za vijijini hasa wakati wa mavuno, wapendwa wanavyompenda Mungu na waposomba magunia ya mazao, kuku, mbuzi, ng’ombe kuleta kanisani kumbaliki Mungu wao, mtumishi na mipango ya kanisa lao? Au kwakua hanjaonyeshwa kwa TV basi ndio inakua nongwa? Afterall, hata wasipoonyeshwa utoaji wao kwa Tv na kukosa sifa za akina John Paul na Milinga, so what? Inawacost nini? Wakati wanaatwa ma-credits kibao toka kwa Mungu hata wasipojulikana na kuonekana mpaka Yesu arudi, what was is the problem banaaa? Pressure na mahangaiko yenu tu wazee wa kazi.
  4. Swali. “Sasa where was Holy Spirit siku izo atofautiena na wa leo ktk mambo ya msingi?au roho mtakatifu wenu wa leo ameaamka sana na yuko makini saaaana na creative sana kuliko Roho Mt wa wazee hawa ambao wengi wetu ni matunda ya kazi yao ktk nchi hii?”
  Jibu: Mi ninachoona ni kuwa Siyo kwamba Roho mtakatifu amebadilika wala kuamka. Siku za akina mzee Haris Kapiga, Andrea Shimba, Mosea Kulola na wenzake, teknolojia haikuwepo, Hatukuwa na magazeti yenye kusambaa nchi nzima kwa wakati. Hapakuwa na redio sehemu kubwa ya nchi. Hatukuwa na TV kabisa katika Tanzania. Hali hiyo ilisabaisha wanayoyafanya yafayike kama kimya kimya. Ila naamini Kama KUNGEKUWA NA TV, na kazi ya huduma ya wazee hao ikawa inarushwa angani, naamini kabisa wazee hao wangekuwa maarufu sana sana Tanzania, Africa na hata duniani kwa ujumla.
  Mfano mmoja: Palikuwa na mkutano wa Injili pale Nzega, eneo maarufu la PARKING, miaka ya 90, ambapo waliokuwa wanahudumu hapo ni pamoja na Mzee Andrea Shimba. Wakati mkutano unaendelea, kijana mmoja akawa anazunguka na baiskeli. Hata baada ya kuonywa na watu aache yeye aliendelea. Baada ya kuona hivyo, mzee Andrea Shimba aliinuka na kusema kwa sauti: “Bwana na akukemee!” Yule kijana alianguka, akawa kama aliyezimia. Alibebwa na kupelekwa kwenye chumba cha maombezi hadi baadaye alipozinduka. Tukio hilo lingerushwa kwenye TV, nalo lingetosha kabisa kuleta mchango wa kumfanya mzee huyo kuwa “maarufu”!
  Suala la Injili kwa sasa limevamiwa. Na haihitaji hadi kumuangalia T.B Joshua ndipo mtu aone kuwa hali ya Injili kwa sasa ni mbaya. Injili ya sasa ni Ya “mafanikio”. Hivyo kama ni suala la kuhoji HALI YA ROHO MTAKATIFU wa sasa na Wa zamani, Maswli yako mengi sana, hapa hapa nchini Tanzania. Siyo T.B Joshua TU ndiye anayetofautiana na akina Moses Kulola, [Japo ninahitaji kufahamu MAMBO YAMSINGI AMBAYO T.B Joshua anatofautiana na wazee uliowataja], ila ni wengi sana, wanaohubiri Injili ya Mafanikio, ambao ni naamini hao NDIO wanatofautiana na akina Kulola kwa mambo mengi ya msiingi, maana hata hawataki tena kuwaambia watu waache dhambi!
  Response: Tena umejibu vema kuhusu impact ya media kua kama zingekuwepo, wazee hao pia wangefahamika au kua maarufu lakini hasa hilo ndio tatizo langu na baadhi yenu, why umarufu ktk au via media uwe kigezo cha kudhani fulani na mambo yake yatetemekewe na kuchukuliwa kwa uzito wakati hata bila media, tulionao wanatutosha na yanayotendeka yanatutosha kumtukuza Mungu na kusikia toka kwa Mungu? Kwanini basi natusiyache basi yaletwayo na media kama kwetu yapo pia, unless kwenu akina Jonh Paul hayatendeki, hayasiskiki na Bwana asemagi kupitia manabii mambo ya kikanisa, kitaifa na kimabara na kimaisha binafsi ya kiroho hapo kweli papatikieni ya hao waletwao na media. Kama nyumbani kwako Bwana kajaa tele kuna haja gani na chakula cha jirani? Kujifunza SOME issues kwa jirani fine but moyo, hamu, jitihada,ushabiki, admiration kuhamia fully kwa jirani ni kasoro ya mleaji aliyemlea mtoto huyo au ni stubbornness and cronicness ya mtoto mwenyewe japokua atakua amelelewa vema kutunza maadili mojawapo ikiwa ni kupenda na kuthamini vya nyumbani kwanza.
  5. Swali: “From Biblical point of view, all prophesies given in the Bible were at the end of the day aimed to restore back people to God (in the old testament) or bring people to Jesus (in the new testament) or rarely prepared the saints of the prosecution coming for the sake of the work of God (Paul, Peter), nothing more, nothing less, therefore….
  • Can sb tell me what has been the purposes of TB prophesies in reference to the above Biblical context?
  • Will you also categorically establish the differences btn prophesy given out of holy motives vs. human proudness, famousness, uniqueness building, human creativity (crowd pulling), satani/darkness powers etc?
  • Has there been any advantage of his prophesies to the church, children of God, and unsaved?”
  Jibu: From Biblical point of view, ziko Nabii za Hukumu/Adhabu. Wako watu waliotabiriwa KUFA na kweli walikufa, kwa magonjwa, katika Vita na hata kuliwa na Wanyama. Ni aina ya UNABII ambalo lengo lake siyo “kurejesha” bali “kupatiliza”. Yusuph alionyeshwa habari ya NJAA na ile njaa ikaja kweli. Kuna vita vilitabiriwa na kweli vikatokea. Hata Bwana Yesu naye alitabiri habari ya Mti, na mti ule ukanyauka. [Siami kama kunyauka kwa mti ule kulikuwa na lengo la kuwaelekeza watu katika Ufalme wa Mungu]
  Response: nirudie tena kusisitiza kua kila unabii uliotokea lengo ni restorations, salvation and preparation. Kupatiliza simply refers to kuadhibu na kutransfer adhabu from the present generation to the next ….why this, the aim was the same….restoration! wakati watu walivyoambiwa Mungu ni mkali, mwenye ghadhabu na anaweza adhibu mpaka kizazi kijacho…that fear ya kutandikwa na Mungu na mpaka kizazi kifutacho kukumbwa na consequences…made people respect God, come back to him, keep his commandments na ndio kurejeshwa uko. Utabiri wa mnyama kutokea na kuangamiza watoto wale, bado ni restoration ile ile kwa kua hofu iliingia na kuadibisha watu kutotania watumishi na mambo ya Mungu… (1Tim: 1:20). Nachosema Mr. John, umetofautisha wrongly, all unabii aimed ONLY at restoration, salvation and preparation…nothing more nothing less! As a matter of fact, even the other two elements, salvation and preparation can also be summarized in only one major aspect of any unabii wa Mungu and that is Restoration. Nabii zote aidha zilitoka kuonya, kurekebisha, kuleta utiisho, kuua, kuhuisha, kuadhibu, kutoa mwelekeo ujao, kuonyesha yaliyofichika, kuumba imani zaidi kwa Mungu, kutia moyo nk, at the end of day…nikurejesha wanadamu kwa Mungu, basi, hamna kingine.
  Kwa hiyo pamoja na sababu za unabii ulizozitaja, lakini kuna Nabii ambazo lengo lake ni KUJENGA IMANI mioyoni mwa watu, kama ule mti ulionyauka. Kuna mambo yakitabiriwa, kisha yakatokea, huwafanya watu Waamini kuwa kumbe kweli Mungu yupo. [Japo Yesu alisema Heri aaminiye pasipo kuona].
  Response Kujenga imani na kuwafanya au waamini kujua Mungu yupo, wamjue sana na kwa karibu Mungu….bado ni restoration ile ile, hamna jipya hapo mtakatifu John!
  i). Kwa upande wa Nabii za T.B Joshua, Ziko ambazo amekuwa akitoa kuhusu hali iliyoko mbele ya mtu fulani na kumwambia kuwa ushindi wa mtu huyo ni katika Kukaa na Mungu. Wengi huwa anawaonywa juu ya mambo mabaya yaliyoko mbele kama mtu huyo hatabadilika. Ziko nabii amekuwa akizitoa kwa mambo mabaya yajayo na kuwaomba watu wawe katika maombi ili Mungu aepushe jambao hilo {Ndg Milinga alitoa mifano}, na ziko ambazo zimekua ni kuwafanya watu wajenge imani ndani yao, na kubadili mwelekeo walio nao juu ya Mungu.
  Ukitazana Emmanuel TV unaweza kuona Waislam wakishuhudia na Kukiri kuwa Hakika T.B Joshua anatumiwa na Mungu na kumuomba andelee hivyo na pia awaombee na wao hili waweze kumfahamu Mungu huyo anayemtumia.
  Response:Ni jambo jema kwa wiislamu kukiri na kusema hivyo but umeshindwa kuona kwa mapana kua kwa mtu ambae ni empty….hana Mungu wa kweli, doctrine, hana uzoefu na kutembea na Mungu, hawezi kua na reference yeyote aonapo mambo kama hayo ya TBJ! Mtu kama mimi, wewe na wengine ambao tayari tunahazina ya kumjua Mungu wa kweli, hayo kwangu na kwako ni normal and minor issues, na ndio maana wakristo wengi waliookoka kizazi hiki cha media influence, kwakua hawajui tumetoka wapi na kwakua hawakuwahi kumjua Mungu kabla ya vurugu hizi za leo, ni rahisi kwenda na kila kiibukacho na hawawezi kujua nini maana ya imani potofu, watumishi matapeli wa hapa Dar, Tz na nje. Hawawezi kujua ivi hasa mtumishi wa kweli ni yupi na wa kufanya wanadamu kama family na personal project ni yupi? Ni kazi kweli kumng’oa aliookoka wa kileo ktk imani za misukule, kuoga maji kama damu ya Yesu, kutumia socks, vitambaa, miwani, tai, mashuka, chupi zilizoombewa na kuzitumia kila leo kama hirizi, kuvunja laana, kutapishwa mikosi, kuuziwa mafuta ya mti wa mizeituni toka bustani ya gestemane, maji ya Jordan, chumvi ya galilaya, na mbwembwe nyingi, usiniambie mtumishi Paul na ufahamu wa Mungu wote niliouona kwako, umo na wewe ktk utoto kama si uhuni na utapeli huu wa mitume na manabii wa leo hawa?
  Tena wanokaa town, cities kwa wingi but village, kata na tarafani..weee…thubutu..kwani wao wajinga, they know where misimbazi are easily flowing! siyo kwetu uko ushirombo au mpanda wilayani nilipofanyga kazi ambapo sadaka nilikuta katikati ya wiki alfu 5, jumapili labda alfu kumi na x.mass at least alfu 20 na hapo mchungaji anena kwa ndimi na machozi akimshukuru Mungu kwa kua amemuona! kwa misimbazi 2 tena end of the year..x-mass! TB J anaweza kukomaa na kazi ya Bwana huko mpanda na watoa sadaka dizaini hiyo ambao wanatoa sana vitu kuliko pesa live na bado akaendelea kutoa unabii wa vifo vya Bingu wa Mutharika, Saitoti, plane crush Nigeria na may be Bill Clinton, Bush, Barak Obama? manake kuwatabiria kudead wazungu wakubwa hao hafanyagi but yeye anawadedisha wabongo wenzetu tu, da! Milinga unabii huu mkali eeee, kuwalenga wabongo tu but Putin wa Urusi, Sakozy wa Ufaransa wapete kama kawa? mbona Bwana Yesu anawatoto dizaini za ajabu jamani? La!
  ii). Namna ya kutofautisha “btn prophesy given out of holy motives vs. human proudness, famousness, uniqueness building, human creativity (crowd pulling), satani/darkness powers etc?” ni kuwa hizi za PILI huwa hazina jambo lolote la Kufanya mtu amrudishie Mungu utukufu. Baada ya unabii wa namna hiyo watu hubaki wanasifia tu mtu yule na wala hakuna mwongozo wowote kuwataka watu WATOE MAISHA YAO KWA YESU! Lakini kwa SCOAN watu huelekezwa kuwa njia salama ya kulinda miujiza na unabii wanaoupokea ni KUKAA NDANI YA YESU!
  Response: Kusema ni jambo moja na kufanya kwa dhati ni jambo jingine, japo huelekezwa, but the practice on the ground ni tofauti kabisa, embu angalia ktk mitandao waumini wake wa Dar na TZ mnavyo comment na kumrank! Kwahiyo general practice haiendani na specific practice…iyo ya kuwaelekeza tu! Hii inanikumbusha hapa TZ na hasa Dar mtumishi mmoja alipoaanzisha kazi, waumini wake waliiigiliza mpaka sauti achilia mbali kumtukuza na kumuinua hata kama kanisani kwakwe ali…so called waeelekeza watu….geresha tu…kwa kua kama mchungaji wa kweli na uko makini na kundi lako na unajua tabia ya jumla ya kundi lako ni kukuinua na kukupambapamba, na almost kukutukuza na kusifanyike serious jitahada za makusudi na endelevu za kuwatrain watu to never glorify human, nani hata amini kwamba kuna namna mchungaji, mtume au nabii huyo anaenjoy hiyo unGodly crediting attitude?
  iii) Kutokana na sababu nilizoeleza, ni dhahiri kuwa unabii wake umekuwa na faida kwa kanisa, watoto wa Mungu na hata kwa wasioamini pia!
  Response: Kama unabii wake unatija… je kutabiri ushindi na ushindwa wa timu ktk mpira una aim nini au tija gani ktk mambo ya mbinguni na ya kikanisa na ya kuwin souls to heaven? Jibuni tafadhari Paul au Milinga na wengine humu wa pande hiyo and why he always goes for the huge things (national team), people (presidents) and never see kiroho small things-(viteam vya ligi za nchini kwake), small people (me and u)? Tena plz niwaombeni kitu rafiki zangu, mwambieni anitabirie jamani faster ili BoT iwe yangu au niwe TZ next president, nitawakumbuka tu, nitamteua Milinga awe mshauri wangu wa ndani kuhusu religious organizations and faith and Paul atakua international relation religious organizations envoy to Nigeria ili afanye correspondences tumlete TB Bongo..tehe
  6. Swali: “Kwani what happened huko nyuma kabla ya kumfahamu TB Joshua na nabii zake? Tulipata hasara gani kwa kutofuatilia nabii izi au tumeshaadhirika na nini kama kanisa, mtu mmoja mmoja na Africa kwa kutotekeleza nabii izi? mbona ilikua peace tu siku zote za nyuma until recently after tv na settelite technology kuja third world ,yaani tena waaalaa kulikua hatuna mapressure mnayotupa sasa kwa kutuambia anayotabiri kila mara! Na kama ilikua lazima tupate nabii hizi, why Mungu akusababishaga kwa njia yeyote tuzipate? Au kwa wapendwa waliopovijini sasa hivi wasiofuatilia mambo haya wanampenda Yesu na hawana hata tv au ving’amuzi kunasa wahubiri wa nje, wanakosa nini mnafikiri? Watapata hasara gani ambazo nyie wa town/cities hamtatazipata? Hamuoni ni matatizo yetu tu aliyosema Mfalme Suleimani…aongezaye maarifa houngeza masikitiko…au in my own way…the more much know/informed you are…..the more majaribu, mapito an confusion you will have?”
  Jibu: Swali hili ni refu na lina mambo mengi lakini nitajitahidi kujibu kwadri nitakavyoweza:
  Dunia ni kubwa na ina mambo mengi. Kila mtu alipo kuna mambo ambayo huyasikia na mengine ambayo hayasikii. Wahubiri ni wengi na watumishi wa Mungu ni wengi. Ukikaa kwenye TV ukatafuta chaneli zinazorusha habari za Neno la Mungu unaweza kushangaa kuona mambo mengine ambayo yanashangaza zaidi kuliko yanayoonekana kwa T.B Joshua na hata mafundisho yako mengine zaidi ya yale ambayo hufundisha yeye. Jambo ambalo naona limezidi watumishi wengi, T.B Joshua ni MTOAJI. Sijawahi kuona kiwango hicho cha utoaji wa watumishi.Kwa hiyo ukisema tulikuwa tunakosa nini kwa kutokumfahamu T. B Joshua ni vigumu hasa hadi pale Mtu ATAKAPOJUA AMEPATA NINI KWA KUMFAHAMU T.B JOSHUA. Kama kuna mtu hapati chochote toka kwa T.B Joshua basi huyo yeye HAKUWA ANAKOSA CHOCHOTE kwa kutokumfahamu
  Response: Kuhusu utoaji, ni bahati mbaya kua haujakutana na watoaji katika nchi hii na nimekupa mfano wa kanisani kwetu mchungaji alichokifanya ktk utoaji, lakini muda hautoshi kukuorodheshea wapendwa wa kawaida waliotoa mpaka viwanja tena vya Dar kwa kumpenda Mungu wao, unaishi wapi kama hujawaona watu wa Mugu nchi hii walio watoaji mpaka kushangaa utoaji wa mbaaaaali? Hata ivyo sikutegemea kama ungetoa mfano huu na kuufanya kua big issue kwakua, kwa watu makini na wanojua utoaji ktk Biblia na wanaojua namna Mungu ashangazavyo wanadamu kwa njia zake zilivyojuu kuliko zetu ktk kujaji mambo na kuamua, angesita kusema TBJ anatoa .Unamkumbuka yule mwanamke aliyetoa senti but akina TBJ wa wakati ule wakamwaga mapesa na comments za YESU zilivyokua kwa who actually gave much?..Mark 12:41-44. Huo utoaji hautoao kaka TBJ, a u sure kweli umekidhi viwango vya Mungu au viwango vya John Paul na wengine humu? Unajua kiasi akipatacho? Je Alisha wahi kutoa financial statement yeyote ya mapato yote? Ana wakaguzi? Unajua kiasi anachobaki nacho akisha toa hicho kinachowavutia wengi kusema jamaa mtoaji? Mtu makini hawezi toa jibu hili bali atasema……no comment but kwa bw. John labda unajibu muzee…karibu ukizingatia mark 12:41-44
  Jambo jingine ninalofahamu ni kuwa T.B Joshua SIYO MUNGU. Siyo muumbaji wa hayo anayoyatabiri. Ni mambo ambao HATA KAMA ASINGETABIRI, yangetokea tu! Kwa hiyo kutabiri au kutokutabiri HAKUONDOI UWEZEKANO WA MAMBO HAYO KUTOKEA. Kwa hiyo hofu inayopatikana kwa sababu ya kujua kuwa kuna jambo fulani linakwenda kutokea, wale wenye mtazamo CHANYA WANAIBADILISHA HOFU HIYO NA KUWA KATIKA HALI YA MAOMBI ili ikiwezekana Mungu aondoshe hayo mabaya ambayo yameonekana kuwa yanakwenda kutokea. Ndugu Milinga ametoa mfano ambapo T.B Joshua alionyeshwa kuhusu ajali ya Ndege kisha akawasihi watu wawe katika maombi makubwa, na hata alichukua hatua ya kushauri mamlaka husika waangalie namna ya kuepuka tatizo hili. Lakini badala yake watu walidharau, wakafikiri anashida na pesa. Dharau dharau ikaleta madhara.
  Response: Ingawa nakubaliana na Milinga na kwakua nasoma Neno kua moja wapo ya njia sahihi za kibiblia kupima unabii kujua kua umetoka kwa Bwana ni kungojea kuona alivyosema yatokee exactly, lakini utakubaliana nami kua kwa machanganyiko na utapeli wa kizazi cha leo cha mitume na manabii wa ujanja ujanja, pesa-pesa and umaarufu looking, kamwe na haiwezekani kwa mkristo mwenye kujitunza kulainika tu haraka jambo likitokea kama lilivyotabiriwa hasa siku za leo, ni vema kwenda mile nyingine tena, to be patient, why pressure? Je huwajui au hamjawahi kukutana na hata kuwasikia watumishi nje na ndani ya Bongo na Tz, wamtumikiao Mungu na wameookoka na kila kitu kama wapetekoste haswa na wanatabiri exactly na yanatokea perfectly yet ni matapeli, wazinzi, wauza unga, viungo vya albino, watumiaji ndumba, anasa people, wenye kununua ndege, magari ya fahari, maviwanja na kufungua benki account nje ya nchi, kua na miradi mikubwa wakati ndani ya kanisa au huduma hiyo anayoongoza kuna maskini wakutupwa na watu wenye huitaji maalumu kama wajane, yatima, walemavu? Ivi mtumishi wa ivi atakua na mvuto na mamlaka gani kwa mtu mweye Mungu mzima kama mimi na wewe kumsikliza na hata kutii mambo yake?mhuni na dhulumati wa aina izi? To hell with them, wanaudhi sana na nasika hasira kabisa, watu hawa wameharibi picha yetu mbele ya mataifa, ndio maana tuonaonekana waliokoka wote ni matapeli na watafutaji ulaji na life kwa kutumia huduma na makanisa..am serious nasika hasira na nimekwaza siku nyingi na apendwa na watumishi wa aina hii, wanatuvua nguao mbele ya jamii, hatuaminiki na inakua kazi siku izi kushuudia manake ukikukutana na watu wanaojua issues, wanakuachallenge kwa kukutajia watumishi na makanisa na hudama kibao za hawa mitume na manabii wapumbavu kabisa hawa….Ndiyo maana Yesu alikua sometime anakerwa kwelikweli na kuwarurua watu hekaluni,binua mameza yao,chapa bakora na wengine kuwachana live kwa kuwaambia uso kwa uso … wana wa ibilisi, kizazi cha nyoka, kizazi kiovu cha uzinzi na maneno mengine makali kuzidi ya kwangu. Kuliko kuwaamini faster hawa manabii na mitume wa kileo, I can buy my time hata miaka kumi na tano, kwani kuna uharaka gani? Hata ivyo wananiongezea au kunipunguzia nini anyway ktk maisha yangu ya kwenda mbinguni? Will they stop me or in anyway contribute for me to enter mbinguni hata nisiposikia chochote na kufanya chochote chao? Are my pastors whom at least and reeasonably I know closer and for years not enough? Nonsense! Nauliza na kujibu hivi kwa usahihi kabisa kwakua nimeshakutana na wanaotoa utabiri, mitume na manabii wa dot com ya leo na kweli yanatokea exactly but nyuma ya pazia wanavyoishi na walivaa nguvu gani walipokua wanatabiri, utakua na taadhari zaidi yangu mara mia tano! wanadamu hawa ni wanadamu tu, siku zote kuwepo na tahadhari, mwanadamu anaweza akawa chochote wakati wowote.
  Ninanukuu; “Na kama ilikua lazima tupate nabii hizi, why Mungu akusababishaga kwa njia yeyote tuzipate?” Mwsho wa kunukuu.Maneno haya nimeyafananisha na yale ambayo watu husema: “Kwa nini Mungu hakutafuta njia mbadala ya kuleta wokovu badala ya hiyo ya kufa msalabani”Lakini, Hivi ndg Seleli unafikiri wale ambao INJILI HAIJAWAFIKIA ni kwamba MUNGU HATAKI IWAFIKIE? Maana tunaweza kusema “kama anahitaji injili iwafikie, kwa nini hatafuti njia mbadala ya kuwafikishia Injili kuliko kusubiri hadi wahubiri wafike huko? Kwamba kwa nini Mungu hakusababisha njia yoyote, hadi asubiri TV na Satellite ndiyo tupate habari za Unabii wa T.B Joshua? Hapana. Nadhani kuna haja ya kupanua ufahamu na kuangalia kwa upana zababu tunazotoa kama mapingamizi kwa huduma hii ya T.B Joshua.
  Response: Picha iliyojengwa nanyi ni kama vile kuna something special to hear and do what this man of God or god is saying or prophesying while the reality is, hayo hayasemayo(kama yanatokana na devo, yeye au Mungu) si mageni na atakayoyasema(kama yatatokana na devo, yeye au Mungu), si mageni kwakua Roho Mt huwatumiaga watu wa kawaida kanisani kwangu hapa Dar na hata huko nilipokuwepo mkoani, kuona mambo mazito na kuyatabiri ya kikanisa la mahali pamoja, Tanzania, Africa na Ulimwengu, si issue kwangu, sijui why mnaona ya TB ni very special sana? Sisi wenzenu tumeona na nanajua Bwana anawatumia wengi hapa hapa TZ from village to cities ambao huonaga mambo mazito na kuyasema yakatokea exactly na hata baada ya kuyapima na kubuy time na pia kwakua at least tunayajua maisha yao maiaka na miaka, tunadhibitisha ni kweli. Ninamfahamu dada mmoja, akiwa shambani mwake Igunga darasa la 7 failure, very interior uko village, hana hili na lile, Bwana akamtokea na kumwambia kuhusu Rais wa Nchi hii ajaye baada ya Mkapa, Mungu akafanya mazingira mpaka wakakutana na JK, huyu dada alitembea na team ya JK muda wote wa kampeni 2005 akiwa anaomba na kufunga for JK victory na protection ya nguvu za Mungu dhidi ya uchawi, mizimwi, majini na matambiko yaliyokua yanamtandika JK alipokua anakwenda kinyume kwa kutaka kumpata Mungu wa kweli wa dada huyo, mtakumbuka alivyobilingita jukwaani Jangwani siku ya ufunguzi wa kampeni na watanzania mkapigwa fix eti alikua kachoka wakati ktk ulimwengu wa roho, sisi wengine we knew nini haswa kilichotokea. Hatimaye dada huyo from village alikuja kuishi Dar, ikatokea kufahamiana nae kwakua alihitaji nimfundishe English course, ndipo tukafahamiana kwa kirefu na kuniamini kunipa shuhuda hiyo, Tunaweza kaa ivi, ghafla simu za from big house there zinaita, inatumwa benzi jeusi kumchua kanisa or home kwake to ikulu, JK anakua amemuita kwa ajili ya kufanyiwa maombi au yeye mwenyewe akionyeshwa jambo na Mungu kuhusu maisha ya JK au jambo ktk nchi, anapiga na kufuatwa. Kwa ushuuda au taarifa yenu tu, manake kuliwahi kua na debate huko nyuma ktkt ya wapendwa kama JK alikua kweli changuo la Mungu kwa kipindi kile cha kwanza kama watumishi waliosemaga ivyo walikosea ua vipi, kupitia dada huyu ambaye tuliendelea kuishi nae kanisani kwa miaka kadhaa, ni kweli MUNGU alimchagua JK but kama mwandamu, hua wanaachiwa na Mungu kutumia will yao kumfuata Mungu kabisa au kutomfuata, Mungu halazimishi mtu, siku zilivyoendelea kama mtu wa kawaida tu hasiye na Mungu au hasiyemshika Mungu halisi kwa moyo wake wote ili Mungu aliyemuita atende aliyokusudia kwake na kwa Taifa lake, alijichanganya mwenyewe, mara mungu bagamoyo mara Mungu mbinguni, mnajua nasema nini hapa, na hakuna rais aliyewahi kuombewa from day one mpaka anaingia ikilu kama JK. Todate hofu ya Mungu anayo kidogo kama Sauli mteule wa Bwana alayeanza vema na Mungu , madaraka yakamlewesha na kujitenga na Mungu polepole na kutotenda haki…imagine from interior God uses such very local mpendwa…so why mnatetemeka saaaana about TBJ tena from Nigeria! Hahahaha! cheers
  Mfano mwingine ni wa askofu mstafu Emmanuel Lazaro, mnaofuatilia issue za kipentecost nchini mnamjua this one of the long time Tz man of God ambaye 1989 akiwa anaomba chumbani kwakwe, KIUMBE cha mwadamu(siyo picha ukutanai…ni kiumbe skeleton ya mtu kilimtokea na kikawa kinatembea chumbani kwakwe, akaona ni kitu kibaya na akakikema..wala hakikumtii..Mwishowe akakaa aone mwisho wa maono yale ni nini….kisha sauti ikasikika…. KAMA TANZANIA HAITAACHA MAOVU YAKE HAKIKA HAITAPONA. KILE ULICHOKIONA KTK CHUMBA CHAKO CHAKUOMBEA NI MAUTI YATANZANIA. TANZANIA HAITAPONA WALA BURUNDI na RWANDA NAYO. Ilipofika 1992, manajua yalitokea Burundi na Rwanda, sisi tupo ktk grace period sijui…in case tukiacha, tutapona.Therefore, we have very powerful manabii from village to town/cities, from normal wapendwa to leaders, so why do I need to concentrate to TBJ? Ningeweza toa shuuda hata mia za wapendwa kanisani kwangu na nje ya kanisa kwangu, manabii wa kweli walio ktk basics za kipentekoste na kibiblia ktk kuishi na kufanya huduma zao na sisi mambo ya allah kama faith statement na damu ya YESU kuoga na kuuza mafuta ya ‘upako’, nonsense kabisa! Unashangaeje mimi kusita kwa habari ya huduma hii ya TBJ Mr. John na my mate milambo sec school best yangu Milinga? Sababu zipi za kikristo za kumkataa zaidi ya hizo?
  Kipengere kingine ni hili kuwa Yule ambaye hasikii wala kuona habari za T.B Joshua atakosa kile ambacho Wanaoona WANAKIPATA. Lakini pia naomba nikuulize ndugu Seleli Hivi Watu ambao SIYO WASHIRIKA WA KANISANI HAPO ULIPO, WANAKOSA NINI KWA KUTOKUPATA MAHUBIRI YA MCHUNGAJI WAKO? Ukiweza kujibu swali hili, BASI hilo ndilo jibu pia kwa wale ambao wanakosa kuzipata habari za T.B Joshua.
  Response: Kwa msingi wa hoja nilizozieleza juu hapo, hukuna cha msingi anachokosa kwa hasiyeona, kufuatilia, kushabikia na kua mfuasi wa TBJ ikiwa kanisani kwakwe, huduma yake, mchungaji, mtume na nabii wake atakua na haya yafuatayo ambayo yako kanisani kwangu na kwa wachungaji wangu na makanisa na huduma nyigine ninazozifahamu kwa hakika na kwa miaka na udhibitisho mwingi na wa muda mrefu kwa maisha.Baadhi tu ya mambo hayo yaliyoyomo kanisani kwangu na kwa wachungaji wangu ambayo John umeniuliza na ambayo hata niisipofuatilia TBJ sina nalopoteza ni haya:
  • Kanisa linaendeshwa kama taasisi na si mali ya mtu au familia ivyo vipo vyomba vya kuadibisha na kuelekeza toka ngazi ya chini mpaka juu
  • Wako wakaguzi na wasimamizi wa mapato na matumizi ya kanisani wa ndani kanisa la mahali pamoja na kanisa kitaifa ivyo nidhamu ya mali na maamuzi ya kutumia kipatikanacho hayaachwi yote kwa mtu mmoja anayeweza kua mwehu anytime au mwizi au mtu wa tabia ya mwilini na kufuja mali na mapato ya kanisa ndio maana makanisa ya aina yetu, huwezi kuta eti mchungaji na mkewe, mtume na mkwe au nabii na mkwe wananua ndege au hammer ya mil 600 wakati vipao mbele viko vingi. Tukinunua Jet au meli au gari hammer kwa mtumishi ni sawa but after serious vipao mbele kiMungu na kikanisa vimefanyika kwanza. Hata ivyo wachungaji wangu walivyoiva ki Mungu, wasivyo selfish, hawawezi kukubali kununuliwa such deadly expensive material things, never! huu ubitozi na unyonyaji wa kuswaga sadaka za watu kwa Mungu wao kwa ajili ya mambo ya Mungu ya msingi badala yake kuzitumia kihuni kununua mandege, magari ya kutisha, ufyatu huu huukuti kwetu labda kwa private project run churches/ministries kama za manabii wenu!
  • Kanisa lina faith statements, all summarized in one phrase -UTAKATIFU NA UMISHENI, hii haina ukakasi kwakua inaendendana na kusudi la sisi kuokoka na kuendelea kuishi hapa duniani
  • Vikao huutishwa kwa muda ukiopangwa na mara kwa ghafla ikitokea huitaji kama vile kuna mtumishi aliyetamka au kwenda kinyume na Neno na pia desturi sahihi za makanisa na imani ya kipentekoste kama mambo ya kihuni kama kuuza mafuta ya upako ua kutoa toa unabii kama vile kunywa chai, kupitia vikao ivyo vinadhibitiwa kwa utaratibu wa maongozi ya Kibiblia, kihekima ya kitumishi kupitia uongozi uliopo madarakani au wazee wa imani waliotangulia ktk imani na utumishi nchini na kimataifa.
  • Kuna nafasi kubwa ya watumishi wengine wa nje ya kanisa na ndani ya kanisa kuhudumu madhabahuni ili kufaidia karama na vipawa tofauti tofati Mungu alivyoweka ndani ya Watu wake kwa kua kamwe hakuna mwenye vyote na kwaahiyo swala la mtu mmoja tu from jan-dec kua kila kitu ktk yote madhabahuni hakitokei kwakua tunatambua Mungu hutumia watu wote na si lazima mtu mmoja tu
  • Maendeleo ya maisha haya ya watu wenye mahitaji maalumu kanisani kama yatima, walemavu, wajane nk yanatiliwa maanani na yanatatuliwa kwanza ndani kabla ya kukusanya ela zao tuu( sadaka) na kusaidia nje, kutaka sifa na umaarufu wakati ndani mwako watu wanashida kali na frustration nzito na kujuta kwanini walikuja dunuani…mfano siku ya kuwatia moyo wachungaji kanisani kwetu ambapo washirika huja na chochote iwe pesa na vitu na kuviweka madhabahuni ili kuwaambia watumishi kwa matendo kua tunawapenda na kuthamini huduma yao kwetu, mchungaji wetu ameamua vyote vinavyopatikanaga siku iyo ingawa ni haki yake kimadhabahu na kibiblia hasa kwa mtumishi wa kweli wa Mungu kama kuhani wa watu mahali pamoja, hugawanywa kwa wajane wote wa kanisa na hata siku kuu za x-mass, wajane wote hupewa zawadi na kanisa, yatima husomeshwa na walemavu hupewa misaada ya kiutu…..Na mengine mengi, muda haotoshi
  “aongezaye maarifa huongeza masikitiko…au in my own way…the more much know/informed you are…..the more majaribu, mapito an confusion you will have?”
  Sasa ndg Seleli, hivi unamaanisha kuwa SASA TUSITAFUTE TENA KUJIFUNZA HABARI ZA MUNGU? Hatuna haja tena ya kuendelea kuhudhuria semina kwa kuwa the more we know/we are informed the mora majaribu, mapito and confusion we will have? Mi naona kama ni hivyo basim tuache hata kwenda kanisani. Maadam mtu ameshaokoka, hana haja tena ya KUENDELEA KUJIFUNZA maana akishajua ZAIDI atakuwa anakaribisha ajaribu zaidi? Kama ni hivyo Basi wale watu wa Beroya, kwa KUYACHUNGUZA MAANDIKO walikuwa wanajitafutia MATATIZO. Tutawezaje kuzijaribu kila roho kama hatuwezi kujifunza zaidi habari ya Neno la Mungu? Tutajuaje roho zidanganyazo kama hatuna MAFUNDISHO ndani ya mioyo yetu? Ndugu Seleli, unataka kusema WANAFUNZI WA DARASA LA KWANZA WASIENDELEE KUJIFUNZA MAANA WAKIJUA ZAIDI WATALETEWA MASWALI/MITIHANI MIGUMU ZAIDI? Kwa hiyo unawashauri waendelee kubakia katika Darasa LA KWANZA maana hapo ndipo kuna mitihani RAHISI?
  Namalizia kwa kusema hivi, KUJIFUNZA ni jambo jema. Ni vizuri tukaendelea kujifunza. Ni vizuri tukaendelea kujifunza habari za watumishi wa Mungu wanavyofanya kazi ya Mungu. Ni vizuri tukaendelea kujifunza Neno la Mungu. Biblia inasema kuwa KIILA JARIBU HULINGANA NA IMANIYA MTU lakini pia HERI ASTAHIMILIYE MAJARIBU…..! Majaribu ni kama mitihani. Majaribu ndiyo yanafanya mtu amfahamu Mungu zaidi na zaidi. Huu Ukristo wa BILA MAJARIBU au Ukristo wa KUTAKA MAJARIBU MALAINI MALAINI au MAJARIBU MACHACHE nao ni Ukristo Mpya! Ukristo DUMAVU.Mtu huwezikutokoa UTUKUFU HADI UTUKUTU au NGUVU HADI NGUVU ikiwa huongezi lolote katika maarifa ya Mungu au hupitishwi kwenye MOTO WA MAJARIBU. Ayubu alipata MAJARIBU MAKUBWA kwa kuwa ALIKUWA MCHA MUNGU MZURI. Lakini alipopita alitoka kama DHAHABU. Majaribu Makubwa Yanaleta THAWABU KUBWA!
  Response: Ufafanuzi: niliposema…much know ur…the majaribu come, I meant not majaribu uliyosema ambayo ofcoz kwa mtu anayejua Neno hawezi kujenga hoja ya kuishi kwa kukwepa majaribu yatokayo kwa Mungu(tests and trials) kwa kua hii ni portion ya wateule. However, Biblia inatuhimiza kujiepusha na mambo yatutiayo unajisi kwa haraka, au dhambi zituzingazo kwa upesi au majaribu yatokayo na yenye nia ya kumfaidisha devo( tempatations), Ni kweli kjifunza na kutafuta maarifa na elimu ni jambo jema sana, imeandikwa Mshike/kupata sana Elimu- maarifa, ufahamu, kujifunza, ujuzi, kupata habari nk- (Mit 4:13)…… nevertheless, Mungu siku zote huweka self control meachnism au kabalansi katika mambo yahusuyo yale yale aliyoagiza ndio maana ktk (2Tim 4:3-4)…amesema tujiepushe na kujitafutia waalimu wengi, masikia ya utafiti, watu wanaopelekwa huku na kule kwa kila upepo uvumao. Mwamini akijikuta ktk hali hii ndio nimeeita confusion au majaribu kwa maana ya yatokanayo na u-much know na kusaka kila elimu na kujifunza kwa yeyeto na mambo yeyote kwa kisingizio cha kupata maarifa. Mambo yote natuyatende kwa hekima na kuangalia kama yanaleta tija ktk maish yetu ya kiroho. Ni sawa na wapendwa waliookoka miaka ya juzi juzi kidogo waliibuka wengi wenye shuhuda za walipokua kuzimu na shetani na wengine wakajitoa ktk kusaka elimu kwa kusoma aina za majini na kazi zake zote na uchawi na aina ya uchawi… huu ni wehu pia upotofu wa vipao mbele tunavyopaswa kukazania kuvitenda kama wana wa Mungu wenye muda mchache duniani hapa, tuzitende kazi zake, tukiokoa muda kuliko kupoteza kwa kusoma na kusaka elimu juu ya majini, nguvu za giza, manabii mbalimbali duniani na kazi au huduma zao
  Lakini la msingi hapa ni kuwa KAMA TUNAMKATAA T.B JOSHUA tumkatae kwa Sababu za Kikristo na kwa wakati Huo huo TUNAPOKUBALI WENGINE nao tuwakubali kwa Sababu za Kikristo pia na wala SI sababu ambazo ukizichunguza hazileti MAANA YOYOTE, Kikristo wala Kimwili.
  Response: Sababu nilizozitaja hapo juu na Neno la Mungu linalothibitisha Mungu nae anasemaje mbali na ufahamu wangu tu, zinatosha kuonyesha sababu za Kikristo za kusita kukubali huduma hii yenye ukakasi mwingi kwa watu wenye uzoefu na ufahamu wa jinsi imani ya kipentekoste ktk Tanzania, Afrika na ulimwengu kwa ujumla zilivyokumbwa na kuvamiwa na mambo mengi yasiyo na tija na yanayotoa picha ngumu sana kwa wanadamu huko nje wenye uwezo wa kungalia mambo na kuchambua nidhamu zetu kama watu wa Mungu wanaotegemewa kua ni wanamna fulani but ukweli tunakua tofauti na kukatisha tamaa. Kama mtu mwenye Roho wa Mungu kama John Paul alivyoshindwa kuona ukweli na akasema akijibu maswali yangu kwa mara ya kwanza kua ukichungaza sana mambo niliyosema yaliyopita kua HAYANA MAANA YOTOTE kikristo na kimwili ni wazi unaweza kuona mtu alieyeookoka na kuanza na misingi mizuri ya huko nyuma lakini akaishia kukamatwa na wimbi la aina ya upentekoste wa kileo wenye porojo za kibinadamu kibao, A man made Christianity vs. Biblical made christianity
  Dawa ya kusaidia aina ya hawa wapendwa walikua ktk basics vizuri sana but wakatekwa na move ya negative side ya power of globalization and televised Pentecost World, ni Mungu mwenyewe maana aina hii ya wapendwa pia ni wagumu kushaurika. Sishangai kwakua kama wakristo wenye basics za kipentecoste kama Milinga na John Paul wanaweza kuwa twisted na moves za kileo, vipi kwa wanaookoka leo na wasio na references za original Pentecost faith way of life tulioshi na kujua vitu halisi na mbembwe ni zipi? Kwaiyo ktk mjadala huu kwa wale waliookoka wakati wa move hizi za watumishi wa kileo, kweli siwashangai kwakua lazima mtajenga hoja as per todays’ all knowledge u have…..the todays dot com petecost faith but kwa wakongwe kama Milinga na I think John Paul nao wakibehave hivi badala ya kuplay role ya kutoa guidance ya kiutu uzima kiroho na KiMungu, then we are finished! Ops! Sorry, I mean..You are finished…you guys not me!

  Conclusion: Dondoo zifuatazo zinaweza kumsaidi mtu yeyote humu atayetaka kusaidiwa kujilinda na kupambanua mambo kabla ya kuachilia moyo, nafsi, roho, akili na mwili wako ktk imani za kileo za kipentecost na aina ya watumishi tulionao: Watumishi wa kileo
  • Wengine hua kweli wameitwa na Mungu original na wanahuduma ya Mungu kweli na wakaanza vema kweli but utoto,ujana, uanadamu, nguvu ya mapato, umaarufu ukatawala sana huduma zao na wakajikuta kwa kujua au kutojua wamesererekea mbali ingawa watabaki kama vile wana basics za kipentecost. Na kusererekea huku pia huchangiwa na kiburi na mafanikio wayapatayo haraka ivyo kutoonyeka na mtu yeyote hata kaka, dada na baba zao waliowatungaulia kiimani na kiihuduma, ningeweza kutaja majina ya watumishi hapa Tanzania kwa majina ambao I KNOW KWA HAKIKA WALIITWA NA WALIOKOKAGA( lakini nachelea haitakua hekima njema sana hasa kwa points hizi za conclusion nazomalizia) but ujana, utoto-utoto wa kihuduma,ulevi na kiburi cha uzima, pesa, mafanikio yamewatwist na they are no longer watu wale nilio/tulio wajua kwa hakika ktk huduma tulizowahi fanya kwa muda. Habari njema ni kua, wa kundi hili hubaki na wokovu na Mungu wa kweli but si ktk conduct ya kipentekoste inayokubalika

  • Wengine ni kama hao wa group ya kwanza but huenda mbali zaidi wakaacha imani safi na kutumia nguvu ya pepo, uchawi na giza, Hapa pia ningeweza taja mtumishi mmoja ambaye anavuma sana Dar but alikutana na mtu mmoja kwa gwiji mmoja wa uganga wa kuvuta watu na nguvu za kuponesha magojwa kwa njia ya majini,huyo mtu aliyekutana na mtumishi huyo, ni rafiki wa mchungaji wetu msaidizi aliyetushuudia hicho kituko pia yuko rafiki yangu anayemjua mganga mwingine ambaye mpendwa huyu huendaga…namuongelea moja ya watumishi vijana Dar wanaovuma sana…..but tafadhari sijataja jina jamani but ni kijana au kijana mtu mzima kidogo…..btn 35-44 years I think.

  • Wengine ni kama wa group ya kwanza…..huanza na maduduuuu, ukakasiiiiii na mbwembweee but kwa neema ya Mungu na kwakubali kukemewa na kukosolewa, hujirudi, ua-djust mambo mengi na kukua ktk huduma na hatimaye kua watu wa uhakika wenye kuishi na kuendesha huduma zao ktk basics za kipentekoste….hapa nataja kwa mfano bila jina la mtumishi mmoja maeneo ya Dar wilaya ya Kinondoni ambaye toka anaanza huduma yake miaka ya tisini na kitu….. alikua na vituko na madudu mengi but siku izi ni mtu mzima sana ktk hudma na amekuja na kukaa ktk level

  USHAURI KWA WANA TBJ: Give it time, may be TBJ ni pure na atajirekebishika later au ni bomu kabisa, wakati mnaendelea kubuy time, concentrate na makanisa yenu na mchungaji wenu, chapeni kazi ya injili hapo kwenu na Bwana atawabariki, leave TBJ alone! Afterall, hawaitaji kiviiiiiile, ni mahangaiko na pressure zenu tu na sijui kua anajua mnaexist this part of the World! Hahahah, mnakazi watumishi nyie, kaaaaazi kwelikweli.
  TUFANYEJE? Very simple! Vitu viwili kwa hakika vinasaidia na kamwe ni ngumu kutekwa
  • Matayo7:15-16: Kuwatambua kwa matunda yao! Angalia neno Matunda- linawakilisha hints zifuatazo:
  i. Muda umepita mpaka tunda litokee maana tunda haliwezi kutokea kwa muda mfupi, therefore msiwapapatikie, ngojeni, buy time, acheni tu, endeleeni kanisani kwenu kwa uaminifu, yawengine yapeni muda au achana nayo kabisa
  ii. Tunda ni kitu dhahiri shahiri- litaonekana tu, hamna ufunuo hapo
  iii. Tunda ni kitu cha kuliwa na wanadamu, au ndege, mengine huliwa na wanyama, wadudu na kwakua kuonja ni moja ya vitambuzi, kama tunda lina ukakasi au bichi au ni tunda jipya au pori hujaelezwa taarifa zake na kujua au kudhibitisha kwa hakika, kwanini kulila? Why don’t u consume matunda kibao kanisani kwako unayoyajua kwa hakika na ni matamu, unless kama hayapo, go and look for them outside though be carefull when looking for matunda outside, utaconsume poisonous fruits au ni yale no poison but ni yale matunda yakiingia kwa stomach, hayawi-digested na inabidi kumtapisha mtu kitu amabacho ni shughuli nyingine!
  • Yohana 10:1-5: Kondoo wake huisikia sauti yake…wanaijua sauti yake…..hawatamfuata mgeni, watamkimbia kwa kua hawazijui sauti za wageni, angalia neno “kusikia sauti”… kondoo wako so smart mpaka wanajua sauti haswa ya mchungaji wao! Wow! this is so sweet, isn’t it?….hint hapa ni kua jamani Mungu wetu kupitia YESU na Roho Mt huongeaga, huzungumza nasi, husemaga, hutunong’oneza, hutuambiaga, therefore, kama moyoni mwako humeshambiwa kua TB Joshua ni ktk group gani mfano kwa yale niliyoeleza fine, but with me, am sorry, network zote ndani zimezima, zimegoma na kwakua Bwana husemaga nami kwa mambo mengi na kwa namna nyingi, I will wait. However, ni sahihi vilevile kusita kumkubali mtu na huduma yake hata kama anafufua wafu na kutabiri mpaka kujua ya miaka mia ijayo ikiwa hata kwa vigezo vingine vya kawaida tu mbali na kutumia hivi viwili deep, unaona ukakasi zaidi than utamu kuhusu BAADHI ya mambo(siyo yote ofcoz) ayafanyayo kaka huyu TBJ na wengine wa dizaini hii West Africa, Tz, Kenya, Uganda,Congo na USA.

  Amani ya Mungu wetu iwe nanyi wote

 16. Nabii TB Joshua,ni Nabii feki tena hana tofauti na Pweza aliyekuwa anatabiri mchezo wa soka…! Huyu ni mbashiri tu hana Unabii wa Mungu aliye HAI.Tumeshuhudia utabiri wake katka maswala ambayo hayanatija katika wokovu wa mwanadamu,inakuwaje naye anatabiri mchezo wa soka wa timu za ulaya kama Pweza? Msipende kuamini kila Roho zilitalo jina la YESU KRISTO,lazima tuzipime kwenye mizani (Biblia).Kila asoma na afahamu neno hili.

 17. Ndg Lwembe napitia lile bandiko lako la Thursday, July 5, 2012 at 9:50 am
  Uliandika…
  “Kati ya sababu ulizozitoa za mimi kutokumkubali nabii Joshua, zikiwemo ile ya kutokuamini kuwepo kwa Mungu Baba, Mungu Mwana na Mungu Roho Mt”

  Lwembe, Lile bandiko langu sijaandika kama wewe ulivyoniwekea maandishi haya kwenye vidole vyangu kuwa nimeandika’Mungu Baba,Mungu Mwana,Mungu Roho Mt’
  .Hii ni aina ya nguli wa Media Fulani anayejitahidi kupoka hoja kwa werevu(hila) na kuingiza hoja za kwake ktk mjadala,Biblia nayo haijaandikwa hivyo,biblia imeandika hivi, Math 28:19“Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;”soma KJV yako kama wameandika hivyo,

  Math28:19 haijaandikwa mkiwabatiza kwa Jina la Mungu Baba,Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu Na kama kuna watu wanaandika hivyo kwa kutojua maana au hawajui kutafsiri Kiswahili vizuri,Unapotumia udhaifu wa maandishi au tafsiri ya kiswahili ya watu hao ambao wanaandika hivyo kuwa ndio hoja zako sio sawa.Ni aina mashindano na bila Tashwishwi hapo umeshinda.

  Ndugu yangu Millinga funguka, Mtu akitafuta kosa katika maandishi yako na anatumia hayo makosa kwenye maandishi yake wala si hoja uliyowakilisha lazima uwe makini na kiroho chako, ni jaribu lazima ulishinde.

  Asante

  Mjoli Haule

 18. Shalom

  Roho Mtakatifu ambaye ndio Nabii aliyefunua ufunuo wa UTATU,nami ninaweka maandiko yanayosimamia huo unabii.
  UTATU ni ufunuo na si maandiko,UFUNUO unafunuliwa na maandiko siyo hadithi
  Agano la Kale
  Naye BWANA alinena kwa Roho Mtakatifu kwa kinywa cha Daudi, mtumishi wake,

  Zab110,Zab45 msome Mtumishi wa Bwana Daudi akiwa ktk Roho
  Zab 110:1Neno la BWANA kwa Bwana wangu, Uketi mkono wangu wa kuume, Hata niwafanyapo adui zako Kuwa chini ya miguu yako.

  MITUME
  Mdo2:33Basi YEYE, akiisha kupandishwa hata mkono wa kuume wa Mungu, na kupokea kwa BABA ile ahadi ya ROHO MTAKATIFU, amekimwaga kitu hiki mnachokiona sasa na kukisikia.

  Filipi2:6,9,10,11 ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya MUNGU, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho; Kwa hiyo tena (Mungu alimwadhimisha mno), akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina; ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba.
  Mdo2: 34,36Kwa kuwa Daudi hakupaa kwenda mbinguni, lakini anasema, ‘‘ ‘BWANA alimwambia Bwana wangu Kaa wewe upande wangu wa kuume……Mdo.36

  INJILI
  TukiitazamaInjili ya Mathayo inaongelea zaidi juu ya Yesu kama mfalme wa Israel na jinsi alvyoutimiza unabii wa torati na manabii, ndipo unabii wa ufunuo wa UTATU unafunuliwa wazi kwa kinywa cha Bwana Yesu Mwenyewe ktk kitabu hiki tu cha unabii.
  Math 28:19“Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;”

  KUBATIZWA KWA JINA LAKE YESU
  Tunatubu na kubatizwa kwa Jina la Yesu,ni wakati tunanapobadilisha nia zetu(mtazamo)Roho Mtakatifu anakupiga mhuri ya moto(Arabuni ya Roho) Yeye ndiye Mbatizaji,hiyo ndio alama shetani akiiona anajua wewe sio wake maana hata ukifa wakati umeshabadilisha mtazamo wako na hujabatizwa kwa maji unakwenda mbinguni,kwa maana kwa kwa imani tunaaminina kupata HAKI NA KWA KINYWA TUNAKIRI NA KUPATA WOKOVU wewe mwenyewe unamini moyoni kuwa yesu ni Bwana na kukiri kwa kinywa kuwa Mungu alimfufua ktk wafu(Rumi6:3-4kol2:12), hapo umepokea ukristo,wale WAKRISTO watakaobaki dhiki kuu wakati kanisa likinyakuliwa wao wataokolewa kwa imani na ukiri huo tu(Mdo2:20-21),Maana Roho Mtakatifu atakuwa ameondoka na kanisa,wakati huo utatakiwa umkane YESU ukikataa unateswa na kuuawa.kumbe watu wote walimpaYesu maisha yao(tubu) ili awe kwao Bwana na mwokozi na kiongozi/mfalme wa maisha yao wote wamepitia Mdo2:38 kuthibitika mtu amempokea Bwana/amejazwa Roho Mtakatifu,maisha yake yanabadilika anakuwa na maisha ya uungu1kor2:14 ila anaweza baki mototo mchanga1kor3:1kama ambao tunawaona hapa SG,Yeye Aliye pokea wokovu tunda la Roho linachipuka,amani moyoni,furaha,uvumilivu,upole,kiasi,fadhina utu wema.Gal5:22,23
  Maana ya Mdo2;38 tubuni na kubatizwa kwa jina lake Yesu ni hii Mtume Petro anaifunua kwa maandikohaya
  Mdo11:15 Ikawa nilipoanza kunena, Roho Mtakatifu akawashukia kama alivyotushukia sisi mwanzo.
  Mstari16 “Nikalikumbuka neno lile la Bwana, jinsi alivyosema, Yohana alibatiza kwa maji kweli, bali ninyi mtabatizwa kwa Roho Mtakatifu.”
  Hapo hakuna aliyemwagiwa aliyebatizwa kwa Maji, Roho wa Kristo mwenyewe anabatiza na mhuri wa moto linaandikwa Jina la Mwana-Kondoo na Jina la Baba Yake linaandikwa kwenye kipaji cha uso,Ufunuo14;1
  Utafakari sasa Mdo2:38 na yale niliyoandika.
  Mdo2:38Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.
  **Petro anaposema kama vile alivyotushukia sisi mwanzo,alikuwa anamaanisha wamebatizwa bila maji ni kwa Roho Mtakatifu na kwa moto,kumbuka hii sio mara ya kwanza Petro kubatiza Alishabatiza wale 3000 baadaye 5000Mdo2:41;4:4,lakini kwa mataifa imekuwa tofauti ni kama wao walipobatizwa kwa Roho Mtakatifu na Moto bila kumwagiwa maji.Mdo2:1-4
  HII NDIYO PROGRAMU YA WOKOVU.

  KUTIMIZA HAKI YOTE(ubatizo wa maji mengi)
  *Nitaendelea kuandika aina za Mabatizo(ubatizo)kutimiza haki yote,maana ziko nyingi na ufunuo(tafsiri)zake Mungu akipenda.
  Mafunuo ya maandiko mengi nimeyaacha kwakuwa yamesha andikwa kwenye thread uumbaji
  Bwana Awabariki kwa Amani yake
  Mnisamehe kwa maandiko marefu

  Mjoli wako
  Haule

 19. Milinga,

  Kumbe unaendelea kufanya utafiti…! Bado huna majibu…..basi Mungu na Akubariki….Tutasubiri utapofikia tamati na kutupa hitimisho lako…Ndugu yangu Milinga upendo wangu kwa ndugu yeyote anayetofautiana na mimi ni mkubwa mno….hasa ambaye anakiri Yesu ni Bwana na anayemwishia Mungu katika njia ya utakatifu na ku……na kumwabudu katika ROHO NA KWELI…..

  Kutofautiana ndani ya IMANI si kitu kigeni kabisa……Naamini kabisa Paulo alivyosema kwamba KUNA WALIODHAIFU WA IMANI ( ROM 14:1) na WALIO NA NGUVU KATIKA IMANI (ROM 15:1) Paulo vile vile anafundisha kuwa kuna WACHANGA KIROHO…..Hivyo wengine pengine kwa udhaifu na uchanga wetu Nabii Joshua si Nabii wa Bwana…..kwani kwa ufahamu wetu mdogo tumeshindwa kabisa kuona Nabii zake zina msaada gani kwa Kanisa…….Lakini kwa wengine walio na Nguvu katika Imani wao wameweza kuwa na macho ya Kiroho na kuliona hilo……La msingi kuchukuliana udhaifu wetu…….kupendana…….kuombeana.Kumbuka kwamba mimi na LWEMBE pia tuna vingi pia tunavyotofautiana…..kama vile mimi na wewe kuna mengi pia ambayo huko nyuma tumekubaliana KIIMANI…….LAKINI KWA HILI TUMETOFAUTIANA….!

  Ndugu yangu kuhusu jina langu ambalo hujalielewa…..limenistusha kidogo…..mawazo yangu na jina langu au na imani yangu vinauhusiano gani…? Je unawajua hawa maana ya majina yao….? Wana wa Asheri, Imna na Ishva…na wana Beria, Heberi, na Malkieli aliyekuwa babaye Birzaithi……na wana Yetheri, Yefune, na Pispa, na Ara, na wana wa Ula, Ara na Hanieli na Risia…..HAO WOTE NDIO WANA ASHERI…….WATU WETEULE HODARI WA VITA. (1 Nyakati 7:30)…….Kwa kifupi Orbi ni mteule wa Bwana……na nikiamini BWANA ananitia UHODARI WA VITA Kuitetea Imani hii…….naomba unielewe hivyo….UBARIKIWE sana ndugu yangu……Tutakutana kwenye Mada nyingine…….kwangu mimi niliyoyaandika katika Mada hii yanatosha…….

 20. Mpendwa Orbi na CK Lwembe,

  Msinitake nianze kusikitika. Unashindwa kuelewa maana ya sayansi? Umeshindwa kuelewa kwamba Biblia ni maabara ambayo twapaswa kuingia ndani ili kufanya utafiti wa kuthibitisha hoja yoyote?

  Lwembe sasa hapo umenichekesha. Watu wanasomewa andiko moja la , “Yesu akalia machozi” kisha wao wenyewe wakalia machozi kwa zaidi ya masaa 3. Umeshindwa kuelewa kwamba huyo mzee alitoa hoja yenye nguvu iliyowafanya watu wazame ndani kiroho na kueleza hoja nyingi kwa Mungu?

  Maandiko yanasema, “……leteni hoja zenu…..” Mungu anatutaka tumpelekee hoja zetu tena zenye nguvu ili ajibu maombi yetu. Hao uliowatolea mfano walikuwa wameshapata hoja nyingi tokea mkutano wa siku ya kwanza. Aliyesimama siku hiyo alikuja kuongezea hoja za watangulizi wake. Roho Mt. akashuka kuwavuvia watu na kuwazamisha ndani ili wamwage hoja nyingi iwezekanavyo kwa Mungu.

  Huwezi ukaomba zaidi ya saa moja, umepiga magoti au uko chumbani mwako kama huna hoja yoyote kwa Mungu. Ndiyo maana wakristo wengi wanashindwa hata kuomba kwa saa moja kwa sababu hawana HOJA. Unamkuta mtu ana hoja moja tu. Sasa kama una hoja moja tu unawezaje kuomba Mungu kwa dakika 60 au zaidi. Hauna hoja. Una hoja moja au mbili tu. Ndio wakristo wengi wa leo.

  Orbi anataka nimpe hoja za kisayansi kuthibitisha kwamba TB Joshua ni Mtumishi wa kweli au la. Naomba nikukumbushe kwamba hadi sasa, mimi sijatoa msimamo wangu kumhusu TB Joshua kwani ninaendelea kukusanya hoja za kimaandiko na kimazingira kumhusu mtumishi huyu. Hadi sasa sijamaliza kukusanya hoja zangu za kisayansi. Niko kama hatua ya 55% hivi ndipo nitoe hitimisho la utafiti wangu. Mpaka sasa ukisoma maandishi yangu sijawahi kusema Joshua ni Nabii wa kweli au wa uongo. Mimi nimekuwa nikiwataka tu wale wanaompinga watuorodheshee hoja zao wanazosimamia (na ziwe za kisayansi) zinazomweka Joshua nje ya watumishi wa Mungu. Hii nayo ni moja ya kazi za utafiti. Kumbuka , wanafalsafa wanasema, “….No Research No right to speak….”

  Hadi sasa nimeshafuatilia NABII zake zipatazo 35 alizowahi kutoa kuhusu maswala mbalimbali tangua alipoanzisha huduma ya SCOAN. Nimeshakagua “SCOAN Faith Statement” yao ili nione kama wanachokiamini na kukihubiri altereni ni cha Kibiblia ama la. Nimeshafuatilia historia ya maisha yake kabla hajaanza kuhubiri. Nafuatilia miujiza yote inayotendeka pale kanisani kwake na kwenye matawai ya kanisa lake ulimwenguni kote. Nategemea hadi kufikia Februari 2013 nitakuwa nimemaliza kukusanya hoja za kisayansi kumhusu TB Joshua. Ndipo nitatoa hoja zangu za kutoka maabara ya Biblia na kutokana na ushahidi wa kimazingira kumhusu TB Joshua.

  Naomba nihitimishe kwa kuwakumbusha tena nilichowahi kusema awali (rejea posts zangu zote Katika mjadala huu) kwamba ; SIYO KILA UNABII UNAKUJA KWA AJILI YA KUWAFURAHISHA WASIKILIZAJI. AIDHA, SIYO KAZI YA NABII KUKUFANYA WEWE UFURAHIE UNABII WAKE AU UUCHUKIE.

  Hivi akitokea Nabii kama Elisha au Eliya leo hii kweli watu watamkubali? Nabii akija leo akaamuru mvua isinyeshe kwa miezi 36 (3.5years) hapa Tanzania kama alivyofanya Nabii Eliya enzi zile, tutamsemaje? Tutampoea kwamba ni Nabii wa Mungu aliye juu au Nabii wa uongo? Kama akija Nabii kama Elisha aliyeamru watu wapatwe na maafa kwa sababu tu walimzomea kwamba ana upara, leo kweli wewe LWEMBE na ORBI na Mabinza mtamkubali?

  Akitokea Nabii kama Joshua akaamuru Jua lisimame ili vita iendelee kupiganwa vizuri, leo hii nani atamuunga mkono kwamba ni Nabii wa Bwana kanena?

  Leo hii akatokea Nabii kama Petro Mtume alivyowakemea Anania na Safira waliomdanganya Roho Mt. kuhusu kiwanja chao na kiasi cha pesa walichouza uwanja wao, kisha wakafa hapo hapo mbele ya umati wa kanisa lililokuwa likiendelea na ibada ya utoaji, leo kweli akina Lwembe na Orbi watamkubali kwamba huyu ni Nabii wa Mungu?

  Kama unamkataa mtumishi anayetabiri kwamba ndege ya abiria itaanguka na itaua viongozi wa kitaifa kama akina George Saitoti, Nabii anayetabiri kwamba dunia nzima itakumbwa na msukosuko wa kuanguka kwa uchumi, anayetabiri kwamba dunia nzima itakumbwa na migomo na maandamo kila kona, mtu anayetabiri kamba Kenya itavamia na makundi ya Al shababu, mtu anayetabiri kwamba Wakristo na waislam wataingia katika sintofahamu , nk,nk, nk na yote hayo yanatokea, na bado haumkubali kuwa ni mtumishi wa Bwana. Je unazo hoja ngapi za kumkataa?

  Mtumishi ambaye mamia kwa maelfu wanaokolewa kutoka katika vifungo vya giza (mfano wale majambazi 6 waliookoka tarehe 7 Decemba 2009 kwa kutazama TV) na wakajisalimisha kanisani kwake na leo hii wanaendelea na wokovu; mtumishi ambaye ameombea wenye maovu wengi wakaokoka na kuachana na uovu wa UKAHABA (Mfano ni wale wanafunzi 12 wa chuo Kikuu cha Benini =UNIBEN) Waliookoka na kuachana na bishara ya ukahaba waliyokuwa wanafanya ili kupata pesa ya matumizi ya chuo na ada ya chuo, wote wameokoka na kuachana na ukahaba. Na sasa wanaendelea kumtumikia Mungu pale Chuo Kikuu cha Benini kule Togo. Kama mtumishi kama huyu unampinga kwamba siyo mtumishi wa kweli wa Mungu, wewe unatumia hoja gani zenye nguvu kupingana na hii hoja?

  Ama kweli Nabii hana heshima nyumbani kwao. Kama kanisa nilitazamia kwamba tuwe msitari wa mbele kufuatilia unabii wowote unaoletwa kwetu ili tuwe walinzi wa nyumba ya Mungu. Unabii uwe wa kweli au wa uongo siyo kazi ya kanisa kuanza kuukataa na kusema aliyeuleta unabii huo hatumkubali, bali ni juu yetu kuanza kumwomba Mungu aturehemu.

  Ajali ya ndege iliyomuua Saitoti na wenzie, Migomo ya Madaktari na ile ya walimu inayoandaliwa hapa Tanzania ilishatabiriwa na TB Joshua, lakini je, tumeomba Mungu kiasi gani ili kutuepusha na majanga haya?

  Lwembe na Orbi ukisikia Unabii kwamba kuna viongozi wa Tanzania watakufa katika ajali ya ndege wewe unachukua hatua gani kati ya kumwomba Mungu atuepushe nayo na au kuukata unabii huo. Kama ungeeambiwa kwamba MV Bukoba itazama na kuua watu wengi 21 – 05- 1996 wewe unachukua hatua zipi?

  Tukikalia kusema kwamba UNABII anaoutoa TB Joshua ni wa uongo huku anayoyatabiri yakitokea sisi ndio twageuka kuwa wanafiki na waongo. Ama kusema kwamba unabii anaoutoa haulisaidii kanisa kukua au kubarikiwa na kwa hoja hiyo unamweka kuwa siyo mtumishi wa Mungu kwa sababu ya aina za Unabii na miujiza anayotenda naona kwamba ndiyo roho ya ukengeufu zaidi.

  Mimi naendelea kufanya utafiti ili kukusanya hoja za kisayansi kumhusu huyu Bwana Temitope Balogun Joshua (T.B. Joshua) wa Nigeria aliyezaliwa tarehe 12 Juni 1963 katika kijiji cha Arigidi.

  Nawapenda wapendwa wote wanaotofautiana nami kimitazamo hasa CK Lwembe na Orbi na Mabinza LS. Ingawa hivyo vifupisho vya majina yenu sijavielewa. Aidha, nawapenda wote wanaounga mkono mitizamo yangu katika mada hii.

  Stay blessed and stay tuned with SG.

 21. Mpendwa Lwembe,
  Ni kweli kabisa simkubali huyo nabii Roho mtakatifu Yule ajaye ambaye nabii/kuhani/mtume/mhubiri/askofu wake wana kiburi cha kuongeza maandiko kwenye Biblia kuwa kwenye bustani ya kulikuwa na miti 4 na siyo 2 Mw2:9 angalia URL
  https://strictlygospel.wordpress.com/2012/04/26/ni-mti-upi-hawa-alitwaa-tunda/
  Mtumishi wake anayefundisha kuwa shetani(Lucifer) na Mola(Mungu) walishirikiana kwenye uumbaji
  https://strictlygospel.wordpress.com/2012/07/02/wakati-wa-uumbaji-lusifa-alihusika-vipi/
  Mtumwa wake anafundisha kuwa kulikuwa na pentekoste 2,moja wakati wa babeli na nyingine wakati wa kanisa la kwanza
  https://strictlygospel.wordpress.com/2012/03/05/ni-lazima-kuzungumza-kwa-lugha-mpya/
  ukiangalia hizo URL na Lugha za kuwashambulia watumishi wa Mungu na kuwaweka kundi moja na Mzee ambilikile wa samunge,Sam kumtaka John aende kwa mchungaji wake,kuwashambulia tunao amini ufunuo wa UTATU kwa maneno ya dharau nk, ilipelekea lile bandiko ndipo nikaandika..
  “Sawa tunasubiri siku ufunuo ukifunuliwa hapa tukamjua huyo nabii Roho mtakatifu na kanisa la Roho mtakatifu mnayetaka tumfuate maana siku ipo tena yaja”.“Hebu tujadili kama watu waliopokea Roho Mtakatifu,yaani ile kweli,tukitumia maandiko mtu anayetusoma hapa ambaye hajampa maisha yake Bwana Yesu apendezwe nasi na kufanya hivyo’
  hakika namkataa nabii Roho mtakatifu Yule AJAYE ambaye anafanya watumishi wake wadhani wao ni wakuu wa wajenzi wakijenga msingi mwingine usio ule alioweka Yesu kwa mafunuo yanayokosa ushahidi wa maandiko ya kusimamia isipokuwa kwa kupeleleza biblia.huyo sio Roho Mtakatifu ambaye ndio ule ufalme wa Mungu ulio ndani yangu LK17:20-22
  Na alipoulizwa na Mafarisayo, Ufalme wa Mungu utakuja lini? Aliwajibu akawaambia, ufalme wa Mungu hauji kwa kuuchunguza;
  wala hawatasema, Tazama, upo huku, au, kule, kwa maana, tazama, ufalme wa Mungu umo ndani yenu.
  Kama huyo nabii Roho mkatifu AJAYE Ndio mmoja wa wale Wana wawili wa mafuta(mizaituni ili miwili) Eliya ajaye sisi(kanisa) hatuhusu ni ufunuo wa yajao, kanisa litakuwa limesha chukuliwa,Mwana Kondoo kwa ile damu yake atakuwa ameshavunja lakiri ya kitabu na Kumnunulia Mungu watu toka kila taifa,kabila,lugha na jamaa hao ndio kanisa (ukuhani wa kifalme).nilisha kupinga hapa kwa maandiko kwene thread ya Manabii kuwa unapotosha kanisa la Bwana.
  Mpendwa Lwembe nisipopinga hii injili yenu BWANA atainua mtumishi kupinga nikikumbuka Esta4:14 Kwa maana wewe ukinyamaza kabisa wakati huu, ndipo kutakapowatokea Wayahudi msaada na wokovu kwa njia nyingine; ila wewe utaangamia pamoja na mlango wote wa baba yako; walakini ni nani ajuaye kama wewe hukuujia ufalme kwa ajili ya wakati kama huo?

 22. Bwana Hoja Nyingi Milinga,

  Kwa kuhitaji kwako ‘hoja nyingi’ ndio ufunguke umenikumbusha siku nilipouona UPENDO wa Mungu ulivyo Mkuu.

  Kulikuwa na mkutano wa Injili wa ndani. Kulikuwa na wahubiri yapata watano katika hizo siku 5 za mkutano. Katika hizo siku 4 za mwanzo zilikuwa na baraka za kila aina, pamoja na wagonjwa wengi waliombewa na kupona maradhi yao na ulemavu wao. Kadiri ya siku zilivyosogea, watu pia waliongezeka wakiwaleta wagonjwa wao na wenye shida. Ikifikia kuwaita wanaompokea Bwana, madhabahu ilijaa watu katika siku zote kwani mahubiri yaliyokuwa yakitolewa yalikuwa na Hoja Nyingi  zenye Nguvu, tofauti tofauti ambazo zilitusogeza sana uweponi na kuamsha kiu ya kumjua Bwana. 

  Katika siku ya mwisho ya mkutano, tukaona amepanda mimbarani mzee mwenye umri yapata miaka 85 au zaidi, kila mmoja wetu akajua kuwa labda alikuwa amepanda kutoa ushuhuda. Lakini yeye akatuambia kuwa ndiye atakayetulisha siku hiyo! Tulifadhaika kidogo maana tuliwategemea wahubiri machachari wenye Hoja Nyingi zenye Nguvu, kila mtu akashusha pumzi na kipiga moyo konde.

  Baada ya sala fupi, akatuomba tufungue Biblia zetu ili tupate kusoma kutoka humo Neno la Mungu, kwani akasema, “Mimi na ninyi twaweza kukosea, lakini Mungu hakosei, basi Neno lake pekee ndilo liwezalo kutuangazia katika Njia yake tunayopaswa kupita. Yoh 11:35 ‘Yesu akalia machozi’ basi akauchukua umati wote uliokuwa pale akaupeleka msibani, kwa takriban masaa matatu, kila mmoja wetu akijililia nafsi yake, tukaona vile tulivyotembea katika njia pana ya Miujiza na Hoja Nyingi zenye Nguvu siku zote na sasa tunaishia Mwilini! Siku hiyo ya mwisho ya mkutano, akili zetu tukizitupilia mbali, hukukuwa na alter call wala maombezi ya wagonjwa, dhambi ilitimuliwa mbali, wagonjwa waliinuka wenyewe, vilema wakapona, watu wa dini wakizitupilia mbali Hoja zao, tulipotoka hapo, kila mmoja wetu akawa kama wale wanafunzi waliokuja kutoka Emausi baada ya kufunguliwa macho yao!! Hiyo ndio Nguvu ya Neno la Mungu!

  Ktk mchango wako wa mwisho umetumia maneno 404 kuzungumzia “Hoja zenye Nguvu” na haujaleta hata hoja moja!  

  Sisi ni ndugu zako katika Kristo, kwa hiyo USITUZINGUE!!

  Nipe jibu linaloweza kunielekeza ktk Biblia mahali ilpoandikwa hiyo Statement of Faith ya SCOAN; kama haiko mahali popote na mnaitoa kichwani au ni Mafunuo, tuambie tu!!

  Ubarikiwe

 23. Milinga,

  Hoja zako zenye nguvu ni zipi? Wewe mwenyewe hujatuletea hizo hoja ambazo ni “researched facts and doctrinal analysed logical thruth” Kuhusu huyu Nabii anayetabiri vifo, mpira wa miguu na upuuzi mwingi tu toka Mimbarini na kuwavuta Wakristo ambayo hawajajikita katika Maandiko na kuwafanya wamfuate kama mpinga filimbi wa Hamelin……..!
  Kanisa la leo na Waumini wengi wamepinga kambi kwenye miujiza tu…! Na wamekwama hapo hapo tu….! Ufahamu wa Neno la Mungu umekwama katika kuona Pepo zikitoka na katika Miujiza pasipo kuungalia Utendaji wa Mungu kwa upana wake…..Ndugu yangu Milinga unatoa picha ya wengi wa waumini wa leo waliopiga kambi kwenye miujiza na kukwama hapo hapo …..au kukumbwa na wahubiri waliotengenezwa na media…..na wala sio Roho Mtakatifu…….!
  Naona unataka tuhame kwenye Biblia na tuuingia Maabara…..! Je tutaweza kweli….?

  Mungu akubariki…nangojea hoja zako za Kisayansi ili kumuinua Nabii huyu…….ambaye taifa lake linaongoza dunia kwa utapeli wa Kimataifa…..ambao nadhani Nabii huyu kashindwa kabisa kutoa dawa yake…..isipokuwa tiba ya kujitumbukiza katika bwawa la maji….na kudai ni damu ya Yesu itakasayo…..Kweli Bwana na aturehemu…..

 24. Milinga,

  Hebu tupe hoja ya kisayansi kwamba Nabii Joshua ni nabii wa Kweli, Hebu weka Biblia yako kando ili tuone sayansi itakavyotuthibitishia kuwa Joshua ni Nabii Kweli….? Hivi ndugu yangu Kufa kwa Saitoti kweli kunalihusu Kanisa…?

 25. Wapendwa Orbi na Lwembe, enyi watumishi wa Mungu aliye Hai Juu?

  Nimeshindwa kuelewa maoni na michango yenu katika mjadala huu kwani sijaona hata mmoja wenu anayenieleza HOJA ZENYE NGUVU, Bali wote naona mna MANENO mengi kama siyo POROJO nyingi zenye nguvu.

  Kwa mfano; soma maoni ya Orbi hapo juu aliyotoa Julai 4, 2012 saa Saba na Dak. 9. Utagundua kwamba ametumia maneno 387 lakini ameongelea HOJA 3 tu ingawa nazo pia haziendani na ukweli yaani ziko nje ya mktadha.

  Unawezaje kutumia maneno 387, aya 9 na mistari 29 lakini unatoa hoja 3 tu. Hivi unaategemea utawaokoa waliokengeuka kwa roho ya ukengeufu unayoisema bila kufafanua kwa usahihi. Hoja zako tatu mimi nilizoziona ni hizi hapa:
  1. Roho ya Ukengeufu kwamba ndiyo aliyonayo TB Joshua
  2. Ni nabii anayetumia miujiza na ishara ili yamkini awapoteze hata wateule wa Mungu, kwamba “…….BASI SI NENO KUBWA WATUMISHI WAKE NAO WAKAJIGEUZA WAWE MFANO WA WATUMISHI WA HAKI….2 COR:11:13-14″

  3. Utoto wa kiroho ndio unaosumbua wengi kama Orbi ulivyosumbuliwa kwa kuamini kwamba kila anayetembea na Bibila, au kunena kwa lugha, au kujiita kanisa la kiroho basi huyo ni mtu wa Bwana na kwamba baadaye ukagunduaa kinyume chake.

  Ukichunguza hoja hizo za Orbi utagundua kwamba ni hoja dhaifu yaani hazikidhi viwango vya mtu anayeelewa maandiko na kuelewa kuyafafanua kwa watu wachaanga kiroho na wakubwa kiroho kama alivyokwisha kukua kiroho yeye tofauti na sisi watoto wachanga kiroho.

  Hata ukichunguza maandishi ya mpendwa CK Lwembe utagunduaa hali kama hiyo hiyo. Angalia kwa mfano anapomjibu John Haule tarehe 4 Julai 2012 saa 7.16 Mch.

  Lwembe katumia maneno mengi zaidi ya 663 wakati alikuwa anatoa hoja kama 4 tu kumjibu Haule.Hoja zenyewe ni: 1. Utatu wa Mungu, 2. Ubatizo wa Maji, 3. Roho Mt. ndiye Nabii pekee aliyetaabiriwa, 4. Miujiza siyo tamati ya Injili.

  Wakati mimi nasisitiza hoja za kisayansi wapendwa hawakunielewa. Wao wanadhani namaanisha sayansi ya kawaida wanashindwa kuelewa kwamba NENO LA MUNGU ndilo sayansi kuu zaidi ya sayansi zote. Ninaposema kwamba watu walete hoja zilizofanyiwa utafiti wameshindwa kunielewa kwamba namaanisha HOJA ZINAZOCHAMBUA KWA UNDANI ZAIDI BILA KUPENDELEA UPANDE WOWOTE WA USHABIKI. Hii ndiyo maana ya …Researched and well analysed doctrinal logical truths….”

  Hii inanipa pichaa kwamba wapendwa wengi hawafanyi utafiti wakijifanya kwamba wameshaliielwa Biblia sana na wala hawana haja ya kufanya utafiti wowote zaidi. Na kwamba wakishanukuu maandiko wanayoyajua basi inatosha.

  Namalizia kwa kusema kwamba kama huna HOJA NYINGI za kukubali au kukataa jambo ni bora ukaacha kuchangia mjadala kwa kutumia maneno mengi.

 26. Ndugu Milinga,

  Hivi mambo ya Rohoni yanagundulika kwa kutumia “Researched facts and doctrinal analysed logical truths” ? Kama hivyo basi mbona NASA wangeisha mgundua Mungu wake na WOKOVU WAKE……!Mbona Yesu hakutuambia tutumie ” Researched facts and doctrinal analysed logical truth” kutambua Manabii wa uongo?
  Ndugu yangu umesahau kabisa hata mafundisho ya msingi ya Paulo kwamba “Mungu haikuifanya hekima ya dunia kuwa ni upumbavu” na Paulo anasema wazi “MUNGU ALIPENDA KUWAKOA WAAMINIO KWA KWA UPUZI WA LILE LINALOHUBIRIWA…” Sasa kweli unatujia na researched facts and doctrinal analysed logical thruth…katika kumtambua Nabii Joshua!…..What facts…..? Kama sio huo upuuzi wa Nabii zake ambazo haziko sambamba na Maandiko…..? What doctrinal truth unazotaka zitumike kama sio kweli ya Maneno ya Yesu aliyotuonya na Manabii wa Uongo….?
  Tunapopiga Kelele na kuonya kuhusu Nabii Joshua tunasimama katika Maneno ya Mungu tu…..Na wewe ndugu yangu unapopiga Tarumbeta kuhusu huyu Nabii basi simama katika Maneno ya Yesu….sio researched facts….ambazo tayari zitakua biased……..na wala sio doctrinal truth…ambazo zinaweza kuwa formulated na hekima ya mwanadamu tu…….

 27. Ndg Orbi, 
  Neno huonya na kurejesha kwa wenye utayari. Lakini Biblia hiyo hiyo inatufundisha kwamba wako watakaodanganywa. Ni watu wazuri, wanabidii kubwa sana. Wanasaidia jamii, wanajitoa katika mambo mengi. Basi ndugu yangu Maandiko yanapotimia huwa hazigongwi kengele, nukuu hizo hizo ulizoziweka mmoja zitamfungua na kwa mwingine ni ujinga. Kama ilivyokuwa kwa Yusuf kule gerezani alikofungwa, mmoja aliachiliwa na mwingine aliuawa, na pale msalabani pia, mmoja aliingia utukufuni na mwingine kupotea!

  Ndio hivyo, ingawa inasikitisha sana!

 28. Mpendwa Haule,
  Shalom!
  Katika kauli uliyoitoa, napenda niweke sawa kidogo tu ili kuuleta mjadala katika manufaa kwa yeyote anayeufuatilia.

  Kati ya sababu ulizozitoa za mimi kutokumkubali nabii Joshua,  zikiwemo ile ya kutokuamini kuwepo kwa Mungu Baba, Mungu Mwana na Mungu Roho Mt ; na kutokuukubali Ubatizo wa kunyunyizia/maji mengi kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mt. Hizo kweli ndizo sababu za awali zilizonifanya nimtilie shaka nabii huyu na kunifanya niikague zaidi huduma hiyo katika mahubiri yake ili nione kama kuna ujumbe wowote kwa Kanisa. Sijaona ahadi ya ujio wake wala mafundisho yake hayana jipya lolote haswa kulingana na wakati, labda ktk mafanikio ya kimwili, hayo ni sawa, maana yanaendana na hali ya dunia katika siku za mwisho ya kupenda mali; katika hilo naona huduma hiyo, kama zilivyo nyingine nyingi, zinafanya kazi vizuri sana, kwani ni vichocheo vizuri sana katika kuwaleta watu ktk tamaa ya mali! 

  Katika hayo uliyoyaorodhesha, ni “Mungu Baba” tu ndilo neno lililotumika katika Biblia, tena si katika maana unayoitumia wewe na Joshua, ile ya Utatu. Haya mengine ya “Mungu Mwana” na “Mungu Roho Mt” ni maneno ambayo hayamo katika Biblia, kwa hiyo ninaamini kuwa ni hekima ya kibinadamu pamoja na matumizi yake katika ibada kadiri waasisi wa hayo walivyojaribu kumpambanua Mungu kwa ajili ya wafuasi wao!

  Kwa hiyo kama unavyosema, ni kweli nabii huyo angekuwa amekuja katika “Roho Yule” aliyeiandika Biblia na kuwaongoza manabii na mitume ambao kwao aliweka Msingi wa Kanisa, kwangu na kwa wengine wenye kuyapenda Maandiko kama yalivyo, ningempokea, lakini huyo naona kaja katika “Roho” nisiyemjua, ndio maana nimemkataa. Kwenu ninyi mnayemjua Roho huyo muwe na amani, na kama mnalo la kutufundisha, tunapenda kujifunza na imani za wengine, kama ninavyoziona aya za Quran zinavyotiririka, kuanzia SCOAN hadi kwenye blogu, au miungu ya akina Lilith (Babe watoto) nk!

  Mimi simjui TB Joshua kwa tabia isipokuwa ki Huduma kama anavyojiwakilisha. Kwa hiyo nakushauri nawe mpendwa usijiweke mbali sana, maana kama huyo ni baraka ya ulimwengu, ukijiweka mbali naye bila sababu ya msingi, utahesabiwa makosa akiwa ni nabii wa Mungu aliyemleta kwa ajili yako! Lakini pia napenda ujue kuwa Miujiza si mwisho au tamati ya Injili, miujiza ni kwa ajili ya kuwavuta watu waje, kama maelfu wa kwetu walivyovutwa na miujiza inayotendeka huko SCOAN, baada ya miujiza, yaani chambo, inapaswa itoke sauti yenye Mamlaka (iwapo mambo hayo yanaongozwa na Roho Mt), iliyo na ujumbe kwa kanisa kulingana na hali linayokabiliana nayo kiroho, na kimaandiko; hayo ndiyo nilidhani mtakuja nayo katika hizo mnazoziita hoja!

  Haule, kuhusu Ubatizo na hiyo Mdo 2:38 pamoja na kitabu chote cha Matendo, yaani mitume wooote, hao ambao hawakutoka kuifanya kazi ya Bwana hadi walipojazwa Roho Mt, huyo unayesema atuongoze nasi katika majadiliano yetu hapa kwenye blogu, ndiye aliyewaongoza hata wakabatiza kwa Jina la Bwana Yesu Kristo ili hao wanaoingizwa katika Ukristo waondolewe Dhambi. Sasa unapotuambia kuwa huyo Roho atuongoze nasi, ndio sijakuelewa unachosema, kwamba akuongoze wapi, au wewe ndio umuongoze huyo Roho Mt hadi kwa Kristo aliyemleta kisha umshitaki kwa kufundisha Ubatizo potofu kulingana na agizo walilopewa ktk Mathayo 28:19 ambao kwa makusudi ameupotosha na hivyo kuwakosesha mbingu kanisa lote kuanzia lile la siku ya Pentekoste na yote la Galatia, Korintho, Kolosai na yoote waliyoyahudumia!!!

  Wakati mwingine ni vizuri kuwa na ujasiri hata wa kulikataa jambo. Hebu angalia matokeo ya kulikubali Neno nusu nusu, mnamkataa hata Roho Mt kuwa ndiye Nabii wa Kweli, kwa sababu ya kuikataa Mdo 2:38, mmeporwa hata ufahamu wachini katika Maandiko. Tazama hapa Petro anasema hivi, ” Maana unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu ; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.” 2Petro 1:21, halafu mpendwa anakuambia bila uoga eti hiyo ni ZIRO! Unapoanza kulikataa Andiko moja, basi jua pole pole utasogezwa mbali na Mungu mpaka mwishowe utajikuta unasoma aya nyingi za Qurani na site nyingi za kishetani na kuzielewa vizuri kuliko Biblia, kama unavyoona tunaulizwa kama tunajua maana ya Mungu ni Mmoja!

  Hata hivyo nakushukuru ndugu yangu Haule kwa maelezo yako na “upole” uliouonesha kwa wachangiaji wote bila kubagua,

  Bwana akubariki!!

 29. Tatizo lako Milinga ni kushikwa sana na tabia za mitaani mpaka nakuona umeingia nazo kanisani!

  Mwenye hoja huwa hazungumzii hoja, ukiona mtu anazungumzia “hoja, hoja …” basi jua hana hoja ni mbabaishaji tu! Na wababaishaji kipeo chao ni ushabiki ambao ni cantankerous kwa asili, yearning to explode, basi ikielekezwa ktk ubishi, shughuli ndio kama hii yako!

  Angalia kauli zako, “… kama kuna mtu hakubali kuwa TB Joshua ni NABII WA KWELI WA MUNGU atupatie kwa upana HOJA NYINGI ZA KISAYANSI (Researched facts and doctrinal analysed logical truths) ili na sisi tuelewe kwa nini anakuwa na mashaka na watumishi wa Mungu kama Joshua.” ukisikia uhodari wa maneno mtaani ndio huu, unajibebea tu materminology unayoyaokota mitandaoni na kuyabwaga mahali nje ya rejea, kwa vile ulikwisha pewa roho ya kuuamini uongo, basi unainuka na kuona hayo yasiyoeleweka eti nayo ni hoja! Kwa taarifa yako Biblia inahusika na IMANI na si SAYANSI, kwa hiyo kama hizo “Researched facts and doctrinal analysed logical truths” ni sehemu ya mafundisho ya SCOAN, unatutoa kapa wengi, ndio maana unatuona hatuna hoja!

  Jaribu kuupa moyo wako nafasi ya kutafakari mambo, unaukimbiza sana katika ibada zisizoeleweka, mpaka mnaabudu Huduma badala ya Mungu, kujaza ile vacuum, angalia maganda ya ndizi usije ukateleza uvunjike!!

  Bwana akuondolee ushabiki!

 30. Milinga, Lwembe, John Paul, Sam…..na wengineo

  Hivi ndugu zangu hata kwa kuziangalia Nabii zake huyu ndugu , je hazitupi hata ukakasi wa kiroho kujiuliza maswali juu ya Nabii huyu jamani…?

  Hivi mnataka Nabii wa uongo aje na nini hasa ili mtambue ni nabii wa uongo?……Hivi Paulo aliposema maneno haya alikuwa na maana ipi….”MAANA WATU KAMA HAO NI NI MANABII WA UONGO…….WANAOJIGEUZA WAWE MFANO WA MITUME WA KRISTO, WALA SI AJABU MAANA SHETANI MWENYEWE HUJIGEUZA AWE MFANO WA MALAIKA WA NURU….BASI SI NENO KUBWA WATUMISHI WAKE NAO WAKAJIGEUZA WAWE MFANO WA WATUMISHI WA HAKI….2 COR:11:13-14

  Hivi Nabii za huyu Joshua zinajenga nini katika mwili wa Kristo…? Hebu eleza kifo cha Mheshimiwa Saitoti….nakulijenga Kanisa la Bwana….! Hebu rudia nabii zake, kwangu mimi karibu katika nabii zake zote….simuoni kabisa Roho Mtakatifu katika Nabii hizo…na kwa ujasiri kabisa nasema ni ROHO YA UKENGEUFU….!

  Kwa msomaji wa Neno la Mungu na anayelipa nafasi yake halisi utaona wazi WATEULE wa Mungu ni wachache mno…! Na ni wachache Mno wanaoweza kutambua ROHO YA UKENGEUFU inayofanya kazi leo kwa kutumia Jina la Kristo!….

  Bwana wetu alisema wazi….NAO WATATOA ISHARA KUBWA NA MAAJABU WAPATE KUWAPOTEZA KAMA YAMKINI HATA WALIO WATEULE….!

  Kwa kifupi napoona wateule wameingia mtegoni kwa huyu Nabii wa Nigeria inatia uchungu mno….!

  Nakumbuka miaka ya nyuma nilipookoka, kila aliyebeba Biblia nilidhani ni mtu wa Mungu, nikakuta kumbe siyo, mara nilidhani kila anayesema Bwana Asifiwe ni wa Bwana, baadaye nikagundua kumbe siyo, na baadaye nilidhani kila anayenena kwa Lugha ni mwenzangu katika Kristo, nikatambua kuna lugha za mashetani pia……Nikadhani pia kila mtenda miujiza na pepo zikatoka, basi hakika huyo ni Mtenda kazi wa Bwana…..Maandiko yakanionya katika hilo kwamba kwani ile nguvu ya kuasi inatenda kazi hata sasa……Kuna wakati nilidhani pia kila kusanyiko hasa likiitwa ni “kanisa la Kiroho” bali wote waliomo humo ni wa rohoni….lakini Maandiko kakanikataza pia…..kwani hata magugu yamo na hayatishwi na jina la kiroho…. !

  Ndio manaa Paulo alisema wazi….NILIPOKUWA MTOTO MCHANGA, NILISEMA KAMA MTOTO MCHANGA, NALIFAHAMU KAMA MTOTO MCHANGA, NALIFIKIRI KAMA MTOTO MCHANGA,TOKEA HAPO NILIPOKUWA MTU MZIMA NIMEYABATILISHA MAMBO YA KITOTO”

  Wapendwa kutumia kigezo cha miujiza, pepo kutoka……wingi wa watu……misaada……na watu “kufunguka” katika kuipima kazi ya Mungu ni mambo ya kitoto mno…..Mnisamehe sana hapa kwa kusema kwamba mada hii imefanya nione wengi WANASEMA KAMA WATOTO WACHANGA…..WANAFAHAMU KAMA WATOTO WACHANGA…….NA WANAFIKIRI KAMA WATOTO WACHANGA………….Hebu twendeni hatua nyingine katika kumfahamu Bwana…….! Hatutayumbishwa na miujiza……ambayo ndio tuliyoambia kuwapoteza hata Wateule……

 31. Mpendwa Daniel J,

  Nimevutiwa sana na maoni yako na jinsi ulivyojenga hoja zako. Mimi siku zote kinachoniudhi kutoka kwa baadhi ya wachangiaji wa mijadala siyo hapa tu kwenye SG Blog, bali pia hata mitaani; ni jinsi watu wanavyokuwa na maneno mengi badala ya hoja nyingi.

  Kwa mfano ukifuatilia mawazo ya ndg CK Lwembe utagundua kwamba katika mada hii anatumia maneno mengi badala ya hoja nyingi. Hata dada Mabinza LS naye ameingia katika mtego huu wa kutumia maneno mengi badala ya hoja nyingi.

  Mimi nilitegemea kama unatumia muda mwingi kumchambua mtumishi yeyote wa Mungu iwe katika kukosoa au kujenga, kumkubali au kumkataa watu watumie muda mwingi kwa HOJA NYINGI.

  Unakuta mpendwa amekazana sana kuhubiri madhabahuni au kwenye mijadala lakini ukimsikiliza katika muda wa dakika 90 alizohubiri alikuwa ana HOJA MOJA TU.

  Mtumishi wa Mungu unapaswa kuwa na hoja nyingi kadri ujuavyo maandiko na Bwana anavyokufunulia pia. Kama mada ni Manabii wa Uongo au wa Kweli basi uitetee mada yako kwa hoja za kisayansi zaidi kuliko porojo za maneno mengi.

  Kwa mfano mimi nilipendekeza kwenye maoni yangu ya siku ya Jumamosi (Saturday, June 30, 2012 at 11:14 am ) kwamba kama kuna mtu hakubali kuwa TB Joshua ni NABII WA KWELI WA MUNGU atupatie kwa upana HOJA NYINGI ZA KISAYANSI (Researched facts and doctrinal analysed logical truths) ili na sisi tuelewe kwa nini anakuwa na mashaka na watumishi wa Mungu kama Joshua.

  Dada Mabinza na CK Lwembe hawajanipa hoja nyingi iwezekanavyo za kunishawishi nikubaliane nao. Nataka mtu anieleze hoja zisipungue angalau TANO za kiutafiti au za kimaandiko za kwa nini hakubaliani na TB Joshua. Katika mkutadha huu tunajadili Nabii TB Joshua tu tusichanganye watumishi wengine hapa. Tukimaliza mjadala wa Joshua ndipo tuwatafakari watumishi wengine.

  Naomba kama wewe unazo hoja; hoja hizo zifafanue Mafundisho ayafundishayo TB Joshua na unieleze kwamba; fundisho fulani, na fundisho fulani ,na fundisho fulani, nk ; siyo la kweli kutokana na hoja zako za maandiko zifuatazo……… toa mtazamo wako ukizingatia mtazamo wa TB Joshua.

  Kuhusu Unabii mbalimbali ambao huwa anatoa kuhusu maswala mbalimbali duniani na nchini kwake, nakuomba unipe HOJA ZAKO kwa kuchambua hivi; Unabii alioutoa TB Joshua juu ya swala (litaje)………………., siyo wa kweli kwa sababu hizi na hizi (zitaje)……………………….., Pia eleza kwa nini unabii alioutoa TB Joshua siku fulani hukubaliani nao, nk.

  Nakutakia kila kheri katika kujadili kwa hoja nyingi na siyo maneno mengi.

 32. Ndg Daniel,
  Mimi nadhani utakuwa umekwenda mbele sana katika kutaka wajadiliwe manabii wa hapa kwetu. Labda ungechukua wasaa wa kutazama influence au scope ya unabii wao ili uone iwapo wanastahili kujadiliwa katika maana ya UNABII waliowahi kuutoa ambao unaikamata dunia hata mjadala wake uzikamate nchi nyingi. Basi kwa nabii TB Joshua unabii wake uko katka kiwango hicho cha kukata mataifa, na kwa kutumia tv media katika huduma yake, unabii anaoutoa husambaa upesi sana na kuzitikisa nchi nyingi hata kuwachanganya walio madarakani, kama vile kwa Herode alipokutana na Mamajusi. Ndio maana nalo kanisa la hapa kwetu kupitia blogu hii, tunajiuliza katika kiwango cha rohoni, je, huyu ni Masihi?? Ama ni nani huyu? Ametabiriwa wapi katika Maandiko kuwepo ktk siku yetu leo na kwa Huduma ipi kwa Kanisa?

  Huu ndio mjadala uliopo, sidhani kwamba tunajadili watu, kwanza itakuwa ni unafiki, pia lazima ufahamu kuwa sote tunajitahidi kumpendeza Mungu, na kutokana na njia tulizopita katika kumjia Kristo, ile influence sisi hubaki nayo katika namna ya mapokeo ambayo huwa hatuyajui kama mapokeo, bali huyaamini kama sehemu ya Neno mpaka siku ambayo Bwana katika Rehema yake hutupa ujasiri wa kulitazama Neno lake na kuliamini hilo ndipo sisi hubaki HURU kama Neno linavyotuambia!

  2. Kwa jambo hili nadhani jibu ndilo hilo hapo juu, yaani ni kweli hatuwajadili kwa kuwa hatujasikia au kuona miujiza ya kutisha!

  3. Hoja kwamba kwa vile kila mwamino anae Roho Mt ndani yake na hivyo kuwa na potential ya kufanya miujiza, hilo ni kulingana na Maandiko, ” … na ishara hizi zitafuatana na waaminio …” Biblia haisemi ishara hizi zitafuatana na manabii au mitume au wainjilisti au maaskofu au wachungaji, bali inasema WAAMINIO! Ukiwa chini ya uangalizi wa Roho Mt ni rahisi kufundishika na kuongozwa na hivyo kuwapo kusanyikoni huwa ni sehemu ya faraja kwa mwaminio na hapo ndipo watakatifu hukamilishwa!

  4. Siujui umri wako, lakini nadhani anayekuambia kuwa hiyo ni mojawapo ya huduma zilizochipua kama uyoga, anajua anachokisema!

  5. Mimi nadhani haujaitathmini hali ya media kwa kanisa letu hapa, aidha umeamua tu kuwaponda watumishi wa hapa kwetu kama ninavyowaona wengine ktk michango yao, ili kumtukuza Joshua at the expense ya viongozi wetu. Lakini mbona hata hapa kwetu siku hizi tunazo stesheni za radio za kikristo na pia television, na hata za kulipia, huduma nyingi zinarusha vipindi hewani. Tena wako hata vingozi waliopata vyeo vya Utume na Unabii kwa maono ya kuanzisha vituo vya tv tu!! Hata hapa kwenye blogu tunapowasilianai, hauoni kuwa ni hatua kubwa iliyopigwa? 

  Huduma za kinabii ni kweli ziko nyingi duniani, suala sio wingi wa huduma bali Ukweli wa huduma hizo, je, zinafundisha kile walichofundisha mitume??? Nabii wa Uongo huja na Neno mchanganyiko lililo na Upako wa kudanganya ndio maana wengi wanasombwa kwa huo Upako, hata unaweza kudhania kuwa maelfu wanafunguliwa, lakin ukweli ni kwamba wanasombwa na mafuriko!

  Pia naona umeigeuza tv kuwa ndio king’amuzi cha kumjua nabii wa uongo, hiyo nayo ni injili mpya! Nabii wa uongo anapatikana katika Maandiko, hayo ndiyo yaliyo kufahamisha uwepo wao, na ni hayohayo yatakayokuonesha hao ni akina nani, na sio tv!!

  Basi kwa usalama wako jaribu kukagua kila kitu kabla ya kukipokea, yawezekana fursa ikawa ni moja tu, basi ni vizuri kutafakari kwanza katika reflection ya Maandiko ndipo ujitose katika mwelekeo wowote ule utakao uchukua. 

  Ubarikiwe!

 33. Bwana Yesu Asifiwe wapendwa!

  Kwanza kabisa ninachukua nafasi hii kuishukuru Blog hii maana kutokana na michango ya watu mbali mbali kwa namna moja au nyingine yoyote ile tunapata kujifunza kitu. Ila kuna vitu Fulani vinanifanya nifikiri sana…

  1.) Inakuwaje linapokuja suala la kumjadili mtumishi fulani Source yake hasa inaanzia katika miujiza inayofanyika katika huduma hiyo? Mbona wengi ni waalimu na wanafundisha vitu ambavyo havipo lakini hatujawahi kuwajadili?
  2.) Hapa kwetu Nchini tunao Ma-Nabii wengi tu,lakini sijawahi kuona nguvu kubwa ya kuanzisha mjadala kama huu kiini chake kikiwa Mtumishi mmojawapo kutoka hapa Nchini.Au kwa kuwa hatujasikia au kuona miujiza ya kutisha?
  3.) Kuna hoja kwamba watu wengi wanafuata Miujiza wakati Roho mtakatifu mtenda miujiza anakaa ndani yetu sisi wenyewe kwa hiyo tunaweza kumuomba yeye mwenyewe tukapokea muujiza.Kama ni hivyo basi Kanisani tunaenda kufanya nini wakati pia Roho mtakatifu huyo huyo ni Mwalimu anaweza kutufundisha?
  4.) Ni ukweli usiopingika TB Joshua ameweza kuwa Popular kutokana na media yake ya Emmanuel TV lakini huduma yake ilikuwepo miaka mingi . Kusema kwamba huduma yake ni moja kama ya huduma zinazoibuka kama uyoga hatuoni kuwa tunakosea sana?

  5.) Dunia ya sasa ni ya Sayansi na Technologia.Katika mambo mengi yanayoweza kuchangia Wakristo kujisahau na kutokuwa na Muda wa kumtafakari Mungu,Media zinachangia kwa kiasi kikubwa.Ukinunua iwe ni Ving’amuzi n.k. Idadi kubwa ya Channel zilizojaa ni zenye vipindi vya kuwapotosha watu na kuteka ufahamu wetu. Watumishi wengi ukiangalia Huduma zao ziko katika miji mikubwa tu,wakikusanya Sadaka na kujilimbikizia mali. Hata maono ya kuwa na TV Media au hata redio ili wengi waweze kufikiwa na Injili hawana. Na ndio hao wanabaki kuzungumzia huduma za watu wengine badala ya kuleta mbadala wake ili kuwafungua watu kutoka katika wanayoyaita mafundisho ya uongo. Kwa upande wangu ( ama TB Joshua ni nabii wa uongo au Lah! Sijui ) But still Emmanuel TV imebadilisha maisha ya watu. Nimeona watu wakiamua kubadilisha maisha yao na kumgeukia Mungu kutokana na shuhuda tu walizozisikia na kuziona kupitia katika Media hii.

  Mimi Naamini Huduma za Kinabii ziko nyingi sana Duniani pia hata hapa Nchini kwetu.Na kama ingekuwa inawezekana kila Mtumishi aweze kufanya Broadcasting ya Huduma yake kupitia Media TV ndio tungejua kumbe kuna manabii wa uongo kweli kweli kuliko hata hawa tunaowajadili hapa.

  Mob: 0787-454952

 34. Mpendwa wangu MILINGA,
  Nikutoe wasiwasi kwamba CK Lwembe, hatuishi pamoja wala sipajui kanisani kwake, na sikujadiriana naye lolote kabla ya yeye au mimi kuandika yale uliyoyasoma na kusema kuwa yamefanana kama “Nakala” Ninachojua Ndege wa aina moja wanatabi za mfanano! Lakini zaidi sana mimi sisemi tu kwa ujuzi na mafundisho yangu ya kichwani, na kama umegundua hivyo basi nimshukuru sana MUNGU kuwa nami nimepiga hatua kuuelekea ujuzi katika Neno la Mungu, lazima nikili wazi kuwa CK Lwembe yuko mbele yangu sana tu katika ujuzi wa Neno la Mungu,. Mimi nami nimejifunza kwa bidii kupitia mafundisho yake, nimekuwa nikiuona ukweli mwingi katika maneno ayasemayo nikilinganisha na isemavyo Biblia. Nakushauri uyasome nawe Mahubri yake,kwa nia ya kujifunza na si katika ushabiki na msimamo wa ki- Dhehebu, ambao wengi wanao na ninadhani hata wewe hali hiyo nikama imekukamata sana. Kaka yangu usifie kisima kwa kiu eti hutaki kunywa maji yale kwa vile tu, eti si ya NUWA! Siyo mimi au CK lwembe anayepinga kuwa T.B. Joshua si nabii wa Mungu, bali maanbiko yaliyomo katika Biblia ndiyo yanayokataa, kila nikisoma nakuta hana sifa za kinabii wa ukweli! Mojawapo ya sifa ya nabii wa kweli wa Mungu ni kutabili au kutoa unabii ili Roho za waumini zipate ujumbe wenye kuziponya au kujenga ili waumini wakae katika kutegemea na kumwamini Mungu,na si vinginevyo! Sasa, T.B. Joshua, kule kutabili juu ya Ndege iliyoanguka na kuua watu kumekusaidiaje kiroho kama Bibi harusi wa Kristo? Au kufa kwa waziri wa Kenya katika ile Ajari ya Helkopta kumeliambia nini Taifa au Kanisa la Mungu? Mimi naona tofauti yake na Shekh Yahaya ni kwamba T.B. Joshua ana hudumu katika kanisa linalojiita la ki-Kristo, wakati Yahaya alikuwa akihudumu ndani ya Nyumba yake ya kulala tu basi! Maana, yahaya naye alikuwa akitabili juu ya matukio kwa nia ya kuwajulisha watu tu, mara atabili ushindi katka kandanda, ushindi katika vyama vya siasa nk, vivyo hivyo na T.B. Joshua. Kama kunajambo lolote alilotabili tofauti na hayo na linakubalika na maandiko tupe! Usiukatae ukweli utapotea Mkubwa!

 35. Kristo Yesu apewe sifa wapendwa..
  Niwatake radhi sikuwa nanyi ktk jukwaa hili nikimaanisha kuchangia,Nimepitia mabandiko machache,Mungu akipenda nitayosoma yote ili nami nipate ufahamu.

  Mimi sitagusia kabisa nukuu ya Nabii Joshua,
  mosi kinachozungumziwa hapa ukiangalia siyo nukuu yake.
  pili mimi simfahamu vizuri huyu nabii Joshua na hakika sina shauku ya kumfahamu nimewahi kuandika hivyo kwenye Thread mojawapo hapa ya Joshua.

  Tatu Pamoja na mabandiko ya kumkubali/kumpinga Joshua ya wapendwa hapa ukiangalia vizuri utagundua kuwa (niwataje kwa majina Sam.Lwembe na Mabinza,)wao wanampinga kutokana tafsiri ya maandiko vile wao walivyofundishwa/funuliwa na huyo roho anawaongoza.Kwa vile wao hawamini Mungu Baba Mwana na Roho Mtakatifu na kuwa Joshua habatizi kwa Jina lake Yesu kwenye huduma yake vinginenevyo wangemkubali.naye angekuwa anafanana na nabii Yule.

  Kwa bahati mbaya au makusudi mpendwa Sam unandika mabandiko ya kebehi kwa baadhi ya watumishi kwa kuwataja majina,John Paul amekuomba utajae nabii wa kweli ujasiri ziro, taja basi mtumishi wako au hema… sherIa za SG ZINAKATAZA KUTAJA HEMA hapa tunazungumzia maandiko na blahblah ….complex lakini kuwakebehi wa watumishi/mahema mengine SHERIA ZA SG ZINARUHUSU.

  Sawa tunasubiri siku ufunuo ukifunuliwa hapa tukamjua huyo nabii Roho mtakatifu na kanisa la Roho mtakatifu mnayetaka tumfuate maana siku ipo tena yaja.
  Mpendwa Mabinza hayo ndiyo mafuta ya huyo Roho mtakatifu wa nabii yule yanayokufundisha maandiko!!!!!!!!

  CK Lwembe nadhani ni ukamilifu wa nyakati tupitie tena na kuangalia kubatiza kwa Jina la Baba Mwana na Roho Mtakatifu.tukichunguza maandiiko na mafunuo kama waberoya, Roho wa Bwana ashuhudie miyoni mwetu ile kweli,tukipitia na mstari wa Mdo 2:38.tukiangalia pia kumpokea Roho Mtakatifu kwa sehemu.ni wakti muafaka pia kwa mpendwa Sam.

  Hebu tujadili kama watu waliopokea Roho Mtakatifu,yaani ile kweli,tukitumia maandiko mtu anayetusoma hapa ambaye hajampa maisha yake Bwana Yesu apendezwe nasi na kufanya hivyo kama Mabinza alivyowahi shuhudia hapa alivyopokea wokovu.Jinsi tunavyoenenda na kuitafuta kuijua kweli.Utukufu umrudie BWANA na sio sisi kujifanya wajuzi stadi wa maandiko na mafunuo na lugha za kebehi na kuwa kwazo ktk utumishi wetu (2kor6:1-9)
  Nikisoma mabandiko nina shaka kama ni uongozi wa Roho Mtakatifu…ni zaidi ya kiburi c.ha kujua maandiko
  Utukufu ni wa Bwana peke yake,tusijitwalie utukufu wa Bwana kama Herode akaliwa na chango

  Amani ya BWANA na iwe juu yetu
  Amen

 36. Sam,
  Unasema ” Kwa hiyo suala la kumuoneshea kidole mtumishi kuwa huyu ni wa Kweli ni complex kidogo kuliko yule wa Uongo.” ndio hiyo ni kweli iliyo ‘complex’!!

  Unajua complexity yake ikoje? UTAMJUA NABII WA UONGO KWA KUMJUA NABII WA KWELI KWANZA!!
  Nayo Roho ya Unabii ni ya Kristo, naye Kristo ndiye Neno, huyo ndiye PEKEE awezaye kukuonesha hayo makundi kwa usahihi!!

  Mbarikiwe nyoote mlio na KIU ya kuijua KWELI ktk Kristo Yesu aliye Bwana na Mwokozi wetu!

 37. Ndugu yangu Milinga,
  Ulipoanza katika maswali yako ya kutaka uoneshwe Nabii wa Kweli alipo, ilinitatiza kidogo. Naona hata umetutaja kwa jazba kabisa ukitutaka tukuoneshe nabii wa Kweli alipo, unasema: “Mbona sijawahi kuwasikia wapendwa akina Edwin Seleli, akina CK Lwembe, akina Orbi, akina Sam na wengine wanaopingana na manabii kama akina TB Joshua wakituelekeza ni wapi penye mafundisho ya kweli iwe Tanzania au nje ya nchi hii?”

  Kwa jinsi ninavyokufahamu sikutegemea uje na mambo ya jinsi hii. Maana haya ni mambo wanayoweza kutuuliza Waislamu na wapagani wengine na si ninyi wenye kukiri wokovu! Unajua unaponiuliza mimi au mtu yeyote yule kama ulivyofanya, kwamba eti tukuoneshe Nabii wa Kweli, ni sawa na kuukana WOKOVU ulioukiri? Au ni sawa nawe kumchezea Kristo kama wale waliompiga na kisha kumuulize TUFUMBULIE ni nani aliyekupiga? Ndugu yangu, hebu punguza jazba!

  Baada ya kukuonesha kuwa Nabii Joshua ni wa Uongo, sasa unatutaka tukuelekeze tunakoabudia ni wapi, kama anavyofanya mzee Kulola na wahubiri wengine kwenye mikutano yao ya Injili. Mimi nasubiri Upako wa kwendea viwanja vya Jangwani na kurusha matangazo live, vuta subira kidogo, utanisikia nitakapo waitia mje kwangu KWANZA, ila kama Hema yangu haipo basi tawanyikieni kwenye Hema za jirani zangu waliookoka mpaka nitakapo fungua yangu mtahamia hapo!

  Lakini kwa matumizi ya blog nadhani tukianza kuitumia kutangaza mahema yetu tutakuwa tunakiuka utaratibu wa wenye blogu kwani hawafungamani na Fundisho lolote zaidi ya Biblia. Kwa hiyo ninaamini Upendo huzaa heshima, hivyo ni vizuri kubaki ndani ya utashi wa walio kuhifadhi, haswa ikiwa ni ndani ya Msingi wa Kristo. Siwezi kukusemea wewe, labda ukiona kwako yafaa, unaweza kuendelea kuitumia blogu kwa jinsi hiyo unayotutaka kama anavyofanya Precious, pale anapotuitia kanisani kwao Boko, tukajifunze mengi!

  Nilisema nilitatizika hapo mwanzo, lakini nimefarijika sana huku mwisho wa mchango wako ulipotuasa turudi darasani, kwa maneno yako: “Mwisho, NAOMBA wapendwa wote turudi darasani kujifunza kazi za HUDUMA TANO KANISANI.” Katika hili nimefarijika sana kwani sasa nina uhakika kuwa utatulia kusanyikoni kwenu ili ufundishwe mambo hayo badala ya kuzunguka ukifanya UTAFITI. Kipawa cha “mwalimu” kilichopo hapo kwenu, kitakuweka sawa, na nina uhakika kwa jinsi ulivyo mwenye kutafiti, ukifuzu Roho Mt. aweza kukushushia kipawa cha Unabii ukawa msaada mkubwa kwa kanisa linalokosa mwelekeo!!

  Nakusubiri kwa hamu kubwa, Nabii Milinga!

 38. Mpendwa John Paul,

  Asante kwa maelezo uliyotuletea pamoja na changamoto zake.

  Uliyoyasema ni kweli kabisa, Roho Mt hafanyi kazi kutokea angani, bali hufanya kazi kupitia watu. Jambo hili ni kweli na ndivyo Biblia inavyotufundisha. Pia niseme kuwa maelezo uliyoyatoa katika maana ya huyo aliyejazwa Roho Mtakatifu kuwa msaada kwa wengine katika kuwaongoza kukifikia kipeo hicho, ni kweli kabisa, huo ndio utendaji wa kweli kama ulivyo ndani ya Biblia, na unapaswa kuendelea hivyo mpaka Bwana atakapokuja.

  Pia umeendelea katika maelezo yako unasema: “Hao walipokuwa wanafundisha watu hawakuwaambia kuwa Roho Mtakatatifu atawaelekeza kuujua ukweli. Hawakujificha! Waliwaambiwa UKWELI nao WAKAJULIKANA kuwa Ni watumishi wa Injili ya kweli. Lakini kama kwa siku zetu HATUWEZI KUWA NA HATA MFANO WA MTUMISHI MMOJA AMBAYE TUNAAMINI NI WA KWELI, basi ni tatizo kubwa, kubwa sana.”
  Labda hapa kwa sehemu nitatofautiana nawe katika mtazamo wa jambo hilo hivi; Kwamba mambo tunayoyasoma sisi leo hii katika Agano Jipya, yalipokuwa yakitendeka haswa kwa Kanisa la Mataifa, pale Msingi ulipokuwa unawekwa, hawakuwa na rejea ya kusema kwamba watawakagua wahubiri hao waliowaletea Injili, tofauti na sisi ambao tunayo Biblia. Wahubiri wale, Neno walilolitoa lilikuwa ndio Roho Mt mwenyewe (Yoh 6:63 “… maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima), kama inavyoendelea hata sasa. Kwa hiyo ile kweli waliyoipokea kadiri walivyoimarika katika hiyo, waliongezeka katika kimo. Nao wanafunzi wa Yesu walikuwa ndiye Roho Mtakatifu, katika maana ya udhihirisho, basi hata leo akiwako mwanafunzi mwingine wa Yesu anayeitenda kazi hiyo, atakuwa ndiye Roho Mtakatifu pia! Kwa hiyo suala la kumuoneshea kidole mtumishi kuwa huyu ni wa Kweli ni complex kidogo kuliko yule wa Uongo.

  KWELI ni takatifu, ni pure, ni safi, si mchanganyiko, na inasimama yenyewe! Nayo Biblia ndiyo KWELI hiyo. Inakuwa ni KWELI tusipoiongezea au kuipunguzia chochote, kama inavyotuasa. Kwa hiyo ili uwe na uhakika wa jambo hilo kuhusiana na mhubiri yeyote yule, yakupasa kumsikiliza kile anachokiri na kukifundisha, jambo ambalo katika kundi la wahubiri zaidi ya 1000, sijui itakuchukua muda gani na kwa faida ipi katika kuyafuatilia hayo. Lakini iwapo watu wataamka wakaipeleka mioyo yao katika dhamira ya kulijua Neno la Mungu kwa wingi, watakuwa baraka kwa watumishi wengi, hata wale waoga watapata ujasiri wa kuligeukia Neno kikamilifu maana ukija na mafundisho yasiyoeleweka kusanyiko “linakupiga chini”! kwa hiyo suala la kuwaonesha watu mtumishi wa kweli yuko wapi, sio practical, hata ukiwaonesha wanaweza wakamfuata na kumpindisha vilevile!

  UONGO, ni mchanganyiko wa KWELI na MAUTI. Sehemu ya KWELI iliyomo ndani ya mchanganyiko huu ndio inayowavutia watu kuelekea MAUTINI. Basi iwapo unayo ile KWELI yote moyoni mwako, labda tuseme unavyo vigezo 1000 vya ile KWELI moyoni, akija mhubiri anayejishuhudia kujazwa Roho Mt na kuwekwa katika huduma hiyo, naye akakuambia kuwa Allah wa kwenye Qurani ndiye Mungu wetu yuleyule isipokuwa Waislamu hawaelewi tu, lakini tunawavuta na watajifunza kwa Jina la Yesu lenye Mamlaka!! Halafu miujiza mingi akaifanya na kuhubiri wokovu, iwapo kati ya vigezo vyako utakichukua kimoja cha AMRI ya kwanza labda, kama huyo “Allah” hata pita, unapaswa umbwage mhubiri huyo licha ya kupita katika vigezo 999! Wakati mwingine si lazima umpime kwa vigezo vingi maana lile Neno limejaa kwako, kwa hiyo akija na lililo tofauti, halipati nafasi moyoni mwako hivyo kukataliwa, kwani “kilindi huitikia kilindi”!

  Pia, ni vizuri kufahamu kuwa yeyote yule anaposimama na kutangaza kuwa anayo KWELI, kama madhehebu yetu na Huduma zilizopo zilivyofanya pale zilipoinuka, basi kwa maneno mengine wanasema wote waliobaki hawana KWELI. Hebu fikiria jambo hili, kwanini mtu akose amani kwa kuelekezwa kwenye kweli iliyo katika Biblia naye akidai kuwa hiyo ni yake? Mimi nilidhani watu wataitikia AMINA kwa kila Neno la Mungu, maana ndiye Roho Mt.! Nimepigwa na mshangao unaponiuliza: “Una uhakika gani kama mchungaji wangu ANAAMINI KATIKA UBATIZO WALIOBATIZA MITUME? Una uhakika gani kama mchungaji wangu anakubaliana na kitabu cha Matendo ya Mitume?” Maana swali lililonijia moyoni mwangu ni “UNANGOJA NINI HAPO?” kama mchungaji hayaamini hayo anaamini nini basi? Na huo uchangaji kaupatia wapi? Inashangaza lakini sina budi kuelewa hivyo, bali ni hasara tupu kwa roho zilizo chini ya wachungaji wa jinsi hii!

  Basi ndugu yangu, mtazamo ulionao juu yangu kuwa ukristo wangu ni wa “kuona huduma za kukosoa tu” au nawaona watumishi wa kuwalaani tu, au nina orodha ndefu ya WATUMISHI WANAOPOTOSHA watu lakini sina hata jina moja la mtumishi ANAYEFANYA KAZI YA MUNGU KWA USAHIHI” ni mtazamo ambao ni self defeating! Tukiendelea kudumu katika mawazo ya jinsi hiyo, kwamba tunatazamana sana sisi kwa sisi hata kuwekeana vipimo tunavyovijua sisi, ni wazi kuwa tutaishia mabandani. Kipimo chetu ni LAZIMA kiwe NENO la MUNGU, kama ni BARAKA ama LAANA vyote vimo humo; hakuna anayemzuia mtu yeyote asivipate hivyo. Kama ni MEZANI, sote katika ujumla wetu tumekaribishwa, unachagua unachotaka; kama ni bakuri la BARAKA unalivuta hapo na kujipakulia mwenyewe, na mwenye kuitaka LAANA naye anajipakulia!!! Mazungumzo ya MEZANI huwa hayakosi kama tunavyozungumza hapa kwenye “Meza ya Duara ya SG”, nikimkumbuka Milinga, tuko hapa kwenye BUFFET na tunakutana “mezani’ kila mmoja kaja na sahani yake tunashare topic of the day tu kulingana na Injili ikiwa ndio main dish! Spirit ya majadiliano ndivyo ilivyo, huyaweka wazi mambo mengi hata magumu, tuwe tayari kwa hayo, yasituvunje moyo kama wale wanafunzi, Yoh 6:66 “kwa ajili ya hayo wengi miongoni mwa wanafunzi wake wakarejea nyuma, wasiandamane naye tena.”
  Atakayevumilia mpaka mwisho…!!

  Ubarikiwe!

 39. Ndg Primi, asante sana kwa kunitia moyo, na pia kwa kuwavuta wakristo ili kuwatoa huko wanakotokomea kwa kupumbazwa na miujiza, ili hali hawajui kuwa miujiza hiyo inayowavutia huko, na mikubwa zaidi, Mungu alikwisha kuiweka ndani yao, ila wamedanganyika tu kwa pressure za maisha zilizowapelekea kutokuliamini Neno la Mungu kikamilifu, hilo libebalo Ahadi zote wanazobabaika nazo huko nje. Ubarikiwe saana!

  Ingawa hali ya kutolitilia maanani Neno la Mungu iko hivi ilivyo, ukweli ni kwamba tatizo haliko kwa wakristo, individuals, bali katika systems ambazo zimetujaza (saturate) na mafundisho yaliyo nje ya Maandiko na kutuaminisha kuwa wokovu wetu ni wa makundi na hivyo kuua kiu ya utakatifu ndani yetu, tukiyaangalia zaidi makusanyiko yetu!

  Basi ndg yangu kwa vile Roho Mt ndiye atutafutaye, naye akiwa ndiye Neno, basi kadiri utakavyolisema kama lilivyoandikwa, katika utakatifu wake, hilo LITAMFUFUA yeyote aliye kusudiwa hivyo kabla ya misingi ya ulimwengu kuwekwa, maana yeye anasema kondoo wake anawajua!

  Bwana akuzidishie Hekima yake!

 40. Naomba hicho kifungu cha Mwz 1:26 nilichokinukuu kisomeke hivi:
  “ Mungu akasema na tufanye mtu kwa mfano wetu, katika sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.”

  Mnisamehe kwa typing error!

 41. Kwa wapendwa wa SCOAN,

  Shalom!
  Ninawashukuru nyote kwa michango yenu na msimamo wenu unaodhihirisha imani yenu katika mafundisho ya nabii TB Joshua. Juu ya hayo, michango mliyoitoa inazo nukuuu za Maandiko, kwa hizo, mkijaribu kutudhihirishia kuwa Nabii huyo ni wa Kweli, kwa hiyo nasi twapaswa kumpokea. Basi, nanyi mkiwa ni sehemu ya huduma hiyo, kabla ya kumpokea, tunaendelea kuyachunguza hayo mnayotaka kutuaminisha kuhusu huyo Nabii kama yanalingana na Maandiko.

  @ Ndg James,
  Ujuzi wa Maandiko ni jambo la muhimu sana. Hilo laweza kuwa msaada mkubwa sana katika saa yako ya majaribu, haswa pale unapoangaziwa Nuru, ujuzi huo huweza kukurahisishia kuibaini Nuru Bandia! Maandiko yanatusisitiza katika hilo; 1Tim 4:13 “… , ufanye bidii ktk kusoma na kuonya na kufundisha”. Nawe iwapo ungejibidiisha katika hayo, usingekuja na maelezo yasiyo eleweka! Angalia, “Mtu anaposema kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareth pepo toka, mnataka tuanze kuulizana Yesu yupi na roho yupi anatumika. Hili swala Yesu mwenyewe alisha lijibu wanafunzi wake walipompa taarifa kuhusu walio kuwa wanalitumia jina lake wakidai hawapo upande wao” Kwa hiyo James, UNATUFUNDISHA kuwa kila anayefanya miujiza kwa Jina la Yesu ni mtumishi wa Mungu wa kweli?? Mbona Kristo huyo huyo anatuambia kuwa WENGI watakuja siku hiyo na kusema mimi niliwaponya watu kwa Jina lako Bwana, naye anasema atawaambia ONDOKENI siwajui…!! Mimi nafikiri wewe, kwa kukosa ujuzu wa Maandiko umejiingiza katika KUMKUFURU ROHO MT kwa kufundisha Neno la Mungu kinyume na Biblia hivyo kuwadanganya watoto wa Mungu kwa kuwafanya wawapokee na waigizaji! Hiyo ndiyo hasara ya kutoyasikiliza Maandiko, maana Mungu anaweza kuidai damu yao kutoka kwako!!!

  Hivi wewe umemjua Kristo mlipokutana kule Galilaya? Au mlikuwa naye kule Nazareti, nawe ndio umetuletea hitimisho lake hilo la kuwaamini wote wenye ishara? Ninakushauri utulie kwanza katika kusanyiko lenu chini ya ‘mwalimu’ ili ukue kidogo, mbawa zako bado hazijajenga usijaribu kuruka, utakufa kiroho maana Hukumu itakukamata na inawezekana usitoke!!!!

  @ Ndg Nduta
  Nduta, umenishangaza sana kwa ujasiri wako! Umenikumbusha tukio lililowahi kutokea huko Moshi vijijini: kuna mwanakijiji aliyekengeuka katika maadili, akaanza kubaka akina mama na wasichana wanaokwenda kutafuta maji nk. Wanakijiji walipoanza kumsaka, akawa ni mtu wa kukimbia na kuishi maporini, lakini akiendelea na mambo yake hayo. Wakamvizia, wakafanikiwa kumtia mikononi. Katika hasira walizokuwa nazo wakampiga sana mpaka ikaonekana aweza kufa, ndipo wakasimamisha kipigo, wakampa fursa ya kufanya SALA YAKE YA MWISHO, nadhani wanakijiji wale hawakutaka kumuua baada ya kuingiwa na huruma, wakimpa nafasi ya kutubu ili wamwachie HURU katika imani kuwa atakuwa amejirudi. Ndipo akasimama kwa taaabu, akainua mikono yake juu katika ishara ya kuomba, kundi lote ghafla likawa kimyaaa, hata sindano ingeanguka ungeliisikia, akasema kwa sauti kubwa, “SHETANI POKEA ROHO YANGU!!!!” baada ya sekunde chache za mshangao, WAKAMPIGA HADI KUMUUA!

  @ Ndg Eucalyptos,
  Yaonesha umekuwa na one track of mind kuhusu Imani na matendo yake, kwamba ni lazima matendo hayo yawe katika namna ya miujiza! Hiyo ndio conception ninayoiona kutawala katika maisha yetu. Lakini, Tendo Kuu la Imani ni kulipokea Neno LOTE na si mambo hayo ya Uponyo na Miujiza mingine, ingawa hayo pia yamo katika package hiyo ya Imani. Kama wote tuna Imani Moja, yaani tumelipokea Neno LOTE, tofauti zetu zingetokea wapi? IMANI iko moja tu, ila MISIMAMO, ambayo sisi hudhani ndio imani, hiyo iko mingi. Nayo IMANI ni mawasiliano na Mungu, kama tunavyosoma kuwa Habili, kwa IMANI alimtolea Mungu sadaka iliyo bora; lakini hakuna sehemu katika Maandiko inayomuonesha Habili akizungumza na Mungu, basi Imani ni mawasiliano ya siri ambayo Mungu huyafanya na wanaye naye akayaficha kwa wasiouhusika hata tunawaona wakijibidiisha katika kuwa na IMANIili watende Miujiza!

  Ndg yangu nakuona unavyojibidiisha nawe katika kuifunga midomo ya wanaoikataa Huduma hiyo ya SCOAN, kwa kulirahisisha Neno la Mungu na kulifanya si kitu cha kukitegemea sana, bali watu wategemee wanavyoviona na kuvishika! HUO ni UONGO!! Inashangaza sana tena pale unapojaribu kutuambia kuhusu Roho Mt, hivi unakijua unachosema kweli?? Mimi nadhani umejichanganya sehemu fulani!! Yawezekana ujuzi wako umekuzidi na sasa ili mtu wa kawaida akuelewe, inambidi achanganyikiwe kwanza! Angalia unachotuambia, “KAMA HABARI NYINGI NI HIZI ZA KUSOMA NA KUSIKIA” basi hatuna haki ya kuhukumu wala kuzungumzia lolote. Kama una Roho Mtakatifu akakufunulia (kama inavyotakiwa) juu ya huduma, mtumishi fulani then una haki ya kusema hilo ipasavyo.” Hivi wewe ulishawahi kukutana na Roho Mt. akakuambia utuambie haya unayoyasema? Au mlipokutana alikuthibitishia kuwa hiyo Huduma ni ya Mungu? Mlipokutana alikuwa amevaa nguo gani? Umenukuu kutoka 1Cor 2:3, hivi ulikuwepo huko Korintho na mkakutana na mt Paulo alipokuwa akiyafundisha hayo hata unatuletea sisi? Ndio maana nimekuambia kuwa ili kukuelewa inabidi mtu awe amechanganyikiwa!

  Unasema, kuhusu ‘hearsay’: “Kwa mfano wanaosema kuna “andiko la Quran huko SCOAN”, ninaamini hawajawahi kuliona physicaly na kwa wale waliosikia habari zake hata maana yake hawaijui.” Sijui kama hata unafahamu maana ya ‘elimu na hekima na maarifa ya kibinadamu’ kama ulivyojaribu kutufundisha. Maana naona ndiyo unayoitumia katika kututafsiria jambo ambalo liko wazi. Kama jambo hulijui ni vizuri kukaa kimya ujifunze kuliko kuwachanganya watu kwa kujaribu kuwaelekeza kujichanganya na miungu mingine kama alivyofanya Balaam kwa wana wa Israeli! Unatuuliza, “NINI MAANA YA MUNGU MMOJA?” halafu katika maelezo yako unatutaka kwa hila tusihoji uwepo wa ishara za miungu mingine ndani ya Hema la Kuabudia, huo ni unabii wa Uongo in the making!

  Kama ZERO unaiona ina thamani, basi naona nikuache hapo kwenye zero yako, mpaka nabii wako atakapokuja kukutoa!

  @ Ndg Milinga,
  Naona bado uko mwilini saana! Lakini kaza moyo, hapo ndipo mambo huanzia. Ila badala ya kujirundikia vitabu vingi vya rejea vinavyokupa tafsiri nyingi tofauti tofauti za Neno la Mungu, jaribu kufanya jambo moja: viondoe vitabu vyote walivyoviandika watu wa dini, pamoja na vijarida vya Jehova Witness, hakikisha umebaki na Biblia tu! Sasa ichukue hiyo na kadiri unavyoisoma USITAFSIRI CHOCHOTE, tafuta kuyaelewa hayo unayoyasoma kutoka humo unamosoma! Biblia haina vitabu visaidizi, inajitegemea. Ukijitoa kwa namna hiyo ya kuingojea Biblia ijitafsiri yenyewe, Roho Mt. atawajibika juu yako. Mungu alisema na iwepo nuru, tafsiri ya hilo ndiyo nuru tuliyonayo. Mungu akasemana liwe anga… anga likaweko, sio hadithi!

  Lakini ukijirundikia vitabu na vijarida vikusidie kulitafsiri Neno la Mungu, elewa utaishia kukaa zaidi ya mwaka uliokaa kwa ‘mzee Kakobe’ ukitafiti na ukaondoka kwa vile tu unabii wa Mrema kushinda kiti cha urais haukutimia. Kama ungeiamini Biblia nayo ikawa ndio YAKINI yako katika mambo yamhusuyo Mungu, ninakuhakikishia siku ya pili ungeondoka baada ya kuwaona wanawake wote wamefungwa vitambaa vichwani, maana jambo hilo lingekurudisha katika Maandiko kuona ni wapi jambo hilo limeagizwa! Ukristo sio lele mama! Iwapo unaelea ‘from pillar to post’ utayaelewaje mambo ya Mungu? Utakuwa unaongozwa na roho anayeogopa Neno la Mungu lakini mwenye ujasiri wa kupokea yaliyo nje ili mradi limetumika Jina la Yesu. Hebu angalia unavyopotosha mambo unaniambia “niko zaidi kutoa criticism kwa watumishi mbalimbali wanaoshabikiwa na watu …” hivi nikuulize, kuna jambo gani la kushabikia katika Injili? Labda huenda ktk sphere ya mambo ya miujiza pamoja na ile theatrical setup ya SCOAN katika jinsi ya ibada zake na huduma zake kama hao “wise men” aliokuwa akiwashabikia ndg Nduta, lakini hayo ni mambo yenu ninyi, mimi nitawa criticize kwa jambo lipi? Labda mnapotaka kuniingiza nami ktk kundi lenu ndipo katika kukataa kwangu mwaweza kuona nina criticise wakati mimi nafanya exhortation ili mrudi ktk Maandiko muyatimize hayo muachane na ushabiki usiokuwa na tija ktk Ufalme wa Mungu mnaosema mnatumika ndani yake! Matokeo ya ushabiki ndio hali mliyonayo ambayo mnafungua Biblia zenu halafu badala ya kusoma yaliyo andikwa mnasoma toka vichwani mwenu yale mliyoyajaza katika mioyo yenu kutoka kwa walimu wenu.

  Hebu niweke hapa, kwa ajili ya wote wanaofuatilia mada hii hicho kifungu cha Mwz 1:26 ambacho wewe unaniambia kuwa ndicho kinachoithibitisha hiyo Statement of Faith ya SCOAN, tena unasema kifungu hicho kinazungumzia kuhusu UTATU WA MUNGU, ukinishangaa kwamba, SIJAYASOMA HAYO? Ni kweli mimi sijayasoma hayo, kila ninapofungua Biblia yangu kukisoma hicho kifungu ninakiona hivi: “ Mungu akasema na tufanye mtu kwa mfano wake, katika sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.” Nimekirudia kukisoma kifungu hicho zaidi ya mara tatu na sijayaona yote uliyoyaandika kuhusu kifungu hicho zaidi ya hayo niliyoyacopy kutoka Biblia yangu!!! Au Biblia yangu ni tofauti na hiyo mnayoitumia huko SCOAN???

  Wapendwa wa SCOAN, nawatakieni kila la kheri haswa pale mtakapo ifikia ile “Ibada ya Damu ya Yesu” basi muwe wa kwanza ktk kuyakimbilia hayo mabomba, mkajiloweshe mwili wote kwa utukufu wa Huduma hiyo!

 42. KAKA MILINGA, Hoja yako haiwezi kupita bila kupingwa!! Si kweli kuwa MUNGU ni UTATU! Hata mimi naungana na Ndg. CK Lwembe, kuwa sijapata kuona andiko lolote katika Biblia linalosema Mungu ni Utatu! Andiko ulilonukuu kutoka katika Mw. 1:26 ni kweli panasomeka hivyo, “….natuumbe Mtu kwa mfano wetu…..” hiyo haimaanishi kwamba alikuwa akijiambia katika kikao chake Mungu mwenye nafsi tatu zilizo sawa! Kimsingi, Mungu alipokuwa akisema juu ya kumuumba Mtu, alikwisha muumba tayari katika mawazo yake, kabla ya kusema tamko lake hilo. Siku hiyo alipotamka juu ya mpango wake wa kumuumba Mtu ilikuwa ni kuweka wazi mpango wake huo na pia kuonyesha makusudi yake katika uumbaji huo.
  Lakini kiukweli mkutano huo ulikuwa baina ya Mungu na Lusifa wakiwepo na malaika wote wa mbinguni, na mkutano huo ulimlenga Lusifa! Labda kabla sijaendelea niseme ni kwa nini; Kwa mjibu wa ile Mw.1:26. Hebu jiulize, kama Mungu ni nafsi tatu, na kwamba utatu huo ndiyo Mungu mmoja; je, inawezekanaje Mtu mmoja tena anayejua yote, anayeweza na Mfanya yote afanye mkutano, na kujiambia peke yake juu ya mpango Fulani aliokwisha ubuni peke yake na anatazamia kuufanya peke yake? ukiendelea ule mstari wa 27, utaona upekee wa mungu!
  Ukiendelea katika kuipeleleza Biblia utaona kuwa; Kimsingi, Mungu katika uumbaji wa huyo Mtu wa kwanza, alipenda kumshirikisha pia Lusifa kwa kuuweka wazi mpango wake huo ili kuuibua ule uovu uliokuwemo katika moyo wa Lusifa mbele ya malaika watakatfu wa mbinguni. Na kama yangetokea mapatano kati yake na Lusfa, kule kuwapo tu makubaliano japo utendaji unabakia kuwa wa Mungu, basi na Lusifa angeshiriki kumuumba Mtu! Kama hutajari ukiiangalia vema na kwa utulivu Biblia yako, bila kutanguliza ujuzi wako mwenyewe, utuona mpango mzima wa umbaji wa Mungu hadi katika lile shamba, ambalo Yule Mtu alikwenda kuishi ambako pia na huyo Lusifa alikuweko, utaona kuwa Sababu kubwa ya Mungu kuitisha kikao hicho cha “uumbaji Mtu” ulilenga kuweka wazi tofauti ambazo Mungu alikwisha ziona moyoni mwa Lusifa, naaliyekuwa akiambiwa “…natuumbe mtu kwa mfano wetu alikuwa huyohuyo Lusifa, Biblia inasema, Lusifa hakukubaliana na mpango huo na hivyo akakataa na kuwa mwasi.
  Tangia hapo nafasi na kiti chake akanyang’anywa na kutupwa hapa Duniani. Naye akawa mmoja wa watawala katika hii Dunia sawa sawa na TAMAA yake! Lakini, kama ilivyo katika mabalaza na serikali za wanadamu, kiongozi anaweza kuamua kufanya jambo, na kuwashirikisha washirika wake na kuita jambo hilo wanalifanya wote! Pengine utasema ilikuwaje akasema “…Natuumbe mtu kwa mfano wetu” je, malaika nao ni mfano wa Mungu kwa vipi? Ndiyo, nao ni mfano wa Mungu! Ndiyo maana Mungu akasema “kwa mfano wetu” je, mfano wa Mungu ni upi au mfano huo ni nini aliotufanya nao ambao na Malaika pia wanao? Jibu tunalipata katika Efe.4:23-24, inasomeka hivi “Na mfanywe wapya katika roho ya nia zenu; mkavae utu mpya, ulioumbwa kwa namna ya Mungu katika haki na utakatifu wa kweli” Mfano wa mungu tuliyoumbwa nao na ambao na malaika, na hata Lusfa ambaye sasa ni Ibilisi na shetani alikuwa nao ni HAKI NA UTAKATIFU WA KWELI! Kwasababu ya mda ningekuolodheshea maandiko mengi tu yanayokubali kuwa Mungu ni MMOJA tu!

 43. Wapendwa naamini kuwa hamjambo, nilitaka kulaumu kwanini sikuwa nanyi wakati wote katika kujifunza Neno hili la MUNGU; lakini nikakumbuka lile andiko kwamba:- “…..kila jambo lipo kwa wakati wake kwa makusudi ya Mungu” Kwakweli mmeendelea sana! Lakini mimi nimevutwa sana na mjadala juu ya T.B Joshua, kikubwa nimeona yapo makundi matatu makuu ya wachangiaji; Moja, wapo wanaosema kuwa T.B Joshua NI Nabii wa kweli wa Mungu! Pili, wapo wanaosema kuwa T.B Joshwa SI Nabii wa kweli wa Mungu! Na tatu, wapo “wanaosikilizia” upande gani utashinda katika mjadala kisha wajiunge nao – yaani hawako upande wowote – MAANA hawana habari kuwa HATA SASA MANABII WAKO, wanadai kuwa huduma hiyo ilisha koma!
  Kwanza, NAKUBALI KUWA T.B Joshua ni NABII! Nakubali hivyo kwasababu Neno la Mungu ndiyo kweli (Yoh. 17:17). Neno la Mungu linasema, kutakuwepo na manabii katika Kanisa 1Kor. 12:28, Efe 4:11. Kwahiyo, swala la kuwepo manabii ni la wazi kwamba, watakuwepo! Kwakuwa Neno linasema kutakuwepo Manabii wa KWELI (1kor. 12:28, Efe. 4:11) ni wazi pia na wauongo wametajwa na Neno hilo hilo kuwa kutakuwepo (Math.24:11), Kama huamini hilo kwanini unajiita mfuasi na muumini wa Biblia? Eleweni kwamba DHAMBI NI KUTOLIAMINI NENO LA MUNGU. Sasa, Kwa wanaokataa kuwa manabii hawapo – yaani eti huduma ya unabii ilishakoma jibu lao ni hilo!
  T.B Joshua ni nabii, na kwakweli ni Nabii; Swali, ni nabii WA KWELI au WAUONGO? Kujua vizuri hilo ni lazima uwe na kipawa cha ROHO MTAKATIFU, na kupata kipawa chake nilazima utekeleze au uende sawa na ile Mdo 2:38, Ila kama mtu aking’ang’ania uongo mwache apotee! Maana kweli imeondolewa. (Rum. 1:25) Hakuna ujanja tunapaswa kufuata Neno la Mugu kama lilivyoletwa ili kanisa la kweli la Mungu lifuate (Efe.2:20) Watu wengi, ukisemwa yaliyo kinyume na wanavyoamini, utawasikia wkisema, unahukumu au usimnenee mabaya mtumishi wa Mungu bila kujua kuwa hukumu au uzuri au ubaya unapimwa kwa Neno la Mungu. Vigezo vikubwa vinavyomfanya mtu kujulikana kama ni Nabii wa kweli wa Mungu, licha ya Neno au Ujumbe au Unabili wake utimie, ni LAZIMA uwe unatoka kwa Mungu na pili, mnenaji AONGOZWE na Roho mtakatifu!(2Pet.1:21) Unaweza kuona kuwa umuhimu wa unabii ni kutoa ujumbe wa KUSUDI la MUNGU, Umabii unaotolewa kwa njia za kama kinajimu najimu hivi, usiolenga lolote katika ukombozi wa mwanadamu kutoka Dhambini unaozungumzia matukio, majanga, mikasa au utabili wa habali isiyowaziwazi na sahihi yaani ya kubahatisha bahatisha hivi, haitokani na uongozi wa Roho Mtakatifu. Kutabili kuwa mtu atakufa au ajari ya Ndege n.k, bila kuainisha kuwa katika kifo hicho na au Ajari hiyo Mungu anataka nini, au hilo tukio linatokea ili iwe NINI KIROHO, Nabii au mtabili anabaki kimya, ni wazi kwamba ujumbe huo si wetu sisi ila alipaswa kuwafuata aliowatabilia akawambie unabii ule! Sasa jiulize Kufa kwa Saitoti au Ndege kuanguka kunakusaidiaje kiroho?! Maana hakuna maonyo au maelekezo yoyote toka kwa huyo mungu wa mnenaji akitutaka tuache nini ili Helkopta isianguke Kenya? Jiulize kuwa, Nabii T.B Joshua alisema kuwa; Tulipaswa KUACHA DHAMBI gani ili ajari ile isitokee kama ilvyotokea? Binafsi naomba kusaidiwa ili nijue na kisha nielewe hivi; Iwapo, unapotolewa unabii wa tahadhali au wa maonyo, Watu hutakiwa wafanye toba au watu wafanye maombi ili kuepusha kusudi la Mungu? – Maana nasikia Nabii T.B Joshua aliwataka watu wafanye maombi alipopata unabii wa Ajari – Nisaidieni hayo nijue, Hasa nikiwaona ndugu zangu MILINGA na JOHN PAUL Nitafurahi sana. Nitapanga nikatembelee na kuiona huduma ya Nabii huyu siku moja.

 44. Mpendwa Lwembe, Usinitake nikushangae.

  Unasema umeshindwa kuliona andiko linalosema Roho Mtakatifu alishirikiana na Mungu Baba na Mungu Mwana Kuumba ulimwengu?

  Mbona siku zote mimi nilikuwa nakujua kwamba wewe una bidii ya kunukuu maandiko na kututaka pia tuyafuate kwa bidii na yakae kwa wingi ndani yetu. Lakini kama umweza kunukuu “Faith Statement ya kanisa la SCOAN” lililoko nchini Nigeria ukasema hujawahi kuona Statement hiyo imenukuliwa kutoka maandiko gani? Mimi napata wasiwasi. Hata kama umesema uko hapa kujifunza bado nakuona kama uko zaidi kutoa “critisism” kwa watumishi mbalimbali wanaoshabikiwa na watu “whether their doctrines are cults or not cults”. Provided that they seem to be “Charismatic”
  or not.

  Lwembe andiko la Mwanzo 1: 26 linalosema, “……Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi…….” Haujawahi kulisoma kweli? Kama umelisoma unataka kuniambia kwamba halisemi kuhusu UTATU WA MUNGU ulioumba dunia na viumbe wote akiwemo mwanadamu?

  Lwembe, hujasoma andiko la Mwanzo 1:1-2; panaposema, “…Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi. Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji?”.

  Unaposema hujaona hiyo Kaulimwongozo wa Imani ya kanisa la SCOAN (Faith Statement) unataka tuanze kukufikiri kuwa unatutega au unafanya makusudi?

  Hivi Lwembe umeshasoma “Church Faith Statements” za makanisa mangapi. Hilo kanisa lako lina “Faith Statement”?. Hivi umewahi kupitia “Faith Statements” za makanisa ya Tanzania? Hebu fanya utafiti wa hilo ujisomee uone madudu yaliyomo humo. Mengi kati yao hayaendani hata na Maandiko kabisa. Wengi hujitungia tu kama katiba za mashirika ya kiraia (CSOs). Wapo ambao wametunga hizo uitazo “Faith Statements” lakini ukifuatilia mwenendo wa makanisa hayo hauendani kabisa na hizo statements. Ni sifuri. Ni sawa na katiba ya kawaida.

  Mimi nadhani tujadili Hoja zaidi iliyopo hapa. Je, TB Joshua ni NABII WA UKWELI au NABII WA UONGO?

  Wale wanaosema TB Joshua ni Nabii wa Kweli wa Mungu aliye hai; hawa wanatumia vigezo gani vya maandiko? Kama unaunga mkono Joshua kuwa ni Mtumishi wa kweli wa Bwana na ni NABII KWELI KWELI, unatumia Vigezo gani? Una Hoja ngapi? Siyo maneno matupu. Tueleze HOJA NYINGI UWEZAVYO siyo maneno mengi.

  Wale wanaosema TB Joshua anatumikia “mungu tumbo” au anafanya maigizo tu au tuseme ni NABII WA UONGO wala hana lolote, wanaosema hivyo watuambie pia hoja zenye nguvu kutoka kwenye maandiko. Tupatieni hoja kali na siyo maneno makali. Tupatie Hoja nyingi kadri uwezavyo na wala siyo hoja ya maneno mengi. Usitupatie meneno mengi. Tupatie HOJA NYINGI ZENYE NGUVU.

 45. Naam, ndg John Paul, Asante!

  Jibu kwa hilo swali la kwanza kuhusu zile Huduma 5 ni kwamba, kama ulinielewa vizuri pale nilipozungumzia mfumo wa kanisa lililopo sasa hivi, na tofauti zetu za mafundisho, nazo Huduma hizo 5 zikiwa ni udhihirisho wa Uongozi wa Roho Mt., ninaamini kuwa kusanyiko kama kusanyiko likiwa katika mafundisho yasiyokidhi Agizo la Neno LOTE, Huduma zitakazokuwepo hapo zitakuwa ni zile za asili ya teologia inayoliongoza kusanyiko hilo ingawa ndani yake wanaweza kuwamo individuals ambao Roho Mt. ataendelea kushughulika nao hata awafikishe katika ile Kweli.

  Kwa sehemu ya pili ya swali hilo nitasema hivi, katika mambo yote ya Mungu, ili yaeleweke vizuri, NI LAZIMA utoke katika mwili kwanza, kisha uyatazame kutoka ulimwengu wa Roho ndipo hueleweka kirahisi. Huduma hizi 5 ni za Roho Mt., kwa hiyo zinapodhihirika, waaminio huyapokea madhihirisho hayo kutoka kwa Mungu na si kile chombo kinachotumika! Kwa hiyo Huduma hizo 5 ni lazima ujue pia kuwa zinaweza kuigizwa, na hapo ndipo unakuja umuhimu wa Neno la Mungu kujaa kwa wingi ndani yetu ili hilo Neno (Mafuta) lililomo ndani yetu lizipambanue Huduma hizo na kutuondolea waigizaji kati yetu. Muujiza mkuu katika uongozi wa Roho Mt ni kwamba yeye huwaongoza katika vipawa na pia huwaongoza waaminio kuyaamini yote, ukiiangalia nukuu ya 1Yoh 2:27 katika mchango wa ndugu Sam au katika biblia yako, itakupa picha kamili ya jambo hili, ndipo kiu ya kweli ya kuwa na Mafuta hayo yaweza kuzaliwa ndani yako, maana hayo ndiyo Mwalimu mwenyewe!

  Kwa sehemu ya 3, jibu ni NDIYO, vipawa vyote ni vya KWELI.

  Jibu kwa swali lako la pili, ni kweli, ukiyapokea Maandiko katika maana ya kuyaamini, basi Nabii atakaye kuja kulingana na hayo Maandiko uliyoyaamini utampokea, maana ndiye udhihirisho wa yale uliyoyaamini, naye Roho Mt akiwepo kukushuhudia jambo hilo kama tulivyosoma katika 1Yoh 2:27.

  Kuhusu personality ya huyo nabii ni kama nilivyosema hapo juu, yeye anenapo kusanyiko humtambua kuwa ni Roho Mt na si kumtukuza huyo chombo kama desturi ya kanisa la leo ilivyo.

  (Bali kuhusu yule “Nabii ajaye”, nakumbuka ulikwenda kunywa maji, kama ndio umerudi, karibu!!)

  Kwa swali la 3, Statement of Faith ya SCOAN inasema hivi: “The Holy Spirit worked with the Father and the Son to create the world.” Tafsiri ya karibu ya kauli hiyo kuhusu wanachoamini ni: “Roho Mtakatifu alishirikiana na Baba na Mwana kuumba ulimwengu.”

  Nimelitafuta jambo hilo katika Maandiko sijaliona, kwa vile sote tuko katika kujifunza, nitafurahi sana tukisaidiana katika hilo!

  Ubarikiwe!!

 46. Ck Lwembe ubarikiwe sana kwa maelezo yako na japo wapo watu ambao wanakataa ukweli na kuendelea kuwa ni mashabiki wa watu badala ya kumshabikia Yesu na kumwinua yeye. Hakika Roho Mt ndiye nabii wa kweli na neno la Mungu ndio ufunuo halisi wa unabii wa sasa. Tujaribu kutofautisha manabii wa zamani nyakati zile wanatabiri ilikuwa Roho mt anakuja na kuondoka, lakini baada ya ujio wa Yesu na kumwacha Roho Mt kama msaidizi mkuu, watu wote wanaomwamini na kumpokea Yesu na kujazwa Roho Mt wanapokea vipawa na karama tofauti. Unabii wa leo lengo lake ni kuonya, kutia moyo na kulijenga kanisa, soma 1 Kor-14:1-5. Sasa unabii wa T.B Joshua una sehemu gani katika kanisa la leo kama sio roho ya utambuzi ambayo inatafuta kupendwa na kuaminiwa na watu wasiokuwa tayari kuamini neno la Mungu bali wanavutwa kwa ishara na miujiza ambayo wengi wamepotea kwa kukosa mizizi ya neno la Mungu ndani yao. Mungu atusaidie.

 47. Nashukuru ndg Ck Lwembe kwa maneno yako. Jambo kubwa kuliko yote hapa ni kuwa, Sote tunamhitaji Mungu.Na ninaamini kuwa kila anayesoma hapa na kuchangia kaika mada mbali mbali, ana lengo la kujua zaidi HABARI ZA MUNGU wa kweli. Hilo ndilo shauku langu na ninaamini ni shauku la kila mmoja!

  Nashukuru pia kwa ufafanuzi wako, ambao unazidi kunipa mwanga kwa nini tunatofautiana katika baadhi ya mambo. Lakini yamesisitiza kile kile ambacho hatuwezi kupata jibu!

  Kwa sasa naomba nikuulize maswali matatu 3. Mi hupendelea kunukuu ndipo nauliza swali:

  1. “Kila kusanyiko lapaswa kuwa na hizo huduma 5, kama halina linapaswa KUFUNGWA!!!!”

  – i). Kwa hiyo unataka kusema kuwa KWA SASA HATUNA KUiSANYIKO LENYE HUDUMA HIZO 5?

  Na kama lipo, basi hapo kutakuwa na NABII WA KWELI. Sidhani kama ni sahihi tukisema hapo kutakuwa na Mwinjilisti (mtu), Mwalimu (mtu), Mtume (mtu), Mchungaji (mtu) halafu eti Nabii (ROHO MTAKATIFU)??????? Bwana alipoleta vile vipawa aliweka wengine kuwa Mitume, Wainjilisti na wale wengine pamoja na MANABII WATU! Na ni Roho Mtakatifu NDIYE ANATENDA KAZI NDANI YA WOTE HAO.

  iii). Au tuseme kila kusanyiko lenye zile huduma 5, basi NABII aliyeko hapo NI WA KWELI?

  2. “myapokee Maandiko kwanza ndipo mnaweza kumpokea Nabii ajaye kulingana na Maandiko”

  -Kwa hiyo “Nabii ajaye” ndiye Roho Mtakatifu??

  Naomba majibu ya hayo maswali

  3. “lakini kigezo kikubwa ni ule UKIRI wa IMANI yake, haumo ndani ya Biblia”

  Hebu, kwa faida ya mtu anayefuatilia mazungumzo haya, FAFANUA japo kwa ufupi UKIRI WA IMANI YA T.B JOSHUA mbao HAUMO katika Biblia.

  Asante.

 48. Ndugu John Paul,
  Asante sana kwa mchango wako wenye changamoto kubwa kwa kila mmoja wetu!

  Kwa kiasi fulani naona umekwazika sana katika majibu niliyokupa hata naona unaniona ni kama mtu niliyekutega katika nia ya kujionesha ujuzi wangu wa Maandiko, lakini hayo si hivyo, na sijawa na nia kama hiyo katika wakati wowote ule. Huenda ni katika conflict tu ya mtazamo wa jambo tunalolijadili hata tumefika katika hali hii! Basi ndugu yangu tunayo yaongelea yana thamani kubwa kuliko tofauti zetu, hivyo nikushukuru kwa kuyasema uliyoyasema na pia nikuombe msamaha katika yote niliyokukwaza nikiamini kuwa Roho wa Kristo ataendelea kutuongoza katika kujadiliana tukiwa katika ufahamu kamili wa kwamba hatumshambulii mtu yeyote yule, hata nabii Joshua katika mjadala huu, bali tunaitazama Huduma yake katika ulinganishi na Neno la Mungu kama tunavyoweza kuitazama Huduma nyingine yoyote ile!

  Katika swali uliloniuliza kwamba, “kama una mfano wowote wa Nabii aliyeko sasa ambaye Alitabiriwa katika Maandiko. Itakuwa vizuri sana, kwangu”.
  Labda niseme hivi, kwamba swali kama hili likipatiwa jibu kama unavyonitaka mimi Lwembe nilitoe, jambo hilo litakuwa haliendani na Maandiko, kwani nitakuwa natumia akili zangu katika kuelezea Neno la Mungu, jambo ambalo litawatoa katika mawazo ya kuyawazia yaliyo ya Mungu na kuingia katika yasiyo na faida.

  Pia nimeona wapendwa wengine wakiwa na shauku kubwa ya kumjua Nabii wa Kweli aliyeko leo hii. Mimi nadhani shauku hii si ya kweli, bali ni hali iliyowapata wafuasi wa TB Joshua baada ya kuambiwa kuwa huyo ni nabii wa Uongo! Kwa hiyo katika jazba wanajaribu kuniuliza nabii huyo ni nani ili nao wapate fursa ya kusema wanayoyataka. Tena shauku hiyo ime override Neno la Mungu, maana simuoni yeyote anayetaka kulisikiliza, wote wanataka kutusulubisha sote tunaomkataa! Pia hili ni la kutegemewa, kwa hiyo mimi sishangai sana.

  Hata hivyo, napenda nitoe maelezo machache kuhusu swali mnaloniuliza ili itusaidie sote kupata uhakika wa jambo hilo la kumjua nabii wa KWELI aliyetabiriwa aliyepo leo hii. Katika hili la manabii kutabiriwa, ni vizuri mkafahamu kuwa hata hao wa Uongo waliopo leo hii, si kwamba wapo tu, la hasha, hawa nao wapo kulingana na Maandiko yalivyowatabiri kuwepo, kwa hiyo wanafanya kazi zao kulingana na Programu ya Mungu, kwa sababu kama watu hawatadanganywa basi Neno la Mungu LITAPUNGUKIWA!

  Kwa hiyo basi, katika ujumla wake, jambo hili la MANABII, kulingana na Maandiko, linapaswa litufikishe katika kiwango hicho tunacho kiogopa cha kutenganishwa mafungu mawili tungali tukitembea hapa duniani; KONDOO na MBUZI, yaani kule “KUWEKANA KUUME na KUSHOTO!!! Basi unapojikusanya kwa nabii yeyote yule, hata liwe ni dhehebu, unapaswa ujue kuwa Neno hilo ndio linakutimilia!! Kwa hiyo suala la kujua iwapo Nabii wako au dhehebu lako, kama wanawakilisha Neno LOTE la Mungu, lina umuhimu mkubwa sana kuliko wengi wetu tunavyodhania au kulichukulia. “Mtu hataishi kwa mkate pekee, bali kwa KILA NENO LITOKALO KATIKA KINYWA CHA MUNGU”, nayo Biblia ndio NENO hilo, kulikataa katika sehemu yoyote ile, kama kwa yule anayelipokea LOOTE, wawili hao hutenganishwa hapo kwa kadiri ya NGUVU ya UTENGANISHO inako kuvutia! Kinachovutwa kwanza ni roho, kisha mwili huifuata roho iliko, ndivyo mambo haya ya rohoni yanavyotendeka!

  Pia ni vizuri kuelewa kuwa mfumo wa kanisa uliopo leo hii SI mfumo wa ki Biblia ingawa unajiwakilisha hivyo. Jambo hili pia ni sehemu kubwa ya tatizo katika uelewa wa utendaji wa vipawa na mahusiano baina ya makundi yetu. Mfumo wa kanisa uliopo ni wa kidhehebu, nayo makusanyiko yetu madogo madogo huwa ni matawi ya hilo dhehebu. Lakini katika mfumo wa ki Biblia kanisa huwa halina MAKAO MAKUU zaidi ya Roho Mt. nalo huwa kamili yaani sovereign. Ndipo zile Huduma 5 zilifanya kazi katika makusanyiko hayo, na mipaka ya huduma hizo ilikuwa ni makusanyiko yao na hayo mapya watakayoyaanzisha katika kuyalea, yakikomaa, Mungu huwateremshia vipawa humo pia, maana ni wanae! Kile kipawa cha Nabii ambaye nilisema mwenye Neno la wakati ambalo huifunga dunia yote, huyu ujio wake lazima uwe umetabiriwa katika Maandiko, maana huyu huja katika NJIA PANDA ya wakati kuliongoza Kanisa looote la Mungu katika uelekeo mpya kulingana na Programu ya Mungu. Nabii wa kipawa hiki huwa ni MMOJA TU katika wakati! Kristo alikuwa ni Nabii, basi walipokutana na Yohana Mbatizaji, waweza kumuona Yohana akikiri kuwa yeye sasa yampasa kupungua!

  Hiyo ndio tofauti ya utendaji wa kipawa hicho katika jinsi hizo mbili. Ya kwanza ndio hiyo inayopaswa kuwepo katika kila kusanyiko linaloongozwa na Roho Mt., na ile ya pili huja katika wakati huo kanisa linapoifikia Njia Panda ya Wakati, akilitoa kanisa katika ibada zilizokengeuka na kulipeleka mbele utukufuni, na huyu huwa ni MMOJA TU. Basi mnaponiuliza nabii wa kweli leo yuko wapi imeniwia vigumu kulijibu kama mnavyonitaka katika uelewa uliopo leo hii ambapo manabii hujiinukia na kuwaitia watu waende huko, na kwa wito wao huo hudhihirisha uhaba wa vipawa hivyo katika makusanyiko yetu nasi kuishia kuaminishwa jambo hilo kinyume na Maandiko. Nao manabii wenyewe kila mmoja hujiona na kujitambulisha kuwa ni yule wa kundi liifungalo dunia, lakini huduma zao huishia katika kiwango cha wale wa makusanyiko madogo na kwa kiasi kikubwa hata kiwango hicho hawakidhi. Kila kusanyiko lapaswa kuwa na hizo huduma 5, kama halina linapaswa KUFUNGWA!!!! Yaani kwa maana rahisi ni kwamba, kusanyiko hilo haliongozwi na Roho Mt.!

  Kwa hiyo ukiitazama hali iliyopo leo hii na ukailinganisha na mfumo halisi wa ki Biblia, basi mnaponiuliza nabii wa Kweli aliyetabiriwa yuko wapi, licha ya kuwaambia kuwa Nabii wa Kweli ni Roho Mt., imenishangaza kidogo. Mnataka niwaoneshe mtu, yaani mnataka ishara, mnamtafuta mtu wa kum idolise! Labda niwaulize, ninyi mmemjulia wapi Roho Mt.? Maana ninamsikia kila mmoja wenu akimzungumzia Roho Mt. lakini inapofikia katika kuyatii Maandiko, wote mnageuza vichwa na kuendelea ktk mambo yenu! Ndio maana nawashangaa mnavyoning’ang’ania niwaoneshe Nabii wa kweli!. Najiuliza, mtampima kwa kipimo gani, maana Maandiko mnayaamini nusu, hata kung’angania kwenu kuwa Injili ya kuwajua manabii wa Uongo peke yake si Injili, ni udhihirisho wa hilo. Hivi kama kumjua Nabii wa Uongo ingekuwa ni rahisi kama mnavyowazia, basi Mungu angekuwa na haja gani ya kulitahadharisha Kanisa lake zaidi ya mara moja? Maana anasema kama siku zisingefupishwa asingepona mtu! Hivi, hata nikikuonesheni Nabii wa kweli, mnadhania mnaweza kumpokea? Msijidanganye, zishindeni kwanza nafsi zenu, myapokee Maandiko kwanza ndipo mnaweza kumpokea Nabii ajaye kulingana na Maandiko, maana kwa kuyaamini hayo mmempokea tayari! Lakini Maandiko hamuyaamini, mtakosaje kumuamini nabii aliye nje ya maandiko nanyi mna kiu ya kuabudu? Hizo aya za Quran na hizo ibada za “Damu ya Yesu” si issue kubwa sana, kwa medium yeyote yule, ungeyategemea hayo na mengine mengi tu, lakini kigezo kikubwa ni ule UKIRI wa IMANI yake, haumo ndani ya Biblia, kwa hiyo yeyote anayefundisha au kukiri ambalo halimo humo ni NABII wa UONGO!!!!

  Nisiwachoshe kwa maelezo marefu,

  Bwana atujaalie utayari wa kulipokea Neno lake lote!

 49. Wapendwa,

  Nimefuatilia mjadala huu sana. Nashukuru Mungu kwa waliounga mkono maoni na uelewa wangu kuhusu TB Joshua na mafundisho yote kuhusu Manabii na Unabii.

  Naomba nimpongeze sana Kaka John Paul. Huyu kaka amenikuna moyo wangu. Kaka Paul asante sana kwa kuendelea kutoa darasa kwenye meza hii ya mjadala huu. Mimi nilikaa pembezoni kidogo ili nijifunze zaidi.

  Point kubwa ambayo John Paul umenikuna ni ile ya kuwataka wapendwa wenye MLENGO wa kukataa mafundisho na Unabii wa TB Joshua na wengineo duniani au Tanzania (kama wapo) kwamba watueleze upande wao ni upi.

  Kwamba kama wewe unasema fulani ni Nabii wa tumbo lake tu na wala mafundisho na utendaji wake wa kazi ya Mungu hawaukubali na kwamba watu wote tujihadhali na Manabii wa uongo, SASA WATUELEKEZE NI WAPI KULIKO NA MANABII WA KWELI IWE TANZANIA, USA, NIGERIA, UK, INDIA, UFARANSA, KOREA, CHINA , nk.

  Mbona sijawahi kuwasikia wapendwa akina Edwin Seleli, akina CK Lwembe, akina Orbi, akina Sam na wengine wanaopingana na manabii kama akina TB Joshua wakituelekeza ni wapi penye mafundisho ya kweli iwe Tanzania au nje ya nchi hii?

  Unapofuatilia mahubiri ya Mzee Moses Kulola kupitia Star TV kila wiki huwa wanapomalizia kipindi chao wanamwelekeza muumini mpya atafute kanisa la EAGT lililoko karibu naye na kwamba akilikosa ndipo aweze kuelekea makanisa mengine ya kiroho, mbona nyie wapendwa hamfanyi kazi hivyo? Waumini wachanga au tuseme wapya katika Wokovu huwa mwawaambia waende kusali wapi? Au mwawaambia watulie hapo hapo walipo wasitangetange?

  Hivi hapa Tanzania kuna Nabii wa kweli? Unaweza kumtaja jina na jina la huduma yake? Huko nje ya Tanzania je, kuna Nabii wa kweli? Anaitwa nani? Kama yupo unatumia andiko lipi kumtangaza kuwa ni NABII WA KWELI? Swala la kukazania kuwa tuyaangalie maandiko yanasemaje kuhusu Manabii na tuendelee kuchunguza maandiko kwamba yanatosha kuthibitisha NABII WA UONGO NA WA UKWELI nakubaliana nalo. Lakini unatumia andiko gani katika kufikia mwafaka moyoni mwako kwamba funali sasa nimekubali ni NABII WA KWELI wa Mungu?

  Mpendwa CK Lwembe na Sam, naomba jibu HAPA TANZANIA AU AFRIKA MASHARIKI NA KATI KUNA NABII WA KWELI YEYOTE UNAYEMFAHAMU? JE, NJE YA AFRIKA MASHARKI NA KATI YUPO KWINGINEKO AFRIKA? AU NJE YA AFRIKA JE, YUPO?

  Kama yupo; umetumia kigezo gani kumkubali? Naomba majibu.

  Mwisho, NAOMBA wapendwa wote turudi darasani kujifunza kazi za HUDUMA TANO KANISANI.

  Soma maandiko na mafundisho kuhusu: MANABII WA KANISA na UNABII WA KANISA. Jifunze tofauti ya NABII na UNABII.

  Soma somo la: MITUME WA KWELI WA YESU KRISTO. Fanya upembuzi yakinifu na yakini kuhusu mitume bandia na mitume halisi (Original and fake apostles). Jifunce sifa za Mitume wa kweli kwa kuangalia mfano wa Paulo Mtume na kulinganisha na Mitume wa leo (kama wapo).

  Soma somo la: MANABII WA UONGO NA JINSI YA KUWATAMBUA. AU MANABII WA KWELI AGANO LA KALE NA JIPYA NA JINSI YA KUWATAMBUA kwa kutumia Maandiko na ushahidi wa mafundisho yao.

  Soma somo lihusulo mada ya : WACHUNGAJI WA KANISA(JINSI YA KUWABAINI WACHUNGAJI WA MSHAHARA NA WACHUNGAJI WA KWELI WA KONDOO.

  Soma kwa upana masomo yahusuyo: WALIMU WA KWELI NA WALIMU WA UONGO KANISANI.

  Soma somo la WAINJILISTI WA KWELI WANAOMTANGAZA KRISTO KWA HILA AU KWA UKWELI WA DHATI. Jifunze tabia zao na sifa zao. Peleleza kwa kina uone wanavyotofautiana. Tumia maandiko na mifano ya Wainjilisti wa ukweli kama akina Paul na Petro ili kulinganisha wainjilisti wa uongo wanaotumikia matumbo yao na wainjilisti wenye kiu na hamu ya kuokoa ulimwengu.

  Baada ya kuchimba mada hizo kwa kutumia Biblia, na vitabu vingine vya watumishi na mtandao wa intaneti, nk kulingana na muda ulionao, NAOMBA UJE UTUARIFU NI WAPI TWENDE TUKAABUDU NA KUKUSANYIKIA AU KUSALI PENYE NABII, TUME, MWALIMU, MWINJILISTI, MCHUNGAJI WA KWELI TANZANIA.

 50. Ndugu Sam,

  Nashukuru sana kwa maelezo yako ya kina. Lakinii hebu naomba tunendeee kuajdiliana kidogo. Na ninanukuu uliyoandika:

  “Nenda kwa mchungaji wako kamuoneshe kitabu cha Matendo ya Mitume, kamwambie una hamu ya kuona Mungu atakufanyia nini nawe ukibatizwa kama mitume walivyowabatiza wakristo wa kwanza”

  Sasa ndg yangu Sam, hapo ndipo nimekuwa nikiulizia pawekwe wazi! Lakini jambo hili limeonekana ni gumu, gumu kabisa! Nakubali na ninafahamu kuwa Roho Mtakatifu ndiye Mwalimu wa Kweli. Lakini Roho Mtakatifu hufanya Kazi kupitia Watu. Hafanyi kazi kutokea Angani. Hata mtu mwingine, ambaye hana Roho Mtakatifu, hutegemea mwenye Roho Mtakatifu ndiye amsaidie kumwelekeza namna ya Kumpata huyo RMT. Kuna matukio machache ya mtu peke yake chumbani mwake, kuneemiwa na Mungu, kwa sababu anazozijua Mungu mwenyewe, na kufunuliwa Habari za Wokovu na RMT. Lakini hii si kanuni kuwa basi kila mtu, peke yake anaweza kutokewa hivi. Ndiyo maana Yesu akaagiza Wanafunzi wake kuenenda Duniani kote, WAKIWAFUNDISHA WATU yale ambayo Yesu aliwafundisha. Na jambo hili liliendelea na sasa linaendelea kwa nguvu za RMT mwenyewe.

  Hao walipokuwa wanafudisha watu hawakuwaambia kuwa Roho Mtakatatifu atawaelekeza kuujua ukweli. Hawakujificha! Waliwaambiwa UKWELI nao WAKAJULIKANA kuwa Ni watumishi wa Injili ya kweli. Lakini kama kwa siku zetu HATUWEZI KUWA NA HATA MFANO WA MTUMISHI MMOJA AMBAYE TUNAAMINI NI WA KWELI, basi ni tatizo kubwa, kubwa sana.

  Unaona sasa unavyoniambia niende kwa “mchungaji wangu”. Mimi naami kabisa kuwa SITAKUWA SALAMA ikiwa mchungaji wangu huyo HANA ROHO MTAKATIFU katika utumishi wake, au kwa maneno mengine, ni mtumishi wa Uongo. Una uhakika gani kama mchungaji wangu ANAAMINI KATIKA UBATIZO WALIOBATIZA MITUME? Una uhakika gani kama mchungaji wangu anakubaliana na kitabu cha Matendo ya Mitume?

  Nanukuu tena:

  “Unaona , madhehebu yetu katika ujumla wake yanaweza kuwa hayahubiri Injili Halisi kama yanavyopaswa, kwa hiyo iwapo unalo Neno la Mungu kwa wingi moyoni mwako, utawajua kuwa ni manabii wa uongo, hiyo ndiyo ‘the short and long of it’”

  Sijajua ni kwa nini Msisitizo wako ni kuwajua tu wale wa UONGO. Mimi naamini kuwa mtu aliye na Neno la Mungu kwa wingi moyoni mwake, anaweza kuwajua manabii wa Ukweli na wale wa Uongo pia. Siyo kweli kuwa uwepo wa Neno moyoni ni kwa ajili ya Kujua wale wa Uongo tu!!

  Ngoja tu nifupishe kwa kusema kuwa siamini sana katika Ukristo huu wa kuona huduma za KUKOSOA TU lakini hakuna hata moja ya KUITIIA MOYO. Yaani mtu anaona watumishi wa KUWALAANI tu lakini hana hata mmoja wa KUMBARIKI. Kwamba mtu anakuwa na orodha ndefu ya WATUMISHI WANAOPOTOSHA watu lakini hana hata jina moja la mtumishi ANAYEFANYA KAZI YA MUNGU KWA USAHIHI. Kama tunaweza kuwa na ujasiri wa kuwataja wale wa UONGO, kwa nini tusiwe na ujasiri wa kuwataja WALE WA UKWELI?

  Mi naona hii ni chagamoto zaidi kwetu! Na ninaishia hapa, nitaendelea kufuatilia mada hii kwa kusoma michango ya watu wengine.

 51. Mmoja anayo imani bila hayo matendo na mwingine anayo imani pamoja na hayo matendo….IMANI BILA MATENDO IMEKUFA!

  Mimi ni kama baadhi ya wengine wanavyosema “KAMA HABARI NYINGI NI HIZI ZA KUSOMA NA KUSIKIA” basi hatuna haki ya kuhukumu wala kuzungumzia lolote. Kama una Roho Mtakatifu akakufunulia (kama inavyotakiwa) juu ya huduma, mtumishi fulani then una haki ya kusema hilo ipasavyo.
  Wapo wengi wanaopelekwa na upepo wa kusema kwa nguvu zao “hawa/huyu/yule ni (ma)nabii wa uwongo” kwa sababu ambazo wao wanaziona ni za “kimaandiko” but kupitia “hearsay”. Kwa mfano wanaosema kuna “andiko la Quran huko SCOAN”, ninaamini hawajawahi kuliona physicaly na kwa wale waliosikia habari zake hata maana yake hawaijui.

  NINI MAANA YA MUNGU MMOJA?
  Je biblia inasema kuna Mungu wangapi? Je hao wengine unaodhani ni mungu je wao ni Mungu? Yesu mwenyewe alisema Yuko Mungu mmoja wa pekee na wa kweli.-John 17:3 e.t.c.
  Ina maana mtu akisema ameokoka, anamuamini Mungu katika Kristo Yesu inabidi tumhoji sana, tena na tena kuwa Mungu huyo ni yupi basi, kwa maana rahisi hata mshirika mwenzako, mke/mume wako, mtu yeyote na Mchungaji wako yabidi uwe na mashaka ya Mungu wanayemuamini hata kama si mungu (other gods).

  Tuwe makini na “uelewa wetu kwenye maandiko”, nimekuwa ninajifunza na ninaendelea kujifunza kuwa “andiko huua bali Roho huhuisha”, andiko(neno la Mungu) pasipo Roho mtakatifu ni zero, pengine hata zero ina thamani labda niseme andiko pasipo Roho Mtakatifu ni upotevu.

  Mungu atupe neema ili tujifunze “iliyo kweli” kwa njia ya Roho wake wala si kwa “elimu” na “hekima na maarifa ya kibinadamu” bali kwa udhihirisho na uthibitisho wa nguvu ya Roho wa Mungu.-1Corinthians 2:3.

 52. Wapendwa,

  Mimi ninahamasika sana kila ninapoona mamlaka tuliyopewa na Mungu ikitumika kuwakomboa watu walioonewa na shetani.

  Kila ninapoona mapepo yanapiga magoti mbele ya “wise men” na mbele ya Prophet T. B. Joshua, Ninamtukuza Mungu na nina pata somo la wazi kabisa ya kuwa Kila goti litapigwa na kila ulimi utamkiri Yesu.

  TO SEE DEMONS TREMBLING AND BOWING THEIR KNEES BEFORE WISEMEN AND THE PROPHET T.B JOSHUA IS SO INSPIRING BEYOND WORDS.

  Hapa tunafundishana kwa maneno matupu, lakini Pale kwa T.B. Joshua Matendo Makuu yanathibitisha neno la Mungu!

  God bless T. B. Joshua and the SCOAN Ministry. Amen

  Indeed every tongue shall confess that Jesus is Lord and every knee shall bow before Jesus.

 53. Hakika adui namba moja na wapinzani wakubwa wa Yesu walikuwa ni wale walio jiona wanaelimu kubwa kuhusu biblia. Mtu anapo sema kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareth pepo toka, mnataka tuanze kuulizana Yesu yupi na roho yupi anatumika. Hili swala Yesu mwenyewe alisha lijibu wanafunzi wake walipompa taarifa kuhusu walio kuwa wanalitumia jina lake wakidai hawapo upande wao. Jamani wapendwa katika Kristo, akili ya binadamu ndivo ilivo, ukiamua kuchunguza upande wa hasi, kila kinachofanyika utakichukulia hasi. Katika kuhitimisha kuhusu ni roho yupi anayetumika ni vizuri kuwa makini sana usije ukaingia kwenye mtego wa kumkufuru Roho Mtakatifu ambapo msamaha wa hiyo dhambi haupo.

  Inasikitisha kwamba tunatumia taarifa kumkashifu huyu nabii ambazo walio zipublish wengi wao wameshaomba misamaha hadharani. The problem with people are too theoretical, anyone coming up practical will look strange to them. People, bible is for doing not just talking, Love is the major thing Jesus talked about if you want to identify yourself as of him, why are you hating TB JOSHUA? Ona sasa tunataka hata kukasirikiana sisi wenyewe kwenye haya majadiliano wakati yeye yupo kanisani anasaidia watu. People ufalme wa Baba yetu wa mbinguni haujipingi kiasi hicho! Pia anaye taka kufanya hitimisho juu ya huyu Nabii, namshauri aende Nigeria ili atuletee mambo yanayo eleweka, sio kusomba vitu ambavyo watu wameandika kwenye mtandao na kuanza kutoa hitimisho. Naona kwa maelezo ya wengi hapa inaonekana wanakubali kuwa Yesu alikuwa anatoa pepo kwa nguvu za Beelzebub!!!!!!

 54. Unajua ndugu John, ni vizuri kwenda na wakati. Si wakati wa kidunia, hapana, twende na wakati wa kimaandiko. Tujaribu kuyasikiliza yanachotufundisha. Sikio lenye kusikiliza hujifunza jambo.

  Ukristo wetu umegawanyika sana. Jambo la kwanza tunalotakiwa kulikubali ni huo mgawanyiko. Pia twapaswa kujua kuwa katika mgawanyiko wetu hatuaminiani! Bali sisi hufungamana pamoja kwa ajili ya kupata NGUVU ya kisiasa pale tunapotaka kupata mpenyo serikalini. Kwa hiyo, kimsingi hata huu mjadala tunaoendelea nao, unatokana na hali hiyo. Basi kuitambua hali huturahisishia kujua jinsi ya kuenenda na mahusiano, hata kama yatakuwa ni ya kinafiki! Hiyo ndiyo hali ya Ukristo, unafiki ni mwingi sana!!!

  Tukirudi katika Huduma, hizo ni nyingi sana na zinaendelea kuongezeka kila siku ndani ya Roho wa Migawanyiko. Msururu wa Huduma na vyeo vya wahudumu hao ni mrefu sana. Lakini kwa kifupi ni kwamba madhehebu yote na huduma za kimitume nakinabii kimsingi wote katika ujumla wa migawanyiko iliyopo, husimama kama MANABII kimantiki; kuanzia dhehebu la Katoliki mpaka huduma ya nabii Lwembe! Usijihangaishe kuyahesabu maana hata Mambo ya Ndani hawana hesabu kamili maana kila siku zinaibuka Huduma mpya, na kila mmoja akiwaitia watu waende kwake kwani yeye ndiye mwakilishi wa kweli wa Kristo!!! Na kwa vile haya ni yale Majira ya Udanganyifu, maroho yameachiliwa kutimiza hilo, kwa hiyo miujiza ni mingi sana; uponyo, utajiri, na mafanikio lukuki. Huu ni wakati ambao kunafanyika Ibada nyingi sana hata unaweza kudhania kuna UAMSHO! Kwa upande mwingine ni kweli huo ni uamsho wa kuwakusanya watu na kuwaingiza upotevuni!!

  Basi katika hali kama hii makundi yote yakirushiana shutuma, hata kunafikiana kwa serikali ili iwafungie makundi mengine, haja ya kujua ilipo kweli ni kubwa na yenye haki. Lakini haja peke yake haitoshi kumfanya yeyote yule aitafute Kweli ilipo. Utayari wa kuipokea kweli ndio catalyst kubwa ya kuinua haja hiyo. Kwani watu wengi sana hudhania wanayo haja ya kuijua Kweli lakini inapowafikia, hurudi nyuma kuipisha ipite, kama yule kijana tajiri, wakiyarudia yale mapungufu waliyoyaona pale walipoamua kuitafuta ile Kweli! Inasikitisha lakini hiyo ndio hali halisi.

  Hapo nyuma uliponiuliza hilo swali, nilikujibu kuwa, “Mtumishi wa kweli ni Roho Mtakatifu”; bado ninaamini kuwa hilo jibu ndilo sahihi kulingana na utumishi wa mungu katika kuihubiri Injili katika kiwango kilichokusudiwa. Pia pale unapokuwa na utayari wa kuipokea Kweli, basi utayari huo hukuleta katika kiwango cha kuliamini Neno la Mungu kikamilifu na kukuingiza katika UPENDO mkamilifu.

  Kwahiyo, ili kuyajua makundi yanayohubiri kweli yote ni lazima wewe mwenyewe kwanza uwe na uwezo wa kuyaamini Maandiko kama yanavyojifunua kwako. Pia uwe na uhakika kuwa muwajibikaji wa kwanza kwa Injili ni Mungu na si manabii wala maaskofu wakuu wala mitume au wachungaji nk. Ukifika hapo utakuwa umejiondoa katika kuwategemea watu na hivyo kujiepusha na laana. Ukijifunza kumtegemea Mungu, maana yake ni kwamba chochote kinachohubiriwa au kufundishwa na yeyote yule, haijalishi kutukuka kwake, basi utakigagua katika maandiko kama ishara ya kumuweka Mungu mbele, kikiwa sawa na Neno, utambariki mnenaji kikiwa tofauti utajua kuwa huyu hajatumwa na Mungu, maana Mungu anaowatuma huwapa Roho wake huyo aliyeiandika Biblia kwa hiyo Roho hawezi kunena tofauti na kile alichokiandika na kukifundisha!

  Usimwamini yeyote yule, kwanza hata hujui uvuvio wao wameupata wapi. Ndio maana tumeambiwa tuzikague roho zote! Kwa hiyo ndugu John, si kwamba ninaogopa kukuonesha mtumishi wa kimwili wa kweli ni yupi, hapana , bali ninaamini kuwa hata wewe waweza kuwa mtumishi wa kweli pindi utakapo kuwa tayari kuipokea ile Kweli katika moyo wako, si intellectually, bali katika moyo wako ili nafsi yako iwe regenerated. Ni katika hali hiyo tu ndipo unaweza kulipokea Neno la Mungu katika ukamilifu wake hata akakutenga na mambo ya dini, nawe ukawa JESHI. Wingi wa watu ukawa si jambo kubwa kwako bali Roho wa Mungu pekee ndiye Amani yako. Unajua kuna ule usemi usemao, “The Devil counts his crowd but God weighs His!” Hata Elia nabii alikosa kusanyiko la kwenda, lakini Mungu alimwambia wako 7,000 wasiompigia goti Baali. Unaona , madhehebu yetu katika ujumla wake yanaweza kuwa hayahubiri Injili Halisi kama yanavyopaswa, kwa hiyo iwapo unalo Neno la Mungu kwa wingi moyoni mwako, utawajua kuwa ni manabii wa uongo, hiyo ndiyo ‘the short and long of it’. Simama na Mungu, kama Kornelio, atakuletea akina Petro wakati wako ukifika, yeye ni Mungu, awapendao huwabariki!!

  Nenda kwa mchungaji wako kamuoneshe kitabu cha Matendo ya Mitume, kamwambie una hamu ya kuona Mungu atakufanyia nini nawe ukibatizwa kama mitume walivyowabatiza wakristo wa kwanza, hebu jaribu kutembea nchi hiyo kwa kutii Neno hilo,halafu ukirudi hapa kwenye blogu ninaamini utakuwa katika uelewa tofauti wa Neno la Mungu na utalipenda kuliko ulivyowahi kuwazia!

  Huo ndio ukweli ninaoujua, mtumishi wa kweli atakuongoza kuliamini Neno la Mungu lisilo ghoshiwa, yaani atakusukuma kumchallange Mungu kwa kuliamini Neno lake na kukaa hapo chini ya Miguu yake kusubiri chochote kile unachohitaji kwa ajili ya utukufu wake!!

  Hiyo ndiyo Challange yetu kwa siku ya leo, kumwamini Mungu kwa Neno lake na si kuunga katika msururu uliozinguliwa hata hawajui waendako ili mradi wamepumbazwa na miujiza!

  Nafasi ya kujifunza Mungu bado ametukirimia, karibu!!!

 55. Kwa ndg Ck Lwembe,

  Nitakuwa nanukuu kisha ninafafanua:

  1. “Ndio maana kila ninapowauliza ni wapi katika Maandiko nabii huyo alitabiriwa, sipati jibu. John anasema eti huyo ni wa Huduma 5, lakini tena anairuka kauli yake kwa kukiri kuwa wengi wanaifuatilia! ”

  -Mimi Kabla ya kujibu swali hilo nilihitaji ufafanuzi, ambao ndio umeuleta sasa. Sasa ni kosa gani nimefanya kwa kuhitaji kufafanuliwa swali, kama sikuwa nimelielewa vizuri?

  Nimejaribu kuangalia mahali ambapo “nimeiruka kauli yangu” ili nifafanue lakini bahati mbaya sikupaona. Lakini la msingi ni kuwa nami niliandika yale ninayofahamu, ili kama ninakosea nikosolewe. Ninajua kuwa Ukristo ni mpana, na hata inawezekana tukakubaliana kuhusu T.B Joshua lakini kumbe mahali fulani kuna meeengi ambayo yanatutofautisha. Kwa hiyo nadhani tukiandika kwa upole jinsi mtu anavyofahamu jambo fulani, tunaweza kufanya vzr zaidi kuliko kutegana, ama kuonyeshana nani anajua zaidi!

  “”””Lakini pia nitapenda sana kufahamu kutoka kwako ndg Lwembe, kama una mfano wowote wa Nabii aliyeko sasa ambaye Alitabiriwa katika Maandiko. Itakuwa vizuri sana, kwangu””””””

  2. “Lo, ndugu zangu, Injili yote hii inayohubiriwa, haijawafanyia lolote! Ni bora ukawa chini ya hawa manabii wetu uchwara wanaowakamua watu pesa zao kuliko huko mlikoenda, maana huko ndiko maandiko yanakotimia kwa uhakika kuhusu kudanganywa! Angalia makusanyiko yenu jinsi yamebakiziwa misukule baada ya nafsi zenu kutwaliwa katika ulimwengu wa roho na ngome hiyo”

  -Kwanza naona ndg Lwembe umekwenda mbali mno. Hapa tunajadiliana tu!. Ila najua shahidi wa mambo ya mtu ni nafsi yake mwenyewe. Kule kusema nafsi Yangu imechukuliwa msukule na T.B Joshua, una uhakika gani? Au unadhani T.B Joshua ana nafasi kiasi gani moyoni mwangu? Au unajua kusanyiko langu lina mtazamo gani kuhusu T.B Joshua? Mi nadhani, badala ya kuanza KUWEKANA KUUME na KUSHOTO ni vema tu tukajadili mada iliyopo kwa kufafanuliana USAHIHI au KUKOSEWA KWAKE. Tusije jikuta tunakosea!

  3. “kwa kifupi huo ndio ufahamu wangu kuhusu huduma hiyo ya Unabii katika utendaji wake kwa kadiri nilivyoyaelewa Maandiko”

  -Ni kweli kabisa kuwa kila mmoja anaandika hapa kwa kadri anavyoelewa. Hakuna Mungu kati yetu. Wote ni wanafunzi wa Yesu, tukiwa wote tunategemea Roho Mtakatifu huyo huyo, ambaye SI MALI YA MTU bali ni kwa kila mtu anayefungua moyo wake kwa ajili ya kumpokea.

  Na kile tunachoekwa basi, kama kinatofautiana, ndipo tunapata sababu ya kushirikiana, kusaidiana na kuelekezana katika Ukweli. Kama tungekuwa na uelewa mmoja, hakuna basi sababu ya kujadiliana hapa. Lakini twatakiwa kutambua kuwa mimi, Sam, Orbi, Nduta, Seleli kila mtu ana ufahamu tofauti, kutoka kwa Mungu na hata wa kimwili. Kwa hiyo kukutana kwetu hapa kutatusaidia ikiwa tutatambua tofauti hizo na tuwe tayari kusikilizana. Ili anayejua sana amsaidia asiyejua kabisa na yule anayejua kidogo naye aongeze ujuzi wake.

  4. “Je, nyie mnaokiri kwamba huyo ni baraka ya ulimwengu pamoja na ndugu John uliyesema unaifuatilia huduma hiyo, kama swali nililowauliza mmekosa jibu, mwaweza kutueleza lile bandiko la Qurani linalokiri kuwa “Mungu ni mmoja tu, Allah” lililobandikwa humo ndani ya Sinagogi hilo linawakilisha nini kulingana na Injili ya Kristo!!!”

  – Nimeandika kuwa mimi si kwamba NILIKOSA JIBU, lakini kabla ya kujibu nilikuwa nimehitaji ufafanuzi ili nisije nikajibu nisichokijua. Lakini badala ya kuja ufafanuzi niliouhitaji umekuja ufafanuzi na maelezo mengine marefu na kutoa hitimisho kuwa NILIKOSA JIBU LA SWALI HILO.

  -Kuhusu bandiko la Quran linalokiri kuwa “Mungu ni mmoja tu, Allah” lililobandikwa humo ndani ya Sinagogi mimi Nasema kuwa HAYO NDIYO MAMBO YA KUFUNDISHANA. Yaani ungekuwa umeandika hayo mapema ungekuwa umesaidia sana, kuliko kuja na mashambulizi.

  Sasa, kwa kule kusema kuwa mi nafuatilkia huduma hiyo ni kuwa nafuatilia kwa njia ambayo naamini siwezi kupata habari zote kuhusiana na T.B Joshua. Sijawahi kuwa pale, na sidhani kama kwenye TV Nukuu hiyo ya Quran huwa inaonekana. Kwa hiyo namfuatilia T.B Joshua kwa kiwango ninachokipata. Na si kwa kusema vile haina maana kuwa Mimi ni mfuasi wa huduma hiyo. Mi hufungua TV na kuangalia, kwa hiyo nikipata ninayopata, nachukua ninayoona ya muhimu na yale yasiyo ya muhimu, ikitokea nimeyaona, nayaacha. Kuna wakati nafungua mtandao, nasoma ninayoweza kuyapata, nachukua mawili matatu ninayoona yanafaa, na nikiona yasiyofaa nayaacha!

  Hebu niishie hapa kwa sasa!

 56. Ndugu Orbi,
  Kwanza nikushukuru kwa kunitia moyo, Bwana akubariki sana katika uyafanyayo kwa kusimama na Neno lake, yaani pale ulipo msikiliza Roho na kubaki ndani ya yale Mafuta!

  Ni kweli nimeukumbuka ule mchango wako kuhusu ile aya ya Quran iliyobandikwa humo ndani ya Sinagogi. Unajua ndugu yangu, Maandiko yana namna yake ya kutimia ambavyo huwa si rahisi kwa wahusika kufahamu hata wakimbie kutimiliwa! Kama tunavyofahamu kuwa mambo yote huanzia katika ulimwengu wa roho kwanza ndipo hujidhihirisha katika mwili. Basi ni muhimu kutambua kwamba huduma ya nabii huyu ni ya KIROHO, yaani ile aliyoisema mt Paulo – PRINCIPALITIES!!

  Kwa hiyo, huduma kama hizi, ambapo yale maroho yanajua hayana umbali sana wa kwenda, basi hufanya kejeli kweupe yakilidhihaki kanisa kadiri yanavyolivutia nje ya Neno la Mungu kwa miujiza, na kulitumbukiza kwenye maporomoko ya kuzimu, kama unavyoyaona mabandiko ya Qurani, lakini watu wamekuwa mesmerized na vituko vya miujiza hata hawana tena macho ya kuona wala akili ya kufikiri! Wokovu wote waliokuwa wakijisikia umewaondokea, wametekwa upande wa pili na sasa wanaipigania huduma iliyo NJE ya UTENDAJI wa ROHO MT na HAWAJUI!!!! Kila mmoja akimtukuza kivyake!

  Lakini Neno la Mungu lile walilodai Wokovu kwalo linasema hivi, “Nanyi, mafuta yale mliyoyapata kwake yanakaa ndani yenu, wala hamna haja ya mtu kuwafundisha; lakini kama mafuta yake yanayowafundisha habari za mambo yote, tena ni kweli wala si uongo, na kama yalivyowafundisha, kaeni ndani yake” (1Yoh 2:27). Roho anatusisitiza tukae ndani yake jamani, tuutunze Wokovu wetu tuliokirimiwa, tusitoke humo, yeye anajua Shetani anatafuta kututoa humo kama alivyomtoa mama yetu Hawa! Yakimbieni hayo mazingaombwe!!!!!

  Bali, Mungu wetu ni Mwingi wa Rehema, basi ikiwa Rehema yake ingalipo kwa ajili yetu, twapaswa kuwaombea ili Mungu awatoe huko walikojiingiza kwa kuliacha Neno la Mungu lililojaa ahadi wakakimbilia mambo ya mwilini yenye kufisha!

  Bwana aturehemu!!

 57. Ha ha ha ha! Mh! Inafurahisha na kusikitisha sana.
  Hongereni kwa michango mizuri yenye changamoto na mafunzo mengi.
  Mimi ninaomba niseme hivi; Watu wanasisitiza saana “TUZIPIME / TUZICHUNGUZE ROHO”, hili ni jema na la msingi sana lakini swali kubwa kuliko yote ni “Je KIPIMIO chenyewe wanacho hao wanaotakiwa kupima?” Kimsingi mimi ninaendelea kujifunza kuwa wengi wa waitwao Wakristo hawana “KIPIMIO” cha kupima wachungaji , wainjilisti, walimu, manabii, mitume, marafiki, wachumba, wabia n.k walio wa uongo ama walio wa ukweli.

  Mungu atupe neema ya kuwa na “kipimio” kwani kama mtu akiwa hana hicho kipimio sio wake Mungu.-Romans 8:14.

  Mbarikiwe!

 58. Ndg Sam,

  Nashukuru kwa jibu lako, na nashukuru zaidi kwa ufafanuzi wa ndg Ck Lwembe, kwa ufafanuzi wa kile alkichokileta. Lakini kutokana na ufafanuzi huo, ninachoona ni kuwa kuna mda nyngine. Tulishawahi kujadili mtazamo huo, sikumbuki katikamda gani, ila ilikuwa inahusu mambo ya MANABII, ampo kuna mtu (Sikumbuki vzr kama ni ndg Lwembe] aliyemalizia kuwa “Anayesubiriwa sasa ni Nabii atakayetenda kazi kwa Roho ya Elia, ambaye atakuja kurejesha mioyo ya watoto iwageukie wazazi. Hata hivyo suala hilo halikufikia Muafaka mzuri.

  Sasa tunaposema kuwa ni wapi ambapo Nabii Joshua ametabiriwa kwenye Bible, nadhani baada ya majadiliano marefu, vyovyote vile, sidhani kama tunaweza kuona kwenye maandiko mahali ambapo Nabii ye yote aliyepo leo,atakuwa maetabiriwa kwenye Bible. nA MWISHONI tunaweza tu kukubaliana kuwa HAKUNA TENA MANABII KWA SASA!

  Vinginevyo tuelekezane basi ni Nabii gani ambaye anafanya huduma ya Kinabii, ambaye ALITABIRIWA KWENYE MAANDIKO MATAKAIFU? Kama hiyo ni siri, basi hii elimu ya KUFUNUA vitu vibaya tu halafu vile vizuri vinakuwa ni Siri ya mtu mwenyewe, sasa tutawasiaidiaje ambao wanahitaji kuelekezwa mahali palipo salama? Kumbuka: Kwa kuwa tuna maandiko mengi ya na Sababu nyingi za Kibiblia za Kumkataa T.B Joshua, angalau kama siyo kumkataa yeye, basi kuyakata mafundisho yake, HIVI KWA NINI TUSIWE NA HATA MTU MMOJA AMBAYE MAFUNDISHO YAKE TUNAYAKUBALI, kwa kigezo hicho hicho cha Biblia?

  Sina uhakika kama mtu akiisha kuhubiri mkutano wa injili, kisha akawaambia watu Mahali fulani msiende na pale na pale na kule, lakini Tafuteni wenyewe mahali mtakakokwenda kujifunza maneno ya Mungu, kama atakuwa sahihi. Hiki ndicho nakiona mnachotaka kufanya. Hapa tuko wengi tunaosoma hapa. Mi ni mmoja wa wengi, ambao hata hivyo ni mimi menyewe ndiye najua ni kwa nini nimeamua kukaa upande huu katika mjadala.

  Mtume Paulo katika Nyaraka zake, kuna mahali aliweka wazi kabisa kuwa fulani na fulani hawafai kwa kuwa wameshaiacha njia ya kweli; Lakini fulani na fulani hao ninawaamini, naujua moyo wao. Lakini hapa naona tunakuwa upande mmoja tu: Wa kuelekezana tu palipo na MAFUNDISHO YA UONGO, lakini hatuwezi kuelekezana Palipo na Mafundisho sahihi. Ni kwa nini Tunakuwa na UJUZI zaidi wa KUUTAMBUA UONGO ulipo badala ya UKWELI ulipo?

  Tulipoambiwa kuwa Tutawatambua kwa matunda, naamini kabisa maana yake ni kuwa, WA UONGO tutawajua na WA UKWELI tutawajua pia. Sasa sina uhakika, na sijuwi kama naweza kupata jibu la swali hili hapa kuwa HIVI, NI KWELI HATUNA HANATA MFANO MMOJA, ambapo mafundisho yake ni YA KWELI? Au wa UKWELI kila mtu ATAJUWA kutokana na Uhusiano wake na Mungu? Kama ndivyo sasa TUTAMWELEKEZAJE yule ambaye ndiye kwanza anangia katika Ukristo? ili aendele mahali salama?

  Nimefikiri mfano huu Mwalimu ye yote huwa anakifundisha anatoa na mifano sahihi. Hawezi kuwafundisha wanafunzi kwa kuwapatia majibu YASIYO SAHIHI TU kisha akawaabia majibu SAHIHI watajitafitia wenyewe.

  Hilo suala la Tanki la maji_Damu ya Yesu, mbona hata hapa Tanzania ni mengi tu? Hizo anointing water hapa ndiyo usiseme. Yako mafuta ya mizeituni mengi tu yanauzwa kwenye huduma nyingi. Juice mbali mbali kama vile Fruto, Chumvi. Ndiyo, najua twaweza kutangaza hadharani kuwa Huduma zoote hizo ni za Upotofu. Lakini tunaposita Kuelekezana kwenye mafundisho Sahihi hapo ndipo pananiacha niendelee kuwaza. Yani hatuna Ujasiri wa kuelekezana palipo sahihi lakini Tuna ujasiri mwiingi wa kuorodhesha sehemu zilipotofu.

  Ngoja tu niishie hapa.

 59. shalom,
  may ALMIGHTY GOD fogiv us all,TANZANIAS,because we dont knw the effect of our own WORDS,lets us use our own lips, to build and and not to destroy.,jamani tutumie sehemu kama hizi kuongea vitu ambavyo vitatujenga watanzania na kutuelimisha katika maisha yetu na kristo,

  Nina hakika kuwa hakuna hata mmoja wetu hapa mwenye HAKI ya kumnyooshea mwenzake kidole,the bible says every body lie to his neighbor who can we belive GOD.so if we ve to belive GOD.,HE himself INSTRUCTED US TO “JUDGE NOT”
  Wen Jesus say JUDGE NOT he was telling us not to JUDGE HYPOCRITICALLY OR SELF-RIGHTEOUS JUDGEMENT TO OUR FELLOW BROTHERS AND SISTERS.
  GOD is SPIRITY AND IF U WANT TO BE INCANT WITH HIM YOU HAVE TO BE IN HIS SPIRITY, so my fellow tanzanians lets not analyse God”s WORK by using our feeling and thought of wat we think is right or wrong.
  2TIMOTH 4:2 instruct us -” preach the word be prepared in season and out of season – corret,,rebuke and encourage,-with patience and careful instruction” from HOLY SPIRITY.
  and those who are lead by Holy spirity wil not use thr mouths to CONDERM Other but to BUILD.

  NDUGU ZANGU WATANZANIA EBU TUACHE MAMBO YA USHABIKI KWENYE MAMBO YA ROHONI,MIM NASHAURI IF DEEP DOWN WE KNOW THAT WE DNT VE THE HOLY SPIRITY LETS KEEP OUR MOUTH SHUT.
  LOVE YOU ALL.

 60. Ndugu Lwembe,
  Asante mno kwa mchango wako, Ingawa naona umekuwa mwalimu aliyekasirika……hasa kwa lugha yako.Umefafanua vizuri kwa kujikita katika Maandiko kuhusu aina za Manabii, naungana nawe kwa hilo.
  Jambo ambalo naona linawaumbisha Wakristo wengi na wale ambao wanaonekana wana “misimamo” nadhani ni miujiza tu…! Biblia ianasema “CHACHU KIDOGO HUCHACHUA DONGE ZIMA” Haiitaji ufahamu mkubwa wa Maandiko kuona chachu ndani ya mafundisho ya Nabii Joshua, na vile vile haiitaji ufahamu wa rohoni uliofichika kutambua kuwa nabii zake nyingi hazipo kabisa kuujenga mwili wa Kristo.Katika mjadala kama huu huko nyuma niliuliza swali ulilouliza ndugu Lwembe….kuhusu nukuuu ya Quraan ndani ya sinagogi la Nabii huyu, Kama kweli Nabii huyu ni wa Bwana sidhani angelishindwa hata kuliona hilo kuwa si sahihi,hili tu linatosha kuleta uvundo katika huduma yake. Je kweli kuna tofauti gani na yule mchimba mizizi aliyetokea Loliondo na wengine katika blog hii wakasema ni baraka ya “bwana” Tanzania? Na wengine wakaogopa kukemea kwa ukali wakasema bado wanajifunza na kuaangalia waone huduma ya babu wa loliondo itafika wapi.
  Wakristo wengi wa leo ni wa hamasa “sensational christians” Kwa wengi wetu leo maadamu jina la Yesu linatajwa hawana haja ya kujiuliza ni Yesu yupi…! Maadamu Roho anazungumzwa…..hawajiulizi ni roho yupi….maadamu Injili inahubiriwa hawajulizi ni Injili ipi…..!
  Kama kuna upotovu unaoweza kuwaondoa Wakristo leo katika imani hai, basi ni ule unatoka mimbarini…! Paulo alipowaita Wazee wa kanisa kutoka Efeso alipokuwa Mileto alisema wazi….”najua baada ya kuondoka Kwangu Mbwa mwitu wakali wataingia Kwenu wasilihurumie kundi……tena katika ninyi wenyewe watainuka watu…….”
  Hebu mwagalieni nabii huyu wa Nigeria kwa kigezo cha maandiko…! Sio kwa publicity ya kusaidia maskini mbele ya kadamnasi ya Kamera za TV, Hebu angalieni Nabii zake kama zinafanya hata wasiomjua Mungu wawe na hofu ya hukumu itakayoupata ulimwengu……Hebu angalieni ujumbe wake kama unawafanya watu wachomwe mioyo yao na waseme tutendeje ndugu zetu..” Au ujumbe wake unafanya watu “wachomwe mioyo yao na wamsagie meno”……tunachoona ni sensationalism……nabii akitukuzwa na wala si Yesu……..Kweli naamini kuwa siku zikichelewa nata wataule wanawezwa kupotezwa……

 61. Mpendwa John Paul,
  Shalom!
  Ni kweli kama unavyosema, nikikunukuu:”Nina uhakika kwamba MIMI SIJAANDIKA LOLOTE kuhusu T.B Joshua kuwa katika kundi la KUIFUNGA DUNIA”. Sina uhakika kwa kule kusema “kundi linaloifunga dunia” MNAMAANISHA NINI! Naomba ufafanue. Na ninaamini swali lote la Ck Lwembe limekaa juu ya msingi huo wa “KUIFUNGA DUNIA” hilo ni kweli kabisa, na kwa vile nami nipo nikiufuatilia mjadala huu na kujifunza zaidi, basi naona ni vyema nikawajibika kwa kauli nilizozitoa ili kuuleta mjadala mzima katika hali ya kueleweka kwa yeyote anayeufuatilia pia. 

  Iwapo utaurejea mchango wangu wa June 16 unaweza kuona nilichokiandika, labda kwa kifupi nirudie: “Kimsingi kipawa hicho cha unabii kimegawanyika katika mafungu mawili. Moja ni lile la manabii waliowekwa katika makusanyiko ili kuyahudumia, kama akina Agabo. Kundi hili huwaletea habari kusanyiko kulingana na kile Mungu anachotaka kuwajuza kusanyiko lake. Mipaka ya kundi hili ni kusanyiko lao tu! Kipawa hiki hakiwezi kuvuka kusanyiko lake kwani katika makusanyiko mengine wanavyo vipawa hivyo pia, kama ni makusanyiko yaliyo chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu. Hata suala hili la nabii huyu walipaswa kupewa majibu ya Huduma hiyo katika makusanyiko yao! … labda kundi hili la manabii tuliite ‘manabii wa kanisani’ katika maana ya kusanyiko.

  Kundi la pili ni la manabii wanaokuja na Neno la Wakati kulingana na Majira katika Programu ya Mungu ya Ukombozi, kama Yohana Mbatizaji. Huduma ya hawa huifunga dunia yote katika ujumbe unaoletwa, ikiwa ni Nuru kwa kanisa kama Mwili wa Kristo, Ujumbe huo ukilivusha kanisa kutoka hatua liliyomo na kuliingiza katika hatua ya mbele zaidi. Yaani kwa ujumbe wa nabii wa fungu hili, dunia hutenganishwa, kulingana na Maandiko, yakijithibitisha kutimia kwake; nao wampokeao nabii huyo hupata thawabu ya nabii au huipokea hiyo Neema, na wamkataao, pia hubaki huko nje ya huo Ujumbe!” kwa kifupi huo ndio ufahamu wangu kuhusu huduma hiyo ya Unabii katika utendaji wake kwa kadiri nilivyoyaelewa Maandiko.

  Kwa hiyo swali langu lililenga kupata ufafanuzi katika kiwango hicho nilichokiulizia kutokana na ukiri wa wapendwa kuwa huyo nabii ni ” Baraka ya ulimwengu na bara la Afrika”. Pia watu wengi wakijitoa na kufunga safari kwenda kufanya ibada katika Sinagogi hilo katika shauku ya kujiwakilisha mbele ya nabii huyo wa Mungu na kutabiriwa mambo yao kama mnavyoyashuhudia kutoka kwa wachangiaji hapa katika mada. Pia yako makundi kwa maelfu katika nchi mbali mbali pamoja na Tz yetu wanaojikusanya kwenye luninga zao na kuzifuatilia ibada hizo moja kwa moja katika maana hiyo hiyo kiroho, licha ya kwamba bado wanaendelea na madhehebu yao!!!

  Kwa hiyo swali langu ndio hilo ndugu John, wewe mwenyewe ukikiri kuwa mafunuo ya kinabii ya nabii huyo yanawasaidieni hata ninyi mlio katika makusanyiko ya mbali. Kwamba huduma hiyo imevuka mipaka ya kusanyiko na kuwaleta nyote kutoka makusanyiko yenu madogo, hata yakiwa makubwa, unofficially mmenyofolewa kutoka makusanyiko yenu kiroho na kuingizwa katika kusanyiko la SCOAN, makusanyiko yenu local, yakibaki na makasha matupu! Halafu anawadanganya kuwa mnaweza kwenda kwake mkahudumiwa na kisha kurudi makusanyikoni kwenu, ni ulaghai kiasi gani huo!!! Lo, ndugu zangu, Injili yote hii inayohubiriwa, haijawafanyia lolote! Ni bora ukawa chini ya hawa manabii wetu uchwara wanaowakamua watu pesa zao kuliko huko mlikoenda, maana huko ndiko maandiko yanakotimia kwa uhakika kuhusu kudanganywa! Angalia makusanyiko yenu jinsi yamebakiziwa misukule baada ya nafsi zenu kutwaliwa katika ulimwengu wa roho na ngome hiyo. Wengi wanadhani manabii wa Uongo watakuwa ni waongo wenye kutoa unabii usio timia. Si kweli, nabii wa Uongo ni nabii kabisa isipokuwa kwa Asili Mbegu ya Mungu haimo ndani yake, kwa hiyo mwisho wa siku atakuingiza tu katika ibada kengeufu kama hiyo aliyoisema ndugu Sam ya Misa ya Damu ya Yesu!! Ndio maana kila ninapowauliza ni wapi katika Maandiko nabii huyo alitabiriwa, sipati jibu. John anasema eti huyo ni wa Huduma 5, lakini tena anairuka kauli yake kwa kukiri kuwa wengi wanaifuatilia! 

  Je, nyie mnaokiri kwamba huyo ni baraka ya ulimwengu pamoja na ndugu John uliyesema unaifuatilia huduma hiyo, kama swali nililowauliza mmekosa jibu, mwaweza kutueleza lile bandiko la Qurani linalokiri kuwa “Mungu ni mmoja tu, Allah” lililobandikwa humo ndani ya Sinagogi hilo linawakilisha nini kulingana na Injili ya Kristo!!!

  Nasubiri kutoka kwenu tukikifunza zaidi!!

 62. Ndugu zangu, Milinga, Nduta, John Paul na wengine.

  Ndugu Milinga, umenifurahisha sana, ingawa moyo wangu una simanzi! Huo utafiti wako unaoufanya, nina uhakika utazeeka ukiwa bado haujaumaliza, na sina uhakika kwamba wewe ni mtafiti kweli, maana kwa maelezo yako yaelekea huna hata rejea katika maana ya YAKINI, bali ni utafiti unaongojea kutimia kwa nabii zinazotolewa, sijui ungekuwepo siku nabii Isaya alipotabiri ujio wa Kristo, ungeweza kusubiri miaka hiyo 700 ndio ujue kuwa huyu ni nabii wa kweli? Hebu wazia hili kwamba Utafiti ukuweke mahali kwa mwaka mmoja, mkeo akifungwa vitambaa kichwani ibadani kutimiza yasiyoagizwa, na Biblia yako unayo kwapani halafu eti utuambie unafanya UTAFITI, sioni kichekesho kinachozidi utafiti huo!!! Wewe utakuwa ni muumini wa kawaida wale wanaopeperushwa na kila fundisho jipya na miujiza, ni sawa na boti isiyotiwa nanga!

  Ndugu zangu, kwa maelezo ya ndugu Milinga, kujibidiisha kwa jinsi hii ni hasara isiyo ya lazima. Ni uongo unaoweza kukuingiza katika matatizo usiyoyalalia. Tena ni uongo utakaokuibia muda, amani, na imani yako pia! Milinga angalia utafiti wako ulikokufikisha; eti unauliza kama Shetani anakaaga juu ya mawingu? Muda wote unaoupoteza kwa kukimbizana na huduma hii na ile kama ungemwamini Mungu katika Neno lake yasingekukuta hayo!

  Kama ungekuwa mtafiti wa kweli kwanza ungeyatazama Maandiko, ujishibishe Neno lake likae kwa wingi ndani yako, ndipo utoke kwenda kutafiti. Lakini wewe yaelekea umetoka ukiwa mtupu, bila nanga, nayo mapepo ya dini yamekuona, kama yalivyowaona mitume wakiwa peke yao nayo yakataka kulizamisha boti, wewe sasa yanakupeperusha, leo hapa kesho kule…!

  Basi unapokutana na watu wa jinsi yako kama navyowaona wengi wa wafuasi wa manabii walivyo, hawana rejea ya Maandiko bali miujiza tu, ya uponyo na utajiri, ni vigumu sana kufika nao mahali mkajadili jambo, YAKINI yenu ikiwa ni Biblia, kama ninavyowaona katika mjadala huu! Hebu wazia hili, unamuuliza mpendwa Maandiko yanayomthibitisha nabii huyu ni yapi, hajui chochote kuhusu hilo!

  Miujiza ndugu zangu ni mingi sana na inakuja. Au wenzetu mnatumia vitabu vingine tofauti na Biblia katika ibada zenu kama alivyosema Milinga, pale mnapokuwa katika kufuatilia huduma hizo, kama vile Misale ya Waumini au Katekesimu nk, kwa hiyo Biblia na mambo yake huwa haihusiki!?

  Ndugu John Paul, kwanza nikushukuru kwa kunipa jibu la swali langu Licha ya kwamba nilikutaka unieleze kwa uwazi jinsi unavyomchukulia nabii Joshua, hujaweza kuwa wazi, ila naona umejaribu kuyachanganya vizuri maelezo yako ili yasitoe jibu la kueleweka. Angalia jibu lako; “Kwa kuongezea ni kuwa mi humuona T.B Joshua kama mmoja wa watumishi ndani ya zile huduma 5 ndani ya kusanyiko la SCOAN, lakini pia kwa mwili wa Kristo, popote ambapo mtu anaweza kufikiwa na ujumbe wake. Zaidi ni kuwa T.B Joshua siyo tu NABII, mi naona Unabii ni huduma inayotenda kazi ndani yake sambamba na Kufundisha, na pia ni Mchungaji kwa kuwa SCOAN ni Kanisa, likiwa na taratibu zote za kikanisa.” Kwa hiyo kwa jibu lako unatuambia kuwa Ndani ya TB joshua kuna huduma ya Unabii, Ualimu, na Uchungaji. Ila naona umesahau kutaja Utume na Uinjilisti huduma ambazo zimedhihirika ndani yake kwa kulisimika kanisa hilo la SCOAN na pia katika kuhubiri kwake hadi huku kwetu ambako nako pia amewaleta wengi katika kundi hilo. Basi katika ujumla huo tunaweza kusema kuwa nabii huyo atakuwa anawakilisha Huduma kamili ya Kristo kwa kuzibeba Huduma zote 5 (Efe 4:11)! Yaani huyo kwa taarifa yako “T.B. Joshua ni baraka ya ulimwengu wote na zaidi sana baraka ya Afrika” kama alivyokiri ndugu Nduta, nadhani nawe hauko mbali sana na hayo!!!

  Hata hivyo, nikirudi katika lile swali lako, kwa kadiri ya Maandiko, nilikuorodheshea msululu wa viongozi wa Madhehebu na Huduma tofauti tofauti, wote wakidai kuwa ni watumishi wa Mungu, na wakidai kuongozwa na Roho Mtakatifu, nayo Maandiko yakitufundisha kuwa ROHO ni mmoja; basi kwa ushuhuda wako mwenyewe umetuonesha kuwa hao viongozi wana tofautiana!!! Kwa hiyo kwa kiasi fulani jibu la swali lako, kama nitalijibu kama unavyonitaka, basi nitakuwa ni mnafiki. Maandiko yanatutahadharisha kuhusu Manabii na Walimu na Wapakwa mafuta wa Uongo, kwa hiyo ni muhimu kutambua kuwa Mungu hawezi kukupa tahadhari bila kukupatia jinsi ya kuiendea tahadhari hiyo ili usitumbukie katika uongo huo utakao sambaa dunia yote! Ndio maana Kristo anasema kondoo wake wamjua na sauti yake wanaijua! Kwa hiyo mimi nikikuambia nabii fulani ndio wa kweli, itakubidi uniamini MIMI kwanza kama mtumishi wa Mungu, ndipo umeze hicho nitakachokuambia, wewe mwenyewe ukiwa hauna kipimo ndani yako! Kama ulifikia kumuamini TB Joshua kuwa ni mtumishi wa Mungu aliye hai bila kipimo au kwa kipimo cha kutoa kwa kuwasaidia wenye shida na mambo mengine ya mwilini, kwa hayo ukajiridhisha kuwa huyo ni nabii wa Kweli, au kwa vile amekataa kata kata kuwanenea vibaya watumishi wenzake wa Mungu pia anaotofautiana nao kwa Mafundisho hayo wanayoongozwa na Roho Mtakatifu, bado hayo hayatakusidia sana. Kagua wanachokifundisha kama kiko sawa na Maandiko ndipo utaiponya roho yako na uharibifu tunaouendea!!!

  Hivi ninyi mnaosema ni watafiti na wafuatiliaji wa huduma ya TB Joshua, na mmejiridhisha kuwa ni nabii wa Mungu na mnatushangaa tunao mbeza, je, mnaijua ile ‘Missa ya Damu ya Yesu’ ambayo nabii Joshua hulibariki tanki kubwa la maji, akiyagusa yale mabomba 12 yakutolea maji na kuyatangaza hayo kuwa sasa ni ‘Damu ya Yesu’; kisha kusanyiko huyaendea maji hayo, wakiyakimbilia na kuvutana kati yao kila mmoja akijaribu kuwahi ili aweze kuyanywa, kujimwagia hata wakati mwingine kujiosha katika ‘Damu hiyo ya Yesu’!! Katika hali kama hii, basi twawauliza, ibada ya jinsi hii, ni wapi katika Maandiko ilipo?? Haya, huduma hiyo inauza Maji ya Upako ambayo yameandikwa hivi: “ANNOINTING WATER, FOR BREAKTHROUGH IN ALL AREAS AND FOR THE SALVATION OF YOUR SOUL”. Kwa tafsiri isiyo rasmi ni sawa na kusema: “MAJI YA UPAKO, KWA USHINDI WA HALI ZOTE NA WOKOVU WA NAFSI YAKO”!! basi hayo na mengine mengi sana naamini kuwa ndiyo yamewaaminisha ndugu zangu kuwa huyo ni nabii wa Mungu!!!!

  Mbarikiwe nyoooote!

 63. Wapendwa,

  Shalom, Naomba nichangie kidogo tu katika hii mada. Kwanza kabisa namuunga mkono John Paul na wengine wengi tu wanaokubaliana na huduma ya T.B. Joshua.

  Ninaonavyo mimi hapa ni kwamba TUNAWEZA FIKIRIA TUNAMJADILI T.B. JOSHUA HAPA LAKINI UKWELI NI KWAMBA TUNAJADILIANA JUU YA UFAHAMU NA UELEWEWA WETU JUU YA MUNGU. YAANI MUNGU NI NANI NA ANAWEZA KUFANYA NINI?

  HILI NDIO MADA HASWA INAYOJADILIWA. TUNAMKUBALI AU KUMKATAA T.B. JOSHUA KUTOKANA NA JINSI TUNAVYOMUELEWA NA KUMJUA MUNGU, SIFA NA UWEZO WAKE.

  NINASEMA HIVI KWA SABABU UFAHAMU WETU KUHUSU MUNGU ALIVYO NDIO UNAOPELEKEA KUKUBALI HUDUMA YA T. B. JOSHUA AU KUIKATAA.

  KUNA WATU WANA UELEWA MDOGO SANA JUU YA MUNGU NA SHETANI KIASI KWAMNA KAZI ALIZOFANYA MUNGU WANAMPATIA SIFA SHETANI, NA KAZI ZA SHETANI WANAMPA LAWAMA MUNGU.

  KUNA WENZETU HUWA WANAKWENDA HUKO MEKKA SAUDI ARABIA KUMPIGA SHETANI NA MAWE. ILIHALI MAJINI WANAYAFURAHIA NA KUSEMA NI NDUGU ZAO WA KIIMANI.

  SASA SWALI KUBWA NI KUJIULIZA MUNGU UNAYEMWAMINI ANAWEZA KUFANYA MAMBO GANI AU HAWEZI MAMBO GANI.

  NA SHETANI NI NANI KUTOKANA NA UELEWA WAKO!

 64. Ndugu Sam,

  Nashukuru kwa maelezo yako, ingawa hujanijibu swali lolote katika hayo niliyokuuliza kutokana na maoni yako yaliyopita. Lakini kwa lengo ili twende pamoja ngoja niyaache kwanza maswali hayo, pengine utanijibu baadaye baada ya kuwa mimi nimekujibu. Maana tukiendeleza maswali juu ya maswali tunaweza tusifikie suluhu. Asante.

  Hebu soma niliyoandika wakati namjibu Seleli, kuhusu ninavyomuona T.B Joshua, kisha nitaongezea kidogo:

  “Nimekuwa Mkristo kabla ya kumfahamu T.B Joshua, na hata pasipo T.B Joshua nitaendelea kuwa Mkristo. Mwokozi ni Yesu na si T.B Joshua. Yako mengi ambayo Mungu ananitendea kwa kupitia MIMI MWENYEWE. Hivyo sitegemei NABII ye yote kuendesha maisha yangu BALI NAMTEGEMEA Yesu. N wala T.B Joshua SIYO NABII WANGU bali namuona kama Mtumishi tu wa Mungu sawa na watumishi wengine. Napenda kujifunza kwake kwa habari ya utoaji na mafundisho anayoyatoa kwa kuanzia yeye mwenye kuwa MFANO. Akifundisha watu wawe watoaji, yeye mwenyewe ANAONYESHA JINSI ANAVYOTOA. Hii ni tofauti sana na watumishi wengi, hasa wa Tz, ambao wakifundisha kutoa BASI HUWATAKA WATU WATOE WAMPE YEYE/HUDUMA YAKE!”

  Kwa kuongezea ni kuwa mi humuona T.B Joshua kama mmoja wa watumishi ndani ya zile huduma 5 ndani ya kusanyiko la SCOAN, lakini pia kwa mwili wa Kristo, popote ambapo mtu anaweza kufikiwa na ujumbe wake.

  Zaidi ni kuwa T.B Joshua siyo tu NABII, mi naona Unabii ni huduma inayotenda kazi ndani yake sambamba na Kufundisha, na pia ni Mchungaji kwa kuwa SCOAN ni Kanisa, likiwa na taratibu zote za kikanisa. Na yeye ndiye kiongozi wa kanisa hilo. [Na mimi siyo muumini wa hapo lakini huwa ninaona tu kwenye TV na kufuatilia kwenye Mtandao.]

  Ninasema hivyo kwa kuwa siyo lazima Mtu mwenye huduma ya Unabii awe na Kanisa. Wapo ambao wanatumiwa na Mungu kwa ajili ya Unabii lakini ni washirika tu wa kanisani. Wako chini ya Mchungaji na wanaendelea na ukristo wao kama kawaida.

  Ndg Sam, naomba nifupishe tu hapo, nisije nikaandika mengi lest I go away from the point in question. Natumaini baada ya kuandika hivi, sasa nitapata jibu la swali langu!

  Karibu!

 65. Mpendwa John Paul!!

  Unajua John ili kulijibu swali lako vizuri kuifikia maana ya kujifunza ni muhimu kwa swali linalo ulizwa kuwa specific. Michango ulioiunga mkono ni ya akina Nduta, Milinga ambao wanaamini huyu nabii ni baraka ya Afrika, kwa ufahamu wangu Afrika sio nchi wala taifa katika maana ya sovereignty ya makusanyiko, nayo Maandiko yakisisitiza huduma zile tano kuwepo ndani ya makusanyiko yetu ndio maana ningependa kufahamu wewe baada ya kuwa umejitenga na kauli za kina Nduta je, nabii T.B Joshua kwako ni nabii yule wa zile huduma tano za ndani ya kusanyiko , kusanyiko hilo likiwa SCOAN kwamba wewe ni muumini wa hapo au kwako ni nabii anayeleta ujumbe kwa Kanisa likiwa kama mwili wa Kristo duniani kote?

  Ukinijibu hapo itakuwa ni rahisi kwangu nikujibu nini kinachofanania na hali utakayo niambia.

  Ubarikiwe!!

 66. Ndugu Sam,

  Labda nianzie mwishoni mwa maoni yako. Umeandika kuwa “Mkristo anayetegemea kuonyeshwa mhudumu wa kweli kwa kidole, huyu bado ana safari ndefu maana Neno la Mungu linapswa lijae kwa wingi ndani ya Mkristo ambalo ndicho kipimo cha kuzipima hizo roho”. Ni kweli. Nami naamini hapa tuko pia kujifunza Neno la Mungu, ili aliye na safari ndefu basi angalau ipungue pungue. Nami yawezekana ni mmoja wa hao ambao bado wana safari ndefu. Ndiyo maana naulizia ulizia ili nami nipate la kujifunza.

  Lakini pamoja na kujifunza huko ninafikiri kuwa kule kusema T.B Joshua ni Nabii wa Uongo, tayari tunakuwa tunamnyooshea kidole. Sasa kama tunaweza kumyooshea kidole NADII WA UONGO kuna ubaya gani kumnyooshea kidole na NABII WA KWELI au Mtumishi wa Kwleli? Na waza kuwa KAMA KUMFAHAMU MTUMISHI WA KWELI KUNAHITAJI TU ROHO MTAKATIFU, yaani hakuna sababu ya kuambiana kuwa fulani ndiye mtumishi wa kweli, nilifikiri ingekuwa hivyo pia kwa MTUMISHI WA UONGO. Kwamba badala ya kusema kuwa T.B Joshua ni wa Uongo basi tungeambiana tu kuwa KILA MTU AMTEGEMEE ROHO MTAKATIFU KUMFUNDISHA.

  Pamoja na hayo lakini bado nina duku duku kuwa KAMA TUNAWEZA KUWA NA UJASIRI au UJUZI wa KUTAMKIANA HADHARANI WALE WABAYA, huku tukwa hatuna Ujuzi au Maarifa ya KUTAMKIANA WALE WA KWELI, inaweza ikawa vigumu sana kwa msimamo huo KUELEWEKA.

  Lakini pia, yawezekana kweli T.B Joshua ananena yaliyo KINYUME na matakwa ya Roho Mtakatifu. Basi angalau tungesaidiana basi kuwa KATIKA HUDUMA TA T.B JOSHUA , jambo hili na lile yako KINYUME NA ROHO MTAKATIFU. Lakini kama hilo nalo haliwezekani basi, itakuwa vigumu sana kwa mtu ambaye “bado ana safari ndefu” kuweza kupunguza safari yake.

  Hebu, nakuomba basi kwa kadri ua ufahamu ulio nao tusaidiane mambo ambayo kwa hayo T.B Joshua anakwenda kinyume. Lakini kama hilo nalo haliwezekani, basi! Ila kwa namna hiyo sidhani kama tutakuwa tunasaidiana kwa lolote hapa.

  Suala jingine ni hii hoja ya kuwa T.B NI NABII MKUU. Hii ndiyo naisikia kwako: Umeandika hivi:

  “basi kama Roho ni Mmoja tulitegemea manabii na maaskofu wakuu ambao wote, haswa manabii kama wakina Mwingira, nabii Malisa, mtume na nabii Fernandes , mzee Kulola, mzee Lazaro, maaskofu kama Pengo ,Gamanywa, Kakobe au mchungaji Ambilikile babu wa Loliondo na wengineo pamoja na hao wanaosimamisha mvua, watueleze kuwa T.B Joshua ndio nabii wao Mkuu, lakini kimyaaaa, mpo nyinyi wakina Nduta, John Paul,……… ”

  Hii kauli imenishangaa sana! Sijuwi nani kachangia hapa kuwa T.B Joshua ni NABII MKUU. Lakini hao uliowaorodhesha hapo , Je, UNAFAHAMU WANASEMANAJE WAO KWA WAO? Je, wanatambuanaje ili hadi kwa pamoja waje WAMTAmBUE T.B Joshua kwa Pamoja, kama nabii wao Mkuu?

  Lakini kingine ni kuwa Una maana ni Askofu tu, au mchungaji tu, au nabii tu NDIYE MWENYE UWEZO WA KUTAMBUA NABII AU MTUMISHI FULANI KUWA NI WA KWELI? Je, mkristo asiye mchungaji wala askofu, kama mimi hapa, HANA UWEZO WA KUTAMBUA MTUMISHI WA KWELI AU WA UONGO?

  Hoja nyingine ni kwa KWA NINI MLITEGEMEA hao uliowataja ndio waje na CONLUSION kuhusu T.B Joshua? Ina maana hao kwako NDIO WAHUDUMU WA KWELI?

  Bado natamani kujifunza Ni kwa Vipi T.B Joshua anakwenda kinyume na Roho Mtakatifu!

  Halafu suala la Ck Lwembe, hili hapa:

  “Lakini kwamba huyu ni nabii wa lile kundi linaloifunga dunia, nawaombeni ninyi mnaotusisitizia hivyo, hebu tuonesheni ni wapi katika Maandiko Mungu alisema atatuletea huyo na kwa Huduma ipi katika Programu ya Mungu???”

  Nina uhakika kwamba MIMI SIJAANDIKA LOLOTE kuhusu T.B Joshua kuwa katika kundi la KUIFUNGA DUNIA”. Sina uhakika kwa kule kusema “kundi linaloifunga dunia” MNAMAANISHA NINI! Naomba ufafanue. Na ninaamini swali lote la Ck Lwembe limekaa juu ya msingi huo wa “KUIFUNGA DUNIA”

  Kama utaona inafaa, naomba ufafanue ili tuendelee kujifunza!

 67. Mpendwa John Paul

  Narudia tena ili kukusisitizia kuhusu mambo ya Mungu yalivyo “Mtumishi wa kweli ni Roho Mtakatifu. Kwahiyo yeyote anayenena tofauti na Roho Mtakatifu ambaye ni Neno ni mtumishi wa UONGO!!!” na haijalishi ni nani au amesifika kiasi gani. Ili kuwa mtumishi katika huduma ya Kristo, haukulupuki kwa hisia au tamaa ya kazi, yaani hautumii akili, bali unapaswa ukutane na Roho Mtakatifu ili akusimike kuwa mtumishi kama ilivyokuwa kwa mitume.

  Basi twafahamu kulingana na Maandiko ya kuwa Roho ni Mmoja ambaye ndiye Mwalimu, tunaamini hivyo juu ya nafsi zetu, yaani “sold, lock stock and barrel” basi kama Roho ni Mmoja tulitegemea manabii na maaskofu wakuu ambao wote, haswa manabii kama wakina Mwingira, nabii Malisa, mtume na nabii Fernandes , mzee Kulola, mzee Lazaro, maaskofu kama Pengo ,Gamanywa, Kakobe au mchungaji Ambilikile babu wa Loliondo na wengineo pamoja na hao wanaosimamisha mvua, watueleze kuwa T.B Joshua ndio nabii wao Mkuu, lakini kimyaaaa, mpo nyinyi wakina Nduta, John Paul,……… Mmeulizwa swali jepesi kwamba ni wapi katika Maandiko huyu ametabiliwa,hamna jibu!!! Ni dalili ambayo inaonesha Roho anaye hudumu kwa viongozi na wafuasi wake si mmoja, vingenevyo ingekuwa ni huduma ya Roho Mtakatifu ingewaongoza katika Maandiko yake!!!

  Juu ya wingi wa watumishi, mwaminio au mkristo anayetegemea kuoneshwa mhudumu wa kweli kwa kidole, huyu bado ana safari ndefu maana Neno la Mungu linapaswa lijae kwa wingi ndani ya mkristo ambalo ndicho kipimo cha kuzipimia hizo roho “ imeandikwa zipimeni roho zote”

  Nasubiri kwa hamu kubwa jibu la swali la ndugu Ck Lwembe kutoka kwenu.

  Mbarikiwe.

 68. Kwa kuwa lengo hapa ni kujifunza kwa kubadilishana ujuzi wa Neno la Mungu, mi nitajibu maswali ya ndugu Edwin Seleli. Na majibu hayo yawezekana kabisa nikawa ninakosea, na nikikosolewa ndipo nitakuwa najifunza mimi mwenyewe au mtu mwingine yeyote anayefuatilia mjadala huu:

  1.Swali: “Tell me guys tofauti iyo ni ipi kwa kutumia viwango vya Ki Mungu na ki Biblia inapokuaja maswala ya utumishi na kumtumikia Mungu na Mungu anavyopima na atakavyo pima watu wake kuwalipa sawasawa na kazi zao?”

  Jibu: Kwa kuwa Mungu atalipa watu sawa sawa na kazi zao, mi naona hivi, yule afanyaye kazi kubwa atalipwa sawa sawa na ukubwa wake. Muinjilisti ambaye anahubiri kwenye mikutano ya Injili, mfano Moses Kulola, and allies, na watu wakaokoka maelefu kwa maelfu, mi naona kama watalipwa zaidi kuliko muinjilisti ambaye kwa mwaka mzima atakuwa amesababisha mtu mmoja tu kuokoka!.

  Kwa kuwa Mungu ni wa haki, naamini kabisa watumishi ambao walitoa maisha yao yote, wakitembea kwa miguu kwenye milima na mabonde, mito na misitu, wakipeleka Injili, hao watalipwa zaidi kutokana na tabu waliyopata.

  Sasa, mchungaji ambaye kanisani kwake ana washirika kumi naamini atalipwa sawa na kazi anayoifanya, na T.B Joshua naye, kwa wingi wa watu anaowahudumia, naye atalipwa sawa na kazi yake. Hii ndiyo tofauti yao. Na hii ni ikiwa tu wawili hawa wote wanamtumikia Mungu, Maana uchache wa washirika kanisani nacho SIYO KIGEZO KUWA MCHUNGAJI HUYO NDIYE WA KWELI!

  2. “Swali: Hivi kutoa unabii kuhusu mtu au wtu, taifa, jamii na ulimwengu na kusafisha maliwato ya kanisani kwako, kuosha magari ya mchungaji kanisani, kumsaidia mdada mmoja gauni mbili tu yule anayekuja na nguo moja tu nusu mwezi kanisani, kumshuudia mtu mmjoa teja akaookoka, kuna tafauti mbele za Mungu? nani zaidi? nani kapiga kazi kuuuuuuubwaaaaa ya utumishi mbele za Bwana?”

  Jibu: Neno la Mungu linatuagiza kutenda mambo pasipo MASHINDANO. Yule anayefagia kanisani ASIJIDHARAU kuwa anafanya kazi ndogo wala yule Anayehubiri pale Jangwani, mbele ya watu elfu 10, naye hatakiwi KUJISIFU kwamba nafanya zaidi. Jambo la Muhimu hapa hapa ni KILA MTU AFANYE KWA UAMINIFU katika nafasi yake aliyopo na huduma anayojisikia ndani yake. Hivyo ukubwa wa Kazi kwa Mungu ni ULE UAMINIFU WAKO katika kazi unayoifanya.

  Gari la uwezo wa kubeba mzigo tani 5, likitumika kubeba tani 4.5 litakuwa limetumika VIZURI ZAIDI kuliko gari lenye uwezo wa kubeba tani 60 likitumika kubeba tani 20. Kwa hiyo unaweza kushangaa kuwa Mtu anayefagia kanisani, mbele za Mungu anaweza kuwa kafanya kazi kubwa zaidi kuliko anayehubiri mikutano ya injili ya watu elfu 10 kwa kuwa kilichoko ndani kilitakiwa kiwafikie watu laki 1

  Kwa hiyo yule aliye na KARAMA anatakiwa atende kwa kuliingana na kiwango cha Karama kilichowekwa ndani yake, na yule aliyeko upande wa HUDUMA ZA MASAIDIZANO naye anatakiwa afanya kwa nguvu zake na kwa uaminifu.

  3. Swali: “What real made TB Joshua TB Joshua the “true prophet of God” to you? Is it TV and other media advertisements or……what if there was not media to bring him to your room, country, who would be your prophet?”

  Jibu: Mimi nikiangalia namna wanavyohudumiwa watu, baada ya kufanyiwa maombezi, huwa inanipa kuamini kuwa pale panafanyika kazi sahihi ya Injili. Watu huwa wanashahuriwa kuwa kwa kuwa sasa ameshapokea muujiza toka kwa Mungu, kilicho cha muhimu zaidi sasa ni kUKABIDI MAISHA YAKE MIKONONI MWA MUNGU, KWA KUMFANYA YESU AWE BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YAKE. Maneno haya ni adimu kwa watumishi wetu wa hapa nyumbani, ambao habari za huduma zao huonekana kwenye TV na kusikia kwenye maredio. Sitasahau siku niliposikika mtumishi mmoja, anayefahamika sana nchini, akitangaza kwamba BAADA YA MAOMBEZI KILA MTU ARUDI TU ALIKOTOKA. HATA WA MSIKITINI ARUDI TU MSIKITINI KWA KUWA MUNGU NI WA WATU WOTE! Japo siwezi kuamua moja kwa moja kuwa yule ni Nabii wa Uongo lakini bado naendelea kuyatfakari maneno hayo kama Nayo yana lengo la KUMFANYA ANAYEYASIKIA AMGEUKIE YESU.

  Mara nyingi sana T.B Joshua amekuwa akisema kuwa SIYO LAZIMA mtu ahangaike kwenye SCOAN, Bali anaweza kutafuta MAHALI POPOTE AMBAPO NENO LA MUNGU LINAFUNDISHWA KATIKA USAHIHI. Hayo nayo ni maneno adimu nchini kwetu Tanzania!

  Nimekuwa Mkristo kabla ya kumfahamu T.B Joshua, na hata pasipo T.B Joshua nitaendelea kuwa Mkristo. Mwokozi ni Yesu na si T.B Joshua. Yako mengi ambayo Mungu ananitendea kwa kupitia MIMI MWENYEWE. Hivyo sitegemei NABII ye yote kuendesha maisha yangu BALI NAMTEGEMEA Yesu. N wala T.B Joshua SIYO NABII WANGU bali namuona kama Mtumishi tu wa Mungu sawa na watumishi wengine. Napenda kujifunza kwake kwa habari ya utoaji na mafundisho anayoyatoa kwa kuanzia yeye mwenye kuwa MFANO. Akifundisha watu wawe watoaji, yeye mwenyewe ANAONYESHA JINSI ANAVYOTOA. Hii ni tofauti sana na watumishi wengi, hasa wa Tz, ambao wakifundisha kutoa BASI HUWATAKA WATU WATOE WAMPE YEYE/HUDUMA YAKE!

  4.Swali. “Sasa where was Holy Spirit siku izo atofautiena na wa leo ktk mambo ya msingi?au roho mtakatifu wenu wa leo ameaamka sana na yuko makini saaaana na creative sana kuliko Roho Mt wa wazee hawa ambao wengi wetu ni matunda ya kazi yao ktk nchi hii?”

  Jibu: Mi ninachoona ni kuwa Siyo kwamba Roho mtakatifu amebadilika wala kuamka. Siku za akina mzee Haris Kapiga, Andrea Shimba, Mosea Kulola na wenzake, teknolojia haikuwepo, Hatukuwa na magazeti yenye kusambaa nchi nzima kwa wakati. Hapakuwa na redio sehemu kubwa ya nchi. Hatukuwa na TV kabisa katika Tanzania. Hali hiyo ilisabaisha wanayoyafanya yafayike kama kimya kimya. Ila naamini Kama KUNGEKUWA NA TV, na kazi ya huduma ya wazee hao ikawa inarushwa angani, naamini kabisa wazee hao wangekuwa maarufu sana sana Tanzania, Africa na hata duniani kwa ujumla.

  Mfano mmoja: Palikuwa na mkutano wa Injili pale Nzega, eneo maarufu la PARKING, miaka ya 90, ambapo waliokuwa wanahudumu hapo ni pamoja na Mzee Andrea Shimba. Wakati mkutano unaendelea, kijana mmoja akawa anazunguka na baiskeli. Hata baada ya kuonywa na watu aache yeye aliendelea. Baada ya kuona hivyo, mzee Andrea Shimba aliinuka na kusema kwa sauti: “Bwana na akukemee!” Yule kijana alianguka, akawa kama aliyezimia. Alibebwa na kupelekwa kwenye chumba cha maombezi hadi baadaye alipozinduka. Tukio hilo lingerushwa kwenye TV, nalo lingetosha kabisa kuleta mchango wa kumfanya mzee huyo kuwa “maarufu”!

  Suala la Injili kwa sasa limevamiwa. Na haihitaji hadi kumuangalia T.B Joshua ndipo mtu aone kuwa hali ya Injili kwa sasa ni mbaya. Injili ya sasa ni Ya “mafanikio”. Hivyo kama ni suala la kuhoji HALI YA ROHO MTAKATIFU wa sasa na Wa zamani, Maswli yako mengi sana, hapa hapa nchini Tanzania. Siyo T.B Joshua TU ndiye anayetofautiana na akina Moses Kulola, [Japo ninahitaji kufahamu MAMBO YAMSINGI AMBAYO T.B Joshua anatofautiana na wazee uliowataja], ila ni wengi sana, wanaohubiri Injili ya Mafanikio, ambao ni naamini hao NDIO wanatofautiana na akina Kulola kwa mambo mengi ya msiingi, maana hata hawataki tena kuwaambia watu waache dhambi!

  5. Swali: “From Biblical point of view, all prophesies given in the Bible were at the end of the day aimed to restore back people to God (in the old testament) or bring people to Jesus (in the new testament) or rarely prepared the saints of the prosecution coming for the sake of the work of God (Paul, Peter), nothing more, nothing less, therefore….
  • Can sb tell me what has been the purposes of TB prophesies in reference to the above Biblical context?
  • Will you also categorically establish the differences btn prophesy given out of holy motives vs. human proudness, famousness, uniqueness building, human creativity (crowd pulling), satani/darkness powers etc?
  • Has there been any advantage of his prophesies to the church, children of God, and unsaved?”

  Jibu: From Biblical point of view, ziko Nabii za Hukumu/Adhabu. Wako watu waliotabiriwa KUFA na kweli walikufa, kwa magonjwa, katika Vita na hata kuliwa na Wanyama. Ni aina ya UNABII ambalo lengo lake siyo “kurejesha” bali “kupatiliza”. Yusuph alionyeshwa habari ya NJAA na ile njaa ikaja kweli. Kuna vita vilitabiriwa na kweli vikatokea. Hata Bwana Yesu naye alitabiri habari ya Mti, na mti ule ukanyauka. [Siami kama kunyauka kwa mti ule kulikuwa na lengo la kuwaelekeza watu katika Ufalme wa Mungu]

  Kwa hiyo pamoja na sababu za unabii ulizozitaja, lakini kuna Nabii ambazo lengo lake ni KUJENGA IMANI mioyoni mwa watu, kama ule mti ulionyauka. Kuna mambo yakitabiriwa, kisha yakatokea, huwafanya watu Waamini kuwa kumbe kweli Mungu yupo. [Japo Yesu alisema Heri aaminiye pasipo kuona].

  i). Kwa upande wa Nabii za T.B Joshua, Ziko ambazo amekuwa akitoa kuhusu hali iliyoko mbele ya mtu fulani na kumwambia kuwa ushindi wa mtu huyo ni katika Kukaa na Mungu. Wengi huwa anawaonywa juu ya mambo mabaya yaliyoko mbele kama mtu huyo hatabadilika. Ziko nabii amekuwa akizitoa kwa mambo mabaya yajayo na kuwaomba watu wawe katika maombi ili Mungu aepushe jambao hilo {Ndg Milinga alitoa mifano}, na ziko ambazo zimekua ni kuwafanya watu wajenge imani ndani yao, na kubadili mwelekeo walio nao juu ya Mungu.

  Ukitazana Emmanuel TV unaweza kuona Waislam wakishuhudia na Kukiri kuwa Hakika T.B Joshua anatumiwa na Mungu na kumuomba andelee hivyo na pia awaombee na wao hili waweze kumfahamu Mungu huyo anayemtumia.

  ii). Namna ya kutofautisha “btn prophesy given out of holy motives vs. human proudness, famousness, uniqueness building, human creativity (crowd pulling), satani/darkness powers etc?” ni kuwa hizi za PILI huwa hazina jambo lolote la Kufanya mtu amrudishie Mungu utukufu. Baada ya unabii wa namna hiyo watu hubaki wanasifia tu mtu yule na wala hakuna mwongozo wowote kuwataka watu WATOE MAISHA YAO KWA YESU! Lakini kwa SCOAN watu huelekezwa kuwa njia salama ya kulinda miujiza na unabii wanaoupokea ni KUKAA NDANI YA YESU!

  iii) Kutokana na sababu nilizoeleza, ni dhahiri kuwa unabii wake umekuwa na faida kwa kanisa, watoto wa Mungu na hata kwa wasioamini pia!

  6.Swali: “Kwani what happened huko nyuma kabla ya kumfahamu TB Joshua na nabii zake? Tulipata hasara gani kwa kutofuatilia nabii izi au tumeshaadhirika na nini kama kanisa, mtu mmoja mmoja na Africa kwa kutotekeleza nabii izi? mbona ilikua peace tu siku zote za nyuma until recently after tv na settelite technology kuja third world ,yaani tena waaalaa kulikua hatuna mapressure mnayotupa sasa kwa kutuambia anayotabiri kila mara! Na kama ilikua lazima tupate nabii hizi, why Mungu akusababishaga kwa njia yeyote tuzipate? Au kwa wapendwa waliopovijini sasa hivi wasiofuatilia mambo haya wanampenda Yesu na hawana hata tv au ving’amuzi kunasa wahubiri wa nje, wanakosa nini mnafikiri? Watapata hasara gani ambazo nyie wa town/cities hamtatazipata? Hamuoni ni matatizo yetu tu aliyosema Mfalme Suleimani…aongezaye maarifa houngeza masikitiko…au in my own way…the more much know/informed you are…..the more majaribu, mapito an confusion you will have?”

  Jibu: Swali hili ni refu na lina mambo mengi lakini nitajitahidi kujibu kwadri nitakavyoweza:

  Dunia ni kubwa na ina mambo mengi. Kila mtu alipo kuna mambo ambayo huyasikia na mengine ambayo hayasikii. Wahubiri ni wengi na watumishi wa Mungu ni wengi. Ukikaa kwenye TV ukatafuta chaneli zinazorusha habari za Neno la Mungu unaweza kushangaa kuona mambo mengine ambayo yanashangaza zaidi kuliko yanayoonekana kwa T.B Joshua na hata mafundisho yako mengine zaidi ya yale ambayo hufundisha yeye. Jambo ambalo naona limezidi watumishi wengi, T.B Joshua ni MTOAJI. Sijawahi kuona kiwango hicho cha utoaji wa watumishi.
  Kwa hiyo ukisema tulikuwa tunakosa nini kwa kutokumfahamu T. B Joshua ni vigumu hasa hadi pale Mtu ATAKAPOJUA AMEPATA NINI KWA KUMFAHAMU T.B JOSHUA. Kama kuna mtu hapati chochote toka kwa T.B Joshua basi huyo yeye HAKUWA ANAKOSA CHOCHOTE kwa kutokumfahamu.

  Jambo jingine ninalofahamu ni kuwa T.B Joshua SIYO MUNGU. Siyo muumbaji wa hayo anayoyatabiri. Ni mambo ambao HATA KAMA ASINGETABIRI, yangetokea tu! Kwa hiyo kutabiri au kutokutabiri HAKUONDOI UWEZEKANO WA MAMBO HAYO KUTOKEA. Kwa hiyo hofu inayopatikana kwa sababu ya kujua kuwa kuna jambo fulani linakwenda kutokea, wale wenye mtazamo CHANYA WANAIBADILISHA HOFU HIYO NA KUWA KATIKA HALI YA MAOMBI ili ikiwezekana Mungu aondoshe hayo mabaya ambayo yameonekana kuwa yanakwenda kutokea. Ndugu Milinga ametoa mfano ambapo T.B Joshua alionyeshwa kuhusu ajali ya Ndege kisha akawasihi watu wawe katika maombi makubwa, na hata alichukua hatua ya kushauri mamlaka husika waangalie namna ya kuepuka tatizo hili. Lakini badala yake watu walidharau, wakafikiri anashida na pesa. Dharau dharau ikaleta madhara.

  Ninanukuu; “Na kama ilikua lazima tupate nabii hizi, why Mungu akusababishaga kwa njia yeyote tuzipate?” Mwsho wa kunukuu.

  Maneno haya nimeyafananisha na yale ambayo watu husema: “Kwa nini Mungu hakutafuta njia mbadala ya kuleta wokovu badala ya hiyo ya kufa msalabani”

  Lakini, Hivi ndg Seleli unafikiri wale ambao INJILI HAIJAWAFIKIA ni kwamba MUNGU HATAKI IWAFIKIE? Maana tunaweza kusema “kama anahitaji injili iwafikie, kwa nini hatafuti njia mbadala ya kuwafikishia Injili kuliko kusubiri hadi wahubiri wafike huko? Kwamba kwa nini Mungu hakusababisha njia yoyote, hadi asubiri TV na Satellite ndiyo tupate habari za Unabii wa T.B Joshua? Hapana. Nadhani kuna haja ya kupanua ufahamu na kuangalia kwa upana zababu tunazotoa kama mapingamizi kwa huduma hii ya T.B Joshua.

  Kipengere kingine ni hili kuwa Yule ambaye hasikii wala kuona habari za T.B Joshua atakosa kile ambacho Wanaoona WANAKIPATA. Lakini pia naomba nikuulize ndugu Seleli Hivi Watu ambao SIYO WASHIRIKA WA KANISANI HAPO ULIPO, WANAKOSA NINI KWA KUTOKUPATA MAHUBIRI YA MCHUNGAJI WAKO? Ukiweza kujibu swali hili, BASI hilo ndilo jibu pia kwa wale ambao wanakosa kuzipata habari za T.B Joshua.

  Nanukuu:

  “aongezaye maarifa huongeza masikitiko…au in my own way…the more much know/informed you are…..the more majaribu, mapito an confusion you will have?”

  Sasa ndg Seleli, hivi unamaanisha kuwa SASA TUSITAFUTE TENA KUJIFUNZA HABARI ZA MUNGU? Hatuna haja tena ya kuendelea kuhudhuria semina kwa kuwa the more we know/we are informed the mora majaribu, mapito and confusion we will have? Mi naona kama ni hivyo basim tuache hata kwenda kanisani. Maadam mtu ameshaokoka, hana haja tena ya KUENDELEA KUJIFUNZA maana akishajua ZAIDI atakuwa anakaribisha ajaribu zaidi? Kama ni hivyo Basi wale watu wa Beroya, kwa KUYACHUNGUZA MAANDIKO walikuwa wanajitafutia MATATIZO. Tutawezaje kuzijaribu kila roho kama hatuwezi kujifunza zaidi habari ya Neno la Mungu? Tutajuaje roho zidanganyazo kama hatuna MAFUNDISHO ndani ya mioyo yetu?

  Ndugu Seleli, unataka kusema WANAFUNZI WA DARASA LA KWANZA WASIENDELEE KUJIFUNZA MAANA WAKIJUA ZAIDI WATALETEWA MASWALI/MITIHANI MIGUMU ZAIDI? Kwa hiyo unawashauri waendelee kubakia katika Darasa LA KWANZA maana hapo ndipo kuna mitihani RAHISI?

  Namalizia kwa kusema hivi, KUJIFUNZA ni jambo jema. Ni vizuri tukaendelea kujifunza. Ni vizuri tukaendelea kujifunza habari za watumishi wa Mungu wanavyofanya kazi ya Mungu. Ni vizuri tukaendelea kujifunza Neno la Mungu. Biblia inasema kuwa KIILA JARIBU HULINGANA NA IMANIYA MTU lakini pia HERI ASTAHIMILIYE MAJARIBU…..! Majaribu ni kama mitihani. Majaribu ndiyo yanafanya mtu amfahamu Mungu zaidi na zaidi. Huu Ukristo wa BILA MAJARIBU au Ukristo wa KUTAKA MAJARIBU MALAINI MALAINI au MAJARIBU MACHACHE nao ni Ukristo Mpya! Ukristo DUMAVU.

  Mtu huwezikutokoa UTUKUFU HADI UTUKUTU au NGUVU HADI NGUVU ikiwa huongezi lolote katika maarifa ya Mungu au hupitishwi kwenye MOTO WA MAJARIBU. Ayubu alipata MAJARIBU MAKUBWA kwa kuwa ALIKUWA MCHA MUNGU MZURI. Lakini alipopita alitoka kama DHAHABU. Majaribu Makubwa Yanaleta THAWABU KUBWA!

  Lakini la msingi hapa ni kuwa KAMA TUNAMKATAA T.B JOSHUA tumkatae kwa Sababu za Kikristo na kwa wakati Huo huo TUNAPOKUBALI WENGINE nao tuwakubali kwa Sababu za Kikristo pia na wala SI sababu ambazo ukizichunguza hazileti MAANA YOYOTE, Kikristo wala Kimwili.

 69. Ndugu wapendwa Wakristo

  Bwana Yesu asifiwe.

  Mjadala ni changamoto

  Nafarijika kuchukua nafasi hii kusema je hivi kweli tumesimama katika nafasi zetu. Zama hizi siyo za kujadili watu. Tujadili Roho Mtakatifu. Tumeambiwa tuenende kwa Roho Mtakatifu. Pia tumeambia imani yako ndiyo itakayokuponya. Na tukumbuke tumepewa malaka mbinguni na duniani; ukiwa na imani unaweza kuamisha mlima kutoka sehemu uliopo kwenda sehemu nyingine.

  Ukweli tukianza kusema kwamba T.B Joshua na wengineo ni manabii au watumishi wa ukweli au wa uongo ni lazima tuenende kwa roho katika Jina la Yesu.

  Naombeni kujua kama kweli umekuwa kiroho kama kila kitu unachokiona kinatokea halafu kinacost maisha na imani za watu. Kinachostahili ni kumuuliza Mungu nini cha kufanya…………

  Naoomba niishiee tuu hapo ila nitaendele kuchangia

 70. Ndugu Sam,

  Naomba nikunukuu kwanza ndipo niendelee:

  “Mtumishi wa kweli ni Roho Mtakatifu. Kwahiyo yeyote anayenena tofauti na Roho Mtakatifu ambaye ni Neno ni mtumishi wa UONGO!!!
  Naona unashangaa kuibiana hela, mimi nilidhani ungeshangaa zaidi, roho za watu zinavyo ibiwa na manabii wa uongo, kama T.B. Joshua na wengine kama walivyojaa Tanzania na dunia nzima wamejaa hivyo hivyo”.

  1. Naona bado hujajibu swali langu, inabidi niliirudie tena:

  Kutokana na maneno yako hayo, Ni mtumishi GANI ambaye Wewe ndiye unamuona wa ukweli, kwa kuwa ananena SAWA SAWA na Roho Mtakatifu. Noamba umtaje kwa Jina, tafadhali

  2. Kwangu mimi ni jambo la kushangaza kwa Watumishi wa Mungu kugombania sadaka na pesa zilizoletwa kwa ajili ya Injili. Hawa nao wako mbali na huo utumishi wao na kwa namna moja au nyingine watakuwa WAMESHAIBIWA TAYARI. Sasa tukiwa na WATUMISHI ambao TAYARI SHETANI AMAESHAWAIBA, je hao Kondoo wanaowachunga WATAKUWAJE SALAMA ZIZINI?
  Kwa hiyo kitendo cha WACHUNGAJI, amba ndio wanoanekana wako salama kwa ajili ya kuwachunga kondoo, wanapokuwa nao WAMESHAIBIWA, Ni jambo BAYA ZAIDI maana hao MANABII WA UONGO watakuwa hawana kazi tena ya kuiba maana ZIZI LIMESHABOMOKA na MCHUNGAJI NAYE AMESHAIBIWA. Hao manabii wa Uongo watakuwa wanachukua TU wala si kuiba tena.

  Naendelea kusisitiza kuwa kama una mfano hai kuwa T.B Joshua ni Nabii wa Uongo, toa basi japo mfano mmoja wa NABII WA KWELI, ambaye umesema hunena sawa na Roho Mtakatifu.

  Nasubiri toka kwako ndg Sam.

 71. Wapendwa,

  Nikiungana na mawazo ya baadhi yenu, nami najiuliza Je nikionekana kwenye Luninga ndio kunamfanya kuwa Nabii wa Kimataifa? Je Ni kuvuta umati wa watu? Hivi ni Karama za uponyaji ndio zinazomkuza Mtu na kumfanya ni wapekee katika Mwili wa Kristo?
  Mpendwa Seleli kauliza baadhi ya maswala ya Msingi….Je Nabii zake zina sehemu gani katika kuujenga Ufalme wa Mungu…? Zambia kuchukua Kombe la Afrika……! Kufa kwa Rais Bingu Mutharika…….! Kufa kwa Geoge Saitoti….! Je Kweli inahitaji ufahamu na ufunuo wa Kiroho kuyapima haya mafunuo ya Nabii Joshua…? Nadhani kweli Neno la Bwana la “Kuwapoteza Hata Wateule” inabidi tulirudie na Kumuuliza Roho Mtakatifu upya lina maana gani…….

 72. Mpendwa Kinyau Hagai!!

  Nakushukuru kwa swali lako na napenda sana nikujibu ila naona, msingi mzuri wa mjadala huu ni majibu ya swali alilouliza ndugu C.k Lwembe na nukuu “Lakini kwamba huyu ni nabii wa lile kundi linaloifunga dunia, nawaombeni ninyi mnaotusisitizia hivyo, hebu tuonesheni ni wapi katika Maandiko Mungu alisema atatuletea huyo na kwa Huduma ipi katika Programu ya Mungu???” Hapa ndio naona utakuwa msingi mzuri wa mjadala wenye manufaa.

  Karibu ndugu Hagai!!!

 73. Inasikitisha kwamba nguvu ya upofu wa Maandiko inaweza kumfunika mkristo kwa kiasi ninachokiona kwa wapendwa niliotegemea kuwa angalau mijadala kama hii inaweza kuwafumbua macho yao ya kiroho pale jambo linapojitaji kulichunguza katika Maandiko. Badala yake wanaleta siasa za dini! Hivi ni Biblia gani iliyowaeleza kuwa nabii TB Joshua ndio kipimo cha wahubiri au manabii? Mbona mnakuwa kama watu waliopoteza mwelekeo? Mna nukuu maandiko out of context hata nimeshindwa kuelewa mnachotaka kukieleza! Hivi Afrika ni nchi mpaka huyo nabii wenu mseme hakubaliki kwao, huku Tz ni Nigeria? Mnalazimisha kumfananisha na Kristo bila hata aibu, eti TB Joshua ni “Jiwe la Pembeni!!!

  Yesu alipokuja licha ya kukataliwa na viongozi wa dini waliopofushwa na Mungu wasimuone, bado alitimiza wajibu wa kujitambulisha na Neno la Mungu lililoandikwa kumhusu yeye. Na aliwaambia Maandiko yanamshuhudia yeye. Mwanamke msamaria pale kisimani ni shahidi wa utimilifu wa ahadi. Yohana Mbatizaji alipokuwa kafungwa alimpelekea Ujumbe Kristo, jibu alilopewa lilimdhihirishia kuwa NDIYE kwani mhudumu hutambulika kwa kazi zake kulingana na Ahadi iliyotolewa na aliyemtuma, basi kama huyo nabii wenu ametumwa na Mungu, ndio nimewaombeni mnioneshe katika Maandiko ni wapi Mungu alitoa Ahadi ya kutuletea nabii huyu na kwa Huduma ipi?

  Badala ya kuja na jibu, mnaleta hadithi nyingi za kutupumbaza. Jibuni mlichoulizwa kwanza, ili tuwaelewe vizuri iwe rahisi kuchukuliana nanyi, kama ninyi ni wale mashabiki wa MIKUTANO MIKUUUBWA ya Injili ya Masihi Benny Hinn na TD Jake nk au ni wafuasi tu wa TB Joshua na katika ufuasi huo mmeuza hadi Haki yenu ya Wokovu na sasa mnameza tu chochote kitokacho katika mimbara hiyo wala hamna uwezo tena wa kuvikagua kama vinaendana na Maandiko, vingenevyo mngekuja na hoja za kimaandiko badala ya kejeli mnazozileta!!! Jihadharini, Neno la Mungu liko wazi, mnaposhabikia kisichokuwemo katika Maandiko ni sawa na mtu anayejirusha bwawani wakati hajui kuogelea!

  Kwa taarifa yenu, hao wahubiri wenu mnaowaona WAKUUUBWA, itakuwa ni kwa sababu ya uchanga tu wa kuyajua Maandiko au ulimbukeni wa show za injili za kwenye Tv tu, bali hapa bongo wako wakali kuliko hao! Kama huyo TD Jakes wenu ni muhubiri mkubwa kama mlivyodanganyika, mbona dakika za mwisho za safari yake kwenda Zambia, aliposikia kuna Ebola akakacha! Mungu anaogopa Ebola?

  Mungu akitupa uzima tutawaona wengi sana wa staili ya Joshua, tena amesema watashusha mpaka mioto toka juu, yaani ningependa niwaone mnavyojitupa chini kuwasujudia hao na miujiza yao! Kwa leo nimewaona mlivyo jiprostrate kwa huyo medium wa liprincipality linalohudumu kutoka seat hiyo ya Nigeria kiroho! Jambo msilolijua ni kuwa yawezekana mmekwisha tiwa mhuri na huduma hiyo ndio maana wahubiri wenu mnawaona takataka, poleni sana, maana huko mlikovutiwa ndani ni NGOME, na kwa vile mmeingia kwa HIARI yenu wenyewe, WOKOVU ndio BYE BYE maana hakuna Damu tena kwa ajili yenu!!!

  Pooooleni!!!

 74. Hi ! All,
  Some comments hapa nimekubaliana nazo kabisa na nyingine,,,,, I afraid not! Nachangia kwa kuuliza very critical and serious questions hapa na kama wewe ni wale aina ya waliookoka wa majijini na mijini nawa ki dot com fashion plus waki- globalize Pentecost Christianity vs. Basic Biblical Pentecost Christianity au ni wa aina ya wapendwa ambao wana upole na uungwana( kama kweli ni upole na uungwana unatakiwa Ki-Mungu) wa kiiiila kitu aaaaaaamen, kila issue Bwana asema,ameniambia, amenionyesha bila kutumia nafasi yako kama mtoto upendwaye sana na Mungu, hutanielewa na maswali yangu yatakua kwazo kali kwako ,jamba ambalo sijali hasa inapokuja swala la kuuondoa ujinga na upofu uliofunika church siku za leo

  Swali: Katika ufahamu wako kama mtu wa Mungu uliyejaa Roho Mt, uko na Neno kwa usahihi ndani yako na kwa ufahamu wako, uko connected na Yesu na Mungu anaogeaga nawe kwakua Bwana huongea nasi wanae kwa hakika, What do you think is a special difference btn your prophet TB Joshua na mchungaji wako wa kule kijijini anayempenda Yesu na kupiga kazi ya Bwana ktk tabu na hutakaa umuone ktk TV zenu kwakua washirika wake ni may be kumi, au mia na sadaka haitoshi kua katika TZ? Tell me guys tofauti iyo ni ipi kwa kutumia viwango vya Ki Mungu na ki Biblia inapokuaja maswala ya utumishi na kumtumikia Mungu na Mungu anavyopima na atakavyo pima watu wake kuwalipa sawasawa na kazi zao?

  Swali: Kama tofauti haipo, je hamuoni kwamba kinachobaki ni human factor na not God’s factor? Yaani kukuza watu, kuwapandisha saaana, kuaspecialize weeee, kuwafanya wawe semi-gods or superhuman?

  Swali: Ivi kutoa unabii kuhusu mtu au wtu, taifa, jamii na ulimwengu na kusafisha maliwato ya kanisani kwako, kuosha magari ya mchungaji kanisani, kumsaidia mdada mmoja gauni mbili tu yule anayekuja na nguo moja tu nusu mwezi kanisani, kumshuudia mtu mmjoa teja akaookoka, kuna tafauti mbele za Mungu? nani zaidi? nani kapiga kazi kuuuuuuubwaaaaa ya utumishi mbele za Bwana kama ulinganishaji huu unakubalika ki Biblia kwakua comments kwa Joshua na unabii wake ni kama una comparisons elements! In your comments, he is taken to be the hero of Africa…… ooh My God, what a stupidity and spiritual corruption? Jesus Christ! I thought my here is my Jesus (Holy Sp and God the father) and second to him is my man of God….my spiritual dad…my pastors! Kumbe ni another people’s man of “God” or god? spiritual infantry of its kind indeed, What a church in this generation?

  Swali: What real made TB Joshua TB Joshua the “true prophet of God” to you? Is it TV and other media advertisements or……what if there was not media to bring him to your room, country, who would be your prophet?

  Swali: Nimetumia maneno ya dot com or globalization kumaanisha haya tuyaonayo leo ya huduma au kipaji kimoja kukuuuuzwa na kuchukuliwa kua ni unique kuliko vingine ni mambo ya kileo zaidi, na kibinadamu—a man made heretical doctrine kwakua miaka ya 1940-1990 wakati akina watu a Mungu haswaa akina Wazee Moses Kulola, Emmanueli Lazaro, Kapiga, Kishimba, David Kuselya nk…kwa wanojua Historia ya upentecost au imani hii ya KUOKOKA ilivyoanza TZ, haya hayakuwepo,it was typical Biblical basics despite some conservatism of some issues in living the Pentecost faith in their days, sasa where was Holy Spirit siku izo atofautiena na wa leo ktk mambo ya msingi?au roho mtakatifu wenu wa leo ameaamka sana na yuko makini saaaana na creative sana kuliko Roho Mt wa wazee hawa ambao wengi wetu ni matunda ya kazi yao ktk nchi hii labda kama humu yupo aliyeishi ulaya na marekani, otherwise yeyoye aliyekuwepo Tz miaka ya 1940 todate kama ameookoka, trace back ameaokoka kwa kushudiwa nanani au huyo aliyemshuudia nae alishudiwa na nani na huyo pia alihudhauria mkutano wa nani wa injili labda tukiondoa wale wachache saaan walotokewa na Yesu mwenyewe!

  Swali: From Biblical point of view, all prophesies given in the Bible were at the end of the day aimed to restore back people to God (in the old testament) or bring people to Jesus (in the new testament) or rarely prepared the saints of the prosecution coming for the sake of the work of God (Paul, Peter), nothing more, nothing less, therefore….
  • Can sb tell me what has been the purposes of TB prophesies in reference to the above Biblical context?
  • Will you also categorically establish the differences btn prophesy given out of holy motives vs. human proudness, famousness, uniqueness building, human creativity (crowd pulling), satani/darkness powers etc?
  • Has there been any advantage of his prophesies to the church, children of God, and unsaved?

  Swali: Kwani what happened huko nyuma kabla ya kumfahamu TB Joshua na nabii zake? Tulipata hasara gani kwa kutofuatilia nabii izi au tumeshaadhirika na nini kama kanisa, mtu mmoja mmoja na Africa kwa kutotekeleza nabii izi? mbona ilikua peace tu siku zote za nyuma until recently after tv na settelite technology kuja third world ,yaani tena waaalaa kulikua hatuna mapressure mnayotupa sasa kwa kutuambia anayotabiri kila mara! Na kama ilikua lazima tupate nabii hizi, why Mungu akusababishaga kwa njia yeyote tuzipate? Au kwa wapendwa waliopovijini sasa hivi wasiofuatilia mambo haya wanampenda Yesu na hawana hata tv au ving’amuzi kunasa wahubiri wa nje, wanakosa nini mnafikiri? Watapata hasara gani ambazo nyie wa town/cities hamtatazipata? Hamuoni ni matatizo yetu tu aliyosema Mfalme Suleimani…aongezaye maarifa huongeza masikitiko…au in my own way…the more much know/informed you are…..the more majaribu, mapito an confusion you will have?

  Otherwise, bless u all

 75. Wapendwa,

  Nimerudia kusoma karibu michango ya watu wote kuhusiana na mada hii. Katika mchango ulionishangaza sana ni wa Amina wa tarehe 13/6/2012, siku ya Jumatano. Ndugu Amina kwenye mchangao wake aliandika hivi;
  “Mi mwenzenu huwa simuelewi huyu baba.hlf mbona anapenda kushika biblia mkono wa kushoto? tofauti na watumishi wengine wa Mungu wanashika na mkono wa kuume”

  Mchango huu kama nilivyosema hapo mwanzo umeniacha hoi kabisa!! Hivi kweli watu wa Mungu tunataka kuwajua watumishi wa Mungu wa kweli na wasio wa kweli kwa kuangalia namna wanavyoshika biblia zao wakati wanahubiri?

  Kwa mchango kama huu wa dada Amina, anataka kutuambia kwamba Mungu alifanya makosa sana kutupa mikono ya kushoto kwa sababu haifai hata kutumika kushika kitabu kitakatifu yaani biblia?

  Kushika biblia kwa mkono wa kushoto au wa kulia kunatoa ishara gani ya kuonyesha kwamba huyu ni nabii wa uongo na huyu ni wa kweli?

  Hebu watu wa Mungu tukue kiroho, maana tunapobaki kuangalia vitu vidogo vidogo kama hivi alivyovisema Amina, maana yake tumedumaa kiroho na ni hatari sana kwa kanisa kudumaa kiroho. Mungu wetu anasikitika sana anapotuona tumedumaa wakati alituzaa mara ya pili ili tukue katika wokovu, na kukua katika wokovu ni kuwa na uelewa wa maandiko yake kiasi kwamba tunaweza kuyatumia hayo tu kujua yupi ni nabii wa uongo na yupi ni wa kweli. Kama ambavyo mzazi wa kidunia anavyosikitika na kuumia mtoto wake anapodumaa na kutokukua, ndivyo na kanisa la Tanzania linavyosikitisha mbele ya Mungu kwa udumavu wake.

  Kanisa la Tanzania limefika mahali pa kuona kila chakula kigumu cha kiroho hakitokani na Mungu aliye hai na kwa maana hiyo limefika mahali pa kuwakataa hata watumishi wa kweli. Naomba nieleweke vizuri kwamba sisemi hakuna watumishi wa uongo, wapo tena wengi sana, lakini kama watumishi au manabii wa uongo wapo uwe na uhakika kwamba na wa kweli wapo pia. Sasa ni juu yako wewe kama kanisa kuwatofautisha watumishi hawa kwa kigezo cha neno la Mungu tu na wala si kwa kuwatazama wameshika biblia mkono wa kushoto au wa kulia, huo ni mtizamo au kigezo finyu sana ambacho hakistahili kutolewa na mtu aliye na Roho wa Mungu ndani yake.

  Labda kwa kifupi kabisa Ndugu Sam, hebu tueleze ni kwa vipi T.B. Joshua ananena kinyume na Roho Mtakatifu, maana tukilijua hilo nadhani hapo ndipo patakuwa ni msingi wa mjadala huu.

  Mungu awabariki wote.

 76. Sam: Mathayo 6:23, Luka 11:35 inasema LAKINI JICHO LAKO LIKIWA BOVU MWILI WAKO WOTE UTAKUWA NA GIZA.

  Haya ndiyo niliyokuwa nayasema. Walokole wengi wa Tanzania, akiwemo sam hawajui tofauti kati ya shetani na Mungu.

  Mimi nasema kuwa ikiwa “kukomaa au ukubwa wa kiroho” ni kupinga watumishi halali wa Mungu basi aina hiyo ya ukiroho mimi siutaki. Nachagua uchanga ili kumpendeza Mungu.

 77. John Paul!!
  Mtumishi wa kweli ni Roho Mtakatifu. Kwahiyo yeyote anayenena tofauti na Roho Mtakatifu ambaye ni Neno ni mtumishi wa UONGO!!!
  Naona unashangaa kuibiana hela, mimi nilidhani ungeshangaa zaidi, roho za watu zinavyo ibiwa na manabii wa uongo, kama T.B. Joshua na wengine kama walivyojaa Tanzania na dunia nzima wamejaa hivyo hivyo.

 78. Nduta,

  Hivi kunatofauti gani kati ya Sheikh Yahaya na T. B. Joshua??
  Nduta usibaki katika uchanga wa kiroho siku zote, kumbe wewe bado haujakua!!!!

 79. Ajabu kabisa………

  Hivii ni Nabii gani kwenye Biblia au mahali popote ambaye alitabiri jambo ni LAZIMA ALIZUWIE LISITOKEE? Nimesoma maoni ya watu weeengi wanatumia hiyo kuwa ndiyo sababu kuwa T.B Joshua siyo Mtumishi wa Mungu aliye Hai.

  Sasa kwa upande mwingine, Mnataka kusema Nabii akimtabiria Mtu jambo JEMA ni lazima pia ahusike kulifanya LITOKEE? Inabidi kumuomba Mungu tena ili afanikishe lile jambo? Sasa Kutabiri maana yake ni nini basi?

  Ndugu Milinga, Gwamaka GD na Nduta wameandika mambo ya msingi sana. Kwa kuongezea tu ni kuwa kuna tatizo ninaloliona sasa kwa watanzania ni kuwa SI WATAFITI wala WAFUATILIAJI wa mambo, yawe ya Kiroho au hata ya Kimwili. Tuna ushabiki mwingi ambao mtu anaweza asiwe na data za kutosha kumfanya ashabikie jambo hilo. Tatizo hilo limetuingiza hadi katika mambo ya Siasa za nchi yetu na mambo ya kiuchumi. Siyo rahisi sana kumkuta Mtanzania anafuatilia mambo ya Nchi yake. Lakini kila kona ukipita utakuta watu wanalalamika hali mbaya ya nchi. Ukimhoji mtu kuwa anajua nini kuhusu mwenendo wa mambo ya uchumi au ya nchi yanavyokwenda, unaweza ukashangaa kuwa hata hao wanaohusika na mambo ya nchi hawajuwi kabisa!

  Tatizo hili limeingia hadi katika mambo ya kiroho. Inasikitisha kwa kuwa kuna watu hata kanisani huwa hawaendi, lakini ukimsikia anasema kuhusu mtumishi fulani unaweza ukafikiri wanafahamiana kibinafsi. Hili ni tatizo. Mi nafikiri ile kanuni ya “No research No wright to Speak” inahusika pia katika mambo ya kiroho! Ndiyo maana Neno linatushauri KUZIJARIBU kila roho. Kujaribu ni “Research”. Ndugu Milinga ameelezea kwa kirefu jinsi anavyofanya UTAFITI kwa watumishi. Wakati wote BIDII inahitajika katika mambo ya Kiroho pia.

  Nikigusia kidogo aliyoandika mpendwa Nduta, ambayo kwa kweli yameniuma sana, ni kuwa UKRISTO wa Tanzania unaharibika kwa kuwa imekuwa ni BIASHARA Mno! Ngoja nitoe mfano mmoja; (Ni mfano tu japo ni tukio la kweli):

  Kuna mtumishi mmoja huko Magharibi mwa Afrika ambaye alitumiwa pesa na mtumishi Benny Hinn ili aandae mkutano, semina ya Ndani. Benyy Hinn alipofika kule akaona kuwa watu waliohudhuria ni wachache. Akalinganisha na pesa alizotuma kuandaa mkutano huo akaona kama amehujumiwa. Yale maneno yalimfikia Mtumishi huyo, ambaye alikuwa mwenyeji wake. Na ilitokea kuwa mtumishi mwenyeji alisikia maneno hayo wakati Benny Hinn amesharudi kwao. Yule mtumishi akaona kuliko kulumbana, AKAMTUMIA BENNY HINN MARA MBILI YA PESA ALIZOTUMA AFRIKA KWA AJILI YA KUANDAA MKUTANO ULE! Ilibidi Benny Hinn AOMBE RADHI KWA KUZUSHA MANENO YA UONGO!

  Tatizo letu Tanzania ni kuwa watumishi wa Mungu wa kwetu SIYO WATOAJI. Na ikitokea wametoa basi ni kwa wenye MAMLAKA FULANI, kwa ajili yakupata Umaarufu au Ulinzi katika shughuli zake zinazogongana na mambo ya Serikali. Laiti Watumishi wa Tanzania wangekuwa ni watoaji, kutoa kwa wenye Shida, HAKIKA Kanisa la Tanzania lisingekuwa hapa lilipo!

  Kwetu kinachosikika ni KUPADA MBEGU tu na Kuweka masharti magumu kwa watu ili kupata Baraka za Mungu. Ni wakati sasa watumishi wa Tanzania wajifunze Utoaji. Wajifunze kufanyika Baraka, kama afanyavyo T.B Joshua. Hilo litafungua utajiri ambao tunaweza kuandaa mikutano wenyewe na kumualika mtumishi yeyote ili aje ku-Hudumu, pasipo KUTEGEMEA YEYE NDIYE AGHARIMIE KILA KITU.

  Halafu sehemu mbaya ya hili ni kuwa wahubiri wa Ulaya, Marekani na nchi zingine zilizoendelea wamekuwa wakitumiwa kama Chanzo cha Mapato! Wachungaji wengi huingia kwenye mitandao, wakiomba mkutano, na wakikubaliwa huorodhesha gharama watakazotumia kwa ajili ya mkutano. Mtumishi anapotuma pesa hizo nchini, pesa hizo huchakachuliwa huku wakiondoa baadhi ya mambo ambayo waliahidi kuwa watayatekeleza kuandaa mkutano huo. Lengo ni kuwa mkutano ukiisha WABAKIE NA CHOCHOTE kwa ajili ya kuendeleza maisha yao. Na hapo ndipo, inapotokea MGAO umekwenda ndivyo-sivyo Ngumi, Vurugu, kutengana na Mafarakano meeengi yamekuwa yakitokea kila baada ya mkutano mkubwa kumalizika. Ninayo mifano mingi hai, ambayo inasikitisha kabisa! Kwa hali ya namna hiyo siyo rahisi kupata UPENYO katika Uimwengu wa Roho Mtakatifu kwa Ukamilifu.

  Inasikitisha sana kuwa hata kwa Ujio wa Watumishi wa Mungu, watu wanataka kutajirika na “Gate Collection”. Sasa Utumishi wetu kwa Mungu ni upi? Hali hiyo imeathiri sehemu kubwa sana ya Ukristo wa Tanzania.

  Ninamalizia maoni yangu na swali kama ifuatavyo: Sijawahi kusikia nchi hii, mtumishi fulani akisifiwa kuwa ni Mtumishi wa Mungu kweli. Ambacho husikia ni kila mtumishi akisemwa ni wa Uongo, mara anatumia nguvu za Nigeria nk. Sasa mi nauliza hivi:

  Kwa wale wanaosema au ambao hawaamini kuwa T.B Joshua ni Mtumishi wa Mungu aliye Hai, Je, Unamfahamu mtumishi yeyote, Nabii, Mtume, Mchungaji au mtumishi ye yote ambaye UNAWEZA KUMNYOOSHEA MKONO KUWA NI WA KWELI? [Maana kama tunaweza kuwaona wale wa Uongo ni LAZIMA tuwe na uwezo wa kuwaona na wale wa Kweli pia].

  Ninaomba kupata jibu la swali langu.

 80. Biblia inasema, Yesu hakuweza kufanya miujiza huko kwao Nazareth, kwa ajili ya upinzani (ukosefu wa imani) Mathayo 13:58, Marko 6:5,

  Ndio maana Tanzania hata siku moja husikii ikitokea katika unabii. Tanzania mananabii wake ni kama sheikh Yahaya ambao hata walokole wanamwamini.

  Kwa kuwa wanakataa manabii wa kweli kama T.B. Joshua Mungu anawasukumia kwenye akili zao mbovu ili wawaamini wachawi na waganga wa kienyeji. Hapa Afrika mashariki na kati mpaka kusini Tanzania inaongoza kwa ushirikina na uchawi.

  Nchi ambayo mpaka watawala wake wanajulikana kwa ushirikina. Ma albino wanauawa kama wanyama katika nchi hii kwa imani za kishirikina. Yote haya yanaotokea ilhali walokole wakijifanya wako kiroho sana.

  NDIO MAANA HAKUNA UNABII UNAOTOKA KUIHUSU TANZANIA. NDIO MAANA HAKUNA HATA WAHUBIRI WAKUBWA KUTOKA NJE WANAOPATA KIBALI CHA KUJA TANZANIA.

  KINA BENNY HINN, T.F.JAKES, NA WENGINEO IMESHINDIKANA KUJA TANZANIA. KWA SABABU YA MATATIZO YA KIROHO YA “WALOKOLE WA TANZANIA.

  Nilisikia karibuni Kanisa moja likadai kumleta T. D. Jakes na kutoza viingilio vikubwa kisha wakawaletea video tu.

  Na hili kanisa hapa Tanzania ndio kiongozi wa kupinga manabii na watumishi wa kujitegemea (Independent Nondenominional churches).

  Watanzania acheni Kiburi (pride). Mtu mmoja alisema ili kujifunza “uliza maswali badala ya kutoa maoni juu ya mambo usiyoyajua.

  Wahubiri Mashuhuri wanakuja kutembela nchi zinazotuzunguka kama Uganda, Kenya, Malawi, Zambia, Burundi, Rwanda, Mozambique, DRC n.k Lakini Tanzania hawakanyagi ng’oo.

  Walokole watanzania hamna lolote. Ndio maana hata serikali inawadharau walokole wa Tanzania. Kwa wababu ingawa wanajifanya wanajua sana lakini ni mbumbumbu wa maandiko na hekima ya kweli itokayo mbinguni. Yakobo 3:17

  nawapa pole kwa kumbeza nabii mkubwa kama huyu.

  Kwa kumalizia nataka niseme kuwa, ukichunguza nabii zote katika biblia huja katika mfumo wa fumbo. Angalia kitabu cha ufunuo. Hivi unafikiri kwa nini Mungu huwa anaweka fumbo? ili watu wenye viburi wasinufaike na ufunuo huo.

  Hata nabii za agano la kale zilikuja kwa mafumbo. Ndio maana waisraeli mpaka leo bado wanaamini masihi bado hajaja. Kwa sababu Yesu alikuja akiwa katika hali ya “kukanganya” . Jiwe walilolikataa waashi limekuwa jiwe kuu la pembeni.

  HATA SIKU MOJA UNABII HUWA HAUJI MOJA KWA MOJA. UNAKUJA UKIWA KATIKA HALI AMBAYO UNAHITAJI IMANI KUUAMINI.

  Hivi unafikiri ni kwa nini Mama jusi waliona nyota ya Yesu alipozaliwa? Yote ni mazingira yenye utata kidogo.

  Ahsante

 81. Nabii, ndugu zangu, ni kipawa ambacho mtu huzaliwa nacho. Maandiko yanatufunza kuhusu Manabii wa Uongo na si Manabii Waongo! Nabii wa Mungu huleta Neno lenye kuongoza katika wakati unaohusika tena likiwa na rejea ya Maandiko. Hiyo ndiyo Huduma yake Kuu. Pia huweza kupewa maono yanayo husika na jamii, hivyo kuitaarifu jamii kadiri ya Mungu alivyomuonesha au ikiwa ni jambo la kufichika, basi hilo huambiwa kusanyiko, wakati mwingine yeye huoneshwa litakalo tokea na maombi hufungwa kwa hiyo hawezi kuliombea jambo hilo bali atakutaarifu tu ujitayarishe na kama ni mbishi ndio hivyo!

  Sasa, mambo ya utabiri wa matukio ni sehemu ya utendaji wa kipawa hicho, lakini utabiri pekee haumthibitishi nabii kuwa ni wa kundi gani; yule aliye simikwa kwa kazi ya Mungu au ni wa kipawa tu kisicho na majuto. Bali wote wawili huweza kutoa unabii tena unaotoka kwa Mungu; Nabii wa Uongo na Nabii wa Kweli, kama tunavyomuona Balaamu na Musa. Wote wawili walikuwa ni manabii, mmoja wa Uongo na mwingine wa Kweli!

  Kwa hiyo, suala la kumtambua nabii kuwa ni wa kundi gani, ni jambo linalohitaji Uongozi wa Roho Mtakatifu kulingana na Imani yako katika Neno la Mungu. Kwani kimsingi kipawa hicho cha unabii kimegawanyika katika mafungu mawili. Moja ni lile la manabii waliowekwa katika makusanyiko ili kuyahudumia. Kundi hili huwaletea habari kusanyiko kulingana na kile Mungu anachotaka kuwajuza kusanyiko lake. Mipaka ya kundi hili ni kusanyiko lao tu! Kipawa hiki hakiwezi kuvuka kusanyiko lake kwani katika makusanyiko mengine wanavyo vipawa hivyo pia, kama ni makusanyiko yaliyo chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu. Hata suala hili la nabii huyu walipaswa kupewa majibu ya Huduma hiyo katika makusanyiko yao! Haya, labda kundi hili la manabii tuliite ‘manabii wa kanisani’ katika maana ya kusanyiko.

  Kundi la pili ni la manabii wanaokuja na Neno la Wakati kulingana na Majira katika Programu ya Mungu ya Ukombozi. Huduma ya hawa huifunga dunia yote katika ujumbe unaoletwa, ikiwa ni Nuru kwa kanisa kama Mwili wa Kristo, Ujumbe huo ukilivusha kanisa kutoka hatua liliyomo na kuliingiza katika hatua ya mbele zaidi. Yaani kwa ujumbe wa nabii wa fungu hili, dunia hutenganishwa, kulingana na Maandiko, yakijithibitisha kutimia kwake; nao wampokeao nabii huyo hupata thawabu ya nabii au huipokea hiyo Neema, na wamkataao, pia hubaki huko nje ya huo Ujumbe!

  Kwa hiyo kwa watu kudai kuwa sijui nabii huyu ni baraka ya Afrika, nadhani ni uchanga tu wa kutokuyajua Maandiko yanachofundisha, au ni ushabiki tu wa kawaida ambao madhara yake waweza kujikuta katika hali usiyoweza kujirudi na kuishia pabaya! Au waweza kuendeleza sifa hizo ukiwa ni mfuasi wa kusanyiko hilo, si lazima uwe umefika huko Nigeria, bali kulingana na wakati tulionao ambao ni wa kiroho, unaweza kuwa mfuasi wa kusanyiko hilo kwa kushiriki ibada hizo kwa TV au mitandao nk, kwa hiyo huyo kwako huwa ni nabii wa kweli na unapojaribu kumfanya ni wa mataifa, hiyo ni haki yako, nao utakaowaaminisha katika hilo pia ni halali yako maana Mungu huwatunza wanae kwa kuwapa KWELI yote. Basi ukimkuta mkristo ambaye kusanyiko lao hawana Vipawa vya Kweli, huyo ni halali yako!!!

  Lakini kwamba huyu ni nabii wa lile kundi linaloifunga dunia, nawaombeni ninyi mnaotusisitizia hivyo, hebu tuonesheni ni wapi katika Maandiko Mungu alisema atatuletea huyo na kwa Huduma ipi katika Programu ya Mungu???

  Nasubiri kwa hamu kutoka kwenu ili nasi tulio na mashaka mtuondolee hayo!

  Mbarikiwe.

 82. Mpendwa Steve,

  Hebu soma 2 Samweli 12:1-23, uone Nabii Nathani alivyoona kifo cha mtoto wa mfalme Daudi ambaye alizaliwa na Bathsheba, lakini hakuweza kuzuia kufa kwa huyo mtoto. Hata baada ya kujua hilo Daudi naye alifunga na kuomba kwa siku saba, bado mtoto alikufa.

  Kwa hiyo, nabii kuona janga linalokuja mbele yetu na kutuambia, haina maana kwamba ana uwezo wa kulizuia janga hilo lisitokee ingawa ni kweli kwamba anaweza kuomba na Mungu akaepusha janga hilo.

  Nilichotaka kusema ni kwamba kwa Nabii kushindwa kuzuia janga lisitokee sio kipimo pekee cha kuonyesha kwamba nabii huyo ni wa uongo au hatokani na Mungu, vipo vigezo vingi sana ndani ya neno la Mungu la kumjua nabii wa uongo na nabii wa kweli.

  Ubarikiwe na Bwana.

 83. kama anaonyesha matukio ya majanga kwanini nabii huyu havunji roho hizo, hapo mimi ndipo huwa napata ??????? kuhus’iana na nabii huyu. Neno la Mungu linasema wazi tuna mamlaka ya kufunga na kufungua inakuaje kwa nabii huyu!!!???

 84. Thanks Millinga! Naamini umekuwa msaada kwa mwanafunzi ila umekuwa kwazo kwa Mwamini…kwani kunatofati kubwa kati ya mwamini na Mwanafunzi (There is big difference believer and Knower) watu hawapendi kumjua Mungu ila hupenda kuongea ya Mungu..hizi huduma zipo kwaajili ya kulijenga kanisa pia kiliimarisha! Ni sawa sawa na baraka ina maana ni kuwa navyo na uwezo wa kuishi bila kuwa navyo! So hatuko hapa duniani kupata tu pia kukosa lakini tukiwa na amani na Yesu wetu ndani yetu! Wengi wanafanya kama huduma za kikanisa kama zilivyo za waganga wa kienyeji kwamba tuwe washindi tu au tuepushwe na mabaya la hasha! tuitafakari sala ya Bwana msingi wa maombi yetu…Tusiingie katika majaribu..na tuingiwapo tuepushwe na mwovu…yaani tushinde!!
  NAkumbuka niliwahi kuonyeshwa mara tatu kuwa naende kupata ajali katika trance (Maono hai) wakati naendesha kwenda Mbeya kupitia Moro lakini mwisho wa maono yale ilikuwa inaonyehsa nimetoka salama!!! Nilipofika Morogoro nikamshukuru Mungu kuwa hata pale nimefika salama ..nilipotoka Moro kiasi cha saa saba na nusu nilikaribia Melela nikaona kama vile maono yale yamerudia na aina ileile ya gari kumbe ilikuwa halisia!1lile gari likanisbabishia ajali ileile niliyoonyeshwa mara tatu kabla sijafika Moro japo gari lilikuwa ‘written off ‘ lakini hakufa mtu hata mmoja katika watu saba tuliokuwapo mle!!!! nilijifunza kitu kuwa Mungu anaweza kukuonyesha kitu lakini tukawa nje ya uwezo wetu katika kuliondoa jaribu hata tukiomba vipi!! lakini alinipa faraja baada ya kulipoteza gari lile!!!

 85. BWANA YESU ASIFIWE, Jamani huu mjadada ni muhimu sana kwa watu tunaosema tunamsubiri mume wetu Yesu Kristu aje atupose,Unabii ulikuwepo na upo na utaendelea kuwepo kwa maana Yesu ni jana,leo hata milele,na ushuhuda wa Kristo ndio roho ya unabii,hivyo ukijaa Neno, ukaishi maisha ya utakatifu lazima Mungu aseme na wewe tu! kwa maono, ndoto na sauti na kwa ishara, na watu watakutambua kwa matendo yako na unabii utakotoa lazima utimie,Aliposema tuzichunguze hizo roho tatizo watu wanazichunguza kimwili mwili,mtu hujaingia kwenye maombi kuomba kwa ajili ya huyo mtu unayemuona nabii wa uongo,unaanza kubisha,mimi nashauri wote tunaochangia hii mada hebu tuzame mbele za Mungu,halafu Mungu atajifunua juu ya mtumishi wa Mungu huyu kwani huwa hafichi hasa kama maisha yako ni matakatifu,halafu kila mmoja aseme alichoonyeswa juu ya mtumishi wa Mungu.

  Tunataka tuwekane sawa jamani? jibu tulitoe kwa Mungu anasemaje juu ya mtumishi wake huyu amabaye maneno mengi yanasemwa juu yake,sasa basi namna ya kuomba ili Mungu ajifunue kwako kuhusu mtumishi wa Mungu huyu,anza kutubu wewe mwenyewe,jitakase, halafu muinue mtumishi wa Mungu Joshua tubu kwa ajili yake mwisho ungansha umoja wewe, Mungu na huyu mtumishi wa Mungu Joshua,Jamani sisi si ni watu rohoni,basi na tuenende kwa roho,(Galatia 5:16-22) kila mchangiaji amaanishe mbele za Mungu na jibu tutalipata na tuandike kile Mungu alichotuonyesha ,mimi stella nimeona tufanye hivyo kwa ajili ya kumlinda Kristo,adui asije akapata nafasi .nawapenda wote na AMANI yA BWANA wetu Yesu iwe nanyi.Amina.

  muijilisti Stella Rugoye.

 86. Big up Bro malinga,

  Sina cha kuongeza zaidi ya kukupongeza,umeongea kitu cha ukweli na chenye mantiki,jamii kubwa ya watanzania tunapenda kubisha pasipo kufanya utafiti,Nilikuwa synagouge wiki tatu zilizopita na nimejionea anayoyafanya Nabii TB.Jashua.kama hujafika katika kanisa lake na kufatilia mafundisho yake na una bii anaoutoa Utasema ni Nabii wa uongo.Jamani wapendawa na wanawa Mungu tujifunze kufatilia vitu kwa kina kabla hatujabisha na kueleza vitu vinavyo weza kupotosha watu.
  KWa Unabii alioutoa juu ya maisha yangu ninaamini ni nabii wa ukweli aliye tumwa na Mungu.

 87. Wapenzi katika Bwana,

  Nadhani wapendwa wengi siyo waangalifu wala wabunifu. Inaonekana wengi hawaelewi Nini maana ya Nabii na maana ya UNABII.

  Halafu hapa Tanzania wapendwa wengi ni waoga sana. Wengi wetu huwa tuna tatizo la kusoma vitabu mbalimbali vya waandishi wa Kikristo na wasio wa kristo. Wapendwa wengi huwa tunadandia hoja bila hata ya kuifuatilia kwa kipindi kirefu. Wengi wetu huwa hatuchukui muda wa kutosha kuwafuatilia kwa undani wahubiri na Manabii , Maaskofu na Wachungaji kabla ya kutoa msimamo wetu kumhusu huyo mtumishi.

  Nimefuatilia wapendwa wengi hapa wana maneno mepesi sana. Na wengi inaonekana hata kumfahamu T.B Joshua angalau kwa TV, You Tube, Website, Vitabu vyake, Majalida yake, nk bado wengi hawajamwelewa.

  Ile ndege iliyoanguka Nigeria T.B Joshua alitabiri sana. Hata akawaandikia viongozi wa Uwanja wa Ndege kwamba ile kampuni waifuatilie na ikiwezekana siku hiyo ndege ziache kuruka hewani, Uongozi ulipuuza maoni yake na kumsema kwamba ana njaa ya fedha wakamtumia Dola 10,000 akaamua kuwarudishia pesa hiyo. Wakati anaoneshwa aliliomba kanisa lifunge na kuomba ili Mungu aepushe janga hilo lisiwe kubwa sana endapo lingetokea. Walifunga na kuomba kwa siku 7. Jumapili ya Kuamkia siku ya tukio TB Joshua hata kwenye Ibada alikosa amani kabisa akashindwa kuhudhuria Ibada yote. Kila mara akawa amejificha chumba chake chaa maombi akawa anamwomba Mungu aepushe ajali ile. TB Joshua anasema kama yasingekuwa maombi ya kujitoa sana ndege ile isingeanguka na watu wakapona.

  Swala la kenya nalo ni hivyo hivyo, Maandiko yanasema tuwaombee wenye mamlaka kwani nao ni watumishi wa Mungu. Unabii ule kuhusu Kenya ulimaanisha kwamba watu waombe ili Mungu aepushe ajali ile.

  Jambo lingine, watu waelewe kwamba “MANABII” kama una amini kwamba bado wapo, KAZI YAO SIYO KUKWEPESHA YAAJAYO YASITOKEE. KAZI YA KUFANYA MATUKIO YAJAYO YASITOKEE NI KAZI YA KANISA. Ni jukumu la kanisa kuhakikisha linawasikiliza Manabii wanasema nini kuhusu mambo yajayo kama ni ya HATARI kanisa liombe ili kama Mungu ataona rehema basi yasitokee na kama yakitokea yasilete balaa kubwa kwa watu wa Mungu. Kuzuia jambo lisitokee bado pia itabaki katika moyo wa Mungu tu wala sisi wanadam hatuna mamlaka ya kuzuia jambo lolote lililonenwa na NABII lisitokee.

  Mojawapo ya kanuni ya neno lisemalo, “Zijaribuni hizo roho” au Hao ni Manabii wa Uongo” ni kwa kuwasikiliza na kusubiri kuona kama yatatokea. Hii ni mojawapo ya njia.

  Navyowaona watanzania wengi, hata kama tukiambiwa kwamba Tanzania kuna vita ya kidini inakuja mbele yetu miaka kadhaa ijayo, tutabisha sana badala ya kuomba ili kwamba Mungu atuepushe na balaa hilo.

  Wengi wakisikia fulani ametabiri juu ya jambo fulani hukimbilia kusema huyo bwana ni nabii wa uongo wala msimsikilize. Badala ya kuomba Mungu awape watu wake Neema ya ushindi tunakalia ubishi tu na mijadala isiyokuwa na tija.

  Nabii huyu TB Joshua nimemfuatilia kwa sasa yapata mwaka na zaidi. Namfuatilia kwa TV, Wavuti, Youtube, Twitter, facebook, nk. naendelea kujifunza huduma yake.

  Nabii mwingine ninayefuatilia mambo yake na huduma yake ni GeoDavie wa Arusha, wa Ngurumo ya Upako, Josephat Mwingira wa Efatha, BG. Malisa wa Ukombozi Church, Baba Gody Mfalme wa ulimwengu wa Jijini Mwanza na wengineo walioko hapa Tanzania na nje ya Tanzania. Nawafuaatilia kupitia vitabu wanavyoviandika, TV Programu zao, Magazetini, Radioni, nk. Nalinganisha wanachosimamia na kukiamini na kujaribu kukipima mimi mwenyewe kwenye maandiko. Nikitoka hapa ndipo naweza kusema kwamba hawa ni watumishi wa Bwana aliye Juu au ni wasanii tu wanaotumikia matumbo yao.

  Nabii Askofu Kakobe nilimfuatilia kwa zaidi ya miaka 10 kuanzia mwaka 1990 hadi 2000. Yapo mazuri ayafundishayo na yapo kwa mtazamo wangu hayako sawa. Kwa mfano alipotabiri kuhusu Mzee Augustino Mrema wa TLP kwamba angeshinda urais mimi sikukukubaliana naye kabisa. Nilibishana na waumini wake sana waliokuwa wameamini kabisa kwamba Mrema angeshinda Urais wa Tanzania. Yapo maswala kadhaa mimi hadi leo sikubaliani na Mzee Kakobe hasa kuhusu baadhi ya mafundisho yake. Lakini nafanya hivyo kwa sababu nimeyafuatilia kwa kina hadi kusali kanisani kwake zaidi ya mwaka mmoja.

  Wapendwa tujifunze kutafiti Imani na roho hizo ambazo tunadhani kuwa ni roho zidanganyazo ili hata kama tunawafundisha watu wengine tuwaeleze kwa upendo na kwa hoja zilizoshiba. KUDANDIA HOJA NA KUBISHA KWA KUTUMIA MAANDIKO KUTAPENDEZA ZAIDI KAMA UMEFANYA UTAFITI WA KINA.

 88. Ndugu yangu Japhet Kamanyoro si kila matendo ya ishara na miujiza vinatoka kwa Mungu hata shetani anaweza kuja kama malaika wa nuru.Nikujibu swali ulilouliza kwamba hivi shetani ni mkubwa kuliko Bwana Yesu? Jibu ni hapana isipokuwa shetani anaweza kufanya ishara na miujiza mingi tu. Hivyo si kila miujiza na ishara kubwakubwa inatoka kwa Yesu.Hujasoma maandiko?
  Mathayo 24:24-25 Kwa maana watatokea makristo wa uongo na manabii wa uongo,nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza,kama yamkini,hata walio wateule.Tazama, nimekwisha kuwaonya mbele.
  Hizi ni siku za hatari na kama ni mechi ni kipindi cha lala salama au dakika za majeruhi.
  Ubarikiwe sana ndugu yangu Kamanyoro.

 89. Nyie msiomuelewa huyu Mtumishi wa Mungu macho yenu yafunguliwe muweze kuona ukuu na uweza wa Mungu. Hivi ni lini mtaamini matendo makuu na Ishara za miujiza? shetani anauwezo mkubwa kuliko Bwana Yesu?

 90. mi mwenzenu huwa simuelewi huyu baba. hlf mbona anapenda kushika biblia mkono wa kushoto? tofauti na watumishi wengine wa Mungu wanashika na mkono wa kuume.

 91. Jerry, maono yanaletwa ili tuyatendee kazi, maono hayaletwi ilimradi tu mtu aitwe nabii. Shetani anapokusudia mabaya Mungu huinua mtu na kumpa hayo maono ili ayatendee kazi ya kuomba na kuharibu hiyo mipango mibaya ya ibilisi. Tukumbuke utumishi wa nabii Yeremia, alinuliwa ili kuvunja kubomoa na kuharibu kazi za shetani. Yesu mwenyewe anasema alikuja ili wawe na uzima tele. Sasa inaniwia vigumu kusikia mtu analeta unabii/maono mbaya zaidi maono ya mabaya alafu hakuna way forward ya huo unabii. Wote twajua kuwa Mungu wetu hughairi mabaya sembuse nabii tena mwanadamu! Oooh, ninamuomba BWANA YESU atusadie watu wafunguke macho, akili zetu ziponywe, mioyo yetu imwelekee BWANA maana tunaishi katika nyakati ngumu kushuhulika nazo. Mbarikiwe sana!

 92. mimi ninapata tabu hapo….
  Naombeni mnisaidie
  Hivi kama mkristo wa kweli ukiona tatizo katika maono je haikupasi kuliombea hilo tatizo ili lisitokee.

 93. Dada Anna kama ni nabii kweli kutoka kwa Mungu hatakuwa nabii wa afrika pekee yake atakuwa ni nabii wa watu wote hata walioko Korea maana Bwana Yesu alisema enendeni duniani kote mkawafanye mataifa kuwa wanafunzi wangu.Swala la kusema fulani ni nabii mkubwa ina maana wapo manabii wengine ni wadogo.Lakini jambo hili kwa mwanadamu si rahisi kama unavyodhania.Mungu ameweka maaskofu,wachungaji,mitume, manabii, waalimu,wainjilisti na watumishi wengi tu lakini hakusema wengine ni wakubwa na wengine wadogo. Kila mtu ana nafasi yake katika kuujenga mwili wa Kristo maana sote tu viungo katika mwili wa Kristo. Kusema kuwa najivunia nabii fulani kwangu mimi naona jambo hili limekaa kisiasa na kiushabiki zaidi!
  Wanafunzi wa Yesu walipobishana kuhusu nani aliye mkubwa kati yao, Bwana Yesu aliwaambia anayetaka kuwa mkubwa kwenu na awe mtumishi wenu.
  Mathayo 20:25-28, Marko 9:33-37
  Mungu akubariki.

 94. Africa tunajivunia kuwa na nabii mkubwa kama TB Joshua, Songa mbele kuifanya kazi ya Mungu japo upinzani ni mkubwa. Mungu anaendelea kufanya kazi!

 95. Mimi sioni kama zinaoana kwani Saitoti sio kiongozi wa nchi bali ni waziri hapa naona watu wanachukua tuu advantage

 96. Kulingana na utabiri na maelezo yake naona hayaoani kabisa kwani utabiri wenyewe haujanyooka kwani anasema ni Kiongozi ambaye huenda ni Makamu wa Rais na pia ni angani au ardhini na kisha akabaki kujiuliza tu, ina maana alikuwa anabahatisha hana uhakika na hii ni roho ya utambuzi ambayo sio rahisi kuona kitu kamili ila wakati mwingine hubahatisha na kupata kwa sehemu. Unabii wa sasa hauna nafasi kwetu kwani tunalo neno lililokamilika la Bwana wetu Yesu kristo Lk 16:16. Unabii unaotolewa na T.B Joshua ni utambuzi tu kwani manabii wa zamani mara nyingi walitoa unabii kuonya watu juu ya dhambi ili watu wabadilike na kumwelekea Mungu. Wakati mwingine walitaka watu watubu la sivyo wataangamia, sasa unabii huu mbona hauelekezi chochote kwa wanadamu na Mungu ana kusudi gani juu ya unabii huu, tuepuke kuziamini kila roho kwa maana roho chafu zinazidi kuwapoteza wengi. Mungu atusaidie.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s