Rushwa na Mtu aliyeokoka

Hali ya sasa nchini Tanzania ni mbaya sana. Rushwa imesimama kila mahali, kila mahali!

Je, Katika hali ya kiwango cha rushwa cha namna hii,  Inawezekana mtu aliyeokoka akafanya mradi wake wa ujasariamali na anafanikiwa PASIPO kutoa rushwa mahali popote?

Advertisements

13 thoughts on “Rushwa na Mtu aliyeokoka

 1. lkn wapendwa rushwa imesambaa sn ht ktk kz ya Mungu, kwa mfano mwimbaji chipukizi wa nyimbo za injili umerecod nyimbo zako ukipeleka ktk radio station inabidi utoe chochote ndiyo nyimbo yko itakw inapigwa mara kwa mara. au ukitaka ufanyiwe interviwe inabidi utoe chochote. kwa mfano sisi tuna kwaya yetu tumerecod huu mwaka wa tatu tunazunguka nazo cd. ndiyo kuna mwimbaji akatuambia mpaka mtoe kidogo kitu bila ya hivyo mtaendelea kusota.

 2. Ndugu Milinga na wachangiaji wengine rushwa ni ya hatari. Kama ulivyotoa mfano wa hospitali umesema”Ukilazwa pale halafu wewe mkono wako mfupi yaani hutoi chochote kwa wauguzi (nurses) tegemea kuona mgonjwa wako akifa mapema sana. Hali imeshakuwa mbaya kiasi kwamba ukilazwa pale wagonjwa waliopo wanakwambia kabisa kwamba kama una chochote wewe mpe muuguzi eti kama asante vile ili akuhudumie vizuri”. Ili mgonjwa wako ahudumiwe unalipia huduma ambayo ilikuwa ni haki yako. Katika ofisi za umma ili faili lako lipatikane inakulazimu utoe chochote ati wanaita maziwa ya kuondoa vumbi. Na usipotoa faili lako halitapatikana siku nenda rudi. Kwa mifano hii miwili naomba mnisaidie tuliookoka tufanyeje?

 3. Wapenzi,

  Rushwa ipo kila kona. Naomba niseme tu kidogo pale hospitali za umma. Ukilazwa pale halafu wewe mkono wako mfupi yaani hutoi chochote kwa wauguzi (nurses) tegemea kuona mgonjwa wako akifa mapema sana. Hali imeshakuwa mbaya kiasi kwamba ukilazwa pale wagonjwa waliopo wanakwambia kabisa kwamba kama una chochote wewe mpe muuguzi eti kama asante vile ili akuhudumie vizuri.

  Lakini napenda kulitazama swala hili kwa kona ya pili. Rushwa Tanzania hizi ndogo ndogo zinasababishwa na hali ngumu ya maisha. Yaani mtoa huduma na mwomba huduma wote hali zao za kiuchumi ni duni sana. Maisha yako ya kifedha ndiyo yanayokulazimisha kwenda Hospitali za Umma badala ya zile za binafsi. Ukienda hizi hospitali utakutana na mstari mrefu wa wagonjwa wanaomsubiri Daktari. Halafu hapo hakuna utaratibu wa kueleweka, mara unaona watu wanapita mlango wa nyuma wanapata huduma, kama ungekuwa na uwezo na hauna haja ya kutoa rushwa ungesubiri mpaka zamu yako ifike au uende hospitali za binafsi ambako utakamuliwa pesa haswa. Lakini umasikini wa watoa huduma ndio utakaoona unaanza kufanya kazi kwa kuwaambia watu pembeni, “kama una chochote leta nikupeleke faili lako kwa Daktari” Ukimpa Tshs 5,000 tu utaona unapewa huduma.

  Upande mwingine rushwa husababishwa na mifumo mibaya ya sheria za nchi na watendaji wasiojali wenzao wala kuwa na uzalendo wa kuwajibika. Unakuta mwananchi anafuatilia haki yake miaka nendarudi mpaka anaingiwa kishawishi cha kuwahonga chochote watendaji ili wamsaidie. Ukifika ofisi za umma nyingi utaona kwamba watu wanafanya kazi kama hawataki. Ukiwaomba wakupe huduma fulani wanakwambia njoo kesho, njoo tena kesho mpaka unachoka. Ukarimu kwa wananchi hakuna, upendo kwa wateja hakuna, kujali mteja hakuna, yaani uasi mtupu.

  Mungu atuokoe. Mimi nimewahi kubembelezwa kupokea rushwa ili nitoe huduma hapa ofisini nilipo, lakini nimezikataa nyingi sana. Wengine wanaotaka wanipe kitu kidogo ukiangalaia wanachofuatilia ofisi yangu iwalipe ni kidogo hata nusu ya mshahara wangu hakifiki. Huwa nawakatalia siyo kwa hoja hiyo hasa, bali kwa sababu ya uzalendo na upendo nilionao kwa wateja wangu. Niko tayari kugombezana na wafanyakazi wenzangu wanaochelewesha madai ya wateja wetu. Kumbuka mimi niko ofisi ya umma na wala siyo ya binafsi.

  UKIAMUA KUTOTOA RUSHWA WALA KUIPOKEA INAWEZEKANA. KUMCHA MUNGU NI MWANZO WA MAARIFA YA KUKWEPA RUSHWA.

 4. Wapendwa tunapozunguzia rushwa tujue tunazungumza na roho kamili, tunazungumza na roho jina lake “rushwa” roho hii sio ndogo kama tunavyoitazama. Kuna wakati nilikuwa nafuatilia barua fulani kwenye ofisi fulani, afisa husika alinisumbua sana kuweza kupata majibu. Siku nikakutana nae hoteli fulani akaniomba nimlipie chakula, nikamlipia (si zaidi ya elfu 10) kama ambavyo ningemlipia mtu yoyote, cha ajabu baada hapo akaniambia kesho niende ofisini akanikamilishia, hitaji langu. Badae nikajiuliza kulikoni, ROHO MTAKATIFU akanifundisha kuwa hiyo ni roho ya rushwa ilikuwa inataka niitambue, namshukuru Mungu rehema kunijulisha na kuniongoza katika toba. Nachotaka kusema hapa rushwa ni roho, na usipokuwa makini inatafuta aliyeokoka imdhoofishe, tuwe makini na BWANA atuongoze, katika jina la Yesu, ameni!

 5. Upo uwezekano mkubwa wa mtu kufanya biashara au kuendesha kampuni bila hata kujihusisha na kupokea au kutoa Rusha, Tatizo kubwa hapa ni kwamba waliokoka wengi ni wanafiki wamejiweka ktk mazingira ya kutoa na kupokea rushwa, kama utajiepusha na baraza na shauri la wasio haki(watoa rushwa na wapokea rushwa) utafanikiwa tu!

 6. Kuna kipindi nilimpokea kijana kufanya kazi kwangu kibarua tu. Siku moja aliona amechelewa kurudi au basi tu akaamua kulala nyumba ya jirani kwa mwenzie. Usiku wa saa tisa nilikuja kuitwa na watu kijana anaumwa kitu kama kifafa hana fahamu na povu mdomoni ilibidi nimkimbize hospitali huku naomba. Kufika tuliandikiwa kulazwa na drip wakati wanasubiri vipimo vingine, niliambiwa hamna kitanda, kisha walirudi na kusema nitoe elfu tano wanitafutie kitanda pia nitoe elfu tano mtu wa maabara wamwamshe akachukue vipimo…. rushwa sio wafanyabiashara tu hata huduma muhimu tena ugonjwa wa hatari hupewi hadi utoa hela ambayo mie nadhani ni rushwa… Ila kama ni kitu unaweza kusubiri au kuna fursa nyingine usitoe vitu kama upewe tenda, mzigo sijui utoke haraka bandarini, upate kibali au leseni kwa rushwa sio sahihi kabisa.
  Kwakweli tumwombe sana Mungu maana rushwa imekithiri mno na hii ni kwamba hakuna haki ktk taifa hili, ni chukizo mbele za Mungu.

 7. wapo wafanyabiashara wengi ambao hawajaokoka hawatoi wala kupokea rushwa, mimi ninawajua na naweza kuwataja! ni tabia tu ya mtu! wala si kwa sabab ameokoka au la! MUNGU anatambua mamlaka, fuata utaratibu, hata YESU akisema tozen kiasi kilchowekwa ina maana pia lipeni kiasi kilichowekwa, Mfalme daud alisema usile rushwa wala kuitumainia dhuluma. hata utoe rushwa vp!? kama huna RADHI ya YEHOVA ni bure, usijitetee muache MUNGU akutetee,,,,,

 8. Rushwa ipo makanisani hata ukitaka kuhubiri kanisani, pengine wanataka utoe rushwa!

 9. Ukimtanguliza Mungu hakuna vikwazo vya aina yoyote. Tatizo watu wanapenda njia za mkato, wakishindwa ndiyo wanamtafuta Mungu.

 10. Bwana Yesu asifiwe2 napenda nami kuchangia… kama mtu kweli umeokoka kikamilifu sidhani kama kutakuwa na nafasi ya kutoa rushwa.. kama umekaa vema kiroho kweli hata hizo rushwa zitakukimbia na zitakapotokea pia ww u juu ya yote so unamamlaka ya kuweza kuzitupilia mbali mradi ujue WEWE NI NANI NA UNAFANYA NINI NA UNAJIANDAA KWA MAISHA GANI HAPO BAADAYE. mtazamo wangu. asanteni sana kwa mada. Barikiwa

 11. je kuhusu wafanya biashara waliookoka wanapotoa rushwa na kudanganya ili waweze kupitisha Mizigo yao mipakani wenyewe hamkosei Mungu?

 12. Swali lako ni zuri sana, Biblia imesema njia ya kwenda Mbinguni ni nyembamba, mara nyingi huwa hatuelewi misemo ya Biblia, hiyo ni njia moja wapo ya kwenda Mbinguni, ya kwamba ukichagua kutoa rushwa, au kupokea rushwa, umepitia njia ile pana inakwenda upotevuni, ukishinda usitoe rushwa, wala usipokee rushwa, umepitia njia nyemba, iliyosonga, inayoenda uzimani, ambayo inaonwa na wachache. Math 7.13–14 INGIENI KWA KUPITIA MLANGO ULIOMWEMBA, MAANA MLANGO NI MPANA, NA NJIA NI PANA IENDAYO UPOTEVUNI. NAO NI WENGI WAINGIAO KWA MLANGO HUO. BALI MLANGO NI MWEMBAMBA, NA NJIA IMESOMGA IENDAYO UZIMANI.NAO WAIONAO NI WACHACHE. Mith 17.23 ASIYE HAKI HUTOA RUSHWA KIFUANI, ILI KUZIPOTOSHA NJIA ZA HUKUMU. Kut 23.8 NAWE USIPOKEE RUSHWA, KWANI HIYO RUSHWA HUWAPOFUSHA MACHO HAO WAONAO, NA KUYAPOTOA MANENO YA WENYE HAKI. Mwenye haki hatatoa wala hatapokea rushwa.. Asanteni

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s