USIKATE TAMAA, IPO NJIA

Yawezekana unapita katika magumu na unaona hakuna njia tena NA unakata tamaa. Umefika mahali na unasema siwezi kupata kazi tena, hii kazi siwezi tena, haya mahusiano yamenishinda, hii NDOA imenishinda, hawa watoto wamenishinda, hii shule imenishinda, siwezi kujenga, hii biashara imekufa, siwezi kuwa na biashara tena, n.k…….

Ninataka nikuambie ya kwamba IPO NJIA. Inaweza isiwe rahisi na inaweza iwe ndefu. Hata kama panaonekanika kama hakuna njia, kwa Mungu kuna njia wakati wote. Na kama Yesu ni Bwana na Mwokozi wa maisha yako, basi Roho Mtakatifu anaishi ndani yako. Ubunifu wote ulimwenguni upo ndani yake, na kwa kuwa yupo ndani yako, ubunifu utaupata. Roho Mtakatifu ana uwezo wa kukupa fikra ambazo hujawahi kuwa nazo na kukuonyesha njia ya kufanya vitu ulivyofikiri hutakaa uwezekufanya.

Badala ya kukumbatia magumu, inatubidi kuelekeza mawazo yetu kwa Mungu na tujue ya kwamba yeye yupo kwa ajili yetu na nguvu yake ipo kazini kwa ajili yetu. Tufike mahali tuone ya kwamba iwepo njia au isiwepo Yesu ndiye njia, Roho mtakatifu yupo ndani yangu na nitaipata njia ya kutokea tuu.

Mungu ametuahidi katika Isaya 43:19 akisema “tazama, nitatenda tendo jipya; sasa litachipuka, je! Hamtalijua sasa? NITAFANYA NJIA HATA JANGWANI, na MITO YA MAJI NYIKANI”. Katika injili ya yohana 14:16 Bwana Yesu alisema “Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima”. Yeye ndiye njia, atakusaidia kuiona njia pale inapoonekana kama hakuna njia. Pia katika Wakorinto wa kwanza 10:13 tunafundishwa ya kwamba “Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya mwanadamu; ila Mungu ni mwaaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili”.

Kumbuka Mungu aliwafanyia wana wa Israel njia kavu baharini (soma Kutoka 14), walivushwa mto Jordan (soma Joshua 3). Tazama Injili ya Luka 1:37 “kwa kuwa hakuna neon lisilowezekana kwa Mungu”

Kwa maneno mengine ni kwamba, wakati wote na katika hali yeyote, Mungu ana njia kwa ajili yetu kama tukiitafuta, tukiwa na subira na kama tutakataa kukata tamaa.

Emmanuel J Kwayu

Advertisements

13 thoughts on “USIKATE TAMAA, IPO NJIA

 1. Utukufu apewe Mungu mwokozi wetu aliye muadilifu milele daima.nakushukuru na kukutakia baraka zitokazo kwa Mungu kwa kuendeza kipaji alichokujalia kwa kushauri na kuinua moyo wa wale wanao ona kana kwamba wamefika mwisho kwa kundanganywa na ibilisi.

 2. Emmanule L.

  Ujumbe huu unasukumu Mtu hatua nyingine, blessings 2u.

  Kukata tama si PEPO! wala hakuletwi na shetani! Ni sisi Wanadamu tunaweza ruhusu au gomea kukata tamaa hata kama devo,Watu au majaribu toka kwa Mungu kabisaa yatazalisha hali/changamoto zinatufanya tuone marue-rue! Ni maamuzi tu thabit yatamfanya Mtu kutokata tamaa, kuamua kua na tumaini na kungoja au kuamua kukata tamaa na kujifia Kiimani au hata Kimwili. Hakuna haja ya maombi ya kufukuza pepo la kukata tamaa, halipo! badala yake ni vema kutafanya maombi ya Mungu mtie nguvu falani azidi kusimama imara yaani asikate tamaa mpaka siku ya ushindi wake.

  Wakati mwingine hali/mambo/Watu vyaweza kutuletea mambo ya kutukatisha tamaa lakini ni wakati huo huo ndio mzuri wa kujifunza qualities ktk maisha ya Kiroho, kitumishi na hata haya ya Kimwili kama uvumilivu, kusamehe na kuachilia, ku-take things easy, kutunza lengo lako,-keeping focused, kusoma Neno sana, Kuongeza level ya maombi na utakatifu, kuboresha mahusiano na ndugu, jamaa na Wapendwa, kujaribu kujifunza upande bora wa mwenzio na si kuona upande wake mbaya tu(Mke/Mme/Jirani/boss/mpendwa/kwaya master/Pastor/Mze wa kanisa/Kiongozi wa fellowship nk.), kujali, kutuia mbele za Bwana, kuisikiliza sauti ya RM kila hatua unayotaka kuichukua wakati uwapo matatani/majaribuni nk

  Notice: Kujua pia kua tu Wanadamu na tunaishi hapa si Juu na kwamba yanayotutokea ni lazima yaje maana tuko hapa na kwamba wapo pia wengine wetu jana, juzi na leo wanapitia hayo hayo na tena ya kuzidi sisi, ITATUSAIDIA KUA NA SHUKRANI kwa kila jambo MBELE ZA BWANA badala ya kumuwazia Mungu kwa upumbavu, kunung’unika, kulalama, kumtukana au fyonyaa/nzaa Mungu kimya-kimya maana umechukua kwa kua mambo hayakwendi au yamekwama au yamekuzidi kwa mtazamo wako wewe kama Mtu. Lakini pia kujua wako wengine walipitia na wanapitia na wako imara, itatusaidia kupunguza au kuacha kabisa kudeka-deka, kulia-lia na kusumbua/kuchukia Watu/wapendwa/Wachungaji kua hawakupendi au hawajali badala yake utafanya kama Daudi…AKAJITIA MOYO KTK BWANA…hakusubiri ati mpaka wapendwa wa-sense, waje na kufanya, saa ngapi kwanza wako busy na Kaizari na kusaka Mkate, so akawahi-wahi kivyake vyake safi kabisa, akijitia uhai/nguvu/changamko/imani/tumaini/furaha/raha/ ungangari ktk Bwana na kusonga mbele.

  Press on

 3. Barikiwa mtumishi kwa ujumbe wenye upako.kukata tamaa kupo sana kwa watu wasio weka tumaini kwa MUNGU

 4. ASANTE SANA KWA UJUMBE UTIAO NGUVU. KWAKWELI MARA NYINGI MAZINGIRA HUTUMEZA ILI KUTUSUKUMA NJE YA IMANI! TUNAPOPATA UJUMBE AU MAFUNDISHO KAMA HAYA YUMKINI TUNAFARIJIKA NA KUREJESHWA UPYA KTK NGUVU ZA KIIMANI. UBARIKIWE SANA NA BWANA YESU.

 5. Ahsante unatutia moyo sana tuzidi kuishi kwenye iman Mungu akuzidishie mawazo mazuri

 6. Jamani , ninashukuru sana kwa hili somo maana, naona ni kwa jili yangu hasa maana ninapita katika kipindi fulani kigumu sana, na nilikuwa ninatafakari mara nikakutana na hili somo, kweli ipo njia hasa pale tunapovumilia na kusubiri mapenzi ya Mungu yatumie .
  Mungu akubariki sana mtoa somo, limenitia nguvu kubwa.

 7. Haleluya!
  Usikate tamaa ipo njia ,Sikia kukata tamaa ni mpango wa shetani,ktk ufunuo 6:1-2 ,inasema tumempanda farasi mweupe na tumepewa eta ili tupate kushinda,nitafafanua hapo kama roho anavyoniongoza,farasi mweupe ni huduma zetu lazima ziwe safi takatifu,yaani wewe uliyemwamini lazima ujue una huduma gani ili kuipeleka injili ya Bwana wetu Yesu kristo kwa kila kiumbe,ktk zile huduma 5,wewe uko wapi? Mtume,Nabii,mchungaji,muinjilisti na mwalimu,(efeso 4:11)sasa basi nazungumzia Uta ambao tumepewa ili tupate kushinda ,uta kazi yake ni kushinda na kupata kile tunachokitaka,Kumbe sisi tuna ushindi mikononi mwetu ambalo ni neno la mungu, neno ni ushindi si kushindwa,so ,kukata tamaa kwetu hakuna ni kupambana mpaka adui yetu tummalize kwa uta tuliopewa,kam neno haliko kukata tamaa kwako ni rahisi maana hiyo ni silaha tuliopewa na mungu.
  TUNDA LA ROHO:UVUMILIVU.
  amiina ni mie dada
  stella rugoye.

 8. asante kwa somo zuri, Mungu akubariki mpendwa katika Bwana, nikweli njia huja hata pasipo na njia.

 9. Amen, Mungu akubariki kaka Emmanuel Kwayu kwa somo zuri la kutufanya tusifie jangwani.

 10. Hili ni somo zuri la kutufanya tuendelee kudumu katika imani, hata kama yapo magumu. Nitoe mifano miwili pia itusaidie. Dan 4.17 na 18 wakati watumishi wa Mungu walipokutana na jaribu la kutupwa kwenye tanuru. Walisema hivi. Mst 17 Mungu atatuokoa. Mst 18 Hata kama hatatuokoa. Unaona kulikuwa na ukimya kati ya mst 17 na 18. Pia katika Math 26.36 mpaka 44 Bwana Yesu aliomba akisema maneno haya. MAPENZI YAKO YATIMIZWE. Wakati mwingine hatumpatii Mungu nafasi katika maisha yetu atuchagulie kile anataka kifanyike katika maisha yetu. Na hapo UVUMILIVU, SUBIRA Vinatakiwa. Amina.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s