Kasi ya kuongezeka kwa ndoa kati ya wanaoamini na wasioamini

Kwa kipindi kirefu nimekuwa nikitafakari na kushuhudia, hili wimbi linaloshika kwa kasi katika nchi Mbalimbali na hata Tanzania. Inaonekana makanisa hayawezi tena kuzuilia au kusaidia watu kuendelea kuamini kuwa Mungu anaweza kukupa mwenzi aliyeokoka.

Tafadhali tujadili pamoja 

1) Je ni kweli kuwa ni bora kufunga ndoa na asiyeamini kwa kuhofia kuanguka kwenye uzinzi?

2) Au ni dalili ya kukosa imani, kukata tamaa na kutojali tena thamani ya maisha ya kiroho?

3) Watumishi wanaohalalisha ndoa hizo wanatenda sawa?

4) Ni sawa kuamini unaweza ukambadilisha mwenzi wako mkishaoana?

2 Wakorintho 6;14- 16 Msifungiwe nira pamoja na watu wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa, kwa maana pana uhusiano gani kati ya haki na uovu? Au kuna ushirika gani kati ya nuru na giza? Kuna mapatano gani kati ya Kristo na Belialia? Yeye aaminiye ana sehemu gani na yeye asiyeamini? Kuna mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa kuwa sisi tu hekalu la Mungu aliye hai.

Dada Imani Kapinga
Advertisements

28 thoughts on “Kasi ya kuongezeka kwa ndoa kati ya wanaoamini na wasioamini

 1. Dada IMANI KAPINGA

  Mungu aliye hai akubariki mno!

  MAFUNUO YA NENO LA MUNGU HULETA UKOMBOZI.

  Naomba tutafakari 2 WAKORINTHO 6:14-16 kwa muongozo wa Roho
  Mtakatifu.Maandiko yanasema “Msifungiwe nira na WASIOAMINI,kwa
  JINSI ISIVYO SAWASAWA.Kwa maana pana urafiki gani kati ya HAKI
  na UASI? Tena pana shirika gani kati ya NURU na GIZA?

  Hapa Roho Mtakatifu ana maanisha kwamba MTU ASIYEAMINI ni sawa
  na muasi ambaye anaishi gizani.Neno linasema tusifungiwe nira na
  watu wa namna hii KWA JINSI ISIVYO SAWA SAWA,Yaani tusichangamane na watu wa namna hii kwa jinsi ambavyo HAIMPENDEZI Mungu.Kwahiyo unaweza UKAFUNGIWA NIRA na mtu
  asiyeamini kama INAMPENDEZA Mungu!Ni hivi unaweza ukachangamana na mtu asiyeamini kama kuchangamana huko kunampendeza Mungu au ni MAPENZI YA MUNGU.Hii ni kwa sababu
  SI WOTE WASIOAMINI WANAOWEZA KUPATA NEEMA YA WOKOVU!Lakini WAPO WASIOAMINI AMBAO MUNGU ALISHA WAKUSUDIA
  WOKOVU.Na wateule wote kabla ya kuokoka walikuwa miongoni
  mwa watu wasioamini.

  Unasema CHRISTINA unanipeleka wapi? Tumsikilize Roho Mtakatifu
  kwa makini ili tuone kule anakotaka kutupeleka.Unaweza ukaolewa
  na mtu ambaye ANAJULIKANA NA MUNGU, ALISHACHAGULIWA
  KABLA YA KUANZISHWA MISINGI YA DUNIA LAKINI BADO HAJAITWA
  NA KUTUKUZWA(Soma WARUMI 8:29-30).Hapa ni lazima wewe pamoja
  na mchungaji wako MUWE MAKINI KATIKA ULIMWENGU WA ROHO ili Mungu amthibitishe kama KWELI HUYO NI MUME KUTOKA KWAKE
  INGAWA BADO HAJAOKOKA(HAJAAMINI).Hapa inategemea na kanisa
  la kiroho unalosali pamoja na umakini wa kiroho wa mchungaji wako.
  Kama Mungu akithibitisha kuwa huyo ndiye mume wako hapa ni lazima
  mfunge ndoa bila kujalisha hiyo ndoa itafungiwa kanisani kwako
  au kwake!!

  USHUHUDA ULIOTOKEA KANISA NINALOSALI!
  Kuna binti aliolewa na kijana analikuwa anasali kanisa la katoliki.
  Walipokutana na kukubaliana yule binti akaamua kumleta huyo
  kijana kwa mchungaji wetu kwa ajili ya mazungumzo ya kutoa
  maamuzi hiyo ndoa ifungiwe kanisa lipi.Binti ameokoka anasali kanisa
  la kiroho wakati kijana hajaokoka na ana misimamo ya kikatoliki!
  Cha kwanza ambacho mchungaji alifanya ni kuingia katika ulimwengu
  wa roho ili kuangalia UHALALI WA KUKUTANISHWA KWAO.Alipopata
  uhakika kuwa ni mapango wa Mungu akakubali wafunge ndoa
  katika kanisa analosali kijana LAKINI kwa sharti kwamba baada
  ya kufunga ndoa kila mmoja AENDELEE KUSALI KANISANI KWAKE
  HUKU WAKIALIKANA!!Ingawa hapa lengo ilikuwa ni kumualika kijana
  kwenye kanisa la binti.

  Mchungaji alitumia hekima hiyo huku akiendelea na maombi
  ya kumuingiza yule kijana katika wokovu.Pia alimueleza binti kuweka
  bidii katika kumuombea mume wake ili aokoke na kutoka kwa wasiamini.Silaha nyingine ambayo mchungaji alimpa yule binti ni
  kuhakikisha ANAVAA MAVAZI YA YESU NDANI YA NDOA ili kumgeuza
  nia mume wake(Soma 1 PETRO 3:1-6).Taratibu kwa nguvu ya maombi
  yule kijana akaja siku moja kanisani AKAMPA YESU MAISHA YAKE
  NA KUUNGANA NA MKE WAKE KATIKA KUABUDU KWENYE MADHABAHU YA MUNGU ALIYE HAI!!!

  Mpendwa Dada Imani haya mambo bila ya kuwa na MACHO YA ROHONI ni magumu mno na wengi wanaendelea kuangamizwa.Jambo
  hili linahitaji hekima na maarifa ya rohoni na pia linahitaji UHAKIKA
  KATIKA KUVUMILIA KWA JINSI YA ROHONI.Makanisa(madanguro) ya
  manabii wa uongo WAMEKAZANA SANA kufungisha ndoa kati
  ya WASIOAMINI ambao hawana neema ya wokovu na wateule wa Yesu!!Lakini pia wachungaji wazembe ambao hawaingii gharama ya
  kuchungulia katika ulimwengu wa roho WAMEJIKUTA WANARUHUSU
  NDOA KATI YA WASIOAMINI NA WALIOAMINI KWA JINSI ISIVYO
  SAWA SAWA!!Kama kuna sehemu ambapo shetani amewekeza nguvu
  zake zote katika nyakati hizi za mwisho ni suala la KUOA AU KUOLEWA KWA WATEULE WA MUNGU.Kwa sababu ndani ya ndoa iliyobeba kusudi la Mungu ndimo kwenye UMILIKI NA UTAWALA
  WA KUMNYANYASA SHETANI NA WAJUMBE WAKE!Ndoa zilizoanzishwa
  na Mungu ZIMEFICHA SIRI YA USHINDI AMBAYO WAJUMBE WA SHETANI WANAFANYA JUU CHINI ILI TUSIIJUE.Jaribu kifikiri kama huyu binti angepata washauri wabaya mambo yangekuaje?Maana bila
  shaka kulikuwa na tofauti za kiimani ndani ya ndoa yake.

  Mungu aturehemu na kutusaidia……

 2. MUNGU AKUBARIKI DADA ANGU.Unajua dada vijana wengi wengi wa sasa wanajari mapenzi yao tu na kusahau MUNGU anasema nini kati ya kuoa,uoe mtu wa namna gani?

 3. Dada Imani naomba unisaidie contact zako kwa kweli, nimebarikiwa sana na wewe!

 4. kwakweli Mungu atusaidie vijana wengi siku hizi hawako serious na wokovu tamaa za dunia zimewatawala hawawezi kujizuia kwa sababu Roho mtakatifu hasemi tena ndani yao ndiyo maana wanaamua kuacha wokovu na kuoa watu wasio okoka hii ni hatari kubwa siku zote mwili hauko tayari kufanya mapenzi ya Mungu inabidi kuutisha kwa maombi pia vijana wawe wavumilivu wasichoke kuomba Mungu atawajibu kwa wakati wake,mtu anapooa au kuolewa na mtu asiyeokoka wokovu wake unakuwa hatarini maana wengine wanasema nitambadilisha tu,kumbuka Mungu ndiye anaye badilisha mtu na sisi tumeokolewa kwa Neema tu.Hivyo nawasihi vijana kuvumilia na wasichoke kuomba Mungu bado ana jibu maombi.Mimi nimemuona maishani mwangu nilimuomba mume na kwa wakati wake alinipa.Mungu awabariki.

 5. Wapendwa nimejaribu kupitia mchango wa kila mmoja hapa. Kitu ambacho nimejikuta najiuliza ni; kwa nini aliyeokoka anafika mahali pa kujiuliza kuoa/kuolewa na mwamini au asiyeamini? Yaani chanzo cha mjadala huo ndani ya kichwa cha mwamini ni nini!!

  Ivi kuna uhusiano gani kati ya ndoa na imani? Yaani, je ndoa ya mtu inaweza kuathiri imani yake au imani ya mtu inaweza kuathiri ndoa yake? Ivi tunajua kuwa ndoa inaweza kuwa sababu ya maombi yetu kutosikilizwa na Mungu?

  Je niende zangu Zanzibar ghafla nimwone Mwanaidi anatoka msikitini nivutiwe nae,kisha nimpende, baadae nifanye mipango nimwoe tuishi pamoja, yeye Ijumaa msikitini mimi J’pili kanisani,itaathiri imani yangu au la?

  Je kuna chochote biblia imesema kuhusu uhusiano wa ki-ndoa kwa mwamini na asiyemwamini? (1Wakorintho 7)

  Kumbe ndani ya ndoa kuna utakaso (utakatifu- sanctification), na utakaso huo unatokana na kuokoka ambapo aliyeokoka huyo ikiwa atakuwa anaishi na mwenzi ambaye hajaokoka, huyo asiyeokoka anaweza takaswa kwa sababu ya huyo aliyeokoka. Na hii ni kwa ajili tu ya yule ambaye aliokoka akiwa ameolewa/ameoa.(1Cor 7:14 For the unbelieving husband is sanctified by the wife, and the unbelieving wife is sanctified by the husband: else were your children unclean; but now are they holy.)
  Maana kama ingekuwa inawahusu waliookoka ambao wameamua kuoa/kuolewa na wasiookoka Paul asingeongelea suala la kuachana.(1 Cor 7:12-13)

  Pia, kumbe kwa wanandoa kuna kufunga na kuomba. Suala la kufunga na kuomba hapa linahusu watu waliookoka..(1Cor. 7:5 Defraud ye not one the other, except it be with consent for a time, that ye may give yourselves to fasting and prayer; and come together again, that Satan tempt you not for your incontinency).Hakuwezi kuwa na makubaliano ya kufunga na kuomba kwa wanandoa ambao mwingine hajaokoka

  (Samahanini kwa kutumia nukuu ya Kiingereza ndo niliyonayo kwenye komputa yangu)

  (Katika mistari hii nimeongelea tu suala la imani na ndoa sijaongelea masuala mengine yanayohusu ndoa)

  Kuna matukio maalumu kama ya akina Hosea kuoa mwanamke wa uzinifu, hayo hutokea kwa kusudi maalum la Mungu.

  Jamani ndoa ni zaidi ya kujamiana ndio maana Mungu anaiheshimu.

  Na kipimo cha ndoa sahihi hakiko kwenye kutokuwa na matatizo au changamoto ndani ya ndoa, au ngoja niiweke hivi; kukiwa na utulivu ndani ya ndoa haina maana kuwa wanandoa hao walioana kwa kuongozwa na Mungu, na uwepo wa matatizo katika ndoa haina maana kuwa wanandoa hao hawakuoana ktk mpango wa Mungu. Ibrahim alipata tatizo ktk ndoa yake akatembea nje, Beny Hinn amekuwa katika shida ya ndoa pia, haimaanishi kuwa walioa nje ya mpango wa Mungu.

  Namaliza hivi; Kwa nini uoane na asiye mwamini- Je ni Mungu kakuambia au ni kwa sababu tu umepempenda?

 6. Amen wapendwa
  sifa na utukufu kwake Yesu anayetupigania kwakweli am very strong! Ninamshukuru sana Mungu kwa hili na ili kunidhihirishia upendo wake amenizungishia watu wema kila niendapo, hakunipungukia kitu muhimu nilichohitaji. Kifupi maisha yangu ya wokovu ni kuwa ilikuwa nipitie njia hiyo ili nifikie amani niliyomo. Ila ugumu niliopitia ninahofia kwa mwingine inaweza kuwa safari ya kupotezwa ili kulinda hiyo “ndoa”.
  Ninatumaini wengine wenye ndoa zilizoungwa safi na Mungu na kwa kuisikia sauti yake sawasawa watawaelekeza vijana jinsi gani waenende ktk safari yao ya kutafuta mwenza, lakini kikubwa naona ni kuwa karibu na mwalimu wetu mkuu tuliyepewa Roho mt ambaye tuliambiwa atatufundisha yote. Mbarikiwa nyote kwa michango na mafundisho yenu.

 7. Kwanza nikupongeze dada Rosemary kwa rejea za Maandiko ulizoziweka zinazohusiana na suala la ndoa zilizofungwa kati ya waaminio na wasioamini. Mimi ninaamini kuwa iwapo yeyote yule atazisikiliza kwa sikio la rohoni, atapata faida kubwa sana, haswa vijana wanaotarajia kuingia katika ndoa.

  Ndoa, katika mtazamo wa Kikristo ni jambo nyeti sana. Kwa bahati mbaya, kutokana na mashindano ya kidhebu, na mapatano yake, taasisi hiyo ya ndoa imepoteza mwelekeo na sasa hakuna kinachoeleweka si kimafundisho wala kimaisha. Ulaya na Marekani wakiwa ndio viongozi na washawishi wakuu wa uharibifu wa taasisi hii. Lakini Ndoa ni taasisi anayoisimamia Mungu mwenyewe, ndio maana ametuwekea misingi imara katika Maandiko ili tusitetereke. Lakini tunapokwenda kinyume na taratibu alizoziweka Mungu hutusababishia shida na mahangaiko yasiyo na mwisho!

  Basi, ili kufika katika kiwango cha uelewa mzuri wa taasisi hiyo na kwanini Mungu mwenyewe aisimamie, ni vizuri ukauangalia kwanza uhusiano wa Kristo na Kanisa lake. Kanisa katika Maandiko ni mfano wa Bibi Arusi, nae Kristo akiwa ndiye Bwana Arusi. Mtume Paulo anasema amemposea sisi Kristo! Ili tuendelee katika kuposwa kwetu, twalazimika kudumu katika mafundisho ya huyo mshenga ambaye ndiye amjuae Bwana Arusi vizuri na hivyo yeye kutufunza katika hayo yampendezayo. Basi kadiri tutakavyodumu katika mafundisho hayo, yatatubadilisha asili yetu na kutupa asili mpya ya Bwana Arusi nasi kuwa Mwili Mmoja pale tuchukuapo hiyo asili mpya ile ya zamani ikiisha kuzikwa katika utu wa kale. Hiyo ndiyo bottom line ya mahusiano ya ndoa!!!

  Kwa hiyo, mshenga anapokuwa ni dhehebu lolote lile, nalo Fundisho la dhehebu hilo likiwa ndilo Bwana Arusi, basi huyo anayechumbiwa ili wawe mwili mmoja ni lazima bibi arusi afundishwe mambo ya Bwana arusi wake kulingana na dhehebu lake au kikundi chake cha wokovu vinginevyo wote wawili wanaingia katika mateso ya kujitakia huko mbele ambako itakuwa tabu kukichomoa kichwa chako kutoka katika nira uliyojifungia mwenyewe ulipoamua kuifuata tamaa ya mwili wako badala ya Neno la Mungu au Fundisho la dhehebu lako au kikundi chako cha wokovu, ambalo husimama badala ya Neno la Mungu kiuwakilishi. Madhehebu katika nafasi yao ya ushenga ndio yanayowasababishia wakristo vurugu katika ndoa kutokana na kucompromise misimamo yao ya awali iliyowataka wanandoa kuwa dhehebu moja, lakini siku hizi wameingia uoga wa kukimbiwa kwa hiyo wamelegeza msimamo na hivyo wanakubali ndoa hizo zenye kuchanganya imani kinyume na maagizo ya Mungu. 

  Basi, kama unavyoiona hali hii ya mchanganyiko ilivyo katika ndoa, ndivyo hali ya kanisa ilivyo pia, limejichanganya katika mafundisho tofauti tofauti yasiyoendana na Neno la Mungu. Nasi tuliomo katika makusanyiko hayo hatuwezi kuwa tofauti maana asili tuliyonayo ni ya mchanganyiko; Neno la Mungu na mapokeo, yaani chotara. Basi uwajibikaji wa Mungu katika makundi chotara ni mdogo sana katika kiwango cha fukuto tu, maana yeye huhitaji ukamilifu ambao katika imani chotara haupo! Kanisa lina imani chotara, nasi waumini wake imani yetu kwa Neno la Mungu haiwezi ikatuvusha katika dunia ya mashaka juu ya Mungu kulitimiza aliloahidi, bali huyaongeza mashaka yetu na kututamatisha katika kutumia akili zetu na maono chotara ya viongozi wetu ili mradi huo huwa mwanzo wa ngoma ya mashetani lawama zote akirushiwa Mungu!

  Unajua kanisa ni taifa teule, kwa hiyo kama ilivyokuwa kwa Israeli, wao wakiwa ni kivuli chetu, basi leo hii tukiwa katika Nuru Kuu ya Injili, kutoka nje ya maagizo ya Mungu, kunatupeleka katika kile kiwango cha wanawali wapumbavu waliokosa mafuta, nasi bila shaka hiyo ndio hali yetu tuliyonayo katika makundi yetu chotara, nazo ndoa zetu haziwezi kuwa tofauti na imani yetu- chotara! Kwa hiyo imani chotara haiwezi kuzaa matunda halisi, hata vipawa vyake, bado haviwezi kuwa halisi; isipokuwa turudi katika Neno halisi tukiyatupilia mbali mapokeo yote na kujinyenyekeza kwa Bwana aliye lile Neno, haijalishi umekwenda mbali na Neno kiasi gani, au ndoa yako imesambaratika kiasi gani, au hali yoyote ile iliyokukatisha tamaa haswa kutokana na imani chotara, basi jitenge pembeni umlilie yeye mara moja toka kilindi cha moyo wako, ATAKUSIKIA! Usirudi kwa Mungu kumuomba suala moja zaidi ya mara moja, maana yeye hasinzii hata awe hakukusikia ile mara ya kwanza!!! Yaani usiende katika mstari wa maombi kwa tatizo moja zaidi ya mara hiyo moja ni laana!!!

  Mbarikiwe nyoote!

 8. Dada Rosemary,

  Kwa kweli nakupongeza kwa ujasili wako. Ubarikiwe sana kwa ushuhuda wako. Natamani wapendwa wengi wangepata ushuhuda wako.

  Nakuombea Mungu akulinde na akupe baraka na kheri zaidi. Mungu yupo na atakuvukisha majaribu yote. Naomba nisiseme mengi maana Dada Rose ameshayasema. Pokea BARAKA hapo ulipo.

 9. Dada Rosemary Mungu akubariki,

  Mhh, ushuhuda wako mzito sana, nimejifunza kitu kikubwa sana hapo. Ila nafarijika kuona unavyompenda Yesu na moyo wako wa ujasiri katika kumtumikia Mungu pamoja na yote. Mungu ni mwaminifu na ‘everything works together for good for those who love God’ (Romans 8;28). Naamini Mungu karuhusu jaribu hilo kwa kuwa alishakuandalia neema ya kupita salama na kukuinua kiroho zaidi kupitia hilo.

  Kweli bora kumsikiliza Mungu na amani ya Kristo ndani yako. Maana kuna wakati hata wewe ukiwa na amani kabisa ukimsubiri Mungu akamilishe unachoamini , watu (tena wa kanisani) ndo wa kwanza kukutia pressure. Halafu siku ya siku yakikufika wote wanakukimbia.

  Tena umenikumbusha mbali sana, huko kwenye sanamu wengi ndiko tulikotoka, novena na dini kutushikilia. Ilikuwa bahati tu Mungu alininusuru baada ya kumaliza chuo kikuu tu nilipata neema ya wokovu, maana ilikuwa ni hatua ya kuolewa na huyo wa dini nilikotoka na bahati nzuri ugomvi na vita iliyoinuka ililazimu kila mtu ashike njia yake. Namshukuru Mungu kwa ule ujasiri wa ajabu alionijalia licha ya kuwa nilikuwa mchanga kiimani.

  Halafu kuna kitu mama mchungaji alikuwa anawaambia watu ‘Wale mlioolewa / mnaopanga kuolewa na wasiookoka mna kazi kubwa ya kufanya, mtalazimika kuomba, kutoa sadaka na kumlilia Mungu kwa ajili aokoe waume zenu’

  Lol, sasa kama ndo hivyo kwa nini kujiingiza kwenye balaa halafu baada ya kufurahia ndoa wewe kila siku ni kumlilia Mungu na kutafuta sadaka za kumwokoa mumeo……….mhhhhh…………..!!!!

  Ila kwa wale ambao tayari walishaingia, naamini Mungu atawapigania na kuwatengenezea njia. Ila nna mashaka ukaamua kujiingiza kwa makusudi halafu kesho umsumbue Mungu. Kwa wale ambao kweli Mungu amesema nao kwa njia ya pekee na kuwatumia kwa ajili ya wenzi wao kumjua Yesu basi hapo sina la kusema maana, Mungu ana njia nyingi.

  Lakini kila mtu anajua anachokihitaji katika maisha, sawa sawa na kiwango cha imani yake, huduma aliyopewa na mtazamo wake.

  Mbarikiwe
  Dada Imani Kapinga

 10. Kikubwa nilichotaka tujifunze hapa ni
  1, mtu wa imani nyingine uzinzi kwake siyo tatizo
  2. ushirikina ndio kimbilio lake akiwa na shida
  3. hana hofu na huyo Mungu wake na anaweza kukuacha na kwenda funga ndoa nyingine kifupi hawaheshimu ndoa hata kidogo
  4. Imani ni kitu kipana mno na si ibada tu kinajumuisha mambo mengi na hivyo tofauti zenu zitaleta matatizo makubwa kwa watu mnaotakiwa kuishi na kushirkiana kimwli na kiroho.
  5. Katika Biblia tunaona Ibrahimu alivyokuwa na imani kwa Mungu kuwa Mungu aliyemtoa kule kwa baba yake na kumleta nchi ya ahadi atamtafutia mke mwanae Isaka na kumleta huku na si Isaka aende kule. Tunaona mtumishi akiomba na kutengeneza mazingira jinsi gani amtambue huyo mke wa Isaka, tunaona alikataa hata kula hii ni kuwa alifunga na kuweka nadhiri hadi aone alichoomba kimetimia, Tunaona Mungu akimwongoza kwa usahihi kwa mtu aliyemchagulia Isaka Mwanzo 24…. lakini sasa hivi mtu akiomba na kujibiwa anaanza kuangalia vigezo vya kimwili na kisha kukataa jibu, wengine tu wavivu tu wa kuomba tunaulizia tu kwa watu na kusema huyu ndiye, wengine tunataka mtumishi au nabii atutabirie, jamani tukilifuata neno la Mungu haiwezekani Mungu atupe jiwe badala ya mkate, nyoka badala ya samaki hebu tukae na Mungu kwa ukaribu na tuisikilize sauti yake kama Eliya alivyofanya pangoni usitoke ahdi uwe na amani ya Kristo ndani yako….mbarikiwe na Bwana

 11. Shalom wapendwa
  naomba kuwajibu dada Imani na ndg Millinga kuhusu shuhuda zenu. Mungu amemuumba kila mmoja wetu kipekee na kwa namna ya ajabu Zaburi 139; “…..nimeumbwa kwa namna ya ajabu ya kutisha…” kwa sababu hiyo kila mtu anaye mtu aliyewekewa na Mungu kuwa mume au mke kama utakaa na Mungu na kumuuliza na kusubiri jibu na kulikubali. Tatizo la wapendwa siku hizi hatuna tena macho wala masikio ya rohoni hata tungekuwa nayo tunaingiza vigezo vya kimwili zaidi yaani vinavyoonekana zaidi kuliko visivyoonekana, huyo rafikio Millinga liangalia ya nje akauliza na rafikize kwa nje, je Mungu alisema yeye ndiye atakupa mke na muite naye atakuitikia na kukuonyesha mambo makubwa usiyoyajua, kwanini aliwauliza wenzie? hao angemwamba Mungu tu amdhihirishie kupitia wao bila wao kujua na si kuwauliza au kuwatumainia wanjulishe kama binti anafaa, kwa macho yetu haya ya nyama ndio wote wasemao Bwana asifiwe wanafaa lakini Mungu angemwonyesha wazi nani mwenza wake.

  Mimi nitatoa ushuhuda wangu sio mzuri ila kwa vile mmeng’ang’ana sana naona inabidi muambiwe upande wa pili wa hao mnaoona wanafaa… Nilizaliwa na kukulia ktk familia ya “kikristo” mie nilijikuta ndani ya kanisa na kwa kweli hata nafanya mafundisho ya kipaimara nilikuwa std 5 sikuwa hata na maamuzi wala kutambua nini ninafanya. Nilisoma na kulelewa shule za mission na malezi ya maombi na utii kiasi hata sisi tulijichukulia kama walivyo watawa hakuna mahusiano wala urafiki na jinsia tofauti…. nilipotoka chuo nilikaa muda bila kuolewa kwanza kwa hofu ya kupata mtu asiyemkristo au asiye sahihi. Nilikuwa nijbidiisha sana kuomba na nilijua nitapata mtu mwenye hofu ya Mungu ila sikujua kivipi. Kwa kukosa Roho mt niliomba mbele ya sanamu kwamba nipewe mume anayeabudu nami na niliomba ili nijue ni mtu sahihi na atanifuata hapo ktk sanamu….ilikuwa mazoea kila jioni ninapitia kuomba ndio narudi nyumbani baada ya kazi. Kweli alitokea mtu na moja kwa moja aliomba ndoa, sikutaka kuuliza tena maana sikuwa najua niulize nani au vipi….kifupi ndoa ilifungwa ila ktk mwaka mmoja tu yalinikuta hayo anayosema Millinga mume ni mzinzi wa wazi asiyeficha na ukimuuliza anasema samahani kesho anarudia yaleyale, alikuwa anaweza potea hata mwezi anarudi, matusi ugomvi, ushirikina nk. baadaye alikuja na mpya kwamba kwa waganga ameambiwa kuna nuksi inabidi tukatolewe nikamkatalia katakata kuwa mimi sitaki na pia wazazi waliishaniambia mtu asijenipeleka kwa waganga (hii ni baada ya wao pia kuacha kabisa). Ugomvi ukaanzia hapo, kama mnafikiri imani ya mtu ni kwenda nyumba za ibada tu basi ni kila kitu…aligoma kula nyumbani akisema anapata nuksi zaidi, aligoma mtu asimfulie, akikosa kwa kula anakula nyumbani ila anakunywa madawa baada ya kula ili kuondoa sumu! hapo ugomvi kila leo kwamba ninamfanya anakuwa maskini na kukataa kwangu kutolewa nuksi… baada ya mwaka na kuomba weeeeee na kuweka novena weeee niliamua kurudi kanisani na kuwaeleza, ajabu waliniambia kawaambie ndugu zake sisi hayo hatuwezi….. kifupi ni kuwa walipoitwa watu alikuwa wa kwanza kusema niondoke tu maana sina maana kwake…..ni kitu sikutegemea kwamba ndoa ya “kikristo’ inaweza vunjika kwasababu mtu anaendekeza waganga!

  Ilibidi nikae chini na kumlilia Mungu sana na kumuuliza sana kama kweli pale nilipoomba yuko Mungu wa kweli? nilikuwa muda mrefu nafuatwa na wahubiri ila nilikuwa nawagomea kwa kigezo wananitoa kwenye dini yangu…. ilibidi nimtafute Mungu hasa maana sikuwa na amani kabisa, niliomba sana kwa ajili yake na nikamwambia Mungu baada ya kuokoka muokoe huyu mtu… ni mwaka wa 12 ndio kwanza amepotea hata nduguze hawajui yuko wapi? Ni ngumu! ndio maana nasema kaa na Mungu akuonyeshe mtu sahihi kwako, jaribu nililonalo mimi sidhani kama wewe pia utaliweza, kifupi kanisa liliniruhusu iwapo ninataka kuolewa maana huyo mtu hajulikani kabisa alipo na ni yeye aliyesema niondoke kwake pili hatukuwa waamini wote ila huu ni ushuhuda mwinngine….natumaini mtajifunza kitu hapa. Mbarikiwe

 12. AJABU KUU!!!!!! NI AJABU SANA. HATARI KUBWA.

  Namaliza kutuma maoni yangu yenye maswali hapo juu. Natoka nje ya ofisi yangu. Naelekea Posta kutuma barua ya ndugu yangu anayeomba kusoma Dar. Njiani nakutana na mpendwa niliyesoma naye paleeeee Tabora.

  Tunaongea kama dakika 30 hivi. Tunapeana Bwana Yesu asifiwe. Aminaaa. Habari ya siku. Nzuri. Hajambo shemeji? Hajambo? Hatuonani Mpendwa? Aaa wewe ndo huonekani. Mazungumzo yanaendelea.

  Vipi tangu umefunga ndoa mwaka jana hatuonani, hebu nikumbushe uliniambia umeajiriwa wapi? Ananijibu. Nimejishikiza pale tu shule. Mimi ni mwalimu. Kwa nini unasema umejishikiza tu? Si unajua nilijiendeleza na fani ya Sheria? AAAAH, nilikuwa sijui.

  Hebu niambie vipi, shemeji alishapata mtoto? Yaaah, kwa kweli juzi tu alikuwa ameconceive na kisha imetoka kwa bahati mbaya. Ooooh Pole sana. Mungu atakujalia mwingine. Kwa nini sasa ikawa hivyo mpendwa? Kwa kweli mimi nawalaumu “mabest” wangu hawakuniambia ni tahadhari gani za kuchukua pindi tupatapo ujauzito. Nkamuuliza. Kwani ilikuwa ya miezi mingapi? Aaaah ilikuwa kama mwezi mmoja na nusu hivi. Unajua alifanya kazi nyingi sana siku hiyo alishinda anafua nguo. Rundo la nguo alifua siku hiyo. Ilipofika usiku hali ikabadilika na mimba ikatoka.

  Mpendwa Milinga nikwambie, kwa kweli nasikitika hata hivyo. Enhee. Kwa nini? Unajua mimi nilifanya makosa wakati nachagua mke wa kuoa. Kwa nini unaniambia hivyo? Nikamuuliza. Mwaka jana nilipooa mimi nilijitahidi sana kuomba Mungu anipe mke mwema. Baada ya kumpata huyu niliyenaye MAAJABU NI KWAMBA NIMEGUNDUA MKE WANGU NI KAHABA. Nikamuuliza unasemaje? Nakwambia Milinga amini au usiamini, NIMEOA MKE KAHABA. Yaani analeta hadi wanaume nyumbani kwangu mchana. Wewe unajuaje au umemwona wapi akifanya ukahaba? Yaani ni majuzi tu nilipotoka kazini nikamkuta hayuko katika mooood ya kawaida. Nikajiuliza kuna nini mwenzangu? Nikajifanya kama sikumgundua kuwa ana hali ya tofauti. Lakini nilifanya uchunguzi na kujiridhisha kabisa kuwa alikuwa ameleta mwanaume nyumbani mchana!

  Kwani wewe ulipoamua kumwoa hukuwa umefanya uchunguzi wa kutosha? Nikamuuliza. Mimi nilipomuoa nilijua kabisa yeye ni mtumishi wa Bwana maana huduma zote za kanisa anafanya. Yaani ni mtu wa madhabahuni. Ni mwimbaji ni muombaji na hata wapendwa nilioomba ushauri kwao wanaomjua nao walinitia moyo na kusema kwamba hakika yule binti ni kifaa cha Bwana. Yaani hakuna aliyenitonya kwamba ana tabia za ukahaba. Kila mtu alikuwa akinipongeza. Mimi pia nilichunguza lakini sikuwahi kumwona kuwa alikuwa na tabia za UKAHABA.

  Nikamuuliza, sasa Mpendwa unawazaje kama umeshaanza kumtuhumu mkeo kuwa ni KAHABA? Mimi ninampango wa kumtafuta Mchungaji ambaye anayajua maandiko vizuri ili ikiwezekana niachane naye. Kama kanisani itashindikana basi mimi naendelea kutafuta Ushahidi wa kutosha kumtia hatiani ili NDOA YETU ITANGULIWE. Yaani kweli Milinga mimi nije kufa na UKIMWI wakati watu wote wananijua kwamba nina mke? Waje kusema mke wangu ndiye kaniambukiza?

  Mimi nikajitahidi kumtia moyo kwamba asijaribu kuachana naye labda anamshuku tu wala hana tabia hiyo. Lakini mpendwa akakataa kata kata. Yaani hata siku nyingine kuna simu iliita kwenye simu yake akaikata haraka. Nikamuuliza mbona umeikata simu hiyo? akajibu kwa kujikanyaga kanyaga tu. Mpendwa its a long story… nitatafuta siku tukae pamoja tushauriane kwani naona leo hatuwezi kuyamaliza.

  Wapendwa wasomaji wa SG Blog, hii ni habari ya kisa cha kweli kabisa. Nimeona niitoe katika mfumo wa story kama nilivyokuwa napiga story na huyu mpendwa wangu. Yeye kama nilivyosema ameoa mwaka jana 2011. Ameoa mtumishi wa Bwana mwimbaji wa kwaya, mwimbishaji wa sifa, mwombaji, nk. Nimeona kisa hiki nikilete kwenu ili kukuza mjadala huu. Ukisoma kisa chote unaweza kupata somo la kujifunza katika mjadala huu. Hadi tunaachana saa 9.30 alasili ya leo 18/06/2012 alikuwa na msimamo kwamba lazima atafute mwanamke mwingine na kwamba anaamini hatafanya KOSA TENA.

  Wapendwa wangu hebu nipeni maoni yenu maana nimepanga kukaa naye wiki hii mwishoni ili nione kama nitafanikiwa kusuluhisha NDOA YAKE isisambaratike.

  Nawapenda wooote mnaotoa maoni yenu.

 13. Wapendwa,

  Kama nilivyotoa tahadhari awali, swala hili limeleta changamoto sana kwenye meza hii ya majadiliano hapa SG.

  Mimi naona tujiulize maswali haya kabla ya kuweka msimamo wetu uwe wa kimaandiko au wa kimapokeo ya tamaduni za Kitanzania au makabila yetu:

  1. Ni kitu gani humsukuma mtu (pamoja na mlokole pia) hadi kuamua kufunga ndoa

  2. Je, Yesu alipowaambia watu wasiookoka kwamba “….mtu atamwacha baba na mama yake nao watakuwa mwili mmoja…” alimaanisha nini kama aliokuwa anawaambia walikuwa wala siyo wanafunzi wake?

  3. Mababu zetu waliokuwa wanaoana enzi zao zile waliwezaje kuishi miaka mingi kwenye ndoa wakati hawajaokoka?

  4. Je, wokovu ndio kiungo kinachounganisha ndoa kimantiki au ni mitazamo tu?

  5. Je, kama wapendwa wanatakiwa waoane wenyewe kwa wenyewe (kama hoja kuu ndiyo hii?) hatuoni kwamba tunakuwa tunawalazimisha wapendwa kujifanya “wamependana” kumbe hakuna upendo kati yao?

  Bado mimi nina maswali mengi, kabla sijaamua ni upande gani nisimame. Lakini kwa sasa najaribu tu kuchokonoa mada hii ili kutoa changamoto zenye kuwafikirisha nje na ndani ya mktadha wa mada.

  Nitashukuru endapo nitapata hata wachangiaji wawili au zaidi wa kunijibu hoja zangu.

 14. Shalom wapendwa,

  Leo nilikuwa kanisani, dada mmoja ametoa ushuhuda ambao nimeona niwashirikishe.

  ‘Akiwa na furaha kubwa, anasema haamini leo Mungu amejibu maombi yake baada ya miaka 16 aliyokuwa akimlilia Mungu, akiomba toba na kujilaumu labda alikosea kuchagua kuolewa na mume ambaye hakuwa ameokoka’.
  Sababu alikuwa akiteseka sana kwa ugomvi na kunyimwa ruhusa mara nyingine….
  Leo Bwana amemuokoa mumewe baada ya miaka 16………..!!!

  Mbarikiwe
  Dada Imani Kapinga

 15. Mpendwa Mwangomo N,

  Hakuna anayeng’ang’ania lolote. Tunachohitaji ni msaada na pia shuhuda za wale walio na uzoefu wa suala hili. Unaweza kutusaidia pia ili tuone upande wa pili ambao bado hatujauelewa. Ndiyo maana tumeweka wazi tunachofahamu, tunachoamini na tunachotarajia sawa na neno na ahadi za Mungu ili wengine nao watushirikishe wanayoyajua zaidi.

  a) Kuna wanaolia sasa wakisema kuwa sauti walizozisikia hazikuwa toka kwa Mungu, leo wanakatazwa kwenda kanisani, imani zao zimetetereka.

  b) Pia kuna wanaolia kuwa wale waliowaona makanisani wameokoka wengine walikuwa feki, wamebadilika na hawataki kusikia mambo ya kanisani.

  – Sasa inabidi kutembea sana katika roho ili Roho Mtakatifu atupambanulie na kutuonyesha yale yaliyojificha tusidanganyike na yale ya nje tu.

  -Pia inawezekana kuna mambo mengine ambayo si ya kiroho lakini yanaweza kuwa ni changamoto pia; Kiwango cha uelewa, uchumi, elimu, vision, mwonekano na tabia.

  Kaka Ezekiel Lemaso,

  Nakubaliana nawe kuwa hata makanisani waliookoka wanatembea katika viwango tofauti vya imani, kiu ya kumjua Mungu na hata kutambua thamani ya wokovu wao. Labda tuseme hv, Mungu anatambua moyo, nia, haja na matendo ya kila mmoja. Kwa hiyo inawezekana kila mmoja anaweza kupokea kile anachoamini na kumlilia Mungu.

  “Yote yanawezekana kwake yeye aaminiye” (Marko 9:23)

  NATAMANI TUNGEPATA SHUHUDA ZA WATU WALIO-EXPERIENCE BOTH SIDES NA JINSI MUNGU ALIVYOWASHINDIA;

  Barikiwa
  Dada Imani

 16. BWANA YESU ASIFIWE WAPENDWA.kwa upande wangu,sioni kama ni tatizo kwa mtu anayeamini kuoa au kuolewa na asiyeamini.Ishu hapa ni kama huo uhusiano umepata baraka kwa MUNGU mwenyewe.Si ajabu kwa ndio hiyo kwa sababu wakati mwingine MUNGU anapanga kupitia kwa mmoja wa wapendwa hao na mwingine apone.Tatizo ni kwamba ndoa nyingi,na hata za wapendwa tupu ,zinasababishwa na tamaa za mwili na si mapenzi ya MUNGU.
  wATU WANACHOPASWA KUZINGATIA NI MAPENZI YA MUNGU.KILA MTU NA ATIMIZE MAPENZI YA MUNGU NA ULIMWENGU WETU UTAPONA

 17. Mwanzo 2: 18 Bwana Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye….
  Mwanzo 6:2 – 3 wana wa Mungu waliwaona hao binti za wanadamu ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake wo wote waliowachagua. Bwana akasema, Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye naye ni nyama; basi siku zake zitakuwa miaka mia na ishirini.
  Waamuzi 3:6 – 7 wakawaoa binti zao, na binti zao wenyewe wakawaoza wana wao waume, na kuitumikia miungu yao. Wana wa Israeli walifanya yaliyo maovu mbele za macho ya Bwana, nao wakamsahau Bwana, Mungu wao, nao wakawatumikia Mabaali na Maashtorethi.
  Waamuzi 16: 19 – 20 Naye akamlaza usingizi magotini pake. Kisha akamwita mtu akavinyoa vile vishungi saba vya nywele za kichwa chake; akaanza kumsumbua, nguvu zake zikamtoka. Kisha akasema, Samsoni, Wafilisti wanakujia. Akaamka katika usingizi wake, akasema, Nitakwenda nje kama siku nyingine lakini hakujua kuwa Bwana amemwacha….
  1Wafalme 11: 1 – 6 Mfalme Sulemani akawapenda wanawake wengi wageni, pamoja na binti yake Farao, wanawake wa Wamoabi, na wa Waamoni, na wa Waedomi, na wa Wasidoni, na wa Wahiti, na wa mataifa Bwana aliyowaambia wana wa Israeli, Msiingie kwao, wala wasiingie kwenu; kwa kuwa hakika wataigeuza mioyo yenu kuifuata miungu yao. Sulemani akaambatana nao kwa kuwapenda…Sulemani akafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana, wala hakumfuata Bwana kwa utimilifu, kama Daudi baba yake.
  Marko 10: 6 – 8 Lakini tangu mwanzo wa kuumbwa ulimwengu, aliwafanya mume na mke. Kwa sababu hiyo mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe;
  na hao wawili watakuwa mwili mmoja; hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe.
  Hii mistari nimeiweka hapa kuonyesha ndoa inaheshimiwa na Mungu na mnakuwa mwili mmoja sio kama ndugu hapo juu aliyesema hakuna neno ktk Biblia linalopinga unganiko na wasioamini, toka mwanzo tunaona Mungu alikataa kabisa hizi ndoa na pia tunaona madhara yake makubwa hata sasa ktk taifa.
  Iwapo hiki kitu ni Mungu anawaunganisha iweje akuunge na asiyeamini? Pili amesema mke mwema mtu hupewa na Bwana na mume mwema itakuwa vivyo iweje akupe asiyemwamini Yeye Mungu wako? historia yote ya Taifa la Mungu tunaona ndoa zisizofaa ndio kilikuwa chanzo cha kumpoteza Mungu na kuangamia utmwani kiroho na kimwili pia. Tafadhali wapendwa hata mtumishi pia ni binadamu na shetani ana muwinda hivyo akikosea mwambie wazi na usimfuate, Shika na kulitenda neno. Mbarikiwe

 18. Msomeni HOSEA katika HOSEA 1:1- Labda tunaweza kupata akili nyingine kuliko kung’ang’ania tu. UKIONGOZWA NA ROHO MTAKATIFU KUNA SHIDA GANI KATIKA KUONA?

 19. Dada Imani, nakupa hongera sana kwa hayo uliyoyaandika, ebu nikuunge tu mkono hivi, Math 24.4 Bwana Yesu akasema angalieni mtu asiwadanganye. Waalimu wamekuwa wengi mno, na wadanganyaji wamekuwa wengi mno, Isaya 9.13–17 sitaikopi yote, ila someni muone. Nabíi afundishaye uongo ndiye mkia, kwa maana wawaongozao watu hawa ndio wawakoseshao. Watu wengi wamekoseshwa, wakati mwingine watumishi wengi tunaogopa kusema KWELI, Maana wengine wakiambiwa kweli wanahamaga kanisa, wanatafuta mahali nafuu, pa laini, Yer 6.13 na 14, Bwana akasema Wameiponya jeraha ya watu wangu kwa juu juu, tu, wakisema Amani, Amani, wala hapana Amani.. Wakati wa huduma ya Bwana Yesu aliwaambia lazima wamle wamunywe, wengi walikwazika wakaondoka, hilo halikumtisha Yesu, aliuliza tu Petro na ninyi mnataka kwenda! Pia Mtume Paul katika Gal 4.16 anasema Je nimekuwa adui yenu kwa kuwaambia yaliyo kweli? Mwisho nishauri tu, ebu tufanye vile Neno linavyosema, nawaomba msome maandiko yafuatayo ni ulinzi Mungu ambao aliuweka. Kumb4.2 Mith 30.6 uf.22.18-19 thanks.

 20. Dada Rosemary,
  Asante kwa michango yako mizuri. Jamani kuna mambo yanayotogea yanaogopesha sana. Yaani nadhani mtu usipokuwa na msimamo wako mwenyewe na imani yako binafsi kwa Mungu hata watumishi wenyewe wanaweza kukuvunja moyo.

  Mimi nimebahatika kuabudu katika makanisa mbali mbali ya wokovu kwa miaka hii 4 na nusu niliyookoka (kutokana na kuhama hama kwa sababu za kutafuta kazi na shule). Japo umri wangu si mkubwa sana kakini kwa miaka hii michache niliyookoka nimejifunza mengi sana na ninadhani kuna jitihada kubwa za binafsi zinahitajika kumtafuta Mungu na kumjua ili kusimama imara na Mungu.

  -a) Nina ushahidi kabisa mtumishi wa Mungu Tanzania akishauri kuwa hata kama hajaokoka apelekwe na anaweza kumpiga msasa akafaa. Jamani mpaka nikashangaa mtumishi mbona haileti amani binafsi na si jambo ambalo naamini toka kwa Mungu? Kwa nini Mungu aokoe binti yake hata akasababisha aachwe na mchumba wake wa kikatoliki halafu leo amekaa kwenye wokovu amsababishie akose mwezi wa kufanana naye? Kwa nini Mungu asimbadilishe kwanza akafanane na mimi kabla hajamleta?

  a) Kuna raha gani ukaolewe au kuoa mtu ambaye hawezi kukusaidia kuomba, hamuwezi kukubaliana katika mambo ya imani? mwingine rozari, mwingine maji ya baraka, mwingine kuomba kwa marehemu, mwingine kwa Maria.

  b) Kuna raha gani umeolewa au kuoa halafu kila siku kanisani unaenda peke yako kama single? Huna ushuhuda wa furaha au hata kuwatia moyo wanaotafuta wenzi.

  c) Kuna raha gani ukaishi katika ndoa ambayo watoto wanakosa mwelekeo na ni lazima mtaisia kugombana jinsi ya kuwatunza.Mwingine komunio, mwingine abatizwe mchanga, mwingine anasema mpaka akue….mchanganyiko

  d) Kuna raha gani kuwa na mwenzi ambaye hamwezi kuafikiana katika mambo ya uchumi; mwingine hajui fungu la kumi wala maana ya kuchangia kazi ya Mungu?

  e) Mungu kasema ‘two are better than one’ kitu gani kitakuwa better kama hupati support ya kukusaidia kukua kiroho?

  f) Hapa hii nchi ninayoishi ndo kabisa, wa-Afrika tena watanzania waliokuja na imani zao, suala la imani halijaliwi kabisa,. Kinachojaliwa ni kwamba mume au mke atakupa ruhusa ya kwenda kanisani…….yaani ukijitahidi kuonyesha msimamo wako unaweza kuonekana mbaya au mpinga maendeleo.

  -Kinachonisikitisha, watu wanaendelea kuwa kama singles tu kanisani? Maana kila siku wapo pekee yao. Binafsi sioni kama inaleta raha yoyote. Kumbuka hao ndiyo wakubwa wetu makanisani ambao ndo tunategemea kujifunza toka wao, watutamanishe raha ya ndoa……

  -KINACHINISIKITISHA…….KWA NINI TUNA IMANI KUBWA KUWA MUNGU ANAWEZA KUTUPA MAGARI, NYUMBA, UPONYAJI SCHOLARSHIPS, KAZI na VYEO lakini SI KUTUPA MUME au MKE ALIYEOKOKA???????????????

  MUNGU tusaidie, naamini hakuna linalokushinda. Kama ulivyosema……………….!!!

  Hebr 10;23Tushike kwa uthabiti lile tumaini la ukiri wetu bila kuyumba–yumba, kwa maana Yeye aliyeahidi ni mwaminifu

  Dada Imani Kapinga

 21. Kwa ninachoamini kila kitu ni maombi unaweza ukaoa/ukaolewa na asiyeokoka kwa sababu umeona maono mfano katika biblia ni Hosea japo huwa kuna kusudi la mungu.

 22. Mie naona hakuna cha kujadili ni kumuweka Mungu na maneno yake kwenye mizani ni kama shetani alipomuuliza Eva je amesema mkila mtakufa? ndiyo utakufa!

 23. Sipendi kujichanganya sana ha sa hii 2 Wakorintho 6;14- 16 kama ilivyoandikwa na Paul nafikiri tunaitumia vibaya ili kuanzisha nira nyingine isiyo maana ya kiroho! Na hakika hapo Paul alikuwa anajitahidi kuwa elezea watu Wa Korintho nykati hizo ambapo kuabudu sanamu ilionekana ni ustaarabu mkubwa na wasomu wengi walikuwa katika upagani so ustaarabu ule Paul alijitahidi sana kuwafundisha wanafunzi wake kuwa hauendani kabisa na Ukristo (Imani ya Kikristo) maana uliandamana na uabudu sanamu ambao ulikuwa kinyume kabisa na Mapenzi ya Mungu! ilikuwa na mantiki zaidi kiibada kuliko kijamii (NASISITIZA HAPO KIIBADA) maana watu wengi leo wamepoteza maana halisi ya Ibada (Uhusiano binafsi katika yako na MUNGU!
  Mimi kwa upande wangu huwa namwamini Mungu katika mambo rahisi na Magumu nikianza kusema utaanzaje kusema kuwa mwamini kamwoa asiye amini!!! Yeye ndiye ajuaye nafsi yake kama ni mwamini au sio…Na pia naamini kuwa akishakuweka katika kiganja yaani mkononi mwake hakutoi labda ujitoe mwenyewe!
  So pia watu waliokoka wanautashi wa kuamua vitu sahihi katika maisha yao, kijamii na kiroho maana Ukristo si dini bali ni imani yenye ushindi ndani ya Yesu! Nikiwa na maana tukianza kuwapangia watu jinsi ya kuingia katika mahusiano nani wa kuoa na nani wakkuishi naye hizo ni taratibu za kidini zaidi ambazo zinamnyima mtu haki ya kumsikiliza RMT. Tumeona ndoa nyingi zilizofanikiwa na zilizocharazwa na shetani, lakini hayo yote husababishwa na jinsi heshima,kiasi,maisha ya Ibada na Kujitoa kulivyo katika ndoa hizo!!!
  Wokovu ni porcess na mtu napookoka tokana na juhudi yake anakuwa 100% halisi katika hali ya kale 100% halisi katika utu upya sasa kazi ni kwake kundelea kuwa katika hale ya kale au utu mpya…! na ukivichanga ndio utakua 45%40% hata 80% ndio maana imetupasa kuchukuliana!
  Kwangu mimi sioni tatizo kuoa asiyeokakoka kama amekubaliana na imani yako na kaipenda, ila itakuwa tatizo kuoa mwenye malengo ya kukutoa kwenye Imani yako, maana binadamu ni nafsi hai anaweza kuwa ameokoka leo na akaamua kurudi nyuma utamuacha..cha maana ni kuzingatia hayo hapo juu!
  Kuna wahanga wengi ambao waliwaacha wasiookoka wakawaowa walio okoka kama walivyoshauriwa na wapendwa wanaishi kwa taabu na mashaka katika ndoa zao, huku waliowaacha wameokoka na ni watumishi wazuri tu!
  HIVYO TUMSIKILIZE ROHO MTAKATIFU ANAONGEA NA WEWE NINI SI SHERIA AU TARATIBU ZIWEZAZO KUTUKWAZA!

 24. Kuna mapatano gani kati ya Baali na Mungu wa kweli? Je waweza kukota jembe kw akutumia jozi ya ng’ombe na punda au ngamia na ukalima au kufanya ulichokusudia?
  Kama dhana ni kuukimbia uzinzi je una uhakika gani kuwa huyo asiyeamini anaamini ktk:
  1. Mungu wa kweli na hivyo kuwa mwili au kichwa ktk familia, kwa hiyo hii familia itakuwa na imani gani? watoto watafata imani gani? (hapa ninajumuisha mambo mengi mfano mnaabudu wapi na nini baada ya ndoa yenu, mnaambatana na watu wa imani ipi mfano kushiriki ibada za majumbani za imani ipi? matambiko, arobaini, eda? kupunga pepo? uaguzi na utabiri? matoleo yako unapeleka wapi nusu kwa baali. waganga, mizimu nusu kwa Mungu wako?
  2. Je watoto wanalelewa kwa imani ipi, nyumba na familia nzima mnaikabidhi kwa Mungu wa imani ipi? (usiniambie kuwa Mungu ni mmoja!)
  3. Je hii ni ndoa ya mke na mume mmoja na wa jinsia tofauti au hii ni ya mkataba tu, akiamua kuoa au kuomba talaka akaolewe tena itakuwaje? akiamua kuwa na mwenza wa jinsia nyingine je? nyumba ndogo? abortion? uzazi wa mpango gani?
  4. Kwa hiyo wewe unayejiita una wokovu ukiishagundua mkenge au tatizo ulilojiingiza utataka tena uoe au kuolewa baada ya toba? je utavumilia kuishi na mtu huyo hata akianza mambo yaliyochukizo kwa Mungu? akioa au kuolewa tena? mnataka kuwa na “ndoa” ngapi ngapi? Itakuwa ni majuto na mwiba maisha yako yote hata baada ya kumrudia Mungu (mwangalie Sara na Ishmaeli ghafla unaanza dhambi ya kufukuza watoto na kisha kuleta uzao wenye chuki na uchungu)

  Hitimisho
  Mungu aliyetuumba anaujua vema mwili wa kila mmoja wetu, hawezi kutupa jairbu lililo nje ya uwezo wetu hata siku moja, na ndio maana ktk Yakobo anasema kamwe hamjaribu mwanadamu isipokuwa unajaribiwa mwenyewe kwa tamaa zako na tamaa huzaa dhambi kisha mauti. Na ndio hiki kinachotaka kutokea hapa uki focus macho yako ktk ndoa na si Mungu wewe umekazania NDOA iwepo kwa njia yoyote bila shaka unajijaribu mwenyewe na kweli utaingia dhambini kwani unganiko na mtu asiyeamini ni chukizo mbele za Mungu….huo sio uzinzi pia?….tokeni kati yao mkajitenge nao….nami nitakuwa Mungu wenu nanyi watu wangu… sasa wewe utaachaje familia yako iwe inaamini Mungu mwingine nawe ukajiona salama? kukiwa na tatizo wao watakimbilia waganga nawe utaenda wapi? hata wewe ukiwa na tatizo watakusaidia kwa njia zao zisizofaa. Ndoa mseto ni mwanzo wa kuanguka kiimani na kufa kiroho kama alivyosema Yakobo hii tamaa itakuletea mauti ya kiroho.

 25. Ni kweli watumishi, hili ni kubwa sijui ni watu kukosa Imani kwa mungu, tunaomba viongozi wa madhehebu ya kiroho mtusaidie vijana.hebu wekeni misimamo makanisani jamani tusicheze na dhambi

 26. Wapendwa, TAHADHARI:

  Mjadala huu Una maswali yenye maana lakini yanayoweza kukutega kuingia mtegoni.

  Pili maswala ya NDOA ni maswala magumu sana. Hata wahubiri kama akina Benny Hinn Wamekutana na changamoto kubwa za ndoa zao.

  Nakuomba wewe unayetaka kujadili mada hii ujitahidi kufanya utafiti wa maswala ya ndoa kwa undani ili uweze kujadili kwa hoja kali na si kwa maneno makali.

  Mjadala ndio huo umeanza. Mimi sina mengi kwa sasa. Najifunza kwanza.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s