Kanisa, Tunahitaji Mafundisho gani kwa kipindi hiki?

Kanisa limekuwa na changamoto nyingi na maswali mengi kwa waumini na wafuatiliaji wa Imani hiyo, hii hupelekea kuibuka kwa mafundisho mengi tofauti tofauti kutoka kwa wahubiri mbali mbali. Unaona kuna mwelekeo gani wa kanisa, na watumishi wa Mungu, tufanye nini?

Advertisements

17 thoughts on “Kanisa, Tunahitaji Mafundisho gani kwa kipindi hiki?

 1. Bwana Yesu asifiwe wapendwa.Kitu kingine ninachokiona huduma ya Uinjilisti imepoa,wengi wa watumishi wapo katika kuitumikia karama ya kitume na Kichungaji wanaanza na kasi kubwa na wengi tunajikuta tunakwenda kusikiliza mahubiri na kuombewa shida mbalimbali.Hivyo waumini hujikuta tegemezi kwani watumishi wanajikuta muda mwingi wanautumia katika kusikiliza shida za waumini na kuwaombea.Hivyo pia ukiangalia maisha ya kuukulia wokovu yanahitajika sana na taratibu za ushuhudiaji sehemu tunazoishi,mashuleni,makazini,kwenye shughuli zetu za kila siku hiyo itlifanya Kanisa lichangamke katika kazi za Bwana huku tukiwa tunasubiri kuridi kwa Masiya.Tuwaombee Viongozi wa Kanisa waangalie makusidi ya Mungu aliyoweka ndani yao kwa kazi yake wasiyumbishwe na wanadamu na kuangalia makusudi ya wanadamu badala ya Mungu na Watumishi wakiangalia makusudi ya Mungu na sio makusudi yao au ya ulimwengu Kanisa litasonga mbele kwani makusudi ya kilimwengu yamekaa kisiasa Kusudi la Mungu linaanglia uwe maskini uwe tajiri unatimijaze mapenzi ya Mungu

  AMEN

 2. Bwana Yesu asifiwe,hebu tuangalie injili ya Yesu mwenyewe kama walivyoandika Mathayo,Marko,Luka na Yohana.Yesu katika Mathayo 28:19-20….”Basi enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi,mkiwabatiza kwa jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi na tazama mimi nipo pamoja nanyi siku zote hata ukamilifu wa dahari”—Je wahubiri wa sasa walioitwa na waliojiita wanahubiri kweli ya Mungu na waumini wanajitahidi kuwa wanafunzi wa Yesu au waumiuni wa dhehebu au Kiongozi wa Huduma
  Katika Marko 16:15-18…..” Akawaambia Enendeni ulimwenguni mwote mkaihubiri injili kwa kila kiumbe,Aaminiye na kubatizwa ataokoka na asiyeamini atahukumiwa na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio kwa jina langu watatoa pepo,watasema kwa lugha mpya,watashika nyoka hata wakinywa kitu cha kufisha hakitawadhuru kabisa,wataweka mikono yao juu ya wagonjwa nao watapata afya”.—–Wahubiri wa sasa mkazo wao upo kweli kutaka waumini wawe na uwezo wa kutoa wengine mapepo,tuliohubiriwa na kuokoka tuna uwezo wa kuweka mikono juu ya wagonjwa na wapate afya , hapo ndipo tulipopotea wahubiri na waumini Wahubiri wanataka wao tu wawe wanaongoza maombi siku zote,siku zote ni kushambulia matatizo ya waliokoka na wasiokoka badala ya kuwaombea wapokee nguvu za Mungu na kulijua neno kwa ufasaha na kwenda kusaidia kuhubiri injili kwa kila kiumbe badala yake kuna mafundisho ya kuwa waumini watiifu wa huduma vinginevyo utaiwa ajenti au una Roho ya kutanganga.Wahubiri wa sasa wanataka uhakika wa kuwa na waumini soma biblia nzima ni mtume gani au muhubiri gani aliitukuza huduma yake na kushikilia waumini Kinachooendelea sasa ni kama enzi zile za wale waliojitapa sisi ni wa Paulo wale ni wa Apolo na huyu ni wa Kefa hapo kanisa lazima lipoe.

  Tuangalie tena katika Luka 24:47-48….”na kwamba mataifa yote watahubiriwa kwa jina lake habari ya toba na ondoleo la dhambi na kuanza tangu Yerusalem nanyi ndinyi mashahidi wa mambo haya”…..Wahubiri wakazanie mahubiri ya toba na watakaotubu na kubatizwa wafundishwe jinsi ya kushuhudia na kuhubiria wengine,Makanisa yote ya Kipentekosti ya Ratiba za ibada ya wiki nzima ni mafundisho,maombi na matoleo unaweza kukuta kanisa 1 kati ya 100 ya kipentekosti yenye utaratibu wa kwenda kuhubiria wengine ambao hawajamkopea Bwana kama mwokozi wa maisha yao.Neno limewataka wahubiri wawe mashahidi wa haya.Yesu kabla hajapaa kwenda mbinguni aliwaagiza wale mitume12 waende wakahubiri injili ulimwenguni kote hakuwaamuru wakawe wakurugenzi wa huduma zenye matawi ulimwenguni kote bali kuwafanya waaamini na waliobatizwa na kuokoka wawe wanafunzi wa Yesu sio wawe waaumini wa dhehebu au huduma.Kutokuzania maombi ya toba kunafanya walokole kujihesabia haki wakati neno la Mungu linasema hakuna mwenye haki hata mmoja matokea yake Mitume,Manabii,Maaskofu,Wachungaji na Waalimu na hata waliokoka wa sasa baadhi yao wanajikuta wanaangukia kesi za uzinzi,wizi,ushirikina,madawa ya kulevya.

  Kanisa na Huduma pawe ni mahali patakatifu panapotakiwa pawe mkusanyiko wa watu lengo lao ni Kumwamini Mungu kupitia Yesu kumwabudu yeye kujifunza neno la kujisaidia hasa kiroho na kusaidia wengine kumjua Mungu kwa kumpokea Yesu mahubiri yeyote ya mwilini ni batili ole wao wahubiri wanaoshupalia maombi ya mwilini na waumini wanao abudu ibada za mwilini kwani katika Wagalatia 5:17..”kwa sababu mwili hutamani ukashindana na Roho na Roho kushindana na mwili kwa maana hizi ZIMEPINGANA hata hamwezi kufanya mnayotaka ….hivyo ukitamani mambo ya Rohoni utavuna matunda ya Rohoni ukichagua kutamani mambo ya mwilini utaishia kuvuna matunda yake

  Watumishi wa sasa wanampenda kweli Yesu na kulisha kondoo zake neno la kweli kwani hata Yesu alimuuliza Simon wa Yohana mara tatu kama kweli anampenda Simon wa Yohana alimjibu mara zote tatu kwamba anampenda Yesu ndipo Yesu akamwagiza alishe Kondoo zake katika Yohana Mtakatifu 21:15-17 .Kanisa la sasa lisipofundisha injili ya kweli halimpendi Yesu labda litakuwa linajipenda lenyewe bila ya kujali kama kondoo wanapata malisho mema

  Naomba tuagane kwa Neno la 1Wakorintho 14:1 Ufuateni upendo na kutaka sana karama za Rohoni lakini zaidi kwamba mpate kuhutubu.

  AMEN

 3. Naona watu wengi wanalilaumu sana kanisa la leo katika michango yao.Nami najiuliza swali hili kwamba “kwani kanisa la leo linamatatizo gani jamani? Mimi naona kanisa halijapoteza nguvu yake na wala halitapoteza maana Roho mtakatifu bado yuko ndani ya kanisa.

  Sisi wana maendeleo huwa tunasema kuwa huwezi kutafuta dawa ya tatizo pasipokujua kwanza tatizo lenyewe ni nini. Kwanza tujue kanisa linatatizo gani leo mpaka lihitaji dawa, na kisha tutafute hiyo dawa.

  Lakini pia swali lililoulizwa limetaka tu tuangalie mafundisho ambayo kanisa linahitaji kutilia mkazo zaidi leo, bila shaka kulingana na wakati tulionao.

  Mimi naamini kanisa halijapoteza utakatifu, wala kupungukiwa nguvu ya Mungu katika ujumla wake. Usiangalie tu udhaifu wako, matatizo ya mahali unaposali, mkoa ulioko, Tanzania, Afrika halafu ukahitimisha kwamba kanisa halina utakatifu na miujiza haitendeki kwa kiwango cha kanisa la kwanza.
  Ndugu zangu kuna mambo ya ajabu bado yanatendeka na yataendelea kutendeka.

  Tafadhali tupunguzeni kulilaumu kanisa kila kukicha huko nako ni kumkosea Mungu aliyelifia.

  Leo kila mtu anajifanya ni nabii, kila kikicha oh kanisa la leo halina nguvu ya Mungu, mara oh kanisa halina utakatifu, oh wokovu ulikuwa zamani bwana! Wewe ndio huna nguvu ya Mungu na utakatifu.Pona kwanza wewe na kanisa zima litakuwa limepona.

 4. mi naomba watu tuwe macho katika hili kwa kuwa kipindi hiki ambacho dhiki imetawala watu wa dini mbalimbali hasa wachungaji wanatumia muda huu kupata vkwa watu kwa kuhubiria kuhusu utajiri na mambo mengine ambayo kwa kweli utaona kuwa hayana msingi na neno la bwana jamani hizi ni nyakati za mwisho na watu waone kuwa hali tuliyo nayo hivi sasa si ya kutaka mali ni ya kumtafuta Mungu awe karibu nasi wapendwa na sio kurubuniwa na lugha za mali. Bwana Asifiwe.

 5. Wapendwa,
  Katika kuusoma mchango wa ndugu John Paul, maelezo aliyoyatoa na tafakari yake, vimenisafirisha mbali sana katika wakati! 

  Kanisa, huko nyuma, lilikuwa na nguvu nyingi sana ndani ya mwaminio mmoja mmoja, basi wanapokusanyika, kishindo chake, shetani asingeweza kuhimili! Lakini baada ya muda uamsho hupoa.  Kwa hiyo katika safari yake, kanisa, kumekuwepo na hali hiyo; Uamsho na kupoa katika hatua zake zote tangu Kanisa la kwanza la Mitume hadi Uamsho wa Kipentekoste! Labda kimaelezo, katika kuziangalia zile highlights au major reference points za safari ya Kanisa zingetupa mwanga zaidi juu ya hali tuliyomo, tukilitazama Kanisa tokea siku ya Pentekoste lilipozaliwa kwa kifupi.

  Historia ya Kanisa la Mitume imeandikwa katika Biblia. Msingi walioujenga kimafundisho uko wazi, kwa yeyote yule kuukagua ili mradi awe anajua kusoma, naye Roho Mt ambaye ndiye Mtunzi na Mwandishi, yupo karibu nawe kukuthibitishia yote unayoyasoma ili mradi nia yako iwe ni kuyajua hayo ili Kweli yake ikuweke Huru!

  Kanisa hilo la mitume baada ya umbali mrefu likaanza kupoa na mwishowe likazidiwa na kufunikwa kabisa kimafundisho, ule Msingi, na msingi mpya kujengwa kimafundisho, msingi wa Kikatoliki!!!

  Msingi huu mpya wa Kikatoliki, ndio Msingi ambao umeubadili ule wa Mitume, umechanganya mambo mengi sana ya ibada za kipagani na kuzitia maana ya Kikristo. Nasi kwa asili yetu ya kipagani, mengi ya mambo hayo huonekana ni sawa kiungu licha ya kuwa si ya kimaandiko. Ni vigumu kuamini, lakini nguvu ya kimwili ilitumika kuyalazimisha mambo ya kiroho na mwishowe kufanikiwa.

  Basi imani hiyo ya Kikatoliki ndio ukawa Ukristo katika ujumla wake ikilipoozesha Kanisa hata kulileta kuwa kusanyiko la wafu! Sijaona popote katika Maandiko ambapo Roho wa Mungu alichukuliana na mizimu, hali ikiwa hivyo yeye huondoka, basi Uzima ukiondoka kinabaki nini?! Hebu zichunguze sikukuu za Kikristo, utashangaa kuona mipangilio yake haina uhusiano wowote kimaandiko, tarehe ni za uongo lakini huwakilisha jambo fulani katika ibada za kirumi za kipagani, hata hivyo hakuna anayejali au wote waoga! Wamebadili mambo mengi katika mafundisho yao mapya kwenye huo msingi walioujenga. Ubatizo wameuchezea, mambo ya ndoa wameweka tafsiri zao, na hata fundisho kuu la Utatu Mtakatifu ni la kwao, ndio maana wanatatizika sana kuukubali ubatizo wa kibiblia maana utauvunja utatu jambo ambalo litautia ufa msingi wao na watu kufunguka na kupokea wokovu kamili!

  Basi katika matengenezo ya kanisa, pale Mungu alipoileta nguvu ya ufufuo kupitia Martin Luther, Mungu alianzisha kuchipuliwa kwa kanisa tena. Lakini katika uamsho wote uliofuatia hapo umekuwa ukikua kwa sehemu. Kuhesabiwa Haki kwa Imani ndio sauti ya kwanza iliyo lichomoza upya kanisa na kuliacha dhehebu la Katoliki likiendelea kuwa kapi. Lakini hao walipotoka walibeba na miungu mingi ya kikatoliki pasi kujua wakiiona ni Neno la Mungu. Miungu hiyo imeendelea kujipenyeza katika uamsho zote zilizofuata mpaka katika uamsho huu wa mwisho wa kipentekoste, ukiacha ule wa Azusa uliokuja na kipawa cha lugha, bali mpaka huu wa miaka ya 50/60 uliokuja na vipawa vya uponyaji na madhihirisho mengine mengi. Na sasa tunapofikia mwisho  hatutegemei uamsho zaidi ya huu tulio nao leo hii unaoturudisha kwenye Msingi wa Neno tukitakiwa kuachana na madhehebu yetu ambayo yamajengwa juu ya msingi wa kikatoliki na hayataki kutoka hapo licha ya kuuona Ukweli!

  Unaweza kuona jinsi ambavyo Injili inahubiriwa kwa hila. Wahubiri au madhehebu yetu kila mmoja anajaribu kujipandikiza katika mioyo ya watu kwa kusisitiza mafundisho yao badala ya Neno la Mungu. Mt Paulo anasema hakuja na maneno matamu, kama hizi injili za utajirisho zilizojaa leo hii, bali amekuja na Neno la Mungu ili Imani yetu ijengeke juu ya Msingi huo na si maneno matamu yasiyo na lolote zaidi ya kututia ujinga!! Imani mchanganyiko Mungu haikubali, hatuna excuse yoyote kwa jambo hilo maana Mungu amefanya kazi kubwa ya kutuletea Wokovu wake, iweje leo hii tuufumbie macho ukweli uliowekwa wazi na yeye mwenyewe, nasi tukidai kuwa tu wana???

  Oh, unalo jibu la swali hili utakapoulizwa kuhusu ‘Kweli’ ya Mungu nawe ukidai u mwana: “Je, hamkujua? Hamkusikia? Hamkuambiwa tokea mwanzo? Hamkufahamu tangu kuwekwa misingi ya dunia?” (Isa 40:21)

  Mnayaona Maandiko ndugu zangu? Hakuna injili mpya ila mnakumbushwa tu yale mliyoyasikia tangu kuwekwa kwa misingi ya dunia, yaani kama tulikuwepo huko!!!!

  Bwana, zibua masikio yetu ya rohoni tuyakumbuke hayo tuliyoyasikia, Amen!

 6. Ndugu John Paul, swali lako limenikuna kweli kweli. JESHI hilo linaloandaliwa, mahubiri yao au mafundisho yao, yatalieleza kanisa kuyatafuta Mapenzi ya Mungu, unajua siku tulizo nazo wahubiri wanawaambia watu kuwa mje mbarikiwe, mpate magari, majumba, n.k. Yaani ni mwili mtupu, KUMB 15.11 MASKINI HAWATOKAMA KATIKA NCHI. Sasa watu wanaambiwa wote watatajirika, hata Yesu akasema MASKINI MNAO SIKU ZOTE. Math 26.6- 11. Alikaa duniani miaka 33, akawaacha bado maskini, leo tunawaambia waje wapokee magari, majumba, tena tunawaambia walete hahasha nono, hata wanaotaka kuombewa wapate watoto, Jeshi hilo litamalizia hivi. MAPENZI YAKO YATIMIZWE. Math 26.36-46. Nalitamani Jeshi hilo. Watafahamiana. Kaa mkao wa Kimungu..thanks

 7. Ndugu John Paul, Bwana Yesu asifiwe, swali lako ndilo Swala lililokuwa linanihangaisha sana, na nilipokuwa nauliza Mungu tufanyeje? Akasema yeye ndiye ana uchungu kuliko sisi, yeye ndiye alhmwaga damu yake msalabani, hakufanya kazi ya bure. Akasema mpaka sasa yuko kazini, Mbingu na Nchi zitapita, lakini Neno lake halitapita kamwe, lazima litime. Yapo maandiko ambayo yalitabiriwa zamani yanyohusu nyakati zetu, ni sisi kukaa mkao ule yanataka, Mf. Math 24.4 Angalieni mtu asiwadanganye.-( nani aniangalizie?. Biblia haikusema wazuieni manabii wa ungo, ilisema JIHADHARINI. Sasa hivi unabii ufuato unatimia. Nikupe maandiko utayasoma, na mwingine anayetaka, ili akae mkao wa kutimiliwa.. YOEL 2.1 mpaka 8. EF.4.1 Mpaka 7. ISAYA 41.6 LUKA 1.39 Kifupi niseme hivi, Bwana analiandaa jeshi aliloliona Joel, kila alieokoka kweli atalifahamu. Hawatasukumana, watafahamiana, Yesu na Yohana walifahamiana, lao ni kusaidiana. Sio kudharauliana. Msiogope, kaeni mkao wa kimungu. Thanks.

 8. tujitakase nakutambua hizi ni skiku za mwisho tukeshe tukiomba maana hatujui siku wala saa atakayokuja mwana wa mungu,jamani watu wanaangalia miujiza hata isiyo yakawaida jamani tujihadhali na manabii wa uongo.

 9. Mungu atusaidie sana!

  Michango ambayo imetangulia mi naona kama imeshamaliza kabisa kujibu swali hili, mi sina la kuongeza kuhusu Mafundisho gani yanayotakiwa! Lakini ninayo mengine machache ya kuandika:

  Kwa kumbukumbu zangu, siyo jana wala leo, mambo kama hili yameanza kujadiliwa. Dalili za Wakristo kupotoka na kuiacha Njia zilianza siku nyingi. Na kila wakati kumekuwa na mijadala na watu tukipeana tahadhari na kushauriana kuwa “TUKUMBUKE MAHALI TULIPOANGUKIA” kwamba Turudi kwenye mafundisho ya msingi, ili Tupone, nk. nk.

  Lakini pamoja na kuendelea kushauriana hali nayo imekuwa ikizidi kudorora. Viwango vya ukristo vinazidi kubadilika. Wakati zamani (kutokakna na kumbukumbu yangu) wachungaji walikuwa wakipima huduma zao kutokana na kiwango cha Uwepo wa Mungu kanisani, siku hizi wachungaji wanajipima kutokana na Magari aliyo nayo au majumba aliyojenga, au madaktari na maprofesa alio nao kanisani kwake au hata Idadi ya watu alio nao. (Juzi nimekutana na rafiki yangu mmoja ambaye kafungua huduma, nilipomuulizia maendeleo ya huduma yake akanitajia idadi ya watu aliofikisha!) Shuhuda za wakristo enzi hizo zilikuwa zinahusu mambo ambayo Mungu ametenda dhidi ya nguvu za giza: Watu walikuwa wanashuhudia, mfano, jinsi alivyokuwa anatembea mtaani akakutana na mtu, akamshuhudia na kumuombea kisha mapepo yakajidhihirisha akayakemea! Lakini siku hizi utasikia mtu anashuhudia “nashukuru Mungu nilikuwa Dubai kununua bidhaa”….. Shuhuda wa Ushirika na Mungu zimekuwa chache sana, sana!

  Siku hizi tunashindaniana hata vipawa ambavyo Mungu aliviweka ndani yetu, kwa utukufu wake. Sasa tunavifanya kwa utukufu wetu. Tukichumia mapato. Mwendo wa kanisa kwa ujumla si mwema. Siyo mzuri hata kidogo. Sipendi kuendelea kueleza mabaya mengi bali nielekee kwenye point yangu:

  Sasa, Tatizo ninaloliona mimi siyo Kuwa TUFANYE NINI bali tatizo ni TUNAFANYA VIPI! It is not What Should we Do but How do we Do! Maana kama hatuwezi kupata Namna ya kufanya, tutabaki tu kushauriana na kuelekezana kuwa “Tufanye hivi” huku hali nayo inazidi kuwa mbaya.

  Tatizo kubwa ni kuwa wale walio na mamlaka au wale ambao wanamiliki makanisa na huduma zingine wengi wao ni wagumu mno kupokea ushauri WOWOTE, hata kama ni mzuri namna gani. Unaweza ukatoa ushauri kanisani, labda kuongea na mchungaji ukimshauri namna mpya ya kufanya ili kurejeza kanisa (japo indiviadually) katika Njia, sasa, badala ya kupokea ushauri huo ili angalu auchuje, utashangaa kuona wewe unakuwa Adui huku kazi ya Mungu inazidi kuharibika.

  Mtu akiamua kutoka na kufungua huduma yake, ili labda apate nafasi ambapo atakuwa huru kufanya anachosikia moyoni mwake, huyo ataitwa muasi na kusemewa kila aina ya maneno mabaya. Lakini kibaya zaidi tena ni kuwa huyo aliyeondoka ili akatengeneza kusanyiko Takatifu, naye baada ya muda huingia katika mkumbo huo huo. Naye anabebwa na mkondo wa mafuriko ya dunia. Mungu atusaidie sana!

  Kwa hali hii, japo sote tunaona umuhimu wakurudi kwenye Njia lakini imekuwa ni tabu sana, sana kabisa, kutambua ni kwa NAMNA GANI tunarudi katika misingi hiyo. Ni kama vile msemo ule wa kiswahili usemao “Hakuna wa kumfunga paka kengere”. Kila mmoja amebaki ana shauku ya kuona mambo yanabadilika lakini HAKUNA ajuaye TUNAFANYAJE ILI TUYABADILISHE. Ni wapi pa kuanzia. Je ,ni kwa wachungaji, au ni Kwa washirika? Je, ni kwa Maaskofu au kwa Mitume na Manabii? Ni wapi pa kuanzia?

  Mawazo na tafakari yangu ni juu ya jambo hili kuwa TUFANYE VIPI ili tuweze kugeuka? Au labda ni suala la mtu mmoja mmoja, kama wale 7000 ambao hawakumpigia goti Baali, kwa kificho, kiasi hata Nabii Eliya hakuwa anawafahamu au ni Mass convertion, yaani kama ni kanisani hadi mchungaji atangaze madhabahuni kuwa “Sasa naanza kufundisha kwa msisitizo zaidi mambo ya utakakatifu”……

  Ninaendelea kuwaza na kutafakari jambo hili!

 10. Ndugu zangu,
  Tunamtafuta Mungu katika mambo ya juuuuu sana, bali yeye hayuko huko, ameshuka chiiiiini sana; hebu tushukeni chini huku tuliko muacha na nguvu zake!

  Unajua tunapozungumzia ukristo, ni muhimu sana kujua ni kwa jinsi gani mtu anaweza kuwa mkristo na ni vigezo gani vinavyomfanya mtu kuwa mkristo? Kwanza, katika hali tuliyonayo, ni vigumu sana kusema kwa uhakika nani ni mkristo, katika maana ya anayemfuata Kristo kikamilifu kimafundisho. Kwani tuna tofauti nyingi sana kati ya makundi yetu, yawe ya kidhehebu au ya wokovu. Kwa hiyo linapokuja suala la uhakika, hilo huzua mjadala usioisha. Lakini licha mijadala kutokwisha, hilo bado haliufanyi ukweli kutokuwepo ili mradi Biblia, ambayo ndiyo inayotutambulisha kwa Kristo, ipo!

  Ukiusoma mchango wa Dada Imani, unaweza kuona katika uhalisi jinsi ambavyo licha ya ukiri wetu wa Wokovu lakini bado tumepungukiwa. Yaonekana kuna jambo fulani ambalo lingeleta utofauti linakosekana, hatujui ni nini, lakini tunajua limekosekana! Maandiko tunayaona, tunayasoma kututia moyo, lakini baada ya umbali fulani nguvu zinatuishia, wengine wanaanguka, wengine tunajikokota, na baada ya maombi, mzunguko huanza tena! Dada Imani anamalizia kwa kuielezea hali hiyo hivi: “Watu wanatafuta kukubalika machoni pa binadamu na si machoni pa Mungu. Wepesi wa kuudhika, kukwazika, kukata tamaa na hata kumkasirikia Mungu.” Ni huzuni kiasi gani tuliyonayo katikati ya Wokovu!!

  Ndugu Samuel, katika kukabiliana na hali hiyo, akijaribu kulitafuta hilo linalokosekana, hata kanisa, haswa sisi wenye kukiri Wokovu, kuwa katika hali hii yenye kuhuzunisha ilhali twajua kuwa twapaswa kuwa wenye furaha kupita mtu yeyote yule hapa duniani, basi shauku ya kulitafuta hilo ni kubwa sana. Na katika hilo ndio tunamuona ndugu Samweli akiturudisha pale tulipopaswa kuanzia safari yetu, Juu ya Msingi alioujenga mtume Paulo kwa kanisa la Mataifa, huo ndio ule Msingi wa Manabii na Mitume!!

  Je, ndugu yangu, Ukristo wako umejengwa juu ya Msingi huo?? Usiwe mwepesi wa kudhania katika majibu yako, utapata hasara. Yeyote anayetuhubiria Injili, anapaswa atuhubirie Injili kama ilivyohubiriwa na Mitume kwa mambo yoooote! Hakuna nafasi ya kutafsiri chochote katika Neno la Mungu. Kama maandiko yanasema ni Hukumu kwa asiyeamini, basi ihubiriwe hivyo, nawe uwe umejengeka juu ya msingi huo katika ukristo wako. Kama Maandiko yanasema simpi nafasi mwanamke kufundisha, elewa hivyo na ubakie hapo kwa moyo wa furaha, usianzishe ubishi! Lakini huwezi kufika katika kiwango cha kulitii Neno la Mungu, bila kwanza kuhubiriwa Injili ISIYOGOSHIWA. Injili isiyogoshiwa ndio Msingi Imara anapojengwa Mkristo hata akawa NGOME. Hatua ya kwanza katika kuingia katika Ukristo ni kuhubiriwa Injili, haijalishi umezaliwa katika nyumba ya wazazi wakikristo, wewe mwenyewe katika rika fulani lazima ukutane na Injili ndipo uwe Mkristo halali. Huo ndio Msingi! Ukiisha isikia Injili itakujengea Imani itakayokuongoza katika kuyatimiza yote yapasayo kwa furaha kubwa, maana Imani ni kipawa cha Mungu ambacho hukupa kuelewa Mungu alivyokuepusha na adhabu ijayo kwa Neema akikufungulia Milango ya Ufalme usiouotea ndoto hata siku moja wala kustahili! Basi nawe shauku yako haiwezi kuwa tofauti na wale wenzako wa siku ile katika Mdo 2:37 waliowauliza Mitume, ‘Tutendeje ndugu zetu?’ Kama Maandiko yalivyoliweka sharti la kuingia katika Ukristo, nawe baada ya kuiamini Injili, unatubu dhambi zako na unabatizwa maji mengi kwa Jina la Bwana Yesu Kristo ili upate Ondoleo la Dhambi zako!! Hii ndiyo “abc” ya WOKOVU.

  Kushindwa kwetu kote kunatokana na jambo hilo tu, Dhambi zetu hazijaondolewa!!! Tutajaribu kuutafuta UTAKATIFU, lakini hatutafanikiwa. Tutafanya Maombi na Mikesha yake, lakini kitambo kidogo nguvu zitatuishia tena. Tutayaona mafanikio lakini mbele kidogo yatatupotea. Tutaruka kwa shangwe na kunena kwa Lugha, lakini ni kwa kitambo tu, maana hisia au emotions ndizo hututawala na kujaribu kujaza ule upungufu, maana hao waliotuletea Injili wametushortchange! Wametuletea Injili nyingine kwa makusudi ya kutufikisha hapa tulipo! Je, Tutaponaje iwapo tumeunganishwa na waliokataliwa? Maana Maandiko yako wazi kabisa, katika Wagalatia 1:8, mtume Paulo anasema hivi kwa kanisa, “Lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi injili yoyote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe.” Ndugu zangu kuna jambo lisiloeleweka katika kifungu hicho? Tunapaswa kurudi katika Msingi huo Imara wa Neno la mungu kama tunataka kupona, makundi ya watu hayawezi kumbadilisha Mungu katika wazo lake kwa ukengeufu, ndio maana tuna njaa ya ukamilifu mioyoni mwetu maana injili tuliyolishwa haishibishi! Pia, hauwezi ukakosea njia mwanzo wa safari, halafu njia hiyo hiyo ikakufikisha uendako, lazima mwisho uwe wa kilio maana umeishia kusiko!!

  Basi ndugu zangu turudini huku chini tuliko muacha Mungu, tukamilishe kwanza HATUA ya KWANZA, tuisikilize Injili inachotuambia, kama wahubiri wanaipiga chenga Injili ya Kweli, chukua Biblia yako, soma kitabu cha Matendo ya Mitume, humo utalikuta Kanisa la Kwanza likichipua. Utakutana na Mitume wote humo watakuhubiria, ukiwaamini katika wanachokufundisha, pamoja na UBATIZO wanaokuelekeza, Mungu atawajibika kwako kukuletea ‘Mwili’ wake kama alivyomfanyia Kornelio, maana ‘Yesu Kristo ni yeye yule, jana na leo na hata milele’, habadiliki!

  Nawaombeeni nyooote, Bwana awape nguvu zake ili mpata UJASIRI wa KUJINYENYEKEZA kwa Neno lake, na furaha yenu iwe kamili katika yeye!

 11. Kweli Mungu atusaidie kanisa turudi ktk msingi kama alivyosema ndugu Samwel. Binafsi nimechoshwa na injili ya mafanikio maana ndio inayotawala kwa sasa japo inakuja kwa njia nyingi!

 12. Kanisa lirudishwe kwenye MSINGI. Zab 11.3 KAMA MISINGI IKIHARIBIKA MWENYE HAKI ATAFANYA NINI? MSINGI ni muhimu sana, msingi ndio mwanzo wa kitu, kanisa nalo lina msingi wake, Mtume Paul alisema hivi katika 1KOR 3.10-11 KWA KADRI YA NEEMA YA MUNGU NILIYOPEWA,MIMI KAMA MKUU WA WAJENZI MWENYE HEKIMA, NALIUWEKA MSINGI, NA MTU MWIN4NE ANAJENGA JUU YAKE. LAKINI KILA MTU NA AANGALIE JINSI ANAVYOJENGA JUU YAKE. MAANA MSINGI MWINGINE HAKUNA AWEZAYE KUUWEKA, ISIPOKUWA NI ULE ULIOKWISHA KUWEKWA YAANI KRISTO. Biblia inatueleza kuwa msingi wa Kanisa ni Kristo, na alipokuja duniani alichagua watu aliowaita MITUME, akawafundisha kazi, wakafanya kazi, halafu Kanisa likaendelea kufanya wajibu wa lenyewe, inabidi Kanisa lirudishwe kwenye MSINGI, EFESO 2.20 MMEJENGWA JUU YA MSINGI WA MITUME NA MANABII, NAYE KRISTO YESU MWENYEWE NI JIWE KUU LA PEMBENI. Kwa mujibu wa Neno la Mungu, kanisa lifundishwe Msingi wa Mitume na Manabii, likifundishwa vizuri, yale yote tunayoyasoma katika Matendo ya Mitume tutayaona, yale yaliyowapata pia yatalipata Kanisa, na litashinda. Thanks.

 13. Kanisa linahitaji kuwekwa kwenye NJIA. Yoh 14.6 Yesu akasema mimi ndio NJIA na KWELI na UZIMA, MTU HAJI KWA BABA ILA KWA NJIA YA MIMI. Kwa kuwa kusudi la viöngozi wa kanisa ni kulifika Mbinguni kwa Baba, basi ni kuliweka kwenye NJIA. ISAYA 30.20-21 NA INGAWA BWANA ATAWAPENI CHAKULA CHA SHIDA NA MAJI YA MSIBA, LAKINI WAALIMU WAKO HAWATAFICHWA TENA, ILA MACHO YAKO YATAWAONA WAALIMU WAKO, NA MASIKIO YAKO YATASIKIA NENO NYUMA YAKO, LIKISEMA NJIA NI HÍI IFUATENI, MGEUKAPO KWENDA MKONO WA KULIA, NA MGEUKAPO KWENDA MKONO WA KUSHOTO. ISAYA 35.8. NA HAPO PATAKUWA NA NJIA KUU, NA NJIA, NAYO ITAITWA NJIA YA UTAKATIFU, WASIO SAFI HAWATAPITA JUU YAKE, BALI ITAKUWA KWA AJILI YA WATU HAO, WASAFIRIO, WAJAPOKUWA WAJINGA, HAWATAPOTEA KATIKA NJIA HIYO. Njia ya kwenda Mbinguni ipo wazi, ambayo ni YESU, Kanisa lifundishwe namna ya kutembea katika njia hiyo. Mwisho Kanisa lifundishwe KUMAANISHA, 1Yoh 3.18. WATOTO WADOGO, TUSIPENDE KWA NENO, WALA KWA ULIMI, BALI KWA TENDO NA KWELI. Wengi wetu tunampenda Mungu theoreticaly, ebu Kanisa lifundishwe kuwa Matendo yanasema kuliko maneno. Thanks.

 14. Shalom,

  Utakatifu ni msingi wa wokovu sababu unagusa maisha a ndani ambayo ndo msingi wa kuwezesha kubadilisha maisha ya nje. Utakatifu unaleta hofu ya Mungu, hekima na kupambanua lipi sahihi katika kuongea, kutenda, kuvaa na kila eneo la maisha.

  Hebr 12;13
  Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao;

  a) Wapendwa siku hizi wokovu umekuwa ni title tu lakini si uhalisia wa Yesu ndani yetu. Hatutafuti kukua kiimani, kumjua Mungu na kujifunza jinsi ya kusimama sawa na mapenzi ya Mungu. Infact wengi wanafocus kwenye ahadi za vitu vya mwilini na si vya kiroho (UTAJIRI WA MALI vs USHINDI WA DHAMBI)

  a) Wapendwa tunataka ‘short cut’ ili kupata utoshelevu wa mwili (ambayo si ya kudumu) na kutotilia mkazo ya ndani. Pamoja na msisitizo mkubwa unaopewa juu ya miujiza lakini ndicho kipindi unaposhuhudia wakristo wengi hawana nguvu za kiroho. Kila siku watu wanaombewa na mapepo yanarudi, majaribu yale yale kila kukicha hakuna ushindi na wengine ndo yanawatoa kabisa katika imani.

  b) Tunadhani kupiga kelele kumkemea shetani na kutoa sadaka ndo ‘substitute’ ya kuishi maisha matakatifu. Hatukubali kutambua mapungufu yetu, kutubu na kukubali kuchukua hatua kuyafanyia kazi. Tumekuwa tukijihesabia haki sana badala ya kuchukua hatua na kumruhusu Mungu atubadilishe. Ndo maana shetani anazidi kuburuza watu.

  “Basi mtiini Mungu. Mpingeni shetani naye atawakimbia” (Yakobo 4:7).

  d) Maisha ya utegemezi kiroho yamekuwa makubwa. Kuishi kutegemea kuwekewa mikono, kupaka mafuta, kutumia vitambaa na kupewa uanabii tu. Ndo maana watu hawawezi kushinda changamoto ndogo ndogo. Manung’uniko, kukata tamaa, kulaumu na kubadili makanisa kila kukicha. Majaribu yamekuwa yakionekana ni kama laana na si fursa ya kukua kiroho na kuthibitisha uthabiti wa imani yako.

  e) Watu wanatafuta kukubalika machoni pa binadamu na si machoni pa Mungu. Wepesi wa kuudhika, kukwazika, kukata tamaa na hata kumkasirikia Mungu.

  Mungu atusaidie
  Dada Imani Kapinga

 15. Tukifundishwa na kufundishana juu ya utakatifu, namna gani tunastahili kuishi kulingana na neno la Mungu tutakuwa tumepiga hatua kubwa katika maisha yetu ya mbinguni.Ni bahati mbaya sana kwamba kutokana na nguvu za shetani tunaona yale yaliyoko karibu na sisi tu wakati yale yaliyofichwa hatuyaoni.Kumbe yaliyofichwa ni sawa na Roho wa Bwana ambaye hatumwoni lakini ni yeye anayetusaidia kuokoka.na kitu kingine wakristo wa leo hupenda kujionyesha mbele za watu kuwa wameokoka kwa kutoa misaada mingi makanisani lakini ndani ya mioyo yao hawana Kristo wa kweli wamekataa kuubeba msalaba wao.Wanaogopa kuutesa mwili wao kwa kubeba msalaba.Huo ni unafiki katika imani.Na Mungu hapendi unafiki.Kama unataka mtumikie Mungu kwa dhati kutoka moyoni mwako na si vinginevyo

 16. Kimsingi mbali na utakatifu, lazima tujue tuko siku za mwisho zaidi, na kanisa la mwisho limeahidiwa kuwa na utukufu mkuu kuliko kanisa la kina Petro, lakini kina petro vivuli viliponya watu je leo?wakristo wanatakiwa wafundishwe mafundisho yenye kuwawezesha kuishi na Mungu siku zote na kumshinda na kumpuuza shetani.
  Angalia leo bado wakristo wanateswa na wachawi na wanga, wakisikia freemason ndo usiseme! hivyo utajua viwango bado sana. Mkristo wa leo hatakiwi kila kitu akaombewe bali ajue yeye ni nani, Mungu anamwangaliaje, ajue mamlaka yake,haki zake mbele ya Mungu,ajifunze kwa bidii umuhimu wa kuwa na Roho mtakatifu siyo tu ishara ya kunena kwa lugha bali uwezo wa kuomba kwa roho kwa muda mrefu sana nk.

  Mbarikiwe

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s