Mchungaji Mason Betha amerudi kwenye muziki wa kufoka foka!!!

Mason Betha, rapper wa miaka ya 90 aliyetangaza kuacha muziki huo miaka 13 iliyopita na kuwa mchungaji, amerudi kwenye hip-hop tena, na kipindi hiki kwa nguvu zote na ameomba watu wamuombee katika fani yake hii aliyorejea.

Mason  Betha ambaye ni mchungaji kiongozi wa El Elyon International Church na Mason Betha Ministries, amejutia uamuzi wake wa kutoka kwenye uimbaji wa kufoka foka hadi kuwa mchungaji. Soma maelezo yake hapa Article Here!

Hii habari si njema kwa kanisa, tunao watumishi wa Mungu Tanzania ambao walikuwa maarufu kabla hawajaja kwa Bwana Yesu, tunatamani tuone wanaendelea mbele zaidi na si kurudi kule walikotoka, kwenye bongo fleva, taarabu na disko. Mungu atusaidie wote!

Biblia imeandikwa katika Luka 9:62 “Yesu akamwambia, Mtu aliyetia mkono wake kulima, kisha akaangalia nyuma, hafai kwa ufalme wa Mungu”

Advertisements

4 thoughts on “Mchungaji Mason Betha amerudi kwenye muziki wa kufoka foka!!!

 1. Ndugu zangu hapa ndipo inapotakiwa watu kujua maana ya kuokoka: Wokovu ni kitu cha dakika moja baada ya kumkubali Yesu, lakini UTIMILIFU WA WOKOVU ni kuvumilia hadi mwisho.

  Wako watu wengi sana makanisani ambao hawana mpango wa kuvumilia.

  Tusichukulie kila mtu anayeejiita AMEOKOKA kuwa ni ataenda MBINGUNI au kuwa ana mpango na Yesu.

  Tujifunze kumtafuta Yesu, kuung’ang’ania wokovu, na kukaza mwendo badala ya kuhesabiana nani ameokoka na nani bado.

 2. huyo hakuguswa na Yesu alivutwa na vitu aliyeguswa na Yesu hawezi kuludi nyuma anyway kama ni wa Mungu ataludi tu mana Mungu hutumia hata mapigo kumludisha mtu katika mstari!

 3. Sasa ni nini hatima ya Mason Betha Mistries na El Elyon international church? “Namkumbuka huyu alikuwa anatumia jina la Mase, na hata alipotangaza kuokoka niliona kwenye Tv”

  Nadhani kinachosabisha hali hii ni kuwa Watu wa namna hii huwa wakiokoka anakuwa “AMEOKOLEWA” na watu au vitu wala si Yesu, Mwokozi! Na wengi huwa wanafuata maslahi, yaani pesa kwa kiasi kikubwa. Wengine wanaweza kuamua kuokoka kwa kuwa ameponywa magonjwa na sababu nyingine yo yote ambapo mtu huyo huwa mfuasi wa kanisa na si Mfuasi wa Yesu.

  Haiwezekani mtu akaolewa na Yesu, akawa na uhusiano binafsi na Yesu (Mungu mwenyewe), aone wema wa Bwana halafu baadaye AJUTE kuokoka! Hapana. Maana hakuna mahali pengine salama na kwenye amani kama kwa Yesu.

  Mungu awasaidie wote ambao wameamua kukimbilia kwa Yesu, ili kujisalimisha, Wasije wakarudi nyuma!

  Namuombea sana dada Stara Thomas, Renee Ramira, Mzee Makassy na wengine ambao walikuwa wanamuziki wa huko kwa shetani lakini wakaamua kukimbilia kwa Yesu. Mungu awatunze na kuwalinda.

  Amina!

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s