Watu wanaendelea kumpigia Kura Christina Shusho!

VIVA SHUSHO VIVA TANZANIA, PAMOJA KWA UMOJA KWA UTUKUFU WA MUNGU

Zikiwa zimebaki siku 12 kabla kufungwa kwa pazia la upigwaji kura kwa waimbaji watakaotwaa tuzo za Africa Gospel Music Awards(AGMA) 2012, Watu mbalimbali wameendelea kuitikia mwito kwa kumpigia kura mwimbaji pekee wa Tanzania aliyependekezwa kuwania tuzo hizo kwa mwaka huu Christina Shusho ili kuhakikisha Tanzania tunakitu cha kujivunia kwa mwaka huu baada ya kuondoka mikono mitupu mwaka jana.

Ambapo kampeni mbalimbali zimeendelea kufanywa kupitia Blog mbalimbali za kikristo nchini, Radio za injili pamoja na zile zisizo za injili lakini wana kipindi cha gospel,pamoja na mitandao ya kijamii kama Facebook,Twitter na mingineyo, kati ya radio ambazo tayari kampeni hizo zimefanyika ni pamoja na Wapo Radio Fm( Nuru ya Jamii), Praise Power Radio(Faraja kwa watu), Ushindi Fm ya jijini Mbeya na Clouds Fm kupitia kipindi chake cha gospel track kinachoendeshwa na mchungaji na mtangazaji Harris Kapiga.

Katika siku 12 zilizobaki kama hujapiga kura yako fanya hivyo sasa ili kumwezesha mwimbaji wetu Christina Shusho kurudi na tuzo mbili alizopendekezwa kuwania ambazo ni

 Mwimbaji bora wa kike barani Afrika pamoja na Mwanamuziki bora wa mwaka kutoka Afrika ya mashariki, hii itawezekana endapo utampigia kura na kumwezesha Shusho kutwaa tuzo hizo utakuwa umemwinua Mungu kupitia muziki wa gospel nchini pia utakuwa umeitangaza nchi yetu duniani, Viva Shusho, Viva Tanzania. barikiwa sana.

Ili kumpigia kura fuata maelekezo yafuatayo ingia kwenye tovuti ya shindano hilo

http://www.africagospelawards.com/nominate.html kisha fuata maelekezo yafuatayo

VOTE NOW
AGMA 2012 VOTING GUIDELINES
1. Click on the ‘VOTE NOW’ button.
2. Register your email address, confirm and submit.
3. Check your email (inbox) and you will find the link to vote.
4. If you do not find the link in your email inbox, please check your junk mail folder.
5. Once you have connected to the voting page please make your selections and submit (you can only vote for one nominee from each category).
6. You do not have to vote in every category.

   Baadhi ya picha kuhusiana na kampeni hiyo ya kumwezesha Shusho kutwaa tuzo.

Harris Kapiga akiwafanyia mahojiano timu ya bloggers na Christina Shusho j2 asubuhi.
Shusho kushoto pamoja na Victor wakiendelea na mahojiano ndani ya Clouds Fm J2 asubuhi.
Christina Shusho,Papaa Sasali pamoja na Harris Kapiga wakipata picha baada ya mahojiano.
Papaa Samuel Sasali pamoja na Victor Mboya wakiwa full kutabasamu baada ya kumaliza mahojiano ndani ya Clouds Fm Jumapili asubuhi.
Mambo yakiwekwa sawa tayari kwa mahojiano,Unclejimmy Temu pamoja na Victor Mboya mwenye laptop.
Unclejimmy Temu akimfanyia mahojiano Victor Mboya wa Hossanainc.blog kuhusiana na kampeni hiyo.
Unclejimmy Temu akiwa na wadada wa kundi la Double E studio za PPR.

 

Advertisements

2 thoughts on “Watu wanaendelea kumpigia Kura Christina Shusho!

  1. Shusho love love love you dear…such a blessing u are to me n many.Surely the Lord will bless you too

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s