Kusikiliza nyimbo za kidunia haifai kwa Mkristo?

Bwana Yesu Asifiwe, Wapendwa naomba kuuliza je kusikiliza nyimbo za Bongo fleva(za kidunia) ni dhambi? Na kwa nini ni dhambi? Naomba jibu lako.

–Theodory Constantine
Advertisements

56 thoughts on “Kusikiliza nyimbo za kidunia haifai kwa Mkristo?

 1. Obviously kuna falme mbili zinazoitaka nafsi ya mwanadamu.
  1.Mungu
  2.shetani
  kama ni hivyo yakupasa ujue kwamba hata mawazo uwazayo yanaweza kuwa ya kimungu au kishetani hakuna neutral.sasa iwapo unafanya kitu kisicho mtukuza Mungu jua moja kwa moja wamtukuza shetani kwani ndo falme zinazoitaka nafsi ya mtu (ufalme wa Mungu na shetani) na hizi falme zinapingana. wewe nyimbo inaimbwa (you are my number one…my sweety) hapo unamtukuza nani? kama wamtukuza Mungu endelea kuckiliza na kuimba. haijalishi anayetajwa ndani ni nani mfano. nicki minaj aliwah imba “they never thank me 4 opening the door but they ai’nt thank me 4 Jesus for dying on the cross” wadhan nicki ataenda mbinguni kwa kumtaja yesu? nyimbo yoyote inayosifu vitu vya ulimwengu na si Mungu bs jua zinamsifu shetani na kama wamsifu shetani hutaingia ktk ufalme wa Jehovah!
  nafahamu sana kuhusu miziki,kabla sijaokoka nilikuwa nazipenda bt now najua c nzuri hazimpendezi Mungu.
  for more information abt mziki wa kidunia nitafute
  -festoallan@gmail.com

 2. Leo nimesikia ushuhuda wa ajabu kwamba unapotoka wimbo mpya wa secular/bongo fleva au wa kidunia wachawi huwa wanausikiliza na wakiona unawafurahisha huwa wanautumia kujiburudisha wanapokutana kwenye mikutano yao au kwenye tukio la kumroga mtu! Kumbe kuna uwezekano wa kuwsikiliza wimbo ambao ni kipenzi cha wachawi! Sasa hapo utakuwa unajiweka katika daraja gani?

  Nyimbo ambazo hazijaimbwa zikiwa na utukufu wa Mungu au ambazo siyo kwa utukufu wa Mungu zina mambo mengi yanayofanyika katika ulimwengu wa roho ambayo siyo rahisi kuyafahamu iwapo mtu haupo katika roho!

  Hii nichangamoto kubwa kwa watu wa Mungu!

 3. Praise The Name Of The Living God Realy guyz Your Gud And Bright And I Saying Thanx For Copart In Buillding The Live Souls What U Loosing God Will Give To U Much By Dublicate what we have 2 do is listen 4 da holly spirit only he never decided a wrong choice to the heart of the one who blv in god.

 4. guyz what we have 2 do is listen 4 da holly spirit only he never decided a wrong choice to the heart of the one who blv in god.

 5. Ningependa kujua tunachosikiliza ni mziki au ni ujumbe unaotolewa na muimbaji kwa kufafanua kidogo MZIKI ni ala za sauti zinazoundwa na vyombo lakini UJUMBE Unaweza ukatolewa pasipo mziki na unaweza ukaitwa wimbo Sasa mziki ndio unaoongeza tamaa na ushawishi ndo maana kinachowavutia watu ni mdundo na mabiti ukiwa na wimbo mzuri lakini biti ni baya watu hawataupenda wimbo wako(and vice versa) na kama unanguvu ya roho mtakatifu kila uamuzi na tendo unalotenda ni lazima nafsi yako itakuhukumu kama ni baya na mwisho wake ni kujilaumu wakati umeshatenda dhambi KWA HIYO KAMA KITU HAKIFAI NI LAZIMA NAFSI YAKO IKUHUKUMU Ndani yako

 6. Hazifai kabisa maana kila upandacho ndani ya moyo wako ndio kinakuwa kama ulivyowaza na kutamka.

 7. Nyimbo za kidunia ni Dhambi kabisaaaaa,kwa sababu Biblia inasema kwenye Muhubiri 7:5 Inasema Heri kusiki lawama za wenye Hekima Kuliko mtu kusikiliza wimbo wa Mpumbavu.Je!Wapumbavu ni nani?au wakoje?MATHAYO 7:26-27.YESU alisema mtu yoyote atakaye yasikia Maneno yake alafu asiyafanye atafananishwa na MPUMBAVU.Kumbe MPUMBAVU ni yule ambaye afati NENO LA MUNGU, kwa maneno mengine MPUMBAVU ni yule mtu ambaye ajaokoka,kumbe autakiwi kusikia WIMBO za MPUMBAVU yaani mtu ambaye ajaokoka,NENO LA MUNGU NDIO

 8. Wapendwa katika bwana naombeni kuuliza swali!Ni kwanin wakristo wengi wanakuwa wanaokoka na hawadumu katika imani?

 9. Ndg Sungura,

  Kuhusu ‘Mapenzi ya dunia ni nini?’ labda niseme nakubaliana na wewe kuwa kwa kule kuwa umeokoka, basi unayajua, na hayajakuzonga kama Biblia inavyotuonesha hao waliozongwa na hayo: Marko 4 :18 -19 “ Na hawa ndio wale wapandwao penye miiba; ni watu walisikiao lile neno, na shughuli za dunia, na udanganyifu wa mali, na tamaa za mambo mengine zikiingia, hulisonga lile neno likawa halizai.”

  Basi mtu aliye okoka, kama ulivyosema, ni mtu aliyezaliwa mara ya pili, yaani amezaliwa kwa Roho wa Mungu, naye huwa ni mwana wa Mungu kwa jinsi hiyo ya kuzaliwa mara ya pili. Kwa huyo Roho wa Mungu hukaa ndani yake. Yaani huyo huwa ni Kristo katika mwili tena leo hii; basi ukimkuta anasikiliza “Ndombolo ya Solo”, jua mbinguni kumekucha!!!!

  Ubarikiwe ndugu yangu!

 10. Asante sana bwana Milinga.

  Ndg. Lwembe kafanya tu kama ilivyo kawaida ya watanzani; kuleta maneno mengi pasipo kwenda moja kwa moja kwenye “point”. Mimi nimemuuliza maswali mawili, kakwepa kujibu yote badala yake ananiuliza swali tena. Nashukuru Milinga umejibu hilo swali langu la pili.
  Lakini pia Lwembe katika kukujibu comment yako bado hajawa “strait” badala yake kaongea mambo ya giza na nuru.

  Ndg. Lwembe usijaribu kabisa kuwaza kwamba sijui maana ya mapenzi ya dunia. Ninataka tu nijue wewe unavyoelewa kuhusu mapenzi ya dunia maana katika mchango wako huko juu umeyaponda. Na sijui ni wapi biblia imesema kama ungali katika mapenzi ya dunia upendo wa Mungu hauko ndani yako.

  Lwembe mtu aliyeokoka ni mtu aliyezaliwa mara ya pili kwa njia ya kumwamini Yesu Kristo na kufanyika kuwa mtoto wa Mungu. Ingawa sioni kama hii ni ya lazima sana katika kujibu swali la mapenzi ya dunia. Pia nafikiri unaweza kuongeza hapo katika mtu aliyeokoka ni yupi.

  Ubarikiwe

 11. Milinga,
  Maisha ya gizani kwa aliyekulia gizani ni mazuri na ya kawaida hadi siku itakapomfikia Nuru na kujiona alivyoishi katikati ya mende na uchafu mwingineo, ndipo akiwa Nuruni aweza kuhadithia mambo ya gizani! Ndio maana nikauliza, “Mtu aliye OKOKA ni yupi?” maana ninaamini ni huyo pekee awezaye kutupa jibu la mapenzi ya dunia ni yapi, maana Mapenzi ya Mungu – ile Nuru, yamejaa ndani yake, kuliko wengi wetu tunaojidhania tumeokoka, na sasa hatujui hata mapenzi ya dunia ni nini, hii kama si michezo ya hatari ni nini? Ndugu zangu tujitahidi, Kuzimu na Moto wake ni halisi kama ambavyo Kuokoka na hayo kulivyo!!
  Hii “drunk sober man” position ya wokovu tuliyonayo ina hasara!

  “Mtu aliye OKOKA ni yupi, wapendwa?”

 12. Kuna wimbo wa Bob Ludala ulipigwa siku ya harusi yangu “NIMEKUCHAGUA WEWE” Huo wimbo huwa nikiusikia nakumbuka siku ya kufunga pingu za maisha na Mke wangu mpendwa ambaye hadi leo ninaye na ni mhudumu kanisani (Mwimbaji na kiongozi wa Kwaya).
  Huo wimbo ingawa ni bongl flava mahudhui yake yanadumisha mapenzi kwenye ndoa yangu ambapo amri kuu ya kwanza na ya mwisho ni UPENDO.
  MNASEMAJE KUHUSU HILO?
  Si kila bongo flava ni mahudhui ya kishetani, tuachane na mawazo potovu. Itategemeana na wewe mpokeaji wa ujumbe. Wapo watu wa kidunia wanazitumia nyimbo za Injili kugeuza mahudhui na kuonekana ya kishetani au kisiasa.
  Mfano: Wimbo wa Rose Mhando – Utamu wa Yesu; ni mara ngapi unapigwa kwenye mabaa na watu wanaserebuka kidunia?
  Wimbo wa Mwaitege: Matendo – vivyo hivyo; ni mapokeo ya msikilizaji tu wapendwa.
  Wanaojifanya kutosikiliza bongo flava kwa kisingizio kuwa ni nyimbo za kumpa utukufu shetani ni kwa sababu hawajakomaa kiimani; watakuwa wamempokea Yesu hivi karibuni na hivyo wana ulimbukeni wa kirokole.
  Niliokoka nikiwa primary; hadi sasa nampenda Yesu (japo kuna kipindi sikuwa imara kwenye wokovu; na hilo ndo limenifanya kufahamu mengi kuhusu kumtumikia Mungu na kuishi maisha ambayo sibagui mtu wala kazi ya mtu kuiita ya kishetani)
  Nyimbo zipo nyingi, Reggae, Blues, Kwaito, Taarabu, n.k Ukitunga wimbo wako wa kumsifu Mungu ukatumia maadhi ya taarabu kuuimba utachezeka tu hata kwenye miduara ya kwenye club.
  NAAMINI MWENYE KUNIELEWA AMENIELEWA VYEMA.

 13. Sungura,

  Kwani wewe hujui kwamba wapendwa nao hufanya ngono? Kwani “ngono” ni nini?
  Ina maana Lwembe wewe hufanyi ngono? Hakuna binadam mzima wa afya asiyefanya ngono. Ngono ni muhimu kwa afya ya ndoa yako. Au wewe hujawa na ndoa? Ngono pia ni muhimu kwa wanandoa tu, Ni kiungo cha lazima katika ndoa.

  Lwembe naye atueleze ana maana gani asemapo, “mapenzi ya dunia”. Hii ndiio mambo gani?

 14. Ndg Sungura,
  Mpaka sasa bado najaribu kukujibu swali lako, ila natatizika pale linapokuja suala la “walio okoka” ; labda tungeliangalia hili kwanza, huenda lingetuongoza vizuri zaidi hata kuyajua mapenzi ya Mungu ambayo yangetuonesha kwa usahihi mapenzi ya dunia ni nini!. Je, Mtu aliye okoka, ni yupi?

  Nikushukuru kimbele, na
  Ubarikiwe!

 15. Bwana Lwembe mapenzi ya dunia ni nini?
  Je wapendwa nao huwa wanafanya ngono, au yenyewe ni ya wasiookoka tu?
  Nisaidie Lwembe!
  Asante.

 16. Nyimbo zote hubeba ushawishi. Ushawishi wa mapenzi, mali, ibada, ngono, uhalifu na mambo mengi mengineyo.

  Kwa hiyo suala la kusikiliza nyimbo zipi litategemeana sana na unachopenda ushawishiwe, kama ni mapenzi au utajiri au masikitiko, au ngono, nk!

  Biblia inasema kama ungali katika mapenzi ya dunia, basi Upendo wa Mungu haumo ndani yako!

  Mbarikiwe nyoote wapenda muziki!

 17. Selelii Edwin,

  I like the way you show up here. Ubarikiwe saaana. Umenena ukweli mtupu. Maelezo yako yanatakiwa kila mpendwa ayasome. Natamani sasa ningekopi na kumpestia kila mpendwa kwenye Laptop yake ili awe anasoma comments zako kwani kuna wapendwa wanadhani wameshafika mbinguni ambako hakuna hata tone la muziki wa “dombolo ya kongo” utakaosikika.

  Mimi nimesema na ninarudia, KIPIMO CHA MLOKOLE ALIYEKUA KIROHO NI VILE ANAVYOWEZA KUISHI NA WATENDA DHAMBI BILA YEYE KUZITENDA DHAMBI WATENDAZO.

  Kama wewe huwezi kutazama picha mbaya na ukaondoka bila kukwazika wala kuvutwa na picha hiyo kwa minajili ya kutenda dhambi, wewe umekua kiroho.

  Mpendwa, Kama hujafikia kiwango cha kuweza kumtazama mwanamke akiwa amekaa vibaya au amevaa nguo nyepesi au fupi sana bila kumtamani wala kugeuka geuka mara mbili mara tatu kumtazama, mara unatupia jicho kumcheki tena alivyokaa kaa, alivyovaa hovyo, basi wewe hujakua kiroho. Nakushauri kabisa usisogelee maeneo yenye watu wa namna hiyo.

  Ukiona kanisani watu wanahangaika na watu wanaovaa “vinguo” vifupi eti wanawarushia kanga wavae maana wamevaa vimini, ujue kanisa hilo lina watu ambao hawajaokoka na wala hawajakua kiroho na kimaandiko. Ni watoto wachanga mtupu.

  Mtu mzima hawezi kubabaika amwonapo mtoto mchanga amekaa uchi au anatembea bila nguo. Wewe kama umeokoka na umekua kiroho kwa nini ukimwona mtu amevaa vibaya au kimini unashangaa nini? Kitu gani kinakuuma wakati yule ni mtoto mchanga kiimani au hata Imani ya Mungu hana? Unachanganyikiwaje kumuona mtoto amevaa nguo fupi?

  Mpendwa, kama wewe huwezi kusikiliza mziki wa dunia na maneno yaliyomo yawe mazuri au mabaya, wawe wananengua kwa sana (kama ilivyo hata makanisani leo), kama wewe huwezi kusikiliza bila kushawishika kutenda maovu, kama wewe ukisilikiza tu muziki wa “kidunia” unaanza kuvutwa na “tamaa za dunia” wewe hujakua kiroho. Wewe bado ni mtoto mchanga kiroho. Mtu yeyote anayevutiwa na tamaa za dunia hii kwa sababu tu zimepita karibu naye, au amesikiliza kupitia muziki, huyo anatupa picha mbili: Kwanza HAJAOKOKA, Pili, kama ameokoka basi, HAJAKUA KIROHO NA KIIMANI. Ukweli ndo huo.

  Mimi nakupa mfano wangu, ofisi kwangu nimewahi kufanya kazi na watu wanaokunywa pombe sana na maasi mengine. Ninasafiri nao kikazi, ninapata chakula pamoja nao safarini kwa zaidi ya miaka 5. Bado sikushawishika kunywa pombe wala kutenda maovu kama wayatendayo tukiwa safarini. Hadi wengine wakawa wanataka kunilazimisha nifanye kama wao lakini hawakufanikiwa hadi leo. Wanakunywa bia mimi nakunywa maji, soda, maziwa au juisi basi. Wanaendelea kunywa pombe mpaka saa 7 usiku mimi nawaaga zangu naenda kulala ikifika saa 3 usiku tukimaliza kula chakula. Na wananijua wala sibadiliki msimamo wangu. Hata wangefanyaje, hata wafanye ngono mbele ya macho yangu, mimi sibabaiki. Hata wanywe pombe sana, waibe sana wake za watu au mabinti za watu, mimi nawatazama tu. wala siyumbishwi. HUKU NDIKO KUKUA KIIMANI. HUKU NDIKO KUISHI NA WATENDA DHAMBI NA KUWAHUBIRI KWA MATENDO BAADA YA INJILI YA MANENO.

  Kumbuka wewe hupaswi kuniiga kama hujafikia viwango vyangu. Kama ukisikiliza muziki unayumba kiimani, unashauriwa usisikilize kabisa. Kwani ni ishara kwamba wewe bado unakua, yaani wewe ni mchanga kiimani hata kama una miaka 20 tangu umwamini Kristo. Usiishi kwa kufuata mkumbo. Jifunze maandiko ukue.

  Nahitimisha kwa kusema, KUSIKILIZA MUZIKI WOWOTE ULE PASIPO KUYUMBA KIIMANI NA KIROHO, NI ISHARA YA KUKUA KIROHO NA KIIMANI.

 18. My only comments this time——– sometime msiicomplicate saaaaaaaaan mbingu, ndio maana Paul kujua hili aliwasimplifaia wapendwa enzi izo akawaambia….wasiulize ulize e.g. mfano unataka kununua maembe sokoni…huwezi anza kuukiza eti samahami.kaka..kwani haya maembe haya umeyapata wapi? umeyapataje?….ni kwa nji ya Bwanaaa kweli?……..Paul anasema msiulize ulize….ni sawasawa na kusema msifuatilie fuatilie…… maana kama ni ivyo basi mtangulieni mbinguni tutatawakutaga huko wapendwa, hapa hamtapaweza kuishi tena maana kila kona kila saa ni mambo ya duniani tele siyo muziki tu…. Mishahara mnayopokea pesa yote imetoka BOT…. na uko hata wafanyabishara ya madawa ya kulevya na madanguro huweka pesa huku hata viwanda vya bia na sigara huchangia pato kubwa kabisa la Taifa kuzidi nyimbo zetu za upako na bado mpendwa ukilamba mshahara wako au kufanya bisahara na kupata wateja wengine wanakuletea pesa za kutoka kufanya uchangu doa usiku…aaaa unazichukua tu kama kawa na kumuhudumia chai mgahawani kwako …..tena jioni unapohesabu income…unapomoka na kunena kwa ndimi shadarakabokorobosalalalla ukisema asante Bwana kwa kukupa biashara tamu siku iyo…of which ela ya kahaba nayo imechangia na ya sigara plus bia kwa wafanyakazi wanaolipwa na serikali na mashirika ya umma…….hapo vipi… si bora hata ya bongo flava…or atleast SOME bongo flava na muziki mwingine…ndo maana nkasema msikomplicate mbingi maana kama tukifuatilai kila kitu…hapakaliki hapa chini but yet BWANA AMEEONA VEMA TUDUNDE HAPA HAPA.

  By the way, when do we say hii au muziki huu ni wa dunia? because iwe disco, zuku, kwato, blues, chakacha, twist, bolingo, dance nk hizi zote ni music style na can be coded ktk music instruments kama keyboard etc. Je Mtu akitumia style izo au programe izo au rythem izo kutwangia muziki wa mambo ya mbinguni kuna tatizo? ndio maana nauliza when do /can we say this music is dunia and this is mbingu?…..aaa jamaani some time tunacomplicate tu

  Pia si kweli kiiiiiiiiiila ambaye hajaookako akitunga nyimbo na kuimba anapepo au anatumiwa au ametumia nguvu za giza….mmmmmh uwongo tu. Wengine ni kipaji kabisa cha Mungu wala si devo neither vibabu vya bagamoyo…it is.by that God given kipaji cha utunzi…anang’amua burning issues ktk jamii mfano ufisadi, migogoro kazini, kudumisha muungano, mageuzi n.k. then atunga nyimbo kama…. ”nidhamu ya kazi ni msingi wa mafanikio mema kazini eeeee..viongozi na wafanyakazi..lazima wooote tuwe na nidhamu. eeeee..migogoro na migonganoooo… ya kazini ni ukosefu wa nidhamu…by Mlimani Park kama siyo OTTU jaz…. wimbo na utunzi kama huo…pepo iko wapi…majini yako wapi….kuzimu iko wapi hapo? acheni izo. Au Tazama ramani utaona nchi nzuri….lalalalalalalalala Tanzaniaaaa kuna tabu gani kusikiliza? ndo eti itanifanyanyaje kiroho na kumpenda kwangu Yesu na wokovu nilionao?

  Ushauri tu ni kwamba ni kua na kiasi na pia kua selective kusikiliza zipi maana nyingine zimevuka mpaka kwa maneno yake na staili ya uchezaji kama vile baadhi ya nyimbo za dini zilivyozidisha mambo, maneno na uchezaji ambao unaweza hata kutotaka kusikia wala kuziona.

 19. Mpendwa ktk Kristo, Bwana akubariki sana
  Jehovah alimwambia Joshuwa kutafakari sana neno lake yani usiku na mchana ili aweze kufanikiwa katika mission zake, na zaburi yakwanza inatuonyesha mtu anaye tafakari sheria za Bwana usiku na mchana kwamba atafanikiwa katika jambo lolote alifanyalo; sasa tuelewe kwamba mtu anakitafakari kile alico kisikiya. kama Mungu anatuambia tulitafakari neno lake inamaana kwamba yapo mengine tungeweza kutafakari ila matunda si ya kumpendeza Mungu.
  Ukweli ni kwamba ukisikia tu hutajizuia kutafakari na mwisho utajikuta chakula hico ca roho kimeoza. Tafadhari soma “wakolosai 3; 16-17. ubarikiwe sana. From BURUNDI

 20. Bwana Yesu asifiwe wapendwa!!!
  Mmi naona. Kuna nyimbo zingine zina ujumbe katika jamii. Na si kwamba zote ni mbaya!! Ya Mungu mpe Mungu na kaisari Mpe kaisari. God bless you!!!

 21. Tunasikiliza nyimbo ili kupata ni nini hasa mtunzi ama msanii amekusudia kwenye jamii anayoishi.
  Kusikiliza nyimbo za HipHop sio tatizo,bali shida ipo pale unaposikiliza wimbo usio na maadili mazuri kwenye jamii
  Kwa mfano kusikiliza wimbo ambao kiujumla unazungumzia mapenzi tu.Kwa mkiristo aliyeokoka kwelikweli ajuaye Neno la Mungu haimpasi kwani huchochea tamaa za kimwili.
  Lakini kwa nyimbo hizohizo za HipHop au za Kurap kama zina maadili ni nzuri.Tatizo la wakati huu kwa vijana wengi wajiitao wameokoka wanasikiliza nyimbo hizo na KUKARIRI hata kama wimbo hauna maadili wao wanakariri tu na kujaz memory za vichwa na mioyo yao ubatili badala ya Neno la Mungu

 22. Bwana Yesu asifiwe!

  Kuhusu hoja hii, wapendwa naona kuna kutokueleweka vizuri kwa baadhi ya maneno yaliyotumika.

  Kuna tofauti kubwa kati ya kusikia na kusikiliza. Unaweza ukawa unasikia lakini husikilizi. Kusikia ni sehemu katika kusikiliza. Sauti yoyote katika mazingira tunayoishi husikika kama masikio ya mtu ni sawa na yanafanya kazi yake vizuri. Kusikia ni kazi ya sikio la mnyama yoyote akiwamo binadamu. Kunapokuwa na ushirikishwaji wa ubongo kuanza kutafakari kile kinachosikika na hata kuleta mvuto wa mtu kuendelea kutega sikio lake kusikia sauti fulani, huko ndiko kusikiliza. Kusikiliza kunahusisha mwitikio wa ndani ya hisia za mtu kuyatafakari, kukariri na hata kuhifadhi kile kinachosikika.

  Kwa maana hiyo, kusikia si dhambi kwa kuwa huwezi kuzuia kusikia hadi uzibe masikio. Kusikiliza kwaweza kuwa dhambi au makosa kwa mpendwa. Kusikiliza mfano nyimbo za bongofleva au za kidunia kwa mpendwa si sahihi kwa kuwa huko kunadhirisha kabisa mapenzi aliyonayo na mambo ya kidunia. Mtoto wa Mungu hapendezwi na mambo ya dunia. Tayari hayo ni kama matapishi au mavi kama mtume Paulo alivyosema. Hayo ni ya kale, tumekuwa wapya kwa kufanywa upya nafsi zetu kwa kutakaswa kwa Damu Ya Yesu Kristo. Makosa na dhambi ni tofauti ila vyote vyatufanya tufe Kiroho na kuwa wafu kama mwanzo kabla ya wokovu.

  Tukielewa hayo, nadhani tutahitimisha mjadala na kuafiki kwamba kusikiliza nyimbo za bongofleva/ za kidunia ni makosa kwa mtoto wa Mungu. Tunapaswa kugeuka na kuiacha dunia. Tunapaswa kusonga mbele kumfuata Bwana Yesu (Neno) bila kupinda kwenda kushoto au kulia.

  Mungu awabariki!

 23. Shalom ndg Millinga
  pole kwa kushinda njaa! ni kawaida tu sie wafanyakazi, naona tupo pamoja ingawa mleta mada alikiri amepata kitu kwa mafundisho ya mwanzo tuliyoweka hii inadhihirisha nae alimaanisha kule kusikiliza kwa kupenda.
  Nimesoma sana hoja zako, naona unasisitiza “tunapaswa kuona, kusikiliza” mie naona sio sawa na hata kama ikitokea niko naangalia taarifa ya habari matangazo yao yasiyo ya kujenga yakija ni wakati wa kuangalia dinner leo ni nini na kuangalia mambo ambayo sijapata taarifa zake hapo home, kelele za nyumba ya pili, ukumbi wa disco, bar au daladala huwa nazizima kwa aidha kuzama kwenye neno au miziki au gazeti yangu ya injili au kuomba. Ktk ufahamu wangu kwa mbali nitazisikia ila hazina umuhimu wala hazitakaa kichwani mwangu kwani hakuna udongo aina yake wa kuzioteshea!
  Kumbuka Daniel na wenzie walipoomba kila siku ujue kuna taifa zima lilikuwa likiabudu kwa sanamu ya Nebukadneza, sauti ya taifa zima! sijui kama wangesikiliza kwanza na wao wangeweza vipi kuomba. Ikiwa kila mvaa vibaya anayepita mbele yetu tunageuka shingo na kuangalia kwa ufasaha maungo yake nini kitabaki ktk kumbukumbu zetu? Tunapaswa tuwe chumvi na mwanga kwa ulimwengu, sisi tuubadili ulimwengu na sio sisi tubadilishwe na mazingira tuliyomo, ni ngumu lakini inawezekana! nimezunguka Tanzania hii yote isipokuwa mikoa mitatu tu bado, na kwingine hakuna hata mkristo wala kanisa achilia redio au TV ya Kikristo lakini sikumbuki hata TV wala redio zao zinaonyesha nyimbo gani? Tunapoomba usitutie majaribuni, lakini na sie tujiepushe na vishawishi. Barikiwa

 24. Mpendwa Rosemary,

  Swali linauliza hivi, ” Bwana Yesu Asifiwe, Wapendwa naomba kuuliza je kusikiliza nyimbo za Bongo fleva(za kidunia) ni dhambi? Na kwa nini ni dhambi? Naomba jibu lako.

  Awali katika post yangu nimefafanua. Naona wewe hukusoma maelezo yangu ya kwanza katika posti zangu 2 zilizofuatana.

  Hoja hapa ni, JE KUSIKILIZA NYIMBO HIZO ZA BONGO FLEVA NI DHAMBI? Unapaswa uelewe swali kwanza hapa. Neno kiongozi hapa ni “KUSIKILIZA” na neno “NYIMBO ZA BONGOFLEVA”

  Rosemary unapaswa kufafanua hapa maneno haya: “NYIMBO”, “BONGOFLEVA” “KUSIKILIZA”, “DHAMBI” Yaani utuambie ni maana ya “WIMBO/NYIMBO?” Pia utuambie nini maana ya “BONGOFLEVA” , “DHAMBI” na uteleze maana ya “KUSIKILIZA”.

  Ukifafanua hayo ndipo mada nzima itajadilika vizuri bila kupoteza mwelekeo wa mjadala.

  Nimetoa mifano mingi sana kwamba kama unataka usisike mziki wa bongofleva unapaswa kutimiza masharti niliyoyataja katika post yangu hapo awali. Nikatoa mfano wa matumizi ya simu za mkononi kwamba unaweza kumpigia simu mtu ukakutana na muziki wa bongofleva kabla hajapokea simu yako, utaacha kuusikiliza wimbo huo kwa sababu tu ni bongofleva na utakata simu ghafla?

  Mimi naona kwamba tunachanganya mambo hapa. Tuelewane kwamba swali hili kama linataka kutuuliza mapendeleo yetu (Our Hobbies) na swali lingeuliza hivi:, JE KUWA NA UPENZI WA NYIMBO ZISIZOMSIFU MUNGU NI DHAMBI? (Is it a sin for a christian to have hobbies in non-gospel/secular musics?)

  Kama swali lingeuliza hivyo mimi ningejibu haraka kabisa: NI DHAMBI. Lakini unaponiuliza nitoe maoni yangu kuhusu “KUSIKILIZA” mimi nitakwambia kwamba SIYO DHAMBI” kwa sababu kila siku iendayo kwa Mungu utasikia muziki wa bongofleva upende au usipende.

  Unaweza kuzisikiliza nyimbo hata za dini lakini ukawa “HUZIPENDI”. Je, mtu akiuliza swali, “KUTOZIPENDA NYIMBO ZA INJILI NI DHAMBI” Utamjibuje ikiwa kuna nyimbo za Injili ambazo huzipendi. Siyo kila wimbo wa Injili utausikiliza wala kuupenda kila uimbwapo. Ndivyo ilivyo pia hata kwa nyimbo zisizomsifu Mungu.

  Kusikiliza BONGOFLEVA unapaswa kuzisikiliza lakini hupaswi “KUZIPENDA” . Ni kama kusema, “AMTAZAMAYE MWANAMKE KWA KUMTAMANI”. Maandiko hapa hayatuzii kuwatazama wanawake. Unapaswa kumtazama mwanamke lakini ukiingiza KUMTAMANI a.k. a KUMPENDA KWA AJILI YA NGONO, Hapo ndipo umekwishazini naye.

  Hata nyimbo zisizomsifu Mungu unapaswa kuzisikiliza siyo kwa kuzitamani. Huku ndiko kukua kiroho. Kama unaweza kumtazama mwanamke pasipo kumtamani hata angekuwa amekaa vibaya au amevaa nguo fupi au yuko anaoga peke yake naa wewe ukamwona uchi wake lakini usimtamani wala kusisimka viungo vyako na kuanza kuwaza jinsi ungefurahi kuwa naye kimapenzi, HUKU NDIKO KUKUA KIROHO.

  Kipimo cha kukua kiroho ni vile unavyoweza kustahimili kuzungukwa na mambo yasiyokuwa ya Mungu bila wewe kutenda dhambi. Aidha, kipimo cha uchanga wa kiroho ni vile mtu anavyoshindwa kujizuia kuanguka dhambini pindi tu anapozungukwa na watenda dhambi kila kona. Yaani kila kona ni bongofleva, pombe, zinaa, ulaghai, wizi, rushwa, uongo, umbea, nk. lakini wewe hutetereki wala kuyumba. Hivi ndivyo akina Daniel, Meshack, Abdenego walivyoishi na wakaitwa vijana waliobadilisha ulimwengu wao. Kuna wapendwa wengi leo wako kama Rosemary wanadhani kujitenga na watu au “manyimbo mabaya” kwa kutosikiliza kabisa ndipo watauteka ulimwengu. Mhhhuuuuu, sijui bwana, labda.

  Rosemary mimi naomba niishie hapa kwa leo, niende nyumbani kula nina njaa sijala tangu asubuhi.

 25. Bwana Yesu asifiwe!

  Kwanza kabisa, swali hili ni zuri sana na linahitaji mjadala wa kina zaidi. Wapendwa tunaishi katika dunia yenye mambo mengi mno, mazuri na mabaya kulingana na msimamo ambao mtu ameamua kuufuata.

  Katika kitabucha 1Timotheo 1: 4, Paulo anamkataza Timotheo asiangalie hadithi na nasaba zisizo na ukomo, ziletazo maswali na si madaraka ya Mungu yaliyo katika imani.
  Pia Zaburi 1:1 inatukataza kama wapendwa kwenda katika shauri la wasio haki. Wala kusimama katika njia ya wakosaji.
  Wapendwa, maisha tuliyochagua si lelemama. Ni maisha ya kujikana na kumfuata Bwana Yesu Kristo. Si sisi tena tuishio, bali Kristo ndiye anayeishi ndani mwetu( maishani mwetu). Tunatimiza mapenzi yake yeye wala si yetu, tunatimiza makusudi yake wala si yetu. Mapenzi ya Mungu na Makusudi ya Mungu ya kutuumba sisi yako wazi katika Neno lake. Neno la Mungu ndio taa ya maisha yetu. Humo kuna uzima wa Nafsi, Roho na Miili yetu. Kuna utakaso na ukombozi humohumo.

  Sasa, kama kusikiliza nyimbo za kidunia kunakusogeza karibu na Mungu, ambayo si kweli, unaweza kusikiliza! Swali Gumu ni kwamba, Je wale wanaoimba ni wenzako katika safari ya kwenda Mbinguni! Wanaye Yesu kama wewe? Nijuavyo mimi na ndiyo imani yangu, waimba nyimbo za dunia hawamtukuzi Mungu. Hata kama kuna maneno yanayomtaja Mungu, haimaanishi wanaweza kuwa na maneno yenye maana kwa mpendwa, mtu aliyeokoka. Waimbaji wanaitwa wa “Nyimbo za Kidunia” Dunia inatawaliwa na shetani (ibilisi). Hivyo wanamsifu ibilisi.
  Mimi nakushauri mpendwa, kama umeamua kumfuata Yesu katika maisha yako, epuka mambo ya dunia, kuchanganya changanya na kujifariji kwamba uko sawa. Usije ukakutwa na kiama ukiwa vuguvugu. Utatapikwa kwenda kwenye ziwa la Moto ambamo utalia na kusaga meno. Penda kusoma neno, sikiliza nyimbo halisi za injili, shiriki kanisani, fanya maombi na maombezi, uwe na marafiki waliookoka kweli kweli n.k
  Ukifanya hayo, utatawala mwili upendao dunia na upendo wa Mungu kwako na wewe kumpenda Mungu kutathibitika.
  Mungu akubariki sana, huo ni ukweli halisi. Nuru haichangamani na giza!

 26. Shalom ndg Millinga naomba rudia swali: kusikiliza nyimbo za dunia haifai kwa Mkristo?
  mleta hoja anapouliza hivi ina maana anaouchaguzi kuacha au kusikiliza (its a matter of choice) vinginevyo asingeuliza
  Suala kwamba tunaepinga ni wanafiki sio kweli tumefafanua kuwa tunakutana nazo kila leo kwani bado tupo ulimwenguni…ndio maana Yesu alisema kiingiacho sio haramu bali kile kiutokacho moyo wa mtu.
  kitu muhimu hapa ni ule uamuzi wa kuamua kusikiliza hizi nyimbo wewe mwenyewe pasipo kulazimishwa…ile dhamira ya kutaka kusikiliza toka rohoni mwako nadhani hata mleta hoja aligundua kusutwa na kuona sio sawa (kwa yeyote mwenye Roho mt)
  kwamba unavutwa kila mara kusilikiza hizi tu basi ni tatizo na ndg John Paul amesema mtu wa hivyo ujikague…pia tumejaribu kuweka wazi zile ambazo ni muhimu au zina maana ktk maisha yetu haya hata kama sio Gospel. Kaka Sungura kama hata ktk “kanisa’ lako mnasikiliza nyimbo za R Kelly sio vibaya maana mie hata sizijui ila tu imetokea nilisoma kuhusu kesi yake….
  Mbarikiwe wote

 27. Bongo fleva? Acheni UNAFIKI, KILA MKRISTO ANAZISIKILIZA.

  Kusema kweli kama ukitaka kutosikiliza nyimbo za Bongo fleva fanya yafuatayo:

  1. Usipande daladala yoyote uwapo miji mikubwa yenye kutumia usafiri wa mabasi maarufu kama daladala.

  2. Usipande mabasi yaendayo kokote hapa nchini, bali utembee kwa mguu kila unakoenda, au utumie usafiri wako binafsi na uweke kanda ya Rose Mhando au Bonny Mwaitege, au Upendo Nkone, nk.

  3. Usinunue TV nyumbani kwako, na endapo utanunua uwaombe mafundi wa TV waifunge TV yako isioneshe vituo vya ITV, TBC1, TBC2, CHN 5, CHN 10, Bali ioneshe vituo vya dini tu tena dini za kilokole peke yake kwani kama itakuwa chini ya kanisa la RC Bongofleva ni kama kawa.

  4. Usinunue Radio kabisaa yenye kusikika vituo vya redio za hapa nchini labda uwe miji yenye redio za kilokole tu. Miji kama Kigoma, Rukwa, Kagera, nk hakuna redio wala TV za kilokole sijui itakuwaje? Wapendwa wa huko poleni sana, mtaikosa mbingu? Shauri yenu!

  5. Usiangalie maigizo ya akina Kanumba wala michezo yoyote ya kuigiza kwani nayo yamejaa bongofleva hata maigizo yenyewe yanaitwa, “Bongo movies”.

  6. Usisikilize taarifa ya habari Wala kuangalia kipindi chochote cha TV wala redio. Utashitukia katikati ya matangazo au taarifa ya habari imetumbukizwa bongofleva, mara tangazo la COCA COLA, Mara Vodacom, mara Tigo, nk.

  7. Usikae nyumba ya kupanga pamoja na wasiookoka. Jenga nyumba ya kwako, tena mbali na watu kabisa kwani huyu atafungulia redio sauti ya juu ili na wewe usikie burudani za bongofleva au TAARAABU ziungurumapo hasa ifikapo alasili mjini Dar, redio zote za FM huweka nyimbo za bongo fleva au taarabu.

  8. Usinunue wala kutumia simu ya mkononi kwani ukimpigia mtu asiyeokoka utakutana na muziki wa bongo fleva, tena utausikiliza hadi atakapopokea simu yako. Utasikiliza bongofleva weeeeeee hadi simu ikipokelewa. Dawa ni kutotumia simu za mkononi, turudi kutumia zile za TTCL ambazo nyingi hawaweki bongofleva sana sana utakutana na tu na muziki wa ala bila maneno.

  Hivyo ndivyo unaweza kufanya ili kuepuka kusikiliza nyimbo hizo unazoziita za kidunia kama zipo.

  Je, kuna mkristo yuko safi hapa? Ukitaka kuwa msafi kwa kuepuka kusikiliza nyimbo za kidunia fanya hivyo.

  Naomba mimi nisiwe miongoni mwa wanaojifanya wameshaondoka dunia na sasa wako mbinguni na nikiri na kutamka kwamba nitaendelea kusikiliza nyimbo za bongo fleva hadi mwisho wa dunia, YES hadi tukiwa paradiso ya mbinguni ambako huko hatutasikia bongofleva tena milele.

 28. Wapendwa,

  Swali linauliza hivi, ” Bwana Yesu Asifiwe, Wapendwa naomba kuuliza je kusikiliza nyimbo za Bongo fleva(za kidunia) ni dhambi? Na kwa nini ni dhambi? Naomba jibu lako.

  Naomba wale wote wanaojibu swali hili wato hoja za kutosha. Swala la kujibu kama maswali ya darasa la Saba ; NDIYO / HAPANA, imepitwa na wakati. Wapendwa toeni maelezo yenye hoja za kutosha kumshawishi mpendwa asiendelee au aendelee kuzisikiliza nyimbo hizo.

  Kuna maswali ya kujiuliza ili kujenga hoja pana zenye mashiko kimaandiko na kiimani katika mjadala huu: Maswali ni haya hapa ukiyajibu ndipo utakuwa umejenga hoja za kutosha:

  1. Wapendwa wanawezaje kuepuka mambo ya kidunia wakati wako duniani?

  2. Mambo ya kidunia maana yake ni ipi? Toa mifano ya mambo ya kidunia?

  3. Kama nyimbo za “Bongo Flavour” ni za kidunia za kimbingu zi ni zipi? Taja hata nyimbo tano tu za kimbingu amabzo siyo za kidunia na ueleze kwa nini siyo za kidunia.

  4. Je, Wapendwa wamezuiliwa na Maandiko kupenda vitu vya kidunia ikiwemo bongo flavour songs?

  5. Kama ni NDIYO wamezuiliwa kupenda nyimbo za kidunia mbona wanaimba nyimbo makanisani kwa kutumia vyombo vya kidunia? Au drums, Guitar, Keyboards, filimbi, zeze, malimba, vipaza sauiti, Microphones, nk. siyo vitu vya kidunia?

  6. Je, mavazi wavaayo wapendwa, nyumba waishizo wapendwa, magari, mabaiskeli, mapikipiki, ndege, treni, meli, nk. wanayotumia siyo mambo ya kidunia? Kama ni ya kidunia mbona wakristo huyatumia tena sana?

  7. Kinachofanya jambo au wimbo au kitu kuitwa cha kidunia nini? Sifa ya kuitwa , “…… a – dunia…. ni ipi?

  8. Kuzipenda au kuzisikiliza nyimbo za Bongofleva ni kipi kimekatazwa na maandiko. Je, Kupenda nyimbo au kusikiliza nyimbo hizo ndilo swali kuu katika mjadala huu? Eleza kwa kina au Tofautisha maana ya KUPENDA NYIMBO ZA BONGOFLEVA na KUSIKILIZA NYIMBO ZA BONGOFLEVA. Mkristo mtiifu wa maandiko achague kipi? Kutozipenda au Kutozisikiliza?

 29. sungura usiangalie kwa nje na kucomment kwamba ndoa za wasiookoka zina amani sana, mambo ya ndoa ndani anayajua mtu binafsi, watu huwa hawasemi tu. hii mada ni pana sana kuzungumzia labda Mungu akitupa neema.

 30. Ngoja nifafanue tena labda nitaeleweka vyema zaidi.
  Tukumbuke kuna ndoa za wasiookoka ambazo hazina matatizo yoyote,lakini hawa watu ki msingi wala hawana upendo wa Agape ndani yao, kwa nini? Ni kwa sababu upendo wa ndoa nimesema sio wa agape pekee,bali ni ule ambao unaitwa fileo, ni upendo ambao lazima una mahaba ndani yake. Usipokuwa na mahaba kwa mwenzuio wako huwezi kumpenda ki ndoaila utampenda tu kama ambavyo unampenda mtu yeyote.

  Grace kinachokufanya umpende mumeo mpaka kiasi cha kuwa na wivu sio upendo wa kristo, maana kama ingekuwa hivyo hata shemeji yako ungemwonea wivu maana pia unampenda kwa upendo wa kristo/agape.

  Kwa hiyo upendo wa kristo ni upendo ambao aina nyingine zote za upendo ziko ndani yake, kwa mtu ambaye anamwamini Yesu kristo. Kama utawaza kwamba nimeupuuza upendo wa kristo utakuwa hujanielewa kabisa.

  Kama ndoa ingekuwa inasimama just kwa sababu tuna upendo wa Agape pekee basi ndoa zote za wasiookoka zingekuwa zimejaa matatizo. Na kama ndoa ingekuwa inasimama tu kwa sababu mtu ana upendo wa Agape pekee basi kusingekuwa na ndoa za wapendwa na watumishi wa Mungu zenye matatizo.

  Ukiacha kumwonyesha upendo wa mapenzi/ mahaba mwenzi wako ukamwonyesha tu upendo wa Agape lazima ndoa yako itapatwa na shida.
  Ubarikiwe.

 31. sungura unaposema upendo ktk kristo hauwezi shikilia ndoa yako, naona unakosea sana na Mungu aturehemu, bila Yesu kristo kwa upendo wake kushikilia ndoa yako mtagombana, mtafarakana, mtatengana ,mtaachana, mtasalitiana na mkeo tu, upendo wa Yesu kristo wa kuimwaga damu msalabani ndo wa thamani sana na (ndo upendo huo) maana damu yake iliyomwagika inanena mema hata sasa maeneo mbalimbali mfano ndoa, kazi biashara n.k kama utaitumia.
  mimi binafsi naithamini damu ya Yesu sana na inafanya kazi kweli kwenye ndoa yangu na maeneo yote ninapoitumia, kama ulikuwa huoni uthamani wake basi itumie damu ya Yesu huharibu magomvi, mafarakano, makahaba wasiguse ndoa yako. sio kutegemea nyimbo za mapenzi zitaboresha na kutatua tatizo kwenye mahusiano
  kuhusu nyimbo za kidunia kwa kweli hazifai kwa mtu alieokoka, maana imeandikwa kimjazacho mtu ndicho kimtokacho.
  mbarikiwe sana

 32. Rosemary sina uhakika kama nimekuelewa na sina uhakika kama wewe umeielewa comment yangu hapo juu.
  Niliuliza maswali kadhaa hapo juu ila jujajibu hata moja, mojawapo lilikuwa ni je wimbo fulani ni wa kidunia kwa sababu umeimbwa na asiyeokoka au kwa sababu hauna ujumbe wa kibiblia?

  Na kama ni kwa sababu aliyeimba hajaokoka, nikasema inakuwaje wimbo wa storm is over version ya R. Kelly inatumika sana makanisani?
  Ndoa yangu katika kristo imeshikiliwa na nini?

  Upendo katika kristo hauwezi kushikilia ndoa ikawa kamili, maana upendo huo ni wa agape ambao unampenda nao mtu yeyote, lakini upendo kwa mke wangu lazima uwe fileo(kama sijakosea) kwa sababu lazima uwe na mahaba ndani yake.

  Kumpenda mwenzi wako kwa upendo wa kristo (Agape) pekee kutafanya ndoa iyumbe kwa sababu uhusiano wa wanandoa lazima uwe na mahaba ndani yake.
  Rose sio kila kitu kiwe muhimili wa injili ili kujua kuwa ni cha muhimu, yako mambo mengi sana tuanayafanya hapa duniani ambayo hayana muunganiko wa moja kwa moja na injili. Ndio maana Yesu akasema ya Kaisari mpe Kaisari na ya Mungu mpe Mungu.

  Mimi huwa nasikiliza nyimbo za secular japo si kila wimbo, huwa nachagua kinachonifaa. Huyo ni mimi!!
  Ubarikiwe.

 33. Shalom ndg Sungura
  labda nikuulize nawe ktk kitabu cha mithali kuna mistari inyoelezea malaya, inayoelezea mtu kutulia na mkewe, mke mwema, ktk biblia kuna maelezo ya ndoa sehemu nyingi, kuna ubakaji, wizi ulawiti vyote hivyo vimo ktk Biblia.
  Vile vile kuna matendo mema, kuna kuabudu, kusifu, kuonya, kukufuru nk
  Sisi agizo tulilopewa ni nendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi wangu…hili ni agizo la kwanza baada ya kupewa Roho mt na agizo la mwisho kwa wanafunzi wake baada ya kufufuka.
  Najua mapenzi na mengineyo ni sehemu ya maisha yetu ya kimwili hapa duniani ila sio muhimili wa Injili na kwasababu hiyo yana sehemu ndogo ktk kumfanya mtu kuingia ufalme wa Mungu, pili hayo unayosema mapenzi na hizo nyimbo ulizotaja si ktk mpango wa Mungu:
  Unafahamu kuwa R. Kelly alishitakiwa kwa kesi ya kubaka vitoto vidogo, je unaelewa wakati anaimba hizo nyimbo alikuwa anamaanisha nani mpenzi wake? si hivyo vitoto vidogo? unaelewa mtu akisikiliza sana na anamfanya huyu mtu kuwa “role model” wake? ndio maana tunasema shetani anazitumia hizi nyimbo kuwaingiza watu dhambini. umeambiwa ujazwe Roho mt wewe unasisitiza kujazwa blues na nyinginezo za mapenzi kwa kigezo tu cha wewe na ndoa yako. Je ndoa yako imeshikiliwa na nini? upendo wa kimwili (umbo sura ufanisi wa mapenzi nk) au upendo safi ndani ya Kristo?
  na je hayo yanayoimbwa ni jinsi ya kutenda mambo ya sirini, je yawe wazi hata kwa watoto ambao hawajakua kupambanua lipi jema na lipi baya? wewe unafanya haya ya sirini mbele ya kadamnasi? iweje kushabikia mtu anayeimba hayo mapenzi hadharani akiwaharibu watoto na kuwahamasisha vijana wasio na ndoa.
  Rudia tena wimbo ulio bora kila baada ya mistari anakuasa “….usiyachochee mapenzi kabla ya wakati wake…” ulielewa nini hapo? Ubarikiwe sana

 34. Kama wachangiaji wengi walivyochangia na kunifundisha mengi naona wametaja Bongo Fleva kama kikundi cha nyimbo za kidunia. Hapa pia nina swali moja tu la kimsingi ni zipi za kidunia na zipi zisizo za kidunia? Je tuna nafasi ya kumwuliza Mungu wetu aliyetuumba sote swali hili na kumwomba atujibu? Ninajua ya kwamba Sprituals ni nyimbo ambazo zimetokana na watu ambao hawakuwa Wakristo bali walikuwa na nyimbo zao za kitamadumi ambazo baadaye walizitumia katika ibada wakati wa kumtukuza Mungu. “Kum baya my Lord” ni moja ya hizo. Ninamkumbuka Mzee Makasi wakati wa enzi zake kwenye nyimbo zilizokuwa si za kanisani alifundisha wengi katika jamii, Hayati Dr Lemi katika jamii alielezee kuhusu kifo na kutufahamisha juu ya uwezo wake. Dhamiri yako katika kusikiliza nyimbo ambazo si Kanisani ndiyo ambayo itakusuta kwanini unashawishika kusilkiliza: maana hata Wimbo ulio Bora wa Sulemani ambao umo katika Biblia waweza kuutumia isivyo. Ushauri wangu ni kwamba kama unaona una udhaifu wa klusikiliza basi usijinjgize katika hili.

 35. SIO DHAMBI!!!!
  Naamini wachangiaji wengi si wachanga kiroho.Lakininashawishika kuamini kuwa mtume Paul angesoma michango yetu mingi angetuambia tujapopaswa kuwa walimu kulingana na umri wetu wa kumjua Bwana kumbe bado tunahitaji mafundisho ya kwanza kabisa ya neno la Mungu,yaani maziwa na chakula kigumu au mifupa wengi wetu hatujakiweza bado.

  Ivi kule Kana ya Galilaya ambako Yesu alihudhuria harusi,mbaya zaidi akawatengenezea na pombe hao watu walikuwa wanasikiliza au wanapiga nyimbo za namna gani, ulishawahi kujiuliza?
  Ivi nyimbo tunazosema za kidunia ni za kidunia kwa sababu zimeimbwa na asiyeokoka au kwa sababu ya ujumbe wake (hasa mapenzi), au?.
  Ndio maana kwenye harusi za wapendwa tunapigiwa nyimbo za nibebe na njoo ufanyiwe maombi.

  Sasa sisi wapendwa ambao tunasema kusikiliza bongo fleva ni dhambi tulijuaje kama kuna bongo fleva kama hatukuisiliza? Sio wanafiki kweli sisi?
  Ya Kaisari mpeni Kaisari ya Mungu mpeni Mungu. Hata nyimbo zinazoitwa za kiroho uwe makini sana unapozikiliza maana si zote zifaazo.

  Hata tunazoziita za kidunia (secular songs) uwe makini unapoacha kuzisikiliza maana si zote hazifai.Katika nyimbo zote hizi (za dini na zisizo za dini) kuna zinazofaa kusikilizwa na sisizofaa.

  Mapenzi yanayoimbwa na dunia mara nyingi ni yaleyale ya wapendwa pia,tusidanganyane mapenzi yetu wapendwa si ya kiroho bali kimwili tu kama wengine. Tatizo la waimbaji hao wasiojua Mungu huabudu wapenzi wao kwa sababu mioyo yao iko tupu.
  Hebu niambie ubaya wa nyimbo hizi:
  1. One Love – Bob Marley
  2. Storm is over – R.Kelly version
  3.Nimekuchaga wewe uwe wangu – Bob Ludala
  4.Will always love u -Whitney Houston

  Nashauri hivi ukiwa katika hali ya mahaba na mkeo/mmeo(mpenzi) sikiliza wimbo wa mapenzi usilazimishe kusikiliza njoo ufanyiwe maombi, ukiwa katika kazi ya uanaharakati sikiliza One love n.k

  Namaliza hivi:
  “Ivi Wimbo ulio bora Suleman alikuwa anamwimbia nani, mbona umejaa maneno ya mahaba?”

 36. Wapendwa nimebarikiwa sana na mawazo yenu kwa wote mulio changia’ kitu nilichojifunza ni kwamba MOYO WAMTU NIKAMA MTOTO MCHANGA(MTOTO UMLEAVYO NDIYO AKUAVYO) kwahiyo tukiulea moyo wetu vizuri utakua vizuri na tukiulea vibaya(kwakusikiliza nyimbo za kimwili) itatupelekea kutenda dhambi hiko ndicho nilicho jifunza kutokana na swali nililo uliza. Mubarikiwe wote.

 37. Kuna kusikiliza na kuna kusikia…kusikia sio dhambi tunasafiri kwenye mabasi zinapigwa nyimbo mbalimbali…pia hata kama ukisikiliza mimi nadhani swala zima nineno KIASI. Kunawahubiri wanatoa mifano wakiwa madhabahuni ya nyimbo hizo na wanafikisha ujumbe vzr tu kwa waumini…pia lazima tujue definition ya dhambi…siwakati wote tendo fulani linaweza kuwa dhambi..likifanywa kwa wakati muafaka na katika sehemu muafaka hakliwezi kuwa dhambi…KIASI..KIASI..then msikilize roho anakuambia nini wakati huo unaposikiliza

 38. Mimi naona si vema mtu unayemcha Mungu kusikiza nyimbo za bongo fleva. Kwa kama mkristo una mambo mengi ya kufanya yamhusuyo Mungu kama kuomba, kuangalia wagonjwa, wajane na yatima haya mambo ndiyo yanayompasa mkristo kufanya na kusikiza Neno la Mungu ambalo ndiyo taa ya miguu yetu hutuongoza popote tunapokwenda na ndilo linahitajika likae kwa wingi katika Mioyo yetu ili tusimtende Mungu dhambi. Achana na Bongo Fleva haimpi Mungu utukufu kwanza nyimbo zake hazina heshima kwa kucheza hata utunzi wake haumtukuzi Mungu humtukuza shetani na kwa jumla mazingira ya nyimbo hizo zinauwepo wa kishetani.
  Nashauri achana nazo.
  betty kipala.

 39. Kutokana na uzoefu wangu mdogo, Kile anachopenda kusikiliza mtu ndivyo mtu huyo alivyo au atakavyokuwa!

  Malengo mawili makubwa ya nyimbo za kidunia ni Kuburudisha na Kuelimsha jamii. Mambo haya yanakwenda pamoja. Malengo haya hufanyika pia kwa Namna ya “Kidunia”.

  Ziko nyimbo za kidunia, ambazo kwa lugha sahihi twaweza ziita “za kimwili” ambazo zinahusiana na mambo ya kimwili, kwa kila mwenye mwili. Nyimbo hizo ni kama ambazo dada Rose amezitaja. Kusema kweli hizo ni sawa tu na kusoma gazeti au kusikiliza taarifa ya habari ili kufahamu mambo mbali mbali yanavyoendelea duniani.

  Tatizo kuwa lililoko sasa ni kuwa tuko katika nyakati mbovu sana. Nyimbo nyingi sana za kidunia zinaendana na mambo ya uasherati. Inashagaza sana kwa kuwa kuna station za redio kama hapa Tz, unaweza kukuta kwa wiki nzima wakapiga nyimbo za “mapenzi” tu. Na mapenzi yenyewe ni kwa namna ya kiduni pia wala si kwa namna ya kimungu.

  Nifupishe tu kwa kusema hivi:

  Kusikiliza Nyimbo za kidunia, zinazohosu mambo ya kidunia, yaliyo kinyume na Neno la Mungu, SIYO dhambi BALI NI KIELELEZO CHA MTU ANAYESIKILIZA ALIVYO! Naweza kusema kuwa Mtu MWENYE DHAMBI ndiye ANAWEZA KUSHAWISHIKA/KUFURAHIA kusikiliza nyimbo hizo!

  Kwa hiyo ndg Theodory Constantine ukiona unavutika kusikiliza nyimbo hizo, JICHUNGUZE sana moyoni mwako, maana hiyo ni dalili kuwa HAUKO SALAMA MOYONI!

 40. kusema ukweli nimejua zaidi ya kile nilichokuwa ninajua kuhusu hizi nyimbo kwasababu mimi sio mtu wa kwenda kwenye hayo matamasha ya hao wanoimba hizo nyimbo ila ni kwamba sikuwa nikiwaza kuwa kusikiliza kunaweza kuwa ni dhambi. Na nimekuwa convinced kwasababu kuna mtu ameongelea kuhusu moyo “kile unachokijenga moyoni ndicho utakachokuwa nacho” sina jingine kwasababu huo ni ushauri ambao naona umebeba maana yote ya kile ambacho nilikuwa nahitaji kujua. Asanteni wapemdwa

 41. kusikiliza sio dhambi,ila kuna vishawishi katika hizi nyimbo,ila ukiwa mkristo simamia mkristo,mimi napenda sana gospel na zinanichukulia sana muda kuliko ya dunia.napenda sana miziki ya Don moen

 42. Nakubaliana na wewe Ebenezer kwani hata Yesu alisema hawezi kututoa ulimwenguni…. hata nami ninakutana nazo hizo nyimbo na pia hata magazeti vitabu nk kwani tunaenenda kimwili ili tule tufanye kazi tuzalishe ili tuweze kutumika. Linachokosolewa ni mtu pasipo haja yoyote unakwenda kusikiliza miziki ya kidunia nadhani hata muulizaji anaelewa kuwa hizi ni zile nyimbo za sijui mapenzi, majigambo, mipasho kutiana moyo kwa namna ya kidunia na sidhani ni za kupigania tuseme haki, kupinga rushwa, kilimo kwanza, kupinga umaskini sidhani….mara nyingi zinazoitwa za kidunia unakuta hata ujumbe wa maana hamna lugha chafu nk. Kikubwa ni wewe uangalie unjaza nini moyoni mwako ukijaza kilimo kwanza, mapenzi, pesa sio ajabu ukamwacha Mungu mradi tu ufanikiwe uko!

 43. Shallom, ni kweli si kila wimbo wa kidunia una ujumbe mbaya kuna za kuamasisha kilimo, kutunza mazingira, na nyinginezo nyingi lakini asilimia kubwa ya hizi nyimbo hazifai kwa kusikilizwa na wacha Mungu.

 44. Shalom wapendwa,

  Unajua si kila kitu lazima kiwe dhambi ili usikifanye. Unajua kadiri unavyokua na kiu yako kumtafuta Mungu kuna vitu vingine automatically hauna kiu navyo. Mie binafsi wala sinaa hata hamu kuzisikiliza, si kwamba ni dhambi…La hasha ila sioni faida zake kwangu……Watu wanoziimba wenyewe hawafanyi hayo maadili coz bila Yesu vitu vingi ni artificial. Hata bila kuokoka watu wanajua kipi ni dhambi au si dhambi ila hakuna nguvu inayowawezesha kushinda au kutumainia kushinda.

  1 Cor 6;12‘‘Vitu vyote ni halali kwangu,’’ lakini si vitu vyote vyenye faida.

  Swali kuu la kujiuliza katika tuyayofanya.

  1) Je hiki ninachofanya kinaongeza kumjua Mungu au uhusiano wangu na Mungu?

  2) Hiki ninachofanya kinaleta utukufu kwa Mungu?

  3) Hiki ninachokifanya kitanisaidia kuwasaidia wengine kiroho?

  Ila si kwamba tunafanikiwa kulifikia siku moja. Ni process na kila siku tutamani kukua zaidi kiroho, kumjua Mungu zaidi, kumpenda na kutafuta kufanana na Yesu. Kiu nyingine zitaondoka tu.

  Mbarikiwe
  Dada Imani Kapinga

 45. Bwana Yesu apewe sifa wapendwa.

  Mimi husikiliza nyimbo za watu ambao hawajaokoka na hasa unakuta anaimba kitu ambacho kinaweza kuisaidia jamii. Kuna nyimbo zenye ujumbe ambao hata watu waliookoka wanaweza wasiupate kanisani au kwenye mahubiri na pia niseme tu kuwa kuna nyimbo za watu waliookoka ambazo siwezi kusikiliza kwa sababu ni za kuburudihsa kuliko kuelimisha, kufundisha au kukemea.

  Kuna kundi fulani liliimba (najua hiki kisehemu tu huko kwingine sijui) ‘ Kwani wao wameweza wana nini na sisi tushindwe tuna nini” mimi hapa hunitoi hata kama ni mvuta bangi aliimba kwani kuna ujumbe unaweza kunipeleka mbali sana.

  Mtu mwingine Michael Jackson aliimba kuhusu “Unity”, wagosi wa kaya waliimba kuhusu Rushwa, nk. Naweza kusikiliza lakini sio wimbo wote. KWA HIYO KUSIKILIZA NYIMBO ZA KIDUNIA SI DHAMBI INATEGEMEA WEWE UNA KUSUDI GANI LA KUUSIKILIZA.

  Hayo ni mawazo yangu tu, na Mungu awabariki.

 46. Zaburi 1: 1 Heri mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha.

  sijui ndugu unafaidika nini kwa ujumbe zao? ukiishasikiliza itakuwa sio vibaya kucheza kwa namna yao, kisha kwenda kucheza nao kabisa, halafu itakuwa kuna haja gani kutofanya wafanyavyo pia (ulevi, uzinzi nk)?
  1. tamaa huzaa dhambi kisha mauti ya kiroho…
  2. unatakiwa neno la Mungu ndio lijae kwa wingi ndani yako…,
  3. utafakari yale tu uliyofundishwa (Biblia)….
  4. ukae na Mungu karibu na kumpinga shetani naye atakukimbia….
  5. mwisho unatakiwa kuzaa matunda, je utazaa nini bongo fleva?
  Tafakari chukua hatua!

 47. mimi naongezea tu Ili nikupe msisitizo zaidi, soma Mithali 4:23 LINDA SANA MOYO WAKO KULIKO VITU VYOTE ULINDAVYO MAANA HUKO NDIKO ZITOKAKO CHEMCHEMI ZA UZIMA.. Moyo unamilango mlango wa kwanza ni MASIKIO(Kusikia) na mlango wa pili ni MACHO (kuona na kusoma). MASIKIO ukisikiliza chochote nje ya Kristo imani yako inayumba,kwa masikio tumeruhusu YESU kukaa ndani yetu,kwa masikio tumeruhusu hofu,mashaka na kila aina ya takataka za shetani hadi zimetutenga mbali na YESU.
  JIULIZE KWANINI UKISIKIA KITU NAFSI YAKO INADAKA(haijalishi kizuri au kibaya?) JIEPUSHE NA UNAVYOSIKIA.NYIMBO ZA DINI SAIZI ZIPO KILA ENEO

  kwa MACHO, tumesoma na kuona ndiyo maana ukiona na kupendezwa nacho ulichoona unavutwa na hicho..kwanini watu walimwiga TEMBEA YAKE JOTI, jiulize kuna uhusiano gani kati ya kuona na mwili wako.

  wafikishie na wengine

 48. Wapendwa bwana asifiwe ahsanteni xana kwa mawazo yenu na mafundisho yenu nimewaelewa vizuri xana xaxa nimeamua kujiepusha kusikiliza hizo nyimbo.MUNGU AWABARIKI SANA.

 49. Mpendwa nafsi huwa inalishwa, i wish ungepata mafundisho ya nafsi through Radio safina, ukiilisha nafsi yako mambo ya dunia ndicho kitakachokujaa moyo ww km umeokoka badala ya kujaa roho na sifa za Bwn utajaa yale ya dunia, me maoni yangu HAIFAI.

 50. Mpendwa katika Bwana nyimbo zote tunazozisikia zikiimbwa na watu wa Mungu au watu wa dunia lazima zina utukufu kwa aliyekusudiwa. Mara zote wimbo unamtukuza Mungu au shetani. Ukitaka kujua ubaya wa nyimbo za Bongo fleva(za kidunia) angalia filamu zake na hutauliza zinampa nani utukufu kwani ni dhahiri mtunzi hakukusudia kabisa kumpa Mungu utukufu bali shetani. Angalia hata jinsi uvaaji na unenguaji/uchezaji. Sasa basi kwa kusikiliza nyimbo hizo kwa kukusudia (yaani kuweka wimbo wewe mwenyewe kwa lengo la wewe kujiburudisha) ni dhahiri kwamba unaungana na hao watunzi kumpa shetani utukufu. Hazifai tuziepuke, hazimtukuzi Mungu. Neno la Mungu linasema ” jiepushe na maneno yasiyo na maana ambayo si ya dini kwa kuwa wataendelea zaidi katika maovu” 2Tim 2:16.

  Mungu awabariki

 51. biblia inasema imani chanzo chake ni kusikia na kusikia huja kwa neno la kristo, kwa hiyo ukisikia kinyume na neno la kristo itajengeka imani ya bongo flava maana ndicho unacho kisikiliza ! N pia mtume Paulo alisema kila kitu ni kizuri lakini si vyote vifaavyo, ukiwa ni mtu uliejawa RohoMtakatifu hutataka kutumia hata dk 1 kusikiliza huo upuuzi!

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s