Sababu za wakristo kuabudu Jumapili

Siku ya JUMAPILI, ambayo ndiyo siku ya kwanza ya juma, SIKU YA BWANA aliyoshinda mauti na kufufuka [UFUNUO1:10] Tunaitenga maalum kumwabudu Bwana kwa sababu:-

a) Ni sikukuu ya malimbuko ya mavuno ambayo ilifanywa katika Agano la Kale, SIKU YA PILI baada ya Sabato; Ikiwa ni utabiri wa Kristo ambao ni LIMBUKO lao waliolala [WALAWI23:9-14;1WAKORINTHO15:20].

b) Ni siku ya ushindi ya Bwana wetu Yesu aliyofufuka, na kujidhihirisha kwa wanafunzi wake baada ya kufufuka kwa Yesu [YOHANA 20:1,19,26 WARUMI 10:9].

c) Siku ya kuja Roho Mtakatifu, Mwangalizi mkuu wa kazi yote ya Mungu katika kanisa, ilikuwa siku ya Pentekoste ambayo ni Jumapili, siku ya pili baada ya sabato [MATENDO 2:1]

d) Siku ya Pentekoste, Jumapili ndiyo siku ya kwanza ambayo kanisa la kwanza lilianza mahubiri na watu 3,000 wakaokoka na kuanza kusanyiko la kwanza la Ibada kanisani [MATENDO 2].

e) Wakristo wa kanisa la kwanza walikusanyika Jumapili [MATENDO 20:6-12;1WAKORINTHO 16:1-2].
Sababu hizi, zinadhihirisha pia wazi wazi kwamba kuabudu Jumapili hakukuanzishwa na mfalme CONSTANTINE wala kanisa Katoliki.

Hakuna andiko lolote linalosema mtu yeyote anayeabudu Jumapili ana alama ya 666 ya mnyama. Huo ni uzushi. Biblia inatupa uhuru wote katika kuchagua siku ya kumwadhimisha Bwana [WARUMI14:5-6]. Vilevile ni muhimu kufahamu kuwa siku zote ni siku za kujifunza Neno [MATENDO 17:11;2:46].

KUSHIKA SIKU, SIYO NJIA YA KUOKOKA

Kushika siku yoyote hata iwe Jumapili, sio njia ya kuokoka.Tunaokolewa kwa kumuamini Yesu kuwa ni BWANA na MWOKOZI na sio kwa kushika siku yoyote [WARUMI 10:9-10,13].

Anin Gift

Advertisements

204 thoughts on “Sababu za wakristo kuabudu Jumapili

 1. “Warumi 8: 1 Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu.
  2 Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti.
  3 Maana yale yasiyowezekana kwa sheria, kwa vile ilivyokuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu, kwa kumtuma Mwanawe mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa sababu ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili;
  4 ili maagizo ya torati yatimizwe ndani yetu sisi, tusioenenda kwa kufuata mambo ya mwili, bali mambo ya roho.
  5 Kwa maana wale waufuatao mwili huyafikiri mambo ya mwili; bali wale waifuatao roho huyafikiri mambo ya roho.
  6 Kwa kuwa nia ya mwili ni mauti; bali nia ya roho ni uzima na amani.
  7 Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, kwa maana haitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kuitii.
  8 Wale waufuatao mwili hawawezi kumpendeza Mungu.
  9 Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake.
  10 Na Kristo akiwa ndani yenu, mwili wenu umekufa kwa sababu ya dhambi; bali roho yenu i hai, kwa sababu ya haki.
  11 Lakini, ikiwa Roho yake yeye aliyemfufua Yesu katika wafu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho wake anayekaa ndani yenu.
  12 Basi, kama ni hivyo, ndugu, tu wadeni, si wa mwili tuishi kwa kufuata mambo ya mwili,
  13 kwa maana kama tukiishi kwa kufuata mambo ya mwili, mwataka kufa; bali kama mkiyafisha matendo ya mwili kwa Roho, mtaishi.
  14 Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu.
  15 Kwa kuwa hamkupokea tena roho wa utumwa iletayo hofu; bali mlipokea roho ya kufanywa wana, ambayo kwa hiyo twalia, Aba, yaani, Baba.
  16 Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu;
  17 na kama tu watoto, basi, tu warithi; warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo; naam, tukiteswa pamoja naye ili tupate na kutukuzwa pamoja naye.
  18 Kwa maana nayahesabu mateso ya wakati huu wa sasa kuwa si kitu kama utukufu ule utakaofunuliwa kwetu.”

  John, John, John, toka usingizini ili uyasome maandiko kwa Roho ndipo utatambua kama ikiamini kabisa Yesu Kristo wewe ni ndani ya urithi wake, hiyo raha ya milele, ao hiyo sabato ya kiroho. Jameni, ni nafasi ya kuingia wala siyo siku ya kuheshimisha. Hebu fikiria wewe unaendelea heshimisha siku na wengine wamekwisha ingia! Si utabaki nje tu! Soma vizuri Biblia yako katika Waebrania 4: 1-11, uone kama Roho anasemaje juu ya Sabato iliyokuwa kivuli tu kwa wakati wa agano la kale ambayo sasa imefunuliwa rohoni kama sabato, raha, pumziko ya milele inayotungoja sisi kuingia ndani.
  Hebu jithahidi ndugu yangu uingie ndani usije ukabaki nje.

  Ni uamzi wako kuingia ndani ya hiyo raha ao kubaki ukifunikwa na hicho kivuli ambacho ni matendo ya mwili na torati.

  Unasema Mungu hajabadilika, ndio. Lakini ukiwa umepokea Yesu Kristo atatumika rohoni mwako kitofauti na ile sheria ya zamani ambayo ilikuwa imekuzamisha ndani ya dhambi, atakufungua toka minyororo ya Ibilisi; pia utaenenda kwa Roho kwani hutatimiza sheria ya mwili.

  Halafu Ufunuo 13, nadhani ni mada ingine ambayo haina uhusiano na hii mada. Tafadhari uiweke kwa nafasi yake.

  Bwana Yesu Kristo apewe sifa!

 2. Kwani amri ya mungu baada ya hayo ilibadilika , na huku biblia inatudhibitishia kuwa mungu habadiliki na ni yeye aliyesema siku ya saba ndio tuabudu na imebalikiwa. Je huku si kupinga amuli ya mungu na kuibadili? Isitoshe unasema ukweli kwamba siku ya jumapili ni siku ya kwanza ya juma kwa nn tusiabudu siku iliyo ya kweli kama amri ya mungu isemavyo????.

  Harfu tutofautishe kuhumu na kuambiwa ukweli kwa maana mnatumia fungu kuwa mtu asiwahukumu juu ya sabato, je mlishawahi kupewa adhabu kwa kuvunja sabato? Au kama adhabu walokuwa wanapewa zamani ya kuwa mtu akidhini kwa mfano anapigwa mawe? Ukweli utasemwa uzuri ata nyie mnatambua kuwa si siku sahihi kuabudu siku tofauti na mungu alivyosema, na mtambue biblia haipingani ndugu zangu.

  Hamhukumiwi ila mnaambiwa ukweli. Tutumie hekima kuyatafakari maandiko ya mungu. Hukumu ni adhabu itolewayo kwa mtu aliyekosea hivyo hata mkiendelea kukataa ya kuwa siku ya kuabudu ni yoyote mungu ndiye atakayetoa adhabu na si mwanadamu ila ukweli ni lazima muambiwe mkatae msikatae.

  Vilevile wana STRICTLY GOSPLE ningependa mnifafanulie juu ya ufunuo -13 . Asanteni sana tudumu kuyachunguza maandiko ya mungu ilivyo vyema kwa uongozi wa roho mtakatifu. MBARIKIWE SANA.

 3. Kariri mistari yote ya Biblia lakini hutapata sheria ya kuhukumu yeyote anaekusanyika jumapili.

  “Wakolosai 2:16 Basi, mtu ASIWAHUKUMU ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au SABATO;
  17. mambo hayo ni KIVULI cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo.”

  Siyo kubahatisha kama chaguo la rangi!!! Biblia inasema waziwazi. Kwani Siku ya saba ao Sabato ingelikuwa na uhusiano na dhambi Biblia isingelisema hakuna hukumu. Kuendelea kuhukumu ni kuelewa vibaya sana maandiko, pia ni hisia za kutaka Biblia ndo ikuelewe kuliko wewe kuielewa.
  Unisikilize mtu wa Mungu, Biblia inaposema “mtu asiwahukumu”, inamaanisha nani asihukumu wanani? Bila shaka jibu ni wasiyoamini wasihukumu wakristo kwani hili andiko liliambiwa wakristo. Alimradi, unapohukumu mwenzio juu ya Sabato wewe huamini kabisa.

  Pia usidhani kama jumapili haina tangu agano la kale. Biblia inaongea hivi: “Kutoka 12:16 Siku ya kwanza kutakuwa kwenu na kusanyiko takatifu, na siku ya saba kutakuwa kusanyiko takatifu; haitafanywa kazi yo yote katika siku hizo, isipokuwa kwa hiyo ambayo kila mtu hana budi kula, hiyo tu ifanyike kwenu.”

  Sisi wakristo hatuitakase siku lakini tunashiriki ibada. Ina maana tunatakasa ibada. Halafu hii shairi inatuzungmuzia kusanyiko siku ya kwanza na siku ya saba. Ndipo sione nafasi ya kujivunia kusanyiko la siku ya saba tu.

  Siku ya pumziko iko, ile ambayo ni ufunuo wa kivuli cha siku ya saba. Hii hakikisho utaisoma kwenye waebrania 4: 1-11.
  Agano jipya likiwa ufunuo wa agano la kale, katika agano jipya alichokifunua Mungu siyo SABATO bali maana yake. Ilibaki siku moja bila kurudilia tena siku nyingine; pumziko la milele. Kinachotakiwa ni kutulia mbele za Bwana ili tupate huo ufunuo. Jamani, Tusibaki tukifunikwa macho!!!!!!!!

  Bwana Yesu awabariki.

 4. sio mtu akikuambia chagua ragi nawe una mwambia weka yoyote namanisha kwamba hata mungu aliona kuna siku nyingi mungu akusema abudu yoyote upendayo alisema kutoka 20:8 ikumbuke siku ya saba uitakase maana hata bwana mungu wako alistare siku hiyo kwa kuangalia alivyo umba vipendezavyo na akakuamuru na wewe uabudu siku special yakuabudu ni siku ya sabato kama ilivyo andikwa kwenye hesabu 23:19-20 amebariki kwahiyo tusigeze agano lake zaburi 89:34 ato libadili agano lake kwaiyo wewe badili MUNGU ata kuonesha tu

 5. usiji changanye kumbuka ime andikwa katika isaya 66:22-23 yakwamba sabato hata mbinguni kwaiyo lazima ujue yakua ikijidai na na sikuzote ila mungu ana sema amebariki sabato mbinguni ni sabato hata sabato mwezi hata mwezi tuta kusanyika mbele zake kwaiyo wewe kwa nini haja sema kila siku kwa sababu sabato ni upatanisho yeye pamoja na watu wake kwaiyo lazima ufahamu ya kwamba mungu habadiliki soma zaburi 89:34 yeye ni yule yule sabato zake ni zile zile za jana na leo na hata MBINGUNI ISAYA 66:22-23

 6. Hiyo maana ya fungu haiendani kabisa na maana ya siku ya Sabato ya amri ya nne. Soma biblia vizuri

 7. kutoka 20:8-11 ukubuke siku ya sabato huitakase siku sita fanya kazi yako yote lakini siku saba punzika kwa kumwabudu kwa sababu nikumbukumbu lake pamoja na wana damu na pia amei bariki siku hiyo waebrania 4:8-10 kwa maana yeye alieingia katika raha yake amestarehe kama vile MUNGU katika kazi zake Mathayo 5:17 hakuja kutengua torati bali kutimiliza au kukamilisha alicho kinena kwa manabi alafu kwa ambao mnafahamu sabato ni lazi mhukumiwe na MUNGU kwa wasio fahamu wala hawaku wai kusikia hawata hukumiwa ila kwa nilio wa fahamisha mtahukumiwa na MUNGU

 8. skilizeni niwapi imeandikwa siku yakua kufufuka kwa yesu ilikua siku yaku abudu nasiku ya pentekoste paulo alipokua akihubiri makutato ilikua siku ya sabato na jua ilipo zama ilianza siku ya kwanza ya juma na walishiriki meza ya bwana baada jua kuzama nailikua siku ya kwanza ya juma jumapili kwa sababu ya muda kwenda sasa ninyi wa pentekoste na wengine mnaosali jumapili mjue mkibisha duniai mtambishia mungu hata mbinguni kwa sababu ukisoma isaya 66:22-23 kama mna sabato zenu badaala ya sabato yake mjue mumepotea hesabu ya mungu inasema 10-1=0 kwanye amri zake ni kumi ukitoa moja umeharibu zote kwa hiyo watu mnao habudu jumapili mnajidanganya kama mnahisi nimambo ya AGANO LA KALE soma ZABURI 89:34 Hato lihalifu agano lake na watakao ingia mbinguni watakua na chapa ya SABATO (7)nawanao ipingana na sabato watakua na chapaa ya 666 kwa sababu wameshindwa kuitunnza naku fanya mambo yao na SABATO nalazima wapoke na wanao soma hii wajue kwamba mnao andika jumapili kama siku ya kuabudu MTAPOKEA CHAPA YA MNYAMA MUDA SIMUREFU msishituke kwa sababu hamjashituka kwa nini watu wengi wana henda kazini ,shuleni,nakadhalika jumamosi shetani amewaficha na kuwa zidi kujidanganya na BIBILIA NA MESHINDWA KIUSOMA VIZURI NDO MAANA MNAALALISHA SIKU YA KWANZA YA JUMA AU JUMAPILI mjue hata YESU aliheshime SABATO ndo maana alifufuka siku ya kwanza ya juma jumapili kumpenda mungu nikuzishika AMRI ZAKE soma WARAKA KWANZA WA YOHANA 5-3 ISHIKENI SABATO AU SIKU YA SABA YA JUMA AU JUMAMOSI MSIDANGANYE NA SHERIA ZA JUMAPILI MAKE NI WAHONGO HAWANA HUWALALI WOWOTE FUATILIA POPOTE HATA KWA WA ISLAMU HUWA ULIZE SABATO NI SIKUGANI WATA KUJIBU JUMAMOSI
  MUNGU HAWA BARIKI

 9. Gladness,

  Hakose nikupachikie tena hii shairi ndipo utasikia!!!!

  “Wakolosai 2:16 Basi, mtu ASIWAHUKUMU ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au SABATO;
  17. mambo hayo ni KIVULI cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo.”

  Swali ni hili: Unapohukumu mtu mwengine kwa ajili ya SABATO, hapo umeliheshimu neno la Mungu?

  Ina maana hapa hatubahatishe, ni mambo ambayo yamewekwa wazi. Hii ni moja wapo wa tofauti ilioko kati ya Agano la kale na Agano jipya. Mungu habadiliki lakini anapotaka anabadili mapatano yake na watu.

  Mungu alichobadili hapo siyo SABATO baali maana yake. Ilibaki siku moja bila kurudilia tena siku nyingine; pumziko la milele. Sasa pale waebrania inasema kama tufanye bidii tuingie huko. Itakuwa hasara kubwa ukiridhika na siku moja kwa juma bila kujali hiyo siku moja ya milele ambayo Mungu aliweka kwa watu wote wanaoamini.

  Ukiwa na swali ninaamini kama nitapata shauri la kukutolea.

  Ahsante sana.

  Ahsante

 10. Wapendwa siku zote ndio tunapaswa kuabudu na kuomba Hilo sawa na tunapaswa kukesha na kuomba sawa.lakini jueni siku ya SaBa ambayo ni sabato si tu kwa ajili ya ibada Bali ni zaidi ya Hilo.kwanza ni muhuri Wa Mungu
  Pili inakiri uumbaji Wa Mungu kwa kutunza siku hii.tatu ni siku ambayo Mungu mwenyewe aliichagua na kuibariki naye pia alipumziki.jueni neno la Mungu halibadiliki wala halipitwi na wakati. Mwanzo 2:1-3.

 11. Mungu wetu hana kigeugeu na kamwe hata badili sabato kuwa siku takatifu aliyo ifanya na kuibariki na kuitakasa. Sikieni wanadamu tumeumbwa na akili nyingi na uhuru Wa kuchagua tuangalie na tumuombe Mungu sana Uhuru huu usiwe unaenda kinyume na mapenzi ya Mungu.matukio yote hayo yaliyotokea hayakuwa Yana halalisha kuwa jumapili ni takatifu na ndo watu waifanye siku hiyo kuwa ya ibada.alafu sikia Yesu mwenyewe aliitii sabato ya Bwana na siku ya saba that’s why yeye mwenyewe anait Wa Bwana Wa sabato.marko 2:27,28.wapendwa sabato ndiyo muhuri Wa Mungu usiseme siku haina wokovu au haita tupeleka mbinguni hapana….soma neno na achilia moyoni mwako neno likae na lifanye kazi Mungu atakuongoza hakika.jua vita kuu iliyobaki duniani ni Yule mwovu kutaka kuisimamisha siku yake na kuiangamiza siku ya Bwana,, sasa kwa namna hiyo unaweza SEMA kweli siku si ya muhimu? Tafakari zaidi na ujihoji tena zaidi ubarikiwe sana.

 12. Bwana Yesu Asifiwe!

  “Matendo 11: 28. …… Na wakristo waliitwa Wakristo kwanza hapo Antiokia.”
  Wakristo hawakujiita wakristo wenyewe. Wayahudi waliowaona katika mwenendo wao ndo waliwaita wakristo. Ni ule mwenendo uliowapeleka kumchukia Yesu. Na moja wapo wa kile kilichowasukuma kumchukia ni kwamba Yesu alivunja sabato. Kwa lugha ingine hakuiheshimisha kama vile sheria iliiweka.
  “Yohana 5;18. Basi kwa sababu hiyo Wayahudi walizidi kutaka kumwua, kwa kuwa hakuivunja sabato tu, bali pamoja na hayo alimwita Mungu Baba yake, akijifanya sawa na Mungu.”

  Sasa ukiwa mukristo udake hili neno. “Kwa hili jambo la sabato hutakwepa kuhukumiwa na wapinga Kristo” kwani Yesu mwenyewe alihukumiwa nao.

  Biblia inasema kama Agano la kale ni kivuli cha Agano jipya,

  “Wakolosai 2:16 Basi, mtu ASIWAHUKUMU ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au SABATO;
  17. mambo hayo ni KIVULI cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo.”

  Ina maana Agano la kale linaonyesha kwa namna ya picha kitakachofanyika ndani ya Agano jipya. Na kwa ajili ya sabato ni hiki:

  “Waebrania 4: 1 Basi, ikiwa ikaliko AHADI YA KUINGIA KATIKA RAHA YAKE, na tuogope, mmoja wenu asije akaonekana ameikosa.
  2 Maana ni kweli, sisi nasi tumehubiriwa habari njema vile vile kama hao. Lakini neno lile lililosikiwa halikuwafaa hao, kwa sababu halikuchanganyika na imani ndani yao waliosikia.
  3 Maana SISI TULIOAMINI TUNAINGIA KATIKA RAHA ILE; kama vile alivyosema, Kama nilivyoapa kwa hasira yangu, Hawataingia rahani mwangu:
  4 Kwa maana ameinena siku ya saba mahali fulani hivi, Mungu alistarehe siku ya saba, akaziacha kazi zake zote;
  5 na hapa napo, Hawataingia RAHANI MWANGU.
  6 Basi, kwa kuwa neno hili limebaki kwamba wako watu watakaoingia humo, na wale waliohubiriwa habari ile zamani walikosa kuingia kwa sababu ya kuasi kwao,
  7 AWEKA TENA SIKU FULANI, akisema katika Daudi baada ya muda mwingi namna hii, Leo; kama ilivyonenwa tangu zamani, Leo,kama mtaisikia sauti yake, Msifanye migumu mioyo yenu.
  8 MAANA KAMA YOSHUA ANGALIWAPA RAHA, asingaliinena SIKU NYINGINE baadaye.
  9 Basi, imesalia RAHA YA SABATO KWA WATU WA MUNGU.
  10 Kwa maana yeye aliyeingia katika raha yake amestarehe mwenyewe katika kazi yake, kama vile Mungu alivyostarehe katika kazi zake.
  11 Basi, na TUFANYE BIDII KUINGIA katika raha ile, ili kwamba mtu ye yote asije akaanguka kwa mfano uo huo wa kuasi.”

  Wapendwa, siku yetu ya sabato siyo ya kushika ao la, bali ni nafasi ya kuingia. Ni ndani ya raha ya milele.

  Lakini siku ya kuabudu ni kila siku tukikaza mwendo ili tuingie katika hiyo RAHA (Sabato) ya Mungu.

 13. Jaokou,
  Ninakushukuru sana kwa ushauri na usomaji wako wa mapachiko yangu. Nikusihi uniombee pia ili hasira kama umeziona, zinitoke! Lakini pia, Mungu akubariki na azidi kukufunulia kama yote niliyoyaandika yamekusaidia kiasi cha kuyafanyia tathmini hadi ukaona kuna hasira ndani yake. Achana na hiyo hasira. Wewe chota mbaraka wa mengine kwa ajili ya wokovu wako na familia yako pia. Neema ya Bwana ikufunike ndugu yangu.
  Tuzidi kumtafuta Mungu maadamu ni mchana.
  Siyi

 14. siyi kwa mada ulizochangia twashukuru ila mwombe Mungu akukwepue na hasira ili umtumikie kwa usahihi. ukimrushia mwenzio maneno basi upendo wa Kristo Yesu haupo ndani yako

 15. naamini wote ni wazima, Ndg Pendael: nithibitishie kuwa ww huna dhambi unapomwambia mwingne asijifananishe na wewe kuwa yeye mwenye dhambi: pia humu ndani tunapojaribu kujenga hoja tujenge kwa hekima naona wengne wanafula kama wanaimba taarabu,tena kuweka mistar ming ya biblia siyo hoja ya unachotaka kueleweka,huenda ukaiweka bila kuielewa, unaweza ukawa mkongwe kwenye maandiko na bado usielewe mantiki yake, nafikir busara ni kumfundisha kwa busara,hekima na uvumiliv kuliko kuwaita wengne makafir ki2 ambacho ni dhambi pia. tutumie blog hii kufundishana na kuelimishana, sio majigambo ya kujua mambo zaid ya mwingne kama siasa. “MUNGU ATUTAKASE WOTE”

 16. wapendwa ndugu zanguni mliochangia mada,naomba mnielewe vizuli kutokana na hoja niliyoitowa tarehe 16/08/2015 nyuma ya hii comment yangu ya sasa. lengo la hoja yangu ya awali sio kutaka niwatatize kutokana na mnachokiamini katika dini na madhehebu yenu.bali lengo langu ni kujalibu kuleta ufumbuzi wa mjadala huu tulionao ambao kiukweli umetuweka muda mrefu sana bila ya kuwa na uhakika wowote kama tumekubaliana kimawazo. nimetaka kuijuwa siku sahihi iliyotajwa kwenye amri ya nne ikiwa tutahukumiwa kwa kile kilichoandikwa ndani ya amri kumi za mungu tu. lakini pia nina maoni yangu binafsi kuhusu sheria. Kwa kuwa hatuko chini ya Torati ya Mungu aliyoitoa kupitia kwa Musa hakumaanishi kwamba hatuko chini ya sheria za Mungu zilizotolewa kwa Kristo. Paulo alitaja waziwazi katika andiko tulilosoma la Warumi kwamba hatupaswi kutenda dhambi. Bila shaka ni kwamba kama tunaweza kuwa na hatia ya dhambi basi kuna kiwango cha kujipimia. Sheria lazima iwepo ili dhambi iwepo. “Maana pasipokuwapo sheria, hapana kosa” (Warumi 4:15).
  Chini ya agano jipya kuna sheria inayotufunga. Si njia ya kujipatia wokovu kwa sababu wokovu wetu unatokana na neema ya Mungu. Lakini, ni sheria inayotakiwa kufuatwa na kuitii, la sivyo isingetolewa. Sheria hiyo inaitwa na Maandiko, “Sheria ya Kristo.” Sheria ya Kristo ni kila kitu alichoamuru Kristo, kama ambavyo “Torati ya Musa” ni kila kitu alichoagiza Musa. Kumbuka kwamba Yesu alitwambia tukawafanye watu kuwa wanafunzi, tukiwafundisha kuyashika yote aliyotuamuru (Mathayo 28:18-20).
  Hebu tutazame mistari mingine, mahali ambapo Paulo anasema waziwazi kwamba yeye hayuko chini ya Torati ya Musa, lakini yuko chini ya sheria ya Kristo. Anasema hivi:
  Maana, ingawa nimekuwa huru kwa watu wote, nilijifanya mtumwa wa wote, ili nipate watu wengi zaidi. Nalikuwa kama Myahudi kwa Wayahudi, ili niwapate Wayahudi; kwa wale walio chini ya sheria, nalikuwa kama chini ya sheria, (ingawa mimi mwenyewe si chini ya sheria,) ili niwapate walio chini ya sheria. Kwa wale wasio na sheria nalikuwa kama sina sheria, (si kwamba sina sheria mbele za Mungu, bali mwenye sheria mbele za Kristo,) ili niwapate hao wasio na sheria (1Wakor. 9:19-21).
  Sasa, hiyo sheria ya Kristo inalinganishwaje na Torati ya Musa? Kujifunza amri za Kristo hufunua kwamba, katika maeneo mengine, aliweka pembeni sheria zingine za agano la zamani. Katika maeneo mengine, alianzisha sheria mpya ambazo hazikuwepo chini ya agano la zamani. Na katika maeneo mengine, alifafanua maana na kuunga mkono sheria fulani za agano la zamani. Hebu tutazame mifano kuhusu hayo yote matatu.
  Mfano wa eneo la kwanza ni Yesu kuondoa vizuizi vyote kuhusu vyakula, kama ilivyo katika agano la zamani. Tunasoma katika Injili ya Marko kwamba alitangaza vyakula vyote “kuwa ni safi” (Marko 7:19). Chini ya agano la sasa tunaweza kula nguruwe bila ya kuwa na hatia (ona pia Matendo 10:10-15; 1Timotheo 4:3-5).
  Mfano wa eneo la pili ni amri ya Kristo kuanzisha ubatizo wa maji, kitu ambacho hakikutakiwa kwa yeyote katika watu wa Mungu wa agano la zamani (ona Mathayo 28:19). Pia, kuna wakati Yesu alitupa sisi kitu alichoita amri mpya, kwamba tupendane sisi kwa sisi kama Yeye alivyotupenda (ona Yohana 13:34).
  Mfano wa eneo la tatu ni jinsi Yesu alivyounga mkono amri ya saba, inayozuia kuzini. Alipohubiri mahubiri Yake ya Mlimani, alifafanua maana ya kukatazwa huko, akifunua kusudi la Mungu la tangu mwanzo. Inaonekana kwamba wengi waliokuwa wanamsikiliza hapo walijihesabu kuwa watakatifu kwa habari ya uzinzi, ingawa mara kwa mara wote walikuwa wanatamani katika mioyo yao. Lakini, kama Yesu alivyoonyesha, kama ni makosa kuwa na mahusiano ya kimapenzi kimwili na mke wa jirani yako, ni makosa pia kumvua nguo katika mawazo yako.
  Sisi sote ambao tuko katika Kristo kweli tuna wajibu – na msukumo kutoka ndani – na uwezo wa kuitii sheria ya Kristo. Tuko chini ya sheria Yake. Amri za Yesu zimehusisha matakwa yote ya kiadili yaliyokuwepo katika Torati ya agano la zamani.

 17. Barikiwa sana katika jina lake yesu kristo. swali langu ni dogo tu kwa wasabato wote. Ni wapi jumamosi ilipoandikwa ndani ya amri kumi za mungu?

 18. YOHANA STANLEY,
  Umeniita Dada na sijawahi kujitambulisha kuwa mimi ni dada hapa SG.Pia sikushangai kwa sababu “roho ya kike” imekukaa ndio maana mwalimu wako ni Mama ELLEN G. WHITE, hivyo si ajabu unamuiita baba yako dada.Biblia inasema “AONAVYO MTU NAFSINI NDIVYO ALIVYO” hivyo sikushangai kwa sababu akina dada ndio waliokujaza moyo na MTU HUYANENA YALIYOUJAZA MOYO.
  Ukitaka kujua una Kundi (jeshi) la PEPO, angalia baadhi ya mafundisho ya WASABATO yaliyomo moyoni mwako;
  1.Unahubiriwa na mwanamke( ELLEN G. WHITE).
  2.Unaabudu SIKU( Jumamosi) kuliko kumwabudu BWANA wa SIKU (BWANA YESU KRISTO).
  3.Wanawake hunyoa PANKI, huvaa VIMINI na nguo zenye mipasuo (yawezekana ndio iliyokupeleka SDA)
  4.Unaamini NAFSI TATU za mungu ( miungu mitatu) kama ndugu zako WAKATOLIKI.
  5.Umebatizwa na Mnabatiza Kwa Jina la Baba, na Mwana na Roho Mtakatifu Wakati WAKRISTO walibatuzwa Kwa JINA LA YESU KRISTO ( MATENDO 2:38-39)
  6.Unaongozwa na LESONI kama ndugu zako wanavyoongozwa na QURAN.
  Pia Umejaa Mafundisho mengi ya kipepo kama WAMILERI (WASABATO WA MWANZO) waliojivika MANYOYA na kupanda kwenye miti na wengine kupanda milimani ili WANYAKUILIWE kwa sababu mwisho wa dunia ingekuwa March 21, 1843, ambayo haikutimia. Kisha ikasogezwa mbele hadi March 21, 1844 ambayo pia haikutimia.Pia unafanana na WASABATO WENZAKO WALIOTAKA KUSAFIRI BILA NAULI hadi wakafukuzwa uwanja wa ndege.
  KUMBUKA; Hapa SG si MAHALI PA KUROPOKA kama huna kitu chenye maana kwa watu wa Mungu, ni heri ufunge mdomo wako au kama huwezi nenda Hospitali ya MIREMBE.

 19. dada pendaeli simon biblia inasema “kila neno la Mungu limehakikishwa yeye ni ngao yao wamwaminio usiongeze neno katika maneno yake asije akakulaumu”sabato ilianzia edeni baada tu ya uumbaji wala usidhani kua ellen ndo kaianzisha.najua kwamba nawewe si wewe unae sema hayo ila ni nguvu ya yule mwovu shetani.yesu alimwambia petro wewe shetani rudi nyuma yangu kwasababu alijua maneno aliyo tamka petro si yeye bali shetani,pendaeli yachunguze maandiko.lakini pia ukinitajia fungu lolote linalosema tuabudu jumapili kutoka kwenye biblia nabatizwa leoleo.Ahsante.

 20. GILBERTO, kweli WASABATO na WAISLAMU ni kitu kimoja!Naona jinsi unavyosisitiza undugu na umoja wenu hata unasihi kwa kutumia QURAN.Ni ukweli usiopingikika kwamba QURAN na LESONI ni kitu kimoja.Endelea kufunua siri za Wasabato!!

 21. Gilberto,

  Kulingana na maelezo yako, kwa asili unaonekana ni kunguru mla mizoga iliyooza na nafaka!

  Basi nenda ukajikusanye na hao majirani zako, ukawape ujumbe huu muutafakari kwa pamoja: Mdo 20:7 “Hata SIKU YA KWANZA YA JUMA, tulipokuwa TUMEKUTANA ILI KUMEGA MKATE, Paulo akawahutubu, akiazimu kusafiri siku ya pili yake, naye akafuliza maneno yake hata usiku wa manane.” (Msisitizo ni wangu)

  Ufu 1:9-10 “Mimi Yohana, ndugu yenu na mwenye kushiriki pamoja nanyi katika mateso na ufalme na subira ya Yesu Kristo, nalikuwa katika kisiwa kiitwacho Patmo, kwa ajili ya Neno la Mungu, na ushuhuda wa Yesu. Nalikuwa katika Roho, SIKU YA BWANA; nikasikia sauti kuu nyuma yangu, kama sauti ya baragumu.”

  Unaliona Kanisa! Liko ktk Agano Jipya, hili la kamili, hivyo lile la sehemu lazima liachie! Hili lililo kamili linaongozwa kwa Ufunuo ambao ndiyo Imani, wale waliomkataa Kristo, pamoja na wanafiki waliokula mikate halafu wakampigia makelele pilato amsulubishe, wanaendelea na Torati pamoja na wanafiki wa leo, ninyi msiokujua mtokako wala muendako; mwisho nguvu ya upotevu huwasomba ktk mafuriko yake kama hayo ya masalia, matengenezo na mengine yajayo, tena yenye nguvu zaidi ili kuusomba uchafu wote wa dini, na kuufurikishia huko Ziwani lile ziwa la moto!!!

  Uwe makini ndg yangu, fuata Injili ya mitume uokoke

 22. hebu ndugu zangu wa kristo na waislamu pamoja tumrudie Mungu wa kweli.

  sasa ni zamu ya Qur-an iseme, je siku gani tumuabudu Mwenyezi Mungu?

  surat Al-Nisai 4: 154
  “…….. na pia tukawaambia msiluke mipaka kwa kuvunja taadhima ya jumamosi……”

  Surat Al-Baqarah 2: 65
  ” Nakuyakiri nimekwisha kujua, habari za walioasi miongoni mwenu katika amri ya kuiheshimu jumamosi, basi tukawaambia kuweni manyani wadhalimu”

  Surat Al-Baqarah 2: 65
  ” kwa hiyo tukaifanya adhabu hiyo kuwa onyo kwa wale walio katika zama zao na waliokuja nyama yao, natukaifanya (sabato) kuwa mawaidha kwa wamchao Mwenyezi Mungu”

  Ezekiel 20:12
  ” Tena naliwapa sabato zangu ziwe ishara kati ya mimi na wao, wapate kujua kuwa mimi Bwana ndimi niwatakasaye”

  Ndugu zanguni wa Kristo, haya ndiyo mnayoyataka mpaka muambiwe na jirani zenu kana kwamba wenyewe hamuoni. Rudi kwa Yesu haraka sana. Bado Yesu anagonga.

 23. Maandiko yanasemaje?
  Marko 2:27 Yesu ndiye ndiye Bwana wa sabato
  Luka 4:16 – Yesu alisali sabato kama desturi yake, na Luka anaelezea mafungu zaidi ya matatu.

  Matendo 17:2 – Hata kumbe mitume walisali sabato

  Ebrania 4:9 kumbe raha ya watu waliyo wa Mungu ni sabato bwana.

  Yakobo 2:10 shika amri zote maana hii ni amri ya milele
  Isaya 66:22-23 – kumbe na mbinguni sabato itaendelea, na kama huitaki, jibu ni rahisi tu kwamba mbingu siyo yako.
  2 petro 3:15-16 – kama huna elimu sawasawa usipotoshe maandiko ya paulo (1 korintho 16:6-12) eti siku ya kwanza ni ibada, ng’o, hiyo inatakiwa iwe siku ya kukusanyika kwa ajili ya vikao tu na mambo mengineyo kwa ajili ya maendeleo ya kanisa.

  2 Thesolonike 2:10-11-12 ukiikataa kweli, hata Mungu atakufanya uukubali uongo kama ndo kweli yako ili hukumu ikukute sawasawa.

  Hebu tuwaache kina PAPA, ELLEN WHITE, IGNATUS LOYOLA, DALAI LAMA na wengineo, Tumuulize Mungu anataka tufanye nini.

  Mbarikiwe nyote

 24. Lwembe,
  Ha ha ha ha haa!!
  Umesema kuwa, “Amri Kumi ndg yangu zilikwisha kufungwa kwenye zigo la Maagizo yaliyokwisha muda wake kwa wale ambao Amri hizo zimewapeleka kwa Kristo wakabadilishwa asili, kutoka ya Dhambi na kupewa asili ya Mungu.”
  Kimsingi hiki ni kichekesho rafiki yangu Lwembe. Kama unakataa kuwa siyo kichekesho, niambie ni kwa nini Adamu na mkewe walipewa sheria kabla hawajatenda dhambi bustanini? Kwa nini Mungu aliwapa amri? Mungu alizitoa wapi kama kweli na YEYE hana amri katika serikali yake? Je, asingekuwa na amri kweli, Shetani angekuwepo leo? Kama kweli maelezo yako hayo ni ukweli, hebu thibitisha hoja zangu hizi kwa majibu ya Kibiblia!! Kabla sijajibu pachiko lako hili japo jibu lake ni fupi sana, nakungoja kwanza nikuone kwa majibu ya hoja zangu hizi. Ubarikiwe.
  Siyi

 25. Siyi,

  Tafsiri ya hilo neno unalolisoma ktk Kol 2:14- 19 iko kama linavyojieleza lenyewe! Kinachokusumbua ni kule kuliamini Neno hilo kama unavyolisoma bila ya kuongezea hayo mambo yenu. Hebu tazama unachoniambia:
  “”Kwa hiyo unataka kutuambia kuwa watu wasituhukumu kwa Sabato, uzinzi, wizi, nk kisa Kristo alitufia msalabani??””
  Maswali kama haya ndiyo yanayoonesha kwamba HUNA imani, una msimamo tu unaotokana na masomo ya dini yenu ambayo utakuwa ni mwanafunzi mzuri wa kupata A+!

  Kama umeambiwa kwamba mtu asikuhukumu, sasa unashangaa nini? Badala ya kutafuta kujua inakuwaje mpaka tusihukumiwe, wewe unalikataa neno hilo kwamba haliwezekani! Jamani, hata dunia inalo jambo hilo, mwendesha mashtaka anaweza kuamua kutokuendelea na kesi ya mzinzi licha ya ushahidi wa jambo hilo kuweko wazi au kukiri kwa mshtakiwa mwenyewe; jambo hilo linaitwa “Nolle prosequi”, hili ndilo linaloelezwa ktk vifungu hivyo! Mfano mzuri wa jambo hilo ni wa yule “Magdalene” wenu, nafasi ya Kristo ktk tukio la mwanamke huyo mzinzi ilikuwa ni ya mwendesha mashtaka ndio maana alimwambia yule mwanamke kwamba “sikuhukumu” akaiondoa kesi hiyo kwa Hakimu, kwahiyo hakuna ambaye angeweza kumhukumu tena mwanamke huyo kwa kosa hilo! Hii hapa hukumu iliyompasa kwa kuivunja Amri hiyo: Law 20:10 “Na mtu aziniye na mke wa mtu mwingine, naam, yeye aziniye na mke wa jirani yake, mtu mume aziniye, na mwanamke aziniye, hakika watauawa.”

  “Usi zini” ni mojawapo kati ya zile Amri Kumi. Halafu, kama unafikiri kwamba watu hawaivunji Amri hii, hilo laonesha jinsi ulivyo mbali na Kweli. Mungu alisema inapokaribia ujio wa Kristo, dunia itakuwa ktk hali ya Sodoma. Jaribu kutafuta hali ya Sodoma ilikuwaje hata ikapelekea kuchomwa moto! Ukiisha kuiona hiyo, sasa njoo makanisani, usiiangalie dunia huko nje, hapana huo ni ujumbe wa Kanisa. Kanisa litakuwa ktk hali ya Sodoma; wataanzisha mafundisho ya kusamehewa kwa wazinzi, msingi wake ukiwa yule “Magdalene” wenu, wakiitangua Torati, watawakumbatia mashoga kwa visingizio vya kutenda wema, kama unakumbuka huko nyuma, niliwahi kukutaarifu ndg yangu kusudi ukimbie mapema, kwamba Wasabato pia wanayo programu hiyo ya mashoga ktk makusanyiko yao na hivyo damu ya hao mashoga kuchanganywa na ya kwenu mnaolihalifu Neno la Mungu kwa makusudi ya kulihalifu; Law 20:13 “Tena mtu mume akilala pamoja na mtu mume, kama alalavyo na mtu mke, wote wawili wamefanya machukizo; hakika watauawa; damu yao itakuwa juu yao.”

  Basi huo utii wenu ni utii wa kitu gani? Utii wa Sabato? Acheni mambo ya kujitungia, Mungu analiheshimu saaaana Neno lake kuliko mnavyojidanganya, hawezi kuacha lishindwe kutimiza alichokisema; na alisema atawachoma moto wote wa staili hiyo!!!

  Mwisho napenda nizidi kukushauri ndg yangu, najua ni uamuzi mgumu sana kwa mtu aliye ktk tabia ya akina Esau, lakini mifano ya hao inapaswa iwe changamoto ya kukufanya uyafikie hayo maamuzi magumu ya kulikataa bakuli la dengu ili uendelee kubaki na Haki yako ya mzaliwa wa kwanza! Amri Kumi ndg yangu zilikwisha kufungwa kwenye zigo la Maagizo yaliyokwisha muda wake kwa wale ambao Amri hizo zimewapeleka kwa Kristo wakabadilishwa asili, kutoka ya Dhambi na kupewa asili ya Mungu. Umewahi kusoma popote pale kwamba Mungu alijiwekea sheria ya kutokuzini? Uzinzi una mwanzo; na chochote chenye mwanzo kina mwisho, nao mwisho wa Uzinzi ni Kristo kama ulivyo mwisho wa amri ya sabato!

  Hebu wazia jambo hili kama litakusaidia, ulitazame ktk hali yako ya sasa ya huo “utii” wako wa sheria. Mvunja Sabato, msingi wa kesi yake utakuwa hiyo Amri, na hukumu yake vivyo. Iwapo hakuna anayeivunja Sabato, hiyo Amri itakuwa na nguvu yoyote juu ya mtu huyo? Au kwamba hakuna Mzinzi, watu wote hawatamani tena wake za jirani zao; je, hiyo Amri ina kazi tena; itamshitaki nani? Asili ya dhambi ikiisha kubadilishwa, sheria haina kazi tena kaka, ndio maana nilikuambia jitahidi utafute maelekezo ya kukupatia ONDOLEO la dhambi ndio na mambo haya utayajua jinsi yake, lakini naona umekazana na uongo wa dini unaoendelea kukuongoza huko maporini! Mambo ya Ufalme huwezi ukayajua kwa kuchungulia dirishani, ni sharti uingie humo ndani, na humo ndani hakuna kichafu au dhaifu kinachoingia!

  Gbu!

 26. @ Lwembe,
  Kwanza, mbona unachekesha kabisa. (‭KOL.‬ ‭2‬:‭14-19‬) inazungumzia sheria za hukumu (hukumu)!! Sasa jiulize ni sheria gani iliyokuwa na hukumu ya papo kwa hapo??? Kwa hyo unataka kutuambia kuwa watu wasituhukumu kwa Sabato, uzinzi, wizi, nk kisa Kristo alitufia msalabani?? Wadanganye wavivu wa maandiko lakini siyo Siyi!! Sikia, watu wengi sana leo, hawamweshimu Mungu kama wanavyomweshimu binadamu mwenzao!! Ni sheria zile tu zinazomhusu Mungu kama vile kuabudu sanamu, kuvunja Sabato yake, kulitaja bure jina lake n.k., ndizo watu huzivunja sana!! Kwa nini?? Hakuna wa kuwatia hatiani kwa wakati huo japo Mungu anaweza kuwashughulikia!! Sheria zingine zinazomhusu Mungu pamoja na wanadamu k.v. wizi, uzinzi, uongo n.k., huwa hawazivunji kabisa ovyovoyo!! Kwa nini?? Sababu kubwa sana, wanaogopa adhabu za kibinadamu ya papo kwa hapo!! Kwa hiyo watu wa leo (waasi), wanamweshimu zaidi binadamu mwenzao kuliko Mungu aliyewaumba!! Hata sishangai kuwaona mkiivunja sabato yake pasi sababu!! Kikombe chenu kikijaa, mtakiona cha mtema kuni tu!!
  Siyi

  @ Pandael
  Wewe ni mungu unayeona dhambi za wengine!! Wewe huna dhambi!! Wewe mtakatifu sana!! Wewe songa mbele na utakatifu wako uone kama utakufikisha mbinguni!! Ninakuhakikishia kuwa, usipotubu mapama, usiitarajie mbingu kijana!! Huo ndio ukweli, japo kwako unaoonekana ni upuuzi!! Maswali yaako yooooote niliyajibu. Hata mbele za mbingu sidaiwi kitu kwa nafsi yako!!
  Hata siku ile nilikwambia kuwa wewe huna akili hata chembe rafiki yangu!! Huwezi hata kujitetea!! Huwezi hata kujenga hoja!!?? Kwa nini ukalie kunukuu ya watu wengine?? Sema ya kwako?? Mimi nilishakwambia kuwa, Miller na nduguye Ellen G. White, siyo waanzilishi wa kanisa la Wasabato!! Mbona huelewi?? Nilitarajia uniulize kama si hao, ni akina sasa?? Lakini huulizi, na badala yake umeng’ang’ana na ufedhuli wa akina Lwembe, Kenye, Pandael nk. Utakufa kibudu wewe!! Kila la kheri mtakatifu wa mungu!!
  Siyi

  @ Joyce,
  Jitahidi kuwa unapata taarifa sahihi kutoka kwa watu sahihi!! Kama unaamini habari za akina Lwembe na kuzichukulia kama ni za ukweli, ilhali wao siyo wasabato, nalo ni jambo jema tu kwako!! Endelea tu!! Maana hivyo ndivyo ulivyofundishwa na kukaririshwa!! Ila nakwambia kuwa, walikudanganya sana!! Ghairi mapema!! Vinginevyo, uliza mambo sensitive tujadili sasa, badala ya kuendelea kupoteza muda kwa hili!!
  Siyi

 27. WAPENDWA;
  Ufuatao ni Mchango wa Ndugu KENY, alioutoa tarehe 21/05/2014 at 11:39 AM kwenye Mada isemayo WAADVENTISTA WASABATO HAWAKIDHI VIWANGO VYA KUITWA WAKRISTO?
  Ndugu KENY;
  ” Wasabato (SDA) umeanzishwa kutoka Marekani, miaka ya 1860 baada ya mkutano wa Hiram Edson, Joseph Bates na Ellen White kwa kufuata mafundisho ya aliyekuwa nabii wa uongo (William Miller), ndiye aliyetabiri kama mwisho wa dunia ingekuwa March 21, 1843, haikutimia. Kisha ikasogezwa mbele hadi March 21, 1844 ambayo pia haikutimia. Alitumia baadhi ya vifungu kutoka kitabu cha Daniel na Ufunuo kwa kutoa tafsiri potofu ya unabii wake.”
  >>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
  ***Hakika USABATO ni wazo la mtu/mwanadamu (WILLIAM MILLER na ELLEN G.WHITE, na WASABATO hawajaandikwa mahali popote kwenye BIBLIA zaidi ya kuwa ni JINA LA KUFURU (UFUNUO 17:3-5). Hivyo MSITISHWE na ” Imani Feki” ya WASABATO waliojiita majina mengi kama vile WAMILERI,WASABATO MATENGENEZO,WASABATO MASALIA,WAADVENTISTA …nk. Kwa kweli USABATO na WASABATO ni MCHAFUKO***

 28. Siyi,

  Duuu watu wana Archarve za hatarrriiii mi nilikuuliza kwa nini wamwabudu mama yenu Ellen ukakataaa unaona hesabu hizoooooooooo, pili nikakuuliza maana ya nembo ukakataaa mhhh haya sisi sote tu wana wa Baba mmoja haijalishi wewe umefata tabia za bibi au Aunt woteee Baba yetu ni huyo huyooooooooooo

  Asante

 29. WAPENDWA,
  Nimebarikiwa na MAELEZO Yafuatayo ya Ndugu CK LWEMBE hasa kuhusu William Miller na Ellen G.White WAANZILISHI WA USABATO ambao SIYI amekataa kuwaelezea kutoka na SIASA zao katika UKRISTO. Maelezo haya,aliyatoa Ndg CK LWEMBE kwenye Mada isemayo HUKO BWANA AJAPO.
  Hebu fuatlia UKAFIRI wa WASABATO ” Wanaojiita wakristo/Wayahudi”
  NDUGU CK LWEMBE;
  ” Neno ‘Adventist’ ni neno la kawaida linalomaanisha “ujio” wa jambo au mtu fulani. Katika teolojia ya Kikristo, neno hilo humaanisha lile “Tegemeo la Tukio la Kuja kwa Pili kwa Kristo” kama ilivyoahidiwa ktk – Yn 14:1-3, “Msifadhaike mioyoni mwenu; … Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali. Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu…” na mahali pengine ktk Mt 24 na 25

  Lakini baada ya kujitokeza kwa kundi la Kiprotestanti ktk miaka ya 1830, lililoongozwa na mhubiri wa Kibaptist William Miller, ambalo lilijikita ktk kulichunguza jambo hilo la “Kuja kwa Pili kwa Kristo”, ktk mtazamo wa kisasa, ndipo neno hili, “Adventist” lilichukua maana mpya pale lilipohusishwa na kundi hilo lililojengeka ktk msimamo au imani ya “Kuja kwa Pili kwa Kristo”, nao wakatambulika kama wa “Adventists” ktk maana hiyo hata leo hii. Kwahiyo kucheza na neno hilo ukijaribu kulirudisha ktk maana yake ya kablaya 1830s kimatumizi, ili maana hiyo uisimamishe leo hii, ni hila ya kuwachanganya watu kama Baalamu alivyowashauri Moab jinsi ya kuwanajisi Israeli!

  Miller ktk kuyachunguza kwake kwa kina Maandiko ktk vitabu vya unabii vya Daniel na Ufunuo, ndipo akabaini na kutangaza kwamba Tukio hilo la Kuja kwa Pili kwa Kristo litatukia ktk mwaka 1843 au 1844. Ndipo ktk kujitayarisha na Tukio hilo la karne, kundi hilo likajitengenezea na mbawa ili waruke huko hewani wakamlaki Bwana!!! Unawaona hao wanao tumia akili? Ndio hawa hapa ktk Kol 2:18, wenye “…Kunyenyekea kwa mapenzi yake mwenyewe tu, na kuabudu malaika, akijitia katika maono yake na kujivuna bure, kwa akili zake za kimwili”; mnayaona hayo maono yao? Wamejitengenezea mbawa, wakiongozwa na ile sadistic spirit iliyokuwa juu ya malaika wao Miller waliomuabudu! Yaani walipopandishwa huko milimani, kuzimu yote iliangua vicheko kama ilivyokuwa kwa wale Sabato Masalia huko ktk mabonde ya Kinyerezi/Segerea walivyoishia kuumwa na nyoka na wengine kufa ktk jitihada yao ya kwenda kuhubiri Biblia huko ulaya bila nauli!!!

  Ktk miaka yote miwili halikutokea; na haswa pale utabiri wake uliokuwa na uhakika zaidi uliposhindwa kutimia tarehe 22 Oktoba, 1844, basi wengi wa wafuasi wake wakavunjwa moyo kwa “Aibu hiyo ya Karne”. Ndipo kundi dogo kutoka kundi hilo wakajitenga ili kufanya mapitio, wakiitafakari upya Imani ya Kikristo ili kuyavuka mapokeo kulingana na yalivyorithiwa ktk karne zote ili wajirudishe huko kwenye asili halisi ya mwenendo wa Kikristo na tabia zake.

  Ktk shauku hii, ndani ya miaka ipatayo kumi ya matengenezo ya Teolojia ya “imani” hiyo, baada ya unabii kushindwa, ktk miaka ya1850-60 ndio yakalizaa dhehebu la Adventist ambalo liliendelea na unabii huo ambao sasa ulirekebishwa kutoka Kuja kwa Pili kwa Bwana, na kufanywa kwamba ktk tarehe hiyo Kristo ndipo aliingia Patakatifu pa Patakatifu ili kuianza kazi ya Upatanishi!

  Naye nabii Ellen Gould White, alihudhuria mikutano mingi ya Miller na hivyo kuwa mfuasi wa kundi hilo. Baadaye alichukua nafasi ya “malaika” wa kusanyiko hilo pale alipotambuliwa rasmi kama nabii wa dhehebu hilo, hivyo wakayapokea maono na mafundisho yake kadiri ya uvuvio alioupata kutoka kwa roho anayeliongoza kusanyiko hilo.

  Wakatoliki walipowasikia Wasabato wakimuita papa kwamba ndiye Mpinga Kristo, na kuiona hesabu ya cheo chake ktk namba za Kirumi ikiifanya jumla yake kuwa namba ya Mpinga Kristo – 666; kwa vile huyo ni mtoto wao aliyekata kamba, basi wakawaonesha uhalisi wa mamlaka, kadiri ya utumishi kwamba nabii wao huyo ni sehemu yao, ndipo kulidhihirisha hilo, wakawapigia hesabu ya jina la ELLEN GOULD WHITE ikafanya jumla ya 666 pia, (ktk Kilatini U imekokotolewa kutoka V nayo W ni U2 au V2)!!!
  E = 0
  L = 50
  L = 50
  E = 0
  N = 0

  G = 0
  O = 0
  U = 5
  L = 50
  D = 500

  W = 10 (U2 au V2)
  H = 0
  I = 1
  T = 0
  E = 0
  JUMLA 666 !!!!

  Mambo ndio kama mnavyoyaona, “wote dugu moja”!!!

  Gbu!”

 30. Siyi,
  Wewe kweli u kipofu ukiwaongoza wenzako (WASABATO) shimoni.Umeshindwa kwa USHAHIDI WA WAZI kujibu hata swali moja kati MAWSWALI NILIYOKUULIZA.
  Sihitaji kupoteza muda na mtu kama wewe anayetetea UKAFIRI.
  Mungu airehemu nafsi yako yenye dhambi.

 31. “…Akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwepo tena, akaigongomea msalabani; akiisha kuzivua enzi na mamlaka, na kuzifanya kuwa mkogo kwa ujasiri, akizishangilia katika msalaba huo. Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato; mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo. Mtu asiwanyang’anye thawabu yenu, kwa kunyenyekea kwa mapenzi yake mwenyewe tu, na kuabudu malaika, akijitia katika maono yake na kujivuna bure, kwa akili zake za kimwili; wala hakishiki Kichwa, ambacho kwa yeye mwili wote ukiruzukiwa na kuungamanishwa kwa viungo na mishipa, hukua kwa maongeo yatokayo kwa Mungu.” (‭KOL.‬ ‭2‬:‭14-19‬)

  Kichwa ni Kristo, naye mtume Paulo anasema nifuateni mimi kama ninavyomfuata Kristo. Ndipo anasema mtu asiwahukumu kuhusu mambo ya sabato, hiyo ambayo wamejinyenyekeza kwa mapenzi yao wenyewe tu, na kuabudu malaika, wakijitia katika maono yao na kujivuna bure, kwa akili zao za kimwili; wala hawakishiki Kichwa; kwa hila hiyo wanatafuta kwa bidii watunyang’anye thawabu yetu!!!

  Wanaabudu siku badala ya Mwenye siku. Wanaihalifu Amri ya Mungu, wamejitengenezea sanamu ya Siku wakaiunganisha na Mungu kwa hila ya ibada na kuwalisha kufuru kusanyiko lao,wakaabudishwa mungu wa Jumamosi badala Mungu wa Kweli; wakiisha kuyatupilia mbali yote yaliyofunuliwa kupitia mitume!

  “Mtu mmoja afanya tofauti kati ya siku na siku, mwingine aona siku zote kuwa sawasawa. Kila mtu na athibitike katika akili zake mwenyewe.” (‭RUM.‬ ‭14‬:‭5‬)

  Basi akili tulizo nazo ni za Kristo, ile nia iliyomo ndani yetu pale tulipozaliwa kwa Roho ndipo na njia yetu ikaongozwa kwa huyo Roho aliyetuzaa, hilo Taifa Jipya. Hao hapo mitume, hao ambao wako ktk siku mpya ndani ya Agano Jipya, viumbe vipya wakiongozwa kwa Roho na si Torati tena;
  “Hata siku ya kwanza ya juma, tulipokuwa tumekutana ili kumega mkate, Paulo akawahutubu, akiazimu kusafiri siku ya pili yake, naye akafuliza maneno yake hata usiku wa manane.” (‭MDO‬ ‭20‬:‭7‬)

  New Order!!!! Hatuko tena chini ya Sheria, tumerudi uweponi mwa Mungu, TUMEPUMZIKA, hatuhangaiki tena na masuala ya kumtafuta Mungu, anaishi ndani yetu akituongoza ktk Njia yake ili tuwahubiri wote walio ktk vifungo ya kwamba Kristo alizichukua dhambi zetu zote, akatolewa kuwa Sadaka au dhabihu ya dhambi, akaibeba na Torati yote, yule mshitaki, pamoja na Amri Kumi zake, akashuka navyo vyote kuzimu, akaviacha huko; nasi tulikuwa ndani yake, ndipo alipofufuka, nasi tulifufuliwa ktk upya wake, ndio sababu pekee tunayokutana siku ya kwanza ya Juma, kama unavyowaona mitume walivyoongozwa kukutana siku hiyo ya Bwana, ktk uhuru wa Roho tunakutukuza kufufuka kwake, maana kama hakufufuka, basi hata kusulubiwa kwake kusingeleta Uzima wa milele; ndio maana tumetenganishwa kwa jambo hilo, wenye kuiabudu siku ya Jumamosi wakiukana Ufufuo na hivyo kuukosa Uzima wa milele nasi tulio ktk ufufuo!!!

  Bwana na azidi kutupatia fursa ya kuyatubia maovu yetu!

 32. @ Pandael,
  Umenirudia tena rafiki yangu!!! Ha ha ha ha!!
  Kwanza, Pole sana kwa kuniona nimefiliska kimwili na kiroho!! Ni mtazamo wako!! Niko hapa kujifunza tu!! Na nimejifunza mengi mpaka sasa!! Kwa kiasi fulani (japo siyo saaana), nina vitu vingi kidogo!! Unaweza kunizidi kweli kiuelewa, lakini huwezi kunizidi kiusahihi!! Machache ninayoyajua, najua kiusahihi kijana!! Ukija na vimaswali vyako ukitarajia nikujibu kama ulivyodanganywa huko nyuma, kimsingi utachemka tu, maana mimi sitaki kukupoteza!! Nataka kukwambia ukweli ili ufanye uamuzi sahihi wewe mwenyewe japo unaonekana kushikilia udanganyifu ulioupokea enzi zile, na cha ajabu zaidi, hutaki kusikiliza!! Kama kweli wewe ungekuwa NGULI wa NENO, ungeleta usahihi wa kile nilichokikosea mimi badala ya kuendelea kupiga kelele za chura!! Narudia tena, kusema kama kweli wewe ni nguli wa Biblia na Historia, leta usahihi wa kile nilichokosea mimi Siyi!! Tuko hapa kusaidiana!! Leta sasa na wengine tujifunze kwako pia!!
  Pili, narudia kukwambia tena kuwa, akina Miller na Ellen G. White, kwangu mimi Siyi, siwatambui kama ni waanzilishi wa kanisa la Wasabato. Hata ukienda kwa msabato yeyote mwenye akili, atakwambia hivyo!! Usabato haujaanzishwa na Miller wala Ellen G. White!! Kama wewe walikufundisha hivyo, walikudanganya kaka!! Dini ya Mungu au kanisa la Mungu aliye hai, halijaanzishwa na watu kama hao!! Rudi darasani tena Pandael!!
  Tatu, kama wasabato si wakristo, ni watu gani sasa? Hebu tuambie kwa vigezo vya Biblia yako??
  Kama unabaki kutukana watu tu bila ya kutoa hoja zenye maana, ni heri ukaniacha na upumbavu wangu wa kuitwa msabato, maana walao nina sababu ya kuutetea upumbavu wangu huu!! Nakushuru sana bro!!
  Neema ya Bwana ikufunike.
  Siyi

  @ Landelinus
  Mungu akubariki sana. Umenigusa sana kwa aya nzuri za Biblia. Sijui wewe ni dini gani, lakini ulivyoyaleta haya, yamenigusa sana!! Ni kweli, mwenye macho ya kusoma, masikio ya kusikia na akili ya kuelewa, ataelewa tu, yepi ni magugu na zipi ni ngano!! Ubarikiwe sana.
  Siyi

 33. Joyce,
  Asante kwa aya za Biblia!! Nimesoma na nimezielewa vyema. Mungu akubariki sana!!! Uwe na Sabato njema
  Siyi

 34. matendo20:28Jitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake, mpate kulilisha kanisa lake Mungu, alilolinunua kwa damu yake mwenyewe.29 Najua mimi ya kuwa baada ya kuondoka kwangu mbwa-mwitu wakali wataingia kwenu, wasilihurumie kundi;
  30 tena katika ninyi wenyewe watainuka watu wakisema mapotovu, wawavute hao wanafunzi wawaandamie wao.

  2timotheo 4:2 lihubiri neno, uwe tayari, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho. 3 Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia waalimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti;
  4 nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo

  2petro3:15 Nanyi uhesabuni uvumilivu wa Bwana wetu kuwa ni wokovu, kama vile na ndugu yetu mpenzi Paulo alivyowaandikia kwa hekima aliyopewa;
  16 vile vile kama katika nyaraka zake zote pia, akitoa humo habari za mambo hayo; katika nyaraka hizo yamo mambo ambayo ni vigumu kuelewa nayo; na mambo hayo watu wasio na elimu, wasio imara, huyapotoa, kama vile wayapotoavyo na maandiko mengine, kwa uvunjifu wao wenyewe.
  17 Basi, wapenzi mkitangulia kujua hayo, jilindeni nafsi zenu, msije mkachukuliwa na kosa la hao wahalifu mkaanguka na kuuacha uthibitifu wenu.
  NIMEFURAHIA MJADALA HUU NAMI NATAMANI KUCHANGIA
  NILICHOJIFUNZA NI KUWA KATIKA MJADALA HUU YAPO MAKUNDI MAKUU MAWILI

  MOJA LINATETEA SABATO LINADAI BADO WAKRISTO INAWAPASA KUIHESHIMU SIKU HIYO AMBAYO WANADAI NI JUMAMOSI

  LINGINE LINAIPINGA SABATO KWA HOJA NYINGI NAMI NAORODHESHA BAADHI
  1) SABATO NI YA WAYAHUDI SI WAKRISTO
  2) SABATO NI KIVULI CHA SABATO IJAYO YA KRISTO
  3) YESU ALIIVUNJA SABATO
  4) WAKRISTO HAWAPASWI KUTII AMRI KUMI
  5) KUTUNZA SABATO AU KUSHIKA SHERIA NI LAANA
  6) SHERIA NI LAANA

  Nimegundua makundi haya yote mawili yaliwahi kufundishwa na wachungaji ,wahubiri,makasisi na viongozi wengine wa dini pia makundi haya yanasoma bibilia japo si kwa kiswango sawa.

  mimi nayatazama makundi haya kama matokeo au utimilifu wa utabiri wa paulo (matendo20:28,2timotheo4:2-4) na petro (2petro3;15-17)
  Nagundua lipo kundi ambalo ni matokeo ya kazi za mbwamwitu na lipo kundi la Mungu (matendo20:28-30)
  Nagundua lipo kundi la imani ya kweli lenye umoja na lipo kundi linaloundwa na makundi makundi yenye waalimu tofauti tofauti na mitizamo tofaut japo linasmama kuipinga kweli(2timotheo4:2-3)
  Nagundua lipo linalotumia nyaraka za Paulo kupotosha watu kwa kuzitafsiri visivyo pia hupotosha maandiko mengine(2petro3:15-17) na lingine halipotoshi maandiko
  Nagundua kundi moja linaitwa wahalifu nisijue wanaarifu nini labda majo ya swala wanalohalifu lipo(Isaya58:13) na linge linadumu katika uthibitifu wao(2petro3:17) KAMA UNACHUNGUZA VIZURI UTAGUNDUA WAPI WANASEMA UKWELI KWA KUZINGATI SIFA ZAO ZILIZOTAJWA NA MANABII WA MUNGU LABDA NITAKUWA MCHOYO WA FADHILA NISIPOKUACHA NA FUNGU LINALOFAFANUA SIFA ZA MBWAMWITU ILI IKUWIE VYEPESI KUWAJUA
  EZEKIELI22:23 Neno la Bwana likanijia, kusema,
  24 Mwanadamu, uiambie nchi, Wewe u nchi isiyosafika, wala kunyeshewa mvua siku ya ghadhabu.25 Fitina ya manabii wake imo ndani yake, kama simba angurumaye akirarua mawindo; wamekula roho za watu; hutwaa kwa nguvu hazina na vitu vya thamani; wameongeza hesabu ya wajane wake ndani yake .26Makuhani wake wameihalifu sheria yangu, wametia unajisi vitu vyangu vitakatifu; hawakuweka tofauti ya vitu vitakatifu na vitu vya kutumiwa sikuzote; wala hawakuwafundisha watu kupambanua vitu vichafu na vitu vilivyo safi, nao wamefumba macho yao, wasiziangalie sabato zangu, nami nimetiwa unajisi kati yao.27 Wakuu wake kati yake wamekuwa kama MBWA MWITU wakirarua mawindo; ili kumwaga damu, na kuharibu roho za watu, wapate faida kwa njia isiyo halali.
  28 Na manabii wake wamewapakia chokaa isiyokorogwa vema, wakiona ubatili, na kuwatabiria maneno ya uongo, wakisema, Bwana MUNGU asema hivi; iwapo Bwana hakusema neno.
  NENO MBWAMWITU NIMELIANDIKA KWA HERUFI KUBWA KUKUKUMBUSHA ALILOSEMA PAULO KWENYE (matendo20:28-30) SIFA ZA MBWAMWITU SASA UMEZIFAHAMU JE UPO TAYARI KUENDELEA KUDANGANYWA NA KUPOTEZWA. YESU ANASEMA ufunuo18:4 Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake. UBARIKIWE YESU ANAKUPENDA

 35. matendo20:28Jitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake, mpate kulilisha kanisa lake Mungu, alilolinunua kwa damu yake mwenyewe.29 Najua mimi ya kuwa baada ya kuondoka kwangu mbwa-mwitu wakali wataingia kwenu, wasilihurumie kundi;
  30 tena katika ninyi wenyewe watainuka watu wakisema mapotovu, wawavute hao wanafunzi wawaandamie wao.

  2timotheo 4:2 lihubiri neno, uwe tayari, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho. 3 Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia waalimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti;
  4 nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo

  2petro3:15 Nanyi uhesabuni uvumilivu wa Bwana wetu kuwa ni wokovu, kama vile na ndugu yetu mpenzi Paulo alivyowaandikia kwa hekima aliyopewa;
  16 vile vile kama katika nyaraka zake zote pia, akitoa humo habari za mambo hayo; katika nyaraka hizo yamo mambo ambayo ni vigumu kuelewa nayo; na mambo hayo watu wasio na elimu, wasio imara, huyapotoa, kama vile wayapotoavyo na maandiko mengine, kwa uvunjifu wao wenyewe.
  17 Basi, wapenzi mkitangulia kujua hayo, jilindeni nafsi zenu, msije mkachukuliwa na kosa la hao wahalifu mkaanguka na kuuacha uthibitifu wenu.
  NIMEFURAHIA MJADALA HUU NAMI NATAMANI KUCHANGIA
  NILICHOJIFUNZA NI KUWA KATIKA MJADALA HUU YAPO MAKUNDI MAKUU MAWILI

  MOJA LINATETEA SABATO LINADAI BADO WAKRISTO INAWAPASA KUIHESHIMU SIKU HIYO AMBAYO WANADAI NI JUMAMOSI

  LINGINE LINAIPINGA SABATO KWA HOJA NYINGI NAMI NAORODHESHA BAADHI
  1) SABATO NI YA WAYAHUDI SI WAKRISTO
  2) SABATO NI KIVULI CHA SABATO IJAYO YA KRISTO
  3) YESU ALIIVUNJA SABATO
  4) WAKRISTO HAWAPASWI KUTII AMRI KUMI
  5) KUTUNZA SABATO AU KUSHIKA SHERIA NI LAANA
  6) SHERIA NI LAANA

  Nimegundua makundi haya yote mawili yaliwahi kufundishwa na wachungaji ,wahubiri,makasisi na viongozi wengine wa dini pia makundi haya yanasoma bibilia japo si kwa kiswango sawa.

  mimi nayatazama makundi haya kama matokeo au utimilifu wa utabiri wa paulo (matendo20:28,2timotheo4:2-4) na petro (2petro3;15-17)
  Nagundua lipo kundi ambalo ni matokeo ya kazi za mbwamwitu na lipo kundi la Mungu (matendo20:28-30)
  Nagundua lipo kundi la imani ya kweli lenye umoja na lipo kundi linaloundwa na makundi makundi yenye waalimu tofauti tofauti na mitizamo tofaut japo linasmama kuipinga kweli(2timotheo4:2-3)
  Nagundua lipo linalotumia nyaraka za Paulo kupotosha watu kwa kuzitafsiri visivyo pia hupotosha maandiko mengine(2petro3:15-17) na lingine halipotoshi maandiko
  Nagundua kundi moja linaitwa wahalifu nisijue wanaarifu nini labda majo ya swala wanalohalifu lipo(Isaya53:13) na linge linadumu katika uthibitifu wao(2petro3:17) KAMA UNACHUNGUZA VIZURI UTAGUNDUA WAPI WANASEMA UKWELI KWA KUZINGATI SIFA ZAO ZILIZOTAJWA NA MANABII WA MUNGU LABDA NITAKUWA MCHOYO WA FADHILA NISIPOKUACHA NA FUNGU LINALOFAFANUA SIFA ZA MBWAMWITU ILI IKUWIE VYEPESI KUWAJUA
  EZEKIELI22:23 Neno la Bwana likanijia, kusema,
  24 Mwanadamu, uiambie nchi, Wewe u nchi isiyosafika, wala kunyeshewa mvua siku ya ghadhabu.25 Fitina ya manabii wake imo ndani yake, kama simba angurumaye akirarua mawindo; wamekula roho za watu; hutwaa kwa nguvu hazina na vitu vya thamani; wameongeza hesabu ya wajane wake ndani yake .26Makuhani wake wameihalifu sheria yangu, wametia unajisi vitu vyangu vitakatifu; hawakuweka tofauti ya vitu vitakatifu na vitu vya kutumiwa sikuzote; wala hawakuwafundisha watu kupambanua vitu vichafu na vitu vilivyo safi, nao wamefumba macho yao, wasiziangalie sabato zangu, nami nimetiwa unajisi kati yao.27 Wakuu wake kati yake wamekuwa kama MBWA MWITU wakirarua mawindo; ili kumwaga damu, na kuharibu roho za watu, wapate faida kwa njia isiyo halali.
  28 Na manabii wake wamewapakia chokaa isiyokorogwa vema, wakiona ubatili, na kuwatabiria maneno ya uongo, wakisema, Bwana MUNGU asema hivi; iwapo Bwana hakusema neno.
  NENO MBWAMWITU NIMELIANDIKA KWA HERUFI KUBWA KUKUKUMBUSHA ALILOSEMA PAULO KWENYE (matendo20:28-30) SIFA ZA MBWAMWITU SASA UMEZIFAHAMU JE UPO TAYARI KUENDELEA KUDANGANYWA NA KUPOTEZWA. YESU ANASEMA ufunuo18:4 Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake. UBARIKIWE YESU ANAKUPENDA

 36. Siyi,
  Narudia kukuambia, unahitaji UTAKASO NA WOKOVU kutoka kwa BWANA YESU KRISTO.
  Maneno yako YASIYOMSAIDIA MHITAJI hayana maana.
  Mwenye Akili timamu anelewa kuwa HUJAJIBU HATA SWALI MOJA kati ya Maswali niliyokuuliza.Zaidi ya yote umeleta NGONJERA za WILLIAM MILLER na ELEN G. WHITE ambazo WASABATO ndio wamejaliwa kuziimba.
  Naona WASABATO Wenye UFAHAMU kama OSWARD na WASABATO wengine WALIYAKWEPA HAYO MASWALI kwani wanaujua UKWELI kuliko wewe
  unayethubutu kusema eti ‘Mungu’ ni Msabato!!!
  Unaposema, eti nilete ‘Maswali yenye akili’ inaonesha wazi kuwa huna UFAHAMU wa kutosha katika KUPAMBANUA MAMBO, na hii inathibitisha wazi kwamba
  Umeishiwa/umefilisika kiroho,kimawazo na kimwili.
  WASABATO WENYE AKILI WAMENYAMAZA KIMYA hawataki kujiaibisha kama wewe unavyofanya.
  Wasomaji wa HISTORIA wanaelewa kuwa katika NYAKATI au VIPINDI ambavyo KANISA LIMEPITIA HAKUNA KITU KINAITWA “USABATO” wala MSABATO bali ni mojawapo ya “Cult” iliyoibuliwa na WILLIAM MILLER na ELEN G.WHITE kati ya karne ya 18 na 19.
  Mimi siabudu Jumapili bali NINAMUABUDU BWANA WA SABATO na ninamuabudu KILA SIKU.
  Nashawishika kuamini ASILIMIA 100% kuwa WASABATO si WAKRISTO kwa kuzingatia vigezo vingi vya BIBLIA,( vigezo vingine nimekwishavitaja), na hata wewe mwenyewe umethibitisha hilo kwa kusema ” Mtu anapomwamini Bwana Yesu, daima huwa ni Msabato…”
  Sihitaji kukuuliza Maswali zaidi kwani hata “ABC” bado hujui, utaweza ALGEBRA?
  ***MITHALI 27:22 ” Hata ukimtwanga mpumbavu kwa mchi kinuni pamoja na ngano; Upumbavu wake hautamtoka.” ***

 37. Siyi,

  Naomba upitie hapa:

  1) Wakolosai 2: 16-23
  2)Wakolosai 3:11-13
  3) Wakolosai 3:23-25

  Na hii Wagalatia 4:9-11

  Asante

 38. @Joyce,
  Ha ha ha ha haaa!!
  Hata wewe unachekesha sana Joyce!! Ninachokisema ndicho unachokiamini hata wewe!! Ngoja nikwambie kidogo leo!! Kanisa lina mfumo na utawala wa kifamilia. Ni familia kubwa ile!! Jinsi unavyoilea familia yako ukiwa kama baba/mama wa mji, ndivyo utakavyolilea hata kanisa!! Ukiwa punguani usiyejua kulea vyema familia, utawezaje kulilea kanisa?? Na mambo haya yoooote, yamewekwa bayana kwenye Biblia Joyce!!
  Mimi ni mwanaume, ambaye kwa mujibu wa Biblia, napaswa kujifunza kuchukua majukumu yangu yaliyoko kwenye Biblia kwa familia yangu (bila kujali kama ninayo kwa sasa ama la). Najua unafahamu kuwa familia zote zina changamoto za hapa na pale!! Hata ya kwako (kama unayo), inazo tu!! Mbona hujazisema hapa!! Najua unafahamu ethics zake!! Na mojawapo ya ethics za Baba ndani ya nyumba, ni kufundisha na kutiisha familia yake -kutosemasema mambo ya ndani ya familia yake kwa watu wa nje!! Hata kama kuna matatizo ya hapa na pale, mtu wa nje hapaswi kujua. Akija kwangu akawa mmojawapo wa wanafamilia, ndipo atajua sasa na tutamwambia namna tunavyopambana na changamoto hizo ili na yeye aelewe kudeal nazo!! Hivi ndivyo tunavyoishi kwa kuuakisi mpango wa Mungu!! Mambo ya ndani ya familia ya Mungu, ni ya kushughulikia ndani kwa ndani na si kwa kuyatoa nje!! Na Biblia iko wazi katika hilo!! Au unataka aya??
  Kama mimi kwa kukataa kuzungumza matatizo ya wasabato hapa mtandaoni, kanisa la wasabato limekuwa ni waongo, basi acha na liwe!! Lakini mimi najua kuwa, kukataa huko, nazingatia matakwa na ethic za maadili ya viongozi wa familia ambao ndio viongozi wa makanisa pia!! Sifa za kiongozi mzuri wa familia, ndizo zinapaswa kuwa sifa za kiongozi mzuri wa kanisa!!
  Hata siku ile nilisema kuwa, ukiona msabato anazini, anaiba, anavunja sabato n.k., msaidie tu!! Ukimuona anamnyanyasa mkewe, msaidie ndugu yangu!! Hiyo ndiyo dini!! Tunachojifunza hapa, siyo madhaifu ya watu mmojammoja, bali tunajifunza habari za Kweli ya Biblia, ambayo ndiyo tunapaswa kuifuata. Tukianza kuwafuata watu, hatima yetu itakuwa matatani!!
  Ubarikiwe sana
  Siyi

 39. @Pandael,
  Kwanza, kama sijatakaswa, sijaokoka, naropoka, nimefiliska kiroho na kimwili, kimsingi haya hayatakusaidia lolote ukijua kama ninayo!! Hata mimi yatosha kukwambia kuwa wewe ni fedhuli!! Hilo tu linatosha kwako!!
  Pili, nimekwambia kuwa, maswali ya kifedhuli kama hili “Nilikuuliza swali hili;Ni wapi kwenye Biblia kuna neno MSABATO?Unaona pumba uliyoingea badala ya kujibu Maswali uliyoulizwa?” Sitayajibu maana hata wewe mwenyewe una majibu yake!! Haya ni maswali ya kipuuzi!! Huwezi kuuliza embe ni nini bila kuujua mti unaozaa embe!! Wewe vipi bro!! Yaani mtu mzima kabisa bado unang’ang’ana kabisa, eti, mtanzania ameandikwa wapi kwenye katiba, ilhali hata Tanzania yenyewe huifahamu!!! Inawezekana kweli kwa watu wazima!! Kama si ufedhuli ni nini huo basi!! Nilikujibu kwa ustaarabu kabisa kama ungekuwa na akili, usingeendelea kuuliza maswali ya namna hii!! Nilikwambia kuwa, wewe hebu nioneshe hata aya moja, inayotaja jumapili, kabla sijakuuliza kunionesha neno mjumapili ndani ya Biblia!! Umeleta mashairi ya Abunuwasi!! Kama si ufedhuli, ni nini rafiki!!
  Tatu, usabato masalia, matengenezo, unafiki, nk., unaujua wewe!! Kama Siyi ana injili mfu, unayejua ni wewe!! Kuwasifia wenzako kwa namna wanavyoleta hoja, wakitetea wanachokiami, sikuona kama ni kosa!! Mtu akifanya vizuri, kumsifia ni vizuri!! Hata wewe ungeuliza maswali yenye akili, ningekusifia tu!! Kama unaona mimi ni mnafiki, jiangalie wewe zaidi!! Ukisema kuwa nijiondoe kwenye blog, kisa wewe hujakubaliana na majibu yangu, huoni kuwa wewe ndiyo mwenye tatizo!! Moderators wa SG wanayaruhusu machapisho yangu kwa muda mrefu tu, unafikiri kama ni mafundisho mfu, wangeeendelea kuyaruhusu!!?? Anyway, kama unaweza kuwaambia hoja mathubuti za kutoyaruhusu mapachiko yangu kuanzia sasa kwa sababu sijakujibu vizuri (kama unavyodhani), waambie sasa wayazuie!! Na nikiandika kweli nisiyaone, si nitaacha tu!! Kwani shida ni nini!!?? Kwani ni blog yangu hiyo!! Inakupasa kuwaelewa watu ndugu yangu!! Ukiwaendea kama unavyodhani wewe, watakuacha tu bila ya kuambulia chochote!! Uliza maswali yenye akili, utajibiwa kiakili pia!! Na huu ni udhaifu wa kibinadamu ambao huwezi kuukosa kwa kila mtu. Ni changamoto yetu sote, maana sharti tuishinde!! Biblia inasema, “Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema” – Warumi 12:21. Mimi linanihusu, hata wewe unayedhani kuwa una injili hai, mzee jitathmini!!
  Nne, akina Miller na Ellen G. White hawatakusaidia lolote. Nimekwambia kuwa, hao sio waanzilishi wa kanisa la wasabato. Sasa unachotaka ni nini zaidi?? Au kuijua Biblia ni kuwajua akina Miller na Ellen G. White? Kama niko uchi, poa!! Wasamaria wakiona, watanivika nguo!! Wakiniona nina njaa ya neno la Mungu, watanilisha!! Wakiniona sina uwezo wa kujibu maswali yako tu(ya kifedhuli), ni heri kuchukua pima kuliko shubiri kabisa!!
  Neema ya Bwana ikufunike.
  Siyi

 40. Duh,

  Kumbe wasabato wana mambo mengi huko ndani. Yaani ile minyoo ya nywele za wanawake wa kisabato kumbe ina siri eh!!?

  Siyiiiiii!

 41. Siyi

  Unachekesha kwa MUNGU hakuna siri sasa kumbe mna mambo ya siri ya ndani watu wasijue hilo si kanisa Pole sana .

  Hata ufalme wa Mungu u wazi kwa kila jambo ili uchague uingie au usiingie sasa wewe kufanya siri kwa jema washanganza pole baki na usiri wenu. Ndo mana mnatesa wake zenu kwa kuwanyoa denge na nyie mwapendeza kwa suti na kuchukua vimada wabandika nyweleeee kisa siri za Elen G White hii kaliiiiiiiiiiiiiiiii

  Kila la Kheri

 42. Siyi,Naona unaendelea ‘kutapika’ Theolojia ya Kisabato iliyokufa.Sihitaji kujua wewe ni mwanaume au mwanamke kwa sababu hainisaidi kitu.Naelewa kuwa Umeishiwa/umefilisika kiroho,kimawazo na kimwili ndio maana unapayuka/unaropoka.Narudia kusema hujatakaswa na haujaokolewa na hili linathibitishwa na kauli zako pamoja na mafundisho yako ya kuzimu.Kuonesha kuwa huelewi hata ulichoulizwa unazungumza kuwa ‘SABATO’ ipo kwenye BIBLIA, aliyekuuliza “SABATO” ni nani?Hili linathibitisha kwamba Unahitaji UTAKASO na WOKOVU kutoka kwa Bwana Yesu.Nilikuuliza swali hili;Ni wapi kwenye Biblia kuna neno MSABATO?Unaona pumba uliyoingea badala ya kujibu Maswali uliyoulizwa?Pia umetumia ujanja wa Ibilisi wa kuniambia niwe kama akina Joyce,Lwembe…nk…ili niweze kujifunza Kwangu mimi Mafundisho yako ni UPAGANI ULIOBANDIKWA JINA LA DINI YA KIKRISTO.Huwezi kunilisha MATANGO MWITU na kunifundisha ‘injili mfu’ ya Kisabato ya akina WILLIAM MILLER na ELEN G. WHITE ili niwe Mkristo huko ni kunirudisha kwenye UPAGANI.Halafu wewe ni mnafiki (yaani unafanana na KUNGURU mwenye rangi nyeupe na nyeusi) kwa sababu ulikuwa ulikuwa unamponda Lwembe kwa kile anachoamini kama vile UZAO WA NYOKA,KUTIMILIZA TORATI….,halafu bado unamsifia!! Unaposema tusijadili Dhehebu la mtu ni sawa na tumzungumzie Bwana Yesu bila kumtaja Shetani hivyo kama hutaki Dhehebu la Kisabato kuzungumzwa hapa, ni heri ujiondoe katika “blog” hii kwani kinachotakiwa hapa ni INJILI HALISI na si injili ya WASABATO MASALIA NA WASABATO MATENGENEZO waliochanganyikiwa na wanaokana Maandiko kutokana na kulishwa MATANGO MWITU na kujiona wao ni WAYAHUDI kimwili na kiroho!!Umejibaraguza kuwa, eti wewe una uwezo wa kujibu maswali wakati ulichojibu katika Maswali yangu ni ‘pumba’ tu na habari za WILLIAM MILLER na ELEN G. WHITE ulikwepa kwa sababu unajua ungejiangamiza.Pia sijakulazimisha ujibu maswali yangu kwani uwezo wa kujibu hayo Maswali huna na pia KWELI YA MUNGU (NENO LA MUNGU) haimo ndani yako.Vilevile huwezi kupangua hoja zangu kwa sababu Ibilisi amekunyang’anya Neno La Mungu ambalo ni Vazi, hivyo uko Uchi (huna Neno la Mungu) UFUNUO 3:17-18.

 43. Joyce,
  Unashangaza kidogo dada!! Ellen G. White siyo Mungu!! Sisi tunamwabudu Mungu – YEHOVA!! Kama YEHOVA ni Ellen G. White, basi nisikatae!! Lakini kitakuwa ni kichekesho kweli!!
  Aidha, Nembo ya kanisa haina wokovu!! Hata kama kanisa lisingekuwa na nembo, bado lingeendelea kuwa kanisa tu!! Makundi ya wasabato hayatakusaidia kadhalika!! Lililopo ni wewe kumtafuta Mungu kwa bidii tu!! Na nilidhani kuwa hii ndiyo ingekuwa shabaha ya kila mtu -kumtafuta Mungu!! Wewe kama unakalia kujadili kanisa la wasabato, makundi yao, nembo yao n.k. endelea tu, maana una uhuru huo!! Mimi nimekataa kwa sababu, ukiwa mwanafamilia unayetoa siri za nyumbani hadharani kwa watu, unakuwa mjinga!!! Na mimi sitaki kuwa mjinga!! Natambua kuwa kama ilivyo kwa madhehebu mengine, ndani ya kanisa la Wasabato kuna changamoto za hapa na pale!! Na sidhani kama ni sahihi kujadili changamoto hizo, badala ya kupoteza muda mwingi kumtafuta Mungu!!
  Mungu akubariki sana. Kumbuka, kuwa msabato ni mojawapo ya kigezo kikuu cha kupata tiketi ya kuurithi uzima wa milele. Madhehebu mengine, ni mawakala tu wa yule adui!! Hakuna wokovu huko!! Ni ngumu kuamini, lakini ukweli ndiyo huo!!
  Ubarikiwe sana.
  Siyi

 44. Duh Siyi,

  Umenipa burudani ya kicheko jioni ya leo mpaka basi. Nimecheka kwa kweli.

  Umebenjuliwa na Pendael kwenye nyonga nini mzee?
  Yaani umefoka na kutema cheche mpaka basi.

  Hasa kuambiwa kuwa hujatakasika naona imekuuma sana. Lol, hatari!!!

  Lakini nikwambie ukweli kuwa, hujafikiri sawa kabla ya kutoa mfoko.

  Katika kufoka kwako ndo unejitoa kabisa akili na kuongea hovyo kuliko huko nyuma ambako angalao umeongea ngonjera.

  Kwanza unamwambia kuwa hutaki injili za michapo (japo sijui kama neno michapo umelitumia sawa hapa), lakini wewe katika kumjibu kwako style na lugha uliyotumia ni mithili ya mipasho ya watu wa pwani.

  Hebu fikiria, ivi mtu anayemwambia mwenzake kuwa ni fedhuli na anayemwambia mwenzake kuwa hajatakaswa lipi ambalo si la kibiblia zaidi?

  Tena ona unavyolipuka nje ya key kabisa: Pendael kakutaka umwonesha mahali ambapo kuna neno “Msabato” kwenye maandiko, lakini wewe unakuja kumwambia habari za neno “Sabato”, tena ukisema limesemwa mara 145.
  Huko siyo kuimba ngonjera ni nini?

  Kisha unataka akuoneshe neno “Jumapili” kwenye maandiko. Hii inahusiana nini na suala la wewe kuonesha neno msabato Siyi? This is out of key brother.

  Kingine cha ajabu umekisema kikanikumbusha mwalimu wangu mmoja chuoni aliyekuwa anssema hivi;- ukikosa swali la kujibu kwenye pepa, basi tunga swali la kwako unaloweza kulijibu na ulijibu, angalao naweza hata kukufikiria nikupe alama ngapi kwa kile ulichoandika, kuliko kukusanya answersheet isiyoandikwa chochote.

  Siyi umeshindwa kujibu alichokuuliza Pendael, lakini unaanza kumfundisha au kumtungia maswali unayotaka akuulize, maana hayo ndo una majibu yake.

  Unamwambia aulize maswali ya kwa nini wasabato mnanyoa denge, kwa nini mnakataza watu kula vyakula vilivyotakaswa, n.k! Kwani kakwambia hayo hajui najibu yake?

  Halafu kwa fikra hiyo,unamwambia aliyekwambia kuwa hujatakaswa kuwa anatakiwa kupelekwa Milembe, bila hata kuona kuwa kumwambia mtu apelekwe Milembe laweza kuwa neno baya zaidi kuliko wewe kuambiwa hujatakaswa!!!

  Onesha neno “Msabato” limeandikwa wapi, usituoneshe neno “Sabato” maana hatujataka hilo.

 45. Siyi,

  Mama Elen G White Mnamuabudu usikataee, umekataa kutoa maelezo ya nembo yenu tatizo umelijua kua nyie ni wababaishaji hamjitambui .

  umeshindwa elezea makundi katika kanisa umejua nyie mna shida kubwa kazi kunyonya watu na kutaka wawe maskini tu.

  Mna ubinafsi sana .

  KARIBU KITIMOTO

  Asante

 46. Pandael,
  Kwanza, naona kama unaumwa rafiki yangu!! Sina uhakika kama uko mzima!! Kama vipi tukupeleke milembe!! Huwezi kusema Siyi sijatakasika, kisa nimetangua uelewa wako kuhusu akina Miller na Ellen G. White!! Una kipimo cha kupima kutakasika kwangu? Halafu wewe uko zizi lingine, na mimi lingine na wachungaji wetu ni tofauti, unafikiri kweli kwa mawazo yako, unaweza kupima utakaso wa mtu?? Tafadhali sana acha ufedhuli Pandael!! Sitaki injili yenu ya michapo!! Kama umekosa la kuzungumza kwa mujibu wa Biblia, ni heri ukanyamaza kaka!! Mimi sitaki kujua wewe ni dhehebu gani wala dini ipi!! Na hata siku moja sitapoteza muda kujifunza habari za dini yenu maana hazitanipeleka kokote!! Kama hapa mtandaoni sote tungekuwa tunajadili habari za dini za watu tofauti na kuijadili Biblia, tusingefika kokote!! Tunachokijadili ndugu yangu, ni Biblia then wewe sasa unabaki kujitathimini kama dini yako inashabihiana na kile Biblia inachofundisha!! Ukiona kuna kasoro, unarekebisha!! Nadhani hili ndilo kusudi kubwa la mijadala hii hapa kwenye mtandao –kujengana kiroho kwa njia ya kuiangalia Biblia inasemaje full stop!! Wewe kama una ngonjera zako, kaimbe huko!!
  Pili, mimi sikulishi fundisho hapa!! Na wala sikulazimishi ukubaliane na kile ninachokisema hapa!! Siko hapa kwa ajili hiyo!! Niko hapa tu kwa ajili ya kukifunua kile Biblia inachokisema, then nakuwaachieni fursa ya kutafakari na kuamua kukifuata ama la!!
  Tatu, ndani ya Biblia, kuna Neno Sabato limetajwa mara nyingi sana kuanzia Agano la Kale hadi Agano Jipya!! Kwa ufupi tu, Biblia yote, ina aya 145 zinazozungumzia habari za Sabato tu!! Wewe kama una akili timamu kweli, na una utashi wa kutosha kwa hicho unachokiami, nioneshe hata aya moja tu inayotaja jumapili!! Ukipata hata aya moja tu, una airtel money mwanaume!! Kazana sasa!!
  Nne, sitajadiliana na wewe lolote kama unazidi kuleta mambo ya kifedhuli hapa!! Nikusihi sana kama wewe ni mwanaume au mwanamke mwenye nia ya kujifunza kama ilivyo ada yetu wengine hapa, leta hoja za kibiblia. Toa hoja!! Kwa mfano, sema, ‘Kwa nini wasabato mnazuia watu vyakula eti ni najisi ilhali vimetakaswa vyote?, Au mbona wasabato mnanyoa denge ilhali Biblia imekataa?? Au mbona mnasali Sabato ya Wayahudi ilhali sisi tu wamataifa?? N.k.. Nakuhakikishia akina Siyi tuna majibu ya hoja kama hizi!! Ukiuliza tu, majibu mbashala hayo!! Lakini ukianza kulalama, kuzomea, kutukana na kukejeli n.k., akina Siyi hatutakuelewa!! Katika uandishi wa hoja zako, Muige Joyce, Mhina, Lwembe na wengine wenye shauku ya kujifunza!! Vinginevyo, utabaki kuwa mtu wa vijembe tu, usiye na maana!! Neema ya Bwana ikufunike.
  SIyi

 47. Siyi,Naona UMELOGWA na Theolojia ya Kisabato.Hayo Maneno uliyoyaongea ndiyo yanayayothibitisha kwamba hujatakasika.Hutaki kuwaongelea WILLIAM MILLER na ELEN G. WHITE kwa sababu ndio waliowalisha MATANGO MWITU na pia ndio waliowafunza UKAFIRI mnaoshikilia.USABATO ni imani ya ‘WASTAARABU’ ndio maana wanaume wamekazana kuvaa SUTI na Wanawake WANAKATA NYWELE (PANKI).WASABATO wanakana WOKOVU ndio Maana mmeshia kukariri Maandiko mkafikiri mna Uzima kumbe ‘mmechanganyisha mbegu’ ikawazalia Mauti.Mimi silishwi ‘chakula cha Kunguru’ unachojaribu kunilisha.WASABATO hawabitizi kwa KWA JINA LA YESU KRISTO kulingana na MATENDO 2:38, 8:14-16, 10:48, 19:1-5. Pia WASABATO wanamwamini ‘mungu’ mwenye nafsi tatu, na hili fundisho la ‘mungu’ mwenye nafsi tatu WASABATO wamelitoa kwa ‘ Mama yao’ KATOLIKI (UFUNUO 17:5).Mafundisho mengine ya Kisabato yanayopingana na Biblia ni pamoja na KURUHUSU WANAWAKE KUHUBIRI,KUVIITA BAADHI YA VYAKULA KUWA NAJISI,HAWAAMINI KAMA KUNA KUOKOKA,…nk.Kwa kuwa mmejikita kwenye Ustaabu,endelea kuwafunza ustaarabu wale wanaohitaji.Utawadanya tu wale ambao hawakuwa WATEULE (MATHAYO 24:24). SWALI kwa mtu mwenye ‘akili’ kama wewe ni; NIONESHE NI WAPI BIBLIA IMETAJA NENO MSABATO, kama si unaongea ngonjera tupu.

 48. Pandael
  Kwanza, nilikwambia kuwa, huwezi kuuzungumzia usabato kwa kuambiwa na wachungaji wako wafedhuli!! Wewe endelea kuamini hayo wanayokulisha ukidhani kuna wokovu ndani yake!! Songa mbele kijana!! Kwani ni nani mwenye hasara? Ni Mungu!!!?? Ni Siyi au wewe mwenyewe!!??
  Pili, sijadili habari za akina Ellen G. White na Miller watu ambao hawatanisaidia lolote kwenye wokovu!! Wewe kama unawaamini kuwa ndio waasisi wa wasabato, songa mbele na ufedhuli huo!! Mimi niko hapa kujadili Biblia na Biblia pekee!! Ushahidi niliokupa wa Kibiblia wa mwanzo 1-12, unatosha kabisa kukuthibitishia kuwa Wayahudi asili yao ni Adamu. Na dini yao imekuwa ni usabato tangu zama na zama!! Wewe kama unakimbilia mabaali wa Ashtoreth na Asherah, songa mbele na ibada hizo za kuzimu!!
  Tatu, dini ya Mungu ni dini ya kufikiri/kutafakari!! Ukiona watu wanahimiza tu kuwa rohoni badala ya kufikiri kama yanayosemwa yako sahihi ama la, jua wana kekundu huku wakiamini kuwa wana keupe!! Wameliwa!! Wako chali vibaya!! Bila ya kufikiri, huwezi kujua jema na baya, la uongo na la ukweli!!! Wewe kama unabisha na una ubavu wa kubisha, bishia hayo maandiko niliyokupeni ya mwanzo 1-12. Nilipokwambia nipe muda nikupe majibu stahiki, nilienda kuisoma mwanzo 1-12 ndipo nikaja na majibu!! Sasa wewe ulitaka nije na majibu yepi?? Kama hayo ni uongo, leta yaliyo sahihi unayoyajua wewe!! Acha kusema Siyi mzushi, muongo, nk ilhali hujapangua au kuonesha uongo wake hata mmoja kwa hayo aliyoyasema!! Be smart brother!! Wewe mtu mzima!! Ni aibu kutapatapa unakokufanya hapa!! Zungumza. Jibu hoja, toa hoja!! Kama huwezi, kaa kimya usome ya wengine!!
  Ubarikiwe na Bwana.
  Siyi
  Sabato njema

 49. Siyi,Maelezo yako hayana chochote cha kunisaidia.Nimekutaka Unipe Uthibitisho wa Kibiblia kuhusu Majibu yako Matokeo yake unaongea hovyo. Mara ya kwanza nipokuambia nipe uthibitisho wa Kibiblia kuhusu Majibu yako ‘ulijibaraguza’ kwa kuniambia nikupe muda wa kuleta uthibitisho na hatimaye ukaanza kuleta ‘ngonjera’.Kama ni ‘ufedhuli’ nimeuona kwako kwani unaropoka Maneno usiyoyajua.Wewe unawajua Wachungaji unaowaita mafedhuli Walionifunza kuhusu Usabato?Mbona unaongea kama mtu asiye na ufahamu?WASABATO si Wakristo kwa vigezo vingi na mnakazana kwenda Jehanamu mbiombio kwa mafundisho ‘feki’. Hivi unafikiri unaweza kumpa ‘Hua’ mzoga wa ‘kunguru’ ili aule?Mafundisho yenu ni ya kiakili wala hayana nguvu za Mungu.Mnachohubiri ni Injili Chotara (hybrid gospel) ambayo hayamsaidii anayetaka kwenda Mbinguni.Ufahamu wako umefungwa sana hata neno ‘MMATAIFA’ na ‘MYAHUDI’ huelewi maana yake wala tofauti zake.Haya, hebu tueleze WILLIAM MILLER na ELEN G. WHITE ni nani katika Usabato.WASABATO na WAKATOLIKI na MADHEHEBU mengine ni kitu kimoja.Hivi, unajua unapojiita MSABATO umekwishakufuru na unakuwa ni KAHABA kwa MUNGU?UFUNUO 17:3 ” Akanichukua katika Roho hata jangwani, nikaona mwanamke, ameketi juu ya mnyama mwekundu sana, mwenye kujaa majina ya makufuru, mwenye vichwa saba na pembe kumi.” WASABATO ni mojawapo wa ‘MAJINA YA MAKUFURU na hilo hupelekea kuwa KAHABA kwa Mungu (UFUNUO 17:5).

 50. Pandael
  Kwanza, tatizo ulilonalo kaka, wanalo wajumapili wengi sana!! Wengi sana hujidai kuujua usabato, historia yake, waanzilishi wake, n.k. kwa kusikiliza wachungaji wao makanisani kwao!! Na wengi wameshazungumza maneno ya namna hii kama ya kwako takribani kila sehemu nilipoenda/kujadiliana na wajumapaili!! Hata wewe, sikushangai sana, maana ni jambo ambalo nimekuwa nikiliona kwa macho yangu sehemu ya timu hiyo kubwa ya watu inayoenda upotevuni!!
  Pili, Kama una ushahidi kuwa yote niliyoyasema ni uongo, thibitisha!! Nilikupa sura kadhaa za Biblia ukasome ujiridhishe. Na nikakupa pia vitabu vya historia!! Sasa, uongo umetoka wapi tena!! Mimi nakwambia kuwa, wale waliokufundisha kuwa kanisa la wasabato lilianzishwa na akina Miller na Ellen G. White, walikudanganya!! Hii ni kauli kutoka kwa msabato sasa!! Nataka uelewe hivyo, kuwa sisi hatukuzaliwa na Miller wala Ellen G. White!! Sawa baba!!!?? Kanisa letu lilianzishwa na Mungu mwenyewe!! Shida yako, huna historia sahihi ya kanisa la Mungu!! Na kama utaendelea kuwasikiliza hao wachungaji wako wafedhuli wakikwambia habari za wasabato ilhali wao siyo wasabato, watakupotezeni haswaaa!! Wewe endelea tu!! Unafikiri kuna usalama!! Thubutu!!
  Tatu, wasabato ni kweli kuwa wao ni wayahudi!! Hilo halina ubishi!! Hata wewe utakuwa myahudi tu ukiwa msabato siku moja!! Wasabato ni wayahudi kwa maana ya kwamba, wao ni sehemu ya wayahudi wa leo wa kiroho!! Unapokuwa mkristo, huitwi mmataifa tena!! Wewe vipi?? Biblia imeandika kuwa, tunapokuwa wakristo tu, tunafanyika wana wa Israel (Wayahudi) kwa njia ya imani, -yaani warithi sawasawa na ile ahadi ahadi, -uzao halisi wa kiroho wa Ibrahimu!! Wana wa Israel, ni Wayahudi!! Sasa ukisema kuwa sisi ni Wayahudi, utakuwa sahihi kabisa!! Lakini ukisema kuwa sisi ni wamataifa, aaaah, hapo unakosea sana!! Sisi siyo watu waasi!! Wamataiafa ni watu waasi!! Pole kama ulikuwa huelewi habari hizi!!
  Nne, kwa habri ya unabii wa akina Miller wa kuvaa manyoya, nakupa pole tu. Maana ukiona kipofu anatembea barabarabi huku anafikiri anaona kumbe sivyo, ni vyema ukamshika mkono kumuongoza ili asije akapotea/kutumbukia shimoni. Unabii wa majuma sabini unauelewa rafiki yangu?? Hebu ukokotoe sasa tuone!! Unajua kama ni kukosea hao jamaa walikosea wapi!!!??? Nakushauri, uache kuwasikiliza walimu wafedhuli kukufundisha mambo ya kanisa lingine!! Hao ni walimu wenu tu!! Kwetu watachemka tu tena asubuhi na mapema!!
  Tano, Biblia imesema kuwa Mungu alikuwa ni msabato, Yesu alikuwa ni msabato. Wanafunzi wake unafikiri wao walikuwa ni wajumapili?? Au Yesu kuitwa Kristo, inabadilisha Usabato wake na kuwa ujumapili?? Una aya yoyote kwenye Biblia inayounga mkono ibada za kijumapili tangu kitabu cha mwanzo hadi ufunuo?? Sasa, kama siku zote hizo watu wamekuwa wakiabudu siku ya Sabato, wewe leo unapata wapi ujasiri wa kutudanganya hapa kuwa hata jumapili nayo ni sabato!!?? Yesu alikuwa msabato, Bwana wa Sabato na hata mitume, nao walikuwa ni wasabato, japo walijulikana kama wafuasi wa Kristos – wakristo au kwa jina lingine, Wamasihiya –wafuasi wa Masihi!! Sasa kuitwa hivyo, shida iko wapi?? Wewe ndugu yangu, hata kama utapindaje, ukweli wa Sabato, huwezi kuukanusha hata kama ni kwa dau lenye thamani za pesa za kuujuza ulimwengu huu. Huwezi!!
  Mungu akubariki anapokufunulia nuru ya uso wake kujifunza Neno lake kwa kila kuitwapo leo!! Neema ya Bwana ikufunike.
  Siyi

 51. Joyce,
  Yaelekea unawafuatilia vizuri sana wasabato kama hukuwa msabato kwa huko nyuma!! Zaidi ya hapo, nikupe hongera, maana unauliza maswali ya wasabato!! Maswali hayo unayoyauliza, si rahisi mtu mwingine nje ya imani hiyo kuyauliza!! Wengi huishia tu kwenye udanganyifu wa jumapili kama ndiyo siku maalumu ya ibada, japo ukiwaomba hata aya moja ya kibilia, watakwambia torati iliishia msalabani!! Ukiuwauliza ni torati ipi, maneno huwa mengi na pengine kukukemea ‘ushindwe kwa jina la yesu’. Huwa navunja mbavu kweli!!
  Maswali yako uliyouuliza, ni maswali makubwa sana na marefu mno. Kwa sasa, nikwambie tu hivi, kihistoria, ni jambo la kawaida kuwa na makundi mbalimbali na yenye uelewa tofauti ndani ya kanisa moja!! Hata nyumbani tu, wewe na mumeo (kama unaye), hamfanani kwa kila kitu!! Kwa hiyo wasabato masalia, wa wanawake nk, hao ni wasabato wote!! Ila ndani ya hayo matabaka, wapo walio sahihi zaidi kuliko wengine mbele za Mungu!! Na Mungu anawafahamu!! Nina imani kadri wanavyoendelea kukua katika imani, wenye mtazamo wa kumfuata Mungu, watabainika tu!! Maana kwenda mbinguni, si kwa sababu tu ulikuwa ni msabato!! Bali ni kwa sababu ulikuwa ni msabato, aliyeishi sawasawa na msabato wa kwanza anavyosema-Mungu mwenyewe!!
  Kuhusu nemba ya kanisa na alama zake, hilo ni fundisho gumu sana kulielewa kwa wewe hapa mtandaoni tu!! Labda kama una ufahamu wowote na mwingine tofauti na wa wasabato, nitakushauri tu, tujaribu kuona namna ya kushikirishana na kusaidiana zaidi!! Na tunapotaka kujadili mambo mazito kiasi hicho, tena yanayohusu kanisa moja tu, nisingependa kuyajadili hapa. Labda, wewe leta email yako, tujadiliane huko.
  Ila kama unataka kuwa msabato, kuwa msabato tu tena bila shida yoyote. Baada ya kuwa msabato, jitahidi kuwa mtu wa neno na siyo mtu wa dini!!! Ukiwa mtu wa dini, utapotea tu pamoja na kuwa msabato!! Na wokovu, uko ndani ya wasabato tu, japo si wasabato wote watakaookolewa!! Maana hata kwa wasabato, watu wa yuda 4, wapo!! Ni unabii huo, sharti utimie!!
  Karibu sana dada!!
  Neema ya Bwana ikufunike
  Siyi

 52. Siyi,Nimeamini wewe ni mbabaishaji na Kweli (Neno la Mungu) haimo ndani yako. Unajua ‘Ukishalewa Mvinyo wa Dhehebu lako’ huwezi kutetea Ukweli Wa Neno La Mungu.Majibu yako yote yapo “OP”.Rafiki kwa nini usiwe Mnyofu kusema Kweli kuliko kusema Uongo wa wazi?Kutoka MWANZO hadi UFUNUO hakuna Watu wanaoitwa WASABATO hii ni mojawapo ya ‘Cult’ iliyozuka kati ya Karne ya 18 na 19 na iliasisiwa na WILLIAM MILLER na hatimaye ELEN G. WHITE kama Nabii mwanamke (Kike). Kabla ya ujio wa ELEN G.WHITE, ‘WASABATO’ walikuwa wanaitwa ‘WAMILERI’. Ndiyo maana Dhehebu la Kisabato lina MAFUNDISHO MCHANGANYIKO na Wamekanganyikiwa hawaelewi hata tofauti baina ya Mafundisho ya kweli na ya Uongo.Dada Joyce alipokugusia habari za Elen G. White ulilijibu kiakili sana na hukukanusha kuhusu nafasi yake katika Usabato kama nabii.Wasabato mnajifanya ninyi ni ‘WAYAHUDI’ na kutotambua kuwa ninyi ‘WAMATAIFA’ ndiyo kwa Kujaribu kuangalia ‘MAJUMA SABINI YA DANIELI’ kiakili WAMILERI (WASABATO) walijivika Manyoya bandia ili wakamlaki YESU angani wakajikuta WAMELOWA UMANDE na Manyoya yamenyonyoka.HAYO MASWALI SIVYO KAMA UNAVYOFIKIRI.Umenialika nikuulize Maswali mengine hebu jibu kwanza hayo niliyokuuliza kwa usahihi kuliko kuyajibu ilimradi.Nimekutaka unipe Ushahidi wa Kibiblia (Biblical Evidence) kwa Majibu yako bado umetumia ujanja uleule wa Mwanzo.Wanafunzi waliomwamini Bwana Yesu waliitwa “WAKRISTO” si Wasabato kama unavyosema wewe, MATENDO 11:26.”……….Na wanafunzi waliitwa Wakristo kwanza hapo Antiokia.”

 53. Siyi,

  Angalau umekubali makosa asante.

  Hebu niambie haya matabaka yenu ya WASABATO MASALIA,WASABATO WANA MATENGENEZO, WASABATO WANAORUHUSU MWANAMKE KUHUDUMU , NA WASABATO WASIORUHUSU WANAWAKE KUHUDUMU.

  Pia MAANA KAMILI NA VIELELEZO VYOOTE VILIVYO KATIKA NEMBO YENU YA SDA CHURCH USILUKE HATA KIMOJA NA KWANINI KIPO PALE KATIKA NEMBO HIYO.

  Asante

 54. @ Pandaeli
  Maswali yako nimeyasoma tena na tena, nikaona yooote yamejengwa kwenye kitabu cha Mwanzo sura ya 1 hadi ya 12 tu!! Nikushauri usome historia ya sura hizo. Nakupendekezea kitabu kizuri cha kusoma ukaeewa ni Biblia yenyewe, Patriches and Prophets (1890) ukurasa wa 1 hadi ya ukurasa wa 125 kwenye sura ya The Call of Abraham…. Baada ya kukisoma kitabu hiki, rudia tena kuisoma Biblia yako ili kujihakikishia kile kilichoandikwa ndani ya kitabu hiki kinaakisi yaliyomo ndani ya Biblia. Mungu akutangulie katika hilo!!

  Maswali
  1.WAYAHUDI ni WASABATO?
  Jibu
  Wapo waliokuwa Wasabato na wapagani!! Wale Wayahudi waliofuata imani ya baba yao Ibrahimu (Myahudi wa kwanza), walikuwa ni wasabato. Wale waliokiuka imani na mafundisho ya Ibrahimu baba yao, walikuwa ni waasi, ndiyo maana baadhi yao hawakumwamini hata Masihi alipokuja!! Kwa sasa, Wayahudi wengi ukienda Yerusalemi, siku ya Sabato utajionea mwenyewe!! Maduka hayafunguliwi, shule haziendeshwi, na kila shughuli husimama kabisa siku ya Sabato kwa taifa zima, japo waasi wapo tu!!
  Uthibitisho wa jibu hili kibiblia
  Kwanza, ufahamu kuwa, chanzo cha Wayahudi, ni uzao wa Adamu na mkewe!! Baada ya mgawanyiko wa lugha hapo kwenye mnara wa Babeli, palikuwa na mtu mmoja jina lake Tera!! Soma historia ya zama za mfalme Nimrodi aliyejitangaza kuwa na yeye ni mungu!! Tera ndiye baba wa Ibrahimu. Mnyororo wa imani, uchaji Mungu sahihi ulikuwa ukiendelezwa na watu wachache sana pale uaasi ulipoonekana kuongezeka!! Soma histora nzima kuanzia Adamu utaona!! Hata hao watoto wa Tera (enzi za utawala wa Nimrodi), nao waligawanyika!! Mmoja wao alikuwa ni Abram, baadaye Ibrahimu!! Hawa wototo wote, walililelewa katika malezi ya usabato, dini ya baba zao tangu Adamu. Lakini pamoja na malezi hayo mazuri, waasi bado walikuwepo!! Na Mungu alijidhihirisha kwa hao waaminifu wachache waliojitoa kikamilifu kumfuata na kumtii Mungu wa baba zao!! Kwa hiyo, Wayahudi, dini yao ya kwanza, ilikuwa ni usabato, ambao waliurithi kutoka kwa vizazi vya Adamu, mwanadamu msabato wa kwanza!! Wayahudi, walikuwa ni wasabato –Soma mwanzo 1-11 na umalizie na sura ya 12 utamkuta Ibrahimu hapo (Abram) ili ujipatie maarifa zaidi

  2.WASABATO walitokea wapi na mwaka gani?
  Jibu
  Wasabato walitokana na Mungu mwenyewe baada ya kuwapatia wazazi wetu wa kwanza maagizo na taratibu za namna ya kuishi baada tu ya uumbaji. Mungu aliye msabato wa kwanza (mwanzo 2:1-3), aliwaambia watu kuishi sawasawa na maagizo yake likiwemo la kuwa wasabato. Kwa hiyo, wasabato walitokea kwa Mungu pale Mungu alipoizindua Sabato kwa mara ya kwanza siku ya saba, mwezi wa kwanza na mwaka wa kwanza (leo tungeita tarehe 7/1/1). Hii ndiyo tarehe inayoaminika kuwa Mungu pamoja na Adamu na mkewe, walimpumzika siku ya Sabato. Adamu na mkewe wakimwabudu Mungu na kumsifu. Mungu akipokea sifa, ibada na shukrani kutoka kwa ma-couple hao!!
  UShahidi
  Nadhani hili halihitaji maelezo zaidi kwa mujibu wa ushahidi wa kwanza hapo juu!!
  3.WASABATO wanapatikatana wapi Kwenye BIBLIA?
  Jibu
  Wasabato wanapatika kuanzia kitabu cha Mwanzo hadi cha ufunuoa ndani ya Biblia. Kila kitabu kilichotaja habari za Amri 10 za Mungu, kimetaja na Sabato pia maana Sabato ni mojawapo ya amri 10 za Mungu. Wale woote ambao wamekuwa wakitii amri 10 za Mungu kuanzia Agano la Kale hadi Jipya, hao wote ni wasabato. Ndani ya Biblia nzima, hakuna watu waliomwabudu Mungu akafurahi na kutambua ibada yao tofauti na wale walioabudu siku ya Sabato kwa kufuata taratibu zote za ibaada wakizitii na amri zingine kwa ukamilifu wote.
  UShahidi
  Na hili nalo yaleyale. Nimesema Wasabato wanapatikana kwenye Biblia nzima!! Anza na sura nilizokupendekezea hapo juu ili uwajue Wayahudi ambao baadaye tunawafahamu kama Waisrael. Dini yao ya tangu Baba yao wa kwanza, ilikuwa ni usabato!!
  4.Mtu anapomwamini BWANA YESU anakuwa MKRISTO au MSABATO?
  Jibu
  Mtu anapomwamini Bwana Yesu, daima huwa ni Msabato japokuwa kuna watu wanamwabudu bure Kristo wakifundishana maagizo yao wenyewe!! Neno Kristo ni neno la Kigiriki –Christós lenye maana ya “Mpakwa mafuta” Kibrania -Masihi. Hivyo Mahisi aliye Bwana wa Sabato, ukimwamini huyo na kuyafuata yote anayoyaagiza kwenye neno lake, daima utakuwa msabato tu!! Vinginevyo kama unatataka kubaki kwenye kundi la watu wa mathayo 7:20-24, au utaamua kumwabudu Kristo mwingine, maana kuna makristo wengi siku hizi.
  5.Nini MAANA ya hili andiko, WAKOLOSAI 2:16-17 ” Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato; mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo” ?
  Jibu
  Maana ya aya hizo ni kwamba, Paulo alikuwa akiwafundisha wakolosai kumwamini Kristo na kuachana na taratibu za kutekeleza sheria za sabato za kafara za miandamo ya mwezi, zilizokuwa zikihusisha watu kujinyima kula na kunywa baaddhi ya vitu ili kujitesa kama ilivyokuwa imeagizwa kwenye torati ya Musa!! Ndani ya Biblia kuna aina nyingi za sabato. Tofauti na Sabato ya siku ya Saba ya kila wiki, kulikuwa na sabato za sdaka za kuteketezwa zilizokuwa zikifanyika kwa vipindi tofautitofauti. Maadhimisho ya sabato za namna hiyo pamoja na mifungo yake, wakolosai walikuwa wakiendelea navyo, japo yalikuwa ni mambo ambayo yalikuwa ni kivuli cha kafara ya Kristo! Hivyo, Sabato ya Amri ya nne, ni tofauti na sabato hizo. Kwa maelezo zaidi, rejea majibu yangu ya leo kwa Mhina, kwenye maada ya KUITIMILIZA TORATI, nimembainishia japo kwa uchache tu aina za sabato ndani ya Biblia.
  Ushihidi
  Kama unaamini kuwa Yesu ndiye aliyeumba mbingu na nchi na vyote vilivyomo, na baada ya uumbaji akaanzisha Sabato, ndiye anayewasihi leo wanadamu walioasi kuurudia utaratibu wa ibada ya Ibada ya Sabato aliouanzisha YEYE mwenyewe bustanini.
  Nadhani utakuwa umenielewa vyema!! Kama una swali particulary, leta!!
  Ubarikiwe sana
  Siyi

 55. Joyce,
  Kwanza, niruhusu nicheke kwanza, ha ha ha ha ha ha !!! Umenifurahisha sana!! Anyway, yote ni majibu uliyotoa!! Huenda kweli tunakosea. Nising’ang’ane tu na hoja yangu. Ila mimi ninachojua ni hicho kwamba, katika Agano Jipya, hakuna cha mchungaji, shemasi, mhazini wa kanisa, mgonga kengele, mrusha matangazo redio redio/TV ya kanisa, mwimbaji n.k., hawa wote, ni watenda kazi shambani mwa Bwana!! Tofauti yao ni majukumu na wadhifa tu!! Ila wote wanaitwa kuwa ni waajiriwa wa kanisa kwa kazi ya kanisa ya kuponya roho za watu. Siku ya Sabato, matangazo ya redio/tv yakiwemo mahubiri, nyimbo n.k, husaidia watu kuwaponya kiroho esp wale ambao hawajafanikiwa kwenda kanisa au wale waliofungulia kwa kutokea tu!! Kazi inayofanywa na chombo hicho, haina tofauti na ile inayofanywa ndani ya kanisa kwa siku za Sabato. Tena matangazo ya redio/tv, huwafikia watu wengi zaidi kuliko wale walio na mchungaji ndani ya kanisa!! Hebu fikiria watu walioko magerezani, wagonjwa mahospitalini, majumbani, walemavu wasioweza kwenda kanisani na hawana msaada wowote wa kuwafikisha huko kona zote za nchi, n.k., isingekuwa vyombo hivi, injili ingewafikiaje?? Au wewe unataka redio/tv, navyo vingetajwa kwenye Biblia?? Niseme tu kuwa ni kweli vimetajwa lakini ni kiunabii sana, na sidhani kama unafahamu hilo!! Ninavyojua mimi, hata kama kuna matangazo mengine ya kibiashara, siku ya Sabato hayatarushwa, badala yake, vipindi na masomo yenye mtiririko wa ibada wa siku ya Sabato, hurushwa hewani ili kuwajumuisha na makundi ya wengine ambao ambao nimewataja hapo juu.
  Pili, taratibu za mahekalu katika agano jipya, hazipo. Patakatifu, patakatifu sana na patakatifu pa patakatifu, ndani ya agano jipya, hakuna!! Ndani ya agano jipya, kuna kanisa dada Joyce!! Na kanisa hilo, linaanza na wewe mwenyewe (mwili wako), ambao ndio nyumba ya Mungu –hekalu la Roho Mtakatifu!! Wasabato tuko makini kiasi hicho (japo si wote) katika maandiko!! Sheria zooote zilizokuja baada ya dhambi, Yesu aliziondoa pale msalabani. Sheria zote zilizokuja kabla ya dhambi, bado zipo hata milele!! Sijui wapi sijaeleweka kwako!! Nitakuomba urejee mahali ambapo nimekuacha ili tueleweshane ndugu yangu.
  Tatu, nashukuru kwa ukarimu. Nitakula ndizi tu na nguruwe sitakula maana Biblia imenionya kuwa “Watu wale wajitakasao, na kujisafisha katika bustani, nyuma yake aliye katikati; wakila nyama ya nguruwe, na machukizo, na panya; watakoma pamoja, asema Bwana”- Isaya 66:17. Nakushauri na wewe uache maana kuna ole imewekwa kwa wale walao vitu najisi ikiwemo nguruwe!Unaunajisi mwili wako ambao ni hekalu la Mungu!! Hatari iliyoje!!!
  Acha mpendwa!! Bwana akubariki sana!!
  Siyi

 56. Siyi,

  Yaaani katika wachemkaji ndo nyinyi, radio sio sehem ya kuabudu hapo ndugu kubalini tu mnachemka maana mnatenda ndivyo sivyo RADIO HAIPO KWENYE BIBLIA NA KUSEMA ETI NI HEKALU LA BWANA NENDA KATUBU DHAMBI HII .NA BWANA MITAMBO YEYE SI MPAKWA MAFUTA ALIEPEWA KIBALI CHA KUTENDA KAZI KAMA WASEMA MCHUNGAJI ANARUHUSIWA .YEYE MCHUNGAJI ANAFANYA KAZI HEKALUNI KWA KIBALI ALICHO PEWA , HUYU MZINZI WA MITAMBO NAE KIBALI HICHO KATOA WAPI ACHA KUDANGANYA WATU KAKA.

  Usijidanganye kupata ajira Morning star eti uko hekaluni hahahahahaaaa wewe muongo kubali kuwa mtalekebisha hilo. Hapa wa Radio one wa Morning star wooote wanafanya kazi .

  Pia hizo Enzi za makuhani mara mseme hamzifati kwa kua YESU alikuja na hayo hayatendwi ya sadaka za kuteketezwa sasa hapa wajitia kufata inshu za mizimu za kale sasa nyie vipi ? YESU AU BADO MNA SADAKA ZA KUCHINJA? MBONA HAULEWEKI AU PENATI IMEKUSHINDA BRO HAAAAA

  Karibu KITIMOTO KAKA NA NDIZI HAPA.

  Asante

 57. @ Joyce,
  Nakushukuru kwa mwitiko!!
  Naomba kujibu swali lako moja kwa moja kama ifuatavyo;
  Swali
  “swali siku hii (sabato) si siku ya kufanya kazi sasa MIMI NIKIAJILIWA RADIO ONE NIKIWA KAMA FUNDI MITAMBO NA WEWE UPO MORNING STAR RADIO KAMA FUNDI MITAMBO WOTEE TUKAENDA KAZINI NANI ATAKUA KAVUNJA SABATO NA NANI HAJAVUNJA . MAANA HII NI KAZI YETU SOTE TUIFANYAYOO KWA SIKU THELATHINI NA MSHAHARA TWALIPWA SIKU 30”??? mabano nimeongeza!
  Jibu
  Kwanza, ni kweli kuwa mshahara mnalipwa kwa siku 30. Je, nikuulize swali, hivi ni kweli kabisa wewe huwa unaenda kazini kwa siku zote 30?? Huna siku ya ibada? Na kama siku ya ibada unayo ambayo huwa unapumzika, je mwajiri wako huwa anakukata mshahara?? Je, mchungaji wako, siku ya ibada kwako na yeye huwa hahesabiki kama yuko kazini? Mpaka hapa unaweza kunotice chochote cha tofauti dada Joyce!!??
  Pili, ngoja twende taratibu. Enzi za Agano la kale, makuhani walifanya kazi hekaluni hadi siku za Sabato na Mungu asiwahesabii kama ni dhambi!! Biblia inasema kuwa, makuhani waliokuwa waajiriwa (wakila madhabahuni), walifanya kazi siku za Sabato. “Tena katika siku ya Sabato watasongezwa wana-kondoo wawili, waume wa mwaka wa kwanza, wakamilifu, pamoja na sehemu ya kumi mbili za efa za unga mwembamba kuwa sadaka ya unga, uliochanganywa na mafuta, pamoja na sadaka yake ya kinywaji; hii ndiyo sadaka ya kuteketezwa ya kila Sabato, zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote, pamoja na sadaka yake ya kinywaji” Hesabu 28:9-10. Je, swali la kjiuliza, kwani Mungu hakujua kuwa kwa makuhani kufanya hivyo siku za Sabato ni dhambi?

  Sikiliza Yesu anavyosema pia;

  “Wala hamkusoma katika torati, kwamba siku ya sabato makuhani hekaluni huinajisi sabato wasipate hatia?” Mathayo 12:5.

  Kwa ufupi tu dada Joyce, Leo hatuna makuhani kama ilivyokuwa agano la kale. Leo tuna watenda kazi tu wanaomfanyia Bwana kazi usiku na mchana!! Walioko morning Star, hawana tofauti na wachungaji wa kisabato au wachungaji wenu wanaofanya kazi siku za ibada!! Tofauti ni imani tu, kwamba wao ni wasabato na ninyi hamuitunzi sabato!! Hata kama ungekuwa ni wewe unafanya kazi morning star redio, bado kwako kufanya kazi hiyo siku ya Sabato isingekuwa ni dhambi maana umo ndani ya shamba lake!! Haya siyo mawazo yangu mimi Siyi!! Ni Biblia yenyewe imesema!!
  Hivyo wewe usiye mtenda kazi wa Bwana (yaani si mwajiriwa wa kanisa), siku ya ibada ukienda kazini kwako, watenda dhambi, full stop!! Ni rahisi tu kiasi hicho dada Joyce!!
  Zaidi ya hayo, nikupe pongezi kwa kuwa msikilizaji mzuri wa vipindi vya morning star redio 1055.3 FM. Endelea kufanya hivyo. Ina vipindi vizuri sana vitakavyobadilisha maisha yako na familia yako!!
  Mungu akubariki sana. Karibu kwa maswali na hoja kama sitakuwa nimeelweka vyema!!
  Neema ya Bwana ikfunike Joyce!!
  Amina
  Siyi
  @ Pandael
  Nashukuru kwa mwitiko wako pia rafiki yangu. Nikuombe kama hukurizika na majawabu yangu, kimsingi itanibidi nifanye ile kazi ya ziada uliyonitaka ya kuthibitisha ukweli wa hicho nilichokiandika kwenye majibu yangu ya msingi!! Na kwa vile ni kazi ndefu, naomba niifanye kazi hiyo muda mwingine (ujao) ili nikutendee haki rafiki yangu. Endelea kujifunza. Tuko pamoja sana. Neema ya Bwana ikufunike pia!!
  Siyi

 58. Siyi , Kama haya majibu ni ya Kweli nithibitishie Kimaandiko (Biblical evidence).Tafadhali naomba majibu ya MISTARI YA BIBLIA yanayothibitisha majibu yako kuliko Kutumia tungo za wanadamu kwa ajili tu ya kutetea DHEHEBU LA KISABTO.

 59. Siyi,

  Asante kwa maelezo yako sasa kama siku ya sabato kazi hazifanyiki ni siku iliyotakaswa kiimani yako safii .

  swali siku hii si siku ya kufanya kazi sasa MIMI NIKIAJILIWA RADIO ONE NIKIWA KAMA FUNDI MITAMBO NA WEWE UPO MORNING STAR RADIO KAMA FUNDI MITAMBO WOTEE TUKAENDA KAZINI NANI ATAKUA KAVUNJA SABATO NA NANI HAJAVUNJA . MAANA HII NI KAZI YETU SOTE TUIFANYAYOO KWA SIKU THELATHINI NA MSHAHARA TWALIPWA SIKU 30.

  Elewa vizuri maelezo hayo maaana naona mnalusha vipindi siku yenu sasa huyo bwana mitambo atokapo nyumbani anasema anaenda Morning star kupumzika na Bwana au kufanya kazi mitambo isikorofishe ili watu wasikie radio yenu ikirusha vipindi vyenu saffiiii .

  Asante

 60. @ Joyce,
  Shalom mjoli!!
  Nimefurahi kukuona umerudi tena.
  Nafurahi kukwambia kuwa, hakuna hata aya moja ndani ya Biblia inayosema kuwa, kushinda kanisani siku ya Sabato ndiyo utunzaji sahihi wa Sabato. Mimi sijaiona aya ya namna hiyo!! Na hakuna ukweli wowote kwamba, mtu akirudi nyumbani siku ya Saabato anashawishika kutenda/kuvunja Sabato!! Uchaji Mungu, hauangaliwi kwa matendo ya nje ndugu yangu Joyce. Kabla ya watu hawajakuona ukitenda dhambi kimwili, Mungu alishakuona zamani sana moyoni mwako. Wanadamu huangalia kwa nje bali Mungu huuangalia moyo!! Utendaji wa dhambi, unapaswa ukome kuanzia kwenye mawazo yetu/fikra zetu, ndipo udhihirishaji kwa nje utakuwa bayana!! Na kuna waumini wengine hutenda dhambi za mawazoni/kifikra bila ya kuzitubu wakifikiri wako salama!! Ni vizuri ushindi dhidi ya dhambi, ukaanzia moyoni/mawazoni kwanza, halafu utiifu na mwenendo mwema kwa nje, ukawa ni matokeo tu ya kile kilicho ndani yetu.
  Na katika kujibu swali lako la pili, nipende kusema kuwa, siku ya Sabato hatupaswi kufanya kazi yoyote ile nje ya utakatifu na utukufu wa Mungu!! Kama wewe ni kiongozi wa kanisa, siku ya Sabato, fundisha waumini kumjua Mungu. Ongoza waumini kufanya mambo mema kama vile matendo ya huruma ya kwenda kuwaona wajane, wagonjwa, waliofiwa n.k. na kuwaombea!! Siku ya Sabato unaweza ukaipangia ratiba za kutenda mambo ambayo Kristo siku ya mwisho, atakwambieni kuwa, “kwa kuwatendea hao walio wadogo, hakika mlinitendea mimi”!! Ikitokea unaenda kanisani siku ya Sabato, njiani ukakutana na mgonjwa sana au mtu yeyote anayehitaji msaada wako, msaidie. Ikiwa ni njaa, mpatie chakula, ikiwa ni fedha, mpatie, ikiwa ni tatizo lolote ambalo unaweza kumsaidia kwa namna yoyote, fanya mtu wa Mungu!! Hayo ndiyo maisha aliyoyaishi Kristo na wanafunzi wake.
  Mkapa hapo, nina imani sijajichanganya mtumishi. Karibu tu tena kama una maswali zaidi!! Neema ya Bwana ikufunike. Uwe na Sabato njema.
  Siyi

  @ Pandaeli na Joyce
  Joyce, ameniomba niyajibu maswali yako kaka. Kimsingi samahani, sikuayaona hapo kabla!! Huenda kwa sababu ninajadiliana na watu wengi kiasi hapa mtandaoni, ndiyo maana yalinipita kidogo. Namshukuru dada Joyce kwa kuyaleta. Nami naomba niyajibu kwa ufupi kabisa.
  Maswali
  1.WAYAHUDI ni WASABATO?
  Jibu
  Wapo waliokuwa Wasabato na wapagani!! Wale Wayahudi waliofuata imani ya baba yao Ibrahimu (Myahudi wa kwanza), walikuwa ni wasabato. Wale waliokiuka imani na mafundisho ya Ibrahimu baba yao, walikuwa ni waasi, ndiyo maana baadhi yao hawakumwamini hata Masihi alipokuja!! Kwa sasa, Wayahudi wengi ukienda Yerusalemi, siku ya Sabato utajionea mwenyewe!! Maduka hayafunguliwi, shule haziendeshwi, na kila shughuli husimama kabisa siku ya Sabato kwa taifa zima, japo waasi wapo tu!!

  2.WASABATO walitokea wapi na mwaka gani?
  Jibu
  Wasabato walitokana na Mungu mwenyewe baada ya kuwapatia wazazi wetu wa kwanza maagizo na taratibu za namna ya kuishi baada tu ya uumbaji. Mungu aliye msabato wa kwanza (mwanzo 2:1-3), aliwaambia watu kuishi sawasawa na maagizo yake likiwemo la kuwa wasabato. Kwa hiyo, wasabato walitokea kwa Mungu pale Mungu alipoizindua Sabato kwa mara ya kwanza siku ya saba, mwezi wa kwanza na mwaka wa kwanza (leo tungeita tarehe 7/1/1). Hii ndiyo tarehe inayoaminika kuwa Mungu pamoja na Adamu na mkewe, walimpumzika siku ya Sabato. Adamu na mkewe wakimwabudu Mungu na kumsifu. Mungu akipokea sifa, ibada na shukrani kutoka kwa ma-couple hao!!

  3.WASABATO wanapatikatana wapi Kwenye BIBLIA?
  Jibu
  Wasabato wanapatika kuanzia kitabu cha Mwanzo hadi cha ufunuoa ndani ya Biblia. Kila kitabu kilichotaja habari za Amri 10 za Mungu, kimetaja na Sabato pia maana Sabato ni mojawapo ya amri 10 za Mungu. Wale woote ambao wamekuwa wakitii amri 10 za Mungu kuanzia Agano la Kale hadi Jipya, hao wote ni wasabato. Ndani ya Biblia nzima, hakuna watu waliomwabudu Mungu akafurahi na kutambua ibada yao tofauti na wale walioabudu siku ya Sabato kwa kufuata taratibu zote za ibaada wakizitii na amri zingine kwa ukamilifu wote.

  4.Mtu anapomwamini BWANA YESU anakuwa MKRISTO au MSABATO?

  Jibu
  Mtu anapomwamini Bwana Yesu, daima huwa ni Msabato japokuwa kuna watu wanamwabudu bure Kristo wakifundishana maagizo yao wenyewe!! Neno Kristo ni neno la Kigiriki –Christós lenye maana ya “Mpakwa mafuta” Kibrania -Masihi. Hivyo Mahisi aliye Bwana wa Sabato, ukimwamini huyo na kuyafuata yote anayoyaagiza kwenye neno lake, daima utakuwa msabato tu!! Vinginevyo kama unatataka kubaki kwenye kundi la watu wa mathayo 7:20-24, au utaamua kumwabudu Kristo mwingine, maana kuna makristo wengi siku hizi.
  5.Nini MAANA ya hili andiko, WAKOLOSAI 2:16-17 ” Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato; mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo” ?
  Jibu
  Maana ya aya hizo ni kwamba, Paulo alikuwa akiwafundisha wakolosai kumwamini Kristo na kuachana na taratibu za kutekeleza sheria za sabato za kafara za miandamo ya mwezi, zilizokuwa zikihusisha watu kujinyima kula na kunywa baaddhi ya vitu ili kujitesa kama ilivyokuwa imeagizwa kwenye torati ya Musa!! Ndani ya Biblia kuna aina nyingi za sabato. Tofauti na Sabato ya siku ya Saba ya kila wiki, kulikuwa na sabato za sdaka za kuteketezwa zilizokuwa zikifanyika kwa vipindi tofautitofauti. Maadhimisho ya sabato za namna hiyo pamoja na mifungo yake, wakolosai walikuwa wakiendelea navyo, japo yalikuwa ni mambo ambayo yalikuwa ni kivuli cha kafara ya Kristo! Hivyo, Sabato ya Amri ya nne, ni tofauti na sabato hizo. Kwa maelezo zaidi, rejea majibu yangu ya leo kwa Mhina, kwenye maada ya KUITIMILIZA TORATI, nimembainishia japo kwa uchache tu aina za sabato ndani ya Biblia.

  Naomba nikomee hapa ili kuwapeni fursa ya kuuliza maswali mengine kama yapo au na nyie kuleta michango yenu. Neema ya Bwana iwafunike.
  Sabato njema kwenu.
  Siyi

 61. Siyi

  Jibu maswali ya huyu ndugu Pendael usijikaushe

  Naomba unijibu maswali yafuatayo;
  1.WAYAHUDI ni WASABATO?
  2.WASABATO walitokea wapi na mwaka gani?
  3.WASABATO wanapatikatana wapi Kwenye BIBLIA?
  4.Mtu anapomwamini BWANA YESU anakuwa MKRISTO au MSABATO?
  5.Nini MAANA ya hili andiko, WAKOLOSAI 2:16-17 ” Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato;
  mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo” ?

 62. Asante Bwana Siyi kwa mualiko ila mi sijasoma sehemu ya kushinda kanisani eti watunza sabato, unaogopa kusali na kuludi home utavunja sabato ?kama wewe yesu yu ndani yako waogopa nini ? hata unapo funga kwa kujinyima hutakiwi kujionyesha sasa wewe kukaa church eti waogopa vishawishi utaibomoa sabato mpo weak sana Mungu mnamdhihaki tu .

  Pia nijibu hili kuna sehemu imeandika siku hiyo washinda church wastarehe hakuna kufanya kazi ?ni kazi gani wafanya siku hiyo na kazi gani hamfanyi kuwa makini unapo jibu hili swali .Usije jichanganya na usiandike mambo mengi be cleare

  Asante

 63. Joyce,
  Ha ha ha ha !!
  Unafurahisha sana. Ni vyema ukawa unawasikiliza wasabato wenyewe kabla ya kusema mambo yao!! Au ni vyema ukawa unaujifunza usabato kwanza, kabla ya kuanza kuuzungumzia!! Nasema hivyo kwa sababu, watu wengi wa namna yako wanaouzungumzia usabato pasi kuujua, huwa wanafanya vichekesho sana.
  Kwanza, niseme tu kuwa, sisi hatumwabudu EGW na maandiko yake. Hata ukiyaondoa leo maandiko yake kwetu, hakuna hata kitu kimoja kitakachopungua kwetu. Hakuna!! Ellen G. White aliamini Biblia na sisi tunaiamini Biblia!! Yale aliyoyaandika, ni sawa tu na yale mnayoandikiwa ninyi na viongozi wenu wa dini, kama misale ya waumini, vitabu vile vya Gwajima vya mafundisho yake, vitabu vya Bill Graham, Joseph Smith n.k. Ninyi mnaweza kukosa kweli mwelekeo wa kiimani siku mkinyang’anywa vitabu hivyo, maana hamna kingine zaidi mlichokiweka mbele zaidi. Kwenu Biblia ni kitabu cha ziada. Sisi wasabato, Biblia ni kitabu cha kiada!! Hata kama ukitoa syllabus, tutaendelea kudunda tu na usabato wetu, maana uko bayana kiasi hicho, na hakuna awezaye kuupinga ndani ya Biblia hata kama kwa dau la milioni miangapi!! Hakuna!!
  Pili, unachukulia udhaifu wa msabato mmoja uliyemwona na kusema kuwa wasabato wote wako hivyo!! Labda nikwambie hivi, kama ilivyo kwenu, hata kwa wasabato wapo wezi, wapo wazinzi, wauaji, waongo, wavunja sabato n.k. Wapo ndugu yangu!! Wapo, tena wengi sana!! Tunachokifanya, ni kuendelea kusaidiana tu, maana ndiyo safari yenyewe, na Yesu hakuja kufia wasafi bali wadhambi tu!! Na watakaoenda mbinguni, ni wadhambi waliosamehewa tu ndugu yangu!! Kama huyo anayetesa watoto wa mwenzake ni msabato, ingekuwa heri ungemsaidia!! Kwani wewe kwenye dini yenu, mnafundishwa kuwa ukimuona mwenzako ameanguka ndio umcheke????!!! Sasa kama sivyo, wewe unachokifanya hapa ni nini??? Kwani Biblia imesemaje kwa yule anayekukwaza au kukukosea?? Unaisoma vizuri mathayo 18 dada yangu kweli?? Nilidhani, kama mkristo wa kweli, ungemsaidia tu na kumwelekeza impasavyo kutenda badala ya kuupaka matope usabato. Labda hujanielewa nikupe mf. mwingine. Hivi wale mapadri waliobainika kubaka hivi majuzi, ndio tuseme mapadiri wote wako hivyo?? Au ndiyo tupate sababu ya kuupondea ukatholiki kwa sababu hiyo??? Hasha!! Tutauponda ukatholiki kwa kukiuka maandiko ya Mungu na si madhaifu ya mtu mmoja mmoja!! Halikadhalika na wewe, ungesema hoja kama ipo ya sisi kukiuka maandiko ya Mungu!!
  Tatu, Joyce sina uhakika kama sisi huwa tunahukumu watu. Wala sina uhakika wasabato kama huwa wanawafukuza watu wengine makanisani kwao. Ninachojua ni kwamba, Wasabato ni watu wa kusema kweli licha ya madhaifu yao pengine ya mtu mmojammoja!! Na kwa kuusema ukweli huo, huonekana kama wanahukumu vile kumbe sivyo!! Ikumbukwe kuwa, daima na siku zote, ukweli huumiza sana na hivyo kuhesabika kama ni hukumu hivi!! Kumbe siyo!! Aidha, wasabato badala ya kufukuza watu wengine, huwa ni wakaribishaji wazuri sana wa wenzao kwenye ibada zao. Kama sikosei, leo hii kuna program alimaarufu –“SABATO ZA WAGENI” ambazo hukaribisha watu wa kila aina kujumuika kusali pamoja siku za Sabato na pengine kushiriki na vyakula pamoja. Zaidi ya hapo, wasabato hutoa zawadi kwa wageni wanaofanikiwa kwenda kusali siku hiyo. Sisemi haya kwa ajili ya kuwakweza wasabato. Hasha!! Siwafafagilii wasabato mimi!! Ninachokiinua ni ile hali ya kuona umuhimu wa wao kutaka kuwa pamoja na watu wa dini zingine agh. kwa siku moja tu baada ya miezi mitatu kwa kila kanisa!! Sasa,kama wewe dada Joyce, hujabahatika kupata walau hata mwaliko mmoja, tafadhali nipatie mawasiliano yako ya emaili au simu ili nije nikukaribishe siku moja tujumuike pamoja katika kumwabudu na kumsifu Mungu siku ya Sabato.
  Nne, Mwisho (but not least), niseme kuwa, hakuna safari nyingine yoyote ya watu kwenda mbinguni isipokuwa kwa kumsikiliza na kumtii Mungu anachosema. Kama weweunadhani u msafiri ilhali uko nje ya ngalawa, nakupa pole tu. maana huko hakuna usalama dada yangu. Najua utayabeza na kuyadharau maneno haya!!Lakini ipo siku, utayatafuta kwa machozi, nayo yatakukimbia!! Kila siku, umekuwa wito wangu kwa kila mtu, kuichunguza imani yake, dini yake na hicho akifanyacho akidhani kuwa ni cha kiimani, kama kina ukubalifu mbele za Mungu. Tofauti na hapo, ni kujilisha upepo na kugonja maangamizi ya moto uliondaliwa kwa ajili ya Ibilisi, malaika zake pamoja na wale waliomwasi Mungu kwa makusudi ama kwa kudanganywa!!
  “Jitahidi(soma) kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli” – 2 Timotheo 2:15.
  Neema ya Bwana ikufunike.
  Siyi

 64. Sungura,
  Tafadhali soma between lines
  Kwanza, sasa naona tunaanza kuelewana vizuri. Hoja ya Sabato siyo ishu tena kwako. Habari ya siku maalumu ya ibada siyo ishu kwako tena. Ukweli kwamba Mungu ana siku maalumu ya kuabudiwa na wanadamu wote, unaufahamu vizuri sasa kwa mujibu wa Biblia. Mambo hayo yote unayaelewa vizuri kwa mujibu wa Biblia ila hutaki tu kuwa msabato kwa vile ndani ya Biblia waumini wa zamani na wafuasi wote wa Yesu, hawakuitwa wasabato. Zaidi ya hapo, pengine hutaki kuwa msabato kwa sababu zingine fulanifulani ambazo mimi si rahisi kuzifahamu!!
  Pili, kwa upande mwingine, pamoja na kuufahamu vyema usabato, bado unaubeza na kuushushua. Kimsingi hii ni ishara ya mtu aliyekosa/ishiwa na hoja. Maana umeuliza maswali mengine ambayo kwa mtu kama wewe sikutarajia uyaulize. Kwa mf. umeuliza;
  “Hebu niambie wanapata wapi sasa kujua ile jinsi/namna ya kuikumbuka na kuitenga hiyo siku ya sabato?”
  Swali hili, huulizwa na watoto wadogo sana. Watoto wale wenye umri wa kuuliza “Hivi, baba/mama, mimi mlinipata wapi?” Kimsingi, sidhani kama nitakupa jibu la moja kwa moja, badala yake, nitakujibu kwa kukuuliza swali pia.
  ‘Kwa nini unaamini dini hiyo uliyonayo sasa?’ ‘Au imani uliyonayo uliipataje?’
  Aidha, kusema kuwa ninyi akina Sungura hamuelewi jinsi Sabato inavyotunzwa, nadhani labda hukunielewa au sikueleweka vyema. Nirudie tena kusema kuwa, ninyi akina Sungura, siyo kwamba hamuelewi jinsi ya kuitunza Sabato, bali mnaivunja Sabato kabisa!! Kwa maneno mengine, mnafanya kinyume na Mungu alivyoagiza. Kifupi, ninyi ni waasi!!! Mmh, umekasirika!!!?? Tafadhali, usighadhabike ndugu yangu. Ninyi mnahesabika kuwa ni wavunja sheria zote mbele za Mungu, hata kama mnaivunja amri moja tu ya Sabato. Mungu anawaita mghairi njia zenu, mkamrudie YEYE kungali mapema. YEYE ndiye mwenye uelewa wa namna ya kuitunza Sabato. Hata mimi bado najifunza kutoka kwake namna ya kuitunza Sabato. Ameniagiza ili niwe wake, sharti niitambue ISHARA au ALAMA yake –Sabato!! Hii ndiyo ishara pekee anayoitumia Mungu kuwatambua walio wake. YEYE ameniagiza na kusema,
  “Ikumbuke siku ya Sabato (Jumamosi) uitakase. Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; lakini siku ya saba ni Sabato ya Bwana, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. Maana, kwa siku sita Bwana alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo Bwana akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa” Kutoka 20:8-11.

  Nami ili niwe wake, sharti nitii amri hii. Vinginevyo, Mungu hatanitambua kama na mimi wake. Maana YEYE amejitambulisha kuwa, YEYE ndiye Bwana wa Sabato na alitupa Sabato zake, ziwe ishara kati ya YEYE (Mungu) na sisi (wanadamu), ili tupate kujua ya kuwa YEYE(Mungu), ndiye Bwana atutakasaye – Ezekiel 20:12. Wewe Sungura (na wengine), ukijifanyia sabato(siku ya kwako) ya kwako, Mungu hatakutambua kamwe!! Utaendelea kuona ishara na miujiza inatendeka ukidhani ni ya Mungu mwenyewe kumbe sivyo!! Na wengi wenye mawazo ya ujuvi, ujuaji na ukaidi kama ya Sungura, watapotea hakika wasipotubu mapema na kumtafuta Mungu!!
  Tatu, suala la amri za Musa na zile za Mungu nimekuwa nikiliweka bayana hapa kila mara. Nadhani hii itakuwa ni mara ya nne kama siyo ya tano kulirudia kuiweka. Na kwa vile umeliomba, nami nakupatia kama ifuatavyo;
  TOFAUTI KATI YA SHERIA ZA MUNGU NA ZILE ZA MUSA
  SHERIA ZA MUNGU SHERIA ZA MUSA
  1. Ziliandikwa na Mungu mwenyewe kwa kidole chake Kutoka 31:18 1. Ziliandikwa na Musa mwenyewe kwa kidole chake, Torati 31:18
  2. Ziliandikwa kwenye mbao mbili za mawe yaliyochongwa, Torati 10:1-4 2. Ziliandikwa kwenye chuo(kitabu
  cha dini-ngozi ya wanyama), Torati 31:24
  3. Baada ya kuandikwa, ziliwekwa ndani ya Sanduku la Agano lililochongwa kwa mbao za mti wa mshita Torati 10:1-4 3.Baada ya kuandikwa, ziliwekwa nje pembeni ya Sanduku la Agano, Torati 31:24-27
  4. Waliozivunja, alionekana kutenda dhambi 1Yoh. 3:4, na iliwapasa hukumu ya kifo, Torati 17:2-5 4.Waliozivunja, hawakuonekana na dhambi, isipokuwa walionekana na makosa yaliyosababisha adhabu vilevile, naam hata kifo kwa waliokaidi zaidi japo zilikuwa ni kivuli cha Kristo. Wakolosai 2:14-17
  5. Yesu alikuja kuzitilia nguvu zaidi kwa kuzifanya ziwe ni matokeo ya driven force ya upendo uliomo ndani ya mtu kwa Mungu wake na mwenzake, na wala hakuzitangua. Mathayo 22:37, Mathayo 22:39 na Mathayo 5:17-19 5.Baadhi ya sheria hizi, zilikoma Yesu alipokufa msalani. Miongoni mwa sheria alizokuja kuziondoa Yesu zilikuwa ni sheria za kafara kwa maana zilikuwa ni sheria za maagizo tu yaliyokuwa yakisimama kama kivuli cha kifo chake. Kolosai 2:15. Aidha, utaratibu wa kula pasaka, nao ulibadilika kidogo, kwa mf. badala ya kukatwa govi na kukaa nyumbani mwa waisrael ndipo mtu ashiriki pasaka, ubatizo wa maji mengi ulikuja kama mdadala.
  6. Sheria(Amri 10) ya Bwana ni takatifu, njema na ya haki, nayo yadumu milele na milele, Warumi 7:12 6.Zile za kafara, zilikuwa ni kivuli cha kazi ya Yesu aliyoifanya msalabani, nazo zilikomea hapo. Ebran. 10:1-12
  7. Sheria za Bwana ni kamilifu, za adili, kweli na za milele. Zaburi 111:P7-8 7.Zile za kafara na chache za pasaka, ziliishia na kubadilishwa pale Kristo alipokufa Msalabani. Waebran. 9:10-12, Luka 22:37

  Nne, nikisema kuwa ninyi akina Sungura ni waasi na mko gizani, usikasirike kaka. Huo ndio ukweli. Sema hivi, kila mtu huwa hapendi kukosolewa!! Hilo ndilo tatizo kubwa tulilo nalo wanadamu tulioasi!! Lakini ukweli utaendelea kubaki ukweli. Na mimi niko hapa kwa ajili ya kuwaambia watu ukweli ili mwenye kupona apone na mwenye sikio la kufa, takaufa tu!! Sheria za Mungu zimekuwepo zamani hata kabla ya dhambi. Siku ile nilikuonesha ndani ya Biblia kabisa. Hata kabla ya Ibrahimu Myahudi wa kwanza, sheria za Mungu zilikuwepo!! Na ushahidi mwingi wa maandiko nilikuonesha. Wewe, sema tu kuwa, hutaki kuwa mtu wa Mungu kwa kuivaa ALAMA au ISHARA yake –Sabato!! Lakini ukweli wote, naamini unao!!
  Tano, naomba kujibu maswali yako kama ifuatavyo;
  Swali la 1
  1. Sasa kama unajua kuwa sabato si mzigo mbona unatutaka J’mosi tushinde kanisani?”
  Jibu
  Kwani imeandikwa wapi kwamba siku ya Sabato ni lazima ushinde kanisani!! Biblia inasema kuwa, siku ya Sabato ni ya kutofanya yoooote yatupendazayo sisi. Badala yake, ni kumwabudu Mungu pamoja na kutenda mambo yote yaliyo mema na kubalifu kufanyika siku ya Sabato; mambo ambayo yana faida kwa Mungu
  Swali la 2
  “Hiyo ya kushinda kanisani J’ mosi umeitoa kwenye andiko lipi?”
  Jibu
  Hakuna andiko lolote linalosema kuwa siku ya Sabato waumini sharti washinde kanisani!! Ni suala la utaratibu tu wa ratiba ambayo kanisa moja linaweza kupanga tofauti na kanisa lingine, ilmradi tu, watu wasivunje Sabato. Sabato siyo mzigo. Wewe kama unaijua kuwa Sabato ni mzigo, leta aya!! Basi!!
  Sita, kama zamani uliwaona Wasabato wanakula viporo, hao walikuwa sahihi kabisa. Wasabato wa leo unaowaona wanapika chakula siku ya Sabato au kununua kilichopikwa na wengine, hao wanaivunja Sabato, full stop!! Huo ndio ukweli!! Neno la Mungu ni upanga ukatao kuwili. Kwa mhubiri na mhubiriwa!! Ukinikuta mimi Siyi nanunua chakula au napika chakula siku ya Sabato, jua kuwa ninavunja Sabato, isipokuwa nifanye hivyo kwa dharura tu lakini siyo kwa kupanga/kukusudia kabisa!! Na leo wapo Wasabato koko wanaohalalisha kupika au kununua vyakula/maji siku ya Sabato kwa visingizio vya kiafya n.k. Kwa kutumia blog hii nawaambia waache mara moja!! Wasabato wa zamani walikula viporo vya manna jangwani, hakuna aliyeugua hata mmoja kwa kula viporo hivyo!! Mungu aliyewanusuru wasabato wa zamani kutougua kwa kula viporo, ndiye Mungu tunayemwabudu leo!! Wafuasi halisi wa Mungu, hawana budi kumtii Mungu kwa kila hali/namna, vinginevyo, tutakuwa tunamfanyia ibada ibilisi tukidhani tunamwabudu Mungu. Mungu atusaidie wasabato wenzangu tupone katika hilo. Nawaombea kwa Neema za Mungu!!
  Saba, nijibu swali lako la mwisho kwa leo…
  “Siyi, wewe umetahiriwa kwa sababu torsti inataka hivyo au kwa sababu za kwako tu za kiafya?”
  Jibu
  Naona hoja hapa si torati wala nini, ila unataka kujua tu kama Siyi ametahiriwa ama la!! Ha ha ha ha haa!! Napenda kusema hivi, Nadhani tendo hilo lilifanyika kwangu kwa sababu za kiafya zaidi na si torati. Maana katika torati ndani ya Agano Jipya, tohara imekuja kwa maana ya ubatizo wa maji mengi.
  Neema za Bwana zikufunike.
  Siyi

 65. Siyi, Elen G. White ana uhusiano gani na Usabato?Pia tarehe 16/12/2014 katika MADA HII (hapo juu) nimemuuliza Osward Maswali ambayo hakuyajibu, je unaweza kumsaidia kujibu hayo Maswali?

 66. Siyi, Mama Ellen White usiseme hamumuabudu kama hamuuabudu hiyo lesson yooote ni makatazo yake hadi mnafikia hatua ya kusema mama kakataza matumizi ya sukari sijui uamsho sijui matengenezo .Na hata kanuni mnayoitumia ni mama huyo yumo humo sasa kama yeye hamumuabudu ni nini? mnaacha maagizo laini na mazuri ya Yesu mwafata inshu za mtu aaminie hata wewe sasa nyumbani kwako utataka uabudiwe hamna tofauti na waabudio ng’ombe nyinyi.

  Hiyo siku ya mapumziko unayo sema si mapumziko ufikilivyo au mfikilivyo wasabato bali ni kujitesa hasa wafanyakazi wenu wa ndani mnawatesa sana kuwafanyisha kazi za kupika usiku wa manane na kubebelea mivyombo eti kuwai kanisani kupumzika wakati mnatesa watoto wa wenzenu yaaani nyie mtakua vichocheo vya moto kha!

  Amri kuu ya upendo kwa wasabato haipo mmebaki na Amri ya kupumzika tu sabato na mnazani ni tiketi ya kuingia mbinguni hilo halipo kama upendo ni mdogo poleni sana .

  Ila MUNGU ANATUPENDA SANA NA ANAZIDI KUWA NASI SIKU ZOTE ZA MAISHA YETU .

  Wasabato punguzeni kuhukumu watu hayo mamlaka hakuna alie kabiziwa hapa duniani sisi sote ni wasafiri tu . Eti mnafukuza watu kanisani mnawatenga wewe hujatoa boriti katika jicho lako wajitia kutoa kibanzi kwenye jicho la mwenzako loh!

 67. Siyi,

  Mimi kuwa mkristo hilo ndo lililobora, sihitaji kuwa msabato. Sijawahi kuona mtu anaitwa msabato kwenye maandiko, ila kuna wakristo.

  Punguze kusema kuwa sisi hatuelewi badala yake jitahidi zaidi kuthibitisha huko kutokuelewa kwetu.

  Wasabato nawajua, na walishawahi kunishawishi sana kuwa msabato miaka mingi iliyopita, tangu miaka ile wanaenda siku moja kukesha milimani kumsubiri Yesu ati anarudi kuwachukua wakaambulia patupu.

  Usabato ni dini ambayo ni ikabodi, imejaa maneno zaidi kuliko nguvu. Huu ufalme wa Mungu si manenomaneno, bali ni ktk nguvu.

  Jitahidi kuongea tu substance zaidi Siyi, vijimanenomaneno acha, ni kupoteza muda.

  Mungu anawaagiza Israel waikumbuke siku ya sabato na waitenge.

  Hebu niambie wanapata wapi sasa kujua ile jinsi/namna ya kuikumbuka na kuitenga hiyo siku ya sabato?

  Kwa vile umesema kuwa sisi akina Sungura hatuelewi namna sabato inavyotunzwa, naomba Siyi wewe utuoneshe kwenye maandiko jinsi ya kuitunza sabato.

  Kisha naomba unionyeshe zipi ni sheria za Musa na zipi ni za Mungu, nitafurahi sana.

  Halafu sikiliza brother, wazo kwamba niko gizani hilo ondoa kabisa. Usijaribu kujustify jambo kwa sababu ya kutokuelewa kwako.

  Kama una akili timamu utajua kutambua maneno ya mtu aishie gizani na ya mtu aishie nuruni. Usijaribu kuropoka chochote kwa bababu tu tuko hapa tujadili.

  Watu wamemtumikia Mungu kabla ya amri ya kutunza sabato haijakuwepo, Israel limekuwepo kama taifa kabla ya amri ya kutunza sabato haijawepo.
  Jiulize waliwezaje kumpendeza Mungu.

  Sasa kama unajua kuwa sabato si mzigo mbona unatutaka J’mosi tushinde kanisani?

  Hiyo ya kushinda kanisani J’ mosi umeitoa kwenye andiko lipi?

  Ninaona ni jinsi gani hujui maana ya ibada , ndo maana umekwepa kulijibu hilo swali langu la nini maana ya ibada, mahali inapopaswa kufanyika na inahusianaje na kushinda kanisani.

  Nani kakwambia kuwa kushinda kanisani ndo kutunza sabato, wapi imeandikwa hivyo?

  Eti oh leo sabato si mzigo tena;, nani kaupunguza mzigo wa sabato? Hebu nionyeshe hayo maandiko ambayo yanasema mzigo wa sabato umepinguzwa uzito.

  Zamani wasabato mlikuwa mnakula vipolo siku ya sabato, siku hizi naona mmeacha,mnapika siku ya sabato au mnakula hotelini kilichopikwa na wengine.

  Yaani mnayabadili masharti ya sabato kama mnavyoona inafaa halafu mnajigamba kuwa mnashika sabato.

  Hakuna sabato mnayotunza hapo, ni kelele tu za bure na kupiga panda ili kujionesha kwa watu.

  Siyi, wewe umetahiriwa kwa sababu torsti inataka hivyo au kwa sababu za kwako tu za kiafya?

  Asante!

 68. Sungura,
  Kila mtu anamwambia mwenzake kuwa yuko hatarini karibu na kupotea… Sasa ni nani mwenye ukweli hasa??!!! Tutaujuaje ukweli!!?? Unafikiri ni nani atamwamini mwenzake zaidi? Mimi nikushauri tu tuiache Biblia ijifafanue yenyewe. Ukiweka fikra zako na kutaka kwako uaminiwe na watu esp. akina Siyi utakesha tu!! Acha Biblia inene yenyewe kaka.
  Ni kweli sisi hatuwezi kuishika torati kama mafarisayo maana wao, walijitungia sheria mbadala (sheri ndogondogo) zinazowalazimisha kuitunza torati nzima. Sisi sheria hizo hatunazo!! Sasa utatufananishaje na mafarisayo kaka??!! Huoni kufanya hivyo ni kutotutendea haki tu!!!?? Haki ya mafaridayo iliishia kwenye utunzaji tu sheria/torati kwa uongozi wa sheria zao za kijadi/kiutamaduni (sheria ndogo2 nilizozitaja hapo juu). Wakristo wa NT, hatuna hizo sheria wala haki yetu mbele za Kristo, haipaswi ifanane na ile ya Mafarisayo bali iwe beyond ile ya mafarisayo. Wakati mafarisayo wakiiti torati kwa nguvu zao wenyewe, sisi tunaitii torati kama matokeo ya upendo wetu kwa Kristo ulio mioyoni mwetu. Mafarisayo walitii torati kwa nje, sisi tunaitii kuanzia ndani ya moyo then utii huo hujidhihirisha kwa nje baadaye. Kwa maneno mengfine, utii wa torati leo, ni matokeo ya kile kilichomo ndani yetu (upendo), tofauti na enzi wa za mafarisayo.
  Ndiyo maana ukimwangalia Yesu na wanafunzi wake waliokuwa wakitembea naye bega kwa bega, wao walimfahamu vyema. Binafsi sijasoma popote ambapo wanafunzi wa Yesu walimhoji Yesu kwa nini anavunja Sabato??!! Sijauona huo mstari ndani ya Biblia. Kama wewe unao ulete nami nijifunze kwako. Ninachokiona mara kwa mara ni wale mafarisayo, watu ambao hawakuwa wakitembea na Kristo, wakijifunza na Kristo kwa ukaribu nk, ndio waliokuwa wakimhoji mara kwa mara Yesu kuhusiana na Sabato. Kwa nini?? Hawakuelewa maana ya utunzaji wa Sabato hasa. Hata ninyi akina Sungura, Milinga na wengine, mtaendelea kulalama tu mnapotuona wasabato tukishiriki katika matukio ya lazima siku za Sabato, maana hamuelewi, ni mpaka mtakapoamua kutembea na Kristo –kuwa wasabato/kuujifunza huo usabato kwanza. Siku mkielewa maana ya utunzaji wake, mtakuwa huru kwelikweli. Kazaneni tu kujifunza habari za Sabato kungali mapema.
  Huduma alizozifanya Kristo siku ya Sabato, kama vile kuponya, kuamuru watu kubeba magodoro na kadhalika, ndizo shaghuli tunazozitenda hata sisi wasabato pia. Panapo dharura, tunachimba dawa za kutibia watu, tunanunua dawa, tunapeleka wagonjwa hospitali siku ya Sabato, madaktari wasabato huwahudumia wagonjwa siku za Sabato, n.k. Yaani Sabato si mzigo kwa leo kama ilivyokuwa kwa mafarisayo kaka. Changamka tu kuijifunza, usije ukachelewa mno kuijua!! Vinginevyo, utabaki kupika kelele kama chiriku tu huku ukiendele kubaki gizani.
  Neema ya Bwana ikufunike.
  Siyi

 69. Milinga,
  Ndugu Milinga, umeuliza maswali mengi kuhusu Sabato. Lakini yaeleka huijui hiyo Sabato, maana maswali yako yanadhihirisha hilo. Nami nimekujibu kwa njisi ulivyouliza!! Kama hutatosheka na majibu yangu, karibu tena, nitajibu tu maana ndiyo kazi yangu kuu!!
  1. “Kama Mungu alistarehe siku ya Sabato mbona Wasabato hawastarehe siku hiyo?”

  Jibu
  Tunastarehe sana. Labda ungesema kustarehe unakokujua wewe kukoje? Mimi najua huwa tunastarehe sana siku ya Sabato – Jumamosi.

  2. “Kama Jumamosi ni siku ya KUPUMZIKA mbona Wasabato hawapumziki bali wanachakarika kwenda KUSALI? Au KUSALI siyo KAZI? Kama utasema siyo KAZI inayoleta KIPATO mbona huwa mwachoka saaana baada ya ibada, miguu, akili na viuno vyenu vimechoka sana jioni mnaporudi nyumbani?”

  Jibu
  Hata Yesu alichakarika kwenda kusali siku ya Sabato. Na kusali kama ni kazi, basi Yesu muumbaji alifanya kazi siku hiyo!! Hivyo nasi hatuna budi kufanya kazi (ya mtindo huo) siku ya Sabato. Zaidi ya hapo, mengine ni uzushi tu usio na maana. Wewe unajuaje kuwa huwa tunachoka sana siku ya Sabato?? Au wewe ni nani aliyekwambia kuwa kazi inayochosha ni ile ya kujipatia kipato tu??!!! Kutembea hakuwezi kumchosha mtu siku ya Sabato? Je, kutembea huko kwa vile kunamchosha, kunampatia kipato? Kuhubiri hakuwezi kumchosha mtu!!?? Akichoka kwa kazi hiyo anakuwa amevunja Sabato kwa akili zako? Nikushauri uijifunze Sabato kwanza. Sabato si kama unavyojaribu kuidodosa hapa kaka!! Enzi za Agano la Kale hatuko. Utunzaji wa Sabato leo, ni matokeo ya upendo wetu kwa Mungu kama ilivyo kwa amri zingine 9. Acha kuchanganyikiwa kwa kuiona Sabato kama mzigo!!

  3. “Kama Mungu aliitakasa JUMAMOSI na akaifanya ikawa ndiyo siku pekee ambayo Mungu anapokea dua za wanadamu, na kuwataka wakusanyike JUMAMOSI peke yake ndiyo kusema kuwa SIKU nyingine mbali na JUMAMOSI Mungu hasikii kabisa dua za wanadamu wamuombao?”

  Jibu
  Tofautisha Sabato na ibada za siku zingine!! Maombi ya siku zingine husikia kama anavyosikia maombi ya siku ya Sabato tu. Pamoja na ibada za mida mifupi ya siku zingine za kazi, bado Mungu alitaka watu wamwabudu YEYE tu kwa siku nzima ya Sabato. Hata watu wa zamani walimwabudu Mungu siku zote, lakini siku ya Sabato ilikuwa ni maalumu kwa kumfanyia Mungu ibada tu. Kwa hiyo hata kama unafahamu kuwa Mungu anakusikia maombi yako ya kila siku, kumbuka kuwa una deni la kuikumbuka siku ya Sabato kwa ajili ya kumwabudu Mungu tu, maana YEYE mwenyewe ndiye aliyeamua iwe hivyo! Siku sita ufanye kazi zako zote, ya saba ni yake!!

  4. “Kama ni kweli kuwa JUMAMOSI ndiyo siku Pekee tukufu na takatifu ya kukusanyika kanisani na kila anayekusanyika kusali siku tofauti naJUMAMOSI ni muasi wa sheria za Mungu, Je, siku nyingine tofauti na Jumamosi ni siku CHAFU?”

  Jibu
  Hakuna siku chafu kwa Mungu. Yeye ndiye aliyeziumba siku zote na akaona kuwa kila kitu kilikuwa ni chema!! Wewe u nani unaziita chafu siku ambazo ni kazi ya mikono yake!!?? Siku zote ni za Mungu. Sabato ni ya Mungu vilevile!! Zingekuwa chafu, tusingefanya yale maombi ya mida mifupi ya kila siku majumbani/kanisani kwa siku hizo. Pamoja na ibada fupifupi za siku 6 zingine za kazi, Mungu alitaka watu wake wamwabudu siku ya Sabato ndiyo maana aliitenga na kuiweka wakfu kwa ajili ya kumfanyia ibada YEYE tu.

  5. “Je, Mungu amewakataza wanadamu wasifanye KAZI zenye kuwaletea vipato wanadamu siku ya JUMAMOSI na wakati huo huo akawaruhusu wachakarike huku na kule kenda kusali tena umbali mreeefu sana? Mbona yeye MUNGU alikaa akatulia tuli AKASTAREHE huku akiinjoi kazi za mikono yake? Kwa nini wewe usikae nyumbani ukala bata tu kama Mungu alivyofanya siku ya JMOSI?”

  Jibu
  Swali hili nimelijibu hapo juu. Nimesema kuwa, Yesu ndiye Bwana wa Sabato. YEYE ndiye aliyeiumba hiyo Sabato. Na alipofanyika mwili, siku ya Sabato hakulala nyumbani, bali tunamwona alisafiri tena umbali mrefu tu kwenda kusali. Nikasema kuwa, kwa vile Kristo ni kielelezo chetu, hebu na sisi tuige mfano wake wa kwenda kusali kanisani siku ya Sabato kama alivyofanya YEYE. Utunzaji wa Sabato ni mrahisi sana ukiuelewa kaka!! Lakini ukiuchukulia kama farisayo au myahudi wa kuzaliwa, utashindwa tu maana wao walitunga sheria nyingi sana (za kiutamaduni) za namna ya kuitunza sabato mambo ambayo wewe leo hauna!! Wewe leo una Sabato tu!! Jitahidi kumwangalia Yesu alivyoitunza Sabato pamoja na mitume wake halafu ukajifunze kwao. Na mwisho wa siku, utaifurahia Sabato!!

  6. “Je, kwenda KUSALI JUMAMOSI kanisani Ndiyo KWENDA KUSTAREHE?”

  Jibu
  Ndiyo. Tena siyo kustarehe tu, bali starehe ya kuzungumza na Mungu, kumjifunza na kumwimbia sifa.
  “Kwa taarifa yako:
  1. JUMAPILI = SIKU YA BWANA
  JUMAMOSI = SIKU YA SABATO”
  Taarifa hii ninaifahamu ya kwamba, hakuna andiko lolote ndani ya Biblia linalosema kuwa, Jumapili ni siku ya Bwana. Hakuna!! Isipokuwa kuna mistari mingi sana inayosema kuwa, siku ya Saba – Sabato ni Jumamosi. Nashangaa sana kuwaona watu na akili zao wakienda kusali siku ambayo Mungu hakuagiza watu wamfanyie ibada!! Ni aibu sana na inatia huzuni mno!!
  2. “JUMAPILI NI SIKU YA KUFUFUKA BWANA WA SABATO
  JUMAMOSI NI SIKU YA SABATO, BWANA YUKO KABURINI”
  Jibu
  Ni Kweli jumapili ni siku ya kwanza ambayo Kristo alifufuka katika wafu. Hata hivyo, baada ya kufufuka, Kristo hakusema kuwa ameibadilisha siku ya Ibada –jumamosi na kuifanya kuwa jumapili!! Hakusema hivyo!! Hata mitume wake waliendelea kusali jumamosi hata baada ya Kristo kupaa kwake mbinguni. Wanadamu wa leo hawataki kuikumbuka siku ya Sabato kwa ajili ya kumfanyia Bwana ibada, siku ambayo Kristo mwenyewe, alipumzika alipokuwa hai na alipokuwa amekufa!! Ni ajabu sana wanadamu wa leo tunapozidiwa akili hata na mfu (Kristo) aliyeiheshimu Sabato akiwa kaburini ilhali sisi tuko hai leo hatuiheshimu!! Sijui shida ni nini??!!!
  3. “JUMAPILI NI SIKU YA UJIO WA ROHO MTAKATIFU
  JUMAMOSI NI SIKU YA KUSUBIRIA AHADI ZA BWANA”
  Jibu
  Binafsi sijasoma kuwa siku ya ujio wa RM ilikuwa ni siku ya kwanza ya juma (jumapili). Kama wewe una aya hiyo ndani ya Biblia, nitafurahi kujifunza kwako na mimi nielimike kwa hilo. Halikadhalika, sina uelewa kamili kuwa jumamosi ilikuwa ni siku ya kumngoja RM. Zaidi ya hapo, hakuna aya yoyote ndani ya Biblia inayosema kuwa, ujio wa RM ulihamisha utakatifu wa Jumamosi na kuupeleka jumapili. Kama una aya, leta tujifunze sote.
  Mwisho, ukweli wa siku ya Sabato utaendelea kubaki palepale. Pamoja na jitihada mbalimbali za kuhalalisha kazi siku ya jumamosi kiserikali, bado Mungu hatabadilisha utaratibu wake wa siku kisa wanadamu wamebadili!! Mungu ni yuleyule hata siku zote. Neno lake halitapita kamwe na wala halitabadilika milele. Ni kazi kwentu ya kulitii neno hilo au kuliasi. Na hatima ya pande zote mbili iko bayana mno!! Mungu atusaidie kufanya uchaguzi sahihi wa kumuheshimu YEYE pamoja na Sabato yake.
  Neema ya Bwana ikufunikeni nyote!!
  Siyi

 70. WASABATO; Tarehe 16/12/2014, katika MADA hii kuna ASWALI nilimuuliza OSWARD mpaka sasa ameshindwa kutoa majibu.Tafadhali naombeni majibu.

 71. Siyi,

  Yaani huwa nikiamua kupita kwa umakini mtulivu katikati ya mistari yako, huwa nagundua kuwa wasabato mna safari ndefu mno kuifikia kweli ya zama hizi kuliko unavyofikiri.

  Believe me, kuna maswali mngemuuliza Yesu na kumlaumu just kama mafarisayo walivyofanya. Lakini kinachofanyika ni kwamba ninyi kwa vile ziko kweli za injili hamwezi kuzikana, mnachokifanya ni kuzikubali hizo kweli kijanja kijanja na kulazimisha kuzimix na torati ili nanyi muonekana kuwa ni waumini wa agano jipya, but in actual sense u are not.

  Ninyi hamjawahi kuijua na kuishika torati kama mafarisayo, kwa hiyo wao popote walipomlauma Yesu kuwa kavunja torati ni kweli alikuwa amevunja(ispokuwa pale biblia inaposema walimsingizia)

  Kwa mfano kwa habari ya kuivunja sabato, ni kweli Yesu aliivunja, yaani alifanya kitu ambacho hakikupaswa kufanywa siku hiyo kulingana na zile sheria za kulinda amri.

  Kwa mfano: kwa nini Yesu badala ya kunyoosha tu kwenda hekaluni sabato anapita Bethesda siku ya sabato, alikuwa anaenda kufanya nini huko?

  Kwa nini anafanya kazi ya kuponya mtu siku huku anajua kabisa ni kinyume na sabato?

  Kwa nini anamwamuru mtu kubeba mzigo( godoro) siku ya sabato huku akijua kanuni za sabato hazitaki mzigo ubebwe siku hiyo.

  Kwa hiyo siyo yeye tu anavunja sabato hapo, ila anaamuru na mtu mwingine aivunje.

  Lakini pia, ivi kuanza kumhoji mtu kwa nini kabeba mzigo siku ya sabato, yuko wapi aliyemfanya abebe mzigo, nayo ilikuwa ni ibada kwa Mungu, kama kweli siku ya sabato inatakiwa kuwa siku ya kusali tu?

  Lakini ona majibu ya Yesu yalivyo ya ajabu.
  Kwa mara ya kwanza watunza sheria wanashangaa kuambiwa kuwa Mungu hufanya kazi siku zote, kwa hiyo na siku hiyo ya sabato alikuwa anafanya kazi ndo maana Yesu nae akaamua kupiga mzigo.

  Oh, lakini nakuona Siyi ukinijibu kuwa siku hiyo tunapaswa kufanya kazi ya kuokoa uhai.
  Je, kubeba godoro ilikuwa ni kuokoa uhai?

  Yohana 5:1-23

  Nani kati ya hawa wawili alikuwa anaokoa uhai; huyu aliyebeba godoro siku ya sabato na hakupigwa mawe, au huyu mama anayeamua kuokota kuni apike chakula kuokoa uhai wa mwanae, lakini anapigwa mawe hadi kufa?

  Believe me brother, hamjawahi kujua essence ya agano jipya, na hamjawahi kujua nini fate ya agano la kale.
  Mnacheza makidamakida tu bila kujua undani wa mnachohangaika nacho.

  Siyi hamwezi leo kuishika torati na kutimiza matakwa yake, mnajidanganya tu, lakini katk uhalisia mnaivunja kuliko hata mafarisayo by far.

  Israel wenyewe pamoja na kutomtambua wa kumkubali Yesu, hawaitimizi torati jama inavyotakiwa.

  Lini wewe umesikia myahudi kapigwa mawe kwa sababu alikwenda ofisini siku ya sabato, kapigwa mawe sababu ya kuzini?

  Unajikanyagakanyaga kuwa ati siku ya sabato ni ya kushinda unafanya ibada, japo siku zote tunafanya ibada.

  Ivi unajua maana ya ibada katika agano jipya, na mahali inapotakiwa kufanyika, na ina uhusiano gani na kushinda kanisani?

  Hamjawahi kuelewa hizi ni zama gani,matokeo yake mnalazimisha divai mpya ndani ya kiriba cha zamani, matokeo yake kimewapasukia, na hamtaki kukubali kuwa kimepasuka.

  Hakuna sabato mnayotunza ninyi, mnachokifanyaga huwa ni kusali tu siku sabato traditionally!

 72. Ok maelezo yote ni mazuri kwamba JUMAMOSI NI SIKU YA SABATO. Mimi sitapinga hata kidogo. Lakini maswali yanabakia kichwani mwangu kama siyo rohoni au moyoni mwangu ni haya yafuatayo!!!

  1. Kama Mungu alistarehe siku ya Sabato mbona Wasabato hawastarehe siku hiyo?

  2. Kama Jumamosi ni siku ya KUPUMZIKA mbona Wasabato hawapumziki bali wanachakarika kwenda KUSALI? Au KUSALI siyo KAZI? Kama utasema siyo KAZI inayoleta KIPATO mbona huwa mwachoka saaana baada ya ibada, miguu, akili na viuno vyenu vimechoka sana jioni mnaporudi nyumbani?

  3. Kama Mungu aliitakasa JUMAMOSI na akaifanya ikawa ndiyo siku pekee ambayo Mungu anapokea dua za wanadamu, na kuwataka wakusanyike JUMAMOSI peke yake ndiyo kusema kuwa SIKU nyingine mbali na JUMAMOSI Mungu hasikii kabisa dua za wanadamu wamuombao?

  4. Kama ni kweli kuwa JUMAMOSI ndiyo siku Pekee tukufu na takatifu ya kukusanyika kanisani na kila anayekusanyika kusali siku tofauti naJUMAMOSI ni muasi wa sheria za Mungu, Je, siku nyingine tofauti na Jumamosi ni siku CHAFU?

  5. Je, Mungu amewakataza wanadamu wasifanye KAZI zenye kuwaletea vipato wanadamu siku ya JUMAMOSI na wakati huo huo akawaruhusu wachakarike huku na kule kenda kusali tena umbali mreeefu sana? Mbona yeye MUNGU alikaa akatulia tuli AKASTAREHE huku akiinjoi kazi za mikono yake? Kwa nini wewe usikae nyumbani ukala bata tu kama Mungu alivyofanya siku ya JMOSI?

  6. Je, kwenda KUSALI JUMAMOSI kanisani Ndiyo KWENDA KUSTAREHE?

  Kwa taarifa yako:
  1. JUMAPILI = SIKU YA BWANA
  JUMAMOSI = SIKU YA SABATO

  2. JUMAPILI NI SIKU YA KUFUFUKA BWANA WA SABATO
  JUMAMOSI NI SIKU YA SABATO, BWANA YUKO KABURINI

  3. JUMAPILI NI SIKU YA UJIO WA ROHO MTAKATIFU
  JUMAMOSI NI SIKU YA KUSUBIRIA AHADI ZA BWANA

  Nakutakia nyote Jumapili njema? Mr. Siyi naomba majibu ya maswali yangu

 73. Joyce,
  Una safari ndefu sana ya kwenda. Wasabato hawamwabudu mtu awaye yote. Hata huyo Ellen G. White unayemsema, haabudiwi na mtu yeyote. Wanachokiabudu wasabato, ni Mungu -YEHOVA. Na wanamwabudu YEYE kwa sababu Biblia (siyo watu) imewaagiza kufanya hivyo.
  Kuhusu kuokolewa, ni kweli kabisa tutaokolewa endapo tutaitii sauti ya Mungu -kuwa na upendo kwake YEYE mwenyewe na wanadamu wenzetu. Tukiliweza hili, amri na sheria zote, zimekamilika kwalo (upendo). Kwa maelezo mengine, ukimpenda Mungu, utamwabudu YEYE tu, hutakuwa na miungu mingne ya kuabudu isipokuwa YEHOVA peke yake. Hutalitaja bure jina lake na zaidi ya hapo, utaikumbuka siku yake ya kumwabudu YEYE ndani ya siku 7 za wiki -Sabato. Na siku hiyo, ni jumamosi. Hii ndiyo amri iliyo kuu na ya kwanza -(kuanzia amri ya 1-4). Na hili ndilo fundisho la Biblia.
  Na kuhusu kuwapenda wanadamu wenzako, itakubidi uwafanyie kama ambavyo ungependa wewe ufanyiwe!! Na maelezo hayo, yanapatikana kwenye amri ya tano hadi ya kumi -mpende jirani yako kama nafsi yako. Na hii ndiyo jumla ya maneno yote ya kwamba, “Nawe mpende Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote, (Kumbukumbu la Torati 6:5, Mathayo 22:37), na “… umpende jirani yako kama nafsi yako; Mimi ndimi Bwana” (Mambo ya Walawi 19:18, Mathayo 22:39).
  Ukikiuka amri mojawapo kati ya hizi, utakuwa umekosa juu ya yote.
  Tafakari neno hilo.
  Siyi

 74. Tatizo ninalo liona hapa ni MAFUNGU YA KUKARIRI NDO YANAFANYA MTU AJIONE ANAIJUA SABATO NA MAANDIOKO. Mi naomba niwaulize wasabato huyu mama Elen G White ni nani katika biblia hadi wamwabudu? mana Muda mwingi wanautumia kumsoma yeye na si biblia huko kanisani .

  Kukariri mafungu kama wimbo hayakuokoi kitakacho kuokoa ni matendo mema kama bwana alivyosema nawaachieni AMRI KUU YA UPENDO NA SI MENGINE

 75. Lwembe,
  Acha ufedhuli kaka. Acha kupotosha watu!! Ndani ya Biblia, aya inayosema kuwa jumamosi ni siku yA SABA IPO!! Sema wewe hujaiona!! Na kwa vile ni wewe, ungesema mimi lwembe, sijapata aya hiyo, ili akina Siyi tukakusaidia kukuonesha!! Majina na mpangilio wa siku za juma/wiki, niliutolea maelezo yakinifu sana kwenye mada ya kalenda 2015. Chanzo cha majina haya tuliyo nayo sasa, jumamosi, jumapili n.k. nimeeleza pamoja na changamoto zake. Kilichosalia ni kwa watu wenyewe kufanya uamuzi wa kumwabudu Mungu sawasawa na alivyoagiza au la!!
  Mungu ana siku maalumu ya kufanyiwa ibada pamoja na kwamba siku zote ni zake. Kwa kulitambua hilo, bado aliona umuhimu wa kuwa na siku maalumu ya kumwabudu YEYE tu. Na siku hiyo ni Jumamosi na si vingvinevyo!! Biblia iko bayana. Vitabu vya historia viko bayana vilevule. Tii uishi, asi ufe! Full stop!!
  Siyi

 76. Paulo, elly na Siyi,

  Kazi ya Shetani ni kukuchanganyia mambo ili kulipindua neno la Mungu, akikubembeleza uupokee mchanganyiko huo ambao mwishoni hukutoa kabisa ktk Njia ya Kweli kama ninavyowaona!

  Maandiko yanasema, Kut 20:11 “Maana, kwa siku sita BWANA alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo BWANA akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa.” Mungu anazungumzia “siku sita”; Kut 34:21 “Utafanya kazi siku sita, lakini katika siku ya saba utapumzika”

  Hakuna mahali ktk Biblia ambapo Mungu amesema siku ya saba ni “Jumamosi”, au kwamba siku hiyo ya saba inaitwa “Sabato” ktk maana ya jina lake, kama tunavyoiita Jumatatu au Ijumaa! Mungu HAKUZIPA majina siku zaidi ya kuzihesabu, hapo alipoziumba. Kwahiyo unapolipindua Neno lililowazi na kulipachika tafsiri yako inayolitoa ktk maana iliyokusudiwa, hiyo yenye kuwapa wana wa Mungu kuvitawala vyote, wewe ukawaingiza ktk utumwa wa miungu ya “siku”, wakaanza kuiabudu siku badala ya Mwenye siku, ukiwavunjisha Amri ya Kwanza ktk ujinga wao; ni balaa kiasi gani kwenu mliokaririshwa mambo hayo na kuwa “mitume” wa hiyo injili yenye kufisha!!!!

  Maana ya Sabato ni “Pumziko”, au “Starehe”; yaani “”Rest””, hivyo siku ya Sabato maana yake halisi kulingana na Maandiko ni “Siku ya Kupumzika au Pumziko”. Basi kulingana na utamaduni wa kwenu, ndipo ungezihesabu siku kwa kadiri ya nuru uliyomo, kama ni ya kipagani au kimizimu au vyovyote utavyofanya, utaishia kuwa na siku saba tu, na kama huna ufahamu basi utaishi kama ng’ombe bila siku. Bali Mungu ameziumba siku saba ambazo ametupatia tuzitawale, ndiko huko kuzipa majina!

  Hebu fikiria hili, kwamba Adamu ameumbwa ktk siku ya sita, ndipo iwapo naye alipumzika ktk hiyo siku ya saba aliyopumzika Mungu, ndio kusema alipumzika ktk siku yake ya kwanza, akiiondoa maana nzima ya “Fanya kazi siku sita…”; au ingembidi aitafute siku yake ya saba ambayo ingekuwa ni tofauti na hiyo ya Mungu!!!!

  Pia kwa kadiri ya Maandiko, hesabu ya siku tuliyonayo leo hii imeanza ktk siku ya nne, ndio tunapata masaa 12 ya nuru na 12 ya giza kuifanya siku tuliyonayo leo hii. Kabla ya hapo ktk hizo siku 3 za mwanzo halikuwapo jua wala mwezi ili tuweze kubaini siku ilikuwa na masaa mangapi hata tujifikishe ktk uelewa kwamba urefu wa siku hizo saba za mwanzo ulikuwa sawa na siku saba tulizo nazo leo hii, hata Sabato aliyopumzika Mungu iwe ndio hii inayoadhimishwa ktk siku ya Jumamosi kulingana na utamaduni wa Kiyahudi wa kuzihesabu siku pamoja na miezi yake, waliotokanao huko Misri utumwani; kwahiyo kujilazimisha kuamini uongo ni zaidi ya ujinga!!!

  Sabato waliyopewa Israeli huko jangwani ilikuwa ni kivuli cha Sabato halisi inayotimilika ktk ujio wa Kristo. Ilikuwa ni halisi ktk maana kamili ya kuwa hicho kivuli kwani kivuli cha simba hakiwezi kufanana na cha kuku! Huko utumwani walikotoka kulikuwa HAKUNA kupumzika; ni kazi tu mtindo mmoja, mwaka mzima; kwahiyo mtu wa jinsi hiyo anapopewa siku ya kupumzika, kwake linakuwa ni jambo la ajabu, ndio maana kulingana na mazoea, walitoka wakaokote mana licha ya kuambiwa kwamba haitadondoshwa!!!

  Kwahiyo Mungu ndiye aliyewapa Israeli kupumzika. Akupaye kitu ndiye mwenye hicho kitu anachokupa; hivyo basi, “Pumziko” wanalopewa Israeli ni la Mungu, akiwaingiza ktk “Pumziko” lake, ktk kiwango kipi; cha mwilini, waipumzishe miili yao hapo wanapoingizwa ktk darasa la kumjifunza Mungu; kwamba ni nani; na uhusiano wao na huyo Mungu ni kivipi; wakipandishwa kiwango chao cha kiroho kutoka kuku asiyeweza kuruka kwenda kuwa tai arukaye huko juu sana!!!

  Kiwango cha kiroho cha kuku ni cha chini sana, ndio hicho cha mwilini, kile kivuli anachokiona hapo chini ardhini, ndizo hizo siku zilizogeuzwa miungu na kuabudiwa na nyingine kulaaniwa; Jumamosi ikiabudiwa na Jumapili ikilaaniwa kwamba ni siku ya “mungu jua”; siku za Mungu wakizigawa kwa miungu yao!!!

  Lakini Kanisa, wakiisha kujifunza hayo mambo kutoka hicho kivuli, ambacho ndani yake kuna Ahadi ya Ujio wa huyo Mwenye kivuli chake, hicho wanachojifunza, wao ndani yao huzaliwa shauku na kiu kubwa ya kumuona Huyo, aliye Halisi na Ukamilifu wa Kivuli hicho Chema kilichowapa pumziko; na sasa wakiwa ktk tegemeo la kuyapokea yaliyo makamilifu: “Najua kuwa yuaja Masihi, (aitwaye Kristo); naye atakapokuja, yeye atatufunulia mambo yote”

  Huyo mwanamke wa Kisamaria, aliubwaga mtungi wake wa maji akatimua mbio kwenda mjini na kuwaambia kuhusu “utamu wa maji” aliyopewa ambayo sasa yamekuwa chemchemi inayobubujikia uzima wa milele, hauhitaji tena ule mtungi wa maji wala kisima chake ambavyo vilikuwa ni kivuli cha hiyo chemchemi aliyo sasa!!! Umeliona hilo Pumziko aliloingizwa huyo mwanamke? Hendi tena kisimiani kule aliko Kayafa na maji yake yaliyojaa vyura, na viluwiluwi vya typhod ya kiroho, yeye sasa ni chemchemi!

  Je, mitume si zaidi ya huyo mwanamke Msamaria? Je, wakiisha kuwa chemchemi, wangeweza kurudi tena kunywa maji ya kisimani?? Labda wawe mazezeta au misukule ya dini!!! Hamuoni kwamba waliporudi huko kisimani watu wengi walizigeukia chemchemi hizo ili wayanywe maji hayo matamu yaliyojaa uzima ukilinganisha na hayo maji ya kisimani yenye vijidudu, na ndio sababu wakafukuzwa na wenye kufanya biashara ya maji ya visima, ambao wanaendelea hata leo hii!!?

  Roho Mtakatifu ndiye Sabato ya mwaminio, ndiye ile Raha aliyoahidiwa, ndiye lile Pumziko tuliloahidiwa, kwamba akiisha kutujilia atatuweka ktk Kweli YOOOOOTE!!! Basi hebu wazieni hili, kwamba yeyote asiye na Kweli, huyo yuko ktk MAHANGAIKO, ya kiroho na kimwili maana ni mtumwa wa fikra za watu; Lakini aliye ktk Kweli yote, huyo yu HURU na ni rubani wa maisha yake, maana ile Kweli aliyonayo humuongoza na kumfanya awe mtawala; hilo ndilo PUMZIKO lililowekwa mbele yetu, someni Ebr 4:1-7mlione hilo Pumziko, muache na kunywa maji ya visima, kiroho yanawaua polepole!

  Tukilikataa hilo basi tuupokee UJINGA utakaotuingiza ktk UPUMBAVU ili tuhesabiwe pamoja hao wasioandikwa majina yao ktk kitabu cha Uzima cha Mwana Kondoo! Basi tukiwa ktk hilo fungu la ujinga, ndipo tukisoma, Mt 17:1 “Na baada ya siku sita Yesu akawatwaa Petro, na Yakobo, na Yohana nduguye, akawaleta juu ya mlima mrefu faraghani.” Hapa tutasema alipanda nao huo mlima mrefu siku ya Sabato, maana hiyo ndiyo inayofuatia baada zile “siku sita”! Ujinga wa kujitakia haunaga aibu wala elimu, bali ni jasiri!!!

  Njooni huku ktk Jumapili, ile Siku ya Bwana, tuumege mkate ktk furaha ya kufufuka kwake, Kristo ndiye aliye tununua kwa Damu yake, hivyo sisi ni subjects wake, acheni “ufedhuli” wa kujifanya mnamjua sana Mungu Baba, hata anapowakabidhi kwa Kristo, kwa jeuri ya ufedhuli mnagoma, mnaendelea na Torati msiyoijua, ndio maana wengi mtaishia mtaroni, kwani hao Israeli watafunguliwa macho yao wampokee Kristo awe Bwana na Mwokozi wao; na kwa vile wao ni halisi, wataungana na Kanisa wakiibwaga Order yoote ya zamani na kuipokea Order Mpya, ninyi mtabakia kulia na kusaga meno huko maporini mlikojipeleka!!!

  Gbu!

 77. Ni kwa neema ya bwana nawapongeza wote mnaochangia maada ya bwana sababu kubwa ya kusali jumapili ni ukumbusho wa ufufuko wa yesu kristu pia kushuka kwa roho mtakatifu kwa njia ya hua na tunaambiwa tuwe na imani kipindi tusalipo. TUMSIFU YESU KRISTU

 78. haha mchungaji unasahau ya kwamba kuna amri kumi za Mungu ambazi zimeamrisha kuitunza siku ya sabato. ikumbuke siku ya sabato uitakase , siku sita fanya kazi na utende mambo yako YOOTE( usibakize hata limoja) …. kwa maana kwa siku sita Mungu aliifanya mbingu na nchi na akastarehe siku ya saba. siku hiyo alifanya mambo matatu. 1. alipumnzika,2 akaibariki 3 akaitakasa. kwa maana hiyo sabato ni agano takatifu la Mungu baina yake na watakatifu wake. sabati sasa ni siku ipi. umseshaitaja kwamba ni Jumamosi. hivyo kwa kutunza jumapili utakuwa unavunja amri ya 4 inayoagiza kutunza siku ya sabato, na aliyesema ikumbune sabato ndiye aliyesema usizini, usiue na mtu akikosa katika amri moja basi umezivunja zote.

 79. Kimsingi hakuna sehemu yoyote ndani ya biblia iliyobadilisha amri ya sabato. Matukio yaliyotokea jumapili wakati wa mitume hayakumaanisha kubadiliha amri ya sabato.kukusanyika jumapili sio kosa kama amri ya sabato utaishika. Tusibadilishe biblia kwavile tunataka tu iwe upande wetu. Biblia inajieleza vizuri kuhusu siku ya sabato. Yesu hakuondoa sabato maana hata ilivyofika sabato aliingia hekaluni kufundisha. Msichanganye matukio na amri. kushuka kwa roho mtakatifu siku ya pentecosti ni tukio na wala sio amri, sabato ni moja wapo ya amri kumi za mungu

 80. NAKANUSHA kwa kuwa naona hapo mlipo fika si kweli. MUNGU si kama mwanadam leo aseme hili na kesho ageuke. kabla sijasema chochote naomba mjibu na kuelezea mafungu yafuatayo: ebrania 4:1-11, ufunuo 14:12 , marko 7:7-9, mathayo 5:17…, matendo 17:1-3 yohana 14:15, yakobo 2:10, 1yohana 2:3-5

 81. Ama kweli sikio la kufa halisikii dawa. Ni ajabu kuwa pamoja na elimu kubwa hii ambayo roho mtakatifu amewawezesha watumishi wake kufafanua kuhusu umuhimu wa kuishika na kuitunza sabato bado watu wameendelea kuwa wabishi na waongo. Siku ya sabato ilikuwepo, ipo na itaendelea kuwepo milele. LWEMBE, ruhusu Roho Mtakatifu awe mwalimu wako sasa, nawe utaitambua kweli nayo kweli itakuweka huru.

 82. OSWARD,
  Tarehe 25/02/2014 at 9:28 PM,Ulianza hivi;
  “HALELUYA WAPENDWA
  MASWALA YA KUPOTOAMAANDIKO YALIKUWEPO TANGU ZAMA ZA AGANO LA KALE TUSISHANGAE KUONA LEO WATU WAKI PINGA NA KUPOTOA PIA KAMA ZAMANI SWALI LA KUJIULIZA NA KWAMBA MIAKA YA 33AD-3OOAD KULIKUWA NA MADHEHEBU MANGAPI? NINA CHOFAHAMU NI KUWA KULIKUWA NA MATABAKA MA 2 LA KWANZA WALIKUWA WAYAHUDI{WASABATO} WANAO MWAMINI YESU KRISTO NA WAYAHUDI{WASABATO }AMBAOHAWAKUMWAMINI YESU…..”
  Nakubaliana na wewe kwamba upotoshaji wa MAANDIKO haukuanza leo.Naona kama na wewe UMELIPOTOSHA NENO.
  Naomba unijibu maswali yafuatayo;
  1.WAYAHUDI ni WASABATO?
  2.WASABATO walitokea wapi na mwaka gani?
  3.WASABATO wanapatikatana wapi Kwenye BIBLIA?
  4.Mtu anapomwamini BWANA YESU anakuwa MKRISTO au MSABATO?
  5.Nini MAANA ya hili andiko, WAKOLOSAI 2:16-17 ” Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato;
  mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo” ?

 83. Dismas,
  Sabadoina dili ila hujui tu. Na kwa vile hujui, jaribu kukaa na wasabato watakueleza udili wake. Changamka kijana
  Siyi

 84. SABATO HAMNA DILI

  SOMENI NA MTAFAKARI UPYA MLIPO ANGUKA MKATUBU. MAANA BWANA AMESHARUDI NA BADO HAMTAKI KUMPOKEA YOH 1;12 WOTE WALIOMPOKEA ALIWAPAUWEZO WA KUFANYIKA WATOTO WA MUNGU.

 85. HALELUYA WAPENDWA
  MASWALA YA KUPOTOAMAANDIKO YALIKUWEPO TANGU ZAMA ZA AGANO LA KALE TUSISHANGAE KUONA LEO WATU WAKI PINGA NA KUPOTOA PIA KAMA ZAMANI SWALI LA KUJIULIZA NA KWAMBA MIAKA YA 33AD-3OOAD KULIKUWA NA MADHEHEBU MANGAPI? NINA CHOFAHAMU NI KUWA KULIKUWA NA MATABAKA MA 2 LA KWANZA WALIKUWA WAYAHUDI{WASABATO} WANAO MWAMINI YESU KRISTO NA WAYAHUDI{WASABATO }AMBAOHAWAKUMWAMINI YESU HAYA MATABAKA NDIO YALIO PIGANA VITA CHINI YA UTAWALA WARUMI NA KUPEWA SAPOT BADAE MNAMO MIAKA YA 321AD MABADILIKO YALIFANYWA NA WARUMI WAKIKUBALIANA NA WAZEE WA KANISA WALIO OGOPA VITISHO NA KUPENDA KUJULI KANA KWA WATU KAMA VIONGOZI WAKUBWA SASA BASI KABLA YA MITUME KUFA WOTE KANISA LILIKUWA SAFI HAKUKUWA NA IBAADA ZA JUMA PILI AU SIKU YA KWANZA YA JUMA IBAADA HIZO ZILIKUWA ZIKIFANYWA NA WAPAGANI{WAMATAIFA} ZILIZO AZISHWA NA WAFALME KAMA WAKINA NIMLODI………ZILIENDELEA KUENZIWA MPAKA LEO SASA TUJIULIZE JE SISI TUNAUJUA UJUMBE WA NENO KULIKO YESU NA MANABII WENGINE AU MITUME? NADHANI HILI C KWALI KAMA SI KWELI YATUPASA TUFUATE BIBLIA ISEMAVYO TUPATE KUJUA WAO WALIISHI VIPI NA SWALA ZIMA LA SABATO TUWE WAISLAELI WA KIROHO NDIPO TUTAPATA KUPONA KAKA LWEMBE SIJAONA MAANDIKO MATA KATUFU YANAPO SEMA KUWA TABIA YA MUNGU ILIONDOKA .UNAPOSEMA KUWA HAIPO UNAMKUFURU RM PIA UNATHIBITISHA KUWA MUNGU NI MZINZI MWIZI MUUAJI ………MAANA AMRI 10 NI NAKALA YA TABIA YAKE HALAFU UNAPOSOMA NYARAKA ZA PAULO YA KUPASA UOMBE UWEZA WA RM MAANA NIMEONA UNAVO ZIELEZA SIVYO ZINAVO MAANISHA
  USHAULI WANGU NI KWAMBA CHAGUA M1 WA KUTUMIKIA YESU BWNA WA SABATO AMA MNYAMA BWANA URUMI AMA KAHABA

 86. Kaka Lwembe naomba nikupongeze kwa mafundisho yako yenye ukweli na uwazi. Ndugu zetu wasabato kweli wanaijua lakini kinachowasumbua ni uwoga na aibu ya kukiri ukweli huo. Kristu alishafuta laana ya sheria pale msalabani lakini kwa wenzetu wanashindwa kuliamini hili na ndio maana ukifuatilia mafundisho yao yamejaa vitabu vya agano la kale.

 87. KUJA KWAKE KULITABIRIWA
  Mamia ya miaka hata kabla ya Yesu kuzaliwa, maandiko yaonyesha wanabii wa Israeli wakitabiri kuja kwake. Agano la kale, lililoandikwa na watu wengi katika muda wa miaka 1,500, lina unabii zaidi ya 300 kuhusu kuja kwa Yesu. Yote yaliyotabiriwa yalitendeka, pamoja na kuzaliwa kwake kimiujiza, maisha yake matakatifu, kufa na kufufuka kwake.

  Maisha aliyoishi Yesu, miujiza aliyotenda, maneno aliyosema, kufa kwake msalabani, kufufuka kwake, kupaa kwake mbinguni – yote yathibitisha kwamba yeye hakuwa mwanadamu peke yake bali alikuwa zaidi ya mwanadamu. Yesu alisema, “Mimi na Baba tu umoja” (Yohana 10:30), “Aliyeniona mimi amemwona Baba” (Yohana 14:9) na, “Mimi ndimi njia, na ukweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.” (Yohana 14:6).

 88. asanteni sana kwa maoni yenu na fikra zenu za kuweza kufikiri na kujadili kuhusu swala la kuabudu ila ninacho washauri ni soma injili ya luka utakuta kuna msemo ulisemwa na yesu kristo alipo mponya mgongwa aliyekuwa na pepo, alisema kuwa imani yako itakayokuokoa, kwa hiyo unacho kiwaza /unacho amini kile kile usibadili maana wala mawazo dunia imeisha manabii wamejaa wengi wanao muasi mungu makanisa yanaongezeka kila sehemu hebu fikiria mtu anaanzisha kanisa na kujiita yeye ni mungu, au kanisa gani utakalo enda kufanyiwa maombi unapata utajiri, mwisho wa dunia huu japo kila mwanadamu anamwisho wa dunia mwake lakini binadamu analizimisha, tubadilike tusidanganyike

 89. KAKA LWEMBE MBONA UELEWI MM SIJASEMA SHERIA ZINAOKOA ILA ANAYEOKOA NI YESU KWA HIYO TORATI KAZI YAKE ILIKUWA NI KUKUELEKEZA KWA YESU…….NDIYO,,,,,,LKN BILA AMRI ZA MUNGU TUSINGEJUA DHAMBI UNAKUBALI HAPO………SHERIA AU AMRI NI KIOO LKN KIOO HAKIONDOI UCHAFU UNAKUBALI HAPO,,,,,,NA UKISHAONA UCHAFU AMBAYO NI DHAMBI PELEKA KWA YESU PALE MSALABANI ATAZISAFISHA UPO HAPO?……. ,,, NA UKIWA NDANI YA YESU UTAVUNJA AMRI ZA MUNGU…….PIA ILI TUWEZE KUZITII AMRI LAZIMA TUWE NA ROHO MTAKATIFU KWANI HUYU NDO ANATUPA NGUVU ZA KUWEZA KUSHINDA DHAMBI KWA KUZITII AMRI ZA MUNGU

  SOMA MATHAYO 5:20 ,,,,,,,KAMA YENU HATAZIDI YA WAANDISHI NA MAFARISAYO HATUTA URITHI UFALME WA MUNGU…….UNAELEWA?
  SOMA MATHAYO 24;15—– NIELEWESHE BASI PIA LUKA 4:16 NISAIDIE KAKA
  MATENDO 13:15 NISADIE BASI
  MATENDO 16:13 NAOMBA UNISAIDIE BASI HAYA MAFUNGU UFUNUO 14:12——-NAOMBA UFAFANUZI WAKO BASI HAPA NDUGU

  MWISHO NAOMBA TUELIMISHANE JUU YA HAYA MAMBO SHIDA TUNAFANYA USHABIKI JUU YA NENO LA MUNGU
  KWANI KWA MUNGU HAKUNA KULAZIMISHA MTU MUNGU ANA DEMOCRACY SANA

  KWA UPANDE WANGU MM SIONI HAJA YA MM KUKULAZIMISHA UWE MSABATO ILA MUNGU AKIKUITAJI UTAKUJA TU ……… ILA TUTAFUNDISHANA KAMA HIVI..

  MWISHO WASABATO HUWA HAWAWEKEI WATU VIKWAZO LABDA KTK KUSALI,,,,,,LKN NYIE WENZETU MNALAZIMISHA SANA WATU WAENDE HUKO KWENU KWA KUWAWEKEA VIKWAZO MBALIMBALI SANA PIA MNASAIDIWA NA SERIKALI SANA ….UKITAKA KUJUA LEO SERIKALI ITANGAZE JUMAPILI KUWA NI SIKU YA KAZI KAKA UTAKUTA MTU YUPO JUMAPILI KANISANI———KWA HIYO WASABATO TUNAENDA BADO KANISANI KWA NGUVU ZA MUNGU TU LKN INGEKUWA DUNIA HII TUNAVYOWEKEWA VIKWAZO VINGI MARA WANAFUNZI HADI SHULE ZA SERIKALI WANAAMBIWA WAENDE JUMAMOSI KUSOMA ,,,UKIENDA MAKAZINI ACHA KILA MAENEO,,,, NAAMINI HAYA YOTE YATAPITA TU……HII YOTE NI MIPANGO YA MAKANISA YENU,,,,,,LKN SISI WASBATO TUNAISHI NA WENZETU VIZURI SANA TUNAFUNDISHANA HAKIKUBALI AWE MSABATO OKEYYYYY…..KAKA NYIE MNALAZIMISHA KWA KUWEKA VIKWAZO AU KUFANYA MIUJIZA ,,,,,,,FUNDISHA NENO……..

  KUNA MCHUNGAJI MMOJA WA KILOKOLE NAMPENDA SANA HUWA ANASEMA HIVI,,,,,,,NAMNUKUU ::: KAMA WAKIRISTO WOTE WANGEKUWA WANAFUNDISHA BIBLIA KAMA WASABATO HAKIKA DUNIA YOTE INGEOKOKA….

  TATIZO KAKA HATA NYIE MKO KIFEDHA SANA MMEWEKA FEDHA MBELE SANA,,,,NA MIUJIZA LKN NENO AU KWELI HAIMO
  MFANO NENDA PALE MWANZA UTAKUTANA NA BABA GOD,,,,,NENDA ARUSHA GEO DEVI SIKIA MAMBO YAO NA VISA VYAO

  KANISA LA SDA WAMETULIA SANA ULISHAONA WAMO KWENYE MAMBO YA SIASA KAZI YAO NI KUHUBIRI NENO NA NDO MAANA SASA MNAANZA KUWAAMBIA TUACHANE NA SABATO YA WAISLAELI TWENDE KWENYE SABATO BANDIA YA KIROMA…

  MWISHO TUACHANE NA HUU MJADALA HAUNA MSINGI WOWOTE KAKA TUMWACHIE ROHO MTAKATIFU MWENYEWE AFANYE KAZI YAKE
  KWANI MM NAAMINI SISI WOTE NI WA MUNGU NA MUNGU NDO ANAWEZA KUMBADILISHA MTU MFANO SAULI

  NAOMBA USIHUKUMU USIJE UKAHUKUMIWA KAKA,,,,,UKISEMA FULANI NI KIPOFU UNAWEZA WW UKAWA KIPOFU ZAIDI YAKE

  NAOMBA MUNGU AKUBARIKI SANA ILA NAOMBA UFAFANUZI JUU YA HAYO MAFUNGU PIA NA ISAYA 66:22- NA KUENDELEA
  NA DANIEL 7 YOTE

 90. Matiku,

  Mbona unamoyo mgumu namna hiyo? Unaona tabu gani kuipokea Injili? Achana na mambo ya kujitungia ndg yangu, si unaona yalivyokuharibu!

  Habari Njema inatangaza hivi kwamba: “Kristo ni Mwisho wa Sheria”!
  Jambo hili la maanisha kwamba Torati yoote inakomea hapo, ukiisha kuwa umeielewa kikamilifu, ndiposa unaweza kuipokea Neema!

  Tunapitishwa katika Agano la Kale, ili kumjua Mungu, nayo Sheria ndiyo inayoiweka Dhambi na Nguvu yake peupe! Na mwisho wa mafunzo hayo lazima UKUONE KUSHINDWA, la hujakuona basi jua ya kwamba mafunzo hayakukusaidia kitu, umebaki mkavu kama ulivyokutwa, tena yawezekana ukawa umekauka zaidi baada ya kuwa umeizoelea Dhambi katika namna ya kinafiki kunakokufanya udhani kwamba unaliamini Neno la Mungu, kumbe ni Mpingaji uliyekubuhu!

  Hakuna Mkristo aliyezaliwa mara ya pili anayeishi kwa hizo Amri Kumi! Hayo ni mambo ya Kale ndg yangu, wewe una umri gani mpaka una ng’ang’ana na mambo ya kale?! Mafundisho yenu yamewalaza usingizi wa pono mchana huu wenye Nuru kali, mpaka mnashangaza!! Njoo huku katika Nchi Mpya ujazwa RM uyafurahie maisha, huku hakuna mambo ya kumheshimu baba yako, sijui Usiibe au usizini sijui mpende Bwana Mungu wako, sijui USIABUDU SIKU nk, huku brother unapewa kila kitu kipya, moyo safi uliojaa upendo, roho mpya yenye kiu na Mungu na Roho wa Mungu mwenye kukuongoza katika Njia zake. Si unaona mnavyojiongoza safari ya msikokujua kwa udanganyifu mlioupokea!

  Uyahudi mnaoung’ang’ania ni wa fadhila za Mungu tu kwamba nanyi mtahesabika katika kundi hilo katika Urithi na si kinasaba! Lakini hata hiyo fadhila yenyewe mmeikataa kwa kulikataa Fundisho la mitume linalowakataza kuwa na mwalimu mwanamke, ambavyo kwa ujeuri mmemsimika Ellen White nanyi kama wakatoliki!

  Kuhusu Kornelio, kaka kwa vile uko gizani tu ndio maana unakuja na maneno yasiyoeleweka! Kornelio sadaka zake na sala zake zilipokelewa mbinguni, lakini yeye asingepokelewa maana Mungu hanazo FUNGUO za Ufalme wa Mbingu, Kristo alizikabidhi kwa Petro, ndio maana ilimbidi aje AMFUNGULIE aingie!!! Mitume ndio Mwili wa Kristo!

  Wewe huna imani ya kukufanya usiwe Mmataifa, wewe ni mpagani wa kilsasa “Mtu hataishi kwa mkate pekee bali kwa KILA neno litokalo katika kinywa cha Mungu” kinywa cha mungu ni nani? Mitume na manabii! Hebu nawe vitafute vifungu nilivyowapa wajoli wenzako mjipime pamoja nao, nawe najua utavikataa kama nduguzo, basi kwa kulikataa kwenu neno moja tu, ni wafu tayari! Nao wafu hawajui neno lolote!!!

  Kuhusu “hela” nitumie basi mdogo wangu hata kidogo tu!!! Au hizo na vimiradi vya kanisa ndio vinawapiga lock mpaka hamna jinsi ya kulipokea Neno la Mungu? Jihadhari yasikukute ya Yuda Iskariote!!

  Ubarikiwe, Matiku, rafiki yangu wa siku nyingi, ulikuwa chuo nini?!

 91. PIA MBONA WAPO WATU WANAJIITA MANABII HAPA TANZANIA MNAWAKUBALI KWA HIYO ILIKUWA NI KOSA BI WHITE KUSEMA YEYE NI NABII?,,,,,,,,, TAFUTA SIFA ZA NABIII HALAFU PIA SOMA VITABU VYA ELENI G WHITE KAMA VINAPINGANA NA BIBLE?,,,,,,,,,,JAMANI MBONA BABU WA LOLIONDO ALIWATEKA TENA KWA MDA MFUPI MKAAMINI AU KWA SABABU HAKUWA MSABATO?

 92. DENIS NA WENGINE BWANA YESU AWE NANYI;;;;;;;

  KAKA LWEMBE IMANI CHANZO CHAKE NI KUSIKIA NENO LA KRISTO…….NAAMINI UMESIKIA SANA NA UMESOMA .

  SAWA SANA KAKA LWEMBE KWA HIYO HUYU MUNGU AMRI 9 ZILE ALIWAPA HATA WATU MATAIFA ILA ISIPOKUWA SABATO TU,,,,,,NDO ALIWAPA WAYAHUDI TU

  ACHA CHEKESHA WW TAFUTA HELA TU KAKA……..

  NDO MAANA YULE KORNELIO AKIDA WA KIITALIA SOMA MATENDO 10 YOTE HUYU ALIKUWA NI MTU WA MATAIFA LKN MUNGU ALIMWEELEKEZA KWA PETRO ILI AKAMWAMBIE MAMBO YA KUFANYA,,,,,NA PETRO ALIKUWA NI MYAHUDI SIJUI HAPA UNASEMAJE MBONA AKUMWELEKEZA AENDE KWA WARUMI KULE ROMANI………HATUWI WAISLAEL KWA KUZALIWA ILA NI IMANI MBONA MUNGU AKUPITIA KWA WATU WAMATAIFA ,,,,,,,NASEMA MM NI MUISLAELI KWA IMANI SIYO MTU WAMATAIFA KWANI MTU WAMATAIFA NI YULE MPAGANI AMBAYE BADO AMWAMINI YESU NA ANAKATAA 10 AMRI ZA MUNGU

  SIKU NJEMA

 93. Denis,
  Pole ndg yangu, sikuyaona maswali yako, mpaka leo hii!
  Tatizo ulilonalo Denis ni kubwa kuliko unavyowaza! Umepoteza Identity, haujitambui wewe ni nani, walimu wako wamekutumbukiza katika “assumed identity”; ndio maana unajidhania kuwa wewe ni Myahudi!

  Ndg yangu wewe ni Mmataifa, Mungu alitutengea Paulo ili awe mwalimu wetu katika kutuleta kwa Kristo kupitia Torati, tukiunganishwa pamoja na Wayahudi walioipokea Habari Njema! Hayo unayoyadhania ni yako si yako. Wayahudi ambao hawakumpokea Kristo wangali wanaendelea katika Sheria yoote. Nao unabii unaowahusu ungali kazini na unaendelea kuwatimilia. Ndio maana niliwahi kuwaambia jiungeni nao kikamilifu, msikae nusu nusu, mguu mmoja ndani mwingine nje! Sabato ya Kiyahudi ndiyo hiyo hapo, siku ya Jumamosi, hiyo ndiyo siku yao ya saba katika hesabu zao, ambayo ninyi mnaiabudu!!!

  Tena nilikuambia kuwa kuanzia makundi yalipogawanywa, kila kundi linaendelea katika Unabii wake. Ni ninyi pekee ndio ambao mnaelea na kusombwa ovyo na kila wimbi! Kwa Kristo hamko na wala kwa Musa hamko!!! Ah sawa mko kwa Ellen White, na nabii zake!!!

  Hebu rudi kwenye vile vifungu nilivyowaletea mjipime kama kweli ninyi mnaiamini Biblia halafu ndio uje tuzungumze, kuliko sasa hivi ambavyo hamueleweki, hata imani yenu iko wapi!

  Gbu

 94. Mkaka,
  Ha ha ha ha Ubarikiwe kwa utenzi makini. Nimeupenda sana.
  Denis,
  Kazi yako si bure mjoli wa Bwana. Songeni mbele kwa umoja mkiuangazia ulimwengu kweli ya Mungu. Amina

 95. Napa lipo NAHALISI jihadhari na BANDIA.

  Yesu alionya mbele UNABII UMETIMIA.

  Ndugu yangu zingatia maonyo usije ukaangamia.

  Dunia imefika mwisho kimbilia kwa Mwokozi.

  Dunia imefika mwisho kimbilia kwa Mwokozi.

  Anza leo tafuta sasa kwaBwana imani yako iimarike.

  Jee unampenda Yesu ?

  Jee unafanana naye, unashika amri zake?

  IBADA ni NYINGI inashangaza YESU ni BWANA wa SABATO.

  Anza soma leo, NENO TAFUTA SASA IMANI YAKO ITHIBITIKE.

  Kwa rehema na fadhili ughairi na mabaya. YESU akuita kwake na fidia amelipia.

  Ndugu yangu kimbilia wokovu usije ukaangamia.

  ITIIKA AKUITA SASA SHIKAMANA NA MWOKOZI.

  Anza leo tafuta sasa kwaBwana imani yako iimarike.

  Jee unampenda Yesu ?

  Jee unafanana naye, UNASHIKA AMRI ZAKE?

  IBADA ni NYINGI inashangaza YESU ni BWANA wa SABATO. .

  Anza soma leo, NENO TAFUTA SASA IMANI YAKO ITHIBITIKE.
  Mbarikiwe.

 96. Ndugu lwembe,sijaona chochote ambacho unakibishia hapa na maelezo yako yote ni ya bure na hayapo kwenye msingi wa kimaandiko unazidi tu kujidanganya mwenyewe na hutozidi kumdanganya mtu yeyote hapa,
  ”lakini watu wabaya na wadanganyaji wataendelea,na kuzidi kuwa waovu,wakidanganya na kudanganyika”(2timotheo 3;13)
  Sasa wewe lwembe usijichukulie vifungu na kuvisoma juujuu bila ya kuvielewa maana yake na hata kama umekielewa kimoja hebu tafuta na kingine uzidi kuvielewa kwa undani zaidi jinsi maandiko matakatifu yanavyosema,”kwa maana ni amri juu ya amri,amri juu ya amri,kanuni juu ya kanuni,kanuni juu ya kanuni,huku kidogo na huku kidogo”(isaya 28;10) na utavielewa kiundani zaidi na sio kubisha hapa bila msingi wa kimaandiko.
  Hivi lwembe huwa unajifikiria nini Mungu anaposema ya kwamba ”kwa ajili ya hayo wana wa israeli wataishika hiyo sabato katika vizazi vyao vyote,ni agano la milele na ni ishara kati ya mimi na wana wa israeli milele;kwani kwa siku sita Bwana alifanya mbingu na nchi,akastarehe kwa siku ya saba na kupumzika (kutoka 31;16-17) na Mungu anaposema milele kwa vizazi vyao vyote huwa ana maana gani au hilo fungu hulielewi? na pia anaposema ya kwamba
  ”msifanye kazi yoyote;ni amri ya milele katika vizazi vyenu vyote,na katika makao yenu yote,na itakuwa kwenu sabato ya kustarehe kabisa ,nanyi mtazitesa nafsi zenu; siku ya kenda ya mwezi wakati wa jioni,tangu jioni hata jioni,mtaishika hiyo sabato yenu (mambo ya walawi 23;31-32) na huwa mna maana gani kwenu ninyi nyote mnaoibeza sabato ya Mungu wetu
  Na tena anaposema ya kwamba”kama vile mbingu mpya na nchi mpya ,nitakazo fanya ,zitakavyokaa mbele za Mungu ,asema Bwana ,ndivyo uzao wenu na jina lenu litakavyokaa na itakuwa ,mwezi mpya hata mwezi mpya na sabato hata sabato wanadamu wote watakuja kuabudu mbele zangu asema Bwana(isaya 66;22,23)
  AU LWEMBE KWA UCHACHE MAFUNGU HAYO NILIYOYATAJA HUYAELEWI?AU UNAENDELEA TU KUBISHANA NA BIBLIA JINSI INAVYOSEMA,NAWASHAURI NINYI NYOTE MRUDIENI MUNGU,NA JIFUNZENI BIBLIA AMBAYO NDIYO KWELI NA KWELI ITAWAWEKA HURU

 97. Siyi,
  Mbona umerudi nyuma saana ndg yangu? Siamini kuwa ni wewe, maana haya uliyoyaleta ni mkanganyiko mtupu, hayafai hata kwa hadithi za kijiweni! Ngoja nikuoneshe machache tu kama Mungu atakufungua macho yako kama alivyomfungua Gehazi, ili angalau ujionee mwenyewe bila kuhadithiwa!

  “”2. Hii iliweka muhuri [katika] siku hiyo kama siku ya Mungu kupumzika, au siku ya Sabato, kama siku ya Sabato [basi] humaanisha siku ya kupumzika.””
  Hii ni sehemu ya ule uongo mlioaminishwa, wewe mwenyewe wafahamu kwamba Haukuna Andiko linalotamka kuwa Sabato ni Muhuri wa Mungu. Na tamko kama hili si jambo dogo katika wakati huu ambao sote tunafahamu ni ule wakati wa Roho Mtakatifu, kwa hiyo kumsingizia jambo kama hili, inahuzunisha sana sijui mnategemea nini, au ndio sikio la kufa?

  “”3. Kwa hiyo siku ya saba lazima iwe siku ya Sabato ya Mungu.””
  Jambo hili ukilirejea bila kulazimisha, ni jema saana! Mwa 2:2 “Na siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya; akastarehe siku ya saba, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoifanya.” Hii ndiyo Sabato ya Mungu, huyo aliyefanya kazi siku sita!

  “”6. Aliifanya siku ya Sabato katika bustani ya Edeni. Mwanzo 2:1-3.””
  Huu ni uongo mwingine mliolishwa na matokeo yake umewafanya muwe ni watu wenye kujiridhisha katika uongo na hivyo kudumu katika hali hiyo kwa furaha yote! Hiyo Mwa 2:1-3 hii hapa, “Basi mbingu na nchi zikamalizika, na jeshi lake lote. 2-Na siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya; akastarehe siku ya saba, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoifanya. 3-Mungu akaibarikia siku ya saba, akaitakasa kwa sababu katika siku hiyo Mungu alistarehe, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoiumba na kuifanya. “ Ni wapi katika vifungu hivi vya Maandiko panaposema kuwa Mungu “Aliifanya siku ya Sabato katika bustani ya Edeni”?

  “”7. Ilifanywa kabla ya kuanguka [kwa Adamu]; na hivyo basi si kivuli, kwani vivuli havikutolewa mpaka baada ya kuanguka.””
  Ukiisha umeza huo uongo wa na. 6, huu wa 7 unateleza tu bila hata ya mate!!!

  “”8. Yesu alisema kuwa ilifanywa kwa ajili ya mwanadamu (Marko 2:27 ); ina maana, kwa ajili ya jamii, kadiri ambavyo neno mwanadamu halijawekewa mipaka, hivyo, kwa Mataifa na hali kadhalika Wayahudi.””
  Punguzeni kujiongopea! Huyo Yesu anayeyasema hayo katika hiyo Marko kwamba sabato ilifanywa kwa ajili ya mwanadamu, yeye anaijua hiyo sabato anayoizungumzia kuliko ninyi akina Siyi mnaoyarukia tu Maandiko kujenga hoja zenu za kujinyonga! Yesu ndiye Bwana wa Sabato, yeye ndiye mwenye Sabato yake uliyoisoma kule Mwa 2:2; na huko jangwani ndiko aliwapa hizo sabato zake, hizo anazokuambia kwamba zimefanywa kwa ajili yao, Eze 20:12 “Tena naliwapa sabato zangu, ziwe ishara kati ya mimi na wao, wapate kujua ya kuwa mimi, BWANA, ndimi niwatakasaye.” Umeelewa kwanini Yesu aliwaambia kuwa sabato ilifanywa kwa ajili ya mwanadamu na si mwanadamu kwa ajili ya sabato, yaani msije kwa kiu yenu ya kuabudu miungu mkaanza kuabudu siku, kwamba muigeuze hiyo siku kuwa ndio muhuri wa Mungu na mtakaswe kwayo, ni upagani wa kisasa katika jina la ukristo!!!

  “”9. Ni kumbukumbu ya uumbaji. Mwanzo 20:11; 31:17. Kila wakati tunapopumzika siku ya saba, kama Mungu alivyofanya wakati wa uumbaji, tunaadhimisha tukio kuu.””
  Unapoyachukua mafundisho yenu yaliyojaa uongo, jaribu kuyahakiki kidogo badala ya kuyapachika tu mbele ya watu ukitegemea uvivu mlionao ninyi wa kuyakagua hayo kabla ya kuyameza, basi watu wote watakuwa hivyo, au umewawekea hao wadogo zako ili wasije wakakukimbia? Haya tazama ukweli wa Maandiko uliyoyanukuu ili ukusaidieni kuwa na uhakika kuhusu uongo mnaolishwa:
  Mwa 20:11 “Ibrahimu akasema, Kwa sababu naliona, Yakini hapana hofu ya Mungu mahali hapa, nao wataniua kwa ajili ya mke wangu”
  Mwa 31:17 “Ndipo Yakobo akaondoka, akapandisha wanawe na wakeze juu ya ngamia.”
  Vifungu hivi vina uhusiano gani na kumbukumbu ya uumbaji? Mnasikitisha saana nyie watoto wa Ellen White, msizisome Biblia zenu kutoka vichwa vilivyojazwa uongo!

  10-11 Ilitolewa kwa Adamu, kichwa cha jamii ya wanadamu. Marko 2:27; Mwanzo 2:1-3.”
  Sina hata haja ya kuyanukuu Maandiko hayo pamoja na hiyo Mdo17:26 maana ni uongo ule ule unaoendelea bila ya aibu! Adamu hajawahi kupewa Sabato na wala hakuna fundisho linalosema kuwa “Adamu, kichwa cha jamii ya wanadamu.” Sijui ni Biblia gani mnayoitumia!!!

  “”12 13. Siyo taasisi [fundisho] ya Kiyahudi, kwani ilifanywa miaka 2,300 kabla hata Myahudi kuwepo.””
  Azima Biblia ya KJV kwa rafiki yako yeyote yule, soma kwa taratibu, utagundua kuwa Sabato ilikuwa ni kwake Mungu, Pumziko lilikuwa ni la Mungu ndio maana anasema nikawapa Sabato zangu; na aliwapia huku jangwani! Kama mnakuwa na ubishi wa dini, huo hautawafaa kitu, vinginevyo jaribuni kusoma na vitabu vingine muone kama Wamisri walikuwa na sabato, au wao Adamu hawahusu? Ndio maana inaitwa “sabato ya Kiyahudi” kwa sababu ni wao tu katika dunia nzima ndio waliopewa hiyo, na ndio wenye kujua kuwa kumbe Mungu alipumzika siku ya saba!

  14. Rejea zenye ushahidi zinafanywa kuhusiana na Sabato katika kipindi chote cha Wazee wa zamani. Mwanzo 2:1-3; 8:10 , 12; 29:27, 28, n.k.
  Haya hebu tuendelee na Uongo wa mafundisho yenu:
  Mwa 2:1-3 Hakuna hata mzee wako hapo bali yuko Mzee wa Siku tu akiizungumzia Sabato yake.
  Mwa 8:10 “Akangoja na siku saba tena; kisha akamtoa yule njiwa katika safina mara ya pili” Sioni ni kwa vipi sabato inahusika hapa katika siku za Nuhu kwa kifungu hiki hata huo mstari wa 12 unaosema, “Akangoja na siku saba tena, akamtoa yule njiwa; naye asimrudie tena kamwe”! Au kila mnapoliona neno “saba” katika Maandiko basi ninyi kwenu ni sabato??

  Mtakuwa mmejichanganya saana kwa kule kudhani kwenu kwamba Mungu ameishiana na Wayahudi! Mlipolikataa Neno la kurejezwa kwa Israeli wakati wetu utakapokwisha, ndipo mlipojikabidhi kwa roho zidanganyazo!! Hebu ninyi wenyewe yatazameni hayo uliyoyaleta Siyi, amabyo nduguzo wanayashangilia sana kwamba ndio ukweli wa Biblia, je si aibu hiyo?

  Kwa sababu wewe ni ndg yangu, kwa upendo inanibidi niishie hapa ili nisiendelee kukuumbua maana ni sawa na kujiuumbua mwenyewe na zaidi kumuumbua Bwana hapo watu watakapo tusoma na kukumbuka jinsi tunavyojidai kuifuata Biblia halafu wanakuta madudu kama haya!

  Wasaidie na hao nduguzo walioikimbia Nuru na kulifuata GIZA! Hao ni kweli walikuwa katika Nuru, hili Agano Jipya liutangazao Wokovu kwa wote kwa Neema iliyo katika Kristo; lakini wakajirudisha huko kiliko KIVULI ambacho sasa hivi, wakati huu wa jioni, tunapomngojea Masihi, huko kumekwisha kuwa GIZA TOTORO, ndio maana unaona mnajibandikia tu Maandiko halafu mnadhani ni sawa tu kwa vile hamuoni huko Gizani! Ondokeni huko Gizani, hilo Agano mnaloling’ang’ania halipo limekwisha toweka siku nyingi sana zaidi ya miaka 2000 iliyopita! Ebr 8:13
  “Kwa kule kusema, Agano jipya, amelifanya lile la kwanza kuwa kuukuu. Lakini kitu kianzacho kuwa kikuukuu na kuchakaa ki karibu na kutoweka.” KJV inasema “… is ready to vanish”, haya ni siku hizo za akina Paulo, walipokuwa wakifundisha, nao wote waliojazwa Roho Mtakatifu kuanzia siku hizo, kwao Agano hilo lilifutika,. Ndio maana ninawasisitizia ndg zangu tubuni kuhusu haya mambo yenu ya uongo mnayofundishana, mpate kuokoka!

  Mbarikiwe nyoote!!

 98. LWEMBE huwa anabishana na maandiko yaliyo wazi na kuleta tafsiri zake.

  na kuandika maneno mengi ili kushawishi kwa hoja. Badala ya kushawishi kwa

  maandiko. Kama ingekuwa kweli strictly Gospel bila maneno ya mdomo wake injili

  ingemshinda.

 99. SIYI, MUNGU AZIDI KUKUBALIKI KWA KAZI UNAYOIFANYA YA KUIELIMISHA JAMII JUU YA SABATO YAKE TAKATIFU,NA TENA TUMSUBIRIE LWEMBE TUONE ATAKACHOBISHIA NI NINI KWA MAANA HUPENDA KUBISHA SANA HATA KWA VITU VILIVYOWAZI KWETU SISI WANADAMU KUTOKA KWENYE BIBLIA TAKATIFU.

  BALIKIWA.

 100. SABABU 100 ZA UKWELI WA SABATO

  Kwa nini kutunza siku ya Sabato?
  Ni nini kusudi la Sabato?
  Je, ilifanywa lini, nani aliifanya, na kwa ajili ya nani?
  Siku ipi ni Sabato ya kweli?
  Wengi hutunza siku ya kwanza ya juma, au Jumapili.
  Ni mamlaka gani ya Biblia waliyo nayo kwa kufanya hivyo?
  Wengine hutunza siku ya saba, au Jumamosi.
  Ni Maandiko gani waliyo nayo kwa kufanya hivyo?

  Hapa kuna ukweli kuhusiana na siku zote mbili, kama zilivyoelezwa
  wazi wazi katika neno la Mungu.

  Sababu Sitini za Biblia Kuhusiana na Siku ya Saba

  1. Baada ya kufanya kazi siku sita za kwanza za juma katika kuumba dunia hii, Mungu mkuu alipumzika siku ya saba. Mwanzo 2:1-3.

  2. Hii iliweka muhuri [katika] siku hiyo kama siku ya Mungu kupumzika, au siku ya Sabato, kama siku ya Sabato [basi] humaanisha siku ya kupumzika. Kwa kufafanua: Wakati mtu anapozaliwa siku fulani, siku hiyo huwa siku yake ya kuzaliwa. Kwa hiyo wakati Mungu alipopumzika siku ya saba, siku hiyo ilikuwa siku yake ya mapumziko, au siku ya Sabato.

  3. Kwa hiyo siku ya saba lazima iwe siku ya Sabato ya Mungu. Je, waweza kubadili siku yako ya kuzaliwa kutoka katika siku uliyozaliwa kwenda katika siku ile ambayo hukuzaliwa? Hasha. Wala huwezi kubadilisha siku ya mapumziko ya Mungu kwenda katika siku ambayo hakupumzika kamwe. Hivyo basi siku ya saba bado ni siku ya Sabato ya Mungu.

  4. Mwumbaji aliibariki siku ya saba. Mwanzo 2:3.

  5. Aliitakasa siku ya saba. Mwanzo 20:11.

  6. Aliifanya siku ya Sabato katika bustani ya Edeni. Mwanzo 2:1-3.

  7. Ilifanywa kabla ya kuanguka [kwa Adamu]; na hivyo basi si kivuli, kwani vivuli havikutolewa mpaka baada ya kuanguka.

  8. Yesu alisema kuwa ilifanywa kwa ajili ya mwanadamu (Marko 2:27 ); ina maana, kwa ajili ya jamii, kadiri ambavyo neno mwanadamu halijawekewa mipaka, hivyo, kwa Mataifa na hali kadhalika Wayahudi.

  9. Ni kumbukumbu ya uumbaji. Mwanzo 20:11; 31:17. Kila wakati tunapopumzika siku ya saba, kama Mungu alivyofanya wakati wa uumbaji, tunaadhimisha tukio kuu.

  10. Ilitolewa kwa Adamu, kichwa cha jamii ya wanadamu. Marko 2:27; Mwanzo 2:1-3.

  11. Hivyo kupitia kwake [Adamu], kama mwakilishi wetu, na kwenda kwa mataifa yote. Mdo 17:26.

  12. Siyo taasisi [fundisho] ya Kiyahudi, kwani ilifanywa miaka 2,300 kabla hata Myahudi kuwepo.

  13. Biblia kamwe haiiti Sabato ya Kiyahudi lakini mara zote “Sabato ya Bwana Mungu wako.” Watu wanapaswa kuwa waangalifu namna wanavyoipatia jina lisilofaa siku takatifu ya Mungu ya kupumzika.

  14. Rejea zenye ushahidi zinafanywa kuhusiana na Sabato katika kipindi chote cha Wazee wa zamani. Mwanzo 2:1-3; 8:10 , 12; 29:27, 28, n.k.

  15. Ilikuwa ni sehemu ya sheria ya Mungu kabla ya Sinai. Mwanzo 16:4, 27-29.

  16. Kisha Mungu aliiweka katika kiini cha sheria yake takatifu. Mwanzo 20:1-17. Kwa nini aliiweka pale ikiwa isingekuwa kama mausia mengine tisa, ambayo yote yanadhihirisha kuwa hayabadiliki?

  17. Sabato ya siku ya saba iliamuriwa na sauti ya Mungu aliye hai. Kumb 4:12, 13.

  18. Kisha aliiandika amri kwa kidole chake mwenyewe. Mwanzo 31:18.

  19. Aliichora katika jiwe linalodumu, ikidhihirisha asili yake ya kutokuharibika. Kumb 5:22.

  20. Ilitunzwa kitakatifu katika sanduku [la agano] katika patakatifu pa patakatifu. Kumb 10:1-5.

  21. Mungu alikataza kazi siku ya Sabato, hata katika nyakati za kuharakisha sana . Kutoka 34:21.

  22. Mungu aliwaangamiza Wayahudi jangwani kwa sababu waliinajisi Sabato. Ezekieli 20:12, 13.

  23. Ni ishara ya Mungu wa kweli, ambayo kupitia hiyo tunatakiwa kumjua yeye [Mungu] kutoka kwa miungu ya uongo. Ezekieli 20:20.

  24. Mungu aliahidi kwamba Yerusalemu ingesimama milele kama Wayahudi wangetunza Sabato. Yeremia 17:24, 25.

  25. Aliwapeleka utumwani Babeli kwa kuivunja [Sabato]. Nehemia 13:18.

  26. Aliuangamiza Yerusalemu kwa kuinajisi [Sabato]. Yeremia 17:27.

  27. Mungu ametangaza mbaraka wa pekee kwa Mataifa yote yatakayoitunza [Sabato]. Isaya 56: 6, 7.

  28. Hii [Sabato] iko katika unabii ambao unarejea kikamilifu katika kipindi cha Ukristo. Isaya 56.

  29. Mungu ameahidi kumbariki kila mtu anayetunza Sabato. Isaya 56:2.

  30. Bwana anatutaka kuiita “siku yenye heshima.” Isaya 58:13. Jihadhalini sana , enyi mnaofurahia kuiita “Sabato ya Kiyahudi ya zamani,” “nira ya kifungo,” n.k..

  31. Baada ya Sabato takatifu kuwa imekanyagwa chini kwa “vizazi vingi,” itarejeshwa katika siku za mwisho. Isaya 58:12, 13.

  32. Manabii wote watakatifu waliitunza siku ya saba.

  33. Wakati Mwana wa Mungu alipokuja, aliitunza siku ya saba maisha yake yote. Luka 4:16; Yohana 15:10. Hivyo, alifuata kielelezo cha Baba yake wakati wa uumbaji. Je, hatutakuwa salama kwa kufuata kielelezo cha Baba na Mwana?

  34. Siku ya saba ni siku ya Bwana. Angalia Ufunuo 1:10; Marko 2:28; Isaya 58:13; Kutoka 20:10.

  35. Yesu alikuwa Bwana wa Sabato (Marko 2:28 ); hii ina maana [kuwa], kuipenda na kuitunza, kama mume alivyo bwana wa mwanamke, kumpenda na kumthamini. 1 Petro 3:6.

  36. Aliitetea Sabato kama amri ya rehema iliyopagwa kwa ajili ya mema ya mwanadamu. Marko 2:23-28.

  37. Badala ya kuitangua Sabato, kwa uangalifu alifundisha namna ilivyotakiwa kutunzwa. Mathayo 12:1-13.

  38. Aliwafundisha mitume wake kwamba hawatakiwi kufanya lolote siku ya Sabato lakini kilichoamuriwa “kisheria.” Mathayo 12:12.

  39. Aliwaelekeza mitume wake kwamba Sabato kwa maombi ilipaswa kuangaliwa miaka 40 baada ya ufufuo wake. Mathayo 24:20.

  40. Wanawake watauwa waliokuwa wamekaa pamoja na Yesu kwa uangaifu walitunza siku ya saba baada ya kifo chake. Luka 23:56.

  41. Miaka thelathini baada ya ufufuo wa Kristo, Roho Mtakatifu kwa wazi anaiita “siku ya Sabato.” Mdo 13:14.

  42. Paulo, mtume kwa Mataifa, aliita “siku ya Sabato” mwaka 45 BK. Mdo 13:27. Je, Paulo hakujua? Au tuwaamini walimu wa kisaa, wanaodai kwamba ilikoma kuwa Sabato wakati wa ufufuo wa Kristo?

  43. Luka, mwanahistoria wa Kikristo aliyevuviwa, akiandika baadaye mwaka 62 BK, anaiita “sikuya Sabato.” Mdo 13:44.

  44. Waongofu Mataifa waliita Sabato. Mdo 13:42.

  45. Katika Baraza kuu la Kikristo, mwaka 52 BK, mbele ya mitume na maelfu ya wafuasi, Yakobo anaiita “siku ya Sabato.” Mdo 15:21.

  46. Ilikuwa ni desturi kuwa na mikutano ya maombi katika siku hiyo. Mdo 16:13 .

  47. Paulo alisoma maandiko katika mikutano ya hadhara katika siku hiyo. Mdo 17:2, 3.

  48. Yalikuwa ni mazoea yake kuhubiri katika siku hiyo. Mdo 17:2.

  49. Kitabu cha Matendo ya Mitume hutupatia kumbukumbu ya yeye kuendesha mikutano themanini na nne katika siku hiyo. Angalia Mdo 13:4, 44; 16:13 ; 17:2; 18:4, 11.

  50. Hayakuwepo mashtaka yoyote baina ya Wakristo na Wayahudi kuhusiana na siku a Sabato. Huu ni uthibitisho kwamba Wakristo bado waliitunza siku ile ile ambayo Wayahudi waliitunza.

  51. Katika mashtaka yao yote dhidi ya Paulo, hawakumshtaki kwa kuiacha siku ya Sabato. Kwa nini hawakufanya hivyo kama hakuitunza?

  52. Paulo mwenyewe alitangaza wazi wazi kwamba alikuwa ameitunza sheria. “Mimi sikukosa neno juu ya sheria ya Wayahudi, wala juu ya hekalu, wala juu ya Kaisari.” Mdo 25:8. Je, ni namna gani hii ingekuwa kweli kama angekuwa hajatunza Sabato?

  53. Sabato inatajwa katika Agano Jipya mara 59, na mara zote ni kwa heshima, ikibeba heshima iliyokuwa nayo katika Agano la Kale, “siku ya Sabato.”

  54. Hakuna neno lililosemwa katika Agano Jipya kuhusu Sabato kuondolewa, kutanguliwa, kubadilishwa, au kitu chochote cha aina hiyo.

  55. Mungu alikuwa hajapata kutoa ruhusa kwa mtu yeyote kufanya kazi katika siku hiyo. Msomaji, ni kwa mamlaka gani unatumia siku ya saba kwa kazi za kawaida?

  56. HakunaMkristo wa Agano Jipya, ama kabla au baada ya ufufuo, aliyepata kufanya kazi ya kawaida siku ya saba. Tafuta mfano wa kitu kimoja tu cha aina hiyo, na tutalisalimisha suala zima. Kwa nini Wakristo wa kisasa wafanye tofauti kutoka kwa Wakristo wa Biblia?

  57. Hakuna kumbukumbu kwamba Mungu alipata kuondoa mbaraka wake au utakaso kutoka siku ya saba.

  58. Kama tu Sabato ilivyotunzwa katika Edeni kabla ya kuangka, ndivyo itakavyotunzwa milele katika nchi mpya baada ya ukombozi. Isaya 66:22, 23.

  59. Sabato ya siku ya saba ilikuwa ni sehemu ya sheria ya Mungu, kulingana na ilivyotoka katika kinywa chake mwenyewe, na ikaandikwa kwa kidole chake mwenyewe juu ya jiwe katika Sinai. Angalia Kutoka 20. Wakati Yesu alipoanza kazi yake, alitangaza wazi wazi kwamba hakuja kuitangua torati. “Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii.” Mathayo 5:17.

  60. Yesu kwa ukali aliwashutumu Mafarisayo kama wanafiki kwa kujifanya kumpenda Mungu, na wakati huo huo waliitangua moja ya Amri Kumi kwa mapokeo yao . Utunzaji wa Jumapili ni mapokeo tu ya watu.

  Tumetoa sasa sababu za wazi 60 kutoka katika Biblia kuhusiana na ukweli wa siku ya Saba . Je, utazifanyia nini?

  Sababu Arobaini za Biblia Kuhusiana na Siku ya Kwanza ya Juma

  1. Kitu cha kwanza kabisa kilichowekwa kwenye kumbukumbu za Biblia ni kazi iliyofanywa siku ya Jumapili, siku ya kwanza ya juma. Mwanzo 1:1-5. Hii ilifanywa na Mwumbaji mwenyewe. Ikiwa Mungu aliumba dunia siku ya Jumapili, je itakuwa ni vibaya kwetu kufanya kazi siku ya Jumapili?

  2. Mungu anawaamuru watu kufanya kazi siku ya kwanza ya juma. Kutoka 20:8-11. Je, ni makoa kumtii Mungu?

  3. Hakuna hata mzee wa zamani aliyepata kuitunza.

  4. Hakuna hata manabii watakatifu waliopata kuitunza.

  5. Kwa amri iliyofafanuliwa ya Mungu, watu wake watakatifu walitumia siku ya kwanza ya juma kama siku ya kawaida ya kufanya kazi kwa miaka 4,000, angalao.

  6. Mungu mwenyewe huiita “siku ya “kufanya kazi. Ezekieli 46:1.

  7. Mungu hakupumzika katika siku hii.

  8. Hakuibariki kamwe.

  9. Kristo hakupumzika katika siku hii.

  10. Yesu alikuwa seremala (Marko 6:3) na akafanya shughuli hiyo mpaka alipokuwa na miaka 30. Aliitunza Sabato na kufanya kazi kwa siku sita katika juma, kama wote wanavyokiri. Hivyo basi alifanya kazi nyingi ngumu za siku ya Jumapili.

  11. Mitume walifanya kazi katika siku hii wakati wa kipindi hiki hiki.

  12. Mitume kamwe hawakupumzika katika siku hiyo.

  13. Kristo kamwe hakuibariki.

  14. Haijapata kubarikiwa kwa mamlaka yoyote ya Mungu.

  15. Haijapata kutakaswa kamwe.

  16. Hakuna sheria iliyopata kutolewa kulazimisha kuitunza [Jumapili], hivyo basi hakuna dhambi kufanya kazi katika siku hiyo. “Maana pasipokuwapo sheria, hapana kosa.” Warumi 4:15; (1 Yohana 3:4).

  17. Agano Jipya halikatazi kazi kufanyika katika siku hii.

  18. Hakuna adhabu inayotolewa kwa kuivunja.

  19. Hakuna mbaraka unaoahidiwa kwa kuitunza.

  20. Hakuna maelekezo yaliyotolewa juu ya namna inavyopaswa kutunzwa. Je, hii ingekuwa hivyo kama Bwana alitutaka kuitunza?

  21. Haiitwi kamwe Sabato ya Kikristo.

  22. Haiitwi kamwe siku ya Sabato kabisa.

  23. Haiitwi kamwe siku ya Bwana.

  24. Haiitwi kamwe hata siku ya mapumziko.

  25. Hakuna heshma yoyote takatifu inatumika juu yake. Ikiwa ni hivyo basi ni kwa nini tuiite takatifu?

  26. Inaitwa tu kirahisi “siku ya kwanza ya juma.”

  27. Yesu kamwe hajataja katika njia yoyote–hakuweka jina lake kinywani mwake kulingana na kumbukumbu zinavyoonyesha.

  28. Neno Jumapili kamwe halionekani katika Biblia kabisa.

  29. Wala Mungu, Kristo, hata watu waliovuviwa, waliopata kusema neno moja kuipendelea Jumapili kama siku takatifu.

  30. Siku ya kwanza ya juma imetajwa mara nane tu katika Agano Jipya lote. Mathayo 28:1; Marko 16:2, 9; Luka 24:1; Yohana 20:1, 19; Mdo 20:7; 1 Wakorintho 16:2.

  31. Kati ya haya, ni mafungu sita yanayorejea katika siku ile ile ya kwanza ya juma.

  32. Paulo aliwaelekeza watakatifu kuangalia mambo yao ya kidunia katika siku hiyo. Wakorintho 16:2.

  33. Katika Agano Jipya lote tuna kumbukumbu ya mkutano mmoja tu wa kidini ulioendeshwa katika siku hiyo. Mdo 20:5-12.

  34. Hakuna siri kwamba walikuwa na mkutano siku hiyo kabla au baada yake.

  35. Haikuwa desturi yao kukutana katika siku hiyo.

  36. Hakukuwa na umuhimu wa kumega mkate katika siku hiyo.

  37. Tuna kumbukumbu tu ya tukio moja ambamo ulifanyika. Mdo 20:7.

  38. Huo ulifanyka usiku–baada ya usiku wa manane. Mistari ya 7-11. Yesu aliisherehekea siku ya Alhamisi jioni (Luka 22), na mitume mara nyingine walifanya hilo kila siku. Mdo 2:42-46.

  39. Biblia kamwe haisemi popote kwamba siku ya kwanza ya juma huadhimisha ufufuo wa Kristo. Haya ni mapokeo ya wanadamu, ambayo huifanya sheria ya Mungu kuwa bure. Mathayo 15:1-9. Ubatizo huadhimisha mazishi na ufufuo wa Yesu. Warumi 6:3-5.

  40. Mwishoi, Agano Jipya liko kimya abisa kuhusiana na badiliko lolote la siku ya Sabato au utakatifu wa siku ya kwanza.

  Kwa hiyo baada ya kupitia sababu hizi za ukweli wa Biblia juu ya suala hili, zikionyesha kwa kuhitimisha kwamba siku ya saba ya juma, au Jumamosi, ni Sabato ya Bwana ktika Agano la Kale na Jipya, ni nini unapaswa kuwa mwitikio wetu kwa amri hii ya nne ya Mungu?
  “Kwa maana ameinena siku ya saba mahali fulani hivi, Mungu alistarehe siku ya saba, akaziacha kazi zake zote….Basi, imesalia raha ya sabato kwa watu wa Mungu. Kwa maana yeye aliyengia katika raha yake amestarehe mwenyewe katika kazi yake, kama vile Mungu alivyostarehe katika kazi zake. Basi na tufanye bidii kuingia katika raha ile, ili kwamba mtu yeyote asije akaanguka kwa mfano uo huo wa kuasi.” Waebrania 4:4, 9-11.

  “Na katika hili twajua ya kuwa tumemjua yeye, ikiwa tunashika amri zake. Yeye asemaye, Nimemjua, wala hazishiki amri zake, ni mwongo, wala kweli haimo ndani yake. Lakini yeye alishikaye neno lake, katika huyo upendo wa Mungu umekamilika kweli kweli. Katika hili twajua ya kuwa tumo ndani yake….Katika hili twajua kwamba twawapenda watoto wa Mungu, tumpendapo Mungu, na kuzishika amri zake. Kwa maana huku ndiko kumpenda Mungu, kwamba tuzishike amri zake; wala amri zake si nzito.” 1 Yohana 2:3-5; 5:2-3.

  “Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake. Huko nje wako mbwa, na wachawi, na wazinzi, na wauaji, na hao waabuduo sanamu, na kila mtu apendaye uongo na kuufanya.” Ufunuo 22:14-15.

  “Hii ndiyo jumla ya maneno; yote yamekwisha sikiwa; Mche Mungu, nawe uzishike amri zake, maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu. Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila kazi, pamoja na kila neno la siri likiwa jema au likiwa baya.” Mhubiri 12:13-14.

 101. Ndugu matiku,
  Ubalikiwe kwa uamuzi wako mzuri na Bwana azidi kukubaliki,nami mwenyewe nilikuwa hukohuko kwa wakatoliki wa roma na sasa nimeuelewa ukweli na nimetoka huko Bwana azidi kutubaliki sote,
  AMEN

 102. JAMANI KWANINI MNABISHANA SANA SABATO NI AMRI YA MUNGU KABISAAA NA MUNGU SI KIGEUGEU,,,,,,,,LKN KAMA UNAIVUNJA UTAHUKUMIWA TU ,,,,,,,,,,,,,PILI TUTAOKOLEWA KWA NEEMA YA KRISTO NA UKUMBUKE HII NEEMA ILIANZA TOKA BUSTANI YA EDENI,,,,,,,BASI TUENDELEE KUTENDA DHAMBI ILI NEEMA IZIDI????????????,AMRI ZA MUNGU NI ZA MILELE KABISA NA KUSHIKA TU AMRI HAKUKUOKOWI YESU NDO ANAOKOA KWA HIYO AMRI ZIPO ILI KUKUONYESHA KWAMBA HII NI DHAMBI …..NA UKISHAJUA IPELEKE MSALABANI KWA YESU,,,,

  MTU YEYOTE ALIYE NA NEEMA LAZIMA ATAZITII AMRI 10 ZA MUNGU IKIWEMO SABATO…………JAMANI DINI YA KWELI NI YA WAYAHUDI AMBAYO MUNGU ALIWAPA……..LEO SISI WATU WA MATAIFA TU AMBAO WENGI WETU TULIKUWA WAPAGANI SANA LEO HATUTAKI DINI YA KIYAHUDI YAANI SABATO YA BWANA,,,,,,,ANGALIENI MSIJE MKAPOTEA KAMA WENGINE WALIVYO POTEA KWA KUDHARAU AMRI ZA MUNGU…….

  SWALI NI HILI KAMA KWELI SI MPANGO WA SHETANI KUANZISHA KUSALI JUMAPILI,,,,,,NI KWANINI SASA MAJINA YA SIKU YALIBADILISHWA?
  SIKU YA KWANZA——-IKAITWA JUMAPILI
  SIKU YA 2————–JUAMATATU
  SIKU 3—————–JUMANNE
  SIKU YA 4———JUMATANO
  SIKU YA 5———–ALHAMIS
  SIKU YA 6———-IJUMAA
  SIKU YA 7——–JUMAMOSI

  HUU WOTE ULIKUWA NI UONGO WA SHETANI NA LEO DUNIA YA SASA SIKU ZINGEENDELEAA KUWA KAMA HAPO ZAMANI HAKUNA MTU ASINGEEENDA KUSALI JUMAPILI ,,,,…..JAMANI LUKA 4:16 IPO WAZI NA LUKA 23:50-55…….MITUME WALIKUWA WANAMEGA MKATE NYUMBA KWA NYUMA KILA SIKU LKN SIKU YA SABATO WALIKUWA WANAENDA KWA AJILI YA KUSANYIKO TAKATIFU SABATO SOMA VIZURI ICHO KITABU CHA MATENDO YA MITUME VIZURI UTAGUNDUA KITU

  TUACHE LIGI NA SISHANGAI KWANI HATA KIPINDI CHA YESU WALIKUWEPO WATU KAMA NINYI SOMENI KAKA

  MM NILIKUWA HUKO KWENYE MIUJIZA SANA YAANI MLOKOLE LKN NILIGUNDUA HAKUNA KWELI HUKO KAZI MIUJIZA TU,,,,,,,NA KUWA TAJIRI TU…..LKN UKWELI HAUPO KABISA NDUGU ZANGU FANYENI MATENGENEZO JAMANI NDUGU ZANGU
  ILI MUINGIYE KWENYE HII RAHA YA SABATO,,,,,,,,,

  IKUMBUKE SIKU YA SABATO NA UITAKASE …….SABATO KWA WAISLAELI NI YA MILELE KUTOKA 31:13-

  MUNGU AWABARIKI SANA

 103. ”Basi, mtu asiwahukumu ninyi kwa vyakula,au vinywaji au kwa sababu ya sikukuu, au mwandamo wa mwezi,au sabato;mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo;bali mwili ni wa kristo”(wakolosai 2;16-17)

  1: Sikukuu na miandamo ya mwezi: Sabato hizi za maadhimisho ya sherehe na kafara zake na sadaka zake

  2: Sabato: siku ya saba waliyopewa huko jangwani Wayahudi kupumzika, wanayopaswa kuitunza milele (a period of time) na si ETERNALY!

  Kwahiyo mambo yote haya yanakoma katika ujio wa Kristo, kwa hao waliompokea na kujazwa Roho Mtakatifu ambaye ndiye anayewaongoza katika hiyo Nchi Mpya ambayo hawajawahi kuitembea, mfano wao ukiwa ni jinsi Joshua alivyowaingiza Israeli katika nchi Mpya akiwavusha Jordani ambayo iliashiria Kifo., na ndipo alipowaamuru wote wakae hatua nyuma ya Sanduku la Agano, hilo ndilo lilitangulia, Walawi wakayakanyaga maji ya Yordani yaliyofurika nayo yakatenga NJIA!

  Basi ninakushauri nawe Josephat, usiheshimu tu ufufuo wa Kristo, upitie huo ili nawe ufufuke uyaone mambo ya waliofufuka ndio utawaelewa! Usiupitie ufufuo katika namna ya dini, hautafanikiwa, wanakuchovya ndani maji marefu na unaibuka mzima wanakudanganya kuwa eti nawe “umefufuka”, wamekulowesha tu!!! Ubatizo unaofufua huu hapa katika Mdo 2:38
  “Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.”
  Jipime hapo, kama hukupitia Njia hiyo, basi hutaelewa chochote, utaendelea kujibebesha mafurushi ya Torati yasiyokuhusu mpaka utashindwa hata kuinuka!!!

  Jaribu kusoma kitabu cha Matendo ya Mitume ili upate sampuli ya Kanisa la Kwanza, na mafundisho yake, inaweza kukusaidia KUOKOKA!

  Gbu!

 104. NIWASHUKURU NYOTE MLIO ANDAA MAANDIKO HAYA WENGINE HATUKUWA NA LOLOTE LA KUELEWA MAANA UKIWASIKILIZA WASABATO WANAVUTIA KWAO. MUNGU YUPO NA TUMHESHIM

 105. Ndg Josephat,
  Karibu sana, ndg yangu na mwalimu!
  Ukimaliza huo mfungo, ninaamini utakuja na mengi mazuri!!!

  Gbu!

 106. Basi na tuendelee kulichunguza kwa makini fungu la ck lwembe alilopost hapo juu kwa makini na kwa undani zaidi;
  ”Basi, mtu asiwahukumu ninyi kwa vyakula,au vinywaji au kwa sababu ya sikukuu,au mwandamo wa mwezi,au sabato;mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo;bali mwili ni wa kristo”(wakolosai 2;16-17)
  Jamani neno la Mungu haliwezi kujipinga lenyewe kama mfikiriavyo ninyi; na fungu hili haliondoi sabato ya bwana na hebu tuangalie fungu hili kwa umakini zaidi ;
  a) lugha hiyo inazungumzia sheria ya zamani za taratibu za maadhimisho ya kidini- sadaka za vyakula,sadaka za viywaji,sikukuu za mwezi mpya,na ”siku za sabato” zilizokuwa za maadhimisho ya sherehe, na orodha kamili ya sikukuu hizo saba za maadhimisho za kila mwaka zinapatikana katika mambo ya walawi 23,ambapo zinatofautishwa na sabato ya kila juma;”sikukuu za bwana ni hizi,ambazo mtazipigia mbiu ya kuwa ni makusanyiko matakatifu ,ili mmsongezee bwana sadaka kwa moto,sadaka ya kuteketezwa ,na sadaka ya unga,na dhabihu,na sadaka za vinywaji,,na kila sadaka kwa siku yake ,zaidi ya hizo sabato za bwana”(mambo ya walawi 23;37-38)

  Sabato hizi za maadhimisho ya sherehe na kafara zake na sadaka zake zilikuwa ni ”kivuli cha mambo yajayo”,na kitabu cha waebrania kinatuambia kwamba huduma zote za patakatifu pa walawi zilikuwa ni ”kivuli cha mema yajayo” (waebrania 10;1),zikielekeza mbele kwenye msalaba wa kalvari,kwa hiyo Yesu alipokufa msalabani,mambo hayo yote yalikoma.

  b)Sabato ya kila juma sio ”kivuli cha mambo yajayo” bali ni ukumbusho wa mambo yaliyopita- yaani kuumbwa kwa ulimwengu.

  c)mfumo wa taratibu za kidini za patakatifu katika agano la kale ulianzishwa baada ya dhambi kuingia ulimwenguni ,lakini sabato ya bwana ya kila juma ilianzishwa kabla ya dhambi kuingia ulimwenguni.

  d)hakutakuwa na sadaka au sabato zilizohusiana na maadhimisho ya kidini zitakazoadhimishwa katika nchi mpya baada ya dhambi kuangamizwa milele. lakini sabato ya bwana ya kila juma itaadhimishwa milele zote(angalia isaya 66;22-23).

  Na kuhusu usherehekewaji wa siku ya kwanza ya juma(jumapili) hauendani kabisa na maandiko yasemavyo,
  Je,tuadhimishe siku ya kwanza ya juma kwa kuheshimu ufufuo wa kristo? Biblia inasema kuwa ubatizo kwa njia ya kuzamishwa majini ndio uwe ukumbusho wa kufufuka kwake(warumi 6;3-7) na mapokeo hayapaswi kuruhusiwa kupingana na ”asema bwana”
  BALIKIWA NINYI NYOTE

 107. CK LWEMBE ACHA KUWAPOTOSHA WATU WA MUNGU, NA KAMA HUELEWI MAANA FULANI YA FUNGU USIJARIBU KABISA KUPOST HAPA,NAJIPANGA VEMA KULIELEZEA HILO FUNGU ULILOPOST HAPA,
  BALIKIWA

 108. Mkaka,
  Usiitese akili yako changa kwa kuyaendea mambo magumu, ‘Logic’ haijawahi kutoa jibu la kudumu, kwa sababu ni akili za kibinadamu tu, zinazojiboresha kila kunapokucha!

  Nimekuuliza swali dogo kutoka ulichokiandika; “Hebu niambie Mkaka, hivi walikula matunda ya mti gani?” Badala ya kunipa jibu la kiMaandiko, unaniletea mambo ya Logic! Angalia:
  “Kuhusu tunda, pale bustani ya Edeni kulikuwa na miti ya aina mbili. Miti yenye matunda yanayofaa kwa kuliwa na mti wenye matunda yasiyofaa kuliwa. Kimsingi, yale yaliyofaa kwa kuliwa yalikuwa ni kwa ajili ya mwanadamu. Na yale yasiyofaa kwa kuliwa hayakuwa kwa ajili ya mwanadamu. “Logically” kama hayakuwa kwa ajili ya mwanadamu, yalikuwa ni kwa ajili ya Mungu mwenyewe. Mungu aliyaweka pale bustanini kwa ajili ya makusudi maalum. Na inavyo-onekana , Mungu aliweka pale bustanini yale matunda ili kumdhibiti shetani. Adam na Hawa waliona ni jambo dogo kula yale matunda waliyokatazwa.”

  Hivi, ni kweli kwamba kulikuwa na miti ya aina mbili tu katika Bustani? Wewe mwenyewe unapoyasoma haya maelezo yako, unaamini kabisa kuwa ndilo Neno la Mungu? Kama unaweza kujiaminisha katika mambo ya kitoto ya jinsi hii, hauoni kwamba ni kwa akili hiyo hiyo ndio unaamini kwamba kifungu cha Mwa 2:3 kinasomeka hivi, “Mungu akaibarikia siku ya saba, SATURDAY, akaitakasa kwa sababu katika siku hiyo Mungu alistarehe, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoiumba na kuifanya.”!!!

  Hebu changamsha akili hiyo ndugu yangu, kupotea njia ni rahisi sana kama utatembea huku umefumba macho, rudi tena usome vizuri Maandiko halafu ndio uje!!!

  Nukuu kutoka kitabu cha Wagalatia ni nzuri sana na zinashibisha iwapo nawe unao uwezo wa kuyaamini Maandiko; ngoja nikuongezee fungu moja ulilolisahau ili uendelee kujipima mwenyewe iwapo unalo FURUSHI au la:

  KOL 2:16
  “Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato”

  Umeelewa? Yaani unapowahukumu hao unaowaita wa J2, basi unakuwa umejiunganisha na hao anaowasema mt. Paulo wenye kung’ang’aniza sabato na vyakula, hao wenye kulisumbua Kanisa! Basi wewe mwenyewe jaribu kufikiri, toka uanze kuimba mapambio ya kutuhukumu sisi tulio Kanisa, hilo FURUSHI lako litakuwa KUBWA kiasi gani?

  Gbu, brother!

 109. Asanteni sana ndugu zangu MJ,N,Siyi na Ck Lwembe kwa kurejea bustani ya Edeni. Ni muhimu kwa sababu pale ndipo penye chanzo cha mateso yote tunayoyapata wanadamu hapa duniani.

  Kuhusu tunda, pale bustani ya Edeni kulikuwa na miti ya aina mbili. Miti yenye matunda yanayofaa kwa kuliwa na mti wenye matunda yasiyofaa kuliwa. Kimsingi, yale yaliyofaa kwa kuliwa yalikuwa ni kwa ajili ya mwanadamu. Na yale yasiyofaa kwa kuliwa hayakuwa kwa ajili ya mwanadamu. “Logically” kama hayakuwa kwa ajili ya mwanadamu, yalikuwa ni kwa ajili ya Mungu mwenyewe. Mungu aliyaweka pale bustanini kwa ajili ya makusudi maalum. Na inavyo-onekana , Mungu aliweka pale bustanini yale matunda ili kumdhibiti shetani. Adam na Hawa waliona ni jambo dogo kula yale matunda waliyokatazwa. Lakini ona madhara yake yalivyo mabaya tokea kipindi chao mpaka siku hizi za leo. Binadamu hawapendani, wakati wote chanzo chao ni kimoja.

  Siku ya sabato Mungu aliitakasa na kuibariki. Siku nyingine sita hakuzitakasa wala kuzibariki.
  Nianavyo mimi, tujiulize, Mungu anataka tufanye nini siku hiyo ya sabato. Na je siku ya sabato ni lini hasa katika siku hizi za leo?

  Namalizia kwa mafungu mawili :-
  1) WAGALATIA 6 : 7
  “Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi. Kwa kuwa kile apandacho mtu ndicho atakachovuna. Apandaye kwa mwili, katika mwili wake, atavuna uharibifu, lakini yeye apandaye katika Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele. Hivyo, tusichoke katika kutenda mema, kwa kuwa tutavuna kwa wakati wake tusipokata tamaa.”

  2) WAGALATIA 6:3-5.
  “Maana mtu akijiona kuwa ni kitu,nae si kitu,ajidanganya nafsi yake,lakini kila mtu na aipime kazi yake mwenyewe,ndipo atakapokuwa na sababu ya kujisifu ndani ya nafsi yake tu,walą si kwa wenzake,maana kila mtu atachukua FURUSHI lake mwenyewe.”
  Mbarikiwe.

 110. Mkaka, 
  unajua hata mimi nimeipenda sana hii unayoturudisha kule Edeni, “Yale yote yalikuwa ni matunda. Wakakatazwa kula tunda mojawapo. Lakini wao wakala. Au walikula mboga za majani?”
  Naona hili laweza kutusaidia kumaliza mgogoro wa siku, haswa unapokutana na mwana Biblia! Hebu niambie Mkaka, hivi walikula matunda ya mti gani?

  Gbu!

 111. Mkaka,
  Ha ha ha ha!! Hiyo nimependa sana. Yote yalikuwa ni matunda ya kula, isipokuwa moja. Na leo zote ni siku za kazi sipokuwa moja-Sabato. Na siku hii ni j2, ijumaa wala j5. Ni Sartuday. Ubarikiwe sana Mkaka.

 112. Jamani kumbukeni pale bustani ya Edeni. Yale yote yalikuwa ni matunda. Wakakatazwa kula tunda mojawapo. Lakini wao wakala. Au walikula mboga za majani? Naamini walikula tunda. Vivyo basi hata siku zinamata. Akisema siku ya sabato ikumbukwe anamaanisha hivyo. Kama uasi ulivyokuwa wakati ya bustani ya Edeni ndiyo ilivyo hata sasa. Kwa sababu yote yale yalikuwa ni matunda lakini wakakatazwa mojawapo lakini hawakusikia. Asanteni

 113. Gidion,
  Maelezo yako mengi yamejengeka ktk hisia za mafundisho ya Kisabato na ulaghai wake. Nafikiri ktk mafundisho yenu, nawe umekubuhu kama Siyi, hivyo huna uwezo hata wa kuelewa hata vitu vilivyo wazi, na badala yake mnajizidisha katika kujiondoa ufahamu, kama mnavyojipachika makabila ya Israeli!!!!

  Maelezo yako kuhusu “muhuri” ni ulaghai mliouzoea kuwadanganyia watu wasio na ufahamu wa mambo haya na sasa unauleta huku hadharani. Hebu nikunukuu:
  ““Muhuri au sahihi halali ya mtawala ni lazima iwe na mambo matatu ya kuitambulisha ;jina la mtoa sheria ,cheo chake ambacho huashiria mamlaka yake ,na eneo la kiutawala ambapo mamlaka yake huishia…””

  Hili jambo lina uhusiano gani na kutiwa muhuri inakokusema Biblia? Hakuna mahali Biblia inaongelea kutia sahihi chochote kile. Biblia inaongelea kuwatia watu Muhuri, ambapo muktadha unaozungumziwa humo ni katika tafsiri hii hapa, kikamusi:
  seal n 1 muhuri, chapa, alama. ~ (up) tia (piga) muhuri. ~ (close) ziba, funga kabisa.
  Huu ndio muktadha Biblia, inawatia Muhuri hao waliokamilika. Yaani hao ambao walihubiriwa Injili, wakaiamini, wakatubu na kubatizwa kwa jina la Yesu Kristo na kuondolewa dhambi zao, wakafundishwa yaipasayo mila na desturi mpya, wakiwa ktk kusanyiko ambalo lina zile Huduma Tano (wachungaji, walimu, wainjilisti, mitume na manabii), zenye kuwakamilisha katika Utakatifu; hawa ndio ambao hutiwa huo Muhuri, kudhihirisha kwamba ni kazi iliyokamilika!!

  Lakini wewe kwa makusudi umeipindisha maana ili kukidhi mafundisho yenu ya uongo kwa kuubadilisha muktadha mzima kutoka huo uliokusudiwa kiBiblia na kuuleta kimafundisho yenu hapo neno hilo “muhuri” ulipolifanya kuwa “sahihi”; bali hii hapa tena tafsiri ya neno hilo “sahihi” kikamusi:
  sign n 1 dalili, ishara. weka/tia sahihi/saini, tia mkono.

  Ukiisha liwekea msingi jambo hilo sasa unaendelea mbele, ukiwakokota woote “…wasioandikwa majina yao katika kitabu cha uzima tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu…”; ndipo unawaongoza kama mazezeta katika huo “mpindo” wa Maandiko, nina kunukuu:
  ”Tena naliwapa sabato zangu, ziwe ishara (muhuri) kati ya mimi na wao ,wapate kujua ya kuwa mimi, BWANA, ndimi niwatakasaye” (ezekieli 20;12, 20)

  Basi hao walioaminishwa hivyo kwa tafsiri yako hii, “Tena naliwapa sabato zangu, ziwe MUHURI kati ya mimi na wao…”, ni dhahiri wataishia kuwa mazezeta wa kiroho, baada ya kulishwa tafsiri hizo za kufisha! Biblia zenu ndivyo mlivyozifanya? Mmezichezea chezea kukidhi mafundisho yenu! Lakini tafsiri ya Maandiko hayo mliyoyapindisha, hii hapa ktk KJV: – “Moreover also I gave them my sabbaths, to be a SIGN between me and them…” Unaona, a SIGN, not a SEAL!!! Hata huo mstari wa 20 pia hausemi “muhuri” bali “ishara”! “20 zitakaseni sabato zangu; zitakuwa ISHARA kati ya mimi na ninyi…” Ishara ni Sign, acheni mizaha ya dini!

  Gidion, pole sana, umekamatwa katika makucha ya dini isiyo na uzima, ni dini mfu, upako ulio juu yake ni ule uletao KUTO KULIAMINI NENO LA MUNGU! Najua utalibishia jambo hili, lakini jaribu kuyatafakari hayo uliyoyaandika, katika mpindo uliouleta, jibu utakalolipata haliwezi kuwa tofauti na hiki ninachokuambia, labda nawe uwe ulikwisha pitiliza kama wenzako ambao wamekushawishi nawe pia kuwa eti ni wa kabila la Gadi, au wewe ni wa Manase?! Eti ninyi ndio mtasimama/sijui mtapita kuingia kwa kabila mlizojibambika, katika yale mageti 12 ya Yerusalemu Mpya! Ufu 21: 12 “ulikuwa na ukuta mkubwa, mrefu, wenye milango kumi na miwili, na katika ile milango malaika kumi na wawili; NA MAJINA YAMEANDIKWA AMBAYO NI MAJINA YA KABILA KUMI NA MBILI ZA WAISRAELI.” Punguzeni kujiongopea, mnakuwa vituko saana, wenyewe wakiyasoma mafundisho yenu, nadhani wanacheeeeeka mpaka basi!!!

  Hebu niambie Gidioni, Unayaamini Maandiko haya?:
  1. 1Sam 28:11-14
  “Ndipo yule mwanamke aliposema, Je! Ni nani nitakayekupandishia? Naye akasema, Nipandishie Samweli. Hata yule mwanamke alipomwona Samweli alilia kwa sauti kuu; na yule mwanamke akamwambia Sauli, akasema, Mbona umenidanganya? Kwa kuwa wewe ndiwe Sauli.”
  2. Luka 23:43
  “Yesu akamwambia, Amin, nakuambia, leo hivi utakuwa pamoja nami peponi.”
  3. Mdo 2:38
  “Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu. “
  4. Mdo 19:5
  “Waliposikia haya wakabatizwa kwa jina la Bwana Yesu.
  5. 1Petro 1:18-20
  “For Christ also hath once suffered for sins, the just for the unjust, that he might bring us to God, being put to death in the flesh, but quickened by the Spirit: By which also he went and preached unto the spirits in prison; Which sometime were disobedient, when once the longsuffering of God waited in the days of Noah…”

  Jipime mwenyewe hapo unapoyasoma hayo, angalia kilichokutangulia mbele katika ufahamu ni kipi, miwani ya dini au nafsi yako iliyo huru?!

  Ndipo nami ninairudisha kwako kauli yako, nawe nakuomba kwa kipimo hicho uukubali UONGO wako unaoufundisha ili Neno lililonenwa na nabii Isaya, hilo ulilolinukuu liwe limekutimilia kisawa sawa kwa kadiri utakavyo ng’ang’ana na UONGO: “”Na waende kwa sheria na ushuhuda ikiwa hawasemi kulingana na neno hili kwao hapana asubuhi”(isaya 8;20)
”na neno asubuhi” lina maana ya kuwa kwao hawana ijara na wala tumaini lolote bali husema kwa maneno yao mapotofu yatokayo kinywani mwao.””

  Asante kwa leo!

 114. Dah, Nzala!
  Unataka sifa za nabii, awe mwembamba, mrefu ana nywele nyingi, mfupi mweusi; Au awe hapepesi macho na hapumui anapoingia katika maono? Biblia iko kamili ndg yangu, yaani hakuna lililosalia kwa Mungu kunena, ndio maana tunasema hivi nabii yeyote yule ni lazima awe ametabiriwa kuja na huduma yake kuorodheshwa. Hawa manabii waliojaa duniani leo hii akina TB Joshua na wengineo pamoja na hawa wa Bongo ni sawa tu na Ellen White, pamoja na kwamba wanacho kipawa cha unabii, bado hawana sehemu ktk Maandiko kwa hivyo wanahesabika ktk kundi la Mt 24:24, Manabii wa Uongo!

  Nabii wa kweli huja kulingana na Maandiko, huyo huwa ni sehemu ya Maandiko! Kwa kadiri mnavyo jaribu kumleta Ellen White kwa kipimo cha Agano la Kale ili muwachanganye watu, yaonesha kuwa ninyi mnao uvuvio wa baba wa Uongo! Kwa nini mumfananishe na manabii wa AK wakati yeye ni wa Agano Jipya? Baba wa Uongo anajua kuwa huku kuna KIPIMO ambacho hawezi kukivuka!

  Lakini, nabii wa kweli hana shida, mtazame Yohana Mbatizaji, Yn 1:19-23
  “Na huu ndio ushuhuda wake Yohana, Wayahudi walipotuma kwake makuhani na Walawi kutoka Yerusalemu ili wamwulize, Wewe u nani? Naye alikiri, wala hakukana; alikiri kwamba, Mimi siye Kristo. Wakamwuliza, Ni nini basi? U Eliya wewe? Akasema, Mimi siye. Wewe u nabii yule? Akajibu, La. Basi wakamwambia, U nani? Tuwape majibu wale waliotupeleka. Wanenaje juu ya nafsi yako? Akasema, Mimi ni sauti ya mtu aliaye nyikani, Inyosheni njia ya Bwana! Kama vile alivyonena nabii Isaya.”
  Hao wanaomuuliza wanalo tegemeo la ujio wa nabii, lakini dini zimewapofusha na sasa hao hapo wanakisia kisia, tena, hawa wana afadhali kuliko ninyi wa leo mnaojipokelea tu manabii, eti hapepesi macho, sijui hapumui, fungu la kuongopewa halinaga macho wala masikio! Lakini mtazame Yohana, hababaiki, yeye si mwana haramu, anajua yeye ni nani, anamjua Baba yake! Tena si Isaya tu kati ya nduguze walioujua ujio wake, huyu hapa pia Malaki, 3:1,
  “Angalieni, namtuma mjumbe wangu, naye ataitengeneza njia mbele yangu; naye Bwana mnayemtafuta atalijilia hekalu lake ghafula; naam, yule mjumbe wa agano mnayemfurahia, angalieni, anakuja, asema BWANA wa majeshi.”

  Nayo Huduma yake ilikuwa kulingana na alivyopangiwa, ndani ya utaratibu, Malaki 4:5-6, hii hapa ikiwekwa wazi:
  “Angalieni, nitawapelekea Eliya nabii, kabla haijaja siku ile ya BWANA, iliyo kuu na kuogofya. NAYE ATAIGEUZA MIOYO YA BABA IWAELEKEE WATOTO WAO, na mioyo ya watoto iwaelekee baba zao, ili nisije nikaipiga dunia kwa laana.” (msisitizo ni wangu)
  Hii hapa tena katika Lk 1:16-17 (kwa mashahidi wawili neno lithibitike)
  “Na wengi katika Waisraeli atawarejeza kwa Bwana Mungu wao. Naye atatangulia mbele zake katika roho ya Eliya, na nguvu zake, ili KUIGEUZA MIOYO YA BABA IWAELEKEE WATOTO…” (msisitizo ni wangu)
  Hivi ndivyo yalivyo mambo ya Mungu, ameyaweka wazi kwa wanawe!!

  Ndipo makundi yaliyo rejezwa na kutayarishwa katika Huduma hiyo ya Yohana, anayakabidhi kwa huyo aliyemtangulia, Kristo, Yn3:28-30
  “…Ninyi wenyewe mwanishuhudia ya kwamba nalisema, Mimi siye Kristo, bali nimetumwa mbele yake. Aliye naye bibi arusi ndiye bwana arusi; lakini rafiki yake bwana arusi, yeye anayesimama na kumsikia, aifurahia sana sauti yake bwana arusi. Basi hii furaha yangu imetimia. Yeye hana budi kuzidi, bali mimi kupungua.”

  Unaona Siyi, siyo mradi nabii tu mnajipokela mtapokea na mapepo! Mambo ya Mungu yanakwenda kwa mpangilio, kaka!

  Haya, si kwamba mambo yameishia kwa Kristo, hapana, kutoka kwake wanapewa mitume, Kristo akiwa ndani yao wanalijenga Kanisa juu ya Msingi wa Injili waliyopewa na Kristo na manabii, nalo Kanisa hilo ndilo sisi tunao yarejea hayo yote katika ujumla wake kama yalivyokusudiwa kwa ushahidi wa Maandiko! Ndipo tunapoendelea ktk Injili humo pia tunayo ahadi ya “manabii wa uongo” ktk Mt 24:24, si ahadi ya nabii mmoja au wawili, bali manabii, hawa wanapaswa kuja na kupokelewa pia, ndio maana nakushangaa unavyotaharuki, kwamba yawezekana hata kipimo huna!

  Lakini wana wa Mungu, lile Kanisa lililo hai, wanayo ahadi ya kipekee, kwamba wakiisha kupita akina Ellen White, na hao wengine, wanayo Ahadi ya Nabii Eliya ya kuwarejeza katika Msingi ule waliouvuruga hao akina Ellen kwa mafundisho ya uongo kama hili la kwamba “Israeli si Taifa Teule tena, nafasi yake imechukuliwa na watu wa Mataifa”, mara “Yesu aliingia patakatifu pa patakatifu mwaka 1844” wakificha aibu ya kushona mbawa za kurukia kwenda kumlaki mawinguni, ile michezo ya mapepo (sadism), wakiwadhihakisha wafuasi wao!

  Basi, nabii anayengojewa na Kanisa ni huyo Eliya anayeonekana ktk Malaki 4:5-6, na Huduma yake iko wazi kama ilivyokuwa kwa Yohana Mbatizaji, huyu anamalizia ile nusu ambayo haikufanyika wakati wa Yohana, “kuigeuza MIOYO YA WATOTO IWAELEKEE BABA ZAO, ili nisije nikaipiga dunia kwa laana”; na pia manabii wawili kwa Israeli (hao ambao mnasema hawatahudumiwa tena), unaowaona ktk Ufu 11, bali hawa hawalihusu Kanisa maana litakuwa limekwisha ondolewa uwanjani, likiwa Utukufuni!

  Nakusubiri Siyi na washirika wako nanyi mniletee mtiririko wa kiMaandiko unaomdhihirisha nabii Ellen White kutumwa na Mungu.

  Karibuni sana!!!

 115. Napenda kuwasalimu kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo,na natumai ya kuwa tunaendelea vema kuelimishana kuhusu neno la Mungu katika blog hii na Mungu azidi kutubaliki,

  Nimemfuatilia sana ndugu ck lwembe na wenzake wanavyojichanganya kuhusu majina ya siku kama yalivyo sasa,

  Na hapo awali nilimweleza ya kuwa katika siku za mwanzo hayo majina ya siku hayakuwepo ni fikra tu za wanadamu hasa warumi walioamua kuzipa siku majina kulingana na miungu yao ya kirumi na ndipo mpaka mida hii tulipo sasa tumezizoea na zimeingia sana katika bongo zetu na tunaendelea nazo mpaka sasa,

  Lakini hapo awali siku zilikuwa zinahesabika kuanzia siku ya kwanza hadi ya saba lakini kwa sasa ndipo zikapewa majina kulingana na jinsi zilivyo kwa miungu ya kirumi kwa kiingereza from sunday to suturday na hawakuweza kubadilisha hata siku kwenda siku nyingine na kama historia inavyoelezea na jinsi ya kulizibitisha hilo fuatilia maelezo ya hapo awali nilipoanza kuandika katika blog hii,

  Napenda sana kuwashauri ndugu zangu msijichanganye na hizi siku za juma na mnaposoma ushauri wowote katika blog hii au katika biblia msisome kama gazeti lisomwavyo fikiria kwanza kwa makini na ndipo fuatilia kile kilichoandikwa humu na toa maoni kama hujaelewa sehemu uliza na sio kubisha bila mantiki yoyote na usibishe kwa fikra zako na kwa maneno yako mapotofu bila rejea yoyote kutoka kwenye biblia na hata historia yenyewe inazungumzia nini kama wanavyofanya akina ck lwembe na wenzake ambao wanachukua tu vifungu vya kibiblia na kujitolea maana yao wenyewe na kuwapotosha watu wa Mungu bure,

  Na nikifuatilia tena katika maelezo mengine ndugu ck lwembe anaendelea kupingana na biblia jinsi ilivyoandikwa bila rejea yoyote ya kibiblia na bali ni maneno yake tu mapotofu ambayo hayana msingi wowote wa kimaandiko na kama jinsi ninavyoenda kumnukuu,

  kwa kifupi ya kwamba anapingana na Muhuri wa mungu ambao ni sabato kama biblia inavyojifunua yenyewe,na kingine ni mnyama anawakilisha nguvu, na anakiri ya kwamba kitabu cha ufunuo hakipo wazi kwa mtu yeyote bali kipo kwa kanisa la kristo tu,

  Sasa namuomba ndugu ck lwembe atudhibitishie hayo yote anayoyaongea kwa msingi wa kimaandiko ya kwamba ni kweli na kama hatothibitisha basi ni muongo kama isaya anavyosema ”Na waende kwa sheria na ushuhuda ikiwa hawasemi kulingana na neno hili kwao hapana asubuhi”(isaya 8;20)
  ”na neno asubuhi” lina maana ya kuwa kwao hawana ijara na wala tumaini lolote bali husema kwa maneno yao mapotofu yatokayo kinywani mwao.

  BALIKIWA.

 116. Lwembe,
  Ha ha ha ha haa!!
  Nakuona umenipa maelezo mareeeefu ya sifa za nabii kaka. Mimi niliomba unitajie 1, 2, 3,4.. in releation to the Bible. Maana leo tuna manabii wengi wa uongo. Hivyo ungenitajia sifa zao ambazo ni biblical, ningejaribu kumpima Ellen G.white na kumwona kama ni mbabaishaji ama la! Lakini sasa umenipa hadithi za abunuwasi rafiki weeee!!Te te te te !! wewe kiboko kweli. Tafadhari nikuombe tena, leta hizo sifa plz.
  Nilibatizwa ka Jina la Baba, Mwana na RM kama Yesu alivyoagiza. Suala la mitume kafanya kinyume na maagizo ya Yesu, sijapata sababu kuntu za kuniridhisha kwa nini walifanya hivyo. Nikipata ukweli juu ya hili, tena ukweli wa kibiblia kabisa, uliotulia, acha porojo zako hizo kaka na mabinza wako, nikiipata ile nuru yenyewe juu ya hili, nitabatizwa tena kwa jina la Yesu. Na mimi nasimama kama mimi Siyi mbele za Kristo na wala si SDA kanisa.
  Suala la utatu mtakatifu, Biblia nilipoisoma mimi mwenyewe, niliamini hivyo kuwa Mungu yuko katika nafsi tatu, japo yeye ni Mungu Mmoja huyohuyo. Na hawa watatu ni Mungu mmoja!! Nitakuletea dondoo zilizonifanya niamini hivyo ili na wewe uzipime kinaga ubaga na kisha ulinganishe na zile za kwako. Aidha makala yako ile ndefu ikikandia utatu niliiona. Hoja zako hazina nyama ya kimaandiko isipokuwa porojo ni nyingi sana. Anyaway, bado naendelea kuusoma mjadala mzima na hatima yake. Nikipata kitu kipya, mimi ni mkweli nitakwambia kuwa nimepata kitu kipya mwanaume. Mf, Umoja, siyo sahihi kweli, sahihi ni Mmoja. Hiyo naikubali vizuri sana. Hapo nakupa hongera sana.
  Sisi hatujajipachikia makabila kaka. Ila Bibla ndiyo imetupachikia, nasi hata hatuoni haya!! Tunashangilia tu maana Mungu mwenyewe kaandaa huo mji kwa ajili yetu. Huo ndio unabii wa Biblia unavyosema. Ndiyo maana kipindi kile nikakwambia uje tuoanishe unabii wa kwenu na ule wa kwetu, halafu tuone ni unabii gani unaoungwa mkono na Biblia na vitabu vya historia. Tena hata kama uko tayari, sema tuanze na kitabu gani!!! Wewe sema tu, sindimba lianze.
  Lile kusanyiko kubwa aliliona Yohana, ni ile jumla ya watakatifu wooote waliopitia kwa malango 12 ya mji wa Yerusalemi mpya na si vinginevyo. Tunajua kuwa Yesu ni njia, mbona kwenye ufunuo mji hauoneshi kama kuna mlango wa mataifa wengine au wa Yesu (yaani mlango wa 13) kwa ajili ya mataifa? Hivi hata wewe hushutki tu? Yaani unasoma tu Biblia kama gazeti kaka? Hebu changamka bwana. Hebu tufanye tathmini ya kila mmoja wetu kama unavyoshauri ndg yangu.
  Ubarikiwe sana

 117. Siyi,
  Nilikuambia huo “unga wa ndele” mliolishwa na hao manabii wenu akina Ellen White, na walimu wenu umewatia upofu wa kiroho na ufahamu hata wa kawaida tu pia mmeondolewa! Angalia hiki kituko ulichokiandika:
  “Ukisoma Biblia na hata wanamatengenzo kama akina Martini Luther, wameelezea sawia maana ya Israel kuja kuwa taifa teule tena!! Si taifa kama lilivyo sasa, bali ni wamataifa wote watakapofanyika kuwa wana wa Ibrahimu kwa njia ya imani ktk Kristo Yesu na si vinginevyo.”

  Ni Biblia gani unayosoma? Au mafundisho yenu yamegeuka kuwa Biblia kwenu? Kwanza nikuambie kuwa wanamatengenezo kwa taarifa yako HAWAKUWA manabii! Hao walipewa sehemu ya Neno tu kwa wakati wao ili kulitoa Kanisa kutoka ktk makucha ya kikatoliki. Martin Luther alipewa Neno la “Kuhesabiwa Haki kwa Imani” tu. Kwahiyo kama alijichanganya katika hayo mafundisho hilo lawezekana kabisa na huo ndio udhihirisho wa kwamba huyo hakuwa Nabii. Nabii hubeba Neno Kamili la Mungu, ndipo iwapo Mungu aliwatabiria Israeli kuwatawanya na kisha kuwakusanya tena, basi yeyote aliye nabii hawezi akazungumza kinyume, kwani Roho ayanenaye hayo ni mmoja, ndio maana kwa mafundisho yenu, nabii wenu huyo anakosa vigezo vya kuitwa nabii!

  Israeli walitabiriwa kutawanywa, iwapo nawe huwa unasoma Biblia yako kweli, basi inashangaza mnalikosaje jambo lililo wazi kiasi hiki, Law 26:33,
  “Nanyi nitawatapanya-tapanya katika mataifa, nami nitaufuta upanga nyuma yenu; na nchi yenu itakuwa ukiwa, na miji yenu maganjo.”
  Hekalu lao lilivunjwa na taifa kusambaratika katika ujio wa Titus, 70AD, nao manabii wa kidhehebu na walimu wa dini na jumuia zote za watu wa dini, wasinge jua lolote zaidi ya taifa hilo kutoweka na kusahaulika kabisa! Ni nani awezaye kulikumbuka jambo lililotoweka miaka 2000 iliyopita? Kwanza hakuna anayeweza kuishi miaka hiyo. Ndio maana manabii wenu walifikia kuyatafsiri Maandiko yahusuyo Israeli kwamba eti Kanisa ndio hao Israeli, na udhihirisho wa kujichanganya huko ndio haya mafundisho yenu yanayokiri kwamba hao 144,000 ni watu wa Mataifa! Nawaonea aibu kuubandika ukweli huu hapa, lakini sina namna ya kuwasaidia zaidi ya kuwaonesha ukweli wa Biblia na mkiwa ni wale wa kuokoka basi iwasaidie la sivyo, basi iwe ushuhuda kwenu kwamba ni lile fungu la kupotea! Isaya 11:11-12:
  ”Na itakuwa katika siku hiyo, Bwana atapeleka mkono wake mara ya pili, ili ajipatie watu wake watakaosalia, kutoka Ashuru, na kutoka Misri, … atawakutanisha watu wa Israeli waliotupwa, atawakusanya watu wa Yuda waliotawanyika, kutoka ncha nne za dunia.”

  Wakiisha kukusanywa, kama unavyowaona sasa hivi katika nchi yao (1947), ndipo haya unayoyasoma katika Ufu 7:2-8 yatawatokea, watatiwa muhuri hao, Mungu anawajua woote licha ya kujichanganya kwao ambako nawe kumekupeleka porini zaidi katika imani. Si unaona anavyowaita:
  “Nikasikia hesabu yao waliotiwa muhuri katika kila kabila ya Waisraeli, watu mia na arobaini na nne elfu.
  Wa kabila ya Yuda kumi na mbili elfu waliotiwa muhuri.
  Wa kabila ya Reubeni kumi na mbili elfu.
  Wa kabila ya Gadi kumi na mbili elfu.
  Wa kabila ya Asheri kumi na mbili elfu.
  Wa kabila ya Naftali kumi na mbili elfu.
  Wa kabila ya Manase kumi na mbili elfu.
  Wa kabila ya Simeoni kumi na mbili elfu.
  Wa kabila ya Lawi kumi na mbili elfu.
  Wa kabila ya Isakari kumi na mbili elfu.
  Wa kabila ya Zabuloni kumi na mbili elfu.
  Wa kabila ya Yusufu kumi na mbili elfu.
  Wa kabila ya Benyamini kumi na mbili elfu waliotiwa muhuri.”

  Labda nikuulize Siyi na wenzako, nanyi mmejigawa na kujiita kwa makabila hayo? Wewe Siyi kusanyiko lenu ni la kabila gani, Gadi? Kumbe nanyi hamko mbali sana na wale wa Siloamu, wale wa ukoo wa Eliya, sijui Eliya Mtishbite pori? Hivi ninyi kweli mnayo masikio ya kuisikilizia Injili na macho ya kuonea Maandiko????

  Siyi, hiyo sio dini, na wala haiwaaminishi Biblia kama mnavyodhani bali inawapoteza kwa kuwabebesha mizigo ya ukaidi na hivyo kuwapeleka Hukumuni, kimbieni kungalipo Nuru!

  Gbu!

 118. Lwembe,
  Naona unamchechefya saaana huyo mjoli wa Bwana Gidioni. Kimsingi unampa changamoto za yeye kuichimba zaidi Biblia. Wakati anaandaa nondo za kukushughulikia, ngoja mimi nianze kwa kukupa hints na siyo majibu, ili ufuatilie mwenyewe ukajifunze na wewe ili ufunguliwe uwe huru kaka. Maana nakuona umefungwa mno.
  Moja, Ni kweli neno Mosi ni la Kiswahili lenye asili ya kiarabu likiwa na maana ya moja, au –a kwanza. Nao waislamu wameipa jmosi kuwa siku ya kwanza ya juma ili ijumaa kwao iwe ya saba, siku ya ibada kwao. Ukifuatilia kuanzia jmosi hadi ijumaa, utakuta ukakasi na mkanganyiko kwenye siku ya alhamisi, neno alhamisi lenye asili ya kiarabu pia likiwa na maana ya tano au –a tano. Sasa jiulize, utatokaje jumatano, uende ya tano au –a tano yaani alhamisi? Yaani mambo haya hata waislamu wenyewe hawafahamu wanakokotwa tu kama waj2 wanavyokokotwa kwa kuabudu j2 huku wakimsingizia kuwa Yesu/Mungu hakuweka utaratibu wa siku ya ibada. Tena bila aibu kama Lwembe, wanadiriki kabisa kusema kuwa, wao (waj2), kalenda za dunia zimewapoteza na hivyo wameamua kujichagulia siku ya kuabudu. Kalenda za dunia zimewapoteza na hata hivyo hawataki kulisoma neno la Mungu ambaye katoa kalenda isiyo na utata. Neno la Bwana wamelipa kisogo na kuligeukia jua wakiliabudu jua bila ya aibu yoyote.
  Pili, Biblia iko wazi mnokwwa habari za siku ipi ni ya ibada Mungu aliyoiteua. Kama mnapotea, poteeni tu kibudu lakini msisingizie kuwa Mungu hajawaambia kumbe hamsomi ninyi wenyewe na pengine ni ushupavu wa mioyo yenu tu.
  Aidha, nikupe pole kaka Lwembe, kama bado unaamini kama kanisa ni entity Fulani. Kanisa la Mungu ni wewe mwenyewe pamoja na uhusiano ulo nao na Mungu wako. Kanisa la Mungu ni yule na huyo wanaoenenda sawasawa na neno la Mungu-sheria za Mungu. Unaweza ukawa msabato na bado ukapotea japo kuwa msabato ni mojowapo ya ishara ya kutembea ktk mapito ya Kristo. Sasa wewe mj2, usidanganyike kwa kuendelea kuabudu j2 ukidhani kuwa Mungu atakuokoa ilhali huenendi sawasawa na neno lake. Yaani wewe hata fursa ya kuitwa u heri, haipo kwako. Jitahidi tu kulifuata neno la Mungu na siyo kuangalia watu kama entity(kanisa) halafu ukaanza kuwakosoa. Utapotea na wewe kama wao kama kweli wamepotea. La msingi, ni wewe kuliangalia neno then lifuate. Mtazame Kristo kijana na siyo makanisa na mafundisho yake. Ndiyo maana nimekuwa nikipaza sauti kila siku weee kuwa watu wanapswa kulifuata na kulitii neno, ambalo kwa hilo automatically watakuwa wasabato na siyo wasabato jina tu, bali ni wasabato halisia waliojengwa kwenye misingi ya neno.
  Tatu, Dhana ya Wayahudi kulijenga hekalu upya, hiyo ni Luceferian Policy. Ikoje hiyo? Hiyo ndiyo kazi ya Lucifer aifanyayo na ana mkakati wa kuja kuihamishia vaticani pale Uyahidini. Makao makuu ya Papa, yanapangwa kuhamia pale, hiyo ndiyo ajenda ya siri inayowanya mataifa hayo wapigane hadi kesho. Ukisoma Biblia na hata wanamatengenzo kama akina Martini Luther, wameelezea sawia maana ya Israel kuja kuwa taifa teule tena!! Si taifa kama lilivyo sasa, bali ni wamataifa wote watakapofanyika kuwa wana wa Ibrahimu kwa njia ya imani ktk Kristo Yesu na si vinginevyo. Lakini kwa vile akina Lwembe wamelishwa unga wa ndele, hawatasikia haya wala hawatajibidisha kusoma ili wapate ufahamu, badala yake, wataendelea kubaki na kanisa la Kristo, kanisa lililoanza karne ya 20 lenye hatima ya kupoteza waumini wake.
  Kati ya watu waliopotea ni waj2. Yaani hawa hata njia bado hawajaiona. Heri kwa wasabato hata ambao ni wasabato jina tu maana njia wameshaiona, mabadiliko wapaswayo kuyafanya ni madogo sana. Watu msipobadilika na kutafakari vizuri, nasikitika kusema kuwa mtapotea na sisi akina Siyi na Gidion na wengine tutakuwa tulishanawa mikono kabisaaa. Kazi kwenu kuamua ni nani leo hivi mtakayemtumikia? Ni Mungu wa mbinguni au ni Baali?
  Bwana wabariki sana.

 119. Gidion,
  Nikushauri kidogo ndg yangu, hapa sio kanisa la Kisabato, kwahiyo kiongozi wetu ni Biblia, na si hisia za dini!

  Neno “Mosi” ni neno la Kiswahili ambalo maana yake ni “Moja” au “Kwanza”; hauwezi ukalifanya neno hilo liwe kitu kingine! Mimi nadhani jambo la kuyageuza maneno yaseme tofauti na asili yake ndilo linalo wasumbua ndg zangu! Tena niliwahi kuwaambia wenzako kuwa ninyi ni sehemu ya Uongo wa Kikatoliki, ninyi ni tawi lao tiifu ila hamjui tu! Tena nikawaeleza kuwa hata hizi siku za wiki katika majina yake ninyi mnazifahamu zaidi kuliko sisi mnaotuita wa J2. Ukweli ni kwamba hakuna kati yetu sisi wa J2 ambaye anaweza kusema kwa uhakika kuwa siku hii tunayoiita J2 ndiyo kweli siku ya Kwanza ya wiki kulingana na uumbaji, bali tumeikubali kalenda iliyopo na tunaendelea tukijua kuwa majina ya siku si muhimu sana kwetu, maana Mungu ametupa siku zote, ndipo J2 hii tunayosherekea KUFUFUKA kwa Kristo ni katika maana ya tukio hilo tu na si SIKU! Nanyi nikawaambia kuwa ktk kuiinua saana siku ya Jumamosi, mtakuwa mnaiabudu miungu ya kipagani kwa kificho! Nayo siku hiyo ya Jumamosi, ni siku ya ‘mungu’ wa kale wa kilimo wa Warumi ambaye anayeitwa SATURN, nayo siku yake ya kumsherekea inaitwa SATURDAY! Ni siku ya kufurahi na kucheza na mengineyo, ile ibada!!!!

  Pia kuhusu MHURI WA MUNGU kuwa ndiyo Sabato, maelezo yako yamenifurahisha sana, ni ya mtu aliyeshiba Mafundisho, bali hayana virutubisho, ndipo huyo ni lazima aishie kwenye “Kwashakor” ya kiroho!

  Umeongelea kuhusu Alama ya Mnyama, unachonishangaza ni jinsi unavyotaka kutupeleka mbali na jambo hilo ilimradi sasa hivi tunalo na linaendelea, mamilioni yetu tunaipokea Chapa ya Mnyama bila kujua, nawe ukiwa ni sehemu ya propaganda za huyo mpiga chapa! Kaka, Mnyama huwakilisha Nguvu! Basi liangalie kanisa leo hii linaitafutia wapi Nguvu hiyo, ni katika UMOJA!!! Nanyi Wasabato ni sehemu ya Umoja huo, maana kigezo cha kwanza, yaani mosi, ni kuukiri UTATU MTAKATIFU, ndipo nashindwa kuwaelewa mnapopiga piga makele ya kutuzubaisha, huku mnajua fika kwamba mlikwishaga kupigwa Chapa ya Mnyama zamaaaaani, basi kama ninyi si wanafiki ni nini!

  Kuhusu kitabu cha Ufunuo unasema, kiko wazi kwa yeyote yule. Huo pia ni uongo, kama kiko wazi mbona hujajiona ulivyopigwa Chapa ya Mnyama? Unayapeleka mbele mambo yanayotutokea sasa hivi! Kitabu hicho kimefunuliwa kwa Kanisa la Kristo tu, hilo alilolinunua kwa Damu yake, hilo ambalo amelitia Muhuri wake, yaani likiwa limeyapitia yote aliyowaambia mitume walifundishe, nalo likisha kuyapokea hayo, ndipo hutiwa huo Muhuri unaodhihirisha KUKAMILIKA kwao, huko KUJAZWA RM, na si huo uongo wa sabato mnaojishibisha!! Hao ndio pekee wanaoweza kuyaelewa hayo katika Ufunuo na si huyo roho wadini anayependa kujitambulisha kama RM akiwadanganya ilhali Biblia zenu zinawashuhudia kuwa ili kuwa Mkristo ni lazima uhubiriwe Injili kisha uiamini na Kubatizwa kwa Jina la Yesu Kristo ili upate ONDOLEO la DHAMBI, ndipo utamjua hata huyo RM!!!

  Kwahiyo nikuambie tu kuwa maelezo yako karibu yote ni hadithi za dini tu, huna hata kimoja unachokielewa, hata unapooneshwa ukweli nakuona unashindwa kabisa kuuona! Angalia, nimekuonesha kuwa hao unao wadhania kuwa ni Kanisa, sio, ni Wayahudi hao yale makabila 12, nayo idadi yao ndiyo hiyo, 12,000 kwa kila kabila ndio inawafanya wawe 144,000, kanisa katika wakati wa kuitwa kwao litakuwa limekwisha kuondolewa hapo muda waliopangiwa watu wa Mataifa utakapo koma, Mungu akiwarudia Israeli tena hao wanao endelea ktk Torati hata leo, tena watalijenga upya HEKALU lao ili wamwabudu Mungu tena! Wayahudi mpaka sasa hawana mahali pa kufanyia Ibada, ndio maana unaona wanataka kuuvunja ule msikiti uliojengwa juu ya msingi wa Hekalu lao!!!!

  Ndg yangu, umepotea sana huko msituni, itazame Nuru ya Injili inayokuangazia ili upone, ikimbie hiyo miungu ya Kirumi unayoiabudu nawe hujui, hiyo miungu ya Mapokeo; usiwe mwepesi kupokea kila kitu, ipokee Nuru kwanza, nenda nawe ukatubie mafundisho haya unayoyamwaga hapa, kisha wakubatize kwa Jina la Bwana Yesu Kristo ili uondolewe Dhambi zako, uwe HURU!!

  Gbu!

 120. Lwembe,
  Ninamshukuru Mungu kwa vile umeelewa hadi ukakiri kwa kinywa chako mwenyewe, kuwa Sheria ni Neno la Mungu. Mungu akubariki sana rafiki yangu.
  Sehemu zingine, unaonekana kubisha tu ndg yangu. Labda huenda ni kwa vile nilitumia maneno kama vile “kugundua”, ndiyo maana umepatwa na ukakasi wa kukubaliana nayo. Lakini ukiangalia tena bila ya kutumia akili nyingi sana, utaona iko wazi kuwa, Sheria kama neno la Mungu, limegawanyika. Kugawanyika kwa neno la Mungu ni matokeo ya dhambi. How? Sikiliza,
  1. Isingekuwa dhambi, Neno la Mungu lisingeandikwa kama kitabu leo maana lilikuwa ndani ya mioyo ya watu tayari tangu mwanzo.
  2. Dhambi ilipoingia, iliondoa sheria za Mungu (neno la Mungu) ndani ya mioyo ya watu. Watu wakawa hawamfahamu Mungu. Na kwa sababu ya upendo wa Mungu kwa wanadamu, Mungu aliamua Sheria-Neno lake, liandikwe kama kitabu ili kudhihirisha kilichokuwepo mwanzo ndani ya mioyo ya watu kabla ya dhambi.
  3. Kilichokuwepo ndani ya mioyo ya watu kabla ya dhambi, kilikuwa ni pamoja na
  a. Tabia ya Mungu (sheria za Maadili-Katiba yake-yenye msingi wa upendo)
  b. Sheria za Asili-Jinsi Mungu alivyoviumba vitu vyote kwa amri na kwamba vitu hivyo bado vinatii sheria za maumbile hayo.
  c. Sheria za vyakula kwa binadamu aliyekuwa ameumbwa kwa sura na mfano wa Mungu.
  Neno la Mungu kabla ya dhambi kuingia duniani, lilieleweka hivi katika mioyo ya watu. Na ukiangalia hapa, utaona kwamba, Neno hili(Sheria hizi) hazikuwa na shida yoyote wala hazikuhusika na chochote kilichoitwa dhambi. Dhambi ilipoingia, na kuondoa neno hilo mioyoni mwa watu, Mungu ilibidi kupitia RM aliandike neno hilo ili watu waje kumfahamu Mungu tena kama ilivyokuwa hapo awali. Kwa vile hofu au upendo wa awali wa watu kwa Mungu katika mioyo ya uliondolewa na dhambi, basi, Mungu ilibidi atengeneze by-laws za kuwafanya watu kuishi kwa matumaini. Miongoni mwa by-laws hizi, zilikuwa ni sheria za kafara, sheria ambazo wafasiri wa Biblia wameziita TORATI tu. Na ndani ya Biblia, Sheria za kabla ya dhambi na zile za baada ya dhambi, zote kwa pamoja zinaitwa TORATI.
  Tatizo la watu ni kushindwa kubainisha mjumuiko wa torati hizi. Kimsingi siyo tatizo lao, ila ni tatizo la uelewa tu. Siku RM ambaye ni mwalimu wetu sote atakapowafunulia, wataelewa tu. Sisi hatuwezi kuelewa au kugundua chochote pasipo msaada wake.
  Mtu akisema Kristo kuwa ni mwisho wa sheria(torati), yuko sahihi. Tatizo ni pale atakaposhindwa kubainisha kuwa ni mwisho wa sheria zipi?? Akishindwa kufahamu kuwa Kristo ni mwisho wa Sheria za Kafara, na badala yake akajumuisha Sheria(torati) zote, kwa maana ya neno la Mungu lote, atakosema sana. Sheria(neno) za baada ya dhambi zilikuwa ni kivuli tu cha Kristo. Kwa maneno mengine, Kristo alikuja kuondoa zile Sheria(neno) zilizoingia baada ya dhambi na siyo neno/sheria alizozifanya YEYE mwenyewe kabla ya dhambi, yoh 1.
  Kristo aliyekuwepo tangu mwanzo kabla ya dhambi, Kristo aliyeviumba vyote, Kristo ambaye ndiye Sheria(neno la Mungu) kabla ya dhambi, ndiye aliyekuja kurejesha hali ya awali kuliweka neno lake ndani ya mioyo ya watu wake kwa njia ya YEYE mwenyewe kukaa ndani ya mioyo ya watu kupitia RM. Na anasema kuwa, bila YEYE kukaa ndani yetu, sisi hatuwezi lolote.
  Tutayaweza yote katika YEYE atutiaye nguvu pindi atakapokaa ndani yetu. Tatizo jingine ninaloliona ni ile maana ya “Kristo Kukaa ndani yetu”. Kristo kukaa ndani yetu ni ile hali ya ukamilifu ambayo wafuasi halisi wa Kristo huifikia baada ya kufikia kiwango cha kutowaza/kunia mabaya moyoni. Mtu au Mkristo anayenia mabaya moyoni, huyo hana Kristo ndani yake, maana Kristo hakai wala hana nasaba za dhambi, japo awapenda wadhambi.
  Mkristo yeyote aliyempokea Yesu, huwa ana tabia ya kukua(kuukulia wokovu) chini ya mafundisho ya Biblia. Katika hatua hii ya makuzi, mtu huyo huanza na kutotenda dhambi kimwili(jambo ambalo wengine huwachukua kwa muda mrefu sana), na hatimaye, hufikia kiwango cha kutofikiria kabisa hata hayo maovu-uongofu halisi. Kuufikia uongofu huu, hufanywa na RM.
  Mtu aliyefikia kiwango hiki, huitwa mtoto wa Mungu, mtu aliyezaliwa na Mungu. Maana huwezi kuwa mtoto wa Mungu wakati huwa unawaza mabaya, licha ya kutonekana kuyatenda kwa mwili. Huku ndiko kuzaliwa na Mungu anakokuzungumzia Yohana.
  Tatizo la wakrito walio wengi leo, wanafundishwa na walimu eti kwamba, mtu anapompokea Kristo tu, hapohapo anakuwa tayari ni mzaliwa wa Mungu. Wanashindwa kufahamu kuwa sifa ya uzaliwa wa Mungu anayo Kristo na wale watakaokubali kuishi kama Kristo. Ni muhimu watu waelewe kuwa, mtu anapompokea Kristo, hutangaza vita kati yake na mamlaka za giza. Hivyo majaribu, kuanguka na kuinuka huwa ni sehemu ya maisha yake hadi hapo atakapofikia UKAMILIFU HALISI. Na hii ndiyo siri ya utauwa unayoisema ndg yangu.
  Karibu kwenye Neno(Sheria) la Mungu. Tii Sheria(Neno la Mungu) upate kuishi.
  Ubarikiwe

 121. Lenda,
  Kaka Lwembe nampenda sana kama ninavyowapenda wengine hapa Sg. Tuna historia naye ndefu kidogo ya kujifunza neno. Ukimwangalia juujuu tu, unaweza kufikiri kuwa jamaa huyu ni mbishi saana, kumbe sivyo. Huwa anaelewa ila huwa hataki kuonesha moja kwa moja kuwa kaelewa!! Ukimfuatilia, utamgundua taratibu kuwa, alielewa ama hakuelewa. Karibu kaka Lenda tumsaidie huyu jamaa na wengine. Namwona Gideon mjoli wa Bwana anatiririka hapa si mchezo. Huyu jamaa(Lwembe) kama ana masikio ya kusikia, ataelewa tu. Ana katheolojia ka unyakuo wa siri, sijui kakapata wapi ndani ya Biblia!! hatari kweli. Yaani watu wanapotea hivihvi!!

 122. Siyi,
  Nimefurahi sana kwamba angalau umesogea katika ufahamu ingawa ni kwa ‘mafungu’, lakini nina amini ukiyaunganisha mafungu hayo utapata kitu cha kukufaa, ambacho pia unaweza ukawasaidia nacho akina Lenda na Gidioni!

  Ni kweli kabisa, Sheria ni Neno la Mungu! Tena uumbaji wote, kama ulivyosema, umefanyika kwa Neno ambalo ndilo Sheria.

  Hayo mambo mengine ya “UGUNDUZI” ndani ya Neno la Mungu au hiyo Sheria, hapo unaponishawishi kwamba, “Ukiendelea kusoma mwanzo 1 na 2 utagundua kuwa, kuna sheria za aina takribani tatu”, hii ni hekima yako Siyi na walimu wako. Nikikusikiliza nitakuwa sawa na Hawa aliyemsikiliza Nyoka katika hekima na akaishia kuivunja Sheria ya Mungu! Neno la Mungu, hiyo Sheria yake, inanitosha, kama Mungu aliigawa Sheria yake katika mafungu matatu, kwa kusudi lolote lile, ni dhahiri angetuambia hivyo badala ya kutuachia sisi “tugundue”!

  Kuhusu kushake, unaponiambia “kulisababishwa na kuvunjwa kwa Sheria za Maadili, ambao ndio Msingi wa Sheria zote,” hapa tena naona utakuwa umechepushwa njia katika ufahamu. Hapo mwanzo nilikuelewa vizuri sana uliposema “Sheria ni NENO la Mungu” na si MANENO ya Mungu ambavyo hayo ndio yangefanya ‘Sheria “ZOTE” kama hizo unazosema “Sheria ZA Maadili” na “Sheria ZA Viumbe” nk mwisho unaweza ukawa na mafungu hata zaidi ya kumi! SHERIA ni majumuisho ya mambo yote yapasayo uongofu, maagizo yooote ndio yanayoifanya SHERIA na si hadithi zako hizo Siyi, sijui sheria za Maadili, za Viumbe, za Makafara, za Asili … unaona, hapo tu kidogo yamekwisha fika mafungu manne nawe ulisema ni matatu!!!

  Ukiisha ligawa Neno la Mungu ni vigumu sana kuendelea katika muelekeo sahihi. Maelezo yako mengi ni hekima ya mafundisho yenu ambayo ya kujichanganya changanya sana, angalia hapa ulichokisema hapo mwanzoni, “Neno(sheria) lililoamuru nuru iwepo, ndilo neno hilohilo lililoifanya nuru hiyo idumu kung’aa, dunia ilizunguke jua, na vitu vyote kufuata mfumo huo hadi leo, ndilo neno hilohilo litakaloviondoa vyote. Neno halijabadilika. Uwezo wa neno ni uleule.” Ndipo unashindwaje kuelewa hayo yanayofuatia yakiyatimiza haya unayoyakiri? Kama kwa Neno hili, “Kristo ni Mwisho wa Sheria”, ndipo Neno hilo linaitowesha Sheria, basi kwa nini unalikataa Neno hili? Au Biblia yako imeandikwa “”Kristo ni mwisho wa sheria ya kafara”?? Au mnasomaga Biblia zenu kama gazeti? Hii ndio hasara ya kutokuwa makini!

  Haya unaendelea kuniambia, “Nina imani kama utashuka chini ukubali kuongozwa na Roho, huwezi ukawa na mawazo dhaifu kama haya: “Lakini Mkristo HATENDI DHAMBI,…” halafu unasisitiza kwamba, “Kama wakristo hatutendi dhambi, hii ina maana kwamba, hatuna haja ya msamaha, na kama hatuna haja ya msamaha, hatuna haja ya mwombezi wetu Yesu Kristo, na kama hatuna haja ya Mwombezi, Yesu alikufa bure msalabani.
Yesu awajua walio wake (wale waliomkiri na wanaoukulia wokovu kila siku anawapatia nguvu). Wale walio upande wa Ibilisi hahangaiki nao.”
  Bado ninakushangaa, maana kama hauwezi kuyaamini Maandiko, tegemeo lako ni nini? Hata huyo Roho Mtakatifu unayeniambia nikubali kuongozwa naye nadhani labda ulimaanisha roho wa dini yenu! Dini yenu inayo mbingu ya kuwapelekeni? Mnatia huruma, inawachanganya sana dini yenu hiyo!

  Angalia ulichokinukuu hapa, Yeremia 31:33 “Bali agano hili ndilo nitakalofanya na nyumba ya Israeli, baada ya siku zile, asema Bwana; Nitatia sheria yangu ndani yao, na katika mioyo yao nitaiandika; nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.” Si unaona hapo Mungu anasema atatia Sheria yake ndani yao, nawe si ulisema Sheria ni Neno la Mungu, nayo Biblia yako si imekuambia kwamba Kristo ndiye Neno la Mungu; Naye Kristo si amekuambia kuwa atakuwa ndani yako, sasa usichokielewa ni nini kuhusu Mkristo huyo aliyefanyiwa hayo kutokutenda dhambi? Au wewe ukisoma Maandiko haya huwa unaelewa nini, 1Yn 5:18 “Twajua ya kuwa kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi” au 1Yn 3:9 “Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu.” Huu ndio ukomo wa mambo hayo Siyi, Mungu anakaa ndani ya wanawe kama huko Mwanzo, bali sasa katika ukamilifu, hii ndiyo ile “MYSTERY of GODLINESS” yaani “SIRI ya UTAUWA”, Ibilisi hawagusi!!!

  Karibu Siyi, Neno la Mungu, ile SHERIA, inayo uweza ndani yake wa KUKUBADILISHA, jinyenyekeze, ipokee Injili waliyoihubiri mitume, hao aliowatuma ili upate kuifanya kazi ya Mungu!!!!

  Ubarikiwe!

 123. Unajua kama mtu amejaaliwa kubisha, atabisha hadi Yesu atakaporudi ataendelea tu kumbishia! na si kosa lake ni la viongozi wake wanaomfundisha hivyo ambao wamekula viapo vya wanadamu hadi kufa,nawashauri ndugu zangu jaribuni kumwogopa mungu auwaye mwili na roho na si mwanadamu auwaye mwili na jaribuni kulielewa neno la MUNGU lisemavyo na si kwa matakwa yenu yalivyo, na MUNGU mwenyewe anasema ”watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa;kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa ,mimi nami nitakukataa wewe ,usiwe kuhani kwangu mimi kwa kuwa umeisahau sheria ya MUNGU wako,mimi nami nitawasahau watoto wako”(hosea 4;6) sasa kama ck lwembe na wengine wengi wanavyoendelea kubishana na neno la MUNGU lisemavyo,yatupasa kuwaombea kwani hawajui walitendalo,

  Ninapoendelea kumnukuu lwembe anavyosema ya kwamba hatujui hata neno ”mosi ” kwa kibinadamu linamaanisha nini,napenda kumshauri ya kwamba hapo mwanzo hizi siku kwa majina ambazo tunazo leo hii hazikuwepo,lakini zilikuwa zinajulikana kwa,siku ya kwanza,ya pili,hadi ya saba kwa MUNGU, lakini ndo wanadamu wakaanza kuzipa majina hizo siku kwa miungu ya kirumi ambazo ni sunday up to suturday kwa kiingereza,lakini kama ni mfuatiliaji mzuri sana wa vitabu vya historia utaligundua hilo na kama hufuatilii we ni kukalia tu kuzikariri tu ya kwamba neno ”mosi” ni moja utaishia kubaya ndugu yangu lwembe nakushauri uwe mfuatiliaji mzuri wa vitabu vya historia na ujue jinsi Dunia inavyokwenda,na kama huna facts zozote za kubishia ni afadhali kukaa tu kimya na sio kubisha bila msingi wowote wa kimaandiko na unakalia tu kukariri vifungu vya kibiblia bila ya kuvielewa vinamaanisha nini na ukiwa unavisoma omba kwanza roho mtakatifu aweze kukuelimisha na sio kwa fikra zako mwenyewe,

  Na swali lako la pili umejaribu tu kunakili kifungu cha biblia na bila ya kukielewa kinasemaje ambacho umesema, angalia muhuri wa MUNGU ndio huu ”wala msimhuzunishe yule,roho mtakatifu wa MUNGU ambaye kwa yeye mlitiwa muhuri hata siku ya ukombozi”(waefeso 4;30) na bila ya kumwomba roho mtakatifu apate kukuongoza ili kukitolea maana yake jinsi ilivyo na kama unajua huwezi kukielewa kifungu chochote ni afadhali tu kuomba msaada kwa mtu yeyote anayeelewa biblia vizuri na sio tu kupost vitu ambavyo hujui vinamaanisha nini.
  Na ngoja tuangalie kwa undani zaidi;

  MUHURI WA MUNGU NINI.

  Kama MUNGU angechagua kuandika ujumbe wake kuhusu alama ya mnyama katika mawingu,usingeweza kuwa na matokeo ya kufaa sawa na mbinu aliyotumia.mawingu yanatoweka,lakini biblia imestahimili nayo inapatikana kwa ajili ya mabilioni ya watu duniani ili waweze kujisomea wao wenyewe majumbani mwao.Bila shaka unajua kuwa inayo maonyo ya kutisha kutoka kwa MUNGU dhidi ya mtu yeyote atakayepokea ”alama ya mnyama” katika mkono wake au katika kipaji cha uso wake .

  Hili sio jambo dogo,kwani onyo hilo ndilo la mwisho analolitoa MUNGU.na MUNGU husema kwa ukali mara chache sana,lakini anautangaza kwa sauti kubwa ujumbe wake wa haraka kuhusu ”alama hiyo”
  Kuwa mkristo maisha yako yote na kisha ukapokea alama hiyo ya mnyama katika saa ya mwisho ya historia ya ulimwengu huu utakuwa ni msiba wa kutisha .
  Alama ya mnyama itakuwa ni hatua ya mwisho katika uasi dhidi ya MUNGU ;lakini utakuwa ni uasi uliofichwa kwa werevu sana kuliko mwingine ambao shetani amewahi kuwashirikisha wanadamu.na litakuwa ni jaribu lake kubwa kuliko mengine yote,na la kisasa zaidi,na lenye udanganyifu mkubwa kuliko yote aliyowahi kuyabuni,kwani litakuwa limevaa ”ukristo ndani yake”. nalo litabuniwa na kutekelezwa katika kipindi cha mgogoro mkubwa wa kiuchumi,wakati itakapoonekana ya kuwa ni lazima watu wote waungane ili kuepusha janga la ulimwengu mzima.na itaonekana kana kwamba alama ya mnyama ndio ufumbuzi pekee, na neno la MUNGU linatuambia kuwa mtu yeyote atakayepinga ,atatishwa vikali na mamlaka ”itayokuwepo”
  tunayasoma hayo yote katika ufunuo 13 na 14.na haya ni mambo yaliyosimuliwa kabla ya matukio ya mwisho ambayo yatasababisha mwisho wa historia ya ulimwengu mzima.
  Tunaweza kugundua jinsi alama ya mnyama itakavyokuwa .na hakuna hata mmoja ulimwenguni kote aliyekwisha kuipokea hadi sasa,lakini kila roho ya mwanadamu inajiandaa ama kupokea alama hii ,au kinyume chake,muhuri wa MUNGU .na kupokea alama ya mnyama itakuwa ni mwisho ya kuabudu nafsi,kituo ambacho kila nafsi hukiendea; ”Na mwingine,malaika wa tatu,akawafuata,akisema kwa sauti kuu ,mtu awaye yote akimsujudu huyo mnyama na sanamu yake,na kuipokea chapa katika kipaji cha uso wake ,au katika mkona wake ,yeye naye atakunywa katika mvinyo ya ghadhabu ya MUNGU iliyotengenezwa,pasipo kuchanganywa na maji”(ufunuo 14;9,10)
  ”Naye (mnyama mwenye pembe mbili ) awafanya wote ,wadogo kwa wakubwa,na matajiri kwa maskini,na waliohuru kwa watumwa ,watiwe chapa katika mkono wao wa kuume au katika vipaji vya nyuso zao ;tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza ,isipokuwa ana chapa ile,yaani ,jina la mnyama yule ,au hesabu ya jina lake”(ufunuo 13;16-17)
  Baadhi ya watu husema ya kwamba haiwezekani mtu yeyote kuelewa maana ya maneno hayo .lakini tukumbuke ya kuwa kitabu cha mwisho katika biblia ni ”ufunuo”,yaani ,kitu kilichofunuliwa,ambacho;hakijafichwa ,MUNGU atakuwa hajatenda haki kama akitoa maonyo kama haya katika kitabu chake kwa mamilioni ya familia ulimwenguni kote,na bila kuturuhusu kuelewa maana yake !
  Njia pekee ya kuepuka kupokea alama ya mnyama ni kuupokea muhuri wa MUNGU .na wale wasioupokea muhuri wa MUNGU moja kwa moja watakuwa wanajiandaa kupokea alama ya mnyama.
  Muhuri wa MUNGU ni kitu chema ;na alama ya mnyama ni kitu kibaya,na hebu tuanze na chema kwanza;

  Muhuri wa mungu ni kitu cha kweli ,ambapo alama ya mnyama ni kitu cha bandia .kabla ya kristo hajarudi ,kila mtoto wa MUNGU atakuwa ameupokea muhuri wa MUNGU katika ”kipaji cha uso” wake .Ndio ,lugha ambayo MUNGU anaitumia ni ya mfano ,lakini ujumbe unatujia ukiwa dhahiri; ”Baada ya hayo nikaona malaika wanne wamesimama katika pembe nne za nchi ,wakizizuia pepo nne za nchi ,upepo usivume juu ya nchi,…..nikaona malaika mwingine ,akipanda kutoka maawio ya jua ,mwenye muhuri ya MUNGU aliye hai ;akawapigia kwa kelele na kwa sauti kuu wale malaika wanne waliopewa kuidhuru nchi na bahari,akisema ,msiidhuru nchi ,wala bahari,wala miti,na hata tutakapokwisha kuwatia muhuri watumwa wa MUNGU wetu juu ya vipaji vya nyuso zao .nikasikia hesabu yao waliotiwa muhuri ….watu mia na arobaini na nne elfu”(ufunuo 7;1-4)
  Hata mtoto anaweza kuelewa maana ya maelezo haya ;

  (a) ”pembe nne za nchi” zinamaanisha kuwa huu ni ujumbe kwa ulimwengu wote. kuna mahali pengine pamoja tu katika ufunuo ambapo tunaona ujumbe unaokwenda kwa ”kila taifa ,na kila kabila ,na lugha ,na jamaa”- yaani ujumbe wa ”malaika wa tatu” wa (ufunuo 14;6-12) .kwa kuwa ”malaika wa tatu” anaonya dhidi ya kuipokea alama ya mnyama ,ni wazi kwamba ujumbe huu wa kutia muhuri unafanana kabisa na wa malaika watatu.

  (b) ”pepo nne” ni ishara ya uharibifu utakaotokea duniani kote kama vile inavyoweza kutokea tufani au kimbunga na kuikumba dunia yote .kwa wakati huu roho mtakatifu wa MUNGU anazuia pepo kali za hisia kali za kishetani ambazo kwa sasa zinachemka katika mioyo ya mamilioni ya watu wengi duniani .na ninapokumbuka vizuri niliposhuhudia matukio ya kutisha ya uhalifu wa kutumia nguvu na uporaji yaliyotokea katika jiji fulani wakati udhibiti wa serikali ulipolegea kwa masaa machache tu katika jaribio hilo la kimapinduzi ya kijeshi,Washukuru wale ”malaika wanne ” kwa kile wanachokifanya kwa sasa ;kwani watakapoachilia zile pepo nne,hakuna maisha ya mtu yeyote yatakayokuwa salama mahali popote .Huu ni mwonekano wa haraka wa jinsi MUNGU anavyowalinda watu wake sasa.Na hii ndio sababu vita kuu ya tatu ya dunia haijatokea ambayo imekuwa ikihofiwa sana.

  (c) ieleweke kwamba muhuri wa MUNGU unaweza kupokelewa katika ”kipaji cha uso” na si katika mkono.MUNGU huridhia huduma yetu ya hiari na anayotolewa kwa kujua ;lakini ”mnyama” yeye hajali .na kwake ni sawa tu sisi kujua kwamba kile anachofundisha ni makosa na kutokiamini ni makosa kabisa ,maadamu kwa nje au kwa unafiki tunaambatana naye ,Hii ndiyo maana ya kupokea alama ya mnyama katika mkono ,na sio katika kipaji cha uso wake . (Ndiyo ,wengine kwa unyofu kabisa wanauamini ujumbe wa uongo wa mnyama -na hao wanapokea alama katika vipaji vya nyuso zao .na unyofu peke yake hauwezi kutuokoa!

  (d) muhuri ni sawa na sahihi .Huwezi kutia sahihi kwenye barua mpaka inapokuwa imemalizika .na unapoweka muhuri au sahihi yako kwenye kitu fulani ,unakuwa unamaanisha ya kwamba umekipatia ukubali wako wa mwisho .Hivyo muhuri wa MUNGU ni ushahidi wa ukubali wake wa mwisho wa tabia ya watu wake,ushahidi wa kukua kwao ndani ya kristo .Wakala anayefanya kazi ya kutia muhuri ni ”Roho mtakatifu wa MUNGU ,ambaye kwa yeye mlitiwa muhuri hata siku ya ukombozi”(waefeso 4;30)

  (e) Muhuri sio roho mtakatifu; bali ni ushawishi ambao Roho mtakatifu anautia katika tabia .Na tabia hufafanuliwa katika vipengele vya sheria ya MUNGU ;kwani ”pendo ni utimilifu wa sheria ”(warumi 13;10) ikiwa mtu anapenda kama kristo anavyopenda ,ataonyesha mapatano ya kweli na sheria ya MUNGU maishani mwake .Maisha ya jinsi hiyo yatakuwa ni muhuri wa MUNGU ,kwa maana bwana alitangaza ya kwamba muhuri wake unapatikana katika sheria yake,”ufungue huo ushuhuda ,ukaitie muhuri sheria kati ya wanafunzi wangu”(isaya 8;16)

  (f) Muhuri au sahihi halali ya mtawala ni lazima iwe na mambo matatu ya kuitambulisha ;jina la mtoa sheria ,cheo chake ambacho huashiria mamlaka yake ,na eneo la kiutawala ambapo mamlaka yake huishia .Hivyo ,kwa malkia wa uingereza kutia sahihi hati kama ”elizabeth”hakuhitaji tu jina lake (kwani wapo ”elizabeth” wengi sana duniani ,lakini pia cheo chake cha ”malkia ” (kuna malkia wengi pia ),na eneo lake la kiutawala ;uingereza ,jumuiya ya madola ,n,k,na yupo elizabeth mmoja tu wa jinsi hiyo!

  (g) kwa dhahiri Bwana anaitambulisha sabato yake ya siku ya saba kama muhuri wake ;”Tena naliwapa sabato zangu,ziwe ishara (muhuri) kati ya mimi na wao ,wapate kujua ya kuwa mimi ,BWANA ,ndimi niwatakasaye”(ezekieli 20;12; angalia pia aya ya 20) Hii ni kwa sababu sabato hujumuisha pamoja roho ya upendo ambayo imeenea pote katika sheria kamili ya mungu ya amri kumi alizoandika kwa kidole chake mwenyewe ,mlimani Sinai na akampatia Musa. na Huonyesha uaminifu wa kweli wa moyoni kwake yeye . Kuishika Sabato katika ulimwengu usioijali ni ishara maalumu ya kuwa tofauti;lakini, na la muhimu zaidi ,inahitajika muungano wa kweli wa moyoni pamoja na kristo kama ”Bwana wa sabato” (angalia mathayo 12;8). Kwa hiyo nawashauri ndugu zangu akina ck lwembe na wengine wengi mnaoibeza sabato ya Siku ya saba ya Bwana MUNGU wetu muweze kubadilika na kufanya Toba na MUNGU atawasamehe kwani hamjui lile mtendalo,na muombeni sana MUNGU apate kuwajaza na roho wake mtakatifu atawasaidia, BALIKIWA NINYI NYOTE,AMINA.

 124. Lwembe,
  Haha ha ha haa!! Umeanza kwa kuniuliza maswali. Nami ngoja nijibu kidogo tu.
  1. Siyi, hivi unaposoma neno “Sheria” huwa unaelewa nini?-
  Jibu.
  Ninaposoma neno sheria, huwa naelewa kuwa ni Neno la Mungu. Najua unashangaa!!! Sikiliza kaka, dunia na vyote viliumbwa kwa neno la Mungu. Zaburi 33: 6 Kwa neno la Bwana mbingu zilifanyika, Na jeshi lake lote kwa pumzi ya kinywa chake. Kama tunakubaliana sote ktk hilo….Sasa, hebu angalia jinsi Mungu alivyoumba…

  Mwanzo 1:
  3 Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru.
  6 Mungu akasema, Na liwe anga katikati ya maji, likayatenge maji na maji.
  9 Mungu akasema, Maji yaliyo chini ya mbingu na yakusanyike mahali pamoja, ili pakavu paonekane; ikawa hivyo.
  11 Mungu akasema, Nchi na itoe majani, mche utoao mbegu, na mti wa matunda uzaao matunda kwa jinsi yake, ambao mbegu zake zimo ndani yake, juu ya nchi; ikawa hivyo.
  14 Mungu akasema, Na iwe mianga katika anga la mbingu ili itenge kati ya mchana na usiku; nayo iwe ndiyo dalili na majira na siku na miaka;
  20 Mungu akasema, Maji na yajawe kwa wingi na kitu kiendacho chenye uhai, na ndege waruke juu ya nchi katika anga la mbingu. Nk

  Zingatia,
  Maneno niliyopigia mstari. Maneno hayo ni KAULI SHURUTISHI au AMRI. Kwa ufupi Biblia inasema kuwa kaka Lwembe, Dunia na vyote viliumbwa kwa AMRI au KAULI SHURUTISHI za MUNGU.
  Maana Yeye alisema, ikawa; Na Yeye aliamuru, ikasimama,
  Zaburi 33: 9.
  “Na vilisifu jina la Bwana, Kwa maana aliamuru, vikaumbwa” Zaburi 148:5 .

  Hivyo kaka Lwembe, Uumbaji ni matokeo ya neno la Mungu (amri za Mungu). Kila kitu kiliumbwa kwa amri za Mungu. Na kwa sababu vyote viliumbwa kwa AMRI za Mungu, vitatoweshwa kwa neno lilelile(Amri zizohizo).
  2Petro 3:5 Maana hufumba macho yao wasione neno hili ya kuwa zilikuwako mbingu tangu zamani, na nchi pia, imefanyizwa kutoka katika maji, na ndani ya maji, kwa neno la Mungu;
  2 Petro 3:7 Lakini mbingu za sasa na nchi zimewekwa akiba kwa moto, kwa neno lilo hilo, zikilindwa hata siku ya hukumu, na ya kuangamia kwao wanadamu wasiomcha Mungu.

  Neno(sheria) lililoamuru nuru iwepo, ndilo neno hilohilo lililoifanya nuru hiyo idumu kung’aa, dunia ilizunguke jua, na vitu vyote kufuata mfumo huo hadi leo, ndilo neno hilohilo litakaloviondoa vyote. Neno halijabadilika. Uwezo wa neno ni uleule.

  Ukiendelea kusoma mwanzo 1 na 2 utagundua kuwa, kuna sheria za aina takribani tatu. Sheria za Asili(zilizotolewa kwa viumbe na vitu vingine kama jua, mwezi, maji, nk, tofauti na mwanadamu.) Aidha, Utakumbana na Sheria za Maadili-Msingi wa Sheria zote (Mungu anamwagiza Adamu, usi…) Hali kadhalika, utakumbana na sheria za ziada kwa Adamu kuhusu chakula(kula miche yenye kutoa mbegu …). Mpaka hapa ndg yangu Lwembe, tunaweza kuona kuwa, Vitu vyote viliumbwa kwa sheria, vinafuata sheria, na vitaondolewa kwa sheria hiyohiyo. Na hoja ya kuondolewa kwa kutumia sheria hiyohiyo, ilikuja baada ya Adamu kuanguka dhambini-yaani kuvunja msingi wa sheri zote(sheria za Maadili – ile amri ya usi…), pale aliposikiliza sauti ya Nyoka badala ya ile ya Mungu-Muumbaji wake.

  Kuvunjwa kwa sheria za Maadili(Msingi wa sheria zote), kulisababisha kushake hadi kwa sheria za viumbe wengine pia. Mf. miti ilianza kupukutisha majani na kudondosha mapooza, wanyama wa mwitu wakaondokewa na ile hofu kwa mwanadamu kama mtawala wao, nguvu za asili, matetemeko, nyota, jua, mwezi nk vikawa na shida kwenye mifumo yake.

  Najua unaweza kujiuliza kuwa Siyi anatufundisha legalism?
  Jibu lake ni hapana. Sheria za Maadili ni za kiroho. Na makusudi ya Mungu yalikuwa ni kumwona mwanadamu anaziishi tu kama matokeo ya kupenda kutokuwa na miungu wengine ila YEYE YEHOVA. Na kwa sababu ni sheria za kiroho, Mungu aliziandika ndani ya mioyo ya watu wake…Baada ya dhambi, Mungu aliendelea kufanya kwa kiazi cha Israel kama alivyokuwa amekusudia tangu mwanzo-
  Yeremia 31:33 Bali agano hili ndilo nitakalofanya na nyumba ya Israeli, baada ya siku zile, asema Bwana; Nitatia sheria yangu ndani yao, na katika mioyo yao nitaiandika; nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.

  (Katika kulithibitisha hili, kumbuka post yangu niliyoitoa kipindi cha huko nyuma iliyokuwa inaonesha Kuwepo kwa Sheria za Maadili ndani ya Biblia, kabla ya mlimani Sinai- Rejea huko).

  Unachochanganya wewe na wengine, ni zile sheria za Kafara ambazo hazimo kabisa kwenye makundi matatu ya sheria za Mwanzo 1 na 2 (Sheria za Asili, Maadili na Vyakula). Sheria za kafara zinaanzia bustanini Edeni mara tu baada ya anguko la Adamu na Hawa dhambini. Mungu anachukua kondoo amchinje amwage damu ili kupoza makali ya dhambi na siyo kuondoa dhambi kabisa. Sheria hizi ktk kipindi cha wana wa Israel zinajulikana kama sheria za Musa, lakini kimsingi, mwanzilishi wake siyo Musa bali ni Mungu mwenyewe, pindi dhambi ilipoingia. Na sheria hizi, zinakuwa kivuli cha kutuleta kwa Kristo, damu ya Mwanakondoo pekee wa Mungu, ambayo inaondoa dhambi kabisa tofauti na zile za mafahari ya ng’ombe, mbuzi, kondoo nk.
  Ukisoma vizuri Biblia yako, Mafarisayo, Masandukayo na Waandishi wengi waliamini kuwa kwa sheria hizi za kafara(maana walijizuia kutovunja sheria za maadili wengine kwa kuogopa adhambu za kupondwa mawe, wengine kwa kuhofia gharama ya kutafuta fahari la mbuzi, kondoo nk) wangehesabiwa haki. Watu hawa walijihesabia haki kwa mfumo huo, japo haukuwa sahihi mbele za Mungu. Walikuwa na utii wa kimwili wa sheria za Maadili ilhali sheria za maadili zenyewe asili yake ni rohoni. Ndipo Yesu anawaambia wanafunzi wake kuwa, “Maana nawaambia ya kwamba, Haki yenu isipozidi hiyo haki ya waandishi na Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni” Mathayo 5:20. Yaani kutotenda dhambi kusipoanzia moyoni, hamwezi kuurithi ufalme wa Mungu. Kwa maelezo mengine, Yesu alikuja ku-rise the standard of keeping His Holly Laws kuliko ilivyokuwa inafahamika kwa mafarisayo naa masandukayo!!

  Yesu alitaka kuona utii wa sheria zake unaanzia mioyoni mwa watu na siyo kwa sababu ya hofu fulani za adhabu za kimwili. Kuja kwa Yesu kufa duniani, ilikuwa ni kurejesha hali ile ya awali ya mahusiano mazuri kati ya Mungu na watu wake. Lakini kwa vile dhambi ilikuwepo ndani ya mwanadamu tayari, na mwenye dhambi hawezi kumkaribia Mungu, Yesu alifanyika kuwa daraja letu la kumwendea Mungu na kuzungumza naye tena. Hivyo Yesu alichokiondoa ni sheria za kafara tu na siyo Sheria zile za Mwanzo 1 na 2(sheria za kabla ya anguko la adamu dhambini).

  2. Pia nikuulize, kati ya wewe na Roho Mtakatifu, ni nani aliye na uelewa zaidi wa moyo wa Mungu?
  Mimi siwezi kujilinganisha na Mungu. Maana RM ni Mungu. Na ili na mimi nielewe mambo ya RM, sharti Roho huyo akae ndani yangu maana, siwezi kuyaelewa mambo ya rohoni nikiwa katika mwili. Sharti niwe rohoni, yaani nikubali kuongozwa na RM(Mungu), ambaye pia mambo ya rohoni ni ya kwake.
  Na usipokuwa na RM, utaona maluweluwe tu kwenye neno la Mungu, ndiyo maana unasema hata mgawanyo wa sheria za Mungu huuoni ndani ya Biblia!! Kama siyo kichekesho ni nini!!! Hii ni ishara tosha kabisa kuwa, hauna RM, ndiyo maana huwezi kuyaelewa mabo haya ya rohoni japo yako wazi sana kwa wanaojinyenyejeza kujifunza chini ya uongozi wa RM.
  3. Nina imani kama utashuka chini ukubali kuongozwa na Roho, huwezi ukawa na mawazo dhaifu kama haya: “Lakini Mkristo HATENDI DHAMBI, nalo jambo hilo ndilo linalodhihirisha kukomea kwa Kristo Sheria yote pamoja na Amri zake Kumi na vyote!”. Kama wakristo hatutendi dhambi, hii ina maana kwamba, hatuna haja ya msamaha, na kama hatuna haja ya msamaha, hatuna haja ya mwombezi wetu Yesu Kristo, na kama hatuna haja ya Mwombezi, Yesu alikufa bure msalabani.
  Yesu awajua walio wake(wale waliomkiri na wanaoukulia wokovu kila siku anawapatia nguvu). Wale walio upande wa Ibilisi hahangaiki nao.
  4. Kuhusu unabii, naona wewe una tafsiri tofauti na mimi ya unabii wa Biblia. Mf Daniel 9:29 wa juma la 70, wewe unaamini kuwa ni unabii ambao haujatimia. Mimi ninavyoifunua biblia, inanieleza kuwa, unabii wa juma hilo la 70, ulitimia zamani kabisa kati ya miaka 27 AD hadi 34 AD. Chunguza na wewe nani yuko sahihi kati ya mimi na wewe!! Nazidi kukusihi tena na tena ujitahidi kuchunguza sana badala ya kuwa mbishi tu.
  Ubarikiwe na Bwana

 125. Ndugu Siyi
  Lwembe angekua karibu nawe angekukata masikio, akisikia Sabato au Wasabato moyo unamwaka. Mlimfanya nini huyu mtu wa Mungu.

 126. Siyi, hivi unaposoma neno “Sheria” huwa unaelewa nini?
  Pia nikuulize, kati ya wewe na Roho Mtakatifu, ni nani aliye na uelewa zaidi wa moyo wa Mungu? Maana nimetafuta nipaone ambapo Mungu amezigawa Sheria sijapaona, naona ni elimu za dini ndizo zinazigawa Sheria kwa manufaa ya mafundisho yenu yenye kufisha!

  Lakini hata hivyo, ili kulielewa hilo ninalolisema, nilikuambia kuwa ni lazima uwe ni yule aliyezaliwa mara ya pili, vinginevyo si rahisi kuyaelewa hayo! Mkristo aliyezaliwa mara ya pili ni huyo ambaye Kristo anaishi ndani yake. Kwahiyo asili yake imebadilishwa! Tamaa yake si haya yanayokusumbua wewe ambaye ni “borderline believer”, hapana, yeye tamaa yake ni kumdhihirisha Kristo aliye ndani yake! Najua bado hutaelewa, lakini ili uelewe angalau hata kidogo tu cha hicho ninachokuambia, chukua Biblia yako jaribu kutafuta sehemu yoyote ile ambayo Kristo alijizuia kumsengenya mtu, au kumtukana, au kutamani mke wa jirani yake au kuzini na wanawake waliomzunguka, au kuipokea heshima ya Baba yake iwe yake, au kumshuhudia uongo yeyote yule, au kuwadharau wazazi wake, au kuiba, au chagua dhambi yoyote unayoijua, halafu tafuta ni wapi ALIJIZUIA kuitenda dhambi hiyo!!

  Ukiona umepakosa, na ni lazima upakose, maana wote walioisimamia Sheria ili kutoa Hukumu ya Haki, walimuona hana makosa, isipokuwa makuhani wanafiki na viongozi wengine wa dini, ambao muendelezo wake ndio hawa walimu wenu wa leo wanaowafundisha kuwa kamwe hamtaweza kuwa si watenda dhambi! Nanyi ndivyo mlivyo kweli kulingana na imani yenu, ni zambi ,zambi, zambi, mwanzo mwisho! Lakini Mkristo HATENDI DHAMBI, nalo jambo hilo ndilo linalodhihirisha kukomea kwa Kristo Sheria yote pamoja na Amri zake Kumi na vyote!

  Unabii unaosema nimeupotosha, hata sijui nikwambie nini! Labda nikuulize, hao 144,000, ni Wasabato? Si unaona mnavyojichanganya! Halafu mnakuwa waoga wa kukubali ukweli. Hao 144,000 ni Wayahudi, tena wakati huo wanapotiwa muhuri Kanisa litakuwa limekwisha ONDOKA katika nusu ya hilo Juma la Sabini la Danieli!

  Haya umekuja tena na unabii wa Danieli 9:27, “Naye atafanya agano thabiti na watu wengi kwa muda wa juma moja; na kwa nusu ya juma hiyo ataikomesha sadaka na dhabihu; na mahali pake litasimama chukizo la uharibifu; na hivyo, hata ukomo, na ghadhabu iliyokusudiwa imemwagwa juu yake mwenye kuharibu.”
  Unabii huu unapouhusisha na Kanisa ni kichekesho kingine! Huyo anayekomesha sadaka na dhabihu ni yule Mpinga Kristo na si Kristo! Unaona mnavyojichanganya? Umeuchukua unabii utakao tokea katika ile nusu ya Juma la Sabini kwa Israeli, huko mbele Kristo atakapowarudia, na wao kulijenga Upya Hekalu lao ili waendelee na sadaka na dhabihu zao, ninyi mmeupachika huku nyuma kwa Kanisa ili muichukue nafasi ya Israeli!!!! Huko ndiko kuchanganyikiwa kwa kiroho kulikowapata! Ninyi ndio “watu wa Danieli”?!!!!!

  Nawaona ni watu mliochanganyikiwa, yaani mko katika Bumbuwazi la Kiroho, ile Spiritua Amnesia!!!! Poleni sana kama pole itawafaa!

 127. Lwembe,
  Ndiyo Kristo ni mwisho wa Sheria!! Lakini inabidi ufahamu kuwa ni sheria zipi hizo?? Jibu, za kafara tu peke yake!! Hata unabii unaoupotosha kuitafsiri, unzungumzia kuwa Masihi atakomesha sadaka za kuteketezwa na siyo na sheria za maadili bro. Acha kuchanganyikiwa!! Soma hii upate kidogo.. Daniel 9: 27 Naye atafanya agano thabiti na watu wengi kwa muda wa juma moja; na kwa nusu ya juma hiyo ataikomesha sadaka na dhabihu; na mahali pake litasimama chukizo la uharibifu; na hivyo, hata ukomo, na ghadhabu iliyokusudiwa imemwagwa juu yake mwenye kuharibu.
  Je, jiulize, sadaka za dhabihu ni sheria za maadili? Sadaka za dhabihu ni sheria za asili? Mbona kichwa chako kizito kaka kuelewa mambo rahisi kama haya?
  Yesu alichokomesha , ni sheria za kafara na si vinginevyo. Acha kudanganyika. Ngoja nimwache kidogo Gideon akuelimishe zaidi, huenda utaelewa bro.
  Mimi nipo tu kwa mijadala ya neno la Mungu tena wakati wote. Wewe ukipost hoja zinazonihusu, plz, email me as well ili niione kirahisi maana several times nakuwa kwenye email zaidi kuliko kwenye blog hapa. Tuko pamoja kaka. Jitahidi tu, usipotee

 128. Mwanzo 1:5-31, siku zote sita za uumbaji zinahesabika kuanzia siku moja hadi siku ya sita, kwa mgawanyo wa “Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya …” Siku ya Saba, hiyo aliyopumzika Mungu, haina “Ikawa jioni ikawa asubuhi, …” Mungu alirudi katika Umilele, huko anakorudishwa Mkristo aliyezaliwa mara ya pili, huyo ASIYEKUFA!!!

  Tazama hapa na kwingineko maagizo wanayopewa Israeli ukione hicho kuvuli cha hayo Mambo Makuu ya Mungu aliyoyaficha, na sasa akiyafunua kwao katika hatua ya awali kimwili, bado pia hakuwapa majina ya siku!

  Kut 16:26,
  “Siku sita mtaokota; lakini siku ya saba ni Sabato, siku hiyo hakitapatikana.”

  Kut 20:9-10,
  “Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; 10-lakini siku ya saba ni Sabato ya BWANA, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako.

  20:11
  “Maana, kwa siku sita BWANA alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo BWANA akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa.”

  Kut 34:21,
  “Utafanya kazi siku sita, lakini katika siku ya saba utapumzika; wakati wa kulima mashamba, na wakati wa kuvuna pia, utapumzika.”

  Hakuna sehemu yoyote ile katika Biblia inayosema kuwa siku ya Saba au Sabato ni “Jumamosi”! Mstari unaougawa uelewa wa ki Mungu na wa ki Dini ni mwembamba sana, ndio maana ninyi mmeupitiliza na kuanza kuabudu Siku badala ya Mwenye siku! Mmejirudisha katika ibada za kipagani bila uelewa!!!

  Hivi huwa hata hamuwazi kwanini Mungu hakuzipa majina siku? Mungu ni mjanja kuliko Ibilisi, alimuachia Ibilisi azitumie kuwakusanyia watu wasio na Hekima! Mnahangaika na Siku kuliko maelekezo mnayopewa. Wayahudi wenzenu wanaendelea katika Sheria, tena nimekuambia kuwa sabato yao waliihesabu kutoka hesabu ya siku ya ki Misri, huko walikokuwako kwa miaka 400, hawakupewa hesabu mpya ya siku jangwani! Wala Mungu hajawahi kuzipa siku majina!!!

  Hata kwa akili ya kawaida tu kwamba unajua Kiswahili, Je, haujui kuwa neno ‘Mosi’ maana yake ni moja? Kama mosi ni moja je, Jumamosi itakuwa ni saba? Tusemeje basi, kwamba hesabu yako ya siku umeitoa katika uongo wa Kikatoliki? Wewe unajuaje kuwa Jumamosi ndio siku ya saba, hiyo aliyopumzika Mungu? Acheni kuutukuza uongo wa dini! Kama kalenda imechezewa, vipi kuhusu mpangilio wa siku, unauhakika gani kuwa siku ziko kama zilivyokuwa katika uumbaji, hata ukijitia unazijua, utazijua kwa rejea gani???

  Angalia jinsi mnavyojikoroga na dini yenu hiyo:
  “”“7; Sabato ni ”muhuri wa MUNGU”
  ”nikaona malaika mwingine ,akipanda kutoka maawio ya jua ,mwenye muhuri ya mungu aliye hai ;akawapigia kelele kwa sauti kuu wale malaika wanne waliopewa kuidhuru nchi na bahari ,akisema ,msiidhuru nchi ,wala bahari ,wala miti,hata tutakapokwisha kuwatia muhuri watumwa wa mungu wetu juu ya vipaji vya nyuso zao,nikasikia hesabu yao waliotiwa muhuri katika kila kabila ya waisraeli ,watu mia na arobaini na nne elfu (ufunuo 7;2-4)na neno ”israeli” linamaanisha wale wanaomwamini kristo kwa kweli ;yeye ni myahudi aliye myahudi kwa ndani; na na tohara ni ya moyo ,katika roho na si katika andiko ”(warumi 2;29) ”Na kama ninyi ni wa kristo ,basi mmekuwa uzao wa ibrahimu ,na warithi sawasawa na ahadi ”(wagalatia…””

  Haya mambo unayoyanukuu hapo ya hao wanaotiwa muhuri, hao “watumwa” wa Mungu ni Waisraeli halisi wa kimwili, hayo makabila 12 na hesabu yao iko wazi 12,000 kila kabila, tena Israeli ndiye Mtumishi wa Mungu na si watu wa Mataifa, wao ni Bibi Arusi, nao Israeli ndio wanaomhudumia!!! Unaona unabii wenu wa uongo unavyowadanganya mchana kweupe? Muhuri wa Mungu toka lini ukawa ni siku? Muhuri wa Mungu huu hapa, Efe 4:30, “Wala msimhuzunishe yule Roho Mtakatifu wa Mungu; ambaye kwa yeye mlitiwa muhuri hata siku ya ukombozi.” Umeuona muhuri wa Mungu? Kama Biblia inafundisha kuwa Muhuri wa Mungu ni RM, nawe unafundisha kuwa “Sabato ni Muhuri wa Mungu”, Je, utakwepaje kwamba wewe ni Mpinga Kristo? Tena kwamba unafundisha injili tofauti na hiyo waliyofundisha mitume ni kwamba utakuwa umelaaniwa!!!

  Umekazana na Torati, ni dhahiri kwamba hujui hata Kristo alifanya nini! Ndio maana mnajikoroga sana. Sabato kwa Wayahudi HAIJAISHA, wangali wanaendelea nayo hata leo hii na Sheria zake zooote, wanazitimizaje, hiyo ni issue yao haituhusu sisi Kanisa, labda ninyi Wasabato mliopoteza Identity na muelekeo, Uyahudi (Sheria) mnautaka na Ukristo (Neema) mnautaka, mko hapo mkining’inia katika JINAMIZI la dini!!!

  Julius Gidion, Mungu hachezewi ndg yangu! Ikifika saa ya kibano utakuwa peke yako kama ulivyozaliwa, hatakuwepo mwalimu wako anayekudanganya leo hii, huenda alikwisha kuuvuka mstari wa Rehema siku nyingi, angalia asije akakuvusha nawe!

  Uwe makini!

 129. Samahani ndugu zangu kwa kuwakatisha katika hilo fungu hapo juu na sasa tuendelee tuone ni nini kinachofuata;
  na Yesu mwenyewe akawaambia ”ombeni” ili kukimbia kwenu kusiwe wakati wa baridi,wala siku ya sabato”(mathayo 24;20).ndugu zangu kukimbia huko lilikuwa ni jambo la lazima wakati wa kuharibiwa kwa yerusalemu takribani miaka arobaini baadaye.hakuna ushahidi wowote ya kwamba yesu aliifuta sabato,alisema ”msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii;la sikuja kuitangua,bali kutimiliza.kwa maana, amini,nawaambia mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka ,yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka,hata yote yatimie.Basi mtu yeyote atakayeivunja amri moja katika hizi zilizo ndogo,na kuwafundisha watu hivyo,ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni…..(mathayo 5;17-19) kama mimi ninawezaje kuthubutu kuwaelimisha watu na kuwafundisha kwa kusoma maelekezo haya kudharau hata ”moja ya amri hizi” za MUNGU ,kama vile amri ya sabato?Yesu alitimiliza sabato kwa kuiadhimisha kabisa na kwa ukamilifu.na maisha yake yote ni ”kielelezo” kwetu (yohana13;15),kwani anatuita ”tushinde kama yeye alivyoshinda”(ufunuo 3;21)

  Na wengine wanasema kwamba Yesu aliifuta sabato alipokufa msalabani.lakini hilo hasa ndilo alilosema kwamba hakuja kulifanya !na hakusema lolote kuhusu kutangua sabato .kwa nini wanafunzi wake waaminifu waliendelea kuiadhimisha baada ya kusulubiwa kwake ? tunasoma ”Na siku ile (siku aliyosulubiwa) ilikuwa ni siku ya maandalio(tunaiita ijumaa kuu),na sabato ikaanza kuingia na wale wanawake ……wakaliona kaburi ,na jinsi mwili wake ulivyowekwa.wakarudi ,wakafanya tayari manukato na marhamu.na siku ya sabato waliistarehe kama ilivyoamriwa ”(luka 23;54-56)

  kwa kweli wanafunzi wake tunaona ya kuwa waliendea kushika sabato hata baada ya hapo.Paulo alinena kwa niaba yao wote wakati aliposema ,”je,twaibatilisha sheria kwa imani hiyo?hasha! kinyume cha hayo twaithibitisha sheria ”(warumi 3;31)
  pia tunaona mitume wakiishika sabato pamoja na waongofu wa mataifa (matendo 13;44) ,wakihubiri na kuwabatiza waongofu wa kwanza wa ukristo katika ulaya siku ya sabato (matendo 16;10-15)na je,si jambo la ajabu kwamba baadhi ya watu wa ulaya watahubiri na kuandika vitabu kinyume cha ukweli na huku mwongofu wa kwanza wa ukristo katika ulaya alipatikana siku ya sabato? kitabu cha matendo ya mitume kinataja siku za zaidi ya sabato 84 ambazo mitume walizishika (linganisha na matendo 18;4,11).

  NA TENA NGOJA TUANGALIE NI ”SIKU IPI NI SIKU YA SABA” YA ASILI

  Zipo njia kadhaa ambazo tunaweza kuzitumia kujua hakika kuwa siku ya saba ni ipi.
  1; Historia inathibitisha ya kuwa hakujawahi kuwa na badiliko katika mzunguko wa juma wa siku saba .ingawa kalenda ya Julian ilirekebishwa kuwa kalenda ya Gregory mnamo mwaka 1582k.k ,na hakukuwa na mabadiliko katika siku juma .Alhamisi ya tarehe 4 oktoba ,ilifuatiwa na ijumaa ,oktoba 15.

  2; wayahudi wameendelea kuishika sabato ya siku ya saba kwa maelfu ya miaka,bila ya ya kuipoteza ..

  3; Warumi wamekuwa wakiishika jumapili kama siku ya kwanza ya juma tangu karne ya tatu baada ya kristo. kama mtu anaweza kuipata siku halali ya kwanza ya juma ,haiwezi kuwa vigumu kuhesabu kuanzia hapo na kuipata siku ya saba .

  4; kwa njia ya sayansi ya mahesabu ,wanajimu wanaweza kutabiri tukio la kupatwa kwa jua au mwezi miaka mingi kabla .wanaweza pia kutambua tarehe ya kupatwa kwa jua au mwezi ya miaka maelfu iliyopita .na wanatambua kuwa hakuna wakati uliowahi kupotea.

  5; kama tutasoma biblia zetu,tutaona siku gani ni siku ya sabato leo ”kulingana na amri”.Mamilioni ya wakristo wanaadhimisha ”ijumaa kuu” kama siku ambayo kristo alisulubiwa,kwa sababu kusulubiwa kwake kulikuwa ”siku ya maandalio na sabato ikaanza kuingia ” .na pia wanaadhimisha jumapili kuwa kama siku ya kufufuka kwake ,”siku ya kwanza ya juma ” sasa katikati ya ijumaa na jumapili tunapata siku ambayo biblia inaiita sabato ”kama ilivyoamriwa (angalia luka 23;54-56 na 24;1) .Ni ile siku ambayo tunaiita jumamosi .Na Biblia ya habari njema inaliweka wazi jambo hili ;”Yoseph…..mwenyeji wa kijiji……kiitwacho arimathaya ……akaushusha mwili huo kutoka msalabani ,akauzungushia sanda ya kitani ,akauweka katika kaburi lililokuwa limechongwa kwenye mwamba ,ambalo halikuwa limetuka .na siku hiyo ilikuwa ni ijumaa ,na maandalio ya siku ya sabato yalikuwa yanaanza …na siku ya sabato walipumzika kama ilivyokuwa desturi .jumapili,alfajili na mapema ,wale wanawake walikwenda kaburini wakichukua yale manukato waliyoyatayarisha.Walikuta lile jiwe limeviringishwa mbali na kaburi(luka 23;50-56;24;1,2)

  TENA TUANGALIE MAANA HALISI YA SABATO NI NINI

  Wote ambao wanampenda Yesu kama mwokozi wao kutoka dhambini watajifunza pia kuipenda siku yake ya sabato ,sabato imefungamanishwa kwa karibu sana na injili ya neema ya kristo. na haiwezekani kabisa kuiamini ”injili ya milele” pasipo kuipokea na kuishika sabato ya kweli ya Bwana .na zipo sababu kama saba kwa jambo hili..
  1; sabato ni ishara ya nguvu ya mungu ya uumbaji ”maana, kwa siku sita Bwana alifanya mbingu na nchi,na bahari …kwa hiyo bwana akaibarikia siku ya sabato akaitakasa ”(kutoka 20;11) wakati dhambi ilipoingia ulimwenguni,nguvu mpya ya uumbaji ilipaswa kudhihirishwa ; ”kwa maana mmeokolewa kwa neema ,kwa njia ya imani ….maana tu kazi yake ,tuliumbwa katika kristo yesu,tutende matendo mema….”(waefeso 2;8,10) ”Hata imekuwa,mtu akiwa ndani ya kristo amekuwa kuimbe kipya ”(2wakorintho 5;17) ”Eee MUNGU,Uniumbie moyo safi”(zaburi 51;10) wokovu katika kristo ni urejeshwaji tena wa yote yaliyopotezwa kutokana na dhambi .na ni ukamilishaji wa kusudi la awali la kristo katika uumbaji.kwa hiyo sabato ni ishara ya mambo mawili -uumbaji wa mwanzo,na pia ya ”kuzaliwa kwetu upya” .Bwana anasema ,”tena naliwapa sabato zangu,ziwe ishara kati ya mimi na wao ,wapate kujua ya kuwa mimi ,Bwana,ndimi niwatakasaye ”(ezekieli 20;12,20)
  2; sabato ni ishara ya pumziko kutoka dhambini,ndani ya kristo .”Basi imesalia raha ya sabato (pumziko)kwa watu wa MUNGU kwa maana yeye aliyeingia katika raha yake amestarehe mwenyewe katika kazi yake ,kama vile MUNGU alivyostarehe .Basi na tufanye bidii kuingia katika raha ile ….”(waebrania 4;9-11). Yesu anasihi,”njooni kwangu …..nami nitawapumzisha ”(mathayo 11;28).ni kwa njia ya mibaraka ya ushikaji wa kweli wa sabato ambayo Bwana ametupatia ”pumziko” hilo

  3; furaha mpya na shangwe huujaza moyo wa mtu anayeishika sabato.na katika biblia tunasoma hivi ”wimbo kwa ajili ya siku ya sabato ”, ”kwa kuwa umenifurahisha ,bwana ,……kwa ajili ya matendo ya mikono yako .na mtu mjinga hayatambui hayo ,na wala mpumbavu hayafahamu”(zaburi 92;4,6) ”matendo ya mikono yako ”ni mara mbili ;uumbaji wa awali,na kuumbwa kwetu upya katika kristo kama mwokozi .Na bwana pia ”anafurahi” ;Bwana ,MUNGU wako ,yu katikati yako shujaa awezaye kuokoa;atakushangilia kwa furaha iliyo kuu ,atatulia katika upendo wake .na atakufurahia kwa kuimba ”(sefania 3;17) ,ushikaji wa kweli wa sabato ni ”umoja na kristo” ,kwani bado ”anastarehe ” na kuimba kwa furaha wakati anapoona watu wake ”wakiingia katika raha yake”
  Hebu fikiria kwenda kanisani pamoja na MUNGU na kumsikia yeye akiimba !
  ”kutakuwa na furaha mbinguni kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye”(luka 15;7)

  4; sabato huleta mibaraka .”Bwana akaibarikia siku ya sabato na akaitakasa ”(kutoka 20;11) na hebu angalia jinsi sabato inavyokwenda pamoja na kristo ;”Atukuzwe mungu ,Baba wa Bwana wetu yesu kristo ,aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni ,katika ulimwengu wa roho ndani yake kristo (waefeso 1;3) kwa hiyo ,tunapopokea mibaraka ya kiroho kupitia sabato ,kristo ndiye chimbuko halisi .
  Sabato ni mfereji ambao kwao mibaraka ya kiroho hububujika kutoka kwa kristo kwenda kwa watu wake ambao ni sisi sote ni kama mto unaoburudisha unapokuwa unatiririka kupitia katika jangwa kame…

  Ni siku ya furaha,na ni siku ya nuru;
  Nasi twaona raha,kuja kushukuru;
  Leo watu wa mungu,wadogo wakubwa,
  Hukaribia mbingu,lilipo baraka;
  5; pumziko la sabato huleta uwepo wa kristo.Bwana akamwambia musa ,”uso wangu utakwenda pamoja nawe,nami nitakupa raha ”(kutoka 33;14) ,Haiwezekani kwa yeyote kati yetu ”aliyechoka na kuelemewa na mizigo ”kupata raha hiyo isipokuwa katika uwepo wa mwokozi ;

  6; Uwepo wa kristo hutakasa.”bali kwa yeye MUNGU ,na haki,na utakatifu,na ukombozi”(1 wakorintho 1;30) .Yesu alimwambia paulo,”wapate msamaha wa dhambi zao na urithi miongoni mwao waliotakaswa kwa imani iliyo kwangu mimi”(matendo 26;18) na ndipo watu wake watakapokuwa tayari kwa ajili ya kurudi kwake ;”MUNGU wa amani mwenyewe awatakase kabisa ;nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe mwe kamili ,bila lawama ,wakati wa kuja kwake Bwana wetu yesu kristo”(1 wathesalonike 5;23) kisha sheria ya MUNGU itashuhudia kazi kamilifu ya haki ya kristo itayodhihirishwa ndani ya waaminio;

  7; Sabato ni ”muhuri wa MUNGU”

  ”nikaona malaika mwingine ,akipanda kutoka maawio ya jua ,mwenye muhuri ya mungu aliye hai ;akawapigia kelele kwa sauti kuu wale malaika wanne waliopewa kuidhuru nchi na bahari ,akisema ,msiidhuru nchi ,wala bahari ,wala miti,hata tutakapokwisha kuwatia muhuri watumwa wa mungu wetu juu ya vipaji vya nyuso zao,nikasikia hesabu yao waliotiwa muhuri katika kila kabila ya waisraeli ,watu mia na arobaini na nne elfu (ufunuo 7;2-4)na neno ”israeli” linamaanisha wale wanaomwamini kristo kwa kweli ;yeye ni myahudi aliye myahudi kwa ndani; na na tohara ni ya moyo ,katika roho na si katika andiko ”(warumi 2;29) ”Na kama ninyi ni wa kristo ,basi mmekuwa uzao wa ibrahimu ,na warithi sawasawa na ahadi ”(wagalatia 3;29) Wakati elimu ya kristo inapoteka akili yote ,kiasi kwamba ahadi yake aliyoisema ”Mpende bwana MUNGU wako kwa moyo wako wote ,na kwa roho yako yote na kwa akili zako zote”(mathayo 22;37) inatimia ,na ndipo muhuri wa mungu unapoweza kuwekwa juu yetu na hapo ndipo ”siri ya MUNGU itakapotimizwa ”, ”nayo ni kristo ndani yenu ,tumaini la utukufu” (ufunuo 10;7;wakolosai 1;27) ”yeye ashindaye ,nitamfanya kuwa nguzo katika hekalu la MUNGU wangu ,na wala hatatoka humo tena kabisa ,nami nitaandika juu yake jina la MUNGU wangu”(ufunuo 3;12) ”ishara au muhuri ”wa hiyo kazi iliyotimilizwa ni sabato (ezekieli 20;12,20) ”kama ukiigeuza mguu wako isiihalifu sabato,….na ukiita sabato siku ya furaha ….ndipo utapojifurahisha katika Bwana (isaya 58;13,14) Watu wengi wanatumia muda mwingi na fedha nyingi wakitafuta furaha .hii hapa bure ! lakini kama sabato ni muhuri wa mungu ,ishara ya wokovu katika kristo ,ni kwa nini wakristo wengi hawaijali na badala yake wanashika jumapili?hili ni swali muhimu sana ambalo hatuna budi kulizungumzia,wakati ujao. kwa hiyo mbarikiwe ninyi nyote katika kristo Bwana wetu, AMINA

 130. Napenda kuwasalimu tena ndugu zangu kwa jina la bwana hamjambo!na hebu tuendelee na mada yetu na kabla ya kuendelea napenda kuwashauri wenzangu ambao wako tu kwenye huu mjadala kwa kubisha tu na hawafatilii kile ambacho kinaongelewa humu wenyewe ni kubisha hawana ukweli wowote kutoka kwenye biblia na wamejawa na roho za kutosikia na kuelewa kama neno la MUNGU linavyosema (yeye aligeuzaye sikio lake asiisikie sheria ya MUNGU,hata sala yake ni chukizo )mithali 28;9.
  2; Akaibariki siku ya saba .neno kubaliki lina maana kufurahisha .”pumziko” kutoka dhambini na katika ubinafsi ndio msingi pekee ndio msingi pekee wa furaha .”MUNGU akiisha kumfufua mwana wake, alimtuma kwenu ninyi kwanza,ili kuwabalikikwa kumwepusha kila mmoja wenu na maovu yake ”matendo 3;26)na furaha safi na ya kweli ambayo mtu anaweza kuwa nayo imefungamanishwa na siku ya bwana ,yaani sabato.
  3;akaitakasa;neno ”kutakasa” kitu ni kukitenga kwa matumizi maalum.na neno hilo hutumika kuelezea kuweka wakfu makuhani,hema pamoja na vyombo vyake vyote vitakatifu (angalia mambo ya walawi 8;10,11,12,15,30) hema pamoja na vyombo vitakatifu havikufichwa mbali kwenye jumba la makumbusho bali kutumiwa daima na hiyo ndoo maana ya ”kutakasa”kwa hiyo ni wazi kwamba Bwana hakuificha sabato yake takatifu mbali na watu kwa miaka maelfu,kama ambavyo wengine wamekuwa wakidai katika juhudi zao za kuikataa .wakati ”alipoitakasa” akampa mwanadamu kama zawadi ya thamani .na alikusudia sisi sote tuishike sabato na kuifurahia.watu wengine watatuambia kuwa sabato ilifanyika kwa ajili ya wayahudi tu. la,”sabato ilifanyika kwa ajili ya mwanadamu (marko 2;27) na sabato ni mbaraka uliokusudiwa kwa ulimwengu wote!

  HEBU TWENDE KATIKA HISTORIA JE SABATO IMEWAHI KUSAHAULIKA?
  Tangu siku za adamu na hawa hadi leo ,siku zote MUNGU amekuwa na watu waaminifu ”waliosalia”wanaoikumbuka ”sabato na kuitakasa ”.na jambo la kwanza walilofanya adamu na hawa lilikuwa ni kushika sabato,kwa sababu waliumbwa ijumaa ,siku ya sita .na maandiko yanatuambia kuwa inaanza ijumaa jioni,jua linapozama(angalia hesabu 23;32 na marko 1;32) na fikiria furaha waliokuwa nayo Adamu na Hawa kwa mara ya kwanza katika bustani ya edeni na mibaraka miwili ya thamani imetufikia kutoka katika mazingira yale matakatifu ya edeni ,yasiyo na dhambi;ndoa takatifu, na sabato takatifu na vyote viwili vinaendelea kuwa mbaraka kwetu sisi wanadamu (Na tunaweza kuona kwa urahisi kuwa vyote ni vitu ambavyo shetani anavichukia sana na anavyotafuta kuviharibu ulimwenguni kote)
  Wana wa waisraeli waliotoka misri waliijua sabato kabla ya amri kumi kutangazwa katika hali ya utukufu mlimani Sinai, kule jangwani,Bwana aliwajaribu waisraeli juu ya kuishika sabato ,”nipate kuwajaribu ,kwamba katika sheria yangu,ama sivyo”(kutoka 16;4)na kila siku aliwaletea mkate kutoka mbinguni ,ulioitwa ”mana ”Basi ikawa siku ya sita wakaokota kile chakula sehemu maradufu ,na kila mtu pishi mbili ,na wazee wote wa makutano wakaenda na kumwambia musa.Akawaambia ,ndilo neno alilonena Bwana ….siku sita mtaokota ;lakini siku ya saba ni sabato takatifu,na siku hiyo hakitapatikana ”(kutoka 16;22-26)na hii inaonyesha kuwa sabato haikusahaulika kwa hawa watu japo baadhi wanaweza kuwa walikuwa wazembe katika kuishika katika siku za utumwa wao kule Misri.

  Kutokana na tukio hilo tunagundua kuwa mtu yeyote anayeichukulia siku ya saba kama siku ya kawaida ya kazi haenendi ”katika sheria yangu”,kama bwana alivyosema .Wakati baadhi ya watu walipokwenda kufanya kazi siku ya sabato ,Bwana aliuliza ,”mtakataa kuyashika maagizo yangu na sheria zangu hata lini?(aya ya 27,28)na inawezekana MUNGU anakuuliza swali hili leo!
  tunaona sabato ikiwa imeelezwa pote katika agano la kale na jipya kwa mfano zaburi 92 inatajwa kama ”zaburi au wimbo kwa ajili ya siku ya sabato ”ni neno jema kumshukuru Bwana ,na kuliimbia jina lake ,ee uliye juu…….kwa kuwa umenifurahisha ,Bwana kwa kazi yako nitashangilia .”(aya 1,4)”mtafanya kazi siku sita ;lakini siku ya saba ni sabato ya kustarehe kabisa, kusanyiko takatifu;msifanye kazi ya namna yoyote ;ni sabato kwa Bwana katika makao yenu yote;(mambo ya walawi 23;3)
  ”kusanyiko takatifu” lina maana ya ”kukusanyika pamoja”.Huu ni mkutano wa kawaida kila sabato kwa ajili ya ibada na ushirika wakati watu wote wanaompenda Bwana wanapoyaacha mahangaiko yao na matatizo ya kidunia na kwenda kukusanyika mbele zake asema Bwana wa majeshi na saa hii ya ibada ni wakati wa furaha sana kuliko wakati mwingine wowote wa juma !sabato ni ”siku ya bwana ” ,anayoiita siku ya utakatifu wangu ”(isaya 58;13)na sisi sote ni wageni katika nyumba yake,kama ilivyo ,tukilishwa naye,tukiburudishwa naye,na kwa kuwa wale wote wanaoiamini injili wanakuwa ni ”mwili wa kristo”, na kujumuika kwetu pamoja siku ya sabato ni kwa furaha ,kwani ni ”ndani ya kristo”.na labda inawezekana kuna watu wanaokutana kila sabato kumwabudu Bwana,jirani na mahali ulipo nakushauri nenda ujumuike nao.

  na pia isaya anatuambia kwamba sabato sio kwa ajili ya wayahudi tu bali kwa watu wa mataifa pia,na ni kwa ajili ya watu waoishi katika siku za mwisho wakati kurudi kwa Bwana kunapokaribia.na ”Bwana asema hivi ….wokovu wangu ukaribu kuja ,na haki yangu kufunuliwa ….na wageni(watu wa mataifa),walioandamana na Bwana ili wamhudumu,na kulipenda jina la bwana,kuwa watumishi wake ;kila aishikae sabato na asiivunje ,na kulishika sana agano langu ;nitawaletea hao nao hata mlima wangu mtakatifu na kuwafurahisha katika nyumba yangu ya sala…….kwa maana nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote”(isaya 56;1,6,7)
  kwa hiyo wewe na mimi tunaalikwa na MUNGU !na je usingependa kuupokea mwaliko huu kwa furaha?
  furaha ndio neno kuu katika kuishika sabato na furaha hupatikana kwa Bwana ,amani ya moyo,na pumziko la roho na vyote ni zawadi zinazounganishwa na sabato na ifuatayo ni ahadi ya Bwana wetu”kama ukigeuza mguu wako usiihalifu sabato,usifanye anasa zako siku ya utakatifu wangu;ukiita sabato siku ya furaha na siku takatifu ya Bwana yenye heshima ;ukiitukuza,kwa kutokuzifanya njia zako mwenyewe ,wala kuyatafuta yakupendezayo wala kusema maneno yako mwenyewe,ndipo utakapojifurahisha katika Bwana ;nami nitakupandisha mahali pa nchi palipoinuka ;nitakulisha urithi wa yakobo baba yako;kwa maana kinywa cha Bwana kimenena hayo ”(isaya 58;12-14)

  na hebu tuchunguze mambo muhimu katika andiko hili;
  1;Bila kutambua watu wa MUNGU wamekuwa wakiikanyaga sabato,wakifanya anasa zao za kidunia katika siku hiyo takatifu,bila kuijali.
  2;itakuwa ni ”kumheshimu”Bwana kama tutaacha kuikanyaga sabato yake.
  3;kushika sabato ni zaidi ya kupumzika kimwili;kunajumuisha mawazo na maneno matakatifu.
  4;kama ”unaifurahia” siku ya sabato ”utajifurahisha” pia katika Bwana.
  5;na kamwe bwana hatakuacha;”atakulisha” kama unaishika sabato

  shetani atakufanya ufukiri kwamba huwezi kumudu kuishika sabato,kwamba utapoteza kazi yako kama ukifanya hivyo.lakini Bwana amekuwa mwaminifu kutimiza ahadi yake kwa kila mtu anayeliamini neno lake.na mamia kwa maelfu ya watu wanaweza kushuhudia kuwa,ingawa imani yao zilijalibiwa wakati walipojaribu kuishika sabato ya kweli,kamwe MUNGU hakumwacha hata mmoja wao !na wengi walipata kazi nzuri zaidi kuliko zile walizopoteza;na hakuna hata mmoja aliyewahi kukosa chakula kwa sababu alikuwa mwaminifu katika Bwana.Imani zao ziliimarika kwa kujifunza kumtumaini.

  NA HEBU TUANGALIE TENA KIELELEZO CHA YESU NA MITUME.

  Wakati mwana wa mungu alipofanyika mwili na kukaa kwetu,alifurahia kushika sabato na akajiunga katika ”kusanyiko takatifu”pamoja na watu wa mungu ”Akaenda nazareti,hapo alipolelewa;na siku ya ya sabato akaingia katika sinagogi(nyumba ya ibada) kama ilivyokuwa desturi yake,akasimama ili asome ”(luka 4;16) na kwa njia ya mafundisho na miujiza yake aliitukuza sabato na kuiondolea mipaka iliyokuwa imewekwa na wanadamu ambayo ilikuwa imepotosha maana yake kwa watu wa MUNGU wa zamani.Kwa sababu hakujali zile taratibu za ukandamizaji zilizokuwa zimewekwa na wanadamu,wayahudi waliomkataa Yesu walimshutumu kwa kuvunja sabato.
  lakini mashtaka hayo yalikuwa ni ya uongo,kwani alisema,”kama mimi nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake”(yohana 15;10) kwake yeye kuvunja sabato ingekuwa ni kukataa ”kuyashika maagizo yangu na sheria zangu”(kutoka16;28).na baadhi ya wakristo wanarudia mashtaka hayo ya uongo ya wayahudi,kwa kusema kuwa kristo ”aliivunja” sabato,na kwa hiyo hatupaswi kuijali.siyo tu kwamba hawako makini katika kusoma ushuhuda wa maandiko,lakini pia wanakosa kumheshimu Bwana yesu mwenyewe .kwa kutenda matendo ya uponyaji na huruma siku ya sabato ,”alivunja” tu sheria zilizokuwa zimewekwa na wanadamu yaani marabi wa kiyahudi.na alifundisha kwamba ”ni halali kutenda mema siku ya sabato ”(mathayo12;12)
  na kristo mwenyewe aliwahimiza wanafunzi wake kuikumbuka ”siku ya sabato na kuitakasa” miaka mingi hata baada ya kusulubiwa kwake ,kwani aliwaambia ”ombeni,ili kukimbia kwenu kusiwe wakati wa baridi

 131. Mr. Gidion,

  Hujasoma post zote au niseme screen ya computer ndogo ebu rudi tena. Haya uliyoeleza nikutoka rejea za wikipedia na vitabu vya hadithi. Maelezo yako hayana chochote kuhalarisha sabato ya jumamosi.

  Barikiwa

 132. Napenda sana kuwasalimu ninyi nyote katika kristo bwana wetu,nimejaribu kuzisoma coment zenu zote sana hapo juu zinazohusiana na mabishano yenu yaliyopo kati yenu,sasa ningenda tujifunze yafuatayo juu ya SABATO YA KWELI NI IJUMAA,JUMAMOSI,AU JUMAPILI? Waafrika wa leo yani sisi tunafanya kazi kwa bidii sana,huenda kuliko watu wa mataifa mengi yaliyoendelea.Hebu tembelea mji wowote mkubwa wa kiafrika toka mashariki hadi magharibi,kaskazini hadi kusini,nawe utaona mamia kwa maelfu ya watu wakiwahi kwenda kazini kila siku asubuhi.Wengi wanalazimika kutembea kwa miguu au kutumia baiskeli;wale wanaoweza kupata nafasi ya kusimama katika mabasi yaliyojaa watu mara nyingi wanalazimika kuvumilia hali hiyo kwa umbali mrefu zaidi.Na wakati masaa ya kazi yanapokwisha,kunakuwa na safari ndefu tena ya kutembea kurudi majumbani kwao,na unaporejea tena nyumbani kunakuwa tena na kazi zingine na kulala usiku ukiwa umechoka sana. Na kila mmoja atakubaliana kwamba mwanadamu wa leo anahitaji siku moja ya kupumzika ya kila juma na wanadamu wengi wa leo wengine wanachukua kuwa siku ya ijumaa kuwa ya kupumzika wengine jumapili na wapo watu zaidi ya millioni kumi na nne wanaoadhimisha jumamosi kwa uaminifu kabisa kama sabato,au siku ya Bwana ya kupumzika. Lakini jambo ambalo wengi hawalifahamu ni kwamba mwanadamu wa siku hizi anahitaji siku ya kupumzika kiroho na kimwili pia.Ni ahisi sana kutambua kuwa mwili wa mtu aliyechoka unahitaji siku moja ya kupumzika;lakini lile tusilotambua ni kuwa huwa tunasumbuka kutokana na mahangaiko na uchovu wa kiroho.Na ni hakika ya kuwa roho ya mwanadamu isiyo na pumziko la kiroho itajiangamiza yenyewe kiroho baada ya muda si mrefu .na biblia inatueleza hivyo kama ‘wafu katika makosa na dhambi'(waefeso 2:1). Na shetani amejaribu kuwanyang’anya wanadamu zawadi ya thamani ambayo mungu alitupatia yaani siku ya kupumzika ya sabato .Kwa sababu ya kugundua mafundisho ya kweli ya biblia,lakini baadhi wameanza kurejesha tena zawadi hii iliyoibiwa matokeo yake ni kwamba maisha yao yanakuwa na mibaraka tele na hakuna mtu yeyote aliye na sababu ya kuendelea kudanganywa zaidi na shetani.Kama MUNGU amekupatia zawadi ya thamani,, je hupaswi kuifurahia?na kwa nini uishi ukiombaomba wakati unaweza kuwa tajiri kwa kupokea tu kile ambacho tangu mwanzo kilikuwa ni haki yako? WAKATI NA JINSI SABATO YA KWELI ILIVYOANZA. mara ya kwanza nilivyokuwa mtoto nilijiuliza kwa nini kuna siku saba barabara katika juma.na kwa nini watu wanaanza kuhesabu siku zao wakianza na jumapili hadi jumamosi na kuanza tena upya? na kwanini tusiwe na juma lenye siku nane?au kumi?na hata hivyo kwa nini kuwe na juma? katika juma la kwanza la uumbaji MUNGU alifanya kazi kwa haraka sana katika siku ya kwanza aliumba vitu kwa kutamka hadi ya sita alipomuumba mwanadamu kwa kumfinyanga kwa udongo na akamfanya mtu kwa mfano wake (mwanzo 1:1-27) na kazi ilipokuwa imemalizika ‘MUNGU akaona kila kitu alichokifanya yeye na tazama ni chema sana. ikawa jioni na asubuhi siku ya sita. na siku ya saba MUNGU alimaliza kazi yake yote na akastarehe siku ya saba akaacha kufanya kazi yake yote (mwanzo 1:31;2:1,2).na hapa tunapata chanzo halisi cha juma ambalo kila mtu ulimwenguni analifuata hata wale wanaokana uwepo wa MUNGU!. Josephus,mwanahistoria wa kiyahudi (37-100BK) anashuhudia kuenea kwa maadhimisho ya sabato ya siku ya saba katika ulimwengu wa kale ,’Hakuna mji wowote wa kiyunani,wala wa wapagani,wala wa taifa lolote lile ambapo desturi yetu ya kupumzika siku ya saba haikufika ”(kitabu cha 2 ,par.40 works of flavius joseph,Winstoned.,uk 899) na moja ya moja ya mataifa hayo ni waashanti wa Ghana walikuwa na dhana ya MUNGU kama ”Nyame Kwame”maana yake MUNGU wa jumamosi ”na maana ya ”kwame”ni aliyezaliwa siku ya jumamosi”.na kwa vizazi vingi waashanti walitambua kuwa siku ya mungu ni jumamosi,kwamba anapaswa kuabudiwa siku hiyo na hiyo ilikuwa muda mrefu kabla mmishonari yeyote kuwasili Afrika magharibi.na walitoa kafara jumamosi na kuvaa nguo nyeupe zilizoashiria utakatifu wa MUNGU .Hawakusafiri katika siku hiyo,na hawakufanya kazi yoyote mpaka jioni na wakati wamishonari walipowasili wakifundisha kushika jumapili waliitwa ”wazungu wa jumapili” na jambo hilo hilo linapatikana pia upande wa pili wa bara hili miongoni mwa wavugusu nchini kenya imani yao ya kimapokeo imekuwa kwamba ”MUNGU alimaliza kazi yote ya uumbaji kwa siku sita na siku ya saba alipumzika kwa sababu ilikuwa siku mbaya…..Wavugusu wana imani na miiko mbalimbali inayohusu siku hiyo na namba saba”.(G.Wagner,imenukuliwa katika D.Ford,African worlds,oxford,1954,uk.28) na inaelekea kabisa kwamba desturi ya uumbaji wa siku saba ilishikiliwa na watu wa Afrika miaka mingi iliyopita,na hawa wanaopatikana magharibi na mashariki ni mifano tu. KWA NINI MUNGU ALIPUNZIKA SIKU YA SABA? Bwana MUNGU alipomaliza kazi yake,hakuwa amechoka kama sisi tunavyochoka baada ya kazi ngumu za juma zima ”je wewe hukujua?hukusikia?yeye MUNGU wa milele,BWANA muumba miiisho ya dunia,hazimii,wala hachoki;na akili zake hazichunguziki”(isaya 40;28) na ipo sababu nyingine iliyomfanya apumzike,na haikuwa tu kama mfano kwetu sisi tunaochoka kirahisi. MUNGU alikuwa amefanya jambo ambalo hakuwa amewahi kulifanya hapo kabla alikuwa amemuumba mtu kwa ”mfano wake” akiwa na uhuru kamili wa kuamua kumpenda kwa uaminifu na kumwasi na kumchukia na hatimaye kumwua mwanaye.kuumbwa kwa ”mfano wa mungu”haimanishi katika mwonekano wa kimwili.ina maana ya akiwa na uwezo wa uhuru kamili wa fikra na maamuzi na MUNGU asingeweza kufurahia kumaliza kazi yake ya uumbaji kama asingempatia mwanadamu uhuru huo kamili lakini pamoja na uhuru huo ,MUNGU alijua kuwa msalaba ungeweza kumsibu !na MUNGU alipomaliza kazi yake siku sita na ya saba akapumzika na wakati Adamu na Hawa walipomtenda dhambi ,uvuli wa msalaba uliinuka juu ya bustani ya edeni na kristo akawa ni mwanakondoo aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia hii (ufunuo 13;8) na sabato ni ishara halisi ya msalaba huo,na ilikuwa ni siku gani ya juma walipompigilia yesu juu ya ule mti ,wakati alipotamka yale maneno ya ushindi ,”Imekwisha”? siku ile ilikuwa ni siku ya sita ya juma ambayo tunaiita ijumaa,siku ya juma ambayo MUNGU alimaliza kazi yake ya awali ya uumbaji.na ilikuwa ni siku gani ambayo yesu alipumzika kaburini baada ya kumaliza kazi yake ya ukombozi?ilikuwa ni siku ya sabato,siku ileile ya saba ambayo katika hiyo MUNGU alipumzika hapo mwanzo. Na mwana wa MUNGU aliyekufa pale msalabani alikuwa ndiye muumbaji wetu na dunia kwa ujumla”Hapo mwanzo kulikuwako neno naye neno alikuwako kwa mungu naye neno alikuwa mungu na vyote vilifanyika kwake”(yohana 1;1-3)labda unaweza kujiuliza Neno ni nani?naye neno alifanyika mwili na akakaa kwetu nasi tukaona utukufu wake utukufu kama wa mwana pekee atokaye kwa BABA;amejaa neema na kweli(aya ya 14) Yesu ni mfano wa MUNGU asiyeonekana na mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote na katika yeye vitu vyote viliumbwa kwa ajili yake(wakolosai 1;15-17) hii ina maana ya kwamba kwa kuwa ulimwengu wote uliumbwa na kristo, sabato ya siku ya saba nayo ilifanywa na yeye.na kama ambavyo vitu vyote viliumbwa hapo mwanzo vilikuwa ni kwa ajili ya mwanadamu”vivyo hivyo Yesu mwenyewe anasema,”sabato ilifanyika kwa ajili ya wanadamu ambao ni sisi sote(marko 2;27)na MUNGU akaibarikia siku ya saba na kuitakasa (mwanzo 2;3) hiyo ndio sababu watu wamekuwa wakiishika sabato tangu hapo mwanzo wa ulimwengu na baada ya kusahau utakatifu wa sabato,bato waliendelea kufuata juma lenye siku saba!na ni rahisi kuelewa kwa nini tuna mwezi?huu ni muda unaofuata mzunguko wa mwezi na neno mwezi linadhihirisha ukweli huo;kadhalika mwaka ni kipindi kinachotokana na jua na majira mbalimbali ya mwaka.lakini hakuna kiumbe chochote cha asili kinachogawanya muda katika majuma ya siku saba na ni nani aliyeanzisha juma? yakupasa kuchunguza kila ensaiklopidia au kitabu cha historia katika kila maktaba kubwa duniani.na utagundua kuwa hakuna mwanasayansi au mwanahistoria yeyote anayeweza kukupatia jibu la swali hili isipokuwa lile unalolipata kutoka kwenye biblia takatifu ;MUNGU aliumba dunia hii kwa siku sita na akapumzika siku ya saba na tangu zamani watu wameujua ukweli huu. na juma la siku saba liliadhimishwa kule Hindustan,na wabara-hamani wa india na warabu na watu wa china ,miongoni mwa wayunani na warumi na wamisri na hata miongoni mwa wasaxon,wapagani wa kale wa ulaya kaskazini -watu ambao hawakujulikana na waebrania.na saba ilikuwa ni namba iliyoheshimiwa katika mataifa hayo. Hesiod (900k.k),mshairi mpagani wa kiyunani ,aliitangaza siku ya saba kuwa ni takatifu ,kama walivyofanya Homer na callimachus,waliokuwa wandishi wa kale wa kiyunani.Dalili za juma zimepatikana pia miongoni mwa wahindiwa kale wa bara la Amerika ya kaskazini na chimbuko la juma limelezwa wazi katika amri kumi;kwamba uikumbuke siku ya sabato na uitase…………(kutoka 20;8-11) tafadhali angalia mambo matatu aliyoyafanya kristo hapo mwanzo; 1;alipumzika; Na kwa kuwa ”sabato ilifanyika kwa ajili ya mwanadamu” anakusudia kwamba mwanadamu aweze kuifurahia hiyo siku na Yesu mwenyewe anasema ”njooni kwangu ninyi nyote mnaosumbuka na kuelemewa na mizigo nami nitawapumzisha”(mathayo 11;28) je hili ni pumziko la namna gani?”basi imesalia raha ya sabato kwa watu wa MUNGU .kwa maana yeye aliyeingia katika raha yake amestarehe mwenyewe katika kazi yake,kama vile MUNGU alivyostarehe katika kazi yake ”(waebrania 4;9,10) ”na kazi zetu wenyewe ni kazi za dhambi,ubinafsi.kiburi,mashaka na hofu. jamani tutaendelea tuone ni nini kinachofuata asanteni.

 133. Siyi ndugu yangu, mbona ghafla pozi yote ya utakatifu wa Kisabato imekukimbia! Mbona unaniunganisha katika mambo mengi ambayo siyajui, mara sijui Mathew mara niliikubali sabato, vipi kaka, unga wa ndele umekufurikia?

  Sabato nimekuambia zaidi ya mara 10, kuwa hilo ni Agano la Israeli, ninyi watu wa Mataifa mmejipachika tu katika jambo ambalo si lenu! Nimekuambia mara nyingi sana kuwa changamsha akili yako usiishie katika ushabiki wa jambo ambalo halina tija! Tena nimewahi kukuambia pia kuwa katika kujichanganya kwenu mmeuvamia unabii wa kitabu cha Danieli unaowahusu Israeli mkajivika ninyi, na sasa unawapeleka mbali zaidi na Injili huko gizani, maana ninyi si Israeli, kwahiyo hakuna litakalowatimilia! Jaribu kuyarejea mafundisho yenu kwa taratibu unaweza kuona jinsi ambavyo Israeli isivyoonekana katika mafundisho hayo, kwenu ni taifa lililotoweka!! Lakini Mungu aliahidi kuwarejesha, nao kuwa tena taifa kama unavyouona unabii huo mlioukosa ukiwatimilia Israeli, ukiwaacha katika aibu ya unabii wa uongo mnaoushikilia mpaka leo mkijitoa ufahamu kuficha kuanguka kwenu!

  Hebu uangalie unabii huu katika Hos 6:1 uliotolewa yapata miaka 700/800 kabla kuzaliwa kwa Kristo :
  “Njoni, tumrudie BWANA; maana yeye amerarua, na yeye atatuponya; yeye amepiga, na yeye atatufunga jeraha zetu. Baada ya siku mbili atatufufua; siku ya tatu atatuinua, nasi tutaishi mbele zake. Nasi na tujue, naam, tukaendelee kumjua BWANA; kutokea kwake ni yakini kama asubuhi; naye atatujilia kama mvua, kama mvua ya vuli iinyweshayo nchi.”

  Haya ichukue miaka hiyo 700 uijumlishe na na miaka 1947 ( hapo Israeli ilipozaliwa upya) utapata jumla ya karibu miaka 2647. Haya siku moja ya Mungu ni miaka 1000, ndipo siku hiyo ya kuzaliwa upya Israeli, huo mwaka 1947, ingekuwa ni katika siku ile ya Tatu kama utabiri unavyosema! Endelea tena hapa uuone unabii mwingine unaowahusu, Eze 37:21-22:
  “Ukawaambie, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, nitawatwaa wana wa Israeli toka kati ya mataifa walikokwenda, nami nitawakusanya pande zote, na kuwaleta katika nchi yao wenyewe; nami nitawafanya kuwa taifa moja katika nchi hiyo, juu ya milima ya Israeli; na mfalme mmoja atakuwa mfalme wao wote; wala hawatakuwa tena mataifa mawili, wala hawatagawanyikana kuwa falme mbili tena, hata milele.”

  Taifa la Israeli hilo hapo Siyi, huo ndio muujiza wa Injili ambao dunia nzima imeushuhudia, Mungu akijitukuza kupitia watu wake, akiukamilisha unabii, kinyume na roho zisizoamini ambazo zilijiridhisha kuwa Israeli haitakuwepo tena na hivyo kujipachika nafasi yake, ule “unga wa ndele!”

  Pia Siyi, Sheria inajumuisha pamoja na hizo Amri Kumi, zoote, huo uongo mwingine mnaojidanganya, sijui Sheria za Maadili nk unaonesha ni jinsi gani ufahamu wenu umefungwa kwa mafundisho yenu potofu. Vyovyote utakavyojiridhisha, hakuna namna ambayo utaugeuza ukweli wa Maandiko zaidi ya kujiongezea mapigo. Sheria yote kama Maandiko yanavyoifundisha, iliishia kwa Kristo. Kristo ndiye Mwisho wa Sheria kwa mkristo aliyejazwa Roho Mtakatifu. Lakini ninyi ambao bado mko katika mambo ya dini, mkiongozwa na hizo roho za dini, mambo haya ya Rohoni kwenu ninyi si rahisi kueleweka! Hakuna Sheria isiyo na Msimamizi. Naye Msimamizi wa Sheria hiyo anapojiondoa katika usimamizi huo, Sheria hiyo hukoma Nguvu yake! Nalo kundi lililokuwa likiongozwa kwa Sheria hiyo husubiri Maelekezo Mapya kutoka kwa huyo aliyemsimika huyo Msimamizi ambaye sasa anajiondoa kwa HIARI yake kulingana na DISPENSATION yake kumalizika!

  Haya Siyi angalia jinsi ambavyo Msimamizi wa Sheria unayoing’ang’ania, huyo Kuhani Mkuu, alivyojivua Ukuhani:
  “Ndipo Kuhani Mkuu akararua mavazi yake, akisema, Amekufuru; mna haja gani tena ya mashahidi? Tazameni, sasa mmesikia hiyo kufuru yake” (MT. 26:65)

  Nayo Sheria ya Ukuhani inasema hivi:
  “Na yeye aliye kuhani mkuu katika nduguze, ambaye mafuta ya kutiwa yamemiminwa kichwani mwake, naye akawekwa wakfu ili ayavae hayo mavazi, yeye hataziacha wazi nywele za kichwa chake, wala hatazirarua nguo zake” (LAW. 21:10)

  Hapa ndipo Sheria na Torati yake vinapokomea KIROHO! Hao hapo, Kuhani Mkuu akirirarua vazi lake mbele ya Kristo aliye Mwana wa Mungu, unafiki umemuongoza kumkiri Kristo na kuuvua Ukuhani alioushikilia kwa Sheria iliyo Halali na sasa akilazimika kuuvua maana huyo aliye zaidi ya huo Ukuhani amefika! Isingewezekana akaendelea katika Ukuhani ilhali KUHANI mwenyewe amekwisha kuja!
  HAPA NDIO MWISHO WA SHERIA!!!!!!!!!

  Kuhusu miungu ndg yangu, iko mingi sana duniani! Hata hii mitatu ya Kirumi mnayoiabudu, hii inayowakataza kuliamini Neno la Mungu, unaponiuliza mimi majina yao, huku wewe mwenyewe unayo majina yao, mungu baba, mungu mwana na mungu roho mtakatifu au kwa jina lao moja TRINITY, inashangaza sana unavyojizubaisha! Huu hapa ukiri wako kuhusu hiyo miungu yenu iliyo katika umoja:
  “”The most difficult thing about the Christian concept of the Trinity is that there is no way to perfectly and completely understand it. The Trinity is a concept that is impossible for any human being to fully understand, let alone explain.”
  Kwa tafsiri nyepesi, unaweza kunisahihisha iwapo nimekosea, kifungu hiki kina eleza hivi kuhusu UTATU:
  “”Jambo ambalo ni gumu sana kulingana na dhana ya kikristo ihusuyo Utatu ni kwamba hakuna namna ambayo kwayo waweza kulielewa jambo hili katika ukamilifu wake. Utatu ni dhana ambayo haiwezekani kueleweka kikamilifu na binadamu yeyote yule, achilia mbali kuielezea.””

  Hiyo ndiyo miungu yenu mitatu ambayo kwa hekima yake imewazuieni msiitafakari bali muisujudie tu kichwa kichwa!! Bado nawapeni pole kwa miungu hiyo ya kirumi iliyojibanza ktk aya za Biblia!!

  Waeleze na akina Kisika, Gidioni na wengine, wanatwanga maji kwenye kinu, kwa Sheria mmeirudia Laana, huko mlikotolewa, 2Petro 2:22, “Lakini imetukia kwao sawasawa na ile mithali ya kweli, Mbwa ameyarudia matapiko yake mwenyewe, na nguruwe aliyeoshwa amerudi kugaa-gaa matopeni.”

  Bwana atusaidie!

 134. Napenda sana kuwashukuru wale wote ambao mnaendelea kuieneza ile kweli kama ilivyo katika biblia na kuongozwa na roho mtakatifu ili waweze kuwaleta kondoo wote waliopotea kutoka gizani kuja nuruni na MUNGU aweze kuwabariki,na katu msikatishwe tamaa na watu wachache ambao shetani huwatumia ili kulidhoofisha neno la MUNGU kwa tafsiri zao zisizo na maana yoyote na ambao roho mtakatifu hayuko pamoja nao,na kwa hao ambao wanalipinga siku ya kiama watakunywa mvinyo wa gadhabu ya MUNGU isiyochanganywa na maji,na hakuna mwanadamu yeyote ambaye ana uwezo wa kuyapinga maandiko matakatifu ya MUNGU na katika mjadala huu yanini kutoleana matusi?yatupasa kujibu kwa hekima na sio kutoleana matusi na kama mtu hataki kuilewa sabato ya mwenyezi MUNGU aliyoiweka na kuitakasa msimrazimishe kuilewa inaonekana roho mtakatifu hayupo pamoja naye hata umuelimishe kuhusu kitu chochote kuhusu sabato hawezi kuielewa atazidi tu kukufuru na kupata laana bure na inaonekana hao ni manabii wa uongo ambao wanatumia tafsiri zao wenyewe ili kupotosha watu, kwa hivyo basi ‘na waenende kwa sheria na ushuhuda na kama hawasemi kulingana na neno hilo kwao hapana asubuhi’isaya 8:20.na BWANA AZIDI KUWABALIKI amen.

 135. ck lwembe kwa kweli unajitahidi kujibu maswali lakini, unachokisema ukichunguza kwa umakini utagundua kuwa sheria ni sehemu ya mkristo.

  1. umesema
  “Rum 3:20 “…kwa maana kutambua dhambi huja kwa njia ya sheria.” unakubaliana na mimi kuwa pasipo sheria hakuna dhambi, na ili kujua kuwa kuna dhambi au huyu mtu ni mdhambi ni lazima uiangalie sheria ndiyo itakwambia/itakuonyesha.

  sasa basi kama sheria inaonyesha dhambi na pasipo sheria hakuna dhambi hivyo basi kila asiye na dhambi hajaivunja sheria na aliye na dhambi ameivunja sheria. kwa hiyo sheria ni ya muhimu sana kwa kila aitwae mkristo.

  Mr lwembe.
  kila anayeivunja sheria anaitwa mdhambi, na ili huyu mdhambi kujua kuwa yeye ni mdhambi anapoiangalia tu sheria, inamuonesha kuwa yeye ni mdhambi, sikia lakini sheria hiyo hiyo haina uweza wa kuiondoa dhambi, ndipo huyu mdhambi sasa anamuhitaji KRISTO ili kristo apate kuiondoa dhambi yake.

  huyu mdhambi anamwendea kristo na kumwambia mimi ni mdhami, naamini YESU akimuuliza mtu huyo nani amekwambia wewe nini mdhambi, huyu mtu atajibu sheria imeniambia.

  ndipo yesu humusamehe mtu huyu na kumpa uwezo wa kushinda dhambi. baada ya hapo huyu mtu tena siyo mdhambi tena. na sheria bado iko palepale anapoingalia sheri anamshukuru YESU kwani sheria haina cha kusema juu yake. ila huyu mtu anaposema uongo, sheria inamwambia wewe ni muongo hivyo huyu mtu tena humkimbilia KRISTO ili apate kusamehewa.

  na ndiyo maana YESU alipo msamehe mtu alimwambia enenda zako na usitende dhambi tena akimaanisha sheria bado i hai ili kumshitaki/kumuonyesha kuwa ni mdhambi.

  hivyo ndugu yangu kuikataa sheria ni kinyume na maandiko.

  sheria ni moja tu UPENDO.
  SIKILIZA
  AMRI YA UPENDO IMEGAWANYIKA KATIKA SEHEMU KUU MBILI
  1. UPENDO KWA MUNGU
  2. UPENDO KWA WANADAMU

  NINI MAANA YA UPENDO KWA MUNGU?

  1. Usiwe na miungu mingine ila mimi.
  -Kama unampenda MUNGU huta kuwa na miunge wengine.

  2. Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia. 5. Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi. BWANA Mungu wako, ni Mungu wenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, 6. nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu.
  -kama unampenda MUNGU hatukuwa na sanamu na kuziabudu na kuzitumikia, utamuabudu Mungu wako tu.

  3. Usilitaje bure jina la BWANA hatamhesabiwa kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure.
  -kama unampenda Mungu huta chezea jina lake maana ni takatifu sana.

  4. Ikumbuke siku ya sabato uitakase. 9. Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; 10. lakini siku ya saba ni sabato ya BWANA, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya mlango yako. 11. Maana kwa siku sita BWANA alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo akastarehe siku ya saba; kwa hiyo BWANA akaibarikia siku ya sabato akaitakasa.
  kama unampenda Mungu atamwamini na kukubaliana naye kuwa aliumba ulimwengu kwa siku sita na siku ya saba alistarehe, aliibariki na kuitakasa nawe utafanya kama Bwana wako alivyofanya kwa kuwa unampenda.

  NINI MAANA YA UPENDO KWA WA WANADAMU

  1. Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na BWANA, Mungu wako.
  kama unampenda mzazi wako (mwanadamu) utamheshimu kabisaaa

  2. Usiue.
  kama unampenda ndugu yako huta muua.

  3. Usizini.
  -kama unampenda ndugu yako huta zini naye kabisa bali utatenda sawasawa na neno la Mungu.

  4. Usiibe.
  -kama unampenda ndugu yako huta mwibia.

  5. Usishuhudie jirani yako uongo.
  -kama unampenda ngugu yako huwezi kumsingizia/kumsemea uongo jambo lolote.

  6. Usiitamani nyumba ya jirani yako; wala mke wake, wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng’ombe wake, wala punda wake, wala cho chote alichonacho jirani yako.

  SIKIA MPENDWA.
  Yesu aliposema “Amri mpya nawapa, Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo”. (YN. 13:34)

  hakuzivunja hizo amri maana zimejengwa katika upendo.

  katika kitabu cha ufunuo 12:17 neno la BWANA.
  Joka akamkasirikia yule mwanamke(kanisa) akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia wazishikao AMRI ZA MUNGU na kuwa na USHUHUDA wa Yesu, naye akasimama juu ya mchanga wa bahari.

  wale wote wanaokataa amri za MUNGU shetani hana shida nao maana wameukataa upendo wa MUNGU.

  TAFAKARI SANA.

 136. Duuu!! Unga wa ndele huo Lwembe!!
  Biblia iko wazi sana kuhusu Sheria. Lwembe, ukiwafundisha watu kuwa sheria zilianzia mlimani Sinai, utakuwa unakosea sana. Ukiwafundisha kuwa torati kwa maana ya torati yote(yaani unajumuisha hadi sheria za maadili na zile za asili), nako umeangukia pua. Ukimwambia kuwa huioni siku ya sabato ikiwa bayana kabisa kwenye Biblia, huko nako ni kushuhudia uongo!!
  Mwambie vizuri ndg Felix, kuhusu utakatifu wa neno la Mungu, sheria za Mungu na hivyo aache mapokeo. Au hujui kuwa unabeba damu ya mtu/watu wengine juu yako kwa kuwadanganya watu?
  Mimi na wewe tulijifunzaga vizuri sana habari za sabato huko nyuma. Ukakiri kwa kinywa chako na meseji ukaleta, leo hii tena unamfundisha huyo kijana kuwa sabato huijui!! Huo ni unafiki Lwembe!!
  mwisho nakuomba unieleze utatu mtakatifu ni miungu watatu wa kirumi, miungu gani hao? Hebu wataje na utupe source ya majibu yako ili nasi tumakinike!!

 137. Alex, Sabato maana yake ni Pumziko, na si Jumamosi kama ulivyofundishwa! Siku ya saba ndiyo unayopaswa kupumzika. Sabato wanayopumzika Wayahudi ni siku ya saba kulingana na siku walivyozihesabu kutokana na utamaduni wa Wamisri waliouishi kizazi hicho kilichotoka huko kwa mkono wa Musa na si kwamba eti jangwani walipewa hesabu mpya ya siku! Ukiwa ni fanatic wa “siku”, unaweza ukatafuta kwa kiMisri siku ya saba waliiita kwa jina gani, maana nimesikia kuwa Jumamosi, hii mnayoiabudu, ni jina la mojawapo ya miungu ya Kirumi!!!

  Lakini kuhusu Kanisa kupewa siku ya kuabudu katika namna ya Agizo lililowazi, HAKUNA siku waliyopewa, si Jumamosi wala Jumapili. Pia Agano Jipya limefurika mambo ya Rohoni ambayo yanahitaji Ufunuo ili kuyadaka, ndio maana katika jambo hilo la siku, kukusanyika kwa Kanisa katika siku ya kwanza ya wiki, hiyo ambayo Mungu ameitukuza, kwa Kanisa ni kurudi kwake katika umilele, ndio maana unawaona wakikusanyika siku hiyo wakikutukuza kufufuka kwake, KWA UFUNUO! Bali kwa hawa wengine, yaani Waisraeli na makundi ya Mataifa yaliyojiunganisha nao, kama Wasabato, hao wanaendelea katika mwili, ile Torati, wakiwa hawana ufunuo kamili wa kile Mungu alichokifanya kwa Kanisa lake, maana ni vipofu, basi anayemlaumu kipofu kwa kukanyaga nyanya atakuwa ni kipofu zaidi ya huyo kipofu!

  Kwahiyo kwa kifupi, kuhusu haya makundi ya mataifa yaliyojichomekeza kwa Israeli, kiroho, sijui itakuwaje juu yao maana nafahamu kwamba Mungu ndiye aliyewapofua Israeli, akiwanyima Ufunuo ili sisi tuingie; basi hawa waliogoma kuingia katika Siku Mpya kwa hiari yao, sioni Ahadi ya Mungu kwao zaidi ya wao kuwa makapi!

  Unaujua ule wimbo wa “Usinipite Mwokozi”?ukimsikia mtu anaita usinipite, basi jua kuwa wako waliopitwa, jitahidi usiwe mmoja wa hao waliopitwa!!

  Ubarikiwe.

 138. Bado sijaona siku iliyotajwa kwani hoja za siku ya kuabudu zilizotolewa zimefuata matukio tu lakin hakuna si halisi kama sabato ilivyo tajwa na kuelekezwa kuwa ni agano la milele kati ya Mungu na watu wake…kwani hata Yesu ndiye Bwana wa Sabato.

 139. 1. NI WAPI BIBLIA INAONYESHA BADILIKO LA SABATO KUTOKA JUMAMOSI (SIKU YA SABA) KWENDA SIKU YA KWANZA YA JUMA (JUMAPILI)
  Sabato ni siku ya saba katika uumbaji, kwa hiyo suala la kubadilika kwa siku ni gumu sana, kwanza zinabadilika ili iwe nini? Labda kama unajaribu kujenga msingi wa hizo siku kubadilika kutokana na Joshua kulisimamisha jua lisizame na mwezi kutulia na hivyo siku hiyo kuwa na masaa mengi zaidi, lakini yawezekana kuwa usiku wa siku hiyo ulikuwa na masaa mafupi tu na hivyo kutokuathiri masaa ya siku! Bali kulingana na uumbaji siku zimebaki hizo saba, na kuhusu hayo majina ya hizo siku sijayaona katika Biblia kwahiyo sina nukuu yoyote ya Jumamosi wala Jumapili na wala sijui kama ndizo hizi kweli, maana majina hayo ni majina ya miungu ya Kirumi!
  Kut 35:2 “Fanyeni kazi siku sita, lakini siku ya saba itakuwa siku takatifu kwenu; ni Sabato ya kustarehe kabisa kwa BWANA” kisha fananisha na siku ya Bwana ukiwa nje ya upofu wa Utatu Mtakatifu, utaiona ni siku moja tu, hilo pumziko! Au labda nikuulize, Je, kaburini au kuzimu, kuna starehe? Basi siku ya Sabato alikuwa huko!!!
  Mdo 20:7 “Hata siku ya kwanza ya juma, tulipokuwa tumekutana ili kumega mkate, Paulo akawahutubu,”

  2. KAMA SABATO HAINA MAANA, JE KWA SASA ZIPO AMRI TISA NA SIYO KUMI TENA?
  Kwa sasa iko Amri ya 11 tu ndiyo inayofanya kazi kwa Kanisa, yaani hao waliozaliwa mara ya pili, UPENDO!
  “Amri mpya nawapa, Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo.” (YN. 13:34)
  Amri nyingine hizo 10 zilizotolewa huko jangwani, hao waliopewa hizo wangali wanaendelea nazo katika ukamilifu wake, ikiwa ni pamoja na Baraka na Laana zinazo ambatana nazo!

  3. YESU ALIPOSEMA MKINIPENDA MTAZISHIKA AMRI ZANGU ALIKUWA ANAMAANISHA NINI? AMRI TISA AU? NAOMBA MAANDIKO.
  Amri mpya nawapa, Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo. (YN. 13:34) Hii ndiyo Amri pekee inayolipasa Kanisa lake, maana yeye anatuhakikishia kuwa, “…Kristo ni mwisho wa sheria…” Rum 10:4, lakini kwa makanisa ya mwilini hayo yalipewa hizo zilizotimilizwa, unaweza kuzisoma hapo ktk Mt 5:21 na kuendelea, “Mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiue, na mtu akiua, itampasa hukumu. Bali mimi nawaambieni, …”

  4. FUNGU HILI LINA MAANA GANI YAKOBO 2:10. LIKO AGANO JIPYA MAANA KWAKO AGANO LA KALE NI LA MWILI.
  “Maana mtu awaye yote atakayeishika sheria yote, ila akajikwaa katika neno moja, amekosa juu ya yote.” (YAK. 2:10 SUV)
  Maana ya fungu hili iko kama inavyosomeka na kueleweka hivyo, ili kwamba yeyote anayeendelea katika Sheria, basi awe makini kuzitimiza zooote. Kwahiyo huwezi kujisifia kuitimiza Amri ya Nne na hizo nane nyingine ilhali unaivunja Amri ya Kwanza, Kut 20:2-3 “Mimi ni BWANA, Mungu wako, … Usiwe na miungu mingine ila mimi” kwani ninyi mna miungu mingi, nadhani mnayo miungu watatu, ile miungu ya Kirumi, inayojiwakilisha katika UTATU MTAKATIFU! Kifungu hicho ulichokinukuu kinawazungumzia waamini wa jinsi hiyo, ambao hawajaiamini Injili ili waingizwe katika Agano Jipya, kwahiyo wamebaki wanawaya waya, Agano la Kale hawamo, maana si lao, na Agano Jipya pia hawajaingia!

  5. KAMA AGANO LA KALE NI LA MWILINI NA AGANO JIPYA NI LA ROHONI, MBONA BADO MNATUMIA AGANO LA KALE KATIKA MAFUNDISHO YENU?
  Hauwezi kukamilika katika Agano Jipya bila kulipitia hilo kuukuu au Agano la Kale. Ndio maana tunaambiwa kazi ya Torati ni kutuleta kwa Kristo! Basi sisi huyarejea hayo ya mwilini ili kuyadhihirisha ya Rohoni na si katika namna ya kuyatimiza hayo!
  Gal 3:24 “Hivyo torati imekuwa kiongozi kutuleta kwa Kristo…”

  6. JE MUNGU ATATUMIA NINI KUUHUKUMU ULIMWENGU.
  Mungu anasema atatuhukumu kwa Injili ya Paulo! Rum 2:16 “…katika siku ile Mungu atakapozihukumu siri za wanadamu, sawasawa na injili yangu, kwa Kristo Yesu.”

  7. JE SHERIA, AMRIA HAZINA MAANA MBONA MNAWATENGA WAZINZI MAKANISANI MWENI.
  Wazinzi hawatengwi makanisani, bali hujitenga wao wenyewe kwa uzinzi wao! Tena ni afadhali kama kutengwa huko kungekuwa katika mamlaka ya kanisa, wangeweza kupona, lakini Neno lilikwisha kuwahukumu adhabu ya kifo, kwahiyo hauwezi kumtenga mfu! Mt 5:28 “…lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake”

  8. NIONYESHE DHAMBI PASIPO SHERIA.
  Kazi ya Sheria ni kukuonesha dhambi, Rum 3:20 “…kwa maana kutambua dhambi huja kwa njia ya sheria.” Basi, kwa Sheria tulijitambua kuwa tu wenye dhambi nayo Neema ikatunyakua kutoka katika njia ya mauti, nasi tukaipokea Injili ya Bwana Yesu Kristo, tukaiamini kama Sheria ya Neema hiyo inavyotutaka, Mk 16:16, “Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa”, nasi katika kuyatii hayo tukabatizwa kwa Jina la Bwana Yesu Kristo, na kupata Ondoleo la dhambi zetu hizo tulizozitambua kwa Sheria, ndipo vyote vikatoweshwa Sheria na Dhambi zake, nasi sasa ni viumbe vipya tuliozaliwa kwa Roho wa Mungu!

  9. MTU ANAPOOKOLEWA KWA NEEMA, HUONI AKIAACHA KUSENGENYA TAYARI AMEITII SHERIA,
  Yeyote anayeitii Sheria, Neema haijamfikia bado!

  10. BIBLIA INAPOSEMA TUNAOKOLEWA KWA NEEMA WALA SI KWA MATENDO MTU AWAYE YOTE ASIJE AKAJISIFU ANAMAANISHA MATENDO SIYO SEHEMU YA MTU ALIYEOKOKA?
  Neema hudhihirika katika matendo, wala matendo hayaghihirishi Neema! Imani bila matendo imekufa! Umeelewa Neema ndiyo huleta Imani!!!

  Mwisho unaniambia ENDELEA KUJIFUNZA MAMBO YAFUATAYO YANAVYOHUSIANA. Ninaamini ilikuwa ni typing error tu, bali ulitaka niendelee kukufundisha uhusiano wa mambo haya
  1. NEEMA
2. SHERIA/AMRI
3. REHEMA
4.UTII

  NEEMA ni Wema na Upendo Mungu Mwokozi wetu, nasi tumeipokea Neema hiyo si kwa matendo ya Sheria tuliyoyafanya hata yatustahilishe kupata Haki, lakini kwa Rehema zake. Tito 3:4-7 “Lakini wema wake Mwokozi wetu Mungu, na upendo wake kwa wanadamu, ulipofunuliwa, alituokoa; 5-si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi; bali kwa rehema yake, kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu; 6-ambaye alitumwagia kwa wingi, kwa njia ya Yesu Kristo Mwokozi wetu; 7-ili tukihesabiwa haki kwa neema yake, tupate kufanywa warithi wa uzima wa milele, kama lilivyo tumaini letu.”

  SHERIA/AMRI: Kama kanuni, basi Neema ni kinyume cha Sheria maana kwa Neema sisi hukirimiwa Haki, bali kwa Sheria Mungu hudai Haki kutoka kwetu kulingana na hizo Sheria. Rum 3:20 “kwa sababu hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki mbele zake kwa matendo ya sheria”

  REHEMA: Rum 9:15-16 “Nitamrehemu yeye nimrehemuye, nitamhurumia yeye nimhurumiaye. Basi, kama ni hivyo, si katika uwezo wa yule atakaye, wala wa yule apigaye mbio; bali wa yule arehemuye, yaani, Mungu”

  Efe 2:4-5 “Lakini Mungu, kwa kuwa ni mwingi wa rehema, kwa mapenzi yake makuu aliyotupenda; 5-hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu; alituhuisha pamoja na Kristo; yaani, tumeokolewa kwa neema.”

  Basi ni katika Rehema ndiko Neema ilikozaliwa hiyo iliyotuondoa katika kongwa la Sheria!

  UTII: “Kutii ni bora kuliko dhabihu”!
  Sauli alikataliwa na Mungu kwa kosa la Utii, “Mbona, basi, hukuitii sauti ya BWANA, bali ukazirukia nyara ukafanya yaliyo maovu machoni pa BWANA?” 1Sam 15:19 sauti ya Bwana ndiyo inayokitangulia kila kitu:
  22-23 ” Naye Samweli akasema, je! BWANA huzipenda sadaka za kuteketezwa na dhabihu Sawasawa na kuitii sauti ya BWANA?
  Angalia, kutii ni bora kuliko dhabihu, Na kusikia kuliko mafuta ya beberu.
  Kwani kuasi ni kama dhambi ya uchawi, Na ukaidi ni kama ukafiri na vinyago;
  Kwa kuwa umelikataa neno la BWANA, Yeye naye amekukataa wewe usiwe mfalme.”

  Loh, ni hasara kiasi gani kwa huyo aliyeukosa Utii! Hebu watazame hao wenye huko kusikia kuletako Utii: Mdo 19:2-5 “…akawauliza, Je! Mlipokea Roho Mtakatifu mlipoamini? Wakamjibu, La, hata kusikia kwamba kuna Roho Mtakatifu hatukusikia. Akawauliza, Basi mlibatizwa kwa ubatizo gani? Wakasema, Kwa ubatizo wa Yohana. Paulo akasema, Yohana alibatiza kwa ubatizo wa toba, akiwaambia watu wamwamini yeye atakayekuja nyuma yake, yaani, Yesu. Waliposikia haya wakabatizwa kwa jina la Bwana Yesu.” Hiki ndicho kiwango cha utii kama kinavyojidhihirisha hapo walipoipokea hiyo Sauti, na hawa ndiyo warithi wa Agano Jipya!!!

 140. Ndg CK LWEMBE
  NINAOMBA NISAIDIWE MAMBO YAFUATWA KWA UFUPI KABISA HUKU UKITUMIA NUKUU KUTOKA KATIKA BIBLIA,

  1. NI WAPI BIBLIA INAONYESHA BADILIKO LA SABATO KUTOKA JUMAMOSI (SIKU YA SABA) KWENDA SIKU YA KWANZA YA JUMA (JUMAPILI)

  2. KAMA SABATO HAINA MAANA, JE KWA SASA ZIPO AMRI TISA NA SIYO KUMI TENA?,

  3. YESU ALIPOSEMA MKINIPENDA MTAZISHIKA AMRI ZANGU ALIKUWA ANAMAANISHA NINI? AMRI TISA AU? NAOMBA MAANDIKO.

  4. FUNGU HILI LINA MAANA GANI YAKOBO 2:10. LIKO AGANO JIPYA MAANA KWAKO AGANO LA KALE NI LA MWILI.

  5. KAMA AGANO LA KALE NI LA MWILINI NA AGANO JIPYA NI LA ROHONI, MBONA BADO MNATUMIA AGANO LA KALE KATIKA MAFUNDISHO YENU?

  4. JE MUNGU ATATUMIA NINI KUUHUKUMU ULIMWENGU.

  5. JE SHERIA, AMRIA HAZINA MAANA MBONA MNAWATENGA WAZINZI MAKANISANI MWENI.

  6. NIONYESHE DHAMBI PASIPO SHERIA.

  7. MTU ANAPOOKOLEWA KWA NEEMA, HUONI AKIAACHA KUSENGENYA TAYARI AMEITII SHERIA,

  8. BIBLIA INAPOSEMA TUNAOKOLEWA KWA NEEMA WALA SI KWA MATENDO MTU AWAYE YOTE ASIJE AKAJISIFU ANAMAANISHA MATENDO SIYO SEHEMU YA MTU ALIYEOKOKA?

  MWISHO
  ENDELEA KUJIFUNZA MAMBO YAFUATAYO YANAVYOHUSIANA.

  1. NEEMA
  2. SHERIA/AMRI
  3. REHEMA
  4.UTII

  UBARIKIWE ANAPONISAIDIA. TAFADHALI NAOMBA NUKUU KWA WINGI ZIWEZE KUNISAIDIA.

 141. Mungu aweza na kweli jumapili ni siku ya kuabudiwa ila watu husema kila mtu na imani yake

 142. Unajua Matiku,
  Unapoisoma Biblia yako, jaribu kuyatafakari unayoyasoma, hata ikiwa ni aya moja, ili upate context ya jambo linalozungumziwa au maelekezo unayopewa. Maelezo yako mengi naona ni rejea za mafundisho yenu unayoyatetea na si kile Biblia inachofundisha!

  Punguza jazba, Israeli ni taifa teule, tena ni mtumishi wa Mungu. Walipotawanywa huko 70 AD na Taifa kutoweka, wengi mlidanganyika kuwa huo ndio mwisho wake, hawatakuwa taifa tena. Kwahiyo mkajiaminisha kuwa ninyi sasa ndio “Israeli” kinyume na kile Biblia inachotufundisha kuhusu nafasi tuliyokirimiwa sisi wa Mataifa. Hakuna mahali sisi tunapooneshwa kuchukua nafasi ya Israeli. Pia unapaswa kuelewa kuwa Myahudi anayeongelewa katika mafundisho ya mtume Paulo, hapo anapoujenga Msingi wa Kanisa la Mataifa, asilimia kubwa ya Myahudi huyo ni yule aliyeipokea Injili, kuhusu huyo ndiyo hakuna tofauti kati yake na wa Mataifa katika Kristo, maana hao wote ni warithi wa ile Sheria ya Kifalme!

  Lakini hao waliobaki katika Sheria (sio hizo mnazojidanganya ninyi, sijui za Maadili nk) yaani Torati yao na vyote, hao wanaendelea katika mkondo wa unabii unaowahusu, na hawa ndio wanaokuwa refered to kama WAISRAELI au WAYAHUDI kulingana na desturi na mila zao ambazo ndio hiyo Torati. Hawa ndio Taifa la Israeli. Tatizo mlilonalo kwa sehemu kubwa linatokana na waasisi wenu kujaribu kuufungua unabii uliofungwa, ule wa kitabu cha Danieli, wakaufungua nje ya wakati, kwahiyo wakaishia katika mafundisho potofu kama haya yanayoliondoa Taifa la Israeli katika Uteule na unabii, na hivyo mafundisho hayo kuwaletea upofu wa kiroho unaojidhihirisha kimwili pale mnapoichukua nafasi yake na kujitwisha nusu ya mzigo wa Torati huku ile nusu nyingine mliyoibwaga ikiwasababishia LAANA. Gal 3:10 “Kwa maana wale wote walio wa matendo ya sheria, wako chini ya laana; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu asiyedumu katika yote yaliyoandikwa katika kitabu cha torati, ayafanye.” Unaona? Kujidanganya kwako kwa kuigawa Torati hakukufanyi uikwepe Laana!

  Pia yametolewa maelezo mengi sana Matiku kuhusu Sabato na huko walikopewa hao waliokuwa watwana. Tena umeelezwa wazi kuwa kazi ya Torati ilikuwa ni kutuleta kwa Kristo. Sasa sijui umekwamia wapi katika ufahamu! Tena umefundishwa kuwa Kristo ndio MWISHO WA SHERIA, nadhani ungejaribu kwanza kutafuta kujua KRISTO ni nani, na umwisho wake wa SHERIA ni kivipi, hilo lingekusaidia saana kukuweka sawa na kuikimbia hiyo laana uliyojitwisha!

  Unaambiwa barabara hii ukiifuata itakufikisha Kigoma. Sasa ni lazima ufahamu pia kuwa ukamilifu wa barabara ili iweze kukuongoza katika safari yako ni pamoja na zile alama za barabarani zinazokuongoza kwa kukutaarifu na kukuonya, hata ikiwa ni Torati na hizo sheria zake 600+. Basi utakuwa ni mtu wa ajabu sana utakapong’ang’ana kuendelea kuitembea barabara hiyo (Torati) licha ya kwamba umekwisha fika Kigoma ambako unapaswa kuchukua maelekezo mapya, ndio maana Mungu anaisisitiza Laana hiyo katika Agano Jipya kwa ajili yenu mlioikataa Neema yake!

  Haya mambo mengine ya Katekesimu za Kikatoliki na uongo wao, naona wewe utakuwa ni mmoja wa wale wanaoutukuza sana uongo huo bila kujua. Umeuamini sana huo uongo mpaka unajaribu kutuaminisha nasi! Katoliki hawajawahi kuibadili siku ya Ibada, huo ni uongo wao tu nanyi ni sehemu ya uongo huo! Tumekuonesha wazi kuwa Biblia ndiyo inayoyashuhudia yaliyojiri katika siku za kuzaliwa kwa Kanisa, inasema wazi kuwa mitume walikutana siku ya kwanza ya juma kwa ajili ya kuumega “mkate”, Yoh 6:35 “And Jesus said unto them, I am the bread of life”. Umeelewa huo mkate walioumega ulikuwa ni nini?

  Matiku acha kulaza akili, itakugharimu nafsi yako katika jambo ambalo liko wazi sana. Hebu rudi tena katika Maandiko uyatafakari unayofundishwa na Mungu mwenyewe. Waangalie wanafunzi wa Yesu na Sabato, ilikuwaje, na utafakari walifikaje katika hatua hizo. Mt 12:1
  “Wakati ule Yesu alipita katika mashamba siku ya sabato; wanafunzi wake wakaona njaa, wakaanza kuvunja masuke, wakala.”

  Hao walikuwa ni wale watu wa Sheria, si wababaishaji kama ninyi wa leo mnaozigawa gawa sheria ili mpate unafuu wa kuigiza kuzifuata, la hasha, hawa walikuwa ni Wafarisayo, wajuzi wa Sheria. Wanafahamu fika kuwa kitendo kile kinawapasa adhabu ya kupigwa mawe mpaka wafe. Lakini wao waliivunja ile “sabato ya Kifarisayo”, si kwa kudhamiria, si kwamba wawe tofauti, HAPANA, walikuwa ndani ya SHERIA ya KIFALME kwa kuongozana na MFALME!! Wasingeweza kuzitumikia Sheria mbili, ya kitwana na ya kifalme. Sheria ya kitwana ilikuwa inafanya kazi ndani ya washitaki, lakini Sheria ya Kifalme iliwazuia kuitimiza ya kitwana kwa wafalme, maana hii ya kitwana inakomea hapo, ndio maana waliyaleta mashtaka yao kwa mfalme na si kwa makuhani wao!

  Sheria hizo mbili ndizo zinazoyatawala maisha yetu. Kiroho tumetenganishwa na sheria hizo. Ndio maana nikakuambia kuwa nakutakia Dhiki kuu yenye fanaka baada ya kukuona kuwa wewe ni subject wa Sheria ya kitwana, baada ya kuikataa ile ya Kifalme!!!

  Hata hivyo, kwa kadiri ya hicho unachotufundisha, hizo Amri Kumi, kwamba hizo tulipewa sisi kwamba nasi ni Waisraeli, mimi ningekuomba unioneshe ni wapi ulipopewa wewe mtu wa Mataifa!

  ACHENI KUJILISHA UPEPO!!!

 143. JE! WENGI WANAWEZA KUKOSEA?

  Katika Mwongozo 16 tuligundua kwamba kulionja pumziko la Sabato ni tiba muhimu kwa maisha ya siku hizi yaliyojaa msongo mwingi. Kwa kuwa Mungu anaelewa kila haja tuliyonayo , aliiweka kila siku ya saba kwa ajili ya pumziko letu la kimwili na burudiko letu la kiroho. Baada ya kuiumba dunia yetu kwa siku sita, yeye “akapumzika” katika siku ile ya saba, “akaibariki” na “kuifanya takatifu” (mwanzo 2:1-3).

  Mungu alipowapa watu wake Amri kumi, yaani, wana wa Israeli, aliiweka amri ya kuitunza Sabato ya siku ya saba katikati ya sheria yake (Amri kumi) (Kutoka 20:8-11). Kulingana na amri hiyo, Sabato ni ukumbusho wa uweza wa Mungu wa Uumbaji, ni siku ya kutulia na kutafakari juu ya uzuri na maajabu ya kazi zake alizoziumba, ni siku ya kustarehe na kumkaribisha sana Muumbaji wetu, siku ya kuchunguza kwa kina zaidi uhusiano wetu na yeye.

  Katika kipindi kile cha maisha ya kibinadamu ya Yesu aliyoishi hapa duniani, yeye pia aliitunza Sabato (Luka 4:16) na kuiidhinisha kama siku inayowaletea Wakristo manufaa (Marko 2:27,28.) Mafungu kadhaa katika kitabu cha Matendo yanaonyesha wazi kwamba wanafunzi wake Kristo waliabudu katika siku ya Sabato baada ya ufufuo wake (Matendo 13:14, 16:13, 17:2, 18: 1-4, 11).

  1. Suala Lenye Utata

  Hiyo inatufikisha sisi kwenye somo ambalo wengi huliona kuwa lina utata kwao. Kwa kipindi fulani ulimwengu wa Kikristo umekuwa ukizitunza siku mbili tofauti. Kwa upande mmoja, Wakristo wengi sana kwa unyofu wa moyo wanaitunza Jumapili, siku ya kwanza ya juma, ambayo wao wanaamini kwamba ndiyo ukumbusho wa ufufuo wake Kristo. Kwa upande ule mwingine, kundi kubwa la Wakristo, nao vilevile wakiwa ni wanyofu wa moyo, wanaamini kwamba Biblia inaipa heshima siku ya saba peke yake kama ndiyo Sabato na ya kwamba hakuna mahali popote inapothibitisha utakatifu wa Jumapili.

  Je! inaleta tofauti yeyote juu ya siku gani tunayoitunza kama Sabato? Sisi kama watu walio wanyoofu wa moyo na wenye ari tunaotaka kuijua kweli, ni lazima tujiulize wenyewe swali hili. “Je! Ni jambo gani ambalo ni maana kwa Yesu? Hivi Yesu anataka mimi nifanye nini?

  Katika kufikiria uamuzi wa jambo hilo, mambo kadhaa ya maana hayana budi kuwekwa wazi, je ni nani aliyeibadili Sabato kutoka Jumamosi siku ya saba ya juma, kwenda Jumapili siku ya kwanzia ya juma? Je! Hivi Biblia inatoa idhini kwa badiliko kama hilo?Kama jibu ni ndiyo, Je, Mungu, Kristo, au labda wale mitume ndio waliofanya badiliko hilo?

  Tutaendelea mbele kwa kuangalia uwezekano wo wote uliopo

  2. Je! Ni Mungu Aliyebadili Siku?

  Je! Kuna tamko lolote toka kwa Mungu ambalo linaibadilisha Sabato kutoka siku ya saba kwenda siku ya kwanza ya juma?

  Wakristo wengi sana wanazikubali Amri kumi kama mwongozo halali ambao kwa huo sisi tunpaswa kuishi. Huu ni ujumbe wa pekee ambao Mungu mwenyewe amepata kuandika kwa ajili ya wanadamu. Ni za muhimu sana, aliziandika juu ya mbao za mawe kwa kidole chake mwenyewe (Kutoka 31:18).

  Katika ile amri ya nne Mungu anatuagiza sisi anasema:
  “Ikumbeke siku ya Sabato uitakase. Siku sita fanya kazi na kutenda mambo yako yote, lakini SIKU YA SABA NI SABATO YA BWANA, MUNGU WAKO. Siku hiyo usifanye kazi yoyote, … maana kwa siku siku sita BWANA alifanya mbingu, na nchi, na bahari na vyote vilivyomo, lakini AKAPUMZKA siku ya saba. Kwa hiyo BWANA AKAIBARIKI siku ya Sabato AKAITAKASA” – Kutoka 20:8-11.

  Mungu alipowapa watu wake zile Amri kumi, pia alieleza wazi kwamba maagizo yale yaliyotoka kinywani mwake asiwepo mwanadamu yeyote wa kuyafanyia marekebisho yeyote ili kuyafanya yawe bora zaidi au kuondoa maneno yake yeyote anapofanya uhariri wake.

  “MSIONGEZE neno lolote katika yale niwaamuruyo, wala MSIPUNGUZE neno lolote, bali zishikeni amri (kumi) za BWANA, Mungu wenu ninazowapa ninyi” – (Kumbukumbu la Torati 4:2).

  Mungu mwenyewe anatoa ahadi kwamba hawezi kuzibadili amri zake [kumi]:
  “MIMI SITALIVUNJA agano langu, wala SITABADILI NENO LILILOTOKA MIDOMONI (MWANGU) – (Zaburi 89:34).

  Biblia inaeleza waziwazi kwamba Mungu hakubadili Sabato kutoka siku ya saba kwenda ile ya kwanza ya juma.

  3. Je! Yesu Aliibadili Sabato?

  Kulingana na maneno ya Yesu, Amri kumi haziwezi kubadilika kamwe:
  “Msidhani ya kuwa nimekuja kutangua sheria na mafundisho ya manabii. Sikuja kutangua bali kukamilisha. Kweli nawaambieni, mpaka hapo mbingu na dunia zitakapopita, hakuna hata nukta moja au sehemu ndogo kabisa ya sheria itakayoondoka mpaka yote yametimia” – (Mathayo 5:17-18).

  Katika Mwongozo 16 tuligundua kwamba desturi ya Yesu ilikuwa ni kwenda kuabudu katika sinagogi siku ya Sabato (Luka 4:16). Pia tuligundua kwamba Yesu alitaka wanafunzi wake waendelee kuionja raha ya kuitunza ile Sabato ya kweli (Mathayo 24:20)

  Ni dhahiri, basi, kwamba kutokana na mafundisho ya Yesu na kielelezo chake sisi bado tunayo haja ya hilo pumziko la Sabato, yaani, kustarehe na kuutumia wakati wetu pamoja na Mungu.

  4. Je! Wale Mitume Waliibadili Sabato?

  Yakobo, kiongozi wa kwanza wa kanisa lile la mwanzo, aliandika maneno haya kuhusu zile Amri kumi:
  “Anayevunja amri mojawapo ya sheria, atakuwa na hatia ya kuivunja sheria yote. Maana yule yule aliyesema: “USIZINI, “alisema pia” “USIUE.” Kwa hiyo, hata ikiwa hukuzini, lakini umeua, wewe umeivunja sheria” – (Yakobo 2:10, 11).

  Luka, tabibu na mwinjilisti katika kanisa lile la kwanza, anatoa taarifa hii.

  “Siku ya Sabato tukatoka nje ya mji, tukaenda kando ya mto, ambapo tulidhani kuwa mahali pa kusali. Tuliketi, tukiongea na wanawake waliokusanyika mahali hapo” – (Matendo 16:13).

  Kitabu cha Matendo cha Agano Jipya kinataja mara 84 ilipotunzwa. Sabato hiyo na wafuasi wa Kristo, zote hizo zilikuwa zikitunzwa zaidi ya miaka 14 baada ya ufufuo wa Yesu: Sabato 2 pale Antiokia (Matendo 13:14,42,44); 1 pale Filipi (Matendo 16:13), 3 pale Thesalonike (Matendo 17:2,3), Sabato 78 pale Korintho (Matendo 18:4,11).

  Yohana, wa mwisho kufa miongoni mwa wale mitume kumi na wawili, aliitunza Sabato. Aliandika hivi:
  “Siku ya Bwana nilikuwa katika Roho” – (Ufunuo 1:10).

  Kulingana na maneno ya Yesu, siku ya Bwana ni Sabato:
  “Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa Sabato” – (Mathayo 12:8).

  Uchunguzi wa ushahidi wa maandiko unaoonyesha wazi kwamba wale mitume hawakufanya jaribio lolote la kuibadili siku ya Mungu ya mapumziko kutoka siku ya saba kwenda ile siku ya kwanza ya juma. Agano jipya, linaitaja siku hiyo ya kwanza ya juma mara nane tu. Katika mifano hiyo yote hakuna ambapo siku ya kwanza ya juma inatajwa kuwa ni takatifu, wala hata kudokezwa kuwa tunapaswa kuitenga kama siku ya ibada. Uchunguzi uliofanywa kwa makini sana wa hayo mafungu manane yanayoitaja siku ya kwanza ya juma huonyesha matukio haya yaliyotokea Jumapili:

  (1) Wanawake walikwenda kaburini siku ile ya kwanza ya juma (Mathayo 28:1).
  (2) “Hata Sabato ilipokwisha” wanawake wakaanza tena kufanya shughuli zao za kidunia katika siku ile ya kwanza ya juma (Marko 16:1,2).
  (3) Yesu alimtokea kwanza Mariamu Magdalena mapema siku ile kwanza ya juma (Marko 16:9).
  (4) Wafuasi wa Yesu walianza tena kufanya shughuli zao katika ile siku ya kwanza juma (Luka 24:1).
  (5) Mariamu alikwenda kwenye kaburi lile la Yesu na kulikuta kaburi liko tupu katika ile siku ya kwanza (Yohana 20:1).
  (6) Wanafunzi wale walikusanyika mahali pamoja “kwa hofu ya Wayahudi” (si kwa ajili ya kuendesha ibada ) Katika ile siku ya kwanza ya juma (Yohana 20:19).
  (7) Paulo aliwaomba washiriki wa kanisa kufanya mahesabu ya fedha zao walizopata katika ile siku ya kwanza ya juma, na “kuweka kando kiasi fulani cha fedha” kwa ajili ya maskini kule Yerusalemu (I Wakorintho 16:1,2). Kifungu hicho hakitaji mkutano wowote wa dini ambao ulifanyika.
  (8) Katika Matendo 20:7 Luka anaongea habari za hotuba (mahubiri) ya Paulo aliyoitoa katika ile siku ya kwanza ya juma wakati wa mkutano ule wa kuagana ambao haukutazamiwa kufanyika. Kusema kweli, Paulo alihubiri kila siku, na mitume wale walimega mkate kila siku (Matendo 2:46).

  Hakuna hata moja kati ya mafungu hayo linalodokeza ya kwamba wale mitume waliazimu kuacha kuitunza Sabato ya siku ya saba. Mitume wale hawakulitaja badiliko lolote la Sabato kutoka siku ya saba kwenda ile ya
  kwanza ya juma. Hakuna ushahidi wowote ulio wazi katika Agano Jipya unaoonyesha badiliko hilo la Sabato kutoka Jumamosi, siku ya saba ya juma, kwenda Jumapili, siku ya kwanza ya juma. Badiliko hilo lilikuja baada ya siku zile za Yesu na mitume wake, kwa hiyo, yatupasa sisi kuigeukia historia ili kuona ni lini na kwa jinsi gani badiliko hilo lilitokea.

  5. Jumapili Ilitoka Wapi?

  Mitume wale wanatuonya sisi waziwazi kwamba Wakristo fulani wangetangatanga na kwenda mbali na mafundisho ya Ukristo ule wa Agano Jipya: “Iweni macho ” (Matendo 20:29-31). Na ndivyo ilivyotokea hasa. Wanahistoria wanaoaminika wanaandika waziwazi kuonyesha jinsi Wakristo walivyoanza kupotea na kuuacha usafi ambao kanisa lile la mitume lilikuwa nao. Mapokeo na mafundisho ambayo hayakuungwa mkono kamwe na Paulo, Petro na waasisi wale wengine wa kanisa lile la Kristo, yakaanza kuingia taratibu ndani ya kanisa.

  Badiliko lililofanyika kutoka katika utunzaji wa Sabato kwenda kwenye utunzaji wa Jumapili lilitokea baada ya kukamilika kuandikwa kwa Maandiko ya Agano jipya na baada ya kufa mitume wale wote. Historia inaandika katika kumbukumbu zake ya kwamba hatimaye Wakritsto wakahama kutoka katika kufanya ibada yao na kupumzika siku ya saba kwenda katika siku ile ya kwanza ya juma. Lakini, kwa kweli, waumini hawakuacha kuitunza Sabato ile ya siku ya saba mwishoni mwa juma fulani lililowekwa na ghafla kuanza kuitunza Jumapili kama siku ya Bwana. Mfano mmoja uliothibitishwa ambao ulitokea mapema sana wa utunzaji wa Jumapili na Wakristo ulitokea katika nchi ya Italia, katikati ya karne ile ya pili baada ya pale Wakristo wengi walizitunza siku zote mbili, ambapo wengine bado waliendelea kuitunza Sabato peke yake.

  Tarehe 7 Machi, 321 B.K Konstantino Mkuu alitoa amri ya kwanza ya Kiserikali ya Jumapili, akawalazimisha wote, isipokuwa wakulima, katika Dola ya Kiroma kupumzika Jumapili. Hivyo pamoja na sheria nyingine zipatazo tano za kiserikali zilizoamriwa na Konstantino kuihusu Jumapili, ziliweka mfano wa sheria zote za Jumapili kuanzia wakati ule mpaka leo. Katika ile karne ya nne Baraza la Laodikia liliwakataza Wakristo wasiache kufanya kazi siku ya Sabato, huku likiwashurutisha kuiheshimu Jumapili kwa kuacha kufanya kazi endapo uwezekano ulikuwapo wa kufanya hivyo.

  Historia inaonyesha kwamba ibada ya Jumapili na utunzaji wake ni desturi iliyowekwa na wanadamu. Biblia haitoi kibali chochote ili kuifutilia mbali Sabato ya siku saba ya amri ile ya nne. Nabii Danieli alitabiri kwamba katika kipindi kile cha Kikristo mamlaka fulani yenye hila ingejaribu kuibadili sheria ya Mungu (Amri Kumi) (Danieli 7:25)

  6. Ni Nani, Aliyefanya Badiliko?

  Je! Ni nani aliyeihamisha rasmi Sabato kutoka siku ya saba kwenda siku ya kwanza ya juma? Kanisa Katoliki linadai kwamba limefanya badiliko hilo. Katika jitihada ya kutaka kuiokoa Dola ya Roma iliyokuwa inavunjika, viongozi wa kanisa waliokuwa na kusudi zuri wakafanya maridhiano na kujaribu kubadili siku ya ibada kutoka Jumamosi kwenda Jumapili.

  Katekisimo ya kanisa Katoliki la Roma inasomeka hivi:
  “Swali: Ipi ndiyo siku ya Sabato?
  “Jibu: Jumamosi ndiyo siku ya Sabato.
  “Swali: Kwa nini sisi tunaitunza Jumapili badala ya Jumamosi?
  “Jibu: Tunaitunza Jumapili badala ya Jumamosi kwa sababu kanisa Katoliki …. Liliihamisha ibada toka Jumamosi kwenda Jumapili”.
  – Peter Geirmannn, The Convert’s Catechism of Catholic Doctrine (toleo la 1957). Uk. 50.

  Kwa majivuno kanisa Katoliki linatangaza kwamba viongozi wa kanisa ambao ni wanadamu tu ndio waliofanya badiliko hilo.

  “Siku ile takatifu, yaani, Sabato, ilibadilishwa kutoka Jumamosi kwenda Jumapili… si kutokana na maagizo yo yote yaliyoonekana katika Maandiko bali kutokana na hisia ya kanisa kwamba linao uwezo wake lenyewe… watu wale wanaofikiri kwamba Maandiko ndiyo yangekuwa mamlaka peke yake, kwa mantiki hiyo, ingewapasa kuwa Waadventista Wasabato , nao wangeitakasa Jumamosi.” – Cardinal Maida, Askofu Mkuu wa Detroit, Saint Catherine Catholic Church Sentine, Algonac, Michigan, Mei 21, 1995.

  7. Je! Makanisa Ya Kiprotestanti Yanasemaje?

  Hati rasmi zinazotoa muhtasari wa itikadi za madhehebu kadhaa ya Kiprotestanti zinakiri kwamba Biblia haitoi kibali cho chote cha kuitunza Jumapili.

  Martin Luther, mwasisi wa kanisa la Kilutheri, aliandika katika ungamo la Augusiburgi (Augusburg Confession), sharti la imani la 28, aya ya 9, maneno haya: “Wao [Wakatoliki wa Roma] wanadai kwamba Sabato ilibadilishwa na kuwa Jumapili, siku ya Bwana, kinyume na ile sheria ya Amri kumi,.. wala hakuna mfano wanaojivunia sana kama huo wa kuibadili siku ya Sabato. Ni mkuu, wasema wao, uwezo na mamlaka ya Kanisa, kwa kuwa liliiondoa mojawapo ya zile Amri kumi.”

  Wanatheolojia wa Kimethodisti Amosi Binney na Danieli Steele walitoa maoni yao haya:
  “Ni kweli, hakuna amani dhahiri ya ubatizo wa watoto wachanga….wala hakuna yo yote ya kuitakasa siku ya kwanza ya juma.” Theological Compend (New York: Methodist Book Concern, 1902), Kurasa 180,181.

  Dk. N. Summerbell, mwanahistoria wa wanafunzi wa Kristo (Disciples of Christ) au Kanisa la Kikristo (Christian Church), aliandika, alisema:
  “Kanisa la Roma lilikuwa limeasi kabisa…..Liliigeuza Amri ya Nne kwa kuiondoa Sabato ile ya Neno la Mungu, na kuiweka Jumapili kama siku takatifu” A True History of the Christian and the Christian Church, kurasa za 417,418.

  8. Suala Lenyewe hasa ni lipi?

  Jambo hilo linatuleta ana kwa ana kupambana na maswali haya: kwa nini Wakristo wengi sana huitunza Jumapili bila kuwa na idhini ya Biblia? La maana zaidi ni hili, Je! Niitunze siku gani? Je! Niwafuate wale wasemao, “Sidhani kwamba inaleta tofauti yoyote kuhusu siku gani ninayoitunza mradi tu mimi naitunza moja katika zile saba”? Au, Je! Niihesabu kuwa ni ya maana ile siku ambayo Yesu, Muumbaji wetu, aliianzisha alipoiumba Dunia yetu hii, tena ni siku ile aliyoiteua Mungu na kuiweka katika zile Amri kumi: yaani, kwamba “siku ya saba ni Sabato”?

  Hapa tunashughulika zaidi ya utunzaji wa nje tu, bali juu ya siku ipi yaonekana kibiblia kuwa ni sahihi. Hoja muhimu inayohusu hapa ni ile ya utii kwa Yesu. Muumbaji wetu aliitenga Sabato kama siku “Takatifu,” kama ndio wakati uliowekwa kwa ajili yetu na familia zetu kumkaribia yeye zaidi ili tupate kupewa nguvu na burudiko. Nitamtii nani? Je! Nimtii Kristo, mwana wa Mungu, au mapokeo ya wanadamu katika suala hili la siku ninayoitakasa? Uchaguzi uko wazi: mafundisho ya wanadamu au amri za Mungu. Neno la wanadamu au Neno la Mungu. Siku mbadala iliyowekwa na wanadamu au amri ya Mungu.

  Nabii Danieli anatoa onyo kwa wale ambao wange”jaribu kubadili majira yaliyowekwa pamoja na sheria” (Danieli 7:25,NIV) [“azimu kubadili majira na sheria” (Daniel 7:25, NKJV)]. Mungu anawaita watu wake warudi na kumtii yeye. Anawaita ili wapate kuitunza Sabato kama ishara ya Utii na upendo wao kwake yeye.

  Yesu alisema, “Mkinipenda, mtakishika kile niwaamurucho” (Yohana 14:15). Tena yeye anaahidi kuwapa furaha kamili wale wampendao hata kuweza kuzitii amri zake (Yohana 15:9-11). Tunaye Mwokozi wa ajabu. Anayo shauku nyingi kwa ajili yetu ili sisi tupate kuuonja upendo wake kwa utimilifu wake wote. Moyo ule ulio na utii wa hiari unafungua mlango wazi ili kuupokea upendo huo.

  Katika ile bustani ya Gethsemane Kristo alijinyenyekeza kikamilifu chini ya mapenzi ya Baba yake – licha ya kukabiliwa na msalaba na dhambi za ulimwengu mzima zilizokuwa zikiyaangamiza maisha yake. Alipomlilia Mungu, na kusema, “Uniondolee kikombe hiki,” alikuwa amejinyenyekeza katika maombi yake, kisha akaongeza kusema hivi “Walakini, si kama nitakavyo mimi, bali utakavyo wewe” (Marko 14:36).

  Kristo anatamani sana kwamba sisi tupate kuuonja utimilifu ule uletwao na maisha yaliyosalimishwa kweli kweli. Pia anataka sisi tuionje furaha ya pumziko la Sabato. Anataka sisi tumtumainie yeye kiasi cha kutosha kumtii katika mambo yote ya maisha yetu. Endapo wewe utaitika anapokuita na kuzitii amri zake zote [kumi], basi, wewe utaweza kuionja ahadi ya Yesu isemayo kwamba furaha yake itakuwa “ndani yenu” na “furaha yenu” ita “timizw[a]” (Yohana 15:11).

  © 2004 The Voice of Prophecy Radio Broadcast
  Los Angeles, California, U.S.A.

 144. MM NAONA HAKUNA TABU SANA KILA MTU AENDELEE KUABUDU SEHEMU YAKE KWANI SABATO MUNGU AKUWAPA WAYAHUDI BALI NI WANA WAISLAELI NDO SISI NDO WW …….KAMA NI HIVYO YESU ASINGEKUWA ANAENDELEA KUABUDU SABATO SOMA LUKA 4:16 NA MITUME WAKE WALIENDELEA KUDUMU KUABUDU SIKU YA SABATO SOMA MATENDO YA MITUME……………………..PIA HATA MATAYO 24:15-24 KIPINDI CHA DHIKI YESU ANAWAONYA WANAFUNZI WAKE KUWA KUKIMBIA KWAO KUSIWE SIKU YA SABATO……….PIA MM NAJUA KUPITIA HATA KATIKA HISTORIA JINSI UFALME WAROMA ULIVYOWATESA WAKIRISTO KIPINDI CHA ZAMA ZA GIZA ZAMA ZA UJINGA,,,,,,,,KIPINDI HICHO UHURU WA KUABUDU ULITOWEKA KABISA KWANI WATU WALILAZIMISHWA KUABUDU SIKU YA KWANZA YA JUMA ,,,,,HAYA NDO MAMBO YANAYOENDELEA TENA HAPA DUNIANI MKITOKA HAPA MNAJIITA WAPROTESTANT WAKATI MMEYARUDIA YALE MLIYOYAKATAA,,,,,,,,,,UBATIZO WATOTO WADOGO. KUSUJUDIA SANAMU NA MAMBO MENGI MENGI TU,,,,,ILA BIBLIA INASEMA HUYO MNYAMA WA 4 WATU WENGI WATAMSUJUDIA SANA SOMA DANIEL 7 NA UFUNUO12 NA 13……….PIA SOMA HUO UFALME KUPITIA KWENYE KATEKISIMU YAKE ULISEMA WENYEWE NDO ULIBADILI SIKU YA KUSALI TOKA JUMAMOSI KWENDA JUMAPILI LEO WW UNAPINGA SIJUI UNA MAANA GANI?? HATA BIBLIA IMEANDIKA HAYO SOMA DANIEL 7:25………… NAKUOMBA USOME SANA KWANI MUNGU ALIWAAMBIA WANA WAISLAELI KUWA SABATO NI AGANO LA MILELE SOMA KUTOKA 31:13……LEO UNA NG’ANG’ANIA WAYAHUDI TU KUMBE WENYEWE PIA WALIMUASI MUNGU KWA KUTO ISHIKA SABATO VIZURI NA KUTENDA YANAYOPASWA KWA HIYO YATUPASWA SISI TUISHIKE SABATO VIZURI NA KUTENDA MAMBO MEMA…. NA PIA ELEWA HUYU YESU ALIKUJA KUBADILI SABATO TU AMRI NYINGINE AKAZIACHA? HIZI NI AMRI ZA MILELE KAKA LWEMBE LABDA HUYU MUNGU BASI NI KIGEU GEU SOMA ISAYA 66:22- ANASEMAJE? ………..JAMANI MSIWAANGALIE SANA WAYAHUDI HAWA PIA WALIASI NA HATA WANAWAISILAELI WAKAANZA KUABUDU SANAMU HATA JUA KWA HIYO HAWA WASIWE MFANO KAMA UNAFUATA WAYAHUDI AU WAROMA KAKA UMEUMIA FUATA BIBLIA KWANI SIJAONA AMBAPO MUNG AMETULETEA AMRI MPYA HATA YESU ALICHOKIFANYA NI KUYATIMILIZA MAANDIKO SIYO KUYABADILISHA……WENZAKO WAYAHUDI ILIFIKIA KIPINDI WAKARUSHA HADI JIWE HAPO LITAKAPOFIKIA NDO MWISHO WA KUTEMBEA SIKU HIYO YA SABATO KUMBE HATA HAWA WALIASI BASI NA WW USIENDELEE KUASI KWA MFANO HUU……..WW SASA NDO INABDI UENENDE NA MAANDIKO NA UYATIMIZE…….

  KAKA POLE NENDA KWENYE MADUKA YA VITABU VYA KIKATOLIKI UNUNUE ZILE BIBLE ZAO UZISOME VIZURI ……UTAONA NINI KINACHOENDELEA KATIKA HUU ULIMWENGU KWANI KATIKA JARIBIO LINALOTUIJIA WATU WA MUNGU WALE WAPROTESTANT WA KWELI WATATESWA SANA ………….KIJANA KAA ILI UENDELEE KUWASAIDIA WENZAKO ILI WAITIZE HIYO SHERIA YA JUMAPILI YAANI SUNDAY LAW ……..LEO VIPINDI VYA MASOMO VINAFANYWA HADI JUMAMOSI HAPO KUNA UPENDO HIZO NI MBINU ZA SHETANI ILI KUTAKA KUISHAMBULIA SABATO YA MUNGU TU………….BASI WANGEACHA ZILE SIKU ZIJULIKANE KAMA SIKU YA KWANZA YA JUMA HADI YA SABA…..HATA LEO MNAOSALI NAO WANAJUA JUMAPILI NDO SIKU YA SABA …… JE KULIKUWEPO NA LOGIC GANI KUBADILISHA HAYA MAJINA WAKAANZA HADI KUITA MAJINA YA MIUNGU WA KIROMA??? JIULIZE KAKA……………SISI WASABATO HATUWALAZIMISHI WATU MJE KUSALI JUMAMOSI ILA TUNAWAHUBIRI WATU….NYIE WA JUMAPILI MNALAZIMISHA WATU KUPITIA VYUO VYENU SHULE ZENU TENA KWA KUWEKA VIPINDI SIKU YA JUMAMOSI ILI KUWAKOMOA WASABATO HAPO PENDO HALIMO NDANI YENU HAMTAKI KUWAFUNDISHA WATU JUU YA KILE MNACHOKIAMINI ILA MNATUMIA NGUVU NA MIUJIZA ILI KUWAVUTA WATU SIYO KWELI YA MUNGU SISEMI KWA USHABIKI…………….

  TUWENI NA UPENDO TUWACHE KUWA NA TABIA ZA BAADHI YA WAYAHUDI KWANI SIYO WOTE WALIYOKUWA NA ROHO MBAYA KUNA WATU KAMA AKINA DANIEL YOHANA PETRO NA WENGINE AMBAO NI KIELELEZO KWETU …..HATA LEO WAPO WAKRISTO JINA TU NA WAPO WA KWELI KWA HIYO UKISEMA WAYAHUDI USISEME WOTE KWANI WALIKUWEPO AMBAO WALIKUWA NA UPENDO SANA NA WANASOMA NENO LA MUNGU ILA WENGI WALIKUWA HAWASOMI BIBLIA KAMA LEO WATU WANABAKI KUSIKILIZA TU NENO NA HAWASOMI NA HAWALITENDI………………….KWA HIYO WAYAHUDI KUWEPO NI FAIDA KWETU ILI TUWE NA UWEZO WA KUPAMBANUA MAMBO MEMA……..NI SAWA NA MTU KAMA FARAO MUNGU ALIKUWA NA UWEZO WA KUMWANGAMIZA HATA KABLA YA,,,,,LKN UELEWE MUNGU NAYE ANATUMIA BINADAMU ILI KUTIMIZA UNABII………………………………. KAKA MUNGU WA ISLAEL AKUBARIKI SANA

  NAOMBA USOME SANA VITABU UTELEWA KWELI IPO WAPI? UTAELEWA NINI MAAANA YA PROTESTANT?,,,USIJE UKAWA UMERUDIA MATAPISHI KAKA

 145. Tatizo ninaloliona kwenu ninyi akina Matiku na wenzio, ni UFAHAMU! Mmejichanganya kwa kupanda basi ambalo si lenu, mmepanda basi la Wayahudi wakati ninyi ni wa Mataifa!! Ndio maana mnaambiwa kuwa ninyi si Wakristo, kwa sababu ni watu mliochanganyikiwa, mnataka kutembea njia mbili kwa wakati mmoja!

  Kanisa la Kristo limezaliwa katika Agano Jipya, huku ndiko watu wa Mataifa mlikoitiwa Wokovu, wa miili na roho zenu. Roho zenu zilizokombolewa zikiitiisha miili yenu. Basi imekuwaje tena mmerudi mwilini na kuanza kuyarukia mambo yasiyo wahusu ilhali mkiyaacha Mema mliyokirimiwa? Kanisa la Kristo ndugu zangu ni la ROHONI, ni lazima mfike katika hali hiyo ya “Kuzaliwa mara ya Pili” ndipo mtaweza kuyaelewa mnayoelekezwa!

  Kanisa halijawahi kupewa siku ya kuabudu, acheni kuvamia mambo msiyo na ujuzi nayo. Angalieni mlivyoishia kuungana na wanaopinga Ufufuo huku nanyi mkijifanya ni wenye kuutukuza, ni unafiki kiasi gani! Hivi hao Katoliki waliowadanganya kuwa eti wao ndio walioibadili siku ya ibada, hamjiulizi wameibadili siku ya ibada ya akina nani? Kwanza hao Katoliki wenyewe wanayo siku ya kwao waliyoiumba? Kwamba wanaiabudu Jumapili kwa kuipa mojawapo ya miungu yao ya uongo siku hiyo, hilo ndilo linaweza kuifanya siku ya Jumapili kuwa ni siku ya mungu Jua? Au nanyi bila kujua mmeungana nao katika kumtukuza huyo mungu jua nanyi kwa kukosa Maarifa wala hamulijui hilo??

  Kanisa linakusanyika katika SIKU YA BWANA kwa sababu hilo ni mali yake! Wao hukusanyika katika siku hiyo wakikutukuza kufufuka kwake, ambako bila huko kufufuka, kanisa lisingekuweko! Yasome Maandiko uwaone mitume jinsi kusulubishwa kwake kulivyo wasambaratisha, halafu kutazame kufufuka kwale kulivyowakusanya!!!

  Matiku, acheni mambo ya kuigiza, sabato unayoishabikia ni ya Wayahudi ambao mpaka leo hii wao wanakukataa kufufuka kwa Kristo, wanaishi katika ule uongo kwamba wanafunzi wake waliuiba mwili wake, kama nanyi mnavyoishi katika uongo wa Wakatoliki kuwa wao ndio walioibadili siku ya ibada. Mmeona jinsi mlivyo wepesi wa kuupokea uongo kuliko KWELI ya Injili? Angalia jinsi mlivyokuwa wanafiki, mnapiga kelele kuwa Katoliki wamebadili siku na kalenda na miezi, halafu hiyo sabato yenu mnaifuata kutoka katika kalenda hiyo hiyo ya Wakatoliki iliyopotoshwa, unakuona kujichanganya kwenu, unajihesabia haki kwa kuutukuza uongo!

  Ila jambo moja Matiku ninalokusifia, ni hayo maono uliyoyaona: “NIKAGUNDUA WASABATO NDO WATAKAO TESEKA KWENYE DHIKI KUU INAYOKUJA……..”, hii ni kweli kabisa kwa mafundisho mliyonayo, yaani hiyo shuka mliyojiviringisha nayo, hiyo ‘sanda’, ni matayarisho mazuri ya kuipokea hiyo DHIKI KUU inayowajia, kwa sababu mmeikataa Neema iliyo katika Kristo kwa Imani na badala yake mmeng’ang’ana na Sheria isiyo na Imani!

  Ninawatakia fanaka za Dhiki Kuu, na asiwepo kibogoyo kati yenu na akiwepo basi apewe meno, ili kule “kulia na kusaga meno” kuwatimilie kulingana na ONO lako ulipendalo!

 146. JAMANI WAPENDWA HATA MKIBISHA SANA LKN UKWELI JUU YA SABATO UKO PALE PALE MM BAADA YA KUSOMA MAELEZO YENU NIMEONA KUWA SABATO NI SIKU YA KUPUMZIKA, KUSTAREHE KUABUDU NA KUSANYIKO TAKATIFU………NIMEJARIBU SANA PIA KUONGEA NA WACHUNGAJI WENGI UKIWAULIZA NI KWANINI WANASALI JUMAPILI WANA SEMA NDO SIKU AMBAYO YESU ALIFUFUKA KWA HIYO NI SHEREHE,,,,,,,,,,PIA HAYA MAJINA YA SIKU YALIBADILISHWA NA WATU MFANO SUNDAY ILIKUWA NI SIKU YA MIUNGU JUA………..SASA NIKAULIZA NI KWANINI JUMAPILI ISINGEBAKIA SIKU YA KWANZA YA JUMA HADI KWENYE KALENDA????? NIKAGUNDUA HAPA KUNA MTU ALIFANYA HAYA MABADILIKO,,,,,,,,,,,,,PIA MUNGU WETU SI WA KIGEU GEU KAMA MWANADAMU…….MUNGU ALISEMA SABATO NI AGANO LA MILELE……………TATIZO WATU KUMBE HATUSOMI BIBLE WASABATO WENZETU WANASOMA SANA BIBLIA NDO MAANA HAWA WATU WAKO TOFAUTI SANA

  MWISHO MM NIMEAMUA KUWA MSABATO KABISA HAYA MADHEHEBU MENGINE HAYAFUNDISHI BIBLIA KAZI NI SADAKA ,,,,,,,,,HALAFU MBONA WANATAKA KULAZIMISHA SHERIA YA JUMAPILI LEO HADI VYUO VYA KIKATOLIKI NA MORAVIAN WAMEWEKA RATIBA HADI JUMAMOSI ILI KUWAKOMOA WASABATO,,,,,,,,,,,NIMEGUNDUA HAWA HAMNA PENDO NA HAWANA KWELI YA MUNGU NDO MAAANA WANATUMIA NJIA HII YA KULAZIMISHA ,,,,,,NIKAGUNDUA WASABATO NDO NWATAKAO TESEKA KWENYE DHIKI KUU INAYOKUJA……..

  PIA MNAJUA MAANA YA NENO PROTESTANT????????

  hii ilikuwa kwenda kinyume na serikali ya kipagani ya kirumi iliyoanzisha kanisa katoliki leo naona bado watu tunazini naye tumeisha sahau yaliyowapata babu zetu kipindi cha zama za giza

 147. Ndugu Juma Alli,
  Nimefurahi kuusikia ukweli wako katika wokovu ulioujia!

  Basi kwa kadiri ya Neema aliyotujalia Bwana, nitajaribu kuyajibu maswali uliyoyauliza kama ifuatavyo:

  1. Je amri kumi ni mojawapo ya mambo ya mwilini hivyo basi uhalali wake umeondoka baada ya ujio na kifo cha Yesu msalabani?
  JIBU: Ni sawa, uhalali wa Amri Kumi unaishia katika ujio wa Kristo kwa huyo aliyempokea, maana huyo hubadilishwa asili yake kwa hiyo Injili na kuwa kiumbe kipya. Yaani, kimfano, ni sawa na kumchukua mbwa aliyekubuhu kwa tabia za kimbwa, kisha ukamfanyia upasuaji ukaiondoa ile asili ya mbwa na kumuwekea ya kondoo, basi jua kuwa mbwa huyo atalia kama kondoo na atakuwa na tabia za kondoo! Kwa hiyo Mkristo aliyefika katika kiwango cha kujazwa Roho Mtakatifu, huyo huwa na tabia za Kristo! Basi kwa kadiri unavyoendelea na mafundisho, ndipo utajua kwa uhakika kuwa Kristo hakuwahi kujizuia asizini au kuikiuka amri yoyote ile kati ya hizo kumi, huko ndiko KUWA JUU YA SHERIA!
  Rumi 8:1-5 “Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu. Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti. Maana yale yasiyowezekana kwa sheria, kwa vile ilivyokuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu, kwa kumtuma Mwanawe mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa sababu ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili; ili maagizo ya torati yatimizwe ndani yetu sisi, tusioenenda kwa kufuata mambo ya mwili, bali mambo ya roho.”

  2. Je matendo ya mwili wakati wa agano la kale yaliamua hatima ya wokovu wa mtu, sasa je matendo ya mwili ni muhimu au la?
  JIBU: Matendo ya mwili kwa Mkristo katika maana ya kumstahilisha Wokovu hayana nafasi tena. Kuyategemea matendo ya mwili ni ushuhuda wa kutokufikiwa na ile Neema, maana hao walioifikia Neema huenenda katika roho miili ikiwa imekwisha kutiishwa, kama tulivyosoma hapo juu!

  3. Kuna tatizo gani kama mimi rohoni mwangu ninamwamini na kumpenda Mungu lakini baadhi ya matendo yangu huvunja amri zake.. je nitahesabiwa makosa au kwakuwa sasa kila kitu ni katika roho nisiwe na mashaka? (Huwa na tamani na mara moja moja nazini)
  JIBU: Kwa kifupi, kuhusu hali uliyonayo nitakuambia hivi, kulingana na Biblia, wewe ni kweli umeokoka, yaani hapo ulipoipokea Injili na kuiamini na kubatizwa kwa jina lake Bwana Yesu Kristo, ukaondolewa dhambi zako kwa Kuhesabiwa Haki. Hiyo ndiyo hatua ya kwanza katika Wokovu, yaani Kuokoka. Sijajua unalelewa wapi, lakini wanao kulea wanao wajibu wa kukuza kwa mafundisho ya Neno la Mungu ili likulete katika hatua ya pili ya Utakaso, upate kusafishwa tabia zote za kufisha ulizofungamana nazo tokea huko ulikotoka au kabla ya Kuokoka, kama hizo tamaa zinazokushikilia za uzinzi ambazo huko kabla ya kuokoka, zilikutia mautini, lakini ulpoujia wokovu Mungu akazitupilia mbali ili akufinyange uwe kiumbe kipya. Lakini sasa unapozirudia tena baada ya kuvuka lile bonde la mauti, ni sawa na mbwa kuyarudia matapishi yake; ndipo sasa kwa uzinzi huo Mungu anasema hakuna Damu tena! Yaani HAKUNA wokovu kwako!!! Sasa ndugu yangu ninamsikitikia huyo anayekulea, maana iwapo hakukufundisha hilo ili ljae moyoni mwako kwa wingi, badala yake akakufundisha injili ya utajiri tu na kukemea vibwengo, basi anayo hatia juu yako, yaani huyo ndiye atakayeubeba huo uzinzi wako! Kama ulikuwa huyajui hayo basi upesi itafute Rehema ya Mungu jitahidi umfuate huyo mwenye mke ukiwa umeongozana na mkeo, ukayatubie hayo mbele yenu nyote wanne ili upate kuifukuza hiyo dhambi!!!

  4. Tutakapoirithi nchi (mbingu mpya na nchi mpya) tutakuwa na miili hii ikiwa haina dhambi au tutakuwa katika roho tu?
  JIBU: Sisi ni viumbe vya duniani, kama utakumbuka huko Mwanzo tulipewa bustani ya kuilima na kuyala mazao yake, tunarudi katika miili ile iliyotukuzwa! Lakini ni vizuri ukafahamu kuwa licha ya kuokoka kwako bado unaweza KUPOTEA, ilikupasa kuwasikiliza walezi wako ili Neno likutakase sawa sawa, ndipo Mungu akutie Muhuri kwa kukujaza Roho Mtakatifu ambaye kwaye haya ninayokusimulia yangekuwa ni Halisi, kule kuwa juu ya sheria na dhambi zake! Sijui iwapo walezi wako walikudanganya kuwa kuokoka ndiko kujazwa Roho Mtakatifu, wakakutiririsha na “Asante Yesu x 666, nawe ulipoflow bila kumeza mate ukajiona unanena na kujiaminisha katika hilo, hata ulimi wako ukawa laini kwa upako na kutongoza wake za watu, ndugu yangu Jehanamu na moto wake ni halisi!!!

  Mwisho, “Mr. Juma”; kujengeka kwako au kubomoka, kutategemea saana jinsi utakavyoihandle hiyo issue ya UZINZI, hebu ifanyie kazi hiyo!!!

 148. Bwana Ck Lwembe ninahitaji kufahamu zaidi toka kwako, (mimi nilikuwa mwislamu na sasa nimeokoka). Kwamba agano la kale lilikuwa ni kwa mambo ya mwilini na agano jipya ni kwa mambo ya rohoni.. nakubaliana na wewe kabisa, lakina nina maswali yafuatayo:-

  1. Je amri kumi ni mojawapo ya mambo ya mwilini hivyo basi uhalali wake umeondoka baada ya ujio na kifo cha Yesu msalabani?

  2. Je matendo ya mwili wakati wa agano la kale yaliamua hatima ya wokovu wa mtu, sasa je matendo ya mwili ni muhimu au la?

  3. Kuna tatizo gani kama mimi rohoni mwangu ninamwamini na kumpenda Mungu lakini baadhi ya matendo yangu huvunja amri zake.. je nitahesabiwa makosa au kwakuwa sasa kila kitu ni katika roho nisiwe na mashaka? (Huwa na tamani na mara moja moja nazini)

  4. Tutakapoirithi nchi (mbingu mpya na nchi mpya) tutakuwa na miili hii ikiwa haina dhambi au tutakuwa katika roho tu?

  Tafadhali naomba msaada wako ili kuweza kunijenga zaidi.

 149. sikiliza ni waambie ukitaka kujua mambo mema siku zote lazima uwe mtu wa kutafakari.
  haya mambo ya kubisha pasipo kutafakari ni tatizo.
  MASWALI YA KUJIULIZA
  1. biblia ni moja kwa nini tunatofautiana, kama siyo uasi ni nini?
  2. mambo haya yalikuwepo kabla ya dhambi mfano
  a. NDOA
  b. sabato, yaani siku ya saba baada ya uumbaji.
  sasa inakuwaje leo mambo haya yanaonekana kuwa shida kama kabla ya dhambi yalikuwepo maana yake yalikuwa matakatifu. fikiria Mungu anaweza kuwewka kitu kisichofaa kabla ya dhambi basi dhambi ilikuwepo kabla ya anguko la Adamu kama sabato haiona maana. MPENDWA SABATO NDIO ISHARA PEKEE ILIYOWEKWA NA MUNGU KUMTAMBULISHA KWAMBA YEYE NIYE MUUMBAJI NA ALIUMBA KWA SIKU SITA. MUNGU KUONYESHA MSISITIZO AKAAMUA KUIWEKA KATIKA AMRI KUMI.
  SIKILIZA INAVYOSEMA AMRI YA NNE
  8. Ikumbuke siku ya sabato uitakase. 9. Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; 10. lakini siku ya saba ni sabato ya BWANA, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya mlango yako. 11. Maana kwa siku sita BWANA alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo akastarehe siku ya saba; kwa hiyo BWANA akaibarikia siku ya sabato akaitakasa.

  WATU WANAOIKATAA SABATO NDIO WALE WA KWANZA KUSEMA MTU ALITOKANA NA NYANI.

  SASA SIKILIZA
  1. ukitunza sabato alafu we ni msengenyaji mbinguni huendi na maanisha kushika sabato hakumpeleki mtu mbinguni.
  2. kuvunja sabato pia kutakufanya kutokwenda mbinguni kwani hujayatimiza mapenzi yote ya Mungu.
  3. nini kitakachomfanya mtu aende mbinguni ni yule aliye moto, si baridi wala vuguvugu na maana ni yeye afanyaye mapenzi yote ya Mungu
  yakobo 2:10 inasema mtu ikishi sheria yote ila akajikwaa katika neno moja amekosa juu ya yoye
  inaama UKISHIKA AMRI ZA TISA ZA MUNGU UKAACHA AMRI YA SABATO UMEKOSA JUU YA ZOTE KUMI.
  4. MTU AOKOLEWI KWA KUSHIKA SHERIA/MATENDO BALI ANAOKOLEWA KWA NEEMA NA HII NEEMA INAMFANYA MTU KUBADILI TABIA MAANA YAKE KUANZA KUSHIKA SHERIA mfano mtu ataacha kuzini, kuiba na pia kutunza sabato akikili kuwa Mungu ndiye aliye muumba na siku ya saaba alipumzika.

  ACHA USHABIKI ELEWA KWA NINI YESU ALITUNZA SABATO HAPO HAPO ALIP[INGA NA MAFARISAYO YESU ALITAKA WAELEWE NAMNA YA UTUNZA SABATO KWANI SABATO INAAMBATANA NA UPONYAJI HURUMA NA SIYO ANASA ZAKO MWENYEWE NA SHUGHULI ZAKO MWENYEWE

  ZAIDI CHUNGUZA MAANDIKO UTAPONA KULIKO KUSIKILIZA TU WATU.

 150. Hallo MR. RICHARD E. MHINA!
  Nimesoma machapisho yako yote yaliyo katika safu hii, ni mengi umesema, nimeshindwa kukuelewa, kunasehemu unakubali na kuna sehemu unakataa, sasa nisaidi nijue baadhi, hasa maana uliyokuwa nayo katika kusema hivi nanukuu ”…SWALI JINGINE NI MAHALI GANI KATIKA BIBLIA PANAPOSEMA WAZIWAZI KUWA YESU NI MUNGU MWENYEZI?…Acheni kufundishwa tuuu..mjisomee wenyewe kuthibitisha mnachofundishwa tena pia myachunguze kwa umakini maandiko na kuyatafakari vyema nae kristo atawafundisha ambaye kiroho ndiye mwalimu pekee wa kweli katika mambo haya mazito ya kiroho”

  Swali la kwanza:
  Je, zipi ni sifa za MUNGU ili awe na aitwe MUNGU?
  Swali la Pili:
  Biblia inasema mwenye kufumbua mafumbo ya Mungu ni Roho 1kor.2:10. Na inaendelea Pia katika Yh.4:24, inasema Mungu ni Roho. Na katika Yh. 14:26 inasema Roho ni mwalimu! Sasa nawe unakataa YESU si Mungu mwenyezi, kisha unakubali kwamba “Kristo” ni mwalimu, unamaanisha nini, unapo sema Yesu si Mungu, au una maana Yesu si kristo?

  Swali la Tatu:
  Biblia inasema Yesu ndiye Neno, Katika Yh.1:1-3, inasema hapo mwanzo kulikuwepo na Neno, naye Neno alikuwa Mungu na kila kitu kilifanyika kutokana naye…! Pia imesemwa katika Ebr. 5:10 na Ebr. 7:1-3 kuwa, Yesu hana baba, hana wazazi, hana mwanzo wala mwisho wa uhai wake, ila amefananishwa na mwana wa Mungu! Katika Isa.9:6, Yesu anasemwa ni MUNGU mwenye nguvu na ni Baba wa milele! (a) Je, Biblia yako haikuandikwa hayo? (B) Kama imeandikwa hivyo, wewe unapata wapi ujasiri wa kumpinga Bwana Yesu Kristo kuwa si mungu mwenyezi?
  Nitafurahi kupata majibu ya maulizo yangu hayo matatu, ili nipate kujifunza kitu kwako!

 151. MITHALI6:23 “Maana maagizo hayo ni taa, na sheria hiyo ni nuru, Na maonyo ya kumwadilisha mtu ni njia ya uzima.”

  Zaburi 119:105. “Neno lako ni taa ya miguu yangu na mwanga wa njia yangu.”

  Warumi 7:12 “Basi torati ni takatifu, na ile amri ni takatifu, na ya haki, na njema.”

  AMRI KUMI ZA MUNGU katika KITABU CHA KUTOKA 20:2–17

  2. Mimi ni BWANA, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa.

  3. Usiwe na miungu mingine ila mimi.

  4. Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia. 5. Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi. BWANA Mungu wako, ni Mungu wenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, 6. nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu.
  7. Usilitaje bure jina la BWANA hatamhesabiwa kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure.
  8. Ikumbuke siku ya sabato uitakase. 9. Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; 10. lakini siku ya saba ni sabato ya BWANA, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya mlango yako. 11. Maana kwa siku sita BWANA alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo akastarehe siku ya saba; kwa hiyo BWANA akaibarikia siku ya sabato akaitakasa.

  12. Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na BWANA, Mungu wako.
  13. Usiue.
  14. Usizini.
  15. Usiibe.
  16. Usishuhudie jirani yako uongo.
  17. Usiitamani nyumba ya jirani yako; wala mke wake, wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng’ombe wake, wala punda wake, wala cho chote alicho nacho jirani yako.

  AMRI KUMI ZA MUNGU katika KITABU CHA KUMBUKUMBU LA TORATI TORATI 5:6–21

  6. Mimi ni Bwana, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa.
  7. Usiwe na miungu mingine ila mimi.
  8. Usijifanyie sanamu ya kuchonga, mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, au kilicho chini duniani, au kilicho majini chini ya nchi. 9. Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu, nawapatiliza wana uovu wa baba zao; hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, 10. nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu.
  11. Usilitaje bure Jina la Bwana, Mungu wako; maana Bwana hatamhesabia kuwa hana hatia, mtu alitajaye jina lake bure.
  12. Ishike siku ya Sabato uitakase, kama Bwana, Mungu wako, alivyokuamuru. 13. Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; 14. lakini siku ya saba ni Sabato ya Bwana, Mungu wako; siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwanao, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala ng’ombe wako, wala punda wako, wala mnyama wako ye yote, wala mgeni aliye ndani ya malango yako, ili mtumwa wako na mjakazi wako wapumzike vile vile kama wewe. 15. Nawe utakumbuka ya kuwa wewe ulikuwa mtumwa katika nchi ya Misri, na ya kuwa Bwana, Mungu wako, alikutoa huko kwa mkono wenye nguvu, na mkono ulionyoshwa; kwa sababu hiyo Bwana, Mungu wako, alikuamuru uishike sabato.
  16. Waheshimu baba yako na mama yako; kama Bwana, Mungu wako, alivyokuamuru, siku zako zipate kuzidi, nawe upate kufanikiwa katika nchi upewayo na Bwana, Mungu wako.
  17. Usiue.
  18. Wala usizini.
  19. Wala usiibe.
  20. Wala usimshuhudie jirani yako uongo.
  21. Wala usimtamani mke wa jirani yako; wala usiitamani nyumba ya jirani yako, wala shamba lake, wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng’ombe wake, wala punda wake, wala kitu cho chote alicho nacho jirani yako.

  KWA MAANA SHETANI NA WANADAMU WAMEINGILIA AMRI ZA MUNGU NA KUZIBADILISHA NA KUZIVUNJAVUNJA HATA KUTUMIA HILA ZAO KUZIFAFANUA WATAKAVYO NA SIYO KAMA ATAKAVYO MUNGU,
  .
  ROHO MTAKATIFU UKUONGOZE UPATE KUZIELEWA NA KUZISHIKA AMRI ZA MUNGU AKAISHI.

  POLE SANA KWA WALE WANAODHANI KUWA SHERIA (AMRI ZA MUNGU) ZILIWEKWA KWA AJILI YA WAYAHUDI AMA KWA WAADVENTISTA WABATO.

  MTAWACHEKA SANA WENYE KUTUNZA AMRI ZILE, ILA WAKATI WA HUZUNI YAJA KWA WACHEKAO SASA, NA ITAKUWA FURAHA NA HERI KWA WENYE HUZINI SASA, KWA MAANA WATAPUMZISHWA MILELE NA SHUGHLI WALIOIFANYA KWA UKAMILIFU.

  Ufunuo 22:18-19, 18 “Namshuhudia kila mtu ayasikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mtu ye yote akiyaongeza, Mungu atamwongezea hayo mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki.”

  19 “Na mtu ye yote akiondoa lo lote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima, na katika ule mji mtakatifu, ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki. ”

  Ufunuo 22:11 “Mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu; na mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu; na mwenye haki na azidi kufanya haki; namtakatifu na azidi kutakaswa.”

 152. Watoto wa MUNGU,
  Nimepitia nami katika sehemu hii, nimeufuatilia mjadala huu, nimeupenda, kwa sababu mjadala wenyewe umetaka watu wajifunze NENO LA MUNGU! Mwenyekujifunza ni mwanafunzi, na hii ndiyo aliyoisema Yesu mwenyewe, kama alama ya kwanza ya Watu wanaotaka kufanyika “Wana wa Mungu” “……..nendeni duniani kote mkawafuanye watu kuwa WANAFUNZI………..” Kama Sisi wote tunakubaliana kuwa Bwana Yesu Kristo ndiye MUNGU, basi hoja yetu hii itakuwa ndogo na fupi sana!
  Nimezitazama hoja na kuziona zipo katika ”makundi” mawili makuu kama ifuatavyo:-
  1. KUJUA KWAMBA; JE, SABATO NDIYO SIKU ILYOWEKWA PEKEE KWA AJILI YA IBAADA?
  2.KUJUA KWAMBA; JE, SABATO IPO KAMA AMRI NA KWA AJILI YA NANI?. YOHANA14:15 “Mkinipenda mtazishika amri zangu
  Kwakuwa Yesu ndiye Bwana wa Sabato (LK. 6:5) ni wazi kuwa ni huyohyo ndiye mfanya Amri, sasa tujiulize Yesu alitekelezaje sabato. Hilo pekee litatupa ukweli kuwa sabato ipo hasa kwa kazi gani! Ukiangalia Kut. 20:8-9, inaelekezwa na Mungu jinsi ya watu kuitumia siku hiyo, lakini ule mstari wa 10 unamtaja aliyefanya hiyo Sabato sawa na Lk.6:5, na watu wasifanye kazi yoyote. ( Kwenda popote na kufanya ibaada nayo ni kazi!). Sasa wanadamu waifanyie nini siku hiyo ya Sabato? Jibu, WAITAKASE {(Kut.28:8-9)Wafanye mema – mambo matakatifu, ndiyo maana hata Yesu akamponya Yule Mtu siku ya Sabato! } na WAFANYE KUSANYIKO LA STAREHE tu basi! (Kut. 23:12,Law.23:3, Lk. 23:56) Kwa nini “ni siku ya kuyatazama mazuri, siku ya tathimini” Hadi hapo maandiko hayajasema wazi kuwa Sabato ndiyo siku pekee ya watu kwenda kumwabudu Mungu!

  Lakini ukiitazama ile Mt. 19:16-19 utaona jinsi habari ya Mtu mmoja aliyetaka kujua ni jambo gani jema akitenda ataweza kuupata uzima wa milele. Yesu alimuuliza Mtu huyo kama anazijua amri, Yule Mtu alipotaka kujua ni Amri zipi hizo, Yesu alijibu ni hizi “…..Usiue, usizini, usiibe, Usishuhudie uongo. Waheshimu Baba yako na Mama yako na umpende jirani yako kama nafsi yako….” Utona hapo hakutaja “Ishike sana sabato!” Lakini bila kuishia hapo, tuone zaidi juu ya Amri itupasayo sana ambayo Yesu mwenyewe aliielekeza kwetu. Ukisoma katika Mt.22:36, inaelezwa kuwa Amri ya kwanza ni kumpenda Mungu kwa KILA KITU na ile ya pili ni kumpenda jirani yako kama NAFSI yao, hapo pia hajitajwa Sabato! Hebu angalia piaYh.13:34-35 inatajwa kuwa Amri mpya ni kuwa tupendane. Kumbuka kwamba watakaokubalika na MUNGU ni wale tu WATAKAOISHIKA AMRI YAKE, soma Yh.14:15 “Mkinipenda mtazishika amri zangu…”
  kwa kuishika Amri (Sheria) hiyo ndipo tutajulikana kuwa ni wanafunzi wake (Yesu). Kumbe utaona kuwa kitambulisho cha mwanafunzi wa Yesu ni Upendo na siyo Sabato, kama ilivyokawaida kama huna kitambulisho hutapita “Getini” Mtu atakaye “ivaa” shingoni SABATO na kutouvaa UPENDO kama kitambulisho atabaki nje ya Geti, maana imeandikwa Tutajulikana kama ni wanafunzi wa YESU tutakapokuwa na UPENDO, na siyo SABATO maana hakuna aliyeyatekeleza matendo ya sheria na akampendeza Mungu! – UPENDO ndiyo Amri yake (1Yh 2:8-11).

  Ieleweke kuwa sheria (Amri) ndiyo huihuhisha na kuisimamisha Hukumu, kwa maana hiyo, juu ya matendo ya upendo ndiyo hukumu itasimamia, maana watakaotenda matendo ya huruma na upendo ndiyo watakaoonekana wenyehaki – Ndiyo maana Yesu atauliza hayo tu katika kuhukumu ulimwengu soma Yh.25:35-41! Katika miandamo ya mwezi, Sikukuu, majira, nyakati au Sabato hukumu haitasimamia hayo, maana yote hayo ni matendo ya sheria ya “Mwili” ambayo ni kivuli kilichokuja kutimilizwa na Mungu kwa njia ya Yesu Kristo. Wakati Upendo ni sheria ya “Rohoni” kuifuata na kuitekeleza Sabato hakukupi haki ya kumhukumu mwingine kuwa ati amepotea! Ukisoma wakolosai 2:16 inasema “….. Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au SABATO;
  mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo…..” Utaona kuwa Shida hapa ni kwamba, watu hupenda na kutii sana mafundisho ya wanadamu kuliko kutii na kushika Neno la MUNGU, kama alivyopata kusema Mungu mwenyewe kwa kinywa cha Isaya. Biblia inasema katika Mk.7:9, kuwa mwaikataa Amri ya Mungu mpate kuyashika MAPOKEO YENU.
  Hadi hapo tufanye nini kumbe? Maana lengo, watu wote wanatamani kuiona ile siku ya kukabidhiwa uzima kwa mjibu wa Ahadi ya Mungu. Kama mtu azaniaye amesimama na kwamba anaitetea ahadi ya kweli ya Mungu, kisha akajikuta siyo, eti kwa maelezo tu kwamba alichodhani amekishikilia kilikuwa kumbe ni “Kuti kavu!” kilio kitakuwaje na hasa utakapowaona uliowadhani “siyo” wakipita mbele yako wakiwa na mavazi na taji na majina mapya, wakikwambia tulikwambia huko siko ukatuzoea! Mbaya zaidi utakapo mkuta Yule kiongozi wako wa kidini katika lile ziwa la moto na kuona wazi wazi kuwa alikudanganya, maana utakapomuuliza hivi Bwana wewe uliyapata wapi mafundisho haya yaliyokuwa kumbe si yenyewe? halafu yeye atakuwa akikwangalia tu bila ya kukujibu neno, utajisikiaje, au utaona anakufanyia dharau? WAPENDWA TUJIFUNZENI NENO LA MUNGU KWA MIOYO ILIYOTAYARI KATIKA KUIJUA KWELI, MAANA KWELI NI NENO LA MUNGU NALO NENO LITATUWEKA HURU, NENO LOLOTE AMBALO LINAELEZWA KWA MITAZAMO YA WATU (THEOLOJIA) NA HALIKUANDIKWA KAMA LINAVYOSEMWA TULITAFAKALI KWA MAKINI KABLA YA KUKUBALI!
  Mwendelee kubarikiwa na BWANA YESU KRISTO.

 153. Ndugu yangu Kinyau, ni kweli, nguvu ya roho za cults ni kubwa saana, na zinang’ang’ania saaana kupita ung’ang’anizi wa Farao! Wanatembea na kanda za mafundisho ya Kisabato moyoni mwao, umeiona hii aliyoifungulia Nashon!!?

  Ukweli ni kwamba akina Nashon wamepotezwa njia na wanaendelea kutokomea! Sabato wanayoing’ang’ania ni ya Kiyahudi, wakati wao ni wa Mataifa, wamejichanganya vibaya sana! Au labda ni waFalasha wa kiroho!!!

  Kwanza, Mungu anasema tufanye kazi siku sita na ya saba ndio tupumzike!! Hakuna Andiko linalosema tupumzike Jumamosi!!! Tena basi Sabato halisi si hii wanayoigiza akina Nashon. Ukirudi ktk uumbaji utaona kwa uwazi kabisa kuwa ile siku ya saba ilikuwa ni pumziko lake Mungu na si mwanadamu. Wala hakuna mahali si Adamu wala Ibrahimu wanapopewa maagizo ya kuitunza siku hiyo. Hata ukizitazama siku hizo sita za uumbaji utaona: “ikawa asubuhi…. ikawa jioni” Lakini kwa siku ya saba hakuna asubuhi wala jioni, ni eternity, Mungu alirudi ktk umilele! Hiyo ndio Sabato halisi, hii waliyopewa Israeli ilikuwa ni kivuli tu cha hiyo halisi ambayo sasa kanisa linaingizwa ktk Kristo, yaani ile predestination ikijidhihirisha kwa wana wa Mungu wakiungana naye tena baada ya kutengwa na dhambi! Mambo haya ni vigumu kueleweka kwa walioikataa Injili ya Kweli wakawasikiliza manabii wao wa uongo, na kwa huo uongo walioumeza wamekusanywa kuwa jeshi kuuubwa linaloipinga Injili!!! 

  Hebu yatazame Maandiko, yote yanawaonesha Mataifa kuwa ninyi hamhusiki na Sabato ya Kiyahudi, yaani Mungu akiwafafanulia tena na tena, lakini wameziba masikio ya mioyo yao kwa nta, mpaka anawauliza “Mmerogwa?” Wamerogwa kweli, na wamerogeka! Kama nabii wa kweli kwa ule upako uliojuu yake anavyokuunganisha na Mungu na ukaokolewa, hata nabii wa uongo vivyo, kwa upako uliojuu yake, ambao unajumuisha na ulozi, naye anakuunganisha na kuzimu bila kujijua akiijiwakilisha kama malaika wa Nuru. Ndio maana ukiwauliza ni wapi ninyi watu wa mataifa mlipo itwa mkapewa hizo Amri Kumi? Kumbe maskini hata amri zenyewe hawazijui, wanaijua hiyo ya Sabato tu, ambayo pia wamedanganywa kuwa ni Jumamosi; nadhani yule nabii wao aliwaambia iliandikwa hivyo kwenye vile vibao alivyovivunja Musa!

  Basi Ndugu yangu Kinyau, tukiyarejea Maandiko ili kukiona kinachoendelea, hali inatisha sana. Hebu liwazie jambo hili: kwamba Kristo leo hii yuko ndani ya mwaminio kama alivyoahidi (Mt 28:20), basi Kanisa leo hii ndiye Kristo. Kwa hiyo ulipomkatia tamaa ndg Nashon, kulingana na alivyoishupaza shingo yake, basi iwapo Kristo amekukatia tamaa, yaani lile Neno, utaokolewa na nani tena!?? Unajua wengi wetu kwa uoga wa kuhukumiwa, hujaribu kuisogeza Hukumu huko mbele, ni kujidanganya, Neno lipo kamili nalo linaendelea kuuhukumu ulimwengu wa Kidini hata saa hii likiwa limejificha ndani ya waaminio, likiwatenganisha kondoo na mbuzi!!!

  Mbarikiwe nyote mlio katika pumziko la milele ktk Kristo, ile Sabato!

 154. Habari za leo wapendwa? nina iamni mtakuwa wazima.
  Napenda kumshukuru Mungu kwa kuiwezesha hii blog kwa kuwekwa huu mjadala
  Kwa maana wengi wameujua ukweli wako na wengine nina imani waujua pia…

  Vilevile napenda kuwashuru wachangiaji ambao wameonekana kutetea maandiko ya Mungu kama biblia inavyosema na wala siyo kama mapokeo ya wanadamu. Hawa ndugu ni wafuatao, Michael John Nzala, Lenda na Gabriel Mashambo.

  Hivi ni nani aliyekuwepo hapo awali kabla ya mwenzie, yaani kati ya Mungu na mwanadamu?

  Jibu linapatikana katika kitabu cha Mwanzo 1:1, “Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi. ” Mwanzo 1:28, “Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.”

  aaah! kumbe mwanadamu aliumbwa na Mungu na siyo binadamu amemuumba Mungu…!
  Sasa kwa nini mwanadamu wanatii amri za Mung nusu…..!?
  Ama mtu akiongeza wala kupunguza Mungu atamfurahia..!?
  Hebu soma nami katika kitabu cha KUMBUKUMBU 4:2, “Msiliongeze neno niwaamurulo wala msilipunguze, mpate kuzishika amri za BWANA , Mungu wenu, niwaamuruzo.”

  Je maandiko ya Mungu yana faida gani kwa mwanadamu..?
  soma tena nami katika kitabu cha 2 Timotheo 3:16-17.

  2 Timotheo 3:16-17 “Kila andiko lenye pumzi ya Mungu lafaa kwa mafundisho na kwa kuonya watu makosa yao na kwa kuwaongoza na kwa kuwaadibisha katika haki; ili mtu wa Mungu awe kamili amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema.”

  Pamoja na mafungu hayo machache niliyoyatoa, naomba niitishe kwa kuangalia chuo cha Nabii ISAYA 66:22-24

  22 “Kama vile mbingu mpya na nchi mpya, nitakazofanya, zitakavyokaa mbele zangu, asema Bwana, ndivyo uzao wenu na jina lenu litakavyokaa.”

  23 “Na itakuwa, mwezi mpya hata mwezi mpya, na sabato hata sabato, wanadamu wote watakuja kuabudu mbele zangu, asema Bwana.”

  24 “Nao watatoka nje na kuitazama mizoga ya watu walioniasi; maana funza wao hatakufa, wala moto wao hautazimika nao watakuwa chukizo machoni pa wote wenye mwili.”

  Ni afadhali kutiwa upofu na usabato (amri za Mungu) kuliko kutiwa upofu na amri za mwanadamu.

  Amani ya Bwana iwatawale.

 155. NASHONI

  Pole sana.

  Neno ndio msingi wa yote hapa duniani.
  kwa mantiki hiyo biblia ni mambo ya rohoni huwezi kuyapambanua kama hauna Roho Mtakatifu hivyo unaposoma neno au kutaja neno kila neno lina maana yake na wewe uliyelitaja una maana yako ndio maana ukataja neno husika. pamoja na yote wewe maneno yako yanafanya neno la MUNGU Kuwa maneno sio neno kama alivyokusudia MUNGU BABA KTK JINA LA YESU KSIRITU WA NAZARETH.

  Siku yoyote ukitaka kutamka neno lolote muulize kwanza Roho nitamke, akikupa kibari tamka kama hajakupa kibari kaa kimya.

  Hivyo kama unamtumikia MUNGU fuata taratibu zake za msingi.

  Kwa mfano. mtu anayekubali kufundishwa ni muungwana maana amechagua jambo jema ikiwa na maana kwamba mtu huyo amekubali KUFUNDWA na akifundwa AKASHIKA atahesabiwa kuwa AMEFUDWA-AKASHIKA kwa kifupi zaidi atakuwa AMEFUNDISHIKA.

  Pia ktk yote UMAKINIFU ni muhimu sana katika mambo yote maana mtu ambaye si MAKINI hawezi KUMAKINIKA au KUMAKINISHA wale wanaoitaji KUMAKINISHWA maana ndani mwake hakuna UMAKINISHO, ambao utampelekea muitaji kuwa MAKENIKA makinifu.

  Ukisoma BIBLIA (WAEBRANIA 5:11-14) unaona kuwa MUNGU anataka watu wasio na kibiri na ambao wanakubali kurudi nyuma kufundishwa ata kama ameisha anza kuwatumia akiwa na maana kuwa ata kama unatumika bado unaitaji kufundwa.

  Kuna mtu alikuwa mbishi kama wewe alipoambiwa kuwa kifupi cha YERUSALEMU ni YESU akauliza swali kuwa kama ni hivyo hicho ni KISWAHILI je kwa KINGEREZA Akapata jibu kuwa JERUSALEMS Kifupi chake ni JESUS Akaona iweje nishindwe akauliza imeandikwa wapi?

  Sasa huo ni uchanga kiroho maana wa kuulizwa maswali zaidi unaposikia ujumbe wowote kutoka kwa binadamu mwenzako hili uakikishe muulize Roho Mtakatifu.

 156. Ndugu Lwembe,

  Ubarikiwe kwa yote unayojaribu kumuelimisha Nashon. lakini kwa jinsi ambavyo nimesoma machapisho yake ndani ya blog hii, kamwe hawezi kuelewa kwa sababu u-sabato wake umemtia upofu, anasoma maandiko ya Mungu kwa jicho la kidhehebu yaani kwa jicho la Kisabato. Kila asomaye neno la Mungu kwa jicho la dhehebu kamwe hawezi kuona kweli iliyopo ndani ya neno na hivyo hawezi kuwekwa huru na kweli hiyo, ataendelea kuwa kwenye kongwa la kidhdhebu mpaka mwisho wa maisha yake.

  Nasi tutaendelea kumshangaa kama Mtume Paulo alivyowashangaa wale Wagalatia hadi kufikia kusema wamerogwa na nani!!! Kwa lugha nyingine ni kwamba Paulo alikuwa anawashangaa kwa nini hawa watu hawauoni ukweli uliowekwa na yeye wazi kabisa machoni pao. Ndivyo pia sisi tunavyomshangaa Nashon kwa nini hauoni ukweli huu kwamba kila anayeenenda kwa sheria wakati huu baada ya sheria kutuleta kwa Kristo, mtu huyo amekufa ingawa bado yupo anatembea.

  Mimi sidhani kama nina haja ya kuendelea kujibizana na Nashon, ninachoweza kukifanya ni kumuombea kwa Mungu ili Mungu mwenyewe afungue macho yake ya rohoni na masikio ya ndani ili aweze kuonana kusikia wazi wazi juu jambo hili na Mungu aingilie kati kumtoa kwenye kifungo cha dhehebu kama alivyomtoa Mtume Paulo kwenye kifungo kama hicho.

  Barikiweni nyote

 157. Ooh, ndg Nashon,
  Ninajaribu kurudi nyuma katika wakati. Ninajiona nilivyokuwa mzabibu pori, niko katikati ya ibada za mizimu ya kwetu, tunamwaga pombe na damu ya ng’ombe wa sadaka kuuzunguka mti mkuuubwa! JICHO la MUNGU likinitazama na kunihurumia kwa jinsi ninavyojichafua! Yeye Mungu akinijua mimi ni nani, kwa kadiri alivyoniumba, mimi ni UDONGO (Mw 2:7 “BWANA Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi”), ule alioulaani kule Mwz 3:17 “… ardhi imelaaniwa kwa ajili yako”; huo ndio mimi na wewe!! Kisha kwa Huruma yake akaanza kazi ya kutukomboa, akimchagua mtu mmoja tu kuwa kielelezo cha ukombozi wetu, Ibrahim. Kutoka katika kiuono chake limezaliwa taifa la Israeli. Basi ndugu yangu Nashon, hata siku ile ya Ijumaa aliposulubiwa Kristo, mimi na wewe tulikuwa bado tuko kwenye mizimu yetu, hatuna Sabato wala Amri Kumi!

  Hao waliopewa hizo Amri Kumi, ziliwashinda vibaya sana! Katika mpango huo wa Mungu, hawezi akaanza na mimi wa mizimu bali anaanza na hao aliowachagua kuwa kielelezo. Waliposhindwa kuzishika Sheria ndipo akaleta mpango mpya. Sasa huwezi kumbishia Mungu kwa kile anachokuletea maana yeye huyajua yote. Hata hizo sheria zilizowashinda, si kwamba yeye hakujua kuwa zitawashinda, hapana, bali ilikuwa ni ktk hatua za kuuendea ukamilifu kama alivyotutayarishia. Hebu wazia hili, kwanini wale watakatifu wa Agano la Kale hakuna aliyeingia mbinguni kwa sheria?

  Kwa hiyo hata Kristo aliposulubiwa na Damu yake kumwagika juu ya nchi, ikiikomboa ardhi, ule mwili, yaani sote, Israeli na sisi wa Mataifa katika siku ile pale Kalvari, hata siku ya tatu alipofufuka mimi na wewe tulikuwa bado tuko kwenye mizimu yetu, hatujui chochote kuhusu hilo licha ya kujumuishwa kwetu!

  Hakuna wa Mataifa aliyekuwemo katika Ufufuo wa Kwanza baada ya ile DAMU KUIKOMBOA ARDHI! Pia hawatakuwemo wote wanaoendelea katika Sheria katika Ufufuo wa pili wakati wa kuja kulinyakua Kanisa, maana huo ni kwa wale waliosafishwa kwa ile Damu ambayo ilikuwa ndani ya Viriba vya Kibinadamu (mitume), waliyopewa ili tunyunyiziwe sisi wa Mataifa (Eze 36:25) ili tusafike kama Mungu alivyotukusudia, alipowatuma hao, Mark 16:15-16.

  Nashon, inasikitisha jinsi unavyovibeba vifungu vya Maandiko na kwenda kujishtaki navyo mwenyewe kwa Hakimu. Wewe mwenyewe unajua fika kuwa umebatizwa ubatizo wa Kisabato ambao Mungu hautambui, halafu unabeba vifungu vinavyokushtaki unampelekea! Katika Hukumu zake Mungu hawatazami wanaojipendekeza, anawatazama watumishi wake tu! Mtazame Abimeleki, alikuwa na haki juu ya jambo alilolifanya pale alipomchukua Sara maana Ibrahimu mwenyewe alikiri kuwa yule ni dada yake (ingawa ni kweli alikuwa ni dada yake), lakini Mungu alimwambia UMEKUFA usipomrejesha kwa Ibrahimu! Tena si kumrejesha tu halafu yaishe, hapana, alitakiwa aombewe na Ibrahimu ndio apone!! Sasa ninyi mnaoibishia Injili ya Paulo, kweli hamjarogwa nyie kama Paulo mwenyewe anavyowashangaa?? Paulo amefundisha kwa pumzi kubwa saaana, ili kuliondoa fundisho potofu hilo la sheria kwani linaikataa kazi ya msalaba! Mnaambiwa Sheria kwa mkristo imekufa maana yeye ndiye SHERIA sasa hivi “Je, hamjui kuwa mtauhukumu ulimwengu?”

  Kwa taarifa yako hakuna mkristo anayejitahidi asiuwe au asizini, au asiseme uongo au asimchukie Msabato nk! Mtazame kunguru, je, hujitahidi asile mizoga? Au njiwa, je, hujitahidi kujizuia asile mizoga? Hao ni ndege wawili walio na asili tofauti, vivyo mkristo anapozaliwa mara ya pili, Roho wa Mungu hukaa ndani yake kumuongoza, basi hiyo ndiyo tofauti yetu. Mungu akiwa ndani ya kanisa hawezi kuliongoza kusanyiko kinyume na Upendo wake, hata ikiwa ni Jumapili!!

  Basi ndugu yangu Nashon, jihadhari na Injili, maana mtume Paulo anasema Kristo atahukumu kwa Injili yake, sijui mtakwepea wapi!

  Mbarikwe nyooote mliowapokea mitume!!!

 158. Ndugu Mlaki JB ama umesahau mafundisho yale yaliyo mema katika kitabu cha…
  UFUNUO 22:18 “Namshuhudia kila mtu ayasikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mtu ye yote akiyaongeza,
  Mungu atamwongezea hayo mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki.
  19 Na mtu ye yote akiondoa lo lote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima, na katika ule mji mtakatifu, ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki.”

 159. Hakika manabii wa uongo wataibuka siku za mwisho kama biblia inavyonena….!!??

  Hivi ndugu Mlaki JB unaweza kusema ni wapi kwenye biblia ikasema kuwa zamani ibada ilikuwa ni siku ya ijumaa, na jumamosi ilikuwa ni siku ya kwanza ya juma na jumapili siku ya pili ya juma….!!!??

  Kweli huko kwenu nyie ndio mnamwabudu Mungu wa kweli….!
  pole sana rafiki..!
  Kwa nini maandiko mnayabadilisha hivi hivi…!?
  Ama umesahau andiko linalosema kuwa

  Unaweza kuonesha ni wapi Yesu alibadilisha siku ya saba ya juma na kuwa jumapili..!?
  Je ni fungu gani ndani ya biblia linaonesha kuwa Yesu alifufuka siku ya saba ambayo ndio jumamosi uliyoitaja hapa juu..!?
  Nina wasiwasi kanisa lako unalolisifia…..!?
  Kwa kusaidiana naomba usome Mathayo 28:1, nna imani utabarikiwa sana.

  Halafu ndugu CK Lwembe, Amri za Mungu hizo kumi unazoziona, hata kama utazivunja zifike elfu moja, lakini chimbuko ni huko kwenye amri unazoziona katika kitabu cha kutoka……..!

  Ndugu CK Lwembe unamisha kuwa watu wasisome agano la kale… kama ni hivyo basi biblia ingekuwa na agano jipya. kukataa agano la kale ni sawa na kumpinga Muumba wako…….! mwogope sana Mungu kwa huo uwongo mnaoendelea nao… kwa maana lango lile kinyonge hakitaingia.

  Sasa ndugu Kinyau inaonekana hujasoam biblia vizuri kama umesoma basi rudia kusoam tena na utaelewa ni siku gani mtu anapaswa kutenga katika kumwabudu Mungu, soma Kutoka 20:8-11.
  Mwanzo2:2-4 na mengine mengi ambayo tumeyataja hapo juu toka mjadala umeanza na hat ambayo hatujataja unaweza ukafungua bibli yako usome upate maarifa. acha kufuata mapokeo ya mwanadamu…

  Je wewe Kinyau unadhani Yesu alikuwa na desturi ya kuingia kwenye masinagogi siku gani ya juma…?
  ukishasoma na kupata majibu. basi utakuwa umeelewa, ukishelewa wajulishe na wenzio.

  Kwani mmesahau Yesu alivyosema ya kuwa katika kitabu cha Mathayo 5:17-20 “Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii. La! Sikuja kutangua, bali kutimiliza. Kwa maana, amin nawaambia, mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie. Basi mtu yeyote atakayevunja amri moja katika hizi zilizo ndogo na kuwafundisha watu hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni. Bali mtu atakayezitenda na kuzifundisha, huyo ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni. Maana nawaambia ya kwamba, haki yenu isipozidi hiyo haki ya waandishi na Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.”
  Warumi 7:12 “Basi torati ni takatifu, na ile amri ni takatifu, na ya haki, na njema.”

  Sasa ukitaka kuamini SABATO ni ya milele, soma nami katabu cha ISAYA 66:23-24. 23, “Na itakuwa, mwezi mpya hata mwezi mpya, na sabato hata sabato, wanadamu wote watakuja kuabudu mbele zangu, asema Bwana.”
  24 “Nao watatoka nje na kuitazama mizoga ya watu walioniasi; maana funza wao hatakufa, wala moto wao hautazimika nao watakuwa chukizo machoni pa wote wenye mwili. ”

  Ufunuo 22:10-15 “10 Akaniambia, Usiyatie muhuri maneno ya unabii wa kitabu hiki, kwa maana wakati huo umekaribia.

  11 Mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu; na mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu; na mwenye haki na azidi kufanya haki; na mtakatifu na azidi kutakaswa.

  12 Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo.

  13 Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho.

  14 Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake.

  15 Huko nje wako mbwa, na wachawi, na wazinzi, na wauaji, na hao waabuduo sanamu, na kila mtu apendaye uongo na kuufanya. ”

  Ufunuo 22:18-20 “18 Namshuhudia kila mtu ayasikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mtu ye yote akiyaongeza, Mungu atamwongezea hayo mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki.

  19 Na mtu ye yote akiondoa lo lote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima, na katika ule mji mtakatifu, ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki. ”

  Mbarikiwe ndugu.

 160. @ ndg Kinyau
  Asante kwa understanding! Unajua, ndg yangu Nashon ameniona nimetumia pumzi nyingi na “matusi”, ni kwa vile tu hana mazoea ya kujifunza au kuyasoma maandiko privately, badala yake yeye hujifunza kutoka kwa walimu wa dini (teologia) na kuyarejea Maandiko kwa kuongozwa na masomo yaliyotayarishwa na walimu hao na hivyo kukosa uhuru unaoweza kukufungua kutoka vifungo vya kidhehebu pindi unapoyapa Maandiko nafasi ya kujitafsiri.

  @ Ndg Nashon
  Agano la Kale ni la mwilini na Agano Jipya ni la Rohoni. Basi kumjia kwako Mungu kunatambulika katika Maagano hayo tu. Haiwezekani ukawa katika Maagano yote mawili kwa wakati mmoja!

  Ktk A/J mwili wa Kristo ni mitume. Kifungu ulichokinukuu cha Mt 28:19 kingekudhihirishia hilo kama ungekuwa umejiachilia ktk Maandiko. Tazama, “… mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.” Basi huwezi ukasema unampenda Kristo halafu usiwatii mitume, utakuwa ni mtu usiyekielewa unachokisema, maana hao ndio Kristo!!! Basi hata Paulo alipokuwa akiwakemea Wagalatia, iwapo bado uko mwilini, yaani hujavushwa kuja Rohoni, utawafikiria wale Wagalatia wa mwilini, lakini ukweli ni kwamba wale walikuwa ni kasampuli tu ka kundi kuuubwa la sasa linaloongozwa na roho ile, maana roho hazifi! Kumpokea Kristo, halafu kurudi nyuma na kujitahidi kuzitimiza Sheria, ndiko “ Kuanzia Rohoni na kuishia mwilini” anakokusema mtume Paulo. Tena anawasisitizia Laana wote wanaofundisha Injili tofauti na hiyo aliyowahubiri, hiyo inayowatoa ktk Sheria Mataifa, sasa sijui mnaujasiri wa jinsi gani kukaidi jambo la wazi kama hili!!

  Ndugu wengi wamekunukulia vifungu vingi vya Maandiko kukuonesha kuwa KANISA kama kusanyiko HALIJAWAHI kukutana siku ya Sabato. “Siku ya Bwana”, haijaitwa hivyo kwa bahati nzuri au mbaya. Wala hakuna jambo linalojifanyikia lenyewe tu, si duniani wala mbinguni bila kusudi la Mungu. Kama umewahi kuimba ktk kwaya, utauelewa umuhimu wa kumtazama kiongozi kwa makini, ili beat linapobadilika usiachwe nyuma na kuvuruga pattern nzima ya wokovu kama mnavyofanya Wasabato! Kiongozi wetu wa wokovu ni Kristo, hajawahi kuondoka, Yeye alikaa ndani ya mitume akiendelea kuhudumu, akii-magnify sheria na kutuingiza ktk mfumo mpya uliokamilika ambao kwao sasa sisi ni wana tukiwa tumekwisha kutolewa katika utumwa wa dhambi, na sheria zake na laana zake!

  Kanisa, ndugu yangu Nashon haliko mwilini tena bali rohoni ndio maana liko juu ya sheria. Sheria zinawahusu watu wa mwilini au watumwa katika himaya yoyote ile. Nazo sheria huambatana na adhabu, yaani laana. Basi kwa adhabu watumwa hujengwa katika tabia ya kuzitii sheria nao hujibidiisha ktk hizo. Lakini wana wa Mfalme sheria haziwahusu. Kwani hizo zimewekwa ili kuwaongoza hao walio gizani ili kwa hizo sheria, zikiwa ni mfano wa nuru ya kurunzi, ziwalete katika NURU kamili ambayo ni KRISTO, hata watumwa hao kufanyika Nuru na hivyo kubatilika kwa matumizi ya tochi! Nuru ya tochi ktk usiku wa giza totoro ni baraka sana, lile pumziko la Sabato, walilopewa Israeli katika safari yao ya kuujia wokovu. Lakini sisi tuko katika Nuru Kamili sasa! Hata hizo Sheria hazikuwa tu amri kumi, hapana, ziko zaidi ya mia sita! Kuzizungumzia amri kumi tu ni kujidanganya, yaani kujitoa akili, vinginevyo unapaswa uzishike zote ndio uHesabiwe Haki kama unataka kuikimbia laana inayoambatana sheria, jambo ambalo HALIWEZEKANI!

  Hivi Nashon, hizo nukuu ulizoziweka hapa, hizo zinazowaonesha mitume wakihudhuria ktk masinagogi “yao”, ndio tuseme kuwa wewe unaamini kuwa wakiwa humo ndani walikuwa wanaihubiri Injili wakiwaita wagonjwa wawaombee na mwisho kuwaambia kusanyiko kuwa “Wanaokubali kumpokea Bwana Yesu Kristo kuwa BWANA na Mwokozi wa maisha yao wapite mbele!”?? Acheni kujitoa akili, licha kuendelea kuhudhuria ibada za Sabato kwa desturi, bado uwepo wao ulileta mabishano ambavyo mwisho hawakutakiwa tena na wenye masinagogi “yao” na hivyo kuendelea na makusanyiko yao ktk siku hiyo ya Bwana ktk kuileta ktk ukamilifu ibada takatifu ambayo wao pia ni mashahidi wa matendo makuu ya Mungu, kwani hapo ndipo yalipozaliwa makusanyiko mawili pacha kama Esau na Yakobo; kundi moja la Mwilini na moja la Rohoni. Si kwa mapenzi yao, la hasha, kwa Mapenzi Makamilifu ya Mungu akilitimiza Neno lake!

  Sasa ninyi ndugu zangu kwa kadiri ninavyowaona, hamko katika kundi lolote kati ya hayo mawili, yaani Hamko katika Mapenzi ya Mungu kama yanavyojiwakilisha. Maana Mungu anasema nalimchukia Esau (hiyo ni kabla hajazaliwa!), yaani kiulinganishi, Mungu aliwapofua Israeli wasiingie katika Sabato halisi ili sisi tuingizwe humo kwanza, sisi tusiostahili. Halafu amesema atawafungua macho nao waingie, je, ninyi mna ahadi gani ya kuondolewa huo upofu mliojitakia, kama huko si kurogwa ni nini?

  Halafu Nashon unaniambia, “Sasa umeujua ukweli….. fanya maamuzi ubatizwe kwa maji mengi kama yesu alivyobatizwa mtoni Yordani…..
.” Unajua ndugu yangu, labda kwa jambo hili unaloniasa, laweza kuwa ndio UFUNGUO wa “pandora’s box”, kwani tunaweza kuwa wa mwilini tunaojidhanisha kuwa ni wa rohoni, kwa hiyo mjadala wetu usitunufaishe kabisa! Basi hebu jaribu kutazama iwapo umebatizwa sawa sawa ili kuwa mkristo au walikuloweka tu mtoni kwa “Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mt” badala ya kukufanyia ule ubatizo wa kweli kama alivyoutimiza Kristo mwenyewe akiwa ndani ya mitume (kitabu kizima cha Matendo)! Huenda ukilitatua hilo utaingizwa ktk urithi wa ahadi zote za rohoni na hivyo ule utaji kutolewa na Injili kuwa Mpya na tamu badala ya kubaki utumwani.

  @ Ndg Lenda,
  Hivi unayo taarifa kuwa uongozi wenu wa juu ulikwisha tia saini kurudi Roma? Kumbukumbu zinanionesha hivyo, na pia kuwa mlitaarifiwa wote muache kuwasakama Wakatoliki na vitabu vyenu vile vya “666” mviondoe ktk mzunguko. Ndio maana ninakushangaa unapowahusisha wakatoliki na uongo wa kiteologia wa madhehebu mbali mbali au ninyi Tz wote ni wale Masalia?

  Mbarikwe Nyoote!

 161. Ndg Mlaki JB,
  Umenitoa kapa!
  Hata hivyo kanisa lenu liko wapi, ili tuwalete hao wa kundi la kwanza wanaosali J’mosi?

 162. IBADA ya jumapili. Hapo mwanzo jumapili ilikuwa siku ya pili ya juma, ibada ilikuwa ni ijumaa hila zoezi lilibadilika kwa kukamatwa mwana mpendwa wa Baba yetu wa mbinguni Yesu Kristo ambaye alitoka kaburini siku ya kwanza ya juma yaani juma-mosi ikapelekea kuwepo kwa mgawanyiko wa utatu ktk habari ya ibada wa kwanza waliposikia amefufuka wakakimbia saa hiyo hiyo na kuanza ibada maana walishindwa kuingia kwenye ibada walibaki kuangalia kitu gani kinaendelea kwa kukamatwa kwake MWOKOZI. hao leo hii ndio wana ibada juma-mosi.

  Kundi la pili liliamua kufanya usafi ikiwa ni wa mwili mpaka wa kiroho-toba- maana walijuwa kuwa inabidi ujipange kuingia Patakatifu na patakatifu pa patakatifu hivyo hawa wakaingia kanisani juma-pili baada ya kuona majibu ya Kristo Yesu wa Nazareth. Kundi hili ndio tunasali juma-pili.

  Kundi la tatu wao walikataa kujihusisha na walisema huyo si mwana wa MUNGU huyo ni Binadamu kama cc wakasahau kuwa hapo tayari wanakiri kuwa huyo ni MUNGU maana kama c mwana wa MUNGU ni nani basi? maana ata wao ni wana wa MUNGU, Kundi hili bishi liliendelea kafanya IBADA siku ya ijumaa mpaka leo.

  AMINI YESU NI MWEMA YOTE HAYA NI KWA AJIRI YA WANAOKUBALI NA WANAOKATAA Kanisa letu ni dogo maana liko ktk mji mgumu kwa imani tumerudisha misukule 105, HIV AIDS tumeponya watu 398, kansa, utasa, kufungua vipato, nk zaidi ya yote wanaongoza kufunguka ni wale wanaomkana YESU Wamefunguka Chini ya Pastor Kiongozi Mlaki Jeremiah Mlaki.

  MUNGU AKUBARIKI NA KUNA NGUVU YA MUNGU INATENDE KAZI NDANI MWAKO NAWE UNAKUWA HURU KTK JINA LA YESU Kristo WA NAZALETH.

 163. Wapendwa,

  Inasikitisha sana pale mtu anaposhindwa kuuelewa ukweli wa neno la Mungu ulio wazi kabisa.
  Ndugu Lwembe, nakupongeza sana kwa machapisho yako mawili ya jana tarehe 4 Sept 2012, you expressed yourself clearly and vividly. Namshangaa sana ndg Nashon kwa kusema kwamba umetumia pumzi nyingi na kutoa matusi, kitu ambacho mimi sijakiona kwenye hizo post.

  Hata hivyo ni muhimu ndg Lwembe kutumia pumzi kubwa kwa sababu Shetani amekamata shingo za watu na kuzishupaza sana kiasi kwamba hata mtu akieleza kwa lugha nyepesi kabisa kama alivyofanya ndg. Lwembe, bado akina Nashon na wengine hawaelewi.

  Shida kubwa niliyoiona hapa ni kwamba watu kama akina Nashon wanadhana au wanaelewa kwamba amri za Mungu ni zile kumi tu zilizotolewa katika Torati, huu sio ukweli wa Neno la Mungu kwa kuwa katika Agano Jipya amri au sheria za Mungu ni jumla ya maneno yote ya Mungu yaliyomo ndani ya Biblia ambayo Mungu anayaandika ndani ya mioyo ya kanisa (waamini) baada ya kumpokea Yesu Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wao.

  Mimi naamini kwamba muumini wa kweli (kanisa) anapaswa kumwabudu Mungu wakati wote, mahali popote na siku zote, ila taratibu za siku ya kukusanyika kwa waumini linabaki kwa hao waumini wenyewe, maana sijawahi kuona katika maandiko yaani neno la Mungu mahali palipotajwa majina ya siku kama tunavyozijua sasa. Mtume Paulo alisema msiache kukutanika kama ilivyo desturi yenu……. Kwa maana hiyo siku ya kuabudu kwangu mimi si hoja, hoja ipo kwamba Mungu anaabudiwa katika roho na Kweli? (Yohana 4:24). Angalia neno linavyosema ukisoma sura hiyo kuanzia mstari wa 23;

  “Lakini saa yaja, tena ipo, ambapo wale waabuduo HALISI, watamwabudu Baba katika roho na kweli. Watu wanaoabudu NAMNA HII (yaani katika roho na kweli), NDIO BABA ANAWATAFUTA. Mungu ni Roho na WOTE wanaomwabudu IMEWAPASA kumwabudu katika roho na kweli” (maneno ya kwenye mabano ni yangu).

  Nashon, Neno hapo juu halijasema Mungu anawatafuta wale waabuduo siku ya Jumamosi au siku ya Jumapili, bali linasema Mungu anawatafuta wanaoabudu katika roho na kweli kwa sababu ibada haiko katika siku bali ibada ya kweli ipo katika roho ya anayefanya ibada hiyo!

  Baraka kwenu nyote.

 164. Ndugu Ck Lwembe. kutumia pumzi nyingi wala kutoa matusi hakuhitajiki …. sana sana ni roho mtakatifu, ndio ukiongoze katika mjadala huu.
  Umeusikia ukweli na kuukataa shauri yako……!?

  PETRO 5:29 “Petro na mitume wakajibu wakisema, imetupasa kumtii Mungu kuliko kumtii mwanadamu.”

  YOHANA14:15 “Mkinipenda mtazishika amri zangu.”
  hivyo ndivyo Yesu alivyoamuru…. sijui wewe unampenda kwa kutii amri tisa, nane ama kumi….!?

  2 TIMOTHEO 3:16-17 “Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema.”

  MITHALI 30:5-6, Kila neno la Mungu limehakikishwa; Yeye ni ngao ya wamwaminio. Usiongeze neno katika maneno yake; Asije akakulaumu , ukaonekana u mwongo.

  ISAYA 40:8 “Majani yakauka, ua lanyauka; Bali Neno la Mungu wetu litasimama milele”

  Je! ni ibada gani ambayo Mungu anaonya isiyo ambatana na amri za Mungu. Imeandikwa,
  Mathayo 15:9 “Nao waniabudu bure wakifundisha maagizo yaliyo maagizo ya wanadamu..”

  Sasa umeujua ukweli….. fanya maamuzi ubatizwe kwa maji mengi kama yesu alivyobatizwa mtoni Yordani…..
  Kumbuka hili rafiki…
  Yesu akajibu, “Amin, Amin, nakuambia, mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuingia ufalme wa Mungu.

  Kwa kufanya hivi utaaza kutuza amri kumi za mungu ikiwamo amri ya nne na kutunza SABATO kama Yesu mwenyewe alivyofanya hata alipokuwa duniani. mafano huu hapa chini.

  LUKA 4:16 “Akaenda Nazareti, hapo alipotelewa; na siku ya sabato akaingia katika sinagogi kama ilivyokuwa desturi yake, akasimama ili asome.”
  Kwani
  LUKA 6:6 “Ikawa siku nyingine ya sabato Yesu alikuwa akifundisha katika sinagogi, na alikuwepo mtu ambaye mkono wake wa kuume uli kuwa umepooza.”

  Na hata Yesu alipofufuka, hakubadilisha sabato wala amri mpya ya kutunza siku ya siku ya kwanza ya juma, ila alichowaamuru wanafunzi wake, ni kuwafanya mataifa na kuwa wanafunzi wake na kuwabatiza ikiwa ni kuyashika maagizo (amri zote kumi) na kuishi kama Yeye alivyooishi duniani..

  MATHAYO 28:19-20 “Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;
  na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.”

  Yapo mafungu mengine mengi ambayo sijayataja yanavyodhihisha namna ambvyo Mwana wa Adamu alivyoabudu siku ya saba ya juma, (Sabato takatifu) katika masinagogi na siyo ya kwanza ya juma ilyotengenezwa na wanadamu….!

  UFUNUO 14:12 “Hapa ndipo penye subira ya watakatifu, hao wazishikao amri za Mungu, na imani ya Yesu.”

  Bwana akuongoze unapofanya, na kuwaongoza wengine pia wanapofanya maamuzi ya kujitoa kwa Yesu na kuachana na dhambi hii ya kutotii agizo la Mungu.

 165. Maandiko yanatufundisha wazi, kwa jinsi ya rohoni, juu ya kuyashika Maagizo ya Mungu na sheria zake. Yanasema, “lakini ijapo ile iliyo kamili, iliyo kwa sehemu itabatilika”. Sasa kama Torati ni kamili, wokovu au Kristo anahusu nini tena? Lenda unajaribu kumuhusisha Ibrahim na Amri Kumi, ni kwa Andiko gani? Au Adamu, ni wapi alipewa Amri Kumi? Maelezo yako yanayojaribu kuwahusisha na hizo Amri umeyaleta out of context. Neno la “kuzishika amri zangu” Mungu analolizungumzia halihusiani na hizo Amri Kumi. Amri kumi zinahusiana na Laana, ambayo hupozwa kwa sadaka ya kuchinja. Kwa hiyo yeyote aliye katika Sheria anapaswa aendelee kutoa sadaka za jinsi hiyo. Kujiweka chini ya Sheria halafu usitoe sadaka ya kichinja, ni zaidi ya upofu! Au kuipokea Sadaka (Kristo) inayobatilisha ule mfumo (sheria) uliokulazimu utoe sadaka kila wakati, halafu ukaendelea kujiweka chini ya Sheria, ni zaidi ya kudanganywa, ambako kunapelekea kuchanganyikiwa, kiroho! Hakuna Injili ya jinsi hii, ni ulaghai wa mapepo ya dini ambayo kazi yake ni kutengeneza na kuziimarisha CULTS, ambamo ndani yake waliomo hufungwa katika furushi la laana lisilo weza kukombolewa, maana hao walianzia Rohoni na sasa wanaishia mwilini, Damu ya kuwakomboa HAKUNA tena! Ebr 6:4-8

  Sheria za Mungu leo hii zinazozungumziwa si hizo amri kumi. Hizo zimeshindwa kutukamilisha, Mungu ametuletea jambo jipya. Tazama hapa anachotufanyia, si kwa jitihada zetu, hapana, bali katika Mapenzi yake Makamilifu yeye Mungu anatufanyia sisi ktk siku hii ya leo ili atuendeshe katika Sheria zake, tukizishika Hukumu zake na kuzitenda : Eze 36:26-27 anasema, anauondoa moyo wa jiwe, huo uliojaa uongo wa theologia, unaokataa kila Jema la Mungu, akiisha kuuondoa huo anatuwekea Moyo mpya wa Nyama. Kwa moyo huu mpya, sasa waweza kulipokea na kulihifadhi Neno la Mungu. Yaani huko ndiko Kuhesabiwa Haki. Hauhesabiwi Haki kwa kuzishika Sheria, la hasha, bali kwa imani “Kama vile Ibrahim alivyomwamini Mungu akahesabiwa haki.” Ukiisha kupewa huo moyo wa nyama, Neno la Mungu huhifadhika ndani yako na si Mapokeo. Baada ya hapo Mungu akatupa ROHO MPYA, sasa huyu si Roho Mt bali ni ule Utakaso. Basi kadiri Neno la Mungu linavyohifadhika kwa wingi ndani ya moyo huo mpya wa nyama, hilo ndilo lililotutakasa. Maana tulipo Hesabiwa Haki si kwamba tulistahili, la hasha, Mungu alitukubali pamoja na mapungufu yetu yote, ndipo akatufanyia upasuaji, akauondoa ujeuri wetu wote wa Kisabato au kidhehebu na mapokeo yake, akatuwekea moyo mpya na safi wa nyama, ndipo akaendelea na kazi ya kutuumba upya nje ya sheria na laana yake akiwa amevitupa katika shimo la usahaulifu! Mwisho wa kazi hii ya uumbaji mpya, ikiwa ndiyo kupiga Muhuri wake wa Ukamilifu, safari hii hakumuachia Lusifa atie Muhuri huo (Eze 28:11), yeye mwenyewe Mungu aliipiga Muhuri wa Ukamilifu kazi yake kwa kuwajaza Roho Wake kanisa (Efe 1:13), akiingia nao katika Pumziko yaani Sabato mpya,ambayo ni ya milele!!! Huo ndio mfumo mpya unaojiwakilisha katika Millenium kwa kanisa lililo ktk Wokovu kamili! Hakuna mtu anayeweza kumuingiza mwingine ktk Sabato hii mpya isipokuwa Mungu mwenyewe akuingize, “Hakuna awezaye kuja kwangu asipovutwa na Baba…”

  Lenda hebu sikia hii sauti, “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha”, kwa hiyo Lenda ikifika Jumamosi ndio unaokoka na mahangaiko yako ya kukimbizana na sheria? Kristo ndiye Sabato yetu!! Wote wanao ukataa wito huo hawataingia katika Pumziko lake!

  Angalia Lenda, Mungu anachokuonesha, Ebr 8:13 “Kwa kule kusema, Agano jipya, amelifanya lile la kwanza kuwa kuukuu. Lakini kitu kianzacho kuwa kikuukuu na kuchakaa ki karibu na kutoweka” Geuza hiyo shingo ngumu Lenda, isikilize Injili kwa unyenyekevu, sauti ya Mungu iko chini sana ili asitupasue ngoma za masikio yetu, punguza kelele za Mapokeo uisikie sauti yake ili nawe akufanyie Upasuaji!

  Mbarikiwe kadiri mnavyoipokea Habari Njema inayowatoa katika Konga la sheria mlilojivika kwa kurogwa!!

 166. “Enyi Wagalatia msio na akili, ni nani aliyewaroga…? Gal 3:1
  Ni rahisi sana kwetu kuwashangaa Wagalatia, lakini ukweli ni kwamba mtume Paulo hakuwa anaongea na hao tu, bali sote tutakaokumbwa na roho huyo aliyekuwa amewapagawa kama tunavyowaona Wasabato leo hii! Lakini pia twafahamu, kama tunavyooneshwa ya kuwa hao wamerogwa, yaani wametupiwa majini, sijui “jini makata”, akili zimewaondoka ndio maana wamechanganyikiwa na sasa wanajitambulisha na kundi ambalo si lao!

  Mungu ana makundi mawili; Kanisa (Yesu Kristo), na Israeli (Torati) ambayo yanajiwakilisha ktk Neema na Sheria. Makundi haya hayachanganyiki.

  Wokovu kwa Myahudi kwanza, halafu kwa Mataifa. Nayo safari yetu ya wokovu haifanani. Mapito ya Israeli, kwetu sisi ni rejea ya kumjua Mungu, Gal 3:24 “Hivyo torati imekuwa kiongozi kutuleta kwa Kristo”. Maagano ya Mungu kwa Israeli sisi hayatuhusu. Nchi ya urithi waliyopewa Israeli, ile Kaanani, ni tofauti na “nchi” tuliyopewa Kanisa! Kumbukumbu walizonazo Israeli ni tofauti na za kanisa. Pasaka ya Israeli huwarudisha Misri ktk kumbukumbu, lakini sisi huturudisha Kalvari!

  Mataifa hatukuipokea Torati bali Injili ya Yesu Kristo. Tazama Paulo anavyotushangaa, “Je, mmekuwa wajinga namna hii? Baada ya kuanza katika Roho, mnataka kukamilishwa sasa katika mwili?” Kanisa (Usabato), ambalo ni mzabibu mwitu, kwa Neema limekuwa grafted katika Kristo, na sasa linajiondoa katika Neema hiyo na kujipachika ktk nafasi ya Israeli, na kwa kitendo hicho kustahili kukatiliwa mbali, nalo halijui! Hii kama si ishara ya kuchanganyikiwa au unafiki au uongo tu wa kawaida ya waongo, ni nini? Wamerogwa!

  Kanisa haliko chini ya Sheria, sheria hazilihusu kabisa! Tunazisoma tu ili kupata uelewa wa mambo yalikotokea mpaka kutufikia sisi. Mtu yeyote anayejitahidi kuzifuata Sheria, huyo yuko mbali sana na Mungu, hajui hata kilichofanyika!! Kanisa halina jambo lolote la kutimiza, hata ikiwa ni Sabato katika yanayowalazimu. Sabato inawahusu Israeli, hao waliotoka utumwani, na sasa wanapewa Mwongozo wa ‘maisha mapya’ ya wokovu ktk nchi hiyo mpya wanamokwenda kuishi. Kumbuka maagizo ya Sabato kwa Israeli kama kanisa yamejitokeza kwa mara ya kwanza jangwani!

  Pia lazima kanisa lifahamu kuwa mitume walikuwa ni wayahudi, hao walio ktk Torati. Nao ujio wa Masihi uliwavusha kutoka ktk Sheria na kuwaingiza ktk SABATO ya milele, yaani Sabato ya kanisa ni Roho Mt! Najua jambo hili kwako Lenda linaweza kukutatiza. Lakini jaribu tu kurudi nyuma kidogo umtazame Kristo pale alipokuwa kazini. Yeye mwenyewe pamoja na wanafunzi wake walishutumiwa kwa kuivunja Sabato, kama zilivyo shutuma za leo. Majibu ya shutuma hizo yanaweza kuwasaidieni nyote mliojivisha konga la sheria, mkaikimbia Hukumu mnayoiendea!

  Sabato ilihusiana na Israeli katika kumwabudu Yehova. Wakijiwakilisha katika Sheria ili kuyatimiza yote yawapasayo, ndipo ile Rehema ya Mungu iwafunike pale uwepo wa Mungu unapojidhihirisha kwao. Kwa hiyo Mungu alipowapa amri hiyo ya Sabato, kwao iliwakilisha “PUMZIKO” katika harakati zao za kupambana na Sheria, hapo wanapoingia uweponi mwa Mungu wakijituliza na kumwabudu Yeye. Nayo amri hiyo husimama mpaka pale Mtoaji amri hiyo atakapoibatilisha, kama alivyotuletea Agano jipya!

  Lakini kwa Kanisa ni tofauti. Kanisa, kwa maana ya mwaminio, pale anapojazwa Roho Mt, kuanzia dakika hiyo yeye huingia katika PUMZIKO la milele. Huyo hamtafuti Mungu tena, anapumzika katika harakati zake za awali za kumtafuta Mungu maana sasa anaye ndani yake. Sheria zote hazina nguvu tena juu yake maana hizo ziliambatana na LAANA, lakini yeye akiisha uvua ule utu wa kale uliokuwa chini ya sheria, basi kwa yule Roho Mt yeye huwa kiumbe kipya, akiuvaa utu wa Kristo mfufuka, na kuenenda katika Nguvu zake zishindazo mauti, hiyo inayowakamata wote waishio chini ya sheria, na sasa ikibatilishwa kwa ujio wa NEEMA katika Kristo. Basi kwa yule aikataae Neema hiyo, huyo huikimbilia MAUTI kwa hiyari yake mwenyewe. “Je, ! Mlipokea Roho kwa matendo ya sheria, au kwa kusikia kunakotokana na imani? Wasiwasi wangu ni kuwa Wasabato wanaweza kuwa hawajui hata kwamba kuna Roho Mt; Mdo 19:2 “… Wakamjibu, La, hata kusikia kwamba kuna Roho Mt hatukusikia.” Lakini ninyi mnaong’ang’ania sheria leo hii, Neno liko wazi kuwahusu, “Kwa wale wote walio wa matendo ya sheria, wako chini ya laana” tena linaongeza, “Nidhahiri ya kwamba hakuna mtu ahesabiwaye haki mbele za Mungu katika sheria” basi ninyi wenyewe mwaweza kuipima hiyo roho inayowaongoza kuirudia Laana, je, si roho ya kujinyonga hiyo, ile iliyokuwa juu ya Yuda Iskariote???

  Basi uongo wowote ule haubadilishi ukweli wa jambo; haswa uongo wa kiteologia! Kama wapagani wa Kirumi walikuwa wakiabudu Jumapili kulingana na mizimu yao, nalo kanisa la Roma katika kuchanganya kwake mizimu na Injili, siku hiyo ikawa imelifavour katika kujumuisha ibada hizo mbili, jambo hili haliwezi kuugeuza ukweli wa Kimaandiko unaowaonesha mitume wakijikusanya siku ya jumapili kwa ajili ya kufundisha na kuumega mkate, nao mkate huo ukiwa ni Injili ya Yesu Kristo!! Au hamuijui “Siku ya Bwana” ni ipi? Bila ufufuo HAKUNA INJILI! Wakristo ni viumbe vipya, tumezaliwa katika Neema itokanayo na Msalaba, katika hiyo utu wetu wa kale ulitundikwa na Kristo pale msalabani na siku ya tatu, ile Jumapili, nasi tumefufuka siku hiyo ndio maana unatuona makundi yetu makubwa tukiwa katika shangwe hiyo pamoja na Mungu wetu!!!

  inaendelea….

 167. Ndugu A wakristu wengi hatujui maana ya Kuamini lakini pia imani inapatikanaje.

  ndugu unasema Anthony imani tu ndio itatuokoa lakini imani huja kupitia neno la Mungu.

  “Basi Imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.” Warumi10:17

  “Uzishike amri zangu ukaishi” Mithali 7:2

  ”Ziandike juu ya kibao cha moyo wako” Mithali 7:3

  Yesu alitumia maneno ya Biblia kumjibu shetani wakati wa majaribu yake.

  Neno la Mungu ni nuru, shetani hupingwa kwa nuru hii kwa kuwa yeye ni wa giza. Nakusihi usisahau kuweka moyoni neno la Mungu kadili anavyokujalia kwa neema yake ili iwe chepeo ya wokovu pale adui yako anapokushawishi lakini hata manabii wengine waliambiwa wameze magombo ya chuo maana yake kuyasoma na kuyatia moyoni. Na pale utakapohubiri si rahsi kuwaambia watu mafundisho ya mapokeo kwa maana roho wa Mungu atakukumbusha yote . Wakristu msiache kukariri mafungu kwa Neema ya Mungu.

  KUHUSU NUKUU ZA MAJIBU YA VIONGOZI MBALIMBALI WA DINI WALIVYOJIBU KUHUSU SABABU GANI ZINAWAFANYA KUABUDU JUMAPILI:

  ANGLIKANA

  “Na niwa wapi katika maandiko tunaambiwa tutitunze siku ya kwanza,tumeamriwa kuitunza siku ya Saba…….Isaac Williams,Plain Sermons on the catechism volume 1:334

  Watu wengi hufikiri kuwa Jumapili ndiyo sabato……Sabato ilikuwa na bado ni siku ya Jumamosi” Mchungaji Lionel Beer

  VIONGOZI WAEPISKOPO (EPISOPALIAN)

  “Tumefanya mbadiliko kutoka siku ya saba kwenda siku ya kwanza kwa kufuata mwongozo wa

  kanisa moja takatifu katoliki la mitume” Askofu Seymour kutoka kwa Kevin Morgan,Pumziko la Sabato

  VIONGOZI WAMETHODIST

  “Ni kweli kuwa amri yeyote chanya juu ya ubatizo wa watoto wadogo wala… kuitunza siku ya kwanza ya juma.Wengi wanafikili kuwa kristu alibadili Sabato…lakini kwa maneno yake anasema hakuja kwa lengo hilo”Amos Binney The Kitabu cha Wamethodisti (NewYork 1902)

  VIONGOZI WAPRESBITARIAN

  “Katika kupumzika Jumapili hakuna amri ya kimbingu……”Canon Eyton ,Amri Kumi za Mungu 63.65

  VIONGOZI WA WABAPTISTI WA KUSINI

  “Jina takatifu la siku ya Sabato,… hakuna hata mahali pamojamitume walipoilazimisha Amri ya

  Sabato iende siku ya kwanza ya juma…ni ujanja uliofanyika miaka ya baadae sana, wala

  hakuna mahali waliposema siku yaa kwanza itachukua nafasi ya siku ya Saba” Nathan L.Rice “Sabato ya wakristu.(New York:Robert carter and Brothers)

  VIONGOZI WA WALUTHERAN

  “haikuwa dhumuni la mitume wala kanis ala kwanza la mitume kuhamisha Amri ya Sabato kwenda Jumapili” Augustus Neander na Henry John Rose (Historia ya didi ya Kikisto)

  VIONGOZI WA WAKATOLIKI
  “Kama waprotestanti wangefuata Biblia, wangemwabudu Mungu siku ya Sabato. Kutunza

  Jumapli ni kuitunza amri ya wakatoliki” Chancellor wa Jimbo kuu la Baltmore akimjibu Kadinali February 10.1920

  “HATA NITAKAPOKUJA, UFANYE BIDII KATIKA KUSOMA NA KUONYA NA KUFUNDISHA” 1Timotheo 4:13

  NDUGU KUSOMA NA KUKARIRI MAFUNGU NI MUHIMU TUKIMBIE MAPOKEO
  NA WALE WANAOSEMA NI IMANI BILA KUSHIKA NENO, IMANI HAIUKUWI BILA NENO Soma Warumi10:17

  “Uzishike amri zangu ukaishi” Mithali 7:2

  ”Ziandike juu ya kibao cha moyo wako” Mithali 7:3

 168. Ndugu Anthony ni kweli tunaokolewa kwa kumwamini Yesu kuwa ni BWANA na MWOKOZI wetu. ila kumwamini kote huko ni kwa kushika amri nusunusu za Mungu (YESU). Ama katika biblia ni wapi inapoonesha kuwa amri ya nne (4) iliondolewa na Mungu ama Yesu baada ya kuja duniani ama kufufuka…!!???.

  Pia ndugu Anthony Yesu alipotaja amri katika kitabu cha
  Mathayo 19: 18Yule mtu akamwuliza,’’Amri zipi?’’
  Yesu akamjibu, ‘‘Usiue, usizini, usiibe, usishuhudie uongo, 19waheshimu baba yako na mama
  yako na umpende jirani yako kama nafsi yako.’’
  20Yule kijana akasema, ‘‘Hizi zote nimezishika. Je, bado nimepungukiwa na nini?’’
  21Yesu akamwambia, ‘‘Kama ukitaka kuwa mkamilifu, nenda, kauze vitu vyote ulivyo navyo na hizo fedha uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni. Kisha njoo, unifuate.’’

  Kwani unafikiri ya kuwa Yesu aliisahau hiyo amri..!?.ama aliona haina umuhimu..? kama alijua haina umuhimu basi ujue ya kuwa hata amri ya kwanza, ya pli na ya tatu pia hazina umuhimu…!!
  wala hakuisahau kama unavyofikiria, sana sana yeye alichozungumzia ni kuhusu Amri zinazohusu upendo kwetu sisi wanadamu…. Ndio maana yule kijana baada ya kuambiwa kuwa akauze mali zake ili awagawie masikini. alitoka akiwa amenyong’onyea.

  Sasa jiulize kuwa kuna amri ngapi za Mungu….?? ikiwezekana uziandike vizuri na kuziweka hapa…!!
  Je wewe unatunza amri ngapi..!!??

  “Hii ndiyo jumla ya maneno; yote yamekwisha sikiwa; Mche Mungu, nawe uzishike amri zake, maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu. Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila kazi, pamoja na
  kila neno la siri likiwa jema au likiwa baya.” Mhubiri 12:13-14.

  Asante wanamjadala.

 169. Wapendwa wale walio mabingwa wa kushika Sheria na kukariri vifungu mjue hivi,

  Kushika siku yoyote hata iwe Jumapili, sio njia ya kuokoka.Tunaokolewa kwa kumuamini Yesu kuwa ni BWANA na MWOKOZI na sio kwa kushika siku yoyote na kukariri vifungu vya biblia na kubishana huku ukiwa unasema hakuna kuokoka ila kuongoka ndio unakubali. Mpokee Yesu ili tuzungumze lugha moja.

 170. Ndugu yangu Lenda@ maelezo yako ni mengi but it contain nothing hapa hatuzungumzii ukatoliki na abii zenu za mnyama, tunaongelea sheria ya sabato na Jumapili. Kitaka kuzungumzia Katoliki kama dini lazima pia tuzungumzie Msabato kama dini.

  KWA KIFUPI TU TAFAKARI HAYA AMBAYO UMEYANUKUU BILA KUMALIZIA VIZURI. Mathayo 19: 18Yule mtu akamwuliza,’’Amri zipi?’’
  Yesu akamjibu, ‘‘Usiue, usizini, usiibe, usishuhudie uongo, 19waheshimu baba yako na mama yako na umpende jirani yako kama nafsi yako.’’
  20Yule kijana akasema, ‘‘Hizi zote nimezishika. Je, bado nimepungukiwa na nini?’’
  21Yesu akamwambia, ‘‘Kama ukitaka kuwa mkamilifu, nenda, kauze vitu vyote ulivyo navyo na hizo fedha uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni. Kisha njoo, unifuate.’’

  sijui hii tafsiri yake kama unaielewa vizuri, maana Yule kijana alishika amri kama alivyojibu na wewe unavyosistiza kwamba tushike amri hasa ya sabato. ambayo ktk hapo juu hajaitaja kabisa sasa sijui utasema Yesu alikuwa haijui??

  Mimi nakushauri uokoke na Yesu afanye makao ndani yako ndio jambo la msingi na sio kujitahidi kushika sheria tu.

 171. Yesu alisema sikuja kutangua torati na yesu alitoa Amri kuu ya upendo.

  Ni kweli Kuu ni Ya Upendo.
  Amri kuu ambayo ni ya Upendo
  a) Upendo kwa Mungu (kumpenda Mungu)
  b) Upendo kwa mwanadamu(Kumpenda jirani)
  Mungu ni Pendo ,Na Yesu ni Immanueli (Mungu pamoja nasi), Yesu ni Mungu hivyo utimilifu wa Pendo upo ndani yake ndio maana alitaka tuzishike Amri zake kwa kuweka kipaumbele Upendo si kama mafarisayo ambao walihukumu kwa kupiga wenzao mawe.
  a) Mtu aliyetanguliza Upendo kwa Mungu
  b) Upendo kwa wanadamu (jirani) atajikuta amezishika amri zote kumi kwa moyo wote na bila shuruti (maana Yesu huziandika moyoni) “Nitatia sheria zangu mioyoni mwao, na katika niaa zao nitaziandika” WAEBRANIA 10:16
  -Yesu anajua tukimpenda Mungu atakaa ndani yetu na amri zote zitazaliwa na kuandikwa mioyoni mwetu bila kujitegemea wenyewe alitaka kwa Imani.(kumwamini yeye kama mshindi) kuwa ndiye aliyetushindia vikwazo vyote. Tumwamini yeye na kwa kumruhusu atushike mkono na tuwe kama mtoto mdogo Kwenye mikono ya Baba yake. Hii ndio Imani yenyewe.Kisha tutakuwa tumekaandani yake kwa kuwa Yeye ni Pendo,pendo litazaliwa mioyoni mwetu na tutazishika amri zake.
  “Kwa hili twajua kwamba twawapenda watoto wa Mungu,tumpendapo,Mungu, na kuzishika amri zake.3. KWA MAANA HUKU NDIKO KUMPENDA MUNGU, KWAMBA TUZISHIKE AMRI ZAKE.”
  1 YOHANA 5:2
  -Na kama Yesu anasema tumpende Mungu kwa moyo wote na ameshatuambia Kumpenda Mungu ndiko kuzishika amri zake na amri zake tunazijua (KUTOKA 20:1) na Biblia inatuambia “Pendo halimfanyii jirani neno baya; basi Pendo ndilo utimilifu wa sheria”WARUMI 13:10 neno baya kwa jirani ni lipi? amri 5-6 hadi 10
  -Ndio maana siku zote joka ametumia mbinu mbalimbali kuanzia mbinguni ambako alipinga utii kwa Mungu na hata aliposhushwa chini akaendeleza Mungu anasema wasile matunda watakufa, Yeye akasema hakika hamtakufa, (MWANZO 2 :17)
  SWALI LA UCHUNGUZI:kwa nini wakristu wengi hutuma salamu zao za rambirambi waakisema tunakukumbuka kwa mtu aliyekufa (imetokea wapi Ibada ya hii mizimu) biblia inasema wafu hawajui lolote) Muhubiri anasema mwili huyarudia mavumbi na pumzi humrudia aliyeumba) hivyo hili ni danganyo la “hakika hamtakufa” la shetani lili la Mapokeo)
  “Kutahiriwa si Kitu, na kutokutahiriwa si kitu bali kuzihifadhi amri za Mungu”1 WAKORINTHO 7:19
  Ndio maana siku zote Joka ametumia mbinu mbalimbali kutengua amri za Mungu.
  Amri zote za Mungu zilitunzwa na kanisa la mwanzo na kujzwa na Roho wa kweli, mpaka miaka ya 300. Pale amri ya nne na kisha ya pili ya Sanamu kuondolewa.
  -Baadae amri zote ziliandikiwa katika katika catechism na kuwazuia waumini kusoma biblia. Mpaka leo asilimia 90 ya waumini hufundiswa kutumia Catechism na chuo cha sala na si Biblia maana Biblia ni Nuru isije kuangaza mioyo. Makanisa mengine yakiruhusiwa kufanya namna zao za Ibada bila kukaidi Kukaidi amri ya Mkuu wa makanisa yao .MAANA KWA MANENO YAO WALIMCHAGUA KUWA MSEMAJI WA MAKANISA YOTE YA JUMAPILI KATIKA MKUTANO WA VATICAN. Soma unabii katika Bibliawa mama(kanisa) aliyesema sitakuwa Mkiwa .
  1. SWALI LA UCHUNGUZI: KWA NINI NYIMBO ZA MAKANISA YA NEW AGE ZIMEFANANA UKIENDA MAKANISA YA KIROHO JAPO HUONEKANA WAMETOFAUTIANA
  (soma Vatican II and liturgy in church union)

  2. KWA NINI WACHUNGAJI WENGI HUKWEPA SANA VITABU VYA UFUNUO NA DANIEL?
  (SIRI NZITO)

  3. KWA NINI WACHUNGAJI WENGI HUCHAGUA AMRI CHACHE TU NA KUZISEMA HUKU WAKIKWEPA KUZUNGUZIA NYINGINE.?(MKUBWA HANYOOSHWEWI KIDOLE)

  4. KWA NINI SIMON MCHAWI ALIWAONGOZA WAISRAELI KWA MIAKA MINGI TANGU UTOTO WAKE KABLA YA UJIO WA KWANZA WA KRISTO? NA WASIJUE KUWA MCHAWI?

  5. KWA NINI JOKA SIKU ZOTE AMEFANYA VITA NA WATU WAZISHIKAO AMRI ZA MUNGU?
  “joka akamkasirikia Yule mwanamke, akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda waa Yesu; Ufunuo wa Yohana 12:17
  “Hapa ndipo penye subira ya watakatifu hao wazishikao amri za Mungu na Imani ya Yesu”
  SOMA CATECHISM KATOLIKI (BPNP)TANZANIA 2002 UKURASA 28 KISHA FANANISHA NA AMRI ZA MUNGU KUTOKA 20:1, UANGALIE AMRI HIZI ZIMETOFAUTIANAJE NA MAKANISA MENGINE YAMEZIFUATA ZIPI,NA TAFUTA YAMEKUBALIANA NINI NA VATICAN?
  UFUNUO WA YOHANA 14:12
  MATENDO YA MITUME 16:4
  MATENDO ,, 16:13
  MATENDO ,, 13:42
  Amri za Mungu Kumi hazikutenguliwa na Yesu Yeye mwenyewe alisema

  “…Lakini ukitaka kuingia katika uzima,zishike amri. Akamwambia zipi? Yesu akasema,ni Hizi, Usiue,usiibe,Usishuhudie uongo…….. “Mathayo 19:17

  Kumbuka amri KUMI za Mungu zipo katika UPENDO KWA MUNGU na UPENDO KWA WANADAMU (JIRANI)

  “KUTAHIRIWA SI KITU, NA KUTOKUTAHIRIWA SI KITU BALI KUZIHIFADHI AMRI ZA MUNGU”
  1 WAKORINTHO 7:19

  “KWA MAANA HUKU NDIKO KUMPENDA MUNGU, KWAMBA TUZISHIKE AMRI ZAKE.”
  1 YOHANA 5:2

 172. lenda, kama nitaamini sabato naokolowa Je Yesu alikuja kwa ajili ya nini? naona hapo umeongeza ya kwako mpendwa. halafu mnang’ang’ania sabato tu kwa usipo fuata hiyo hutaokoka, Je ktk zile amri za Mungu(zinahusu Mungu na mwanadamu mmeona amri ya sabato tu ndio kuu??. unaweza kunidhibitishia kimaandiko kama hii ndio amri kuu?? Je Amri kuu alizotoa Yesu, ambazo ni kama mbili (2 in one) kuhusu upendo mmeiweka wapi hapa??

 173. thank you ilenda,sasa tumejua vizuri kwa nini dunia yote inahamasishwa kuiona sabato sio jambo la msingi,hii ni kwa sababu kuna kikundi cha watu chenye maslahi yao na si ya mungu wa mbinguni maana wanatafuta uasi na kupotosha wengine na sio kuwahekimisha watu wamrudie mungu wa mbinguni,wakati watu wanapoona sabato sio jambo kubwa la kiimani ndivyo wanavyopotoka na kikundi hiki kujipatia umaarufu miongoni mwa watu na sio mungu,yawezekana hata sisi wengine tunaochangia humu mada hii kwa kung’ang’aniza sabato sio jambo la muhimu badala ya kujifunza, tunakipa nguvu kikundi hiki kwa kujua ama pasipo kujua,tutafakari utume wetu kwa mungu na sio utume wetu kwa kikundi cha watu,ambao wao wameamua kuasi na kuangamia,

  uchaguzi bado unabaki kwetu maana hamna yeyote atakayetulazimisha kufuata matakwa yake kwa lengo lake kwamba sisi tumwasi mungu na tupotee kwa sababu yeye ameamua kupotea,biblia inasema kila mtu atauchukua msalaba wake,tusibebee watu misalaba yao wapendwa maana hata sisi tunayo mengi tutakayojibu yanayotuhusu ambayo wao(kikundi) hawatubebei.

  kwa maelezo hayo hapo juu,nikuombe tena utupatie maelezo ya kutosha kuhusu suala hili la watu kuibadilisha sabato ya mungu namna watakavyo, lakini ukweli utabaki kuwa ukweli hata kama utatuumiza na ni muhimu kuufuata ukweli hata kama tutaumia kwa namna yeyote ile,

  ni vyema kwa watu kupenda kujifunza na kuelewa mambo haya badala ya kubisha na kushindana kwa kitu kisichohitaji ushindani baada ya kukielewa,kushindana kuthibitisha kwa mafungu ya biblia ambayo kwa hayo tutahukumiwa kuwa wakososaji

  kwa kuwa mkweli kwa kusoma mafungu yaliyotolewa hapo juu na wachangiaji wote na kufuata blog aliyotoa NASHON nimegundua ukitaka kujua kitu vyema usikilize kwanza kisha uende usome zaidi umwombe mungu akupe utulivu na busara ya uelewa,na ujifanye hujui lolote na unahitaji kuelewa ukweli ambao hujawai kuupata, kwa makini kabisa,utagundua kuwa hata kwa kutumia akili tu ya kwaida sabato ni jambo la msingi na lazima kwa binadamu awaye yote.kama si lazima kwako jambo moja ni hakika hukubali uumbaji wa mungu aliyesema tuikumbuke sabato kama siku iliyotakaswa na kubarikiwa kupita siku zote, mungu aendelee kunifundisha zaidi maana sabato ni pana na nahitaji kuielewa zaidi na wanaoitetea wataheshimiwa na mungu.endelea kutupatia maelezo mngine mengi na mungu akujalie uzima watu waelewe vizuri ujumbe wa mungu kupitia kwenu

 174. Soma habari za ecumenical movement na kuingia katika Muungano huo, utambue makanisa yanayoabudu Jumapili kuwa kwa kufanya hivyo ni kumkiri papa kama mkuu na Mungu wao. Ikimbie Jumapili ukaokolewe. SABATO NI YA KWELI na YA MILELE SOMA VIZURI.
  maelezo yangu ya tarehe 1 August ufunguke kuwa Sabato ni Muhuri wa uumbaji wa Mungu na sifa juu ya kazi yake,kuikubali jumapili ni kukana maagizo ya Mungu na Amri zake . ISHIKE SABATO UKAOKOLEWE

 175. “NITAJIBU KWA KUTUMIA MAFUNGU KUWA SABATO NI YA KUPUMZIKA,KUABUDU NA KUKUSANYIKA”
  “Leo, kama mtaisikia sauti yake, msifanye migumu mioyo yenu.” Waebrania 4:7
  “Maana sisii tulioamini tunaingia katika raha ile kama vile alivyosema, kama vile alivyoapa kwa hasira yangu, hawataingia rahani mwangu…….Waebrania 4:2
  A. SABATO KWA AJILI YA KUPUMZIKA:
  (i) “Utafanya kazi siku sita, lakini katika siku ya saba utapumzika; Kutoka 34:21
  (ii) “Kazi itafanywa siku sita; lakini siku ya saba ni Sabato ya Kustarehe kabisa,takatifu kwa BWANA;
  B. SABATO NI KWA AJILI YA KUABUDU:
  (i)“Na itakuwa, mwezi mpya hata mwezi mpya, na sabato hata sabato, wanadamu wote watakuja KUABUDU mbele zangu,asema BWANA.” Isaya 66:23
  “Hata siku ya Sabato tukatoka nje ya lango, tukaenda kando ya mto, ambapo tukadhani ya kuwa pana mahali pa kusali;” Matendo 16:13
  c. SABATO NI KWA AJILI YA KUKUSANYIKA:
  (i) “mtafanya kazi siku sita; lakini siku ya saba ni Sabato ya kustarehe kabisa,KUSANYIKO takatifu;
  (ii)“Na itakuwa, mwezi mpya hata mwezi mpya, na sabato hata sabato, wanadamu WOTE WATAKUJA kuabudu mbele zangu,asema BWANA.” Isaya 66:23
  (ii) na walipokuwa wakitoka, wakawasihi waambiwe maneno haya Sabato ya pili. Matendo 13:42
  (iii) Hata Sabato ya pili, watu wengi karibu mji wote, wakakusanyika walisikie neno la Mungu.Matendo 13:44
  D. SABATO NI YA MILELE HAIJAISHA:
  (i) “Ombeni,ili kukimbia kwenu kusiwe wakati wa baridi, wala siku ya Sabato.”
  Mathayo 24:20 (Hapa hata Yesu anazungumzia nyakati za dhiki ambazo akiwambia watu juu ya mambo ambayo yangewatukia hata baada ya yeye kupaa akawaambia wanafunzi wake waombe Mathayo 24:3”
  (ii) Kwa ajili ya hayo wana wa Israeli wataishika Sabato, kuiangalia sana hiyo Sabato katika vizazi vyao vyote, ni agano la milele. (usipojiamini kuwa umeunganishwa na tawi kuwa Mwisraeli soma Warumi 11:11-25)
  (iii) “Baasi, imesalia raha ya Sabato kwa watu wa Mungu” Waebrania 4:9
  (iv) “Kama vile mbingu mpya na NCHI MPYA NITAKAZOFANYA, zitakavyokaa mbele zangu,asema BWANA,ndivyo uzao wenu na jina lenu litakavyokaa. Na itakuwa, mwezi mpya hata mwezi mpya, na sabato hata sabato, wanadamu WOTE WATAKUJA kuabudu mbele zangu,asema BWANA.Isaya 66:22
  Tuwasikilize walioanzisha Kuabudu Jumapili wanasemaje;
  “Tunaitunza Jumapili na si Jumamosi kwa sababu Kanisa katoliki lilihamisha utukufu kutoka Jumamosi kwenda Jumapili” Peter Geiermann, CSSR,Doctrinal Catechism, 1957 edition

  “Ili makanisa yapate wokovu lazima yatii mamlaka ya Papa na kumkubali kama msemaji wa makanisa Yote ikiwa ni pamoja kupokea muhuli wa uwezo na mamlaka kuifuata Jumapili”
  Vatican II ilianzisha Ecumenical movement Makanisa kuwa pamoja yakitii kwa mtu mmoja aliye na muhuri wa mamlaka ya Ukuu wa Kubadili Amri za Mungu kwa sababu Yeye mwenyewe ni Kristu na kukana ukuu wa kuwa Mungu aliumba kwa kutoheshimu kazi ya Siku sita kukiriri kwa maneno kukataa kwa vitendo ili Wanaosema wanaaona watiwe upofu. UFUNUO 3:18 (MUHULI WA UKUU WA PAPA KUWA NA UWEZO WA KUBADILI AMRI KWA KUWA SI MWAKILISHI TU ILA MWENYEWE NI MUNGU MWENYE MAMLAKA WAO WENYEWE WANASEMA HIVYO SOMA nukuu za Mapapa na UKUU MOJAWAPO NI ILA ZIPO NYINGI) (Soma Katiba ya Umoja wa Makanisa)
  QUATATION:”Papa sio mwakilishi wa Yesu tu, lakini ni Yesu mwenyewe,katika mwili” Source The Catholic National, JULY,1985
  Mama wa makanisa, Ufunuo 17:1-6.

 176. ndugu michael john nzala,
  kuna mahali umesema sabato ni muhuri wa Mungu hii sio kweli maana haijaandikwa popote kwenye biblia , roho mtakatifu ndio muhuri wa Mungu.
  efeso 1:13 nanyi pia ktk huyo mmekwisha kulisikia neno la kweli, habari njema ya wokovu wenu,tena mmekisha kumwamni yeye na kutiwa muhuri na roho yule wa ahadi alie mtakatifu.
  efeso 4:30 wala msimuhuzunishe yule roho mtakatifu wa Mungu ambae kwa yeye mlitiwa muhuri hata siku ya ukombozi.
  mimi nimesoma baadhi ya waandishi wa vitabu wa kisabato wameandika sabato ni muhuri wa Mungu mi nakushauri tafuta biblia yote kama utaona imeandikwa hivyo tuletee hapa tufaidike, roho mtakatifu ndo muhuri wa Mungu imeandikwa.

 177. MILINGA

  KUKUSANYIKA PAMOJA, KUABUDU na KUPUMZIKA. hapa ndipo watu tunaitaji Roho Mtakatifu atupe ufunuo na Maarifa ya kulijua neno la Mungu Maana Andiko uua bali Neno uuisha

  Naomba nisaidiwe MUNGU ALISEMA SIKU YA 1 HADI YA 7 AU JUMAMOSI HADI JUMAPILI?

 178. Wapendwa,

  Mada hii ni ya muhimu sana ikajadiliwa na isiachwe iende kimya kimya bila watu kutoa hoja nyingi za nguvu.

  Nawasubiri wapendwa wote wenye hoja za nguvu wajitokeze kujadili hoja hii kuhusu sababu za kuabudu Jumapili.

  Karibuni sana wapendwa. Hebu anza kutoa maoni yako sasa.

 179. Wapendwa,

  Somo kuhusu SABATO ni somo lenye mjadala mkali. Hata hivyo nawaomba wachangiaji wajitahidi kutofautisha mada TATU hapa. KUKUSANYIKA PAMOJA, KUABUDU na KUPUMZIKA.

  Watu wengi huchanganya mada hizi TATU: 1. AMRI YA KUABUDU, 2. AMRI YA KUPUMZIKA. na AMRI YA KUKUSANYIKA PAMOJA Kuna wapendwa wanachanganya wakidhani kuwa KUPUMZIKA ni sawa sawa na KUABUDU au kwamba KUKUSANYIKA PAMOJA ni kuabudu. Huu ni upotoshaji wa maandiko.

  Hakuna maandiko yanayosema siku ya KUABUDU ni JUMAPILI au JUMAMOSI. Mungu alipumzika siku ya 6 siyo kwamba aliabudu. Mungu haabudu bali anaabudiwa. Kuabudu ni kumcha Mungu. Kupumzika ni kuacha kufanya kazi yoyote na kukaa kabisa raha mstarehe. Hii ndiyo maana ya SABATO. Watu wanadhani kwenda kanisani siku ya JUMAPILI, JUMAMOSI au IJUMAA eti ni KUABUDU. La hasha. Kwenda kanisani kwa siku yoyote siyo kutimiza moja wapo ya amri 10 za Mungu kwa wana wa Israel bali ni kutimiza agizo la Mungu la, “……..WALA TUSIACHE KUKUSANYIKA PAMOJA KAMA ILIVYO DESTURI YA WENGINE……..” Ebr. 10:25.

  Kukusanyika pamoja siyo kuabudu. Tunakusanyika pamoja kwa lengo la Kuonyana, kufundishana, kutiana moyo katika Imani ili KILA SIKU TUMWABUDU MUNGU KATIKA ROHO NA KWELI. Kuabudu ni swala la mahusiano ya kila siku baina ya mwanadamu na Mungu katika roho. KUABUDU HUFANYWA KILA SIKU. Lakini kukusanyika pamoja siyo lazima iwe kila siku.

  Wasabato wanapotea kwa kudhani kwamba KUKUSANYIKA SIKU YA JUMAMOSI wanakuwa wanashika AMRI KUU YA KUPUMZIKA KILA BAADA YA SIKU SITA. Kupumzika anakokutaka Mungu na hii ni AMRI YA MILELE ni kuacha kufanya kazi yoyote ikiwemo kutokutembea umbali wowote wa zaidi ya mita 200 hivi. Hii ni amri ya milele kwa wanaojua kwamba kila baada ya siku 6 lazima wapumzishe akili na mwili kwani ndicho Mungu alichokusudia milele hapa duniaani kwa watu wake.

  Siku ya KUPUMZIKA haipaswi kuchanganywa na SIKU YA KUABUDU kwani hakuna siku maalum ya kuabudu (No special day for worshiping God but all days are special for worshiping in spirit and truth). Ukienda kanisani siku ya JUMAMOSI usidhani umeishika AMRI YA SABATO kwani hujapumzika kabisa. KUKUSANYIKA PAMOJA ni kazi ngumu sana inayohitaji mtu atembee kwa mguu au kwa magari au baiskeli umbali mrefu kufuata jengo la kukutania. Hili silo Mungu alilokusudia kuweka SABATO. Mungu alikusudia SABATO imsaidie mwanadam kupata pumziko la mwili na akili baada ya siku 6 za kazi.

  Watu wanashindwa kushika SABATO (Yaani KUPUMZIKA) na kukimbilia makanisani wakidhani eti ndiyo wanashika AMRI 10 za Mungu. Upotofu Mtupu. Kuna walokole wanaodhani kuwa JUMAPILI NI SABATO YA BWANA. Nao wanakosea sana. JUMAPILI siyo siku ya SABATO hata kidogo wala JUMAMOSI siyo SABATO hata kidogo. Kuna makanisa ya Kipentekoste yanamtenga muumini atakayeonekana akifanya kazi yoyote siku ya Jumapili kama wafanyavyo wasabato kwa muumini wao anayeonekana aakifanya kazi yoyote (ingawa wanafanya kazi ya kutembea na kupika siku ya Jumamosi). Huu nao ni upofu na ujinga wa kutoelewa maandiko.

  SABATO YA KWELI ni kule kuelewa kanuni za Mungu kwamba kila baada ya Siku 6 za kazi mwanadamu mwenye damu naa nyama anapaswa KUPUMZIKA KABISAA (a total rest). KUABUDU anakokutaka Mungu ni kule kumwamini na kumcha kila siku kila mahali na kumtumainia yeye tu bila kumshirikisha na miungu mingine hata siku moja. Huku ndiko kumwabudu Mungu na wala siyo kule kwenda kwenye MIKUSANYIKO YA JUMAPILI na JUMAMOSI au IJUMAA. Hata waovu na waabudu sanamu nao hukusanyika.

  Wewe unayedhania kwamba unashika AMRI ZA MUNGU kwa kuelekea kanisani siku ya JUMAMOSI, JUMAPILI au IJUMAA unajidanganya kabisaa. Huku siyo kuzishika amri 10 za Mungu hata kidogo endapo huna siku nyingine ya kuwa na mapumziko kabisa ili kupumzika kimwili na kiakili.

  Lazima wapendwa tujifunze kuwa na siku maalum kila baada ya siku 6 tupumzike kabisaa wala tusifanye kazi yoyote kabisa. Pia kila mwaka lazima tujipangine kuwa na siku 28 nzima za kupumzika kabisa. Pumzika siku 28 yaani mwezi mmoja kila mwaka. Hapa ndipo utakuwa umeshika amri 10 za Mungu. Siku ya KUPUMZIKA kwako ndiyo SABATO yako. Hii lazima iwe tofauti na siku ya KUKUSANYIKA PAMOJA NA WENGINE KAMA ILIVYO DESTURI YA WATAKATIFU.

  Naomba leo niishie hapa kwanza nitaendelea kujadili baadaye.

 180. Asante sana Samwel umenikumbusha neno moja la wakolosai 2:16 ambalo linasema “16 Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato;
  17 mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo.

 181. Mdo 17.2…8 Paul alihubiri akifunua kuwa huyo ni Kristo. Wengine wakaamini na kushikamana na Paul. Wayahudi wakaona wivu, wakasema Walioupindua ulimwengu wamefika na huku. Wanasema yupo Mfalme mwingine aitwae Yesu. ( Ndio ni Mfalme). Mdo 18.4…8. Paul akajaribu kuwavuta( kuwatoa wapi na kuwapeleka wapi? Ni kweli walikuwa kwenye Sabato. Yoh 9.16.. Mafarisayo wakasema huyu hakutoka kwa Mungu, wengine wakasema mwenye dhambi hawezi kuponya watu. Yoh 9.22.. Wazazi wake wakaogopa Wayahudi, walikuwa wamekubaliana kuwa mtu akimkiri kuwa ni Kristo atatengwa na Sinagogi ( hata ww ukimkiri tu ukaokoka utatengwa usijali). Mdo 7.51.,60 Muone Stephano akipambana nao, na Sauli ambaye ndiye Paul alikuwa anaona sawa, akaomba kibali akawasake Dameski, Mdo 9, 1….31 hiyo ni huduma ya Paul, soma kwa makini, Yesu akamtokea akamwambia anamudhi, Paul aliyesema katika Gal 1.13…17 kuwa hakuwa hatia katika dini yake ya Kiyahudi, lakini kumbe alikuwa akiliudhi kanisa. Kumbe Kanisa kitu kingine na dini ya kiyahudi kitu kingine. Ebu tusome Yoh 5,39…40 Mwayachunguza maandiko kwa sababu mnadhani kwamba ninyi mna uzima wa milele ndani yake..

  Na hayo ndiyo yanayonishuhudia, wala hawataki kuja kwangu, mpate kuwa na uzima. Mimi siupokei utukufu kwa wanadamu. Walakini niwajua ninyi ya kuwa hamna upendo wa Mungu ndani yenu, nimekuja kwa jina la Baba yangu wala ninyi hamnipokei, mwingine akija kwa jina lake mtampokea huyo akaendelea kusema atakayewashtaki ni MUSA, KWA KUWA ALIANDIKA HABARI ZANGU LAKINI MSIPOYAAMINI MAANDIKO YAKE YAKE MTAYAAMINI WAPI MANENO YANGU ? Sikia hiyo . Mpaka UTAJI UONDOKE I1kor 3..12…18 soma kwa utulivu, kwa nia kabisa ya kutaka jua, utaji utaondoka, utaelewa Paul alikuwa anawaambia nini Wakorintho.na pia nimalizie hivi. I1 kor 3..6 Naye ndiye aliyetutosheleza kuwa wahudumu wa Agano jipya, sio wa andiko bali wa roho, kwa maana andiko huua, bali roho huhuisha, Ndiyo maana Yesu aliwaambia wasitoke Yerusalem mpaka msaidizi aje ambaye ni mwalimu pia, awafundishe awatie kwenye kweli yote, bila huyo, Biblia kama Biblia ni ngumu, aliona hawataijua na ni kweli. Mdo 1.4,.8. Naamini ukifuata kwa makini malekezo hayo, utakuwa umesogea mahali, na baadae utakuwa Paul wa siku zetu. Ubarikiwe. Thanks.

 182. Ndugu Michael, kwanza nikupongeze kabisa kwa mafundisho uliyoyaandika, kama ungekuwa umezaliwa kipindi cha akina Paul kabla Yesu hajaja, nadhani ungekuwa mstari wa mbele kabisa kupambana naye kama ndugu yetu Paul alivyofanya. Nikuombe tu kuwa, nenda kwa unyenyekevu kabisa mbele za Mungu mwambie nisaidi e nielewe unachosema, kwa nini nasema hivyo’.? Maandiko karibu yote uliyoyatumia, hasa ya Yesu kuwa aliitunza Sabato yanatosha kabisa kukufanya ukampokea Yesu -na kuokoka. Fuatana nami, ulikuwa unakopi tu kitu kinaitwa SABATO, Rudi usome tena kilichotokea baada ya Yesu kufika au kuingia humo. Mark 1.21-28 WAKASEMA ELIMU MPYA. Mark 6.2-6 WAKAJIKWAA KWAKE. Luk 4.16-30 WAKAJAA GHADHABU WOTE, WAKAMTOA NJE. Luk 4.31-37 MSHANGAO UKAWASHIKA. Luk 13.10-17 MKUU WA SINGOGI ALIKASIRIKA, Luk 6.6 WAANDISHI NA MAFARISAYO WAKAJAWA UCHUNGU, WAKASHARIANA WAMTENDEJE. Mdo 13.14…39 Amwaminiye huhesabiwa haki katika manbo asiyoweza kuhesabiwa haki kwa Torati ya Musa.. Mdo 13.44…46 WAYAHUDI WAKAJA WAKAKANUSHA, WAKIBISHA NA KUTUKANA. Mdo 15.21 Musa alikuwa na watu waliokuwa wakihubiri mambo yake, haya ni ya Yesu. Inaendelea

 183. Ndiyo, kufanya ibada, ni kila siku, lakini si siku zote Mungu alizitakasa. Siku ya Sabato Pekee ndiyo Mungu aliitakasa na kuiweka wakfu kwa ajili ya wanadamu Marko 2:26-7. Angalia Mwanzo wa siku hiyo.

  Sabato ilianza lini???

  Mwanzo 2:2-3… “Na siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya; akastarehe siku ya saba, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoifanya. Mungu akaibarikia siku ya saba, akaitakasa kwa sababu katika siku hiyo Mungu alistarehe, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoiumba na kuifanya”.

  Kutoka 16: 23… Akawaambia, Ndilo neno alilonena Bwana Kesho ni starehe takatifu, Sabato takatifu kwa Bwana; okeni mtakachooka, na kutokosa mtakachotokosa; na hicho kitakachowasalia jiwekeeni kilindwe hata asubuhi…

  Muhimu: Sabato ilikuwepo hata kabla ya Amri 10 kutolewa pale Sinai.

  Wana wa Israeli waliitunza Sabato

  Waisraeli walizitunza Amri za Mungu kama Babu yao Ibrahimu

  Mwz 26:5 Kwa sababu Ibrahimu alisikia sauti yangu, akayahifadhi maagizo yangu, na amri zangu, na hukumu zangu, na sheria zangu.

  Kwa nini Mungu alifanya Sabato??
  Sabato ni pumziko
  Ishara ya Uumbaji
  Sabato ni muhuri wa Mungu
  Humtambulisha kuwa Mungu ni muumbaji wa vyote
  Aliitenga kwa ajili ya mwanadamu ili mwanadamu aweze kuwasiliana na Mungu kila wiki
  Mungu aliifanya kuwa tofauti (aliitakasa) na siku zingine zote sita
  Jumapili haijatakaswa na Mungu, naam, hata kwenye Agano Jipya
  Sabato ni siku ya furaha
  Ajabu zaidi, Sabato ilianzishwa hata KABLA YA DHAMBI duniani, iweje ikomeshwe msalabani au kubadilishwa.

  Hata baada ya taifa la Israel kupelekwa utumwani Misri kwa muda miaka 400, Mungu aliamua kuwatoa Waisrael utumwani kwa maana walikuwa wameshasahau kumwabudu Mungu na kugeukia miungu ya Misri. Wakiwa njiani, Mungu aliwataka wakumbuke na kumwabudu Mungu kama Baba zao walivyofanya hapo zamani. Ndiyo maana Mungu hakuanza na tunzeni sabato yangu, bali Ikumbuke…

  Kutoka 20:8-11 Ikumbuke siku ya Sabato uitakase. Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; lakini siku ya saba ni Sabato ya Bwana, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. Maana, kwa siku sita Bwana alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo Bwana akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa.

  Zingatia yafuatayo:-

  Ni siku iliyokuwepo tangu uumbaji na itadumu milele maana ni agano lake na watu wake
  Kutoka 31:16 Kwa ajili ya hayo wana wa Israeli wataishika Sabato, kuiangalia sana hiyo Sabato katika vizazi vyao vyote, ni agano la milele.

  2. Ni siku inayomtambulisha Mungu kuwa yeye ni muumbaji wa mbingu, nchi na vyote vilivyomo.
  Kutoka 20:11 Maana, kwa siku sita Bwana alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo Bwana akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa.
  Mambo ya Walawi 23:3 Mtafanya kazi siku sita; lakini siku ya saba ni Sabato ya kustarehe kabisa, kusanyiko takatifu; msifanye kazi ya namna yo yote; ni Sabato kwa Bwana katika makao yenu yote.

  3. Ni ishara kati yake na watu wake (Sabato ni utambulisho wa watu wa Mungu)
  Ezekieli 20:12 Tena naliwapa sabato zangu, ziwe ishara kati ya mimi na wao, wapate kujua ya kuwa mimi, Bwana, ndimi niwatakasaye.
  Ezekieli 20:20 zitakaseni sabato zangu; zitakuwa ishara kati ya mimi na ninyi, mpate kujua ya kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wenu.

  4. Ni amri 4, Mungu ameaza na neno IKUMBUKE, maana waisrael waliisahau na Mungu alifahamu kuwa wakristo wengi watakuja kuisahau
  Ezekieli 8:16 Akanileta mpaka ua wa ndani wa nyumba ya Bwana, na tazama, mlangoni pa hekalu la Bwana, kati ya ukumbi na madhabahu, walikuwako watu kama ishirini na watano, wamelipa kisogo hekalu la Bwana, na nyuso zao zimeelekea upande wa mashariki, nao wanaliabudu jua, kwa kuuelekea upande wa mashariki ( Jumapili ni Sun + Day = Sunday, siku ya jua).

  Kuabudu siku hii ya Jumapili, ni Kupokea alama ya Mpinga Kristo ( Vicarius Filii Dei = 666, nenda google). Siku si nyingi, Mpinga Kristo atasimama na kuulazimisha ulimwengu wote kutunza Jumapili na watakaokubaliana na hilo, watakuwa wamepoteza nafasi zao katika ufalme wa Mungu. Soma Ufunuo 13…

  5. Ni amri ndefu kuliko zingine zote 10
  Kutoka 20:8-11 Ikumbuke siku ya Sabato uitakase. Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; lakini siku ya saba ni Sabato ya Bwana, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. Maana, kwa siku sita Bwana alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo Bwana akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa.

  Mungu amerudia mara mbili kirai “ …fanya kazi kwa siku sita” na “…siku ya Saba ni Sabato ya Bwana…” Hii ilikuwa ni kuonesha “UMUHIMU WA SIKU HII”
  Je, Yesu aliitunza Sabato ???

  Ndiyo, Yesu aliitunza Sabato

  Marko 1:21 Wakashika njia mpaka Kapernaumu, na mara siku ya sabato akaingia katika sinagogi, akafundisha.

  Marko 6:2 Na ilipokuwa sabato, alianza kufundisha katika sinagogi; wengi waliposikia wakashangaa, wakisema, Huyu ameyapata wapi haya? Na, Ni hekima gani hii aliyopewa huyu? Na, Ni nini miujiza hii mikubwa inayotendeka kwa mikono yake?

  Luka 4:16 Akaenda Nazareti, hapo alipolelewa; na siku ya sabato akaingia katika sinagogi kama ilivyokuwa desturi yake, akasimama ili asome.

  Luka 4:31 Akashuka mpaka Kapernaumu, mji wa Galilaya, akawa akiwafundisha siku ya sabato;

  Luka 13:10 Siku ya sabato alikuwa akifundisha katika sinagogi mojawapo.

  Luka 6:6 Ikawa siku ya sabato nyingine aliingia katika sinagogi akafundisha; na mlikuwamo mtu ambaye mkono wake wa kuume umepooza.

  Je, ni kweli kuwa Sabato iliishia msalabani ???

  Sabato ya amri ya nne haikuishia msalabani. Ni agano la milele Kut. 31 :16. Sabato iliyoishia msalabani, ilitokana na amri za Musa, amri ambazo ziliwaongoza Waisrael kutii Amri 10 za Mungu. Angalia tofauti zake ;

  Tofauti ya Amri za Mungu na za Musa

  Amri za Mungu Amri za Musa

  1. Ziliandikwa na Mungu mwenyewe 1. Ziliandikwa na Musa mwenyewe kwa kwa kidole chake Torati 31:18 kwa kidole chake, Kutok 31:18

  2. Ziliandikwa kwenye mbao mbili za 2. Ziliandikwa kwenye

  mawe yaliyochongwa, Torati 10:1-4 chuo(kitabu cha dini),

  Torati 31:24

  3., Ziliwekwa ndani ya Sanduku 3. Baada ya kuandikwa,

  la Agano Torati 10:1-4 ziliwekwa nje pembeni

  ya Sanduku la Agano,

  Torati 31:24-27

  4 . Waliozivunja, walionekana kutenda 4. Waliozivunja, hawakuonekana na

  dhambi 1Yoh. 3:4, na iliwapasa dhambi wala haikuwapasa kufa

  kufa. Torati 17:2-5 kwani zilikuwa ni kivuli cha Kristo.

  Wakolosai 2:14-17

  5. Yesu alikuja kuzitimiliza wala si ku- 5. Yesu aliziondoa pale msalabani

  zitangua. Watu wote wanapaswa maana zilikuwa ni sheria za maa gizo

  kuzifundisha…Mathayo 5:17-19 tu yaliyosimama kama kivuli cha

  mema yajayo. Kolosai 2:15

  6. Sheria(torati) ya Bwana ni takatifu, 6. Zilikuwa ni kivuli cha kazi ya

  njema na ya haki, nayo yadumu mi- Yesu aliyoifanya msalabani, nazo

  lele na milele, Warumi 7:12 zilikomea hapo. Ebran. 10:1-12

  7. Sheria za Bwana ni kamilifu, za 7. Ziliishia pale Kristo alipokufa

  adili, kweli na za milele. Msalabani. Waebran. 9:10-12,

  Zaburi 111:7-8 Luka 22:37

  A. Mfano wa sheria ya Musa

  1. Kuchinja kondoo kama mbadala wa mdhambi. Kutoka 29…, Walawi, Torati, Nyakati nk

  2. Kifo yeyote aliyevunja mojawapo au Amri zote 10 za Mungu

  Kutoka 31:14… Basi mtaishika hiyo Sabato; kwa kuwa ni takatifu kwenu; kila mtu atakayeitia unajisi hakika yake atauawa; kwa kuwa kila mtu afanyaye kazi katika siku hiyo, nafsi hiyo itakatiliwa mbali na watu wake.

  B. Sheria za Mungu, Kutoka 20 :1-17

  Hivyo basi Yesu alipokufa Msalabani sheria za kuchinja kondoo tena ziliisha maana mwanakondoo wa Mungu (Yesu) aichukuaye dhambi ya ulimwengu alikuwa ameshachinjwa tayari.

  Yohana 1:29 Siku ya pili yake amwona Yesu anakuja kwake, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu!

  Kama kifo cha Yesu mmsalabani kilibadilisha Sabato, tuangalie Mitume wake waliabudu siku gani ??

  Matendo ya Mitume 13:14 Lakini wao wakatoka Perge, wakapita kati ya nchi, wakafika Antiokia, mji wa Pisidia, wakaingia katika sinagogi siku ya sabato, wakaketi.

  Matendo ya Mitume 13:27 Kwa maana wakaao Yerusalemu, na wakuu wao, kwa kuwa hawakumjua yeye, wala maneno ya manabii yanayosomwa kila sabato, wameyatimiza kwa kumhukumu.

  Matendo ya Mitume 13:42 Na walipokuwa wakitoka, wakawasihi waambiwe maneno haya sabato ya pili.

  Matendo ya Mitume 13:44 Hata sabato ya pili, watu wengi, karibu mji wote, wakakusanyika walisikie neno la Mungu.

  Matendo ya Mitume 15:21 Kwa maana tangu zamani za kale Musa anao watu wahubirio mambo yake; katika kila mji husomwa kila sabato katika masinagogi.

  Matendo ya Mitume 16:13 Hata siku ya sabato tukatoka nje ya lango, tukaenda kando ya mto, ambapo tukadhani ya kuwa pana mahali pa kusali; tukaketi, tukasema na wanawake waliokutana pale.

  Matendo ya Mitume 17:2 Na Paulo, kama ilivyokuwa desturi yake, akaingia mle walimo, akahojiana nao kwa maneno ya maandiko sabato tatu,

  Matendo ya Mitume 18:4 Akatoa hoja zake katika sinagogi kila sabato, akajaribu kuwavuta Wayahudi na Wayunani.

  1. Paulo bado anasisitiza

  Waebrania 4:9 Basi, imesalia raha ya sabato kwa watu wa Mungu.

  2. Isaya anasema hadi mbinguni, tutaitunza Sabato ya Bwana
  Isaya 66 :22 Kama vile mbingu mpya na nchi mpya, nitakazofanya, zitakavyokaa mbele zangu, asema Bwana, ndivyo uzao wenu na jina lenu litakavyokaa. 23 Na itakuwa, mwezi mpya hata mwezi mpya, na sabato hata sabato, wanadamu wote watakuja kuabudu mbele zangu, asema Bwana.

  Kwani siku ya Sabato in Ipi ??

  Mathayo 28:1 Hata sabato ilipokwisha, ikipambazuka siku ya kwanza ya juma, Mariamu Magdalene, na Mariamu yule wa pili, walikwenda kulitazama kaburi.

  Marko 16:2 Hata alfajiri mapema, siku ya kwanza ya juma, wakaenda kaburini, jua lilipoanza kuchomoza;

  Marko 16:9 Naye alipofufuka alfajiri siku ya kwanza ya juma, alimtokea kwanza Mariamu Magdalene, ambaye kwamba alimtoa pepo saba.

  Luka 24:1 Hata siku ya kwanza ya juma, ilipoanza kupambazuka, walikwenda kaburini, wakiyaleta manukato waliyoweka tayari.

  Yohana 20:1 Hata siku ya kwanza ya juma Mariamu Magdalene alikwenda kaburini alfajiri, kungali giza bado; akaliona lile jiwe limeondolewa kaburini.

  Yohana 20:19 Ikawa jioni, siku ile ya kwanza ya juma, pale walipokuwapo wanafunzi, milango imefungwa kwa hofu ya Wayahudi; akaja Yesu, akasimama katikati, akawaambia, Amani iwe kwenu.

  Yesu alifufuka siku ya jumapili ambayo Biblia inaiita kuwa ni siku ya kwanza ya juma. Kama Yesu alifufufuka siku ya kwanza ya juma(jumapili), Sabato itakuwa lini??
  Jibu: Jumamosi

  Upendo wetu kwa Yesu

  Je, mtu anaweza kumpenda Yesu bila kushika Amri zake 10???

  Hasha!! Yeye anasema;

  Yoh 14:15(mkinipenda mtazishika amri zangu)

  Yohana 14:21 (Yeye aliye na amri zangu, na kuzishika, yeye ndiye anipendaye; naye anipendaye atapendwa na Baba yangu; nami nitampenda na kujidhihirisha kwake).

  Yohana 15:10 (Mkizishika amri zangu, mtakaa katika pendo langu; kama vile mimi nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake).

  Je, inawezekana kushika Amri 9 tu isipokuwa Sabato???

  Hasha!! Haiwezekani kabisa, Biblia inasema;

  Yakobo 2:10 Maana mtu awaye yote atakayeishika sheria yote, ila akajikwaa katika neno moja, amekosa juu ya yote.

  1 Yohna 2:3-5 Na katika hili twajua ya kuwa tumemjua yeye, ikiwa tunashika amri zake. Yeye asemaye, Nimemjua, wala hazishiki amri zake, ni mwongo, wala kweli haimo ndani yake. Lakini yeye alishikaye neno lake, katika huyo upendo wa Mungu umekamilika kweli kweli. Katika hili twajua ya kuwa tumo ndani yake.

  1 Yohana 5:2-3 Katika hili twajua kwamba twawapenda watoto wa Mungu, tumpendapo Mungu, na kuzishika amri zake. Kwa maana huku ndiko kumpenda Mungu, kwamba tuzishike amri zake; wala amri zake si nzito.

  Wateule wa Mungu ni wapi???

  Ni wale wamwaminio na wampendao Yesu kwa kuzishika Amri zake

  Ufunuo 14:12.(hapo ndipo penye subira ya watakatifu wale wazishikao amri za Mungu na imani ya Yesu).

  Karibu tujiunge kwenye kundi dogooo. Kundi dogo liendalo Uzimani.

  Matt 7:13 Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo.
  14 Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache.

  Fuata Sabato ya Biblia tu.

  Mwenye sikio, na asikie.

  Nawaombea Mungu awafungue akili zenu.

 184. Katika Torati, hawakuwa wakifundishwa kushinda Dhambi, katika Agano jipya Yesu, akasema. Yoh 5.14 Yoh 8.11 USITENDE DHAMBI TENA. Yesu akiwa ndani yako, kiu ya dhambi inaondoka kabisa. Mafarisayo wakasema. MTU HUYU HAKUTOKA KWA MUNGU, KWA SABABU HAISHIKI SABATO. Yoh 9.16. Bwana Yesu akasema kazi ninazozifanya nanyi muniaminio mtazifanya Yoh 14.12 pia akasema yeyote aniaminiye ishara ni hizi, siyo hewa tu, Mark 16.15- na Biblia inaendelea kusema Mitume wakatoka wakafanya kazi, Bwana akitenda kazi pamoja nao, akilithibitisha Neno kwa Ishara. Katika kitabu Yoh 10.31-39 walitaka kumpiga mawe, wakimwambia amekufuru, akawauliza kwa lipi mnataka kunipiga kwa mawe? Wakasema kwa kazi njema hatukupigi, ila umekufuru, aliposema ni Mwana wa Mungu, akawaambia kama haniamini ZIAMINI KAZI NI ZIPI?. Yoh 14.12 Mark 16.15.- kama Injili itahubiriwa kazi hizo hazionekani, basi hiyo ni dini tu kama dini zingine ulimwenguni, lakini kwa kuwa Yesu anaishi, ni kweli alikufa, ni kweli alifufuka, ni kweli anaishi. Kama utashika siku, kama utashika sabato, na usimuone akifanya kazi hizo, elewa kuwa hiyo ni dini kama dini zile ambazo wanzilishi waliisha kufa, na hawakufufuka.thanks.

 185. Yoh 1.11 Yesu alikuja kwake( wayahudi, wasabato) hawakumpokea, mst 12 wote waliompokea akawapa uwezo wa kufanyika WATOTO wa Mungu. Yoh 5.16-18 mambo mawili yaliyowafanya wamsulubishe. 1.Ameivunja Sabato. 2. Amemwita Mungu Baba yake. Hakuna dhambi nyingine waliomshtaki kwayo. Tatizo Wasabato wa Kiyahudi hawakujua Nyakati na majira ya kuijiliwa, nikuonyeshe kifupi jinsi walivyopambana na Yesu. Yoh 7.14-24 Wakatafuta kumua, akawaambia HAKUNA HATA MMOJA ATENDAYE TORATI, Kifupi Torati iliwaleta kwa KRISTO, Rum 10.4 wakakataa kumpokea, bado waking’ang’ania Torati, na Paul anasema UTAJI unawakali ona 2Kor 3.12-18. Kanisa la Kristo wala halisali jumapili tu, haitoshi. Luk 19.47, Luk 21.37 ni kila siku, siyo j2 tu wala jmosi tu. Inahitaji mafunzo marefu kuhusu Yesu na Sabato, Paul na Sabato, ili wafunguliwe macho wampokee Kristo, wawe WANA WA MUNGU, Kwa sasa ni WATU WA MUNGU. Yesu alipowahubiri Luk 4.16- 29 wakamtupa nje. Sabato iliwashinda Wayahudi, ndio maana Yesu akaja. Okokeni mtaelewa Yesu alichokuja kufanya. Thanks.

 186. Shalom. Ndugu, nashukuru kwa mada hii kwani imekuja kwangu kwa wakati muafaka.hivi karibuni nimekuwa nikitafakari na kujiuliza juu ya habari ya siku ya kuabudu ambayo inetajwa ktk biblia. Ktk kutafakari na kusoma neno nikakutana na mistari hiyo,baadhi, ya uliyoitaja hapo juu na hivyo kunihakikishia kuwa sifanyi makosa kwenda kukusanyika na kumwabudu Mungu siku ya jumapili.hivi karibuni wenzetu wasabato walifanya mkutano ktk viwanja vya biafra na nimekuwa nikiufuatilia ktk TV na ktk mojawapo ya siku hizo mhubiri alitumia muda mwingi kuchambua kuhusu sabato na kuhusu siku ya ibada iliotajwa ktk biblia.alisisitiza sana kwamba jumamosi ndio siku ya kukusanyika,yaani siku ya 7 ya juma na sio jumapili! Ndugu zangu hawa watambue kuwa siku ya kukusanyika pamoja, iwe ijumaa,jumamosi,jumapili si jambo la kushikilia sana.MUNGU ni ROHO, na wamwabuduo halisi imewapasa kumwabudu ktk roho na kweli-Yh4:24. Sio kwa habari ya siku.la msingi hapa ni je umeokoka?umempa Yesu maisha yako?soma Yh 9:31.haijalishi unasali siku ipi, km hujamkiri Yesu kuwa ni BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YAKO, ni kazi bure. YESU ni Zaidi ya siku ndugu zangu mnaoamini zaidi ktk siku kuliko ktk Yesu!

 187. Katika agano jipya sabato ya Bwana imewekwa katika viwango vya juu. Badala ya kuabudu siku ya sabato sasa yatupasa “kuomba siku zote” Kumbe kama ibada yako ni Jumamosi tu au Jumapili tu upo mbali na sabato ya Bwana. Soma Lk 21:36 “Basi kesheni ninyi kila wakati mkiomba…”

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s