Kanisa lako lina kurasa wa Facebook??

 

Ni mtazamo tu!

Mahudhurio kanisani yamepungua kutokana na matumizi ya mitandao ya kijamii kuongezeka kwa kasi, Kwenye facebook kuna kila kitu. Kwa upande wa kuhubiri Injili, ziko kurasa nyingi ambazo zinatangaza Neno la Mungu pia ushauri na maombi. Makundi hayo yanafanya kazi nzuri na watu wengi wanaifahamu kweli ya Mungu kupitia Facebook.

Sasa, katika hili ninawasiwasi na mahudhurio ya watu kanisani, Je ni kama zamani? Na vile Idadi kubwa ya wahudhuriaji iko Facebook, Vipi huko kwenye makusanyiko yetu? kanisa lako lina ukurasa wa Face book?

Ebu tujadiliane wapendwa, Je online social networks inahudumia sawa na kanisa la mahali pamoja?

Barikiweni sana!

Advertisements

8 thoughts on “Kanisa lako lina kurasa wa Facebook??

 1. Ukwel mitandao ya kijamii ktk kumuabudu mungu ni sawa na kumkufuru Mungu na kumtukuza shetani coz kama Mungu amekupa afya njema, nguvu, uwezo na nafasi unashndwaje kwenda mahali alipopachagua bwana ili kuliweka jina lake mpk umwabudu kwenye sim, laptop, computer n.k.
  Huo ni mmomonyoko wa maadil ya dini.

 2. Mitandao ya kijamii ni mpango wa shetani wa kumfanya mwanadamu awe busy aweze kumsahau mungu maana ukiwa on net uwezi kukumbuka kuwatembelea wagonjwa,yatima, wajane,wazee,nawatu wengind wanaofanana na hao

 3. Je unajuwa kuwa tabia za kale ndio umfanya mtu kutofaidi wokovu? Kama umeokoka inabidi utubu kwa kina, pia ujifunze Biblia kwa kina yaani uitafsili kiroho sio kimwili yaani jitahidi kufumbua mafumbo yake kwa mfano mlima-ulime, student-stad, Yesu-Yerusalem, Jesus- Jerusalems. Pia kumbuka kuwa matoleo kanisani yana sababu kubwa kwa mfano FUNGU la 10 ni lazima (ada) kusaidia wajane yatima nk.ni wajibu.sio mlango wa kufungua kipato. walokole hawafunguki eneo la kufungua njia hawalitendei haki yaani sadaka ya kawaida wanatoa sivyo fungu la kumi tu ndio wanatenda haki, ok tubadilike.

 4. Kwa mtazamo wangu naona kwenda kanisani ni lazima kwasababu ibada inakamilika kwa sifa,utoaji na neno la Mungu ili upate ukamilifu huu sawasawa ni lazima uende kanisani.Siyo mbaya kutumia kurasa za facebook kwa mda wetu wa ziada.

 5. mimi naona kanisani ni muhimu sn. hyo mitandao labda itumike km mtu upo kzn huna kz yoyote basi uutumie muda huo kupitia mitandao na kujifunza zaid neno la Mungu.

 6. Mitandao yote ya kijamii. Inajenga na pia inabomoa kwa kiasi kikubwa kuna michanganyo mingi sana kule, nakubaliana na mawazo ya mpendwa Jerry, kama kweli unafuatilia Ibada basi ni vyema ukazima vifaa vyote vitakavyo kuondoa mawazo yako.

 7. Mitandao ya kijamii ni mizuri lakini isimfanye mtu kuwa mtumwa na kusahau wajibu wake kama inavyopaswa.

 8. Nafarijika kuchukua nafasi hii kwamba kusema ukweli kwenda kanisani au kwenye mikusanyiko ya injili ni bora sana kuliko kufuatilia kwenye online social Networks
  Ukweli tumeambiwa wakutanapowawili watatu na Mungu anakuwa pamoja nao.

  Siyo kwamba nina kataa Online Social Network siyo nzuri la hasha tatizo ni kwamba ni lazima uwe na nidhamu ya kuitumia kama kweli unafuatilia Ibada basi ni vyema ukazima vifaa vyote vitakavyo kuondoa mawazo yako kama vile simu. Na pia usifungue kurasa nyingi ; kwa sababu nazo zitakufanya uache kuangalia na kufuatilia kwa uangalifu.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s