Yuda alipata pesa lakini alijinyonga. TUBU UISHI

Je wajua ya kwamba kuna uhusiano mkubwa sana kati ya vyanzo vya mapato yako na maisha unayoishi au utakayoishi wewe, watoto wako na vizazi baada yako?

Je wajua usafi wa pesa yako utajidhihirisha kwenye maisha yako na hata kwa watoto wako?

Neno la Mungu linasema “Baraka ya Bwana hutajirisha, wala hachanganyi huzuni nayo” (Mithali 10:22). Maana yake ni kwamba pesa yako ikiwa safi utaona raha yake lakini ikiwa ya damu au itakayosababisha mateso kwa binadamu wengine uchungu wake hautaukwepa. Hi nisheria ya mwenendo wa dunia iliyo hai na isiyobadilika.

Katika injili ya Matayo 27:3-5 tunapata habari ya Yuda aliyejinyonga baada ya kumsaliti Yesu. Wale makuhani wakuu na wazee waliifahamu hii sheria. Pamoja na kwamba alijuta na kuwaambia “Nimetenda dhambi kwa maana nimemsaliti mtu asiye na hatia” na kuzirudisha zile fedha, walizikata wakamjibu, “Hilo latuhusu nini sisi? Ni shauri yako.”

Kwa kuwa hakutubu alikwenda kujinyonga.

Waiona sheria ilivyo sio? Hata waliozitoa pesa walifahamu hatari ya ile pesa.
Je ulishawahi kuiona hii sheria ikiwa kazini?
Ukiziangalia mali zako unaona nini?
Ukiziangalia mali zako unakumbuka nini?
Je wafahamu ya kwamba hii sheria haibagui?
Je unapenda uzao wako uishi kwa amani?

Je wajua ya kwamba Mungu “si mwenye kumhesabia mtu mwovu kuwa hana hatia kamwe?; Je wajua ya kwamba “huwapatiliza watoto uovu wa baba zao, na wana wa wana wao pia, hata kizazi cha tatu na cha nne” (Kutoka 34: 7).

Je wajua ya kwamba mzazi wako akilamba pesa serikali hatari ya ile pesa haikuachi? Je wafahamu pesa za wizi zimejenga nyumba? zimepeleka watu shule? Zimelisha na zinalisha familia?

Hata hivyo, Je wajua ya kwamba Mungu ni “mwingi wa huruma, mwenye fadhili, si mwepesi wa hasira, mwingi wa rehema na kweli; mwenye kuwaonea huruma watu elfu elfu, mwenye kusamehe uovu na makosa na dhambi? (Kutoka 34: 6).

Yuda alijuta lakini hakutubu. Matokeo yake alijinyonga.

Je wajua ya kwamba Neno la Mungu katika Kitabu cha Isaya 1:18 linasema “Haya, njoni tusemezane, asema Bwana. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu”?

Je wafahamu ya kwamba “Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi; bali kama mkikataa na kuasi mtaangamizwa kwa upanga”? (Isaya 1: 19-20)

Katika Injili ya Yohana 8:11 Yesu alimwambia Yule mwanamke “Hata mimi sikuhukumu. Unaweza kwenda, lakini usitende dhambi tena.”

Je UMEAMUA NINI?
Katika Injili ya Matayo 4:17 Yesu alianza kuhubiri akisema: “Tubuni, kwa maana Ufalme wa mbinguni umekaribia.”

Na katika Injili hihi ya Matayo 6:33 Yesu alifundisha na kusema “Lakini utafuteni kwanza Ufalme wa mbinguni na haki yake, na haya yote mtaongezewa”.

UMEAMUAJE???

Emmanuel Kwayu

Advertisements

5 thoughts on “Yuda alipata pesa lakini alijinyonga. TUBU UISHI

  1. Ujumbe umefika kwani neno la Mungu ni sawa ma mvua kwamba ikinya hairudi tena juu bali huichipusha mimea ya kondeni. Hivyo neno la Mungu likitoka kinywani haliwezi kurudi hivi hivi mpaka lizae matunda.

  2. Hakika kila mmoja anatakiwa kutubu hata kw taifa zima lama alivyofanya Daniel ktk sura ya tisa ya kitabu chake. Mungu wetu mwenye huruma.

  3. “Huyo ndiye yule aliyeshuhudia mambo haya na kuyaandika. Nasi twajua kwamba aliyoyasema ni kweli”

  4. Emanuel Mungu akubariki, ujumbe huu umefika, la Mungu ni la Mungu, halisahihishwi, likiishamfikia mtu basi kazi inabaki kwake, ama achague UZIMA( KUTII) MAUTI( KUTOTII) kazi ni kwetu, ambao tumeambiwa siku za mwisho WATU WATAZIPENDA PESA. Ukiipenda pesa utaitafuta kwa hali na mali, na bahati nzuri tunasoma Maandiko, Shetani akamwonyesha Yesu milki ( mali) akamwbia amsujudie ili ampatie, Bwana akamwambia, anayesujudiwa ni Mungu, leo wengi wamesujidia VIUMBE, SANAMU, zenye pesa, hata Wachungaji wengi leo, wategemea sanamu zenye pesa makanisani, wakajikuta WAMELAANIWA, Yer inasema amelaaniwa amtegemeaye mwanadamu, wamesomesha watoto wao kwa hayo, yanaitwa MAPATO YA AIBU. Mtoto amesomeshwa na na hayo, kumbuka SHETANI HAKUPI KITU BURE BILA MALIPO. Tuko kwenye siku za hatari, siku za kua budu sanamu, NiAKINA NANI WATAKAOPONA? 1.SHADRACK 2.MESHACK 3. ABEDNEGO, hawatasujudia sanamu. Ni akina MORDEKAI ndio hawatampi gia magoti HAMANI ( wapenda vyeo ) ni hao, hata kama wataishi kwa shida, watazingoja Baraka za Bwana, hawatakimbilia pesa za kuwafanya wajin yonge baada ya majuto, pesa za kuwaletea watoto wao laana. Ee Mungu tusaidie. Thanks.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s