IMANI – 1

                       

MWENYE HAKI ATAISHI KWA IMANI (HABAKUKI 2:4)

Mimi ni mtumishi wa Mungu namtumikia Mungu kwa njia  ya uimbaji nina albam 3 na ni mhubiri wa neno la Mungu sehemu mbalimbali.Pia ni dakitari katika hospitali ya KCMC Moshi na ninafundisha chuo cha kutengeneza viungo sanifu viungo bandia vya wanadamu hapa KCMC.

Napenda kukukaribisha rafiki uliyeamua kusoma makala haya nina hakika Mungu atasema na moyo wako na utauona utukufu wa Bwana.

Imani ni nguvu inayoishi,kama tunavyosoma katika (Ebrania 11:1) imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo ni bayana ya mambo yasiyoonekana.Rafiki yangu katika maisha ya mtu aliyeokoka swala la imani ni la msingi sana.Imani yetu inatoka kwa Mugu na Mungu tunamuelewa kwa kulisoma neno lake, hivyo imani yetu ikichaganyika na neno la Mungu inakuwa na uwezo wa kuzalisha nguvu.(Ebrania 4:2) lakini neno  lile lililosikiwa halikuwafaa hao,kwa sababu halikuchanganyika na imani ndani yao waliosikia.Hapa tunoona ni jambo moja kuwa na neno na ni jambo lingine kuchanganya neno na imani.Watu wengi wameshika sana neno ila matokeo ya utendaji kazi wa neno hayaonekani  kwa sababu nguvu ya kuamini  lile neno haipo .Mazingira yanakuwa na nguvu kuliko Mungu anachokisema juu ya mazingira na hili  limesababisha watoto wengi wa Mungu kuwa waitaji na kuendelea kuonewa na shetani.

Biblia inasema pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu (Waebrania 11:6).Unaweza ukajitahidi kutenda kama Mungu anavyotaka ila kama hauna imani bado haujampendeza Mungu.Kama nilivyosema mwanzoni mwenye haki wa Mungu ataishi kwa imani inamaanisha bila imani huwezi kushinda changamoto za duniani.Katika makala mengine nitazungumza juu ya viwango mbalimbali vya imani usikose makala hiyo rafiki.Imani tuliyonayo ndiyo inayofanya jambo litokee naye heri aliyesadiki;kwa maana yatatimizwa aliyoambiwa na bwana (luka 1:45).Najua rafiki yangu bwana amesema na wewe mambo mengi sana juu ya maisha yako na huduma yako,unachopaswa kufanya ni kuendelea kusadiki ili umpe njia ya kutimiza alichokiahidi kwako.Ngoja nikupe ushuda huu wangu binafsi ili uendelee kumwamini Mungu

Mimi nilikutana na changamoto kubwa nilipomaliza kidato cha sita.Kidato cha nne nilifaulu vizuri sana nilipata daraja la kwanza (div 1.11)  nikafaulu kwenda shule ya vipaji maalumu Kilakala secondary masomo ya physics,chemistry na biology.Nilijaliwa akili sana ila nilipoanza kidato cha tano niliuguwa sana hadi kupelekea matokeo yangu ya kidato cha sita kuwa mabaya . Nilipata daraja la tatu na nililia sana nikijua ndoto zangu za kwenda chuo kikuu zimekufa,ila kwa sababu nilikuwa mwombaji na mcha Mungu niliamua kutumia ulimwengu wa imani wa kuyataja yasiyokuwepo kana kwamba yamekuwapo na Mungu akasema na mimi kuwa yeye ndiye awapae watu vyuo vikuu na hatimaye nilipata chuo kikuu cha private na serikali ikajitolea kulipa ada yangu kwa miaka yote ya masomo na leo ni mwalimu wa madactari hapa kcmc hospitali.Na Mungu kanipa kazi nzuri nikiwa na umri mdogo sana. Huyo ndiye Mungu ninayemsema na isitoshe kanipa karama ya kuimba na hadi sasa nina albam 3.  Nina shuhuda nyingi za kukujenga msomaji wangu kadri Roho atakavyokuwa ananiongoza nitakuwa nakupa pia kwa sababu shuhuda zinajenga sana.

UTAJUAJE IMANI INAFANYA KAZI?

MATENDO YAKO

Yakobo 2:18 lakini mtu akisema, wewe unayo imani ,nami ninayo matendo.Nionyeshe imani yako pasipo matendo,nami nitakuonyesha imani yangu kwa njia ya matendo.Mstari wa 26 maana kama vile mwili pasipo roho umekufa,hivyohivyo na imani pasipo matendo imekufa.Imani sio maneno matupu ni kile  unachokifanya baada ya kukutana na changamoto fulani.Rafiki jitahidi kadri uwezavyo uweke imani yako kwa matendo.Namwomba Roho mtakatifu afungue ufahamu wako na kila roho inayokuzuiya ikuachie kwa jina la Yesu.

Tukimwangalia Abrahimu baba yetu wa imani alikuwa mtu wa kuweka imani kwa matendo,kila Mungu alichomwamuru afanye alifanya.Mwanzo 12:1 Bwana akamwambia Abrahamu,Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako,uende mpaka nchi nitakayokuonyesha.Hapa tunaona Abrahamu alikuwa na imani akaondoka,pia bwana alimwambia mwanzo22:2 Akasema umchukue mwanao,mwana wako wa pekee,umpendae Isaka,ukaende zako mpaka nchi ya Moria,ukamtoe sadaka ya kuteketezwahuko juuya mlima mmojawapo nitakaokwambia.Tunaona Abarahamu alifanya kama bwana alivyomwambia na akahesabiwa kama baba wa imani.Mungu anapima matendo yako kuidhibitisha imani yako na matendo yako yanaweza kukana ua kukubaliana na imani.Matendo yako yakiwa kinyume yanakukana mbele za Mungu.Kama nilivyosema imani ina uhakika na uhakika unaonekana kwenye matendo yako

Nataka ufahamu kwamba vitu vyote vinavyoonekana havikufanywa kwa vitu dhahiri (Ebrania11:3) Mungu alitumia imani  kuumba ulimwengu. Na sisi ni miungu lazima tutumie imani kwa matendo kuumba vitu tunavyoviitaji maishani.Rafiki nakutia moyo endelea kuchochea karama yako ya imani siku hadi siku ili umpendeze Mungu na atajibu mahitaji yako.Wewe ni mtu wa thamani na Mungu anatanani ufanane na yeye iliuwe balozi mwema wa Kristo. Nakupenda sana, tutaendelea na makala haya katika kipindi kijacho na somo letu la imani.Kama unahitaji msaada zaidi wasiliana nami kwa njia hizi.

Doca LIGHTNESS WILLIAM NG’UNDA , 14 June 2012

Advertisements

14 thoughts on “IMANI – 1

  1. Nimelipenda sana hili somo naona kila nikisoma imani yng inazidi kuongezeka na kuzidi kuamini. Naona ushindi

  2. Barikiwa mdada,nifannyeje ili nimpate mume niliyeoneshwa kwenye ndoto? maana kila nipatatapo mchumba ile ndoto uludia kuwa mmewako ndio huyu.Mungu akubariki.

  3. Upendo wa Mungu Baba, na nehema ya Bwana wetu Yesu Kristo, na ushirika wa Roho Mtakatifu, viwe nawe daima. Shadrack from kenya

  4. Ubarikiwe dada. Mungu aendelee kukutumia, mchungaji Samuel ubarikiwe umeniongezea kitu kikubwa

  5. Dada Lightness, Bwana akubariki sana kwa somo zuri la IMANI. Katika mstari ulioutumia, anasema ( MWENYE HAKI ATAISHI KWA IMANI YAKE) Unajua wengi wetu tunakwama pale tunapojaribu kutembelea Imani za watu wengine, nikakumbuka kuwa Musa aliambiwa apige bahari, nayo itaachia njia, na ndivyo ilikuwa, na kweli Israel wakapita pakavu, na Wamisri walifikiri kuwa hata wao watapita kama Waisrael, walipojaribu walizama, hata siku za leo, wengi wetu mara nyingi tunajaribu kuvuka kwa kutumia imani za watu wengine, kinachotokea ni kuzama. Biblia pia inasema, KILA MTU ATENDE KAMA ALIVYOKUSUDIA MOYONI MWAKE, SIYO KWA HUZUNI WALA SIYO KWA LAZIMA. 2 KOR 9..6,7. Unaona watu wengi tumefanya kazi ya Mungu kwa HUZUNI ama kwa LAZIMA, halafu tukadai kuwa tumefanya kwa Imani, na kwa hali hiyo tukangojea baraka, oh hatukuzipata tulizozitegemea, asante kwa ushuhuda wako, umenijenga. Ubarikiwe, Roho Mtakatifu aendelee kukutumia, japo hujasema kama umeolewa, mimi ni Mchungaji, nawaombea mabinti ambao hawajaolewa ili waolewe, nimewaorodhesha kwenye diary yangu, huo mzigo ninao, hilo limekuwa tatizo kubwa kwa mabinti wengi hasa WASOMI kama wewe. Mungu akubariki. Asante.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s