Nimeanguka kwa dhambi ya ulevi

Shalom watu wa Mungu naomba mniombee kwani mimi ni muimbaji wa nyimbo za injili lakini nimeanguka katika dhambi ya kunywa pombe plz wapendwa naomba maombi yenu kwangu, Mungu wangu awabariki. its me

Ev, Elibariki Zablon

This entry was posted in Uncategorized. Bookmark the permalink.

8 thoughts on “Nimeanguka kwa dhambi ya ulevi

  1. Pole sana mtumishi ila cha muhimu funga na kuomba utapata jibu kumbuka lipo jibu kwa yesu

  2. nawasalimuni wote katika jina la Yesu Kristo Mungu wetu wapendwa watu wa Mungu nashkuru Mungu amenifanikisha kutoa albam yangu ya kwanza ila cjaua nitaanza vip kuitangaza radioni plz naomba ushauri wenu kwangu

  3. BWANA YESU asifiwe wewe ndugu siotu unahitaji maombi bali kwa hakika unahitaji Delivarance(ufunguliwe!) uwehuru ulevi ni roho kamili kama unavyoona ilivyo ktk roho zingine,unakuta mtu mzinzi anashindwa kuacha lakini hapendi pata huduma inayo fanya maombi ya Delivarance ufunguliwe ktk kifungo cha ulevi na endelea kukataa hiyo roho huku ukiomba nguvu za MUNGU zikutoe hapo ulipo kwama uta fanikiwa bila hivyo itakuwa nirahisi kuanguka anguka mwisho uta vunjika (uta angukia na mambo mengine!) Naomba tuombe pamoja Baba ktk jina la YESU kristu wa nazaret nina mleta ndugu huyu aliye kwama ktk mtego wa pombe nikiomba huruma yako na rehema zako juu yake sawasawa na neno lako linalo sema BWANA ukituweka huru tunakuwa huru kweli kweli! kama ulivyo tufungua sisi ktk kifungo hicho cha pombe kwa miaka mingi na ukatuweka huru nina kuomba kwa upako wa ROHO mtakatifu kila roho iliyoko nyuma ya unywaji wake wapombe imwachie sasa ! Ninatamka kumfungua roho na fsi na mwili wake ktk jina la YESU kristo wa nazaret aliye hai!asante BWANA YESU kwa kumfungua Ndugu huyu nimeomba nikiamini na kumfunika kwa damu ya YESU yenye thamani iliyo mwagika msala bani!AMEN!(Frederick

  4. Yesu wa nazareth anapendezwa na watu walio wazi.umekuwa mkweli na yupo tayari kukurehemu.ukishatambua udhaifu wako,YESU huitaji kitu kimoja.Yaani,usirudie tena!.

  5. pole sana mrudie mungu tubu na kuiamini injili, achana na ulevi endelea kumtumikia mungu kwa njia ya uimbaji, pole sana

  6. Ndugu Elibariki, nakusalim katika Jina la Yesu. Pole na yaliyokupata, lakini bado kungali na matumaini. Nianze hivi, inaonekana wewe ni MTU WA MUNGU. maana ndio maana umeomba watu wa Mungu wakuombee, ebu piga hatua uwe MWANA WA MUNGU Yoh 1.12 BALI WOTE WALIOMPOKEA ALIWAPA UWEZO WA KUFANYIKA WATOTO WA MUNGU. Baada ya kufanyika mtoto wa Mungu, ndipo IYOH 5.1-5. Kila kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu..( soma mistari hiyo kwa utulivu) pamoja na hayo yote, liko jambo la ziada unalotakiwa kufanya. 1.KUKATAA 2. KUJILINDA. Mungu amempatia mwanadamu uhuru wa kuchagua, alimwambia Adam USILE TUNDA. Haikuwa kazi ya Mungu kumchunga asile. Soma mist. Ifuatayo kwa makini. 1YOH 5.18 TWAJUA YA KUWA KILA MTU ALIYEZALIWA NA MUNGU HATENDI DHAMBI, BALI HUJILINDA, WALA YULE MWOVU HAMGUSI. Tito 2.11. NEEMA YATUFUNDISHA KUKATAA UBAYA. Ndio nikasema, jifunze kukataa, jifunze kujilinda, ukifanya hivyo utashinda na maombi ya wana wa Mungu yatakuwa na matokeo. Ukitaka msaada zaidi tafadhali nipigie simu.0765 446611. Ubarikiwe.

  7. ingawa msalaba wa Yesu upo na kazi ya msalaba bado ipo, na damu ya Yesu bado mbichi, ingia kwenye toba. usingojee watu wa kuombee, kwasababu hawataomba. Ingia katika toba, uombe rehema na neema, Mungu atakusamehe, kazi ya msalaba ni kwa walioanguka na si wale wanaojiona wasafi, jinyenyekeze mbele za Mungu kwa toba naye atakusamehe na kukupa moyo mpya, atakutakasa.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s