Sala ya Toba, imeandikwa kwenye biblia?

Bwana Yesu asifiwe sana, tuambizane wapendwa kuhusu sala ya Toba kwa ajili ya kuwaongoza watu kumpokea Bwana Yesu, Je imeandikwa wapi kwenye Biblia?

– Sijaona Yesu akimwongoza mtu sala ya Toba

– Wanafunzi wake pia hawajafanya hivyo

-Hata Mtume Paulo naye haijaandikwa kamwongoza mtu sala ya toba

–Richard

Advertisements

18 thoughts on “Sala ya Toba, imeandikwa kwenye biblia?

 1. NDUGU ZANGU NIMEZIONA COMMENT
  Lakini naomba tusipende kujaji vitu kabla hujafanya research SALA YA TOBA IPO NA IMEANDIKWA KWENYE BIBLIA SOMA ( ZABURI 51:1—19)
  Hapo ndo watumishi wengi wanatumia kama sala ya toba.

 2. JE NENO LA MUNGU LINAHITAJI NYONGEZA, ILI LIPATE SAPORT, KUTOKA KWA WANADAMU?

 3. Mungu awabariki watumishi kwa mafundisho mazuri. Nifanyeje ili niweze kuwa ninapata mafundisho moja kwa moja kutoka hapa Strictly Gospel?.

 4. Wapendwa, hebu tuacheni utani, hivi huu mchezo wa kuigiza tunaojidanganya nao, eti Mungu “AMETUPA FUNGUO NA MAMLAKA YA KUFUNGUA NA KUFUNGA na anasema lolote mtakalofungulia duniani na mbinguni limefunguliwa, lolote mtakalolifunga duniani na mbinguni vivyo hivyo.” halafu kwa maelezo hayo kila mtu anaanzisha jambo lake kama hiyo sala ya toba na kujiaminisha kuwa Mungu ameupokea utaratibu huo!

  Hivi kama jambo hili la ‘kufunga hapa duniani’, iwapo Mungu angeliachia bila kulifunga ktk Neno lake ingekuwaje? Maana kama angeliacha lielee, basi hakuna mprotestant ambaye angeingia, kwani Katoliki walikwisha kuwafungia nje zamaaani! Na hata waprotestant tumefungiana sana mmoja kwa mwingine, na bado tunaendelea kufungiana! Lakini ukweli ni kwamba hayo ya kufunga na kufungua yalikwisha fanywa na mitume na miongozo hiyo kuwekwa katika Maandiko, UBATIZO ukiwa ni moja ya hayo!!

  Nimeona wapendwa wakimrejea Kornelio katika kuhalalisha mafundisho yao yenye kuukimbia mpango wa Mungu wa wokovu kwa kujidanganya na mafundisho dhaifu ili kujihalalishia wokovu. Wanasema wale watu pale walipoisikia ile hotuba ya Petro wakabadili mwelekeo wao, yaani wakaingia ktk toba, na kumpokea Kristo ndipo wakajazwa Roho Mt., kwa hiyo nao pia wakiisha kunena kwa Lugha hujihesabia haki nje ya mpangilio wa Mungu wakijiaminisha kuwa wamekwisha kutiwa mhuri nk!

  Ili kujua kilichotendeka kwa Kornelio, ni lazima usome jambo hilo lilikoanzia. Biblia inasema sadaka zake zilipokelewa mbinguni na kuwekwa kuwa ukumbusho, wakati huo hata Petro hamjui! Petro akiwa ni mwili wa Kristo aliletwa hapo ili akamilishe mzunguko kulingana na mpango wa Mungu, na pia tukio hilo lilikuwa ndilo kielelezo cha kwanza cha kuwaonesha Wayahudi kuwa Mungu amewaita pia Mataifa kama ilivyosema ile hotuba maarufu ya Petro akiwa chini ya uvuvio wa RMt, ile sehemu ambayo RMt alitangaza njia ya wokovu kwetu sote tulioitwa tumjie Bwana Mungu wetu. Na sasa jambo hilo likitimia, Mungu akiithibitisha ile kauli yake kwa Kornelio na pia utaratibu mpya wa wokovu kulingana na Injili iliyokabidhiwa mitume kama ilivyotangazwa na Petro ktk ile hotuba. Naye RMt anapotawala tukio, huwa hatoki nje ya kusudi lake, ndio maana kwa uthibitisho huo, Petro anatangaza tena kuwa kama Mungu amewafanyia hao jambo hilo ni nani awezaye kuzuia wasibatizwe, ndipo AKAAMURU WABATIZWE KWA JINA LAKE YESU KRISTO!! (Hebu wazia hili, kama ni Roho Mt. tayari wamejazwa, wana haja gani tena ya kwenda kubatizwa? Bali akiwepo RMt yeye hukuongoza ktk Neno). Hakuna sala ya toba hapo wala toba iliyofanyika wala hakukuwepo haja ya toba kwani kulingana na mlolongo wa matukio, hapo kulifanyika uthibitisho tu wa wokovu! Tofauti na mafundisho yetu tunayojipangia ambapo tunavitafsiri vifungu vya Maandiko ktk namna tuipendayo sisi na kumsingizia RMt kutuongoza ktk hayo. Sisi tunajiongoza katika sala ya toba kwa kuyarudia yaliyoandikwa ktk Rum 10:9 na kisha kujivika wokovu tukiyalazimisha Maandiko kuifuata hiari yetu, ndio maana tunaishia ktk hali tuliyomo inayojiwakilisha zaidi kimapokeo na si ktk uongozi wa RMt kama alivyohusika hapo kwa Kornelio na matukio mengine ya aina hiyo! Nyumba ya Kornelio chini ya uongozi wa RMt, naye Petro akimuwakilisha Kristo, lile Neno, alikamilisha mzunguko wa wokovu kwa kuwaingiza katika UBATIZO WA JINA LA BWANA YESU KRISTO; huo ndio uongozi wa RMt unavyotenda kazi!! Mmeona ndugu zangu? Hakuna maelezo ya kimahiri ya kurasa kumi kuukwepa Ubatizo na kujiridhisha kuwa unaongozwa na RMt na kujitungia sala nyingi za kuamsha hisia. Injili ikihubiriwa katika uhalisi wake, INAYO NGUVU ndani yake ya kumkamata mwenye dhambi na kumuongoza ktk toba. Maana toba hutokana na Imani katika kile ulichokisikia, hiyo Injili, nayo Imani hukuleta uweponi mwa Mungu hata ukamuomba msamaha kwa jinsi ulivyokwenda kinyume na “Baba yako mpenzi” na sasa umeisikia Sauti yake nawe umemwitikia! Huo ndio utaratibu wa kweli ambao msingi wake, milango ya kuzimu haiwezi kuutikisa, kwani wewe mwenyewe ni shahidi wa hayo na si ku mimic sala ya toba kama kasuku; ukija upepo wa kusi, unakungoa hadi tumizizi twako!

  Mungu yu ndani ya Neno lake, hakuna Mungu nje ya Neno lake. Yeyote anayeyashikilia mambo au mafunuo ambayo yako nje ya Neno la Mungu, anajipotezea wakati na uzima, maana hayo yote ni hekima ya mwanadamu na hivyo Mungu haitambui, yaani ni UBATILI!

  Bwana na atujaze Imani yake!

 5. haijaandikwa.ni makosa makubwa kuwaongoza watu sala ya toba.binadamu yabidi atubu kwa kinywa chake na aamue mwenyewe kuacha tabia mbaya kama Zachayo alivyofanya.

 6. Wapendwa,

  Sala ya toba haijaandikwa mahala popote. Ukiacha neno lisemalo, “TUBUNI” kwa kuwa ufalme wa Mungu umekaribia….” hakuna sehemu zaidi.

  “Sala ya toba” ni utamaduni tu ulioletwa na makanisa ya kipentekoste na kievangeliki. Ni utamaduni wa kurithi toka kwa waitwao, “mababu” zetu wa imani aka mababa wa kiroho.

  Kwani mtu akifa ghafla kwa ajali au kwa kularuriwa na simba au nyoka mkali anapata wapi muda wa kuongozwa kwa sala ya toba. Kule kuomba Mungu kwa dakika chache au sekunde chache kabla ya kifo, huenda kunaokoa walio wengi sana ambao mauti huwakuta kwa ghafla. Ndiyo maana Yohana alioneshwa maelf na maelfu ya watu wakiwa mbinguni kwa idadi kubwa sana isiyohesabika.

  Wewe unadhani wanaoenda mbinguni ni wale tu wanaoongozwa kwa sala ya toba? Thubutu yako? Kuna maelfu na maelfu wasiohesabika wataingia mbinguni bila kupitia taratibu na desturi za madhehebu yetu.

  Unajua idadi ya Wakristo hapa duniani wako wangapi? Kwa taarifa yako kati ya watu zaidi ya Bilioni 6 walipo duniani kwa sasa, wakristo hawajafika hata bilioni 3 ya watu wote duniani!!!!!!! Yaani hata 50% haifiki. Na hapa ni kama ukihesabu kila aijiitaye Mkristo bila kujali utauwa na utakatifu kama kigezo. Sasa hao watu aliooneshwa Yohana wasiohesabika wanatoka wapi kama siyo wale wanaotubu papo kwa papo wanapokabiriwa na kifo?

  Ubarikiwe.

 7. haleluya watumishi wa Mungu. hii sala ya toba biblia imeiandika kwa wale wanaosoma bible watakubaliana nami, Kinachogomba hapo ni kutafuta ule mtirirko ambao tunautumia. hhhahahaha hii sio retrujia,,,, basi ukitaka kujua mtiririko ulipo basi hata mahubiri tunayo hubiri yawe na mtiririko wa kufanana na yaandikwe kwenye biblia nadhani itakua hatuongozi tena na roho bali kitu kingine, Imesema TUBUNI, Katubu..,,,, inatosha na kwa muelewa wa bible atajua,,,, naomba Bwana awape moyo wa hekima amen

 8. Ndugu Richard,

  Asante kwa makala nzuri inayoelezea wokovu unavyopatikana kulingana na maandiko yanenavyo, yaani kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua Yesu kutoka kwa wafu ili kuhesabiwa haki na kukiri kwa kinywa chako ya kuwa Yesu ni Bwana ili uokoke (Warumi 10: 8 – 10)

  Jambo moja labda umepitiwa au hukuliwaza ni kuwa unapochukua makala ya mtu mwingine na kuitumia kama ulivyofanya ni uungwana kuweka hilo wazi ama sivyo unaweza ukaeleweka kuwa unaibia kazi ya mtu mwingine, sidhani kama hilo ndio lengo lako.

  Mwandishi wa makala uliyoibandika ni Greg Stier ambaye anaandikia jarida la Christian Post mara kwa mara.

  Ubarikiwe na Bwana Yesu!

 9. Listen to this zinger Jesus shot in Matthew 7:21 about those who think they can just say the right words and be saved, “Not everyone who says to me, ‘Lord, Lord,’ will enter the kingdom of heaven, but only he who does the will of my Father who is in heaven.”

  And what is the Father’s will? Jesus answers that question clearly in John 6:40, “For my Father’s will is that everyone who looks to the Son and believes in him shall have eternal life, and I will raise him up at the last day.”

  Saying a prayer is not believing in Christ, believing in Christ is believing in Christ. Now, having said that, somebody may be expressing their faith in Jesus in the form of a prayer which is great! But just saying “the magic words” (aka “Lord! Lord!”) doesn’t save anyone.

  Many, “just say these words” defense attorneys turn to Romans 10:9,10 to make their case, “…if you confess with your mouth, ‘Jesus is Lord,’ and believe in your heart that God raised him from the dead, you will be saved. For it is with your heart that you believe and are justified, and it is with your mouth that you confess and are saved.’

  But it’s hard for me to believe that, if saying a prayer is essential for salvation, God would confine this command to just one passage of Scripture. And it’s impossible for me to believe that, if saying a prayer is required for salvation, that some form of Sinner’s Prayers wouldn’t be sprinkled across the Gospels and the book of Acts.

  Actually, if you read Romans 10 in context, it has just as much to do with evangelism as it does salvation. Romans 10 is the “How will they hear without a preacher?” passage. Confessing that “Jesus is Lord” in this context was a way of preaching to friends, neighbors and relatives that you were now a follower of Jesus, that you now believed that “Jesus is Lord.” This confession was considered heresy by the Jewish community (who believed only the Father, YAWHEW, was Lord) and treason by the Romans (who thought only Caesar was Lord.)

  This controversial confession accompanied public baptism in the closest river or lake and was very public in nature. This public confession of faith identified you as a Christian and steeled and sealed your faith and your fate (which could include being mocked, marginalized or murdered by angry neighbors!)

  Believing in our hearts justifies us (declared us righteous in the eyes of God.) Proclaiming with our mouths saves us in the sanctificational sense of the word. In other words, our internal faith saves us from hell and confessing our faith verbally and publicly saves us from a stunted Christian walk. Faith gets us in the kingdom. Confession makes us more like the King because we are boldly identifying ourselves with Jesus!

  All this to say that I have no problem leading someone through a salvation prayer (and I do it a lot!) with this important caveat. I ALWAYS tell the person that saying a prayer doesn’t save them, it’s just a simple way of expressing their newfound faith in their newfound Savior to their newfound Father.

  No, the Bigfoot of the Bible is nowhere to be found. But what is found is a victorious Savior who died the death that we deserved then rose to offer us the new life we didn’t. Let’s put our focus and faith in the rock-solid reality of Jesus, not the legends of the mysterious and elusive sinner’s prayer.

  If you agree then just say these words outloud to God…(just kidding!)

 10. Kwa ufahamu wangu, sala ya toba haijaandikwa popote kwenye Biblia kama watumishi waliotangulia walivosema. Isipo kuwa ni utaraibu na ufunuo ambao Mungu aliweka ndani ya mtu fulani mahali fulani, utaratibu ukaendelea vizazi na vizazi, na sisi tukaona ndivyo inavyotakiwa.

  Utaratibu huu hauna madhara na Mungu pia anauheshimu. Kwani amesema litakalofungwa Duniani na Mbinguni limefungwa. Kwa ujumla naona ni utaratibu ambao Mungu aliruhusu tuwe nao kwa ajili ya kujihakikishia wenyewe kuwa mtu tunayemuongoza sala ya toba yuko tayari kutubu, japokuwa si kipimo chenye uhakika sana ila Roho Mtakatifu hushuhudia na nafsi zetu.

 11. Sala ya toba tyunayowaongoza watu haijaandikwa popote kwenye biblia,ila tumejitungia tu wenyewe. Kutubu ni sahihi, biblia imesema tutubu, lakini haijasema tuwaongoze watu sala fulani maalum ya kutubu kama tunavyofanya leo.

  Mara nyingi hii sala huwa iko hivi: Sema baba Mungu, mimi ni mwenye dhambi,nisamehe dhambi zangu leo, lifute jina langu katika kitabu cha hukumu, liandike jina langu katika kitabu cha uzima……

  Sijawahi kusoma katika biblia mahali ambapo kanisa la kwanza walimwongoza mtu sala ya toba, hata Paul mwenyewe hakuongozwa sala ya toba.

 12. Biblia inasema tubuni nakuiamini Injili, pia unaposali tusiwe kama wanafki, tujifungie ndani kwa kumtukuza Mungu aonae sirini atatujazi

 13. Tusizunguke zunguke sana, jibu ni kuwa Sala ya Toba kama tulivyoizoea, haijaandikwa popote kwenye Biblia, lakini sioni kosa kwa mtu kumuongoza mwingine sala ya toba. Cha msingi ni kuelewa toba ni nini? Kutubu ni kubadilisha mawazo yako na kugeuka toka upande mmoja na kuelekea mwingine. Katika suala la wokovu toba ya kweli ni pale unapogeuka na kuachana na mawazo yako, mitizamo yako, dini yako, jinsi unavyoweza kujiokoa mwenyewe na vitu vingine vyote na kumgeukia Bwana Yesu upokee wokovu.

  Kuna mpendwa hapo juu amegusia wale watu kwa Kornelio waliokuwa wakimsikiliza Petro halafu wakajazwa Roho Mtakatifu. Sasa wote tunaelewa ya kwamba huwezi kujazwa Roho Mtakatifu kama hujaokoka, hivyo basi hawa ndugu waliokoka wakati wanamsikiliza Petro ndipo wakajazwa Roho Mtakatifu. Kwa maneno mengine walipokuwa wakimsikiliza Petro walibadili nia zao, waligeuka toka walichokuwa wakikiamini na kumwamini Yesu kama mwokozi wao, na ndipo wakajazwa Roho Mtakatifu.
  Tunasoma katika Matendo 10:43 -44 ;- Huyo manabii wote humshuhudia, ya kwamba kwa jina lake kila amwaminiye atapata ondoleo la dhambi. Petro alipokuwa akisema maneno hayo Roho Mtakatifu akawashukia wote waliolisikia lile neno.

  Petro wala hakuwa ametumia maneno kama “lazima mtubu” lakini tuna kila sababu ya kuamini kuwa walitubu na kuamini, maana hata baadaye wakati Petro alipotoa ushuhuda kwenye baraza Yerusalem, mitume walisema hivi: Waliposikia maneno haya wakanyamaza, wakamtukuza Mungu, wakisema, Basi, Mungu amewajalia hata mataifa nao toba liletalo uzima – Matendo 11:18.

  Hivyo wale mataifa walijaliwa TOBA LILETALO UZIMA bila ya kuongozwa kile tunachokiita leo “sala ya toba”.

  Mbarikiwe!

 14. Ndugu Richard, bwana akubariki kwa swali zuri uliloliuliza, ebu tuchange mawazo, siku tulizomo ni siku za hatari kama Biblia inavyotujulisha, ebu nikupe mfano mmoja kwenye Biblia kabla sijatoa mawazo kuhusu Sala ya toba. Mdo 10.34 mpaka 43 Petro alikuwa anahubiri nyumbani kwa Kolnelio, na wale watu ndio siku hiyo walikuwa wamekusanyika kwa Kolnelio, ona mst 44. PETRO ALIPOKUWA AKISEMA MANENO HAYO ROHO MTAKATIFU AKAWASHUKIA WOTE WALIOLISIKIA LILE NENO. Hii inaonyesha jinsi mioyo ya watu hawa ilivyokuwa tayari, walipokea tu hata bila kuwekewa miko, lakini Mdo 19.6 Paul akaweka mikono juu yao, Roho akaja juu yao WAKAANZA KUNENA KWA LUGHA, unaona watu siku tulizonazo mioyo iko mbali, hata ungeweka mikono na miguu bado kupokea inakuwa kazi, mpaka wahubiri wapige hendeli, wanawaambia. Semeni ASANTE YESU, ASANTE YESU, mpaka wengine ndipo wanafanikiwa, wengine wanaambiwa nenda umejazwa kwa Imani, nije kwenye SALA YA TOBA. Mdo 2.37,38, WALIPOYASIKIA WAKAULIZA TUTENDEJE ? Jibu TUBUNI. Hapo ndipo Petro alifakisha kuwafikisha, na ili mtu aokoke lazima AMKIRI YESU KWA KINYWA. So naona aliwatubisha. Yoh 21.25 yote yangeandikwa Ulimwengu usingetosha. Barikiwa.

 15. Bwana YESU asifiwe!

  RICHARD
  sisi ni makuhani wa YESU yeye aliye kuhani mkuu,KUHANI maana yake mtu/mwanadamu asimamae mbele ya YESU kuwaombea msamaha wengine waovu/wakosaji Soma ZABURI ya 94:16 (Ukisoma mstari huo Mungu anauliza nani atakaye simama MBELE YAKE kwa ajili ya waovu? jibu swali hilo. MUNGU aanze kufanya kazi na wewe kama kuhani wake hapa Duniani

  PILI, Unakuwa wakili au balozi wa siri za Mbinguni na kwa kuwa sisi watakatifu(Tuliookoka) wa duniani, Mungu ametufanya miungu wadogo wa uungu wake, AMETUPA FUNGUO NA MAMLAKA YA KUFUNGUA NA KUFUNGA na anasema lolote mtakalofungulia duniani na mbinguni limefunguliwa, lolote mtakalolifunga duniani na mbinguni vivyo hivyo.

  Elewa kwa kuwa umekuwa Kuhani wa YESU duniani,hayo yote unayafanya,ukiokoka na kuishi katika waokovu warumi 10.9…. na Roho Mtakatifu anaushirika na wewe hata ukiwa kwenye basi mtu akiwatayari kuokoka,unaweza kumuongoza sara ya Toba kadri Roho Mtakatifu atakavyokuongoza KUTAMKA TOBA YA HUYO MTU na akaokoka hapo hapo.

  TAFADHARI SANA,USING’ANG’ANE SANA NA KULISHIKA NENO KICHWANI KAMA WAISLAMU BALI NG’ANG’ANA NA ROHO MTAKATIFU AKUPE UFUNUO,MAARIFA NA HEKIMA YA KULIJUA NENO NA MAFUNUO YAKE.
  maana andiko uua,bali neno uuhisha

  AHSANTE ROHO MTAKATIFU

 16. Injili ya Yesu ilitanguliwa na Yohana na yeye kazi yake kubwa ilikuwa kuaambia watu “tubuni ufalme wa Mungu umewaijia…” waliotubu wakabatizwa na wakawa wanafunzi wake kisha wanafunzi wa Yesu pia wlaibatiza je unategemea waliobatizwa hawakufanya toba? inategemea mahali na jinsi gani mtu ameongozwa na Roho mt kwingine mtu akihubiriwa tu na kujua yupo na alikuwa akitenda dhambi walianza wao kutubu mfano Petro alipowahubiria wayahudi jinsi Yesu alivyoteswa na kuuawa ktk matendo ya mitume ni wao walimuuliza tufanyeje sasa maana tumekosa….tubuni mkabatizwe ndilo jibu.
  Huwezi kuokolewa bila ya kukiri kwa kinywa chako….Rumi 10: 9-10 utakiri nini? kama umeamua kumfanya Yesu ni Bwana na mwokozi wa maisha yako basi ni lazima ujutie yale yote uliyokuwa ukifanya kinyume na wokovu.
  Sio kila kitu kimeandikwa directly ktk Biblia lakini ukisoma kwa makini utaelewa. Ubarikiwe

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s