Friends On Friday yamtukuza Mungu kwa kufikisha mwaka mmoja

Friends On Friday (FoF) ni kundi la vijana wa kikristo ambalo linaunganisha vijana wakristo na kutengeneza mtandao wa wafanyabiashara wa kikristo, kubadilishana uzoefu wa fani mbali mbali, kufahamiana, kufurahi pamoja, Muziki, chakula cha jioni nk

FoF ilianza Mwaka jana tarehe 2 July, 2011 ambapo Mkondo wake katika jiji la Dar-es-Salaam kama idea mpya kabisa katika ulimwengu wa Kikristo, mpaka wamefikia mafanikio makubwa na kumshukuru Mungu kwa jinsi alivyowawezesha tangu wameanza mpaka sasa.

Matarajio ya FoF ni Kutengeneza Matukio makubwa ya kikristo yenye viwango, ambapo wakristo watakuwa wakikutana na kuufurahia upendo wa Mungu pamoja na burudani mbali mbali.

Maono yanabebwa na Wanakamati 9

Sam Sasali kama Mwenyekiti

Renee Lyatuu kama Katibu

Protace Godwin kama Finance Director

Antony Luvanda kama Afisa mahusiano

Prosper Mwakitalima (kushoto) kama Mchambuzi wa biashara

Amani Paul, Idara ya Ufundi

Chris Mauki, Mshauri Mkuu

Jimmy Uncle kama Mkuu wa masoko

Clara Kolle, Mratibu wa Matukio

Kama inavyoonekana pichani ” FoF Moja Juu” theme ya mwaka huu!

Katika tukio la kufikisha mwaka, siku ya Ijumaa tarehe 6, July 2012 walifanya tukio kubwa eneo la Makumbusho kuanzia saa 1 Jioni na kumalizika saa 6 Usiku. Baadhi ya waimbaji walioimba usiku huo ni Miriam Lukindo wa Mauki, Pastor Wambura, Amani Kapama, Sarah Shila na wengine.

FoF wanakutana kila Ijumaa ya kwanza ya mwezi hukutana na kubadilishana mawazo, kuburudika na kujenga mtandao. Kwa mawasiliano zaidi kuhusu FoF wasiliana moja kwa moja na mwenyekiti Sam Sasali 0713 494 110

Advertisements

4 thoughts on “Friends On Friday yamtukuza Mungu kwa kufikisha mwaka mmoja

  1. nawaombea Maisha malefu Mungu awabariki ili mtimize malengo mliyo jiwekea kuielimisha Jamii,Mungu awape Maarifa msije kufanikiwa,sana Mkamkufuru.

  2. kweli kundi hili lina malengo mengi lakini hili suala la uvaaji nami naungana na dada Grace kweli Biblia inasema tuitimize haki yote, wapendwa hasa wadada mimi sijui yamkini ni akili zangu lakini naomba mumuombe tena Roho Mtakatifu hasa katika mavazi awaoneshe je mpo sahihi? Mnisamehe kama nitakuwa sijasema vizuri lakinilengo langu si baya. Mbarikiwee

  3. kundi ni zuri sana maana linajumuisha wakristo wote bila kujali ameokoka au hajaokoka na malengo ni mazuri, ila kwa kweli kuna tatizo la uvaaji wa baadhi ya waliokoka kwenye kundi hili maana hautofautishi nani kaokoka nani hajaokoka, wapendwa mliokoka kwenye kundi hili jaribuni kuonekana ni wana wa Mungu kweli hususani uvaaji haumbariki Mungu kabisa, samahani kama mtakwazika.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s