Strictly Gospel yaongoza Blog bora Tanzania, 2012

Tuna kila sababu ya kuwashukuru watembeleaji wote na walioipigia kura blog ya SG katika uchaguzi wa kutafuta blog bora ya mwaka nchini, Blog ya Strictly Gospel imekuwa nafasi ya kwanza kwenye kipengere cha “Best Religion Blog” hii ni kwa mujibu wa website ambayo imeandaa shindano hilo Tanzanian Blog Awards.

Siyo jambo dogo kwetu, inaonesha watu wanabarikiwa kutokana na blog hii, nasi tunamrudishia Mungu sifa na Utukufu kwa kila kinachofanyika kwa ajili ya kuliinua jina la Mungu mahala hapa.

Tuzidi kuombeana, kushauriana na kuonyana pale tunapokesea ili mwili wa Kristo uzidi kujengwa na watu wakamjue Mungu kupitia blog hii.

Mungu awabariki.

Advertisements

19 thoughts on “Strictly Gospel yaongoza Blog bora Tanzania, 2012

 1. its A time to say thank you Jesus, by the way Strictly tutafika mbali, i am also a member and a friend of SG. stay in touch.

  Ev.moses Mayila
  New hope world wide ministry

 2. Amen! hongereni sana dada Mary na washiriki wote wa Strictly Gospel!!! Hii blog naipenda sana ic very informative. Ushindi ni mojawapo wa changamoto na inatia moyo kwa wamiliki, wahariri, n.k.

 3. Amen….Mungu atukuzwe kwa kuinua Blog hii. Barikiwa dada Mary.

  Wengi wametiwa nguvu kusimama vizuri katika imani, kupitia, mafundisho, faraja na maonyo sawa sawa na neno la Mungu. Nina imani wengi pia wamempokea Yesu kupitia blog hii.

  Mbarikiwe

 4. Shalom wapendwa,
  tunashukuru sana kwa comment zenu na kututia moyo, tunashukuru kwa maombi yenu watakatifu ambayo yameiwezesha SG kusimama hadi leo. Tuzidi kuombeana kama kaka Samuel anavyosema, tuzidi kumwombea zaidi Mary asimame imara ktk utumishi wake huu. Kila mmoja ni sehemu ya SG kwa namna moja ua nyingine hivyo namuomba Mungu pamoja na tofauti zetu za kimadhehebu tuwe na Umoja kama Yesu alivyotuombea. Mbarikiwe sana wapendwa.

 5. Shaloom Watumishi wa Mungu, Pastor ELIA kisigila. Anthony Mwenda. Iqualiptus Malle. RoseMary Lusinde. Herman Mapunda, John Paul, Mary Damian. Pamoja na Washauri wa Blog hii, sasa twaweza kuwaombea (effectively) kwa majina yenu kabisa, tofauti na tulivyokuwa tunawaombea (Generally) Nawatakia kila la kheri, nikisema Ikor 15.58. BASI NDUGU ZANGU WAPENDWA, MWIMARIKE,MSITIKISIKE, MKAZIDI SANA KUTENDA KAZI YA BWANA SIKU ZOTE, KWA KUWA MWAJUA YA KWAMBA TAABU YENU SIYO BURE KATIKA BWANA, Mbarikiwe. Ndugu yenu.

 6. Asanteni kwa maoni yote.

  Kipekee nawashukuru watu wanaofanya huduma nami, SG Ministry kwa kutaja majina ya viongozi wakuu. Pastor Elia Kisigila, Anthony Mwenda, Iqualiptus Malle, Viongozi wa maombi dada Rosemary Lusinde, kaka Herman Mapunda. Na wanaosaidizana pamoja nao.

  Pia tunaoshirikiana kuendesha Blog hii kaka John Paul na kaka Iqualiptus Malle. Bila kuwasahau washauri wa blog hii.

  Bila nyie wote SG isingekuwepo, nawapenda sana, barikiweni mno kwa muda wenu!

 7. Hongera Dada Maria kwa vision hii nzuri sana ambayo Mungu alikupa nawe ukaitendea kazi, Mungu akubariki sana

 8. Congrats Mary for the good work.., i suggest you change tha background to a lighter colour. I find this one too dark and stressful for the eyes.

 9. Dada Mary,

  Ubarikiwe……kutuletea uwanja wa kufundishana….kubadilishana mawazo…..na mitazamo….Naamini kwa wengi wetu kuna mambo mengi ya kujifunza toka kati yetu…ambayo labda hatuwezi kuyapata makanisani mwetu…..UBARIKIWE DADA MARY……

 10. Naona tunahitaji kuwaombea ndugu hawa wanaoiendesha blog hii, japo hatuwajui, lakini haitakuwa vibaya tukiwafahamu, ili tunapowaombea tuweze kuwataja hata kwa majina yao itapendeza, ni kweli wanafanya kazi nzuri, Mungu awabariki, awaongezee Hekima na Maarifa, pia na Miaka mingi ya kuishi. Kwa jina la Baba Mwana na Roho Mtakatifu. Amina

 11. Sifa apewe Mungu pekee! hata mie nashangaa kwasababu halikuwekwa hapa ili watu wapige kura isipokuwa watu wenyewe wameichagua kwa kuongozwa na Roho mt.
  Wakati ni kweli hatuitaji barua ya sifa (CV) ili kujitambulisha kiroho lakini vilevile ushuhuda wa wengine kwa Blog hii ni habari njema yenye kuiwezesha kuwafikia wengine na injili kuendelea kutangazwa. Dada Mary na wengineo Mungu azidi kuwatia nguvu.

 12. Amina, utukufu kwa Mungu kwa sababu anawawezesha watumishi wake kutenda sawasawa na utume mkuu aliotuachia Bwana wetu Yesu Kristo.

 13. Hizi ni habari njema kwa blog hii na wote wanaoifurahia. Mungu awape neema ya kuyakuza na kuyatunza maono ya kazi yenu.
  ”Furahini katika Bwana siku zote……”

 14. Shalom wapendwa, kama SG hatukujua hili shindano wakati likianza pia hatukushirikisha watu kutupigia kura. Website iliyoandaa mashindano hayo inaweka vipengere na watu kupendekeza majina ya blogs na kupigia kura kutokana na vipengere husika, katika kipengere cha Best Religion Blogs

  Best Religion Blogs
  1. https://strictlygospel.wordpress.com
  Tied for 2nd place
  2. http://hosannainc.blogspot.com
  2. http://mungupamojanasi.blogspot.com
  3. http://godfaithfull.blogspot.com
  4. http://gospelcorner.wordpress.com

  Mwaka jana blog iliyoongoza ni http://hosannainc.blogspot.com

  Kwavile kuna watu wamependekeza blog ya SG na wengine kupiga kura, tumeona si jambo jema kuwa kimya kutojali muda wao na mitazamo yao.

  kufahamu zaidi kuhusu mashindano haya fuata link hii
  http://www.tanzanianblogawards.com/2012/07/matokeo-ya-2012.html#more

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s