Maandishi ya kiarabu?

Maandishi pichani yanasomeka kama SALAAM kwa maana ya AMANI

Naomba jibu wapendwa, Je, ni kwa nini maandishi yanayohusiana na uchawi na ushirikina huandikwa kwa Lugha ya KIARABU?

Advertisements

12 thoughts on “Maandishi ya kiarabu?

 1. Hata mimi nashidwa kuelewa labda wanapenda maneno hayo coz watu weng hawafamu nini maana ya maneno hayo

 2. Wapendwa,

  Kwanza eleweni kwamba Majini ni Mapepo, Pili, majini yanajua Lugha za wanadamu, Tatu, maandishi ya Kiarabu kama Lugha nyingine yeyote hutumiwa katika ushirikina. Si hoja Kwanini Kiarabu kitumike katika Ushirikina. Mapepo yapo kote na yanaendesha shughuli zake kwa kufuata, Lugha, mila, Desturi, Kanuni na taratibu za Sehemu na Mahali husika! Wote tunajua katika sehemu nyingi za Mwambao wa Pwani, ndiko kulikuwa Makazi na Tawala za Waarabu. Kwa maana hiyo, wakazi wote wa sehemu husika waliweza kuzungumza na kufuata mira na desturi za kiarabu na hata matendo ya Kiimani.

  Itakuwa kioja kwa Mkazi wa Pwani (Kabla ya sasa ambapo kunamuingiliano mkubwa wa tamaduni) Umfanyie uuguzi kwa Lugha ya Kisukuma, Kifaransa, Kikelewe, Kinyaturu, Kisubi, kingureme, Kikabwa, Kijaruo nk! Atajua labda unanena kwa Lugha, na kama maandiko yasemavyo, Kunena kwa Lugha ni kwa manufaa ya mnenaji! Usukumani ukipeleka uuguzi wa mambo ya Nazi na Maandishi ya Kiarabu, wataona wewe ni Mwizi huna lolote! Huko nenda na Mambo ya Nyoka, fisi, Bundi, Mitungha, Kabebha nk! Vivyo hivyo, ukienda Sengerema Bila habari za “Lutegho”, nako hutaeleweka! Shetani anayajua haya fika,. Ushirikina ni Matendo ya Imani, ujue Shetani Imani yake iko juu sana, Biblia husema kuwa, Imani ya Shetani ipo kwa kiwango cha kutetemeka! Kwa njia hiyo Shetani hufanikiwa sana katika Mambo yake! Kuuoanisha Uislamu na Ushirikina ni kukosa uelewa! Hakuna mantiki wala maelekezo popote kuwa majini huongea Kiarabu tu. Ni kweli Kruan hukubali kwamba Mungu huabudiwa na Majini na kwamba Kruan imeandikwa kwa Lugha ya Kiarabu, lakini hilo halitoi ushahidi wa moja kwa moja kuwa Kiarabu ni Lugha maalumu inayotumika kishirikina!

  Mimi Binafsi, nakumbuka nilipo kuwa Darasa la Nne,(Kwetu ni Bara) Baba yngu Mdogo akishirikia na Rafiki yake, walikuwa na Jini lililokuwa likitwa ‘Biheko’ Sielewi jina hilo lilikuwa la Kabila gani, ila nakumbuka Biheko alikuwa akizungumza Lugha nyingi sana, alikuwa na uwezo wa kutaja majina bila kuambiwa, kutambua aina ya tatizo alilonalo mgonjwa, aliweza kuleta pesa kwa wingi kila siku! Kilichonishangaza kuliko vyote ni pale Mimi , mdogo wangu (Kwa sasa ni Mchungaji huko Mbeya) pamoja na Mama mdogo tulikuwa Shambani tukimteta Biheko (Yule Jini). Tuliumbuliwa vibaya sana, usiku ule wazi wazi. Biheko alitaja bila kusitasita kwa Lugha yetu wnyewe, jinsi tulivyokuwa Tukimteta na kumdhihaki katika huduma yake ya Kijini, aliendelea kufoka kuwa tulimponda na kusema kuwa yeye (Biheko) hakuwa Mtu wala kitu halisi ni uongo tu wa wale wazee yaani Yule Baba mdogo na Rafikiye, ili wapate pesa! Nakwambia, Biheko alitutishia maisha kiasi kwamba tuliishi kwa hofu na mashaka kwa mda mrefu sana. Beheko alisema kwamba, anauwezo wa kutugeuza katika umbo lolote apendalo kama tutaendelea kuongea Upuuzi tukiwa huko shambani au mahali popote bila kujari umbali yeye atajua na kusikia yote. Habari hii ilikuwa mbaya sana kwangu, maana baadaye Mdogo wangu nilikumbusha ile Hadithi ya Mzee Shaban Robart katika kitabu chake Adili na nduguze – Wakati Huria Binti mfalme wa Majini alipo wabadili Hasidi na Mwivu nduguze adili katika umbo la Nyani! Biheko alisema, huo utakuwa mwisho wenu wa kuwa Binadamu! Lakini mdogo wangu alinitia moyo kwa kusema, hawezi Bwana! Nikamuuliza, hawezi kwanini?……alikaa kimya, baadaye akasema, Mbona alishindwa kumuua Yule Mchungaji ambaye amejenga kanisa katika kiwanja kinachogombea? Tukiona tu dalili yoyote tutamwambia Yule mchungaji…….tukikaa kwa Yule mchungaji Biheko ataogopa kuja! Nilikubali kwa kichwa, nikatabasamu!

  Na katika kudhibitisha kuwa yeye (Biheko) ni kitu halisi, kesho yake (Usiku – Maana yeye Biheko, alikuwa akija usiku tu ili kuagua watu!) Biheko alikuja na Mke na Watoto wake wapatao 100 na Mke mmoja na wote walitaja majina yao (lakini jina moja moja tu), sauti zao zilikuwa za kitoto, kivulana, kisichana na sauti ya Mwanamke halisi – lakini hawakuonekana kwa macho, wala husikii kishindo kama wanatembea au kujongea au kuja kila wanapo karibishwa na Baba yao kujitambulisha. Kitu kingine kilichotushangaza, Wote waliingia mmoja mmoja katika kile chumba kidogo na kuishia humo(Maana tulisikia sauti zao za kunong’ona), chumba chenyewe, tayari kilikuwa kimejaa watu waliokuwa wamekuja kufanyiwa uuguzi! Biheko aliongea Kiingeleza kwa ufasaha sana kwa rafidhi ya Kizungu hasa! Viyo hivyo aliongea Kisomari, Kinyarwanda, Kisubi, Kirundi, Kisukuma, Kikelewe, Kizinza na mara yangu ya kwanza kusikia Kiarabu nilikisikia akiongea Yeye na Mzee mmoja Mwarabu aliyekuwa na Duka kubwa sana hapo senta!

  Majini ni Mashetani na kupitia Biheko niliona mambo mengi ambayo jini Yule aliyoyafanya, lakini kuna Mengine yalimshinda, aliposhindwa aliahidi uongo au kutoa vitisho, nk (Sina mda wa kusema yote) Ila nimeona nitoe Uhshuhuda huo mdogo ambao ni wa kweli kabisa, ili watu wajue kuwa Uislamu au Lugha ya kiarabu si pekee hutumiwa na Shetani!

 3. Hiyo ni kweli kabisa na hata majina ya Majini Ni kama yale yanayotumiwa na Waislamu (Mf Maimuna,Sharifa ,Makata n.k)

  na ni kwa Nin majini wengi huwashia Wanadamu wenye Jinsia ya Kike na siyo sisi

 4. mh….,NAONA KAMA MWANICHANGANYA ZAIDI HEBU TAFAKARINI KIROHO NA KIELIMU LABDA NITAPATA KUWAELEWA

 5. Iko hivi, uchawi mwingi unaotumika ni uchawi wa kutumia majini na uislam unaamini kuwa majini ni viumbe kama viumbe wengine na wanaweza kufugwa, hivyo jini litakalo fugwa na muislam nilazima litakuwa linajua lugha ya kiarabu na lugha inayotumika katika uislam ni kiarabu, hivyo mchawi au mganga yeyote anapotaka kutumia jini ni lazima atatumia lugha ya kiararabu kwani ndio lugha inayotambuliwa na viumbe hao. NOTE: Nimalachache sana kwa mtumiaji wa nyama ya nguruwe kuendeshwa/kukumbwa na majini kwani yanajua na kuamini kuwa mtu huyo ni najisi… (fanya utafiti utaona)

 6. Ndugu mpendwa, nathani kuna uhusiano kati ya lugha ya kiarabi na uchawi, maana wanaamini mapepo na majini ni viumbe vya mwenyenzi Mungu na baadhi yao ni viumbe wazuri kabisa.

 7. kiarabu ni lugh kama lugha nyingine, inawezekana wachawi wa kwanza walikuwa wanaongea lugha hiyo. mimi nimeokoka na ninampenda bwana, lakini pia nimebarikiwa kuwa na degree ya 2 la kiswahili na ualimu, hivyo ntakujibu kama mwalimu na muumini. Kwanza nilidhani Allah ni mungu wa waislamu, hadi siku niliyokutana na wapendwa waafrika weusi wa kisudan, wanaoongea kiarabu na kiingereza tu, walikuwa wanasikiliza kanda ya DVD ya kisudan, maneno yaliyokuwa yanaimbwa kwenye ile miziki ya kumwabudu mungu ilikuwa inamsifu Allah, na maneno mengi ya kiarabu, hadi nilipomuuliza, kwanini wanamtaja allah, akasema biblia ya kwao inamtaja mungu Yehova kama Allah, Hivyo ni lugh tu, naamini kama kuna wachawi wanaojua kuandika kwa lugha zao, wataweza kuandika uchawi wao kwa lugha wanayoijua.

 8. Mpendwa Primi, Ubarikiwe?

  Una maoni gani sasa kuhusu Biblia zilizoandikwa kwa Kiarabu kama uyasemayo unayaamini? Je, Wakristo walioko Urabuni wanatumia lugha gani zaidi ya Kiarabu ambacho umesisitiza kwamba ni lugha ya majini?

  Je, unakubaliana na mazingaombwe? Unajua hilo alilofanya huyo maganga wako ni mazingaombwe tu ya kawaida? Wakati naishi pale Magomeni Makuti Dar, nilikuwa naenda mitaani kushangaa wanamazingaombwe? Wanaweza kukwambia kwamba wakichoma makaratasi yataoa noti mpya mpya tu za shs 10,000 sasa wewe utakubaliana nao?

  Hivi unaelewa kwamba waauguzi wengi wa kutoka Kongo (Zaire) hawatumii Kiarabu kwenye manjonjo yao ya kiganga? Unajua kwamba wanaotumia lugha ya kiarabu kuagua wengi ni wale waliowahi kuwa waislam au walipewa dawa hizo na waislam? Kama wakipewa na dawa hizo na mganga wa kifipa au wa kiha toka Manyovu au Kibondo na hajawahi kuwa mwislam nakuhakikishia hatatumia lugha ya kiarabu.

  Usichanganye mazingaombwe na ukweli halisi? Kiarabu kama lugha kilikuwepo hata kabla ya Uislam kuanzishwa karne ya 6 kule Maka na Madna.

  Je, Waarabu ulimwenguni kote wasiojua lugha zaidi ya kiarabu wakiokoka na kumfuata Yesu Kristo wanaacha kusema au kutumia lugha ya kiarabu?

  Naomba majibu ya maswali yangu yote.

 9. Mr Milinga ulichoeleza ni ukweli kabisa lakini kwa upande wa pili tukubali kuna uhusiano kati ya lugha ya kiarabu na ushirikina. Mi mwenyewe kabla sijamjua Mungu niliwahi kwenda kwa mganga akaandika maandishi ya kiarabu kwenye karatasi kisha akaombea halafu akaichoma moto ile karatasi lkn nilishangaa yale maandishi yalitokea yanan’gaa kwa mwanga mkali nikamuuliza yule mganga akasema alitaka kunidhibitishia kuwa yale maandishi ya kiarabu kuna nguvu ya ajabu kupitia majini.
  Ni kweli waislamu safi hawaamini ushirikina lkn wana majini na huyatumia japo wanadai kuna majini mema na mabaya lakini hatuamini hicho kwa maana wanaseme hata hayo mema ukiyakosea yanakushughulikia, kwahiyo kuna uhusiano mkubwa kati ya hiyo lugha na ushirikina. Nilimuuliza yule mganga ikiwa ataandika kwa kiswahili kisha kuyaombea itakuwa hivyo akasema majini yake hayatambua lugha nyingine katika utendaji wa kazi zao kwahiyo haitatokea. Tukiangalia kihistoria aliyemwambia mtume ajitabirie kuwa ni mtume alikuwa mganga wa kienyeji kwa hiyo kuna connection na pia hata Quran inatambua kuwepo kwa majini na huwa kuna ibada ambazo wanafanya na majini.
  Tujuavyo sisi tuliomwamini Kristo kama Bwana na mwokozi wa maisha yetu majini ni viumbe hatari na hatuwezi kushirikiana navyo kwa kuwa ni wakala wa shetani bali tumepewa mamlaka ya kuwaamuru kuondoka ili wasiendelee kumtawala mtu.

 10. Mpendwa Emanuel Sameji, nadhani hujaeleza ukweli. Lugha haina uhusiano na mapepo. Wanaotumia lugha ya kiarabu kwenye maswala ya ushirikina ni waislam wanaojua lugha hiyo ya kiarabu. Hata hivyo, ukiwahoji waislam wanaoufuata uislam kwa dhati kabisa watakwambia kwamba ushirikina haujaruhusiwa katika imani yao.

  Mimi hapa nilipo naishi nyumba ya Shekhe, ndipo nimepanga kwake. Ninaishi bila matatizo kwa kupanga pamoja na Waislam. Mimi tu ndiye Mkristo lakini wapangaji wote waliosalia pamoja na mwenye nyumba ni waislam.

  Lugha ya kiarabu haiwezi kutumiwa na Mkristo au mpagani aliyeamua kurudi kufanya matambiko na ushirikina.

  Kuna wakristo wengi sana wanaozungumza lugha ya kiarabu. Kuna Biblia za kiarabu nyingi. Nenda Dubai utazikuta. Hata hapa kwa Shekhe wangu ipo. Ipo pia ile ya Kiebrania kabisa. Shekhe anayo na huwa tunajaribu kuisoma ingawa sijui lugha hiyo.

  Watu wengi wanaofanya uhuni huo wa ushirikina hutumia KIARABU kama njia ya kuwaghilibu watu tu. Ni njia ya kuwaaminisha watu (hasa waislam) wadhanie kwamba kwa kuwa KIARABU ndiyo lugha iliyotukuzwa na uislam, hivyo Mungu anahusika na hayo maswala ya ushirikina na kwa hiyo wanachokifanya wafikirie kuwa Mungu anahusika. Lakini kiukweli KIARABU ni lugha tu kama zilivyo lugha za kawaida.

 11. Ni kwa sababu uchawi ulizaliwa huko!na falme za kipepo zinatumia lugha hio hio!kwahio ni rahisi kuelewana!pia wenzetu wanatambua kwamba mapepo ni viumbe vya mwenyezi Mungu,na kwa mana hiyo wanayafuga kwa maelewano yao,kwahiyo kwa lugha yao wanaelewana.

 12. To my side I think hayo maandishi huwa yanakuwa na ujumbe fulani kutoka katika kitabu fulani kinachohusiana na mambo hayo ya kishirikina. Lakini Lugha kama lugha haina uhusiano wowote na uchawi, maana Wako pia Waarabu ambao wanamjua Mungu na wanaisoma Biblia yao iliyoandikwa kwa maandishi ya Kiarabu.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s