Mbunge aibua hoja Tanzania kujenga ubalozi Israel

Mh. Asumpta Mshama

Mbunge wa Nkenge Kwa tiketi ya CCM, Bi Asumpta Mshama, ametumia andiko hili kujenga hoja ya Tanzania kufungua ubalozi kamili huko Israeli. “And it shall be, that whoso will not come up of all the families of the earth unto Jerusalem to worship the King, the LORD of hosts, even upon them shall be no rain” (Zechariah 14:17). Kwa wale wasiomfahamu, ni mama yao wale akina “J sisters”, mabinti wanaoimba nyimbo za injili.

Nakumbuka alijibiwa na naibu Wa Wizara Ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Mahadhi Juma Maalim alieleza kuwa Tanzania haendeshi mambo yake Kiroho sababu kama Taifa halina dini ispokuwa Waumini wake, vile vile alieleza kwa sasa Tanzania haijatenga fedha za ajili ya Uanzishwaji huo wa Ofisi ya kibalozi, aliendelea kueleza kuwa Tanzania ina Mwakilishi wa Heshima huko Tel Aviv.

Joel Msella

Advertisements

26 thoughts on “Mbunge aibua hoja Tanzania kujenga ubalozi Israel

 1. Achana kumwabudu Mungu wa Agano Jipya kwa Agano la kale, hayuko kwenye Agano la Kale sasa hivi.
  Mimi nilishawaambia kuwa maombi yenu hayawezi kubadili mpango wa Mungu juu ya Israel, kila kitu kwa Israel kitatimia kwa wakati ulioamuriwa. Kutimia kwa mpango huo haiko kwenye mapenzi ya Mungu yanayohitaji mwingilio wa mtu, bali kwenye mapenzi ya Mungu yasiyohitaji mwingilio wa mtu.

  Kuweni makini sana na maandiko ya Agano la Kale ambayo mnajaribu kua-apply ktk Agano Jipya- Kuna gap kubwa la kiagano kati ya hivi vipindi viwili vya Mungu kushughulika na mwanadamu.

 2. Israel Taifa unique tofauti na mengine kwa utawala huu Mungu awape na kuwaongeza hekima viongozi Hawa maana wameona mbali ,,,,,,Nyerere huenda hakusoma neno aliweka siasa mbele hicho ndicho kilichomfanya akurupuke Baba yetu ila Mungu Amlaze apanapositahiri kutii ni bora kuliko mafuta ya beberu, ….Amani idumu nchini hili ndilo ombi langu kwa Mungu.

 3. ndugu tusome biblia zetu vzr tutajua nn wajib wetu juu ya kuombea Israel na Jerusalem, ni wajib na lazma kwa wanaomwabudu mungu wa israel kuitakia amani nchi hyo na watu wake

 4. ISRAEL NI TAIFA TEULE HATA WOKOVU UMETOKA KWAO HVYO TUIHESHIMU ISRAEL HATA KAMA IKFANYA NN BIBLIA INASEMA MTU AKIILANI ATALAANIWA NA M2 AKIBARK ATABARKIWA JIULZE KWA NN USA INA MALI NYING JE TANZANIA KUNA V2 VNG VYA KU2PATIA MAL MADINI MENGI MITO ARDH MISITU ISRAEL NI NCHI NDOGO LAKINI MUNGU AMEIBARIKI. TUKIBARIKI NASI TUTABARIKIWA

 5. Inasemekana kwamba MAREKANI huwa wanatoa fungu la kumi la mapato yake kila mwezi au mwaka nchini Israeli ili kutafuta baraka ya Mungu iwakalie

 6. kitendo cha kuwa na ubalozi wa Israeli nchini Tz,ni hali yakuleta mahusiano zaidi na Israeli nakuwathamini maana MUNGU amesema atayeibariki Israeli atabarikiwa na atakayeilaani atalaaniwa,kwahiyo kutokuwa na ubalozi wa Israeli Tz ni tafsiri tosha kwamba hatuna mahusiano mazuri sana na Israeli,kwahiyo inawezekana tupo ktk laana fulani maana viongozi wa juu hawajui umuhimu wake kiroho tumuombe Mungu ili viongozi wetu wafunguliwe macho.maana wenzetu kenya wana ubalozi wa israeli nchini kwao ndio maana hata bidhaa zao zinavutia kuliko zetu,mfano hata sabuni,blue bend nk za kenya zinamvuto sana kuliko zetu.

 7. Ninachouliza ni kwamba, kwani, Tanzania kuwa na Ubalozi Saudi Arabia ni kigezo gani kilitumika??

  Lakini pia, kuwe na hekma katika kuhitaji nasi tuwe na ofisi ya ubalozi Israeli, huwezi hata kama wewe ni mtu wa Imani kuuliza na kwa kunukuu maandiko au andiko kama hilo (ZEK. 14:17) kwa suala la kisiasa parce kama hilo la kufungua ubalozi.

  Nami ni mtu wa imani, ninantambua umuhimu wake, lakni pia, ni lazma kujua namna ya kupigana vita, naam, vita nyengine ni kwa kutumia hekma katika kutambua ya kuwa, hii nchi, hatuko peke yetu tu, wako Waislamu pia, na madhehebu mengine ya Kikristo ambayo, wao, umuhimu tunaouona wa kufungua ubalozi Israeli, is not their priority kabisa. Pia, ni lazma kujua ya kuwa, mtawala aliyepo sasa si mwenzetu kiimani, na wala hawezi kuelewa hilo jambo. Akhsante na Mungu awabariki.

 8. “Siasa na Neno la Mungu ni kama maji na mafuta” vitu hivi wilwili havichanganyikani -nanukuu aliyoyaimba Munishi. Maendeleo ya nchi fulani hutegemea watu wake na juhudi zao. Kufungua ubalozi nchini Israel au kutofungua hakuna maana ya kuleta mabadiliko ya Wanzania kama Watanzania wenyewe hawatabadilika. Tumshukuru Mungu ya kwamba sisi ni Watanzania na wala si Waisrael au taifa jingine. Tumshukuru Mungu kwa vile sisi tumebarikiwa na Serengeti, Manyara, Oldvai, Ruaha Mlima Kilimanjaro na pia Watanzania wenye makabila 121 nk. Tuna Ziwa Viktoria lililo chanzo cha mto Nile. Bila hilo Wamisri wasingiweza kumwagilia mashamba yao; tena tuma majirani zetu aha!!!!!. Sisemi ya kwamba tusishirikiane na nchi hiyo ya Israel bali nasema isiwe kupitia Maaandko. Mbunge wetu aangalie yawezayo kutubadilishia maisha na kuleta amani nchini mwetu.

 9. Ndugu Mpendwa,

  Tanzania hata kama itafungua ubalozi na Israel haifanikiwa. Labda itafanikiwa ikijaribu kuwaleta kwa maksudi Waisrael wapewe mashamba makubwa pale Morogo, Kigoma, Rukwa, Ruvuma na Kagera ili walete ufundi wao wa kisasa katika kilimo. Lakini kama tutafungua ubalozi kwao au wao wakafungua kwetu halafu mambo yakaendelea kama yanavyoendelea kwa sasa itakuwa ndoto tu.

  Waisrael wakipewa kandarasi ya kujenga Reli yetu ya Kati, ile ya kwenda Moshi na Musoma hadi Kampala, ile kwenda Rwanda na Burundi wanaweza wakaitengeneza ndani ya Miaka 10 tu. Lakini sisi huenda itatuchukua miaka 200 hadi kuzikamilisha reli hizo.

  Waisrael wakija kwa kushirikiana na Marekani wakapewa kandarasi ya kusambaza umeme nchini, Tanzania baada ya miaka 10 itakuwa na umeme hadi vijijini kwa zaidi ya 90% ya watanzania. Lakini sisi peke yetu na umbea mwingi, maneno mengi na blaa blaa nyingi, kujipenda kwa sana, kupenda sifa sana, tunapenda kuhusudiwa sana na wananchi, mikogo mingi mno; Waziri Mkuu akienda sehemu umati wote wa wafanyakazi wa wilaya humfuata kila aendako, wanachoenda kuzindua au kukagua hukioni.

  Waisraeli wakipewa nafasi Tanzania wao wana utamaduni wa kupenda kazi. Wanafanya bila unafiki wala kupendeleana kama ilivyo sisi wabongo. Mbongo akipewa kazi mshahara wote anaumalizia kwenye ngono, pombe, na ushirikina na kuvaa viwalo vya nguo za bei kubwa balaa. Muisrael yeye anachapa kazi. Sisi ni wavivu kwa kwenda mbele. Hatujui tuendako. Waisraeli wanajua wafanyalo na waendako. Nako waendako ni kuitawala dunia. Wanataka wawe kichwa kwa kila kitu. Sisi tumejaa maneno matupu, mara ……aliyeko juu mungojee chini, mara pole pole ndio mwendo, mara, Mungu akipenda, mara aliyekupa wewe ndiye kaninyima mimi, mara tunawafukuza ombaomba wa mitaani hala Rais unamsikia kaenda kuomba misaada Uarabuni, mara Marekani, mara Sweden, nk. Yaani hatuna mwelekeo.

  Inakuwaje, Taifa kama hili lipange kutumia bajeti ya shilingi Trilioni 15 wakati mapato yake halisi ni Trilioni 8 tu kwa mwaka? Hii ni akili kweli?

  Inakuwaje, Taifa hili lipange kutumia shilingi trilioni 10 kwa matumizi ya kawaida yaani mishahara, posho, ukarabati wa majengo na mafuta ya magari serikalini wakati mapato ya taifa ni Trilioni 8 tu. Hapa akili ipo kweli. Jamani mpaka tuwalete waisraeli watuelekeze namna ya kupanga mapato na matumizi? Hata hili la kujua KIPATO CHAKO NI KIASI GANI KWA HIYO UTUMIE KIASI GANI, Inahitaji UBALOZI WA ISRAELI?

  Hivi jamani, hadi tuwe na ubalozi wa Israeli hapa nchini au kule nchini kwao ndipo tutaweza kudhibiti matumizi mabovu ya fedha zetu na rasilimali za taifa.

  Je, Ubalozi wa Israeli ndio utazuia mafisadi wasiendelee kuuza wanyama kutoka mbuga zetu za Wanyama na kuwauzia waarabu? Hadi ndege inapakia TWIGA wakiwa hai na kuruka nao hadi nchi za kiarabu, waisraeli ndio waje kutufundisha uzalendo jamani?

  Jamani Ubalozi wa Israeli tukiupata ndipo tutaweza kutengeneza madawati ya shule za msingi na sekondari? Miti yote tuliyonayo tumeshindwa kutengeneza madawati ya kutosha watoto wetu wa shule waache kuketi chini wakati wakiwa darasani? Hili nalo mpaka tuwe na Ubalozi wa Israeli?

  Mpaka tuwe na ubalozi wa Israeli hapa kwetu eti ndipo tutaweza kusaini mikataba yenye akili badala ya walowezi kuchukua fungu la 97% na sisi kuambulia fungu la 3% kwenye migodi ya madini eti tukipata ubalozi wa Israeli tutabadilika tusiwe tunasaini mikataba kama ile ya akina Mangungo enzi za utumwa na ukoloni. Eti Waziri Mzima na PhD yake au Masters Degree yake anasaini Mkataba unaotaka Mgeni achote madini yetu kwa 97% sisi aturushie kakipande ka 3% tu. Hapa unasubili ubalozi wa Israeli ndio uokoe jahazi? Utangoja sana mpendwa?

  Je, tunasubiri Ubalozi wa Israeli uje ndipo tuwabane wale jamaa wenye mabilioni ya fedha kule Uholanzi? Eti watu wasiozidi 6 wanamiliki akaunti zenye zaidi ya shilingi bilioni 300 Uholanzi? Halafu hakuna hata kiongozi wa serikali anayeshituka na kuchukua hatua za kufreeze akaunti hizo? Ni mtanzania gani mwenye uwezo wa kuwa na bilioni kama hizo kama siyo mwizi? Hapa tunasubiri Ubalozi wa Israeli uje kwetu ndipo tuchukue hatua?

  Mimi bado ninayo mengi ya kujiuliza. Ubalozi wa Israeli kuwepo au kutokuwepo Tanzania je itabadilisha chochote bila watanzania kubadilika?

 10. Asante bwana Kinyau.

  Najibu maswali yako:
  1.Si lazima kwamba utafanikiwa kama yeye alivyofanikiwa,itakuwa hivyo tu kama utaweza kuyafanya yaliyomfanya yeye afanikiwe. Lakini umuhimu wa kujiunga nae ni kwamba utaweza kupata siri ya mafanikio yake.

  Ukimpinga,kwanza hutaweza kumfanye asifanikiwe kwa huko kumpinga kwako, pili unaweza kukosa siri za mafanikio yake na matokeo yake ukabaki hujafanikiwa katika hilo eneo. Ndio maana nikasema ni vizuri kama nchi tukawa na uhusiano mzuri wa kibalozi na Israel maana wamefanikiwa katika mambo mengi ambayo tunahitaji na sisi tufanikiwe.

  2. Jibu liko wazi; Israel wamebarikiwa na Mungu baraka ya milele katika kila kitu ikiwemo ardhi, ndio maana inatoa mazao japo ni jangwa. Lakini suala si udongo wao tu kubarkiwa, wao wenyewe kama watu wamebarikiwa sana na maarifa ya kutosha katika kilimo. Hata wakija kulima Tanzania watafanikiwa.

  3.Maana ya baraka kwa kifupi ni nguvu ya kukuwezesha kufanikiwa, na Laana ni nguvu ya kukuwezesha kushindwa. Hakuna taifa kwenye biblia ambalo Mungu amelilaani milele,ispokuwa kama kuna taifa watu wake watakubali kufanya mapenzi ya Mungu bado Mungu atalibariki taifa hilo. Tofauti na Israel, hata wanapokuwa wamemkosea Mungu bado huwaangalia kama wana wake,kiasi kwamba ukiwagusa katika hiyo hiyo hali ya kumwacha Mungu, Mungu anakushughulikia.

  Kwa hiyo siyo kila ambaye hajafanikiwa kalaaniwa,hapana, yawezekana hajajua tu jinsi ya kuitumia nguvu ya kumfanikisha (baraka) iliyo ndani yake. Na nasikitika kusema kwamba wakristo wengi hawajafanikiwa kwa sababu ya kutokujua jinsi ya kutumia hiyo nguvu iliyo ndani yao.

  Ki ukweli, kila aliyeokoka alitakiwa afanikiwa kama mwisraeli wa kimwili au zaidi, na hilo ndio lilikuwa kusudi la Mungu kuleta wokovu kwa mataifa.
  Ubarikiwe.

 11. Shalom wapendwa
  kuungana na Israeli kwa vigezo vya kimwili yaani kiserikali ni sawa tu ingawa nao wanamisimamo yao jinsi ya kuwa na ubalozi. Ni kweli Israel iko juu, kiulinzi, kiuchumi na technolojia. Kabla ya kuvunja uhusiano nao usalama wa taifa walikuwa wakipewa mafunzo na Israel na kwa kweli ilikuwa ni kikosi kizuri kwani nimetoka familia hizo, pili majengo ni kweli yapo, mojawapo ni iliyokuwa ubalozi wa USA kabla yakupigwa maboma na ndiyo kilichowaponya wote waliokuwa ndani ya jengo waliouwawa ni wale waliokuwa getini na nje tu. Jengo lilikuwa imara sana. Kimwli kama alivyosema Ndg Sungura lile ndio shina sie matawi lakini mzabibu huu umependwa na Yesu na unashikiliwa na mizizi yake, ni wajibu wetu kujibidiisha ili matawi yetu yakue na kustawi na kuzaa matunda sio tu kukaa tukibweteka kwamba tuna shina takatifu. Tukumbuke Yesu alisema tawi lisilo zaa atalikataa jee sisi tunazaa? Au tunajifurahisha kwa kutumia mamilioni kwenda kunyonya ktk shina kitu ambacho hatukuagizwa. Tumeungwa kiroho hivyo tunawaombea, tunawabariki na tukiweza kama ilivyo kwingine tunapaswa kupeleka Injili (kuzaa matunda)
  Nilichokosoa kwa mbunge huyu ni kule kutumia kifungu hiki kwa mambo ya mwilini, tufaidike kimwili sio vibaya kwani ni bora hawa ndugu zetu kuliko Iran na wengineo.
  Swali langu mie ni jee huko bungeni hawaoni umuhimu wa kutetea hoja ambazo zingelisaidia kanisa Tanzania hata kimwli tu? Kuna mambo mengi ambayo kimsingi serikali inakiuka haki za wanyonge, inapuuzia rushwa, inajipa posho na malipo makubwa ukilinganisha na hali ya maisha ya mtanzania, inapuuzia watu wanaponyimwa uhuru wa kuabudu baadhi ya sehemu, wanapofungwa kwa kuhubiri injili ila wanaokashifu Biblia hawafanywi kitu, wanapochomewa makanisa na kunyimwa vibali kujenga makanisa, ndugu zetu waliopelekwa kule na Mungu haya hawayaoni????????????
  Tunahitaji akina Modekai wawaamshe hawa wakina Esta wajue walipelekwa pale kwa kusudi maalumu na wasipotimiza wajibu wao Mungu atatuinulia wokovu kupitia wengine na wao wataangamia…
  Ndio maana nilitoa wito tuombee taifa kwani kama kanisa hapa Tanzania hatuna kibali wala mamlaka, naomba tutengeze hapa nyumbani kwanza, tuzae matunda kwanza, tuhubiri injili tukianzia na Yerusalem yetu hapa kama alivyoagiza Yesu ktk matendo tusije tukakatwa na kutupwa motoni. Wapendwa tusimame ktk zamu zetu kabla hatujaanza kujiburudisha.

 12. Ndugu Sungura,
  Umemalizia vizuri sana comment yako kwamba “Mtu aliyebarikiwa/fanikiwa usimpinge, jiunge naye”. Sasa nina maswali naomba unisaidie;

  1. Bila shaka umemaanisha kwamba ukijiunga naye utafanikiwa pia kama yeye alivyofanikiwa, Je, ukimpinga mtu huyo nini kitakupata?

  2. Kwa nini Israeli imefanikiwa katika kilimo wakati nchi yao asilimia zaidi ya 70 ni jangwa? Na kwa nini nchi zingine wanazopakana nazo ambazo ni jangwa pia hazijafanikiwa kama Israeli?

  3. Je, jibu la ujumla la maswali mawili hpo juu ni kwamba Mungu kawabariki wao milele kama ulivyosema kwenye post yako na wale ambao hawajafanikiwa Mungu kawalaani milele?

  Natumaini utatufafanulia kwa undani kuhusu maswali hayo matatu.
  Baraka nyingi kwako.

 13. Fred nadhani comment yako imelenga moja kwa moja nilichosema kwenye comment yangu. Kuna sehemu mimi na wewe tuko na mawazo sawa.

  Ninapoongea kuhusu kanisa naelewa vizuri sana naongelea kitu gani, naelewa kanisa ni nini na Israel ni nini.
  Mimi siko kwenye mambo ya kwenda hija Israel kana kwamba ni suala la lazima, lakini uhusiano wa kanisa na Israel upo kwa maana ya kwamba Israel ndio mzabibu wa asili na kanisa( hasa sisi wa mataif) ni mzabibu wa kupandikizwa. Kwa maana ya kwamba Israel walipomkataa mwokozi wokovu uligeukia kwa mataifa ambao ni sisi. Wakristo kokote duniani hatuwezi kuikana Israel hata siku moja,huko ndiko historia ya kanisa na wokovu wetu ulikoanzia.

  Hata hivyo sihitaji kwenda kuhiji Israel ndipo mambo fulani ya Mungu niyapate, sihitaji kuiombea Israel ili niwe na amani nchini kwangu,hatuhitaji kuwa na ubalozi wa Tanzania Israel ili Tanzania iondokane na umasikini.Ila kama nchi tunapaswa kuwa na mipango mizuri pamaoja na vpaumbele sahihi ndipo tutafanikiwa.

  “In fact” hata tukiombaje, mambo mabaya au mazuri ambayo Mungu ametaka yatokee Israel lazima yatatokea. Hata tukiombea amani ya Israel lazima mgogoro kati yake na Palestina utaendelea. “There is nothing we can change about Israel no matter how much we pray”.

  Umuhimu pekee wa kuwa na uhusiano mzuri wa kibalozi na Israel ni kwamba hao jamaa wako mbele sana katika mambo yote ya kimaendeleo, iwe teknolojia, kilimo,sayansi, n.k maana Mungu kawabariki milele. Tukiwa nao karibu watatusaidia sana katika hayo.
  Mtu aliyebarikiwa/fanikiwa usimpinge, jiunge nae.

 14. Na pia nasikia hata Tanzania, projects nyingi walizokuwa wanatutengenezea hapa kama pale udsm, kuna majengo nasikia waliyaacha bila kuyamalizia….walivyofukuzwa na utawala wa awamu ya kwanza ….mpaka leo majengo yale hayakumaliziwa vizuri….na nasikia ni moja ya majengo ambayo hayajachakaa sana toka kipindi kile…ndio kusema wanautaalam mkubwa katika mambo…(hii habari nimesikia tu sijui ni kwa kiasi gani ni sahihi na ni majengo gani pale yalijengwa na wao….mtu aliyeniambia nilikosa muda wa kumwambia anionyeshe kabisa hayo majengo)

 15. Naomba kujua lile andiko la biblia linalosema UTAKUWA KICHWA NA SIO MKIA linawahusu wayahudi tu au hata mataifa walioamini( au kwa mataifa ni kuwa kichwa zaidi katika Mambo ya kiroho). Kwa sababu nimeona kwa kupitia literature mbalimbali zinaonyesha wazi wayahudi ni watu waliofanikiwa/wanaofanikiwa zaidi katika mambo yao regardless wanaamini Mungu au hawaamini. Na pia hata watu wasioamini Mungu huko Europe na USA wanakiri kuwa ukifanya business na wayahudi business yako inakuwa successful au hata katika bank/financial institution kama wewe ni owner ukiajiri wayahudi inaenda vizuri. Pia hata USA Professors wengi kwenye Ivy League University in jewish ingawa jews kwa ujumla ni wachache. Naomba msaada kwa anayeelewa kuhusu hili.

  http://www.soc.washington.edu/users/burstein/Burstein_Jewish_Success_SP07.pdf

  http://en.wikipedia.org/wiki/List_of_Jewish_Nobel_laureates

 16. Wapendwa,

  Nadhani swala Tanzania kuwa na uhusiano na Israel tumewahi kulijadili kwa kirefu….sikumbuki katika mada gani dada Mary anaweza kutukumbusha….

 17. Kweli ni muhimu nasisi watanzania kuwa na ubalozi kama jengo na wawakilishi yaani mabalozi wanao ishi nchini kwetu na wala si wanaoishi nchi nyingine.

  Hivyo basi sisi kama watu wa Mungu alie hai tuzidi kuliombea hili.

 18. Mbunge alilisoma kutoka Biblia ya Kiswahili (Swahili Union Version)
  tuliyoizoea. Mimi nimenukuu toka Kiingereza cha Mfalme Yakobo (King James
  Version) kwa kuwa ndiyo niliyokuwa nayo karibu. Hiyo ni taarifa!

  Joel

 19. Shalom
  mie nilifikiri kauliza makanisa kuchomwa moto na kunyimwa vibali vya kuabudu baadhi ya maeneo kama Zanzibar, Bagamoyo nk. Hivi hili hawalioni wabunge wetu? Bajeti ya mambo ya ndani imepita kwa amani tu? Kweli hatuna wawakilishi sisi.
  Mungu atusaidie sana.

 20. Hayo uliyoandika kweli Sungura,
  Huyu Mbunge ametumia maandiko haya siyo wakati wake
  Mimi kwa sehemu ufahamu wangu ninavyoelewa maandiko,hiyo Zak14:17,ni maandiko ya unabii.yanazungumzia wakati wa miaka 1000 ya utawala wa Kristo wakati shetani atakuwa amefungwa,.watu wote ambao hawakutwaliwa siku ile ya unyakuo na pia walibaki wakati wa dhiki kuu(kuwa hai) itawapasa kila mwaka kwenda Jerusalem kwenye sikukuu ya vibanda wasipokwenda ndio mvua haitanyesha kwa hao mataifa, Rudi ule mstari wa 16

  Neema ya Bwana izidiyo na hiwe juu ya kanisa

  Mjoli Haule

 21. Mungu ambariki sana huyu Mh Mbunge kwa kuliona hilo na kulitambua na kuliongelea bungeni.Tunahitaji sana ushirikiano na taifa la Israel ili kupata kibali na baraka kwa Mungu wetu ,vinginevyo Tanzania itaendelea kuwa masikini pamoja na rasilima zote tulizo nazo

 22. Suala la Tanzania kuwa au kutokuwa na ubalozi Israel halina uhusiano wowote na maandiko. Wala kanisa siyo lazima liwe na uhusiano na Israel. Huu ni mtego wa ibilisi, tuache ushabiki bila undani wa mavunuo. Mtu anaposema kanisa anajua maana yake au ndo mazoea? Swali kuna nini Israel cha kuhusiana kanisa ili kulazimisha uhusiano? Ukungu utakapotutoka tutashangaa na kushtushwa jinsi tulivyobebeshwa uongo kwa miaka mingi kuhusu Israel. Ndugu tujitakase na kumfuata mwanakondoo wa Mungu kokote aendako.

 23. Kama ilivyo nia ya shetani kupotosha ukweli naibu waziri naye anachanganya dini na Mungu, serikali kutokuwa na dini haina maana haina Mungu, hata Mungu hana dini, hata biblia haina dini, tunajua ama hatujui Israel inatuhusu. Kusema nchi haiongozwi kiroho nako anakosea, kila kinachoonekana kimetokana na roho ama ya giza au nuru.

 24. Ni vizuri kuwa na ubalozi wetu Israel kwa faida mbalimbali za ki-diplomasia na kimaendeleo. Lakini haihusiani na hili andiko la (Zechariah 14:17). Hatuhitaji kwenda kuabudu Yerusalem au kuwa na ubalozi wetu huko ili mvua inyeshe kwetu, au ili kuwa na baraka za Mungu. Uhusiano wetu na Israel unatakiwa kuwa wa ki- kanisa zaidi kuliko kisiasa. Hata kama wanasiasa hawataki, kanisa la Tanzania lazima liwe na msimamo wake wa kiuhusiano na Israel. Kwa sababu leo Mungu haangalii sana viongozi wa kisiasa wamefanya nini ili nae afanye nini, bali analiangalia kanisa limefanya nini ili afanye nini.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s