Unaweza kuombea juu kifo chako?

Bwana Yesu asifiwe!

Hivi mtu ambaye ameokoka anaweza kufanya maombi kwa Mungu ili siku yake ikifika ya kuondoka hapa duniani asiondoke kwa kifo cha ghafla? sababu Neno linaruhusu kuomba lolote kwa jina lake.

Grace

Advertisements
This entry was posted in Uncategorized. Bookmark the permalink.

11 thoughts on “Unaweza kuombea juu kifo chako?

 1. Kuna fulsa nzuri sana ambayo tumepewa wanadamu juu ya kufahamu siku ya kufa kwetu ikiwa tutajenga mahusiano mema na Mwenyezi-Mungu.
  Ki msingi, ikiwa tunaenenda vyema mbele za Mungu tutarejea kwake baada ya kufa.
  Tofauti kubwa kati ya kuzaliwa na kifo ni kuwa unaweza kujifahamu kwa akili timamu wakati wa kufa lakini si rahisi kujitambua wakati wa kuzaliwa.
  Kama ilivyo hapa duniani ukitaka kuonana na mtu mkubwa lazima upate ahadi ya siku gani ufike kuonana naye.Hivyo ikiwa tunarudi kwa Mungu kama watoto wake wapendwa kuna uwezekano mkubwa kabisa wa kupata “appointment” ya lini tutapokelewa naye kulingana na jinsi tulivyoenenda wakati wa uhai na kusiliza sauti ya Roho Mtakatifu.
  Mungu ajichanganyi; amesema hatafanya kitu bila kutufahamisha.Tatizo ni JINSI tunavyompa nafasi mjumbe wake i.e Roho Mt. ili kusikia sauti yake rohoni mwetu .
  Kwa vile hatiingii kwa dhati katika ‘vyumba vyetu vya rohoni’ kusikia sauti ya Roho Mt. mara nyingi sauti za makelele ya nje (mambo ya kimwili) hutufanya hata tusijue siku ya kufa. (2 Nya.32:24-25)
  Hivyo unaweza kuomba kifo kibatilishwe (2 Nya.32:26, 2Fal.20:1-3),kuomba kifo chema na hata kujua ikiwa muda wako unakaribia ili kutengeneza sawasawa mambo yako.
  Sospeter

 2. Ni kweli kabisa kwa mtu aliyeokoka anaweza kukizuia kifo kwa kumuomba Bwana naye anazuia. mfano mzuri ni mfalme Hezekia alipoletewa habari za kifo na nabii aliyetumwa na Bwana, naye akamlilia Mungu akamuongezea miaka 15, habari hii inapatikana katika kitabu cha 2 WAFALME 20: 1 – 10. Hivyo Mungu wetu ni mwaminifu na hakuna analoshindwa all he needs is faith inside u

 3. Nashukuru wapendwa kwa michango yenu,nimejifunza mazuri kutokana na mawazo yenu, tuendelee kujifunza pamoja.Mbarikiwe

 4. si hivyo tu bali kumuomba Mungu aharishe siku yako ya kufa tu ili utimize vision yako hapa duniani kabla ya maisha yajayo.

 5. Tuzidi kumtafuta Mungu kwani Mungu ni BaBa awezi kufanya jambo bila kuwataharifu watoto wake,tujitaidi kuwa karibu na Mungu kwani Mungu ni mwaminifu kwa walio waaminifu. amen

 6. Sioni haja ya kuombeya kifo cangu kwa sababe ninajuwa mimi kama mtoto wa Mungu, mambo yote kuhusu maisha yangu Bwana mwenyewe hushugulika

 7. Mimi nadhani ni sana kuomba ufahamu siku ya kifo chako , kwa sababu hivi kama Mungu asingemwambia Musa kwamba siku zake za kuishi zimekaribia asingeliweza kufanya maandalizi ya kumkabidhi Joshua kazi ya kuwavusha wana wa Israel mto Yordan hadi nchi ya ahadi.
  Kwa hiyo ni vema tuombe Mungu atuonyeshe siku yetu ya kufa ili tuweze kufanya maandalizi ya kiroho na kimwili.

 8. Ni kweli kabisa mtu aliyeokoka anaweza kuomba kwa Mungu ili siku ya kuondoka ikifika “asiondoke ghafla”.

  Ni siri kubwa lakini Mungu amesema hatafanya jambo pasipo kuwafunulia watumishi wake – Shida ni mahusiano ya mtu na Mungu.
  Pili ni kuwa watu wengi wamekuwa si tu wanaondoka / kufa kwa ghafla ila “wanauwawa / wanakufa kabla ya wakati / ghafla”. Kwanini nasema hivi?
  Maandiko yananena wazi katika Isaiah 65:20-25, “There shall be no more thence an infant of days, nor an old man that hath not filled his days: for the child shall die an hundred years old; but the sinner being an hundred years old shall be accursed.
  21 And they shall build houses, and inhabit them; and they shall plant vineyards, and eat the fruit of them.
  22 They shall not build, and another inhabit; they shall not plant, and another eat: for as the days of a tree are the days of my people, and mine elect shall long enjoy the work of their hands.”-KJV
  Hakuna mtoto atakayekufa chini ya miaka 100…mzee asiyetimiza siku zake…NA UMRI WA WATU WA MUNGU UTAKUWA KAMA VILE MITI IISHIVYO…
  Sasa basi hivi leo nani anayekufa akiwa na miaka walau 100? Je ni wangapi hufa wakiwa na taarifa? Jibu ni wachache sana, na hili linategemea mahusiano ya mtu na Mungu. Kumbuka baadhi ya babu zetu, bibi zetu, wazazi wetu waliokuwa wazee na ikifika kipindi chao kuondoka huwaita watoto waagane kabla.

  Mungu atujalie mahusiano mema naye ili tujue yatupasayo na wakati wa kujiliwa kwetu.

 9. Shaloom dada Grace, Baada ya kusoma swali lako, mambo haya yafuatayo yamekuja moyoni mwangu. Zab 116.15 INA THAMANI MACHONI PA BWANA MAUTI YA WACHA MUNGU WAKE. (anajali vifo vya watakatifu). Zab 90.12. BASI UTUJULISHE KUZIHESABU SIKU ZETU. TUJIPATIE MOYO WA HEKIMA. Zab 39.4. BWANA UNIJULISHE MWISHO WANGU, NA KIASI CHA SIKU ZANGU NI KIASI GANI, NIJUE JINSI NILIVYO DHAIFU. Ndiyo mmoja akasema AMEONYESHWA. 2 pt 1.14. NIKIJUA KWAMBA KULE KUWEKEA MBALI MASKANI YANGU KWAJA UPESI KAMA BWANA WETU YESU KRISTO ALIVYONIONYESHA. Kila aliyemcha Mungu hafi kama kuku, anajulishwa, maandalizi ya kumpokea huwa yanafanyika, na anataarifiwa akiwa sawa na Mungu. Ubarikiwe.

 10. Haleluya, kama ulivyosema tumeruhusiwa kumwomba Mungu wetu jambo lolote maadam si uovu. Bila shaka ni jambo jema ikifika muda ujue unakaribia kufa na ujiandae kufa vizuri. Ukisoma nyaraka za Paulo utaona anamwambia Timotheo kuwa “tazama wakati wa kumiminwa kwangu umekaribia” ndipo akaanza kumuusia namna alivyovipiga vita vya imani vizuri, akailinda imani na mwendo akaumaliza. Mimi naamini unaweza kumwomba Mungu hivyo.

  Ila usiombe Mungu akuchukue leo wakati hujafanya kazi ya Mungu! we endelea kumtumikia Mungu huku ukiombea mwisho wako. Unakumbuka Eliya alipokimbizwa na Yezebel? akajificha mahali pa siri na akamwambia Mungu amuue pale lakini tunaona kwa kuwa haukua mpango wa Mungu Eliya afe muda ule Mungu akamtuma malaika ampelekee chakula na kumwambia amka ule maana una mwendo mrefu mbele yako.

  OMBEA MWISHO WAKO USIOMBE UCHUKULIWE SASA

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s