Inakuhusu, uwe kwenye ndoa au la, soma

Inahuzunisha lakini kuna fundisho kuu kwetu sote.

“Nilipofika nyumbani usiku ule, mke wangu aliponitayarishia chakula, nilimshika mkono na kumwambia, Kuna kitu nataka nikwambie. Mke wangu alikaa chini na kula chakula kimya akiwa tayari kunisikiliza. Tena nikagundua macho yake yalionyesha anaumizwa. Nilishindwa hata namna ya kuanza kufumbua kinywa changu. Lakini ilibidi nimwambie ili ajue nilikuwa nikifikiri nini juu yake.

Nataka kukupa talaka. Nilianza kusema kwa utulivu. Alionekana kutokereka na maneno yangu badala yake aliniuliza kwa sauti ya upole ‘kwa nini?’ Sikumjibu swali lake. Kutojibu kulimfanya akasirike. Akatupa kijiko na akanikaripia, ‘wewe si mwanamume!’ Usiku ule, hakukuwa na maongezi kati yetu. Alikuwa akilia kwa kwikwi. Nilifahamu kwamba alitaka kujua ni nini kimetokea kwenye ndoa yetu. Lakini kwa hakika nisingeweza kumpa jibu wala sababu ya kuridhisha; alionekana si mali kitu kwangu penzi langu lilihamia kwa Jane. Sikumpenda tena mke wangu mawazo yote yalikuwa kwa Jane. Kwa kweli nilimdharau mke wangu!

Huku moyo wangu ukijua wazi kwamba nafanya kosa, niliandika talaka ambayo ilionyesha kwamba yeye (mke wangu) angepata nyumba yetu, gari na atakuwa na hisa 30% ya kampuni yetu. Aliangalia talaka ile na kuichana vipande vipande.

Mke ambaye tumeishi nami kwa miaka 10 alionekana mgeni machoni mwangu. Nilimuonea huruma kwa muda, rasilimali na nguvu alizopoteza lakini sikuweza kurudi nyuma kwa sababu Jane aliuteka moyo wangu kisawasawa. Hatimaye mke wangu alilia kwa sauti mbele yangu, jambo ambalo kwa hakika nilitarajia. Kwangu mimi kilio chake kilinipa nafuu.

Wazo la kuachana na mke wangu limenisumbua kwa majuma kadhaa na sasa limeendelea kuimarika na kuwa jambo la hakika zaidi.

Siku iliyofuata nilikuja nyumbani kwa kuchelewa sana nikakuta mke wangu akiandika jambo mezani. Sikutamani hata kula chakula alichonipikia nilikwenda moja kwa moja chumbani na usingizi ulinichukua mara moja kwa sababu nilikuwa nimechoka baada ya kula raha za kufa mtu na Jane.

Usiku nilishtuka usingizini mke wangu alikuwa bado akiandika. Sikujali kabisa nikajifunika vyema shuka na kulala tena. Asubuhi yake alinikabidhi masharti ya talaka yake: hakutaka kitu chochote kutoka kwangu lakini alihitaji apate angalau mwezi mmoja wa kujiandaa kabla hajaachika. Akaomba kwamba katika kipindi hicho cha mwezi mmoja sote mimi na yeye tujitahidi kuishi maisha ya upendo au kawaida kwa kadiri itakavyowezekana. Sababu yake ilikuwa ndogo lakini muhimu: mwanetu wa kiume alikuwa akikaribia kufanya mtihani katika mwezi uliofuata kwa hiyo hakupenda mtoto aathirike kisaikolojia kwa sababu ya kuachana kwetu. Hili halikuwa tatizo kwangu, nilikubali mpango wake. Lakini alikuwa na sharti la ziada, aliniomba nikumbuke jinsi nilivyombeba siku za fungate yetu hasa siku ya harusi yetu. Akaniomba na kunisihi kwamba katika kipindi hicho cha mwezi mmoja niwe nambeba kutoka kitandani kwetu mpaka mlango wa kutokea kila asubuhi. Nilidhani anakaribia kuwa kichaa. Ili kufanya siku zetu za mwisho zisiwe na migogoro nilikubaliana na masharti yake ya ajabu.

Nilimsimulia Jane kuhusu masharti ya kuachana na mke wangu. Jane alicheka sana, aliona ni ujinga. ‘Hata akitumia ujanja wa namna gani talaka ni lazima’, alisema Jane tena kwa dharau. Mimi na mke wangu hatukuwahi kugusana tangu nilipomweleza dhamira ya kumtaliki. Kwa hiyo nilipombeba kwa mara ya kwanza sote tulinuniana. Mwanetu alifurahi sana na kupiga makofi nyuma yetu, ‘aah baba kambeba mama mikononi mwake’. Maneno yake yalinichoma moyoni moja kwa moja. Kutoka chumbani kwetu hadi sebuleni, halafu tena mpaka mlangoni, ni zaidi ya mita kumi nimembeba mke wangu. Alifumba macho na kusema kwa sauti laini na ya upole; usimwambie mwanetu juu ya talaka. Nilikubali kwa kichwa, ingawa nilijisikia vibaya. Nilimuweka chini nje ya nyumba.

Alienda kituoni kusubiri basi la kazini kwake nami nikaendesha gari kwenda ofisini kwangu. Siku ya pili, zoezi lilikuwa rahisi kwetu sote. Aliegemea kifuani pangu. Nilisikia harufu nzuri ya uturi aliofukiza kwenye blauzi yake. Nikagundua kwamba sijamuangalia kwa makini mke wangu kwa kipindi kirefu sana. Nikagundua hakuwa binti tena. Kulikuwa na mikunjo usoni na nywele zake zilianza kuwa nyeupe! Ndoa yetu imekula urembo wake. Kwa dakika moja nikafikiri kwa nini namfanyia hivi.

Siku ya nne nilipombeba hisia za mapenzi kati yetu zilirejea. Huyu ni mwanamke aliyejitoa kuishi nami na tumeishi kwa miaka kumi sasa. Siku ya tano na ya sita ilikuwa wazi kwamba mapenzi yetu yalikuwa yakimea upya. Sikumwambia Jane kuhusu jambo hili. Kadiri mwezi ulivyokaribia kwisha niliona raha kumbeba mke wangu na zoezi likawa rahisi zaidi. Pengine kufanya kazi hii kila siku kuliniimarisha zaidi.

Alikuwa akichagua nini cha kuvaa asubuhi. Alichagua mavazi kadhaa hakupata linalomfaa. Kisha akaguna, ‘nguo zangu zote zimekuwa kubwa’. Nikagundua kwamba mke wangu amepungua sana, nadhani ndiyo maana niliweza kumbeba kirahisi. Ghafla jambo likanichoma… mke wangu ana uchungu na maumivu makuu moyoni mwake. Bila kujitambua nikamgusa kichwa chake. Mara mtoto wetu akatokeza na kusema ‘baba ni wakati wa kumbeba mama muende kazini’. Kwake kumuona baba akimbeba mama likawa ni jambo la furaha sana. Mke wangu alimuonyesha ishara mwanetu asogee karibu na akamkumbatia kwa upendo mkuu. Niligeuza uso wangu nisije nikabadili mawazo katika dakika ya mwisho. Kisha nikambeba mikononi mwangu kutoka chumbani, sebuleni halafu mpaka mlangoni. Mkono wake laini ulikuwa umeizunguka shingo yangu kwa upendo. Nilimkumbatia mwili wake; ilikuwa ni mithili ya siku ya ndoa yetu. Lakini wepesi wake ulinitia mashaka.

Siku ya mwisho nilipombeba nilipata shida hata kupiga hatua moja. Mtoto wetu alishakwenda shuleni. Nilimshika kwa karibu na kumwambia sikubaini kwamba maisha yetu yalikosa upendo. Nikaenda zangu ofisini…. Nikashuka garini hata bila kufunga mlango. Maana nilihisi nikichelewa tu ninaweza kubadili nilichoamua…. nikapand ngazi. Jane alifungua mlango nikamwambia, ‘Samahani, Jane, sihitaji tena kumtaliki mke wangu’. Akaniangalia kwa kustaajabu, halafu akagusa kichwa changu. Akaniuliza ‘Unaumwa?’ Nikaondoa mkono wake kichwani kwangu. ‘Samahani, Jane, nimesema sitaki kumtaliki mke wangu. Nadhani ndoa yangu haikuwa na furaha kwa sababu sikuthamini undani wa maisha yetu, mimi na mke wangu, si kwamba hatupendani. Nimetambua hilo tangu nilipombeba siku ya ndoa yetu nilitakiwa kumbeba siku zote za maisha yetu, nampenda mke wangu sitamuacha mpaka kifo kitakapotutenganisha.’

Ikawa kama Jane alizinduka usingizini. Akanizaba kibao cha nguvu, akajiegemeza mlangoni na kuanza kulia. Nikashuka ngazi na kuondoka zangu. Nikaingia kwenye duka la maua nikaagiza maua mengi mazuri kwa ajili ya mke wangu. Muuzaji akaniuliza aandike nini kwenye kadi. Nikatabasamu na kuandika “Nitakubeba kila asubuhi mke wangu mpaka kifo kitakapotutenganisha”. Jioni ile nilifika nyumbani na maua mikononi mwangu, tabasamu kubwa usoni nikakimbia mpaka chumbani, nikapokelewa na maiti ya mke wangu kitandani.

Kumbe mke wangu alikuwa akisumbuliwa na saratani kwa miezi kadhaa nami nilishindwa kubaini kwa sababu nilihamishia akili yangu kwa Jane. Alijua kwamba angekufa karibuni na alitaka asiniingize katika chuki na mwanetu kama ningelazimisha talaka mapema.

Angalau machoni mwa mwanangu naonekana ni mume mwema….

Jamani vitu vidogo vidogo vizuri ni vya msingi sana katika mahusiano yetu… Siyo majumba au magari au fedha zilizoko kwenye benki. Hivi vitakupa tu mazingira ya kufurahi lakini vyenyewe siyo furaha. Kwa hiyo jitahidi kuwa na muda mzuri na mazingira rafiki ya kuwa na mwenzi wako, kuwa rafiki wa mwenzi wako. Fanya vitu mlivyofanya wakati wa uchumba na wa ndoa yenue ambavyo vitawaweka karibu siku zote. Muwe na ndoa yenye furaha. Mara nyingi watu hushindwa katika ndoa kwa kutotambua ni kwa kiasi gani walikuwa karibu wakati wa kujenga uhusiano wao

Mungu awabariki nyote mliosoma na kujifunza hapa.

–Ntwa Ntumwalisa

Advertisements

21 thoughts on “Inakuhusu, uwe kwenye ndoa au la, soma

 1. duh! simulizi hii inafundisha sana, yaani imeniingia sana moyoni na inasikitisha sana. hakika Mungu atusaidie sana katika ndoa zetu. maana kuna magumu mengi sana, pasipo yeye hatuwezi. Mungu akubariki sana.

 2. Nashukuru fundisho nimelipata, kama habari hii ni kweli wengi watabadilika mie nikiwa mmoja wao kwani tunajifunza kupitia makosa waliofanya wengine ili sisi tusiingie katika makosa “ukweli unaishi”, na kama habari hii ni ya kufikirika hawatabadilika, itakuwa kama stori tu ya magazeti ya udaku. Hongera mwandishi wa habari hii kwani kilichokusudiwa kwenye ujumbee huu kimetufikkia kikamilifu.Be blessed.

 3. Nashindwa hata nisemaje kwa uzito wa huu ujumbe, tunahitaji neema ya Mungu katika kutiwezesha kuwa na ujasiri mkuu na uvumilivu mwingi katika kuchukua maamuzi ili kutengeneza miujiza katika maisha yetu ya mahusiano. Mungu akubariki kwa ujumbe huu mzito uliobeba huzuni nyingi na furaha kubwa.

 4. Kwa kweli Mungu ana njia zake alimuonyesha huyu mama na amieachia familia yake upendo mkubwa mbele zake na mbele za Mungu. Maana yake hakuwa mbinafsi yeye alifanya vile inapendeza mbele za Mungu na mwanae na alijua hata akimueleza mumewe ndio kisha kuwa sikio la kufa halisikii dawa ila pia nampenda sana huyu baba kukubali kumbeba mke wake maana wengine wangekataa katu katu ila uponyaji wake umeanzia pale alipokubali kuwa mtii kwa mke wake wa ujana nadhani ameumia sana kwakuwa alikuwa tayari kukaa na mkewe ila nafasi haikuwapo tena Mshukuru sana Mungu mkeo kakuepusha na moto wa milele

 5. ………..”nitakubeba kila siku asubuhi mpaka kifo kitakapotutenganisha”……….nilifika na maua mikononi mwangu,tabasamu kubwa usoni nikakimbia mpaka chumbani nikapokelewa na maiti ya mke wangu kitandani……..”mmh…..HOW SAD IS THIS

 6. Sharom….
  Hiki kisa kimeniudhunisha sana… Huu ni ukweli usiopingika kuwa mara nyingi mwanamke huwa mvumilivu saana ktk ndoa na uvumilivu huu unapelekea matatizo ya kiafya yanayosababishwa na mkanganyiko wa akili….Cha kusikitisha sababu kubwa ya hili tatizo ni huyohuyo mwanamke..kwa mf…
  1. Anaweza akawa kwenye nafasi ya kimada au
  2. ktk nafasi ya mama/mke…
  . M’ke akiwa ktk nafasi ya kimada anajisahau kabisa km hana haki juu ya m’me aliyenae, atafanya jitihada zote ili ammiliki wakati anajua kuwa huyo m’me ana familia yake ( kesha milikiwa.) Na wakati mwingine anaweza kuwa yeye ndio aliyemtega huyo m’me mpaka akanasa. Hii inatokana na makuzi/malezi, uelewa mdogo, utegemezi na pia kutojiamini kwa huyu m’ke. Vituko atakavyovifanya vitamsababishia m’ke muolewaji aingie kwenye somo hilo la uvumilivu wenye machungu yasiyomithilika…..Hivyo hapa tunaona chanzo ni m’ke………….
  M’ke ktk nafasi ya mke…. naye pia anaweza akawa tatizo ebu tusome mith 14;1,na mith 17;16….hapa tunaona jinsi upumbavu unavyoweza kumuingiza m’ke kwenye somo la uvumilivu wenye machungu,
  M’ke wa namna hii akifanya haya yafuatayo anaweza akapata ufahamu utakaoweza kumsaidia..
  1. Akikubali kumfanya mungu wa kwanza juu ya familia yake
  2. Akikubali kujifunza… na kusoma neno la mungu…. kwa mf…mith 31;10-31
  3. Akiwa mtu wa maombi……….n.k.

  Nataka kusema hivi wanawake wapendane na ikibidi washirikiane ,,, Hakuna kiwezacho kuleta mabadiliko isipokuwa kwa kujitoa kwa wanawake wenyewe…….

  Na kwa wanaume wajue kuwa M’ke ni chombo cha thamani sana ambacho kiliumbwa kwa makusudi ya kiungu ili afanyike km msaada kwao. Wewe umeoa m’ke uliyempenda, anakulea vyema na anatekeleza majukumu yote aliyopewa na mungu juu yako…. tatizo nini sasa… mbona unamfanya akuvumilie, unafikiri angejua mapema km atahitajika kukuvumilia angekubali kuolewa nawe? Sikia m’me uvumilivu ni wa pande zote mbili,, Neno la Mungu linasema apataye mke amepata kibali mbele za mungu,yaani inamaanisha kibali chako mbele za mungu kinatokana na huyo m’ke uliyemuoa, ebu basi mfanye achekee/afurahi ili familia iwe na baraka na afya tele… Ebu tusome mith 29;3, mith 31;3. Asanteni..
  .

 7. That is amazing story. Tunamuhitaji Roho Mtakatifu Katika maisha yetu ya kila siku ili atuongoze maana kwa akili zetu hatuwezi.

 8. Upendo ni mbegu isiyo oza, hata ikipandwa kwenye jiwe ilimradi tu mwenye kupenda ajuwe jinsi gani ya kuyihwekea maji pia na kupalilia kazi yake Mungu ni kukuza mbegu hiyo.

  Jamani kupenda ni maono na mama huu amepewa siri ya ajabu ili ayatengeneze mazingira kabla ya kuachana na mpenzi wake. Jina la Bwana libarikiwe.

 9. inasemwa hata wakati wa kufunga ndoa “kuvumiliana” that’s the issue. awe mke , ndugu au rafiki wa kweli, bila kuvumiliana hamtafika mbali. lkn ndo dunia, nyoyo hazifanani!!!!

 10. Asante sana kwa fundisho hilo la ndoa. Watu wengi wanaziona ndoa kama ndoano. Si wanawake wala wanaume, kwani shetani anazifuatilia ndoa nyingi ili apate kuziangusha. Wapo wanaume wengi ambao wameoa kwa sababu ya tamaa za mwili tu, wengine wameoa ili wafanyiwe kazi mashambani na nyumbani, wengine wameoa kwa ajili ya watoto. Wamewafanya wanawake kuwa manamba katika ndoa na si wasaidizi tena kama Biblia inavyosema. Mfano katika familia ya ndugu zetu hawa hakukuwa na ndoa bali kuishi pamoja tu, kwani matakwa ya ndoa hayakutimizwa. Ni muhimu kwa wanandoa kukaa katika upendo na uaminifu mkubwa na Mungu atawasaidia. Na kwa yule ambaye hajaoa au kuolewa, asiingie kwenye ndoa kwa ajili ya tamaa ya mwili au mali, kwa kufanya hivyo ndoa yenu haiwezi kudumu. AMEN

 11. Shalom wapendwa
  iwe ni hadithi au ni tukio la kweli nimejifunza kitu kimoja.
  1. Upendo wa ndoa ulipoa kupita kiasi, wakati mmoja akiumwa mwingine wala hajui,
  2. ndoa haithaminiwi na baadhi ya wenza, akimuona mwingine nje yuko tayari kuvunja ndoa
  3. mama alijitoa kwa ajili ya familia yake, aliteseka kimya akihofia akitaja ugonjwa wake kwa mumewe angevunja ndoa na hivyo kujipatia laana na kumwachia mtoto uchungu, aliteseka kimya ili tu familia yake isibebe laana ya kuachana!
  4. ukiomba na kubembeleza yawezekana upendo ukarudi ndani ya ndoa iliyokuwa tayari kuvunjika
  wapendwa tubadilike, tuwe walau na muda wa kuwasikiliza wenza la tutabakia na uchungu kama huyu ndugu aliyeishia kuja na maua kuomba samahani wakati mwenzie keshakufa. Majuto ni mjukuu isitutokee!
  Ubarikiwe kwa fundisho zuri, lakini kama imekutokea kweli mwombe Mungu msamaha na akuondolee uchungu, mwombe akupe mwenza mwema kama ulimpoteza, simama ktk wokovu maana shetani aliishakupata mwanzo anakuwinda.

 12. Napenda kutoa pole Kwa ndugu Yangu Ambaye amenipitia jaribu zito na lenye fundisho Kwangu, kiufupi nimeguswa sana na ushuhuda huu, kiasi cha kwamba mengi Nakumbuka nakuona ni ya msingi kwakila Mwenye mwili kujua upendo wa kwanza Kwa mahusiano yetu. Iwe ktk ndoa au Kwa habari ya wokovu au mahusiano ya kirafiki. Tunapokumbuka lengo au msingi uliokuwepo ktk mahusiano ndio Nguvu ya maana sana hata ktk kuhamua kwetu.
  Mimi nimeoa ni fundisho pia Kama ujaoa nifundisho kujua kwamba kile unachokwenda kuamua siku yakwanza ni cha muhimu sana kukilinda hata mwisho au siku za misukosuko. Tatizo ni kusahau. Mwanadamu amepewa kusahau. Na ni Neema ya ajabu Kwa mama aliyefariki yaani mke wa uyo jamaa, kufanya tendo la kukumbusha ili kumrejesha jamaa ktk kumbukumbu ya msingi wa ndoa Yao. Ufahamu huo niwaki Mungu kabisa aliotumia tofauti na kawaida ya watu wanavyofanya Leo, hii ni fundisho kwetu kuhamua mambo Kwa busara wakati wa mambo mazito yanapotokea. Kwani kutofanya ivyo ni ugomvi chuki nk. Vyaweza tokea nakuharibu kabisa mpango mzuri wa Mungu.
  Mwisho
  Mungu atusadie kujifunza na kuyaishi Yale mema tunayojifunza.
  Naomba Huyo kaka aludi ktk kusudi la Mungu Wala sio kuendelea kukaa chini nakulia, Kwani kufanya ivyo atachelewesha kusudi la Mungu. Na hasirudi tena Kwa Jane Kwani hatari nyingine ya tofauti ipo mbele Yake Kwa kasi ya ajabu. Sijuhi nini anawaza?

 13. Nashukuru sana kwa mafundisho safi ya ndoa. Ila wanawake zetu hawa Bwana hata uwafanyie nini huwa hawatambui upendo , atanuna bila sababu ya msingi, ukimwonyesha upendo kama hiyo ,njoo nikubebe mke wangu au twende tukaoge wote au njoo uninyweshe soda au Juice , njoo nikulishe pipi litakuangalia kwa jicho baya , lenyewe constration yake ni kitchen party , kikundi cha kina mama majirani ,kukimbilia misiba ya watu ambao hata hawajui , hebu niambie mtu ukienda kwa Jane kuna kosa hapo??????

 14. Tunamshukuru Mungu kwa fundisho hili kwani linagusa sana mioyo ya watu wengi,
  upendo katika ndoa na kumtanguliza Mungu kwa kila jambo, lazima ibilisi ataaibika
  hatopata nafasi kwani sikuhizi delila wapo wengi, mkiwa wote wawili mnahofu ya
  Mungu shetani na malaika zake hawatopata nafasi katika ndoa yenu, na neno la
  Mungu likae kwa wingi ndani ya mioyo yenu ili mpate kibali cha kuongozwa na Roho
  mtakatifu Amen mmebarikiwa.

 15. Mtumishi Ntwa,

  Kwanza tueleze hiyo hadithi umeitunga wewe, yamekupata wewe au umekopi na kupesti kutoka vitabu vya hadithi? Naomba jibu.

 16. Kwa hakika JINA LA BWANA LIBARIKIWE kwa fundisho hili. Kwa kweli ndoa zetu zinakwama kwa sababu ya vijimambo vidogovidogo. MUNGU akubariki, mtumishi Ntwa.

 17. Ndugu Ntwa Ntumwalisa, nimeshukuru kwa ujumbe huu. Sijajua kama ni HADITHI au ni Kitu halisi. Kama ni hadithi, nadhani inafundisho zito la kuwakumbusha wanadamu yale yawapasayo, ili Ndoa zao zipate kudumu. Lakini kama ni jambo halisi, lililotokea, hapo nasema POLE sana kwa hayo yaliyokusibu, na kwa kuwa MUNGU anakupenda, pia alimpenda mkeo mpendwa, alipotaka kumchukua alitengeneza mazingira ambayo amekuacha katika upendo wa kweli, moyo wake ukiwa safi, hapo nasema jina la Bwana litukuzwe. Asante.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s