Usiionee haya Injili ya Kristo, iende mbele

Huu ni wakati wa tofauti kabisa, huu sio ule wakati wa kumsubiria mtu mmoja tu ahubiri , wengine wakikaa na kumpigia makofi tu, Katika siku za mwisho, asema Bwana, nitamimina Roho wangu juu ya wote wenye mwili. Wana wenu na binti zetu watatabiri, vijana wenu wataona maono na wazee wenu wataota ndoto. Matendo 2:17 Huu ni wakati wa JESHI LA BWANA, watu hodari, wenye maarifa, Imara na watendaji zaidi si wa maneno matupu tu maana imeandikwa Kwa kuwa Ufalme wa Mungu si maneno matupu tu bali ni nguvu 1Wakorintho 4:20…Roho tuliyepewa si wa kujivunia wala kutambia watu bali ni wa kazi na tunakuwa washindi sababu ya Roho mtakatifu “‘Si kwa nguvu, wala si kwa uwezo, bali ni kwa Roho yangu,’ asema BWANA Mwenye Nguvu. Zekaria 4:6 huu ni wakati wa kila mtu awe mwana injili, kila mtu ASIIONEE HAYA injili, ni wakati wa kila mtu kuhubiri/kushare/kushuhudia/ kueleza/ kupasha habari…habari gani ? HABARI NJEMA! …

Ni kila mtu kutumia kila alicho nacho, kwa kila namna , na kila mbinu, kusema/kutenda/kuishi maisha yanayovuta wengine kwa Yesu… kwa kushirikiana, kwa kuhimizana….kwa sms, kwa Facebook, kwa mitandao, ana kwa ana, kwa Tshirts za maandishi, kwa ringtone, kwa sticker ya kwenye gari, kwa maandishi kwenye kikombe cha chai….Are you a winner? True Winner ni winner of souls….Kupunguza idadi ya watu wanaokwenda Jehanamu na iwe ni KIPAUMBELE cha kila mmoja…Kama kweli tunampenda Yesu basi tufanye kile ambacho Moyo wake wote upo hapo – “KUOKOA” roho…!!!!!++++!!!!!. Kama kweli unampenda Yesu utatafuta Pesa ya kupeleka Injili mbele, Utatumia uwezo na akili na ujuzi ulio nao kumwinua Yesu na kutetea Injili…Mimi siionei haya Injili ya Kristo kwa maana ni uweza wa Mungu uletao wokovu kwa kila aaminiye, kwanza kwa Myahudi na kwa Myunani pia Warumi 1:16 – msemo huu uwe msemo wa kila mmoja!

–“B”family ministry!

Advertisements

4 thoughts on “Usiionee haya Injili ya Kristo, iende mbele

  1. Shaloom Pastor Abel, Bwana akubariki kwa himizo hili, nilipokuwa nasoma himizo hilo, nikakumbuka mstari mmoja kwenye Biblia usemao, KILA ALIYE NA MWANA ANAO HUO USHUHUDA. Ni ukweli usiopingika kwamba kila aliyeokolewa, analola kusema, la kufanya kwa ajili ya Kristo. Vinginevyo watakuwepo. 1.WACHEZAJI na 2.WASHANGILIAJI. Ukienda uwanjani wakati wa mpira, ndipo utaelewa tofauti ya watu hao wawili, Mchezaji na Mshangiliaji. Mshangiliaji…SI LAZIMA AJE UWANJANI, SI LAZIMA AWAHI UWANJANI, AKIWA UWANJANI, HUTAFUTA MAHALI NA KUKAA, ANAWAKOSOA WACHEZAJI, HUPIGA KELELE, HUONDOKA WAKATI ANAOTAKA HATA MPIRA KABLA HAUJAISHA, ANA UHURU, AWEZA KUKAA AU KUSIMAMA. Lakini mchezaji hana sifa hizo, asante Pastor kutuhimiza, kama kila mmoja atacheza, ASIIONEE HAYA, UVIVU, INJILI, Adui yetu atanyang’anywa watu aliowabeba kuwapeleka motoni. Ebu TUCHEZE. Barikiwa.

  2. Ni kweli walokole wengi wa siku hizi kwanza hawapendi wajulikane kuwa wameokoka na wengine wanaionea haya injili Mungu atusaidie.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s