UJUMBE KWA AJILI YA TANZANIA

Mtumishi wa Mungu aitwaye Umaru Steven Bugwegwe, Kutoka Uganda Alikuja Tanzania June 2012 kuleta Ujumbe ufuatao. TANZANIA ITUBU KWA MAOVU YAKE. Maovu yenyewe ni haya: … Viongozi wa kanisa waliotegemewa kusimama na kuomba kwa ajili ya Taifa na kukemea maovu, badala yake wameuza kanisa kwa wanasiasa kwa ajili ya kutafuta misaada na kula nao. Hata wao huenda kwa waganga/wachawi, kutafuta nguvu. Ni wenye kiburi hata wakionywa hawasikii, Tena kazi yao ni kuangalia sadaka na matoleo tu na sio roho za watu. Viongozi hao hao wa dini ni Waasherati,wanafanya Uzinzi na kusema uongo.Wameshindwa kusimama katika nafasi zao ili kuikomboa nchi na kuiombea Rehema.

Nchi iko katika ukiwa na matatizo makubwa kwa sababu wale waliotegemewa kuisimamia ndio walioiuza. Mungu anachukizwa sana na mauaji ya Albino kwa ajili ya kutoa kafara kwa shetani. Watu wameabudu miungu,wamejiuza kwa shetani, wachawi na Ulozi.Wanasiasa nao badala ya kumtegemea Mungu wanategemea uchawi na Ulogi kwa kukosa msaada na Ushauri wa Viongozi wa makanisa (Watumishi wa Mungu)Matokeo yake kanisa halina mwelekeo wala nguvu za Mungu tena kwa sababu limeshiriki maovu!

Kanisa la Tanzania ni kama Yona!! Limemezwa na nyoka (chatu) linatakiwa kutapikwa!! Kutokana na haya Watanzania wasipotubu ..matukio haya yafuatayo yatatokea kwa kipindi cha miaka mitatu yaani 2012 hadi 2015…

1.NJAA KUBWA ISIYO NA MFANO WAKE.

2.TAUNI /MAGONJWA YASIYO NA TIBA .

3.VITA VITAKAYOWAFANYA WATANZANIA KUIKIMBIA NCHI YAO NA KUWA WAKIMBIZI.

4.JIJI LA DAR ES SALAAM KUMEZWA KABISA NA BAHARI.

5..MUNGU ATAIPATIA NCHI HII TAIFA LINGINE KIITAWALA NA KUUFAIDI UTAJIRI ALIOKUWA AMEWAANDALIA WATANZANIA ..

Kinachotakiwa ni TOBA ya kweli..kutitirisha MACHOZI ya kweli , KUOMBOLEZA na .Kuacha kabisa maovu.!!2Mambo ya Nyakati 7:14

Kwa maelezo zaidi au kuthibitisha ujumbe huu piga simu zifutazo :
+256 712 928984..Rev Steven Umaru Bugwegwe..
+255 757 619647 Mrs Miriam Dhudha .
Mratibu Kilimanjaro Intercessors waliopokea mjumbe huyu!
+255 754 650515 Apostle Moses Bakilana .
Mjumbe Kilimanjaro Intecessors (.Alimpokea alimhifadhi na kunfadhili Nabii huyu.)
+255 754 285783
Apostle Aimana Well ministry International walio-host ujumbe huu kufikia Watanzania . Wapatie Watanzania wote ujumbe huu hamasisha kuomba na kulia sana ili nchi hii itapikwe kama Yona !

UKIPOKEA UJUMBE HUU TUMIA WATU WENGI UWEZAVYO /WATANZANIA ILI WAFAHAMU NA KUHAMASISHA WATU KUOMBA

!!! Thanks

Advertisements

20 thoughts on “UJUMBE KWA AJILI YA TANZANIA

 1. hakuna kitu kinachonisikitisha kama kuona wakristo wakiwaziana mabaya,wakitazamiana mabaya na kuneneana maneno mabaya.kama mtaendelea hivyo naamini Mungu atamuinua farao kuwarudisha kwenye mstali.hivi hamjui msingi wa wakristo ni amani,upendo na haki,ninyi mnaomtamkia maneno yasiyofaa mtu anayesema katumwa mnatamka hivyo mkisukumwa na nani?Yesu hakuwa anatamka matamshi kama hayo na wala hakuwa anawawazia mabaya wengine.mnasikitisha

 2. naona kama yanatimia, maana yameanza kupigwa makanisa mahali pa kuabudia, pia KUNA MWINGINE ANATOKA KENYA NAYE AMEZUNGUMZA THE SAME MSG NA KAZUNGUKA MAKANISA MENGI ALIYOPEWA NAFASI KUWASILISHA UJUMBE. JAMANI TUJITAKASE

 3. Mwezi wa 7 mwaka huu nilisafiri kwenda Kampala,Uganda kikazi na nilipata nafasi ya kuonana na kuongea na huyu mtumishi kuhusu ujumbe huu kwa kina. Naamini ujumbe wake umekuja kama tahadhari kwa kanisa ili tujipange na kusimama katika nafasi yetu kama chumvi nchini. Mambo yanayoendelea Tanzania yanahitaji kanisa lililo macho sana katika ulimwengu wa roho na kama kanisa bado limelala tunaweza kufikiri kwamba ujumbe wa mtumishi huyu wa Mungu ni wa kawaida kama wengine.2 Nyakati 7:14.Mpelumbe,Oslo.

 4. Nipo Morogoro, kuna mtumishi anaitwa Mama Sabina Gereja naye kapewa ujumbe exactly kama huu. Kongamano la kutubu litakuwa tarehe 04/08/2012 na linatangazwa sana na Radio Okoa F.M. Tumshukuru Mungu kwa ajili ya rehema yake kwa Tanzania.

 5. Wapendwa Taifa la Mungu,

  Ingawa mwenye macho haambiwi tazama sasa tunaongezewa tazama mbele ya ukweli ulio wazi. Ni kwa sababu tunajidai kutokuona na kuendelea na kumuasi Mungu. Unabii wa sasa uko kwa kila mtu anayemuamini Mungu kutokana na kupewa utashi mkubwa unaotokana na Roho Mtakatifu aliyejaa duniani akituangazia, nasi kubaki na kazi moja ya kuchagua ama kumtumikia Mungu au Ibilisi.

  Angalia mambo yanayodhihirishwa na mienendo ya wengi wenye dhamana na mambo Muhimu yahusuyo mihimili ya dola. Kumekuwa na Ubinafsi ambao tulishaonywa na Mtumishi ambaye Mungu aliliteulia Taifa la Tanzania Mwl. J. K. Nyerere. Alionywa viongozi kutojihusisha nauwaniaji mali, angalia leo jinsi gani kila mwenye nafasi anavyjitahidi kujinufahisha hata kama ni kula rushwa ili kutotekeleza wajibu wa kupitisha mambo yanayofaa au kupitisha yasiyofaa.

  Wanadamu tumuombe Mungu atusamehe na awaonyeshe wale wanaoipeleka nchi pabaya kuwa wanafanya wasilostahili, na matokeo yake ni kuiangamiza nchi. Aihurumie nchi kwa niaba ya wachache ambao wahahisi kuwa wako ahera kutokana na dhiki wanaosababishiwa na hao waliopewa nafasi ya kutumikia lakini wakawa wahujumu wa mapaji ambayo Mungu aliwaandalia watu wake.

  Sisemi Zaidi bali namshukuru Mungu aliyempa Karama huyu aliyeweka maono yake katika mtandao ili tuamke.

  Mawaziri wetu, wakurugenzi wetu wa idara mbalimbali, wakuu, wabunge hasa wanaoogoza kamati, viongozi wa Dini, wanaodhani ni maskini na kutumia nafasi hiyo kutomjali Mungu kwa kuwa maandiko yanatoa onyo kwa matajiri na ufalme wa Mungu, watu wa umri mbalimbali kwa kujali mno mitindo ya maisha inayoibuka huku na kule na kuchukuliwa nayo kama mafurikiko yasombavyo kila kitu, tujichunguze.

 6. Shalom,nashauri tusicheze na Mungu.tuchunge midomo yetu tusihukumu huyu mtu kama katumwa na Mungu au la si juu yetu.Mtu ambaye yupo vizuri na Mungu na Roho Mtakatifu anamwongoza anajua taifa hili lipo katika wakati gani; hivyo hatasubiri kuambiwa lia na kutubu kwa ajili ya Tanzania aliye na sikio na asikie.Let’s pray for our nation hali ni mbaya,tatizo tunaenenda kimwili na si kiroho.

 7. Issue siyo kuombea nchi kwani kuombea taifa na viongozi wote ni jukumu na wajibu wa kanisa, (1 Timotheo 2: 1 – 4) hilo halina ubishi . Huo unaoitwa unabii ndio tatizo, hauendani na maandiko. Najua wengi mtatoa mifano ya Agano la Kale, lakini kumbukeni ya kwamba Bwana Yesu alikuwa bado hajaja kuchukua dhambi za ulimwengu na kufa msalabani na kufufuka, kitu ambacho kimepellekea sisi kuishi chini ya agano lililo bora zaidi, Agano Jipya.

  Katika Agano Jipya kulikuwa na wenye dhambi wengi tu katika mataifa ya wakati ule, Israeli ikiwa mojawapo, lakini mataifa hayo hayakuadhibiwa na Mungu kwa ajili ya dhambi zao, hebu jiulize, kwanini? Mtume Paulo alipofika Athena roho yake ilichukizwa sana na masanamu yaliyokuwa yametapakaa katika mji ule, lakini hakutoa unabii wa kuwaangamiza watu wasipotubu, hakuwaambia kuwa kuabudu sanamu ni dhambi na wataishia motoni wasipotubu (pamoja na kwamba huo ndio ukweli wenyewe) bali alitumia fursa aliyopata kuwahubiria injili waokoke, huo ndio mfano wa kuigwa.

  Vilevile tukumbuke ya kwamba hapa duniani siyo nyumbani kwetu, wwenyeji wetu uko mbinguni siyo hapa, tuwaze yaliyo juu Kristo aliko. Hazina yako ilipo ndipo na moyo wako utakapokuwa. Lengo la Mungu kututaka tuwaombee wote walio katika uongozi ni ili tuweze kuwahubiria wengine injili waokoke waupate uzima wa milele,

  Kanisa la Yesu Kristo kamwe haliwezi “kumezwa na chatu” kama huo unabii unavyodai, hilo pekee ni kigezo cha kuukataa unabii huo na kuuita batili! Yesu alisema wazi kabisa milango ya kuzimu haitalishinda Kanisa lake na yeye ndiye kichwa cha kanisa hilo, sasa iweje leo kanisa limezwe halafu linahitaji kutapikwa? tumuamini nani Bwana Yesu au huyo nabii? Mimi nachagua kumuamini Bwana Yesu. Mbarikiwe!

 8. Sikilizeni, Mungu hajishughulishi na watu wasiojielewa! 
  Hivi huyo anayetaka kujiingiza ktk toba, si bora asipoteze nguvu na wakati wake, maana siku zote alizokuwepo hapa hakuwahi kujua kuwa kanisa liko ktk hali hiyo mpaka huyo nabii alipokuja? Sasa utamuomba Mungu akufanyie nini? Bora mfunge safari mwende kwa huyo nabii mkatubu ninyi kwanza halafu ndio awaombee kwa Mungu hayo mnayoyataka! 

  Kweli, kanisa, yule mwanamke, “atajirundikia walimu” ndio tunayaona sasa hivi! Kanisa linaingizwa katika dhiki mchana kweupeee, kisa? Limeliacha Neno sasa linameza kila uongo na kuutukuza kuwa ni Unabii!!

  Ndugu zangu hayo ni maroho ya WIVU tu, hayanaga aibu, msijisumbue, kama mmedanganyika na mambo ya mwilini aliyokuja nayo huyo nabii, hayo yaliyojaa dunia nzima, leo kaja kuwashindilia uongo wa kuwatia uchungu na kuwachonganisha! Mlikwisha ambiwa mtawala wa dunia hii ni nani au mmekwisha sahau? Kanisa linajazwa mashaka, manabii uchwara wanalitoa ktk imani polepole!!!

  Sodoma ilipigwa kiberiti kwa ushoga, Uganda ushoga umeshamiri, hakuna wakristo mashoga huko? Angemaliza shida ya nyumbani kwao kwanza ndio aje huku. Paulo alianzia kwao kwanza kabla ya kutugeukia mataifa.

  Kanisa iweni IMARA katika Neno mlilopewa msiwe wepesi wa kuliacha!

  Milinga unameza kila kitu, mbona “nabii Lwembe” unamkimbia?! 

  Poleeeni saaana!

 9. Shalom Alinda,
  umeuliza swali zuri, unabii unaweza kuwa wa kuonya kwamba fanyehi hivi la sivyo hiki kitatokea, hii inaweza badilika
  na kuna nabii kama ninaona maafa yanatokea, ninaona moto sehemu fulani, hapa ni maono nadhani hata anaposema muombe ni ktk kupata tu nguvu kusimama ktk hili jaribu sio kuepusha, labda ndio maana wengi hawamuelewi kwasababu ana maono ya maafa au vitu vitakavyotokea bila kuwa na uwezo wa Mungu kuvizuia…?
  Kinachoupa nguvu huu unabii ni mambo yaliyo dhahiri nchini kwetu je haya maovu hayapo? Na je ktk maovu haya tunategemea kuvuna nini? Hata bila ya unabii huu hebu tujikague hivi Mungu anapendezwa na taifa lisilo na haki? mauaji ya wanyonge, ufisadi nk na badala ya watu wa Mungu kukemea tumekaa kimya maana serikali ndio kimbilio letu ktk misaada ujenzi wa makanisa nk tukikemea tutakosa huo ukaribu….Kuna baraka ktk hili?

 10. Najua kazi ya nabii si kuzuia kile wanachokitabiri, ni kufuata maelekezo tusijekumezwa kwenye tundu kama Yona. Ila nina swali hivi nabii za TB Joshua, watu huwa hawaombi? mbona sijasikia zilizopinduliwa kwa maombi?

 11. Kwani tukitubu tutakuwa tumefanya dhambi?
  Kwani tukijinyenyekeza kwa Bwana Mungu tutakuwa tumepotea? Sala zetu, juhudi yetu itakuwa bure? Yesu alisema “OMBENI MSIINGIE MAJARIBUNI”.
  Ni hasara gani tutaipata/ tunaipata?

  Mimi nadhani tutumie hekima ndogo tu; kuwa “tukinyenyekea kwa Bwana, tukitubu na kuomba rehema. YEYE ATAIPONYA NCHI” that’s all.
  Tusijifanye hatuoni wala kuelewa magumu ambayo kanisa linapitia na nchi inapitia.

 12. Shalom
  samahani kuna watu wanapinga huu unabii, huku nyuma Mwl Mwakasege aliwahi kusema yale matetemeko/mafuriko yaliyoua Haiti ni kwasababu nchi ile ina abudu mizimu (voodoo) hawana hofu ya Mungu kabisa. Matukio kama hayo Japan pia yalitabiriwa kwenye kitabu kimoja “The Bible code” na mengine mengi.
  Huu unabii mie sioni cha ajabu kwani iwapo yatatokea maovu aliyotaja hayapo hapa Tanzania?
  1. Mauaji ya albino: google hili neno ni Tanzania pekee inayoongoza hili halipo kwa jirani zetu wote Afrika mashariki, kusini wala magharibi
  2. Rushwa: hii sina haja ya kutoa takwimu nakumbuka hii ikiwepo tu ina maana wanyonge hawana haki
  3. Kuanguka kwa kanisa: kagua kila leo tunasikia, tunasoma viongozi au wapendwa walioingia uzinzi, wizi, uasherati, ushirikina nk. Sikatai wapo wanyoofu lakini waovu pia wapo!
  4. Tunaanza kukosa uhuru wa kuabudu na vitisho kwa kanisa baadhi ya maeneo

  Sasa pamoja na yote haya mnaopinga naomba mnitajie viongozi au wakristo walionyesha nia ya wazi
  1. Kuamsha taifa liombe toba
  2. Kukemea serikali na kudai haki kwa wanyonge wanaonyimwa haki kwasababu ya rushwa, ufisadi, ubinafsi, udini au ukwasi wa serikali na mengineyo
  3. Kutumia nafasi walizomo kuihoji serikali au kuishauri kuhusu mwelekeo wa taifa (mfano viongozi wakuu wa kanisa, serikalini, bungeni au kila mmoja ktk nafasi yake) kila mtu kimya anaogopa kupoteza nafasi, ukaribu na upendeleo! ni kwamba kanisa LIMELALA!

  Kutokana na hayo hapo juu unategemea utavuna nini ktk taifa hili? Baraka?
  Ni kweli Tanzania tumebarikiwa mno na kila leo maeneo mapya ya madini uranium, dhahabu na mengine yanatambuliwa. Lakini ukichunguza historia ya nchi nyingine zeneye madini hayo bila ya uongozi imara wenye haki na kama laana ya kuingiza mataifa kugawana mali hizo, angalia DRC, Ivory coast nk.
  Ukiona unapokea baraka nyingi jiulize Mungu anataka nifanye nini na hiki? ni wakati wa kuhoji Mungu anakusudi gani ktk kila baraka na matukio mapya ktk nchi yetu… Jaribuni kuangaza macho nini maana ya mataifa makubwa kuwa na interest na Tanzania na nia yake. wapendwa tunapaswa kusimama ktk zamu kuwaombea viongozi wetu waamke, waliamshe taifa kuomba, Mungu atupe uongozi unaojali haki za watu wenye hofu ya Mungu! Siamini ktk manabii, ila ninapima unabii kama ni kwa kulijenga kanisa na vigezo vipo sawa nitaufanyia kazi. Bwana azidi kutulinda!

 13. Wapendwa,

  Ujumbe huu ungeletwa kwetu na TB Joshua wa Nigeria watu wote nadhani wangeukataa na kusema kwamba huyu mnaigeria ni nabii asiyetoka kwa Mungu. Huyu Mganda naye tunasemaje? Je, watanzania hukubali manabii toka nchi zingine tofauti na Nigeria tu?

  Kuna mambo kadhaa TB Joshua amekuwa akiyatoa sana hata yanayohusu Tanzania na afrika yote, lakini watu wamekuwa wakiyapuuza wala hawaombi Mungu. Kwa mfano kuhusu migomo na migogoro ya kisiasa na kiuchumi. Yote ameyatabiri akiliomba kanisa pia liombe sana. Lakini kuna watu tumepuuzia tu.

  Kuna mambo Mzee wa “Upako wa Upako” alishwahi kutabiri yakatokea lakini wapendwa wengi tulipuuza tu na kusema huyo naye ni njaa tu.

  Kuna mambo mengi Danstan Maboya aliwahi kutabiri kuhusu Tanzania, lakini wengi tulipuuza na kusema huyu naye……anatafuta pesa tu.

  Yaani watanzania tuna ugonjwa wa kupuuza manabii wa Mungu. Tunawahukumu kwa kila jambo na kupuuza kila wanalolisema.

  Watanzania hebu topone. Hebu tuwakubali manabii. Hata kama hatuna imani na yale wayatabiriyo, < BASI TUSEME , KAMA NI UNABII TOKA KWA BWANA UTATIMIA, KAMA SIYO WA BWANA HAUTATIMIA.

  Kisha tuombe Mungu REHEMA ZAKE ZA MILELE ATUNUSURU. AMINA.

 14. Kila mmoja wetu ajichunguze mwenyewe katika nafsi na nafasi yake anachangia vipi madhambi tajwa na huyu ndugu yetu. Sio kwamba hasemi ukweli wala sio kwamba yeye ni nabii alieyeitwa na kuteuliwa na Mungu awe nabii kwa maana ya Agano la Kale. Na tusifikirie mbwembwe za vitisho anvyopenyeza katika maonyo yake ya kinabii kwani kama anavyosema Patric G Kamera hivivitisho haviingii akilini katika nyakati hizi za mwisho za ujio wa pili wa Bwana. Bali, ni dhahiri kwamba vitendo vya dhambi vimekithiri sio tu uraiani bali pia katika makanisa (taasisi na waamini) na ndani ya vyombo vya Dola: Kiburi na majivuno/majigambo, Uzinzi, uonevu, ukaidi, dhulima, ushirikina, na hasa kwa upande wa dola na siasa-uchwara, utesaji wa kinyama na mauaji. Yote haya yanaathiri hasa watu wa hali za chini kijamii na kiuchumi; hali hatarishi kimaisha (vulnerable circumstances); na, hivyo, ni machukizo kwa umma na kwa Mungu. Je wewe na mimi hatuhusiki kwa namna fulani na hayo maovu. Kila mbatizwa na hivyo Mkristu halisi ni: Kuhani, mchungaji na nabii. Kiidadi tu wengi. Haya maovu yanatoka wapi kama sisi hathusiki nayo. KWELI TUTUBU KWA DHATI TUEPUSHE GADHAU NA MATESO YA KRISTU BWANA WETU ILI SISI NA WENGINE WENGI TUWAOMBEAO TUWEZE KUISHI HAPA DUNIANI KWA AMANI NA KUUKWAA UZIMA WA MILELE MBINGUNI KWA BWANA MFUFUKA!

 15. Jamani eee huu “ujumbe” ni ushauri na mawazo mazuri tu ya huyo ndugu yetu mpendwa sioni vigezo vya kudai kuwa ni unabii toka kwa Mungu.

  Kwanini nasema hivyo:

  1. Bwana Yesu alisema atalijenga kanisa lake na milango ya kuzimu haitalishinda, iweje eti leo Kanisa la Yesu Kristo (sizungumzii dhehebu hapa,) limezwe na chatu, ibilisi? Wapi na wapi… kama kweli limemezwa basi halikuwa kanisa, ni kitu kingine hicho. Kanisa la Yesu Kristo liko, tena liko imara, Yeye ndiye Kichwa cha kanisa, sasa je na Bwana Yesu Kichwa cha kanisa naye kamezwa na huyo chatu?! !! Hebu tuacheni utani!!

  2. Unabii wa Agano jipya unajenga, unafariji na kutia moyo. Hata kama ujumbe uhahusu janga kutokea utaletwa kwa njia inayoendeana na 1 Wakorintho 14:3 Hata Agabo alipotoa unabii kuhusu njaa kuu iliyokuwa inakuja,, kulikuwa na hekima ya Mungu namna ya kupeleka msaada kwa watakaoathirika. Unabii ulitolewa kwa namna ya kuwaandaa wapendwa na kinachokuja na si kuwatisha.

  3. Wapo viongozi wengi tu wa makanisa Tanzania ambao ni waaminifu mbele za Mungu, na Mungu wetu ni Mungu wa Haki, iweje leo awalundike wote kundi moja na kuiadhibu nchi nzima bila kutofautisha wakati Bwana Yesu alishaadhibiwa kwa ajiili ya dhambi zao? Na isitoshe kuacha maovu si tija, hakuna atakayeingia mbinguni kwa sababu ya matendo mema, wokovu ni njia pekee. HIvyo sidhani kama Mungu atawasisitizia watu waache uovu wakati anajua kwamba hawajaokoka. Ukishaokoka matokeo yake utaachana na uovu.

  4 . Je, Mungu anaiadhibu Tanzania kwa sababu ipi? Dhambi za viongozi wa kanisa? Dhambi za wale wanaoua albino? washirikina? Au? Kama ni kwa sababu ya wote hao, basi hebu tuelezane Bwana Yesu alikufa msalabani kwa ajili ya nini na nani? Yohana alisema, “tazama Mwana kondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu” (Yohana 1: 29) Hukumu ya adhabu itatolewa na Bwana Yesu siku ya mwisho. Bado yuko kwemye Kiti cha rehema, hajakalia kiti cha hukumu bado!

  5. Je, ni wapi kwenye Agano JIpya kuna unabii unaofanana na huu? Jibu: Hakuna! Je unabii huu unawavuta ama kuwaelekeza watu kwa Bwana Yesu? Au unaishia kuwatisha na kuwakatisha watu tamaa? Neno linasema ushuhuda wa Yesu ndio roho ya unabii (Ufunuo 19: 10) Vitisho vya tauni, vita, DSM kumezwa na bahari, n.k kama matokeo ya Tanzania kutotubu kunaonyesha uelewa hafifu wa maandiko na neema ya Mungu.

  6. Kudai kuwa hayo majanga yatatokea kwa miaka mitatu kuanzia 2012 – 2015 maana yake nini? Kama baada ya miaka hiyo mitatu Tanzania isipotubu je? Haya madai mengine hayana mantiki kabisa,, sasa ikipita hiyo miaka mitatu ndo inakuwaje? Hii peke yake ni sababu tosha ya kutokuutambua huu kama unabii wa kweli! Maana hata kwenye Agano la Kale walipoambiwa kuwa watapata majanga fulani fulani kila mara iliishia na maneno kama “ndipo mtakapojua ya kuwa mimi ni Bwana”. Sasa unabii huu unaishia na vitisho vya miaka mitatu halafu basi, ndo Mungu ataisusia Tanzania au…?

  Ngoja niishie hapo, ila labda niseme tu, wakati umefika tukue kiroho tufikie mahala pa kuwa na ujasiri wa kuupima unabii kwa vigezo vya Neno la Mungu bila kuangalia ni nani aliyeutoa. Neno linasema tusitweze unabii, jaribuni mambo yote lishikeni lililo jema.

  Kama nilivyosema haoo awali nachukulia ujumbe huu kuwa ni mawazo, ushauri ama mawaidha ya huyo ndugu yetu Umaru ambaye anaonekana kuwa anaitakia mema Tanzania na si ajabu ameitwa kuiombea Tanzania.

 16. Shalom
  mie nadhani Taifa linahitaji toba ya kweli, wapendwa unabii huu tuufanyie kazi. Tujikague ingawa ni ngumu kumeza na tumrudie Mungu kwa toba na maombi tuokoe Taifa letu hili. Ujumbe huu ungependeza ukawekwa hata kwenye magazeti ili watu wote waweze kuusoma.
  Mbarikiwe

 17. Huu ujumbe ni kweli, ukifuatilia kinachoendelea katika Nchi yetu utaona ni kweli. Hakuna njia nyingine ya kufanya ni TOBA tu, tulie mbele za Mungu, ni mwingi wa Rehema, ni mwingi wa Huruma, ataisamehe Nchi yetu. Kwa maana imeandikwa . IKIWA WATU WANGU, WALIOITWA KWA JINA LANGU WATAJINYENYEKESHA NA KUOMBA, NA KUZIACHA NJIA ZAO MBAYA, NITASIKIA MAOMBI YAO, NA NITAIPONYA NCHI YAO. Pia tukimkumbuka Ibrahim alivyoiombea SODOMA, Alipouliza swali. Wakipatikana 50 wenye haki utafanyaje? Akasema nitausamehe, akauliza tena, na tena. Hawakupatikana Hiyo idadi ya kustahili kusamehewa, mwisho ikachomeka. Ebu kila anayejua kuwa ni MWENYE HAKI AMLINGANE MUNGU. Nchi yetu itaponywa. Asanteni.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s