Umoja wa makanisa Tanga na mapendekezo ya katiba mpya

Umoja wa makanisa Tanga, ukijumuisha wachungaji wa madhehebu ya Kikristo yaliyopo Tanga, umetafakari na kubaini kwamba, ni vema Watanzania waone umuhimu wa kujitokeza kwa nia moja, na kutoa mchango wa mapendekezo ya katiba mpya kwa uhuru, hasa kwa kuweka angalizo katika maeneo nyeti yanayoweza kuhatarisha amani, ustawi, uhuru wa kuabudu na hatma ya nchi yetu. Aidha kuombea mchakato mzima, tangu kutoa na kupokea maoni, kuyaratibu, kuyaandika, chapisho la awali, na mchakato mzima hadi kupitishwa na kuwa katiba kamili.

Baadhi ya maeneo nyeti ya kuzingatia ni kama ifuatavyo.

UHURU WA KUABUDU

Kifungu namba 19 chenye vifungu vidogo namba (1), (2), (3) na (4). Kama lilivyotolewa chapisho la 2005 Vyote viingie kwenye katiba mpya, kikiainisha ya kwamba, kazi ya kutangaza na kuendeleza dini itakuwa ni ya dini husika, serikali au taasisi yoeyote ya serikali haitahusika, aidha uhuru wa mawazo au wa kiimani utakuwepo kwa Watanzania wote.

Kifungu hiki ni muhimu kina mchango nkubwa kwenye amani ya nchi yetu, kifungu hiki kikiondolewa, nchi inaweza kuingia kwenye hatari ya machafuko ya kidini, kwa dini mojawapo kujihesabia haki zaidi ya dini nyingine, na hata kuzihukumu dini nyingine kuwa hazina haki, kama Somalia, Nigeria na kadahlika.

VYOMBO VYENYE MAMLAKA YA UTOAJI WA HAKI

Kifungu namba 4. (1) na 4(2) vya katika ya 1977 kama ilivyo kwenye chapisho la 2005 viingie kwenye katiba mpya, ikiainisha kwamba vyombo pekee vyenye mamlaka ya kutoa haki ni mahakama ya serikali ya muungano na mahakama ya serikali ya mapinduzi.

MAHAKAMA ZA KIDINI

Wakristo wameagizwa katika mandiko ya Neno la Mungu kuwa na mabaraza yao ya kuamua kesi zao wenyewe. (Je! Mtu wa kwenu akiwa ana daawa juu ya mwenzake athubutu kushitaki mbele ya wasio haki, wala si mbele ya watakatifu? Au hamjui ya kwamba watakatifu watauhukumu ulimwengu? Na ikiwa ulimwengu utahukumiwa na ninyi, je! Hamstahili kukata hukumu zilizo ndogo? Hamjui ya kuwa mtawahukumu malaika, basi si zaidi sana mambo ya maisha haya? Basi, mkiwa na mahali panapohukumiwa mambo ya maisha haya, mwawaweka kuwa waamuzi hao waliohesabiwa kuwa si kitu; katika kanisa? Nasema hayo nipate kuwatahayarisha. Je! Ndivyo, kwamba kwenu hakuna hata mtu mmoja mwenye hekima, awezaye kukata maneno ya ndugu zake?) 1.Kor 6:1-5.  Wakristo wamekuwa wakiendesha mabaraza hawa makanisani mwao, wakiyaita mabaraza ya usuluhishi, kushughulikia masuala yanayohusu wakristo. Hata hivyo mtu asiporidhika anaweza kwena kutafuta haki yake kwenya mahakama ya jamhuri. (pia soma Matayo 18:15-17)

Ikiwa waislam wanataka kuwa na mahakama yao ya kidini (mahakama ya kadhi) basi inawapasa wazifanyie misikitini mwao, kama wakriso wanavyofanyia makanisani mwao, au dini nyingine zote wanavyo suluhisha tofauti zao kwa mujibu wa imani zao kwenye nyumba zao za ibada, na mahakama ya jamhuri kuwa ndio chombo cha mwisho cha kutoa haki, kwa yote yatakayoshindikana kwenye mabaraza ya kidini.

SABABU ZA KUKATAA MAHAKAMA ZA KIDINI KWENYE KATIBA YA NCHI

1)      Dini yoyote inayoamini kuwa inayo haki ya kuwa na mahakama yake, dini hiyo na ifanye hivyo katika nyumba zao za ibada, katika makusanyiko ya waumini wa dini hiyo, maadam hao wote wanaakubaliana na hukumu za imani yao. Hukumu yoyote ya dini mojawapo katika eneo Fulani, huongozwa na imani ya dini hiyo, na mara nyingi huwa haikubaliani na mtazamo au mapokeo ya imani ya dini nyingine. Ni sababu kubwa ya kuleta machafuko ya kidini.

2)      Kuingiza au kutaja mahakama mojawapo ya kidini, mfano mahakama ya kadhi, kwenye katiba ya nchi yetu, ni kitendo cha serikali kujikita katika dini moja au kuiinua dini hiyo dhidi ya dini nyingine, hivyo ni ubaguzi na kunyima haki dini nyingine.

3)      Katiba ya nchi ni kwa ajili ya Watanzania wote bila kujali imani zao za kidini, mahakama ya kadhi ni chombo cha waislam pekeyao. Kwenye katiba ya taifa tujadili mambo yanayowaunganisha na kuwatambulisha Watamzania katika umoja wa kitaifa, jambo lolote linalowatenganisha Watanzania ama kwa dini zao, au kwa makabila yao, kamwe lisipewe nafasi katika katiba ya nchi yetu.

4)      Sheria nyingi za kidini zinapingana na sheria za kiserikali. Mfano sheria ya kiislam inatoa hukumu ya mtu kukatwa viungo vya mwili wake, tofauti na mahakama ya Jamhuri, na makosa mengine hukumu yake ni mauaji ya kikatili kwa mtuhumiwa bila kujali kwamba ni muumini au au sio muumini wa dini ya kiislam. Aidha mtu akiamua kuacha dini ya uislam na kuingia kwenye dini nyingine, au hata mtu asiyekuwa muislam anapokataa kuwa muislam, wote hao hukumu yao ni kuuwawa. Aidha waislam wameagizwa kufanya vita kupigana na kuua wasio waislam. Soma Quran 6:151, Quran 9:111, Quran 9:123, Quran 61:10-12, Quran 5:33,38  (Quran tukufu tafsiri ya Farsihi chapa ya 8)

5)      Sheria za mahakama ya kadhi zimeshawahukumu wasiokuwa waislam, na kuwaita makafir, hivyo yeyote asiyekuwa muislam hana haki mbele ya mahakama hiyo. Kumbuka jamii zetu, hata familia nyingi, zina mchanganyiko wa watu walio waumini wa dini tofauti. Hatma ya familia ikiamuliwa kwa sharia za kidini, ni dhahiri kuwa itawanyima haki wanafamilia walio waumini wa dini nyingine.

6)      Kuingiza mahakama ya kadhi kwenye katiba ya nchi yetu, ni kuligawa taifa katika matabaka ya madaraja ya kidini, na hivyo itachochea mafarakano na uvunjifu wa amani nchini. Mfano yanayotokea nchini Sudan, (kikundi cha janjaweed), Nigeria (boko-haram), Somalia (Al-shabab) ambao wanashambulia raia wasio na hatia, hasa makanisa na wakristo, kwa hamasisho la itikadi ya kidini, kikundi ambacho kimekuwa kikitishia amani Afrika mashariki hususan nchini Kenya,

Matukio ya uvunjifu wa amani yaliyotokea hivikaribuni visiwani Zanzibar, ambayo yalilenga zaidi kushambulia makanisa na ukristo visiwani humo, kwenye harakati za kikundi cha kiislam kiitwacho uamsho.

7)      Si halali kwa mahakama ya kadhi ambayo ni chombo cha kidini cha kiislam, kuendeshwa kwa mafungu ya bajeti ya serikali, fedha inayotokana na kodi ya watanzania wote, ambao wengine ni wakristo na au waumini wa dini nyingine. Hali hiyo inaweza kusababisha chuki kwa wasio waislam kuendelea kulipa kodi, ambayo sehemu yake hutumika kuendeleza shighuli za uislam, hasa kwa wanao amani kwamba ni haram kwake kutoa fedha itakayotumika kufadhili shughuli yoyote ya dini nyingine.

Tanzania iendelee kuwa nchi isiyokuwa ya kidini, bali Watanzania waendelee kuwa na dini zao, Waskristo, Waislam, na watu wa imani za dini nyinginezo, na wote waabudu kwa uhuru ilimradi wasivunje sheria za nchi. HIVYO TUNAHITAJI KATIBA AMBAYO KAMWE HAITAWAGA WATANZANIA KATIKA JAMBO LOLOTE KWA MSINGI  WA  DINI ZAO.

Nchi isiingie mkataba au uanachama wa jumuia yoyote ya kikanda yenye mtazamo wowote wa kidini kama OIC kufanya hivyo ni kuitangaza nchi kuwa ni ya kidini, hususan Watanzania wote ni waislam, kitu ambacho sio kweli.

MUUNGANO

1)      Muungano uboreshwe kwa kutoa uwakilishi unaowiana na idadi ya watu wanaowakilishwa katika mabaraza ya muungano, kwa upande wa bara yenye watu zaidi ya milioni 42, na Zanzibar yenye watu takriban milioni moja. Ikibidi kuwe na  kura ya maoni,

2)      Katiba ya muungano iseme wazi kuhusu haki ya urai wa Watanzania bara wanapokwenda visiwani, na wa Watanzania visiwani wanapokwenda bara.

3)      Katiba ya muungano iweke bayana mipaka ya katiba ya serikali ya mapinduzi ya Zanzibar, katika masuala ya muungano, na au katika eneo la ardhi ya muungano. Mathalan Mtanzania asishurutishwe kufuata nguzo mojawapo ya uislam awapo katika sehem yoyote ya ardhi ya jamhuri ya muungano, iwapo yeye si muumini wa dini hiyo hasa katika mwezi wa Ramadhani, aidha Serikali isitumike kama chombo cha dini, kuwaadhibu raia wasio waislam, kwa kutotekeleza nguzo ya dini ambayo hawaimini, wakati ambapo kwa kufanya hivyo hajavunja sheria yoyote ya jamhuri.

TUME YA UCHAGUZI

Tume ya uchaguzi, ambayo moja ya majukumu yake ni kusimamia uchaguzi mkuu ukiwepo ule wa rais, isiteuliwe na rais, bali taasisi zilizo wadau wa uchaguzi, kama vile vyama vya siasa vilivyosajiliwa na taasisi nyingine. Nao wahusike ama kuteua au kuchagua watendaji wa tume ya uchaguzi. Hii itasaidia kuepusha malalamiko yasiyokuwa ya lazima hasa kwa wanaoshindwa uchaguzi.

Muhimu:- TUNAOMBA WAKRISTO WAYAJUE HAYA, IKIWEZEKANA WASOMEWE, AIDHA WAHAMASISHWE KUJITOKEZA KWA WINGI, KUTOA MAONI YA KATIBA MPYA, PAMOJA NA MENGINE, ILI TUPATE KATIBA NZURI ISIYOINUA DINI MOJA, TOFAUTI NA WENZETU WANAVYOTAKA

–Samsasali.blogspot.com

Advertisements

6 thoughts on “Umoja wa makanisa Tanga na mapendekezo ya katiba mpya

  1. Kimsingi tunapozungumzia mahakama ya kadhi kupewa ruzuku na serikali si sahihi mantiki yake ni kwamba mahakama hizo zitahusu waislamu tu,ni tofauti na shule na hospitali ziwe za kikristo au za kiislamu maana huduma zitakazo tolewa hapo hazitabagua wakristo wala waislam,mf wako waislamu wengi waliosoma kwenye shule za kikristo,lakini pia ni wagonjwa wangapi bila kujali dini zao wanaotibiwa kwenye hospitali kama Bugando na KCMC,lakini pia ni watanzania wangapi waliopita kwenye shule za kiislamu kama JUMUIA SEC iliyoko Tanga,hivyo tusitoe hoja tukachanganya mahakama ya kadhi na huduma nyingine za kijamii

  2. Msemakweli, utakuwa mbumbumbu saana,usiyefaa hata kuelezwa chochote maaana huna hata uwezo wa kuelewa chochote!!!

  3. Huu ni unafiki na upotoshaji wa hali ya juu.Maaaskofu wanazungumzia kuhusu kutokutumia kodi ya watanzania kuendeshea mahakama za waislamu,mbona hoja za waislamu kuhusu serikali kufadhili hospitali za makanisa haijibiwi?Hivi sasa zaidi ya 50% ya bajeti ya wizara ya fedha huelekezwa katika ufadhili wa hospitali za makanisa,mbona maaskofu hawajapiga kelele kudai serikali inawapendelea?Lingine mnajua fika kuwa wakati wa utawala wa Nyerere shule za makanisa zilikuwa zikiendeshwa kwa posho za serikali na mpaka wafanyakazi wengi (waalimu) katika shule hizo walikuwa wakilipwa na serikali.Yajibiwe hayo machache katika ufisadi mwingi na hujuma nyingi za serikali na makanisa dhidi ya raia wengine.

  4. KAMA VILE ILIVYO UMOJA WA MATAIFA KILA NCHI INA HADHI SAWA IWE NDOGO MFANO BURUNDI IKILINGANISHWA NA MARIKANI HIVYO ZANZIBAR NI NCHI YENYE MADARAKA KAMILI NA WALA ISIFIKIRIWE NI MKOA IMEUNGANA NA TANGANYIKA KUUNDA JAMHURI YA MUUNGANO TANZANIA KITENDO CHOCHOTE CHA KUIDHALILISHA ZANZIBAR NI KUIKOSEA ADABU KWANI NI DOLA YA ZAMANI SI AJABU KULIKO TANGANYIKA NI VEMA UWAKILISHI SAWA UZINGATIWE KAMA VILE VIKAO VYA AU NA UNO SI VEMA MADHEHEBU KUBEBA SERA YA CHAMA CHA CHADEMA CHENYE UWAKILISHI MDODO ZANZIBAR WASIOTAKA MUUNGANO UWEPO ILI IWE RAHISI KWAO KUSHIKA DOLA ILA IKUMBUKWE NJE YA MUUNGANO HAKUNA TANGANYIKA WALA ZANZIBAR NA KAMA NI HIVYO UKO UWEZEKANO WA PEMBA NA UNGUJA KUWA NCHI TOFAUTI KAMA ILIVYO VYEPESI TANGANYIKA KUSAMBARATIKA KAMA USSR YA ZAMANI TUSIPOKUWA WAANGALIFU WAKO GORBARCHEV WENGI HAPA TANZANIA NIA YAO NI KUSAMBARATISHA TANZANIA ILI UTABIRI ALIOTOA HAYATI JK NYERERE UTIMIE

  5. Wakristo tuamkeni tusiwe wapole kwani Yesu kutuita sisi ni kondoo wake siyo kwamba tuwe wajinga kama kondoo wanyama,tuombe bila kukona hayo mapepo yawatoke ya kuharibu Amani tunayojivunia Duniani kote pia tujitokeze ktk maoni tuwaaibishe hawa jamaa wanaodai maslahi ya dini yao.MUNGU AWABARIKI SANA.

  6. Amen ni kweli tunashukuru kwamba hawa wanaliona hili, wakristo nasi tuinuke tutoe maoni yetu, katiba ikishaundwa hakuna kwa kukimbilia.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s