IMANI – 2

 Ndugu mpendwa nakukaribisha sana katika mfululizo huu wa makala ya Imani;naamini unazidi kubarikiwa na somo hili.Ni mimi Docta Lightness William Ng’unda karibu tuendelee.

       Makala yaliyopita tulizungumza juu ya imani inayoambatana na matendo, na leo nitaendeleza hapohapo ili nisikuache.Imani ya matendo inaenda pia sambamba na ukiri wetu na ni muhimu kuchunguza sana ukiri wetu sio kwa kinywa tu bali katika matendo pia.Ukiri wa matendo huwa una nguvu hata kuliko ukiri wa maneno.Namaanisha usiishie kusema tu bali weka hayo maneno kwa matendo pia.Ni muhimu ukiri wa maneno uende sambamba na ukiri wa matendo.

      Mfano mzuri ni huu watoto wengi wa Mungu wamekuwa wanaishi maisha ya kutozingatia kazi,na wanapendelea maisha ya mteremko kwa watu wengine huku wakidai wanaishi kwa IMANI.Mungu anashindwa kuwabariki kwa sababu hakuna wanachokifanya,wanaishia kumlaumu Mungu na kumwona Mungu kama muongo na kumbe sivyo ilivyo.Mungu ameweka wazi katika (2Wathesalonike3:10) Asiyefanya kazi na asile.Lazima uweke mikakati yako kiroho,kinafsi,kiakili na kimwili kupitia ahadi za Mungu ili afanikishe mipango yako. Ukiomba pesa fanya kazi fulani ili Mungu atumie huo mlango kukubariki huku ukiamini.

IMANI NI MKONO WA KUPOKEA MAJIBU

     Watoto wengi wa Mungu ni waombaji wazuri lakini sio wapokeaji wazuri.Namaanisha mtu anaweza funga hata siku 21 akiomba tu lakini upande wa upokeaji hayupo wala haelewi.Maombi ni mazuri sana ila usiwe unajitesa bure lazima ujue kupokea pia.Inawezekana mambo unayopitia Mungu alishayajibu siku nyingi lakini hukujua jinsi ya kupokea na ndio maana biblia inasema  (Hosea 4:6) watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa).Nguvu ile ile uliyoitumia kuomba itumie nguvu hiyohiyo kupokea.Namaanisha ukijua umeomba jambo lolote sawasawa na mapenzi ya Mungu hilo ni lako tayari, na kujua kwamba ni mapenzi ya Mungu utaangalia neno lake linasema nini juu ya hilo jambo unaloliomba na hayo ndiyo mapenzi ya Mungu.Na huu ndio ujasiri tulio nao  kwake,ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake,  atatusikia.Na kama tukijua kwamba atusikia,tuombacho chote,twajua kwamba TUNAZO zile haja tulizomwomba.’(1 Yohana 5:14) Hapa inamaanisha nini? tunajua tunazo zile haja, kwa hiyo ukiomba uwe na ujasiri kuwa tayari unazo haja unazoziomba kwa njia ya imani.

USHUHUDA WANGU

    Rafiki najua shuhuda zinajenga sana na zinainua sana imani ya mtu,mimi nina shuhuda nyingi sana ila ni kwa nia ya kukujenga ili ujenge shauku ndani yako na Mungu atafanya zaidi.Nilikuwa natamani sana kuwa lecture/mwalimu wa chuo kikuu.Na nilipomaliza elimu yangu ya udactari ya chuo kikuu niliomba nafasi ya kuwa mwalimu katika chuo nilichosomea.Tulifanya interview na nilikosa ile nafasi, binafsi iliniuma sana  lakini kwa sababu sikuwahi kuwa na uzoefu wa kufundisha,na katika interview wenye uzoefu walikuwepo hivyo wakachukuwa wenye uzoefu mimi nikakosa.Nikamuuliza Mungu akaniambia umeomba sana anza kuamini kuwa wewe ni lecture nikaanza kukiri ingawa ilikuwa ngumu sababu Tanzania kuna chuo kimoja tu cha kazi niliyosomea ya walemavu,ikabidi nitafute kazi nchi za ulaya na Asia kwa vile walitangaza ajira pia.Siku moja baada ya kuendelea kuamini niliitwa chuo hichohicho nikaambiwa wiki inayofwata nije kazini na nilikuwa napenda sana kuanza kufaya kazi Tanzania na Mungu akanijibu haja ya moyo wangu, na sasa ni lectuere.Usiogope hata wewe mpendwa Mungu aliyetenda kwangu namsii atende na kwako pia ili aufariji moyo wako.Usiogope Mungu anajua kilichobora kwa ajili yako maadamu Bwana ni mchungaji wetu hatutapungukiwa na kitu (ZABURI 23:1) halleluya.Mungu ametuumba tutawale dunia nchi na vyote vijazavyo ni mali ya bwana dunia na wote wakaao ndani yake (Zaburi 24:1),inamaanisha kazi zote pia ni mali yake na anajua wapi atakuweka na kwa wakati gani rafiki.

       Nimesema tena imani ni mikono ya kupokea mahitaji na haja zetu tunazoomba.Tunapokea kwa kadiri ya nguvu itendayokazi ndani yetu yaani imani yetu.Inamaanisha imani yako ikiwa na viwango fulani unapokea haraka zaidi kinachotofautisha majibu mengi ya wana wa Mungu ni imani waliyonayo kwa Mungu juu ya hilo jambo.Kila mtu alipookoka alipewa kiwango cha imani sawa na mwenzake lakini huwa imani inakuwa kulingana na unavyoifanyiza mazoezi ya kuiweka kwa matendo, na hapo ndipo tunapotofautiana sisi kwa sisi.Na imani yako ikikaa bila matendo kuna mda itakufa kama bibilia inavyosema (Yakobo 2:18) lakini mtu akisema, wewe unayo imani ,nami ninayo matendo.Nionyeshe imani yako pasipo matendo,nami nitakuonyesha imani yangu kwa njia ya matendo.Mstari wa 26 maana kama vile mwili pasipo roho umekufa,hivyohivyo na imani pasipo matendo imekufa.

        Ni kwa kadiri ya uhakika wa neno la Mungu uliondani yako yaani imani yako ndiyo utapokea na ndiyo maana huwa nasisitizia sana watu wawe wasomaji wa neno ili waongeze uhakika wa mambo yao katika kuzijua ahadi zao na shetani hatakuweza kwa jana la Yesu.Embu fikiria  kuhusu hali unayopta ni kweli hauna uhakia wa neno la Mungu juu ya hali hiyo? Kuna nini Mungu amesema juu ya hali hiyo kwenye neno lake? Anasema (1Petro 5:7) Huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana na mambo yenu. Dai haki yako kwa baba yako maana wewe ni mwana wake na si mtumwa tena.Mungu si mwnadamu hata aseme uwongo ahadi zae zinasimamaa hata nyota zingezimika ahadi zake zadumu hata milele Haleluya.

          Imani ni kuwa na uhakika /ujasiri na udhibitisho moyoni ukisoma tafsiri mbalimbali za kiyunani.Unapoomba ule uhakika wa haja zako kwamba Mungu atakujibu na ujasiri ndio mikono ya kupokea.Ninamaanisha unapokuwa na imani mambo yatarajiwayo yanakuwa wazi au halisi kwako na ndani yako kabla hayajathihirika, nikimaanisha unaanza kuona majibu yako kwa macho ya imani.

         Hivyo imani kama mikono inaambatana na ujasi ili upokee nitafafanua zaidi hapa na kwa mifano ili uelewe zaidi.Kuna kipindi nilikutana na hali fulani nilipoanza kazi,Mungu aliambia nikianza kazi nimpatie mshahara wangu wa kwanza kama malimbuko.Na hata wazazi wangu na marafii walikuwa wananiambia kumbuka mshahara wa kwanza sio wako Lightness.Nilipokuwa nawaza nitaishi vipi mwezi mzima Mungu akanipa wazo la kuanzisha biashara kwa mtaji wa sh alfu 10 tu.Nilikuwaga muoga sana wa kufanya biashara nikawa nikitoka kazini nauza hereni,  mikufu na bangili za wanawake kwa rafiki zangu maofisini na kanisani.Nikaanza kupata hela nyingi sana  hadi mtaji ukafika laki moja na kuendelea, na mpaka sasa najisikia raha sana kufanya biashara na nimeweza hadi kuajiri watu wasiokuwa na kazi nafanya nao na nawalipa.Nitumia ujasiri na Mungu ananibariki sana na sijawahi kupungukiwa au kujuta naipenda kazi yangu na mshahara sasa ni kama mtaji wangu.

         Mpendwa nataka nikwambie unapoomba pesa Mungu hakupi pesa bali anakupa wazo la kitu cha kufanya ili upate pesa, sababu pesa hazipo mbinguni zipo kwa mikono ya watu.Na uwe jasiri na mbunifu kwa kila wazo Mungu analokupa.Watanzania wengi sio majasiri wala wabunifu, ni waoga sana mtu anawaza nikifanya biashara Fulani atanionaje? Huo ni ujinga na uzembe (Hosea 4:6) Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa.Usidharau mwanzo wa mambo madogo nitazungumzia hili kwa makala nyingine na ujasiliamali kwa wana wa Mungu.Ukitaka kuishi maisha ya imani kuwa jasiri biblia inasema wenye haki ni majasiri kama samba.Kwa leo nitaisha hapo naamini Mungu kasema na wewe nakutakia maisha mema ya kuishi kwa imani.Ni mimi

 Docta LIGHTNESS WILLIAM NG’UNDA kutoka Moshi KCMC

Advertisements

10 thoughts on “IMANI – 2

 1. HONGERA DADA YANGU KWA SOMO ZURI.
  Najivunia kuwa na dada kama wewe,
  juhudi zako katika kueneza injili zanipa moyo wa kusonga mbele.

  Natamani muziki wako wa injili na mafundisho kama haya viwafikie wengi.

 2. Nimebarikiwa sana na Mungu akubariki uendeleae kutufundiasha mengi zaidi kuhusu imani.

 3. naomba msaada wa maombi Mungu anipe nguvu mpya,kwan nimevunjika moyo sina aman kabisa toka mamangu anitoke wakat mgumu wa kufunga ndoa yangu sielew kabisa ivi ni mpango wa Mungu au vip

 4. Ubarikiwe Dr. yote uliyofundisha yamenifungua moyo wangu nami naanza kujiandaa kufanya biashara kwa kidogo nilichonacho na Namuomba mungu azidi kunifunulia zaidi mafundisho

 5. Barikiwa sana mtumishi Lightness! Hii ni nzuri.
  Ni kweli imani ndio mkono wa kupokelea yale yasiyoonekana kuwa yanayoonekana. Maarifa na kujua lile Mungu anatuelekeza ni Muhimu sana.
  Watu wa Mungu tuamke “PESA HAZIPO MINGUNI ZIPO KWA MIKONO YA WATU” -Ili tuweze kuzipata yabidi kufanya kitu/kazi ya kuwasababisha wenye nazo wazilete kwa kupata huduma/bidhaa tutoayo.

 6. nawashukuru wote mnaoendelea kusoma makala haya na Roho mtakatifu apande mbegu ndani yako ambayo itazaa sana kama neno lake linavyosema

 7. ASANTE SANA MPENZI USIOGOPE ANZA NA HILO NA SIKU MOJA UTAJIKUTA UNAUZA MAGARI USIDHARAU MWANZO MDOGO NA KANUNI YA MUNGU NI KUMTOA MNYONGE MAVUMBINI NA KUMTUKUZA MUNGU AKUPE UJASIRI NA KIBALI KIKUBWA KWA JINA LA YESU .YUSUFU ALIANZIA GEREZANI HADI KUWA WAZIRI MKUU NJIA ZA MUNGU HAZICHUNGUZIKI

 8. Asante sana mtumishi somo lako limenibariki sana. Ngoja nijipange nione wapi ninakwama na kurudi tena kujaribu. Mungu azidi kukutia nguvu na baraka ktk huduma yako

 9. DOCTA MUNGU akubarirki sana, nimebarikiwa na kutiwa moyo , nimekuwa nikipanga mara nyingi kwamba nitafanya jambo fulani dogo tu kwa mfano kuandaa popcon (bisi) na kuuza, lakini linaishia hewani ,bila kuja sababu , kumbe ni swala la ujasiri na kuthubutu, nimefunguka kwa hilo.Mungu akutumie zaidi.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s