Kuna wachungaji wanaonunua watu kutoa shuhuda za uongo?

Umesikia habari hii kutoka nchini Kenya? mchungaji Michael Njoroge wa Fire Ministries Embakasi, anaaminika kwa ibada za miujiza na upako, ambapo watu wengi hushuhudia kanisani wameponywa, wengine kupakwa mafuta, maji ya uponyaji, pia kumuona ni KSH 1000. nk

Kuona jinsi ibada inaendeshwa tazama hii video

Hivi karibuni umeibuka mjadala juu ya huduma yake baada ya dada changudoa, kwa jina la Ester Mwende alipofanya mahojiano na Televishen ya NTV amedai analipwa kutoa ushuhuda wa uongo kwenye kanisa hilo, na amewatafuta wadada wengine wanaojiuza na kufanya kazi ya kudanganya shuhuda mbali mbali kanisani hapo, Ameamua kuweka wazi baada ya mchungaji kutomlipa pesa kama walivyokubaliana. unaweza kumsikiliza hapa!

Hivi kama kuna ukweli kwenye makanisa yetu haya, Watu watakuja kwa Kristo?

Advertisements

8 thoughts on “Kuna wachungaji wanaonunua watu kutoa shuhuda za uongo?

  1. Hizi ni nyakati za mwisho na shetani anafanya kazi kwa kasi kuliko mwanzo kwasababu anajua muda alionao ni mchache. Hivyo watu wa Mungu kazi yetu ni kukesha na kuomba kwasababu atakayevumilia hadi mwisho ndiye atatkayeokoka

  2. Hao wachungaji na wafuasi wao wote wanatimiza unabii wa siku za mwisho. Shika sana ulicho nacho usije ukautimiza unabii wa siku za mwisho. LAKINI angalia sana ulichonacho kisije kikakupotezea muda na kukupa hasara.

  3. Ndugu usishangae watu wakimiminika, Biblia inasema Njia nyembamba watakaoiona ni WACHACHE, kwa kusema hivyo, njia Pana wengi watamiminika, haijalishi nini KINAWAFANYA WAMIMINIKE. Ukikumbuka Biblia imeeleza wazi, katika Wafilp, 1.WENGINE WANAMHUBIRI KRISTO KWA SABABU YA TUMBO. 2. WENGINE KWA SABABU YA FITINA. 3. WENGINE KWA MOYO MWEUPE. Na pia akasema, hata anawaambia kwa machozi kuwa WENGINE NI ADUI WA MSALABA. Hizo ni Injili mbali mbali. Yesu akasema Math 24.13 ANGALIENI MTU ASIWADANGANYE. Nani aniangalizie nisidanganywe? Ni mimi mwenyewe, kwa kusoma Biblia, kuomba, n.k. Tubarikiwe.amen.

  4. Ni hatari sana, Mwaka jana Dar kuna kanisa lilivuma kwa tuhuma hizi (jina nahifadhi) wingi wa miujiza makanisani na TV hizi, Mungu aturehemu.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s